Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 993 | 994 | (Page 995) | 996 | 997 | .... | 1896 | newer

  0 0

  Keki ya Kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa wateja ya benki ya CRDB tawi la Water Front.
  Mkurugenzi wa Benki ya CRDB tawi la Water Front, Donath Shirima (Kulia) akizungumza na kuwashukuru wateja wa Benki ya CRDB tawi la Water Front kwa kuwa wateja wao wa kudumu kwa kipindi chote.
  Meneja Biashara wa Benki ya CRDB tawi la Water Front jijini Dar es Salaam, Adam Akaro (katikati) akizungumza na wateja pamoja na kuwaribisha katika hafla fupi ya kudhimisha wiki ya Huduma kwa wateja katika tawi lao jijini Dar es Salaam leo.
  Meneja wa huduma kwa wateja wa Benki ya CRDB tawi la Water Front, Mary Ngowi akiwakaribisha wateja wa tawi hilo kwaajili ya kukata keki na kula pamoja na wateja wa tai hilo jijini Dar es Salaam leo.
  Mkurugenzi wa Nemarty Limited, Neema Lyimo akikata keki kwa niaba ya wateja wa tawi la Benki ya CRDB tawi la Water Front wakati wa kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja katika tawi la Water Front jijini Dar es Salaam leo.
  Meneja wa huduma kwa wateja wa Benki ya CRDB tawi la Water Front, Mary Ngowi akisaidiana na Mkurugenzi wa Nemarty Limited, Neema Lyimo  kukata keki wakati wa kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja jijini Dar es Salaam leo.
  .
  Mkurugenzi wa Benki ya CRDB tawi la Water Front, Donath Shirima akimlisha keki Mkurugenzi wa Nemarty Limited, Neema Lyimo.
  Mkurugenzi wa Nemarty Limited, Neema Lyimo akimlisha  keki Mkurugenzi wa Benki ya CRDB tawi la Water Front, Donath Shirima jijini Dar es Salaam leo.
  Meneja wa huduma kwa wateja wa Benki ya CRDB tawi la Water Front, Mary Ngowi akimlisha keki Mkurugenzi wa Nemarty Limited, Neema Lyimo wakati wa kudhimisha wiki ya huduma kwa wateja jijini Dar es Salaam leo.

  Mkurugenzi wa Nemarty Limited, Neema Lyimo akiwalisha keki wateja wa benki ya CRDB tawi la Water front jijini Dar es Salaam leo wakatiwa kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja.


  Mkurugenzi wa Nemarty Limited, Neema Lyimo akialisha keki wafanyakazi wa benki ya CRDB tawi la Water Front jijini Dar es Salaam leo wakati wa kuadhimishi wiki ya hudma kwa wateja jijini Dar es Salaam leo.
  Wafanyakazi wa benki ya CRDB tawi la Water Front wakiwa katika picha ya pamoja jijini Dar es Salaam leo.
  Mkurugenzi wa Nemarty Limited, Neema Lyimo akikabidhiwa zawadi na Mkurugenzi wa Benki ya CRDB tawi la Water Front, Donath Shirima wakati wa kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja jijini Dar es Salaam leo katika benki ya CRDB tawi la Water Front.
  Mkurugenzi wa Nemarty Limited, Neema Lyimo katikati akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Benki ya CRDB tawi la Water Front, Donath Shirima(Kulia) wapili kulia ni Meneja wa huduma kwa wateja wa Benki ya CRDB tawi la Water Front, Mary Ngowi na mmoja ya wafanyakazi wa tawi hilo, Batseba Mwakalobo mara baada ya kukabidhiwa zawadi jijini Dar es Salaam leo wataki wa kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja katika tawi la Water Front.


   Baadhi ya zawadi za wateja.
  Picha ya Pamoja ya wafanyakazi wa Benki ya CRDB tawi la Water Front jijini Dar es Salaam leo.

  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
  BENKI ya NMB, imezindua Wiki ya Huduma kwa Wateja Duniani kwa kuahidi muendelezo wa huduma bora kwa wateja na kupokea ushauri kutoka kwa wateja na wadau, huku ikisisitiza utayari katika kuelekea Tanzania ya Viwanda.

  Akizungumza wakati wa uzinduzi huo uliofanyika NMB Tawi la Msasani, Mkurugenzi Mtendaji wa NMB, Ineke Bussemaker, amesema licha ya kuwa huduma bora ni kipaumbele cha kila siku, lakini wataitumia wiki hii kuboresha zaidi, ikiwamo kufanyia kazi maoni ya wateja.

  Ineke amesema kwamba, kutokana na kauli mbiu ya Serikali ya Awamu ya Tano, chini ya Rais John Magufuli, ya kuigeuza Tanzania kuwa ya viwanda, benki yake iko tayari kuendana na kasi ya mchakato huo, ambao unategemea sana ubora huduma za kibenki.

  Ineke ameongeza , benki yake imekuwa kinara nchini sio tu katika utoaji wa huduma bora kwa wateja, bali pia huduma bora za kijamii kwa ujumla, ambako imekuwa ikichangia katika sekta zote, zikiwemo za afya na elimu.

  Aidha, katika kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja Duniani, NMB imepanga kufanya ziara katika Kituo cha Kulelea Wazee kilichopo Kigamboni jijini Dar es Salaam, ambako pamoja na mambo mengine, watatoa msaada na kuhudumu kwa wazee waliopo kambi hiyo.

  Ineke amewataka wateja wa NMB kuwa sehemu ya maendeleo ya benki hiyo kwa kutoa maoni yatakayoongeza kasi ya huduma bora, huku akiahidi kuyafanyia kazi maoni yote ya maboresho yatakayotolewa na wateja wao nchini kote.
   Mkurugenzi Mtendaji wa Banki ya NMB Inike Bussemaker akimkabidhi Godliver Mwendo cheti cha mfanyakazi bora wa benki hiyo katika uzinduzi a wiki ya huduma kwa mteja tawi la Msasani Jijini Dar es salaam.

   Mkurugenzi Mtendaji wa Banki ya NMB Inike Bussemaker(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa tawi la NMB Msasani katika uzinduzi wa wiki ya huduma kwa mteja leo Jijini Dar es salaam.
  Meneja wa kanda ya Kinondoni Vicky Bishubo akielezea namna benki ya NMB imeweza kuwafikia wananchi na wateja wao kwa uharaka na madhumini yao ya kuendelea kutoa huduma bora katika Wiki ya Huduma kwa wateja iliyozindulia leo. 

   Mkurugenzi Mtendaji wa Banki ya NMB Inike Bussemaker akizungumza na wateja waliofika asubuhi katika tawi la NMB Msasani na kuwaelezea malengo yao ya kuendelea kutoa huduma bora kwa wateja.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Banki ya NMB Inike Bussemaker akiwa na  sambamba na  Kamanda wa Polisi  Mkoa wa Kipolisi Kinondoni SACP Suzane Kaganda katika kuchukua chakula.
   Wateja wa benki ya NMB wakiwa wanachukua chakula.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Banki ya NMB Inike Bussemaker akiwa anasalimia na Kamanda wa Polisi  Mkoa wa Kipolisi Kinondoni SACP Suzane Kaganda leo katika uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja leo NMB Msasani.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Banki ya NMB Inike Bussemaker wakizungumza jambo na  Kamanda wa Polisi  Mkoa wa Kipolisi Kinondoni SACP Suzane Kaganda katika uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja leo Jijini Dar es salaam.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Banki ya NMB Inike Bussemaker akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa tawi la NMB Msasani katika uzinduzi wa wiki ya huduma kwa mteja leo Jijini Dar es salaam.

  0 0


  Baadhi ya maafisa waandamizi wa Vodacom Tanzania,wakiwa wamebeba keki tayari kwa kuwagawia wateja  na wafanyakazi wa kampuni hiyo ikiwa ni sehemu ya kufurahia kwa pamoja kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja duniani.
   Afisa Mkuu wa Idara ya huduma kwa wateja wa Vodacom Tanzania,Harriet Lwakatare akiongea na baadhi ya wateja waliofika kupata huduma mbalimbali katika duka la kampuni hiyo lililopo Mlimani city jijini Dar es Salaam leo ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja duniani.

   Baadhi ya wateja wa Vodacom Tanzania waliofika kupata huduma mbalimbali katika duka la kampuni hiyo lililopo Mlimani city jijini Dar es Salaam leo wakichukua keki kutoka kwa Afisa Mkuu wa Idara ya huduma kwa wateja wa Vodacom Tanzania,Harriet Lwakatare(kushoto) ikiwa ni sehemu ya kufurahia kwa pamoja kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja duniani.
   Mmoja wa wateja wa Vodacom Tanzania aliyefika kupata huduma mbalimbali katika duka la kampuni hiyo lililopo Mlimani city jijini Dar es Salaam leo akifurahi jambo wakati alipokuwa akipewa keki  na Afisa Mkuu wa Idara ya huduma kwa wateja wa kampuni hiyo,Harriet Lwakatare(kulia) ikiwa ni sehemu ya kufurahia kwa pamoja kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja duniani.

  0 0

   Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kushoto), akiangalia taarifa zinazoingia katika mfumo wa kuhifadhi kumbukumbu alipofanya ziara ya kushtukiza katika Kituo mahiri cha kuhifadhi Kumbukumbu cha Taifa (Internet Data Centre), kilichopo eneo la Kijitonyama jijini Dar es salaam. 
   Msimamizi wa masuala ya TEHAMA Bw. John Chorai (kulia), akimuonesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kushoto), namna kifaa cha kurekodia malipo kinavyofanya kazi wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika Kituo mahiri cha kuhifadhi Kumbukumbu cha Taifa (Internet Data Centre), kilichopo eneo la Kijitonyama jijini Dar es salaam. 
   Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (wa pili kulia), akikagua moja ya kifaa cha kuhifadhi Kumbukumbu katika kituo Mahiri cha Internet Data Centre cha Taifa kilichopo eneo la Kijitonyama jijini Dar es salaam.
   Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (wa kwanza kushoto), akifafanua jambo kwa watumishi wa kituo Mahiri cha kuhifadhi Kumbukumbu cha Taifa (Internet Data Centre), kilichopo eneo la Kijitonyama jijini Dar es salaam wakati alipofanya ziara ya kushtukiza kituoni hapo.
  Mwakilishi wa Kibiashara kutoka Ubalozi wa Uingereza anayesimamia nchi ya Tanzania na Kenya Bw. Lord Hollick (wa pili kulia) akifafanua jambo  kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (wa kwanza kulia) wakati alipomtembelea ofisini kwake kuzungumzia masuala ya kuboresha miundombinu nchini. Kushoto ni Balozi wa Uingereza nchini Bi Sarah Cookie.
  Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano


  0 0


   Muweka Hazina wa Benki ya NMB, Aziz Chacha (wa pili kulia), akizungumza  na wafanyakazi wa Benki hiyo na wateja wakati wa hafla ya uzindua wa wiki ya Huduma kwa wateja Duniani kwa benki hiyo uliofanyika Tawi la Mlimani City Dar es Salaam leo asubuhi. Kulia ni Meneja wa Tawi hilo, Seka Urio. 

    Muweka Hazina wa Benki ya NMB, Aziz Chacha (kushoto), akimkabidhi zawadi Amani Mgweno ya kuwa mfanyakazi bora wa benki hiyo tawi la Mlimani City kuanzia mwezi Januari hadi Oktoba.
   Mkuu wa Kitengo cha Uajiri wa benki hiyo, Mbonny Maumba akisalimiana na wateja katika hafla hiyo ya uzinduzi.
   Hapa wafanyakazi wa benki hiyo wakitakiana heri na wateja.
   Ni furaha tupu katika uzinduzi huo.
   Hakika wamependeza meno yote nje kwa furaha ya uzinduzi huo ambao ni muhimu kwa benki hiyo.

   Uzinduzi ulikwenda sanjari na maakuli.
   Hapa ni chai na mahojiano na waterja wa benki hiyo.
   Mteja wa benki hiyo, Regina Cyrillo akitoa maelezo ya huduma bora zinazotolewa na benki hiyo.
   Mdau wa benki hiyo, Novatus Shiyo akitoa maelezo jinsi wanavyotufaika na huduma za benki hiyo. Wengine ni wateja wa benki hiyo tawi la Mlimani City.
   Mhandisi Heriel Muhulo ambaye ni Ofisa Mtendaji wa Kampuni ya Ujenzi ya Hematec Inn Ltd ya Sinza jijini Dar es Salaam akielezea mafanikio wanayopata kwa kuwa wateja wa benki hiyo.
   Mdau wa benki hiyo kutoka kampuni ya Binaisa Ltd, Mr Mapunda akitoa maelezo yake kuhusu benki hiyo.
   Meneja wa benki hiyo tawi la Mlimani City, Seka Urio (kulia), akizungumza kwenye hafla hiyo.
   Viongozi na baadhi wafanyakazi wa benki hiyo wakifurahia uznduzi huo.

  Picha ya pamoja viongozi wa benki hiyo wafanyakazi pamoja na wateja katika hafla hiyo.


  0 0

  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kulia) akifunua pazia kwa ajili ya kuzindua Nembo ya Bodi ya Filamu pamoja na shindano la uandishi bora wa miswada ya filamu wakati wa kikao cha kupitia uchambuzi wa hali ya Tasnia ya Filamu Tanzania kwa ajili ya ukamilishaji wa sera ya filamu na namna ya kuboresha filamu za ndani leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Filamu Bw. Silvester Sengerema na katikati ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo.

  Katibu Mkuu Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) Bw. Methew Biko (kushoto aliyesimama) akitoa salamu za shirikisho hilo kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kulia) wakati wa kikao cha kupitia uchambuzi wa hali ya Tasnia ya Filamu Tanzania kwa ajili ya ukamilishaji wa sera ya filamu na namna ya kuboresha filamu za ndani leo Jijini Dar es Salaam. Wapili kulia ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo.
  Mtendaji Mkuu TaSUBa Dkt. Herbart Makoye akizungumza na wadau wa filamu (hawapo pichani) walioshiriki katika kikao cha kupitia uchambuzi wa hali ya Tasnia ya Filamu Tanzania kwa ajili ya ukamilishaji wa sera ya filamu na namna ya kuboresha filamu za ndani leo Jijini Dar es Salaam.
  Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo (kushoto) akifafanua jambo wakati wa kikao cha kupitia uchambuzi wa hali ya Tasnia ya Filamu Tanzania kwa ajili ya ukamilishaji wa sera ya filamu na namna ya kuboresha filamu za ndani leo Jijini Dar es Salaam. Katikati ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye na kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Filamu Bw. Silvester Sengerema.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na wadau wa filamu (hawapo pichani) walioshiriki katika kikao cha kupitia uchambuzi wa hali ya Tasnia ya Filamu Tanzania kwa ajili ya ukamilishaji wa sera ya filamu na namna ya kuboresha filamu za ndani leo Jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya wadau wa filamu wakifuatilia kwa makini mada zilizokua zikitolewa wakati wa kikao cha kupitia uchambuzi wa hali ya Tasnia ya Filamu Tanzania kwa ajili ya ukamilishaji wa sera ya filamu na namna ya kuboresha filamu za ndani leo Jijini Dar es Salaam.  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (watano kulia) katika picha ya pamoja na baadhi ya wadau wa filamu walioshiriki katika kikao cha kupitia uchambuzi wa hali ya Tasnia ya Filamu Tanzania kwa ajili ya ukamilishaji wa sera ya filamu na namna ya kuboresha filamu za ndani leo Jijini Dar es Salaam. Wane kulia ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo na wasita kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Filamu Bw. Silvester Sengerema.

  Picha na: Genofeva Matemu na Raymond Mushumbusi WHUSM

  ……………………………………………………

  Na Genofeva Matemu na Raymond Mushumbusi.

  Waandaaji wa miswada ya filamu nchini wametakiwa kuhakikisha kwamba maudhui ya miswada inayoandaliwa inazingatia maadili na utamaduni wa Kitanzania ili kuifanya sera shirikishi inayoandaliwa kuwa na tija.

  Rai hiyo imetolewa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye alipokua akifungua kikao cha Wadau wa Filamu kupitia uchambuzi wa hali ya Tasnia ya Filamu Tanzania kwa ajili ya ukamilishaji wa sera ya filamu na namna ya kuboresha filamu za ndani leo Jijini Dar es Salaam.

  “Maudhui ya miswada ya filamu ikiandaliwa kwa kuzingatia maadili ya kitanzania itaboresha tamaduni zetu na kuzifanya kazi za sekta ya filamu kufanywa kwa kuzingatia weledi hivyo kuiona tasnia kama chombo kimojawapo kinachoisaidia Serikali sio tu kutoa burudani bali pia elimu kwa wananchi” amesema Mhe. Nnauye.

  Aidha Mhe. Nnauye amesema kuwa mapinduzi ya sekta ya filamu hapa nchini yanawezekana iwapo kazi zake zitaonekana katika kiwango cha ubora kwa kuangalia maudhui yaliyomo na mapokeo yake kwa jamii.

  “Napenda kuona wasanii wetu wanakuwa wabunifu badala ya kuwa na filamu zenye maudhui ya aina moja kwa kuzingatia weledi na kuendana na maendeleo ya sayansi na teknolojia ili kuweza kukidhi masoko ya filamu nje ya nchi” amesema Mhe. Nnauye.

  Naye Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo amesema kuwa kutokana na kukua kwa Tasnia ya Filamu kuna uhitaji wa Sera ya Filamu ili iweze kuwa dira ama mwelekeo na mwongozo katika kukuza tasnia hii na kuwezesha kuongezeka kwa fursa za uwekezaji, motisha na fursa za mitaji katika tasnia ya filamu nchini.

  Bibi Fissoo amesema kuwa kukamilika kwa Sera ya Filamu kutabadidlisha kabisa taswira nzima ya Sekta ya Filamu hapa nchini kwani itaboresha uzalishaji wa bidhaa bora zenye kuzingatia weledi, filamu kuangaliwa kama chombo cha kukuza uchumi kwa manufaa ya Taifa na watanzania wote.

  Kwa upande wake Katibu Mkuu Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) Bw. Methew Biko ameishukuru serikali kupitia Bodi ya Filamu na Idara ya Sera na Mipango kwa kusikia kilio cha muda mrefu cha wanatasnia wa filamu kuhitaji Sera ya Filamu na kuahidi ushirikiano wa dhati kutoka kwa wadau wa filamu ili kufanikisha uandaaji ya sera hiyo.

  Kikao cha kupitia uchambuzi wa hali ya Tasnia ya Filamu Tanzania kimehusisha Wakurugenzi wa Idara, Wakuu wa Taasisi za Serikali na binafsi, wadau mbalimbali wa Tasnia ya Filamu wakiwemo wanazuoni, waigizaji, watayarishaji, waongozaji wa filamu, waandishi wa miswada, pamoja na wawekezaji.

  0 0

   Muelimishaji kutoka Kitengo cha Huduma na Elimu ya Mlipa Kodi Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Gabriel Mwangosi akielezea jambo wakati wa semina na wanachama wa Chama cha Wasafirishaji wa mizigo mikoani (UWAMI) leo Jijini Dar es Salaam.
  gar2
  Muelimishaji kutoka Kitengo cha Huduma na Elimu ya Mlipa Kodi Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bibi. Valentina Baltazar fafanua jambo wakati wa semina na wanachama wa Chama cha Wasafirishaji wa mizigo mikoani (UWAMI) leo Jijini Dar es Salaam.
  gar3
  Makamu Mwenyekiti wa Chama cha wasafirishaji wa mizigo mikoani (UWAMI), ambaye pia ni mwakilishi wa Kampuni ya Bob Transpoter, Bw. Ally Luwago akifafanua jambo wakati wa semina kuhusu elimu ya mlipa Kodi iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) leo Jijini Dar es Salaam.
  gar4
  Muelimishaji kutoka Kitengo cha Huduma na Elimu ya Mlipa Kodi Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Gabriel Mwangosi akionyesha nakala ya namba ya mlipa kodi (TIN) iliyofanyiwa maboresho wakati  wa semina na wanachama wa Chama cha Wasafirishaji wa mizigo mikoani (UWAMI) leo Jijini Dar es Salaam.
  gar6
  Mmoja wa wanachama wa chama cha usafirishaji mizigo mikoani (UWAMI) aliyefahamika kwa jina moja la David, akichangia mada wakati wa semina kuhusu elimu ya mlipa Kodi iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) leo Jijini Dar es Salaam.
  Picha na: MAELEZO

  0 0

  Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Mohamed Chande Othman akikabidhiwa Bendera ya Taifa na Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali, Kassian Chibogoyo leo ofisini kwake jijini Dar salaam

  Mpicha Chapa Mkuu wa Serikali, Kassian Chibogoyo akizungumza na Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Mohamed Chande Othman kabla ya kumkabidhi Bendera ya Taifa na Ile ya Afdrika Mashariki leo katika Ofisi ya Jaji Mkuu jijini Dar es salaam


  Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Mohamed Chande Othman akizungumza na Waandishi wa Habari (Hawapo pichani) kabla ya kukabidhiwa Bendera ya Taifa na ile ya Afrika Mashariki na Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali, Kassian Chibogoyo ofisini kwake leo jijini Dar salaam.

  Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Mohamed Chande Othman akikabidhiwa Bendera ya Afrika Mashariki na Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali, Kassian Chibogoyo leo ofisini kwake jijini Dar salaam
  Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Mohamed Chande Othman akifurahia Zawadi ya Tai ya Bendera ya Taifa aliyopewa na Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali, Kassian Chibogoyo leo ofisini kwake jijini Dar salaam
  Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Mohamed Chande Othman akimwonyesha Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali kitabu cha Sheria kuhusu matumizi ya Vielelezo vya Taifa kabla ya kukabidhiwa Bendera ya Taifa na ile ya Afrika Mashariki.

  ………………………………………….

  Na Mary Gwera, MAHAKAMA

  JAJI Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman amezitaka Wizara, Halmashauri na Taasisi nyingine za Serikali kutumia vielelezo vya Taifa kama bendera na nembo ya taifa katika ofisi zao ili kuenzi tunu na vielelezo vya Taifa.

  Aliyasema hayo ofisini kwake Mahakama ya Rufani jijini Dar es Salaam alipokuwa akipokea rasmi bendera ya Taifa na Afrika Mashariki kutoka kwa Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali, Bw. Cassian Chibogoyo.

  Alisema kuwa vielelezo hivi vya taifa vinalindwa kisheria kwa hiyo inabidi vipate heshima yake kwa kuwa vinawakilisha taifa. “Sheria pia inavitambua vielelezo hivi hivyo ni muhimu vikapewa heshima yake, kwani hata mtu akichezea vitu hivi anaweza kufungwa kwa mujibu ya sheria,” alisisitiza Jaji Mkuu.

  Aliongeza pia Mahakama ya Tanzania pia iko katika mchakato wa kupata bendera yake kama ilivyo kwa Taasisi nyingine kama Bunge, pamoja na nembo yake ili ziweze kutumika katika Mahakam azote nchini.

  Awali; akiongea na Jaji Mkuu pamoja na waandishi wa habari kabla ya makabidhiano hayo, Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali, Bw. Cassian Chibogoyo pia alizitaka Taasisi za Serikali kutopuuzia umuhimu wa matumizi wa vielelezo vya Taifa.

  Alisema kuwa baadhi ya Ofisi nyeti za Serikali hazina bendera na vielelezo vingine muhimu ambavyo vinaiwakilisha Taifa na kusisitiza matumizi yake ili kuenzi tunu za Taifa.

  “Ofisi nyingi za Serikali zinatumia bendera zilizochakaa na nyingine hazina kabisa, vitu hivi ni muhimu kwa taifa hivyo ni vyema kuvienzi na kuvithamini pamoja na kuvitunza,” alisema Bw. Chibogoyo.

  0 0

   Meneja Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Lulu Mengele, (kulia), akiwasaidia wanakijiji hawa wa Ikwiriri, Wilayani Rufiji mkoani Pwani, kutuma michango kwa njia ya mtandao wa simu, wakati wa kuandikisha wanachama chini ya mpango wa Wote Scheme kwenye chuo cha Maendeleo ya Jamii, Ikwiriri,  Oktoba 3, 2016. Takriban wanakijiji 395 wakiwemo, wakulima, wafuga nyuki, wavuvi na waendesha bodaboda, wamekabidhiwa kadi za uanachama kupitia mpango huo unaoruhusu mtu yeyote aliye kwenye sekta rasmi na isiyo rasmi kujiunga kwa kuchangia kila mwezi kima cha chini shilingi 20,000.

   Meneja wa PPF, Kanda ya Temeke, Erica Sendegeya, (kulia), akimkabidhi kadi ya uanachama wa Mfuko huo kupitia mpango wa uchangiaji wa Hiari, (Wote Scheme), wakati wa kuandikisha wanachama na kugawa kadi kwenye viwanja vya chuo cha ufundi Ikwiriri, wilayani Rufiji mkoa wa Pwani, Oktoba 3, 2016.

   Zawadi Hamza Sule, (kushoto), ambaye ni mkulima huko Ikwiriri, akipokea kadi yake ya uanachama wa PPF kupitia Wote Scheme
  NA MWANDISHI WETU, IKWIRIRI

  MFUKO wa Pensheni wa PPF, kupitia mpango wa Uchangiaji wa Hiari, “Wote Scheme”, umesajili karibu wanachama 400  huko Ikwiriri wilayani Rufiji mkoa wa Pwani.

  Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa zoezi la usajili na ugawaji kadi za uanachama kwenye viwanja vya chuo cha Ufundi Ikwiriri, (IFDC), Oktoba 3, 2016, Meneja wa PPF Kanda ya Temeke, Erica Meshack Sendegeya, alisema,  wanakijiji hao wajasiriamali walihamasika kujiunga na mpango huo baada ya Kanda yake kutoa elimu juu ya umuhimu wa wananchi kujiunga na Mfuko huo kwani kuna manufaa  mengi.

  “Tuliwaeleza, mpango huu wa Wote Scheme umebuniwa ili kutoa fursa ya wananchi walioajiriwa au waliojiajiri wenyewe, wakiwemo wakulima, wavuvi, wafugaji, Boda boda  na mama lishe, kujiunga na Mfuko kwa kuchangia kima cha chini cha shilingi 20, 000 kila mwezi. “Fedha hizo unaweza kuzitoa kwa mkupuo au kwa awamu kulingana na uwezo wa mwanachama,” alifafanua Sendegeya.

  Akielezea faida za kuwa mwanachama, Meneja huyo alisema, “Mwanachama atafaidika na fao la Afya ambapo atapatiwa bima ya afya kupitia NHIF baada ya kuchangia shilingi elfu 60,000 tu.” Alisema na kuongeza kuwa faida nyingine ni pamoja na mwanachama kujipatia mkopo wa maendeleo ambapo sharti kuu la kupata mkopo huu ni mwanachama kuchangia Mfuko kwa kipindi cha miezi sita, mkopo wa elimu, lakini pia fao la uzeeni, alisema Meneja huyo.

  Kuhusu namna mwanachama anavyoweza kuchangia baada ya kujiunga na Mpango huo, Meneja Uhusiano wa PPF, Lulu Mengele alisema, “Kuna njia rahisi ya kuwasilisha michango, ambayo ni kutumia mitandao ya simu, Airtel Money, Tigo Pesa na M-Pesa.” Alisema.

  Baadhi ya wanakijiji waliojiunga na Mpango huo, wameipongeza PPF kwa kutoa elimu ambayo imewafanya wajiunge na Mfuko huo na ni matarajio yao utasaidia kuboresha shughuli zao.

  “Mimi ni mfuga nyuki, kilichonivutia ni jinsi Mfuko huu unavyoweza kutoa mikopo ya maendeleo,” alisema Erasto Joseph, ambaye pia ni mwalimu wa shule.

  Naye Ishara Ibrahim ambaye ni mkulima, alisema, ni matarajio yake kuwa kujiunga na PPF, basi ataweza kumudu kupata huduma ya afya kupitia Bima ya Afya.” Alisema.
    Zawadi Hamza Sule, akionyesha kadi yake baada ya kukabidhiwa
   Seif M. Mgumba akionyesha kadi yake ya uanachama wa PPF, kupitia Wote Scheme
   Khadija R. Kitango, akionyesha kadi yake
   Meneja wa PPF, Kanda ya Temeke, Erica Sendegeya, akizungumza na wanachama hao wapya wa PPF huko Ikwiriri, wilayani Rufiji mkoa wa Pwani Oktoba 3, 2016
   Wanachama wapya wa PPF, wakiwasikiliza viongozi wa PPF 
   Wanachama hawa wapya wakionyeshana kadi zao za uanachama baada ya kukabidhiwa
  Wanachama wakisubiri utaratibu wa kukabidhiwa kadi zao na kufanya malipo ya michango ya awali
   Wanachama wapya wa PPF, wakihudumiwa
   Meenja wa PPF, Kanda ya Temeke, Erica (kushoto), na Meneja Uhusiano wa Mfuko huo, Lulu Mengele, wakiwasaidia wanachama hao kutumia simu zao za mkononi kuweka michango yao 
   Erica, akiwasaidia kuwaelekeza namna ya kutuma michango kupitia simu za mkononi
   Erica (kulia) na Lulu, wakimsikiliza mwanachama huyu wa Ikwiriri baada ya zoezi la kuwapatia kadi za uanachama Oktoba 3, 2016
   Erica, akisoma majina ya wanachama wapya waliojiunga na PPF kupitia Wote Scheme
   Meneja Uhusiano wa PPF, Lulu Mengele, akiwaarifu waandishi wa habari kuhusu shughuli nzima ilivyokwenda
   Lulu akisalimiana na wanachama hawa wenye furaha
  Wanakijiji wa Ikwiriri wakisubiri kupatiwa kadi zao za uanachama baada ya kujiunga na PPF kupitia uchangiaji wa Hiari, (Wote Scheme) Oktoba 3, 2016

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa kimataifa wa Ndege wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere JNIA.
  jos2jos3jos4jos5
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na mgeni wake wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila wakati nyimbo za Taifa za mataifa yote mawili zikipigwa kabla ya ukaguzi wa gwaride lililoandaliwa kwa ajili ya heshima yake.
  jos6jos7jos8
  Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila akikagua gwaride la heshima lililoandaliwa kwa ajili yake mara baada ya kuwasili uwanjani hapo.
  jos9jos11
  Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila akipunga mkono wakati kikundi cha ngoma za asili kilipokuwa kinatumbuiza uwanjani hapo. PICHA NA IKULU

  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametembelea maeneo yaliyopendekezwa kujengwa mji wa Serikali na kujiridhisha kuwa yanatosha kwa ajili ya ujenzi wa makao makuu.

  Katika ziara hiyo aliyoifanya leo mchana (Jumatatu, Oktoba 3, 2016) Waziri Mkuu amesema ameridhishwa na ukubwa wa maeneo hayo ambayo pia yanatosha kujenga miundombinu inayohitajika.

  Katika ziara hiyo Waziri mkuu ameridhishwa na maeneo yaliyotengwa na Mamlaka ya Ustawishaji wa Makao Makuu(CDA) yanayofaa kuwekeza kwa ujenzi wa miundombinu ya biashara kama masoko na hoteli na viwanda na tumejirishisha kuwepo kwa ardhi ya kutosha.

  Wakati huo huo Waziri Mkuu amekaribisha wawekezaji wa miradi mbalimbaliya maendeleo ikiwemo ya ujenzi wa nyumba za watumishi ambao watajenga nyumba za makazi na kuziuza kwa watumishi wa umma na wananchi.

  Aidha amebainisha kuwa muwekezaji atakayekuwa tayari awasiliane na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana ambaye ndiye anayeratibu shughuli hiyo huku akikaribisha wawekezaji wa ujenzi wa hoteli za kitalii na kawaida kwa kuwa wanatarajia kupata wageni wengi.

  “Tumekaribisha pia wawekezaji wa ujenzi wa viwanda tumeiona ardhi inatosha na uzalishaji ni mkubwa Kanda ya kati kwa mkoa wa Dodoma wenyewe, Manyara, Singida na mikoa ya jirani ya Iringa na Morogoro inaweza kunufaika na fursa hizo,” amesema. Awali Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu Dodoma (CDA), Mhandisi Paskasi Muragili alisema maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya ujenzi huo ambayo Waziri Mkuu alimeyatembelea ni Chigongwe lenye hekta 11,297, Kikombo hekta 13,275 na Nyankali hekta 2,370

  0 0


  mmoja wa wanakikundicha Marafiki wa Batuli aliyejulikana kwa jina la Tausi Swalehe akiwa anakabidhi anagawa peniseli kwa baadhi ya wanafunzi ambao ni yatima wanaosoma katika shule ya msingi Ngarenaro ilipo katika kata ya Sokoni one ndani ya jiji la Arusha
  wanakikundi wa kikundi cha marafiki wa batuli wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi waliowagawia msaada wa sare za shule ,penseli ,madaftari na kalamu ikiwa ni moja ya mchango wao kama wao wanakikundi .

  Na Woinde Shizza Arusha.

  Wazazi na watanzania wameaswa kujenga moyo Wa kujitolea kwa makundi maalumu yasiojiweza nakuwapa kile mungu alichowajaalia nakuondoa ubaguzi kwa watoto yatima waliochiwa na ndugu zao.

  Hayo yalisemwa na Tausi swalehe baada ya kikundi cha marafiki Wa batuli kufika kutoa msaada kwenye shule za unga ltd,na Sahel zilizopo kata ya Sokon 1 jijini Arusha nakuwata jamii kuwa na moyo huo wa kusaidia yatima na makundi yasiojiweza.

  Alisema kuwa msaada waliotoa unathamani ya tsh.700,000 vikiwemo madaftari'sare za shule,penseli na pen ambazo zitawapunguzia adha watoto wenye uhitaji wakiwemo yatima na wasiojiweza ambao wameshindwa kujihudumia na kufikia malengo.

  Alisema kuwa ni vizuri kwa jamii kuendelea kuzijali familia zisizojiweza na mayatima iliwaweze kufikia malengo yao yakupata elimu itayowasaidia kujikwamua kimaisha na kuondokana na utegemezi.

  ''Sio wote wenye kuweza kujiendesha kimaisha yatupasa kama jamii kujipanga nakuweza kuwasaidia wenye uhitaji natusingoje kuiachia serikali pekee''alisema Tausi.

  Akipokea msaada huo kwa niaba ya wanafunzi hao wenye uhitaji mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Unga Ltd Rachel Mussa alisema kuwa wapo wengi katika jamii wenye fedha lakini wamekuwa hawatumii vipato vyao katika kusaidia makundi yenye uhitaji.

  Akatoa rai kwa makampuni na wenye kuguswa kuweza kujitolea kwa kile kidogo mungu alichowajaalia kwani wapo watoto wenye uhitaji nao wajitokeza kuwasaidia.

  Nae Mwanafunzi mwenye uhitaji kwa niaba ya wenzake 86 Konsolata Michael alisema kuwa wanashukuru sana kwa msaada huo kwani umukuja wakati muufaka na kuwataka kuendelea kusaidia watoto yatima na wasiojiweza na mungu awazidishie pale mlipopunguza kwa ajili yetu.

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi zawadi ya picha ya mnyama Chui anayepatikana katika mbuga za wanyama za Tanzania Mgeni wake Makamu wa Rais wa Cuba Mh. Salvador Valdes Mesa.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea zawadi ya picha kutoka kwa Mgeni wake Makamu wa Rais wa Cuba Mh. Salvador Valdes Mesa , Kulia ni Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Kikanda na Kimataifa.

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mgeni wake Makamu wa Rais wa Cuba Mh. Salvador Valdes Mesa wakati alipokutana naye Ikuu leo kwa mazungumzo ambapo wamezungumzia jitihada za Serikali hizi mbili ya Cuba na Tanzania katika kuendelea kuimarisha na kudumisha mahusiano mazuri yaliyopo kwa manufaa ya wananchi wa nchi hizi mbili.(PICHA KWA HISANI YA OFISI YA MAKAMU WA RAIS)
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Mgeni wake Makamu wa Rais wa Cuba Mh. Salvador Valdes Mesa wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Tanzania na Cuba.


  Na. Immaculate Makilika- MAELEZO

  Serikali ya Tanzania na Cuba zimeahidi kuendeleza ushirikiano uliopo, ambao umeasisiwa na viongozi wa mataifa hayo Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wa Tanzania pamoja na Fidel Castro Rais mstaafu wa Cuba.

  Akizungumza na waandishi wa habari, Ikulu leo jijini Dar es salaam, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu, amesema kuwa Makamu wa Rais wa Cuba, Mhe. Salvador Valdes Mesa ameitikia mwaliko huo wa kuja nchini kwa vile nchi hizo mbili zimekua na ushirikiano na mahusiano mazuri kwa muda mrefu.

  “Ziara hii ni moja ya jitihada za Serikali hizi mbili ya Cuba na Tanzania katika kuendelea kuimarisha na kudumisha mahusiano mazuri yaliyopo kwa manufaa ya wananchi wa nchi hizi mbili ili kuhakikisha mahusiano yaliyopo yanaimarika zaidi” alisema Makamu wa Rais

  Katika ziara hiyo ya Makamu wa Rais wa Cuba nchini, mambo mbalimbali yalijadiliwa ikiwemo masuala ya Afya, Elimu, Michezo, na Utamaduni, ambapo katika sekta ya afya nchi ya Cuba imepiga hatua na kuahidi kushirikiana na Tanzania ili kujenga kiwanda cha kisasa cha kutengeneza madawa ya binadamu.

  Aliongeza kuwa Tanzania imeomba Serikali ya |Cuba kuendelea kusaidia sekta hiyo kwa kufundisha wataalamu wa afya, ambapo tayari madaktari 24 kutoka Cuba wako nchini kwa ajili ya kusaidia kutoa huduma za kitabibu na mafunzo katika mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara na Visiwani.

  Masuala mengine yaliyojadiliwa katika ziara hiyo ni pamoja na ushirikiano katika sekta ya elimu, biashara, utalii na uwekezaji.Ambapo pia Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Suluhu amesisitiza nia ya Serikali ya Tanzania kudumisha ushirikiano huo ikiwa ni pamoja kupongeza jitihada za kuboresha uhusiano wa Cuba na Marekani.

  Kwa upande wake, Makamu wa Rais wa Cuba, Mhe. Salvador Antonio Valdes Mesa ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa kuendelea kuonesha ushirikiano kwa nchi yake na kuahidi kuendelea kutoa msaada kwa Tanzania.“Tumeamua kuendelea kuboresha mahusiano yetu na Tanzania kwa kuongeza ushirikiano wetu katika sekta nyingine ambazo hatukuwa tunashirikiana hapo awali kama vile sekta ya utalii” alisema Makamu wa Rais wa Cuba

  Aidha, Mhe. Mesa ameiomba Tanzania kuendelea kuiunga mkono Cuba katika masuala ya kimataifa ili kuendeleza ushirikiano na kukuza uchumi kwa nchi zote mbili.

  Makamu wa Rais wa Cuba aliwasili nchini jana jioni kwa ziara ya siku tatu ambapo alipata fursa ya kuonana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa John Magufuli .

  0 0

  Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe. Mhandisi Stella Manyanya akioneshwa baadhi ya majengo yatayojengwa upya katika shule ya sekondari ya Nyakato ambayo pia baadhi ya majengo yake yaliathiriwa na tetemeko la ardhi hiyo kuifanya kuamuliwa kujengwa upya
  Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe. Mhandisi Stella Manyanya akimuonesha jambo mwanafunzi mwenye ulemavu katika shule ya msingi Mgeza Mseto iliyopo mkoani kagera alipoitembelea kuona namna ilivyoathiriwa na tetemeko la ardhi kwenye baadhi ya majengo yake.
  Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe. Mhandisi Stella Manyanya akiwaeleza jambo watoto wenye ulemavu wa ngozi (ALBINISM) wa shule ya Msingi ya Mgeza Mseto iliyopo mkoani kagera alipoitembelea kuona namna ilivyoathiriwa na tetemeko la ardhi kwenye baadhi ya majengo yake.

  Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe. Mhandisi Stella Manyanya akiongea na wanafunzi wa Shule ya Msingi Mgeza Mseto iliyopo mkoani kagera alipoitembelea kuona namna ilivyoathiriwa na tetemeko la ardhi kwenye baadhi ya majengo yake.
  Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe. Mhandisi Stella Manyanya akisaini kitabu cha wageni alipowasili kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera leo Mjini Bukoba.
  Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali (Mst) Salum Kijuu akimueleza Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe. Mhandisi Stella Manyanya hatua zinazoendelea kuchukuliwa na serikali katika kurudisha hali baada ya tetemeko la ardhi kutokea mkoani huko.
  Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe. Mhandisi Stella Manyanya na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali (Mst) Salum Kijuu wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Wizara ya Elimu na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera.
  Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe. Mhandisi Stella Manyanya akikagua vifaa ndani ya maabara katika shule ya sekondari ya Ihungo ambayo pia iliathiriwa kiasi kikubwa na tetemeko la ardhi lililotokea mkoani kagera mapema mwezi September 2016
  Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe. Mhandisi Stella Manyanya akiongea na baadhi ya wafanyakazi waliopo katika eneo la ujenzi mpya wa shule ya sekondari ya Ihungo na kuwataka kufanya kazi kwa viwango stahiki na kwa wakati pamoja na wakijiepusha na vitendo vya wizi wa vifaa vya ujenzi.
  PICHA NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO

  ………………………………………………………….

  Na Benedict Liwenga-MAELEZO

  Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe. Mhandisi Stella Manyanya leo amewasili Mkoani Kagera na kutembelea miundombinu ya sekta ya elimu ili kujionea namna serikali inavyorejesha hali kama awali kutokana na tetemeko la ardhi lililotokea September 10 mwaka huu.

  Akiwa katika shule ya sekondari ya Ihungo, Mhandisi Manyanya amewataka wakandarasi waliopewa dhamana ya kusimamia ujenzi upya wa majengo mapya ya Shule za Ihungo na Nyakato kujenga kwa kuzingatia viwango sahihi kulingana na maelekezo ya wataalam wa miamba.

  “Mmepewa dhamana ya kusimamia ujenzi upya wa shule hii, nawaombeni muzingatie viwango sahihi wakati mnajenga hasa kwa kuangalia mapendekezo ya wataalam wa miamba waliyoyatoa ili kuyaweka majengo katika hali ya usalama” Alisema Mhandishi Manyanya.

  Aidha Mhandisi Manyanya amewatahadharisha wakandarasi wenye tabia ya kudokoa vifaa vya ujenzi kutothubutu kufanya hivyo kwani yeyote atayeiba vifaa hivyo atachukuliwa hatua za kisheria.

  Katika kuhakikisha wanafunzi wenye ulemavu tofauti wanapata elimu sawa Mhandisi Manyanya amewataka walimu wa shule ya msingi Mgeza Mseto kutenda haki sawa wanafunzi wote bila kujali aina ya ulemavu alionao mwanafunzi.

  Katika hatua nyingine Mhandisi Manyanya amezitaka shule hasa za sekondari nchini kuanzisha mashamba darasa yatakayowawezesha wanafunzi kujifunza kwa vitendo shughuli za kilimo na kusaidia kuifanya shule kuwa na hifadhi ya kutosha ya chakula.

  Kwa upande wa walimu Mhandisi Manyanya amewapongeza walimu wa wilaya ya Bukoba kwa kujituma na kuwekeza katika kilimo cha migomba na kuwataka walimu kote nchini kuiga mfano huo ili kuwa na chakula cha kutosha na kujiongezea kipato cha kuendesha maisha yao ya kila siku.

  0 0
 • 10/03/16--09:59: Article 6

 • 0 0


  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (wa pili kulia) akikata keki kuashiria uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja wa TTCL leo kwenye duka la huduma kwa wateja na bidhaa za TTCL lililopo Makao Makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Waziri Waziri Kindamba pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Biashara TTCL Kanda ya Dar es Salaam, Bi. Jane Mwakalebela (kulia) wakishuhudia tukio hilo. Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Waziri Waziri Kindamba (kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kushoto) wakigonganisha glasi za mvinyo mara baada ya mkuu huyo wa mkoa kuzinduwa Wiki ya Huduma kwa Wateja wa TTCL leo kwenye duka la huduma kwa wateja na bidhaa za TTCL lililopo Makao Makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akimlisha keki Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Waziri Waziri Kindamba kwenye uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja wa TTCL leo. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akimlisha keki Afisa Mkuu wa Masoko na Mauzo wa Kampuni hiyo, Bw. Peter Ngota kwenye uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja wa TTCL leo. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akimlisha keki mmoja wa wateja wa kampuni ya TTCL kwenye hafla ya uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja wa TTCL leo.

  MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amezitaka taasisi na mashirika ya umma yaliopo chini ya mkoa wake kuiunga mkono Kampuni ya Simu ya kizalendo Tanzania (TTCL) kwa kuanza kuzitumia bidhaa za kampuni hiyo hasa kwenye shughuli za mawasiliano ili kuonesha uzalendo kwa vitendo. 

  Makonda ametoa kauli hiyo leo Makao Makuu ya TTCL jijini Dar es Salaam alipokuwa akizinduwa Wiki ya Huduma kwa Wateja wa kampuni ya TTCL, huku akiahidi kuzishawishi taasisi na mashirika ya umma yanayofanya kazi chini ya utawala wake kuhakikisha wanatumia huduma za TTCL ili kuiunga mkono kampuni hiyo ya kizalendo ya mawasiliano. 

  Alisema Serikali imeonesha nia njema ya kuirejesha TTCL katika hali nzuri baada ya kuirejesha kwa asilimia 100 chini ya umiliki wake, hivyo kuyataka mashirika na taasisi za umma kuunga mkono juhudi za Rais wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli kuirejesha kampuni hiyo chini ya umiliki wa serikali kwa asilimia 100. 

  Alisema yete kama kiongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam atahakikisha ofisi zote za umma zilizopo chini ya mkoa wake zitatumia huduma za TTCL na endapo watendaji wa TTCL sinazosita kutumia watoe taarifa ili yeye ahoji ni kwanini wanapinga agizo hilo. 

  Aidha Mkuu wa Mkoa huyo alisitaka baadhi ya taasisi za umma wadaiwa sugu wa TTCL walipe madeni yao mara moja na zile zinazokaidi zifikizwe kwenye mkono wa sheria (mahakamani) kwa ajiri ya taratibu za kisheria. Alisema kampuni itafanya vizuri kihuduma endapo wateja wanaopewa huduma wanalipa kwa wakati ili iweze kuboresha huduma zake kwa wateja wote. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akipiga picha na mwenyeji wake huku akionesha alama ya mabadiliko inayotumiwa na TTCL.

  Kwa upande wake, Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Waziri Waziri Kindamba akizungumza kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Mkoa Makonda alisema Kampuni ya Simu Tanzani iliianza mchakato wa kuleta mabadiliko ndani ya kampuni hiyo tangu mwaka 2014, mpango uliopewa jina la 'TTCL Business Transformation Project' ambao ulilenga kuongeza tija na ufanisi katika uzalishaji na uwajibikaji ili kutoa huduma bora kwa Wananchi na Wateja wetu wote wa ndani na nje ya Tanzania. 
  Aliyataja miongoni mwa mafanikio yaliyopatikana kwa kipindi chote cha mabadiliko ya kibiashara ni pamoja na kuirejesha Kampuni ya TTCL kumilikiwa na Serikali kwa asilimia 100 baada ya kuondoka kwa aliekuwa mbia mwenza, kupatikana kwa Masafa yanayowezesha kutolewa kwa huduma za 3G/4G na utekelezaji wa miradi mbali mbali ya kuboresha huduma. 
  Kindamba aliongeza mafanikio mengine ni kupatikana kwa fedha kutoka kwenye vyanzo mbalimbali ikiwemo Benki ya Uwekezaji Tanzania (TIB), Kupatikana fedha kutoka Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) ambazo zinatumika kwa ajili ya kupeleka mawasiliano vijijini na Ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya mtandao wa Mawasiliano, mitambo chakavu, kusimika mitambo ya GSM-2G, UMTS- 3G na LTE- 4G.
   "...pia katika eneo la Biashara; Tumeendelea na juhudi za kutangaza na kuitambulisha huduma ya 3G/4G katika jiji la Dar es salaam, bidhaa nzuri ambazo zinakidhi mahitaji ya wateja zimekuwa chachu ya wananchi kuanza kuvutiwa na bidhaa za TTCL. TTCL tunatoa huduma ya T-TV ambayo wateja wanapata fursa ya kutazama matangazo ya vituo mbalimbali vya Luninga kupitia simu zao za Smartphone na tablet. Pia, TTCL imefanikiwa kuunganisha Hospitali Kuu za Mkoa wa Dar es salaam katika Mkongo wa TTCL, hivyo kutengeneza mazingira mazuri kwa taasisi hizo kuendesha huduma za afya kwa kutumia teknolojia yaani Afya-Mtandao (E-Health)," alisema Kindamba.
   Aidha alisema wiki ya Huduma kwa Wateja, TTCL inalenga kutambua na kuthamini mchango wa wateja, ambao wamekuwa chachu ya ukuaji wa Kampuni, huku kampuni ikijipanga kuwatembelea wateja wake, kuzungumza nao na kuomba ushauri wao ili tuweze kutoa huduma bora na endelevu ambazo zitaongeza tija katika kazi zao. 
  "...Tumejipanga vyema kufanya kazi kwa ufanisi, tunatekeleza kwa vitendo falsafa ya Serikali yetu ya awamu ya tano ya Hapa Kazi Tu. Tutatumia rasilimali zetu vizuri ili Kampuni itoe mchango stahiki mageuzi yanayoendelea ya kuifanya nchi yetu kupiga hatua kuelekea kuwa nchi ya Uchumi wa Kati, Nchi ya Uchumi wa Viwanda. Katika kufikia lengo hili, huduma za Mawasiliano ni muhimu sana, na napenda kukuhakikishia kwamba, kwa kutumia huduma za TTCL, lengo hili litafikiwa," Alisema. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (wa pili kulia) akimpa tuzo mmoja wa wafanyakazi bora wa kampuni hiyo kwenye duka la huduma kwa wateja na bidhaa za TTCL lililopo Makao Makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akipiga picha na wafanyakazi bora wa TTCL waliozawadiwa kwenye uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akipiga picha na baadhi ya viongozi waandamizi wa TTCL kwenye uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja. Meneja Uhusiano wa TTCL, Nicodemus Mushi akitoa ratiba fupi ya hafla hiyo kabla ya uzinduzi.

  0 0

  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akisikiliza maelezo kutoka kwa mwakilishi wa Wakala wa Taifa wa Utafiti wa Nyumba Bora na Vifaa vya Ujenzi (NHBRA) wakati wa maadhimisho ya siku ya makazi duniani leo Jijini Dar es Salaam.
  kuv1
  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akizungumza na waandishi wa habari kuhusu siku ya makazi duniani leo Jijini Dar es Salaam.
  kuv2
  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akakiangalia bango la Wakala wa Taifa wa Utafiti wa Nyumba Bora na Vifaa vya Ujenzi (NHBRA) wakati wa maadhimisho ya siku ya makazi duniani leo Jijini Dar es Salaam.

  Picha na: Jonas Kamaleki, MAELEZO

  0 0


  Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali (Mst) Salum Kijuu akimkabidhi Vifaa vya ujenzi Mjane Agripina Angelo mkazi wa Kitoma Mkoani Kagera kwa Niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
  Mjane Agripina Angelo mkazi wa Kitoma Mkoani Kagera akimuonesha Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali (Mst) Salum Kijuu nyumba aliyoijenga baada ya nyumba yake ya awali kuharibiwa na tetemeko la ardhi lililotokea mkoani kagera mapema mwezi September
  Nyumba ya Mjane Mjane Agripina Angelo aliyoijenga baada ya nyumba yake ya awali kuharibiwa na tetemeko la ardhi lililotokea mkoani kagera mapema mwezi September.SYLVESTER RAPHAEL-AFISA HABARI-KAGERA


  Na Eleuteri Mangi-MAELEZO.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemchangia vifaa vya ujenzi Mjane Agripina Angelo Mkazi wa Kitoma Wilayani Karagwe Mkoani Kagera.

  Akimkabidi vifaa hivyo kwa niaba ya Rais, Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali (Mst) Salum Kijuu alisema kuwa Rais Dkt. Magufuli amefanya hivyo baada ya kuona kupitia vyombo vya habari jitihada za Mjane huyo kuanza kuijenga nyumba yake upya kutokana na kuharibika baada ya tetemeko la ardhi lililotokea mkoani humo mapema mwezi septemba.

  Aidha Mkuu wa Mkoa Kijuu alitoa wito kwa wananchi ambao hawajaanza juhudi za kurejesha makazi yao waige mfano wa mjane huyo kwa kuanza ujenzi wa nyumba zao.Akizungumza baada ya kukabidhiwa vifaa hivyo Bi. Agripina alisema kuwa anamshukuru Rais kwa mchango huo kwani vifaa hivyo vitamsaidia kukamilisha ujenzi wa nyumba yake na hatimaye kupata mahali pa kuishi yeye na familia yake baada ya nyumba yake ya awali kuharibiwa na tetemeko la ardhi.

  Vifaa alivyokabidhiwa mjane huyo ni pamoja na Mbao pisi 30, Mabati 35 ya futi kumi ,Saruji mifuko 25 ,Misumari ya mabati kilo 4, Misumari ya kenchi kg 7 na waya za kufungia makenchi kilo 3.

  0 0

   Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega akifafanua jambo wakati wa kukagua jengo linalotarajiwa kuwa shule mpya katika kitongoji cha kikonda katika ziara yake kijiji kwa kijiji kwa kushukuru wananchi kwa kumchagua pamoja kuangalia maendeleo leo katika Kijiji cha Bupa Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani.
    Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega akizungumza na wananchi katika kitongoji cha Kikonda akiwa katika ziara yake ya kijiji kwa kijiji kwa kushukuu wananchi kwa kumchagua pamoja na kuangalia maendeleo leo katika Kijiji cha Bupa Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani.
    Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega akizungumza katika mkutano wa wananchi wa kitogoji cha Kikonda juu ya changamoto zinazowakabili akiwa katika ziara yake ya kijiji kwa kijiji kwa kushukuu wananchi kwa kumchagua pamoja kuangalia maendeleo leo katika Kijiji cha Bupa Wilaya ya Mkuranga.

   Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega akiwaonyesha wananchi Diwani wao,Abbas Msangule jinsi ya kushirikiana naye kwa maendeleo katika Kijiji cha Kondo Mwelazi katika ziara yake kijiji kwa kijiji kwa kushukuu wananchi kwa kumchagua pamoja kuangalia maendeleo leo katika Kijiji cha Bupa Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani.
  Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega akiwa katika picha ya pamoja na walimu wa shule ya msingi Kondo Mwelazi alipowatembelea kujua mazingira walionayo na kuwashukuru kuendelea na moyo licha ya kuwa na mazingira mgaumu leo. Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.

  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii -Mkuranga

  Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega amewataka wananchi kufanya maendeleo na sio siasa kwa muda huu.

  Hayo ameyasema leo katika katika ziara ya vijiji vya kata ya bupu, Ulega amesema kuwa wakati umefika kwa kabila yake kusomesha watoto kwa ajili ya maendeleo kutokana dunia ya sasa inahitaji watalaam.

  Ulega amesema kuwa changamoto zilizo katika kata ya Bupu ni maji pamoja na miundombinu ya barabara hivyo vinatakiwa kupatiwa ufumbuzi ili wananchi waondokane na changamoto hizo.

  Mbunge huyo ameahidi kutoa Bati 50 katika shule mpya inayojengwa katika kitongoji cha kikonga kutokana watoto wa kitongoji hicho wanatembea kilomita sita. Ulega amesema changamoto zilizopo wilaya ya mkuranga zinatakiwa zitatuliwe kutokana na kuomba kazi ya kuwatumikia wananchi.

  Amesema kuwa suala mfuko wa afya ya jamii CHF dawa hazipatikani na kufanya wananchi wengine washindwe kujiunga. Aidha amesema wananchi waliojiunga na CHF ni 65 ikiwa nia serikali ni watu wote wajiunge ili wasipate adha ya kupata huduma za afya.

  Hata hivyo amesema nia ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli ni kuona wananchi wanafurahia huduma zinazotolewa na serikali na sio vinginevyo.

  0 0


  Afisa Mwandamizi kutoka Idara ya Kimataifa ya Mfuko wa misaada ya OPEC unaofadhili miradi mbalimbali chini Mfuko wa Tasaf nchini,Solomon Amieyeofori kutoka Vienna ,Austria(kushoto)akiwa na maafisa wa Mfuko wa Tasaf nchini kukagua miradi katika Jiji la Arusha.

  Ujumbe huo ukakagua ujenzi wa madarasa mawili katika Shule ya Msingi Azimio jijini Arusha.

  Mmoja wa wanakikundi cha Ushonaji eneo la Kambi ya Fisi Kata ya Ngarenaro,Bupe Anyingise ambaye ni miongoni mwa wanufaikaji wa kunusuru Kaya maskini akishona nyumbani kwake ,Tasaf imewanunulia Vyerehani,Meza na vifaa mbalimbali kuwawezesha kujipatia kipato vilivyogharimu zaidi ya sh 28 milioni.

  Afisa Mwandamizi kutoka Idara ya Kimataifa ya Mfuko wa misaada ya OPEC unaofadhili miradi mbalimbali chini Mfuko wa Tasaf nchini,Solomon Amieyeofori kutoka Vienna ,Austria( wa pili kushoto)akiwa na maafisa wa Mfuko wa Tasaf nchini kukagua miradi katika Jiji la Arusha katika Shule ya Msingi Azimio,Kata ya Elerai.


  Afisa Mwandamizi kutoka Idara ya Kimataifa ya Mfuko wa misaada ya OPEC unaofadhili miradi mbalimbali chini Mfuko wa Tasaf nchini,Solomon Amieyeofori kutoka Vienna ,Austria(katikati)akiwa na maafisa wa Mfuko wa Tasaf nchini kukagua miradi katika Jiji la Arusha,kulia ni Mratibu wa miradi ya Tasaf nchini,Mhandisi Elisifa Kinasha.Walikagua ujenzi wa mabweni ya wasichana katika Shule ya Sekondari Korona ili kuwapunguzia adha ya kutembea umbali mrefu kwaajili ya kupata elimu.  Maafisa wa Tasaf wakiwa katika picha ya pamoja na wanakikundi cha ushonaji katika picha ya pamoja.

older | 1 | .... | 993 | 994 | (Page 995) | 996 | 997 | .... | 1896 | newer