Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live

WIZARA IMARISHENI HOSPITALI YA MKOA WA DODOMA-MAJALIWA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoa maelekezo ya kuboresha usafi wa mazingira ya hospitali ya Mkoa wa Dodoma wakati alipoitembelea  hospitali hiyo Oktoba 1, 2016. Kulia kwake ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu kuboresha upatikanaji wa huduma katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Dodoma kwa kuhakikisha inakuwa na  dawa na vifaa tiba vya kutosha.

Ametoa agizo hilo jana (Jumamosi, Oktoba Mosi, 2016) wakati alipotembelea hospitali hiyo akiwa kwenye ziara ya kukagua maeneo ya kutolea huduma za jamii mjini Dodoma.
                                                               
Waziri Mkuu amesema wakati Serikali ikishirikiana na uongozi wa mkoa huo katika kumaliza changamoto zinazoikabili hospitali hiyo manispaa nazo zinajukumu la kuboresha utoaji wa huduma za afya katika zahanati na vituo vya afya.
 
“Waziri Afya atawajibika kuimarisha hospitali ya mkoa na Manispaa  waimarishe huduma katika zahanati zote na vituo vya afya ndani ya mkoa kwa kuziwezesha kuwa na majengo ya kutosha, kuongeza idadi ya watumishi na kuhakikisha zinakuwa na dawa na vifaa tiba,” alisema.

Aidha, Waziri Mkuu aliwataka watumishi wa hospitali hiyo kufanya kazi kwa uaminifu na uadilifu na isitokee watu wakakosa dawa au vipimo kwa sababu mmoja wao amechukua na kupeleka kwenye duka lake binafsi.

Pia Waziri Mkuu alimuagiza Mganga Mkuu wa Mkoa Dk. James Kiologwe kutafuta vijana watakaoweza kusafisha na kutengeneza bustani ya maua kwenye eneo lililoko karibu na uzio wa hospitali hiyo ili liwe na mandhari ya kuvutia.

Awali Mganga Mkuu wa mkoa, Dk. James Kiologwe aliiomba Serikali kupandisha hadhi hospitali hiyo na kuwa ya kanda kwa sababu mbali ya mkoa wa Dodoma, hospitali hiyo inahudumia wagonjwa wengine kutoka mikoa ya Iringa, Tabora, Singida na Manyara.

Akizungumzia upatikanaji wa tiba wakati Serikali imeanza kuhamia Dodoma, Dk. Kiologwe alisema mkoa huo unaweza kukabiliana na ongezeko la watumishi kwa una hospitali tano ambazo zina madaktari bingwa wa fani mbalimbali.

“Tunazo hospitali tano ambazo ni Benjamin Mkapa, Mirembe, DCMC, St. Gemma na hii ya ya Rufaa ya Mkoa zenye uwezo wa kutoa huduma za upasuaji, huduma kwa mama na mtoto, magonjwa ya moyo, mishipa, figo na saratani na huduma za mionzi,” alisema.

Katika hatua nyingine Dk. Kiologwe alisema hospitali hiyo imedumia wagonjwa wa nje 158,375 walipatiwa huduma katika hospitali hiyo katika kipindi cha Julai 2015 hadi Juni 2016 ambapo ni sawa na wastani wa wagonjwa 13,198 kwa mwezi.

“Magonjwa yanayoongoza kwa wagonjwa wa nje ni mivunjiko, shinikizo la damu, kisukari, homa ya mapafu na upungufu wa damu,” alisema.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
S. L. P. 980,
DODOMA.
JUMAPILI, OKTOBA 02, 2016



TIMU ZA SIMBA NA YANGA MARUFUKU UWANJA WA TAIFA-SERIKALI

$
0
0
 Waziri wa Habari Utamaduni sanaa na Michezo Mhe Nape Moses Nnauye akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uamuzi wa Serikali kuzuia timu za Simba na Yanga kutumia Uwanja wa Taifa kutoka na uharibifu wa miundombinu uliotokea katika mechi yao iliyofanyika Oktoba Mosi 2016.
Waziri wa Habari Utamaduni sanaa na Michezo Mhe Nape Moses Nnauye akiwa amekaa akiangalia jinsi viti vilivyong’olewa katika Uwanaja wa Taifa na Serikali   kuchukua uamuzi wa kuzuia timu za Simba na Yanga kutumia Uwanja wa Taifa na kuzuia mapato ya mechi waliyocheza mpaka watakapolipa fidia  kutoka na uharibifu wa miundombinu uliotokea katika mechi yao iliyofanyika Oktoba Mosi 2016.
Waziri wa Habari Utamaduni sanaa na Michezo Mhe Nape Moses Nnauye akitazama moja ya kiti kilichong’olewa jana katika mechi ya Simba na Yanga na Serikali kufikia  uamuzi wa kuzuia timu hizo kutumia Uwanja wa Taifa kutoka na uharibifu wa miundombinu uliotokea katika mechi yao iliyofanyika Oktoba Mosi 2016.
 Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw. Alex Nkenyenge akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tathimini iliyofanyika mara baada ya mechi wa jana kati ya Simba na Yanga na jumla ya mageti manne yamevunjwa na viti1781 vimeong’olewa katika Uwanja wa Taifa.
  Eneo liliong’olewa viti katika Uwanja wa Taifa katika mechi ya Simba na Yanga iliyofanyika Oktoba Mosi.Habari na Picha na Raymond Mushumbusi - MAELEZO


Timu za soka za Simba na Yanga za Jijini Dar es Salaam zimezuiwa kutumia Uwanja wa Taifa kwa muda usiojulikana kutoka na mashabiki wao kusababisha uharibifu wa miumbombimu ya Uwanja  wa Taifa yakiwemo mageti ya kuingilia Uwanjani na kung’oa viti kwa upande wa mashabiki wa Simba.

Uamuzi huo umetolewa leo Jijini Dar es Salaam  na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye alipokuwa akikagua na kutembelea maeneo yalioathirika na uharibifu uliofanywa na mashabiki wa Simba na Yanga katika mechi iliyochezwa Octoba Mosi 2016 katika Uwanja wa Taifa.
 
Mhe. Nape Nnauye ameongeza kuwa wameendaa mfumo wa kutumia kamera Uwanjani ili kubaini makosa yatakayokuwa yanafanyika ili kuzuia vitendo vya kihualifu na uharibifu katika Viwanja vya michezo.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw. Alex Nkenyenge amesema kuwa wamesikitishwa sana na uharibifu ulitokea katika mechi ya Simba na Yanga na kusababisha uharibifu wa viti na mageti ya kuingilia Uwanjani.

Ameongeza kuwa kwa tathimini iliyofanyika mageti manne yameng’olewa na mashabiki kwa upande wa Simba na Yanga na pia kwa upande wa ndani jumla ya viti 1781 vimeng’olewa katika upande wa mashabiki wa Simba.
“Mara nyingi tumekubaliana kutunza Uwanja huu kwa ajili ya matumizi ya watanzania wote na kama wasimamizi tunasikitika kwa kitendo hiki kilichotokea na tujue kuwa ni kodi za wananchi ndio zilitumika kujenga Uwanja huu na pia ndizo zitazotumika kukarabati Uwanja tuwe na tabia ya kupenda na kutunza vya kwetu.

Klabu za Simba na Yanga zimekuwa na ushindani mkubwa katika soka la Tanzania na kumekuwa kukitokea mambo mbalimbali pale timu hizo zinapokutana ikiwemo uharibifu wa miundombinu katika Viwanja na vurugu kwa mashabiki pale mmoja wao anapofungwa.

Taasisi zaendelea kutoa misaada Kagera.

$
0
0


Mkuu wa Wilaya Bukoba Deodatus Kinawiro akiwashukuru Taasisi ya Kimataifa ya Lions Club ya jijini Mwanza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Salum Kijuu na kusema kuwa mahitaji kwa waathirika wa tetemeko la ardhi bado ni makubwa na misaada inahitajika ili kuwasaida waathirika hao.
Mkuu wa Wilaya Bukoba Deodatus Kinawiro akiwashukuru Taasisi ya Kimataifa ya Lions Club ya jijini Mwanza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Salum Kijuu na kusema kuwa mahitaji kwa waathirika wa tetemeko la ardhi bado ni makubwa na misaada inahitajika ili kuwasaida waathirika hao.
Mratibu Mkuu wa Taasisi ya Kimataifa ya Lions Club ya jijini Mwanza Burhan Mohammed akitoa neno mwishoni mwa wiki mara baada ya ya kukabidhi msaada wa vyakula kuwasaidia wakazi wa mkoa wa Kagera ambao wameathiriwa na tetemeko la ardhi mapema mwezi Septemba mwaka huu.
Mkuu wa Wilaya Bukoba Deodatus Kinawiro (katikati aliyevaa suti) akiwa katika picha ya pamoja na wanachama wa Taasisi ya Kimataifa ya Lions Club ya jijini Mwanza mara baada ya kukabidhi msaada wa vyakula kuwasaidia wakazi wa mkoa wa Kagera ambao wameathiriwa na tetemeko la ardhi mapema mwezi Septemba mwaka huu. Picha na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Bukoba)



Na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Bukoba

Kamati ya maafa mkoani Kagera imeendelea kupokea misaada kutoka kwa wadau mbalimbali wa ndani na nje ya nchi kutoa michango yao kwa lengo la kusaidia waathirika wa tetemeko la ardhi lililoathiri mkoa wa Kagera.

Akikabidhi msaada uliotolewa na Taasisi ya Kimataifa ya Lions Club ya jijini Mwanza Mratibu Mkuu wa taasisi hiyo Bw. Burhan Mohammed amesema kuwa wao kama taasisi wamevutwa na kushikwa kwa moyo wa huruma na kuamua kuchukua hatua ya kuwasidia majirani zao wa mkoa wa Kagera.

Sisi sote ni Watanzania, tuliposikia wenzetu wamepatwa na matatizo, tumeamua kutoa mchango wetu kwa kushirikiana na wanachama wenzetu ili kutoa huduma za kuwapa chakula wenzetu wakati wa matatizo” alisema.

Taasisi hiyo imetoa Mchele, chumvi, mafuta ya kula, Sabuni pamoja na katoni za maji ya kunywa ambapo vyote kwa jumla vinathamani ya sh. milioni 22. Aidha, Kanisa la Anglikana Tanzania Dayosisi ya Lwelu ya mkoani Kagera wametoa vyakula vyenye thamani ya shilingi milioni 2.1 ikiwa ni pamoja na sukari, unga na mchele.

Wadau wengine waliotoa misaada ni kampuni ya Time to Help yenye makao makuu ya jijini Dar es salama ambayo inayomilikiwa Waturuki wametoa mablanket 500.

Akipokea misaada hiyo kwa niaba ya Mkuu Mkoa wa Kagera, Mkuu wa Wilaya Bukoba Deodatus Kinawiro amewaeleza wadau hao taswira mzima ya hali ya maafa katika mkoa Kagera ambapo amesema kuwa mahitaji kwa waathirika bado ni makubwa.

Kwa niaba ya Serikali, Mkuu wa Wilaya Bw. Kinawiro amewashukuru wadau wote wanaendelea kutoa misaada kwa lengo la kuwasaidia wananchi wa Kagera ambao wameathirika wa tetemeko hilo na kuwataka wadau wengine kuendelea michango ya hali na mali katika kukabiliana na hali ya maisha baada ya tetemeko kutokea.

KIBANDA CHA KUTOLEA HUDUMA NJE YA JENGO LA NSSF MJINI BUKOBA CHAONDOLEWA

$
0
0
Gari la kubebea mizigo mizito liking'oa kibanda cha kutolea huduma nje ya jengo la NSSF leo mjini Bukoba kutokana na jengo hilo kusitisha kutoa huduma baada ya kuharibiwa na tetemeko la ardhi Septemba 10 mwaka huu. 

ZIARA YA NAIBU WAZIRI TAMISEMI YAMUINGIZA KIKAANGONI MGANGA MKUU MANISPAA YA KIGOMA

$
0
0

Naibu Waziri wa Tamisemi, Selemani Jafo akikagua mradi wa Maji Katika wilaya ya Mbogwe mkoani Geita.

Naibu Waziri Selemani Jafo akikagua ujenzi wa Hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Mara mjini Musoma
Naibu Waziri wa Tamisemi Selemani Jafo akikagua kiwanda cha vijana cha kutengeneza Chaki mjini Maswa mkoani Simiyu.




Naibu Waziri Selemani Jafo akiwa na mtoto wa baba wa Taifa Madaraka Nyerere pamoja na Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara Edo Mapunda, nyumbani kwa Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere Butiama.

Naibu Waziri wa Tamisemi, Selemani Jafo akiwa na Mbunge wa Mbogwe Silivester Massele wakikagua jenereta la kusukuma maji Katika wilaya ya Mbogwe.

Naibu waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo amefanya ziara katika Mkoa wa Kigoma huku akimuagiza Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma kuunda timu ya uchunguzi juu ya malalamiko ya wananchi kuhusu tuhuma za wizi wa madawa na ujenzi wa wodi ya kina Mama ya Buhando na ujenzi ulio fanyika Katika zahanati zingine ndani ya Manispaa ya kigoma

Hatua hiyo ya Jafo ilitokana na kutoridhishwa na utendaji wa mkuu wa idara ya Afya ya Manispaa ya Kigoma, John Maganga kutokana na usimamizi mbovu wa miradi hiyo katika idara yake sambamba na kuwepo kwa malalamiko mengi ya ubadhilifu wa madawa ndani ya Manispaa hiyo.

Jafo alitembelea jengo la wazazi la Zahanati ya Buhanda ambapo hakuridhishwa kabisa na maelezo ya ubora wa jengo hilo na mganga mkuu huyo kushindwa kumpa Naibu Waziri maelezo ya kuridhishwa juu ya gharama za ujenzi wa jengo hilo ambalo limejengwa chini ya kiwango na kuwepo mashaka makubwa ya upotevu wa fedha nyingi katika ujenzi wa jengo hilo lililo zinduliwa kinyemela na DMO huyo.

Kutokana na simtofahamu hiyo Naibu Waziri amemtaka Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma kuunda timu ya uchunguzi na kwamba lengo la ziara hiyo ni kuleta ufanisi katika kuwahudumia wananchi ndani ya halmashauri mbalimbali hapa nchini.

Jafo katika Mikoa minne ya Mara, Simiyu, Geita na Kigoma ambapo alizifikia Halmashauri 19 na kuongea na watumishi zaidi ya 6000 pamoja na kukagua miradi mbalimbali 25 ya barabara, maji, afya, elimu na ujasiliamali imeleta tija sana kwa kuinua hamasa ya utendaji kazi kwa watumishi wa halmashauri za wilaya.

Ziara hiyo aliifanya baada ya kufunga Mkutano Mkuu wa 32 wa Jumuiya ya Taasisi za Serikali za Mitaa (ALAT) uliofungwa rasmi tarehe 24 September 2016 mjini Musoma Mkoani Mara. Ziara ya Naibu Waziri huyo ilianza tarehe 25 September hadi 30 September 2016 ambapo alikagua miradi na kuongea na watumishi.

Jambo kubwa lililo sisitizwa Katika ziara hiyo ni umuhimu wa watumishi wa halmashauri kufanya kazi kwa kuzingatia taaluma zao pamoja na kuweka maslahi ya Taifa mbele.Aliwataka wakurugenzi kuwekeana malengo ya utekelezaji na wakuu wao wa Idara, na wakuu wa idara kuwekeana malengo na watendaji wao wa chini wanao waongoza.

Kadhalika, Aliwataka watendaji wa halmashauri wabadilike katika utendaji wao. Amewataka wakuu wa idara kutowabagua baadhi ya watumishi katika idara zao.

MAJALIWA ATEMBELEA CHANZO CHA MAJI CHA MZAKWE DODOMA,ATAKA ORODHA YA WADAIWA SUGU DUWASA

$
0
0

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua mitambo ya maji ya DUWASA inayotoa maji yanayosambazwa katika Manispaa ya Dodoma wakati alipotembelea chanzo cha maji cha Mzakwe Dodoma Oktoba 2, 2016.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua mitambo ya maji ya DUWASA inayotoa maji yanayosambazwa katika Manispaa ya Dodoma wakati alipotembelea chanzo cha maji cha Mzakwe Dodoma Oktoba 2, 2016.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 


*Ni wa taasisi za umma, wanadaiwa sh. bilioni 1.4

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameagiza apatiwe orodha ya wadaiwa sugu wa taasisi zote za Serikali mkoani Dodoma ambao wamelimbikiza deni la sh. bilioni 1.4 zikiwa ni bili zao za maji.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumapili, Oktoba 2, 2016) wakati akizungumza na watumishi na viongozi wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dodoma (DUWASA) mara baada ya kukagua utendaji kazi wa chanzo cha maji cha Mzakwe nje kidogo ya mji wa Dodoma.

“Niletee haraka orodha ya wadaiwa wote wa Ofisi za Serikali na taasisi za umma ambao hawajalipa bili zao. Madeni yote ni lazima yalipwe,” amesema Waziri Mkuu.

Waziri Mkuu ambaye yuko katika ziara ya siku mbili ya kukagua maandalizi ya Serikali kuhamia Dodoma, anatembelea sehemu mbalimbali za kutolea huduma za jamii pamoja na kukagua miundombinu ya mkoa huo.

Aliutaka uongozi wa DUWASA na watumishi wote wahakakishe wanaboresha huduma za upatikanaji wa maji hasa kwenye maeneo yanayopimwa viwanja ili wananchi au wawekezaji wanaponunua viwanja wakute huduma hiyo ipo na waanze ujenzi mara moja.

“Tumealika wawekezaji, nataka wajenge viwanda na mahoteli hapa Dodoma, sasa wakikuta maji na umeme kwenye maeneo yao, itakuwa ni kichocheo cha kuharakisha kazi za ujenzi,” amesema.

Pia amemwagiza Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Bi. Christina Mndeme ahakikishe eneo lililo jirani na chanzo hicho cha maji halikaliwi na mtu yeyote na linalindwa dhidi ya uchomaji mioto.

“Uchomaji moto uoto wa asili umeharibu vyanzo vingi vya maji. Ni tatizo kubwa hapa nchini na halina budi kusimamiwa hadi liishe,” amesisistiza.

Amefikia uamuzi huo baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa DUWASA, Mhandisi David Pallangyo kwamba kuna wananchi wameanza kujenga na kufanya shughuli za kijamii jirani na chanzo hicho licha ya kuwa walikwishaondolewa zamani.

Kuhusu wadaiwa sugu, Mhandisi Pallangyo alisema mashirika ya umma na taasisi za Serikali ndiyo wanaongoza kwa kulimbikiza madeni. “Wananchi wa kawaida wapo wanaodaiwa lakini deni lao siyo kubwa na hao tunawamudu,” alisema wakati akizungumza na mwandishi wa habari hizi.

Alisema changamoto nyingine inayowakabili ni uchomaji moto ambapo hivi karibuni uliwashwa moto na kuunguza baadhi ya nguzo za umeme ambazo zinapeleka umeme kwenye chanzo hicho.

Alisema askari wa JKT Makutupora walisaidia kuzima moto huo ili usifike kwenye mitambo mingine ya chanzo hicho cha maji.

Waziri Mkuu pia alikagua maabara ya upimaji maji kwenye chanzo hicho kabla hayajasambazwa kwa wateja na mara yanapokuwa yamefika kwa wateja na kuelezwa kuwa maji hayo yanakidhi viwango vya kitaifa na vya kimataifa vilivyowekwa na Shirika la Afya Duniani (WHO).

Waziri Mkuu anaendelea na ziara yake kwa kutembelea kiwanda cha magodoro Dodoma na kituo cha kuzalisha umeme cha Zuzu.

(mwisho)

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
S. L. P. 980,
DODOMA.
JUMAPILI, OKTOBA 2, 2016

ACT YAZINDUA HARAMBEE YA UJENZI WA KANISA JIJINI DAR

$
0
0
Kanisa la All- Nations Christian Tabernacle (ACT) linaloendesha shughuli zake katika ukumbi wa Utoji, Sinza Mapambano jijini Dar limezindua harambee ya kuchangia ujenzi wa kanisa hilo rasmi .

Akizungumza katika misa iliyofanyika eneo hilo, mchungaji wa kanisa hilo Pastor Sos Mabele alisema kuwa harambee hiyo imezinduliwa kanisani hapo kwa waumini na watu mbalimbali kuweka ahadi au kuchangia moja kwa moja fedha kwa ajili ya ujenzi wa kanisa unaotarajiwa kuanza mwisho wa mwaka huu. 

Mbali na hayo Mchungaji huyo aliwataka watu mbalimbali wajitokeze kuchangia  ujenzi wa kanisa hilo bila kujali madhehebu au dini, kwa kuwa Mungu ni wa wote  ambapo pia alisema kuwa zoezi la harambee  litaisha tarehe 25 mwezi huu kwa walioahidi wote kutimiza ahadi zao.

“Sisi kanisa letu kama linavyosema kuwa ni All- Nations Christian Tabernacle yaani hekalu la makanisa ya mataifa yote, hivyo hatubagui mtu kwa dhehebu wala dini na wote wanakaribishwa kila jumapili kwenye ibada zetu,” alisema Pastor Sos na kuwataka watu waendelee kuwasiliana naye kwa ahadi na michango kupitia namba 0784935855.

Naye mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa Kanisa hilo, bwana Ibrahimu Chanikicha, aliwashukuru wote wanaoendelea kuchangia kwa hali na mali na kuwaomba waendelee kuwa na moyo huohuyo.

Mchungaji wa Kanisa la All- Nations Christian Tabernacle (ACT) Sos Mabele akisali wakati akifungua Ibada hiyo iliyokuwa ni ya ufunguzi wa Harambee ya uchangiaji wa ujenzi wa Kanisa
 Mmoja ya waumini akisoma neno la Mungu wakati Mchungaji akiwaongoza
 Waumini wakimsikiliza kwa makini Baba Mchungaji akifundisha neno
Katibu wa kamati ya ujenzi Debora Simon (wa kwanza Kulia) pamoja na waumini mwengine wakifuatilia neno
 Mchungaji wa Kanisa la All- Nations Christian Tabernacle (ACT) Sos Mabele akiendelea kutoa mahubiri wakati wa Ibada hiyo ya uzinduzi wa Harambee ya uchangiaji kwa ajili ya ujenzi wa Kanisa
 Mweka Hazina wa Kanisa hilo Bwana Geofrey Raymond akifuatilia Ibada kwa makini
 Waumini wakiendelea kufuatilia Ibada kwa makini
 Mmoja wa watoto akisoma Neno la Mungu wakati wa Ibada hiyo ya Uchangiaji kwa ajili ya Ujenzi wa Kanisa
 Wakijiandaa Kumtukuza Mungu
 Baadhi ya watoto wakiwa Ibadani
 Mchungaji wa Kanisa la All- Nations Christian Tabernacle (ACT) Sos Mabele akiimba nyimbo za Sifa
 Mweka Hazina wa Kanisa hilo Bwana Geofrey Raymond akizungumza neno wakati wa Ibada hiyo
Ibrahim Chanikicha Mwenyekiti wa kamati ya Ujenzi akizungumza jambo 
 Waimbaji wakiendelea kumtukuza Mungu  kwa njia ya Nyimbo za Sifa
 Waumini wakiimba nyimbo za Sifa
 Muda wa Maombezi ulifika ambapo Mchungaji wa Kanisa la All- Nations Christian Tabernacle (ACT) Sos Mabele aliwaombea watumishi mbali mbali
 Wakiendelea kusifu na Kuabudu
Picha zote na Fredy Njeje

MAKAMU WA RAIS WA CUBA AWASILI NCHINI KWA ZIARA YA SIKU TATU

$
0
0


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzanai Mhe.Samia Suluhu Hassan (kulia), akiwa na mgeni wake Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Cuba Salvador Antonio Valdes Mesa alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere leo kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku tatu hapa Nchini.Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Cuba Salvador Antonio Valdes Mesa akiangalia ngoma za asili mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Saalaam ambapo atakuwa na ziara ya kikazi ya siku tatu hapa nchini.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Cuba Salvador Antonio Valdes Mesa akiangalia moja ya kikundi kilichokuwa kinatumbuiza kwa matarumbeta mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Saalaam ambapo atakuwa na ziara ya kikazi ya siku tatu hapa nchini.

....................................................................

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Cuba Salvador Antonio Valdes Mesa amewasili jioni hii katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na kupokelewa na Mwenyeji wake Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Cuba Salvador Antonio Valdes Mesa atafanya ziara ya kikazi ya siku Tatu hapa nchini na lengo la ziara hiyo ni kuendeleza na kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Cuba katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu,afya, utamaduni,michezo,kilimo, nishati, teknolojia na kuangalia maeneo mapya ya uwekezaji.

Tarehe 3/09/2016 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Cuba atakutana na kufanya mazungumzo ya faragha na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli ikulu jijini Dar es salaam.

Makamu wa Rais huyo wa Jamhuri ya Cuba Salvador Antonio Valdes Mesa pia atakutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ikulu na baada ya mazungumzo hayo ya faradha viongozi hao watafanya mkutano na waandishi wa habari kuzungumzia masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya nchi hizo MBILI.

Nchi nyingine ambazo Makamu wa Rais huyo wa Jamhuri ya Cuba anazitembelea ni Uganda, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo- DRC-,Botwana na Zimbabwe.


BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

MAKONDA AUNGURUMA LEO BUGURUNI KWA MNYAMANI, AWATAKA WANANCHI KUSHIRIKI KATIKA KUTATUA KERO

$
0
0
 Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo jioni katika eneo la Buguruni kwa Mnyamani, ili kuzungumzia kero na changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi. 
     Katika Mkutano huo Makonda amewataka wananchi kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha wanashiriki katika kupunguza au kuondoa kabisa changamoto zinazowakabili ikiwemo, vibaka, dadapoa na uchafu wa mazingira, akisema, ikiwa wananchi watashitiki kikamilifu ni rahisi kukomesha tatizo la vibaka kwa sababu vibaka na dadapoa wanatoka miongoni mwa familia zao na hali kadhalika uchafu wa mazingira unatokana na takataka wanazozalisha wananchi wenyewe.
 Wananchi wakimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, PaulMakonda wakati akiwahutubia leo jioni katika neo la Buguruni kwa Mnayamani
 Viongozi waandamizi katika Wilaya ya Ilala, wakimsikiliza mkuu wa mkoa Paul Makonda wakati akihutubia wananchi katika eneo la Buguruni kwa Mnayamani leo jioni. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Msongela Palela, Ofisa Tawala wa Manispaa hiyo, Edward Mpogolo, Naibu Meya Manispaa hiyo, Omary Kumbilamoto na Mbunge wa Segerea wilayani humo Bona Kalua
 Mjumbe wa Shina namba tano, Katika Kata ya Myamani, Buguruni Zubeda Lugiga, akieleza kero zinazowakabili wakazi wa kata hiyo, mbele ya Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alipowahutubia katika mkutano wa hadhara leo jioni
 Mkazi wa Buguruni, Sadik Mgaya akieleza changamoto na kero zinazowakabili wananchi wa eneo hilo wakati wa mkutano huo wa Makonda
 Mkazi wa Buguruni kwa Mnyamani, Samweli Ndyanabo, akieleza kero zinazowakabili wakazi wa kata hiyo, mbele ya Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alipowahutubia katika mkutano wa hadhara leo jioni 
 Kamanda wa Polisi Kanda Malum ya Dar es Salaam, Simon Sillo akijibu hoja, kero na changamoto mbalimbali walizouliza wananchi, katika mkutano wa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kushoto), uliofayika leo jioni Buguruni kwa Mnyamani
Kamanda wa Polisi Kanda Malum ya Dar es Salaam, Simon Sillo akijibu hoja, kero na changamoto mbalimbali walizouliza wananchi, katika mkutano wa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, uliofayika leo jioni Buguruni kwa Mnyamani 
 Wananchi wakishangilia wakati hoja zao zikijibiwa na Kamanda Sillo
 Wananchi wakishangilia wakati hoja zao zikijibiwa na Kamanda Sillo 
 Ofisa tawala wa Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam, Edward Mpogolo, akimsikiliza kwa karibu Mkuu wa Wilaya hiyo, Sophia Mjema, aliyekuwa akielezea jambo,wakati wa mkutano wa hadhara wa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam uliofanyika leo Buguruni kwa Mnyamani Dar es Salaam. Katikati ni Mbunge wa Segerea Bona Kalua 
 Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto akitoa maelezo yake kuhusu maswali waliyouliza wananchi, wakati wa mkutano wa Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, paul Makonda uliofanyika leo jioni. Naibu Meya huyo alizungumzia zaidi mradi wa Uwekezaji ulitaka kufanywa na kampuni ya PMM katika eneo la mitaa ya Mnyamani na Kifaru, Buguruni, lakini mradi huo umesimama. 
 Mbunge wa Ilala Mussa Azan Zungu akizungumza wakati wa mkutano huo
 Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akipongezana na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sillo mwishoni mwa mkutano huo uliofanyika leo katika eneo la Buguruni kwa Mnyamani.
 Ofisa Tawala wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Msongela Palela wakifurahia jambo mwishoni mwa mkutano huo 
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema akifunga mkutano huo
 Mkuu wa wilaya ya Ilala, Sophia Mjema, akimshukuru Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, kwa kuendesha vizuri mkutano huo
 Ofisa Tawala wa Wilaya ya Ilala, Edwars Mpogolo akimpongeza Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwa mkutano kwenda vizuri
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akifurahiwa na Wananchi wakati akiondoka baada ya mkutano wake wa hadhara aliofanya katika eneo la Buguruni kwa Mnayamani, leo jioni. Picha zote na Bashir Nkoromo-wa theNkoromo Blog

MKUU WA MKOA WA MWANZA ATAKA MAHAKAMA KUREJESHA IMANI KWA WANANCHI.

$
0
0
Na George Binagi-GB Pazzo @BMG

Watendaji wa Mahakama nchini wamehimizwa kufanya kazi kwa uwazi na uadilifu, ili kurejesha imani kwa wananchi juu ya chombo hicho muhimu katika utoaji wa maamuzi.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, alitoa kauli hiyo jana kwenye Mkutano wa robo mwaka wa Chama cha Majaji na Mahakimu JMAT, tawi la Mwanza na Geita uliofanyika Jijini Mwanza.

Mongella alisema watendaji wa mahakama wakiwemo Majaji na Mahakimu wanapaswa kutenda haki katika shughuli zao na kuhakikisha mchango wa mahakama katika utoaji wa haki unaonekana kwa wananchi.

Mwenyekiti wa Chama cha Majaji na Mahakimu tawi la Mwanza, Francis Kishenyi, ambaye pia ni Hakimu Mkazi Mfawidhi Wilaya ya Ukerewe, alisema miongoni mwa malengo ya chama hicho ni kuhakikisha watumishi wa mahakama wakiwemo Majaji na Mahakimu wanafanya kazi kwa kuzingatia maadili ya mahakama.

Pamoja na mambo mengine, mkutano huo umejadili masuala mbalimbali ikiwemo maadili ya viongozi wa Umma katika kuwatumikia wananchi.


Bonyeza HAPA Kutazama Picha

KAULI YA WAZIRI NAPE NNAUYE KUHUSU KUVUNJWA KWA VITI UWANJA WA TAIFA-DAR ES SALAAM

RC ARUSHA AKERWA NA HALI DUNI YA NGORONGORO,AKUTANA NA WADAU WA TAASISI ZISIZO ZA KISERIKALI ZINAZOENDESHA SHUGHULI WILAYANI HUMO.

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo akifuatilia na kunakili hoja mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa na wadau wa taasisi zisizo za Kiserikali zinazofanya shughuli zake katika Wilaya ya Ngorongoro wakati wa Kikao kilichofanyika katika Ofisi yake.
Mkurugenzi wa Taasisi ya PWC Bi. Manda Ngoitiko(aliyesimama) akiwasilisha taarifa ya NGO anayoiongoza wakati wa kikao maalum na Mkuu wa Mkoa pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama.
Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Arusha wakifuatilia kikao wakati wa uwasilishaji wa taarifa za Taasisi na Kampuni zisizo za Kiserikali zinazofanya kazi katika Wilaya ya Ngorongoro
Wadau toka kwenye Kampuni na Taasisi mbalimbali kutoka Ngorongoro walioshiriki katika Kikao maalumu kilichoitihswa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo(kulia) akiwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Ndg. Richard Kwitega wakati wa Kikao na NGO’S NA Kampuni zinazoendehsa shughuli zake katika Wilaya ya Ngorongoro.
Mkurugenzi wa taasisi ya PWC Bi. Manda Ngoitiko (kushoto) pamoja na Manger wa Kampuni ya Thompson Safaris (kulia) kila mmoja akielezea namna ambavyo mgogoro wa ardhi uliopo unavyoathiri shughuli zao za kila siku.

………………………………………………………….

Nteghenjwa Hosseah – Arusha=

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Mashaka Gambo mwishoni mwa wiki hii amekutana na wadau wa taasisi zisizo za Kiserikali pamoja na makampuni yanayoendesha shughuli zao katika Wilaya ya Ngorongoro lengo ikiwa ni kusikia namna wadau hao wa maendeleo wanavyoendesha shughuli zao halkadhalika Wilaya hiyo inavyonufaika na uwepo wa wadau hao katika maeneo hayo.

Akizungumza wakati wa kufungua Kikao hicho Rc Gambo alisema malego ya Kikao hiki yanaendana sambamba na maandalizi ya Safari yake ya kikazi ya siku tano katika Wilaya ya Ngorongoro itakayoanza tarehe 03-08/10/2016 hivyo angependa kufahamu kwa upana namna ambavyo wadau hawa wanachangia katika kuleta maendeleo ya Wilaya hii ambayo kwa kipindi kirefu imekua nyumba kimaendeleo.

Alisema sielewi kwa nini kwa miaka yote hii Wilaya ya Ngorongoro haina hata kilomita moja ya barabara ya Lami, Stendi ya Kisasa wala masoko yenye hadhi ya kuwahudumia wageni ambao wengi wao ni watalaii wakati kuna taasisi za Kiserikali na siziso za Kiserikali ambazo zina uwezo wa kutosha kuboresha huduma hizi kwa manufaa ya wananchi na wageni wanaotembelea eneo hilo.

Wananchi wa Ngorongoro wamekua na maisha duni na matatizo yasiyoisha, hakika sasa umefika wakati wa kufahamu kazi zinazotekelezwa na kila mdau na tufahamu kwanini uwepo wao hauchangii kulete mabadiliko chanya katika Wilaya hii, huenda mipango kazi yao iko tofauti na malengo na matarajio yetu hivyo tusije tukawalaumu kumbe ni kutofahamu namna ambavyo taasisi zenu zinafanya kazi aliongeza.

“Katika Wilaya hii ukizungumzia Taasisi kubwa za Serikali kuna Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro, Baraza la wafugaji pamoja na Halmashauri ambao wanapata Fedha nyingi kwa ajili ya kuleta maendeleo lakin bado kasi ya maendeleo kwa kweli hairidhishi kabisa, ni vyema basi kwa pamoja tutafute majawabu ya matatizo yanayoikabili Ngorongoro”, alisema Gambo.

Baada ya Taasisi zote kuwasilisha taarifa zao iligundulika kwamba kuna mgogoro wa Ardhi ambao sasa umekua wa muda mrefu kati ya Vijiji vya Sukenya, Soitsambu, Mondorosi na Muwekezaji wa Kampuni ya Thompson.

Rc Gambo alisema ni wakati sasa wa kuketi meza moja na makundi yote kuona namna ambavyo tunaweza kutatua mgogoro huu ili wananchi waweze kuendelea na shughuli zao na Muwekezaji afanye kazi zake kwa amani katika eneo hilo na kupitia kikao hiki nimepata kufahamu vitu vingi ambavyo ntakuja kuvifanyia kazi wakati wa Ziara yangu.

Ziara hii ya Kikazi Wilayani Ngorongoro itakua ya pili tangu Mhe. Gambo alipochaguliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha mapema mwezi Agosti 2016.

Rais Magufuli ateua Mwenyekiti wa Bodi wa NIC

MAJALIWA ATEMBELEA KITUO CHA UMEME CHA TANESCO DODOMA

$
0
0

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea taarifa kutoka kwa Meneja wa TANESCO wa Mkoa wa Dodoma, Mhandisi Zakayo Temu (kushoto) kuhusu hali ya upatikanaji wa umeme kwenye makao makuu ya nchi Dodoma wakati alipotembelea Kituo cha Umeme cha TANESCO cha Dodoma Oktoba 2, 2016. Wengine Pichani kutoka kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama, Mkuu wa mkoa wa Dodoma Jordan Rugimbana na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma , Christina Mndeme.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa TANESCO wa mkoa wa Dodoma, Mhandisi Zakayo Temu (katikati) wakati alipotembelea Kituo cha Umeme cha TANESCO cha Dodoma Oktoba 2, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA ATEMBELEA KIWANDA CHA GYPSUM DODOMA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wafanayakazi na viongozi wa kiwanda cha Gypsum cha Premalt cha Dodoma wakti alipokitembelea mjini Dodoma Oktoba 2, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
gyp2
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akikagua  uzalishaji katika kiwanda  cha Gypsum cha Premalt cha mjini Dodoma wakati alipokitembelea Oktoba 2, 2016. (Picha na ofisi ya Wairi Mkuu)

INTRODUCING Lady Jaydee - Sawa Na Wao (Official Music Video)

KATIBU MKUU WA CCM ABDULRAHMAN KINANA AKUTANA NA MAKAMU WA RAIS WA CUBA, LEO JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisalimiana na Makamu wa Rais wa Cuba,Salvador Valdes Mesa kabla ya kuanza mazungumzo yao leo katika hotel ya Hyatt, Kilimajaro Kempiski jijini Dar es Salaam, leo.Kulia ni Msemaji wa CCM Christopher Ole SendekaKatibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwa katika mazungumzo na Makamu wa Rais wa Cuba, Salvador Valdes Mesa , leo jijini Dar es Salaam. Picha zote na Bashir Nkoromo

Tshs. Bilioni 374.5 zatolewa kwa ajili mikopo ya nyumba nchini

$
0
0
Na Jonas Kamaleki, MAELEZO

Shilingi bilioni 374.5 zimetolewa kwa ajili ya mikopo ya nyumba hapa nchini ili kuwawezesha wanachi kuwa na makazi bora ambayo ni haki ya msingi ya kila mwanadamu.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Makazi Duniani.

“Ili kukidhi mahitaji ya nyumba yanayotokana na ongezeko kubwa la watu, Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imeshiriki katika utoaji wa mikopo ya nyumba ambapo soko la mitaji na mikopo ya nyumba nchini limeongezeka na kufikia asilimia 6.7 kwa mwaka jana,”alisema Lukuvi.

Kwa mujibu wa Waziri Lukuvi, taarifa za Benki Kuu zinaonyesha kuwa idadi ya benki zinazotoa mikopo ya nyumba zimeongezeka kutoka tano kwa mwaka 2010 hadi kufikia 26 Desemba 2015.

Aidha. Lukuvi amesema kuwa utoaji wa mikopo ya muda mrefu ya nyumba umewezesha sekta binafsi na waendelezaji milki kuingia katika biashara ya kujenga na kuuza nyumba za biashara na makazi kwa kuwauzia wananchi kwa mkopo wa muda mrefu.

Aliongeza kuwa ili kuwezesha sekta ya nyumba kuendelea kufanya vizuri, Serikali inafanya mapitio ya sera mbalimbali zinazohusiana na masuala ya nyumba, zikiwemo Sera ya Ardhi ya mwaka 1995 na Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Makazi ya mwaka 2000. Lengo la mapitio hayo ni kuweka mfumo wezeshi ambao utarahisisha uendelezaji wa sekta hiyo.

Serikali kupitia Wakala wa Taifa wa Utafiti wa Nyumba Bora na Vifaa vya Ujenzi (NHBRA) imesaidia kukuza tekinolojia asilia ya vifaa vya ujenzi, kuhamasisha na kusambaza matokeo ya utafiti na utaalam wa ujenzi wa nyumba bora kwa gharama nafuu, alisema Lukuvi.

Lukuvi amebainisha kuwa katika mwaka wa fedha ulioisha, Wakala ulitengeneza mashine 80 za kufyatulia tofali za kufungamana ambapo kati ya hizo, mashine 46 ziliuzwa kwa vikundi 12 vya ujenzi. Wakala pia ulitoa mafunzo ya ujenzi wa nyumba za gharama nafuu kwa vikundi 110 katika wilaya za Kahama, Morogoro na Kinondoni.

Waziri Lukuvi amesema kuwa Shirika la Nyumba limeendela kutekelza miradi yake 64 yenye jumla ya nyumba 4,990. Miradi hii imeliwezesha Shirika kufikia mikoa 24 kwa kujenga nyumba za makazi ya gharama nafuu 1,841, gharama ya kati 2,823 na nyumba za biashara 326.

“Wizara yangu imekuwa ikishirikiana na Mamlaka za Upangaji Miji katika uandaaji wa Mipango Kabambe ya miji, Manispaa na Majiji, hadi kufikia Septemba 30, 2016 Rasimu za Mipango hiyo kwa Jiji la Mwanza, Manispaa za Mtwara, Iringa,Tabora, na Musoma pamoja na Mji wa Kibaha zilikuwa zimekamilika na kutangazwa kwenye gazeti la Habari Leo ili kuwawezesha wadau wa maendeleo kupitia rasimu na kutoa maoni yao,”alisema Lukuvi.

Waziri Lukuvi amesema pia kuwa zoezi la urasimishaji makazi katika jiji la Dar es Salaam unaendelea katika maeneo ya Kimara, Chasimba na Makongo Juu. Hadi kufikia Septemba 2016 viwanja 4,818 vilitambuliwa ambapo kati ya hivyo. Viwanja 4,665 vimepimwa na maandalizi ya umilikishaji yanaendelea.

Siku ya Makazi Duniani huadhimishwa Jumatatu ya kwanza ya Oktoba kila mwaka ikiwa ni utekelezaji wa Azimio Na 40/202 lililopitishwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mwezi Desemba 1985. Kwa mwaka huu Maadhimisho haya yana kaulimbiu isemayo Nyumba Kitovu cha Miji (Housing at the Centre).

TASAF yakutana na Wadau wa Maendeleo

$
0
0
Wadau wa Maendeleo wanaoshirikiana na Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF kutekeleza Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini –PSSN- wameanza mkutano jijini Dar es salaam kupitia mafanikio ya utekelezaji wa Mpango huo.

Akifungua Mkutano huo wa siku moja, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Bwana Peter Ilomo amesema Serikali inathamini na kutambua mchango wa wadau hao wa maendeleo katika kusaidia jitihada za kutokomeza umaskini miongoni mwa wananchi.

Bwana Ilomo amesema utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kupitia TASAF umekuwa wa mafanikio ya kuridhisha ambapo Zaidi ya kaya maskini Milioni Moja zimetambuliwa na kuorodheshwa kwenye Mpango huo nchini kote.

Aidha Katibu Mkuu huyo wa Ofisi ya Rais amebainisha kuwa kwa kutambua umuhimu wa Mpango huo serikali itaendelea kufuatilia kwa karibu utekelezaji wake ili malengo yake yaweze kupatikana kwa haraka na kuwanufaisha walengwa na taifa kwa ujumla.

Hata hivyo Bwana Ilomo amezungumzia hatua zilizoanza kuchukuliwa dhidi ya watu waliopenyezwa kwenye Mpango bila kufuata taratibu ikiwa ni pamoja na kuziondoa takribani kaya 30,000 zilizokuwa zimeandikishwa kinyume cha kanuni za Mpango.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bwana Ladislaus Mwamanga amesema Mfuko huo umefanikiwa kulipa walengwa wa Mpango kwa awamu 17 nchini kote ambako katika maeneo mengi ya Mpango tayari mafanikio yameanza kuonekana ikiwemo walengwa kuboresha maisha,kusomesha watoto na hata kuanzisha miradi midogo midogo ya kiuchumi kwa lengo la kujiongezea kipato.

Wadau hao wa Maendeleo kesho watapata fursa ya kutembelea maeneo mbalimbali nchini na kukutana na walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini ili kuona namna wanavyonufaika na ruzuku itolewayo na Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF. 

Zifuatazo ni picha za tukio la ufunguzi wa mkutano wa TASAF na wadau wa Maendeleo uliofunguliwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Bwana Peter Ilomo jijini Dar es salaam.
  Katibu Mkuu ofisi ya Rais Bwana Peter Ilomo akifungua mkutano wa wadau wa maendeleo ulioandaliwa na TASAF. 

    Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Bwana Peter Ilomo akizungumza na wadau wa Maendeleo Ikulu jijini Dar es salaam.
  Baadhi ya wadau wa maendeleo na watendaji wa TASAF wakisikiliza hotuba ya ufunguzi wa Mkutano wa wadau awa maendeleo jijini Dar es salaam iliyotolewa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Bwana Peter Ilomo( hayupo pichani). 
 Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bwana Ladislaus Mwamanga akitoa maelezo kwenye mkutano wa wadau wa maendeleo jijiji Dar es salaam . 
 Wadau wa maendeleo wakiwa katika picha ya pamoja na katibu mkuu Ofisi ya Rais Bwana Peter Ilomo baada ya ufunguzi wa Mkutano wenye lengo la kutathmini utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya maskini .
 Wadau wa maendeleo wakiwa katika picha ya pamoja na katibu mkuu Ofisi ya Rais Bwana Peter Ilomo baada ya ufunguzi wa Mkutano wenye lengo la kutathmini utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya maskini .

Naibu Waziri wa Afya Dk. Kigwangalla afanya ziara katika Hospitali za Wilaya ya Iramba Mkoani Singida

$
0
0
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla amefanya ziara ya kikazi katika Wilaya Iramba Mkoani Singida na kukagua huduma za Afya katika Hospitali ya Wilaya pamoja na Zahanati ya Kisimba ndani ya Wilaya hiyo.

Katika ziara hiyo, Dk. Kigwangalla ameweza kubaini mapungufu mbalimbali ambayo ameagiza yapatiwe ufumbuzi ndani ya miezi mitatu.

Akiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Iramba, ameweza kujionea huduma mbalimbali zitolewazo Hospitalini hapo hata hivyo ameagiza uongozi wa Hospitali hiyo kuhakikisha wanafunga mfumo wa ukusanyaji mapato wa malipo wa kisasa kwa njia ya kielektroniki.

“Mfumo wa malipo ya kielektroniki umeleta ukombozi mkubwa sana kwenye mahospitali nchini. Mapato yameongezeka. Udhibiti wa mapato umekuwa rahisi. Nawaagiza nanyi Hospitali ya Iramba kuhakikisha munafunga mfumo huu wa malipo wa kisasa hususani kwenye: Maabara,Chumba cha upasuaji (Theatre), Dirisha la dawa, na sehemu zote zenye kuingiza mapato”. Ameeleza Dk.Kigwangalla wakati wa kutoa maagizo hayo.

Katika Zahanati ya Kisimba ambayo ipo umbali wa zaidi ya Kilometa 10, Dk.Kigwangalla ameweza kujionea huduma mbalimbali kwenye Zahanati hiyo ambayo ni mpya huku ikiwa msaada mkubwa kwa wananchi wa vijiji hivyo. Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akisiliza maelekezo kutoka kwa Mganga Mkuu wa Hospitali ya Iramba, Mkoani Singida wakati alipotembelea chumba cha upasuaji Hospitali hapo.Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua vifaa vya Maabara .Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akipata maelezo kutoka kwa Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Iramba namna wanavyokusanya mapato.



Jengo la Utawala la Hospitali ya wilaya ya Iramba na juu ni baadhi ya majengo ya Hospitali hiyo.Picha chini ni Majengo ya Zahanati mpya ya Kisimba iliyopo Wilayani Iramba.Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akisaini kitabu cha wageni kwenye Zahanati hiyo KisimbaJengo la Zahanati ya KisimbaNaibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akisalimia wenyeji (Hawapo pichani) wakati alipotembelea Zahanati hiyo ya KisimbaNaibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na watumishi wa Zahanati hiyo ya Kisimba.Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua chumba cha dawa kwenye Zahanati hiyo.
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live




Latest Images