Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 991 | 992 | (Page 993) | 994 | 995 | .... | 1898 | newer

  0 0
  Mkurugenzi wa Ajira, Ally Msacky akisoma hotuba ya Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde alipoenda kumuwakilisha katika mahafali ya mwisho ya vijana waliopo chini ya mradi wa Uwezeshaji Vijana Kiuchumi – Dar es Salaaam (DYEE) waliohitimu katika Chuo cha Mafunzo ya Ufundi cha Future World, kushoto ni Muwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa Plan International – Tanzania, Bi. Gwynneth Wong na kulia ni Mkuu wa Chuo hicho, Robert Mkolla. Mradi huo umefadhiliwa na Benki ya NBC na kuratibiwa na Shirika la Plan International.   Mmoja wa vijana waliopo chini ya mradi wa Uwezeshaji Vijana Kiuchumi – Dar es Salaaam (DYEE) waliohitimu katika Chuo cha Mafunzo ya Ufundi cha Future World, Hamis Abdallah akimuonyesha Mkurugenzi wa Ajira - Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Ally Msacky jinsi ya kuchanganya vinywaji na kupata kinywaji kimoja (cocktail) katika siku ya mahafali yao. Mradi huo umefadhiliwa na Benki ya NBC na kuratibiwa na Shirika la Plan International.


   Mkurugenzi wa Ajira - Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Ally Msacky akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya vijana waliohitimu mafunzo ya ufundi katika Chuo cha Future World chini ya mradi wa Uwezeshaji Vijana Kiuchumi – Dar es Salaaam (DYEE). Mradi huo umefadhiliwa na Benki ya NBC na kuratibiwa na Shirika la Plan International.
  Na Jacquiline Mrisho - MAELEZO

  Serikali ya awamu ya tano imejipanga kukuza ujuzi wa nguvu kazi kwa vijana takribani 15,000 kwa mwaka wa fedha 2016/2017 ili kuwaongezea uzoefu wa kazi na kuongeza fursa za upatikanaji wa ajira.

  Ujuzi wa nguvu kazi nchini utatolewa kupitia programu maalum ya mafunzo kazini kwa njia ya Uanagenzi (Apprenticeship), mafunzo kwa vitendo  kwa wahitimu (Internships) pamoja na urasimishaji  wa ujuzi uliopatikana kwa mfumo usio rasmi (Recognition of Prior Learning).

  Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Ajira, Ally Msacky alipokuwa akimuwakilisha Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde wakati wa mahafali ya mwisho ya vijana waishio katika mazingira magumu waliohitimu katika Chuo cha Mafunzo ya Ufundi cha Future World.

  Mhe. Mavunde amesema kuwa maendeleo ya nchi yoyote yanategemea nguvu kazi ambayo kwa asilimia kubwa inatoka kwa vijana kwahiyo ni wajibu wa kila mmoja kuhakikisha vijana wanapatiwa elimu na mafunzo ili waweze kujiajiri au kuajiriwa na hatimaye kupunguza utegemezi na kuongeza pato la Taifa.

  “Napenda nitumie fursa hii kuwataarifu kuwa Serikali yetu imetoa kipaumbele cha juu katika kujenga ujuzi wa nguvu kazi, takribani vijana 15,000 watafaidika na programu hiyo kwa mwaka huu wa fedha kwani tayari tumeanza kutekeleza kwa kuingia mikataba na Makampuni ya kutoa mafunzo kwa vitendo katika maeneo ya kazi”, alisema Mhe. Mavunde.

  Ameongeza kuwa Serikali itaendelea kusimamia Sera ya Taifa ya Ajira na Sera ya Elimu ya Mafunzo ya Ufundi Stadi kwa lengo la kuweka msisitizo katika kuweka mazingira na kutoa elimu ya ufundi stadi kwa ngazi mbalimbali ili kuendana na mahitaji ya soko la ajira na hatimaye kuongeza fursa za ajira nchini.

  Aidha Mhe. Mavunde amehaidi kuendelea kushirikiana na Taasisi mbalimbali za ndani na nje ya nchi ili kuhakikisha kuwa ukuzaji wa ajira kwa vijana unapewa kipaumbele pia ameahidi kusaidia kuimarisha utekelezaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Vijana ambao unawasaidia vijana kupata mikopo kwa masharti nafuu.

  Mradi huu wa Uwezeshaji Vijana Kiuchumi - Dar es Salaam (DYEE) kupitia mafunzo ya stadi za kujiajiri (BEST Model) unafadhiliwa na Benki ya NBC na kuratibiwa na Shirika la Plan International, umetekelezwa katika kipindi cha miaka 3 na umetoa mafunzo kwa jumla ya vijana 1,225.

  0 0
  Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, Kulia, akiwahutubia wahitimu na jumuiya ya Bodi ya taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) (Hawako Pichani), wakati wa mahafali ya 38 ya Bodi hiyo, yaliyofanyika katika Kituo cha Bunju, nje kidogo ya Jiji la Dar es salaam, kulia kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa NBAA, Bw. Pius Maneno na Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu na Mafunzo wa Bodi hiyo, Bi. Anne Mbughuni.
  Baadhi ya wahitimu wa taaluma ya juu ya uhasibu (CPA), wakiwa tayari kutunukiwa shahada zao na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango, katika Mahafali ya 38 yaliyofanyika Katika kituo cha Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) kilichopo Bunju, nje kidogo ya  Jiji la Dar es Salaam.
  Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango, akimkabidhi cheti cha kufanya vizuri katika masomo ya taaluma ya juu ya uhasibu (CPA-T), Bi. Happiness Ngowi, wakati wa mahafali ya 38 ya Bodi hiyo yaliyofanyika Katika kituo cha Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), kilichopo Bunju, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
  Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango, akitangaza kuwatunuku vyeti wahitimu wa taaluma ya juu ya uhasibu (CPA-T) waliofanya vizuri katika masomo yao, wakati wa mahafali ya 38 ya NBAA, yaliyofanyika Katika kituo cha Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu, kilichopo Bunju, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
  Wahitimu waliofanya vizuri katika masomo ya NBAA, baada ya kupokea vyeti vya kutambua umahili wao katika masomo pamoja na kupewa zawadi za fedha taslimu zilizotolewa na wadhamini mbalimbali wa Bodi hiyo, wakati  wa Mahafali ya 38 yaliyofanyika katika Kituo cha NBAA, kilichoko Bunju, nje kidogo ya Jiji la Dar es salaam.
  Baadhi ya wahitimu wa shahada ya Juu ya Taaluma ya uhasibu na ukaguzi wa Hesabu CPA-T, inayotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), wakila kiapo cha utii na uadilifu wakati wa mahafali ya 38 ya Bodi hiyo, yaliyofanyika katika kituo kilichoko Bunju, Nje kidogo ya Jiji la Dar es salaam
  Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango, (aliyeketi nafasi ya saba kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Bodi pamoja na wadhamini wa tuzo mbalimbali zilizotolewa kwa wahitimu waliofanya vizuri katika masomo yao, tukio lililofanyika katika kituo cha NBAA, kilichoko Bunju, nje kidogo ya Jiji la Dar es salaam.
  Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango (katikati), Mwenyekiti wa Bodi ya NBAA Prof. Isaya Jairo (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa NBAA Pius Maneno, wakiondoka kwenye viwanja vya mahafali baada ya kumaliza kuwatunuku vyeti na shahada mbalimbali wahitimu wa kozi mbalimbali za NBAA, katika eneo la Bunju, nje kidogo ya Jiji la Dar es salaam.
  Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango (kushoto), akisalimiana na Msajili wa Hazina Bw. Laurance Mafuru, baada ya kumalizika kwa mahafali ya 38 ya Bodi ya taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu(NBAA), yaliyofanyika katika kituo cha Bodi hiyo, Nje kidogo ya Jiji la Dar es salaam. 
  (Picha zote na Wizara ya Fedha)

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia baadhi ya Askari Mgambo walioshiriki katika zoezi la medani liitwalo ''Amphibious Landing'' katika kijiji cha Baatini Wilayani Bagamoyo mara baada ya kufunga maadhimisho ya miaka 52 ya JWT jana. PICHA NA IKULU


  Na: Frank Shija, MAELEZO

  UZALENDO umewapatia ajira takribani vijana 70 baada ya Amiri Jeshi Mkuu,na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kufurahishwa na namna ambavyo washiriki wa zoezi la Amphibia Landing walivyoonyesha umahiri wao.

  Hayo yamebainika jana katika fukwe za kijiji cha Baatani, wilayani Bagamoyo, wakati wa hafla kufunga mazoezi hayo ambapo Mhe. Rais Magufuli alisema kuwa kutokana na alivyojionea mazoezi hayo na amearifiwa kuwa kati ya washiriki wa mazoezi hayo wamo mgambo 30 na JKT 40 aliagiza wote waingizwe kwenye orodha ya waajiriwa wapya wa JWTZ.

  “Katibu Mkuu Kiongozi nakuagiza Kufanya utaratibu waku waingiza kwenye ajira hawa vijana 30 wa mgambo na 40 wa JKT kwani wameonyesha moyo wa uzalendo kwelikweli, tena ikiwezekana ata kesho waingie kwenye orodha ya waajiriwa wapya”. Alisema Rais Magufuli.

  Aidha Rais Magufuli amemuagiza Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Davis Mwamunyange kuangalia namna ya kuwapa motishi wote walioshiriki kufanikisha zoezi hilo ili kuwaongezea morali ya kuwajibika.

  Katika hatua nyingine ametoa wito kwa Majeshi kushirikia hususan katika eneo la unzanzishaji wa viwanda ili kutoa mchango wao katika hasma ya Tanzania kuwa nchi ya Viwanda.

  “Ni lazima sasa tujipange nataka Majeshi yetu muwekeze katika viwanda iwe kwa kuunganishwa nguvu pamoja ama mmoja mmoja naamini hatushindwi, leteni mpango Serikali itasaidia”. Alisema Rais Magufuli.

  Alitolea mfano wa Jeshi la Magereza kuwa na kiwanda cha viatu katika Gereza la Karanga mkoani Kilimanjaro, kushangaa kuona majeshi mengine yananunua viatu kutoka nje ya nchini. Aliwaagiza washirikiane katika kuhakikisha wanafikia malengo ya kuwa na viwanda.

  Alisema kuwa Jeshi letu limekuwa na mafanikio makubwa katika kutekeleza majukumu yake ambayo aliyataja kuwa ni ulinzi wa mipaka ya nchi, kulinda katiba ya nchi, kufundisha wananchi masuala ya ulinzi wa Taifa, uokoaji na utoaji wa misaada katika maafa, kutoa elimu ya kujitegemea pamoja na ulinzi wa amani na ukumbozi.

  Nakuongeza kuwa limeweza kulinda mipaka ya nchi, na kulinda amani iliyopo pamoja na kushirikiana na Umoja wa Mataifa katika kulinda amani katika baadhi ya maeneo ikiwemo Sudan Kusini na DRC Congo.

  Septemba Mosi mwaka huu JWTZ walitimiza miaka 52 ya uhai wake,ambapo ilianza kuadhimsha miaka hiyo kwa kufanya shughuli mbalimbali kama vile usafi, huduma za upimaji wa Afya Bure na zoezi hili la Amphibia Landing ni muendelezo wa maadhimisho hayo.

  Ambapo katika zoezi hilo vifaa kama Meli Vita, Vifaru vinavyo tembea nchi kavu na majini, milipuko pamoja na Ndege vita vilitumika.

  0 0

   Kama kawaida ya watanzania wengi siku hizi suala la matumizi ya mbango kama njia ya kuwasilisha ujumbe wao kwa viongozi  wafanyabiashara  hawakuzubaa  wakati Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipotembelea soko kuu la manispaa ya Dodoma la majengo Oktoba 1, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)  
   Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa   akitembelea soko kuu la Manispaa ya Dodoma la Majengo 
   Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa   akitembelea soko kuu la Manispaa ya Dodoma la Majengo 
   Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa   akitembelea soko kuu la Manispaa ya Dodoma la Majengo 
   Mkuu wa Mkoa wa Dodoma  Jordan Rugimbana akimkaribisha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuzungumza na wafanyabiashara wa soko kuu la Manispaa ya Dodoma la Majengo baada ya kulitembelea Oktoba 1, 2016.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wafanyabiashara wa Soko kuu la Dodoma la Majengo  wakati alipotembelea soko hilo Oktoba 1, 2016. 

   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wafanyabiashara wa soko Kuu la manispaa ya Dodoma la Majengo wakati alipolitembela Oktoba 1, 2016.

  *Aagiza Baraza la Madiwani lipitie upya na kumpa majibu  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameliagiza Baraza la Madiwani la Manispaa ya Dodoma lifanye marekebisho ya kodi inayotozwa kwenye soko la Majengo ambayo imepandishwa kutoka sh. 20,000 hadi sh. 150,000 kwa mwezi.  Amesema anatambua maamuzi ya Baraza ni ya kikao halali lakini hakubaliani na ongezeko hilo ambalo ni sawa na asilimia 650 kwani linawaumiza wananchi.  Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumamosi, Oktoba Mosi, 2016) wakati alipotembelea soko hilo akiwa kwenye ziara ya kukagua maeneo ya kutolea huduma za jamii mjini Dodoma.  Amesema soko hilo linatakiwa lifanyiwe mapitio ili liwekwe kwenye hali nzuri na Manispaa ihakikishe maboresho hayo yanafanyika bila ya kuwaumiza wafanyabiashara.  “Kwa kuwa uamuzi wa kupandisha kodi ulifanyika kisheria na kupitishwa na baraza la Madiwani, sitaki kuvunja sheria. Nawaagiza mkazungumze tena katika baraza na muangalie namna ya kupunguza gharama hizo,” amesema.  “Hali hii haiwezekani kuachwa iendelee, huku ni kuwaumiza wananchi. Mkurugenzi wa Manispaa nenda kaitishe tena kikao, mfanye mazungumzo upya kwenye baraza lenu na mje mnieleze mmekubaliana nini” amesisitiza.  Pia ameitaka Manispaa hiyo ihakikishe makusanyo yote ya fedha katika soko hilo yanakusanywa kwa njia ya kielektroniki ili fedha hizo ziweze kuleta tija na kuwataka Mkuu wa mkoa na wilaya kuwachukulia hatua wotewatakaobainika kuiba fedha hizo.  Amesema Manispaa hiyo inatakiwa kupanua masoko kwa kujenga masoko mapya makubwa katika maeneo ya Nkuhungu, Kisasa, Mlimwa na Barabara ya Iringa ili huduma hizo zisambazwe.  Mapema akisoma risala yake, Mwenyekiti wa soko hilo, Bw. Godson Rugazama alimueleza Waziri Mkuu changamoto zinazolikabili soko hilo kuwa ni pamoja na ongezeko la kodi isiyozingatia uhalisia wa maisha na shughuli za wajasiriamali sokoni hapo. “Kodi imeongezeka kutoka sh. 20,000 hadi 150,000 kwa mwezi,” alisema.  Mwenyekiti huyo alitaja changamoto nyingine ni uchakavu wa mifereji ya maji machafu, kuvuja kwa paa la soko, bidhaa kuuzwa katika maeneo yasiyokuwa rasmi na kusababisha wateja kutoingia sokoni.  Wakati huohuo, Waziri Mkuu ametembelea hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma na kukagua maeneo mbalimbali zikiwemo wodi za wagonjwa, jengo la wazazi na jengo jipya la wagonjwa wa Bima ya Afya (NHIF).  Akiwa hospitalini hapo, pia alizungumza na watumishi wa sekta ya afya na kuwataka wawahimize wananchi wajiunge na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) ambao unawawezesha mtu kulipia bima ya matibabu kwa ajili ya mhusika, mwenza wake na watoto/watemezi wanne na serikali inajazia kiasi kile kile alichochangia.  Akizungumzia miundombinu ya afya mkoani humo, Waziri Mkuu alisema mkoa wa Dodoma hauna shida ya matibabu au utoaji wa huduma ya afya kutokana na miundombinu iliyopo hivi sasa.  Aliwataka wafanye kazi kwa uadilifu na uaminifu na kuongeza tija katika utendaji kazi wao huku wakitanguliza utunzaji wa mali ya umma.  “Ninawasihi mjenge tabia ya huruma kwa wagonjwa huku mkitambua unyeti wa kazi mliyonayo. Ninaamini mtatunza vifaa mlivyonavyo na siyo kuvichukua na kuvipeleka kwenye zahanati zenu au maduka yenu binafsi ya dawa,” alionya.  IMETOLEWA NA:

  OFISI YA WAZIRI MKUU

  S. L. P. 980,

  DODOMA.

  JUMAMOSI, OKTOBA MOSI, 2016  0 0

   KAMPUNI ya TICTS inayojishughulisha na kazi ya uendeshaji wa huduma za bandari, Dar es salaam imeendelea na kampeni ya yake ya "Go GREEN" kwa kupanda miti katika eneo la Shule ya Sekondari Mivinjeni, Wilayani Temeke.

  Akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya upandaji miti jijini hapa, Mkurugenzi wa Maendeleo wa Kampuni ya TICTS, Donald Talawa alisema ili Tanzania ifikie lengo la kuwa na uchumi wa kati kufikia mwaka 2015, suala la upandaji miti ni lazima kufanyika ili kuenda sambamba mkakati huo.

  "Tukiwa na miti michache au miti iliyotoweka, tutaangamia kama taifa na ikiwa tutakuwa na miti mingi, hapo hatuna cha kupoteza, ila tukiruhusu ukataji miti uendelee katika nchi yetu bila kupanda mingine, tutaishia kuwa ombaomba kama si kufa kwa njaa" alisema Talawa.

  Pia alitoa wito kwa makampuni mengine yanayofanya biashara hapa nchini, kuisaidia Serikali kuhamasisha masuala yenye manufaa kwa taifa kama hilo la kupanda miti.
   Mkurugenzi wa Maendeleo wa Kampuni ya TICTS, Donald Talawa akishiriki kupanda Mti katika eneo la Shule ya Sekondari Kurasini, kupitia Kampeni yao ya "Go GREEN" yenye kuhamasisha jamii umuhimu wa kupanda miti. 
   Meneja wa Kitengo cha Teknolojia ya Habari wa Kampuni ya TICTS, Hassan Mageta (kati) akimwagilia maji mti wake muda mfupi baada ya kuupanda katika eneo la Shule ya Sekondari Kurasini, Jijini Dar es salaam Oktoba 1, 2016.
   Meneja wa Masoko na Uhusiano wa Kampuni ya TICTS, Caroline Owenya (kushoto) akishirikiana kupanda mti na Makamu Mkuu wa Shule ya Sekondari Kurasini, Mwl. Marcelino Fussi (katikati) pamoja na mmoja wa wanafunzi wa Shule hiyo, wakati wa maadhimisho ya siku ya upandaji miti jijini Dar es salaam Oktoba 1, 2016.
  Wafanyakazi wa Kampuni ya TICTS wakipanda miti.


  0 0

   Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy A. Mwalimu (Mb.) akikagua usafi wa eneo la soko la wanawake wajasiriamali, alipofanya ziara ya kushitukiza katika soko lililoko Stendi ya Kabwe Jijini Mbeya tarehe 30/9/2016. 
   Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy A. Mwalimu (Mb.) akiongea na wanawake wajasiriamali, alipofanya ziara ya kushitukiza katika soko lililoko Stendi ya Kabwe Jijini Mbeya ili kufuatilia utekelezaji wa Halmashauri kutenga asilimia 5 ya mapato yake ya ndani kwa ajili ya Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake. (30/9/2016)
   Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy A. Mwalimu (Mb.) akiongea na wanawake wajasiriamali, alipofanya ziara ya kushitukiza katika soko lililoko Stendi ya Kabwe Jijini Mbeya ili kufuatilia utekelezaji wa Halmashauri kutenga asilimia 5 ya mapato yake ya ndani kwa ajili ya Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake. 


  * Aagiza Halmashauri kuwapatia mikopo wanawake wajasiriamali waliopo stand ya Kabwe.* Awataka wazazi na walezi kuhakikisha wanasimamia malezi ya watoto wao.

  Na Erasto Ching’oro- Msemaji wa Wizara, Mbeya

  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (Mb.) amefanya ziara ya kushtukiza katika Stendi ya Kabwe Jijini Mbeya kwa ajili ya kuongea na wanawake wajasiriamali wanaofanya biashara katika stendi hiyo ili kufuatilia utekelezaji wa Ilani kuhusu Halmashauri kutenga asilimia 5 ya mapato yake ya ndani kwa ajili ya Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake. Akiongea na Wanawake hao Waziri Ummy Mwalimu amewataka kujiunga katika vikundi ili kuwawezesha kukopesheka na kupata fursa mbalimbali za biashara ikiwemo mafunzo na masoko.

  Mhe. Ummy, alieleza kuwa Serikali itahakikisha inawapa mikopo yenye riba nafuu kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake, na pia kuweka mazingira wezeshi ya kuwajengea uwezo wa kufanya biashara zao katika mazingira salama. Hivyo amewasisitizia kuwa ni muhimu wajiunge katika vikundi ili waweze kufikiwa na fursa za huduma za masoko na mikopo kwa kwa wepesi zaidi. 

  Kwa upande wao, wanawake wajasiriamali hao katika stendi ya Kabwe walisema changamoto kubwa waliyonayo ni kukosa mitaji na masoko hali ambayo ilimlazimu Waziri Ummy kumuagiza Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya kuhakikisha anawapatia mikopo wanawake wa Standi ya Kabwe ndani ya mwaka huu wa fedha wa 2016/17.

  Pia akiwa katika soko hilo, Waziri Ummy ameeleza kufurahishwa na jitihada za Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Amos Makalla na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Mhe William Paul Ntinika kwa kuwahamasisha wajasiriamali hao kufanya biashara zao katika mazingira ya usafi kwa kufanikisha matumizi ya meza za kufanyia biashara katika eneo hilo. Mhe. 

  Waziri Ummy alitoa rai kwa Halmashauri nyingine kuiga mpango wa kufanya biashara katika mazingira ya usafi ili kuhakikisha tunadumisha usafi wa miji yetu na mazingira ya maeneo ya wafanyabiashara wadogowadogo. 

  Aidha, akiwa Mkoani Mbeya Waziri Ummy alitembelea Mahabusu ya Watoto iliyopo katika Jiji la Mbeya. Akiongea na watoto takribani 16 waliopo katika Mahabusu hiyo Waziri alieleza kuwa Serikali itahakikisha watoto waliopo mahabusu wanapata haki zao zote za msingi hususan haki ya kupata elimu kwa maendeleo na ustawi wao. 

  Hata hivyo, Waziri Ummy ametoa rai kwa wazazi na walezi wa watoto wote nchini kuhakikisha wanawalea watoto wao katika misingi bora itakayo wawezesha kuwa na tabia njema. Hii itasaidia kupunguza idadi ya watoto wanaokinzana na sheria na kupelekea kufikishwa katika mahabusu za watoto. 

  Waziri alionya kuwa makosa mengi yanayowakumba watoto waliopo mahabusu msingi wake mkubwa ni malezi mabaya yanayo pelekea watoto kukosa maadili ambayo hujikuta wamehusishwa na makosa ya mauaji, wizi, ubakaji na ulawiti. Hivyo kila mzazi ano wajibu wa kulea watoto katika maadili na tabia njema ili kuepuka migogoro ya kisheria. 

  Aidha, Watoto hao waliopo mahabusu ya watoto Mbeya walimuomba Waziri Ummy kusaidia kuharakisha kusikilizwa kwa mashauri ya kesi zinazowakabili zilizopo mahakamani ili waweze kurudi nyumbani, wakiwa huru na kuendelea na masomo.

  Waziri Ummy yupo Mkoani Mbeya kwa ziara ya Kazi ya siku 2 ambapo pia tarehe 01 Oktoba 2016 atakuwa Mgeni Rasmi kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani yanayofanyika kitaifa eneo la Rujewa, Wilayani Mbarali.  0 0

  HAKUNA mbabe, ule mtanange uliokuwa unasuburiwa kwa hamu kubwa uliohusisha mahasimu wawili Yanga na Simba umemalizika jioni ya leo kwa timu hizo kutoka sare ya 1-1.

  Katika mchezo huo uliokuwa na presha kubwa kwa kila upande, Yanga walifanikiwa kupata goli dakika ya 26, baada ya Amisi Tambwe kumzidi mbinu beki Novat Lufungo wa Simba na kuandika goli la kuongoza huku nahodha Jonas Mkude akipewa kadi nyekundu baada ya kumpiga mwamuzi kwa kudai kuwa Tambwe aliushika mpira kwa mkono.

  Mpira ulisimama kwa dakika takribani tano na vurugu kutokea ikiwemo mashabiki wa Simba kuanza kung'oa viti na kuvirusha uwanjani, hali iliyopelekea Jeshi la Polisi kuanza kupiga mabomu ya machozi ili kutuliza ghasia iliyojitokeza uwanjani hapo.

  Mpaka ilipofika mapumziko, Yanga walikuwa mbele kwa goli 1-0, lakini kipindi cha pili Yanga walifanya mabadiliko kwa kumtoa Kelvin Yondan aliyekuwa na kadi ya njano na kuingia Andrew Vicent "Dante", Saimon Msuva akachukua nafasi ya Juma Mahadhi, Haruna Niyonzima akiingia baada ya Deus Kaseke, Simba wakimtoa Laudit Mavugo na kuingia Fredrick Blagnon, Ibrahim Ajib na kuingia Mohamed Ibrahim na Novat Lufungo na kuingia Jurko Murshid.

  Mchezo uliokuwa wa kasi kwa kila upande huku Yanga wakitafuta goli la kuongoza na Simba wakisaka la kusawazisha, ambapo dakika ya 89 Shiza Kichuya anawainua mashabiki wa Simba baada ya kupiga kona iliyoenda moja kwa moja wavuni na kusawazisha na kudumu mpaka dakika 90. Na Zainab Nyamka.


  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein akilakiwa na Mkuu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Jenerali Davies Mwamunyange alipowasili kushuhudia kufungwa kwa  mafunzo ya medani ya Kijeshi ya kutua ardhini kutoka majini  (Amphibous Landing) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 52 ya JWTZ, katika kijiji cha Baatini, Wilayani Bagamoyo.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein akilakiwa na Mnadhimu mkuu wa JWTZ  Luteni Jenerali Venance Mabeyo  alipowasili kushuhudia kufungwa kwa  mafunzo ya medani ya Kijeshi ya kutua ardhini kutoka majini  (Amphibous Landing) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 52 ya JWTZ, katika kijiji cha Baatini, Wilayani Bagamoyo.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein akilakiwa na Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudence Milanzi  alipowasili kushuhudia kufungwa kwa  mafunzo ya medani ya Kijeshi ya kutua ardhini kutoka majini  (Amphibous Landing) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 52 ya JWTZ, katika kijiji cha Baatini, Wilayani Bagamoyo.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein akipeana mikono na Mkuu wa Majeshi mstaafu, Jenerali Robert Mboma alipowasili kushuhudia kufungwa kwa  mafunzo ya medani ya Kijeshi ya kutua ardhini kutoka majini  (Amphibous Landing) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 52 ya JWTZ, katika kijiji cha Baatini, Wilayani Bagamoyo.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein akipeana mikono naMkurugenzi wa Operesheni hiyo  Meja Jenerali James Mwakibolwa
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalumu za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Haji Omar Kheir akilakiwa na makamanda. Nyuma yake ni Katibu Mkuu Kiongozi wa SMZ  Dkt. Abulhamid Yahya Mzee
  Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudence Milanzi akiongea na Mkuu wa Majeshi mstaafu, Jenerali Robert Mboma
   Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiwasili kufunga mafunzo ya medani ya Kijeshi ya kutua ardhini kutoka ndani ya maji na kukomboa eneo lililokaliwa na adui (Amphibous Landing) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 52 ya JWTZ, katika kijiji cha Baatini, Wilayani Bagamoyo.

  Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akilakiwa na Mkuu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Jenerali Davies Mwamunyange  alipowasili kufunga mafunzo ya medani ya Kijeshi ya kutua ardhini kutoka ndani ya maji na kukomboa eneo lililokaliwa na adui (Amphibous Landing) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 52 ya JWTZ, katika kijiji cha Baatini, Wilayani Bagamoyo.
  Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein alipowasili kufunga mafunzo ya medani ya Kijeshi ya kutua ardhini kutoka ndani ya maji na kukomboa eneo lililokaliwa na adui (Amphibous Landing) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 52 ya JWTZ, katika kijiji cha Baatini, Wilayani Bagamoyo.
  Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Eng. John Kijazi  alipowasili kufunga mafunzo ya medani ya Kijeshi ya kutua ardhini kutoka ndani ya maji na kukomboa eneo lililokaliwa na adui (Amphibous Landing) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 52 ya JWTZ, katika kijiji cha Baatini, Wilayani Bagamoyo.
  Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu  wa Idara ya Usalama wa Taifa Dkt Modestus Kipilimba alipowasili kufunga mafunzo ya medani ya Kijeshi ya kutua ardhini kutoka ndani ya maji na kukomboa eneo lililokaliwa na adui (Amphibious Landing) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 52 ya JWTZ, katika kijiji cha Baatini, Wilayani Bagamoyo.
  Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Ernest Mangu   alipowasili kufunga mafunzo ya medani ya Kijeshi ya kutua ardhini kutoka ndani ya maji na kukomboa eneo lililokaliwa na adui (Amphibious Landing) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 52 ya JWTZ, katika kijiji cha Baatini, Wilayani Bagamoyo.
  Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini Afande  John Casmir Minja alipowasili kufunga mafunzo ya medani ya Kijeshi ya kutua ardhini kutoka ndani ya maji na kukomboa eneo lililokaliwa na adui (Amphibious Landing) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 52 ya JWTZ, katika kijiji cha Baatini, Wilayani Bagamoyo.
  Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Kamishna  Valentino Mlowola alipowasili kufunga mafunzo ya medani ya Kijeshi ya kutua ardhini kutoka ndani ya maji na kukomboa eneo lililokaliwa na adui (Amphibious Landing) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 52 ya JWTZ, katika kijiji cha Baatini, Wilayani Bagamoyo.
  Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na  Kaimu Kamishna Mkuu wa Idara ya Uhamiaji Mama  Victoria Lembeli alipowasili kufunga mafunzo ya medani ya Kijeshi ya kutua ardhini kutoka ndani ya maji na kukomboa eneo lililokaliwa na adui (Amphibious Landing) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 52 ya JWTZ, katika kijiji cha Baatini, Wilayani Bagamoyo.
  Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipokea saluti toka kwa  Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudence Milanzi   alipowasili kufunga mafunzo ya medani ya Kijeshi ya kutua ardhini kutoka ndani ya maji na kukomboa eneo lililokaliwa na adui (Amphibious Landing) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 52 ya JWTZ, katika kijiji cha Baatini, Wilayani Bagamoyo.
  Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudence Milanzi  alipowasili kufunga mafunzo ya medani ya Kijeshi ya kutua ardhini kutoka ndani ya maji na kukomboa eneo lililokaliwa na adui (Amphibous Landing) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 52 ya JWTZ, katika kijiji cha Baatini, Wilayani Bagamoyo.

  Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Majeshi mstaafu, Jenerali Robert Mboma alipowasili kufunga mafunzo ya medani ya Kijeshi ya kutua ardhini kutoka ndani ya maji na kukomboa eneo lililokaliwa na adui (Amphibous Landing) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 52 ya JWTZ, katika kijiji cha Baatini, Wilayani Bagamoyo.
  Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Mama suzana Mlawi
  Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Majenerali wa JWTZ 
   Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa zoezi hizo Meja Jenerali James Mwakibolwa
  Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akijiandaa kuweka saini katika kitabu cha wageni akishuhudiwa na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davies Mwamunyange
  Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiweka saini katika kitabu cha wageni
  Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiongea na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein 
  Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na viongozi wengine akisikiliza muhtasari wa zoezi hilo
  Wanadhimu wa zoezi
  Sehemu ya wasimamizi wa zoezi hilo
  Mkurugenzi Mkuu wa zoezi hizo Meja Jenerali James Mwakibolwa akisoma taarifa 
  Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na viongozi wengine akisikiliza muhtasari wa zoezi hili
  Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na viongozi wengine akisikiliza muhtasari wa zoezi hili
  Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akifurahia jambo na Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali Robert Mboma
  Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiongea na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davies Mwamunyange kabla ya kuelekea kwenye uwanja wa zoezi la Medani

  Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiongozana  na  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davies Mwamunyange kuelekea kwenye uwanja wa zoezi la Medani
  Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiongozana  na  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi kuelekea kwenye uwanja wa zoezi la Medani
  Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiongozana  na  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi na  kuelekea kwenye uwanja wa zoezi la Medani
  Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipiga saluti wakati wa wimbo wa Taifa akiwa  na  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein
  Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipiga saluti wakati wa wimbo wa Taifa akiwa  na  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, Mkuu wa Majeshi Jenerali Davies Mwamunyange (kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa zoezi hilo Meja Jenerali James Mwakibolwa (kushoto)
  Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipiga saluti wakati wa wimbo wa Taifa
  Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudence Milanzi (kulia) na mmoja wa washereheshaji Meja BMP Mlunga wakipiga saluti wakati wa wimbo wa Taifa
  Brass band ya JWTZ ikiwa tayari tayari
  Mcheza ngoma hodari wa kikundi cha sanaa cha JWTZ  Private Juma Abdulrahman Juma akikaribishwa jukwaa kuu kupewa zawadi kwa burudani nzuri iliyooneshwa na kikundi chake
  Mcheza ngoma hodari wa kikundi cha sanaa cha JWTZ  Private Juma Abdulrahman Juma akiendelea kutoa burdani baada ya kukaribishwa jukwaa kuu kupewa zawadi kwa kazi  nzuri iliyooneshwa na kikundi chake
  Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimtuza  Private Juma Abdulrahman Juma kwa niaba ya wenzie kwa burudani nzuri.
  Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimpongexza kwa burudani nzuri  Private Juma Abdulrahman Juma kwa niaba ya wenzie
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein akimtuza  Private Juma Abdulrahman Juma kwa niaba ya wenzie
  Makamanda wakipiga bastola za miali kuashiria kuanza kwa zoezi hilo la medani
  Kazi imeanza....
  Ndege vita zikiwa katika fomesheni 
  Ndege vita angani
  Sehemu ya ndege vita
  Mpiga picha mwandamizi wa magazeti ya Daily News na Habari Leo Mroki Mroki akiwa kazini kurekodi zoezi hilo
  Boti za kikosi maalumu zikielekea ngome ya adui
  Vifaru vinavyotembea majini na ardhini vikikaribia ngome ya adui
  Vifaru vinatoka majini na kuendelea na mashambulizi nchi kavu
  Makamanda wakiongoza shambulizi
  Wapiganaji wakishuhudia zoezi la medani
  Makamanda wakibadilishana mawazo
  Makamanda wakiwasiliana na walio uwanja wa vita
  Hali tete ngome ya adui
  Kikundi cha sanaa cha JWTZ kikitoa burudani wakati wa kusubiri zoezi lingine lianze
  Kikundi cha sanaa cha JWTZ kikitoa burudani wakati wa kusubiri zoezi lingine lianze
  Kikundi cha sanaa cha JWTZ kikitoa burudani wakati wa kusubiri zoezi lingine lianze
  Meja Jenerali Mwakibolwa akitoa maelekezo kwa washereheshaji

  Meza kuu ikifurahia
  Amiri Jeshi mkuu Rais Dkt John Pombe Magufuli akiongea jambo na Mkuu wa Majeshi Jemerali Davies Mwamunyange
  Meza kuu ikibadilishana haya na yale
  Hatimaye zoezi la kumtoa adui limekamilika kwa mafanikio na wapiganaji wanaelekea uwanja wa sherehe
  Wapiganaji wanarudi kishujaa
  Furaha ya ushindi baada ya mapambano ya anga, majini na ardhini
  Meza kuu ikiwapokea wapiganaji
  Mori juu!
  Kikosi maalumu cha majini
  Meza kuu
  Nderemo za ushindi zikishuhudiwa na meza kuu
  Wapiganaji wakiwa uwanja wa sherehe
  Wapiganaji mbele ya wakuu
  Bendera za zikipepea mbele ya wapiganaji
  Bendi ya muziki ya JWTZ Mwenge Jazz Band "Wana Paselepa" ikitumbuiza wimbo wa mashujaa
  Amiri Jeshi Mkuu anajiunga kunogesha burudani wakati  Bendi ya muziki ya JWTZ Mwenge Jazz Band "Wana Paselepa" wakati ikitumbuiza wimbo wa mashujaa
  Amiri Jeshi Mkuu anajiunga kunogesha burudani wakati  Bendi ya muziki ya JWTZ Mwenge Jazz Band "Wana Paselepa" wakati ikitumbuiza wimbo wa mashujaa
  Furaha tu wakati Amiri Jeshi Mkuu anajiunga kunogesha burudani wakati  Bendi ya muziki ya JWTZ Mwenge Jazz Band "Wana Paselepa" wakati ikitumbuiza wimbo wa mashujaa
  Washereheshaji wakipokea maelekezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa zoezi hilo Meja Jenerali James Mwakibolwa
  Wapiganaji wakiselebuka midundo murua ya  Paselepa...
  Wapiganaji kutoka JWTZ, JKT na mgambo walioshiriki kikamilifu katika zoezi hilo
  Wanahabari wakiwa kazini kurekozi tukio hilo la aina yake
  Bingwa wa zamani wa ndondi za uzito wa juu wa Taifa Makoye Isangula (kulia) akiwa na kikosi chake

  Ndege vita zikikaribia kumaliza kazi
  Wapiganaji wa kikosi cha mgambo
  Amiri Jeshi Mkuu akiongea na Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein
  Ndege vita zikipita kwa mara ya mwisho
  Kiongozi wa ndege vita akitoa saluti maalumu kwa Amiri Jeshi Mkuu

  Mkuu wa Majeshi akikabidhiwa bendera ya zoezi hilo la medani
  Mkuu wa Majeshi Jenerali Davies Mwamunyange akikabidhi bendera kwa mpiganaji kuirudisha makao makuu kuashiria hitimisho la zoezi hilo
  Mkuu wa majeshi Jenerali Davies Mwamunyange akisoma risala yake
  Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa Dkt. Husssein Mwinyi akisoma hotuba yake na kumkaribisha viongozi wakuu  kuongea na wapiganaji
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein akiongea na wapiganaji
  Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akihutubia wapiganaji
  Wapiganaji wakimsikiliza kwa makini Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli
  Wapiganaji wakifurahia hotuba ya Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli
  Wakiemndelea kumsikiliza Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli
  Wapiganaji wakimpigia makofi Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli
  Vifijo kwa Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli
  Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiendelea kuhutubia
  Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisisitiza jambo katika hotuba yake
  Wapiganaji wakifurahia hotuba ya Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli
  Wapiganaji wakishangilia hotuba ya Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli
  Wanamgambo wanamshukuru Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa kuwapa ajira papo kwa papo
  Wapiganaji
  Furaha na msisimko
  Mpiganaji
  Mpiganaji
  Jukwaa kuu

  Bingwa wa zamani wa Taifa wa ndondi za uzito wa juu Makoye Isangula na kikosi chake
  wapiganaji wakakamavu kikosi cha mgambo
  Saluti wakati wa wimbo wa Taifa
  Ukakamavu wakati wa wimbo wa Taifa
  Saluti kwa wimbo wa Taifa
  Saluti

  Amiri Jeshi Mkuu akiagana na wapiganaji
  Kazi nzuri vijana wangu.....
  Hongereni sana kwa kazi nzuri.....
  Hongera sana vijana 
  Safi sana....
  Hongera sana....
  Kwaherini vijana
  Amiri Jeshi Mkuu akisalimiana na Mkuu wa wilaya ya Kibaha Mhe. Assumpter Mshama
  Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiondoka eneo la tukio kwa ukakamavu

  PICHA ZOTE NA IKULU

  0 0


  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa serikali na Taasisi zake mjini Dodoma Oktoba 1, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Baadhi ya watumishi wa serikali na Taasisi zake wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao mjini Dodoma Oktoba 1, 2016. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imeunda timu ya wataalamu ambao watatoa ushauri juu ya suala zima la kuhamishia makao makuu Dodoma.

  Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumamosi, Oktoba 1, 2016) wakati akizungumza na watumishi wa Serikali wa mkoa wa Dodoma, wazee wa mkoa huo, wafanyabiashara pamoja na viongozi mbalimbali kwenye ukumbi wa mikutano wa Dodoma (Dodoma Convention Centre).

  “Tumeunda timu ya watu 10 ambao ni wataalamu waliobobea kwenye masuala ya ujenzi wa miji mikuu, hawa wana uzoefu wa kuangalia makao Makuu ya nchi yanafananaje. Watakuja Dodoma, wapitie master plan na kisha watapita kwenye maeneo kadhaa ya mji ili waone hali halisi ikoje ndipo watupe maoni yao,” amesema.

  “Tunataka tusirudie kosa la Jiji la Dar es Salaam la kulazimika kubomoa makazi ya watu kila inapolazimu kufanya uboreshaji wa miundombinu. Hawa watu watatuambia wapi tunatakiwa tuweke njia nne au sita za magari, wapi tuweke bustani au wapi tujenge nyumba za ghorofa moja, mbili, tatu au zaidi,” ameongeza.

  Akifafanua kuhusu miundombinu, Waziri Mkuu amesema timu hiyo pia itatakiwa kutoa ushauri juu ya wapi ijengwe njia ya malori tu au mahali gani zinahitajika kujengwa barabara za juu (flyovers) ili kuepusha msongamano katikati ya mji wa Dodoma.

  Bila kutaja majina ya wajumbe wa timu hiyo, Waziri Mkuu amesema timu hiyo itaongezewa wataalamu kutoka China na Malaysia ambao nchi zao tayari zina uzoefu wa kuhamisha makao makuu ya nchi zao zaidi ya mara moja.

  Alitumia fursa hiyo kuwaeleza watumishi juu ya uwepo wa Tume ya Kuboresha Maslahi ya Wafanyakazi ambayo imekuwa ikifanya kazi tangu mwaka jana. “Kuna vikao vimekuwa vinafanyika tangu mwaka jana baina ya Serikali na viongozi wa vyama vya wafanyakazi kwa lengo la kujadili uboreshaji wa maslahi ya wafanyakazi, na jambo hili linaendelea vizuri,” amesema.

  Kuhusu madeni ya watumishi wa umma, Waziri Mkuu amewasihi watumishi wawe na imani na Serikali yao kuhusu madeni hayo na kwamba ikimaliza uhakiki unaofanyika hivi sasa, kila mwenye stahili zake atalipwa.

  Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu ameutaka uongozi wa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA) ihakikishe inakamilisha upimaji wa viwanja 100,000 kama ilivyojipangia ili watumishi hao pamoja na wananchi waweze kupatiwa viwanja haraka iwezekanavyo.

  “Nimearifiwa kuwa mna mpango wa kupima viwanja 100,000 kwa ajili ya kuwapatia wananchi na watumishi. Kamilisheni utaratibu huo haraka ili watumishi wapewe viwanja na waweze kujenga nyumba zao za kuishi,” amesema huku akishangiliwa.

  Natambua kuwa mmekubaliana kuanzisha utaratibu wa kuingiza viwanja kwenye mfumo wa kompyuta ili kuepuka double allocation. Harakisheni zoezi hilo ili kama itawezekana, kabla ya Novemba kazi hiyo iwe tayari na watu wapatiwe viwanja chini ya mfumo huo mpya,” amesisitiza.

  Kuhusu huduma za kijamii kama elimu, umeme, maji na masoko, Waziri Mkuu amewahakikishia watumishi hao kwamba Serikali imeangalia kila eneo na kuzingatia mapendekezo yaliyotolewa ili kuboresha utoaji wa huduma hizo. Amewataka watumishi hao wabadilike na wawe tayari kuwapokea watumishi wenzao watakaowasili kwa awamu kuanzia mwezi huu.
   
  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  S. L. P. 980,
  DODOMA
  JUMAMOSI, OKTOBA MOSI, 2016.
   
   

  0 0

  Na: Frank Shija, MAELEZO.

  SERIKALI imejipanga kuhakikisha inatatua na kumaliza kero zote zinazoyakabili majeshi yote nchini ikiwa ni jitihada zake za kuhakikisha kuna kuwa na ulinzi imara wa mipaka ya nchi na raia wake.

  Hayo yamebainishwa na Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli alipokuwa akifunga mafunzo ya Kijeshi ya kutua ardhini kutoka ndani ya maji na kukomboa eneo lililokaliwa na adui (Amphibia Landing) ikiwa ni sehemu ya maadhmisho ya miaka 52 ya JWTZ, jana katika kijiji cha Baatini, Wilayani Bagamoyo.

  Rais Magufuli alisema kuwa anatambua kuwa zipo changamoto kadhaa ndani ya Majeshi yetu na kuwahakikishia kwamba atahakikisha zinatatuli kwani nia ya Serikali ni kufanya maboresho makubwa ya majeshi yote.

  Alizitaja moja ya changamoto hizo kuwa ni pamoja na suala la Resheni ambapo suala hilo alikwisha toa maaagizo ya kubadili mfumo wa kuwa na Maduka yasiyolipa ushuru na kodi na badala yake Askari waongezewe fedha katika Resheni zao.

  Ametoa wito kwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini, Jenerali Davis Mwamunyange kufikisha taarifa ya uchambuzi kuhusu Resheni hizo ili utaratibu wa kuanza kulipa kiwango kipya cha Resheni ufanyike.

  “Nataka Wanajeshi wote wafaidike kwa kupewa kiwango bora cha Resheni kuliko kuendelea na maduka yasiyolipa Kodi huku yakiwafaidisha watu wachache, fedha zitakazotoka na maduka hayo zitatumika kuongeza Reshini zenu na Serikali itaongeza pia”. Alisema Rais Magufuli.

  Aidha Rais Magufuli alitumia fursa hiyo kulipongeza Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kwa uimara waliounyesha katika mazoezi hayo ambapo alisema kuwa ameridhishwa na anaamini nchi iko salama.

  Kwa upande wake, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi amewapongeza makamanda wa Jeshi hilo kwa kufanikisha zoezi na kuongeza kuwa zoezi hilo siyo kwamba linaleta sifa kwa wanajeshi pekee bali naTaifa kwa ujumla.

  Waziri Mwinyi amewaomba wanajeshi kuendelea kufanya kazi kwa moyo wa uzalendo huku Serikali ikiendelea kushughulikia changamoto zao.

  Naye Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Davis Mwamunyange amefananisha Jeshi na Kompyuta ambazo zina sehemu ya Hardware na Software, ambapo alisema hardware ni vifaa na software ni rasilimali watu.

  Mkuu huyo wa Majeshi alimuhakikishia Mhe. Rais kuwa wanajeshi wetu ni imara, wanaipenda nchi yao na raia wake, wanajiamini na wako tayari muda wowote.

  “Mhe. Rais, nakuhakishia wanajeshi wetu wako imara sana, ni watiifu, waadilifu, wanaipenda nchi yao, na wanawapenda wananchi wenzao, tena wako kamili kwelikweli, nami najivunia kuwa kiongozi wao”. Alisema Mwamunyange.

  Awali akielezea mazoezi hayo Meja Patrick Sawala amesema zoezi hilo la pamoja la Amphibia Landing katika uwanja wa medani za vita limefanyika kwa lengo la kuonyesha namna wajashi wan chi yetu wako tayari kutekeleza majuku yao ya kulinda amani na mipaka ya nchi yake.

  Alisema kuwa suala kubwa katika zoezi hili ni namna ambavyo wanajeshi wanafanya kazi kwa kushirikiana wakati wa mapambano dhidi ya adui yao.

  Meja Sawala amesema kuwa zoezi hilo ambalo lilihusisha Vikosi vya Anga, Nchi kavu na Majini huku zana za kisasa za kivita zikitumika katika mazoezi hayo.

  Aliongeza kuwa kutokana na Jiografia ya nchi yetu ambayo inasehemu ya visiwa, zoezi hilo ni muhimu sana kwa ajili ya ulinzi na kujihami.

  Mbinu zilizotumika katika zoezi hilo zinafanana kwa kiasi kikubwa zile zilizotumiwa na Majeshi ya Umoja wa Afrika yakiongozwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) mwaka 2008 kwa kushirikiana na jeshi la Shirikisho la Comoro kukikomboa kisiwa cha Anjouan kupitia operesheni ya`Demokrasia Comoro’

  JWTZ inaadhimisha miaka 52 tokea kuasisiwa kwake mnamo tarehe 1, Septemba, 1964 kufuatia Muungano wa Tanganyika na Zanzibar hali iliyopelekea kanzisha Jeshi jipya lenye sura ya muungano lililokuja kurithi Jeshi la Tanganyika Rifle lililokuwa upande wa Bara pekee.

  0 0  0 0

   


  0 0

  Dkt.Helen Kijo-Bisimba
  OKTOBA Mosi (1) ya kila mwaka ni siku iliyoteuliwa na Umoja wa Mataifa kuadhimisha uwepo wa wazee katika jamii kote ulimwenguni. Siku hii ilianza kuadhimishwa rasmi Oktoba 1, 1991 kwa lengo la kuongeza uelewa kuhusu mambo yanayowalenga wazee ikiwemo kutoheshimu haki za wazee, kutazama mahitaji na maslahi ya wazee na kuhakikisha mzee popote alipo ulimwenguni anapata huduma za msingi za kijamii kama vile huduma bora za afya na matibabu. 

  Mahususi, siku hii imekuwa na lengo la kuutambua mchango wa wazee katika jamii kwa wakati husika na wakati uliopita katika mataifa yao. Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu tunatumia fursa hii kuwapongeza wazee wote duniani na hususan wazee wa Tanzania. 

  Pia tunatumia siku hii  kuikumbusha serikali na mihimili mingine ya dola pamoja na wanachi wote kwa ujumla   kuheshimu wazee wetu kama hazina ya taifa. Pia Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kinaitumia siku hii kuungana pamoja na wazee wanaodai haki yao kwa zaidi ya miaka 20. 

  Mathalani, wazee waliotumikia iliyokuwa jumuiya ya Afrika Mashariki kabla ya kuvunjika kwake mwaka, 1977 ambao mpaka leo wameendelea kupambana na kudai haki yao. 

  Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu pia tunaitumia siku ya leo kuitaka serikali ya Marekani kupitia Ubalozi wake nchini Tanzania kutoa msimamo wake juu ya kesi ya madai ya waliokuwa walinzi wa ubalozi wa marekani nchini Tanzania wakijulikana kama 'mission security force' katika Ubalozi wa Amerika kwa serikali ya Amerika – 1984. 

  Sambamba na hayo Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kinakemea vikali vitendo vya mauji ya wazee kwa imani za kishirikina vinavyozidi kupamba moto nchini, watoa huduma wa afya wanaotumia lugha za kuudhi dhidi ya wazee, vijana wanaorubuni wazee kuuza mali zao na kuwatapeli hususani ardhi kuacha vitendo hivi ili kuheshimu tunu hii adhimu ya taifa..

  Tunaungana na jamii ya ulimwengu kusimama kupinga mitazamo hasi juu ya wazee na uzee kiujumla.

  Wazee ni hazina kwa Taifa tuilinde hazina hii kwa uendelvu wa jamii yetu.Tuwatunze na kuwasikiliza wazee wetu.

  Imetolewa jana Tarehe 1/10/2016
  Dkt.Helen Kijo-Bisimba
  Mkurugenzi Mtendaji.

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Bukoba (DC) Deodatus Kinawiro (wa kwanza kushoto) akitembelea maeneo mbalimbali katika Chuo cha Ualimu cha Bukoba kinachomikiwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (BLTC) kinachomolikiwa na Dayosisi ya Kaskazini Magharibi ambapo wanafunzi wa kidato cha tano kutoka shule ya sekondari Ihungo wataenda kusoma wakati shule yao inajengwa upya baada ya kuharibiwa kwa tetemeko la ardhi lililotokea Septemba 10, mwaka huu. Wa kwanza kulia ni Mkufunzi katika chuo hicho Dafroza Protas.

  Mkuu wa Wilaya ya Bukoba (DC) Deodatus Kinawiro (wa kwanza kushoto) akitembelea maeneo mbalimbali katika Chuo cha Ualimu cha Bukoba kinachomikiwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (BLTC) kinachomolikiwa na Dayosisi ya Kaskazini Magharibi ambapo wanafunzi wa kidato cha tano kutoka shule ya sekondari Ihungo wataenda kusoma wakati shule yao inajengwa upya baada ya kuharibiwa kwa tetemeko la ardhi lililotokea Septemba 10, mwaka huu. Wa kwanza kulia ni Mkufunzi katika chuo hicho Dafroza Protas.  Mkuu wa Wilaya ya Bukoba (DC) Deodatus Kinawiro (wa pili kushoto) akikagua moja ya matanki ya kuhifadhia maji katika Chuo cha Ualimu cha Bukoba kinachomikiwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (BLTC) cha Dayosisi ya Kaskazini Magharibi ambapo wanafunzi wa kidato cha tano kutoka shule ya sekondari Ihungo wamehamishiwa kusoma wakati shule yao inajengwa upya baada ya kuharibiwa kwa tetemeko la ardhi lililotokea Septemba 10, mwaka huu. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Bukoba Mwantum Dau.

  …………………………………………………………………..

  Na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Bukoba

  Serikali imesema shule wanapohamishiwa wanafunzi wa kidato cha tano na cha sita baada ya shule za sekondari za Ihungo na Nyakato kuharibiwa na tetemeko la ardhi kuharibu miundombinu ya shule hizo Septemba 10 mwaka huu.

  Akizungumzia miundombinu ya Chuo cha Ualimu cha Bukoba kinachomikiwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (BLTC) kinachomolikiwa na Dayosisi ya Kaskazini Magharibi alipotembelea chuoni hapo, Mkuu wa Wilaya ya Bukoba (DC) Deodatus Kinawiro amesema kuwa mazingira wanapohamishiwa wanafunzi wa kidato cha tano kutoka shule ya sekondari Ihungo ni mazuri kwa kusomea yatawasaidia kupata elimu kama walivyokuwa kwenye shule yao ya Ihungo.

  “Mazingira ya chuo ni mazuri sana, Serikali inaendelea kufanya marekebisho madogo madogo maeneo mbalimbali ya chuo ikiwa ni pamoja na miundombinu ya maji ili wanafunzi waendelee na masomo bila adha yeyote itakayowakwamisha kupata elimu” alisema DC Kinawiro.

  DC Kinawiro ameongeza kuwa Serikali imechukua hatua za haraka za kunusuru athari ambazo zingeweza kuwapata wanafunzi ambao shule zao zimeathirika zaidi kwa tetemeko la ardhi ambapo imelazimu kuwahamishia wanafunzi hao shule nyingi huku shule zao za awali za Ihungo na Nyakato zikiwendelea kujengwa upya.

  Kuhusu kuwasili wanafunzi wa kidato cha tano katika chuo cha ualimu cha BLTC mwishoni mwa wiki hii, Mkuu huyo wa wilaya amesema kuwa walimu na wanafunzi hao wafike kwa wakati ili kuendelea na ratiba ya masomo bila kuchelewa hatua ambayo haitaathiri mtiririko wa kujifunza na kufundisha.

  Akizungumzia mgawanyo wa wanafunzi wa shule za Ihungo na Nyakato, Afisa Elimu wa Mkoa wa Kagera Aloyce Kamamba amesema kuwa shule wanapohamishiwa wanafunzi wa shule hizo mbili zipo tayari kuwapokea wanafunzi hao na walimu wao ili waendelee na masomo.

  Kuhusu mgawanyo wa wanafunzi katika shule walizopangiwa, Afisa Elimu Kamamba amesema kuwa wanafunzi wote wa kidato cha sita katika shule za Ihungo na Nyakato wamehamishiwa katika shule ya sekondari ya Omumwani ambapo wataendelea na masomo yao.

  Shule hiyo ipo manispaa ya Bukoba mjini na miundombinu ya shule hiyo inaruhusu wanafunzi wa kidato cha sita kuendelea na ikizingatiwa wapo darasa la mtihani wa taifa ambao kwao ni muda wa maandalizi ya mitihani pamoja na kusoma kwa vitendo.

  Kwa upande wa wanafunzi wa kidato cha tano kutoka shule ya sekondari Nyakato, Afisa Elimu Kamamba amesema kuwa wanafunzi wanaosoma tahasusi ya PCM ambao idadi yao ni 75 wamehamishiwa katika shule ya sekondari Kahororo, PGM wanafunzi 65 wamehamishiwa shule ya sekondari Biharamulo, CBG wanafunzi 95 wamehamishiwa shule ya sekondari Nyailigamba, HKL wanafunzi 30 wamehamishiwa shule ya sekondari Kishoju, HGK wanafunzi 30 wamehamishiwa shule ya sekondari Nyakahura na HGE wanafunzi 45 wamehamishiwa shule ya sekondari Nyakahura.

  Aidha, Afisa Elimu amewataka walimu na wanafunzi kitunza miundombinu ya shule wanazohamishiwa ili iendelee kuwasaidia wanafunzi katika kizazi cha sasa na kizazi kijacho na kuwahimiza walimu kutimiza wajibu wao wa kuwalea wanafunzi kitaaluma na kijamii kwa kuwa hiyo ndio kazi waliosomea.

  0 0


  0 0

  Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Mstaafu Damian Lubuva akieleza mkakati wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kutoa elimu ya Mpiga Kura kote nchini ili kuwajengea wananchi uelewa sahihi juu  majukumu ya Tume na  chaguzi zinazofanyika nchini.  Na.Aron Msigwa - NEC,Dar es salaam.


  Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Mstaafu Damian Lubuva amesema kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi itaendelea kutoa elimu ya Mpiga Kura kote nchini ili kuwajengea wananchi uelewa sahihi juu  majukumu ya Tume na  chaguzi zinazofanyika nchini.

  Akizungumza jijini Dar es Salaam Jaji Lubuva amesema baadhi ya wananchi wamekuwa wakishindwa kutimiza Haki yao ya Kikatiba ya kupiga Kura kuwachagua viongozi wananowapenda kwa sababu ya kukosa uelewa juu ya Sheria, Kanuni na taratibu zinazosimamia Uchaguzi .

  Amesema Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977 inaipa NEC jukumu la kusimamia na kuendesha Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani kwa upande wa Tanzania Bara  na kubainisha kuwa ili jukumu hilo lifanywe kwa ufanisi wananchi waliotimiza vigezo vya kupiga kura na wale wanaotarajia kupiga kura  miaka  ijayo lazima wapatiwe  elimu sahihi ya Mpiga Kura.

  Amefafanua kuwa baada ya kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani mwaka 2015, NEC ilianza kutekeleza programu mbalimbali ikiwemo kutoa elimu ya Mpiga Kura kuwafikia wananchi moja kwa moja kupitia mikutano mikubwa inayohusisha viongozi mbalimbali,   maonesho ya Sabasaba na  Nane Nane , kutoa elimu ya Mpiga kura kwenye vyombo mbalimbali vya habari pamoja na kuzitembelea baadhi ya shule za Sekondari za mkoa wa Singida na Mara.  

  " Moja ya shughuli za Tume ni kuendesha na kusimamia uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani nchi nzima kwa upande wa Tanzania Bara, ili shughuli hii tuifanye vizuri ni muhimu sana tuwapatie wananchi elimu sahihi juu ya upigaji wa kura, tutafanya jambo hili tukishirikiana na wadau na Asasi nyingine ambazo tutazipa  kibali cha kutoa elimu hii" Amesisitiza Jaji Lubuva.

  Jaji Lubuva amebainisha kwamba utoaji wa elimu hiyo utaongeza idadi ya wapiga kura kwenye chaguzi zijazo akitoa mfano wa idadi pungufu ya wapiga waliojitokeza kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 na ule uliofanyika Oktoba 25 , 2015 ambapo baadhi ya wananchi walioandikishwa kwenye daftari la kudumu la Wapiga Kura na kupewa vitambulisho hawakujitokeza kupiga kura.

  " Tunalenga kuongeza uelewa wa wananchi kuhusu majukumu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi pia umuhimu wa wananchi kushiriki Kupiga Kura, baadhi ya wananchi wamekuwa wakijitokeza ili wapate vitambulisho jambo ambalo sio sahihi,  mfano mwaka 2010 wananchi milioni 15 walijiandikisha kupiga kura lakini waliojitokeza kupiga kura ni milioni 8.626 hii ni idadi ya chini, pia  mwaka 2015 wananchi waliojiandikisha walikuwa milioni 23,161,440 lakini waliojitokeza Kupiga Kura ni watu milioni 15,589,639 hapa kuna ongezeko,  tunaamini tukiwapatia elimu wengi zaidi watajitokeza kuwachagua viongozi wanaowapenda " Amesitiza Jaji Lubuva.

  Amesema katika kuendelea kupanua wigo wa utoaji wa elimu ya Mpiga Kura kwa wananchi wengi zaidi NEC itashiriki Kongamano na maonesho ya Wiki ya Vijana yatakayoambatana na Maadhimisho ya Kumbukumbu ya Baba wa Taifa na Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru 2016 Oktoba 7 hadi 14, 2016 mkoani Simiyu ambapo pamoja na Mambo mengine watendaji na Maafisa wa Tume watatoa elimu ya Mpiga Kura kwa wananchi na kutembelea shule za Sekondari za mkoa huo.

  Aidha, ili kuboresha chaguzi zijazo ametoa wito kwa wananchi waendelee  kushirikiana na Tume kwa kujitokeza kwa wingi kuuliza maswali na kupata ufafanuzi wa hoja mbalimbali katika maeneo ambayo watendaji wa NEC watafika kutoa elimu ya Mpiga Kura.

  0 0

   Waziri wa habari, utamaduni,sanaa na michezo Mh. Mhe.Nape Moses Nnauye (katikati) Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira na Muungano Mh. January Makamba (kulia)pamoja na Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania,Ian Ferrao(kushoto)wakifatilia mpambano wa watani wa jadi Simba na Yanga wakati wa mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara, Uliofanyika jana kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam,ambapo timu hizo zilitoka suluhu 1-1.
   Watoto wanaokota mipira uwanjani(Ball boys)  wakionyesha mabango yenye ujumbe maalum wa wiki ya nenda kwa Usalama barabarani jana, wakati wa mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara kati ya simba na yanga uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam,ambapo timu hizo zilitoka suluhu 1-1.


  0 0

   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitembelea hospitali ya mkoa wa Dodoma
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoa maelekezo ya kuboresha usafi wa mazingira ya hospitali ya Mkoa wa Dodoma wakati alipoitembelea  hospitali hiyo. Kulia kwake ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Mhe. Jenista Mhagama.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoa maelekezo ya kuboresha usafi wa mazingira ya hospitali ya Mkoa wa Dodoma wakati alipoitembelea  hospitali hiyo. Kulia kwake ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa hospitali ya mkoa wa Dodoma baada ya kutembelea hospitali hiyo. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma  Mhe. Jordan Rugimbana.
    Baadhi ya watumishi wa hospitali ya mkoa wa Dodoma wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao baada ya kuitembelea hospitali hiyo
    Baadhi ya watumishi wa hospitali ya mkoa wa Dodoma wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao baada ya kuitembelea hospitali hiyo
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimjulia hali Bi. Fatuma Yassin wa Swaswa Dodoma wakati alipotebelea hospitali ya mkoa wa Dodoma. Kushoto kwake ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimjulia hali Bi. Magreth Kapinga  wa Mpwapwa wakati alipotembelea  hospitali ya mkoa wa Dodoma. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Watendaji  mbali mbali wa  Serikali mara alipowasili katika uwanja wa Ndege wa Karume Pemba alipohudhuria sherehe za Siku ya kilele cha Wazee Duniani zilizofanyika wilaya ya Chake chake katika viwanja vya nje Uwanja wa Gombani Pemba
   Baadhi ya Wazee waliohudhuria katika sherehe za Kilele cha Siku ya Wazee Duniani zilizofanyika katika viwanja vya nje Uwanja wa Gombani Wilaya ya Chake chake Mkoa wa Kusini Pemba
  Baadhi ya Wazee kutoka Mikoa ya Pemba waliohudhuria katika sherehe za Kilele cha Siku ya Wazee Duniani zilizofanyika katika viwanja vya nje Uwanja wa Gombani Wilaya ya Chake chake Mkoa wa Kusini Pemba
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Wazee alipowasili katika  sherehe za maadhimisho ya siku ya   Wazee Duniani zilizofanyika leo Wilaya ya Chake chake katika viwanja vya nje Uwanja wa Gombani Mkoa wa Kusini Pemba
   Mwakilishi wa Wazee Bw.Salum Ali Mata akisoma risala ya Wazee katika sherehe za maadhimisho ya siku ya   Wazee Duniani zilizofanyika lWilaya ya Chake chake katika viwanja vya nje Uwanja wa Gombani Mkoa wa Kusini Pemba
   Miongoni mwa Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar waliohudhuria katika sherehe za maadhimisho ya siku ya   Wazee Duniani zilizofanyika Wilaya ya Chake chake katika viwanja vya nje Uwanja wa Gombani Mkoa wa Kusini Pemba
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipokea risala ya Wazee kutoka kwa Mwakilishi wa Wazee Bw.Salum Ali Mata aliyoisoma katikasherehe za maadhimisho ya siku ya Wazee Duniani zilizofanyika  katika viwanja vya nje Uwanja wa Gombani Wilaya ya Chake chake Mkoa wa Kusini Pemba
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipokea taarifa ya Shirika la HELP AGE INTERNATIONAL Tanzania kutoka kwa Mkurugenzi Amleset Tewodoes mara baada ya kuisoma katika sherehe za maadhimisho ya siku ya Wazee Duniani zilizofanyika   katika viwanja vya nje Uwanja wa Gombani Wilaya ya Chake chake Mkoa wa Kusini Pemba

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Viongozi mbali mbali wa Chama na Serikali mara alipowasili katika uwanja wa Ndege wa Karume Pemba alipohudhuria sherehe za sikuya kilele cha Wazee Duniani zilizofanyika wilaya ya Chake chake katika viwanja vya nje vya Uwanja wa Gombani Pemba

  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameagiza apatiwe orodha ya wadaiwa sugu wa taasisi zote za Serikali mkoani Dodoma ambao wamelimbikiza deni la sh. bilioni 1.4 zikiwa ni bili zao za maji. 

  Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumapili, Oktoba 2, 2016) wakati akizungumza na watumishi na viongozi wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dodoma (DUWASA) mara baada ya kukagua utendaji kazi wa chanzo cha maji cha Mzakwe nje kidogo ya mji wa Dodoma.


  “Niletee haraka orodha ya wadaiwa wote wa Ofisi za Serikali na taasisi za umma ambao hawajalipa bili zao. Madeni yote ni lazima yalipwe,” amesema Waziri Mkuu.
   Waziri Mkuu ambaye yuko katika ziara ya siku mbili ya kukagua maandalizi ya Serikali kuhamia Dodoma, anatembelea sehemu mbalimbali za kutolea huduma za jamii pamoja na kukagua miundombinu ya mkoa huo. 

  Aliutaka uongozi wa DUWASA na watumishi wote wahakakishe wanaboresha huduma za upatikanaji wa maji hasa kwenye maeneo yanayopimwa viwanja ili wananchi au wawekezaji wanaponunua viwanja wakute huduma hiyo ipo na waanze ujenzi mara moja.

  “Tumealika wawekezaji, nataka wajenge viwanda na mahoteli hapa Dodoma, sasa wakikuta maji na umeme kwenye maeneo yao, itakuwa ni kichocheo cha kuharakisha kazi za ujenzi,” amesema.

  Pia amemwagiza Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Bi. Christina Mndeme ahakikishe eneo lililo jirani na chanzo hicho cha maji halikaliwi na mtu yeyote na linalindwa dhidi ya uchomaji mioto.

  “Uchomaji moto uoto wa asili umeharibu vyanzo vingi vya maji. Ni tatizo kubwa hapa nchini na halina budi kusimamiwa hadi liishe,” amesisistiza. 
  Amefikia uamuzi huo baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa DUWASA, Mhandisi David Pallangyo kwamba kuna wananchi wameanza kujenga na kufanya shughuli za kijamii jirani na chanzo hicho licha ya kuwa walikwishaondolewa zamani. 

  Kuhusu wadaiwa sugu, Mhandisi Pallangyo alisema mashirika ya umma na taasisi za Serikali ndiyo wanaongoza kwa kulimbikiza madeni. “Wananchi wa kawaida wapo wanaodaiwa lakini deni lao siyo kubwa na hao tunawamudu,” alisema wakati akizungumza na mwandishi wa habari hizi. 
  Alisema changamoto nyingine inayowakabili ni uchomaji moto ambapo hivi karibuni uliwashwa moto na kuunguza baadhi ya nguzo za umeme ambazo zinapeleka umeme kwenye chanzo hicho. 

  Alisema askari wa JKT Makutupora walisaidia kuzima moto huo ili usifike kwenye mitambo mingine ya chanzo hicho cha maji. 
  Waziri Mkuu pia alikagua maabara ya upimaji maji kwenye chanzo hicho kabla hayajasambazwa kwa wateja na mara yanapokuwa yamefika kwa wateja na kuelezwa kuwa maji hayo yanakidhi viwango vya kitaifa na vya kimataifa vilivyowekwa na Shirika la Afya Duniani (WHO). 

  Waziri Mkuu anaendelea na ziara yake kwa kutembelea kiwanda cha magodoro Dodoma na kituo cha kuzalisha umeme cha Zuzu.


  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU
  S. L. P. 980,
  DODOMA.
  JUMAPILI, OKTOBA 2, 2016

older | 1 | .... | 991 | 992 | (Page 993) | 994 | 995 | .... | 1898 | newer