Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46371 articles
Browse latest View live

WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU NCHINI WATOA MICHE YA MITI 600 KUUNGA MKONO KAMPENI YA UPANDAJI MITI JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano, Luhaga Mpina akipanda mti katika Shule ya Sekondani ya Mama Salma Kikwete, Jijini Dar es Salaam leo ikiwa ni kuunga mkono kampeni ya upanadaji miti Jijini Dar es Salaam iliyoanzishwa na Mkuu wa Mkoa huo Paul Makonda, Kampeni hiyo ijulikanayo kama "Mti Wangu" itazinduliwa kesho Oktoba Mosi na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan. Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania umechangia miche ya miti 600 katika shule hiyo na miche ya miti mingine 3,000 itatolewa kesho wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo kwa ajili ya Jijiji la Dar es Slaam, katika awamu ya pili watachangia tena miche ya miti 5,000.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano, Luhaga Mpina (wa pili kulia) akimkabidhi Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mama Salma Kikwete, Elestina Chanafi (wa pili kushoto) baadhi ya miche ya miti kati ya miche 600 iliyotolewa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kwa ajili ya shule hiyo kuunga mkono Kampeni ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ya upandaji wa miti Jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kulia ni Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Prof. Dos Santos Silayo.
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Prof. Dos Santos Silayo (kulia) akimkabidhi Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano, Luhaga Mpina (wa pili kulia) miche 600 ya miti iliyotolewa na ofisi yake kwa ajili ya shule ya Sekondani ya Mama Salma Kikwete Jijini Dar es Salaam leo ikiwa ni hatua ya kuunga mkono Kampeni ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ya upandaji wa miti Jijini Dar es Salaam ijulikanyo kama “Mti Wangu” . Katika uzinduzi huo TFS imechangia miche ya miti 3,000 kati ya miche 8,000 ambayo imepanga kutoa kwa ajili ya kupandwa katika Jiji la Dar es Salaam. 
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Prof. Dos Santos Silayo akizungumza na waandishi wa habari katika hafla hiyo.
Msanii wa Filamu nchini, Jackline Wolper (katikati) akizungumza na waandishi wa habari katika hafla hiyo kuhusu kampeni yake ya "Think Green" katika kuunga mkono Kampeni ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ijulikanayo kama "Mti Wangu" ambayo itazinduliwa kesho Oktoba Mosi na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan . Kulia ni Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano, Luhaga Mpina.
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Prof. Dos Santos Silayo (kushoto) akizungumza na wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Mama Salma Kikwete Jijini Dar es Salaam leo katika hafla fupi ya upandaji wa miti shuleni hapo kuunga mkono Kampeni ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ya upandaji wa miti, Prof. Silayo amewaasa wanafunzi hao kuwa mstari wa mbele katika utunzaji wa mazingira na upandaji wa miti. Katika hafla hiyo TFS wamekabidhi jumla ya miche ya miti 600.
Picha ya pamoja kati ya Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano, Luhaga Mpina (wa tano kushoto), Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Prof. Dos Santos Silayo (wa sita kushoto), Msanii Jackline Wolper, Watumishi na baadhi ya wanafunzi wa shule ya Sekondari Mama Salma Kikwete.
(Picha na Hamza Temba - Wizara ya Maliasili na Utalii)

TAASISI YA ADLG YABAINISHA SABABU ZA KUWEPO MAENDELEO DUNI KWENYE BAADHI YA VIJIJI VYENYE WAWEKEZAJI WA MADINI NCHINI.

$
0
0



Taasisi ya Demokrasia na Utawala bora nchini ADLG, imebainisha kwamba kukosekana kwa uwajibikaji miongoni mwa baadhi ya viongozi, kunasababisha maendeleo duni kwenye baadhi ya maeneo/vijiji yenye wawekezaji ikiwemo migodi.

Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Jimmy Luhende, ameyasema hayo leo kwenye mdahalo wa kila mwezi unaoendeshwa na taasisi hiyo kujadili masuala mbalimbali yanayohusu rasilimali asilia ikiwemo madini, gesi na mafuta.

Amesema katika tafiti zilizofanywa na taasisi hiyo katika vijiji mbalimbali vinavyozungukwa na migodi katika mikoa ya kanda ya ziwa, wamebaini kukosekana kwa huduma muhimu za kijamii ikiwemo zahanati, shule, miundombinu bora ya barabara pamoja na maji safi na salama.

Amesema taasisi hiyo imeanzisha midahalo mbalimbali inayowahusisha wananchi pamoja na viongozi katika vijiji 147 vya mikoa minne ya kanda ya ziwa yenye uwekezaji wa madini ili kuwajengea uwezo wananchi kutumia uwekezaji ulio kwenye maeneo yao kurahishisha maendeleo.

Afisa Miradi (Sheria na Mikataba) kutoka taasisi ya ADLG, Carolina Tizeba, amesema katika tafiti zilizofanywa na taasisi hiyo kwenye Vijiji vinne vya Nyenze, Ikonongo, Songwa na Maganzo katika Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, umebaini kuwepo kwa ushiriki mdogo wa wananchi pamoja na uwajibikaji wa viongozi wao katika masuala ya uwekezaji wa madini jambo ambalo linasababisha kushindwa kufuatilia manufaa ya uwekezaji katika vijiji vyao na hivyo kuchangia kuwepo kwa huduma duni za kijamii katika vijiji hivyo ambavyo kuna wawekezaji wa madini.
Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Jimmy Luhende, akizungumza jambo kwenye mdahalo huo uliofanyika Isamilo Jijini Mwanza.
Nicholaus Ngelea ambaye ni Afisa Miradi ADLD, akiwasilisha mada kwenye mdahalo huo uliofanyika Isamilo Jijini Mwanza.
Carolina Tizeba ambaye ni Afisa Miradi (Sheria na Mikataba) ADLG, akiwasilisha taarifa ya utafiti uliofanywa na taasisi hiyo kwenye vijiji vinavyozungukwa na migodi mkoani Shinyanga.
Washiriki mbalimbali wakiwemo Wanahabari, Taasisi za Utawala bora, wachumi, wanamazingira na watafiti mbalimbali wakiwa kwenye mdahalo huo.
Washiriki mbalimbali wakiwemo Wanahabari, Taasisi za Utawala bora, wachumi, wanamazingira na watafiti mbalimbali wakiwa kwenye mdahalo huo.
Mshiriki akichangia mada
Mshiriki akichangia mada
Washiriki mbalimbali wakiwemo Wanahabari, Taasisi za Utawala bora, wachumi, wanamazingira na watafiti mbalimbali wakiwa kwenye mdahalo huo.
Washiriki mbalimbali wakiwemo Wanahabari, Taasisi za Utawala bora, wachumi, wanamazingira na watafiti mbalimbali wakiwa kwenye mdahalo huo.

Washiriki wa mdahalo huo
Washiriki mbalimbali wakiwemo Wanahabari, Taasisi za Utawala bora, wachumi, wanamazingira na watafiti mbalimbali wakiwa kwenye mdahalo huo.

Washiriki mbalimbali wakiwemo Wanahabari, Taasisi za Utawala bora, wachumi, wanamazingira na watafiti mbalimbali wakiwa kwenye mdahalo huo.
Washiriki mbalimbali wakiwemo Wanahabari, Taasisi za Utawala bora, wachumi, wanamazingira na watafiti mbalimbali wakiwa kwenye mdahalo huo.
Bonyeza HAPA Kwa Mdahalo uliopita. Imeandaliwa na BMG.

PROF. MBARAWA AAGIZA UJENZI WA BARABARA YA JUU KUKAMILIKA KWA WAKATI.

$
0
0
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (Tanroads), Eng. Patrick Mfugale(Wa kwanza kulia) akitoa maelezo ya ramani ya Ujenzi wa barabara za maingiliono (Tazara Flyover) kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa( Wa kwanza kushoto) wakati alipokagua ujenzi huo Jijini Dar es salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (Wa pili kushoto) akitoa maelekezo kwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (Tanroads), Eng. Patrick Mfugale (Kulia kwake) wakati alipokagua ujenzi wa barabara za maingiliono (Tazara Flyover, Jijini Dar es salaam.


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (Katikati), akifafanua jambo mara baada ya kukagua daraja la wapiti kwa miguu lilopo Buguruni Jijini Dar es salaam. Kulia ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (Tanroads), Eng. Patrick Mfugale na Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa barabara wa Wizara Eng. Light Chobya.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akisalimiana na Wananchi mara baada ya kumaliza kukagua daraja la wapiti kwa miguu lililopo Buguruni Jijijni Dar es salaam.
…………………………………………………………..

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ameitaka Kampuni ya kikandarasi ya Sumitomo Mitsui inayojenga mradi wa ujenzi wa barabara ya juu (Flyover) katika makutano ya barabara ya Nyerere na Mandela eneo la Tazara kumaliza ujenzi huo kwa wakati mradi huo ili kusaidia kupunguza tatizo la msongamano.

Akizungumza mara baada kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi huo jijini Dar es salaam, Profesa Mbarawa amesema kuwa kukamilika kwa mradi huo kutajenga historia nchini kutokana na kuwa ni wa mwanzo kujengwa.

“Nimefurahi kuona mradi huu upo katika hatua nzuri, naomba mkamilishe mradi huu unakamilika kwa ubora na kwa wakati ili tatizo la msongamano lililopo katika maeneo haya kupungua au kuisha kabisa”, amesema Waziri Mbarawa.

Profesa Mbarawa amemtaka Mkandarasi kuhakikisha kuwa anafanya kazi kwa umakini na kwa uangalifu wakati wa kipindi chote cha ujenzi ili kuitokuweza kusababisha foleni katika eneo hilo. Aidha, Waziri Mbarawa amewataka wananchi wa maeneo hayo kutoa ushirikiano kwa Mkandarasi huyo ili kurahisisha kazi za ujenzi huo kukamilika kwa wakati na kupata matokeo chanya.

“Nawaomba watanzania wenzangu kuwa wavumilivu na usumbufu wowote utakaojitokeza katika kipindi hiki chote, kwani ukamilifu wa mradi huu utasaidia kupunguza tatizo la msongamano katika barabara hizi”, amefafanua Waziri Mbarawa.

Katika hatua nyingine, Profesa Mbarawa amekagua daraja la watembea kwa miguu eneo la Buguruni Sheli na kuwataka wananchi wa maeneo hayo kulitunza daraja hilo ambalo uwepo wake umesaidia kupunguza ajali katika maeneo hayo.

“Ni matumaini yangu sasa wakazi wa maeneo haya mtavuka kwa amani kupitia daraja hili, na ajali zilizokuwa zikitokea maramara hazitakuwepo tena”’, amesema Profesa Mbarawa.

Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Eng. Patrick Mfugale amemuahidi Waziri huyo kumaliza kwa wakati ujenzi huo na kumhaakikishia Waziri kuwa ujenzi wa barabara hiyo utakuwa na viwango vilivyo bora.

Mradi wa Tazara Flyover ni msaada kutoka Serikali ya Japan ambao umegharimu shilingi bilioni 93.4 na unatarajiwa kukamilika mwezi Oktoba mwaka 2018.

WAZIRI MKUU ATIMIZA AHADI YA KUHAMIA DODOMA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakiwapungia akiwapungia wananchi wa Dodoma baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma Septemba 30, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea ufunguo ikiwa ni ishara ya kukaribishwa Dodoma na Meya wa Manispaa ya Dodoma Jafar Mwanyemba katika mapokezi yaliyofanyika kwenye makazi yake , Mlimwa Septemba 30, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akionyesha ufunguo aliokabidhiwa na Meya wa Manispaa ya Dodoma, Jafar Mwanyemba (kushoto) kuashiria kupokewa rasmi kwenye manispaa hiyo. Makbidhiano hayo yalifanyika kwenye makazi yake eneo la Mlimwa Septemba 30, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na wazee wa Dodoma baada ya kukaribishwa kimira na wazee hao Septemba 30, 2016.
Mke wa Waziri Mkuu, Mary Majaliwa akizawadiwa kimira na wanawake wa Dodoma ikiwa ni ishara ya kumkaribisha karika Manispaa hiyo, Septemba 30, 2016.
Mke wa Waziri Mkuu, Mary Majaliwa akizawadiwa kimira na wanawake wa Dodoma ikiwa ni ishara ya kumkaribisha karika Manispaa hiyo, Septemba 30, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa na mkewe Mary wakiagana na watuimishi wa Makazi ya Waziri Mkuu ya Dar es salaam kabla ya kuondoka kuelekea Dodoma Septemba 30, 2016
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakisalimiana na Madiwani wa Manispaa ya Dodoma baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma Septemba 30, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakisalimiana na Madiwani wa Manispaa ya Dodoma baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma Septemba 30, 2016.

Waziri Mkuu, Kasim Majliwa akiwapungia wananchi baada ya kuwasili kwenye makazi yake mjini Dodoma Septemba 30, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Wananchi wa Dodoma wakimshangilia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye makazi yake eneo la Mlimwa Septemba 30, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)



Waziri MKUU Kassim Majaliwa amesema kuanzia sasa mtu yeyote mwenye shida ya kuonana naye itabidi amfuate Dodoma na kwamba atarudi Dar es Salaam pindi akiitwa na Mheshimiwa Rais au Makamu wa Rais.


Ametoa kauli hiyo leo jioni (Ijumaa, Septemba 30, 2016) wakati akizungumza na viongozi mbalimbali na wakazi wa mji wa Dodoma waliofika kumpokea mara baada ya kuwasili mjini hapa ikiwa ni utekelezaji wa ahadi yake aliyoitoa Julai 25 kuwa atahamia Dodoma ifikapo Septemba mwaka huu.



“Tukio hili la kuhamia Dodoma si la mzaha, hakuna siasa na wala si jaribio. Tumeshakeleza. Kama kuna waliokuwa wanafiria kwamba halitekelezeki watambua kwamba tayari tumeshafika. Na kuanzia sasa atakayetaka huduma ya Waziri Mkuu



Waziri Mkuu amesema Dodoma si ndogo kama baadhi ya watu wanavyodai na kwamba  huduma zilizopo zinatosha kukidhi mahitaji ya sasa. "Mkakati uliopo wa kupanua huduma za tiba, maji, umeme na masoko utawezesha watumishi wote kuishi bila bugudha yoyote."


“Awamu ya kwanza inaanzia Septemba hadi Februari mwakani. Mimi nimeshatangulia na wanaofuata ni mawaziri na manaibu wao wote, Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu wote. Natambua kwamba wote wana nyumba za kuishi na kama wapo ambao hawana hawazidi asilimia tano na nyumba zipo



Amewataka watumishi wote wa Serikali watambue kwamba safari imeshaanza na kila mmoja ajipange, na akarudia wito wa Mheshimiwa Rais kwamba atakayegoma kuhamia Dodoma atakuwa amejifukuza kazi.



Waziri Mkuu amewataka watendaji wa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu Dodoma (CDA) wasifanye kazi kwa mazoea, bali wabadilike na kwa kuwa amehamia Dodoma ameahidi kuafuatilia kwa karibu zaidi.



Mapema akizungumza katika hafla hiyo, Waziri wa Nchi (OWM SUBKAV), Jenista Mhagama amesema kilichofanyika leo ni uthibitisho kuwa yale ambayo Serikali ya Awamu ya Tano iliahidi sasa hivi imeanza kuyatekeleza.


"Tuliahidi kukusanya kodi, tuliahidi elimu bure, tuliahidi kupambana na mafisadi, tuliahidi kuondoa watumishi hewa, tuliahidi kuifufua ATCL na kununua ndege mpya na yote tumetekeleza,” amesema.



Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Bw. George Simbachawene amesema uamuzi wa kuhamia Dodoma ni uthibitisho kuwa  viongozi wetu kweli wamedhamiria kutekeleza ahadi ya Baba wa Taifa ya kuhamishia makao makuu ya nchi hapa Dodoma.


"Dodoma imeanza kuchangamka na hii ni fursa tosha kwa mkoa wetu kubadilika. Tushirikiane na CDA kuijenga Dodoma mpya. Kitendo cha Mheshimiwa Waziri Mkuu kuingia Dodoma leo hii maana yake ni kwamba Serikali iko rasmi Dodoma," amesema.



Hafla hiyo ilihudhuriwa na Manaibu Waziri Anthony Mavunde na Dk. Ashatu Kijaji, Makatibu Wakuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Rais (Utumishi), Wakuu wa Wilaya za Mkoa huo, wazee wa mkoa huo, viongozi wa dini, viongozi wa taasisi zilizoko mkoani na baadhi ya wananchi.






IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU,

S. L. P. 980,

DODOMA

IJUMAA, SEPTEMBA 30, 2016.

KATIBU TAWALA WILAYA YA CHEMBA AZINDUA MASHINDANO YA DIWANI CUP,MSHINDI KUJINYAKULIA MBUZI BEBERU.

$
0
0
Baadhi ya Washiriki na Washabiki wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye ufunguzi wa mashindano ya Diwani Cup wilayani Chemba mapema leo,ambapo mashindano hayo yamefunguliwa rasmi na Katibu Tawala wa wilaya hiyo,ambaye ni Mweyekiti wa kamati ya michezo,Ndugu Nyakia Ally (hayupo pichani).

Katibu Tawala wa Wilaya kama Mwenyekiti wa Kamati ya Michezo ya Wilaya Ndugu Nyakia Ally,amefungua mashindano
ya Diwani Cup hapa Chemba,huku akiwasihi vijana kucheza mpira wa miguu wakitambua kuwa kwa sasa ni ajira inayolipwa kwa pesa nyingi kulinganisha na michezo mingine hapa nchini.  

 Ndugu.Nyakia alieleza kuwa mashindano hayo yameandaliwa na Diwani wa Kata ya Chemba, Mhe Joseph Saini ambapo yanashirikisha timu sita kutoka katika Vijiji vitatu vinavyounda Kata ya Chemba.

Mshindi wa mashindano hayo atajinyakulia zawadi ya Mbuzi beberu,Katika mashindano hayo yatakayokuwa ya kusimumua wilayani humo,Katibu Tawala wa Wilaya hiyo Ndugu Nyakia Ally ameahidi kuongeza zawadi ya mipira miwili kwa mshindi wa kwanza, mpira mmoja kwa mshindi wa pili na watatu. 

 Vile vile Katibu Tawala huyo aliwataka vijana kushirikiana katika mashindano hayo bila kujali Itikadi zao za kisiasa, dini wala rangi kwani michezo hujenga Udugu, urafiki na upendo miongoni mwa wapenzi wa michezo husika.

Pamoja na hayo Ndugu Nyakia amemtaka Afisa Utamatuduni wa Wilaya hiyo kushirikiana na Waratibu wa mashindano hayo ili kupata timu nzuri miongoni mwa wachezaji wanao shiriki ligi hiyo,ili hatimaye kupata wachezaji watakao kuwa waanzilishi wa timu ya Wilaya ya Chemba, ili siku za usoni washindane na Wilaya nyingine za hapa Dodoma na baadae Kitaifa na kimataifa kwa kushiriki Soka la kiushindani katika ligi mbalimbali.

Rais Magufuli afunga Maadhimisho ya Miaka 52 ya JWTZ ashuhudia Zoezi Amphibious Landing Bagamoyo

$
0
0
Amiri  Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Magufuli akipiga ngoma za bendi ya jeshi ya Mwenge Jazzz wana Paselepa wakati  wa kufunga Zoezi la medani katika kilele cha maadhimisho ya miaka 52 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) huko Baatini, Bagamoyo mkoa wa Pwani leo Septemba 30, 2016
 Amiri  Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Magufuli, Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein na meza kuu wakipiga saluti wakati wa wimbo wa Taifa wakati wa kufunga Zoezi la medani katika kilele cha maadhimisho ya miaka 52 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) huko Baatini, Bagamoyo mkoa wa Pwani leo Septemba 30, 2016
 Ndege vita zikipita angani katika kilele cha maadhimisho ya miaka 52 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) huko Baatini, Bagamoyo mkoa wa Pwani leo Septemba 30, 2016
 Vifaru vinavyopita baharini na nchi kavu vikiwa katika zoezi la "Ambhibious Landing" katika kilele cha maadhimisho ya miaka 52 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) huko Baatini, Bagamoyo mkoa wa Pwani leo Septemba 30, 2016
Amiri  Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Magufuli, Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein na meza kuu wakipiga makofi wakati wa Zoezi la medani katika kilele cha maadhimisho ya miaka 52 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) huko Baatini, Bagamoyo mkoa wa Pwani leo Septemba 30, 2016.PICHA NA IKULU.


  
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 30 Septemba, 2016 amefunga maadhimisho ya miaka 52 ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kwa kushuhudia zoezi la medani liitwalo ''Amphibious Landing'' lililofanyika katika Kijiji cha Baatini Wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani.


Zoezi hilo lililochukua muda wa wiki mbili, limeshirikisha kamandi zote tano za JWTZ  ambazo ni Nyika, Majini, Anga, Kamandi ya Makao Makuu na  Jeshi la Kujenga taifa limefanyika katika ufukwe wa bahari ya Hindi na limetekelezwa kwa mfano wa mapambano ya kivita yaliyohusisha kutua nchi kavu kutoka majini na kukomboa eneo lililotekwa.


Akizungumza baada ya kukamilika kwa zoezi hilo Rais na Amiri jeshi Mkuu Dkt.John Pombe Magufuli amempongeza Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange pamoja na Makamanda na Wapiganaji wote wa JWTZ walioshiriki katika zoezi hilo ambalo limefanywa kwa umakini, uhakika na weledi wa hali ya juu.


''Kwa kweli nimefurahi na nimeamini tuna wapiganaji wa kutosha katika maeneo yote, hii mikakati na mipango iliyotumika inaonesha tuna jeshi imara na linaloaminika''amesema Dkt. Magufuli.  


Rais na Amiri Jeshi Mkuu amewahakikishia Makamanda na Wapiganaji wote wa JWTZ kuwa Serikali yake itahakikisha inaendeleza na kuongeza zaidi juhudi zilizofanywa na Marais waliopita kwa kuimarisha na kuwa na jeshi la kisasa linalotumia vifaa na teknoljia ya kisasa na pia itahakikisha maslai ya askari yanaboreshwa.


Aidha, Dkt. Magufuli ametaka Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kuimarishwa zaidi na kujielekeza katika uzalishaji mali ikiwemo uwekezaji katika viwanda.


Maadhimisho hayo yamehudhuriwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein ambaye pamoja na kuipongeza  JWTZ amesema miaka 52 tangu kuanzishwa kwa Jeshi hilo Watanzania wanashuhudia jeshi lao likiwa imara na makini zaidi kwa ajili ya kulinda nchi.


Nae Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange amemshukuru Rais na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli kwa jitihada zake na nia yake ya kuliimarisha Jeshi na kuboresha maslai ya Makamanda na Wapiganaji na ameongeza kuwa anajivunia kuwa kiongozi  wa Jeshi hilo.


Maadhimisho hayo yamehudhuriwa na Viongozi wengine wakiwemo Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi na Katibu Mkuu Kiongozi wa Zanzibar Abdulhamid Yahaya Mzee.


Rais na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli, amemuagiza Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange kuwapa ajira za JWTZ askari mgambo wote walioshiriki zoezi la Amphibious Landing.





Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Dar es Salaam

30 Septemba, 2016

RC MONGELLA AFUNGUA MKUTANO WA ROBO MWAKA WA CHAMA CHA MAJAJI NA MAHAKIMU MIKOA MWANZA NA GEITA.

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe.John Mongella, akizungumza kwenye Ufunguzi wa Mkutano wa Robo Mwaka wa Chama cha Majaji na Mahakimu JMAT, tawi la Mwanza na Geita, unaofanyika leo kwenye ukumbi wa jengo la NSSF Jijini Mwanza.

Mongella amewataka wajumbe wa mkutano huo kujadili kwa uwazi masuala ya maadili kwa watumishi wa umma na kwamba yawe ajenda ya kudumu katika ngazi mbalimbali za utendaji serikalini hususani katika ngazi ya mahakama.

Amesisitiza mkutano huo kutoka na maadhimio yanayohimiza mahakama kutenda haki na kuleta manufaa kwa wananchi na kuondokana na malalamiko kwamba mahakama hazitendi haki katika maamuzi yake.

Mwenyekiti wa JMAT tawi la Mwanza, Francis Kishenyi, ambaye pia ni Hakimu Mkazi Mfawidhi Wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza, chama hicho kinahakikisha watumishi wa mahakama wakiwemo Majaji na Mahakimu wanafanya kazi kwa kutenda haki na kuwafanya wananchi kutambua umuhimu wa chombo hicho katika utoaji wa haki.

Pamoja na mambo mengine, mkutano huo unajadili masuala mbalimbali ikiwemo maadili ya viongozi wa Umma. 
Na BMG
Jaji Mfawidhi Kanda ya Ziwa, Mhe.Robert Makaramba, akizungumza kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti wa JMAT tawi la Mwanza, Francis Kishenyi, ambaye pia ni Hakimu Mkazi Mfawidhi Wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza, akizungumza na wanahabari nje ya mkutano huo.
Hakimu Mkazi Mwandamizi, Mfawidhi mkoani Mwanza, Mhe.Wilbert Martin Chuma, akizungumza kwenye mkutano wa robo Mwaka wa Chama cha Majaji na Mahakimu mikoa ya Mwanza na Geita, unaofanyika leo Jijini Mwanza.
Viongozi mbalimbali wakiwa meza kuu kwenye mkutano huo
Viongozi mbalimbali wa vyombo vya Ulinzi na Usalama mkoani Mwanza, wakiwa kwenye mkutano huo.
Viongozi mbalimbali kutoka Shirika la Taifa la Hifadhi ya jamii NSSF mkoani Mwanza, wakiwa kwenye mkutano huo.
Wajumbe wa mkuatno huo
Katibu wa JMAT ambaye pia ni Hakimu Mkazi mkoani Mwanza, Bittony Mwakisu (kulia) akiwa pamoja na Domician Mlashani, Hakimu Mkazi Mahakama ya Mwanzo wilayani Sengerema na mjumbe wa Kamati tendaji JMAT (kushoto).
Picha ya pamoja
Viongozi mbalimbali kwenye picha ya pamoja
Picha ya pamoja
Pamoja na mambo mengine, mkutano huo unajadili masuala mbalimbali ikiwemo maadili ya viongozi wa Umma. 

WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU TANZANIA WACHANGIA MICHE YA MITI 3000 KWENYE KAMPENI YA UPANDAJI MITI DAR ES SALAAM

$
0
0
Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania -TFS imechangia miche ya miti 3,000 katika Kampeni ya Upandaji Miti Jijini Dar es Salaam iliyozinduliwa leo na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan.

Akizungumza na vyombo vya habari Jijini Dar es Salaam jana, Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Prof. Dos Santos Silayo alisema hatua hiyo ni kuunga Mkono Kampeni ya Mkuu wa Mkoa huo, Paul Makonda ambayo imetambuliwa kwa jina la "Mti Wangu" kwa ajili ya kupendezesha na kuhifadhi Mazingira ya Jiji hilo.

"Sisi Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania tuna jukumu la kuanzisha na kusimamia misitu na rasilimali zake nchini, katika kumuunga Mkono Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwenye upandaji wa miti, tumetoa miche ya miti 3,000 katika uzinduzi wa kampeni hiyo, na miche mingine 5,000 tutaitoa kwa ajili ya kupandwa wakati wa masika, tunaomba wananchi wajitokeze kwa wingi na kutuunga mkono katika kampeni hizi za upandaji wa miti" alisema prof. Dos Santos.

Awali akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mama Salma Kikwete, Kijitonyama Jijini Dar es Salaam ambapo pia alikabidhi miche mingine ya miti 600 kwa ajili ya shule hiyo, Kaimu Mtendaji Mkuu huyo aliwaasa wanafunzi hao kuwa mstari wa mbele katika kupenda mazingira, kupanda miti na kuitunza. Pia aliiasa jamii kwa ujumla kuacha mara moja uharibifu wa misitu kwakuwa ni kinyume cha sheria.

Naye Naibu Waziri katika Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano, Luhaga Mpina akizungumza na waandishi wa habari katika tukio hilo, alisema asilimia 61 ya nchi inakaribia kuwa jangwa kutokana na uharibifu wa mazingira unaosababishwa na ukataji wa miti kwa ajili nishati ya mkaa na rasilimali nyingine za misitu.

"Takriban hekta laki 3.72 za msitu kwa mwaka zinaharibiwa hapa nchini jambo linalopelekea asilimia 61 ya ardhi kuwa hatarini kuwa jangwa hivyo Serikali imeamua kuchukua hatua za makusudi kunusuru hali hiyo" alisema.

Akizungumzia hatua hizo za Serikali alisema umeandaliwa mpango wa miaka mitano wa kitaifa wa upandaji miti ambapo kila Wilaya nchini imepangiwa kupanda miti milioni 2 kwa mwaka.

Mpina alisema kuwa baadhi ya viongozi wa vijiji na halmashauri wamekua wakifanya kazi kwa mazoea kwa kutoa taarifa za uongo kuhusu kazi za upandaji wa miti katika maeneo yao, hivyo kuahidi kutembelea kila Mkoa na Wilaya kuona kama kweli miti inayotolewa na Serikali inapandwa ipasavyo.

"Sitokubali kuona Ilani ya uchaguzi ikichakachuliwa na baadhi ya viongozi wasio waadilifu, tutafuatilia kila Wilaya na Mkoa kuona kama agizo hilo linatekelezwa" alisema Mpina.

Aliongeza kuwa mpango mwingine ya Serikali ni kupeleka nishati ya gesi kwenye kaya zaidi ya milioni 30 nchini ili ziondokane na matumizi ya mkaa kunusuru misitu na mazingira. Alisema kuwa mpango huo utazishirikisha Wizara mbalimbali ikiwemo Nishati na Madini.

Alitoa wito kwa wananchi kushirikiana na Serikali katika zoezi la upandaji wa miti kutunza mazingira na kuepuka uharibifu wa misitu.


Hamza Temba
Wizara ya Maliasili na Utalii
0713635204

BONGO MOVIE SHINYANGA WAMETULETEA FILAMU YA KIMATAIFA "NYAMA YA ULIMI"

$
0
0
Bongo Movie Shinyanga inakuletea filamu ya kusisimua,kutisha,kuhuzunisha,kufurahisha,kuonya na kuelimisha inaitwa“Nyama ya Ulimi”. 

Nyama ya Ulimi ni filamu matata yenye kiwango cha kimataifa kutoka kwa waigizaji waliobobea katika sanaa ya uigizaji mkoani Shinyanga na itazinduliwa hivi karibuni kwani kila kitu kimekamilika,angalia hapo chini nimeamua kukuonjesha walau kwa picha 8 na video fupi kukuweka mkao wa kula kupokea kazi nzuri ya wasanii kutoka Shinyanga. 

Filamu hii ya kiafrika pamoja na mambo mengine inazungumzia kwa kina masuala ya ukatili wa kijinsia/manyanyaso wanayofanyiwa wanawake katika ndoa na jamii kwa ujumla. Filamu hii inamfanya binadamu yeyote katili kwa wanawake awe na adabu kwa wanawake wote duniani lakini pia inamfanya mwanamme asiyejielewa apate akili timamu kabla ya kujutia kauli zake chafu kwa wanawake. 

Mwongozaji mkuu/Director wa Filamu hii ,David Skela amesema Filamu ya“Nyama ya Ulimi” yenye scene 20 imechezwa na wasanii kutoka Shinyanga. “Project inaonesha mkoa wa Shinyanga na Tabora,ujumbe unafikia dunia nzima,wahusika wakuu wapo wane ambao ni Songoro Gaddafi “Songoro”,Charles Sunday,Mariam Billal “Mercy” na Siha Mtui “Siha”,tunaomba watanzania na wapenzi wa filamu duniani kote waipokee filamu hii,ambayo inaonesha kiasi gani wanaume wenye pesa na wasio na pesa wanavyonyanyasa wanawake katika ndoa zao”,amesema Skela.  

Akizungumza na Malunde1 blog ,mwenyekiti wa Bongo Movie mkoa wa Shinyanga bwana Juma Ibrahim Songoro amesema filamu hiyo iko tayari na itazinduliwa rasmi hivi karibuni wanachofanya sasa ni kutafuta wadhamini wa filamu yao ya “Nyama ya Ulimi” ambayo wanaamini itafikisha ujumbe dunia nzima kuwa sasa ukatili wa kijinsia hasa kwa wanawake sasa unatosha. 

"Kauli mbiu tuliyotumia katika Filamu hii,ambayo itazinduliwa muda wowote kuanzia sasa ni "Kwa pamoja tunaweza kutokomeza Unyanyasaji kwa wanawake",tunaamini itapokelewa siyo tu kitaifa bali ni kimataifa",amesema Songoro. Ninazo hapa baadhi ya picha na video fupi ikionesha walau kidogo mambo mazito yaliyomo katika Filamu/Movie ya “Nyama ya Ulimi”Songoro Gaddafi
Mercy
Charles Sunday Mercy Songoro Siha Songoro
Nimeamua kukuonjesha kidogo...Naomba utumie dakika zako mbili tu kutazama"Filamu ya Nyama ya Ulimi"
Bonyeza hapa chini
 

MAZOEZI YA SERENGETI BOYS WAKIJIANDAA NA MCHEZO WA JUMAPILI DHIDI YA CONGO BRAZAVILLE

$
0
0
Libero wa Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 – Serengeti Boys, Ally Msengi (Kulia) akimiliki mpira huku Mshambuliaji wa timu hiyo, Ibrahim Abdallah akipigia hesabu mpira huo wakati wa mazoezi yaliyofanyika leo kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Alphonse Massamba-Débat – Rais wa zamani wa Congo kabla ya mchezo wa Jumapili. 
bra6
Baadhi ya vigogo wa Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 – Serengeti Boys, kutoka kushoto ni Dk. Gilbert Gilbert Kigadye, Mratibu wa timu, Pelegrinus Rutayuga na Dk. Sheicky Mngazija wakifuatilia mazoezi hayo kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Alphonse Massamba-Débat – Rais wa zamani wa Congo kabla ya mchezo wa Jumapili.
bra7
Kipa Na. 1 wa Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 – Serengeti Boys, Ramadhani Kabwili akifanya vitu vyake kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Alphonse Massamba-Débat – Rais wa zamani wa Congo kabla ya mchezo wa Jumapili.
bra1
“CONGO TUTAWAZIKA HAPA”Ndivyo anavyoonekana kusema Mshauri wa Maendeleo ya soka la Vijana, Kim Poulsen (kushoto) akimwelezea Mkuu wa Msafara wa Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 – Serengeti Boys, Ayoub Nyenzi kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Alphonse Massamba-Débat – Rais wa zamani wa Congo. Uwanja huo ulioko kwenye Makutano ya Barabara za Nkolo na Boko, hapa jijini Brazzaville ndio utakaotumika kwa ajili ya mchezo wa kuwania kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kati ya Tanzania na Congo, Jumapili Oktoba 2, 2016.
bra2
Huyo ndiye Muhsin Malima Makame au unaweza ukamwita ‘Super Sub’ wa Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 – Serengeti Boys, akikokota mpira kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Alphonse Massamba-Débat – Rais wa zamani wa Congo kuonyesha uwezo wake uwanjani pindi anapoingia kipindi cha pili kuokoa jahazi. Akikosa kufunga huwa ni kama bahati mbaya.
bra3
Beki wa kushoto wa Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 – Serengeti Boys, Nickson Kibabage akimdhibiti Kelvin Nashon wakati wa mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika leo kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Alphonse Massamba-Débat – Rais wa zamani wa Congo kabla ya mchezo wa Jumapili.
bra4
Kiungo wa Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 – Serengeti Boys, Kelvin Nashon ‘akisepa na kijiji cha mabeki’ wakati wa mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika leo kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Alphonse Massamba-Débat – Rais wa zamani wa Congo kabla ya mchezo wa Jumapili.

JOZI LOUNGE YADHAMINI MISS TANZANIA 2016

$
0
0
Club maarufu kwa jina la Jozi Lounge iliopo msasani jijini Dar Es Salaam, imejitokeza hivi karibuni kujiunga na moja katika kampuni na taasisi zilizokwisha kujitokeza kudhamini zoezi zima la kutafuta mrembo wa tanzania atakayepeperusha na kuitangaza Tanzania katika anga za kimataifa katika Nyanja mbalimbali yakiwemo utalii na huduma ya jamii yenye mahitaji maalum.

Akizungumza na warembo kutoka mikoa yote Tanzania ambao wanatarajia kuchuana vikali mwishoni mwa mwezi wa kumi huko jijini Mwanza na hatimaye kumpata mshindi wa Miss Tanzania 2016, Mkurugenzi wa Jozi Lounge Bw.Dismas Massawe amesema Jozi Lounge itawadhamini warembo hao kwa kuwapatia malazi, chakula na mahitaji mengine muhimu kwa kipindi cha siku tatu ambapo jana ilikuwa uzinduzi na leo ni siku ya semina mbalimbali na siku ya jumapili itakuwa siku ya kusherehekea ushindi wa mikoa tayari kuelekea katika mapambano ya ngazi ya Taifa.
Washiriki wa shindano la Miss Tanzania 2016 wakiwa katika moja ya pozi jana mara baada ya kuwasili Jozi Lounge, ambapo watakuwa hapo kwa siku tatu mfululizo. Jozi lounge ni mojawapo wa wadhamini wa mashindano ya miss tanzania mwaka huu 2016
 Wakipata vinywaji kwa pamoja huku wakifurahia utulivu mwanana ndani ya Jozi Club
Baadhi ya Washiriki wa shindano la Miss Tanzania 2016,ambapo jana wameingia kambini pia walipata muda wa kuserebuka ndani ya Club maarufu kwa jina la Jozi Lounge iliopo msasani jiji Dar EsSalaam.

 Washiriki wa Miss Tanzania 2016 wakiserubuka ndani ya Jozi Club kwa raha zao

PICHA MBALIMBALI ZA WASHIRIKI WA SHINDANO LA MISS TANZANIA WALIPOTEMBELEA MAENEO MBALIMBALI JIJINI DAR

$
0
0
Mkurugenzi wa Kampuni ya Tomoni, wauzaji wa mbogamboga za majani, nyama, vyakula na juisi za matunda halisi, Franklin Bagalla, akiwapatia maelezo warembo hao walipotembelea duka la kampuni hiyo leo jijini Dar es Salaam. 
Baadhi ya warembo wa Miss Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Kampuni ya Tomoni, wauzaji wa mbogamboga za majani, nyama, vyakula na juisi za matunda halisi, Franklin Bagalla (katikati), nje ya duka la The Farm Fresh Market, Victoria jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Tomoni, wauzaji wa mbogamboga za majani, nyama, vyakula na juisi za matunda halisi, Franklin Bagalla (katikati), akiwapatia maelezo warembo hao, wakati akiwambeza kwenye sehemu mbalimbali za kampuni hiyo, leo jijini Dar es Salaam. 
Baadhi ya warembo wa Miss Tanzania wakiangalia Menu walipofika Mgahawa wa Kampuni ya Tomoni Farms, Victoria jijini Dar es Salaam leo.

Baadhi ya washiriki wa Shindano la Miss Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuwasili Hoteli ya Regency Msasani jijini Dar es Salaam leo kuanza kambi rasmi.(Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Mkurugenzi wa Lino Agency, waandaaji wa Shindano la Miss Tanzania, Hashim Lundega akizungumza na waandishi wa habari hotelini hapo mara baada ya idadi kubwa ya warembo hao kuwasili tayari kuanza kambi rasmi. Kushoto ni Mkuu wa Itifaki Albert Makoye na kulia ni Mjumbe wa Kamati ya Miss Tanzania, Deo Captain. 
Warembo wakiwasili kwenye Duka na Mgahawa wa Kampuni ya Tomoni Farm, la 'The Farm Fresh Market', maeneo ya Victoria jijini Dar es Salaam kujionea shughuli mbalimbali zifanywazo na kampuni hiyo, pia kujipatia chakula cha mchana.



JUMLA ya washiriki 30 wa mashindano ya urembo ya Miss Tanzania wameanza kambi ya mwezi mmoja leo tarehe 30 Septemba 2016 jijini Dar es Salaam.

Washiriki hao ambao ni washindi kutoka Kanda 9 na mikoa mbalimbali Tanzania watapokelewa katika Hotel ya Regency Park iliyopo Mikocheni D’salaam, na baadae watapiga kambi ya siku 4 katika Hotel ya Jozi Lounge iliyopo Msasani jijini D’salaam.

Mara baada ya kuingia kambini washiriki hao 30 pamoja na Wasimamizi wao watakuwa na Semina ya pamoja ambapo watafundishwa masuala mbalimbali yahusuyo mashindano pamoja na kambi kwa ujumla. 

Wakiwa kambini washiriki hao watafanya ziara katika mikoa ya Dodoma, Singida, Arusha, Geita na Mwanza kwa shughuli mbalimbali za kijamii.

Kauli mbiu ya mashindano ya Miss Tanzania 2016 ni Urembo na Mazingira Safi, hivyo washiriki wote watafanya kazi mbalimbali kijamii ikiwa ni pamoja na  usafi wa mazingira, kutunza mazingira na pia kushiriki katika kampeni ya kupanda miti itakayofanyika tarehe 1 Oktoba 2016 nchini pote.

Mashindano ya urembo ya Miss Tanzania kwa mwaka 2016 yamekuwa na changamoto kubwa ya kupata wadhamini wachache waliojitokeza kudhamini mashindano haya katika mikoa na sehemu mbalimbali.

Tunachukua fursa hii kuwapongeza na kuwashukuru Wadhamini wote waliojitokeza na kuchangia kwa njia mbalimbali katika kufanikisha mashindano ya mwaka huu.

Tunawashukuru pia washiriki wote katika ngazi zote waliojitokeza kushiriki na pia shukrani kwa wazazi na walezi walioruhusu watoto wao kushiriki mashindano ya urembo ya miss Tanzania 2016.

Ni matarajio yetu kwamba wadau wote wa tasnia hii ya urembo nchini mtajitokeza kwa wingi katika Fainali za Shindano la Miss Tanzania 2016 linalo tarajia kufanyika mwishoni  mwa mwezi Oktoba 2016.

 ORODHA YA WAREMBO WA MISS TANZANIA 2016 




JINA 

MKOA/ KITUO 

KANDA


  1. JULITHA KABETHE

  2. NURU KONDO

  3. GRACE MALIKITA

  4. SPORA LUHENDE


DAR CITY CENTRE

UKONGA

TABATA

DAR CITY CENTRE

         


KANDA YA ILALA

  1. DIANA EDWARD

  2. REGINA NDIMBO

  3. NDEONANSIA PIUS

  4. HAFSA ABDUL

UBUNGO

DAR INDIAN OCEAN

SINZA

SINZA



KANDA YA KINONDONI

  1. UPENDO DICKSON

  2. ABELLA JOHN

  3. ELINEEMA CHAGULA

  4. IRENE NDIBALEMA


LINDI

MOROGORO

MOROGORO

MTWARA



KANDA YA MASHARIKI


  1. ANNA NITWA

  2. LISA MDOLO

  3. IRENE MASSAWE


DODOMA

SINGIDA

SINGIDA



KANDA YA KATI


  1. LAURA KWAY




IRINGA UNIVERSITY




KANDA YA ELIMU YA JUU


  1. ILUMINATHA DOMINIC

  2. MARIA PETER

  3. LUCY MICHAEL


GEITA

MWANZA

GEITA



KANDA YA ZIWA

  1. MOURINE  AYOUB

  2. GLORY STEPHANO

  3. ELGIVER MWASHA

  4. BAHATI MFINANGA


ARUSHA

KILIMANJARO

TANGA

MANYARA


KANDA YA KASKAZINI


  1. MOURINE KOMANYA

  2. ANITHA MLAY

  3. IRENE MSABAHA

  4. EUNICE ROBERT


IRINGA

IRINGA

RUVUMA

MBEYA


KANDA YA NYANDA ZA JUU KUSINI 

  1. MWANTUMU ALLY

  2. ESTHER MNAHI

  3. ANITHA KISIMA

.

MBAGALA

KIGAMBONI

MBAGALA


KANDA YA TEMEKE


Makamu wa Rais azindua kampeni ya Mti wangu jijini Dar leo

$
0
0

Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan akipanda Mti wakati wa kuzindua kampeni ya MTI WANGU,mapema leo jijini Dar.

Imefahamika kuwa hewa ya ukaa ina asilimia kubwa katika gesijoto hivyo kusababisha kumong’onyoka kwa ozoni na kupelekea kuongezeka kwa kiasi cha nyuzi joto duniani na udororaji wa uchumi wa nchi

Hayo yamebainishwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan katika uzinduzi wa kampani ya upandaji miti ijulikanayo kama Mti Wangu katika mkao wa Dar e Salaam.

Mhe. Suluhu  alisema kwa kutambua athari za ongezeko la gesi joto hususani hewa ya ukaa serikali kupitia mkoa wa Dar es Salaam imekuja na kampeni ya kupanda miti ili kukabiliana na changamoto zitokanazo na mabadiliko ya tabianchi.

Alisema  mkoa wa Dar es Salaam unazalisha tani 4500 kwa kila siku zitokanazo na gesi za viwandani, vyombo vya usafiri, taka ngumu za viwandani na majumbani ikiwa ni pamoja na uchomaji na utupaji taka hovyo hivyo kupelekea serikali kwa kushirikiana na wadau kuanzisha kampeni hiyo jijini Daar es Salaam.

Alizitaja sababu nyingine za kampeni hiyo kuanzia Dar esSalaam ni pamoja na makadirio ya ongezeko la wakazi kufikia 5,895,791 kwa mwaka 2017 hivyo  kusababisha kuongezeka kwa kiasi kikubwa cha uzalishaji wa hewa ya ukaa kutokana na kuongezeka kwa mahitaji mbalimbali ya shughuli za binadamu na viwanda kwa ujumla.

Alisema tafiti mbalimbali zimeonyesha hewa ya ukaa inaongezeka jijini Dar es Salaam kutokana na ongezeko la viwanda na idadi kubwa ya wakazi ambapo kwa mwaka 2015 utafiti umeonyesha mkoa huo una viwanda 1854 kati ya hivyo 480 ni vikubwa na 1374 ni vidogo.

“Nawaagiza viongozi wa Serikali, taasisi binafsi, Asasi za kiraia na kila mtanzania kwa ujumla kutunza mazingira na kupanda miti ni hatua moja mbele katika kutunza mazingira yetu”.Alisema Mh. Suluhu.

Akimkaribisha mgeni rasmi katika uzinduzi wa kampeni hiyo, mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh. Paul Makonda alisema serikali imeweka chuma na minyororo ili kulinda wananchi kuvuka eneo ambalo si sahihi na kuweza kuhatarisha maisha yao kwa kugongwa na magari.

Alisema wananchi wanapaswa kulinda vyuma hivyo kwa kuwa vinasaidia kufanya mazingira yawe mazuri na kukinga miti na nyasi zilizopandwa kando ya barabara hizo zisiharibiwe.

“Wale wanaopita usiku na wale wanaoharibu, mtu yeyote akikamatwa ameiba chuma kimoja faini yake ni kununua vyuma kumi na kuchukulia hatua kwa mujibu wa sheria”.


Benjamin Sawe
Maelezo
Dar es Salaam

KATIBU MKUU WA CCM, KINANA AKUTANA NA KATIBU MKUU WA CHAMA CHA CNDD-FDD CHA BURUNDI, JIJINI DAR ES SALAAM, LEO

$
0
0
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na ujumbe wake, akiwa katika mazungumzo na Katibu Mkuu wa chama cha CNDD-FDD Evariste Ndayishimiye na ujumbe wake, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam.
 Kataibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Katibu Mkuu wa Chama cha CNDD-FD cha Burundi wakifurahia jambo wakati wa mazungumzo yao katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo

 Baadhi ya maofisa katika ujumbe wa Burundi uliofuatana na Katibu Mkuu wa Chama cha  CNDD-FDD Evariste Ndayishimiye, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam. 

Kataibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akimkaribisha Katibu Mkuu wa Chama cha CNDD-FDD, Evariste Ndayishimiye, leo Oktoba 1, 2016, katika Ofis Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kuwa na mazungumzo baina ya viongozi hao kuhusu uhusiano wa vyama hivyo ya CCM na CNDD-FDD. Kushoto ni Mnadhimu Mkuu wa CNDD-FDD, Gelase Ndabirabe.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mnadhimu Mkuu wa Chama cha CNDD-FDD,  Gerase Ndabirabe. Kushoto ni Kaimu Balozi wa Burundi nchini, Prefere Ndayishimiye
 Katibu  Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimsalimia Kaimu Balozi wa Burundi hapa nchini Prefere Ndayishimiye  alipokuwa akiupokea ugeni huo wa Katibu Mkuu wa CNDD-FDD
 Msemaji wa CCM Christopher Ole Sendeka akisalimiana na Katibu Mkuu wa chama cha CNDD-FDD cha Burundi Evariste Ndayishimiye ugeni wa Katibu mkuu huyo ulipowasili leo Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba Dar es Salaam. Wapili kulia ni Balozi David Kapya. 
 Kataibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimpeleka Ofisini kwake, Katibu Mkuu wa Chama cha CNDD-FD cha Burundi baada ya kuwasili kwa ajili ya mazungumzo. Kushoto ni Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka 
 Kataibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimpeleka Ofisini kwake, Katibu Mkuu wa Chama cha CNDD-FD cha Burundi baada ya kuwasili kwa ajili ya mazungumzo.
 Kataibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimkaribisha kuketi kwa ajili ya kuendelea na mazungumzo, Ofisini kwake, Katibu Mkuu wa Chama cha CNDD-FD cha Burundi baada ya kuwasili kwa ajili ya mazungumzo hayo leo katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam. Kulia ni Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka

PICHA ZAIDI/BOFYA HAPA

MAKAMU WA RAIS AZINDUA KAMPENI YA UPANDAJI MITI KATIKA JIJI LA DAR ES SALAAM

$
0
0

Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka udongo katika mti alioupanda eneo la JKT Mgulani Barabara ya kilwa wakati wa uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti katika jiji la Dar es Salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliojitokeza katika eneo la JKT Mgulani ambapo shughuli za uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti katika jiji la Dar es Salaam zilifanyika.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano Mhe. January Makamba akihutubia kwenye hafla ya uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti iliyofanyika JKT Mgulani, barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda akihutubia wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliojitokeza kwenye uzinduzi wa kampeni ya kupanda miti jijini Dar es salaam inayokwenda kwa jina la MTI WANGU iliyozinduliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akijiunga na mtandao kwenye eneo la Gymkhana ambalo huduma ya WI-FI inapatikanika bure kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam.
...................................

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan leo tarehe 1 Oktoba 2016 ameongoza mamia ya wakazi wa mkoa wa Dar es Salaam katika uzinduzi rasmi wa kampeni ya upandaji miti inayojulikana kama Mti wangu Jijini Dar es Salaam.

Akihutubia mamia ya wananchi waliojitokeza katika uzinduzi huo katika eneo la barabara ya Kilwa – Kurasini katika wilaya ya Temeke Jijini Dar es Salaam, Makamu wa Rais ameviagiza vyombo vya dola mkoani Dar es Salaam ambavyo vimepewa jukumu la kutunza miti hiyo iliyopandwa ili isiharibiwe vihakikishe vinatekeleze jukumu ili kikamilifu ili kuhakikisha miti hiyo iliyopandwa inakuwa vizuri ili kulifanya jiji la Dar es Salaam kuwa miongoni mwa Majiji bora katika utunzaji wa Manzingira.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa kampeni hiyo ambayo ameizindua Jijini Dar es Salaam inatakiwa ifanyike nchini kote kama hatua ya kurejesha uoto wa asili na utunzaji wa vyanzo vya maji kote nchini.

Amesema kuwa jitihada za kupanda miti nchini zinatakiwa kuimarishwa maradufu kwani zitasaidia katika uhifadhi wa mazingira hususani katika suala zima la kupambana na athari za mabadiliko ya tabia ya nchi.

Makamu wa Rais katika hotuba yake ameeleza kuwa tafiti mbalimbali zinaonyesha kuongezeka hewa ya ukaa katika jiji la Dar es Salaam kutokana na ongezeko la viwanda na idadi kuwa ya watu hivyo jitihada za pamoja kati ya serikali,taasisi binafsi,asasi za kiraia na wananchi zinahitajika katika kutunza mazingira na kupanda miti.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan pia amepongeza jitihada za uongozi wa mkoa wa Dar es Salaam katika uboreshaji na uimarishaji wa mifumo ya maji katika barabara itakayosaidia kurahisisha umwagiliaji wa miti iliyopandwa.

Amesema anafaraja na matumaini makubwa kuwa kampeni aliyoizindua ya upandaji miti itakuwa endelevu na miaka michache ijayo italifanya Jiji la Dar es Salaam kuwa kivutio na mfano wa kuigwa na mikoa mingine kwa kuwa na mwonekano mpya na wa kuvutia.

Baada ya kuzindua kampeni hiyo jijini Dar es Salaam, Makamu wa Rais ambaye aliambatana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu Rais Mazingira na Muungano January Makamba na Waziri wa Maliasili na Utalii Profesa Jumanne Maghembe alifanya ziara fupi ya kutembelea na kukagua mifumo wa maji katika barabara ya Nyerere na Ally Hassan Mwinyi itakayotumika kumwagilia miti iliyopandwa pamoja na kuongeza na wananchi walioshiriki zoezi la upandaji miti katika eneo la Gymkana.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

SERIKALI IPO PAMOJA NA WANAKAGERA KATIKA KIPINDI HIKI KIGUMU-RAIS DKT MAGUFULI

$
0
0
Editha Karlo,wa blog ya jamii,Kagera.

RAIS John Pombe Magufuli amesema kuwa serekali ipo pamoja na wanakagera katika kipindi hiki ambacho  wamekumbwa na tetemeko la ardhi na lililopelekea kuleta maafa na kupoteza makazi.

 Magufuli aliyasema hayo jana kwenye viwanja vya seminari ya Rubya wakati wa ibada ya misa ya uzinduzi wa jubilei ya miaka 150 uinjilishaji na 100 ya upadre Tanzania.

Waziri wa viwanda biashara na uwekezaji,Mh Charles Mwijage  aliyasema hayo kwa niaba ya Rais, alisema kuwa Rais amemtuma kuwapa pole nyingi wana kagera walioathirika na tetemeko la ardhi lililotokea september 10 mwaka huu.

 Magufuli alisema kuwa serekali yake inaendelea kufanya jitihada mbalimbali ikiwemo kuboresha miundombinu mbalimbali kwa haraka kama vile shule,zahanati,nyumba za ibada na barabara ili huduma za kijamii ziwe kurudi katika hali yake ya kawaida.

 Aliwapongeza wanakagera kwa uvumilivu waliounyesha katika kipindi hiki walichokumbwa na tetemeko la ardhi ambapo hawajayumba kiimani wameendelea kusimama imara.8

 " Sasa hivi mataifa mbalimbali na Dunia kwa ujumla pamoja na Serekali yangu ipo bega kwa bega na wanakagera katika kuhakikisha miundo mbinu iliyo haribiwa na tetemeko ina rudi haraka katika hali yake ya awali"alisema Magufuli.

 Pia Rais Magufuli alilipongeza kanisa katoliki kwa mchango wake mkubwa katika huduma za kijamii kama vile elimu,afya pamoja na huduma zingine  xa kijamii wamekuwa wakifanya vizuri na serekali inautambua mchango wao.

 Naye Askofu mkuu wa jimbo la Mwanza Thadeus Rweiche kwaniaba ya Rais wa baraza la maaskofu Tanzania(TEC) Talicusis Ngaralekumtwa aliwataka wanakagera kuwa wavumilivu katika kipindi hiki cha mpito na kuwataka mapdre wasivunje moyo katika kazi zao za unjilishaji.

Alisema huduma za kiroho zinatolewa katika mazingira mazuri kwasababu serekali inatoa ushirikiano wa bega kwa bega na viongozi wa dini pamoja na waumini.

 Askofu Rweiche alisema semenari ya Rubya ni chimbuko la mapdre kwa Afrika mashariki.
 Waziri wa viwanda na biashara Charles Mwijage akitoa salamu za Rais John Magufuli kwenye ibada ya misa ya uzinduzi wa Jubilei ya miaka 150 ya uinjilishaji na miaka 100 ya upadre Tanzania iliyofanyika kwenye viwanja vya semenary ya Rubya Wilayani Muleba
 Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali mstaafu Salum Kijuu akitoa salam za Mkoa kwenye ibada ya misa ya uzinduzi wa jubilei ya miaka 150 ya unjilishaji na 100 ya upadre Tanzania
 Katibu mkuu wa baraza la maaskofu Tanzania (TEC)Padre Raymond Saba akitoa neno la shukrani 
 Askofu msaidizi wa jimbo katoliki la  Bukoba Method Kilaini akitoa shukrani kwa niaba ya Askofu mkuu wa Jimbo la katoliki Bukoba Askofu Desderius Rwoma kwa wageni na waumi.wote waliohudhuria ibada hiyo
 Baadhi ya maaskofu kutoka majimbp yote Tanzania wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya ibada
 Sehemu ya wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya Tanzania waliohudhuria ibada hiyo.

WANANCHI WAASWA KUTOA USHIRIKIANO KWA UTAFITI WA UKIMWI.

$
0
0

Grace Singida.

Wananchi wameaswa kutoa ushirikiano kwa wataalamu watakaofanya utafiti wa viashiria vya ukimwi utakaofanyika nchi nzima na kuhusisha kaya elfu 16 na kuwafikia watanzania elfu 42,000 wakiwemo watoto elfu nane.

Mkuu wa kitengo cha mawasiliano cha shirika la ICAP-Tanzania linalofadhili utafiti wa viashiria na matokeo ya Ukimwi Mama Mihayo M Bupamba amesema utafiti umepokelewa kwa hisia tofauti ukipotoswa kuwa utahusika kila kaya wakati sio kweli.

Mama Mihayo amesema utafiti utahusisha kaya chache tu za Tanzania nzima ambapo ambapo kaya hizo zitaombwa ridhaa na utafiti utafanyika kwa usiri na kufuata sera na taratibu za wizara ya afya, mila, desturi, usiri na utaalamu wa hali ya juu utazingatiwa hivyo wasiwe na wasiwasi.

Ameongeza kuwa lengo utafiti huo ni kuendleza utafiti wa kuoima hali ya ukimwi kila baada ya miaka mine ambapoa mara ya wisho ulifanyika mwaka 2012

Mama Mihayo amesema utafiti huu utahusisha hali ya ukimwi, maambukizi mapya, wingi wa kinga ya mwili, wingi wa virusi vya ukimwi kwa watu wanaoishi na maambukizi ya Virus vya ukimwi, Uwezo wa mwili wa kumeng’enya dawa za kupunguza makali pamoja na magonjwa ya kaswende na homa ya ini.

Ameongeza kuwa utafiti utasaidia kupata taarifa sahihi kwakuwa nyingi zimekuwa zikipatikana kwa wale tu wanaoenda kupima hospitali hasa wajawazito au wagonjwa bila kuhusisha ambao hawajafika kupima.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew J. Mtigumwe amesema utafiti ni wa muhimu sana na kuwasihi wananchi wa Mkoa wa Singida kutoa ushirikiano wa kutosha kwa wataalamu hao.

Mhandisi Mtigumwe amesema utafiti huo utasaidia watunga sera waweze kupanga kupanga mikakati mizuri zaidi ya kupambana na ugonjwa wa Ukimwi.

Ameongeza kuwa utafiti huo ni wa kipekee kwakuwa utahusisha rika zote tofauti na tafiti zilizotangulia pia utahusisha vipimo vingi na majibu kutolewa hapohapo.
 Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi  Mathew J Mtigumwe akifungua mkutano wa wadau wa utafiti wa viashiria na matokeo ya Ukimwi.
 Mkuu wa kitengo cha mawasiliano kutoka shirika la Icap Mama Mihayo Bupamba akitoa mada katika kikao cha wadau wa utafiti wa viashiria na matokeo ya Ukimwi.
 Wadau wa utafiti wa viashiria na matokeo ya Ukimwi wakisikiliza kwa umakini kikao cha utafiti huo.
 Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi  Mathew J Mtigumwe (katikati) akifuatilia mada katika mkutano wa wadau wa utafiti wa viashiria na matokeo ya Ukimwi kushoto kwake ni katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Utawala na Rasilimaliwatu Buhacha B. Kichinda na Kulia kwake ni Kaimu Meneja wa ofisi ya Takwimu Mkoa wa Singida Naing'oya Kipuyo.

Waziri Nnauye azindua Wiki ya Maonyesho ya Utamaduni wa China Jijini Dar es Salaam

$
0
0
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kushoto) akikagua picha mbalimbali za kiutamaduni wa China wakati wa uzinduzi wa Maonyesho ya Utamaduni wa China leo Jijini Dar es Salaam. (katikati mbele) ni Kaimu Balozi wa China nchini Tanzania Bw. GOU Haodong.
 Kaimu Balozi wa China nchini Tanzania Bw. GOU Haodong (kulia) akiteta jambo na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye alipokua akikagua picha mbalimbali za kiutamaduni wa China wakati wa uzinduzi wa Maonyesho ya Utamaduni wa China leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Kituo cha Utamaduni cha China nchini Bw. GAO Wei.
 Kaimu Balozi wa China nchini Tanzania Bw. GOU Haodong (kulia) akiteta jambo na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye alipokua akikagua picha mbalimbali za kiutamaduni wa China wakati wa uzinduzi wa Maonyesho ya Utamaduni wa China leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Kituo cha Utamaduni cha China nchini Bw. GAO Wei.
 Mkuu wa Kituo cha Utamaduni cha China nchini Bw. GAO Wei akizungumza na washiriki wa maonyesho (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa Maonyesho ya Utamaduni wa China leo Jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Balozi wa China nchini Tanzania Bw. GOU Haodong akizungumza na washiriki wa maonyesho (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa Maonyesho ya Utamaduni wa China leo Jijini Dar es Salaam
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na washiriki wa maonyesho (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa Maonyesho ya Utamaduni wa China leo Jijini Dar es Salaam
 Baadhi ya washiriki wa Maonyesho ya Wiki ya Utamaduni wa China wakifuatilia kwa makini matukio mbalimbali yaliyokua yakiendelea wakati wa uzinduzi wa Maonyesho ya Utamaduni wa China leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto waliokaa ni Kaimu Balozi wa China nchini Tanzania Bw. GOU Haodong
 Kikundi cha Utamaduni na Sanaa cha Jiangxi kikionyesha sarakasi wakati wa uzinduzi wa Maonyesho ya Utamaduni wa China leo Jijini Dar es Salaam.
 Msanii kutoka China akionyesha mchezo wa utamaduni wa mazoezi maalumu yanayojenga afya yaitwayo Qigong wakati wa uzinduzi wa Maonyesho ya Utamaduni wa China leo Jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (katikati) katika picha ya pamoja na Kaimu Balozi wa China nchini Tanzania Bw. GOU Haodong (wapili kulia) wakati wa uzinduzi wa Maonyesho ya Utamaduni wa China leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Kituo cha Utamaduni cha China nchini Bw. GAO Wei na wapili kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Utamaduni kutoka Jiangxi China Bw. Chen Hongmin
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (katikati) katika picha ya pamoja na Kaimu Balozi wa China nchini Tanzania Bw. GOU Haodong (wapili kulia) wakati wa uzinduzi wa Maonyesho ya Utamaduni wa China leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Kituo cha Utamaduni cha China nchini Bw. GAO Wei na wapili kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Utamaduni kutoka Jiangxi China Bw. Chen Hongmin
Washiriki wa Maonyesho ya wiki ya Utamaduni wa China kutoka Chama cha Mchezo wa WUSHU Tanzania katika picha ya pamoja wakati wa uzinduzi wa Maonyesho ya Utamaduni wa China leo Jijini Dar es Salaam.
Picha na:Genofeva Matemu - WHUSM

 
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (katikati) akimsikiliza Kaimu Balozi wa China nchini Tanzania Bw. GOU Haodong (kulia) wakati wa uzinduzi wa Maonyesho ya Utamaduni wa China leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Utamaduni kutoka Jiangxi China Bw. Chen Hongmin.


ASKARI POLISI APATWA KIGUGUMIZI KUSIMAMIA SHERIA

$
0
0
Askari huyo akisalimiana na abiria aliyeshuka katika gari hilo badala ya dereva na baada ya hapo alimwachia bila ya kumchukulia sheria yoyote kama wanavyofanya kwa madereva wengine wanaokiuka sheria za usalama barabarani.

 Askari Polisi wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL), akipiga picha gari lenye namba T 297 AQE baada ya dereva wa gari hilo kukiuka sheria ya usalama barabarani kwa kusimama kwenye reli katika makutano ya reli na barabara ya Nyerere eneo la Gold Star jijini Dar es Salaam majira ya saa sita mchana leo gari hilo lilikuwa likitokea maeneo ya Mnazi Mmoja lilielekea Tazara. 
 Askari huyo akizungumza na dereva wa gari hilo aliweke gari lake pembeni ili alipishwe faini.
Na Dotto Mwaibale

ASKARI polisi anayedaiwa kuwa ni wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL), alikumbwa na kigugumizi na kushindwa kumchukulia sheria dereva wa gari dogo aina ya Corrona lenye namba T 297 AQE baada ya dereva wa gari hilo kukiuka sheria ya usalama barabarani kwa kusimama kwenye reli katika makutano ya reli na Barabara ya Nyerere eneo la Gold Star jijini Dar es Salaam majira ya saa sita mchana leo gari hilo lilikuwa likitokea maeneo ya Mnazi Mmoja lilielekea Tazara. 

Awali askari huyo baada ya kubaini kosa lililofanywa na dereva  huyo alilipiga picha gari hilo likiwa katikati ya reli wakati magari mengine yakiwa katika foleni.

Baada ya kupiga picha hiyo alimfuata dereva wa gari hilo alimtaka dereva wa gari hilo aweke gari lake pembeni ili aandikiwe faini.

Lakini kabla dereva huyo hajaweka gari hilo pembeni abiria aliyekuwa amekaa siti ya mbele ya gari hilo alitelemka na kujitambulisha kwa askari huyo ambapo walianza kusalimiana na kumruhusu aondoke bila kuchukuliwa hatua yoyote kama wanavyofanya kwa madereva wengine.

Akizungumzia tukio hilo dereva wa daladala linalofanya safari zake kati ya Gongo la Mboto na Mnazi mmoja alisema sheria ni msumeno hivyo hata anapobainika ndugu jamaa, au rafiki wa askari kafanya kosa anapaswa kuguswa na sheria zilizopo.

"Yule jamaa kama sio askari polisi basi anaweza kuwa mwanajeshi au usalama wa taifa ndio maana yule jamaa aligwaya kumchukulia hatua" alisema dereva huyo.

Dereva huyo alisema kama kosa hilo lingefanywa na dereva ambaye hafahamiki na askari huyo ni lazima angelipa faini kwani hiyo ni kawaida ya askari hao kumkomalia mtu hata akiomba kusamehewa.

DC DAQARRO AWEKA MAZINGIRA KUHAKIKISHA USALAMA WA CHAKULA

$
0
0
Na Nteghenjwa Hosseah, ARUSHA

Mkuu wa Wilaya ya Wilaya ya Arusha Mhe. Fabian Gabriel Daqarro mwishoni mwa wiki hii amekutana na Maafisa Watendaji wa Kata zote za Jiji la Arusha kuzungumzia kuhusu masuala mbalimbali muhimu yanayotakiwa kupewa kipaumbele katika Wialaya hiii. 

Katika Kikao hicho Dc Daqarro ametilia mkazo masuala ya Usalama wa Chakula katika Mitaa yote, Ulinzi na usalama, usimamizi wa miradi ya maendeleo pamoja na utoaji wa taarifa za matukio yasiyo ya kawaida yanayotokea katika kila Kata.

Akizungumza katika kikao hicho alisema “nahitaji kupata takwimu sahihi kutoka katika kila Kata ya mahitaji ya Chakula, kiasi kilichopo na namna ambavyo mmejipanga kukabiliana na upungufu endapo utatokea, kila afisa ugani wa eneo husika ahakikishe anatoa elimu ya kutosha na kufuatilia kuhusu usalama wa chakula katika eneo lake na kuwasilisha taariha hizo katika Ofisi yangu. Sitamuelewa mtendaji ambaye kwa kutokuwajibika kwake kutasababisha njaa ama upungufu wa chakula kwa namna yeyote ile.

Aidha alisisitiza kusimamia miradi ipasavyo ili iwe na ubora na iweze kudumu muda mrefu, kusimamia Usalama wa Kata kwa kutoa taarifa za kila tukio lisilo la kawaida linalotokea kila siku na kudhibiti uingiaji wa wageni kutoka nje ya nchi wanaofika katika Kata. 

“Wageni wote wa Nje ya Nchi lazima taarifa zao zifikishwe kwa Afisa uhamiaji wa Wilaya ili kujiridhisha kwamba wameingia nchini kihalali na kuwa na shughuli maalumu iliyowaleta katika maeneo yenu aliongeza”.

Sambamba na hilo alisema si ruhusa kwa Mtendaji wa Kata kutoa mihutasarti kwa ajili ya kumilisha upatikanji wa silaha kwa sababu hivi sasa zoezi hilo limesitishwa mpaka pale Uhakiki wa silaha utakapokamilka hivyo kwa kuwa muombaji ni lazima aanzie kwenye ngazi ya kata si ruksa kwa vikao husika kutoa mihutasari ya aina hiyo.

Mwenyekiti wa Watendaji wa Kata katika Jiji la Arusha Ndg. Suleimani Kikingo alisema kwa umoja watahakikisha kwamba maagizo yote yaliyotolewa wanayatekeleza kwa ufanisi ili kuleta mabadiliko ya haraka na kutoa hudma bora kwa wakazi wa Jiji hili.
      Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Fabian Gabriel Daqarro akizungumza na Maafisa watendaji wa Kata wa Jiji la Arusha (Hawapo Pichani) wakati wa kikao maalumu na watendaji hao kilichofanyika miwshoni mwa juma jijini hapa.
 Mwenyekiti wa Maafisa watendaji wa Kata na Mtendaji wa Kata ya Kati Ndg. Suleimani Kikingo akichangia wakati wa Kikao na Mkuu wa Wilaya ya Arusha
      Maafisa Watendaji wa Kata waliohudhuria Kikao na Mkuu wa Wilaya ya Arusha
    Afisa Mtendaji wa Kata ya Levolosi Easter Maganza akitoa ufafanuzi wa hoja mbalimbali wakati wa kikao
     Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Fabian Gabriel Daqarro(kushoto) akiwa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Arusha Ndg. David Mwakiposya wakati wa kikao na watendaji wa Kata.
Viewing all 46371 articles
Browse latest View live




Latest Images