Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46362 articles
Browse latest View live

Naibu Waziri Wambura akutana na wajasiliamali wa Hand Production of Tanzania

$
0
0
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (katikati) akionyeshwa bidhaa ya vikapu vya asili vilivyotengenezwa kwa kitenge kutoka kwa mjasiriamali Bibi. Flora Mosha wa Nancy Tailoring Mart (kushoto) leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Handproduct of Tanzania Bibi. Elizabeth Matarimo.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (katikati) akionyeshwa vazi lililodariziwa na mjasiriamali ambaye pia ni Mwenyekiti wa Handproduct of Tanzania Bibi. Elizabeth Matarimo leo jijini Dar es Salaam.Picha na: Lorietha Laurence – WHUSM

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (kulia) akifafanua jambo wakati wa kikao na kikundi cha wajasiriamali wa Handproduct of Product leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni Mwenyekiti wa Handproduct of Tanzania Bibi. Elizabeth Matarimo.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (kulia) akiangalia matukio ya picha katika album ya wajasiriamali wa kikundi cha Handproduct of Product leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni Mwenyekiti wa Handproduct of Tanzania Bibi. Elizabeth Matarimo.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (kushoto) akiangalia bidhaa zinazotengenezwa na mjasiriamali Bi. Helen Mwamkoa wa Nambua Enterprises Products leo jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (katikati) akionyeshwa bidhaa ya vikapu vya asili kutoka kwa mjasiriamali Bibi. Nicola Boymanda wa Iringa Baskets (kushoto) leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Handproduct of Tanzania Bibi. Elizabeth Matarimo.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (katikati) akisikiliza ufafanuzi kutoka kwa mjasiriamali Bibi. Potamia Nuena wa PAT designs (kushoto) leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Handproduct of Tanzania Bibi. Elizabeth Matarimo.
…………………………………………………………

Na Lorietha Laurence.

Wajasirimali na wabunifu wa kazi za mikono nchini wahimizwa kuwa na hatimiliki ili kudhibiti wizi wa kudurufu bidhaa zao unaofanywa na baadhi ya wafanyabiashara wasio waaminifu.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia James Wambura alipokutana na kikundi cha wajasiriamali cha Handproduct of Tanzania leo jijini Dar es Salaam.

Mhe. Anastazia ameeleza kuwa endapo kazi za wajasriamali zitalindwa kwa kuwa na hatimiliki itasaidia katika kukuza uchumi wao binafsi na kuongeza pato la Taifa. “Ni muhimu kulinda kazi za wajasirimali kama ambavyo kazi za sanaa ya muziki zinavyolindwa kwa kuwa na hatimiliki ili kuwasaidia katika kulinda haki zao za ubunifu” alisema Mhe. Anastazia.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Handproduct of Tanzania Bibi. Elizabeth Matarimo ameeleza kuwa kukosekana kwa hatimiliki katika kazi zao kumeleta changanmoto kubwa na bidhaa feki kutoka kwa wafanyabiashara wa nje ambao wamekuwa wakidurufu kazi zao na kuuza bidhaa kwa bei nafuu.

Aidha Bibi. Elizabeth aliongeza kuwa changamoto nyingine ni ukosefu wa eneo la kufanyia maonyesho ya bidhaa zao kitendo ambacho kinasababisha kukosekana na soko lililoimara kwa bidhaa hizo.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni Wizara Habari, Utamduni, Sanaa na Michezo Bibi. Lilian Beleko amesema kuwa kweli changamoto hizo zipo na wanazifanyia kazi kuwawezesha wajasiriamali hao wa kazi za sanaa na utamaduni ili waweze kufanya kazi zao kiufanisi.

Kikundi cha Handproduct of Tanzania kilisajiliwa mwaka 2006 na kinajumisha wajasiriamali mbalimbali wanaojihusisha na kazi za mikono kutengeneza bidhaa mbalimbali za utamaduni na sanaa katika kuenzi utamaduni wa Mtanzania.

RSM YACHANGIA MADAWATI 50 KATIKA MKOA WA DAR ES SALAAM

$
0
0
RSM, Mtandao wa Kimataifa katika ukaguzi wa mahesabu na tathmini za kodi, umesherehekea madhimisho tano ya kila mwaka ya Siku Maalumu Duniani ya RSM—kwa kuchangia madawati kwa shule mbalimbali za Dar es Salaam.

Mchango wa RSM, Mtendaji Mkuu wa RSM Afrika Mashariki, Bi. Lina Rantasi alisema kuwa timu ya RSM imedhamiria kusaidia jitihada za Serikali za kuokoa maisha na kuendeleza elimu. Bi. Ratansi aliendelea kusema,”Kumekuwa na wito mwingi wa kuchangia madawati, Na sisi hatutaki kubaki nyuma, ndo maana tumetoa madawati 50 (3, 750, 000) ili kusaidia watoto wasika chini tena.”

Amesema madawati utasaidia kuongeza uwezo na akili za watoto katika masomo, hivyo kuongeza ufaulu, kwa sababu “motto akikaa chini hata ufahamu wake unakuwa mdogo.

Akipokea madawati hayo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kamati ya Madawati-Mkoa wa Dar es Salaam, Hamid Abdul Rahaman, amesema mchango wa RSM utasaidi kukuza sekta ya
elimu, na kuwapongeza Mtandao wa RSM kwa kuunga mkono kampeni ya kitaifa ya kuziwezesha shule kuwa na madawati ya kutosha.

hadamu kwani benki ya damu imepungua kiasi cha kutokuwa na damu kabisa. Sisi hapa RSM tumeamua kuchukua hatua na kuwahamasisha wengine kufanya kama hivi. Shime tuungane pamoja kuokoa maisha ya Mtanzania. na sherehe kubwa zaidi za dira na malengo ya pamoja ambayo mtandao huu huru wa sita kwa ukubwa wa ukaguzi, kodi
na ushauri wa kitaalamu haujawahi kufanya.

Kupitia shughuli za aina mbalimbali duniani kote, wafanyakazi katika mashirika ya RSM zaidi ya nchi 120 zilizounganishwa kwa njia ya mshiriki, mteja na matukio ya hisani katika kusherehekea maadili ya msingi ya RSM ya utendaji kazi wa pamoja, uelewa wa kina wa watu, kuchangia wazo na utambuzi kwa manufaa ya mteja.

RSM jijini Dar es Salaam imesherehekea siku hii kwa shughuli mbali mbali za kijamii kama sehemu ya wajibu wake kwa jamii. Timu imeianza siku kwa kuchangia damu katika Damu Salama. Wakati akihojiwa, Vile vile timu ya RSM, itajumuika na wanafunzi wenye mahitaji maalum katika Shule ya Msingi Mchanganyiko. “Watoto hawa wanahitaji mapenzi na misaada ya hali na mali. Sisi hapa RSM tunafurahia kuwaonyesha kuwa wao ni sehemu muhimu ya jamii yetu na wanathaminiwa katika ulimwengu huu.” Alisema Mtendaji Mkuu wa RSM. Shirika na wafanyakazi pia limeichangia shule vyakula mbalimbali na vifaa vingine kwa kwa ajili ya wanafunzi.

Kama sehemu ya kuendelea kusaidia sekta ya Elimu, RSM pia imechangia madawati katika jiji la Dar es Salaam kupitia Kamati ya Madawati Mkoa wa Dar es salaam. Hii ni kuunga mkono kampeni ya kitaifa ya kuziwezesha shule kuwa na madawati ya kutosha.

Chapa ya RSM inaiwezesha kuelezea vizuri uimara na uwezo wake wa kutoa huduma duniani kote kama mshauri wa chaguo kwa soko la kati. Mtandao una mashirika katika zaidi ya nchi 120 na unajumuisha wat

TANZIA: mtangazaji wa Channel Ten kipindi cha "Utalii Tanzania" Bw. Cassius Mdami afariki dunia

$
0
0
Aliyekuwa mtangazaji wa Channel Ten, kipindi cha Utalii Tanzania, Bw. Cassius Mdami (pichani) amefariki dunia leo mchana katika Hospitali ya Mazimbu mkoani Morogoro , ndugu na mwajiri wake  wamethibitisha. Tutawajulisha mipango ya mazishi mara tukipata taarifa.
MOLA AIWEKE ROHO YA MAREHEMU 
MAHALA PEMA PEPONI
-AMINA

MAJALIWA AZINDUA MPANGO MKAKATI NA MRADI WA MABORESHO YA HUDUMA ZA MAHAKAMA YA TANZANIA.

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisaidiwa na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othaman kukata utepe wakati alipozindua  Mpango Mkakati na Mradi wa Maboresho ya Huduma za Mahakama ya Tanzania  mjini Kibaha, Septemba 21, 2016.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akionyesha   Mpango Mkakati na Mradi wa Maboresho ya Huduma za Mahakama ya Tanzania  baada ya kuuzindua mjini Kibaha, Septemba 21, 2016. Wengine pichani kutoka kushoto ni Dkt. Hassison Mwakyembe, Waziri wa Katiba na Sheria, Jaji Mkuu, Mohamed Othman Chande na Naibu Spika wa Bunge, Dkt Ackson Tulia.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimkabidhi Mkurugenzi wa Benki ya Dunia wa Nchi za Tanzania, Burundi, Malawi na Somalia, Bella Bird kitabu cha Mradi wa Maboresho  ya Huduma za Mahakama ya Tanzania  baada ya kuuzindua mjini Kibaha Septemba 21, 2016. Kushoto ni Jaji Mkuu wa Tanzania Mohamed Chande Othman  na kulia ni Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipozindua  Mpango Mkakati na Mradi  wa Maboresho ya Huduma za Mahakama ya Tanzania ulifanywa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa mjini Kibaha Septemba 21, 2016. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya  pamoja na viongozi mbalimbali waliohudhuria katika uzinduzi wa  Mpango Mkakati na Mradi  wa Maboresho ya Huduma za Mahakama ya Tanzania ulifanywa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa mjini Kibaha Septemba 21, 2016.
 (Picha na Ofisi ya  Waziri Mkuu)

Wadau Mkoa wa Shinyanga wamkabidhi RC KAGERA misaada kwa waathirika wa tetemeko la ardhi

$
0
0

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Zainab Telack akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salim Kijuu nguo kwa ajili ya waathirika wa Tetemeko la Ardhi Mkoani Kagera
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salim Kijuu akiongozana na mkuu wa Mkoa wa Shinyanga mara baada ya kupokea misaada kwa ajili ya waathirika wa Tetemeko la Ardhi Mkoani Kagera

Na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Bukoba

Mkoa wa Shinyanga umekabidhi msaada wa vifaa vya ujenzi na chakula vyenye thamani ya Sh. milioni 41,172 kwa uongozi wa mkoa wa Kagera ili kusaidia waathirika wa tetemeko la ardhi lililotokea mkaoani humo hivi karibuni.

Makabidhiano hayo yalifanywa leo mjini Bukoba kati ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Bi. Zainabu Telack ambaye aliambatana na baadhi ya viongozi wa mkoa na viongozi wa dini ambapo mkoa wa Kagera umewakilishwa na Mkuu wa Mkoa wa huo Meja Jenerali Mstaafu Salim Kijuu. 

Wananchi wa mkoa wa Shinyanga wameguswa na kadhia iliyopata wananchi wa Kagera, hivyo tukaamua kukusanya nguvu ya pamoja kama mkoa ili kuwafariji Watanzania wenzetu kutokana na matatizo waliyoyapata” alisema Bi Zainabu.

Mkuu huyo wa mkoa alifafanua mchango wa misaada waliyotoa kuwa ni paamoja na mabati ya geji 28 1400, saruji mifuko 750, mchele kilo 600, mahindi kilo 100 paamoja na nguo.

Bi. Zainabu aliongeza kuwa michango ya msaada huo imeunganishwa nguvu kutoka Serikali ya mkoa wa Shinyanga, taasisi za Serikali na zisizo za kiserikali, sekta binafsi, masshirika ya dini, asasi za kiraia, wafanyabiashara, mogodi ya madini iliyopo mkoani humo na wadau wengine wa maendeleo.

Akitoa shukrani mara baada ya kupokea msaaada huo Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Kijuu amewashukuru wananchi wa Shinyanga kwa kuwafariji, majitoleo yao kwana kuwajali katika kipindi hiki cha mpito cha athari za tetemeko lililoukumba mkoa huo.





RAIS DK SHEIN ATEMBELEA ZBC TV LEO

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akitoa maelekezo kwa Uongozi wa ZBC TV leo alipofanya ziara maalum ya kutembelea kituo cha kurushia matangazo ya TV, Karume House pia kutembelea sehemu mbali mbali katika kituo hicho,akiwepo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Utalii,Utamaduni na Michezo Nd,Omar Hassan Omar (wa tano kulia)  [Picha na Ikulu.] 21/09/2016.
tv5
Mtangazji wa Habari wa ZBC TV Nd,Khamis Fakih (kulia) akitoa maelezo kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) wakati alipotembelea moja  ya studio za kusomea Taarifa mbali mbali muhimu ikiwemo taarifa za Habari katika kituo cha Karume House leo alipofanya ziara maalum, akiwa na Ujumbe wake akiwemo Katibu Mkuu wa baraza la Mapinduzi pia katibu Mkuu Kiongozi Dkt.Abdulhamid Yahya Mzee (wa pili kulia) katibu Mkuu Wizara ya habari,Utalii,Utamaduni na Michezo Nd.Omar Hassan Omar(wa tatu kushoto), [Picha na Ikulu.] 21/09/2016.
tv1
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto) akimuuliza jambo Kaimu Fundi Mkuu wa ZBC TV Nd,Mwadini Ame (kulia) wakati alipotembelea Studio ya kurikodia vipindi mbali mbali akiwa katika ziara maalum katika kituo cha kurushia matangazo ya TV Karume House leo,(wa pili kulia) Mkurugenzi wa ZBC TV Nd,Iman Duwe na (kushoto) Katibu Mkuu wa Baraza la Mapinduzi na katibu Mkuu Kiongozi Dkt.Abduhamid Yahya Mzee, [Picha na Ikulu.] 21/09/2016.
tv2
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Mhariri Mkuu wa ZBC Tv Nd,Suleiman Almasi (wa pili kushoto) wakati alipotembelea chumba cha Habari (News Room) leo  akiwa katika ziara maalum ya kutembelea kituo cha kurushia matangazo ya TV Karume House, [Picha na Ikulu.] 21/09/2016.
tv3
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa utayarishaji wa Vipindi vya ZBC Tv Nd,Halima Mselem (katikati) wakati alipotembelea moja ya Ofisi za ZBC TV katika kituo cha kurushia matangazo Karume House leo akiwa katika ziara maalum, [Picha na Ikulu.] 21/09/2016.

tv6
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) wakati alipotembelea moja  ya studio za kusomea Taarifa mbali mbali muhimu ikiwemo taarifa za Habari katika kituo cha Karume House leo alipofanya ziara maalum, akiwa na Ujumbe wake akiwemo Katibu Mkuu wa baraza la Mapinduzi pia katibu Mkuu Kiongozi Dkt.Abdulhamid Yahya Mzee (wa pili kulia) katibu Mkuu Wizara ya habari,Utalii,Utamaduni na Michezo Nd.Omar Hassan Omar(wa tatu kushoto), [Picha na Ikulu.] 21/09/2016. 

MKUTANO WA WADAU WA UTALII KUFANYIKA ARUSHA KESHO

$
0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii Profesa Jumanne Maghembe anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mkutano wa siku moja wa wadau wa sekta ya Utalii mkoani Arusha unaotarajiwa kufanyika kesho.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amesema hayo wakati akizungumza na wanahabari ofisini kwake,amesema kuwa mkutano kama huo ulifanyika kwa mara ya mwisho mwaka 2012 hivyo wameona ni vyema serikali kushirikiana na wadau wa utalii kukaa pamoja kujadili changamoto mbalimbali zinazowakabili ili kuboresha sekta hiyo,ambayo asilimia 80% ya watalii wanaoingia nchini hufika mkoani hapa .

Amesema kuwa mkoa wa Arusha ni kitovu cha cha utalii na unachangia pato la mkoa kwa asilimia20% na kitaifa kwa asilimia 17%ambapo mwaka 2015 idadi ya watalii iliyoingia nchini ilikuwa 1,137,182 na kuingizia Taifa kiasi cha dola za kimarekani 1.9 milioni,katikaq idadi hiyo asilimia 80%watalii walitembelea mkoa kwasababu ya vivutio vingi vilivyopo mkoani Arusha.

Amesema kwamba madhumuni ya mkutano huo ni kujadili hali ya maendeleo ya utalii ya mkoa ,fursa zilizopo,mafanikio ,changamoto na kuweka mikakati yakuboresha huduma mbalimbali za utalii ambapo wadau watapata fursa ya kubadilishana mawazo na kuadhimisha siku ya utalii duiaani amabayo huadhimishwa kila mwaka septemba 27.

“Maadhimisho haya ya utalii mwaka huu yamebeba kauli mbiu UTALII KWA WOTE,Kwa kuzingatia hilo wadau mbalimbali wa sekta hiyo ya utalii zikiwemo TANAPA,NCAA,HAT,TTB,TATO,TTGA,TRA,TACTO Watawasilisjha mada ambazo zitalenga kuboresha utalii,pamoja na kuhakikisha elimu na fursa za Utalii zinaifikia jamiii “ alisisitiza Gambo.

Amesema kuwa wadau watakaoshiriki mkutano huo ni wahifadhi,Wakala wa waongozaji watalii,Wakala wa wausafirishaji watalii,watoa huduma za malazi,Bodi ya Utalii,na Viongozi watendaji wa serikali ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa maliasili na Utalii Profesa Jumanne Maghembe.

Mkutano huo wa siku moja umefadhiliwa na Shirika la Hifadhi la Taifa (TANAPA)kwa kushirikiana na ofisi ya mkuu wa mkoa kwa kushirikiana na Ofisi ya Kanda ya Utalii ndiyo waandaaji wa mkutano huo wa wadau mbalimbali wa Utalii Mkoani Arusha

NEC YAANZISHA PROGRAMU ENDELEVU ZA KUTOA ELIMU YA MPIGA KURA.

$
0
0



Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhani akizungumza na waandishi wa Habari mjini Musoma kuwaeleza mkakati wa NEC wa kuwafikia wananchi moja kwa moja kuwapatia elimu ya mpiga kura.


Na. Aron Msigwa – NEC, Musoma

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeanza kutekeleza programu endelevu za kutoa elimu ya mpiga kura ili kuwaelimisha wananchi waliofikisha umri wa kupiga kura kutekeleza wajibu na haki waliyonayo kikatiba ya kupiga kura katika chaguzi zijazo.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhani wakati akizungumza na waandishi wa Habari mjini Musoma kuhusu mkakati wa NEC wa kuwafikia wananchi moja kwa moja kuwapatia elimu ya mpiga kura.

Amesema kuwa Tume hiyo imeanza kutoa elimu hiyo kwa kushiriki maonesho na mikutano mbalimbali ukiwemo mkutano wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) unaofanyika mjini Musoma kuanzia Septemba 22 hadi 24 mwaka huu.

“Tumeamua kushiriki kwenye mkutano huu kwa kuwa hawa ni watendaji wa Serikali katika ngazi za mitaa, tumekuja kutoa elimu ya mpigakura kwani suala la elimu tunalipa kipaumbele” Amesema Bw. Kailima.

Amesema Tume imeandaa programu ya kuwafikia wapiga kura moja kwa moja kwa kuweka mkakati wa kuhudhuria mikutano yote ambayo iko kihalali ikijumuisha ile ya Mawaziri na Naibu Mawaziri , Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu, Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya.

Amebainisha kuwa tayari NEC imewasiliana na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ili iweze kupata ratiba ya vikao vya kamati za ushauri za mikoa na wilaya ili iweze kupata fursa ya kutoa elimu ya mpiga kura ndani ya vikao hivyo.

Aidha, amefafanua kuwa Tume imemwomba Katibu Mkuu TAMISEMI ratiba ya vikao vya Mabaraza ya madiwani ya halmashauri zote nchini kwa lengo la kuwezesha wataalam wa Tume hiyo kutoa elimu ya Mpiga kura.

“Tumemwomba Katibu Mkuu TAMISEMI atusaidie kuweka ajenda ya kudumu kuhusu utaratibu mzima wa uendeshaji wa uchaguzi na uelimishaji wa mpiga kura kwenye vikao vya mabaraza ya Madiwani ambapo maafisa wa Tume walio katika ngazi za halmashauri watapata fursa ya kutoa elimu ya mpiga kura katika vikao hivyo” Amesisitiza.

Ameeleza kuwa NEC imejipanga kupanua wigo wa utoaji wa habari kupitia vyombo vya habari hasa Televisheni,Redio, Magazeti na Mitandao ya kijamii ili kuwawezesha wananchi wengi kupata elimu ya mpiga kura na taarifa sahihi kuhusu Tume ya Taifa ya Uchaguzi na majukumu yake.

“Tumejipanga kutumia vyombo vya habari, kila wiki tutakuwa na taarifa na mada fupifupi zinazohusu mchakato mzima wa uchaguzi kwa maana ya uandikishaji na zoezi zima la upigaji kura kujenga uelewa kwa jamii nzima kuhusu Tume ya Taifa ya Uchaguzi” Amefafanua.

Amesema kuwa kifungu Na 4 (c) cha Sheria ya Uchaguzi ya mwaka 1985 kinaelezea wazi kuwa pamoja na mambo mengine Tume ya Taifa ya Uchaguzi ina jukumu kutoa elimu ya Mpiga kura, kuratibu Taasisi na watu wenye uwezo wa kutoa elimu ya mpiga kura ili kuongeza uelewa miongoni mwa jamii.

“Tunategemea kuanzia mwanzoni mwa mwezi Oktoba tutatoa tangazo la kuzialika Asasi na taasisi zinazotaka kutoa elimu ya mpiga kura ziwasilishe maombi yao Tume ya Uchaguzi pamoja na zana zao za kutolea elimu ili tuweze kuwapatia kibali cha miezi 6 na baadaye tutafanya tathmini juu ya ufanisi wa kazi wanayoifanya” Amebainisha Bw. Kailima.

Amesema lengo la kuzishirikisha taasisi na Asasi hizo ni kuondoa ombwe lililokuwa linaonekana la utoaji wa elimu ya mpiga kura wakati wa uchaguzi pekee kwa kuhakikisha elimu hiyo inatolewa kila wakati ili kuongeza uelewa wa wananchi katika chaguzi zijazo.

Aidha, amesema NEC imeandaa mpango mpya wa kuzifikia shule mbalimbali za Sekondari hapa nchini utakaowawezesha wanafunzi wa shule zitakazochaguliwa kuwa na Klabu za elimu ya mpiga kura.

Amesema programu hiyo itaiwezesha Tume kuwaelimisha wanafunzi waliofikisha umri wa kupiga kura na wale ambao bado hawajafikia umri huo ili kujenga uelewa wao kuhusu elimu ya Mpiga kura.

“Tumeanza program hii kwa kuzitembelea shule mbili za Sekondari za Isange (wasichana) na Shule ya Ufundi Musoma zilizo katika Manispaa ya Musoma, tutaongea na wanafunzi ambao wamefikia umri wa kupiga kura lakini bado hawajajiandikisha kupiga kura na wale ambao bado hawajafikisha umri wa kupiga kura, tumenalenga kuanzisha klabu ya Elimu ya mpiga kura kwenye shule moja katika kila wilaya ya Tanzania” Amesema.

Amefafanua kuwa kuanzishwa kwa klabu hizo kutawawezesha wanafunzi kujadiliana kwa kina kuhusu mfumo wa uandikishaji wa wapiga kura kwa mujibu wa sheria iliyopo ili kufikia lengo la kuwa na shule moja yenye Klabu ya elimu ya mpiga kura katika kila wilaya ifikapo Januari 2020.

DC MTATURU: SERIKALI ITAVISAIDIA VIKUNDI VITAKAVYO KUWA TAYARI KUJIHUSISHA NA KILIMO CHA UMWAGILIAJI

$
0
0
Kutoka Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Hassan Tati, Mkurugenzi wa Asasi isiyo ya kiserikali ya RIWADE Mhandisi Ayubu Massau, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Bi Haika Massawe, Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu, Moses Msai Mratibu wa RIWADE mkoa wa Singida na Afisa kilimo wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ayub Sengo
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akisisitiza umakini kwa wananchi waliojitokeza kwenye Kikao cha Mafunzo ya namna bora ya kushiriki katika kilimo chambogamboga na matunda kupitia umwagiliaji
Afisa kilimo wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ayub Sengo akiwasihi wananchi kutumia njia za kisasa katika kilimo cha umwagiliaji na kufuata taratibu wanazoelekezwa na wataalamu wa kilimo
Baadhi ya viongozi wa vikundi mbalimbali vya ujasiriamali sawia na wajumbe washiriki kwenye mafunzo hayo wakifatilia kwa makini Muelimishaji
Kutoka Kushoto ni Mkurugenzi wa Asasi isiyo ya kiserikali ya RIWADE Mhandisi Ayubu Massau, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu, Moses Msai Mratibu wa RIWADE mkoa wa Singida na Afisa kilimo wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ayub Sengo
Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu na kulia kwake ni Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Bi Haika Massawe wakifatiliakwa makini mafunzo ya namna bora ya kujishughulisha na kilimo cha umwagiliaji kwa kutumia Gree House

Dc Mtaturu akisisitiza jambo wakati wa kufunga mafunzo hayo

Na Mathias Canal, Singida

Uongozi wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida umeahidi kuvisaidia vikundi mbalimbali ambavyo vitakubali kujihusisha na kilimo cha mbogamboga na matunda (Perishable Crops) sambamba na kilimo hicho kwa kutumia Kitalu Nyumba (Green House).

Kauli ya serikali imetolewa na Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe Miraji Jumanne Mtaturu wakati akifunga mafunzo kwa wajasiriamali, wakulima na wafugaji yaliyoendeshwa na Asasi isiyo ya kiserikali ya Right Way For Development (RIWADE) kwenye ukumbi wa Mikutano katika Shule ya Sekondari Ikungi na kuhudhuriwa na watu 115 ambao wanatokea katika Kata 24 kati ya Kata 28 zilizopo Wilayani humo.

Katika Mafunzo hayo jumla ya Vikundi 39 vimehudhuria ambavyo vimetakiwa kujishughulisha zaidi kukimbia kilimo cha mazoea ambacho wakulima hulima msimu mmoja hadi mwingine na hatimaye kujihusisha na kilimo cha umwagiliaji ambacho kinatumia muda mchache kukamilika na kuanza kwa mavuno.

DC Mtaturu amevitaka vikundi hivyo kwa pamoja kutumia vyema fursa ya Makao makuu ya serikali kuhamia Mjini Dodoma kwani itakuwa taswira chanya katika kukuza soko la mazao yao pasina kupata ugumu wa uuzaji.

Amesema kuwa Mkoa wa Singida mara nyingi umekuwa ukitajwa kama mkoa masikini nchini Tanzania kati ya mikoa 10 ambayo ipo mkiani katika maendeleo ya kiuchumi kwa sababu ya wananchi wenyewe kutofanya ubunifu katika kilimo chao jambo ambalo linasababisha uzalishaji mdogo na kupelekea kipato kuendelea kuwa duni ilihali maandalizi ya mashamba ni makubwa.

Mtaturu amesema kuwa wananchi wanapaswa kutoa ushirikiano kwa serikali katika kukamilisha adhma yake katika uwekezaji na Tanzania ya viwanda kwani endapo watakubali kulima kilimo cha kisasa na kuwa na uzalishaji mkubwa itakuwa rahisi kwa serikali kuanzisha viwanda vya kusindika mazao.

Kwa upande wake muwezeshaji wa mafunzo hayo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Asasi isiyo ya kiserikali ya RIWADE ambayo imesajili kwa lengo la kiwasaidia vijana wasio na ajira waweze kufanya kilimo, Ufugaji, Uvuvi na Mazingira Mhandisi Ayubu Massau alisema kuwa wananchi wanapaswa kufikia kilimo cha kuachana na kuuza mazao yao kwa madalali badala yake kuuza moja kwa moja kwa mtumiaji jambo ambalo litatoa fursa chanya ya mafanikio makubwa katika pato la mwananchi mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.

Hata hivyo amepigia chepuo zaidi kilimo cha Kitalu Nyumba (Green House) na kusema kuwa ndicho kilimo pekee chenye uwezo wa kuwatoa wananchi kwenye kadhia ya umasikini kwani kilimo hichp kupitia umwagiliaji wa kisasa unatumia maji machache na matokeo yake ni makubwa kama wakulima watafuata taratibu zote za utunzaji wa shamba.

Massau alisema kuwa umefika wakati wa wananchi kuachana na vyama vya kufa na kuzikana badala yake kujihusisha zaidi na vyama vya kujikwamua kiuchumi kupitia vikundi mbalimbali.

Naye Moses Msai ambaye ni Mratibu wa RIWADE mkoa wa Singida alisema kuwa wakulima wanapaswa kutambua kuwa sekta pekee yenye uwezo wa kuajiri watu wengi na kuwatoa kwenye lindi la umasikini ni Sekta ya Kilimo hivyo ni vyema kufanya kilimo cha kisasa kwani ndicho kitakacho wanufaisha wananchi.

Ametoa fursa kwa wananchi kujiunga na RIWADE kwani watapata fursa ya kuunganishwa na wataalamu ili kuelekezwa namna bora ya kulima kilimo cha umwagiliaji.

Hata hivyo Mjasiriamali na mkulima aliyeshika nafasi ya Kwanza kanda ya kati katika sekta ya kilimo Hassan Tati aliwasihi wakulima hao waliopatiwa mafunzo kuwa mafanikio kwenye kilimo ni makubwa endapo wakulima watafuata taratibu za kilimo na kuwasikiliza wataalamu.

Tati amesema kuwa hakuna ajira nzuri duniani kama kuwekeza kwenye kilimo lakini amewasihi wananchi kuing'ang'ania Asasi ya RIWADE kwani ni taasisi muhimu kwa kila mmoja kwa kujitolea kutoa mafunzo ya kilimo na ufugaji.

Asasi isiyo ya kiserikali ya Right Way For Development (RIWADE) ilianzishwa Mwezi June 2016, ikiwa ni dhima ya kutengeneza na kutoa fursa kwa watanzania wote ili waweze kupata elimu ya ujasiriamali na namna ya kutengeneza mitaji kwa ajili ya ukuaji endelevu wa kijamii na kiuchumi.

SERIKALI imetibu wananchi bure ikiwa ni sehemu ya msaada wake kwa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera.

$
0
0
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (kulia) akipokea maelezo juu ya idadi na thamani ya uharibifu katika shule ya Sekondari Mtukula toka kwa Mkuu wa Wilaya ya Misenyi, Luteni Kanali Denice Filangali Mwila wakati alipowasili Wilayani hapo kwa ajili ya ziara ya kushuhudia baadhi ya maeneo yaliyoathirika na tetemeko la ardhi Mkoani Kagera leo 21 Septemba, 2016.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (kulia) akiangalia athari ya tetemeko katika eneo la Shule ya Msingi Bieju Kata ya Mtukula wakati alipowasili Wilayani Misenyi kwa ajili ya ziara ya kushuhudia baadhi ya maeneo yaliyoathirika na tetemeko la ardhi Mkoani Kagera leo 21 Septemba, 2016.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (kushoto) akiongea na wakazi wa Kata ya Bugandika, Wilayani Misenyi wakati alipofanya ziara Wilayani hapo kushuhudia baadhi ya maeneo yaliyoathirika na tetemeko la ardhi Mkoani Kagera leo 21 Septemba, 2016.PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-WHUSM.


Kauli hiyo imetolewa leo Mkoani Kagera na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama wakati alipofanya ziara Wilayani Misenyi kushuhudia baadhi ya maeneo yaliyoathiriwa na tetemeko la ardhi.

Mhe. Mhagama ameeleza kuwa, Serikali hadi hivi sasa imewatibu watu zaidi ya 400 kupitia hospitali zake za Wilaya na Mkoa kwa kuagiza madaktari kutoka nchini China ambapo zoezi la kusambaza damu pamoja na dawa za kutosha kwa waathirika lilifanyika na hakuna mwananchi aliyetozwa fedha kama malipo ya huduma hiyo.

“Tuishukuru Serikali yetu kwa kutusadia kupata dawa na damu ya kutosha na tulihakikisha kuwa kila mtu aliyepatwa na tetemeko na kujeruhiwa anatibiwa kwa gharama za Serikali ndiyo maana tuliagiza madaktari kutoka China pamoja na Mwanza ili kusaidia kuwatibu wananchi waliopatwa na majeraha makubwa”, alisema Mhe. Mhagama.

Aliongeza kuwa jumla ya wagonjwa ambao kwa sasa wanaendelea kutubiwa hospitalini ni 23 na ndiyo ambao wamefanyiwa upasuaji mkubwa na hali zao zinaendelea vizuri tofauti ilivyokuwa hapo awali.

Alifafanua kuwa, Serikali haiwezi kumsaidia kila mtu kwani haina uwezo huo lakini inajitahidi kurejesha miundombinu yake na taasisi zake zikiwemo zahanati, shule barabara kwa kushirikiana na wadau wanaojitokeza kuunga mkono juhudi za kuwasaidia waathirika wa tetemeko hilo, hivyo ametaka wananchi kujitokeza na kushirikiana kwa pamoja katika kuwasaidia waliopatwa na tukio hilo.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Misenyi Luteni Kanali Denice Filangali Mwila amesema kuwa katiika Wilaya yake sehemu iliyoathirika zaidi ni Kata ya Minziro ambapo jumla ya nyumba 512 haziwezi watu kuishi,pia nyumba 1,524 zenye nyufa mbalimbali zinazohitaji ukarabati, Taasisi za serikali 91 na taaisis 71 za watu binafsi ikiwemo makanisa na misikiti imeathirika na tetemeko hilo.

Ameongeza kuwa tayari amepata msaada wa Serikali katika tukio hilo kupitia Kamati ya Maafa ni ambapo jumla ya maturubai 520 amepewa kwa ajili ya maeneo mbalimbali, chakula, blanketi 240 ambazo pia zimegaiwa kwa waathirika pia.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Bugandika Bw. Amudi Migeyo amewataka wananchi wake kutobeza juhudi za Serikali zinazofanywa sasa ambapo amewataka kuridhika na chochote wakipatacho katika kipindi hiki kigumu.

Hivi karibuni siku ya tarehe 10 Septemba, 2016 mkoa wa Kagera ulikumbwa na ukubwa wa nguvu za mtetemo wa ardhi wa tetemeko la 5.7 kwa kutumia skeli ya ‘Ritcher’ ambapo jumla ya watu 17 walipoteza maisha na majeruhi kadhaa ambapo wengi wao wameshapatiwa matibabu na wanaendelea vizuri.

DAR, PWANI KUKOSA MAJI KWA SAA 12

$
0
0
SHIRIKA LA Majisafi na Majitaka jijini Dar es salaam (DAWASCO), limetangaza kuwapo kwa tatizo la upatikanaji wa huduma ya Majisafi kwa wakazi wa jiji la Dar es salaam, pamoja na Miji ya Kibaha na Bagamoyo mkoani Pwani kutokana na kuzimwa kwa mitambo ya uzalishaji Maji ya Ruvu Juu na Ruvu Chini kwa wastani wa saa 12 siku ya Jumamosi.

Meneja uhusiano wa DAWASCO, Bi. Everlasting Lyaro, ameeleza sababu ya kuzimwa kwa mitambo hiyo ni kuruhusu Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kufanya matengenezo kwenye laini kubwa ya umeme inayotoka Ubungo kwenda kituo cha Tanesco Mlandizi, ambacho kinapeleka umeme kwenye Mtambo wa Maji wa Ruvu Juu na Ruvu Chini.

“Kutokana na Matengenezo hayo yatakayofanywa na Tanesco yatapelekea ukosefu wa huduma ya Maji kwa wakazi wa maeneo ya Mlandizi Mjini, Ruvu Darajani, Vikuruti, Disunyara, Kilangalanga, Janga, Mbagala, Visiga, Maili 35, Zogowale, Misugusugu, Tanita, Kibondeni, Kwa Mathias, Nyumbu, Msangani, Kwa Mbonde, Picha ya Ndege, Sofu, Lulanzi, Gogoni, Kibamba, Kibamba Njia Panda Shule Kibwegere, Mloganzira, Kwembe, Kibamba Hospitali, Kwa Mkinga, na Luguruni,”

“Mji Wa Bagamoyo, Vijiji Vya Mapinga, Kerege na Mapunga. Bunju, Boko, Tegeta, Kunduchi, Salasala, Jangwani, Mbezi Beach na Kawe” alisema Lyaro.

Maeneo mengine yaliyotajwa ni Mlalakuwa, Mwenge, Mikocheni, Msasani, Sinza, Manzese, Mabibo, Kijitonyama, Kinondoni, Oysterbay, Magomeni, Upanga, Kariakoo, City Centre, Ilala, Ubungo Maziwa, Kigogo, Mburahati, Hospitali Ya Rufaa Muhimbili, Buguruni, Changombe, Keko pamoja na Tabata. 

“Tunaomba wananchi wahifadhi Maji kwa kipindi hiki ili wasipate shida wakati tutakapozima mitambo hiyo”. alisema Bi.Lyaro 

WASHIRIKI WA DANCE 100% 2016 WAPEWA NASAHA ZA MAISHA NA WAFANYAKAZI WA VODACOM KUELEKEA FAINALI

$
0
0
 Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(wanne kulia) akifafanua  jambo kwa washiriki wa shindano la Dance 100% 2016 wakati walipotembelea makao makuu ya Vodacom Tanzania  zilizopo Mlimani City jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kujifunza na kujionea huduma  mbalimbali za mawasiliano zinazofanywa na kampuni. Washiriki hao walipata nafasi ya  kupewa nasaha na baadhi ya wafanyakazi iliwaweze kujituma wakati wa  fainali itakayofanyika tarehe 24 mwezi huu kwenye viwanja vya Don bosco Oysterbay  jijini Dar es Salaam, Mshindi wa shindano hilo ataondoka na kitita cha shilingi Milioni 7. Shindano hilo linaandaliwa na EATV na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania na Coco-Cola.
 Washiriki  wa shindano la Dance 100%  2016 wakimsikiliza Meneja wa Huduma kwa wateja wa Vodacom Tanzania,Msamo Willnevilline(kulia) alipotembelea makao makuu ya kampuni hiyo Mlimani City jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kujifunza na kujionea huduma  mbalimbali za mawasiliano zinazotolewa na kampuni hiyo na kupewa nasaha na baadhi ya wafanyakazi ili waweze kujituma wakati wa  fainali itakayofanyika tarehe 24 mwezi huu kwenye viwanja vya Don bosco Oysterbay  jijini Dar es Salaam, Mshindi wa shindano hilo ataondoka na kitita cha shilingi Milioni 7. Shindano hilo linaandaliwa na EATV na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania na Coco-Cola, watatu kutoka kuliani  Meneja  Msaidizi wa Chapa ya Coca-cola, Mariam Sezinga.
 Mmoja wa washiriki wa shindano la Dance 100%  2016,akionyesha umahiri wa kucheza wakati washiriki hao walipotembelea makao makuu ya Vodacom Tanzania Mlimani City jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kujifunza na kujionea huduma  mbalimbali za mawasiliano zinazotolewa na kampuni hiyo na kupewa nasaha na baadhi ya wafanyakazi kuelekea fainali itakayofanyika tarehe 24 mwezi huu kwenye viwanja vya Don bosco Oysterbay  jijini Dar es Salaam, Mshindi wa shindano hilo ataondoka na kitita cha shilingi Milioni 7. Shindano hilo linaandaliwa na EATV na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania na Coco-Cola.
Baadhi ya vijana wanaoshiriki katika shindano la Dance 100% 2016 wakimskiliza mfanyakazi wa Vodacom Tanzania,Neema Kisanga(kushoto)alipokuwa akiwapa nasaha za maisha wakati walipotembelea makao makuu ya Vodacom Tanzania Mlimani City jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kujifunza na kujionea huduma  mbalimbali za mawasiliano zinazotolewa na kampuni hiyo na kupewa nasaha na baadhi ya wafanyakazi kuelekea fainali itakayofanyika tarehe 24 mwezi huu kwenye viwanja vya Don bosco Oysterbay  jijini Dar es Salaam, Mshindi wa shindano hilo ataondoka na kitita cha shilingi Milioni 7. Shindano hilo linaandaliwa na EATV na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania na Coco-Cola.
Meneja  Msaidizi wa Chapa ya Coca-cola, Mariam Sezinga(katikati)akiwa na washiriki wa shindano la Dance 100%  2016,wakati  walipotembelea makao makuu ya Vodacom Tanzania Mlimani City jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kujifunza na kujionea huduma  mbalimbali za mawasiliano zinazotolewa na kampuni hiyo na kupewa nasaha na baadhi ya wafanyakazi kuelekea fainali itakayofanyika tarehe 24 mwezi huu kwenye viwanja vya Don bosco Oysterbay  jijini Dar es Salaam, Mshindi wa shindano hilo ataondoka na kitita cha shilingi Milioni 7. Shindano hilo linaandaliwa na EATV na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania na Coco-Cola.

Bodi ya Vyombo vya Habari vya Chama cha Mapinduzi ( CCM ) yajiuzulu

$
0
0

Bodi ya Uhuru Media Group inayosimamia vyombo vya habari vya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambavyo ni Uhuru Publications Limited (UPL) wachapishaji wa Gazeti la Uhuru, Mzalendo na Burudani pamoja na Peoples’ Media Communication Limited (PMCL) inayoendesha kituo cha redio Uhuru imejiuzulu kupitia barua ya Mwenyekiti wa Bodi hiyo Al-haj Adam O. Kimbisa.

Mwenyekiti wa Taifa wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt John Pombe Joseph Magufuli amepokea barua ya kujiuzulu kwa bodi hiyo leo tarehe 22 Septemba 2016 ambayo nakala yake imenakiliwa kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahaman Kinana. Barua hiyo inaeleza kuwa Mwenyekiti pamoja na wajumbe wote wa Bodi hiyo wameamua kwa hiyari yao kujiuzulu nafasi zao.

Bodi ya Uhuru Media Group ndiyo iliyokuwa na majukumu ya kusimamia, kuzielekeza na kuzishauri Menejimenti ya Makampuni hayo na kubuni mbinu na mikakati ya kuongeza ufanisi katika uendeshaji wa vyombo vya habari vya Chama.

Imetolewa na:-

CHRISTOPHER OLE SENDEKA (MNEC)
MSEMAJI WA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)
Tarehe 22/09/2016.

WAANDISHI WA HABARI WATEMBELEA HOSPITALI YA KISASA YA MUHIMBILI-MLOGANZILA JIJINI DAR LEO.

$
0
0





Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi cha Muhimbili, Profesa Ephata Kaaya akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea katika Hospitali ya Kisasa ya kufundishia wataalamu wa afya na kutoa huduma za afya jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Naibu Makamu Mkuu wa chuo Kikuu cha Afya na Sayansi cha Muhimbili, Dkt. Said Aboud.
 Mwonekano wa Jengo la Hospitali ya Kisasa ya kufundishia wataalamu wa afya na kutoa huduma za afya.

 Baadhi ya Madaktari na wakuu wa vitengo wa Hospitali ya Kisasa ya kufundishia wataalamu wa afya na kutoa huduma za afya wakiwa katika mkutano jijini Dar es Salaam leo.
 Mkandarasi kutoka Korea  kusini Kulia akitoa maelekezo jinsi jengo la Hospitali ya kisasa ilivyo.
Mhandisi Umeme katika jengo la hospitali ya kisasa, Omary Killo akitoa maelekezo mara baada ya kutembelea katika mitambo ya umeme ya jengo hilo. 
 
Baadhi ya Mitambo ya kusafishia maji katika jengo la hosptali hiyo ya kisasa.
Mtaalamu wa Tehama, Andrew Fundamali akitoa maelekezo kwa waandishi wa habari walipotembelea katika mitambo ya tehama katika hospitali hiyo.
 Mwongozaji akitoa maelekezo kwenye chumba cha Kufulia nguo pamoja na kunyoosha katika hosptali hiyo leo.




 Wandishi wakipewa maelekezo walipotembelea katika chumba chenye mashine za MRI na CT scan.
 Daktari bingwa wa Tiba ya Dharula, DK. Hendry Sawe akitoa maelekezo kwa waandishi wa habari walipotembelea chumba cha Dharula.
 Baadhi ya Vitanda vya wagonjwa vilivyopo katika hospitali hiyo.

 Daktali wa kitengo cha Koo, pua na masikio akitoa maelekezo kwa waandishi wa habari.
 Naibu Makamu Mkuu wa chuo Kikuu cha Afya na Sayansi cha Muhimbili na mkuu wa maabala Dkt. Said Aboud akitoa maelekezo kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
 waandishi wakipata maelekezo.
 Mkufunzi wa chuo Kikuu cha Afya na Sayansi shirikishi ya Muhimbili, Paschal Ruggajo akitoa maelekezo kwa waandishi wa habari walipotembelea katika wodi ya wangojwa mabalimbali katika jengo la Mloganzila.

 Mkufunzi wa chuo Kikuu cha Afya na Sayansi shirikishi ya Muhimbili, Wangwe Peter akitoa maelekezo.

 Eneo la Gesi.
Eneo la Majenereta.
 Jengo la hospitali ya Afya na Sayansi shirikishi ya Muhimbili ya Mloganzila muonekano wake kwa nyuma.
 Mwonekano wa Jengo hilo kushoto ukiwa mbele ya jengo hilo.  

Mwonekano wa Jengo hilo kwa mbele.
UJENZI wa Hospitali ya kisasa ya kufundishia wataalamu wa afya na kutoa huduma -shirikishi ya Muhimbili iliyopo Mbezi eneo la Mloganzila jijini Dar es Salaam yakaribia kumalizika kufunga vifaa tiba na kuanza kufanya kazi ifikapo Januari 2017 itaanza kutoa huduma mbalimbali  kwaajili ya kufundishia fani za afya na kutoa huduma ya matibabu yapasayo kwa wagojwa.

Hayo yamesemwa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi cha Muhimbili, Profesa Ephata Kaaya wakati waandishi wa habari  walipotembelea katika hospitali hiyo ya kisasa ya kufundishia wataalamu wa  afya na kutolea huduma mbalimbali za afya hapa nchini.

Amesema kuwa eneo la hospitali hiyo linaukubwa wa ekari 3800 na inauwezo wa kuchukua vitanda 571 na ipo umbali wa Kilomita 25 kutoka jijini Dar es Salaam pia inauwezo wa kuchukua wanafunzi 4000 ikitofautishwa na waliopo sasa ni 1500 tuu.

 Profesa Kaaya amesema kuwa upungufu wa wataalamu wa afya katika mikoa na wilaya hapa nchini ndiko kulikosababisha  Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi shirikishi ya Muhimbili kuanza kutafuta maeneo yakupanua na kujenga hospitali ya Kisasa ya kufundishia wataalamu wa afya na kutoa huduma za afya.

Profesa Kaaya amesema kuwa wagojwa watakaopelekwa katika hospitali hiyo ni wale watakaokuwa wamepewa rufaa kutoka hospitali za mikoa mbalimbali ya hapa nchini.

Amesema kuwa jengo hilo lina sehemu mbili na linaghorofa tisa za juu na ghorofa moja chini ya ardhi linaeneo la Mapokezi, Idara ya Utawala, Idara ya Mahesabu, Phamasia, Idara ya Mionzi, Idara ya wagonjwa wa dharula pamoja na upasuaji wa Dharala, Idara ya afya ya kinywa na meno,chumba cha wagojwa  mahututi, chumba cha kusafisha figo na wadi ya kujifungulia.

Eneo jingine ni vyumba vya kufundishia wanafunzi maktaba ya hospitali, ofisi ya mkuu wa hospitali, ofisi za madaktari na waalimu, ofisi ya Muuguzi Mkuu na kituo cha kopyuta.
Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

MHE. JANUARY MAKAMBA AWATOA WASIWASI WAATHIRIKA WA TETEMEKO KAGERA

$
0
0

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mhe. January Makamba (kushoto) akimpa pole waathirika wa tetemeko la ardhi waliolazwa Hospitali ya Rufaa ya Bukoba leo 22/9/2016.
maka2
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mhe. January Makamba (kushoto) akiwapa pole waathirika wa tetemeko la ardhi waliolazwa Hospitali ya Rufaa ya Bukoba leo 22/9/2016.
maka4
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mhe. January Makamba (kulia) akimpa pole Mwalimu Mkuu Shule ya Sekondari Ihunga Bw.Thomas Bonevanture mara alipowasili shuleni hapo kuwapa pole waathirika leo 22/9/2016.
maka5
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mhe. January Makamba (katikati) akiwa ameongozana na Mkuu wa Wilaya ya Misenyi Luteni Kanali Denice Filangali Mwila (kushoto) pamoja na Diwani wa Kata ya Bugandika Bw. Amudi Migeyo kwenda kuangalia maeneo yaliyoathirika na tetemeko la ardhi leo 22/9/2016 Wilayani Misenyi.
maka6
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mhe. January Makamba (wa pili kushoto) pamoja na viongozi wengine wakiwapa pole baadhi ya waathirika wa tetemeko la ardhi Wilayani Misenyi leo 22/9/2016.
……………………………………………………………..
Na Benedict Liwenga-WHUSM, Bukoba.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mhe. January Makamba amewatoa wasiwasi waathirika wa tetemeko la ardhi lilitokea Wilayani Bukoba Mkoani wa Kagera.
 
Mhe. Makamba ameyasema hayo leo mkoani Kagera wakati wa ziara yake ya kutembelea maeneo mbalimbali yaliyokumbwa na tetemeko hilo kwa lengo la kuwapa pole waathirika na kuwap ujumbe wa Serikali kuhusu namna inavyojitahidi kuwasaidia waathirika hao.
 
Amesema kwamba, wananchi wasiwe na wasi wasi kuhusu suala la kupatiwa misaada ya dharura kwani Serikali imejipanga na bado inaendelea na zoezi la kufanya tathmini ya uharibifu uliotokea ingawa zoezi la kuwapatia baadhi ya huduma za msingi linaendele.
 
“Tumekuja kutoa msaada kwa mji kwa ujumla wakati tunapanga namna ya kusaidia katika masuala ya mazingira na tambueni kuwa Serikali inawajali ndiyo maana kuna viongozi wakubwa wako hapa na wengine wanazidi kuja”, alisema Mhe. Makamba.
 
Aliongeza kuwa, suala la kuwasaidia waathirika wa tetemeko hilo limepewa uzito mkubwa na Serikali na suala la kuchelewa kwa kutolewa kwa misaada kunatokana na umakini unaoendelea kufanywa sasa hivi na Serikali ili kuwatendea haki waathirika pekee.
 
Naye Mkuu wa Wilaya ya Misenyi Luteni Kanali Denice Filangali Mwila amesema kuwa katika Wilaya yake sehemu iliyoathirika zaidi ni Kata ya Minziro ambapo jumla ya nyumba 512 haziwezi watu kuishi,pia nyumba 1,524 zenye nyufa mbalimbali zinazohitaji ukarabati, Taasisi za serikali 91 na taaisis 71 za watu binafsi ikiwemo makanisa na misikiti imeathirika na tetemeko hilo.
 
Ameongeza kuwa tayari amepata msaada wa Serikali katika tukio hilo kupitia Kamati ya Maafa ambapo jumla ya maturubai 520 amepewa kwa ajili ya maeneo mbalimbali, chakula, blanketi 240 ambazo pia zimegaiwa kwa waathirika hao.
 
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Bugandika Bw. Amudi Migeyo amewataka wananchi wake kutobeza juhudi za Serikali zinazofanywa sasa na amewataka kuridhika na chochote wakipatacho katika kipindi hiki kigumu.
 
Hivi karibuni siku ya tarehe 10 Septemba, 2016 mkoa wa Kagera ulikumbwa na ukubwa wa nguvu za mtetemo wa ardhi wa tetemeko la 5.7 kwa kutumia skeli ya ‘Ritcher’ ambapo jumla ya watu 17 walipoteza maisha na majeruhi kadhaa ambapo wengi wao wameshapatiwa matibabu na wanaendelea vizuri.

Waziri Jenista afanya ziara wilaya ya Kyerwa.

$
0
0
 Waziri Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu Jenista Muhagama akimpa pole mwalimu Anna Mollel wa shule ya msingi Ileega ambaye nyumba yake imebomoka kutokana na tetemeko la ardhi.
kye8
Waziri Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu Jenista Muhagama akikagua nyumba ya mwalimu Anna Mollel wa shule ya msingi Ileega ambaye nyumba yake imebomoka kutokana na tetemeko la ardhi.
kye9
Waziri Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu Jenista Muhagama akiongea na baadhi ya watoto wilayani Kyerwa wakati akiwa kwenye ziara kujionea madhara ya tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera.
kye10
Waziri Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu Jenista Muhagama akiongea na watoto wakati wa ziara ya kujionea maeneo yaliyoathirika na tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera.
kye12
Waziri Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu Jenista Muhagama akiongea na mkulima wa viazi wilayani Kyerwa Shakiru Issa wakati wa ziara ya kujionea maeneo yaliyoathirika na tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera.Picha na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Kyerwa, Kagera.
kye1
Waziri Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu Jenista Muhagama akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Kanali Mstaafu Shaban Lissu mara baada ya kuwasili wilayani humo kujionea madhara ya tetemeko la ardhi lililotokea mkoani humo.
kye2
Waziri Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu Jenista Muhagama akioneshwa ramani ya wilaya ya Kyerwa na Mkuu wa Wilaya hiyo Kanali Mstaafu Shaban Lissu   inaonesha maeneo yaliyoathiriwa na tetemeko la ardhi. Wa kwanza kulia ni Mbunge wa Kyerwa Innocent Bilakwate.
kye4
Diwani wa Kata ya Itera (CHADEMA) akimueleza Waziri Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu Jenista Muhagama ukame ulivyoathiri mimea ya kahawa na migomba katika kata hiyo leo wilayani humo.
kye5
Waziri Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu Jenista Muhagama akimpa maagizo Mkuu wa Wilaya Kanali Mstaafu Shaban Lissu   kuhusu kuanzisha kampeni ya kupanda mazao yanayokomaa kwa muda mfupi wakati alipotembelea maeneo yaliyoathirika na tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera.
kye6
Waziri Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu Jenista Muhagama akiongea na baadhi ya wananchi wa wilaya ya Kyerwa alipotembelea maeneo yaliyoathirika na tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera.
 

MAGRUPU YA WHATSAPP YA JUKWAA LA UONGOZI NA LEADERS FORUM YAKABIDHI MIL.16 KUSAIDIA WAATHIRIKA WA TETEMEKO KAGERA

$
0
0
Waziri Mkuu Mhe.  Majaliwa Kassim Majaliwa akipokea Mfano wa hundi ya shilingi Milioni 16 kutoka kwa mratibu wa magrupu ya Whatsapp ya LEADERS NA UONGOZI, Dk. Ave Marie Semakafu katika hafla fupi ya makabidhiano hayo ambayo imefanyika ofisini kwa Waziri Mkuu Jijini Dar es Salaam leo.
 Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa na mratibu wa magrupu ya Wasap, Dk.Ave Marie Semakafu akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanachanachama wa magrupu ya Whatsapp ya LEADERS  FORUM NA JUKWAA LA UONGOZI   katika hafla fupi ya makabidhiano hayo ambayo imefanyika ofisini kwa Waziri Mkuu Jijini Dar es Salaam leo.

----------------------------------------------------
Imedhihirika kuwa magrupu ya Whatsapp  yanaweza kuwa chachu ya Maendeleo  baada  ya wanachama wa magrupu mawili ya whatsapp ya LEADERS FORUM na  JUKWAA LA UONGOZI  leo Septemba 22, 2016 kumkabidhi Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa jumla ya shilingi  16m/-, kwa ajili kusaidia waathirika wa tetemeko  la ardhi mkoani Kagera.

Akizungumza katika hafla hiyo, mmoja wa waratibu wa magrupu hayo Dk.Ave Marie Semakafu amesema fedha hizo ni michango ya wanachama wa magrupu hayo yenye jumla ya wanachama 491. Amesema wanachama hao wameguswa na yaliyowakuta Watanzania wenzao mkoani Kagera hivyo waliona njia pekee ya kuungana nao katika majonzi ya janga hilo ni kutoa kidogo walichonacho. 

Dk Semakafu amewaasa watanzania wengine, hasa walioko kwenye vikundi mbalimbali hususani vya mitandaoni, kushiriki katika zoezi hilo la kuwachangia waathirika hao kwa vyovyote wawezavyo, maana hali bado ni mbaya mkoani Kagera. Hatua hiyo ni ya kwanza kwa magrupu ya mitandaoni nchini Tanzania kufanya harambee na kukusanya pesa kwa ajili ya waathirika wa tetemeko la Ardhi mkoani Kagera.

Dkt Semakafu alisema madhumuni ya magrupu hayo ni kujadili maendeleo ya Taifa pamoja na kutoa ushauri mbinu mbadala kuifikia ndoto ya Tanzania tunayoiyaka.

Tetemeko hilo lilitokea Septemba 10, mwaka huu ambapo watu 17 wamepoteza maisha,wengine zaidi ya 200 wameruhiwa,huku nyumba zaidi ya 800 zikiwa zimeharibika,zingine kuanguka. 

Akiongea katika hafla hiyo Waziri Mkuu Majaliwa aliwashukuru wanachama wa majukwa hayo akisema wanapaswa kuwa mfano wa  kuigwa na makundi mengine nchini. 

 "Sisi kama serikali tunawashuru sana kwa moyo huo wa upendo kwa wenzetu wa Kagera,na hatutaishia hapa bali tutafanya hivyo kwa maandishi", alisema Waziri Mkuu na kuyaahakikishia wachangiaji waliokabidhi misaada yao leo yakiwemo  makampuni mbalimbali na vikundi vingine vitano kuwa atahakikisha misaada yote itawafikia walengwa.

Wanachama wa majukwaa hayo ni watu wa kada mbalimbali hususani viongozi wa serikali wa sasa na wastaafu,akiwemo Waziri Mkuu Mstaafu Mh.Mizengo Pinda.Wengine ni Mawaziri,Wabunge, wakuu wa mashirika ya umma na binafsi, wanataaluma wa vyuo vikuu, wanahabari, Wafanyabiashara na Viongozi wa vyama vya Siasa.

Waratibu wengine wa magrupu hayo ni Dereck Murusuli,Benjamin Thompson Kasenyenda,Leila Sheikh, Dr.Michael Francis, Maggid Mjengwa, Mustafa Ismail Kambona, Zamaradi Kawawa na June Warioba.

WAZIRI WA UJENZI PROFESA MBARAWA ATAKA WADAU WA UJENZI WALA RUSHWA WAFUTIWE LESENI ZAO

$
0
0
Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Profesa, Makame Mbarawa (kushoto), akihutubia wakati akifungua Semina ya 26 ya utoaji elimu endelevu kwa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi Dar es Salaam leo asubuhi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi, Ambwene Mwakyusa akizungumza katika semina hiyo.
Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Profesa, Makame Mbarawa (kushoto), akipeana mkono na Msaji wa Bodi hiyo Jehad Jehad baada ya kumaliza kutoa hutuba yake.
Wadau wa sekta ya ujenzi wakiwa kwenye semina hiyo.

Wadau wa sekta ya ujenzi wakiwa kwenye semina hiyo.

Taswira meza kuu katika semina hiyo.

Picha ya pamoja na mgeni rasmi Waziri Mbarawa.
Picha ya pamoja na mgeni rasmi, Waziri Mbarawa (aliyekaa katikati), Wengine kutoka kulia waliokaa ni Mkurugenzi wa Huduma na Ufundi kutoka Wizara ya Ujenzi, Profesa Mhandisi William Nshana, Mwenyekiti wa Bodi, Ambwene Mwakyusa, Msajili wa Bodi, Jehad Jehad na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili, Dk.Adelina Kikwasi.

Na Dotto Mwaibale

WAZIRI wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Profesa, Makame Mbarawa, ameitaka Bodi ya Usajili Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi kuwafutia leseni wadau wa sekta ya ujenzi  watakao bainika kuomba au kupokea rushwa.

Katika hatua nyingine Profesa  Mbarawa ameitaka  Bodi hiyo kuandaa  orodha ya wakadiriaji majenzi na wabunifu  majengo wasiyofuta maadili ya kazi zao ili iwekwe hadharani na wasipate tenda za kufanya kazi popote.

Profesa Mbarawa ametoa kauli hiyo wakati akifungua Semina ya 26 ya utoaji elimu endelevu kwa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi Dar es Salaam leo na kueleza kazi yoyote iwe nzuri na bora ni lazima kuepuka rushwa na kufuata  maadili na kanuni za kazi.

“Napenda niwagize bodi kuanzia sasa nataka wakadiriaji majenzi na wabunifu majengo na wadau wote wa sekta ya ujenzi ambao ni wara rushwa muwafutie leseni zao  ili wasiweze kupata tenda au kutoa tenda.Maadili katika kazi zenu ni jambo la msingi na si vinginevyo,”alisema Profesa Mbarawa.

Mbarawa aliigiza bodi hiyo kuandaa orodha ya watakao kuwa  si waadilifu ili kuonyesha katika jamii kuwa hawa hawasitahili kupewa tenda ya aina yoyote. 

Alisema baada ya kuandaa orodha hiyo  ni vizuri ikatangazwe hata katika vyombo vya habari ili iwe fundisho kwa wengine wenye vitendo hivyo.

Mbarawa aliwataka wakadiriaji majenzi na wabunifu majengo nchini kuchangamkia fursa mbalimbali zilizopo katika serikali ya Awamu ya Tano ili kuweza kjiongezea mitaji.

“Kuna mradi wa ujenzi wa Reli ya kiwango cha kisasa unakuja na serikali imetenga Sh. Trilioni 1, lazima kutakuwa na ujenzi wa majengo hiyo ni fursa mbayo mnaweza kuitumia kujiongezea uwezo, lakini kama mtafanya kazi kwa kuungana njia hiyo inaweza kuwasaidia kupata tenda hizo.” alisema.

Awali, akizungumza katika semina hiyo, Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Ambwene Mwakyusa, alisema semina hizo zimekuwa na faida kwa wakadiriji majenzi na wabunifu, kwani zinawaongezea uwezo wa kujua mambo mbalimbali na kwamba zimekuwa zikifanyika kila mwaka mara mbili na zimewanufaisha wadau wa sekta ya ujenzi 5,328.

WAZIRI SIMBACHAWENE ATEMBELEA BANDA LA MAONESHO LA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI (NEC) KWENYE MKUTANO WA ALAT MJINI MUSOMA.

$
0
0
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi  Bw.Kailima Ramadhani akimkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. George Simbachawene kwenye banda la maonesho la Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakati wa mkutano wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) unaofanyika  mjini Musoma leo.

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi  Bw. Kailima Ramadhani (kulia) akitoa ufafanuzi kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. George Simbachawene kuhusu majukumu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi alipotembe banda la maonesho la Tume hiyo kwenye mkutano wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) mjini Musoma. Tume ya Taifa ya Uchaguzi inaendelea kutoa elimu ya mpiga kura kwa wananchi na wadau mbalimbali nchini.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. George Simbachawene akiangalia vipeperushi na machapisho mbalimbali kwenye banda la maonesho la Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakati wa mkutano wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) mjini Musoma leo. Kulia ni Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi  Bw. Kailima Ramadhani.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. George Simbachawene akisaini kitabu cha wageni alipotembelea banda la maonesho la Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakati wa mkutano wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) mjini Musoma leo. Mbele yake ni Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi  Bw. Kailima Ramadhani, Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Tume Emmanuel Kawishe na Naibu Katibu wa Idara ya Habari na Elimu kwa Umma, Giveness Aswile.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. George Simbachawene (kulia) akifurahia jambo na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi  Bw. Kailima Ramadhani wakati alipotembelea banda la maonesho la Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakati wa mkutano wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) mjini Musoma leo.

 Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi  Bw. Kailima Ramadhani(kushoto) akiwa na Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mkuu Mstaafu wa Zanzibar Hamid M. Hamid (katikati) na Mjumbe wa Tume Mhe. Mchanga Mjaka wakiwa kwenye mkutano wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) mjini Musoma leo.

 Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi  Bw. Kailima Ramadhani (Kulia), akizungumza na Naibu Katibu wa Idara ya Habari na Elimu kwa Umma, Giveness Aswile (mbele yake) kwenye banda la maonesho la Tume hiyo wakati wa mkutano wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) mjini Musoma leo.Wengine ni Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Tume Emmanuel Kawishe, Afisa Habari Christina Njovu na Afisa Utumishi wa Tume Veronica Mollel.

 Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi  Bw. Kailima Ramadhani (kushoto), akimuelimisha mkazi wa Baruti mjini Musoma, Ismail Adudu alipotembelea banda la maonesho la Tume hiyo kwenye mkutano wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) mjini Musoma leo.Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Tume Emmanuel Kawishe, Naibu Katibu wa Idara ya Habari na Elimu kwa Umma, Giveness Aswile.

 Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi  Bw. Kailima Ramadhani (kushoto), akimuelimisha mkazi wa Baruti mjini Musoma, Ismail Adudu alipotembelea banda la maonesho la Tume hiyo kwenye mkutano wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) mjini Musoma leo.

Afisa Utumishi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Veronica Mollel akitoa elimu kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kowak ya Rorya mkoani Mara wakati walipotembelea banda la maonesho la Tume hiyo kwenye mkutano wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) mjini Musoma leo. Picha/ Aron Msigwa na Hussein Makame –NEC.



LAPF NA TAASISI MBALIMBALI ZACHANGIA MIL.172 MAAFA KAGERA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea hundi ya shilingi milioni 20 kutoka kwa Meneja wa Kanda wa LAPF, Amina Kassim (kulia) na Kafiti Kafiti wa LAPF ukiwa ni mchango wa Mfuko huo kwa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera. Makabidhiano hayo yalifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Septemba 22, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea sehemu ya msaada ya vyakula wenye thamani ya shilingi milioni 10 kutoka kwa viongozi wa Mfuko wa Kimataifa wa Art of Living ukiwa ni msaada kwa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera, Septemba 22, 2016. Kutoka kushoto ni Nishitha Kulshreshtha, Nishit Patel, Neha Movaliya,Sharik Choughule ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM wa Shina la Pamba Road, Upanga na Neha Movaliaya.


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea hundi ya Shilingi milioni 16 kutoka kwa Dkt. Ave Maria Semakafu (kulia), Berious Nyasebwa (wapili kushoto) na Benjamin Thomson wote kutoka Group la Whats App la Leaders Forum ukiwa ni mchango wa group hilo kwa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera. Makabidhiano hayo yalifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Septemba 21, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwashukuru viongozi wa Jumuiya ya Ahmadiyya ambao walitoa mchango wa shilingi milioni 10 kwa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera, Septemba 22, 2016. Makabidhiano hayo yalifanyika ofisini kwa Waziri Mkuu jijini .Kutoka kushoto ni Sheikh Tahir Mahmood Chaundhry, Issa Mwakitalima, Khuram Shahzad na Jamil Mwanga.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea mchango wa tani 40 za saruji zenye thamani ya shilingi milioni 16.5 kutoka kwa Dhruv Jog na Lebulu Victor (kulia) wote wa Kampuni ya ujenzi a Advent ukiwa ni mchango kwa waahirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera Septemba 22, 2016. Makabidhiano hayo yalifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea hundi ya shilingi milioni 100 kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya VODACOM TANZANIA, Bw. Ian Ferrao (kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo, Rosalynn Mworia ukiwa ni mchango kwa waarhirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera, Ofisini kwake jijini Dar es salaam Septemba 22, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
 
…………………………………………………………………………..

TAASISI sita zikiwemo za dini na kijamii zimechanga jumla ya sh. milioni 172.5 zikiwa ni misaada kwa wananchi walioathirika na tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera Septemba 10, mwaka huu.

Mchango huo umepokelea leo jioni (Alhamisi, Septemba 22, 2016) na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es Salaam.

Akikabidhi hundi kwa Waziri Mkuu, Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom, Bw. Ian Ferrao alisema kiasi cha sh. Milioni 100 kimekusanywa kutoka kwenye mfuko wa Vodacom Foundation pamoja na wadau wao.

Bw. Ferrao amesema kampuni ya Vodacom imekuwa mstari wa mbele kusaidiana na Serikali katika uboreshaji wa miradi mbalimbali za kijamii…..

Taasisi nyingine iliyochangia ni Mfuko wa Pensheni wa LAPF ambapo Meneja wa Kaya ya Dar es Salaam, Amina Kassim amemkabidhi Waziri Mkuu hundi ya sh. milioni 20.

Pia Jumuiya ya Kiislam Ahmadiyya imekabidhi msaada wa sh. milioni 10 kati ya hizo sh. milioni nne ni fedha taslimu na zilizobaki ni mabati na mifuko ya saruji.

Naye Mkurugenzi wa kampuni ya ujenzi ya Advent, Dhruv Jog amemkabidhi Waziri Mkuu msaada wa tani 40 za saruji yenye thamani ya sh. milioni 16.5 na kusema kwamba wameshtushwa na tukio hilo na tayari saruji hiyo imeanza kupelekwa Kagera.

Kwa upande wake mwakilishi wa Taasisi ya kimataifa ya Art of Living, Neetu Kulshreshtha wametoa msaada wa vyakula mbalimbali pamoja dawa vikiwa na thamani ya sh. milioni 10.

Dk. Ave Maria Semakafu amemkabidhi Waziri Mkuu hundi ya sh milioni 16 kwa niaba ya makundi mawili ya mtandao wa kijamii wa WhatsApp. Makundi hayo yanaitwa Leaders na Uongozi.

Akitoa shukrani kwa waliotoa michango yote hiyo, Waziri Mkuu amewashukuru kwa misaada hiyo na kuahidi kuwa Serikali itahakikisha michango hiyo inafikishwa Kagera kwa walengwa.

“Tunashukuru sana kwa michango yote. Tunashukuru na makundi ya WhatsApp ya Leaders na Uongozi ambayo nayo yameamua kuja kutuchangia. Michango hii inaonyesha kuguswa na mapenzi ya dhati kwa waliopatwa na maafa,” amesema.

Waziri Mkuu amesema Serikali inakamilisha tathmini ya maafa hayo na kuahidi kutoa taarifa ya kiasi kilichokusanywa na kiasi kilichotumika. Amewaomba wananchi waliotoa ahadi zao za michango wakamilishe ahadi zao.

Akaunti ya maafa imefunguliwa katika Benki ya CRDB yenye Namba. 015 222 561 7300 kwa jina la KAMATI MAAFA KAGERA – Swiftcode: CORUtztz na namba za simu za mkononi zinazotumika kupokea michango hiyo ni 0768-196-669 (M-Pesa), au 0682-950-009 (Airtel Money) au 0718-069-616 (Tigo Pesa).

Tetemeko hilo lililotokea Jumamosi, Septemba 10, mwaka huu na kusababisha vifo vya watu 17 na wengine 440 walijeruhiwa kati yao watu 253 walifikishwa Hospitali ya Mkoa, 153 walilazwa, 113 walitibiwa na kuruhusiwa na wengine 38 wanaendelea na matibabu ambapo kati yao watu 23 wamefanyiwa upasuaji mkubwa na wanaendelea vizuri.

Pia tetemeko hilo limesababisha nyumba 2,063 kuanguka huku nyingine 14,081 zikiwa katika hali hatarishi baada ya kupata nyufa na 9,471 zimepata uharibifu mdogo huku wananchi 126,315 wakihitaji misaada mbalimbali.
Viewing all 46362 articles
Browse latest View live




Latest Images