Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live

RAIS WA ZANZIBAR ATEMBELEA SEHEMU MBALIMBALI KUJIONEA MAENDELEO.

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Fundi Mkuu wa Mitambo ya ZBC Redio Nd,Ali Aboud (wa pili kushoto)alipotembelea mitambo ya  kurushia matangazo ya masafa ya Kati kiliopo Bungi Miembemingi leo
Picha na Ikulu. 20/09/2016.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akisalimiana na Waziri wa Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji  Mhe,Ali Abeid Karume pamoja na Viongozi mbali mbali mara alipowasili Kijiji cha Jendele Wilaya ya Kati Unguja kuangalia maendeleo ya Ujenzi wa  barabara ya Jendele-Unguja Ukuu Mkoa wa Kusini Unguja leo ,inayojengwa na Idara ya Ujenzi ya Mfuko wa Barabara wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akisalimiana na  Viongozi mbali mbali mara alipowasili Kijiji cha Jendele Wilaya ya Kati Unguja leo kuangalia maendeleo ya Ujenzi wa  barabara ya Jendele-Unguja Ukuu Mkoa wa Kusini Unguja,inayojengwa na Idara ya Ujenzi ya Mfuko wa Barabara wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,[Picha na Ikulu.] 20/09/2016.

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi Mfuko wa Barabara katika Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Nd,Ali Tahir wakati alipokuwa akiangalia mashine ya kuwekea lami barabarani ambayo imeharibika akiwa katika ziara ya siku moja kutembelea barabara ya Jendele-Unguja Ukuu Mkoa wa Kusini Unguja leo.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akiwauliza masuali Watoto wa Skuli ya Jendele Wilaya ya Kati Unguja leo wakati alipofanya ziara ya siku moja kutembelea barabara ya Jendele-Unguja Ukuu Mkoa wa Kusini Unguja leo,[Picha na Ikulu.] 20/09/2016.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) akifuatana na wasaidizi wake na Viongozi mbali mbali wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika maeneo ya kituo cha kurushia matangazo ya masafa ya Kati cha Redio Zanzibar ZBC huko Bungi Miembemingi leo,pia kujionea uchafuzi wa mazingira unaofanyika katika maeneo hayo


CCM ZANZIBAR YAPIGA MSASA WAWAKILISHI

$
0
0
Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho Zanzibar


Na Is-haka Omar, Zanzibar.

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimewataka Wawakilishi, Wabunge na Madiwani wa Chama hicho kujenga utamaduni wa kutoa taarifa za utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2015/2020 kila baada ya miezi mitatu ili kuongeza ufanisi wa kiutendaji.

Rai hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho Zanzibar, Vuai Ali Vuai alipokuwa akizungumza na Kamati ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wanaotokana na CCM Zanzibar huko Afisini Kwake Kisiwandui Mjini hapa.

Alisema viongozi hao wamekuwa wakifanya kazi mbali mbali za kimaendeleo ambazo ni miongoni mwa utekelezaji wa Ilani ya CCM, lakini zimekuwa hazijulikani kwa baadhi ya wananchi na viongozi wa Chama kutokana na kutofuatwa utaratibu wa kutoa taarifa rasmi kila baada ya miezi mitatu ili zijadiliwe na ngazi husika kama ibara ya 189 ya ilani ya CCM inavyoelekeza.

Vuai aliwakumbusha Viongozi hao kwamba licha ya majukumu waliokuwa nayo katika vyombo vya kutunga sheria bado wana jukumu kubwa la kuhakikisha wanawatumikia wananchi kwa ufanisi katika kupunguza kero na changamoto zinazowakabili katika maeneo yao.

“Nakukumbusheni kwamba suala la kutoa taarifa ya utekelezaji wa ilani ya CCM katika majimbo yenu ni muhimu sana kwani ndio kipimo cha utendaji wenu kwa wananchi, na hatua hiyo itatoa fursa kwa viongozi mbali mbali wa chama kuhoji ni kwa namna gani kila kila kiongozi anatekeleza wajibu wake kwa wananchi na chama kwa ujumla.”

Kwani hata kwa upande wa Chama Makao Makuu tunatoa taarifa mbali mbali za utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa upande wa Zanzibar Makamo wa Pili wa Rais anatoa taarifa na upande wa Tanzania bara Waziri Mkuu atatoa taarifa ili kujua Chama na Serikali wamefanya nini kwa wananchi na zinajadiliwa na kuhojiwa,”, alieleza Vuai na kuongeza kuwa endapo viongozi hao watashirikiana kikamilifu wataweza kupunguza kwa haraka changamoto zinazowakabili wananchi Majimboni.

Alieleza kwamba viongozi hao waliochaguliwa na wananchi, wanatakiwa katika utekelezaji wa Majukumu yao kuhakikisha wanawashirikisha Viongozi wa Chama wa ngazi mbali mbali ili waweze kutathimini na kuweka kumbukumbu za kazi hizo kwa usahihi.

Alisema kila kiongozi aliyetokana na CCM anatakiwa kuendelea kuongozwa na dhana ya ushindani wa maendeleo ndani ya jimbo lake ili aweze kuaminiwa na wananchi waliomchagua.

Naibu Katibu Mkuu huyo, alieleza kuridhishwa kwake na kasi ya kiutendaji ya baadhi ya viongozi wakiwemo wawakilishi, wabunge na Madiwani katika maeneo yao na kuwasihi kuendelea kujituma ili kutengeneza tiketi halali ya kuaminiwa na wananchi waliowapa dhamana za uongozi.

Sambamba na hayo aliwasihi kujenga utamaduni wa kufanya ziara za mara kwa mara katika maeneo mbali mbali yaliyopo katika majimbo yao ili kubaini changamoto sugu zinazowakabili wananchi ili zipatiwe ufumbuzi kwa haraka.

Alisema viongozi wa Chama hicho, wanatakiwa kuwa mfano wa kuigwa kwa kila sekta kwani kufanya hivyo ndio taswira halisi ya ukomavu wa kisiasa wa CCM.

Aidha aliwapongeza Wajumbe hao wakiwemo Mawaziri na Manaibu Mawaziri kwa juhudi zao za kufanya kazi kwa bidii katika kuwaletea wananchi maendeo katika Nyanja mbali mbali za kiuchumi, kijamii na kisiasa.

Alifafanua kwamba kasi ya utekelezaji wa Ilani ya Chama hicho kwa baadhi ya majimbo inaongeza faraja kwa wananchi hasa katika juhudi za kuomarisha miundo mbinu mbali mbali ikiwemo Ujenzi wa vituo vya afya na ununuzi wa dawa na ununuzi wa gari za wagonjwa.

Kwa upande wa sekta ya elimu alizitaja juhuzi za viongozi hao kwamba wameweza kuimarisha mabanda (madarasa) na kununua bati za kuezekea sambamba na kununua madawati ili kuwasaidia wanafunzi wakae katika mazingira bora.

Akizungumzia sekta ya Miundombinu ya Barabara na Maji alisema baadhi ya viongozi wameweza kutengeneza barabara za ndani na kushirikiana na serikali kufikisha huduma za maji kwa wananchi.

Sambamba na hayo amewashauri viongozi hao kuhakikisha wanashiriki kikamilifu vikao vyote vya Baraza la Wawakilishi Zanzibar na Bunge, kwani kupitia vikao hivyo ndio wataweza kuwasilisha, kuhoji, kushauri na kuitaka serikali kutatua kwa haraka changamoto zinazowakabili wananchi.

Pamoja na hayo Naibu Katibu Mkuu Vuai aliwambia viongozi hao kwamba kwa yeyote atakayetaka ushauri na muongozo wa jambo lolote la kichama, Afisi yake ipo tayari kumuunga mkono wakati wowote ili kuhakikisha kazi na majukumu waliopewa na wananchi yanafanyika kwa ufanisi zaidi.

HIVI NDIVYO NDEGE YA KWANZA YA ATCL ILIVYOTUA JIJINI DAR LEO

GLOBAL EDUCATION LINK (GEL) YAONGOZA KWA KUPELEKA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU VYA NJE AFRIKA MASHARIKI

$
0
0

Mkurugenzi Mtendaji wa Global Education Link (GEL), Abdulmaalik Mollel akizunguza waandishi wa habari leo wakati akisafirisha wanafunzi 200 kwenda vyuo vikuu vya nchini China katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Wafatnyakazi wa Global Education Link (GEL) wakifanya uhakiki wa hati za kusafiria pamoja na Viza kwa wanafunzi wanaokwenda kusoma vyuo vikuu vya China leo katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanafunzi wanaokwenda katika Vyuo Vikuu nchini China wakiingia kwenye jengo la maalumu la ukaguzi kabla ya kuanza safari katika uwanja huo Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanafunzi wanaokwenda Vyuo Vikuu nchini China wakiagana na familia zao kwa kupiga picha ya pamoja katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanafunzi wanaokwenda katika Vyuo Vikuu nchini China wakiingia kwenye jengo la maalumu la ukaguzi kabla ya kuanza safari katika uwanja huo Jijini Dar es Salaam.


WANAFUNZI wataokosa nafasi za vyuo vikuu bado na wana nafasi ya kujiunga na vyuo vikuu vya nje kupitia Global Education Link (GEL).

Hayo ameyasema leo Mkurugenzi Mtendaji wa Global Education Link (GEL), Abdulmaalik Mollel wakati kuondosha wanafunzi 200 kwenda katika vyuo vikuu vya nchini China, amesema GEL ni kampuni inayoongoza kupeleka wanafunzi kwenda vyuo vikuu vya nje vya Afrika Mashariki hivyo wazazi watumie nafasi kupeleka wanafunzi katika vyuo vya nje.

Amesema kuwa Global Education Link(GEL) ina uhakika wanafunzi watakayehitimu watakuwa na mchango mkubwa kwa taifa katika Teknolojia ya uhandisi wa petrol , Biashara pamoja na utabibu.

Mollel amesema kuwa wanafunzi wanaweza kukopeshwa kwa asilimia 50 na kulipa ndani miezi sita ikiwa kuhakikisha wanafunzi wanatimiza ndoto zao n kuwa na mchango a taifa. Aidha amesema kuwa wanafunzi wanaokwenda mazingira ya usalama ni uhakika kwa kuanza kwa safari hadi wanafika katika vyuo husika .

Mollel amesema kuwa vijana wasikate tamaa Global Education Link (GEL) iko kwa ajili ya yao katika kuhakikisha ndoto zao hazipotei kutokana na kukosa nafasi katika vyuo vya ndani

Amesema kuwa wazazi waache kuogopa gharama za kusoma vyuo vya nje kwani gharama za kusoma nje ni sawa na vyuo vya ndani hivyo vijana watumie furssa hizo.

TAZAMA TUKIO LA PICHA LA KUWASILI KWA NDEGE YA ATCL JIJINI DAR LEO

$
0
0


Moja ya Ndege mpya mbili zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya kampuni ya ndege Tanzania (ATCL) ikipata saluti ya maji (Water Canon Salutation) toka kwa magari ya Jeshi la Zimamoto na Ukoaji mara tu bada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere saa sita na robo juu alama leo Septemba 20, 2016

Katibu Mkuu wa Uchukuzi Dkt Leonard Chamriho akisalimiana na Rubani aliyerusha Ndege mpya moja kati ya mbili zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya kampuni ya ndege Tanzania (ATCL) ikiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere saa sita na robo juu alama leo Septemba 20, 2016.
Katibu Mkuu wa Uchukuzi Dkt Leonard Chamriho na Mkurugenzi wa Kampuni ya Bombadier Commercial Aircraft Bw. Pardeep Sandhu, na maofisa wengine wakiwa kwenye Moja ya Ndege mpya mbili zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya kampuni ya ndege Tanzania (ATCL) mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius leo Septemba 20, 2016


Katibu Mkuu wa Uchukuzi Dkt Leonard Chamriho na Mkurugenzi wa Kampuni ya Bombadier Commercial Aircraft Bw. Pardeep Sandhu, na maofisa wengine wakiwa kwenye Moja ya Ndege mpya mbili zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya kampuni ya ndege Tanzania (ATCL) mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius leo Septemba 20, 2016
Katibu Mkuu wa Uchukuzi Dkt Leonard Chamriho akipeana mikono kwa furaha na Mkurugenzi wa Kampuni ya Bombadier Commercial Aircraft Bw. Pardeep Sandhu mara baada ya Moja ya Ndege mpya mbili zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya kampuni ya ndege Tanzania (ATCL) kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius leo Septemba 20, 2016, Wengine ni marubani wa ndege hiyo.PICHA NA IKULU


Katibu Mkuu wa Uchukuzi Dkt Leonard Chamriho na Mkurugenzi wa Kampuni ya Bombadier Commercial Aircraft Bw. Pardeep Sandhu, na maofisa wengine wakisubiri kuwasili kwa Moja ya Ndege mpya mbili zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya kampuni ya ndege Tanzania (ATCL) ikiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius leo Septemba 20, 2016
Moja ya Ndege mpya mbili zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya kampuni ya ndege Tanzania (ATCL) ikiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere saa sita na robo juu alama leo Septemba 20, 2016.

Rais Magufuli atuma salamu za rambirambi vifo vya watu 13 ajali ya Super Shem Mwan

$
0
0



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Bw. John Mongella kufuatia vifo vya watu 13 vilivyosababishwa na ajali ya barabarani iliyotokana na basi la abiria la Kampuni ya Super Shem kuligonga basi dogo la abiria (Daladala) katika kijiji cha Mwamaya kilichopo katika Kata ya Hungumalwa, Wilaya ya Kwimba Mkoani Mwanza.

Ajali hiyo imetokea leo tarehe 21 Septemba, 2016 Majira ya saa 12:15 Asubuhi baada ya basi hilo dogo lililokuwa likitoka Kijiji cha Shirima kwenda Nyegezi Mjini Mwanza kuingia ghafla barabara kuu na kisha kugongwa na basi la Kampuni ya Super Shem lililokuwa likitoka Mkoani Mbeya kwenda Mwanza.

Katika ajali hiyo watu wote 13 waliopoteza maisha na majeruhi 15 waliolazwa hospitali walikuwa abiria wa basi dogo lililogongwa.Rais Magufuli ameelezea kupokea taarifa za ajali hiyo kwa mshituko mkubwa hasa ikizingatiwa kuwa imetokea ikiwa ni siku moja tu tangu Watanzania wengine 12 wapoteze maisha katika ajali ya basi la Kampuni ya New Force iliyotokea katika kijiji cha Lilombwi, Kata ya Kifanya, Tarafa ya Igominyi Mkoani Njombe.

"Nimesikitishwa sana na vifo vingine vya watanzania wenzetu waliopoteza maisha katika ajali huko Mwanza, nakuomba Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Bw. John Mongella unifikishie salamu za pole kwa familia zote zilizopoteza ndugu, jamaa na marafiki katika ajali hii.

"Nawaombea wote waliotangulia mbele za haki wapumzishwe mahali pema na pia wote walioguswa na msiba wawe na moyo wa subira, uvumilivu na ustahimilivu katika kipindi kigumu cha majonzi ya kuondokewa na jamaa zao"Amesisitiza Rais Magufuli.

Rais Magufuli pia amewaombea majeruhi wote wa ajali hii wapone haraka  ili waungane na familia zao na kuendelea na shughuli za ujenzi wa Taifa.

Gerson Msigwa.
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
21 Septemba, 2016

Wanafunzi wa Ihungo na Nyakato wapewa uhakika wa kuendelea na masomo.

$
0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Mhe. George Simbachawene akiongea na waandishi wa habari (Hawapo pichani) ambapo alisema serikali imewahamisha kwa muda wanafunzi wa shule za Sekondari Nyakato na Ihungo zilizoathiriwa na tetemeko ili kupisha ujenzi upya wa miundombinu katika shule hizo
Baadhi ya Viongozi wa Serikali na Waandishi wa Habari wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Mhe. George Simbachawene wakati akieleza mikakati ya serikali katika kukarabati miundombinu katika shule zilizoharibiwa na tetemeko lililotokea mkoani Kagera. PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO


Na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Bukoba.

Serikali imewahamisha kwa muda wanafunzi wa shule za sekondari Ihungo na Nyakato za mkoani Kagera zilizoharibiwa na tetemeko la ardhi ili kupisha ujenzi upya wa miundombinu ya msingi ya shule hizo.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) George Simbachawene alipokuwa akiongea na waandishi wa habari leo Bukoba mkoani Kagera.

“Shule hizi mbili za Ihungo na Nyakato zimeharibika sana, majengo yote yameharibika hayafai tena kutumika, zinahitaji kujengwa upya na shughuli za ujenzi zimeanza, kazi hiyo inafaywa na vikosi vya JWTZ, Magereza na VETA wameanza kazi katika shule hizo mbili” alisema Simbachawene.

Waziri Simbaachawene ametaja hatua ambazo Serikali imechukuwa hadi sasa kuwa ni pamoja na kusitisha masomo katika shule hizo mbili, kuwahamisha kwa muda wanafunzi wote 1332 kwenda katika shule 7 tofauti na kuzijenga upya shule hizo ambapo hatua za awali za ujenzi tayari zimeshaanza.

Waziri Simbachawene amewataja wanafunzi wa shule hizo ambao wanahamishiwa shule nyingine kuwa ni wa kidato cha tano na cha sita.

Kutokana na athari za tetemeko hilo jumla ya shule 353 majengo yake yameathirika kwa viwango tofauti ambapo kati ya shule hizo, 110 ni za sekondari na 243 ni za msingi.

Ili kuhakikisha wanafunzi hao wanapata elimu kulingana na ratiba za shule na miataala ya vidato vyao, jumla ya idadi ya wanafunzi 748 kutoka shule ya sekondari Ihungo, kati yao wanafunzi 372 ni wa kidato cha sita na 376 ni wa kidato cha tano.

Waziri Simbachawene ameongeza kuwa kati ya wanafunzi hao wa Ihungo 649 ni wa Tahasusi za masomo ya sayansi na 99 masomo ya sanaa ambapo walimu wanaofundisha shule hiyo idadi yao ni 31.

Kwa upande wa shule ya Sekondari Nyakato, Waziri Simbachawene amesema kuwa wapo jumla ya wanafunzi 567 wakiwemo wanafunzi wa 388 wa masomo ya sayansi na 179 masomo ya sanaa ambapo idadi hiyo inajumuisha wanafunzi 227 wa kidato cha sita na 340 wa kidato cha tano na kuna jumla ya walimu 32.

Ili kutoathiri mwenendo na hatua za wanafunzi kujifunza, Waziri Simbachawene amesema kuwa Serikali kupitia Ofisi ya Rais TAMISEMI imewasambaza wanafunzi hao kwenda shule za sekondari Kahororo na Omumwini zote za Manispaa ya Bukoba, Biharamulo na Nyakahura kutoka halmashauri ya Biharamulo, Kishoju na Nyailigamba halmashauri ya Muleba na Chuo cha Ualimu cha KKKT Bukoba.

Kufuatia hatua hiyo ya kuwahamisha wanafunzi hao, Waziri Simbachawene amesema kuwa wanapaswa kuripoti katika shule hizo Oktoba 1, 2016 badala ya Septemba 26 ya awali ili kuruhusu madogomadogo ya miundombinu katika shule hizo.

Wanafunzi hao watasoma katika shule hizo hadi mwezi Desemba 2016 hatua ambayo inatarajiwa ujenzi wa miundombinu ya msingi itakuwa imekamilika na kuruhusu wanafunzi kurejea kwenye shule zao Januari 2017 ambapo shule zote nchini zitafunguliwa kwa pamoja.

Aidha, Waziri Simbachawene amewataka walimu, wanafunzi na wanajamii katika shule walizopokea wanafunzi hao, wawe faraja kwa watoto hao washirikiane nao na kuishi kindugu.

Orodha ya majina ya wanafunzi waliohamishwa shule watatolewa kwa njia ya vyombo vya habari pamoja na kuwekwa kwenye tovuvi ya Ofisi ya Rais TAMISEMI www.tamisemi.go.tz na wanapaswa kuendelea kutumia sare zao za awali.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Usimamizi wa Elimu Ofisi ya Rais TAMISEMI Juma Kaponda amesema kuwa walimu wa shule za Ihungo na Nyakato wataambatana na wanafunzi wao walipopangiwa.

RC Kagera aipokea Kilimanjaro Queens, Awapongeza kwa ushindi

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Generali Mstaafu Salim Kijuu akipokea kikombe cha ubingwa wa CECAFA kwa wanawake kutoka kwa Nahodha wa Kilimanjaro Queens Sophia Mwasikili.
rck5
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Generali Mstaafu Salim Kijuu(kushoto) akiinua juu kikombe cha ubingwa wa CECAFA kwa wanawake alichokipokea kutoka kwa Nahodha wa Kilimanjaro Queens Sophia Mwasikili(kulia).
rck6
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Generali Mstaafu Salim Kijuu(kushoto) akipokea Bendera ya Taifa kutoka kwa katibu wa Chama cha Mpira mkoani Kagera Bw. Salum Chama mara baada ya Mabingwa wa CECAFA kwa wanawake Kilimanjaro Queens kuwasili kutoka Nchini Uganda katikati ni Mwenyekiti wa Soka la wanawake Amina Karuma.
rck2
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Generali Mstaafu Salim Kijuu akisalimiana na baadhi ya wachezaji wa Kilimanjaro mara baada ya kuwasilini Mkoani Kagera wakitokea nchini Uganda kushiriki mashindano ya CECAFA kwa wanawake ambapo wameibuka mabingwa kwa mwaka 2016.
rck3
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Generali Mstaafu Salim Kijuu akisalimiana na baadhi ya wachezaji wa Kilimanjaro mara baada ya kuwasilini Mkoani Kagera wakitokea nchini Uganda kushiriki mashindano ya CECAFA kwa wanawake ambapo wameibuka mabingwa kwa mwaka 2016.
rck1
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Generali Mstaafu Salim Kijuu akisalimiana na baadhi ya wachezaji wa Kilimanjaro mara baada ya kuwasilini Mkoani Kagera wakitokea nchini Uganda kushiriki mashindano ya CECAFA kwa wanawake ambapo wameibuka mabingwa kwa mwaka 2016.c

(Picha na Idara ya Habari Maelezo)

Waziri Jenista amuagiza Mkuu wa Wilaya ya Misenyi kufanya ukarabati wa haraka

$
0
0
Na Beatrice Lyimo-MAELEZO

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Misenyi Mkoani Kagera kufanya ukarabati wa haraka wa kuziba nyufa zilizotokea katika taasisi za Serikali zilizoathirika kutokana na tetemeko la ardhi lilitokea hivi karibuni Mkoani humo.

Waziri Mhagama aliyasema hayo leo wakati wa ziara yake ya kukagua taasisi mbalimbali za Serikali zilizoathirika kutokana na maafa ya tetemeko la ardhi lililotokea mkoani humo tarehe 10 Septemba mwaka huu.

Katika ziara hiyo, Waziri Mhagama alimtaka Mkuu wa Wilaya hiyo kutoa misaada kwa waathirika waliofanyiwa tathmini ili kuwawezesha kupata huduma muhimu za kijamii.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya hiyo, Luteni Kanali Denice Filangali Mwila alisema kuwa Ofisi yake imeshaanza kuwaga baadhi ya maturubai na chakula ikiwemo sukari kwa waathirika wa tetemeko hilo.

Aidha Waziri Mhagama pia alitembelea Shule ya Msingi Byeju iliyopo Wilayani humo ili kujionea baadhi ya vyoo na madarasa ya shule ambayo yalivyoathirika na tetemeko hilo na kuagiza ukarabati wa miundombinu hiyo kuanza mara moja.

CHANGIA MECHI YA HISANI

WAZIRI SIMBACHAWENE AZUNGUMZIA HATUA ZILIZOCHUKULIWA NA SERIKALI KWA WANAFUNZI WA IHUNGO NA NYAKATO

WAKALA ya Mkemia Mkuu wa Serikali kuendesha kampeni maalum ya kupima matumizi ya vilevi

$
0
0
Na Beatrice Lyimo-MAELEZO
Dar es Salaam

WAKALA ya Mkemia Mkuu wa Serikali imekusudia kuendesha kampeni maalum ya kupima matumizi ya vilevi kwa madereva wanaosafirisha abiria na mizigo ikiwa ni hatua ya kukabiliana na tatizo la ajali za barabarani nchini.

Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Mkemia Mkuu wa Serikali Prof. Samwel Manyele alipokuwa akifungua mafunzo ya siku mbili kwa wadau wa kemikali juu ya matumizi salama ya kemikali nchini.

Prof. Manyele alisema utaratibu wa kuwapima madereva hao utaanza hivi karibuni na utawezesha kupunguza tatizo la ajali barabarani na kuvitaka vyombo vya ulinzi na usalama kutoa ushirikiano katika zoezi hilo.

“Madereva wote wanaosafirisha mizigo na abiria  watatakiwa kupita kwenye kipimo ambacho kitaonyesha kama madereva hao wanatumia vilevi, hali hiyo itasaidia kutatua tatizo la ajali za barabarani nchini”, amesema Prof. Manyele.

Aidha, Prof Manyele alisema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kutoa uwezo na uelewa kwa wahusika  hasa wasimamizi wa shughuli za kemikali na matumizi salama juu ya kukabiliana na matukio au ajali za kemikali pale yanapotokea.

Aliongeza kuwa mafunzo hayo yamekuja kufuatia uelewa mdogo wa elimu kwa baadhi ya wadau wanaojishughulisha na masuala ya kemikali kuhusu uzalishaji, uhifadhi, usimamizi na usafirishaji wa matumizi ya kemikali nchini.

Mbali na hayo, Prof Manyele alisema kumekuwa na ajali na matukio yanayotokana na kemikali ikiwemo ya ajali halisi na mengine kutokana na kukosa uelewa wa matumizi sahihi na salama ya kemikali.

Akifafanua zaidi Prof. Manyele alisema katika kukabiliana na madhara yatokanayo na matumizi yasiyo salama ya kemikali, Serikali ilitunga sheria ya Kemikali za Viwandani na majumbani mwaka 2003 kwa lengo la kuhakikisha kemikali hizo zinatumika katika hali iliyo salama.

MAJALIWA AZINDUA MPANGO MKAKATI NA MRADI WA MABORESHO YA HUDUMA ZA MAHAKAMA YA TANZANIA.

$
0
0
 Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarest Ndikilo akizungumza  katika   uzinduzi  Mpango Mkakati na Mradi  wa Maboresho ya Huduma za Mahakama ya Tanzania ulifanywa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa mjini Kibaha Septemba 21, 2016.
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji  akizungumza katika   uzinduzi  Mpango Mkakati na Mradi  wa Maboresho ya Huduma za Mahakama ya Tanzania ulifanywa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa mjini Kibaha Septemba 21, 2016.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi  Evarest Ndikilo baada ya kuwasili kwenye eneo inapojenjwa Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Pwani na Mahakama ya Wilaya ya Kibaha kuzindua Mpango Mkakati na Mradi  wa Maboresho ya Huduma za Mahakama ya Tanzania Septemba 21, 2016. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman  baada ya kuwasili kwenye eneo inapojenjwa Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Pwani na Mahakama ya Wilaya ya Kibaha kuzindua Mpango Mkakati na Mradi  wa Maboresho ya Huduma za Mahakama ya Tanzania Septemba 21, 2016.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Naibu Spika wa Bunge  Dkt, Tulia Ackson baada ya kuwasili kwenye eneo inapojenjwa Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Pwani na Mahakama ya Wilaya ya Kibaha kuzindua Mpango Mkakati na Mradi  wa Maboresho ya Huduma za Mahakama ya Tanzania Septemba 21, 2016. 


 Mkurugenzi wa Benki ya Dunia katika nchi za Tanzania, Burundi, Malawi na Somalia, Bella Bird  akizungumza katika   uzinduzi  Mpango Mkakati na Mradi  wa Maboresho ya Huduma za Mahakama ya Tanzania ulifanywa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa mjini Kibaha Septemba 21, 2016. 
 Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman akizungumza katika uzinduzi  katika   uzinduzi  Mpango Mkakati na Mradi  wa Maboresho ya Huduma za Mahakama ya Tanzania ulifanywa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa mjini Kibaha Septemba 21, 2016. 

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisaidiwa na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othaman kukata utepe wakati alipozindua  Mpango Mkakati na Mradi wa Maboresho ya Huduma za Mahakama ya Tanzania  mjini Kibaha, Septemba 21, 2016.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akionyesha   Mpango Mkakati na Mradi wa Maboresho ya Huduma za Mahakama ya Tanzania  baada ya kuuzindua mjini Kibaha, Septemba 21, 2016. Wengine pichani kutoka kushoto ni Dkt. Hassison Mwakyembe, Waziri wa Katiba na Sheria, Jaji Mkuu, Mohamed Othman Chande na Naibu Spika wa Bunge, Dkt Ackson Tulia.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimkabidhi Mkurugenzi wa Benki ya Dunia wa Nchi za Tanzania, Burundi, Malawi na Somalia, Bella Bird kitabu cha Mradi wa Maboresho  ya Huduma za Mahakama ya Tanzania  baada ya kuuzindua mjini Kibaha Septemba 21, 2016. Kushoto ni Jaji Mkuu wa Tanzania Mohamed Chande Othman  na kulia ni Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipozindua  Mpango Mkakati na Mradi  wa Maboresho ya Huduma za Mahakama ya Tanzania ulifanywa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa mjini Kibaha Septemba 21, 2016. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka jiwe la Msingi la jengo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Pwani na Mahakama ya Wilaya ya Kibaha  Sptemba 21, 2016.
 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya  pamoja na viongozi mbalimbali waliohudhuria katika uzinduzi wa  Mpango Mkakati na Mradi  wa Maboresho ya Huduma za Mahakama ya Tanzania ulifanywa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa mjini Kibaha Septemba 21, 2016.
 Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa akiondoka baada ya kuweka jiwe la msingi la jengo la Hakimu Mkazi Mahakama ya Pwani na Mahakama ya wilaya ya Kibaha Septemba 21, 2016. Kushoto kwake ni Jaji Mkuu wa Tanzania Mohamed Chande Othman na kulia kwake ni Mkurugenzi wa Benki ya Dunia wa nchi za Tanzania, Burundi, Malawi na Somalia, Bella Bird. 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mkurugenzi wa Benki ya Dunia wa nchi za Tanzania, Burundi, Malawi na Somalia, Bella Bird (kulia kwake) na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman (kulia) baada ya kuweka jiwe la msingi la jengo la Hakimu Mkazi Mahakama ya Pwani na Mahakama ya wilaya ya Kibaha Septemba 21,2016. Wapili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarest Ndikilo.
 (Picha na Ofisi ya  Waziri Mkuu)

KATIBU MKUU WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI ZANZIBAR AFUNGUA SKULI YA MSINGI YA ABDALLAH SHARIA

$
0
0
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mfunzo ya Amali Zanzibar Bi. Khadija Bakari Juma akifungua pazia kwa niaba ya Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali kuashiria ufunguzi wa Skuli ya Abdallah Sharia iliyopo Tomondo Mjini Zanzibar.
Muonekano wa Skuli ya Msingi ya Abdallah Sharia iliyopo Tomondo.
Mkurugenzi Idara ya Elimu Maandalizi na Msingi Bi. Safia Ali Rijali akimkaribisha Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mfunzo ya Amali Zanzibar Bi. Khadija Bakari Juma (hayupo pichani) aliemuakilisha Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali katika sherehe ya ufunguzi wa Skuli ya Abdallah Sharia iliyopo Tomondo Mjini Zanzibar.
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mfunzo ya Amali Zanzibar Bi. Khadija Bakari Juma akizungumza na wananchi na wanafunzi waliofika katika sherehe ya ufunguzi wa Skuli ya Abdallah Sharia iliyopo Tomondo Mjini Zanzibar.
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mfunzo ya Amali Zanzibar Bi. Khadija Bakari Juma akizungumza na wananchi na wanafunzi waliofika katika sherehe ya ufunguzi wa Skuli ya Abdallah Sharia iliyopo Tomondo Mjini Zanzibar.
Baadhi ya walimu na walikwa waliofika katika sherehe ya ufunguzi wa Skuli ya Abdallah Sharia wakimsikiliza Mgeni rasmin (hayupo pichani) Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mfunzo ya Amali Bi. Khadija Bakari Juma.Picha na Makame Mshenga / Maelezo Zanzibar.

TPDC ZATOA MILIONI 30 KUSAIDIA WAATHIRIKA TETEMEKO KAGERA.

$
0
0
Na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Bukoba.
WAFANYAKAZI na Uongozi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) wametoa msaada wa Sh. milioni 20 kusaidia kununua vifaa vya ujenzi kwa waathirika wa tetemekola ardhi mkoani Kagera.

Akikabidhi msaada huo kwa Mkuu wa Mkoa wa huo Meja Jenerali Mstaafu Salim Kijuu, Mwenyekiti wa Bodi ya TPDC Balozi Dkt. Ben Moses amefafanua kuwa msaada huo unalenga kuwasaidia kununua mabati na saruji kwa waathirika wa tetemeko hilo lililoukumba mkoa huo.

“Sisi TPDC tunatoa msaada wetu kama sehemu ya Watanzania na tatizo hili ni letu sote na Watanzania ni wamoja” alisema Dkt. Moses.

Kwa upande wake Meja Jenerali Mstaafu Kijuu amewashukuru TPDC kwa mchango wao na kubainisha kuwa hakuna kitu kidogo katika kutoa na kuwahakikishia wadau wote wanaotoa michango yao kuwa misaada hyote inayotolewa itatumika kwa malengo yaliyokusudiwa na itasaidia kuwarudishia makazi waathirika wa tetemeko hilo.

Aidha, Mkuu huyo wa mkoa amewataka watu wote wenye mapenzi mema kuendelee kuwachangia waathirika wa tetemeko hilo na waige mifano ya watu na taasisi mbalimbali wanaoendelea kutoa misaada kwa mkoa wa Kagera ili kuwarudishia makazi wananchi walioathirika maafa hayo.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa TPDC Kapuulya Musomba  amesema kuwa huo sio mwisho wao katika kuchangia waathirika wa tetemeko la ardhi, bali wanaendelea kuwahamasisha wadau wa mafuta na gesi yakiwemo makampuni ya ndani na nje ya nchi ili kuwafanya wananchi waweze kuendelea na kazi zao za kila siku kwa maendeleo yao na taifa kwa ujumla.
 Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salim Kijuu akipokea msaada uliotolewa na Bodi ya TPDC (kushoto). Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya TPDC Balozi Dkt. Ben Moses msaada ambao unalenga kuwasaidia kurekebisha makazi ya waathirika wa tetemeko hilo lililoukumba mkoa huo.
Picha na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Bukoba.
 Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salim Kijuu (kulia) akimshukuru Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) Kamugisha Kazaura (kushoto) mara baada ya kupokea msaada wa mifuko 600 ya saruji ambayo ni sawa na tani 30 yenye thamani ya Sh. milioni 10.

FILAMU MPYA YA "KARABATI ROBO" KUZINDULIWA SEPTEMBA 23 KATIKA KITUO CHA SIBUKA

$
0
0
Steps Intertainment inazindua kwa mara ya kwanza inazindua filam ya karabati  robo katika kituo cha TV cha SIBUKA katika channel 111 na kwenye king’amuzi cha Startimes Septemba 23 mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Msanii maarufu wa Filamu nchini, Jacob Steven a.k.a JB amesema kuwa filamu hiyo ina ubora wa viwango vya filamu.

Amesema kuwa wadau waipokee kazi hiyo wataburudika kutokana na umahiri uliotumika katika kuandaa filamu hiyo.
Aidha amesema kuwa wasanii waliohusika wana majina ambao wamefanya filamu hiyo kuwa bora wake kuanzia kwa jina karabati robo. Jb amewataka  mashabiki wake kuendelea kupokea kazi zake ikiwemo hiyo na kazi zingine .

Msaani maarufu  wa Filamu, Jacob Steven  a.k.a JB akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaa juu ya uzninduzi wa filamu yake ya karabati robo iliofanyika jijini Dar es salaam leo, Kushoto ni Mratibu wa Kitengo kungalia kazi za wasanii wa Startimes, Paulina Kimweli na kulia ni Meneja wa Steps Intertainment, Myovela Mfwaisa Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii

Waziri Nape aipongeza Kilimanjaro Queens mabingwa kombe la CECAFA

$
0
0
Na: Genofeva Matemu – WHUSM

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye amewapongeza Wachezaji wa Kilimanjaro Queens kwa niaba ya serikali na kwa niaba ya watanzania kwa kazi nzuri waliyoifanya mpaka kuwa mabingwa wa kwanza wa Kombe la CECAFA kwa mpira wa miguu kwa wanawake Afrika Mashariki na Kati.Pongezi hizo zimetolewa na Waziri Nnauye alipokua akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam.

“Kama serikali ni vyema kuipongeza timu yetu ya Kilimanjaro Queens kwa kuiwakilisha vizuri Tanzania katika michuano CECAFA na kuibuka mabingwa kwa kuweza kuruka vizingiti vyote vilivyokuwepo katika muchuano hiyo” alisema Mhe. Nnauye

Serikali itaendelea kuweka nguvu ya kutosha na kuungana na timu zetu kuwasaidia kuhakikisha wanafanya vizuri zaidi katika michezo mbalimbali, amesema Mhe. Nnauye.Mhe. Nnauye amesema kuwa Tanzania inaanza kuona matunda ya uwekezaji wa muda mrefu kwani haikuwa kazi raisi kwa Kilimanjaro Queens kufikia fainali na kuwa mabingwa kwa kupambana na timu ngumu na kuweza kushinda.

Aidha Mhe. Nnauye amewahaidi wachezaji wa Kirimanjaro Queens kuwaalika bungeni katika Bunge lijalo kwa ajili ya kuwapongeza na kuwaandalia mechi ya kirafiki kutambua mchango wao wa kuipeperusha bendera ya Tanzania kati yao na wabunge wanawake. Timu zilizoshiriki katika michuano ya kombe la chalenji la CECAFA ni pamoja na Tanzania, Burundi, Zanzibar, Kenya, Ethiopia, Rwanda pamoja na mwenyeji Uganda. Mashindano ya Kombe la Chalenji la CECAFA kwa timu za wanawake yamefanyika kwa mara ya kwanza jambo linaloleta tafsiri kuwa michuano hiyo inaweza kuinua soka la wanawake kwa ukanda wa nchi za Afrika Mashariki na Kati

KAMATI YA ULINZI NA USALAMA MKOA WA RUVUMA YA WATEMBELEA MAJERUHI WA AJALI YA BASI LA NEW FORCE WALIOLAZWA HOSPITAL YA RUFAA YA MKOA WA RUVUMA

$
0
0
Kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa ruvuma ikiongozwa na mkuu wa mkoa wa ruvuma Dokta Binilith Mahenge amewatembelea majeruhi wa ajali ya basi la New Force waliolazwa katika Hospital ya rufaa ya mkoa wa Ruvuma wakipatiwa matibabu.

MSANII WA KIZAZI KIPYA NCHINI KALLAH JEREMIAH APOKEA CHETI KUTOKA SOCIETY WATCH,

$
0
0

Mkurugenzi Mkuu wa Society Watch, Simon Mnkondya akimkabidhi Kallah Jeremiah cheti cha utambuzi wa kazi ya msanii Kallah Jeremiah kwa kushirikisha watoto katika wimbo wana ndoto, leojijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu wa Society Watch,Issabela Liso


Mkurugenzi Mkuu wa Society Watch, Simon Mnkondya akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa kukabidhi cheti cha utambuzi wa kazi ya msanii Kallah Jeremiah kushirikisha watoto katika wimbo wana ndoto, leojijini Dar es Salaam.kushoto ni Msanii wa kizazi kipya nchini Kallah Jeremiah .

Msanii wa kizazi kipya nchini Kallah Jeremiah akizungumza na waandishi wa habari juu ya kuushukuru uongozi wa Society Watch kwa kumpa cheti kwa kukubali kazi anayoifanya katika jamii.kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Society Watch, Simon Mnkondya
KATIKA kuhakikisha watoto yatima hawaachwi nyuma katika suala zima la elimu nchini ,Taasisi ya Society Watch imeanzisha kampeni maalum kundi hilo kutokana na watotot yatima kuwa changamoto mbalimbali zinazofanya ndoto zao zishindwe kutimia.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam,Mkurugenzi Mkuu wa Society Watch, Simon Mnkondya wakati wa kukabidhi cheti utambuzi wa kazi ya msanii Kallah Jeremiah kushirikisha watoto katika wimbo wana ndoto, amesema kuwa watoto yatima wanakabiliwa na changamoto mbalimbali hivyo kunahitaji jitihada za kuweza kusaidia watoto yatima.

Mkondya amesema kuwa mpango wa utaoji wa elimu kwa serikali kwa kundi hilo inawezekana kutokana na uchache. Amesema kuwa watoto yatima wamepata hamasa kwa wimbo wa Mwanamziki wakikizazi kipya Kala jeremiah ''wanandoto'' ambapo taasisi hiyo imeliona kundi hilo linalo umuhimu wakipekee yakutoachwa nyuma katika suala la kupata elimu .

''Hamasa ya taasisi yetu Society Watch nikuwasaidia watoto yatima walipo vijijini katika kupata elimu hasa kwa watoto wanaishi katikamazingira magumu katikamaeneo yavijijini ,hamasa hii imetokana na wimbo wa wanandoto wakala jeremamiah kwani watoto hawa wanao mchango mkubwa katika kulitumikia taifa ''Alisema Mkurugenzi Simon Mkondya.

Amesema kuwa kutokana na msanii huyo wakizazi kipya Kala jeremiah kuona umuhimu watoto yatima kupewa fusra yakupata elimu kama watoto wengine kupitia wimbo wanandoto unalenga kuihamasisha jamii kulisaidia kundi hilo maalum katika kupata elimu .

Mkondya amesema serikali inaowajibu wakipekee katika kuwasaidia watoto yatima kuwawezesha kundi hilo kuweza kupata elimu kwani kutokana naumuhimu wawatoto hao katika kujenga taifa nakuliletea taifa maendeleo katika hazina yaviongozi wakesho ,hivyo serikali najamii inawajibu wakulisaidia kundi hilo katika kuwapatiaelimu.

Nae Msanii wa kizazi kipya nchini Kallah Jeremiah amesema kuwa yeye pamoja nawanamziki wa kizazikipya wameimba wimbo huo''wanandoto'' kuikumbusha serikali kuwaasaidia watoto yatima walipo katika mazingira magumu kuwa wanao umuhimu wakipekee katika kupata elimu . Amesema kuwa ni mara kwanza kwa watu kumpa cheti kwa kukubali kazi anayoifanya katika jamii.

TAMKO KUHUSU UTUPAJI TAKA OVYO USIO WA KITAALAMU MAHOSPITALI.

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mh. January Makamba akiongea na Vyombo vya Habari juu ya hatua za Serikali za kuzuia utupaji ovyo wa taka hatarishi za Hospitalini na  kupiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki ifikapo Januari mosi 2017. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Mazingira Bw. Richard Muyungi.
­­­­


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA MAKAMU WA RAIS
tz
TANGAZO KWA UMMA

UZUIAJI WA UTUPAJI OVYO   USIO WA KITAALAMU WA TAKA ZA MAHOSPITALI. 

Sheria ya usimamizi  wa Mazingira ya mwaka 2004  inapiga marufuku uchafuzi wa mazingira ikiwa ni pamoja na unaotokana na taka za mahospitali.  Aidha Kanuni za Taka Hatarishi za mwaka 2009, zinasisitiza utenganishi wa taka mbali mbali  zitokazo kwenye mahispotitali kwa kuzitibu katika namna ambayo haitaleta athari katika mazingira na afya ya binadamu. Pia Kanuni zinahimiza matumizi ya teknologia sahihi kama vile matumizi ya incinerators ambazo huchoma taka za mahospitali na  kuziteketeza kabisa.

Ofisi yangu imefuatilia na kugundua kuwa taka nyingi za mahopitali, taka kutoka katika maduka ya  madawa zilizoisha muda wake zinatupwa ovyo  au kuharibiwa kwa utaratibu usio kubalika kitalaamu. Tumefuatalia na kukuta malundo ya madawa chakavu na vifaa vya hospitali vilivyotumika   katika maeneo ya visiwa vya Bongoyo na Mbudya. Aidha madawa chakavu yanatumpwa holela katika dampo la Pungu Kinyamwezi.  Hii ni hatari sana kwa mazingira na kwa afya ya binadamu.

Kuanzia sasa ni marufuku  kutupa taka hizi katika utaratibu usio wa kawaida. Kila hospitali na zahanati  au kituo cha afya kihahakikishe kinatumia incinerators  au utaratibu mwingine ulio sahihi kwa mujibu wa sheria ya mazingira na kanuni zake. Aidha ninaiagiza NEMC kuanzia sasa wafanye msako mkali kubaini mahospitali na watu wanaokiuka agizo hili. Nimewapa mwezi mmoja na   kwa  wale wanaofanya hivyo waache mara moja.   Kwa msako huu atakayebainika kukiuka hatua kali za kisheria zinachukuliwa dhidi yake.Nichukue fursa hii kutoa tena pole kwa wezentu wa Mkoa wa Kagera na maeneo ya jirani kwa athari za tetemeko la ardhi.

Baada ya tatetemeko kuna athari kubwa za kimazingira  ambazo zimejitokeza. Hivyo mimi binafsi ninafuatilia suala hili kwa ukaribu na kuhakikisha  athari ambazo zimejotokeza na zinazoendelea kujitokeza zinashughulikiwa kwa haraka.  Nimeagiza Ofisi yangu pamoja na NEMC washirikiane kwa ukaribu sana na watendaji wa Mkoa na Kamati mbalimbali zilizoundwa kushughulikia maafa haya na kufanya  tathmini  ya athari za mazingira zilizojitokeza na kuelekeza hatua za haraka kuchukuliwa ilikupunguza madhara kwa mazingira na binadamu.

Pia, napenda kutumia fursa hii  kuukumbusha umma  juu ya dhamira ya Serikali ya kupiga marufuku matumizi ya mifuko na vifungashio vya ya plastiki ifikapo Januari Mosi 2017.Adhma ya Serikali ya kupiga marufuku matumizi ya mifuko  na vifungashio vya plastiki ni kuepusha athari za kiafya na mazingira zinazoendelea kujitokeza kutokana na matumizi ya mifuko hiyo. Hivyo basi wazalishaji, waagizaji, wasambazaji, wauzaji  na watumiaji  wa mifuko hiyo wanakumbushwa kuendelea na zoezi la kuondosha pamoja na kusitisha uzalishaji wa mifuko hii.

IMETOLEWA NA
JANUARY  Y. MAKAMBA (MB.)
WAZIRI WA NCHI OFISI YAMAKAMU WA RAIS
MUUNGANO NA MAZINGIRA
21/9/2016
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live




Latest Images