Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live

Waziri Nape Nnauye akutana na waandishi wa Habari za Michezo Jijini Dar es Salaam.

$
0
0
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na waandishi wa habari za Michezo Jijini Dar es Salaam alipokutana nao leo Jijini Dar es Salaam wakati wa semina maalum iliyoandaliwa na Kampuni ya Selcom kujadili kuhusu matumizi ya mfumo wa mashine za tiketi za kieletroniki katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

Rais wa Chama cha waandishi wa habari wa michezo Tanzania (TASWA) Bw. Juma Pinto akizungumza katika semina maalum iliyoandaliwa na kampuni ya Selcom kwa ajili ya kujua matumizi ya mfumo wa mashine za kieletroniki katika Uwanja wa Taifa Jijini dar es Salaam .
Meneja wa Miradi kutoka kampuni ya Selcom Bw. Galus Runyet akitoa maelezo kwa waandishi wa habari za Michezo kuhusu matumizi ya mfumo wa mashine za tiketi za kieletroniki katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Meneja wa Miradi kutoka kampuni ya Selcome Bw. Galus Runyet akitoa maelezo kwa waandishi wa habari za Michezo kuhusu jinsi ya kutumia kadi ya mfumo wa mashine za tiketi za kieletroniki katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya waandishi wa habari za Michezo wakimsililiza Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye wakati wa semina maalum iliyoandaliwa na Kampuni ya Selcom kujadili kuhusu matumizi ya mfumo wa mashine za tiketi za kieletroniki katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam. Picha Zote na Raymond Mushumbusi WHUMS

MKUU WA MKOA WA ARUSHA AMPA WIKI MBILI MKURUGENZI WA JIJI KUHAKIKISHA WALIMU WOTE WANAODAI SEREKALI WALIOPO NDANI YA JIJI LA ARUSHA WANALIPWA FEDHA ZAO

$
0
0

MKUU wa mkoa Arusha Mrisho Gambo akiongea na walimu wote wa shule za msingi 48 zilizopo ndani ya Halmashauri ya jiji la Arusha ,waratibu elimu,wakaguzi elimu pamoja na maafisa elimu kata .
Mkuu wa wilaya ya Arusha Mhe. Gabriel Daqarro akiwa anaongea na walimu waliohuthuria mkutano huo.

Habari picha na Woinde Shizza,Arusha

MKUU wa mkoa Arusha Mrisho Gambo amemuagiza mkurugenzi wa jiji la
Arusha, Athumani Kihamia kulipa madeni yote wanayodai walimu ya
milioni 154 ndani ya wiki mbili ambayo wamekuwa wakidai serikali
kuu kwa muda mrefu bila kulipwa na hivyo kusababisha walimu hao
kukata tamaa ya ufundishaji wanafunzi .

Gambo alitioa agizo hilo jana alipokuwa akizungumza na walimu wote wa
shule za msingi 48 zilizopo ndani ya Halmashauri ya jiji la Arusha ,waratibu elimu,wakaguzi elimu pamoja na maafisa elimu kata katika mkutano wa kujua changamoto zinazowakabili walimu hao ili zipatiwe ufumbuzi.

Alisema kuwa walimu wamekuwa wakifundisha katika mazingira magumu na kwamba hadi sasa wapo walimu wa shule za msingi wanaoadai madeni ya likizo na mengineyo yenye gharama ya milioni 154 ambapo serikali kuu
ndio inayopaswa izilipe na hadi sasa hawajalipwa jambo ambalo
linawafanya walimu hao kupoteza muda wa kufundisha na kufuatilia kila
siku madeni hayo.

“mkurugenzi nakupa muda wa wiki mbili deni hili la milioni 154 kwa
ajili ya walimu akikisha zinalipwa haraka iwezekanavyo wakishalipwa
ndio upambane na serikali kuu ufidie hapo zilikotolewa kwani
haiwezekani walimu wapoteze muda kila siku wakifuatilia tu madeni huku
wakiwa wameacha vipindi bila kufundisha wanafunzi wetu”alisema Gambo.

Mkurugenzi wa halmashauri ya jiji hilo,Athumani Kihamia akijibu agizo
hilo alilopewa na mkuu wa mkoa alisema kuwa fedha hizo ambazo ni
madeni hayo zinapaswa zitokee serikali kuu na kwamba atahakikisha
kuwa ndani ya muda wa wiki mbili atazilipa kupitia fedha za ndani za
halamshauri hiyo ili zikija zirejeshwe.

Alifafanua kuwa deni hilo atalipa kutoka kwenye fedha alizoziokoa
ambazo zilikuwa zinalipwa kinyume cha sheria kwa madiwani ambapo
kiasi cha milioni 130 zilizokuwa zinatumika kuwalipia madiwani
mafuta ,simu pamoja na nauli zitaelekezwa kulipa walimu hao madai
yao ili waweze kujikimu na hali wanayokabiliana nayo.

‘‘Fedha ambazo zimeokolewa kwa ajili ya mafuta ni milioni 40.8,fedha
za simu za madiwani milioni 61.2,nauli iliyookolewa milioni 28 ambapo
jumla ni milioni 130 ambazo zimelipwa kinyume hivyo fedha hizi
zinaelekezwa kwa walimu wa msingi na sekondari ikiwa ni madeni
wanayodai halmashuri hii ambapo fedha zinasubiriwa serikali kuu lkni
tumeona tuwatangulizie hizi fedha ili wajikimu na waweze kufundisha
watoto wetu vizuri”alisema Kihamia .

Kihamia alisema kuwa watatanguliza fedha hizo kwa walimu hao wakati
wakiwa wanasubiria fedha toka serikali kuu ili waendelee kujikimu
kwani zimeokolewa katika mianya ambayo zilikuwa zinateketea hivyo
zitaongeza ufanisi kwa walimu katika kufundisha wanafunzi na akili
zao na kufanya akili zao kuzielekeza kwa wanafunzi ili wapate elimu
bora.

Baadhi ya walimu hao wakieleza kero zao walisema kuwa wanakabiliwa na
tatizo la kutopandishwa madaraja kwa waliokaa kazini muda mrefu huku
wengine walioingia kazini muda mfupi wakiwa wanapandishwa madaraja
bila kujua vigezo hivvyo kumwomba mkuu wa mkoa kuingilia swala hilo.



wa kwanza kushoto ni mkurugenzi wa jiji la ArushaAthumani Kihamia akiwa anasikiliza kwa makini malalamiko ya walimu hao


picha ya juu na chini ni walimu waliouthuria mkutano huo wa mkuu wa mkoa uliofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa AICC uliopo mkoani Arusha


GEREZA LA WILAYA TUKUYU MAHIRI KWA KILIMO CHA CHAI MKOANI MBEYA

$
0
0
Wafungwa wa Gereza Tukuyu, Mkoani Mbeya  wakivuna chai katika Shamba la Gereza hilo kama inavyoonekana katika picha.
mage1
Mkuu wa Gereza Tukuyu, Mkoani Mbeya, SSP. Prosper Kinyaga akionesha  sehemu ya  eneo lenye ekari 26  linaloendesha Kilimo cha chai katika gereza hilo.
mage3
Muonekano wa baadhi ya mashamba ya Kilimo cha chai katika Gereza Tukuyu. Gereza hilo lilijengwa mwaka 1994 na shughuli zinazofanyika ni Kilimo cha chai, Kilimo cha Migomba, Bustani za mbogamboga pamoja na Utunzaji wa mazingira kwa upandaji miti na ufugaji wa samaki kwa majaribio(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

TANGA SIMENTI WAZINDUA BIDHAA MPYA YA MKOMBOZI SIMENTI.

$
0
0
 Meneja Mauzo Kitaifa wa Tanga Siment, Leslie  Massawe(Wapili kutoka Kulia) akiwa na wafanyakazi wa Tanga Simenti wakionesha mfuko wa Simenti wa Kilo 50 wakati wa uzinduzi na kuitambulisha bidhaa hiyo mpya ya Mkombozi-Simenti ya Mwendo Kasi jijini Dar es Salaam leo. 
 Meneja Mauzo Kitaifa wa Tanga Simenti, Leslie Massawe akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, wakati wa kuitambulisha bidhaa mpya ya Mkombozi-Simenti ya Mwendo Kasi jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Meneja wa mambo ya nje na mawasiliano wa Tanga Simenti, Mtanga Noor

 Baadhi ya wafanyakazi wa Tana Simenti wakiwa kwenye mkutano wa kuitambulisha Simenti mpya ya Mkombozi- simenti ya mwendokasi jijini Dar es Salaam leo.
Meneja wa mambo ya nje na mawasiliano wa Tanga Simenti, Mtanga Noor akifafanua jambo kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni  Meneja Mauzo Kitaifa wa Tanga Simenti, Leslie Massawe.

TANGA Cement Public Limited Company (TCPLC) wazalishaji wa simenti hapa nchini wamezindua bidhaa bora ya simenti inayoitwa, MKOMBOZI.
 “Bidhaa hii mpya ya Tanga Cement ni hatua nyingine ya kuwa karibu na Watanzania kwa kubuni na kuwaletea aina nyingine ya simenti, ambayo mbali na kuwa ni ya bei ya kuridhisha kwa Mtanzania wa kawaida bado inawahakikishia ubora dhabiti unaoendana na teknolojia ya kiwango cha juu katika utengenezaji wa simenti”.

Ameyasema hayo wakati wa kuitambulisha bidhaa hiyo mpya ya Mkombozi-Simenti ya Mwendo Kasi, Meneja Mauzo Kitaifa wa Tanga Simenti, Leslie jijini Dar es Salaam leo.

Amesema kuwa mahitaji ya wananchi ni makubwa kukabiliana na ongezeko la miradi ya miundombinu na wakati huo huo mahitaji ya simenti bora katika ujenzi miundombinu na nyumba za makazi katika maeneo ya mijini na hasa vijijini ambapo utaalamu katika ujenzi.

Bidhaa mpya ya simenti ya MKOMBOZI – ‘simenti ya Mwendokasi' inaletwa kwa Watanzania ili kuharakisha maendeleo ya makazi bora na shughuli nyingine za ujenzi kama jina linavyojieleza.

MKOMBOZI, simenti ya daraja la nguvu kwa kiwango cha 32.5 N, ni simenti ambayo   bei yake ni ya kuridhisha ambapo mtu yeyote anayehitaji simenti kwa ujenzi wa aina yoyote anaweza kununua. 

Mkombozi imekuja kuwapatia watanzania kile wanachohitaji katika ujenzi wa miundombinu pamoja na makazi hii ni simenti kwa matumizi yote, simenti kwa aina zote za ujenzi.

Rais Magufuli atuma salamu za rambirambi kufuatia vifo vya ajali ya New Force

KAA MKAO WA KULA

Ndege ya kwanza yatua ya ATCL yatua Dar.

$
0
0


20 Septemba, 2016.

Ndege mpya ya kwanza iliyonunuliwa na Serikali kwa ajili ya kutumiwa na Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) imetua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam ikitokea nchini Canada ilikotengenezwa.

Ndege hiyo aina ya Bombadier Q400 NextGen imetua majira ya saa 6:15 Mchana na kisha kupatiwa heshima maalum ambayo hutolewa kwa ndege yoyote mpya inayotua katika nchi yake (Water Salute).

Baada ya kupokea heshima hiyo, ndege imeegeshwa katika eneo la ndege za jeshi (Airwing Ukonga).Akizungumza baada ya kuwasili kwa ndege hiyo Katibu Mkuu Uchukuzi Dkt. Leonard Chamriho amesema ndege ya pili inatarajiwa kuwasili baada ya wiki moja na kwamba baada ya kuwasili ndege ya pili ndipo yatafanyika mapokezi rasmi, yatakayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa tarehe itakayotangazwa baadaye.

WAKADARIAJI MAJENZI NA WABUNIFU MAJENGO KUNOLEWA KESHO KUTWA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Msajili wa Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadriaji Majenzi, Jehad A. Jehad (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam, kuhusu semina ya 26 siku moja itakayo washirikisha wadau wa Sekta ya  ujenzi itakayofanyika kesho kutwa Septemba 22, 2016 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Ambwene Mwakyusa.
Viongozi wa Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadriaji Majenzi wakiwa kwenye mkutano huo. Kutoka kulia ni Mkuu wa Utawala, Angelo Ngalla, Mwanasheria, Ibrahim Mohamed na Ofisa Uhusiano, Hamisi Sungura.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.

Na Dotto Mwaibale

BODI ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadriaji Majenzi kesho kutwa inatarajia kuendesha semina ya siku moja kwa ajili ya kuwanoa wadau wa sekta ya ujenzi nchini.

Hayo yamebainishwa na Msajili wa Bodi hiyo, Jehad Jehad wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu semina hiyo muhimu itakayofanyika kesho kutwa ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere.

"Semina hii ambayo ni ya 26  ni muhimu sana kwetu sisi watu wa sekta ya ujenzi hasa katika kipindi hiki ambacho taifa linatutegema" alisema Jehad.

Alisema semina ya namna hiyo zilianzishwa tangu mwaka 2003 na hufanyika mara mbili kwa mwaka  ambapo jumla ya wabunifu majengo, wakadariaji majenzi na wadau wengine wa sekta ya ujenzi wapatao 5,328 wamekuwa wakinufaika na semina hizo.

Alisema malengo ya semina hiyo ni kuwanoa wabunifu majengo na wakadariaji majenzi na wadau wengine katika sekta ya ujenzi kutambua fursa ambazo ziko katika soko la Afrika Mashariki (EAC) na lile la Nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC)

Alitaja lengo jingine kuwa ni kuwafahanisha wadau faida na umuhimu wa sheria ya mtandao katika kuboresha huduma zao kwa wananchi na kubadilishana uzoefu wa kazi zao za kitaaluma kwa lengo la kuongeza weredi pamoja na kuwapa fursa waataamu katika sekta ya ujenzi kupata nasaha kutoka kwa viongozi wa Serikali.

Jihad aliswema katika semina hiyo mada mbalimbali zitatolewa na kuwa mgeni rasmi anatarajiwa kuwa ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa.


TAZARA KUZALISHA MATARUMA RELI YA KISASA.

$
0
0
 Muonekano wa mtambo wa kusaga kokoto katika kiwanda cha Kongolo cha TAZARA mkoani Mbeya unaotumika kutengeneza kokoto za kujaza tuta la reli.
Muonekano wa kokoto zinazosagwa na kiwanda cha Kongolo cha TAZARA mkoani Mbeya zinazotumika katika uimarishaji wa tuta la reli.
Baadhi ya nondo zinazotumika kutengeneza mataruma katika kiwanda cha Kongolo cha TAZARA Mkoani Mbeya.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

WAKATI Serikali ikiwa katika hatua za kumpata mkandarasi wa ujenzi wa reli ya kisasa nchini (Standard Gauge), Mamlaka ya reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) imesema imewasilisha andiko kwa Kampuni miliki ya rasilimali za Reli (RAHCO) ili kuanza utengenezaji wa mataruma na uzalishaji wa kokoto zitakazotumika kwenye ujenzi wa reli hiyo.

Kauli hiyo imetolewa na Mhandisi Mzalishaji wa kiwanda cha kuzalisha mataruma cha TAZARA mkoani Mbeya, Eng. Boniface Phiri ikiwa ni siku chache baada ya RAHCO kutangaza zabuni hiyo ambapo amesema kuwa kiwanda hicho kina uwezo mkubwa wa kuzalisha mataruma kwa ajili ya ujenzi wa mradi huo.

Eng. Phiri amesema pamoja na agizo la Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano alilolitoa kwa mamlaka hiyo Mwezi mmoja uliopita alipotembelea kiwanda hicho na kuelekeza kuwa Mamlaka ijipange kuzalisha mataruma na kokoto.

“Mamlaka imejitathmini na kuona kwamba kutokana na uwezo tulionao tumeshawasilisha andiko letu kwa RAHCO na tunasubiri majibu yao ili kuanza kazi ya uzalishaji”, amesema Eng. Phiri.

Amebainisha kuwa kwa sasa Mamlaka inaboresha mitambo na kuangalia namna ya kuanza kutumia teknolojia ya mvuke kwenye uzalishaji ili kuongeza idadi ya mataruma na  ubora unaokidhi viwango ambapo kwa siku kiwanda huzalisha mataruma zaidi ya 200.

Aidha Eng.Phiri ameishukuru Serikali Ya Tanzania na Zambia kwa kuisadia Mamlaka hiyo tani 300 za nondo ambazo zimesaidia kuongeza uzalishaji wa mataruma katika kiwanda.

Kwa upande wake Mhandisi Mzalishaji wa mgodi wa kokoto Eng. Juma Mizambwa amesema uzalishaji wa mataruma unaenda sambamba na uzalishaji wa kokoto ambapo kwa sasa mgodi huo unazalisha tani 180 kwa siku.

Mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa unatarajiwa kuanza Mwezi Desemba mwaka huu ambapo kwa mwaka wa fedha 2016/17 Serikali imetenga shillingi Trilioni moja kwa ajili ya utekelezaji wake.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

WANANZENGO WA 102.5 LAKE FM MWANZA WAJUMUIKA NA MFANYAKAZI MWENZAO KUSHEREHEKEA SIKU YAKE YA KUZALIWA.

$
0
0
Septemba 20 miaka kadhaa iliyopita, alizaliwa kijana mchapa kazi anayefanya kazi na 102.5 Lake Fm Mwanza, Imani Hezron. Katika kusherehekea siku yake ya kuzaliwa, Uongozi wa Lake Fm #RahaYaRock #RedioYaWananzengo umemuandalia Imani tafrija fupi kama picha zinavyoonekana.

Na BMG
Mwananzengo wa Lake Fm Mwanza, Imani Hezron, akiogeshwa kwenye siku yake ya kuzaliwa, na baadhi ya wafanyakazi wenzake.
Mwananzengo wa Lake Fm Mwanza, Imani Hezron, akiogeshwa kwenye siku yake ya kuzaliwa
Mwananzengo wa Lake Fm Mwanza, Imani Hezron, akiogeshwa kwenye siku yake ya kuzaliwa
Mwonekano wa mwananzengo Imani Hezron kwenye kusherehea siku yake ya kuzaliwa
Mwanahabari wa Lake Fm na Blogger wa BMG, George Binagi-GB Pazzo, akimlisha keki Imani Hezron
Mtangazaji wa Kipindi cha Mshike Mshike, Aisha BBM, akilishwa keki.
Mtangazaji wa Kipindi cha Kokoliko cha Lake Fm, Caroline Mwaipungu akilishwa keki
Fundi Mitambo Lake Fm, Benjamin Kanuda, akilishwa keki
Dj Dhifa wa 102.5 Lake Fm Mwanza, akilishwa keki
Mtangazaji wa Kipindi cha Viwanjani, Lake Fm, Ally Ngamba (kushoto) akiwa na Mtangazaji wa Kipindi cha Antena, Lake Fm, Imani Hezron (kulia) aliyesherehekea siku yake ya kuzaliwa hii leo.
Bonyeza HAPA Kujua Zaidi.

Droo ya M-Pawa ya Vodacom yamzawadia mshindi kutoka Arusha.

$
0
0

Meneja masoko Huduma  za kifedha wa Vodacom Tanzania, Noel Mazoya (katikati) akiwaonyesha waandishi wa habari namba ya  mshindi  wa droo ya  promosheni ya Jiongeza na M-Pawa   wakati wa hafla ya kuchezesha droo ya pili ya wiki iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo ambapo mkazi wa Arusha  Isaack Pilemon alijishindia kitita cha shilingi Milioni 20. Wanaoshuhudia kutoka  kushoto ni Meneja  wa Huduma za M-pawa wa beki ya CBA  Eric Luyangi  na Msimamizi wa bodi ya michezo ya Kubahatisha nchini Bakari Maggid.  Hadi sasa  washindi 2,800 wameongezea mara mbili ya akiba zao za M-Pawa washindi 14 wameshinda milioni 1 kila mmoja na washindi 2 wamejishindia milioni 20 mshindi wa jumla washilingi milioni 100 atapatika mwezi wa kumi.
 Meneja masoko Huduma  za kifedha wa Vodacom Tanzania, Noel Mazoya (katikati) akiongea na mmoja wa  mshindi wa droo ya  promosheni ya Jiongeza na M-Pawa   wakati wa hafla ya kuchezesha droo ya pili ya wiki iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo ambapo mkazi wa Arusha  Isaack Pilemon alijishindia kitita cha shilingi Milioni 20. Wanaoshuhudia kutoka  kushoto ni Meneja  wa Huduma za M-pawa wa beki ya CBA  Eric Luyangi  na Msimamizi wa bodi ya michezo ya Kubahatisha nchini Bakari Maggid.

UVCCM YAWAVUA KATIBU NA MWENYEKITI ARUSHA

$
0
0
KAMATI ya Utekelezaji ya Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Taifa, limependekeza kwa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CC) kumvua uongozi Mwenyekiti wa umoja huo mkoani Arusha, Lengai Ole Sabaya, kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo kufikishwa mahakamani akituhumiwa kwa utapeli. 

“Wakati tukisubiria uamuzi wa Chama, Kamati ya Utekelezaji ya Baraza Kuu la UVCCM Taifa imemsimamisha uongozi wa nafasi yake ndani ya UVCCM kutokana na kesi iliyoko Mahakamani na kumtaka kuanzia leo (jana) asijihusishe na shughuli zozote za uongozi wa UVCCM hadi hatima ya tuhuma zake itakapoamuliwa na Mahakama na vikao husika vya UVCCM na CCM. 

Mbali na Sabaya, UVCCM pia imemtimua kazi aliyekuwa katibu wake mkoani humo kwa kukiuka utaratibu na maagizo ya UVCCM na CCM ikiwemo vitendo vya utovu wa nidhamu. 

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana Dar es Salaam na kutiwa saini na Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM, Shaka Hamdu Shaka, ilisema Kamati ya Utekelezaji ya Baraza Kuu la UVCCM Taifa ilikutana Septemba 19, nwaka huu Dar es Salaam chini ya Mwenyekiti wake Sadifa Juma Khamis ambapo pamoja na mambo mengine walifikia uamuzi huo. 

Ilisema kikao hicho kilitanguliwa na kikao cha Kamati ya Maadili na Nidhamu ya UVCCM Taifa, ambapo pamoja na mambo mengine kilipokea na kujadili uhai wa CCM na umoja huo mkoani Arusha. Alisema baada ya kupokea taarifa hiyo walijadili kuyatolea ufafanuzi mambo mbalimbali kuhusu makada wake hao wawili. 

Taarifa ya Shaka ilisema miongoni mwa mambo yaliyomhusu Sabaya ikiwemo kuyaongoza makundi ya vijana wa CCM na wasiokuwa wa CCM ili kumkataa Katibu wa UVCCM aliyehamishiwa mkoani Arusha, Said Goha kuchukua nafasi ya Ezekiel Mollel. Ilisema kuwa Sabaya licha ya kupewa heshima na kuelimishwa na vikao vya juu na viongozi mara kwa mara kupitia Mwenyekiti wa UVCCM taifa, kuhusu mamlaka za kikanuni ikiwemo ya utumishi na maadili ya UVCCM lakini ameshindwa kujirekebisha. 

“Sabaya amesababisha taharuki iliyosababisha ofisi za UVCCM Arusha kufungwa kwa minyororo hadi Jeshi la Polisi kuingilia kati. Vile vile taharuki hiyo imechangia kwa kiasi kikubwa Vijana wa mkoa wa Arusha kugawanyika katika makundi na kusababisha hali ya usalama na maadili kwa umoja huo na Chama kuwa ya wasiwasi. 

“Sabaya kufikishwa mahakamani akikabiliwa na mashitaka mawili likiwemo la kujifanya mtumishi wa Idara ya Usalama wa Taifa. Huku kosa la pili katika muda usiojulikana akidaiwa kughushi vitambulisho vya Idara ya Usalama wa Taifa (TISS) chenye namba MT 86117 wakati akijua ni kinyume cha Sheria za nchi. 

“Kamati ya Utekelezaji ilipitia tuhuma mbalimbali na vielelezo vya utapeli na ulaghai unaodaiwa kutendwa na Sabaya katika maeneo tofauti huku akijua ni kinyume na miiko na maadili ya uongozi wa UVCCM na CCM.
“Kwa makosa yote hayo Sabaya amekukiuka kanuni ya uongozi na maadili ya CCM Fungu la (3) ukurasa wa 16 na 17, na fungu la (4) ukurasa wa 29, 30 na 31. Pia makosa hayo ameyatenda kinyume na utaratibu wa uongozi na maadili ya UVCCM, Ibara ya 6.3.2 Ibara ya 7.5.1, 7.5.4 na 8.2.5,”alisema.


Kuhusu Mollel, alisema alipokuwa Katibu wa Vijana Mkoa wa Arusha, alipewa barua ya uhamisho, kama inavyoelekezwa na Kanuni ya Utumishi ya UVCCM kifungu cha 3(13) ukurasa wa 21 na 22 inayohusu uhamisho wa mtumishi. Kanuni hiyo inasema “Mfanyakazi yeyote atakayekataa kutii amri ya uhamisho bila sababu zinazokubalika atachukuliwa hatua za kinidhamu kwa mujibu wa Kanuni hizi”. Ilisema Mollel amerudia makosa mara kwama kwa kuwa aliwahi kusimamishwa kazi mwaka 2015 akiwa Katibu wa UVCCM Mkoa wa Manyara, jambo ambalo lilisababisha kumnyang’anya kituo na kumsimamisha kazi kwa muda. 

Aidha, pamoja na yote hayo Mollel hakujirekebisha hata pale aliporudishwa kazini na kupelekwa mkoa wa Arusha. “Kamati ya Utekelezaji ya UVCCM Taifa imebariki uamuzi uliochukuliwa na Sekretarieti ya Baraza Kuu ya UVCCM iliyokutana Septemba 14, mwaka huu. Kamati imependekeza kwa Baraza Kuu la UVCCM Taifa kumfukuza kazi mara moja Ezekiel Mollel,”ilisema.

Aidha ilitoa ufafanuzi kuuhusu madai ya tuhuma zinazotolewa na Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Arusha kuwa kuna ufisadi na baadhi ya viongozi wa makao makuu ya UVCCM wanahusika ilisema ikumbukwe kuwa umoja huo ulianza kujitathimini na kuhakiki mali zake Desemba, 2015.

Ilisema mkoa wa Arusha ni miongoni mwa mikoa iliyobainika kuwa taarifa zake hazikuwa na ukweli na kubainisha matakwa ya uhakiki kama walivyoagizwa.

Kikao cha Kamati ya Utekelezaji ya Baraza Kuu la UVCCM Taifa kilichokutana tarehe 18/08/2016 Mjini Dodoma kupokea na kupitia taarifa za uhakiki Mali za UVCCM ngazi ya Taifa, Mkoa na Wilaya kiliagiza Sekretarieti ya Baraza Kuu la UVCCM Taifa kuwaita Viongozi wa Mkoa wa Arusha ili kuendelea kujiridhisha na taarifa walizowasilisha Makao Makuu kwa vile zimebainika kuwa na mapungufu makubwa.

Katika Taarifa hiyo iliyowasilishwa kwa maandishi na kuthibitishwa na Kamati ya Utekelezaji ya Mkoa wa Arusha hakuna sehemu ambayo kumeainishwa ubadhirifu ama upotevu wa fedha kinyume na madai yaliyoibuliwa siku za karibuni baada ya Viongozi hao kuchukuliwa hatua za kinidhamu, kutokana na makosa ya Maadili ya Uongozi.

Hata Kamati ya Utekelezaji ya Mkoa wa Arusha ilipoitwa katika kikao cha Kamati ya Maadili cha tarehe 19/08/2016 kilichofanyika Mjini Dodoma walikana na kudai wao hawajawasilisha malalamiko yoyote kuhusu tuhuma wanazozitoa na kusema wanaendelea na kufanyia kazi na kurekebisha mambo ya msingi kuhusu Uchumi wa Mkoa wao.

Kufuatia hatua hiyo Kamati ya Maadili na Nidhamu na Kamati ya Utekelezaji ya Baraza Kuu la UVCCM Taifa iliagiza Ofisi ya Katibu Mkuu iendelee kufuatilia kwa karibu jambo hilo ili kubaini ukweli baada ya kujiridhisha kuweko na harufu ya ubadhirifu, jambo ambalo limepelekea Viongozi hao kutosema ukweli pamoja na kusisitizwa mara kadhaa kwa maandishi bado taarifa zao hazikujitosheleza.

MAABARA YA HOSPITALI YA MNAZIMMOJA ZANZIBAR YAKABIDHIWA CHETI CHA ITHIBATI YA KIMATAIFA

$
0
0
Afisa wa Viwango vya Ubora wa Maabara ya Hospitali Kuu ya Mnazimmoja Muhamed Soud Muhamed akielezea hatua zilizochukuliwa na Maabara hiyo mpaka kufanikiwa kukabidhiwa cheti cha Ithibati ya Kimataifa.
Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo akibadilishana mawazo na Afisa Mtendaji Mkuu wa SADCAS Maureen Mutasa wakati wa sherehe za kukabidhiwa cheti cha Ithibati ya Kimataifa kwa maabara ya Hospitali ya Mnazimmoja zilizofanyika Hospitalini hapo.
Afisa Mtendaji Mkuu wa SADCAS Maureen Mutasa akizungumza katika sherehe za kukabidhi cheti cha Ithibati ya Kimataifa kwa ajili ya Maabara ya Hospitali ya Mnazi mmoja.
Afisa Mtendaji Mkuu wa SADCAS Maureen Mutasa akimkabidhi Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo cheti cha Ithibati ya Kimataifa kwa ajili ya Maabara ya Hospitali ya Mnazimmoja.
Baadhi ya wafanyakazi wa Wizara ya Afya wakifuatilia sherehe za kukabidhiwa cheti cha Ithibati ya Kimata kwa ajili ya Maabara ya Hospitali Kuu ya Mnazimmoja.
Baadhi ya wafanyakazi wa Maabara ya Hospitali ya Mnazmmoja wakifurahia vyeti walivyokabidhiwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa SADCAS wakiwa ndani ya maabara yao Hospitali ya Mnazimmoja.

Picha na Makame Mshenga/Maelezio Zanzibar.

…………………………………………………………

Na Ramadhani Ali/Maelezo Zanzibar

Hospitali Kuu ya Mnazimmoja imepokea cheti cha Ithibati ya Kimataifa kwa ajili ya Maabara ya Hospitali hiyo kutoka Bodi ya Kimataifa ya Ithibati ya Nchi za Ukanda wa Kusini mwa Afrika (SADCAS) katika hafla iliyofanyika Hospitalini hapo.

Mtendaji Mkuu wa SADCAS Maureen Mutasa alimkabidhi cheti cha Ithibati Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo kutokana na huduma bora zinazotolewa na Maabara hiyo.

Akitoa maelezo ya kupatikana cheti cha Ithibati ya Kimataifa, Afisa wa viwango vya ubora wa Maabara ya Hospitali Kuu ya Mnazimmoja Mohamed Soud amesema ni mashirikiano ya pamoja kati ya uongozi na wafanyakazi wa maabara, Hospitali Kuu ya Mnazimmoja na Uongozi wa Wizara ya Afya .

Amesema haikuwa jambo rahisi kufikia hatua hiyo kutokana na changamoto nyingi zilizokuwa zikiikabili Maabara hiyo ikiwemo vifaa na utaalamu wa kiufundi unaokubalika kufikia viwango vinavyotakiwa na Bodi ya Ithibati ya Kimataifa.

Mohamed ameongeza kuwa kutunukiwa cheti hicho ni uthibitisho rasmi kuwa kuanzia sasa matokeo ya uchunguzi yanayotolewa na maabara ya Hospitali ya Mnazimmoja yanaweza kutumika na kuaminika nchi zote.

Aidha amesema wananchi watajenga imani na huduma za uchunguzi wa maradhi mbali mbali zinazofanywa na maabara ya Mnazimmoja kwa vile imefikia kiwango cha Kimataifa. Faida nyengine itakayopatikana kutokana na cheti cha Ithibati ya Kimataifa amesema ni kutoa fursa kwa Taasisi za kimataifa na wasomi duniani kuitumia maabara hiyo kufanya tafiti mbali mbali zinazohusiana na Afya ya binadamu.

Katika kuthamini cheti hicho, Dkt. Muhamed ameishauri Serikali kuziimarisha maabara za Hospitali nyengine kubwa na zile za Wilaya ikiwemo Makunduchi, Kivunge, Abdalla Mzee Mkoani, Chake chake, Wete na Vitongozi.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya SADCAS Maureen Mutasa ameupongeza uongozi wa maabara ya Mnazimmoja kwa juhudi kubwa walizochukua licha ya kukabiliana na changamoto nyingi kabla ya kupata mafanikio hayo. Amesema cheti hicho ni cha 15 kutolewa na Bodi ya Ithibati ya SADCAS na kwa Tanzania ni maabara ya sita kupata cheti cha Ithibati maabara tano zipo Tanzania Bara.

Hata hivyo ameushauri uongozi na wafanyakazi kwa jumla kuongeza juhudi za kutoa huduma bora ili cheti hicho ambacho kitadumu kwa miaka mitano kiendelee kubaki.

Akipokea cheti cha Ithibati, Waziri Afya Mahmoud Thabit Kombo amewataka wananchi kuthamini juhudi zinavyofanywa na wafanyakazi wa vitengo mbali mbali vya Hospitali Kuu ya Mnazimmoja na kuacha tabia ya kulaumu.

Ameushauri Uongozi na wafanyakazi wa Maabara hiyo kuendelea kuwahudumia wananchi kwa juhudi zao zote kwani juhudi hizo ndizo zilizopelekea kupewa cheti na kutambulika kimataifa.

SERIKALI KUSAMBAZA CHAKULA SALAMA KWA WAATHIRIKA WA SUMUKUVU

$
0
0
Naibu Waziri Wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigangwala akisisitiza jambo mbele ya waandishi wa habari na watafiti mbalimbali hawapo pichani wakati wa uzinduzi wa mkutano wa watafiti wa chakula uliojadili madhara na athari za sumukuvu uliofanyika jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri Wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigangwala wa kwanza kulia akijadiliana jambo na Mkurugenzi Mkuu Bw. Hiiti Silo kushoto na Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma na ubora Wizara ya afya Dkt. Mohammed Mohammed katikati wakati wa uzinduzi wa mkutano wa watafiti wa chakula uliojadili madhara na athari za sumukuvu uliofanyika jijini Dar es salaam.
Watalaamu wa utafiti na wadau mbalimbali wa afya kutoka nchi mbalimbali wakifuatilia kwa makini maelezo ya Naibu Waziri Wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigangwala hayupo pichani wakati wa uzinduzi wa mkutano wa watafiti wa chakula uliojadili madhara na athari za sumukuvu uliofanyika jijini Dar es salaam.

Picha zote Na Ally Daud-Maelezo

………………………………………………….

Na Ally Daud-Maelezo

SERIKALI imesambaza chakula salama na kutoa tiba bure kwa waathirika wa ugonjwa wa mlipuko wa sumukuvu katika mikoa ya Dodoma na Manyara uliotokea hivi karibuni.

Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri Wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigangwala wakati wa uzinduzi wa mkutano wa watafiti wa chakula uliojadili madhara na athari za sumukuvu.

Dkt. Kigwangala alisema Serikali imeandaa utaratibu wa kuwapelekea vyakula salama waathirika wa ugonjwa huo na kuteketeza vyakula vyenye sumukuvu.

“Tumepanga utaratibu wa kupeleka vyakula salama kwa waathirika wa ugonjwa a sumukuvu katika mikoa husika bila malipo ili kusaidia kuondoa ugonjwa huo na kuteketeza mabaki ya vyakula vyenye vizaria vya sumukuvu” alisema Dkt. Kigangwala

Aidha Dkt. Kigwangala alisema kuwa Serikali ipo bega kwa bega na waathirika wa sumukuvu ili kuhakikisha wanaondoa ugonjwa huo kwani tayari umethibitishwa na wataalamu na unapatikana kwenye mazao ya vyakula kama vile mahindi, uwele, mtama na karanga.

Kwa mujibu wa Dkt. Kigangwala alisema katika kukabiliana na ugonjwa huo Serikali imeamua kushirikiana na wataalamu wa kimataifa ili kuweza kuondoa ugonjwa huo kwenye vyakula vinavyolimwa nchini ili kuyawezesha mazao mazao hayo kuuzwa kwa urahisi hapa nchini.

Dkt Kigwangala aliwashukuru watafiti hao kwa kugundua chanzo cha ugonjwa huo ambao unasababishwa na Jamii ya fangasi wanaoitwa Aspergillus wanaojikita zaidi kwenye vyakula na kuwataka wapate matokeo chanya ya kutokomeza sumukuvu.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Bw. Hiiti Silo alisema katika mkutano huo watafiti hao wanatarajia kujadili na kupata ufumbuzi wa tafiti za vyakula mbalimbali ili visiendelee kuleta madhara kwa Watanzania.

Shule ya Sekondari ya Ihungo yaanza kufanyiwa Ukarabati

$
0
0
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Tamisemi  Mhe.George Simba Chawene akizungumza jambo na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako mara baada ya ya kutembelea shule ya sekondari ya Ihungo ambayo imeathiriwa vibaya na Tetemeko la Ardhi.
 Waziriwa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe.Jenista Mhagama akizungumza na wahandishi wa habari kuhusu hatua ambayo serikali imechukua kusaidia ukarabati wa shule ya Ihungo ambayo imeathiriwa vibaya na Tetemeko la Ardhi.KUlia kwake ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Tamisemi  Mhe.George Simba Chawene
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Tamisemi  Mhe.George Simba Chawene akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kutembelea shule ya sekondari ya Ihungo ambayo imeathiriwa vibaya na Tetemeko la Ardhi.Kushoto kwake ni Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe.Jenista Mhagama.
Wafanyakazi wa VETA wakiendelea na ubomoaji wa Shule ya Ihungo ambayo  inavunjwa na kujengwa upya kwa msaada wadau na Serikali baada ya kuathiriwa na tetemeko la ardhi la hivi karibuni Mkoani Kagera.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA APOKEA MICHANGO YA SH. BILIONI MOJA

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea hundi ya shilingi 1,000,030,100/= kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Mhandisi John Kijazi (katikati) na Msajili wa Hazina, Lawrence Mafuru  (kushoto) kwa ajili ya waathirika wa tetemeko la ardhi lililotokea Kagera .  Fedha hizo ni michango ya watumishi wa serikali na  Taasisi zake. Makabidhiano hayo yalifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Septemba 20, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kupokea hundi ya shilingi 1,000,030,100/= kutoka kwa  Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Mhandisi John Kijazi (katikati) na Msajili wa Hazina, Lawrence Mafuru   (wapili kulia) na Msajili wa Hazina Lawrence Mafuru  (kushoto) .Fedha hizo ni michango ya watumishi wa serikali na taasisis zake na makabidhiano yalifanyika Ofisni kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Septemba 20, 2016. 
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepokea jumla ya sh. bilioni 1.040 kutoka kwa watumishi na wadau mbalimbali zikiwa ni misaada kwa wananchi walioathirika na tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera Septemba 10, mwaka huu.

Makabidhiano ya michango hiyo, yamefanyika leo mchana (Jumanne, Septemba 20, 2016) kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es Salaam.

Akikabidhi hundi kwa Waziri Mkuu, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi alisema kiasi cha sh. 1,000,030,100 kimekusanywa kutoka kwa watumishi wa idara na Wizara zote  za Serikali na kwamba michango zaidi bado inaendelea kukusanywa.

“Tunaamini michango hii itasaidia kuwafuta machozi wenzetu waliopatwa na maafa japokuwa tunajua haitatosha kurudisha kile walichopoteza. Tuna imani itasaidia kupunguza makali ya machungu waliyoyapata,” amesema.

Hata hicyo, Balozi Kijazi amemhakikishia Waziri Mkuu kwamba bado wanaendelea kukusanya michango kutoka kwenye nyingine ambazo zilichelewa kupata taarifa na kwamba wakikamilisha wataiwasilisha mapema iwezekanavyo.
               
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amepokea michango ya sh. milioni 40 na kati ya hizo, sh. milioni 20 zimetolewa na kampuni ya ujenzi ya CHICO ya China na sh. milioni 20 nyingine zimetoka kwa Umoja wa Wafanyabiashara na Wenye Viwanda wa India waliopo nchini (India Business Forum).

Akiwasilisha mchango wake, Mwakilishi Mkuu wa kampuni ya CHICO hapa nchini, Bw. Guo Zhijian alisema wamesikitishwa na maafa yaliyotokea mkoani Kagera. “Tumefanya miradi mingi mkoani Kagera ikiwemo ujenzi wa barabara za urefu kilometa 300, kwa hiyo mkoa huu tunaujua zaidi. Tunatoa pole kwa wote waliopatwa na maafa  hayo,” amesema.

Naye Mwenyekiti wa umoja wa wafanyabiashara na wenye viwanda kutoka India (IBF), Bw. Gagan Gupta alimweleza Waziri Mkuu kwamba wameshtushwa na tukio hilo na kwamba wametanguliza kiasi hicho ili kisaidie juhudi za Serikali katika kukabiliana na maafa hayo.

“Bado tunaendelea kuwasiliana na wenzetu wengine na tukipata michango zaidi tutaiwasilisha mapema iwezekanavyo,” amesema.

Akitoa shukrani kwa waliotoa michango yote hiyo, Waziri Mkuu amewashukuru kwa misaada hiyo na kuahidi kuwa Serikali itahakikisha michango hiyo inafikishwa Kagera kwa walengwa.

“Tunashukuru sana kwa michango yote. Michango hii ni muhimu na inaonyesha mshikamano wa dhati uliopo. Michango hii inaonyesha kuguswa na mapenzi ya dhati kwa waliopatwa na maafa. Napenda niwahakikishie kuwa Kamati za Maafa za Mkoa, Ofisi ya Waziri Mkuu na kamati za wilaya, ziko pale kuhakikisha walengwa wanafikiwa,” ameongeza.

Waziri Mkuu amesema Serikali inakamilisha tathmini ya maafa hayo na kuahidi kutoa taarifa ya kiasi kilichokusanywa na kiasi kilichotumika. Amewaomba wananchi waliotoa ahadi zao za michango wakamilishe ahadi zao.

“Ninawaomba wale walioahidi kutoa michango wakamilishe ahadi zao na wale walio mbali na benki watumie namba za simu zilizotolewa mahsusi kwa ajili ya kuchangia maafa hayo,” amesisitiza.
Akaunti ya maafa imefunguliwa katika Benki ya CRDB yenye namba 015 222 561 7300 kwa jina la KAMATI MAAFA KAGERA – Swiftcode: CORUtztz na namba za simu za mkononi zinazotumika kupokea michango hiyo ni 0768-196-669 (M-Pesa) au 0682-950-009 (Airtel Money) au 0718-069-616 (Tigo Pesa).

Tetemeko hilo lililotokea Jumamosi, Septemba 10, mwaka huu, lilisababisha vifo vya watu 17 na wengine 440 kujeruhiwa. Kati yao, watu 253 walifikishwa Hospitali ya Mkoa, 153 walilazwa, 113 walitibiwa na kuruhusiwa na wengine 38 wanaendelea na matibabu ambapo kati yao watu 23 wamefanyiwa upasuaji mkubwa na wanaendelea vizuri.

Pia tetemeko hilo limesababisha nyumba 2,063 kuanguka huku nyingine 14,081 zikiwa katika hali hatarishi baada ya kupata nyufa na 9,471 zimepata uharibifu mdogo huku wananchi 126,315 wakihitaji misaada mbalimbali.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S.  L. P. 3021,
11410 - DAR ES SALAAM.

JUMANNE, SEPTEMBA 20, 2016.

YAH: JINA SAHIHI LA AKAUNTI YA KUCHANGIA MAAFA KAGERA

$
0
0




Ofisi ya Waziri Mkuu Idara ya Uratibu Maafa inaendelea kuwapa wananchi pole na janga la tetemeko lililotupata  katika mkoa wa kagera tarehe 10.09.2016.
Aidha Kitengo cha Maafa kinapenda kutaarifu umma kwamba jina sahihi la akaunti ya Maafa ni KAMATI MAAFA na sio KAMATI YA MAAFA.
Pia Idara inasisitiza watu mbalimbali kuendelea kuchangia misaada kupitia akaunti Rasmi zifuatazo:
CRDB BANK BUKOBA
Akaunti Na: 0152225617300
Swiftcode: CORUtztz
M-pesa: 0768196669
Tigo Pesa: 0718069616
Airtel Money: 0682950009

Idara inakaribisha taarifa za maoni, malalamiko au jambo lolote kutoka kwa waathirika wa tetemeko la ardhi kupitia kitengo cha maafa ofisi ya waziri mkuu na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera kwa simu namba zifuatazo:
OFISI YA MKUU WA MKOA KAGERA-Simu namba 0621155777
KITENGO CHA MAAFA OFISI YA WAZIRI MKUU: 0621155888
IMETOLEWA NA:
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Ofisi ya Waziri Mkuu
2 MTAA WA MAGOGONI,
S.  L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM.
SEPTEMBA 20, 2016

RAIS DKT MAGUFULI ATEUA WENYEVITI WENGINE WATATU JIJINI DAR LEO

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amemteua Luteni Kanali Mstaafu Haroun Ramadhan Kondo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania.

Taarifa iliyotolewa leo tarehe 20 Septemba, 2016 Ikulu Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Luteni Kanali Mstaafu Haroun Ramadhani Kondo umeanza tarehe 05 Septemba, 2016.Luteni Kanali Mstaafu Haroun Ramadhani Kondo anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Yamungu Kayandabila ambaye amemaliza muda wake.

Wakati huo huo, Rais Magufuli amemteua Dkt. Hedwiga Francis Swai kuwa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) kuanzia tarehe 05 Septemba, 2016.

Dkt. Hedwiga Francis Swai ni Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Katika hatua nyingine, Rais Magufuli amemteua Balozi Ladislaus Columban Komba kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC) kuanzia tarehe 05 Septemba, 2016.

Balozi Ladislaus Columbas Komba anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Christopher Celestine Liundi ambaye amemaliza muda wake.

Halikadhalika, Rais Magufuli amemteua Bw. Fidelis Mutakyamilwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya Taifa ya Matumizi ya ardhi kuanzia tarehe 29 Agosti, 2016.Bw. Fidelis Mutakyamilwa ni Mwanasheria Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa LAPF


Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
20 Septemba, 2016

MAHAKAMA ZASHAURIWA KUZINGATIA HAKI YA MSINGI

$
0
0
 Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe. Engera Kileo akipokea shada la maua kutoka kwa mmoja wa wafanyakazi wa Mahakama ya Rufani Tanzania wakati wa hafla ya kumuaga iliyofanyika katika ukumbi wa mahakama Kuu, leo Jijini Dar es Salaam.  Mhe. Kileo ameagwa leo baada ya kutumikia takribani miaka 40 katika nyadhifa mbalimbali ndani ya Idara ya Mahakama Tanzania.
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman (watatu kutoka kushoto)akiwa katika picha ya pamoja na Jaji Msaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe. Engera Kileo (kulia) wakati wa hafla ya kumuga Jaji huyo leo Jijini Dar es Salaam.  Mhe. Kileo ameagwa leo baada ya kutumikia takribani miaka 40 katika nyadhifa mbalimbali ndani ya Idara ya Mahakama.

 Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman akizungumza wakati wa hafla ya kumuaga Jaji Msaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe. Engera Kileo (kulia) wakati wa hafla ya kumuga Jaji huyo iliyofanyika katika ukumbi namba moja wa Mahakama Kuu leo Jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Jaji wa Mahakama ya Rufani Mhe. Shaban Ali Lila,  Mhe. Kileo ameagwa leo baada ya kutumikia takribani miaka 40 katika nyadhifa mbalimbali ndani ya Idara ya Mahakama.
 Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman akizungumza wakati wa hafla ya kumuaga Jaji Msaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe. Engera Kileo (kulia) wakati wa hafla ya kumuga Jaji huyo iliyofanyika katika ukumbi namba moja wa Mahakama Kuu leo Jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Jaji wa Mahakama ya Rufani Mhe. Shaban Ali Lila,  Mhe. Kileo ameagwa leo baada ya kutumikia takribani miaka 40 katika nyadhifa mbalimbali ndani ya Idara ya Mahakama.
 Baadhi ya wageni waalikwa wakifuatilia hafla ya kuagwa kwa Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe. Engera Kileo leo Jijini Dar es Salaam.
 Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe. Engera Kileo akipongezwa na mototo wake wa kike, Bi. Noera Kileo wakati wa hafla ya kuagwa kwake iliyofanyika katika ukumbi wa mahakama Kuu leo Jijini Dar es Salaam. Mhe. Kileo ameagwa leo baada ya kutumikia takribani miaka 40 katika nyadhifa mbalimbali ndani ya Idara ya Mahakama Tanzania.

Picha zote na Frank Shija, MAELEZO.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AMJULIA HALI SPIKA MSTAAFU SAMWEL SITTA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Spika Mstaafu, Samwel Sitta na mkewe Margaret wakati alipomjulia hali jijini Dar  es salaam Septemba 20, 2016.  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live




Latest Images