Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46205 articles
Browse latest View live

Kibaha yatoa msaada wa milioni 5 kwa vijana waliosomeshwa chini ya mradi wa YEE

0
0


Mratibu wa Mradi wa Uwezeshaji Vijana Kiuchumi (YEE) Kanda ya Mashariki, Adolf Jeremiah akiongea na waandishi wa habari juu ya maendeleo ya vijana hao baada ya kuhitimu mafunzo ya ufundi katika Chuo cha Elimu na Ufundi Stadi (VETA), mradi huo unafadhiliwa na Umoja wa Nchi za Ulaya na kuratibiwa na Shirika la Plan International.
 

Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO, Kibaha.

Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha imewasaidia vijana waliopitia katika mradi wa kuendeleza Vijana Kiuchumi (YEE) kwa kuwapa jumla ya shilingi milioni 5 kwa ajili ya kuwawezesha kujisajili katika vikundi mbalimbali vitakavyowasaidia kuendeleza kazi zao.

Msaada huo umetolewa hivi karibuni baada ya vijana hao kuhitimu mafunzo ya ufundi yaliyokuwa yakiendeshwa na Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) Kanda ya Pwani na kutakiwa kuunda vikundi kulingana na fani walizosomea ili kuweza kujisajili katika vyama hivyo vitakakavyowawezesha kupata fursa mbalimbali.

Hayo yamesemwa leo wilayani Kibaha na Afisa Maendeleo ya Vijana wa Wilaya hiyo, Yahaya Mbogolume alipokuwa akiongea na mwandishi wa habari hii juu ya maendeleo ya vijana hao baada ya kuhitimu mafunzo ya fani mbalimbali chini ya mradi huo.

Mbogolume amesema kuwa mradi huo umekuja wakati muafaka kwani umekuwa chachu ya maendeleo ya Halmashauri hiyo kwa sababu asilimia kubwa ya wakazi wa eneo hilo ni vijana ambao walikuwa hawana cha kufanya lakini kupitia fursa hiyo vijana wameweza kujiajiri.

 “Hawa ni vijana wetu wako kwenye eneo letu hivyo, sisi kama Halmashauri ni wajibu wetu kuhakikisha wanajiajiri na kuweza kupata kipato , kwa kutambua hilo tumetoa shilingi milioni 5 kwa ajili ya kusaidia vijana waliopo kwenye mradi wa YEE kujisajili kwenye vikundi vitakavyowasaidia kuongeza vipato vyao”, alisema Mbogolume.

Afisa huyo ameongeza kuwa Halmashauri inaendelea kuwawezesha vijana kwa kuwapa mikopo inayowasaidia kuendeleza biashara zao ambapo kwa mwezi huu halmashauri hiyo imetenga jumla ya shilingi milioni 8 kwa ajili ya kuwaendeleza kiuchumi vijana hao ambao wameonyesha uhitaji baada ya kupata mafunzo ya ufundi wa fani mbalimbali.

Kwa upande wake Mratibu wa Mradi wa YEE Kanda ya Mashariki, Adolf Jeremiah amesema kuwa mradi huo hautoishia kuwapatia ujuzi tu bali utaendelea kuwawezesha kichumi ili kuhakikisha vijana hao wanasimama imara na wanapata maendeleo kupitia fani walizozisomea.

“Shirika la Plan International tumeamua kusaidia vijana kwa hali na mali hivyo ni lazima kuhakikisha wanayafikia malengo yao, kwa sasa tumewasiliana na VETA wafanye tathmini ya vifaa vinavyotakiwa na vijana hao ili tuweze kuvinunua na kuwagawia waendeleze fani zao zinazowasaidia katika maisha yao ya kila siku”, alisema Jeremiah.

Naye mmoja wa wahitimu wa mradi huo, George Geligoali ametoa rai kwa vijana wenzie kuacha kudharau fursa zinazotolewa na makampuni mbalimbali na badala yake wazichangamkie kwa kuwa fursa hizo ni kwa ajili ya maendeleo yao na Taifa kiujumla.

Amelishukuru Shirika hilo kwa kumuwezesha kupata mafunzo katika fani ya umeme ambayo inampatia kipato kinachomuwezesha kujikimu yeye na kuhudumia wazazi wake.

Katika Halmashauri hiyo, jumla ya vijana 355 waishio kwenye mazingira magumu wameshahitimu mafunzo ya ufundi katika awamu ya kwanza na ya pili ya mradi, vijana 188 wanaendelea na mafunzo ya awamu ya tatu. Mradi huo unatekelezwa kwa ushirikiano na mashirika ya VSO, CCBRT, VETA, UHIKI, CODERT pamoja na Serikali ya Tanzania huku ukiratibiwa na Shirika la Plan International chini ya ufadhili wa Umoja wa Nchi za Ulaya (EU).


MOROGORO MABINGWA AIRTEL RISING STARS.

0
0
 Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Nape Nnauye na Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania wakimkabidhi nahodha wa Temeke wasichana Shamimu Hamisi kombe la ubigwa wa Airtel Rising Stars 2016.  Temeke waliishinda Ilala 5-4 katika changamoto ya mikwaju ya penati.
 Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Nape Nnauye akimkabidhi nahodha wa Temeke wasichana Shamimu Hamisi kombe la ubigwa wa Airtel Rising Stars 2016.  Temeke waliishinda Ilala 5-4 katika changamoto ya mikwaju ya penati.
 Timu ya Morogoro wakishangilia baada ya kukabidhiwa kombe la uchampioni wa Airtel Rising Stars 2016 kwa upande wa wavulana. Morogoro iliifunga Ilala 1-0 katika fainali iliyopigwa kwenye uwanja wa Karume, Dar es Salaam jana.
Temeke wasichana wakishangilia baada ya kukabidhiwa kombe la uchampioni wa Airtel Rising Stars 2016. Temeke waliishinda Ilala 5-4 katika changamoto ya mikwaju ya penati.

Goli pekee lililofungwa na mshambuliaji hatari Tepesi Evans wa Morogoro lilitosha kuifanya timu hiyo kuwa mabingwa wa michuano ya vijana chini ya miaka 17 ya Airtel Rising Stars 2016 kwa kuwafunga Ilala 1-0. Mechi hiyo ambayo ilikuwa ya kuvutiwa yenye upinzani mkali ilishuhudiwa na mamia ya mashabiki akiwepo Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Nape Nnauye.

Baada ya kosa kosa nyingi, Evans aliachia shuti kali mnamo dakika 77 ya mchezo, shuti ambalo lilienda moja kwa moja na kuamsha shangwe na nderemo kutoka kwa mashabiki. Juhudi za Ilala kuzawashisha hazikuzaa matunda mpaka mchezo unamalizika.

Mchezo huo ulikuwa ni kama marudio ya mechi ya Alhamisi ambapo timu hizo zilikutana kwenye hatua ya makundi huku Ilala ikitoka kichwa chini kwa kukubali kichapo cha 2-0.

Akifunga michuano hiyo ya kila mwaka, Waziri Nnauye alisema kuwa serikali inaunga mkono juhudi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) pamoja na wadhamini. ‘Kwa kuwapa fursa wasichana na wavulana hawa kuonyesha vipaji vyao, ni kusaidia kubadilisha maisha yao kwani mpira wa soka ni zaidi ya burundani – ni kufahamiana, kupata uzoefu na zaidi, ni ajira’, alisema Nnauye.

Naye Mkurungenzi Mtendaji Airtel Tanzania Sunil Colaso alisema kampuni yake inajivunia mafanikio ya Airtel Rising Stars yaliyopatikana miaka tano iliyopita. ‘Wachezaji ambao waliisaidia Uganda kufuzu kwenye michuano ya AFCON 2017 Gabon ni uzao wa Airtel Rising Stars na ni uhakika hayo yatatokea Tanzania hivi karibuni’. Alisema Colaso huku akiongeza kuwa Airtel mpaka sasa ishawekeza Tshs2.4 billioni kwenye michuano hiyo.

Kwa upande wake Raisi wa TFF Jamal Malinzi alielezea michuano ya Airtel Rising Stars kama michuano ya kutumainiwa katika kuibua vipaji. ‘Serengeti Boys na timu ya Taifa ya Wanawake ni ushuhuda tosha wa mafainikio ya michuano hii’, alisema Malinzi.
Timu bora, wachezaji bora, waamuzi pamoja na makocha walipewa tuzo wakati wa fainali za michuano hiyo.

Timu ya Temeke wasichana walishinda ubingwa wa michuano hiyo kwa penati 5-4 baada ya kwenda sare ya 2-2 kwenye muda wa kawaida.

Wakati huo huo, timu ya Temeke wavulana walishinda nafasi ya tatu ya michuano hiyo kwa changamoto ya mikwaju ya penati ya 5-4 dhidi ya Kinondoni baada ya kutoka sare ya 0-0 kwenye muda wa kawaida.

Kinondoni wasichana walipata nafasi ya mshindi wa tatu baada ya kuwafunga wenzao Arusha 2-0. Magoli yote ya Kinondoni yalifungwa na Veronica Mapunda.

KAMANDA WA POLISI KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI (MOHAMED MPINGA) ATOA ELIMU YA USALAMA BARABARANI KWA MADEREVA WA BODABODA.

0
0

Kamanda wa Polisi Kikosi cha usalama barabarani Tanzania, mohammed Ramadhan Mpinga, akitoa elimu ya usalama bararani kwa waendesha pikipiki maarufu kwa jina la bodaboda, wakati wa mashindano ya kombe la Mpinga Cup 2016 kutoka kundi E, iliyofanyika kwenye uwanja wa Tabata Shule, juzi.
Kamanda wa Polisi Kikosi cha usalama barabarani Tanzania, mohammed Ramadhan Mpinga, akitoa elimu ya usalama bararani kwa waendesha pikipiki maarufu kwa jina la bodaboda, wakati wa mashindano ya kombe la Mpinga Cup 2016 kutoka kundi E, iliyofanyika kwenye uwanja wa Tabata Shule, juzi.(Picha na Traffic Makao Makuu).
Msaidizi wa Kamanda DCP Mpinga, SACP Fortunatus Muslim, akitoa elimu ya usalama bararani kwa waendesha pikipiki maarufu kwa jina la bodaboda, wakati wa mashindano ya kombe la Mpinga Cup 2016 kutoka kundi E, iliyofanyika kwenye uwanja wa Tabata Shule, juzi.
S/SGT Enock Machunde, Kitengo cha Elimu kutoka Traffic Makao Makuu Dar es Salaam, akitoa elimu ya usalama bararani kwa wachezaji wa timu zilizoshiriki kundi E ambao ni waendesha pikipiki maarufu kwa jina la bodaboda, wakati wa mashindano ya kombe la Mpinga Cup 2016 iliyofanyika kwenye uwanja wa Tabata Shule, juzi.(Picha na Traffic Makao Makuu).


PC Abdallah Ismail, Kitengo cha Elimu kutoka Traffic Makao Makuu, akitoa elimu ya usalama bararani kwa wachezaji kabla ya kuingia Uwanjani wakati wa mashindano ya kombe la Mpinga Cup 2016 yanayoshirikisha waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda, iliyofanyika kwenye uwanja wa Tabata Shule, juzi.(Picha na Traffic Makao Makuu).
Mwenyekiti wa chama cha waendesha pikipiki kutoka mkoa wa Kipolisi Ilala, Mademla Bang’ala, akifafanua jambo kabla ya michezo hiyo kwenye michezo ya kundi (E) timu za waendesha pikipiki maarufu kwa jina la bodaboda, wakati wa mashindano ya kombe la Mpinga Cup 2016 iliyofanyika kwenye uwanja wa Tabata Shule, juzi.(Picha na Traffic Makao Makuu).


Na: Uswege John Mwaisemba

Kamanda wa Polisi Kikosi cha usalama barabarani Tanzania, Mohammed Ramadhani Mpinga, Juzi alikuwa ni miongoni mwa Wakufunzi wa kutoa elimu ya Masuala ya Usalama Barabarani wakati wa mashindano ya Mpinga Cup 2016 yanayohusisha madereva wa Pikipiki na bajaji kwa mkoa wa Kipolisi wa Ilala jijini Dar es Salaam katika mfululizo wa michezo hiyo inayoendelea katika viwanja mbalimbali.

Katika mashindano hayo jumla ya timu 59 tayari zimefanikiwa kusonga mbele hatua ya pili ya mtoano wa mashindano haya ambayo mwishoni mwa wiki timu zilizocheza zilikuwa ni pamoja na Matunda fc dhidi ya Zahanati ambapo mashindi alikuwa ni zahanati ,alipatikana kwa njia ya penalt 5-4, wafungaji kwa upande wa Zahanati wakiwa ni Fredy Chambogo, Isaac Elisha, Musa Masho, Shiiko Rashifod , na mfungaji wa timu ya Matunda walikuwa ni Shaaban Awami, Kelvin Sweetbati, Salum MWaikimba, Yusuph Mohamed.

mchezo wa pili ulikuwa ni Kwa bibi fc aliyecheza na Chama fc na Mshindi alikuwa ni Chama Fc kwa jumla ya 1-0, mfungaji akiwa Amani kadodo dakika ya 18 kipindi cha kwanza, mchezo wa tatu ulizikutanisha timu za Tabata Bodaboda na Tabata Old Trafford na mshindi alikuwa ni timu ya Tabata Bodaboda kwa jumla ya mabao 3-1 wafungaji kwa upande wa Traffod walikuwa Abdallah Hussen dk 27 kipindi cha kwanza, Miraji Sarehe dk 36 kipindi cha kwanza na goli la tatu liliwekwa kimiani na Saidi Ngwira katika dakika za majeruhi.

Mchezo mwingine ulikuwa ni kati ya Barakuda Kilimanjaro na Barakuda Fc ambapo mshindi alikuwa ni timu ya Barakuda Kilimanjaro kwa ushindi wa mezani baada ya wapinzani kushindwa kutokea uwanjani. Na mchezo uliofuata ulikuwa ni kati ya timu ya Liwiti fc dhidi ya Luwi Safari fc ambapo mchindi alikuwa ni timu ya Liwiti fc waliopata ushindi wa chee baada ya wapinzani kushindwa kutokea uwanjani.

Timu zilizofuatia katika ku hiyo ya jumamosi ilikuwa ni kati ya Kinyerezi Saloon waliocheza na Mbuyuni Fc ambapo matokeo katika mchezo huo timu ya mbuyuni waliibuka kidedea kwa ushindi wa bao 1-0 mfungaji akiwa Kitenge Kitenge aliyefunga dakika ya 16 kipindi cha kwanza na mchezo uliofuata ulizikutanisha timu za Segerea SBG dhidi ya timu ya Segerea Sheli Bodaboda na matokeo katika mchezo huo timu ya Segerea Sheli Bodaboda waliibuka mshindi wa 1-0 mfungaji akiwa Jackson Hamadi dakika 25 kipindi cha pili.

Mashindano hayo yaliendelea tena siku ya jumapili ambapo jumla ya timu kumi na mbili zilishiriki kuwania nafasi ya kusonga mbele na mchezo wa kwanza ulikuwa ni kati ya Transpoter Fc iliyocheza na Kecha Fc na Timu ya Kecha ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 mfungaji katika mchezo huo akiwa ni Mashaka Hamisi aliyefunga kwa shuti kali dakika 18 ya kipindi cha ili, huku ukifuatiwa na mchezo kati ya White Egle fc dhidi ya timu ya Migombani Fc ambapo mchezo huo timu ya White Egle iliibuka na ushindi wa mabao 8-7 baada ya kupigiana penalt kutokana na timu hizo kushindwa kutambiana kwenye dakika 90 za mchezo baada ya kumaliza zikiwa zimefungana bao 1-1.

Wafungaji kwa timu ya White Egle walikuwa ni Selemani Uswege, Elick Fod, Muso Uswege, Zuberi Hassani, Jofu Tito, Erick Sabuni, wafungaji kwa upanda timu ya Migombani walikuwa ni Shaaban Hamisi, Juma Abdalah, Erick Ndidi, Sifaeli Haule, Patrick Esau, Hamadi Msuyale na Dua Juma.


Akizungumzia mashindano hayo Mratibu wa mashindano ASP Mbuja Saidi Matibu alisema kuwa, mpaka sasa mashindano hayo yanaendelea vizuri na amewapongeza viongozi wa tmu kwa kuweza kufika kwa wakati kwenye michezo yao na kwamba timu zote zimeshiriki na kukubali matokeo kwa timu zote zilizofungwa, na pia wachezaji wamekuwa na hamasa ya hali ya juu na kuomba mashindano haya kuwa endelevu, ili kuwafikia bodaboda kwa wingi ikiwezekana iwe kwa nchi nzima.

Nae Mwenyekiti wa bodaboda mkoa wa Kipolisi Ilala, Mademla Bang’ala alisema kuwa, wanamshukuru kamanda wa Polisi kikosi cha usalama barabarani kwa niaba ya Jeshi la Polisi kwa kuwapa changamoto madereva wa bodaboda kwa kujenga afya zao kwa njia hiyo ya michezo na kuwapa elimu ya Usalama barabarani ili kuepukana na ajali za mara kwa mara, na kwamba wanaomba mashindano haya yasiishie tu mkoa wa Dar es salaam na badala yake yapelekwe kwenye Mikoa yote ya Tanzania.

Mchezo mwingine ulikuwa ni Buguruni sheli fc Bodaboda waliocheza na timu ya Buguruni Sheli Bajaji mshindi katika mchezo huo alikuwa ni timu Buguruni Sheli bajaji kwa jumla ya mabao 3-1,wafungaji kwa upande wa timu ya bodaboda ni Willy Pashau na kwa upande wa Bajaji wafungaji ni Abdul Ismail, moshi Shilingi, na Chrispofe Chibondo, mchezo mwingine uliofuata siku ya jumapili ulikuwa ni kati ya timu Segerea Mangala Fc waliocheza na timu ya Sanene fc na mshindi alikuwa ni timu ya Segerea Mangala fc kwa njia ya matuta 3-1 wafungaji kwa uande wa Segerea mangala ni Abeid Musa, Amani Saidi, Mbonde Ashilafu, baada ya kumaliza dakika 90 timu hizo zikiwa zimefungana bao 1-1, hivyo kufanya matokeo ya jumla kuwa mabao 4-2 na wafungaji kwa upande wa timu ya Sanene fc walikuwa ni Samba John na Mrisho Issa.

Wakati huo huo Afisa habari Msaidizi wa timu za bodaboda Tito Razalo Mpiziwa amemshukuru kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama barabarani kwa kuweza kufanikisha mashindano haya, ambayo kwa muonekano tayari ni zaidi ya bodaboda 6000 wa mkoa wa Dar es salaam walioweza kunufaika na mashindano haya kutokana na kupata mafunzo ya elimu ya usalama barabarani.

Mchezo mwingine ulizikutanisha timu za Kwetu pazuri fc na Segerea Kona Fc ambapo mshindi alikuwa ni timu ya Kwetu Pazuri waliopata ushindi wa mezani baada ya wapinzani wao kushindwa kutokea uwanjani , na mchezo uliofuata ulikuwa ni kati ya Pelalela fc waliocheza na timu ya Relini kwa Mnyamani na mshindi alikuwa ni Timu ya Relini kwa Mnyamani waliopata ushidi wa bure.



Mashindano haya yanadhaminiwa na Baraza la Usalama Barabarani(T), Jeshi la Polisi Tanzania, Cool Blue Tanzania, NMB, Zantel, Reb Bull, Windhoeck, Coc cola, Haki Elimu, Star Times, EFM Radio, Michuzi Blogs, NHIF, BIG BON, GSM, T-Marc Tanzania, Bavaria, Chai Bora, Dar City Promotions, Yono, Mwananchi Communications, Quality Group, Puma, TBL, Milcom, My Way Entertainments, Balozi wa Demokrasia Tanzania, Miss Demokrasia Tanzania, na MpaluleBlogs.

TASWIRA MBALIMBALI BUNGENI LEO,MJINI DODOMA

0
0
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson akiongoza sala wakati wa ufunguzi wa kikao cha Bunge leo Mjini Dodoma.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo akijibu wakati wa kikao cha bunge ambapo alisema serikali ipo katika uhakiki wa maombi ya maeneo mapya utawala kwa kuangalia vigezo katika kuanzisha maeneo hayo.
Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Mhe. Prof. Joyce  Ndalichako akijibu wakati wa kikao cha bunge ambapo alisema serikali serikali itaendelea kuongeza udahili wa walimu wa sayansi katika vyuo vya elimu ili kuweza kukidhi mahitaji husika.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo (kushoto) akimueleza jambo Waziri Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Mhe. George Simbachawene.
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akijibu wakati wa kikao cha bunge ambapo aliwaeleza wabunge kuwa Katiba ya Nchi ibara ya 3(2) inaeleza kuwa mambo yote yanayohusu uandikishaji na uendeshaji wa vyama vya siasa nchini yatasimamiswa kwa mujibu wa masharti ya katiba na sheria iliyotungwa ba Bunge
Waziri Wizara ya Mmabo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu Nchemba akijibu wakati wa kikao cha bunge ambapo alisisitiza watanzania kufuata sheria za nchi na iwapo utakiuka jeshi la polisi litachukuwa hatua bila kujali itikadi ya chama chochote cha siasa.
Mbunge wa Jimbo la Tarime Vijini Mhe. John Heche akichangia hoja kuhusu tetemeko la ardhi mkoani Kagera wakati wa kikao cha Bunge leo Mjini Dodoma.
Mbunge wa Jimbo la Muleba Kusini Mhe. Prof. Anna Tibaijuka akichangia hoja kuhusu tetemeko la ardhi mkoani Kagera wakati wa kikao cha Bunge leo Mjini Dodoma ambapo mbali na mambo mengine wabunge wamekubaliana kuchangia posho ya siku moja kwa ajili ya wahanga wa tetemeko mkoani Kagera.
Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakisimama kwa dakika moja kuungana na wahanga wa tetemeko lililotokea mkoani Kagera.
Waziri Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Mhe. George Simbachawene akitoa taarifa ya serikali kuhusu tetemeko la ardhi lililotokea hivi karibuni Mkoani Kagera. PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO

MeTL Group yazindua kampeni ya “USIKATE TAMAA" jijini Dar leo.

0
0
     
Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL Group, Fatema Dewji akifafanua zaidi kuhusu kampeni ya USIKATE TAMAA,jijini Dar leo .
 Mwanamuziki, Nurdin Bilal Ali maarufu kama Shetta akielezea safari yake ya muziki hadi kufika hatua aliyopo sasa, ambayo  binafsi amekiri kuwa kwake ni mafanikio makubwa. Kulia ni Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL Group, Fatema Dewji.
Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL Group, Fatema Dewji akizungumza kuhusu kampeni ya USIKATE TAMAA, Kushoto ni mwanamuziki Shetta na kulia na Kaimu Meneja Masoko wa Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group), Zainul Mzige.PICHA NA MICHUZI JR.

 kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group) leo imefanya uzinduzi wa kampeni ambayo imepewa jina la USIKATE TAMAA ikiwa na lengo la kuhamasisha watu waliokata tamaa kuwa nao wana nafasi ya kufanikiwa.

Akizungumzia kampeni hiyo, Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL Group, Fatema Dewji alisema kuwa kampeni hiyo inalenga kuleta matumaini mapya katika jamii kwa watu ambao wamekuwa wakipoteza matumaini kutokana na hali ya ugumu wa kimaisha ambayo imekuwa ikiwakabili.

Alisema kampeni hiyo itakuwa ikitumia watu mbalimbali ambao wamefanikiwa na watakuwa wakitoa historia zao katika maeneo mbalimbali ambayo watatembelea, wakielezea jinsi walivyokuwa na maisha magumu hapo awali na sasa wamefanikiwa kimaisha.


“Kuna watu hawana uwezo na wanazungukwa na watu ambao wamekuwa wakiwaambia kuwa hawawezi kufanikiwa lakini kupitia kampeni ya USIKATE TAMAA wataweza kupata matumaini kutoka kwa watu ambao walipita katika maisha magumu na baadae wakafanya vyema,” alisema Fatema.

Mkurugenzi wa masoko huyo aliongeza kuwa kampuni ya MeTL pamoja na kufanya biashara lakini pia inaijali jamii na inapenda kuona watu wakifanikiwa kimaisha hivyo kupitia kampeni ya USIKATE TAMAA itaweza kusaidia watu wa aina mbalimbali waliopo katika jamii ya kitanzania wakipata matumaini mapya na kuongeza juhudi ili wafanikiwe.


“MeTL kupitia chapa yake ya MO inataka kuona watu wakiendelea kupambana na kufanikiwa, tunataka watu wafanikiwe na tuwape tuzo, tuwape sauti ya kusikika na huu ni mwanzo tu, kampeni hii itafanyika kwa muda mrefu zaidi,” alisema Fatema.

Kwa upande wa mwanamuziki, Nurdin Bilal Ali (Shetta) ambaye ametumika kama mmoja wa watu ambao wamefanikiwa, alielezea safari yake ya kimuziki na kusema kuwa awali alikuwa akiishi kwa moja ya wasanii wa muziki nchini na alikuwa akifanya kazi za nyumbani kwa mtu huyo lakini akiwa na nia ya kutafuta njia ya kutoka kimuziki na juhudi alizozionyesha zimemwezesha kuwa moja ya wasanii waliofanikiwa nchini.


“Unaweza kuwa unajiamini katika kipaji chako lakini bado watu wanakudharau, mimi nimewahi kuishi na mwanamuziki mkubwa nchini lakini najijua nina kipaji lakini kwakuwa nilikuwa natafuta njia ya kutoka kimuziki ilinibidi nifanye hivyo,“Ilikuwa naosha gari lake, naosha vyombo na hata kumwogesha mdogo wake lakini nilikuwa najua nini nafanya na nini nataka, msanii yule alikuwa anafahamiana na watu wengi na mimi ikanisaidia kupata njia ya kutokea na leo kwa hatua niliyofikia nimefanikiwa,” alisema Shetta.

CHAMA CHA WAFUGAJI NCHINI CHATOA TAMKO KUFUATIA CHANGAMOTO KUBWA ZINAZOWAKABILI

0
0
Mkuu wa Chama cha Wafugaji Tanzania (pichani kati),Magembe Makoye akizungumza mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) mapema leo jijini Dar kuhusiana na mambo mbalimbali yanayowakabili wafugaji hapa nchini,kushoto ni Mfugaji kutoka Suwambawaga,Mayunga Gamas na kulia ni Charles Mtokambati.

Bwa.Maghembe Makoye alieleza changamoto mbalimbali zinazowakabili wafugaji hao kuwa ni Ukosefu wa Maeneo rasmi ya malisho,Migogoro Baina ya Wakulima na Wafugaji,Migogoro kati ya Wafugaji na Idara ya Maliasili na Wanyamapori.Akaeleza kuwa kwa sasa kuna Mgogoro mkubwa kati ya Idara za Maliasili na Wanyamapori ndani ya Wizara ya maliasili na utalii na Wafugaji,akafafanua kuwa changamoto hizo zimekuwa sugu kutokana na kupanuka kwa maeneo ya Maliasili na kuchukua maeneo ya Wafugaji.

"Wafugaji wamekua wakifukuzwa kutoka kwenye maeneo hayo ambayo hapo awali walikuwa wakiyatumia kwa malisho,baada ya kuchukuliwa na maliasili na kuwa sehemu ya maeneo yaliyohifadhiwa.
Mkuu wa Chama cha Wafugaji Tanzania (pichani kati),Magembe Makoye akionesha baadhi ya Nyaraka kwa waandishi wa habari,zinazoeleza kukamatwa kwa ng'ombe za wafugaji hao zaidi ya elfu moja na Wizara ya Maliasili na Utalii,ambapo mahakama iliamua kuwa Maliasili na Utalii irejeshe Ng'ombe hao kwa wafugaji,ambapo mpaka sasa kwa mujibu wa taarifa ya wafugaji hao hakuna kilichofanyika mpaka sasa

WAHITIMU WA MRADI WA UWEZESHAJI VIJANA KIUCHUMI WAIOMBA SERIKALI KUWAKUMBUKA KATIKA AJIRA.

0
0
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO, Kibaha.
VIJANA waishio katika mazingira magumu waliohitimu Chuo cha Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) Pwani, chini ya Mradi wa kuwawezesha Vijana Kiuchumi (YEE) unaoratibiwa na Shirika la Plan International wameiomba Serikali kuwapatia ajira ili waweze kumudu maisha yao.

Hayo yamesemwa leo wilayani Kibaha na mmoja wa wahitimu wa mradi huo, Rajabu Kilanga alipokuwa akiongea na mwandishi wa habari hii juu ya mafanikio na changamoto anazozipata baada ya kuhitimu mafunzo hayo.

Kilanga amesema kuwa mradi huo umemuwezesha kufahamu jinsi ya kuhifadhi fedha kwa ajili ya maisha ya baadaye pia umemnufaisha yeye pamoja na familia yake kwani kupitia fani ya umeme aliyoisomea ameweza kupata tenda ndogo ndogo ambazo zinamsaidia kuyaendesha maisha yake.
“Pamoja na faida nyingi nilizozipata kupitia mradi huu lakini ukosefu wa ajira za kudumu ni moja ya changamoto ambazo zinatukabili vijana tuliohitimu mafunzo haya hivyo, tunaiomba Serikali itusaidie kutupatia ajira ili na sisi tuweze kutimiza malengo yetu na kuchangia katika kulijenga Taifa letu”, alisema Kilanga.

Kilanga ameishukuru EU na Shirika la Plan International pamoja na wadau wengine kwa kuratibu mradi huo kwani baada ya vijana wengi kuhitimu na kuweza kujiajiri na kupata vipato kupitia mafunzo waliyoyapata chini ya mradi huo wameweza kujikwamua kutoka kwenye hatua moja ya maendeleo kwenda nyingine.

Naye muhitimu mwingine kupitia mradi huo, Simba Musa ametoa wito kwa vijana wenzie kujituma na kufanya kazi kwa bidii kwani kwa kufanya hivyo wananchi wataona kazi zao hivyo kuwapelekea kupata ajira kwa urahisi.

“Nawashauri vijana wenzangu tujishughulishe, hata kama Mhe. Rais akitoa fedha hawezi kukuletea nyumbani kwa hiyo, kila mmoja kwa nafasi yake ajitume ili watu wazione kazi zake”, alisema Musa.
Aidha, ameyataja baadhi ya malengo yake yakiwemo ya kufungua duka la vifaa vya umeme pamoja na kuwafundisha vijana wenzie bila kuwatoza gharama yoyote ili nao waweze kujipatia kipato kupitia ujuzi watakaoupata.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji wa Kata ya Visigo, wilayani Kibaha, Aloisia Nyelo amesema kuwa mradi huo umewasaidia vijana kutozagaa hovyo mitaani kwani wameunda vikundi vinavyosimamiwa na watendaji wa Kata hiyo kwa ajili ya kuwapa ushauri hivyo kuwafanya wawe na adabu na heshima.

Nyelo ameongeza kuwa Kata hiyo iko mstari wa mbele katika kuwasaidia vijana kupata tenda mbalimbali kwa kuwabandikia matangazo nje ya ofisi yao na kuwataka wananchi wanaohitaji wafanyakazi kusaini mkataba na vijana husika mbele ya Afisa Mtendaji ili kuhakikisha wanafanya kazi kwa uhakika na wanalipwa fedha zao kama walivyokubaliana.

Mtendaji huyo alitumia fursa hiyo kuto rai kwa wananchi kuwaamini na kuwasaidia vijana hao kwa kuwapa tenda mbalimbali zinazolingana na fani walizosomea kwani wana ujuzi wa kutosha kufanya kazi hizo katika kiwango kinachotakiwa.
Mmoja wa wahitimu wa mafunzo ya ufundi chini ya mradi wa Uwezeshaji wa Vijana Kiuchumi (YEE) unaofadhiliwa na Umoja wa Nchi za Ulaya na kuratibiwa na Shirika la Plan International, Rajabu Kilanga (chini) akimshikilia kijana mwenzie George Geligoali (juu) wakati wakiendelea na kazi za kuunganisha umeme kwenye nyumba.
 Afisa Mtendaji wa Kata ya Visigo, wilayani Kibaha, Mkoa wa Pwani Aloisia Nyelo, akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mchango wa kata hiyo juu ya kuwasaidia vijana waliosomeshwa chini ya mradi wa Uwezeshaji wa Vijana Kiuchumi (YEE) kupata ajira.

Muhimbili Yapeleka Wataalamu 20 Nje Kujifunza Upandikizaji Figo.

0
0

  Mkuu wa Idara ya Urolojia katika hospitali hiyo, Dk Ryuba Nyamsogoro akizungumza na wenzake kabla ya kuondoka nchini.
  Wataalamu wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) wakiwa wamewasili nchini India kwa ajili ya kujengewa uwezo wa kupandikiza figo kwa wagonjwa wenye matatizo ya figo. Wataalamu hao watakuwapo India kwa muda miezi mitatu na watarejea nchini Desemba 10, mwaka huu.
 Mkurugenzi wa Tiba katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dk. Hedwiga Swai akizungumza baada ya wataalamu hao kwenda India kwa ajili ya kujengewa uwezo wa upasuaji na upandikizaji figo.
 Mkuu wa Idara ya Urolojia katika hospitali hiyo, Dk Ryuba Nyamsogoro akizungumza na wataalamu wenzake kabla ya kuanza kwa safari ya kuelekea India.
 Baadhi ya wataalamu wakimsikiliza Mkuu wa Idara ya Urolojia katika hospitali hiyo, Dk Ryuba Nyamsogoro wakati akitoa maelezo kabla ya kuanza safari ya kuelekea India wiki iliyopita.
Picha na John Stephen, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)

Na John Stephen, MNH.
Dar es Salaam, Tanzania.  Wataalamu 20 wa fani mbalimbali wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) wameondoka nchini kwenda India kwa ajili ya kujengewa uwezo wa upandikizaji figo kwa watu wenye matatizo ya figo.

Wataalamu hao wameondoka wiki iliyopita na wakiwa huko watajengewa uwezo wa kufanya upasuaji na upandikizaji figo kwa wagonjwa wenye matatizo ya figo.

Mkurugenzi wa Tiba, Dk. Hedwiga Swai amesema leo kwamba wataalamu mbalimbali wakiwamo madaktari bingwa wa upasuaji na upandikizaji figo, madaktari bingwa wa magonjwa ya figo, wataalamu wa maabara, madaktari wa usingizi na madaktari wa chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu.

Wengine ni wataalamu wa mionzi, wauguzi wa chumba cha upasuaji na chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu na wataalamu wengine ambao wanakwenda kujifunza. 

“Suala la mgonjwa kupandikizwa figo ni mchakato na haliwezekani kufanywa na mtaalamu mmoja.Ni kazi inayowahusisha wataalamu wengi,” amesema Dk. Swai.
Pia, Dk. Swai amesema upandikizaji figo utapunguza rufaa za wagonjwa kwenda nje ya nchi kwa ajili ya kupatiwa matibabu na kuokoa fedha nyingi za serikali za kuwapeleka nje ya nchi.

Amesema kwamba wataalamu hao watakaa nje ya nchi kwa muda wa miezi mitatu na watarejea nchini Desemba 10, 2016.

“Shughuli za upasuaji na upandikizaji figo zitaanza Januari mwakani,” amesema Dk. Swai.

MAKAMU WA RAIS MHE SAMIA SULUHU HASSAN KATIKA SHEREHE ZA KUAPISHWA RAIS WA 6 WA ZAMBIA MHE EDGAR LUNGU MJINI LUSAKA

0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan akiwasili kwenye uwanja wa Taifa wa Mashujaa (National Heroes Stadium) jijini Lusaka kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwenye sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Awamu ya 6 wa Zambia Mhe Edgar C. Lungu leo Septemba 13, 2016 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan akipungia mkono maelfu ya wananchi waliokuwa wakimshingilia wakati akiingia  kwenye uwanja wa Taifa wa Mashujaa (National Heroes Stadium) jijini Lusaka kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwenye sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Awamu ya 6 wa Zambia Mhe Edgar C. Lungu leo Septemba 13, 2016
 Rais Robert Mugabe akisalimiana na Rais wa Kwanza wa Zambia Dkt Kenneth Kaunda
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Rais wa Botswana Luteni Jenerali Seretse Khama baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Taifa wa Mashujaa (National Heroes Stadium) jijini Lusaka kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwenye sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Awamu ya 6 wa Zambia Mhe Edgar C. Lungu leo Septemba 13, 2016
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan akiwa na Naibu Rais wa Kenya Mhe william Rutto,  Makamu wa Rais wa Namibia Mhe. Nickey Iyambo na Rais wa kwanza wa Zambia Dkt. Kenneth Kaunda baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Taifa wa Mashujaa (National Heroes Stadium) jijini Lusaka kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwenye sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Awamu ya 6 wa Zambia Mhe Edgar C. Lungu leo Septemba 13, 2016
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan akiwa na Naibu Rais wa Kenya Mhe william Ruttona wageni wengine wakielekea jukwaani  kwenye uwanja wa Taifa wa Mashujaa (National Heroes Stadium) jijini Lusaka ambako amemuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwenye sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Awamu ya 6 wa Zambia Mhe Edgar C. Lungu leo Septemba 13, 2016
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan akipitia ratiba kwenye uwanja wa Taifa wa Mashujaa (National Heroes Stadium) jijini Lusaka ambako kamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwenye sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Awamu ya 6 wa Zambia Mhe Edgar C. Lungu leo Septemba 13, 2016
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan na viongozi wengine wakiwa kwenye uwanja wa Taifa wa Mashujaa (National Heroes Stadium) jijini Lusaka ambako kamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwenye sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Awamu ya 6 wa Zambia Mhe Edgar C. Lungu leo Septemba 13, 2016
 Rais mteule wa Zambia Mhe Edgar C. Lungu akiwasili kwenye uwanja wa Taifa wa Mashujaa (National Heroes Stadium) jijini Lusaka kwenye sherehe za kuapishwa kwake kuwa Rais wa Awamu ya 6 wa Zambia Mhe Edgar C. Lungu leo Septemba 13, 2016
 Rais mteule wa Zambia Mhe Edgar C. Lungu akipokea heshima ya mizinga 21  kwenye uwanja wa Taifa wa Mashujaa (National Heroes Stadium) jijini Lusaka kwenye sherehe za kuapishwa kwake kuwa Rais wa Awamu ya 6 wa Zambia Mhe Edgar C. Lungu leo Septemba 13, 2016
 Rais mteule wa Zambia Mhe Edgar C. Lungu akiwa na mkewa Mama Esther Lungu kwenye uwanja wa Taifa wa Mashujaa (National Heroes Stadium) jijini Lusaka kwenye sherehe za kuapishwa kwake kuwa Rais wa Awamu ya 6 wa Zambia Mhe Edgar C. Lungu leo Septemba 13, 2016
 Rais mteule wa Zambia Mhe Edgar C. Lungu akila kiapo kwenye uwanja wa Taifa wa Mashujaa (National Heroes Stadium) jijini Lusaka kwenye sherehe za kuapishwa kwake kuwa Rais wa Awamu ya 6 wa Zambia leo Septemba 13, 2016
 Taswira ya Makamu wa Rais  wa Zambia Mama Inonge Mutukwa Wina akila kiapo ikionekana kqwenye luninga kubwa kwenyeUwanja wa Taifa wa Mashujaa jijini Lusaka  leo Septemba 13, 2016
 Rais Robert Mugabe wa Zambia akizungumza kwa niaba ya viongozi waalikwa wote
 Ndege vita zikipita angani
 Rais Edgar C. Lungu akielekea kukagua gwaride la heshima baada ya kula kiapo
 Rais Edgar C. Lungu akikagua gwaride la heshima baada ya kula kiapo
 Rais Edgar C. Lungu akielekea jukwa kuu baada ya kukagua gwaride la heshima 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan na viongozi walikwa wengine kwenye  sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Awamu ya 6 wa Zambia Mhe Edgar C. Lungu leo Septemba 13, 2016
 Ndege vita zikipamba sherehe angani
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan akimpongeza Makamu wa Rais  wa Zambia Mama Inonge Mutukwa Wina kwenye sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Awamu ya 6 wa Zambia Mhe Edgar C. Lungu leo Septemba 13, 2016
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan na viongozi wengine wakisimama na kushiriki dua kwenye uwanja wa Taifa wa Mashujaa (National Heroes Stadium) jijini Lusaka baada ya shughuli za kuapishwa Rais Lungu.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan akinong'onezwa jambo na Katibu Mkuu Wizara ya Vijana, Michezo na Maendeleo ya watoto Mhe. Agnes Musunga baada ya sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Awamu ya 6 wa Zambia Mhe Edgar C. Lungu leo Septemba 13, 2016
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan akiongea na mwandhi wa habari wa ZNBC baada ya sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Awamu ya 6 wa Zambia Mhe Edgar C. Lungu leo Septemba 13, 2016. PICHA NA IKULU

WABUNGE WAFURAHISHWA NA KASI YA NIDA KATIKA UTOAJI VITAMBULISHO VYA TAIFA

0
0
Mbunge wa Igunga Dkt. Dalaly Peter Kafumu akiwa amejawa na furaha baada ya kupokea Kitambulisho chake kipya chenye saini Kinachotolewa na NIDA katika zoezi la ugawaji wa vitambulisho hivyo kwa waheshimiwa Wabunge, Bungeni Dodoma.
kaf2
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mbunge wa Iramba Magharibi Mheshimiwa Mwigulu Nchemba; akiweka saini katika orodha ya majina ya wabunge baada ya kupokea Kitambulisho chake kipya chenye saini Bungeni Dodoma. Kushoto ni Afisa wa Mifumo ya Kompyuta NIDA Bi. Zainabu Mavere.
kaf3
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mbunge wa Iramba Magharibi Mhe. Mwigulu Nchemba akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Hifadhi Hati NIDA; Bi. Rose Mdami mara baada ya kupokea kitambulisho chake cha Taifa.
kaf4
Mhe. Azzan Mussa Zungu Mbunge wa Jimbo la Ilala (wapili kulia) mara baada ya kuchukua kitambulisho chake chenye saini Bungeni Dodoma. Kulia ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Hifadhi Hati Bi. Rose Mdami, kushoto ni Afisa Usajili NIDA Bw. Thadei Minja na wa pili kushoto ni Afisi Usajili wa Wilaya ya Dodoma Mjini Bwana Khalid Mrisho.
kaf5
Mbunge wa Singida Magharibi Mh. Elibariki Emmanuel Kingu akiwa mwenye furaha baada ya kuchukua Kitambulisho chake chenye saini leo bungeni Dodoma, ambapo NIDA imeanza kugawa vitambulisho vyenye saini kwa waheshimiwa Wabunge. Kushoto ni Afisa Usijili Wilaya ya Dodoma Mjini Bw. Khalid Mrisho.
kaf6
Mh. Seif Khamis Said Gulamali Mbunge wa Jimbo la Manonga kwa furaha akionyesha kitambulisho chake kipya chenye saini baada ya kupokea kutoka kwa Afisa Usajili wa NIDA wilayani Dodoma Mjini Bwana Khalid Mrisho Bungeni Dodoma.
kaf7
Afisa wa Jeshi la Polisi, akithibitisha kupokea kitambulisho chake kwa kuweka saini kwenye daftari maalumu la kumbukumbu, baada ya kuchukua Kitambulisho chake leo bungeni Dodoma. Zoezi la ugawaji wa Vitambulisho vyenye saini limeanza katika ofisi za
……………………………………………………
Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo wamekuwa miongoni mwa wananchi walioanza kuchukua Vitambulisho vipya vya Taifa vyenye saini; kufuatia utaratibu uliotangazwa hivi karibuni na Nida wa kuanza kugawa vitambulisho vipya kwa makundi mbalimbali waliokamilisha taratibu za usajili .

            Shughuli ya kugawa Vitambulisho vya Taifa kwa Waheshimiwa Wabunge imeanza rasmi leo bungeni; pamoja na kuendelea kuwasajili wabunge ambao kwa sababu moja au nyingine hawakusajiliwa wakati wa zoezi la awali la usajili.

            Mbali na waheshimiwa Wabunge; wengine ni wafanyakazi wa Bunge na watumishi katika taasisi na Wizara mbalimbali ambao walisajiliwa katika utaratibu wa kawaida wa Usajili. Zaidi ya waheshimiwa Wabunge 240 wanakusudiwa kupatiwa vitambulisho vyao.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA APOKEA MICHANGO ZAIDI YA BILIONI 1.4 KWA AJILI YA WAATHIRIKA WA TETEMEKO LA ARDHI

0
0

Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akizungumza na Wafanyabishara na Mabalozi wa Nchi Mbalimbali hapa nchini kuwaomba wachangie katika kujenga na kukarabati miundombinu iliyoharibiwa na tetemeko la ardhi mkoani Kagera.Alikutana nao Ikulu jijini Dar es salaam Septemba 13, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepokea michango wa zaidi ya sh. bilioni 1.4 kutoka kwa mabalozi wa nchi za nje nchini Tanzania na Jumuia ya Wafanyabiashara wa Kitanzania kwa ajili ya kusaidia wananchi waliothirika na tetemeko la ardhi lililotokea Mkoani Kagera.

Tetemeko hilo lilitokea Jumamosi, 10 Septemba, 2016 na kusababisha vifo vya watu 17 hadi leo na wengine 253 kujeruhiwa. Pia limesababisha maelfu ya wananchi kukosa makazi baada ya nyumba 840 kuanguka na nyingine 1,264 zikipata nyufa yakiwemo majengo 44 ya taasisi mbalimbali za umma.

Akizungumza katika hafla ya uchangishaji fedha kwa ajili ya kusaidia wahanga hao leo (Jumanne, 13 Septemba, 2016) Waziri Mkuu amewashukuru kwa michango yao ya fedha na vifaa vya ujenzi ikiwemo mifuko 2,800 ya saruji. Amesema tetemeko hilo ni kubwa na halijawahi kutokea nchini.

Amesema tetemeko hilo limesababisha Serikali kuzifunga shule zake mbili za sekondari za Nyakato na Ihungo kati ya nne zilizoathirika vibaya na tetemeko hilo.

“Serikali itajitahidi kuhakikisha inarejesha miundombini iliyoharibiwa na tetemeko hilo katika kipindi kifupi ili wanafunzi na wananchi wengine waweze kuendelea na shughuli zao za kawaida,” amesema.

Waziri Mkuu amesema katika kuhakikisha suala hilo linashughulikiwa haraka tayari Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Muhagama yuko mkoani Kagera akiongoza kitengo cha maafa kufanya thamnili kujua athari zilizosababishwa na tetemeko hilo.

Mawaziri wengine walioko mkoani Kagera wakiendelea kufanya tathmini hiyo ni pamoja na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako.

Amesema Kamati ya Maafa ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na Kamati ya Maafa ya mkoa wa Kagera imefungua akaunti maalumu katika benki ya CRDB kwa ajili ya kupokea michango kutoka kwa watu mbalimbali. Namba za akaunti hiyo ya Kamati ya Maafa ya Kagera ni CRDB 0152225617300.

Pia Waziri Mkuu amewapongeza na kuwashukuru waheshimiwa Wabunge kwa kuamua kutoa posho zao za kikao cha leo kwa ajili ya kuchangia wahanga wa tetemeko hilo na kuwaomba wananchi wengine kujitokeza na kutoa michango yao.

Wakati huo huo viongozi wa makampuni ya mafuta ya GBP, Oil Com na Moil wameahidi kujenga shule mbili za Nyakato na Ihungo ambazo sehemu kubwa ya miundombinu yake imeharibika vibaya. Shule hizo zitajengwa katika kipindi cha siku 30.

Hafla hiyo iliyoongozwa na Waziri Mkuu ilihudhuriwa na Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Suzan Kolimba na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Balozi, Dk. Aziz Mlima.

Tshs. Bilioni 1.4 zachangwa na mabalozi, wafanyabiashara kusaidia waathirika wa tetemeko Kagera

0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea hundi ya shilingi milioni 100 kutoka kwa Charge d’ Affairs wa ubalozi wa China nchini, Bw. Haodong Gou wakati alipokutana na wafanyabiashara na mabalozi wa nchi mbalimbali hapa nchini na kuwaomba wasaidie kuchangia ujenzi na ukarabati wa miundombinu iliyoathiriwa na tetemeko laardhi mkoani Kagera. Mkutano huo ulifanyika Ikulu jijini Dar es salaam Septemba 13, 2016.Katikati ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Dkt. Suzan Kolimba. (Picha na Odisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akizungumza na Wafanyabishara na Mabalozi wa Nchi Mbalimbali hapa nchini kuwaomba wachangie katika kujenga na kukarabati miundombinu iliyoharibiwa na tetemeko la ardhi mkoani Kagera.Alikutana nao Ikulu jijini Dar es salaam Septemba 13, 2016.
Baadhi ya Mabalozi na Wafanyabiashara wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao , Ikulu jijini Dar es salaam Septemba 13, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya mabalozi na wafanyabiashara baada ya kukutana nao Ikulu jijini Dar es salaam Septeba 13, 2016 kuwaomba wachangie katika kujenga na kukarabati Miundombinu ilitoharibiwa na tetemeko la ardhi mkoani Kageza.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya mabalozi na wafanyabiashara baada ya kukutana nao Ikulu jijini Dar es salaam Septeba 13, 2016 kuwaomba wachangie katika kujenga na kukarabati Miundombinu ilitoharibiwa na tetemeko la ardhi mkoani Kageza.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya mabalozi na wafanyabiashara baada ya kukutana nao Ikulu jijini Dar es salaam Septeba 13, 2016 kuwaomba wachangie katika kujenga na kukarabati Miundombinu ilitoharibiwa na tetemeko la ardhi mkoani Kageza. (picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya mabalozi na wafanyabiashara baada ya kukutana nao Ikulu jijini Dar es salaam Septeba 13, 2016 kuwaomba wachangie katika kujenga na kukarabati Miundombinu ilitoharibiwa na tetemeko la ardhi mkoani Kageza. (picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya mabalozi na wafanyabiashara baada ya kukutana nao Ikulu jijini Dar es salaam Septeba 13, 2016 kuwaomba wachangie katika kujenga na kukarabati Miundombinu ilitoharibiwa na tetemeko la ardhi mkoani Kageza. (picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 

Na Sheila Simba, MAELEZO 

Jumla ya shilingi bilioni 1.4 zimechangwa na mabalozi na wafanyabiashara kwa ajili ya kusaidia waathirika wa tetemeko la ardhi lililotokea Mkoani Kagera. 

Michango hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam katika harambee iliyoongozwa na Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa na kufanyika Ikulu. Akizungumza katika harambee hiyo Waziri Mkuu alisema jumla ya nyumba 840 zimebomoka na kuharibika kabisa, wakati nyumba 1264 zimepata hitilafu na zinaweza kufanyiwa marekebisho ili watu waendelee kuishi katika nyumba hizo. 

Mhe. Majaliwa ameongeza kuwa shule 4 za sekondari ambazo ni Nyakato, Ihungo, Kashange na Buhembe zimeharibika na mbili kati ya hizo yaani Ihungo na Nyakato zimefungwa kutokana na kuharibika sana. 

Madhara mengine yaliyosababishwa na tetemeko hilo kwa mujibu wa Waziri Mkuu ni kuharibika kwa vituo vya afya, miundombinu ya barabara, umeme na njia za mawasiliano na kufanya athari za tetemeko kuwa kubwa. 

Kutokana na athari hizo Waziri Mkuu amewaomba mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini kusaidia waathirika kwani ni tukio ambalo halikutarajiwa na limeleta hasara kubwa kwa wanakagera na Taifa kwa ujumla. “Licha ya michango hii ninayowaomba leo, tutaandaa safari kwa anayehitaji kwenda kujionea hali halisi ili aone ni namna gani atakavyosaidia,”alisema Waziri Mkuu. 

Aidha, Mhe. Majaliwa amesema kuwa imefunguliwa akaunti ya kuchangia katika maafa hayo kwenye benki ya CRDB inayojulikana kama KAMATI MAAFA KAGERA akaunti namba 0152225617300 na swift code ambayo ni CORUtztz na kuwaomba wananchi na watu wengine kutumia akaunti hiyo kwa kusudi hilo. Majaliwa amesema pia kuwa utaratibu unaandaliwa ili kuwawezesha watu kuchangia kwa njia ya Mpesa, tigopesa na Airtelmoney. Utaratibu huo utakapokuwa tayari utatangazwa ili kuwarahisishia watumiaji wa mitandao hiyo kuchangia. 

Katika harambee hiyo wafanyabiashara waliochangia ni Mwenyeki Mtendaji wa kampuni za IPP Dkt Reginald Mengi aliyechangia Tsh million 110, Mohamed Dewji ametoa milioni 100, Subash Patel milioni 150 na Salim Turki aliyetoa mifuko 5000 ya saruji na mabati 3000. 

Wengine waliochangia ni kampuni mbali mbali zikiwemo kampuni ya bia ya Serengeti iliyotoa mifuko 800 ya saruji, Sahara Tanzania wametoa shilingi milioni 20, Camel Oil kupitia Camel Cement wametoa mifuko 1000 ya saruji ,Puma wamechangia shilingi million 50, Pepsi Cola wametoa milioni 50 na Azania Group wamechangia milioni 50. 

Baadhi ya mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini waliochangia ni pamoja na ubalozi wa China shilingi milioni 100 na kupeleka madaktari,dawa,mahema na vifaa vingine kwa ajili ya kusaidia waliopatwa na maafa hayo. Kuwait kupita ubalozi wao nchini wamechangi dola elfu 10 za Kimarekani na euro elfu 10, na Nchi ya Kenya iliyopeleka msaada wa mahema,magodoro na dawa. 

Wizara ya Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki wametoa milioni 10, mwakilishi wa China Merchantile Group ametoa milioni 100, Toyota Tanzania milioni 10, Kamal Group milioni 50, Urban Group milioni 20, TBL milioni 100, IPTL 50, Tanzania Agriculturak Processing Zone milioni 30, Umoja wa wafanya biashara ya mafuta ya rejereja milioni 250 na Group Six wametoa tani 80 za saruji. 

Wengine waliochangia ni pamoja Jambo plastic milioni 20, Tanga Cement mifuko 1000 ya saruji, Agusta Tz milioni 10, Oryx milioni 50, Kagera Sugar milioni 100 na tani 10 za sukari, Tipper milioni 20 ambapo GBP, Oilcom na Moil watajenga shule mbili zilizoharibika. 

Uchangiaji huo umejumuisha pia na watu binafsi ambao ni wakili wa kujitegemea, Bwana Protase Ishengoma milioni 5 na Melisa Kataraiya milioni 20. 

Tetemeko hilo la ardhi ni kubwa kuliko yote ambayo yamewahi kutokea hapa nchini na hadi sasa limesababisha vifo vya watu 17 na kuharibu nyumba, majengo na miundombinu mkoani Kagera.

MTU HUYU ANATAFUTWA KWA TUHUMA ZA UTAPELI

0
0



Wapendwa,


Kama kuna mtu ana taarifa za huyu mtu hapa juu, naomba atoe taarifa rasmi kwenye dawati la Detective Matt Vendemio, Montgomery County Maryland Police, Patrol Investigation Unit 4th District , 2300 Randolph Road
Wheaton, Maryland 20902 / 240-773-5500 (front desk).


Tunaomba msaada wenu, mjitokeze kwani hadi sasa ameshachukua pesa zaidi ya $50,000 toka kwa Watanzania wengi walioko Marekani na baadhi ya viongozi toka Tanzania. Tayari kuna Watanzania aliowatapeli wameshafungua mashitaka dhidi yake na uchunguzi unaendelea toka state mabalimbali hapa Marekani.


Jina lake la halali ni WILLBROD FRANK LUKAMILWA . Amekuwa anajitambulisha kwa watu kwa majina tofauti tofauti. Kwa sasa kuna records kuwa ameshajitambusha kwa wengi kama Padri John, Padri Frank, Doctor Frank wa Georgetown Hospital, Pediatrician wa The Children Place, Mwanafunzi wa PhD wa Catholic University, Steve, Frank. Frank Stockman na John. Pia amekuwa akitoa maelezo kuwa ni mtu wa nchi tofauti kama Senegal, South Africa, Kenya, Congo na Belgium wakati ni Mtanzania wa mkoa wa Kagera.

Ametumia maelezo ya watu na mitandao kupata pesa toka kwa watu wengi walioko nje na ndani ya USA. Namba za simu za mkononi ambazo ameshatumia siku za karibuni ni
202-446-7747 na 202-867-2691.

Wilbrod alishashikwa mwaka huu June kwa utapeli pia, na bado anaendelea.



Tunaomba ushirikiano wenu wa hali na mali, hata kuwagundua ndugu zake walioko Tanzania. Ni mwenyeji wa Bukoba, mkoa wa Kagera, Tanzania.


Huyu mtu ni hatari sana usimpe nafasi ya kuwasiliana na wewe kwani anatumia njia nyingi sana za utapeli (scamming schemes), tafadhali toa taarifa zako kama ni mmojawapo wa watu waliokwisha tapeliwa na huyu mtu.

WANAANCHI WAASWA KUWA WAVUMILIVU KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI

0
0
Beatrice Lyimo na Eleuteri Mangi- MAELEZO Dodoma.
13/09/2016
Wananchi wameaswa kuwa wavumilivu na kuendelea kushirikiana na Serikali wakati jitihada mbalimbali zikiendelea kuchukuliwa katika kukabiliana na athari za tetemeko la ardhi lililotokea Mkoani Kagera hivi karibuni.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (TAMISEMI) George Simbachawene alipokuwa akitoa kauli ya Serikali bungeni kuhusu Maafa yaliyosababishwa na tetemeko la ardhi lililotokea Mkoani Kagera siku ya jumamosi tarehe 10/09/2016.
Waziri Simbachawene amesema kuwa hadi leo tarehe 13/9/2016 idadi ya vifo vilivyosababishwa na tetemeko hilo katika Mkoa wa Kagera ni 17, ambapo majeruhi waliolazwa katika hospitali mbalimbali zilizoko Mkoani humo ni 169, majeruhi waliotibiwa na kuruhusiwa ni 83, nyumba za makazi zilizoanguka ni 840, nyumba za makazi zenye nyufa ni 1,264 pamoja na taasisi zilizoanguka na kupata nyufa ni 44.
Aidha, Waziri Simbachawene amesema kuwa mpaka sasa Serikali imechukua hatua za kuwaokoa watu na kuwapeleka hospitali kwa ajili ya matibabu na kuwapatia makazi ya muda baadhi ya wananchi ambao nyumba zao zimeathirika.
Pia Serikali inaendelea kutibu majeruhi bure na wenye Bima za Afya kutumia bima zao na kuongeza nguvu ya madaktari bingwa 15 kutoka mkoa ya Mwanza ili kuweza kutoa huduma ya haraka kwa wahanga hao.
Vilevile Waziri Simbachawene amesema kuwa Serikali imeelekeza wanajiolojia kuwatoa hofu wananchi kwa kutoa maelekezo ya kisayansi kuhusu hali hiyo na kuendelea kufanya tahimini ya athari zilizosababishwa na tetemeko hilo.
Hata hivyo Waziri Simbachawene amesema kuwa serikali imezifunga shule za sekondari Ihungo na Nyakato zilizopo mkoani humo kutokana na athari za tetemeko iliyopelekea kuharibika kwa miundombinu ikiwemo madarasa, vyoo, mabweni na maabara, wakati serikali ikiendelea na taratibu za kushughulikia tatizo hilo.
Waziri Simbachawene ameongeza kuwa Serikali inaendelea kuhakikisha kuwa hatua za dharura zinachukuliwa kwa kushirikiana na wadau wengine ili kuhakikisha ili kuwasaidia wahanga.
Mbali na hayo Mbunge wa Mlalo Mhe. Rashid Shangazi ametoa hoja juu ya wabunge kuchangia posho yao ya siku moja ili iweze kuwasaidia wahanga wa tetemeko hilo lililokadiriwa kuwa na ukubwa wa kiwango cha 5.7 katika vipimo vya Richter ambapo wabunge waliunga mkono hoja hiyo na kuridhia kuchangia kusaidia maafa hayo.
Aidha, Mbunge wa Muleba, Prof. Anna Tibaijuka ameishukuru Serikali kuwepo kwenye eneo la tukio mkoani Bukoba hatua ambayo imewapa faraja wanakagera na kutoa wito kwa wabunge na watu wenye mapenzi mema kuzidi kuwafariji wahanga hao.
Kwa upande wake Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Charles Tizeba amesema kuwa Serikali itafanya tathmini ya kina na ya kitaalamu ili kuepuka wale ambao wanatumia maafa hayo katika kujinufaisha.
Akishukuru kwa niaba ya Serikali Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amewashukuru wadau wote kwa kujitokeza na kushirikiana na Serikali katika kutatua changamoto na kuwahakikishia wabunge kuwa mchango wao utawafika walengwa na kuongeza kuwa jambo hilo limepelekea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kusitisha safari yake nchini Zambia ili kuweza kusimamia suala hilo.
Aidha, Waziri Lukuvi amesema kuwa Serikali inauchungu mkubwa juu ya maafa hayo, hivyo amewataka wadau mbalimbali kujitokeza kusaidiana na Serikali ili kuweza kuwasaidia wahanga hao  na kuwapa pole waathirika wa tetemeko hilo na kuwaombea marehemu wapumnzike kwa amani. 

SERIKALI INAENDELEA KUPOKEA NA KUHAKIKI MADAI YA WATUMISHI WA UMMA YANAYOHUSU MISHAHARA

0
0
Na Beatrice Lyimo-MAELEZO, Dodoma
13/09/2016
Serikali imeendelea kupokea na kuhakiki madai ya watumishi wa umma yanayohusu mshahara na kuyalipa kadri ya uwezo wake kifedha.
Hayo yamebainishwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Angellah Kairuki alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Singida Mjini Mhe. Mussa Sima lililohusu mpango wa Serikali kulipa madeni ya watumishi.
Waziri Kairuki amesema kuwa katika mwaka wa fedha 2014/2015 Serikali ililipa madai ya malimbikizo ya mshahara wa shilingi 56,293,372,627.37 ambapo yalilipwa kwa watumishi 55,688 waliokuwa na madai yatokanayo na kupandishwa vyeo, ajira mpya na sababu nyinginezo.
Aidha, Waziri Kairuki amesema kuwa kwa mwaka 2015/2016 Serikali imeendelea kulipa madai ya malimbikizo ya mshahara wa watumishi wa umma ambapo hadi kufika mwezi Juni, 2016 watumishi 31,032 walilipwa jumla ya shilingi 28,929,095,373.89.
Pia ameongeza kuwa madai ya mishahara ya watumishi 7,871 yenye jumla ya shilingi 13,754,462,429.29 yameshahakikiwa na kuingizwa kwenye mfumo wa taarifa za kitumishi za mshahara yakisubiri kulipwa na madai ya watumishi 8,776 yanaendelea kuhakikiwa ili yaingizwe kwenye mfumo tayari kwa kulipwa.
Akijibu swali la Mhe. Zubeda Sakuru (Viti Maalum) lililohusu changamoto ya maslahi kwa watumishi wa sekta ya afya Waziri Kairuki amesema kuwa Serikali inatambua na kudhamini mchango unaotolewa na madaktari, matabibu na wauguzi nchini.
Hivyo, Serikali imeendelea na jitihada za kuboresha mishahara ya watumishi wake mwaka hadi mwaka ikiwemo ya wataalamu wa sekta hiyo kwa kuzingatia uwezo wa Serikali wa kulipa.
Waziri Kairuki amesema kuwa Serikali inaendelea na utafiti wa tathmini ya kazi, punde itakapokamilika itapanga mishahara na motisha upya kwa watumishi wote wa umma wakiwemo wa sekta ya afya.
Aidha, amebainisha kuwa Serikali itaendelea kuboresha maslahi ya watumishi kadri ya uwezo wake wa kulipa utakavyoimarika ambapo katika shughuli za kila siku madeni huzalishwa lakini ni azma yake kuhakikisha madeni hayo yanalipwa mara yanapojitokea.
Mbali na hayo, Waziri Kairuki ametoa wito kwa wataalamu wa afya na watumishi wote kwa ujumla kufanya kazi kwa bidii na kwa kuzingatia viapo na maadili ya kazi zao.

DONDOO ZA HABARI MAGAZETINI LEO.

0
0

WASHIRIKI 10 WAINGIA FAINALI KATIKA SHINDANO LA GOSPEL STAR SEARCH 2016 JIJINI DAR

0
0
Mshiriki namba 4. Grace Madole akiimba katika jukwaa la Gospel Star Search lililofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika viwanja vya Biafra - Kinondoni jijini Dar es Salaam. Mshiriki huyu hakuweza kupenya hatua ya fainali.
Kikundi cha Makerubi kutoka Manyara ambao walijiandikisha wakitokea Temeke waliweza kufanikiwa kuingia hatua ya nusu fainali katika shindano la Gospel Star Search 2016 kwa kuweza kuimba kwa ustadi mkubwa. Shindano la Nusu fainali lilifanyika katika viwanja vya Biafra - Kindononi jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita.
 PICHA ZOTE NA CATHBERT KAJUNA WA KAJUNASON BLOG. 
Umati wa watu waliohudhuria shindano la Gospel Star Search lililofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika viwanja vya Biafra - Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Mshiriki namba 5. Winnypraise William akiimba katika jukwaa la Gospel Star Search lililofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika viwanja vya Biafra - Kinondoni jijini Dar es Salaam. Mshiriki huyu alipenya kuingia hatua ya fainali.
Shindano la Gospel Star Search lilikuwa ni vuta nikuvute pamoja na mshiriki namba 6. Willansia Lema kuimba kwa hisia ila hakuweza kufanikiwa kuingia hatua ya nusu fainali ambayo iliweza kuingiza washiriki wapatao 10 na kufanya washirikiki watano (5) kuaga mashindano.
Mshiriki namba 10. Flora Kachema alifanikiwa kuingia fainali.
Majaji wa shindano la Gospel Star Search (GSS) kutoka kulia ni Mchungaji Sam Mwangati, Sarah Ndossi na Fred Msungu wakiwa wamenyanyuka kuonyesha heshima ya pekee kwa mshiriki ambaye aliweza kuvuta hisia zao.
Mshiriki Mdogo kuliko wote akiwa aliwavuta hisia majaji wakajikuta wanatoa heshima ya pekee kwa kusimama.
Wageni waliohudhuria shindano hilo wakifurahia kwa shangwe.
Nderemo na vifijo vilitawala.
Mshiriki huyo akiwa amewateka na kujikuta wakiimba kwa hisia wageni waliohudhuria.
Mshiriki Sunday Lunkombe alifanya vyema kuliko wenzake na kufanikiwa kuongoza hakua ya kuingia fainali kwa kujizolea alama nyingi.
Washiriki wakionyesha umahili wa kuimba pamoja kabla ya kutangazwa kumi bora.
Meneja Mradi wa Gospel Star Search 2016, Samwel Sasali akionyesha vijana walifanikiwa kuingia hatua ya fainali (kumi Bora) mara baada ya mchuano mkali.
Kiongozi wa Majaji, Mchungaji Sam Mwangati akisoma majina ya vijana walifanikiwa kuingia hatua ya fainali ya shindano la Gospel Star Search 2016 lililofanyika katika uwanja wa Biafra - Kinondoni jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita. Fainali za shindano hili zinatarajiwa kufanyika jumapili ya Septemba 18, 2016 katika ukumbu wa Milado, Sinza jijini Dar es Salam. 

Na Cathbert Kajuna wa Kajunason blog. 
 Vijana 10 wamefanikiwa kuingia hatua ya fainali katika shindano la kumtafuta mkali wa kuimba nyimbo za injili 'Gospel Star Search 2016' lililofanyika katika viwanja vya Biafra jijini Dar es Salaam. Akizungumza Meneja Mradi wa Gospel Star Search 2016, Samwel Sasali alisema kuwa ni vyema vijana wakazingatia mafundisho yote waliyopatiwa na walimu wao ili waweze kushindana kwa uweledi na ustadi wa hali ya juu.

 Alisema wakati umefika wa vijana kutambua talanta au vipaji walivyopewa na mwenyezi Mungu ili viwaletee manufaa katika kumtangaza Bwana Yesu Kristo. "Tokea tumeanza kuzunguka kukusanya vijana hakika tumeweza kupata vijana wengi wenye vipaji na kuonyesha kuwa mwamko wa vijana katika kutambua vipaji vyao umekuwa mkubwa, hakikuwa jambo jepesi sana ila yote kwa yote tunamshukuru Mwenyezi Mungu aliyeweza kufanikisha yote",  alisema Sasali.

 Aliongeza kuwa shindano la Gospel Star Search 2016 liliweza kupata washiriki wengi ila wakafanyiwa mchujo na kupatikana wapatao 15 ambao waliweza kuingia hatua ya nusu fainali na wakafanya mchuzo katika viwanja vya Biafra wakapatikana 10 ambao wameingia katika kikaango na ipatapo Septemba 18, 2016 Jumapili katika ukumbi wa Milado, Sinza ndipo fainali zitakapofanyika. Vijana 15 waliokuwa wameingia nusu fainali ni 1. Makerubi,  2. Enighenja Mmbaga, 3. Upendo John, 4. Grace Madole,   5. Winnypraise William, 6. Willansia Lema, 7. Rogate Kalengo, 8. Suleiman Wilson, 9. Innocent Eliya. Wengine ni 10. Flora Kachema, 11. Steve Njama, 12. Winnifrida Dudu, 13. Calvin John, 14. Sunday Lunkombe na 15. Beda Andrew. Waliofanikiwa kuingia Fainali ni vijana 10 ambao ni 1. Makerubi, 2. Beda Andrew, 3. Winnypraise William, 4. Rogate Kalengo, 5. Suleiman Wilson, 6. Flora Kachema. Wengine ni 7. Steve Njama, 8. Winnifrida Dudu, 9. Calvin John na 10. Sunday Lunkombe. Shindano la GSS limedhaminiwa na Maendeleo Bank,  Grace Product, Brand exponetial, Kiango media, Clouds Media Group, Fm studios (Faith music lab) na 3D.

WAKURUGENZI WA MANISPAA, MIJI NA HALMASHURI WAAPISHWA TAMISEMI MJINI DODOMA LEO.

0
0

Baadhi ya wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya wakila kiapo wakati wa hafla maalum ya kukabidhiwa majukumu yao katika ofisi za Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) mjini Dodoma Septemba 13.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene akiwapongeza baadhi ya Wakurugenzi wa Manispaa, miji na Halmashauri baada ya kiapo mjini Dodoma jana.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene akiwapongeza Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi baada ya Wakurugenzi wa Manispaa, miji na Halmashauri baada ya kiapo mjini Dodoma Septemba 13 2016.
Baadhi ya wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya wakila kiapo wakati wa hafla maalum ya kukabidhiwa majukumu yao katika ofisi za Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) mjini Dodoma Septemba 13.
Katibu msaidizi wa Sekretarieti ya Maadili ya Umma Ofisi ya Kanda ya kati Dodoma, Cathlex Makawia (kulia) akiwaapisha wakurugenzi 13 wa manispaa, miji na na halmasahuri mjini Dodoma. Kulia ni Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais (TAMISEMI) Bernard Makali. (Picha na Robert Okanda)
Baadhi ya wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya wakila kiapo wakati wa hafla maalum ya kukabidhiwa majukumu yao katoka ofisi za Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) mjini Dodoma.

Baadhi ya wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya wakila wakitia saini viapo vyao baada ya kuapa  wakati wa hafla maalum ya kukabidhiwa majukumu yao katika ofisi za Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) mjini Dodoma Septemba 13 2016. 

Baadhi ya wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya wakila wakitia saini viapo vyao baada ya kuapa  wakati wa hafla maalum ya kukabidhiwa majukumu yao katika ofisi za Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) mjini Dodoma Septemba 13 2016.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angela Kairuki akiwapa mawaidha na ushauri wa kiutendaji Wakurugenzi baada ya kuapa.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene akiwapa mawaidha Wakurugenzi wa Manispaa, miji na Halmashauri 13 baada ya kiapo mjini Dodoma.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene akiwapongeza baadhi ya Wakurugenzi wa Manispaa, miji na Halmashauri baada ya kiapo mjini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angela Kairuki wakifahamiana na baadhi ya wakurugenzi.
Waziri Kairuki akibadilishana mawasiliano na Mkurugenzi wa Manispaa ya Mbulu, Hudson Kamoga.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene akiwapongeza baadhi ya Wakurugenzi wa Manispaa, miji na Halmashauri baada ya kiapo mjini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene (katikati), Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angela Kairuki, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jaffo (wa pili kushoto), Katibu Msaidizi wa Sekretarieti ya Maadili ya Umma Ofisi ya Kanda ya kati Dodoma, Cathlex Makawia (kushoto) pamoja Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais (TAMISEMI) Bernard Makali (kulia) wakiwa katika pichAa ya pamoja na wakurugenzi hao. (Imeanaliwa na Robert Okanda Blogs)

Briana Kagemuro azidi kung'ara. Anyakuwa kombe laTennis USTA L6 -Mid Atlantic

0
0
Mchezaji tennis Briana Kagemuro mwishoni mwa juma alishinda katika michuano ya shirikisho la Tennis Marekani (USTA) Mid Atlantic, kwa upande wa wasichana walio chini ya miaka 12 (12 and under) a yaliyofanyika katika viwanja vya Bullis Potomac -Maryland.
Mashindano hayo yalijumuisha wasichana nane ambapo Kage Briana alifanikiwa kumbwaga mpinzani wake Emory Wilson katika fainali kwa seti 6-4,6-3.

KageBriana akiwa na kombe lake pamoja na mshindi wa pili Emory Wilson
Wakati huohuo yalifanyika mashindano ya mix doubles ambapo KageBriana na kakaye Mwombeki walichukuwa ushindi wa tatu kwa michuano ya vijana wa umri wa miaka 14 (14 and under yaliyofanyika Potomac Maryland.
Bryan na Briana wakiwa na medali zao

SHULE ZA FEZA KUFUNGUA TAWI LAKE MKOANI MWANZA.

0
0
Kutoka kushoto ni balozi wa shule hizo mkoani Mwanza, Faisal Hafidh na Taasisi ya Time To Help, Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza na  Meneja wa Shule za Feza mkoani Mwanza, Metin-Er.
Na BMG

Uongozi wa Shule za Feza (Feza Schools) nchini Tanzania mwakani unatarajia kufungua tawi la shule hizo Jijini Mwanza, ili kuendelea kufikisha karibu upatikanaji wa elimu karibu na jamii nchini.

Balozi wa shule hizo mkoani Mwanza, Faisal Hafidh na Taasisi ya Time To Help (kushoto), aliyasema hayo juzi jumatatu Septemba 12,2016 wakati wa zoezi la kukabidhi msaada wa mboga (nyama) kwa makundi mbalimbali ya wahitaji mkoani Mwanza kama sehemu ya kusherehekea Sikukuu ya Eid El Hajj.

Alisema lengo la Shule za Feza kwa kushirikiana na taasisi yake ya Time To Help ni kusaidia jamii ya watanzania bila kujali dini, kanila wala mipaka ya aina yoyote.

Msaada uliotolewa na Shule za Feza ni nyama kilo 500 ambazo ziligawiwa na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Marry Tesha, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, kwenye Kituo cha Wazee Bukumbi, Bakwata mkoani Mwanza, Taasisi za Juqusuta, Ummy Salama na Masjid Noor Mahina.
Msaada wa mboga uliotolewa Shule za Feza mkoani Mwanza.
Shule za Feza zinapatikana katika mataifa mbalimbali duniani ambapo nchini kuna tawi Jijijini Dar es salaam na sasa mkakati ni kufungua tawi mkoani Mwanza.
Viewing all 46205 articles
Browse latest View live




Latest Images