Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 969 | 970 | (Page 971) | 972 | 973 | .... | 1898 | newer

  0 0


  Mkurugenzi wa kiwanda cha ukamuaji na usafishaji wa mafuta ya alizeti cha Mukta Agro-Proccesing Co Ltd cha mjini Babati Mkoani Manyara, Bakari Mukta akishika mwenge wa uhuru ulipofika kuzindua kiwanda hicho.
  Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kwa mwaka huu George Mbijima, akipokea zawadi ya mafuta toka kwa mkurugenzi wa kiwanda cha ukamuaji na usafishaji wa mafuta ya alizeti cha Mukta Agro-Proccesing Co Ltd Bakari Mukta, mjini Babati Mkoani Manyara.

  0 0


  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akitoa hutuba katika swala ya Idd El Haji iliyofanyika Viwanja vya Mwembe Yanga Dar es Salaam leo asubuhi.
   
   
  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewaomba viongozi wa dini zote  kutumia nyumba za ibada kuwahamasisha waumini wao umuhimu wa kulinda na kudumisha amani na utulivu uliopo nchini.Amesema Serikali itahakikisha amani na utulivu vinaendelea kudumishwa nchini ili Watanzania wawe na uhakika wa kuendelea kufanya kazi zao za kuwaingizia kipato na kuwaletea tija.

  Waziri Mkuu ametoa wito huo leo (Jumatatu, Septemba 12, 2016) wakati akizungumza na waumini wa dini ya kiislam mara baada ya kumaliza kuswali sala ya Eid El Haji kwenye viwanja vya Mwembe Yanga, Temeke Dar es Salaam.

  “Serikali itaendelea kuimarisha ulinzi katika maeneo yote nchini. Wito wangu kwa viongozi wa dini msisitize waumini juu ya utunzaji wa amani pamoja na kukemea vitendo viovu ili Taifa lizidi kusonga mbele,” amesema.

  Wakati huo huo Waziri Mkuu amewasisitiza wananchi kuendelea kuwaombea mahujaji waliopo mjini Makka na Madina nchini Saudi Arabia wakiendelea na ibada ya hijja warudi salama.Pia Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwaomba wananchi kuwasaidia kwa hali na mali watu waliokumbwa na tetemeko la ardhi mkoani Kagera ambako jumla ya watu 16 walifariki na wengine 253 kujeruhiwa.

  Pia maelfu ya wananchi kukosa makazi baada ya nyumba 840 kuanguka na nyingine 1264 zikipata nyufa yakiwemo majengo 44 ya taasisi mbalimbali za umma.Awali akisoma hutuba ya Eid viwanjani hapo Sheikh Nurdin Kishki alisema dini ya Uislamu ni dini ya amani hivyo amewaomba waislamu kujiepusha na vitendo vya uvunjifu wa amani yakiwemo mauaji ya watu wasiokuwa na hatia.

  Sheikh Kishki amesema ni muhimu watu kulinda amani kwani ikitoweka ni vigumu kuirudisha, alitolea mfano wanachi wa nchi za  Libya na Misri ambazo hadi sasa zimeshindwa kuirudisha.Amesema mtu yeyote anayejihusisha na vitendo vya uwamwagaji wa damu, kudhulumu mali za watu pamoja na kuwavunjia heshima wenzake atakuwa ameangamia, hivyo amewataka Watanzania hususan wakazi wa Temeke kujiepusha navyo.

  “Temeke sasa inaongoza kwa matukio ya mauaji, wanaua hadi walinzi. Askari wameuawa bila hatia, jambo hili linasikitisha sana. Watu waliokuwa wanafanya kazi ya kulinda raia na mali zao wanauawa bila ya hatia! Ameongea kwa masikitiko na kuwaomba Watanzania wajiepuszhe na vitendo hivyo.

  Katika hatua nyingine Sheikh Kishki ameipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa kuonyesha dhamira ya dhati ya kuwatumikia wananchi na kuwaletea maendeleo hivyo amewaomba wananchi wawe mstari wa mbele kutoa ushirikiano ili taifa liweze kusomba mbele.

  “Ndugu zangu tumepewa heshima kubwa leo kuswali Eid na Mheshimiwa Waziri Mkuu tena amekuja hapa kwenye viwanja hivi vya Mwembe Yanga, hii inaonyesha ukaribu wa viongozi wetu wakuu kwa wananchi wao hususan wa hali ya chini,” amesema.

   IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  2 MTAA WA MAGOGONI,
  S. L. P. 3021,
  11410 DAR ES SALAAM.
  JUMATATU SEPTEMBA  12, 2016  

   

  Swala ikiendelea.
  Waziri Mkuu alivyojumuika na waislam wenzake katika swala hiyo.
  Sheikh Abdu Kadri akiongoza swala ya Idd El Haji
  Sheikh Nurudin Kishki akihutubia baada ya swala hiyo.
  Waumini wa dini ya kiislam wakishiriki swala hiyo.

  Waumini wa dini ya kiislam wakiswali.

  0 0

   
    Viongozi wapya wa KIDIFA wakiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti aliyemaliza muda wake Hassan Ngubege
   Mwenyekiti wa KIFIDA aliyemaliza muda wake, Hassan Ngubege akimkabidhi Mwenyekiti mpya wa chama hicho Jesse John katiba ya chama hicho.
   
   
  Na Mwandishi Wetu,Kisarawe
  MTANGAZAJI nguli wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Jesse John amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Kisarawe (KIDIFA) katika uchaguzi uliofanyika jana.
  Jesse ambaye aliupata uongozi huo katika uchaguzi uliokuwa na ushindani mkubwa aliibuka kidedea baada ya kupata kura 32 na kumshinda mpinzani wake Karim Wenge aliyepata kura 21.
  Katika uchaguzi huo Mohamed Lubondo alichaguliwa kuwa Katibu baada ya kupata kura 30 na kumshinda Francis Mkamba aliyepata kura 27.Katibu Msaidizi alichaguliwa kuwa Amosi Kisebengo, Makamu Mwenyekiti alichaguliwa kuwa Abdul Mogella.
  Wasimamizi wa uchaguzi huo kutoka Chama Mpira wa Miguu Mkoa wa Pwani (COREFA), Mweka Hazina wa KIDIFA alichaguliwa Iddo Mtangaze na Mweka Hazina Msaidizi alichaguliwa kuwa Sadiki Nasoro.
  Mwakilishi wa klabu kutoka Tarafa ya Mzenga alichaguliwa kuwa Suleiman Mahenge, kutoka Tarafa ya Sungwi alichaguliwa Abdallah Kuga na Mwakilishi wa klabu alichaguliwa kuwa Ally Madega na Mwakilishi wa Mkutano Mkuu wa mkoa alichaguliwa kuwa Mohamed Masenga.
  Mwenyekiti wa KIDIFA aliyemaliza muda wake Hassan Ngubege akimkarisha Jesse kushukuru wajumbe aliwataka viongozi wapya kufufua matumaini ya vipaji vya vijana katika soka wilaya ya Kisarawe kwa kuanzisha mashindano mbalimbali yenye lengo la kutafuta vipaji.
  Jesse akiwashukuru wajumbe hao aliahidi kushirikiana na wadau wa soka ndani na nje ya wilaya hiyo kupata timu ya wilaya itakayoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom kama timu nyingine zinashiriki mashindano hayo.
  Mwenyekiti Jesse alisema wilaya ya Kisarawe ambako yeye ni mzaliwa wa asili alisema anaamini vijana wengi hawajapata nafasi ya kuonesha vipaji vyao hivyo atatumia miaka minne ya uongozi kuzalisha vijana wazuri katika soka.

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akilakiwa na Katibu Mkuu Wizara ya Vijana, Michezo na Maendeleo ya Watoto Mhe. Agnes Musunga mara baada ya kutua  katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kenneth Kaunda jijini Lusaka, Zambia, leo Jumatatu Septemba 12, 2016  tayari kwa kumuwakilisha Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt John Pombe Joseph Magufuli kwenye sherehe za kuapishwa rais wa sita wa nchi hiyo Mhe. Edgar Lungu kesho Jumanne Septemba 13, 2016 katika uwanja wa Mashujaa jijini Lusaka
   Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea shada la maua  mara baada ya kutua  katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kenneth Kaunda jijini Lusaka, Zambia, leo Jumatatu Septemba 12, 2016  tayari kwa kumuwakilisha Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt John Pombe Joseph Magufuli kwenye sherehe za kuapishwa rais wa sita wa nchi hiyo Mhe. Edgar Lungu kesho Jumanne Septemba 13, 2016 katika uwanja wa Mashujaa jijini Lusaka
   Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea shada la maua  mara baada ya kutua  katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kenneth Kaunda jijini Lusaka, Zambia, leo Jumatatu Septemba 12, 2016  tayari kwa kumuwakilisha Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt John Pombe Joseph Magufuli kwenye sherehe za kuapishwa rais wa sita wa nchi hiyo Mhe. Edgar Lungu kesho Jumanne Septemba 13, 2016 katika uwanja wa Mashujaa jijini Lusaka
   Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Katibu Mkuu Katibu Mkuu Wizara ya Vijana, Michezo na Maendeleo ya Watoto Mhe. Agnes Musunga   mara baada ya kutua  katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kenneth Kaunda jijini Lusaka, Zambia, leo Jumatatu Septemba 12, 2016  tayari kwa kumuwakilisha Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt John Pombe Joseph Magufuli kwenye sherehe za kuapishwa rais wa sita wa nchi hiyo Mhe. Edgar Lungu kesho Jumanne Septemba 13, 2016 katika uwanja wa Mashujaa jijini Lusaka
  Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Katibu Mkuu  Katibu Mkuu Wizara ya Vijana, Michezo na Maendeleo ya Watoto Mhe. Agnes Musunga   akipokea heshima mara baada ya kutua  katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kenneth Kaunda jijini Lusaka, Zambia, leo Jumatatu Septemba 12, 2016  tayari kwa kumuwakilisha Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt John Pombe Joseph Magufuli kwenye sherehe za kuapishwa rais wa sita wa nchi hiyo Mhe. Edgar Lungu kesho Jumanne Septemba 13, 2016 katika uwanja wa Mashujaa jijini Lusaka
    Balozi wa Tanzania nchini Zambia Mhe Grace Mujuma akiwa na Balozi wa Zambia nchini Tanzania Mhe Judith  Kapijimpanga wakifurahia wakati ndege iliyomchukua Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ilipotua katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kenneth Kaunda jijini Lusaka, Zambia, leo Jumatatu Septemba 12, 2016  tayari kwa kumuwakilisha Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt John Pombe Joseph Magufuli kwenye sherehe za kuapishwa rais wa sita wa nchi hiyo Mhe. Edgar Lungu kesho Jumanne Septemba 13, 2016 katika uwanja wa Mashujaa jijini Lusaka.

  PICHA NA IKULU.

  0 0


  Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha,Kalist Lazaro akimkabidhi Kombe la ubingwa wa Bonanza la 11 nahodha wa timu ya soka ya waandishi wa Habari za michezo nchini(Taswa FC),Wilbert Molandi katika fainali la Bonanza la Waandishi wa Habari mkoa wa Arusha kwenye uwanja wa General Tyre jumapili,kulia ni Mwenyekiti wa Taswa FC,Majuto Omary na kushoto ni Mratibu wa mashindano hayo,Mussa Juma.

  Nahodha wa timu ya Netiboli ya Waandishi wa Habari za Michezo nchini, Tanzania Sports Writers Association Sports Club (Taswa SC)Zuhura Abdulnoor na mchezaji mkongwe wa Timu ya soka ya waandishi wa Habari za michezo nchini,(Taswa FC),Muhidin Sufiani(kulia)wakifurahia ushindi.

  Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha,Kalist Lazaro akizungumza katika Bonanza la 11 la Waandishi wa Habari mkoa wa Arusha.
  Mchezaji nguli wa timu ya soka ya waandishi wa Habari za michezo nchini(Taswa FC),Muhidin Sufiani akichanja mbuga kupenya ngome ya timu ya Chuo cha Uandishi wa Habari Arusha(AJTC)katika mchezo wa fainali ambao Taswa FC walishinda bao 1-0.
  Wachezaji wa Netiboli wa Taswa SC na Chuo cha Uandishi wa Habari Arusha(AJTC)wakichuana vikali katika bonanza hilo ambalo Taswa SC walibamiza bila huruma 30-2
  Timu ya soka ya waandishi wa Habari za michezo nchini, (Taswa FC) na netiboli ya Waandishi wa Habari za Michezo nchini, Taswa FC Tanzania Sports Writers Association Sports Club (Taswa SC) wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi na waratibu wa bonanza la 11 la Waandishi wa Habari la Arusha.


  Na Mwandishi wetu

  Arusha. Timu ya soka ya waandishi wa Habari za michezo nchini, (Taswa FC) na netiboli ya Waandishi wa Habari za Michezo nchini, Taswa FC Tanzania Sports Writers Association Sports Club (Taswa SC) zimetwaa ubingwa wa bonanza la 11 la Waandishi wa Habari la Arusha.

  Taswa FC na Taswa Queens ambazo zinadhaminiwa na kampuni ya uchimbaji wa madini ya Acacia na Benki ya Posta Tanzania (TPB) zilifanikiwa kushika nafasi ya kwanza katika bonanza hilo la kusisimua na waandishi kushindana katika michezo mbalimbali mbali ya soka na netiboli.

  Timu ya Wazee Club ambao ilishika nafasi ya pili, ndiyo pekee iliyonusurika na kichapo katika bonanza hilo aada ya kuambulia sare ya mabao 2-2. Hata hivyo, timu hiyo ilibidi ifanya kazi ya ziada baada ya kusawazisha mabao mawili katika dakika sita za mwisho. Timu ya Chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji cha AJTC kilishika nafasi ya tatu na timu ya mwisho ni Redio Sunrise.

  aswa FC ilianza kwa kasi na kufunga mabao mawili ya haraka haraka kupitia kwa Saidi Seifu akipokea pasi safi za Majuto “Dr Regret” Omary. Martin Shila, Edrward Mbaga, Muhidin Sufiani, Zahoro Mlanzi, Salum Jaba na kipa wao, Mwarami Seifu walikuwa kizingiti kikubwa katika mechi zote.

  Katika mechi ya pili, Taswa FC ilishinda mabao 4-0n dhidi ya Sunriseb Redio , bao la kwanza likifungwa na kapteni, Wilbert Molandi kwa kuunganisha kona ya Hare Temba na baadaye Saidi Seifu akifunga mabao matatu kufutia pasi ya Athumani Jabir na Majuto Omary ambaye alitoa pasi ya bao la tatu na la nne.

  Katika mchezo wa mwisho, Taswa FC iliibuka na ushindi wa ba 1-0 dhidi ya AJTC, bao la dakika za majeruhi lilifungwa na Ali “Maradona” Salum kufuatia kona safi ya Majuto.Timu ya netiboli ya Taswa Queens ilifanya ‘mauaji’ kufuatia ushindi wa mabao 30-2 dhidi ya AJTC. Mabao ya Taswa Queens yalifungwa na Sharifa Mustapha aliyefunga mabao 22 na Rose Michael aliyefunga mabao nane.

  Taswa Queens ilitawala sana mchezo huo kupitiaa wachezajia wake, Zuhura Abdinoor, Johari William, Elizabeth Mbasa, Tatu, Mage na Vicky Godfrey.
  Timu zote hizo zilizawadiwa kitita cha sh 100,000 kila moja na kombe. Kwa upande wa kukimbiza Kuku, Taswa Queens pia walifanikiwa kuibuka na ushindi wakifuatiwa na Sunrise Radio ambao wote waliondoka na kuku kila mmoja.

  Mgeni rasmi katika bonanza hilo la 11 lillilofanyika katika viwanja vya General Tyre alikuwa Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha Calist Lazaro ambaye alisema kuwa waandishi wa habari ni muhimu kushiriki michezo ya aina mbalimbali ili kuiweka miili vizuri.

  0 0

  Katika kusherehekea sikukuu ya Idd el Hajj, Kampuni ya simu ya ZANTEL kupitia Promosheni yake ya Jibwage na mbuzi, imewazawadia wateja walioshiriki promosheni hiyo jumla ya mbuzi 400, kwa ajili ya kuchinja ikiwa ni sehemu ya kusherehekea sikukuu ya Idd ya kuchinja.

  Washindi hao walipatikana kufuatia wateja 400 wa kwanza kutumia dakika nyingi zaidi katika simu zao. Mbali na kuwakabidhi washindi hao, Kamuni hiyo haikuwasahau Watoto Yatima, ambapo ilitoa Mbuzi100 katika vituo mbali mbali vya watoto Yatima nchini.

  Vituo hivyi ni pamoja na Children's Home, Tanzania Mitindo House, na vituo vingine vilivyo chini ya uangalizi wa BAKWATA, vituo vingine ni vya Tanga, Mtwara na Lindi , Unguja na Pemba.
  Mkuu wa Kampuni ya Zantel Zanzibar, Mohamed Mussa Baucha (wa pili kulia) akikabidhi mbuzi kwa washindi wa promosheni ya jibwage na mbuzi visiwani Zanzibar jana.
  Afisa Habari na Mawasiliano wa Zantel, Winnes Lyaro (wa pili kushoto) akikabidhi mbuzi mshindi Bi. Zulfa mkazi wa Dar huku wateja wengine waliopata nafasi ya kujizawadia mbuzi wakiwa katika picha ya pamoja. Zantel imewezawadia wateja wake 400 nchini waliotumia dakika nyingi zaidi katika ofa ya wiki mbili ya Jibwage na Mbuzi iliyoandaliwa rasmi na kampuni hiyo ili kuwazawadia wateja wake mbuzi kipindi cha sikukuu huku mbuzi 100 kati ya hao wakiwazawadia watoto yatima nchini.
  Meneja mauzo wa Zanztel, Yussuf Ismail (kulia) akikabidhi mbuzi wa mshindi, Hemed Ali Omar.
  Mbuzi wanaosubiri kuchukuliwa na wateja waliopata ushindi wa promosheni ya jibwage na mbuzi.
  Mkurugenzi wa mauzo wa Zantel, Ibrahim Attas (kulia) akikabidhi mbuzi kwa mshindi, Aly Rashid.

  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsalimia Mkuu wa Majeshi Mstaafu, Jenerali David Msuguri wakati alipokwenda kwenye hospitali ya Jeshi ya Lugalo jijini Dar es salaam kuona wagonjwa baada ya kushiriki sala ya Iddi El Haji kwenye uwanja wa Mwembe Yanga, Temeke jijini Dar es salaam Septemba 12, 2016.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary (kulia) wakimjulia hali Mkuu wa Majeshi Mstaafu, Jenerali David Msuguri wakati walipokwenda kwenye hospitali ya Jeshi ya Lugalo jijini Dar es salaam kuona wagonjwa baada ya kushiriki sala ya Iddi El Haji kwenye uwanja wa Mwembe Yanga, Temeke jijini Dar es salaam Septemba 12, 2016.  

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary (kulia) wakiwajulia hali wagonjwa wakati walipokwenda kwenye hospitali ya Jeshi ya Lugalo jijini Dar es salaam kuona wagonjwa baada ya kushiriki sala ya Iddi El Haji kwenye uwanja wa Mwembe Yanga, Temeke jijini Dar es salaam Septemba 12, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

  0 0

  Temeke wasichana wakishangilia baada ya kukabidhiwa kombe la uchampioni wa Airtel Rising Stars 2016. Temeke waliishinda Ilala 5-4 katika changamoto ya mikwaju ya penati.
   Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Nape Nnauye na Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania wakimkabidhi nahodha wa Temeke wasichana Shamimu Hamisi kombe la ubigwa wa Airtel Rising Stars 2016.  Temeke waliishinda Ilala 5-4 katika changamoto ya mikwaju ya penati.
   Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Nape Nnauye akimkabidhi nahodha wa Temeke wasichana Shamimu Hamisi kombe la ubigwa wa Airtel Rising Stars 2016.  Temeke waliishinda Ilala 5-4 katika changamoto ya mikwaju ya penati.
   Timu ya Morogoro wakishangilia baada ya kukabidhiwa kombe la uchampioni wa Airtel Rising Stars 2016 kwa upande wa wavulana. Morogoro iliifunga Ilala 1-0 katika fainali iliyopigwa kwenye uwanja wa Karume, Dar es Salaam jana.

  Goli pekee lililofungwa na mshambuliaji hatari Tepesi Evans wa Morogoro lilitosha kuifanya timu hiyo kuwa mabingwa wa michuano ya vijana chini ya miaka 17 ya Airtel Rising Stars 2016 kwa kuwafunga Ilala 1-0. Mechi hiyo ambayo ilikuwa ya kuvutiwa yenye upinzani mkali ilishuhudiwa na mamia ya mashabiki akiwepo Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Nape Nnauye.

  Baada ya kosa kosa nyingi, Evans aliachia shuti kali mnamo dakika 77 ya mchezo, shuti ambalo lilienda moja kwa moja na kuamsha shangwe na nderemo kutoka kwa mashabiki. Juhudi za Ilala kuzawashisha hazikuzaa matunda mpaka mchezo unamalizika.

  Mchezo huo ulikuwa ni kama marudio ya mechi ya Alhamisi ambapo timu hizo zilikutana kwenye hatua ya makundi huku Ilala ikitoka kichwa chini kwa kukubali kichapo cha 2-0.

  Akifunga michuano hiyo ya kila mwaka, Waziri Nnauye alisema kuwa serikali inaunga mkono juhudi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) pamoja na wadhamini. ‘Kwa kuwapa fursa wasichana na wavulana hawa kuonyesha vipaji vyao, ni kusaidia kubadilisha maisha yao kwani mpira wa soka ni zaidi ya burundani – ni kufahamiana, kupata uzoefu na zaidi, ni ajira’, alisema Nnauye.

  Naye Mkurungenzi Mtendaji Airtel Tanzania Sunil Colaso alisema kampuni yake inajivunia mafanikio ya Airtel Rising Stars yaliyopatikana miaka tano iliyopita. ‘Wachezaji ambao waliisaidia Uganda kufuzu kwenye michuano ya AFCON 2017 Gabon ni uzao wa Airtel Rising Stars na ni uhakika hayo yatatokea Tanzania hivi karibuni’. Alisema Colaso huku akiongeza kuwa Airtel mpaka sasa ishawekeza Tshs2.4 billioni kwenye michuano hiyo.

  Kwa upande wake Raisi wa TFF Jamal Malinzi alielezea michuano ya Airtel Rising Stars kama michuano ya kutumainiwa katika kuibua vipaji. ‘Serengeti Boys na timu ya Taifa ya Wanawake ni ushuhuda tosha wa mafainikio ya michuano hii’, alisema Malinzi.
  Timu bora, wachezaji bora, waamuzi pamoja na makocha walipewa tuzo wakati wa fainali za michuano hiyo.

  Timu ya Temeke wasichana walishinda ubingwa wa michuano hiyo kwa penati 5-4 baada ya kwenda sare ya 2-2 kwenye muda wa kawaida.

  Wakati huo huo, timu ya Temeke wavulana walishinda nafasi ya tatu ya michuano hiyo kwa changamoto ya mikwaju ya penati ya 5-4 dhidi ya Kinondoni baada ya kutoka sare ya 0-0 kwenye muda wa kawaida.

  Kinondoni wasichana walipata nafasi ya mshindi wa tatu baada ya kuwafunga wenzao Arusha 2-0. Magoli yote ya Kinondoni yalifungwa na Veronica Mapunda.

  0 0

  Majagina wa muziki wa Afrika Mashariki na washindi wa tuzo kibao, Sauti Sol (Kenya) wameachia video ya wimbo wao unaofanya vizuri, KULIKO JANA, uliopo kwenye santuri yao ya tatu: Live and Die in Afrika. Bien wa Sauti Sol anaelezea maana ya wimbo huo, “Unamaanisha kuwa uaminifu wa Mungu haukomi kamwe. Huruma yake haiishi – kila uchao ni vipya.” Wakimshirikisha Redfourth Chorus (Upper Hill School), wimbo huo mtamu lakini wenye ujumbe mzito, umezikwea chati na kuwagusa mashabiki barani Afrika na zaidi.

  Video maarufu ya Sauti Sol wakiimba akapela ya wimbo huo wakiwa na Redfourth Chorus, ulivutia masikio ya watu mashuhuri duniani na kwenye vyombo vya habari hadi kumfanya Amber Riley, nyota wa kipindi kilichoshinda tuzo za Emmy, Glee, kuandika kwenye Instagram, “Sielewi wanachokisema lakini najua ni kizuri. Inasikika kimalaika, kuna yeyote anayejua kama kuna video?” Mastaa wengine waliowahi kuiweka video hiyo kwenye mitandao ya kijamii ni pamoja Master P, Anthony Hamilton, Jb Smoove na  WorldstarHipHop, miongoni mwa tovuti zingine za habari za kimataifa.

  Katika video mpya iliyotoka yenye rangi nyeusi na nyeupe ya KULIKO JANA, Sauti Sol wameungana na chipukizi lakini mweye kipawa cha hali ya juu, Redfourth Chorus kwa maajabu ya kimuziki. Sauti Sol wamesema kwenye taarifa yao, “KULIKO JANA ni wimbo maalum sana kwetu. Ulihamasishwa na safari yetu na rehema zisizoisha, mapenzi na baraka ambazo Mungu ametuonesha muda wote licha ya udhaifu wetu.”

  Video ya KULIKO JANA imetayarishwa na Fulfillment Limited, na kufanyika Kenya na waongozaji wakiwa Tim Mwaura na Joash Omondi.  Wimbo umeandikwa na kutayarishwa na Sauti Sol.  Kipande cha akapela kilipangwa na Philip Tuju na Redfourth Chorus.


  0 0

  Mkurugenzi mteule wa Wilaya ya Mbulu, Hudson Kamoga, ambaye ameteuliwa mwishoni mwa wiki jana amesema anaamini ni Mungu aliyemuweka kwenye nafasi hiyo ili  awatumikie wananchi wa Mbulu kwa wakati huu. 

  Akiongea kwenye ibada ya Jumapili hii  ndani ya  Kanisa la Living Water Center Kawe, wakati alipopewa nafasi na mtumishi wa  Mungu  Apostle Onesmo Ndegi  ili asalimia Kanisa Mheshimiwa Kamonga  alisema, anakwenda kwenye wilaya yenye changamoto nyingi za kimaendeleo ila anaamini Mungu atamwezesha kuzitatua kwa nafasi yake akishirikina na wananchi pamoja na  viongozi wengine kati halimashauri ya Mbulu.

  Kamonga alisisitiza kuwa kwa kupata  nafasi hii ya  Ukurugenzi bado  ataendelea na utumishi wake kwa Mungu maana anaamini huo ndio uliomfanya kufikia hatua hiyo,hivyo kuamua kuwa anamtanguliza Mungu kaika kila atakachokuwa anafanya,alisema Kamoga

  Pia alitoa shukurani za dhati kwa Mtumishi wa Mungu Apostle Ndegi pamoja na  watumishi wengine kanisani hapo na kusema kuwa kati ya vitu ambavyo hawezi kuvisahau na malezi mazuri ya kiroho pamoja na mafindisho ambayo amekuwa akiyapata kutoka  kwa Apostle Ndegi na watumishi wengine kanisani hapo, akisema mafundisho hayo yamesababisha kuwa vile alivyo sasa! Mwisho Mtumishi wa Mungu Mtume Onesmo Ndegi  na waumini walifanya maombi kwa ajili yake ili Mungu aambatane naye katika utumishi wake kwenye nafasi hiyo ya Ukurugenzi!.

  Mkurugenzi mteule wa Wilaya ya Mbulu, Hudson Kamoga
  Mkurugenzi mteule wa Wilaya ya Mbulu, Hudson Kamoga akiwa na Baba yake wa Kiroho Apostle Onesmo Ndegi Kiongozi wa Kanisa la Living Water Center Kawe akimsiliza kwa makini akielezea uteuzi wake.
  Mkurugenzi mteule wa Wilaya ya Mbulu, Hudson Kamoga akiwa na Baba yake wa Kiroho Apostle Onesmo Ndegi Kiongozi wa Kanisa la Living Water Center Kawe akimsiliza kwa makini akielezea uteuzi wake.
  Apostle Onesmo Ndegi Kiongozi wa Kanisa la Living Water Center Kawe akimwombea Hudson Kamogaakiwa amepiga magoti
  Waumini wa Kanisani Living Water Center Kawe wakiwa wamenyoosha mikono kwa Hudson Kamoga kuomba kwa ajili yake

  0 0

  Aliyekuwa muwezeshaji katika Mkutano huo Profesa Aldo Lupala Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu Ardhi ambaye ni Mkuu wa Kitivo cha Usanifu Majengo akitoa mwongozo wakati wa mkutano huo.

   Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Mipango na Matumizi ya Ardhi Tanzania, Dr. Stephen Nindi akizungumza jambo juu ya Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kwa pamoja kuhakikisha maeneo yanapimwa na kuweka mpango mzuri wa Matumizi Bora ya Ardhi.
   Wadau wa mkutano huo wakiendelea kufuatiliamkutano huo
  Mratibu wa Mradi wa Ardhi yetu kutoka CARE International Tanzania Mary Ndaro akifafanua jambo wakati wa mkutano huo wa kikosi kazi
  Mwakilishi kutoka Wizara ya Kilimo akielezea mikakati mbalimbali waliyonayo kuhusu mpango wa matumizi bora ya ardhi
  Bw. Amos Mfuga kutoka Tume ya Taifa Mipango na Matumizi ya Ardhi akichangia jambo ikiwa ni pamoja na Tume kuweka vipaumbele kama kuangalia na kumaliza migogoro ya ardhi katika maeneo mbalimbali nchini 
   Wadau wa mkutano huo wa kikosi kazi kutoka Sehemu  mbalimbali wakiendelea na mkutano huo
  Bw. Mdubi kutoka CARE International Tanzania akichangia jambo wakati wa Mkutano huo wa kikosi kazi
  Naomi Shadrack kutoka Shirika la Kimataifa la OXFAM Tanzania akielezea namna shirika hilo likifanya kazi hapa Nchini na jinsi wanavyoshiriki katika mpango huo wa matumizi bora ya Ardhi
  Bw. Jamboi kutoka Ujamaa Community akielezea ushiriki wao katika mpango wa matumizi bora ya ardhi
  Bw.Emanuel Msofe kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii akichangia jambo juu ya ushiriki wao katika kikosi kazi hicho.
  John Lugaso mmoja wa viongozi kutoka Chama cha wafugaji Tanzania , akieleza malengo ya chama hicho ikiwa ni pamoja na mipango ya baadae ya uanzishaji wa viwanda mbalimbali kwa ajili ya bidhaa zinazotokana na mifugo.
  Mkutano ukiendelea
  Picha zote na Fredy Njeje/Blogs za Mikoa

  Katika kupanga matumizi bora ya ardhi nchini Tanzania ikiwa na lengo la jamii kutumia rasilimali hiyo vizuri kwa matumizi ya kawaida, Serikali imesema kuwa hadi sasa imefikia takribani vijiji 1645 na Wilaya 40 nchi nzima. Kutokana na ufinyu wa bajeti na kasi ndogo ya upimaji bado kuna vijiji 11,393 ambavyo havijafikiwa.

  Akizungumza Mkoani Morogoro ,Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Mipango ya Ardhi,Dkt Stephen Nindi wakati wa Mkutano wa  Kikosi kazi cha kuanda mpango kazi wa upangaji,utekelezaji na usimamizi wa maendeleo ya Ardhi nchini.
  Pia Mkutano huo ulijadili kuhusu migogoro ya ardhi inayoendelea nchini na mipango ya matumizi ya ardhi kama inaweza kusaidia kupunguza migogoro hiyo,uliowakutanisha  wadau mbalimbali kutoka Serikalini ,taasisi na Mashirika mbalimbali yanayosimamia masuala ya ardhi.

  Alisema serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wanashirikiana kwa pamoja kuhakikisha maeneo yanapimwa na kuweka mpango mzuri wa matumizi ya ardhi kwa matumizi yaliyokusudiwa katika kujadiliana ni namna gani wataona njia zinazofaa kutumika kukamilisha zoezi hilo la upimaji kwa vijiji vingine ikiwemo kuwepo kwa teknolojia mpya ya upimaji na kuwepo kwa bajeti ya kutosha.

  Aliongeza kuwa lengo la  kupima,kumilikisha na Kupanga kila kipande cha ardhi ni pamoja na kuhakikisha ardhi inakuwa na matumizi mazuri katika nchi.

   Dkt.Nindi alisema tayari serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wametoa elimu katika timu za wilaya 100 kuwawezesha kujua  kupima,kupanga,kumilikisha ,kutekeleza na kusimamia mipango ya matumizi ya ardhi .

  Kwa upande wake Mratibu wa Programu ya Mradi ya Ardhi yetu kutoka Shirika la Kimataifa la CARE nchini Tanzania ,Mary Ndaro alisema mpaka sasa ni miaka mingi tangu nchi ipate uhuru kasi ya upimaji wa maeneo imekua ndogo .

  Alisema kama nchi inajiandaa kuwa na wawekezaji wengi zaidi inatakiwa kuhakikisha inakuwa na mipango bora ya  matumizi ya ardhi ambayo baadae haitaweza kuleta mgogoro wowote kati ya wanakijiji na muwekezaji.Aliongeza kuwa kwa sasa kati ya vijiji 12,545 nchi nzima ni vijiji 1645 ndiyo tayari vina mipango ya matumizi ya ardhi mpaka sasa. 

  Vijiji vingi bado havina mipango kutokana na ufinyu wa bajeti na kuwepo kwa kasi ndogo ya upangaji.Ndaro alisema lengo la mkutano huo wa wadau ni kuona ni namna gani  vijiji   vilivyobaki kati ya vijiji 12,545  vinapangiwa matumizi ya ardhi, kunakuwa na ushirikiano wa karibu wa wadau na namna vipi wanashirikiana kutatua migogoro ya ardhi ambayo inazidi kuongezeka.

  “Pamoja na kuwepo kwa kasi ndogo ya upangaji matumizi  ya ardhi, bado kuna changamoto ya kutoheshimu mipango ya matumizi ya ardhi iliyokwishaandaliwa ambapo  utakuta kijiji tayari kimepangwa lakini kinakuja kukatwa katikati na kuwa vijiji viwili au zaidi,”alisema  Alisema serikali inapaswa kuweka mipango ya matumizi ya ardhi ipasavyo ili kuweza kudhibiti hali ya migogoro ya ardhi kati ya watumiaji mbalimbali, mfano baina ya wawekezaji na wanavijiji kwa kupanga matumizi ya ardhi.“Serikali inapoita wawekezaji nchini inapaswa pia kuhakikisha mpango ya matumizi bora ya ardhi inayoeleweka kwa lengo la manufaa ya mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla,”alisema

  0 0


  0 0

    Mkurugenzi wa Idara ya Rasilimali Watu wa Kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Ltd, Hassan Dewji akizungumza wakati wa Kongamano la Ajira kwa Vijana waliomaliza  vyuo  ambao watapata fursa ya kupata ajira katika makampuni ya MeTL  Group, lililofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Alliance Francaise.(Habari picha na Modewjiblog).
   Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya MeTL Group, Fatema Dewji-Jaffer akizungumzia idara yake ya masoko inavyofanya kazi wakati wa Kongamano la Ajira kwa Vijana waliomaliza vyuo ambao watapata fursa ya kupata ajira katika makampuni ya MeTL  Group, lililofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Alliance Francaise.
   Mtaalamu wa kilimo wa kampuni ya MeTL Group, Bw. George Mwamakula akizungumza wakati wa Kongamano la Ajira kwa Vijana waliomaliza vyuo ambao watapata fursa ya kupata ajira katika makampuni ya MeTL  Group, lililofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Alliance Francaise.
   Mtaalamu wa masuala ya fedha wa MeTL Group, Bi. Hasina Ahmed akizungumza wakati wa Kongamano la Ajira kwa Vijana waliomaliza vyuo ambao watapata fursa ya kupata ajira katika makampuni ya MeTL  Group, lililofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Alliance Francaise.
    Mtaalamu wa idara ya uzalishaji wa nyuzi na nguo ya MeTL Group, Bw. Clement Munisi akizungumza wakati wa Kongamano la Ajira kwa Vijana waliomaliza vyuo ambao watapata fursa ya kupata ajira katika makampuni ya MeTL  Group, lililofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Alliance Francaise.


  Mtaalamu kutoka kitengo cha mauzo wa MeTL Group, Bw. Yusuf Ali, akizungumza kwenye Kongamano la Ajira kwa Vijana waliomaliza vyuo ambao watapata fursa ya kupata ajira katika makampuni ya MeTL  Group, lililofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Alliance Francaise.
   Mtaalamu wa idara ya uzalishaji na matengenezo wa MeTL Group, Bw. Vijay Raghavan akizungumza kwenye Kongamano la Ajira kwa Vijana waliomaliza vyuo ambao watapata fursa ya kupata ajira katika makampuni ya MeTL  Group, lililofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Alliance Francaise.

   Washiriki wakiuliza maswali juu uendeshaji wa vitengo mbalimbali vya makampuni ya MeTL Group wakati wa Kongamano la Ajira kwa Vijana waliomaliza vyuo ambao watapata fursa ya kupata ajira katika makampuni ya MeTL  Group, lililofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Alliance Francaise.

   Mkurugenzi wa Idara ya Rasilimali Watu wa Kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Ltd, Hassan Dewji akijibu maswali yaliyoulizwa na washiriki wa kongamano hilo.
   Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya MeTL Group, Fatema Dewji-Jaffer (katikati) akikabidhi box la zawadi kwa mmoja wa washiriki aliyejishindia kwenye mchezo wa kuokota majina wakati wa Kongamano la Ajira kwa Vijana waliomaliza vyuo ambao watapata fursa ya kupata ajira katika makampuni ya MeTL  Group, lililofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Alliance Francaise. Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Rasilimali Watu wa Kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Ltd, Hassan Dewji.

  Na Mwandishi Wetu
  Safari ya Kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group) kutoa ajira kwa Watanzania 100,000 hadi mwaka 2021 imeanza kufanyika kupitia Job Affairs ambapo limewapa nafasi wasomi mbalimbali nchini kutumia sehemu hiyo kuonyesha uwezo wao, na kati yao wasomi 25 wakipata nafasi ya kujiunga na familia ya zaidi ya wafanyakazi 28,000 wa kampuni ya MeTL Group.

  Wakizungumza na waandishi wa habari baada ya kufanyika kwa kongamano hilo, wasomi mbalimbali waliipongeza kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited kwa kufanya kongamano la Job Affairs kwani licha ya kutoa nafasi za kazi lakini pia limewasaidia kujijengea uwezo mpya ambao hawakuwa nao awali.
  Mmoja wa wasomi hao, Dennis Mtani alisema kupata nafasi ya kuhudhuria kumewajengea jambo lipya kuhusu jinsi ya kuomba nafasi za kazi hadi kuwa wafanyakazi bora katika kampuni.

  Alisema kutokana na ukubwa wa kampuni ya Mohammed Enterprises kwa bara la Afrika ni matarajio yao kuwa wamejifunza jambo ambalo hata kama hawatapata nafasi za kazi basi watabaki na uwezo ambao utawasaidia kujua jinsi ya kuomba nafasi katika makampuni mengine ya kimataifa.

  “Tumekuja katika kongamano hili wengine hata CV walikuwa hawajui jinsi ya kuandika ili kuomba nafasi na kuajiriwana na kutokana na ukubwa wa hii kampuni kwa nchi za Afrika tumepata elimu ambayo inaweza kutusaidia kwenda kufanya kazi kwa makampuni mengine,” alisema Mtani.

  Nae Monica Mziray alisema alijumuika katika kongamano hilo ili kujaribu kutafuta nafasi ya kujiunga na kampuni ya Mohammed Enterprises kwani anaamini ni kampuni kubwa ambayo anaamini ana ndoto za kuifanyia kazi na ambayo inawajali wafanyakazi wake.

  “Nimefanya kazi na kampuni zingine lakini niliacha sababu nataka kampuni ambayo inanilia vizuri na inanipa kitu na mimi naipa kitu, nilisoma historia ya Mohammed Enterprises, nimeona ni kampuni kubwa Afrika, nimeona bidhaa zake na naona inaweza niongezea kitu,” alisem Mziray.

  Aidha akizungumza wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo, Mkurugenzi wa Kitengo cha Rasilimali wa Mohammed Enterprises, Hassan Dewji aliwambia washiriki ambao wametoka katika taasisi mbalimbali za elimu ya juu, kwamba Idara ya Rasilimali Watu ya MeTL imekua ikitoa ajira, mafunzo ya kukuza vipaji kwa watanzania wa kada mbalimbali ili kuchukua nafasi za juu katika Makampuni shiriki ya MeTL.

  Kuhusu kongamano hilo la kazi alisema linalengo la kupata wasomi wenye taaluma mbalimbali kutoka kwa vijana wa Kitanzania. Kwamba Idara ya Rasilimali Watu imelenga kupata wahitimu katika nyanja za Uhasibu wa fedha, Rasilimali watu, Masoko, Uhandisi, Kilimo na Viwanda vya nguo lakini pia vijana wasomi watapewa mafunzo kwa kipindi cha wiki 52 huku wakiwa wanalipwa na watakapomaliza mafunzo watapewa ajira na kuingizwa katika mfumo wa uwajibikaji.

  “Kundi la Makampuni ya MeTL limepata umadhubuti wake kutokana na kuwa na utamaduni wa kuhakikisha kwamba wanakuwa karibu na wafanyakazi wake na kuwajali. Wafanyakazi wa Idara ya Rasimali Watu wamekua wakiandaa mafunzo kuboresha elimu ya wafanyakazi, maarifa na utaalamu,

  “Ushiriki wa wafanyakazi ni sehemu ya maono ya wafanyakazi wa Idara ya Rasilimali Watu katika kundi hili la makampuni. Kampuni hii huhakikisha kwamba wafanyakazi wanapata mapumziko, kujitengeneza upya, wanakuwa na siku ya familia, siku ya michezo na kwamba shughuli hizo zinafanywa kwa mpangilio ili kuwezesha kuwepo kwa utamaduni  wa familia moja  inayofanya kazi kwa kushirikiana kwa kiwango cha juu,” alisema Dewji.

  0 0

   Washiriki katika hali ya utulivu wakati wa mafunzo katka ukumbi wa Chuo Cha VETA mjini Dodoma.
   Washiriki wakifuatilia mafunzo, wanaoonekana mbele, kulia ni Dkt Lorah Madete (aliyevaa nguo za rangi ya bluu) na kushoto ni Bibi Angela Shayo (mwenye koti jeusi), wote (wawili) kutoka Tume ya Mipango.

   Washiriki katika hali ya utulivu wakati wa mafunzo katika ukumbi wa Chuo Cha VETA mjini Dodoma.
   Washiriki wakifuatilia wakimsikiliza mkufunzi (hayupo pichani) moja ya mada katika mafunzo ya Usimamizi na Utayarishaji wa Miradi ya Uwekezaji katika Sekta ya Umma.
   Mkufunzi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Dar Salaam, dkt. Kenneth Mdadila akiendesha mafunzo ya Usimamizi na Utayarishaji wa Miradi ya Uwekezaji katika Sekta ya Umma.
   Naibu Katibu Mtendaji kutoka Tume ya Mipango, Mhandisi Happiness Mgalula akitoa hotuba wakati akifungua mafunzo ya Usimamizi na Utayarishaji wa Miradi ya Uwekezaji katika Sekta ya Umma mjini Dodoma, Kulia ni mkufunzi wa mafunzo hayo, dkt. John Mduma kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kushoto ni Kaimu Naibu Katibu Mtendaji, Klasta ya Uchumi Jumla kutoka Tume ya Mipango dkt. Lorah Madete.
   Picha ya pamoja ya washiriki wa mafunzo ya Usimamizi na Utayarishaji wa Miradi ya Uwekezaji katika Sekta ya Umma kanda ya kati inayojumuisha mikoa ya Manyara, Singida na Dodoma.

  Na Adili Mhina, Dodoma.
  Tume ya Mipango imewashauri maofisa wa serikali wenye dhamana ya kusimamia miradi ya umma kuhakikisha wanatumia mbinu za kisasa katika kuchambua, kuchagua, kutekeleza na kusimamia miradi ya serikali ili kuhakikisha malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo yanafikiwa kwa wakati.

  Ushauri huo umetolewa jana mjini Dodoma na Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango anayesimamia Klasta ya Miundombinu na Huduma, Mhandisi Happiness Mgalula alipokutana na maofisa mipango wa Ofisi za  Mikoa na Halmashauri za kanda ya kati iliyojumuisha Mikoa ya Dodoma, Singida na Manyara kwa lengo la kutoa elimu katika kuandaa, kusimamia, na kutekeleza miradi ya Umma.

  Alisema kuwa Serikali ilifanya tathmini na kugundua kuwa hakuna vigezo vinavyofanana katika kuandaa na kuchagua miradi ya umma katika taasisi mbalimbali za Serikali kitu kinachorudisha nyuma juhudi za kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025.

  “Dira ya Taifa ya Maendeleo inaelekeza kuwa hadi kufikia mwaka 2025 Tanzania inatakiwa iwe inchi ya uchumi wa kati na kwa vile tumedhamiria kwa dhati kifikia hapo ni lazima tujipange upya na kutumia utaalamu wa kisasa na vigezo vinavyofanana katika kuchagua miradi yenye uwezo wa kulifikisha taifa huko,” alisema Mgalula.

  Kukosekana kwa vigezo vinavyofanana kumesababisha upungufu mkubwa katika  miradi ya umma huku  ikipelekea miradi mingine kukosa mikopo katika soko la mitaji la ndani au la kimataifa kutokana na kuwa na maandiko yasiyokidhi vigezo vinavyohitajika.
  Mgalula aliongeza kuwa ili kuwekeza katika miradi yenye tija itakayoharakisha Tanzania kuingia katika nchi za uchumi wa kati, Tume ya Mipango imedhamiria kuendelea na utaratibu wa kutoa mafunzo kwa walengwa nchi nzima ili kuongeza utaalam katika kuweka vipaumbele vichache vyenye ufanisi kwa kila mwaka wa bajeti kuliko kuwa na miradi mingi isiyokamilika.

  Na kwa upande wa maafisa wanaopata elimu hiyo wanakiri kuwepo kwa changamoto nyingi katika maandalizi ya miradi ya umma kutokana kukosekana kwa mfumo unaofanana katika uwekezaji wa miradi ya umma.

  “Tayari tumeanza kuelekezwa namna ya kuandaa miradi kwa kuzingatia vigezo vya kisasa viliyoainishwa katika mwongozo wa usimamizi wa uwekezaji wa miradi ya serikali, hii itatusaidia kuwa na utaratibu mmoja na unaoeleweka  tofauti na ilivyokuwa zamani ambapo kila mradi mpya ulikuwa na mfumo wake” Alisema Bwana Mkama kutoka Dodoma.

  Naye Afisa Mipango kutoka Halmashauri ya Babati Bw. Godlisten Geofray alieleza kuwa kuwepo kwa mfumo wa kisasa kutasaidia kuweka kumbukumbu sahihi za miradi hata ile ambayo haitafanikiwa kupata fedha kwa mwaka husika pale mfumo wa kanzidata utakapoanzishwa ambao utahifadhi kubukumbu za miradi yote nchini.

  Washiriki wa mafunzo hayo wameonesha kuridhishwa na juhudi zinazofanywa na Tume ya Mipango katika kutoa elimu hiyo katika ngazi mbalimbali huku wakieleza kuwa utaratibu huo utasaidia kuimarisha mawasiliano kwenye bajeti ya miradi kati ya serikali kuu na serikali za mitaa.

  Wataalamu hao wamesisitiziwa kuwa miradi yote itakayohitaji fedha za Serikali katika Bajeti italazimu kufuata utaratibu uliobainishwa katika Mwongozo wa Usimamizi na Utayarishaji wa Miradi ya Uwekezaji katika sekta ya Umma ili kuweza kuimarisha ufanisi na kupata thamani ya fedha.

  0 0


  Senpai Esther Thomas (kushoto) akipangua chudan tzuki (ngumi ya kifua) wakati semina hiyo ikiendelea.
  Anafundisha kwa mifano! Shihan Okuma akishambuliwa na Jerome Sensei kama sehemu ya maelekezo katika semina hiyo


  Na Daniel Mbega

  SEMINA kubwa ya Shotokan Karate kwa nchi za Afrika Mashariki, Kati na Kusini, imeanza leo hii jijini Dar es Salaam ambapo kwa mara ya kwanza katika historia ya mchezo huo nchini Tanzania, inaongozwa na mkufunzi mkuu, Shihan Koichiro Okuma (6th Dan), kutoka makao makuu ya chama cha karate cha Japan Karate Association/World Federation (JKA/WF), Tokyo, Japan.

  Semina hiyo – maarufu kama JKA/WF- Tanzania Southern, Central & East African Region Gasshuku – ambayo imeandaliwa na chama cha Japan Karate Association/World Federation-Tanzania (JKA/WF-Tanzania) ni ya nane kufanyika ambapo kwa mwaka huu inashirikisha makarateka 45 kutoka Zimbabwe, Zambia, Uganda, Kenya na wenyeji Tanzania.


  Kwa mujibu wa JKA/WF-Tanzania, semina hiyo ya wiki nzima inatarajiwa kufikia tamati Jumamosi.

  Makarateka ambao wameanza kushiriki leo hii, kutoka Tanzania ni Jerome Mhagama Sensei, Justine Limwagu, Seberian Dagila, Said O. Kissailo, Lulangalila Lyimma, Athumani Kambi, Mikidadi Kilindo Sensei, Marcus George, Khamis K. Sambuki, Hamis Said Mkumbi, Selemani A. Mkalola, Christopher William, Eliasa Mohammed, Adson Aroko Sensei, Nestory Federicko, Daniel Mbega, Willy Ringo Rwezaura Sensei, na Shihan Dudley Mawala Sensei, ambaye alikuwa mgeni mwalikwa.

  Makarateka wengine na nchi zao kwenya mabano ni Gibson Sangweni (Zimbabwe), Robert Chisanga (Zambia), Thobias B. Rudhal (Kenya), George Otieno (Kenya), Joshua Oude (Kenya), George Warambo (Kenya), George Okeyo (Kenya), Florence Kieti (Kenya), Asana Mahmoud Ulwona (Uganda), Ofubo Issa Yahaya (Uganda), Magezi Yasiin (Uganda), Wanyika Abdurahman (Uganda), Frederic Kilcher (Ufaransa) na Koichiro Okuma (Japan).

  Mkufunzi mkuu wa JKA/WF-Tanzania, Jerome George Mhagama Sensei (5th Dan), amesema hata hivyo kwamba, tofauti na miaka iliyotangulia, safari hii hakutakuwa na mashindano ili kutoa fursa kubwa kwa Shihan Okuma kufundisha vyema na kuwapandisha madaraja makarateka mbalimbali kuanzia ngazi ya Sho-Dan, Ni-Dan, San-Dan na Yon-Dan (1st – 4th Dan).

  “Tunataka tupate muda wa kutosha wa kufanya semina pamoja na mitihani, kwani mbali ya kuwapandisha madaraja makarateka mbalimbali, lakini pia kuna ambao watafanya mitihani ya ukufunzi na uamuzi wa kimataifa ili kupanua wigo na kupata walimu na waamuzi wa kutosha katika kanda yetu,” amesema Jerome Sensei, ambaye alipanda daraja Jumanne, Septemba 6, 2016 baada ya kufanya vizuri na kufaulu mtihani wa 5th Dan jijini Nairobi, Kenya chini ya Shihan Okuma.

  Hata hivyo, idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka kesho ambapo makarateka kutoka Zanzibar nao watahudhuria baada ya kushindwa leo kutokana na sababu mbalimbali.

  Jerome Sensei amesema kwamba, changamoto kubwa ambayo inawakabili wao pamoja na mchezo mzima wa Karate nchini Tanzania ni kuwekwa pembeni na wadau mbalimbali wa michezo ikilinganishwa na michezo mingine, hali ambayo imekuwa vigumu kwao kupata udhamini.
  Ameiomba Serikali na wadau wengine kuutupia macho mchezo huo, kwani unailetea sifa kubwa Tanzania kutokana na mafanikio ya mchezaji mmoja mmoja.
  Katika kipindi cha miaka takriban 10, Tanzania imekuwa kinara wa mchezo wa Karate katika kanda ya Afrika Mashariki, Kati na Kusini ukitoa Afrika Kusini pekee, hatua ambayo imechangiwa na mafanikio binafsi ya Jerome Sensei, ambaye kwa jitihada zake ameshiriki mashindano ya dunia ya Karate mwaka 2012 na kurudia raundi ya nne, mashindano ambayo yalifanyika Pataya, Thailand, ambapo alitolewa na mtu ambaye alikuja kuwa bingwa wa dunia.
  Mbali ya hivyo, ameshiriki mashindano mengine jijini Tokyo, Japan lakini pamoja na kutotwaa ubingwa, ameweza kupanda madaraja kwa viwango vya kimataifa na sasa ni mkufunzi, mtahini na mwamuzi wa kimataifa, ambapo ameweka rekodi ya pekee kwa kuwa mkufunzi mwenye umri mdogo kabisa katika historia ya JKA/WF tangu chama hicho kilipoanzishwa Mei 1947.
  Kwa mujibu wa rekodi za JKA/WF, Jerome Sensei (36) ni karateka wa pili wa Afrika Mashariki kuwa na hadhi ya Dan Tano (5th Dan) baada ya David Mulwa Sensei wa Kenya, hivyo ameteuliwa kuwa mkufunzi mwenza mkuu wa Afrika Mashariki.
  Akizungumza katika ufunguzi huo, Shihan Okuma, ambaye ametokea Kenya ambako kulikuwa na semina wiki iliyopita, amesema kuwa ujio wake siyo wa bahati mbaya bali umetokana na jitihada ambazo Tanzania imekuwa ikionyesha katika maendeleo ya Karate, hususan mafanikio yasiyo na kifani ya Jerome Sensei.
  “Nimetumwa na makao makuu kuja kuiunga mkono Tanzania pamoja na kufundisha semina hii, najua semina kama hii mara nyingi huwa inafanyika makao makuu tu au katika kanda maalum, lakini kwa vile Tanzania imeonyesha mafanikio makubwa, hatuna budi kuja hapa ili kuwapa fursa makarateka wengi waweze kushiriki.
  “Kuja Japan ni gharama kubwa, wengi hawawezi kumudu pamoja na kuwa na nia na mchezo huu, ni wachache tu ambao wanapata bahati ya kuja kuhudhuria, lakini hapa nimefurahi kuona kuna makarateka wengi wana viwango vya juu kabisa na hii ni faraja kubwa kwangu na kwa JKA/WF,” amesema.  Shihan Okuma akitoa neno kabla ya kuanza kwa semina leo hii mchana.
  Shihan Okuma akijiandaa kuanza darasa leo mchana. Kushoro ni Willy Ringo Rwezaura Sensei.
  Timu ya Kenya hii
  Makarateka wanapasha misuli.
  Heian Shodan Kata.
  Maelekezo kidogo.
  Picha ya pamoja.
  Haya ni maelekezo wakati darasa likiendelea. Semina za Karate huwa hazihitaji peni na daftari, ni uwanjani tu kwa vitendo, hakuna siasa.

  Kihon Kumite. Ukilemaa atakuvunja mbavu ohooo.
  Hapa Mwanakijiji Daniel Mbega (shoto) akiwa na Gubson Sangweni Sensei kutoka Zimbabwe wakati wanamsubiri Shihan Koichiro Okuma awasili Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam.
  Huyu jamaa kila wakati amekunja ngumi, tehee teheeee. Shihan Okuma akipozi baada ya kuwasili uwanja wa ndege jana.
  Nami Mwanakijiji nilikuwemo kuongoza convoy la Tanzania kumpokea Shihan Okuma.
  Jerome Mhagama Ssensei akifurahia jambo na Shihan Okuma.
  He. Wako wapi? Shihan Okuma alikuwa akiangaza huku na huko baada ya kuwasili kabla sijamnyooshea mkono.
  Pozi la makarateka.

  IMEANDALIWA NA www.maendeleovijijini.blogspot.com.

  0 0

  Apostle Onesmo Ndegi Kiongozi wa Kanisa la Living Water Center Kawe akimwombea Hudson Kamogaakiwa amepiga magoti .
  Waumini wa Kanisani Living Water Center Kawe wakiwa wamenyoosha mikono kwa Hudson Kamoga kuomba kwa ajili yake


  Mkurugenzi mteule wa Wilaya ya Mbulu, Hudson Kamoga

  Mkurugenzi mteule wa Wilaya ya Mbulu, Hudson Kamoga akiwa na Baba yake wa Kiroho Apostle Onesmo Ndegi Kiongozi wa Kanisa la Living Water Center Kawe akimsiliza kwa makini akielezea uteuzi wake.
  Mkurugenzi mteule wa Wilaya ya Mbulu, Hudson Kamoga akiwa na Baba yake wa Kiroho Apostle Onesmo Ndegi Kiongozi wa Kanisa la Living Water Center Kawe akimsiliza kwa makini akielezea uteuzi wake.


  ………………………………………………………………………………………………..
  Mkurugenzi mteule wa Wilaya ya Mbulu, Hudson Kamoga, ambaye ameteuliwa mwishoni mwa wiki jana amesema anaamini ni Mungu aliyemuweka kwenye nafasi hiyo ili awatumikie wananchi wa Mbulu kwa wakati huu.

  Akiongea kwenye ibada ya Jumapili hii ndani ya Kanisa la Living Water Center Kawe, wakati alipopewa nafasi na mtumishi wa Mungu Apostle Onesmo Ndegi ili asalimia Kanisa Mheshimiwa Kamonga alisema, anakwenda kwenye wilaya yenye changamoto nyingi za kimaendeleo ila anaamini Mungu atamwezesha kuzitatua kwa nafasi yake akishirikina na wananchi pamoja na viongozi wengine kati halimashauri ya Mbulu.
  Kamonga alisisitiza kuwa kwa kupata nafasi hii ya Ukurugenzi bado ataendelea na utumishi wake kwa Mungu maana anaamini huo ndio uliomfanyakufikia hatua hiyo,hivyo kuamua kuwa anamtanguliza Mungu kaika kila atakachokuwa anafanya,alisema Kamoga
  Pia alitoa shukurani za dhati kwa Mtumishi wa Mungu Apostle Ndegi pamoja na watumishi wengine kanisani hapo na kusema kuwa kati ya vitu ambavyo hawezi kuvisahau na malezi mazuri ya kiroho pamoja na mafindisho ambayo amekuwa akiyapata kutoka kwa Apostle Ndegi na watumishi wengine kanisani hapo, akisema mafundisho hayo yamesababisha kuwa vile alivyo sasa!
  Mwisho Mtumishi wa Mungu Mtume Onesmo Ndegi na waumini walifanya maombi kwa ajili yake ili Mungu aambatane naye katika utumishi wake kwenye nafasi hiyo ya Ukurugenzi!.

  0 0

  Tope zilizokuwa zimetuama katika mifereji ya kusafirisha maji taka katika kituo kikuu cha mabasi mjini Moshi zikiondolewa.
  Licha ya kuwepo na kampuni iliyopewa kandarasi ya usafi katika kituo kikuu cha mabasi cha mjini Moshi bado changamoto ya kuziba kwa mifereji ya kusafirisha maji taka imekuwepo .
  Wafanyakazi wa Mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira mjini Moshi (MUWSA) walishiriki kuzibua na kuondosha taka zote zilizokuwepo katika mifereji hiyo.
  Kitengo cha maji taka cha Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira mjini Moshi kilihusika zaidi kuhakikisha hakuna mfereji utakao kuwa umebaki na taka.
  Taka ngumu zote ziliondolewa katika mifereji hiyo.
  Baadhi ya wafanyabiashara katika kituo hicho kikuu cha mabasi walijitokeza pia katika kusaidia kufanya usafi .
  Wafanyakazi wa Mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira mjini Moshi (MUWSA) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukailisha zoezi la usafi katika kituo kikuu cha mabasi mjini Moshi.

  Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

  0 0

  Katika kipindi cha JUKWAA LANGU hii leo, tulizungumzia janga kuu la Tetemeko la ardhi nchini Tanzania.

  Wadau Baraka Galiatano wa BukobaWadau Blog na Erick Kimasha walijiunga nasi kwa njia ya Skype kutoka Tanzania kutupa taswira ya nini kilitokea, vipi kilipokelewa na maendeleo tangu Sept 10 na hali ilivyo hivi sasa mjini humo.

  Pia tuliungana na mmoja wa wanaharakati ambao wameanzisha mfuko maalum kuchangia wahanga wa tetemeko hilo Agnetta .

  Ungana nasi kuanzia saa 11 kamili jioni majira ya Marekani Mashariki (5:00pm ET) kupitia www.kwanzaproduction.com ama kupitia TuneIn tun.in/sfeLX
  Kwa walio Marekani na Canada piga 240 454 0093
  Karibuni

  0 0


  Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dkt. Laurean Ndumbaro akisoma risala kwa niaba ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mha. John W. H. Kijazi wakati wa Bonanza la uzinduzi wa Mashindano ya SHIMIWI kwa mwaka 2016 lililofanyika katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
  Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dkt. Laurean Ndumbaro akimkabidhi Kombe la mshindi wa kwanza Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Bi. Theresia Mmbando baada ya watumishi wa ofisi yake kuhudhuria kwa wingi zaidi ya taasisi zote katika Bonanza la uzinduzi wa Mashindano ya SHIMIWI kwa mwaka 2016 lililofanyika katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
  Washiriki wa Bonanza la uzinduzi wa Mashindano ya SHIMIWI kwa mwaka 2016 wakipita katika barabara ya Mandera kuelekea Uwanja wa Uhuru ikiwa ni sehemu ya bonanza hilo.

  0 0

  Hatimaye mvutano wa baadhi ya wanasiasa na wananchi kuhusu kuirejesha tena stendi kuu ya Mabasi kati kati ya mji wa Songea badala ya kuendelea kuwepo eneo la Msamala umefikia kikomo, Ni baada ya Kamati ya wataalamu mbalimbali wa Manispaa ya Songea kutoa ripoti yao ya utafiti na kupendekeza stendi ya Msamala kuwa kituo kikuu cha Mabasi.


older | 1 | .... | 969 | 970 | (Page 971) | 972 | 973 | .... | 1898 | newer