Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AONGOZA WANANCHI KUAGA MIILI YA MAREHEMU WALIOTHIRIWA NA TETEMEKO LA ARDHI MJINI BUKOBA,MKOANI KAGERA LEO

$
0
0
 WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameongoza maelfu ya wananchi wa Manispaa ya Bukoba mjini kuaaga miili ya watu 16 waliofariki kutokana na tetemeko la ardhi lililotokea jana (Jumamosi, 10 Septemba, 2016 mkoani Kagera.

Tetemeko hilo lilitokea jana Alasiri limesababisha vifo vya watu 16 na wengine 253 kujeruhiwa. Pia limesababisha maelfu ya wananchi kukosa makazi baada ya nyumba 840 kuanguka na nyingine 1264 zikipata nyufa yakiwemo majengo 44 ya taasisi mbalimbali za umma.

Kufuatia tukio hilo Waziri Mkuu ambaye alimuwakilisha Mheshimiwa Rais, Dk. John Magufuli amewaomba wananchi kuwa watulivu wakati Serikali ikiendelea kufanya tathmini ya athari zilizotokana na maafa hayo.

“Poleni sana tukio hili ni kubwa na halijawahi kutokea nchini. Haya yote ni mapenzi ya Mwenyezi Mungu. Tuendelee kuwa na imani na watulivu  Serikali ipo pamoja nanyi na haitawatupa mkono,” amesema.

Waziri Mkuu amesema Kamati ya Maafa ambayo ipo katika Ofisi ya Waziri ya Mkuu itakwenda wilaya za Kyerwa, Karagwe na Bukoba mjini kwa ajili ya kufanya tathmini na kubaini athari zilizosababishwa na tetemeko hilo na kuona namna ya kuwasaidia waathirika.

Wakati huo huo Waziri Mkuu amewaagiza viongozi wa mkoa huo kuchukua hatua za haraka kwa kuwatafutia eneo salama la kulala wanafunzi wa Shule ya Sekondari Nyakato ambayo mabweni yake yote yameathirika na tetemeko hilo na hayafai kutumika.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo baada ya kutembelea shule hiyo na kujionea namna mabweni ya shule hiyo yalivyopata nyufa hali iliyosababisha wanafunzi kulala uwanjani.

Pia Waziri Mkuu ameiagiza Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kuangalia kama kuna tetemeko linguine linaweza kutokea nchini ili Serikali iweze kuchukua tahadhari pamoja na kutoa elimu kwa umma namna ya kujikinga.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali Mstaafu, Salum Kijuu amesema kwa sasa wanaendelea na jukumu la kuwatafutia makazi wananchi ambao nyumba zao zimeanguka. Pia mkoa unaendelea kufanya tathmini ya kina kujua athari zilizosababishwa na tetemeko hilo.

Awali Waziri Mkuu alitembelea Hospitali ya Mkoa wa Kagera ambako majeruhi 170 wamelazwa na kutoa pole na kwamba anawaombea kwa Mwenyezi Mungu wapone haraka na wenye matatizo ambayo yanahitaji matibabu kwenye hoispitali kubwa Serikali itahakikisha wanapelekwa huko na kuhudumiwa.

 IMETOLEWA NA:              
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAPILI,SEPTEMBA 11, 2016

Waziri Mkuu Mh.Kassim Majaliwa akiwasili katika uwanja wa mpira wa Miguu wa Kaitaba mjini Bukoba mapema leo,kwa ajili ya kuwapa pole nyingi wakazi wa mji huo na kwingineko na pia kushiriki sala ya pamoja ya kuwaaga na kutoa heshima za mwisho kwa miili ya marehemu,waliokuwa wamekumbwa na tukio la tetemeko la Ardhi ambalo limetokea jana jioni na kupelekea idadi ya zaidi ya watu 15 akiwemo na mama mja mzito kupoteza maisha.

Tetemeko hilo kubwa la ardhi lenye mtikisiko wa kipimo cha Ritcher 5.7 limetokea jana Septemba 10, 2016 katika mikoa mitatu ya Kanda ya Ziwa kadhalika nchi za Burundi na Uganda.Mikoa ya Kanda ya Ziwa iliyopata athari kwa mujibu wa taarifa ni Mwanza, Mara na Kagera nchini na kuripotiwa kuua zaidi ya watu 15 na wengine zaidi ya 120 kujeruhiwa sambamba na kubomoa majengo mbalimbali.
Pichani kulia ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimuelekeza jambo Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salim Mustafa Kijuu ,kabla ya kuanza sala ya pamoja ya kuwaaga na kutoa heshima za mwisho kwa miili ya marehemu,waliokumbwa na tukio la tetemeko la Ardhi ambalo limetokea jana jioni na kupelekea idadi ya zaidi ya watu 15 akiwemo na mama mja mzito kupoteza maisha.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimuelekeza jambo Mbunge wa jimbo la BUkoba Mjini,Mh Wilfred Lwakatare,kabla ya kuanza sala ya pamoja ya kuwaaga na kutoa heshima za mwisho kwa miili ya marehemu,waliokumbwa na tukio la tetemeko la Ardhi ambalo limetokea jana jioni na kupelekea idadi ya zaidi ya watu 15 akiwemo na mama mja mzito kupoteza maisha. 

Baadhi ya ndugu na jamaa waliofika katika uwanja wa Kaitaba kushiriki sala ya pamoja ya kuwaaga wapendwa wao
Askofu Msaidizi wa Jimbo la Bukoba, Methodius Kilaini akisoma majina ya masanduku yaliyobeba miili ya marehemu,tayari kwa kuagwa kwa pamoja katika uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba mkoani Kagera.
Askofu Msaidizi wa Jimbo la Bukoba, Methodius Kilaini akiwa na baadhi ya viongozi wengine wa dini wakitazama majina ya masanduku yaliyobeba miili ya marehemu,tayari kwa kuagwa kwa pamoja katika uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba mkoani Kagera.
Askofu Msaidizi wa Jimbo la Bukoba, Methodius Kilaini akiwa na baadhi ya viongozi wengine wa dini wakiwa katika uwanja wa Kaitaba kushiriki sala ya pamoja ya kuaga miili ya marehemu waliokumbwa na tetemeko la Ardhi hapo jana mjini Bukoba mkoani Kagera.
Baadhi ya Masanduku yenye miili ya marehemu walioathiriwa na tetemeko la Ardhi hapo jana mjini Bukoba mkoani Kagera.

 






















UVCCM WATOA POLE TETEMEKO LA ARDHI

$
0
0
UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), umetuma salamu za pole wananchi wa mkoa wa Kagera kutokana na vifo vya zaidi ya watu 11 vilivyosababisha na tetemeko la ardhi lililotokea juzi.

Katika salamu hizo zilizotolewa na Kaimu Katibu Mkuu wa UVVCM, Shaka Hamdu Shaka kwa niaba ya umoja huo, alisema wamepokea kwa masikitiko na huzuni kubwa taarifa ya vifo hivyo.

Alisema tetemeko hilo ni pigo kwa UVCCM na taifa kwa ujumla kwa kuwa limesababisha vifo vya watu ambao ni nguvu kazi ya taifa pia kusababisha hasara kutokana na uharibifu wa mali mbalimbali na makazi.

"UVCCM tumepokea kwa mshituko mkubwa tukio hilo kubwa na zito ambalo limesababisha maafa na hasara kwa taifa,"alisema.

Alisema umoja huo unawaombea marehemu wa tukio hilo wapate pumziko la milele peponi na kuwaombea majeruhi wapone haraka na kurudi kwenye shughuli zao za kawaida.

"Katika kipindi hiki kigumu Jumuia yetu inaungana na Watanzania wengine kuzipa mkono wa pole familia zote zilizopoteza ndugu zao na pia tukiwafariji wote waliopata hasara ya kuharibikiwa nyumba zao na kupoteza mali,"alisema.

Alisema janga hilo ni limemgusa kila mtanzania mwerevu mwenye upendo na uzalendo hivyo linapaswa kuwaweka pamoja Watanzania wote ili kufarijiana na kukabiliana na magumu yaliyotokea.

Aidha, Shaka alisema wanatoa mkono wa pole kwa Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli kutokana na vifo hivyo na kasara iliyopatikana.

Shaka aliwashukuru na kuwakupongeza viongozi wa umoja huo walioko mkoani humo wakiongozwa na Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Kagera Yahya Kateme, kwa ushirikiano walioendelea kuutoa baada ya kutokea kwa tukio huilo.

Huu si wakati wa siasa bali ni kipindi kigumu cha kukabili yale yote yaliotokea na kudhuru au kuharibu taaswira iliokuwepo awali ya ustawi wa maisha ya wenzetu ambao wamepatwa na janga hilo.

Kila kijana mzalendo ni vyema akaenda kuripoti kwa viongozi wa maeneo husika aidha wakuu wa wilaya au mkoa ili kupewa maelekezo na miongozo katika kila hatua ya kusaidiana kwa hali na mali wakati wote hadi hali itakaporejea kama kawaida.

WAZIRI MBARAWA AZINDUA GATI JIPYA PANGANI MKOANI TANGA LILILOGHARIMU ZAIDI YA BILIONI 3

$
0
0

Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano,Proffesa Makame Mbarawa akizundua gati jipya la Bandari ya Pangani ambalo liligharimu zaidi ya bilioni 3 kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano wa mwisho kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari nchini (TPA)Karim Mattaka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella

Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano,Proffessa Makame Mbarawa akiwa na viongozi mbalimbali akisoma maelekezo yaliyoandikiwa kwenye jiwe la msingi mara baada ya kufanya kuzindua gati jipya la Bandari wilayani Pangani kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) Karim Mattaka kulia ni Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga,Henry Arika,Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella na PRO wa Mamlaka ya Bandari ya Tanga,Moni Jarufu.

Kulia ni Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano,Proffessa Makame Mbarawa akiteta jambo na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA)Karim Mattaka wapili kutoka kulia wakati wa uzinduzi wa gati jipya wilayani Pangani katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella kulia ni Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga,Henry Arika akifuatilia mazungumzo hayo







WAZIRI wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano,Proffesa Makame Mbarawa akisisitiza jambo kwa Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) Karim Mattaka wakati alipofanya ziara ya kuzindua gati mpya wilaya ya Pangani Mkoani Tanga katikati ni Meneja wa Tanroad Mkoani Tanga,Mhandisi Alfred Ndumbaro 


Viongozi waliokaa meza mkuu wakifuatilia matukio yaliyokuwa yakiendelea wakati wa uzinduzi wa Gati Jipya wilayani Pangani

Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga (RAS) Mhandisi Zena Saidi na Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM),Jumaa Aweso wakifuatilia hafla ya uzinduzi wa Gati jipya wilayani Pangani
Viongozi mbalimbali wa Halmashauri ya wilaya ya Pangani na mkoaani Tanga wakifuatilia uzinduzi wa Gati jipya

Baadhi ya watumishi wa Mamlaka ya Bandari Mkoani Tanga wakifuatiliaa uzinduzi huo kutoka kulia ni PRO wa Mamlaka hiyo,Moni Jarufu kushoto ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga,Daudi Mayeji

Baadhi ya Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani wakifuatilia uzinduzi wa Gati hiyo



Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano,Proffessa Makame Mbarawa akisalimiana na wananchi wilayani Pangani mara baada ya kuzindua gati jipya

Rais Magufuli kuwasili Lusaka Zambia kesho kwa ziara ya siku tatu

$
0
0




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kesho tarehe 12 Septemba, 2016 anatarajiwa kuwasili Mjini Lusaka nchini Zambia kwa ziara ya siku tatu ambapo pamoja na mambo mengine atahudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais Mteule wa Sita wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Chagwa Lungu zitakazofanyika keshokutwa tarehe 13 Septemba, 2016 katika Jiji la Lusaka.

Rais Magufuli anafanya ziara hii ya kwanza nchini Zambia akiwa pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Siasa,Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC).

Kamati hiyo inajulikana kwa jina la SADC-Troika.

Dkt. Magufuli alipokea kijiti cha Uenyekiti wa SADC-Troika kutoka kwa Rais wa nne Jamhuri ya Msumbiji Mhe. Filipe Jacinto Nyusi katika Mkutano wa 36 wa SADC uliofanyika katika Jiji la Mbabane nchini Swaziland tarehe 01 Septemba, 2016.

Katika Ziara hii Rais Magufuli anatarajiwa kukutana na Viongozi mbalimbali wa nchi za Afrika watakaohudhuria sherehe hizo zitakazofanyika katika Uwanja wa Mashujaa Jijini Lusaka.
 
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Lusaka
11 Septemba, 2016

SHULE YA SOUTHERN HIGHLANDS MAFINGA YAWAONDOA HOFU WAZAZI

$
0
0
dre
Mwanafunzi  aliyeongoza masomo yote Rahma Mdea akipokea cheti chakuhitimu darasa la  saba na zawadi yake  wakati wa mahafali ya  shule ya  Southern Highlands Mafinga
Mwanafunzi  aliyeongoza masomo yote Rahma Mdeka akipokea cheti cha kuhitimu darasa la  saba na zawadi yake  wakati wa mahafali ya  shule ya  Southern Highlands Mafinga mkur
 Mkurugenzi wa shule za Southern Highlands Mafinga ,Mary  Mungai  kulia akitambulisha watumishi  wa  shule  hiyo.
………………………………….
Na MatukiodaimaBlog 

UONGOZI wa  shule ya  Southern Highlands Mafinga  wilayani  Mufindi umewataka wazazi  wa  wanafunzi zaidi ya 50 waliofanya mtihani wa Taifa  wa darasa la  saba katika shule   hiyo  kuanza  kuwa na uhakika  wa watoto wao  kufaulu mtihani   huo .

Huku ukiahidi  kutoa kuchangia sehemu ya ada kwa  wanafunzi watakajiunga na shule ya sekondari  ya  Southern Highlands Mafinga kama  sehemu ya ahsante kwa  ushirikiano  ambao  wazazi  wamekuwa  wakitoa kwa shule hizo.

Mkurugenzi mtendaji wa Southern Highlands Mafinga  Mary  Mungai  aliyasema haya jana  wakati wa mahafali ya darasa  la  saba  shuleni  hapo .

“Shule hii ilianza mwaka 1994 kama Day Care na Pre-School. Mwaka 1997 ikakuwa na kuanza shule ya msingi-Primary School mwaka 2001 shule ilitoa wanafunzi wa kwanzawa darasa la saba wanafunzi walikuwa 17,wote walifauru vizuri na wote  walichaguliwa kuendelea na masomo ya kidato cha kwanza Katika matokeo ya mitihani ya darasa la 7 ya mwaka 2001 Southern Highlands School ilishika nafasi ya kwanza kitaifa katika mitihani yasomo la kiingereza ”

Alisema kuwa matokeo mazuri ya wanafunzi wote kufaulu mitihani ya kitaifa ya darasa la saba yamekuwa ni kawaida  kwa  shule   hiyo na  kuwa  toka kuanzishwa kwake haijapa pata  kufelisha hata  mwanafunzi  mmoja .

Hivyo kuwataka  wazazi  kutokuwa na hofu  juu ya  wanafunzi hao  waliofanya mtihani mwaka  huu kwani waanze  kujiandaa kwa kuwapeleka  sekondari.

Wakati huo   huo mkurugenzi wa familia  ya Lucy Chawe inayoishi nchini marekani na Tanzania  imepongeza jitihada za  shule  hiyo na  kuahidi kuendelea  kuiunga mkono  serikali kwa  kuhamasisha masomo ya Sayansi na Hisabati kwa  wanafunzi 

Mkurugenzi wa The Chawe Foundation Award , Kitove Mungai  alisema  kuwa  kila mwaka  wamekuwa wakitoa  zawadi kwa  wanafunzi wa Awali   hadi  darasala  saba ambao wamekuwa  wakifanya vizuri masomo ya  Hisabati na sayansi .

Aliwataja wanafunzi  ambao  wamepewa  zawadi hiyo kwa mwaka  huu kuwa ni Brayan Mgomapayo, Rahma Mdeka na Ayub Toss ambao  walifanya  vizuri katika hesabu .

Wakati katika  sayansi wanafunzi waliopewa  zawadi ni  Nimrod Nyakunga , Rahma Mdeka na Erick Mwanjelwa .

ZIARA YA WAZIRI NAPE NA RIPOTI KAMILI YA TFF

$
0
0

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye



Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Jamal Malinzi.

………………………………………………………………………..

Ripoti ya mwenendo wa mpira wa miguu Tanzania na mipango yake inayofanywa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imemfurahisha Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye hivyo moja kwa moja akaupongeza uongozi wa Rais Jamal Malinzi akisema unafanya kazi kubwa.

Kutokana na ripoti hiyo, Nape ambaye ni Mbunge wa Mtama mkoani Lindi, aliridhia wadau wa mpira wa miguu kusapoti timu za taifa hususani Serengeti Boys – timu ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 ambayo kwa sasa imepiga kambi Shelisheli kujiandaa kuivaa Congo-Brazzaville Jumapili ijayo.

Serengeti Boys inawania kucheza Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana wenye umri katika fainali zitakazofanyika Antananarivo, Madagascar sawa na timu ya taifa ya soka la ufukweni ambayo inatarajiwa kusafiri kwenda Abidjan, Ivory Coast kucheza mchezo wa pili wa kuwania kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa mchezo huo.

Timu nyingine ya taifa ni ile ya wanawake ya Tanzania Bara maaarufu kwa jina la ‘Kilimanjaro Queens’ ambayo kwa sasa iko Uganda kuwania taji la Chalenji ikishirikisha timu za taifa za Afrika Mashariki katika michuano ya inayotarajiwa kufanyika jijini Jinja kwa siku tisa kuanzia Septemba 11, mwaka huu.

Nape amefurahishwa na mipango ya TFF baada ya kupeleka timu zote kushiriki michuano mbalimbali kwa vipindi mbalimbali na kwamba Serikali itasapoti lakini hapo baadaye baada ya kufuata taratibu mbalimbali baada ya Rais Malinzi kumfafanualia kuwa gharama za kuendesha mpira kwa mwaka zinafika shilingi bilioni 15, na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) huchangia asilimia tatu (3) tu ya bajeti nzima kwa mwaka.

“Kwa kuanzia msimu huu tu, FIFA imeongeza na sasa itafika asilimia 6 kwa mwaka,” alisema Malinzi jambo ambalo lilimshangaza Nape ambaye leo Septemba 10, 2016 alifanya ziara ya kutembelea TFF kujionea hali halisi na kushangazwa na taarifa za vyanzo mbalimbali zinazotuhumu shirikisho.

Nape alisema: “Serikali inasapoti maendeleo, lakini lazima yafuate taratibu, kanuni na sheria za soka.”

Katika eneo la kufuata taratibu, kanuni na sheria za soka hatua nyingine, Nape alitaka Malinzi na kamati zake kuwa wakali kwa kuwa huwa hawachui hatua mapema, inatokea wadau kutaka kuipanda kichwani TFF.

“Naagiza mchukue hatua mapema kukamua majipu kabla hajajaiva. Sasa ninyi mnasubiri kwa muda mrefu kabla ya kuchukua hatua, ndiyo maana wanawasumbua. Washughulikieni mapema, mkiwabana mapema watakaa kimya, kanuni mnazo, sheria mnazo, wabaneni,” alisema Nape.

Katika hatua nyingine, Nape alisema kwamba kuna mchakato unaendelea kwa sasa ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuhakikisha kwamba wanarejesha mamlaka ya kumiliki baadhi ya viwanja vya soka Makao Makuu ya chama badala mikoa ambako wamegundua kuwa kuna matatizo makubwa katika menejimenti.

NA HIZI NDIZO SALAMU ZA RAIS WA TFF, JAMAL EMIL MALINZI KWA MHESHIMIWA NAPE NNAUYE WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO UWANJA WA KARUME TAREHE 10 SEPTEMBA 2016

Mheshimiwa Waziri,

Nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa kutukutanisha hapa leo.

Ni jambo la heshima na furaha kubwa sana kwetu sisi wanafamilia ya mpira wa miguu Tanzania kwa kutembelewa na wewe Mheshimiwa Waziri na ujumbe wako. Mheshimiwa ahsante sana kwa tukio hili adhimu na karibu sana kwenye makazi ya mpira “home of football”.

Mheshimiwa Waziri tunashukuru kwamba umeweza kutembelea eneo letu na kujionea wapi huwa tunafanyia shughuli zetu mbali mbali za kuendeleza michezo.

Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF limesajiliwa chini ya sheria ya baraza ya mwaka 1967 na marekebisho yake ya mwaka 1971 na madhumuni yake makuu ni kuendeleza na kusimamia mpira wa miguu Tanzania. Katika kutekeleza azma hii shughuli zetu tumezigawanya katika maeneo makuu matano:


Utawala

Shughuli za kila siku za uendeshaji wa mpira wetu zinasimamiwa na Sekretariet ya TFF inayoongozwa na Katibu Mkuu Ndugu Mwesigwa Selestine. Chini yake ana vitengo vikuu vitano: Ufundi ambacho kinasimamia maendeleo ya mpira, Mashindano ambacho kinasimamia mashindano mbali mbali, Fedha na utawala, Sheria na vyama wanachama na cha tano ni cha biashara na masoko. Vitengo hivi kwa pamoja vinashirikiana kuhakikisha mpira unafundishwa, unachezwa na unasimamiwa vyema. Aidha zipo Kamati mbali mbali zinazotusaidia kutushauri kwenye mambo ya kitaalam na kutoa maamuzi vikiwa vyombo huru. Pia tunacho chombo chetu kinachoitwa Bodi ya Ligi kinachosimamia uendeshaji wa ligi zetu kuu tatu Ligi kuu ya daraja la kwanza na ya daraja la pili. Ligi kuu ya vilabu vya wanawake inaendeshwa na kamati ya mpira wa wanawake.
Mashindano

Ili mpira uchezwe inabidi kuwepo na mashindano. Wakati wote TFF inafanya jitihada za kubuni mashindano mapya na kuhakikisha yaliyopo yanafanyika kwa mujibu wa kalenda. Kwa sasa TFF tunaendesha mashindano makuu ya kitaifa saba: Ligi kuu, Ligi daraja la kwanza, Ligi daraja la pili, Ligi ya mikoa, Kombe la Shirikisho, Ligi ya vijana na Ligi ya vilabu vya wanawake. Ukiondoa ligi daraja la pili na ligi ya mikoa mashindano yaliyobakia yote yanaonekana moja kwa moja kwenye (live) kwenye Televisheni. Shirikisho liko mbioni kuanzisha mashindano ya vilabu nane bora vya ligi kuu (Super 8). TFF pia huwa inasimamia mechi mbali mbali za kimataifa za mashindano na za kirafiki kwa timu za Taifa za rika mbali mbali za wanawake na wanaume.
Masoko na Biashara

Kuendesha mpira ni gharama kubwa. Wastani wa bajeti ya Shirikisho ni shilingi bilioni kumi na tano kwa mwaka.Tunawashukuru FIFA ambao hadi mwaka jana walikuwa wanachangia asilimia 3% ya bajeti hii na kuanzia mwaka huu wanachangia asilimi 6% ya bajeti hii. Jitihada kubwa zimekuwa zikifanyika kuhakikisha shughuli za uendeshaji wa mpira hazikwamishwi na ukosefu wa fedha. Kitengo cha biashara na masoko kinafanya jitihada kubwa kuhakikisha kila shindano letu linakuwa na udhamini hata kama sio wa kukidhi mahitaji yote.
Miundombinu

Ni muhimu sana kuwa na miundo mbinu ya kutosha na yenye sifa ya kuchezewa mpira. Kwa kushirikiana na wamiliki mbali mbali wa viwanja vya mpira TFF tumekuwa tukitoa ushauri wa namna ya kuendeleza na kutunza viwanja vyetu vya mpira ili vifae kuchezewa mpira wa kisasa. Aidha tunashukuru Halmashauri ya jiji la Tanga kwa kuiipatia TFF miliki ya eneo la ekari 18 jijini Tanga, kwa kushirikiana na FIFA eneo hilo litajengwa kituo cha kukuza na kuendeleza vipaji vya mpira cha TFF. Michoro yake iko katika hatua za mwisho za maandalizi.
Maendeleo ya mpira wa miguu.

TFF tumejiwekea malengo mawili makuu: Kucheza fainali za dunia mpira wa miguu wa wanawake Paris mwaka 2019 na kucheza fainali za kombe la dunia wanaume mwaka 2026.

Kwa upande wa mpira wa wanawake katika kufikia azma hii mwaka huu tunaanzisha ligi kuu ya vilabu vya mpira wa wanawake (Tanzania Women Premier League). Kutokana na ligi hii vipaji vitaibuliwa kwa ajili ya kuimarisha kikosi cha timu yetu ya Taifa Twiga stars. Kikosi hiki mwakani kitakuwa kikikusanywa mara kwa mara, kufanya mazoezi na kucheza mechi za kirafiki za kimataifa ili kujiandaa na hatua za awali za kombe la dunia mwaka 2018.

Kwa upande wa maandalizi ya Taifa stars kuelekea mwaka 2026 tayari program yetu imeanza kwa kuwa na Serengeti Boys ambayo inapambana kucheza fainali za vijana za Afrika mwakani umri chini ya miaka 17. Kwa sasa kikosi hiki kiko kambini Seychelles kujiandaa na mechi dhidi ya Kongo tarehe 18 Septemba . Timu hii pia ndiyo itapambana kucheza fainali za Afrika za vijana umri chini ya miaka 20 mwaka 2019. Aidha kwenye shule ya Alliance huko Mwanza tayari tuna kikosi cha awali cha timu ya Taifa cha vijana umri chini ya miaka 15 ambacho kinaandaliwa kucheza fainali za Afrika umri chini ya miaka 17 mwaka 2019. Tanzania tutakuwa wenyeji wa fainali hizi kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu.

Pia mwaka huu tunaanzisha ligi ya Taifa ya vijana umri chini ya miaka 20. Kutokana na ligi hii mwakani itaundwa timu ya Taifa ya awali ya vijana umri chini ya miaka 23 itakayopambana mwaka 2019 kutafuta fursa ya kucheza fainali za Olimpiki Tokyo mwaka 2020. Kutokana na makundi haya makuu matatu kuanzia mwaka 2021 walimu wetu wa mpira wataweza kuanza kutengeneza kikosi imara cha Taifa stars kuelekea Fainali za Kombe la dunia 2026. Gharama kubwa zinahitajika kugharimia program hizi na tunaomba Serikali na wadau wengine mtushike mkono ili tufikie azma yetu ya kucheza World Cup 2026.

Mheshimiwa Waziri ninaomba nigusie uendeshaji wa ligi yetu kuu na utoaji wa leseni za vilabu.Kama nilivyosema hapo awali Ligi kuu inasimamiwa na bodi ya ligi kwa maelekezo ya kanuni za mashindano kama zinavyopitishwa na kamati ya Utendaji kila mwaka. Mheshimiwa Waziri kinacholiongoza Shirikisho katika uendeshaji wa ligi kuanzia usajili, upangaji wa ratiba,upangaji wa waamuzi na utoaji wa adhabu ni kwa mujibu wa kanuni tulizojiwekea na kauli mbiu ya #fairplay,haki mchezoni.

Ninaomba nieleze pia kuwa kufuatia maagizo ya FIFA sasa tupo hatua za awali za kutoa leseni kwa vilabu zinazohalalisha vilabu kushiriki katika ligi. Mahitaji makuu ya leseni hizi ni klabu kuwa na menejimenti na kumbukumbu za mahesabu yake ya fedha ,kuwa na maeneo ya kufanyia mazoezi na kucheza mechi,kuwa na program za maendeleo ya mpira wa vijana na mwisho kueleza kinagaubaga nani anamiliki na kuendesha shughuli za kila siku za za klabu (ownership and control). Katika hili la umiliki ni marufuku klabu zaidi ya moja katika ligi moja kumilikiwa na mtu au mamlaka moja. Pia kanuni ya leseni za vilabu ina kipengele cha kipimo cha sifa cha nani anaruhusiwa kumiliki au kuendesha klabu ya mpira wa miguu , mipaka ya mamlaka yake na mahusiano na Shirikisho na mamlaka nyingine za juu zikiwemo Serikali,FIFA,CAF na CECAFA.

Mheshimiwa Waziri, ninaomba nimalizie kwa kukushukuru tena kwa kuchukua muda wako kuwa na sisi leo. Familia ya mpira wa miguu Tanzania inafarijika sana unapokuwa karibu na sisi na tunaahidi kuendelea kudumisha nidhamu katika utendaji wetu na kutoa ushirikiano wa karibu kwa Serikali yetu, vyombo na mamlaka nyingine.

PROF.MBARAWA AZINDUA KIVUKO CHA MV .TANGA NA GATI YA BANDARI YA PANGANI

$
0
0
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa pamoja na watendaji wa Serikali na Wizara wakikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Kivuko cha Mv. Tanga kulia ni Mkuu wa wilaya ya Pamgani Mhe. Zainabu Abdallah Issa .
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa pamoja na watendaji wa Serikali na Wizara wakizindua Gati la Bandari ya Tanga.Ukamilifu wa Gati hiyo utasaidia Meli mbalimbali kuweza kutia nanga wilayani Pangani.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa pili kulia) akisafiri na wakazi katika Kivuko cha Mv.Tanga kutoka Pangani kwenda Bweni mara baada ya uzinduzi. Wanne kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo (Sekta ya Ujenzi) Eng. Joseph Nyamhanga.

Mbunge wa Jimbo la Pangani Mhe. Jumaa Awesu akizungumza na wananchi wa Jimbo hilo katika uzinduzi wa Kivuko cha Mv. Tanga na Gati ya bandari ya Pangani uliofanyika Mkoani Tanga.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) Eng.Karim Mattaka akisoma taarifa ya ujenzi wa Gati ya bandari ya Pangani kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (hayupo pichani) katika uzinduzi wa Kivuko cha Mv. Tanga na Gati hiyo uliofanyika Mkoani Tanga.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Ndg. Martin Shigela akielezea taarifa ya utekelezaji wa Miradi ya Miundombinu katika Mkoa wa Tanga kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (hayupo pichani) katika uzinduzi wa Kivuko cha Mv. Tanga na Gati hiyo uliofanyika Mkoani Tanga.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akifafanua jambo kwa wananchi wa Pangani katika uzinduzi wa Kivuko cha Mv. Tanga na Gati hiyo uliofanyika Mkoani Tanga.

Wananchi wa Pangani wakishangilia ujio wa Kivuko kipya cha Mv. Tanga Wilayani hapo kinachotoa huduma ya usafirishaji kati ya Pangani na Bweni.


…………………………………………………………………

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amezindua kivuko kipya na cha kisasa cha Mv. Tanga kinachotoa huduma ya usafirishaji kati ya Pangani na Bweni na kuzindua Gati ya Bandari ya Pangani wilayani pangani mkoani Tanga.

Akizungumza katika uzinduzi huo Waziri Mbarawa amesema kuwa ujio wa kivuko hicho utafungua fursa za kibiashara na kuchochea maendeleo ya kiuchumi wilayani hapo.

“Naamini ujio wa kivuko hiki utarahisisha huduma za kijamii na maendeleo ya kiuchumi wilayani hapa, hivyo naomba mkitunze vizuri kivuko hiki ili kiweze kudumu kwa muda mrefu”, amesema Prof.Mbarawa.50 242

Ameongeza kuwa katika kuhakikisha huduma za kivuko zinakuwepo muda wote wilayani hapo, Serikali kupitia Wizara hiyo imetenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa boti ambayo itatumika kama mbadala wa usafiri wakati wa usiku katika maeneo hayo ambapo kivuko cha Mv.Tanga hakifanyi kazi.

Kuhusu ujenzi wa Gati ya bandari ya Pangani Waziri Mbarawa ameseama kuwa ujenzi wa gati hiyo utapelekea Meli kubwa kuweza kutia nanga na kurahisisha usafiri wa moja kwa moja kutoka Pangani kwenda visiwa vya Unguja na Pemba.

Amefafanua kuwa Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wataanzisha huduma ya boti za haraka kutoka Pangani kwenda Mkokotoni Zanzibar hivyo kufungua fursa za kibiashara na kitalii baina ya Tanga na Zanzibar.

Kwa upande wa huduma za mawasiliano ya simu wilayani hapo, Prof.Mbarawa amesema kuwa huduma hiyo itaanza mwezi Desemba mwaka huu kwa mkandarasi kufika na kuanza ujenzi wa miundombinu ya simu na hivyo kuondoa tatizo la mawasiliano wilayani hapo.

Katika hatua nyingine Prof. Mbarawa amehahidi kuanza ujenzi wa Barabara ya Tanga-Pangani-Saadani hadi Bagamoyo (KM 242) kwa kiwango cha lami ifikapo mwakani.

Amefafanua kuwa ujenzi wa barabara hiyo utakuwa wa awamu ili kuweza kuharakisha kukamilika kwake ambapo awamu ya kwanza itahusisha kipande cha barabara ya Tanga- Pangani (KM 50) na kuongeza kuwa ujenzi wa barabara hiyo utafungua fursa za kiuchumi kati ya Tanga na Pangani.

“Naahidi kujenga barabara hii ambayo ni kiungo kati ya Tanga na Pangani, naamini ukamilifu wake utalete maendeleo mkoani hapa”. Amesisitiza Prof. Mbarawa.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Eng.Joseph Nyamhanga amezipongeza kampuni za Songoro Marine na Alpha Logistic kwa kumaliza kwa wakati ujenzi wa kivuko na Gati ya bandari hiyo.

Naye Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Eng.Manase Ole-kujan amesema kuwa kivuko cha Mv.Tanga kimejengwa kwa sh.bilioni nne ambapo kina uwezo wa kubeba tani 50 abiria 100 na magari madogo 6 kwa wakati mmoja.

Ujenzi wa Kivuko cha Mv. Tanga ni moja ya utekelezaji wa ahadi ya Mhe.Rais Dkt.John Pombe Magufuli aliyoitoa wakati wa kampeni ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 wilayani Pangani Mkoani Tanga.

MKUU WA MKOA WA RUVUMA,DKT.MAHENGE AZINDUA VODASHOP MJINI SONGEA

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,Dkt. Binilith Satano Mahenge(wanne kutoka kushoto)akikata utepe mwishoni mwa wiki kuashiria uzinduzi rasmi wa Duka jipya la Vodacom Tanzania lililopo songea mjini.Wengine katika picha ni baadhi ya wafanya kazi wa kampuni hiyo. 
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,Dkt. Binilith Satano Mahenge,akikata keki ikiwa ni ishara ya kuzindua rasmi Duka jipya la Vodacom Tanzania lililopo songea mjini mwishoni mwa wiki. 
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,Dkt. Binilith Satano Mahenge(kulia)akipokea zawadi toka kwa Mkuu wa Vodacom Tanzania kanda ya Ruvuma, Amos Vuhahula(kushoto) mara baada ya kuzindua rasmi Duka jipya la kampuni hiyo lililopo songea mjini mwishoni mwa wiki.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,Dkt. Binilith Satano Mahenge,akigonganisha glasi na baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania,Baada ya kuzindua rasmi Duka jipya la Vodacom Tanzania lililopo songea mjini mwishoni mwa wiki. 
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,Dkt. Binilith Satano Mahenge,akisisitiza jambo wakati wa hafla fupi ya uzindua wa Duka jipya la Vodacom Tanzania lililopo songea mjini mwishoni mwa wiki.
Hili ndilo duka jipya la Vodacom Tanzania lililopo Songea mjini.

Dumisheni Michezo kuongeza ufanisi katika kazi; Katibu Mkuu Kiongozi.

$
0
0
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi
 Na Shamimu Nyaki WHUSM. 

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi amewataka Watumishi wa Umma kushiriki katika Michezo mbalimbali ili kuwa na afya imara itakayosaidia ufanisi katika kutekeleza kazi zao. 

Balozi Kijazi ametoa rai hiyo leo Jijini Dar es Salaam katika hotuba yake iliyosomwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Utumishi Dk.Lawrence Ndombaro katika Bonanza la Michezo la ufunguzi wa mashindano ya thelatini na nne yanayojulikana kama SHIMIWI lililofanyika katika Uwanja wa Uhuru wa Jijini humo. 

“Michezo inasaidia mwili kuwa na afya njema na kuondoa msongo wa mawazo pamoja na kuleta nguvu na akili katika mwili vinavyosaidia katika utendaji bora wa Mtumishi kwa maendeleo ya Taifa”.Alisema Balozi Kijazi.
Aidha Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Kijazi amewataka Viongozi wa Serikali na Taasisi zake kutenga muda kwa Watumishi wanamichezo wa kufanya mazoezi pamoja na kuwapatia vifaa vya michezo ili waweze kufanikiwa katika mashindano hayo. 

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel amewapongeza Watumishi wake kwa kushiriki Bonanza hilo na kuahidi kuwapa muda mzuri wa maandalizi ili wafanye vizuri katika mashindano hayo. 

Akifafanua maandalizi ya timu ya Wizara ya Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mwenyekiti wa timu hiyo Bw. John Manyika ameahidi ushindi kwa timu yake kwani wanaendelea kijiandaa vizuri katika mazoezi. 

Mashindano ya SHIMIWI yanatarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu mjini Dodoma kuanzia tarehe 14 ikiwa ni kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kmbarage Nyerere. 

Bonanza hilo lilimalizika kwa timu ya Jiji la Dar es Salaam kutwaa Kikombe kwa kuwa na wanamichezo wengi ikifuatiwa na Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi.

Waziri Moldiline Castico ashiriki uzinduzi wa Baraza la Vijana Shehia ya Kisiwa cha Uzi Wilaya ya Kati Unguja.

$
0
0

Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Wilaya ya Kati Unguja Mhe. Simai Mohammed Said, akizungumza na Vijana wa Kisiwa cha Uzi wakati wa uzinduzi wa Baraza la Vijana la Shehia hiyo lililozinduliwa na Waziri wa Kazi Vijana Uwezeshaji Wanawake na Watoto Zanzibar Mhe Moldiline Castico katika viwanja vya Skuli ya Uzi.
Mc wa Mkutano huo wa Uzinduzi wa Baraza la Vijana wa Shehia ya Kisiwa cha Uzi akisoma ratiba ya Uzinduzi huo katika viwanja vya Skuli ya Uzi Wilaya ya Kati Unguja.
Mwanachama wa Baraza la Vijana la Shehia ya Kisiwa cha Uzi Unguja Khadija Said akisoma Quran Tukufu kabla ya Uzinduzi wa Baraza lao la Vijana la Shehia ya Uzi lililozinduliwa na Waziri wa Kazi Vijana Uwezeshaji Wanawake na Watoto Zanzibar Mhe, Moldiline Castico.
Vijana wa Baraza la Vijana la Shehia ya Kisiwa cha Uzi wakicheza maigizo ya kuhamasisha Vijana kujiunga na Mabaraza ya Vijana kwa Maendeleo yao katika kujikwamua Kiuchumi.
Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu akiwa na Viongozi wa meza kuu wakifuatilia mchezo wa maigizo unaohamasisha Vijana kujiunga na Mabaraza la Vijana katika Shehia zao.,
Mwanachama wa Baraza la Vijana Shehia ya Kisiwa cha Uzi Salma Tunda akisoma risala yao mbele ya Mgeni rasmin wakati wa uzinduzi huo uliofanyika katika viwanja vya skuli ya uzi.
Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Shehia ya Kisiwa cha Uzi Farashuu Mussa akitowa salamu za Baraza lake kwa mgeni rasmin wakati wa uzinduzi huo.

CCM YATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA WAATHIRIWA WA TETEMEKO LA ARDHI KANDA YA ZIWA

$
0
0
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za janga la tetemeko la ardhi lililotokea jana tarehe 10/09/2016 katika Mkoa wa Kagera na baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Mwanza na Shinyanga.

Katibu Mkuu wa CCM Ndg Abdulrahman Kinana amemtumia salamu za rambi rambi Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Mustafa Kijuu kufuatia vifo vilivyotokana na tetemeko hilo.

Katika salamu zake Ndg Kinana amesema Chama cha Mapinduzi kinatoa pole kwa wahanga na kwa familia, ndugu na jamaa waliopoteza wapendwa wao katika janga hilo.

Chama cha Mapinduzi kipo pamoja na wahanga, kushirikiana nao kwa hali na mali katika kipindi hiki kigumu.WanaCCM nchi nzima tunamuomba Mwenyezi Mungu aziweke roho za marehemu pema peponi.

Amina.

Imetolewa na:-

CHRISTOPHER OLE SENDEKA (MNEC)

MSEMAJI WA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)

Tarehe 11/09/2016.

WAKURUGENZI WATEULE KUWASILI DODOMA,KULA KIAPO CHA UADILIFU WA UONGOZI WA UMMA SEPTEMBA 13

$
0
0
Na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Dodoma.

Wakurugenzi wa Halmashauri ya Mji, Manispaa na Wilaya, walioteuliwa siku ya Jumamosi Septemba 10, 2016 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wametakiwa kuwasilisha nakala halisi za vyeti vyao vya taaluma, kabla ya kuapa.

Zoezi la uhakiki wa vyeti hivyo litakalofanyika Ofis ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) katika jengo la Mkapa mjini Dodoma siku ya Jumanne Septemba 13, 2016 kabla ya kuanza kwa zoezi la kuapa.

Wakurugenzi hao 13 ni pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa mmoja, Mkurugenzi wa Mji mmoja na Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya 11, wanatakiwa kuwasili Ofisi ya Rais TAMISEMI mjini Dodoma saa 2:00 asubuhi kwa ajili ya uhakiki wa vyeti vyao vya taaluma.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhandisi Mussa Iyombe na kusainiwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Rebecca Kwandu, Septemba 11, 2016 inawataka Wakurugenzi hao kuhakikisha wanawasilisha nakala halisi ya vyeti vyao vya taaluma kwa ajili ya kiapo cha uadilifu wa uongozi wa umma.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa uhakiki wa vyeti halisi vya kitaaluma, unafanywa kwa lengo la kujiridhisha baada ya mchakato wa kawaida wa uhakiki kufanywa kwa kutumia vyeti visivyokuwa halisi yaani vivuli.

Wakurugenzi hao ni Godwin Emmanuel Kunambi Manispaa ya Dodoma, Elias R. Ntiruhungwa Mji waTarime, Mwantumu Dau Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba, Frank Bahatui Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe, Hudson Stanley Kamoga Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, Mwailwa Smith Pangani, Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo, Godfrey Sanga, Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama na Yusuf Daudi Semuguruka Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga.

Wakurugenzi wengine ni Bakari Kasinyo Mohamed Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea, Juma Ally Mnweke Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo, Butamo Nuru Ndalahwa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi, Waziri Mourice Halmashauri ya Wilaya ya Karatu na Fatma Omar Latu Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo.

WAZIRI WA MAENDELEO YA MIJI NA VIJIJI WA NAMIBIA AFIKA NCHINI KUJIFUNZA UTAWALA WA ARDHI

$
0
0
Waziri wa Maendeleo ya Miji na Vijiji wa Namibia; Sophia Shaningwa akielekezwa na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angeline Mabula (Mb). na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Mipango Miji na Vijiji, Immaculate Senje kutumia mashine ya ATM kwa ajili ya kupata huduma katika Kituo cha Huduma kwa Mteja – Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Waziri huyo amefika nchini kujifunza Utawala wa Ardhi.

Waziri wa Maendeleo ya Miji na Vijiji wa Namibia; Sophia Shaningwa akiwa ameambatana na ujumbe wake ndani ya Kituo cha Huduma kwa Mteja – Wizarani, akiwa ameambatana na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angeline Mabula na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Mipango Miji na Vijiji, Immaculate Senje, akipewa maelekezo na mtumishi jinsi huduma zinavyotolewa katika Kituo hicho. Waziri huyo amefika nchini kujifunza Utawala wa Ardhi. 
 Waziri wa Maendeleo ya Miji na Vijiji wa Namibia; Sophia Shaningwa akikabidhi Dola 300 kwa Mwenyekiti wa kijiji cha Kurui – Kisarawe, kama pongezi kwa kijiji hicho kuwa mfano bora  katika Mpango wa Utekelezaji wa Matumizi bora ya Ardhi. Waziri huyo amefika nchini na ujumbe wake kujifunza kuhusu Utawala wa Ardhi.
 Waziri wa Maendeleo ya Miji na Vijiji wa Namibia; Sophia Shaningwa akimpa mkono wa pongezi Mwenyekiti wa kijiji cha Kurui – Kisarawe, kama pongezi kwa kijiji hicho kuwa mfano bora  katika Mpango wa Utekelezaji wa Matumizi bora ya Ardhi. Katika picha ya pamoja na Watendaji mbalimbali wa Sekta ya Ardhi na ujumbe ulioambatana na Waziri kufika nchini kujifunza kuhusu Utawala wa Ardhi.
  Waziri wa Maendeleo ya Miji na Vijiji wa Namibia; Sophia Shaningwa akiwa amewasili Ofisini kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi, akiwa ameambatana na ujumbe wake, uliofika nchini kujifunza kuhusu Utawala wa Ardhi. 
Waziri wa Maendeleo ya Miji na Vijiji wa Namibia; Sophia Shaningwa, katikati akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ; Angeline Mabula, kushoto kwake. Kulia kwake ni Kaimu Kamishna wa Ardhi ; Mary Makondo na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Mipango Miji na Vijiji, Immaculate Senje pamoja na wajumbe walioambatana na Waziri huyo wa Namibia, waliofika nchini kujifunza kuhusu Utawala wa Ardhi.

BEI YA SAMAKI SOKO LA FERI JIJINI DAR ES SALAAM YASHUKA

$
0
0
Wachuuzi wa Samaki wakisubiri kununua kitoweo hicho katika Soko la Kimataifa la Samaki la Feri jijini Dar es Salaam leo asubuhi. Bei ya samaki katika soko hilo imepungua kutokana kwa kupatikana kwa wingi kwa kitoweo hicho.
Mnada wa samaki ukiendelea


Na Dotto Mwaibale

HALI ya bei ya samaki katika Soko la Kimataifa la Feri jijini Dar es alaam imeshuka kutokana na samaki kupatikana kwa wingi katika kipindi cha mwezi wa Septemba.

Akizungumza na mtandao wa www. habari za jamii.com jijini Dar es Salaam leo asubuhi mchuuzi wa samaki katika soko hilo Mohamed Hassan alisema katika kipindi cha wiki mbili bei ya samaki imeshuka ukilinganisha ni mwezi uliopita.

"Sasa hivi samaki aina ya King Fish, Changua wanauzwa kati ya sh.30,000 lakini kipindi ambacho wakiadimika ufikia hadi sh.35,000" alisema Hassan.Mchuuzi mwingine wa samaki katika soko hilo Shabani Shamte alisema samaki aina ya kibua, ngisi wakati huu uuzwa kati ya sh. 23,000 hadi 25,000 ambapo wakiadimika ufikia hadi sh. 30,000.

Grace Tesha ambaye uuza samaki hao maeneo ya Mabibo Loyola alisema hata wao kipindi hiki biashara yao inakwenda vizuri kutokana na kuwepo kwa samaki wengi."Samaki wakiadimika huwa inatuwia vigumu mno kibiashara kwani wateja wetu wamekuwa wakilalamia kuwauzia kwa bei kubwa" alisema Tesha.

NEWZ ALERT:RAIS DKT MAGUFULI AHIRISHA ZIARA YAKE YA SIKU TATU NCHINI ZAMBIA

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano Mheshimiwa DKT.John Pombe Magufuli ameahirisha ziara yake nchini Zambia ili ashughulikie tatizo la tetemeko la ardhi lililosababisha vifo vya watu 16,mamia kujeruhiwa na nyumba kadhaa kubomolewa mkoani Kagera.



TASW - SACCOSS) WASHEHEREKEA MIAKA MIWILI TANGU KUANZISHWA KWAKE JIJINI DAR.

$
0
0
Mwenyekiti wa Tanzania Saccos For Women Entrepreneurs (TASWE - Saccoss), Anna Matinde na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Plc, Ineke Bussemaker wakimsikiliza mtoa maada wakati wa Dinner Paty Gala na kusheherekea miaka miaka miwili ya Tanzania Saccos For Women Entrepreneurs (TASWE) jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Tanzania Saccos For Women Entrepreneurs (TASWE - Saccoss), Anna Matinde akizungumza katika hafla ya kutimiza Miaka miwili ya TASWE-Saccos jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. 

Alisema kuwa TASWE ipo mikoa Tofautitofauti hapa nchini Lengo kuu la hafla ya Dinner Part Gala ni kuwafikia wanawake wengi zaidi ili kutatua changamaoto zinazowakabiri hasa kwa upande wa kipato cha mwanamke.

Alisema kuwa TASWE inamatawi 14, katika matawi hayo wameona watoe elimu ya Ujasiliamali kwa wanawake wengi zaidi hapa nchini ili kupunguza ongezeko la utegemezi na waweze kuwa wanawake wajasili na wenye nguvu.
 Mshereheshaji, Angela Bondo akizungumza katika sherehe ya kutimiza miaka miwili ya TASWE jijini Dar es  Salaam mwishoni mwa wiki.
 Rais wa Chama cha wenye viwanda Biashara na Kilimo nchini (TCCIA), John Mayanja akizungumza wakati wa kuadhimisha miaka miwili ya Tanzania Saccos For Women Entrepreneurs (TASWE - Saccoss) jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki na kuwataka wanawake watumie fursa zinazojitokeza hasa kwa wale wanaotaka kusindika juisi za matunda hapa nchini kwa kuwa kuna matunda mbalimbali inapofikia msimu wake huharibika na kutupwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Plc, Ineke Bussemaker, akizungumza na wanawake wakati wa kusheherekea Miaka miwili ya Tanzania Saccos For Women Entrepreneurs (TASWE - Saccoss) tangu kuazishwa kwake na kuwa na wanachama wanawake wengi katika mikoa tofauti tofauti zaidi ya 10 hapa nchini. Alisema kuwa Wanawake milango imefunguka kwa benki hiyo hasa wakijiunga kwa makundi ili kupata mikopo yenye riba ya chini katika benki ya NMB hapa nchini.
Mtoa Maada wakati wa Tanzania Saccos For Women Entrepreneurs (TASWE - Saccoss) ikisherekea Miaka miwili jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.


 Wanawake wakiserebuka wakati wa kusherekea miaka miwili ya Tanzania Saccos For Women Entrepreneurs (TASWE - Saccoss) jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Baadhi ya wanawake waliohudhulia katika Tanzania Saccos For Women Entrepreneurs (TASWE - Saccoss)Dinner Party Gala na kusheherekea pamoja kutimiza Miaka miwili ya Tanzania Saccos For Women Entrepreneurs (TASWE - Saccoss) jijini Dar es Salaam.
 Burudani ikiendelea.








 Washiriki wakiwa katika hafla ya Dinner Paty Gala pamoja na Kusheherekea Miaka miwili ya Tanzania Saccos For Women Entrepreneurs (TASWE - Saccoss),jijini Dar es Salaam.



 
Rais wa Chama cha wenye viwanda Biashara na Kilimo nchini (TCCIA), John Mayanja atembelea baadhi ya kazi za wanawake wajasiliamali katika hafla ya Dinner Paty Gala iliyoambatana na Kusheherekea miaka miwili ya Tanzania Saccos For Women Entrepreneurs (TASWE - Saccoss) jijini Dar es Salaam.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AUNGANA NA WAISLAMU KATIKA SWALA YA IDD EL HAJI VIWANJA VYA MWEMBE YANGA, TEMEKE JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, (kushoto), na Sheikh Ponda Issa Ponda, wakiomba dua wakati wa swala ya Idd El Haji kwenye viwanja vya Mwembe-Yanga, Temeke jijini Dar es Salaam leo Septemba 12, 2016. (PICHA NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID)

NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID
WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh.Kassim Majaliwa, amewataka waumini wa dini ya Kiislamu kuitumia sikukuu hii ya Idd el Haji kutenda mema na kuungana na waumini wengine katika kudumisha amani ya nchi yetu.
Waziri Mkuu akiyasema hayo leo Septemba 12, 2016, kwenye ibada ya sala ya Idd el Haji iliyofanyika kwenye viwanja vya Mwembe-Yanga, Temeke, jijini Dar es Salaam ambapo miongoni mw masheikh maarufu walihudhuria ibada hiyo ni pamoja na Sheikh Shariff, Sheikh Nurdin Kishki,(mwenyeji wa hadhara), Sheikh Ponda Issa Ponda na Sheikh Rajab Katimba.
“Kwa niaba ya serikali yenu, nawatakia sikukuu njema, na ninaomba kuwasilisha salamu za upendo kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Joseph Pombe Magufuli, pamona na Makamu wa Rais, Mh. Samia Suluhu Hassan, na niwaombe ndugu zangu muitumie sikukuu hii kudumisha amani na upendo.” Alisema Waziri Mkuu.
Waziri M,uu pia alitumia fusa hiyo kuwataka waumini wa dini ya Kiislamu kote nchini, kuwaombea wananchi wa mkoa wa Kagera waliopatwa na maafa ya tetemeko la ardhi lililosababisha vifo.
Waziri Mkuu ambaye alihudhuria ibada ya kuaga miili ya watu 16 kwenye uwanja wa michezo wa Kaitaba mjini Bukoba, mkoani Kagera Jumapili Septemba 11, 2016, alisema kwa sasa kuna majeruhi zaidi ya 100 ambao bado wanapatiwa matibabu. Tetemeko hilo lilillopelekea uharibifu mkubwa wa nyumba lilitokea Jumamosi alasiri Septemba 10, 2016.
Naye mwenyeji wa Ibada hiyo Sheikh Nurdin Kishki, alimshukuru Waziri Mkuu kwa kuungana na waumini wa dini ya Kiislamu wa Wilaya ya Temeke, katika swala hiyo ya Idd. “Nduhgu zangu napenda nimshukuru Waziri wetu Mkuu kwa kutoka Oysterbay hadi kufika huku Temeke kuungana nasi katika kutekeleza swala hii ya Idd El Haji, mwenyezimungu amjalie heri na busara katika uongozi wake,” Alsiema Sheikh Kishki.

 Sheikh Shariff akiongoza Swala ya Idd El Haji viwanja vya Mwembe Yanga , Temeke jijini Dar es Salaam
 Sheikh Shariff akiongoza Swala ya Idd El Haji viwanja vya Mwembe Yanga , Temeke jijini Dar es Salaam
 Muumini wa Kiislamu akiomba dua
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipeana mikono na Sheikh Ponda Issa Ponda, mara baada ya swala hiyo
 Waziri Mkuu, akiteta jambo na sheikh Ponda
 Waziri Mku, akiwa katika picha ya pamoja na Sheikh Shariff, (kushoto), na Sheikh Nurdin Kishki
 Waumini wa Kiislamu wakiwa kwenye swala
 Waumini wa Kiislamu, wakiomba dua


 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na Masheikh na viongozi wa serikali mara baada ya swala hiyo
 Sheikh Nurdin Kishki, akisikiliza kwa makini hotuba ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwahutubia waumini wa dini ya Kiislamu wakati wa swala ya Idd El Haji viwanja vya Mwembe-Yanga, Temeke jijini Dar es Salaam
 Sheikh Nurdin Kishki, kiwahutubia waumini wa dini ya Kiislamu kwenye viwanja vya Mwembe-Yanga, wakati wa swala hiyo
 Watoto hawa wa Kiislamu, wakionyesha furaha baada ya kushiriki swala ya Idd El Haji, (Mlulu Khalfan (kushoto) na mdogo wake Kuugara.

AZANIA BANK TAWI LA MOSHI YAKABIDHI ZAWADI YA MBUZI KWA WATEJA WAKE NA VITUO VYA KULELEA WATOTO WAISHIO KATIKA MAZINGIRA MAGUMU.

$
0
0
Wafanyakazi wa Benki ya Azania tawi la Moshi ,wakishusha Mbuzi kwa ajili ya kutoa zawadi ya siku kuu ya Idd kwa baadhi ya wateja wake pamoja na makundi yenye mahitaji maalumu.
Meneja wa Azania Bank tawi la Moshi ,Hajira Mmambe akimkabidhi zawadi ya Mbuzi mwakilishi wa Mbunge wa jimbo la Moshi mjini Jafary Michael , Bw ,Bashir Seleman wa kampuni ya Zuhad kwa ajili ya siku kuu ya Idd.
Meneja wa Azania Bank  tawi la Moshi,Hajira Mmambe akikabidhi zawadi ya Mbuzi kwa msimamizi wa kituo cha kulea watoto waishio kwenye mazingira magumu cha Qadria kilichopo kata ya mji Mpya,Alhaji Taqdir Haji Amir kama sadaka ya siku kuu ya Idd.
Baadhi ya watoto wa kituo cha  kulelea watoto cha Qadria kilichopo kata ya Mji Mpya.
Meneja wa Azania Bank akikabidhi zawadi ya Mbuzi kwa mteja wa Benki hiyo Aman Idd Mushi kwa ajili ya siku kuu ya Idd.
Meneja wa Azania Bank tawi la Moshi,Hajira Mmambe pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo wakikabidhi zawadi ya Mbuzi kwa mwakilishi wa kampuni ya Ibra line ,Bi Mosi Shayo kwa ajili ya siku kuu ya Idd.
Meneja wa Azania Bank tawi la Moshi,Hajira Mmambe akizungumza mara baada ya kukabidhi zaadi ya Mbuzi kwa ajili ya siku kuu ya Idd kwa wateja wake pamoja na makundi yenye mahitaji maalumu.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

WAZIRI NAPE NNAUYE AFUNGA MASHINDANO YA AIRTEL RISING STAR MSIMU WA SITA

$
0
0
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akikabidhi kikombe kwa nahodha wa Timu ya wasichana ya Temeke walioibuka washindi wa mashindano ya Vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Star kwa upande wa wasichana katika Uwanja wa Karume Jijini Dar es Salaam Septemba 11, 2016.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akikabidhi kikombe kwa nahodha wa Timu ya wavulana ya Morogoro walioibuka washindi wa mashindano ya Vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Star kwa upande wa wavulana katika Uwanja wa Karume Jijini Dar es Salaam Septemba 11, 2016.
Timu ya wasichana ya Temeke wakishangilia ushindi wao wakishangilia ushindi wao walioupata katika mashindano ya Vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Star kwa upande wa wasichana kwa kuwafunga Timu ya temeke kwa mikwaju ya penati katika Uwanja wa Karume Jijini Dar es Salaam Septemba 11, 2016.
Timu ya wavulana ya Morogoro wakishangilia ushindi wao wakishangilia ushindi wao walioupata katika mashindano ya Vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Star kwa upande wa wavulana kwa kuwafunga Timu ya Ilala kwa goli moja kwa bila katika Uwanja wa Karume Jijini Dar es Salaam Septemba 11, 2016.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akiwa katika picha ya pamoja na Timu ya wavulana ya Morogoro mara baada ya kumalizika kwa mshindano ya Vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Star yaliyofanyika katika Uwanja wa Karume Jijini Dar es Salaam Septemba 11, 2016.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akiwa katika picha ya pamoja na Timu ya wavulana ya Ilala mara baada ya kumalizika kwa mshindano ya Vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Star yaliyofanyika katika Uwanja wa Karume Jijini Dar es Salaam Septemba 11, 2016. Picha zote na Raymond Mushumbusi WHUSM
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo mhe. Nape Moses Nnauye (wa pili kulia) akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa Mawasiliano kutoka Airtel Tanzania Bi. Beatrice Singano (wa pili kushoto) wakati akiwasili katika Uwanja wa Karume kuhitimisha mashindano ya Vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Star Septemba 11, 2016 kushoto ni Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania Bw. Jamali Malinzi.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (wa pili kulia) akijadiliana jambo na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania Bw. Jamali Malinzi wakati wa hitimisho la mashindano ya Vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Star Septemba 11, 2016.
Mkurugenzi wa Airtel Tanzania Bw. Sunil Colaso akizungumza kuhusu maendeleo ya mashindano ya Airtel Rising Star wakati wa hitimisho la mashindano hayo ya Vijana chini ya umri wa miaka 17 katika Uwanja wa Karume Jijini Dar es Salaam Septemba 11, 2016.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akipita katika moja ya geti linalotumia mfumo wa mashine za tiketi za kieletroniki katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam Septemba 11, 2016.

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na wanamichezo, wadau wa michezo na wanahabari kabla ya kushuhudia fainali ya mashindano hayo yiliyohitimisha mashindano hayo kwa Vijana chini ya umri wa miaka 17 Airtel Rising Star katika Uwanja wa Karume Jijini Dar es Salaam Septemba 11, 2016.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akikagua wachezaji wa timu ya Morogoro Boys kabla ya kuanza kwa fainali kati yao na timu ya Ilala iliyofanyika katika Uwanja wa Karume Jijini Dar es Salaam Septemba 11, 2016.

WAZIRI NAPE NNAUYE AKABIDHIWA RASMI MAGETI YANAYOTUMIA MFUMO WA MASHINE ZA TIKETI ZA KIELETRONIKI KATIKA UWANJA WA TAIFA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0


 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akiweka kadi  katika moja ya geti linalotumia mfumo wa mashine za tiketi za kieletroniki tayari kuingia katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam Septemba 11, 2016.
tai2
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akikata utepe kuashiria kuanza kutumika rasmi kwa mageti yanayotumia mfumo wa mashine za tiketi za kieletroniki katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam Septemba 11, 2016.
tai4
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akipita katika moja ya geti linalotumia mfumo wa mashine za tiketi za kieletroniki katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam Septemba 11, 2016.
tai5
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na watendaji wa  Wizara yake, wadau wa michezo, wanamichezo na wanahabari mara baada ya kukabidhiwa na kuzindua rasmi mageti yanayotumia mfumo wa mashine za tiketi za kieletroniki katika Uwanja huo Jijini Dar es Salaam Septemba 11, 2016.
tai6
Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel akizungumzia mradi wa mageti yanayotumia mfumo wa mashine za tiketi za kieletroniki katika hafla iliyofanyika katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam Septemba 11, 2016.
tai7
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Bw. Jamali Malinzi akitoa salamu za wadau wa mchezo wa mpira wa miguu kwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye wakati wa hafla ya mkabidhiano ya mageti yanayotumia mfumo wa mashine za tiketi za kieletroniki kwa Serikali katika Uwanja huo Jijini Dar es Salaam Septemba 11, 2016.
tai8
Mkurugenzi wa Kampuni ya BCEG Bw. Cheng Long Hai akizungumzia utekelezaji wa mradi wa mageti yanayotumia mfumo wa mashine za tiketi za kieletroniki uliotekelezwa na kampuni yake kwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye wakati wa hafla ya mkabidhiano ya mageti hayo yaliyofanyika katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam Septemba 11, 2016.
tai9
Mhandisi Mshauri wa mradi wa mageti yanayotumia mfumo wa mashine za tiketi za kieletroniki Mhandisi Aloyce Mushi akieleza changamoto mbalilmbali kuhusu mradi huo kwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye wakati wa hafla ya mkabidhiano ya mageti hayo yaliyofanyika katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam Septemba 11, 2016.
tai10
Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel pamoja na Mkurugenzi wa Kampuni ya BCEG Bw. Cheng Long Hai wakitia saini hati za makabidhiano ya mageti yanayotumia mfumo wa mashine za tiketi za kieletroniki katika hafla iliyofanyika  Septemba 11, 2016 katika Uwanja wa Taifa  Jijini Dar es Salaam.
tai11
Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel pamoja na Mkurugenzi wa Kampuni ya BCEG Bw. Cheng Long Hai wakionesha  hati za makabidhiano ya mageti yanayotumia mfumo wa mashine za tiketi za kieletroniki katika hafla iliyofanyika  Septemba 11, 2016 katika Uwanja wa Taifa  Jijini Dar es Salaam.
tai12
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akipokea kadi za kuingia katika Uwanja wa Taifa kwa ajili ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa kutoka kwa Meneja Mradi kutoka kampuni ya Selcom Tanzania Bw. Gallus Runyeta wakati  wa hafla ya makabidhiano ya mageti yanayotumia mfumo wa mashine za tiketi za kieletroniki iliyofanyika  katika Uwanja wa Taifa  Jijini Dar es Salaam Septemba 11, 2016.
tai13
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akionesha kadi za kuingia katika Uwanja wa Taifa kwa ajili ya viongozi wakuuwa nchi wakiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa wakati  wa hafla ya makabidhiano ya mageti yanayotumia mfumo wa mashine za tiketi za kieletroniki iliyofanyika  katika Uwanja wa Taifa  Jijini Dar es Salaam Septemba 11, 2016.
tai14
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akipokea Saluti kutoka kwa kiongozi wa Bendi ya Polisi mara baada ya kumalizika kwa hafla ya makabidhiano ya mageti yanayotumia mfumo wa mashine za tiketi za kieletroniki iliyofanyika  katika Uwanja wa Taifa  Jijini Dar es Salaam Septemba 11, 2016.
tai15
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (katikati waliokaa) aliwa katika picha ya pamoja na wadau wa michezo nchini mara baada ya kumalizika kwa hafla ya makabidhiano ya mageti yanayotumia mfumo wa mashine za tiketi za kieletroniki iliyofanyika  katika Uwanja wa Taifa  Jijini Dar es Salaam Septemba 11, 2016 kulia waliokaa ni Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel na kushoto waliokaa ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe. Felix Lyaniva.
tai1
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akisalimiana na Katibu Mkuu wa Wizara yake Prof Elisante Ole Gabriel mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Taifa kwa ajili ya kukabidhiwa rasmi mageti yanayotumia mfumo wa mashine za tiketi za kieletroniki katika Uwanja huo Jijini Dar es Salaam Septemba 11, 2016.
Picha zote na Raymond Mushumbusi WHUSM  
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live


Latest Images