Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 95 | 96 | (Page 97) | 98 | 99 | .... | 1897 | newer

  0 0

   Redds Miss Sinza ambaye pia ni Redds Miss Tanzania, Brigitte Alfred  alisisitiza jambo kwa warembo wa Redds Miss Sinza 2013  alipotembelea kambi ya mazoezi hiyo. Warembo hao watapanda jukwaani Ijumaa kuwania taji la mwaka huu. 
  =======  =======  ========
  BENDI yenye chati ya juu kabisa katika muziki wa dansi nchini,  The African Stars’ Wana Twanga Pepeta’ itaburudisha mashindano ya Redds Miss Sinza yaliyopangwa kufanyika Ijumaa (Juni 7) kwenye ukumbi wa Meeda Club wa Sinza jijini.

  Mratibu wa mashindano hayo, Majuto Omary alisema kuwa bendi hiyo itatumia fursa hiyo kutambulisha baadhi ya nyimbo zake mpya zilizomo katika albamu ya 12 ijulikanayo kwa jina la Nyumbani ni Nyumbani ambayo itazinduliwa rasmi Juni 30 kwenye viwanja vya Leaders Club jijini.

  Majuto alisema kuwa Twanga Pepeta itakuwa ikitumbuiza kwa mara ya kwanza tokea mwaka jana mwezi  julai ambapo ilitumbuiza katika mashindani hayo hayo ya kumsaka mrembo wa Sinza. Alisema kuwa hii ni faraja kubwa kwa mashabiki wa muziki wa dansi na wa masuala ya urembo kwani Twanga Pepeta itakuwa ikimvua taji Redds Miss Tanzania, Brigitte Alfred ambaye atakuwa anavua taji lake la kwanza.

  “Ikukmbukwe kuwa twanga pepeta haijatumbuiza Sinza kwa kipindi kirefu na hivyo kuandaa zawadi maalum kwa mashabiki wake katika mashindano hayo yaliyo dhaminiwa na Redds Original, Dodoma Wine, Chilly Willy Energy Drink, Fredito Entertainment, CXC Africa, Clouds Media Group, Salut5.com na Sufiani Mafoto blog,” alisema Majuto.

  Alisema kuwa jumla ya warembo 12 wamejitokeza kuwania taji la mwaka huu la Sinza nan i matarajio ya waandaaji kuwa Miss Sinza wa mwaka huu atatwaa taji hilo na kufuata nyayo za Brigitte ambaye aliweza kutwaa taji la Miss Kinondoni na baadaye Miss Tanzania. “Tuna warembo bora ambayo wamedhamilia kufanya kweli katika mashindano ya urembo mwaka huu,  wamepania kulinda hadhi ya mwaka jana, hivyo mashabiki waje kuona warembo bora waliopania kufanya kweli katika mashindano hayo,” alisema.


  0 0


  Askari wa Usalama Barabarani katika manspaa ya Dodoma Mjini leo, akiimkagua Mwendesha Pikipiki(Bodaboda) ambaye alikuwa amepakia mzigo kuzidi uwezo wa pikipiki, kitendo ambacho ni hatari na ni chanzo cha ajali za barabarani, (Picha na Shaaban Mpalule)

  0 0

   Wanafunzi wa Chuo cha Dar es Salaam City College(DACICO) wakisalimiana na Mheshimiwa Mbunge Jimbo la Kinondoni Idd Azan,(kati) mjini Dodoma, mara baada ya kuwasili kwenye Viwanja vya Bunge kwa ajili ya Kikao cha Bunge Mwishoni mwa Juma
  Mheshimiwa Mbunge Jimbo la Kinondoni Idd Azan,(mbele) akiwaongoza Wanafunzi wa Chuo cha Dar es Salaam City College(DACICO) kuingia Katika Jengo la Bunge Mjini Dodoma  mara baada ya kuwasili  kwa ajili ya kuhudhuria Kikao cha Bunge Mwishoni mwa Juma(Picha kwa Hisani ya Miss Demokrasia Tanzania).

  0 0

      Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Muhammed Shein amesema ziara yake ya wiki moja nchini China itaisaida sana Zanzibar katika  kuimarisha uhusiano kati ya nchi hiyo na Zanzibar  na kuharakisha maendeleo ya wananchi.
  Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, Dk. Shein amesema katika ziara hiyo amefanya  mazungumza na viongozi wa juu wa China akiwemo Rais, Makamu  wake na Waziri Mkuu wa  nchi hiyo  ambayo yalilenga  kuimarisha uchumi wa Zanzibar katika sekta mbali mbali za maendeleo.
  Amezitaja sekta hizo kuwa ni pamoja na Afya, Kilimo, Huduma za Elimu na Biashara pia waliangalia uhusiano katika maeneo mengine mapya ya uvuvi wa bahari kuu na uwekezaji vitega uchumi.
  Dk. Shein amesema China na Zanzibar wamekubaliana  kuimarisha sekta ya Biashara ambapo Naibu Waziri wa Biashara wa China ameitaka Zanzibar kuandaa rasimu ya mapendekezo ya miradi ambayo itashughulikiwa  na nchi yake.
  Akizungumzia  Kilimo Rais  Shein amesema wamekubaliana na China kuja  kufanya utafiti wa uvuvi wa bahari kuu, kusaidia utaalamu na  kuwekeza miradi mikubwa katika sekta hiyo.
  “ Uvuvi unanafasi kubwa katika maendeleo ya Zanzibar lakini tunahitaji uvuvi wa kisasa wenye tija, na kuanzisha miradi ya ufugaji samaki na yote haya wenzetu wamekubali, ” amesema Dk.Shein.
  Amesema  Zanzibar imepeleka wavuvi wadogo wadogo 59  wa vijiji vya  Unguja na Pemba kujifunza nchini China na waliporudi wamewaelimisha  wavuvi wenzao  na tayari mafanikio yameanza kuonekana.
  Ameongeza kuwa katika mazungumzo yake na viongozi wan chi hiyo amewataka kuimarisha sekta ya Utalii kwa kuitangaza Zanzibar na kuwashajiisha wananchi wa nchi hiyo kufanya ziara za kitalii nchini.
  Rais wa Zanzibar amesema katika kufanikisha ziara  hiyo Ujumbe mkubwa kutoka China utawasili Zanzibar muda mfupi ujao kuangalia maeneo ya uwekezaji na ametaka wahusika kujiandaa.
  “Lazima tubadilike na tujiandae wenzetu hawako katika mchezo katika uwajibikaji na ndio maana nchi yao inapiga hatua kubwa ya maendeleo, ” amesema Rais wa Zanzibar.
  Akizungumzia ujenzi wa Uwanja wa ndege wa Zanzibar uliokuwa ukifanywa na Kampuni ya Ujenzi kutoka China na ambao umekwama, Dk. Shein amesema yapo mategemeo makubwa ya kuanza tena muda mfupi ujao baada ya mshauri muelekezi alieletwa na Zanzibar kutoka Ufaransa kukamilisha kazi yake.
  Dk. Shein na ujumbe wake waliondoka Zanzibar tarehe 27 mwezi uliopita na katika ziara hiyo aliungana na viongozi wengine kutoka  Sirilanka, Papua New Guinea, Singapore na Malaysia  katika mkutano mkubwa wa Kimataifa wa Biashara uliofanyika nchini humo.        
           NA RAMADHANI ALI /HABARI MAELEZO ZANZIBAR      
  IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR.

  0 0

  Baadhi ya Ndugu Marafiki naWadau wa Marehemu,wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa Marehemu Albert Mangwear  kutoka nchini Afrika Kusini,ambapo mwili huo tayari umekwisha pakizwa kwenye ndege ya Shirika la ndege la South African Airways kuja Tanzania,aidha mwili huo inaelezwa kuwa utawasili nchini Tanzania mnamo majira ya saa saba mchana na nusu,Watu mbalimbali wameombwa kujitokeza kuupokea mwili wa mpendwa wetu Albert Mangwea.

  MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI-AMEN.

  0 0


  Gari maalum la Kubeba Mwili Msanii wa Muziki wa Kizaki Kipya,Marehemu Albert Mangwea likiwa tayari tayari kwa kubeba mwili.
  Wadau mbali mbali wakiwa wamekusanyika kwa wingi kwenye uwanja wa Ndege Julius Nyerere kwa ajili ya kuupokea Mwili wa Marehemu Albert Mangwea uliowasili mchana huu kutokea nchini Afrika ya Kusini.
  Wadau kibao wapo uwanja hapa hivi sasa tayari kwa kuupokea Mwili wa Marehemu Mangwea.
  Rafiki kipenzi wa Marehemu Albert Mangwea,Jay Mo akihojiwa na vyombo vya hapari uwanjani hapa.
  Prof. Jay nae alipata wasaha wa kuongea na vyombo vya habari juu ya Msanii mwenzao Albert Mangwea alietangulia Mbele ya haki.
  Wadau.
  Watu kutoka kila pembe ya jiji la Dar wakiwa uwanjani hapa kuupokea mwili wa Msanii wao.
  Wanahabari wakitafakari jambo.
  Wakiwa wamejipanga tayari kwa kuubeba mwili wa Marehemu Mangwea.
  Mkurugenzi wa Zizzou Fashion,Othman Tippo (kushoto) akizungumza na mmoja wa wadau waliofika uwanjani hapo.
  Wasanii mbali mbali wapo uwanjani hapa hivi sasa.
  Madee akimzungumzia Marehemu Mangwea.


  0 0


  0 0   Gari iliyobeba mwili wa Albert Mangwea ikisukumwa na washabiki,wapenzi ndugu jamaa na marafiki mara baada kuanza kuondoka eneo la Eapoti hivi punde wakielekea Muhimbili kwa taratibu nyingine,Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi--Amen


  0 0

  Wanachama wa chama cha mapinduzi tawi la Ikonongo kata ya mkwawa manispaa ya Iringa  wamefanya harambee kwa ajili  ya kukomboa kiwanja ambacho walitakiwa kujenga ofisi ya chama chao.
    
  Akizungumza katika harambee hiyo  Mwenyekiti wa tawi AMRI KALINGA amesema kuwa ujenzi huo umeshindwa kufanyika mapema kutokana na kiwanja hicho kuwa na mgogoro ila kwa sasa wameshafikia muafaka na tayari wamelipa fidia ya shilingi laki tano na nusu.
    
  Naibu meya wa manispaa GERVAS NDAKI ambaye alikuwa mgeni rasmi katika harambee hiyo amewataka wananchi hao kuwa wabunifu kwa vitu ambavyo vitawasaidia kuwainua kiuchumi katika kijiji chao na sio kuishia kujenga ofisi.

  0 0

  Naibu waziri wa malisaili na utalii tanzania NYARANDU amesema hali ya ujangili Tanzania ni kubwa, jambo ambalo linahatarisha usalama wa Taifa.
   
  Hayo ameyasema leo wakati wa akifungua kikao cha wadau wa ulinzi wa malisaili mikoa ya nyanda za juu kusini mwa Tanzania mkoani hapa.

   NYARANDU amewataka wananchi wanaomiliki siraha kinyume na taratibu kuzisalimisha mapema na wanaojihusisha na ujangili kuacha maramoja vitendo hivyo.
   
  kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Iringa CHRISTINE ISHENGOMA amesema anaamini kuwa kikao hicho kinachofanyika kwa siku mbili kitatoa suluhisho la kukomesha vitendo vya ujangiri katika ukanda huu.
   
  kikao hicho cha wadau wa ulizi wa maliasili mikoa ya nyanda za juu kisini kimeandaliwa na mradi wa kuboresha mtandao wa maeneo yaliyo hifadhi kusini mwa tanzania (SPANEST)kikao hicho kimehudhuliwa na wakuu wa mikoa ya mbeya,njombe,dodoma na mwenyeji iringa, wengine ni mkurugenzi wa TANAPA na wakuu wa wilaya na wadau wengine. 

  0 0

  wajumbe wakifutilia mada


  Meneja wa Kanda ya Mshariki na Kusini wa TFDA, Bw. Emanuel Aphonce, akiwasilisha Mada kwa wajumbe.


  Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Bw. Hery Nkunda, akitoa maelezo ya utangulizi katika mkutano huo.


  Mgeni rasmi, Dkt. Saiduma Kaduma akifungua mkutano wa Wakaguzi wa TFDA.

  ========   =====  ========

  Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) imekutana na wakaguzi wa bidhaa za Chakula, Dawa, Vipodozi na vifaa tiba wa kutoka mikoa ya Mtwara na Lindi kwa lengo la kukumbushana maadili na kujadili changamoto mbalimbali zinazowakabili katika udhibiti ususan ukaguzi.


  Mkutano huo wa siku mbili unafanyika mkoani Mtwara kwa tarehe 4 na 5 Juni, 2013, umefunguliwa rasmi na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Dkt. Saiduna Kabuma.

   Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Bw. Hery Nkunda, katika maelezo yake yaUtangulizi alisema kuwa mkutano huo unalenga kukutana na wakaguzi wa TFDA katika Halmashauri walau mara moja kwa mwaka ili kubaini changamoto za ukaguzi, kujadili na kukubaliana mikakati endelevu katika ukaguzi wa bidhaa za chakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba nchini.

  Akihutubia washiriki wa mkutano huo kabla ya kufungua rasmi mgeni rasmi, dkt. Kabuma amewataka wakaguzi kutumia Sheria, kanuni, maadili, hekima na busara katika kufanya kazi za ukaguzi. Aidha aliwataka wakaguzi kutoka ofisini na kwenda nje kuangalia yanayofanyika kama ni kwa mujibu wa Sheria au la.


  TFDA imekasimu baadhi ya majukumu ikiwa ni pamoja na ukaguzi wa bidhaa kwa Halmashauri. katika kuboresha hili, TFDA imekuwa na utaratibu wa kukutana na wakaguzi walio katika Halmashauri Mbalimbali nchini kwa lengo la kubadilishana mawazo na kujadili mikakati ya udhibiti.

  0 0

  Viwanja vinauzwa, Malimbe,Sweya Jijini Mwanza umbali wa Nusu Kilomita kutoka SAUTUniversity. Vipo ziwani (ziwa Victoria) ni low Density, viwanja hivyo ni namba 95 na 96 kama vinavyoonyeshwa katika ramani hiyo.kiwanja namba 95 ukubwa wake ni 2431 sm na namba 96 ni 2766 sm square mmiliki ni mmoja na kuna miti na nyumba,bei 450 milioni.
  Mawasiliano zaidi ni 0757181351,
  Madalali hawahitajiki.

  0 0  0 0

   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Bw. Laurence Bay, Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Singapore. Kushoto ni Balozi wa Tanzania India na Singapre Injinia John  Kijazi na mbele yao ni Naibu Mkurugenzi wa Itifaki wa Singapore Bi. Christine Tay. PICHA NA IKULU

    Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mbunge wa Kasulu mjini Mhe Moses Machali pamoja na wadau wengine wakati akiwasili Singapore..
    Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea jijini Singapore leo wakati alipokutana na wafanyabaishara za ujenzi wa nchi hiyo marav tu baada ya kutua kutoka Japan alikokuweko kwa ziara ingine ya kikazi. Katika mkutano huu  Rais Kikwete aliwakaribisha wafanyabishara hao wa Singapore  Tanzania kuwekeza katika sekta ya nyumba wakati wa chakula cha jioni kilichiandaliwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) .

  0 0

  EXIM Bank Tanzania has continued to consolidate its position in 
  Tanzania’s banking sector with the latest report by audit firm KPMG 
  naming the bank to be among one of the most customer-focused banks in
  Tanzania presently.  According to the Africa Banking Industry Customer Satisfaction Survey   released by KPMG conducted between June and December of 2012 in 14


  countries across Africa including Tanzania, Exim Bank emerged overall   winner in the Customers care sub-category out of 32 banks surveyed in


  Tanzania.


  “Exim Bank achieved 75.2 points beating runner-up Barcla ys Bank and 


  third place Akiba Commercial Bank who recorded 75.0 and 74.9 points 
  respectively,”  Other countries surveyed included Angola, Botswana, Cameroon, Chad,   Côte d’Ivoire, Ghana, Kenya, Nigeria, Senegal, Sierra Leone, Uganda,  Zambia and Zimbabwe.

  Commenting on the survey, the Exim Bank Tanzania Managing Director

  Anthony Grant said the findings of the survey are yet another
  encouragement for the team at Exim Bank.   “Indeed this continues to be a very good year for the bank as the    eport comes out at a time when Exim Bank has been selected as one of   the five best Retail Banks in Africa by the prestigious African Banker    Awards 2013.


  “We will continue to invest in customer service delivery and enhance

  the development of staff skills at the Exim Academy to better serve
  our customers. Our quest is to be Tanzania’s preferred bank, ” Grant
  said.

  The survey findings indicate that banks in Africa will need to focus
  on maintaining their financial stability while simultaneously
  sharpening their customer service capabilities if they hope to capture
  and grow their markets.


  According to Bisi Lamikanra Partner, KPMG Nigeria,Team Lead,Project
  Africa Banking, more than one in two institutional investors see
  Africa as the most attractive region to invest in the next decade,
  with one in three expecting to put at least 5 percent of their
  portfolios into the continent by 2016.


  “Amidst the global economic crisis, several African economies have
  continued to record significant economic growth driven by rising
  commodity prices and strong domestic demand.


  “In the same vein, the financial services industry is continuing to
  experience huge growth as governments and regulators strive to meet
  financial inclusion targets,” she said.Lamikanra noted that the banking sector Africa in particular has  benefited from the rapid penetration of mobile chnology in recent  years across the continent.


  “Such technological advancements are not just shaping how people
  interact with one another; they are also changing the behavior and
  expectation of bank customers who are increasingly becoming used to
  the immediacy offered by technology,” she added.


  The survey results however revealed the dominance of branches and the
  Automated Teller Machine (ATM) over other channels in Africa.
  “We also see exciting trends for adoption of alternate payment
  channels, such as use the Point of Sale (POS),” the survey added.


  The survey also highlights a number of other key areas where African
  banks could make improvements in order to gain market advantage that
  include customer care: Transaction methods & systems (TMS), pricing,
  tailor-made products and services: and convenience.

  0 0


  0 0

    Sanduku lililobeba mwili wa Marehemu Albert Mangwea ukiiingizwa kwenye Wodi maalum ya Dharura
  Baadhi ya watu wakiwa wamelizunguka eneo ambali mwili wa marehemu Albert Mangwea uliposhushwa,na baadae ulipelekwa kwenye chumba cha kuhifadhi maiti kwa taratibu nyingine

  0 0


  0 0

  Meneja masoko wa Heineken Tanzania,Caroline Kakwezi (kushoto) akimeana mkono na Mshindi wa timu ya Liverpool Foosball,Godfrey Musikula (kulia) wakati wakimzawadia mfano wa tiketi ya Ndege ya kwenda mjini Amsterdam mara baada ya kumalizika kwa mashindano hayo hapa nchini.Wengine pichani toka kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Heineken Tanzania,Uche Unigwe, Innocent Venance mmoja wa washindi wa michuano ya foosball kutoka team Liverpool, wadau wa Triniti bar & Restaurant Jackie na Erica.
  Team Champions kutoka Samaki samaki na Team Liverpool Foosball wakichuana vikali katika fainali iliyodhaminiwa na Heineken Tanzania hivi karibuni jijini Dar es salaam.
  Meneja kutoka Hyatt Regency - The Kilimanjaro,Timothy Mlay alishinda taulo pamoja na zawadi nyingine kutoka Heineken Tanzania baada yakupatia score ya mechi kati ya Dortmund na Bayern Munich hivi karibuni jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Heineken Tanzania,Uche Unigwe.

  0 0

   Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga, akizungumza na warembo wanaotarajia kushiriki shindano la Redd's Miss Tanzania, 2013 wakati alipowatembelea kwenye kambi yao ya mazoezi yanayoendelea katika Ukumbi wa Meeda Pub. Shindano hilo linatarajia kufanyika Juni 7 mwaka huu katika ukumbi huo huo.
   Lundenga, akizungumza na Warembo hao leo kwenye ukumbi wa Meeda Pub.
  *****************************

  MKURUGENZI wa Kampuni ya Lino International Agency, waandaaji wa mashindano ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga, leo Jumanne jioni alitembelea kambi ya washiriki wanaojiandaa kushiriki katika shindano la Miss Sinza na kusisitiza hakuna rushwa ya ngono katika mashindano yao.

  Lundenga aliongozana na ujumbe wake, ambao ni Bosko Majaliwa, Katibu wa Kamati ya Miss Tanzania, Albert Makoye Mkuu wa Itifaki na Nidhamu wa kamati hiyo, Hidan Rico, Afisa wa Habari wa kamati hiyo, Yasson Mashaka, Mkuu wa Mipango wa Kamati hiyo na Lucas Luta, ambaye ni mjumbe.

  Lundenga, alifika Meeda Pub, ambapo washiriki wa Miss Sinza wanafanya mazoezi, alifanya nao mazungumzo na washiriki hao kupata fursa ya kuuliza maswali yao yaliyokuwa yakiwakwaza kuhusu tasnia ya urembo.


  Akizungumza na warembo hao, Lundenga aliwaonya washiriki hao kutojirahisi kutoa rushwa ya ngono ili kujihakikishia nafasi katika mashindano hayo.

  ''Msijirahisi kutoa rushwa ya ngono ili kupata nafasi, hata mimi nitakutafuna bure tu au mwandaaji yeyote atakudanganya tu na kukuacha kama ulivyo kwani mashindano haya yanafuata taratibu zake na kanuni za mashindsano yasiyoweza kutoa fursa kwa waandaaji kutoa upendeleo kwa yeyote'' alisema Lundenga

  Ujumbe huo uliofika kuwatembelea katika shindano hilo, uliwataka kuwa makini kuepuka utapeli wa watu wanaowaomba ngono ili wapewe ushindi.

  "Huwezi kupata ushindi kwa kutoa rushwa ya ngono, majaji wako wengi, je utawapa ngono wangapi ili uweze kufanikiwa kuwa mshindi. Hilo liko wazi kwamba huwezi kufanikiwa kwa kutoa ngono," alisema Lundenga.

  Naye Mratibu wa mashindano hayo, Majuto Omary alisema kuwa katika shindano hilo litakalofanyika Juni 7, litasindikizwa na bendi ya Twanga Pepeta, itakayotumia fursa ya kutambulisha baadhi ya nyimbo zake mpya zilizomo katika albamu ya 12 ijulikanayo kwa jina la Nyumbani ni Nyumbani ambayo itazinduliwa rasmi Juni 30 kwenye viwanja vya Leaders Club jijini.

  Aidha Majuto, alisema kuwa Twanga Pepeta itakuwa ikitumbuiza kwa mara ya kwanza tokea mwaka jana mwezi  julai ambapo ilitumbuiza katika mashindano hayo hayo ya kumsaka mrembo wa Sinza. Alisema kuwa hii ni faraja kubwa kwa mashabiki wa muziki wa dansi na wa masuala ya urembo kwani Twanga Pepeta itakuwa ikimvua taji Redds Miss Tanzania, Brigitte Alfred ambaye atakuwa anavua taji lake la kwanza.
  “Ikumbukwe kuwa twanga pepeta haijatumbuiza Sinza kwa kipindi kirefu na hivyo kuandaa zawadi maalum kwa mashabiki wake katika mashindano hayo yaliyodhaminiwa na Redds Original, Mtandao wa Sufianimafoto.com, Dodoma Wine, Chilly Willy Energy Drink, Fredito Entertainment, CXC Africa, Clouds Media Group na Salut5.com” alisema Majuto.

  Alisema kuwa jumla ya warembo 12 wamejitokeza kuwania taji la mwaka huu la Sinza nan i matarajio ya waandaaji kuwa Miss Sinza wa mwaka huu atatwaa taji hilo na kufuata nyayo za Brigitte ambaye aliweza kutwaa taji la Miss Kinondoni na baadaye Miss Tanzania.

  “Tuna warembo bora ambayo wamedhamilia kufanya kweli katika mashindano ya urembo mwaka huu,  wamepania kulinda hadhi ya mwaka jana, hivyo mashabiki waje kuona warembo bora waliopania kufanya kweli katika mashindano hayo,” alisema.

older | 1 | .... | 95 | 96 | (Page 97) | 98 | 99 | .... | 1897 | newer