Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 967 | 968 | (Page 969) | 970 | 971 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Wizari wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalim

  Na Eleuteri Mangi-MAELEZO, Dodoma

  Serikali imewasilisha Miswada miwili inayohusu Sheria ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali wa mwaka 2016 na ule wa Sheria ya Usimamizi wa Wanataaluma wa Kemia wa mwaka 2016 ambayo imesomwa kwa mara ya pili Bungeni ili ijadiliwe na wabunge.

  Awali akisoma Muswada wa Sheria ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali wa mwaka 2016, Wizari wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalim amesema kuwa madhumuni ya Muswada huo ni kuanzisha Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali na kuweka kisheria majukumu yake.

  Aidha, Waziri Ummy amesema kuwa Muswada huo umezingatia masuala mbalimbali ikiwemo kuanzishwa kwa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali pamoja na kuainisha majukumu yake na kuanzisha Bodi ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali.

  Mambo mengine yaliyozingatiwa katika Muswada huo ni kubainisha utaratibu wa uteuzi wa Mkemia Mkuu wa Serikali, majukumu yake na mamlaka yake, kuifanya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kuwa maabara ya rufaa na msemaji wa mwisho wa Serikali katika shughuli za uchunguzi wa kimaabara wa kikemia, sayansi jinai na vinasaba na Muswada huo utawwzesha kuwekwa utaratibu wa kusajili, kuratibu na kusimamia maabara na shughuli zote za maabara za kikemia, sayansi jinai na vinasaba.

  Zaidi ya hayo, Waziri Ummy amesema kuwa kupitia Muswada huo kitawekwa kifungu maalum chini ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kitakachogharimiwa na Serikali kwa ajili ya uchunguzi wa vielelezo vya makosa ya jinai, majanga na masuala mengine yenye maslahi ya taifa ili kuwezesha utekelezaji wa jukumu hilo kwa ufanisi hali itakayosaidia utoaji wa haki katika vyombo vya maamuzi na kuleta utengamano katika jamii.

  Aidha, Muswada wa pili uliowasilishwa unahusu Sheria ya Usimamizi wa Wanataaluma wa Kemia wa mwaka 2016 ambapo maoni na ushauri yaliyotolewa na Kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma ya Maendeleo ya Jamii yaliyosawilishwa na Jasmin Tisekwa (Mb) kwa niaba ya Mwenyekiti wakamati hiyo Peter Serukamba amesema kuwa Muswada huo utasaidia kutungwa kwa sheria ambayo italeta tija kwa maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla.

  Zaidi ya hayo, Jasmini amesema kuwa Muswada huo utasaidia wanataaluma ya Kemia kukabiliana na maendeleo ya sayansi na teknolojia pamoja kwa kuzingatia taaluma hiyo kwani ina mchango mkubwa katika maendeleo ya sekta za elimu, kilimo, viwanda, sheria, afya, mazingira na jamii kwa ujumla wake. 

  Akisoma maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Waziri Kivuli wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ester Mtiko amepongeza jitihada zinazofanywa na wataalamu wa kemia katika sekta mbalimbali kwa kuwa wana wajibu mkubwa kwa maslahi ya taifa kwa ajili ya usalama na kuendeleza maarifa ya kisayansi.

  0 0

  ZILIZOTUFIKIA HIVI PUNDE: Viongozi wa Ukawa wamekutana jijini Dar es Salaam kwa kikao cha faragha kinachoendelea muda huu jijini Dar es Salaam.

  Kikao hicho kinachomshirikisha kada wa zamani wa CCM, Kingunge Ngombale Mwiru, kimewakutanisha Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Profesa Mwesiga Baregu.
  Stori kamili iko hapa http://www.mwananchi.co.tz/…/1597578-3375530-39k…/index.html


  0 0

    Muonekano wa ndani wa jengo jipya la Abiria la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa J.K. Nyerere, jijini Dar es salaam ambalo bado linaendelea na Ujenzi.
   Mafundi wakiendelea na kazi ndani ya jengo (terminal 3).


  0 0  Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson LwengeAkizungumza katika kipindi cha TUNATEKELEZA kinachoratibiwa na Idara ya Habari (MAELEZO) na kurushwa na Televisheni ya Taifa (TBC)

  Na. Aron Msigwa -Dar es salaam.
  Serikali imesema kuwa itaendelea kuchukua hatua kali za kinidhamu na kisheria kwa watendaji wa sekta ya maji watakabainika kujihusisha na vitendo vinavyohujumu miundombinu ya maji kutokana na maslahi binafsi na kusababisha wananchi kukosa huduma maji katika maeneo mbalimbali nchini. 

  Akizungumza katika kipindi cha TUNATEKELEZA kinachoratibiwa na Idara ya Habari (MAELEZO) na kurushwa na Televisheni ya Taifa (TBC) leo jijini Dar es salaam, Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge amesema baadhi ya watumishi wasio waaminifu wamekuwa wakijihusisha na vitendo vya kuhujumu miundombinu na miradi mipya ya maji inayoanzishwa na Serikali ili waweze kunufaika na biashara ya kuuza maji. 

  Amesema Wizara yake imekwisha kuwasimamisha kazi Mameneja 9 waliokuwa wakihushishwa na wizi wa kimtandao wa maji katika maeneo mbalimbali hususani katika jiji la Dar es salaam.

  ‘’ Nimewasimamisha Mameneja karibu 9 waliokuwa wakihusika na wizi wa kimtandao wa maji na kuwafanya wananchi wakose huduma hii kwa muda mrefu, ninaomba wananchi watoe ushirikiano ili tuwakomeshe wahujumu hawa, tunahitaji kuondoa hali hii kwa kuwa maji ni uhai wa Taifa’’ Amesisitiza 

  Amewaomba wananchi waendelee kutoa taarifa  kwa mamlaka zinazohusika pale watakapobaini vitendo vinavyoihujumu sekta hiyo ili ili hatua stahiki kwa wahusika zichukuliwe ikiwemo kuwafikisha mahakamani wale wote wanaojihusisha na vitendo vya wizi wa maji na kuwafanya wananchi wawe na malalamiko ya kukosa maji.

  Akizungumza kuhusu vipaumbele vya Serikali ya awamu ya tano katika kuboresha sekta ya maji nchini amesema kuwa kiasi cha shilingi Trilioni moja kimetengwa kwa ajili ya kuboresha huduma ya upatikanaji wa maji mijini na vijijini.

  Amesema lengo la Sera ya Maji ni kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma ya maji safi ndani ya umbali wa mita 400 jambo ambalo linaendelea kutekelezwa na kuongeza kuwa tayari miradi ya maji 1200 kati ya 1800 mijini na vijini imekamilika na kuwezesha asilimia 72 ya wananchi vijijini kupata maji na asilimia 80 ya wananchi walio mijini kupata huduma hiyo.

  Amesema Serikali imejitahidi kuwekeza kwenye miundombinu mikubwa ya maji katika maeneo ya mijini hasa katika mikoa yenye idadi kubwa ya watu ikiwemo jiji la Dar es salaam, Mbeya, Mwanza na miji mingine na kuongeza kuwa awamu inayofuata ni ujenzi wa miundombinu ya kusambazia maji katika maeneo mbalimbali.

  ‘’Katika awamu ya kwanza tumefanikiwa sana kuwekeza katika miundombinu mikubwa ya maji hasa kutoa maji kwenye vyanzo vya maji ikiwemo chanzo cha maji cha Ruvu Chini na Ruvu juu na mradi wa kuyatoa maji kutoka ziwa Victoria, sasa tunakwenda awamu ya pili ya ujenzi wa miundombinu ya kusambazia maji hayo’ Amebainisha Mhandisi Lwenge.

  Ameongeza kuwa awamu hiyo ya pili pia itahusisha uondoaji wa miundombinu chakavu katika maeneo mbalimbali ambayo imekua ikisababisha upotevu wa maji kwa asilimia 47 pamoja na kuimarisha mifumo hiyo ili kutimiza lengo la Serikali la kufikia asilimia 95  ya kuwaunganishia maji wananchi ifikapo mwaka 2020.   

  Akifafanua kuhusu utekelezaji wa miradi ya maji maeneo yanayozunguka ziwa Victoria amesema kuwa katika mwaka wa fedha wa 2016/2017 mradi wa maji katika vijiji 100 vilivyo pembezoni mwa bomba kuu la maji linalotoka ziwa Victoria hadi Kahama na Shinyanga itatekelezwa ili kuwawezesha wananchi wanaoishi katika vijiji hivyo kupata huduma ya maji safi.

  Amesema mradi wa kuvipatia maji vijiji hivyo utakwenda sambamba na uboreshaji wa huduma ya maji kwenye vijiji 40 vilivyotambulika katika Halmashauri za Misungwi, Kwimba, Shinyanga na Msalala, Nansio, Geita na  Buselesele pamoja na uboreshaji wa miundombinu ya maji katika jiji la Arusha na mkoa wa Morogoro, Rukwa na Sumbawanga chini ya ufadhili wa Benki ya Maendeleo ya Ufaransa.

  Aidha, kuhusu kilimo cha Umwagiliaji Mhe. Lwenge amesema kuwa Serikali imeanzisha Tume ya Umwagiliaji itakayokuwa na jukumu la kujenga mifumo na miundombinu ya maji pamoja na kusimamia na kutoa ushauri wa kitaalam kwa wananchi katika maeneo ya kilimo.

  Ameeleza kuwa katika mwaka wa fedha 2016/2017 ,Serikali imetenga kiasi cha shilingi Bilioni 39 ili kuiwezesha sekta  hiyo kufanya vizuri na kuwaondoa wakulima kwenye kilimo kinachotegemea mvua pekee kwa kuwa na kilimo endelevu cha umwagiliaji na kutoa wito kwa wananchi kuanza kuvuna maji ya mvua katika maeneo yao.

  Kuhusu ujenzi wa mfumo wa kusafisha maji taka katika jiji la Dar es salaam amesema kuwa katika mwaka wa fedha 2016/2017 Serikali itatekeleza mradi huo kwa kuweka mfumo mpya wa uondoaji na usafishaji wa majitaka yanayozalishwa katika jiji la Dar es salaam ili kuliweka jiji hilo katika hali ya usafi

  Amesema mradi huo utahusisha upanuzi wa miundombinu ya maji taka kwenye maeneo ya katikati ya jiji, ujenzi wa miundombinu mipya ya kupitishia maji hayo katika maeneo ya Ilala, Kinondoni na Temeke.

  "Serikali tumeanza kutekeleza mpango wa kupanua mfumo wa uondoaji na usafishaji wa majitaka yanayozalishwa na watumiaji maji , usanifu wa awali wa miradi mipya ya majitaka umekamilika,kazi inayoendelea ni usanifu wa kina ili kuweza kupata vitabu vya zabuni na michoro itakayotumika kumpata mkandarasi wa ujenzi" Amesisitiza Mhandisi Lwenge.

  Amesema kuwa kupitia mpango huo bomba linalomwaga majitaka baharini litaacha kutumika na badala yake maji hayo yatapelekwa katika mtambo mpya wa kisasa wa kusafisha majitaka ambapo maji hayo ambayo yatakua yamesafishwa yatauzwa na kutumiwa katika shughuli mbalimbali za upozaji wa mitambo na umwagiliaji.


  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasalimia wakazi wa kijiji cha Kitema I wilayani Tandahimba  waliojitokeza kwa wingi kumlaki wakati akiwasili kwenye wilaya hiyo ikiwa sehemu ya ziara yake mkoani Mtwara.

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokelewa kwa burudani ya ngoma wakati akiwasili kwenye makao makuu ya wilaya ya Tandahimba, mkoani Mtwara.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakazi wa wilaya ya Tandahimba  kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Kiwanda cha kubangua korosho cha AMAMA kilichopo wilayani Tandahimba mkoani Mtwara.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kutoka kwa Msimamizi na Mdhibiti wa ubora wa bidhaa Bw. Karim Hassan (kushoto) ya hatua mbali mbali ambazo korosho hupitia wakati wa kubanguliwa kwenye kiwanda cha AMAMA kilichopo Tandahimba mkoani Mtwara.

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amemaliza ziara yake ya siku NNE mkoani Mtwara kwa kuwahakikishia mamia ya wakazi wa wilaya ya Tandahimba mkoani Mtwara kuwa serikali imetenga zaidi ya bilioni 170 kwa ajili ya utekeleza wa mradi mkubwa wa maji katika wilaya hiyo ili kuondoa tatizo la uhaba wa maji kwa  wananchi wa Tandahimba.

  Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo kwa nyakati tofauti wakati akihutubia mkutano wa hadhara mjini Tandahimba na wakati amesimamishwa njiani na wananchi wa vijiji vya Kitama I na Kitama II  ambao walitaka kumsalimia akiwa katika ziara yake ya kikazi wilayani Tandahimba mkoani Mtwara.

  Makamu wa Rais amesema mkakati wa serikali wa sasa unalenga kuhakikisha wananchi wa Tandahimba na wa maeneo mengine nchini wanapata maji safi na salama hali ambayo itaondoa usumbufu wa wananchi kutumia muda mwingi kutafuta maji badala ya kufanya shughuli za maendeleo.

  Amesema anaimani kubwa kuwa mradi huo wa maji utakapokamilika wilayani Tandahimba mkoani Mtwara utakuwa ni suluhu ya kudumu ya uhaba wa maji kwa wananchi hao wa Tandahimba.

  Kuhusu usafirishaji wa korosho kwa njia ya magendo, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ameonya kuwa serikali kamwe haiwezi kuwavulia watu wanaofanya vitendo hivyo na watakaobainika watachukuliwa hatua kali za kisheria ili kukomesha tabia hiyo.

  Makamu wa Rais amesema kuwa biashara ya magendo ya korosho inainyima serikali mapato mengi ambayo yangesaidia shughuli za maendeleo za wananchi hivyo ameuagiza uongozi wa mkoa wa Mtwara uchukue hatua za kukomesha biashara hiyo haramu ambavyo ameifananisha na uhujumu uchumi kwa serikali.

  Kuhusu ubovu wa barabara kutoka mjini Mtwara hadi wilaya ya Tandahimba, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema serikali itajenga kilomita 50 za awali kwa kiwango cha lami katika barabara hiyo ili kuimarisha shughuli za usafiri na usafirishaji kati ya Mtwara mjini na wilaya ya Tandahimba.

  Makamu wa Rais pia ameuagiza uongozi wa mkoa wa Mtwara kukutana haraka na Watendaji wa Wakala wa Barabara wa mkoa wa Mtwara ili kujadiliana kuhusu namna gani ujenzi huo utakavyotekelezwa.

  Akiwa mjini Tandahimba, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ameshiriki katika zoezi la utoaji wa zawadi mbalimbali kwa uongozi wa shule ya sekondari ya Tandahimba kwa kuingia katika shule 10 bora kitaifa katika matokeo ya Kidato cha  Sita ambapo Kampuni ya Startimes imetoa hundi ya shilingi milioni Mbili kwajili ya ujenzi wa mabweni ya wanafunzi wilayani humo.
  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI  0 0


  Ofisi za Mikaela Professional Tailors zinapatikana Ghana Green View, barabara ya Airpot Jijini Mwanza. Wapigie kwa nambari 0767 68 28 88 ili wakuhudumie kwa wakati na kwa ubora.

  Tofauti na ilivyo katika majiji mengine nchini kama vile Jijini Dar es salaam, Jiji la Mwanza halina mwamko mkubwa katika ubunifu wa mavazi.

  Ni kutokana na hali hiyo, Wataalamu na Mabingwa wa Ushonaji wa mavazi ya aina mbalimbali (Kike na Kiume) Jijini Mwanza, Mikalela Professional Tailors, wameahidi kulitambulisha Jiji hilo katika ubunifu wa mavazi ili kuendana na kasi iliyopo katika majiji mengine.

  "Awali nilikuwa nateseka sana. Nguo zangu nilikuwa nikishea Jijini Dar au Arusha na nikizivaa watu wengi wakawa wanauliza niliposhonea na kutamani niwapeleke. Nikaona kumbe Mwanza kuna uhitaji mkubwa wa ubunifu na ushonaji wa mavazi hivyo nikaamua kuanzisha kampuni ya ubunifu na ushonaji wa mavazi ya Mikaela Professional Tailor ili kukata kiu hiyo.

  0 0


  Katika kusherehekea Sikukuu ya Idd El Hajj siku ya Jumatatu Septemba 12, 2016, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli, ametoa msaada wa vyakula wenye thamani ya shilingi laki saba na elfu themanini (780,000), kwa ajili ya Kituo cha kulelea Wazee na Walemavu wasiojiweza cha Bukumbi Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza.

  Akikabidhi msaada huo jana, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, aliuhimiza uongozi wa kituo hicho kusimamia vyema ugawaji wa vyakula hivyo li kuwafikia walengwa, ikizingatiwa kwamba kumekuwa kukiibuka malalamiko kutoka kwa wazee wanaoishi katika kituo hicho kwamba misaada ambayo imekuwa ikitolewa na serikali pamoja na wafadhili mbalimbali imekuwa haiwafikii yote.

  Hata hivyo Kaimu Afisa Mfawidhi wa kituo hicho, Georgina Kwesigabo, alitanabaisha kwamba vyakula na misaana ambayo imekuwa ikitolewa na serikali pamoja na wafadhili mbalimbali kituoni hapo, yote imekuwa ikiwafikia walengwa wote isipokuwa kuna changamoto ya baadhi yao kuuza misaada wanayopatiwa ikiwemo vyakula, jambo ambalo linaulazimu uongozi wa kituo hicho kuandaa utaratibu wa kusimamia misaada hiyo hususani kuwapikia chakula wanaoishi kituoni hapo badala ya kuwagawia chakula ili wajipikie wenyewe.

  Wazee wanaoishi kituoni hapo waliishukuru serikali kwa msaada huo ambapo walisema wanaendelea kumuombea Rais Magufuli na Serikali yake ili iendelee kuboresha kituo hicho ikiweo kuwekewa uzio ili kuondokana na hofu ya kiusalama waliyonayo kwani wakati mwingine wamekuwa wakiibiwa mali zao ikiwemo kuku ambazo wamekuwa wakizifuga.

  Vyakula vilitolewa na Mhe.Rais Magufuli ni, mchele gunia sita (kila gunia kilo 50), mafuta ya kupikia madumu manne (kila dumu lita 20) pamoja na mbuzi wawili.
  Baadhi ya wazee wanaoishi kwenye Kituo cha Bukumbi, wakifurahia mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza baada ya Rais Magufuli kuwapatia msaada wa vyakula kwa ajili ya kusherehekea Sikukuu ya Idd El Hajj, itakayofanyika kesho kutwa jumatatu.
  Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe.John Mongella (mwenye kofia), akimsikiliza mmoja wa wazee katika Kituo cha Wazee Bukumbi.
  Mmoja wa akina mama kwenye Kituo cha Bukumbi akiishukuru Serikali kwa msaada wa chakula ilioutoa kituoni hapo
  Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Mhe.Juma Sweda (kulia), akizungumza wakati wa kukabidhi msaada wa chakula uliotolewa na Mhe.Rais Magufuli katika Kituo cha Wazee Bukumbi wilayani humo. Alisema Serikali inawajali Wazee wanaoishi katika kituo hicho na kwamba ina upendo kwao ndiyo maana inaendelea kuwahudumia.
  Kaimu Afisa Mfawidhi wa kituo hicho, Georgina Kwesigabo, alitanabaisha kwamba vyakula na misaana ambayo imekuwa ikitolewa na serikali pamoja na wafadhiri mbalimbali kituoni hapo, yote imekuwa ikiwafikia walengwa wote isipokuwa kuna changamoto ya baadhi yao kuuza misaada wanayopatiwa ikiwemo vyakula, jambo ambalo linaulazimu uongozi wa kituo hicho kuandaa utaratibu wa kusimamia misaada hiyo hususani kuwapikia chakula wanaoishi kituoni hapo badala ya kuwagawia chakula ili wajipikie wenyewe.
  Vyakula vilivyotolewa na Mhe.Rais Magufuli kwa ajili ya Makao ya Wazee na walemavu wasiojiweza Bukumbi, Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza.
  Huyu mbuzi, tehe tehe tehe!!
  Makao ya Wazee na walemavu wasiojiweza Bukumbi, Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza.

  Imeandaliwa na George Binagi-GB Pazzo wa BMG

  0 0
  TANZANIA
  KENYA

  0 0  TANZANIA
  KENYA

  0 0


  0 0

  Watumishi wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, leo wameshiriki katika Bonanza Maalumu la Michezo ya SHIMIWI kwa watumishi wa Umma, ambalo limefanyika katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.

  Katika Bonanza la leo Mgeni rasmi alikuwa ni Katibu mkuu Utumishi, akimwakilisha Katibu mkuu Kiongozi Balozi JOHN KIJAZI.

  Watumishi wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambao wameshiriki Bonanza la Michezo ya SHIMIWI liliofanyika leo kwenye Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam, wakiwa wamepozi katika Picha ya pamoja. 
  Waliosimama Kutoka Kulia ni Naibu Katibu Mkuu Dkt Kusiluka, Mkurugenzi wa ICT Eliasi Nyabusani pamoja na Msajili wa Hati Subira Sinda wakibadilishana Mawazo leo wakati wa Bonanza la Michezo la SHIMIWI kwa watumishi wa Umma  lililofanyika katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi wa ICT Eliasi Nyabusani ( katikati ) na Mwenyekiti wa Michezo wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ndugu Swagile Msananga wakiwa Sambamba na Katibu ndugu Mwikari Mshana wakati wa Bonanza la Michezo ya SHIMIWI lililofanyika leo Jijini Dar es Salaam Kwenye Uwanja wa Uhuru.

  0 0

  Baadhi ya Wananchi wakiwa wamekusanywa mahali pamoja kwa ajili ya kupatiwa huduma ya kwanza mara baada ya kuathiriwa na taharuki hiyo kufuatia tetemeko la ardhi kutokea mkoani humo

  Nyumba kadhaa Mkoani Kagera zimebomoka baada ya tetemeko la Ardhi lenye nguvu ya 5.7 kipimo cha Ritcher kupita kwenye mikoa hiyo ya Kanda ya Ziwa.

  Taarifa zinadai Mji wa Kamachumu Mkoani Kagera ndio umeathiriwa Vibaya na tetemeko hilo, ambapo nyumba nyingi zimebomolewa.

  Hadi sasa hakuna idadi ya vifo au Majeruhi iliyotolewa na Mamlaka zinazohusika mkoani Kagera.

  Globu ya Jamii bado inaendelea kufuatilia kwa ukaribu taarifa za tukio hilo.


  Gari ya Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji Mjini Bukoba likiwa katika harakati za Uokoaji.

  Nyumba Moja wapo ambayo imeathirika na Tetemeko hilo lililotokea Muda mfupi uliopita Mjini Bukoba.

  Nyumba ikionekana kupata nyufa baada ya tetemeko la Ardhi kuutikisa Mji wa Bukoba hivi Punde

  Milango ya Geti katika nyumba hiyo ikionekana kuanguka chini baada ya kukumbwa na dhoruba ya tetemeko la Ardhi, lililotikisa Mji wa Bukoba.
  Baadhi ya Nyumba za Wananchi wa Mji wa Bukoba Zikiwa katika hali Mbaya baada ya Tetemeko la Ardhi Kupita. 


  0 0


     Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 10 Septemba, 2016 amemteua Bw. Eliya Mtinangi Ntandu kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe.

  Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa nafasi ya Katibu Tawala Mkoa wa Songwe ilikuwa wazi na uteuzi huu umeanza leo.

  Bw. Eliya Mtinangi Ntandu pamoja na Makatibu Tawala walioteuliwa jana tarehe 09 Septemba, 2016 ambao ni Ado Steven Mapunda aliyeteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara na Bw. Tixon Tuliangine Nzunda aliyeteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa wataapishwa katika tarehe itakayotangazwa baadaye.

  Wakati huo huo, Rais Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya 11, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji 1 na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa 1 ili kujaza nafasi zilizokuwa wazi katika Halmashauri hizo.
  Wakurugenzi walioteuliwa ni kama ifuatavyo;

  1.      Godwin Emmanuel Kunambi - Manispaa ya Dodoma
  2.      Elias R. Ntiruhungwa             - Mji wa Tarime
  3.      Mwantumu Dau                     - Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba
  4.      Frank Bahati                          - Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe
  5.      Hudson Stanley Kamoga        - Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu
  6.      Mwailwa Smith Pangani         - Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo
  7.      Godfrey Sanga                       - Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama
  8.      Yusuf Daudi Semuguruka      - Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
  9.      Bakari Kasinyo Mohamed     - Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea
  10.   Juma Ally Mnwele                 - Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo
  11.   Butamo Nuru Ndalahwa       - Halmashauri ya Wilaya ya Moshi
  12.   Waziri Mourice                    - Halmashauri ya Wilaya ya Karatu
  13.   Fatma Omar Latu                 - Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo


  Wakurugenzi wa halmashauri wote 13 walioteuliwa wanatakiwa kuripoti Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mkoani Dodoma siku ya Jumanne tarehe 13 Septemba, 2016 kwa ajili ya kupata maelekezo zaidi.

  Gerson Msigwa
  Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
  Dar es Salaam  10 Septemba, 2016

  0 0


  0 0

  Rais Dkt John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa Wakurugenzi wapya 13,katika Wakurugenzi hao wa Halmshauri,Rais amemteua Mtangazaji wa Clouds Tv, HUDSON KAMOGA Kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mbulu

   


  0 0

  mmg_6544
   Beki wa Yanga, Vicent Andrew akiruka juu kuondosha hatari iliyoelekezwa langoni kwao, katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania bara dhidi ya Timu ya Maji Maji ya Songea, uliopigwa jioni ya leo kwenye Uwanja Uhuru, Jijini Dar es salaam. Yanga imeshinda bao 3-0.
   Hii ni bambi kwa bambi: hapo ni Donald Ngoma wa Yanga, akichuana vikali na Beki wa Maji Maji, Bahati Yussuf.
   Kiungo wa Yanga, Thaban Kamusoko akiwania mpira na Beki wa Maji Maji, Selemani Kibuta wakati wa Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania bara dhidi ya Timu ya Maji Maji ya Songea,
  uliopigwa jioni ya leo kwenye Uwanja Uhuru, Jijini Dar es salaam. Yanga
  imeshinda bao 3-0.
   Kipa wa Timu ya Maji Maji, Aghaton Anthony akiruka kuwania mpira sambamba na Mshambuliaji wa Yanga, Simon Msuva na kugongana.
   Kikosi cha Yanga.
   Kikosi cha Maji Maji “Wanalizombe”.
   Beki wa Yanga, Juma Abdul akijaribu kuuzuia mpira usitoke nje katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania bara dhidi ya Timu ya Maji Maji ya Songea, uliopigwa jioni ya leo kwenye Uwanja Uhuru, Jijini Dar es salaam. Yanga imeshinda bao 3-0.
   Mshambuliaji wa Yanga, Simon Msuva, akionyesha uwezo wa kuuchukua mpira kwa adui yake, wakati wa Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania bara dhidi ya Timu ya Maji Maji ya Songea, uliopigwa jioni ya leo kwenye Uwanja Uhuru, Jijini Dar es salaam. Yanga imeshinda bao 3-0.
   Mshambuliaji wa Yanga, Obren Chirwa, akimtoka beki wa Maji Maji, Ernest Raphael, katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania bara dhidi ya Timu ya Maji Maji ya Songea, uliopigwa jioni ya leo kwenye Uwanja Uhuru, Jijini Dar es salaam. Yanga imeshinda bao 3-0.
   Amis Tambwe wa Yanga, akimpiga tobo maridadi, beki wa Maji Maji, Ernest Raphael, katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania bara dhidi ya Timu ya Maji Maji ya Songea,uliopigwa jioni ya leo kwenye Uwanja Uhuru, Jijini Dar es salaam. Yanga imeshinda bao 3-0.
   Haji Mwinyi anakwenda na mpira.
   Mwamuzi wa Mchezo huo, Emmanuel Mwandembya akiwaamuru wachezaji wa Maji Maji waache kumzonga baada ya kutoa adhabu ya Penati kufuatia mchezaji wa mmoja kuushika mpira ndani ya 18.
   Hii ni pale mzuka wa kushangilia umekupata, halafu ghafla mwamuzi anaamua kuwa hukuupiga vyema mpira huo na kuamuru kurudiwa.
   Mzozo kidogo kati ya Mwamuzi na Wachezaji wa Yanga.
   Inapigwa tena na inapiga besela na kurudi uwanjani.
   anatokea Deus Kaseke na kutupia tena na kuiandikia Yanga bao la kuongoza dhidi ya Maji Maji.
   
  Kipa wa Maji Maji akitafakari baada ya kufungwa.
   Tobo lingine kwa Beki huyu.
   Hii ni bambi kwa bambi: hapo ni Donald Ngoma wa Yanga, akichuana vikali na Beki wa Maji Maji, Bahati Yussuf.
   
   Chenga ya mwili: Mchezaji wa Yanga, Simon Msuva akimkwepa Beki wa Maji Maji, Hamad Kibopile, wakati wa Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania bara dhidi ya Timu ya Maji Maji ya Songea,uliopigwa jioni ya leo kwenye Uwanja Uhuru, Jijini Dar es salaam. Yanga imeshinda bao 3-0.
   Hapo ni ajali kazini.
   Matokeo baada ya ajali hiyo.
   
   

  0 0


  TANZANIA  KENYA
  0 0


  Jumamosi Septemba 10, 2016 kuamkia leo jumapili, kinyang'anyiro kikali cha kumsaka mlimbwende wa Kanda ya Ziwa, (OZONA MISS LAKE ZONE 2016), kimefanyika ambapo Mlimbwende, Eluminatha Dominick (pichani) kutoka mkoani Geita ameibuka mshindi miongoni mwa walimbwende 17 (baada ya mmoja kujitoa) waliokuwa wakiwania taji hilo.

  Ushindi wa mlimbwende huyo ulionekana kuwafurahisha mamia ya watu waliohudhuria kwenye shindano hilo lililofanyika kwenye Viunga vya Rock City Mall Jijini Mwanza, likiwa nimeandaliwa na kampuni ya Flora Talent Promotions chini ya Mkurugenzi wake, Flora Lauwo na kudhaminiwa na makampuni mbalimbali ikiwemo mdhamini mkuu, kampuni ya vipodozi ya OZONA pamoja na 102.5 Lake Fm Mwanza.

  Mbunge wa Jimbo la Geita Vijijini, Mhe.Jeseph Linzwa Kasheku Msukuma, alisema ni furaha kubwa mkoa wa Geita kunyakua taji la Ozona Miss Lake Zone 2016 na kwamba matarajio ni kujiandaa vyema kwa ajili ya kunyakua taji la Miss Tanzania 2016 ikiwa ni sawa sawa na matarajio aliyoyaeleza mlimbwende wa Ozona Miss Lake Zone 2016.

  Na BMG


  Mlimbwende wa Ozona Miss Lake Zone 2016, Eluminatha Dominick (katikati) kutoka mkoani Geita. Mshindi wa pili ni Mery Peter (Miss Mwanza 2016, kushoto) na Mshindi wa tatu ni Lucy Michael (Geita, kulia).
  Mlimbwende wa Ozona Miss Lake Zone 2016, Eluminatha Dominick (katikati) kutoka mkoani Geita. Mshindi wa pili ni Mery Peter (Miss Mwanza 2016, kushoto) na Mshindi wa tatu ni Lucy Michael (Geita, kulia).
  Aliyekuwa akishikilia taji la Miss Lake Zone
  Aliyekuwa Miss Lake Zone (kulia), akikabidhi taji la Miss Lake Zone mpya (kushoto)
  Mgeni rasmi, Mkuu wa Wilaa ya Nyamagana, Mhe.Mary Tesha (kushoto) akimkabidhi mshindi wa Ozona Miss Lake Zone mfano wa ufunguo wa gari alilokabidhiwa kama zawadi. Mshindi wa Ozona Miss Lake Zone amewazadiwa gari lenye thamani ya shilingi Milioni 12 na kampuni ya Ozona.


  Mlimbwende, Eluminatha Dominick (pichani) kutoka mkoani Geita ameibuka mshindi wa Ozona Miss Lake Zone 2016, miongoni mwa walimbwende 17 waliokuwa wakiwania taji hilo.
  Kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Mary Tesha, Mshindi wa Ozona Miss Lake Zone 2016, Eluminatha Dominick, Mbunge wa Jimbo la Geita Vijijini, Joseph Msukuma pamoja na Mkurugenzi wa Kampuni ya Ozona, Dr.Thobias Mkina, wakiwa katika picha ya pamoja.
  Mshindi wa Ozona Miss Lake Zone 2016, Eluminatha Dominick (kushoto) akiwa katika picha na Mbunge wa Jimbo la Geita Vijijini, Joseph Msukuma (kulia).
  Washiriki walioingia nafasi tano bora ni, Eluminatha Dominick (wa pili kushoto kutoka Geita), Mery Peter (wa tatu kushoto kutoka Mwanza, Lucy Michael (wa kwanza kushoto kutoka Geita), Rose Masanja (wa pili kushoto kutoka Shinyanga) na Farida Hassan (wa kwanza kulia kutoka Mara).
  Washiriki 17 wa Ozona Miss Lake Zone 2016
  Ozona Miss Lake Zone akizungumza na Wanahabari baada ya kukabidhiwa gari

  Mchekeshaji Eric Omond kutoka nchini Kenya akizungumza na Vesterjtz wa BMG baada ya show  Kushoto ni Christian Bella, akizungumza na Vesterjtz wa BMG baada ya kudondoka burudani kali  Katikati ni mbunge Joseph Msukuma akizungumza na BMG  Kulia ni mmoja wa wanakamati akihojiwa na BMG  George Binagi-GB Pazzo (ushoto) katika picha ya pamoja na Christian Bella (kulia) baada ya show  Mwanahabari Sadam Sadick (kulia) akishow love na Bella  Ozona Miss Lake Zone 2016 (kushoto) akiwa na Vesterjtz


  Kijukuu kutoka RFA akiwa na Ozona Miss Lake Zone 2016

  Mambo ya karanga fotooo na Ozona Miss Lake Zone 2016  Bonyeza HAPA Kwa Picha za Awali

  0 0


  Mkuu wa Wilaya ya Same Rosemary Staki Senyamule akikagua magunia yaliyokutwa yakiwa yamejazwa Rumbesa
  Mkuu wa Wilaya ya Same Rosemary Staki Senyamule akizungumzia unyonyaji wanaokumbana nao wananchi kutoka kwa wafanyabiashara wanaotaka magunia yaliyojazwa Rumbesa
  Gari aina ya Fuso likiwa limekamatwa mara baada ya kubainika kuwa limebeba magunia ya vitunguu ambayo yamejazwa Rumbesa

  Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Same Anna-Claire Shija akisisitiza jambo wakati wa mkutano na wananchi Wilayani humo

  Dc Staki akikagua mashamba ya wakulima mara baada ya kuzuru katika maeneo hayo


  Mkuu wa Wilaya ya Same Rosemary Staki Senyamule akisisitiza jambo wakati wa mkutano wake na wananchi
  Mkuu wa Wilaya ya Same Rosemary Staki Senyamule pamoja na kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya hiyo wakisikiliza malalamiko ya wananchi  Na Mathias Canal, Kilimanjaro

  Wakulima wa mazao mbalimbali likiwemo zao la vitunguu wametakiwa kutofanya biashara kwa kujaza rumbesa ili kuwanufaisha wafanya biashara ambao wanajitokeza vijijini kunua mazao kwani jambo hilo linawanyonya zaidi wakulima na kuwanufaisha wafanya biashara.

  Marufuku hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Rosemary Staki Senyamule mara baada ya kuitisha mkutano wa wananchi katika ziara yake ya kuwahimiza kwa pamoja kujitokeza kushiriki katika zoezi la upimaji ardhi linaloendeshwa na Halmashauri ya Wilaya ya Same.

  Hata hivyo lengo mahususi la kuamua kuwapo kwa zoezi la upimaji ardhi ni kutaka kuondoa migogoro ya ardhi iliyokithiri katika maeneo mbalimbali Wilayani humo sambamba na kupinga kipimo cha Rumbesa kinachowanyonya wakulima wengi nchini.

  Katika mkutano huo uliofanyika Katika Kitongoji cha Jitengeni na Mvungwe uliwahusisha pia wataalamu wa kilimo na ardhi kutoka katika Halmashauri ya Wilaya hiyo sambamba na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama katika Wilaya hiyo.

  Katika mkutano huo Mkuu wa Wilaya hiyo aliwataka wakazi wa Kijiji cha Ruvu Jiungeni kushiriki kikamilifu katika zoezi la upimaji ardhi hivyo kuwaarifu pia wananchi wote kujitokeza katika mashamba yao wakati wa zoezi la upimaji ili kuondoa adha inayochochea migogoro kati ya wakulima na wafugaji.

  Dc Staki alisema kuwa wananchi wanapaswa kupinga kuzidisha kipimo halisi kinachokubalika kwani kutofanya hivyo ni kukubali kupunjwa na kuinyima Halmashauri mapato.Alisema kuwa wakulima wanapaswa kujiamini kwani mazao wanayolima yana soko popote nchini hivyo kidanganywa kwa kuweka Lumbesa ni kujinyima haki yao ya msingi katika kukabiliana na wimbi la umasikini.

  Aidha kabla ya mkutano na wananchi Dc Staki alitembelea mashamba ya vitunguu na kujionea jinsi ambavyo Rumbesa inavyofungwa.

  Sambamba na hayo pia Mkuu huyo wa Wilaya alimtaka mkuu wa Polisi Wilaya ya Same Asteriko Maiga kusimamia na kulikemea suala la Rumbesa kwenye mageti yote na endapo watawabaini wafanya biashara wanaofanya hivyo wanapaswa kukamatwa na kuchukuliwa hatua.

  Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Same Anna-Claire Shija alisema kuwa wananchi wanapaswa kuwa makini katika kuimarisha kilimo na kujitokeza kwa wingi katika shughuli za maendeleo.

  0 0older | 1 | .... | 967 | 968 | (Page 969) | 970 | 971 | .... | 1897 | newer