Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 961 | 962 | (Page 963) | 964 | 965 | .... | 1904 | newer

  0 0


  Jana Septemba 04, 2016 ilikuwa siku njema kwa waumini wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza, Bwana Robson Mkesha Baliyanga na Miss Penina Mkama, baada ya kufunga ndoa takatifu katika Kanisa la EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza, chini ya Mchungaji Kiongozi Dkt.Daniel Moses Kulola.

  Baada ya ndoa, Hafla ilifanyika kwenye Ukumbi wa Maendeleo House Jijini Mwanza, kama picha inavyoonesha maharusi wakiingia Ukumbini.
  Na BMG
  Maharusi, Bwana Robson Mkesha Baliyanga (kushoto) na Miss Penina Mkama (kulia) wakiingia ukumbini
  Mc Joel Maduka, akitoa mwongozo kabla maharusi kuingia ukumbini
  Mwenyekiti wa kamati ya harusi (kushoto) akiwakaribisha maharusi
  Mchungaji wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya, Dkt.Daniel Kulola, akifungua sherehe kwa maombi
  Maharusi wakikata utepete kuingia ukumbini
  Maharusi wakilishana keki, ishara ya upendo
  Mwanamke heshima
  Wasimamizi/Wapambe wa maharusi nao wakilishana keki
  Maharusi na wapambe wao
  Maharusi wakinyweshana shampeni
  Ndugu, jamaa na marafiki wakiwapongeza maharusi
  Ndugu, jamaa na marafiki wakiwapongeza maharusi
  Mwenyekiti wa kamati ya harusi akitoa neno kwa maharusi
  Kamati ya harusi
  Kamati ya harusi
  Wageni waalikwa
  Waalikwa
  Taswira ukumbini
  Bonyeza HAPA Kwa Picha za Kanisani

  0 0

   Ally Masoud  maarufu kwa jina la Kipanya akiwa katika kijiji na Babu mwenyeji wa kijiji cha Maisha Plus wakijadili jambo wakati wakiwangoja washiriki wa shindano hilo hapo jana ambapo pia ilikuwa ikirushwa live na kituo cha Luninga cha AZAM TWO chaneli 102
   Babu mwenyeji wa kijiji cha Maisha Plus akiwa anaandaa mazingira ya kijijini hapo
   Haya ni Baadhi ya maeneo katika kijiji cha Maisha Plus ambapo washiriki hao kutoka Nchi Tano za Afrika Mashariki watakaa kwa wiki 8
   Washiriki wa shindano la Maisha Plus Msimu wa tano wakiwa wanaingia kijijini huku kila mmoja akiwa amefungwa kitambaa usoni wasijue wapo wapi.
  Mwenyeji wa Kijiji Babu wa Maisha Plus akiwa anawakaribisha washiriki kwa namna yake
   Hapa Washiriki wakiendelea kuingia katika kijiji cha Maisha Plus huku wasifahamu wapo wapi.
   Masoud Kipanya akiwapa maelekezo washiriki wa Shindano la Maisha Plus kabla hawajafugua rasmi vitambaa na kujua wapo wapi
   Hivi ni Baadhi ya Vifaa na vitu ambavyo vijana wa Maisha Plus watakuwa wakivitumia kipindi wapo kijijini kwa Muda wa Wiki8
   Masoud Kipanya akitoa msisitizo wa Jambo kwa washiriki wa shindano la Maisha Plus Msimu wa tano
  Washiriki wa wa Shindano la Maisha Plus Msimu wa tano wakiwa wanafungua vitambaa kuona rasmi kijiji ambacho wataishi kwa wiki 8
  Hapa ilikuwa ni kasheshe baada ya kufungua vitambaa na kukuta wapo porini sehemu wasiyo ijua huku kukiwa hakuna jengo lolote.
  Hapa washiriki wa shindano la Maisha Plus wakiwa wanajipanga kuanza kufanya mchakato wa kuanza kujenga nyumba zao
  Bado shughuli ilikuwa ni Pevu sana hawaelewi kabisa wanaanzia wapi wanaishia kujishauri kwanza huku kila mmoja akiwaza Milioni 30 atazipata vipi?
  Hapa bado shughuli ndio kwanza ilikuwa inaanza washiriki hawa pia walikuwa wakibadilishana mawazo wafanyaje.
  Babu wa Kijiji cha Maisha Plus akiwa anatoa maelezo ya kina kwa washiriki wa shindano hilo ambao wanatoka katika Nchi 5 Afrika Mashariki jinsi gani wataishi, watakavyojenga nyumba zao na watakavyo ishi katika kijiji cha Maisha Plus
  Wakiwa wanaleta mizigo yao ndani ya Kijiji cha Maisha Plus
  Mmoja wa washiriki wa Shindano la Maisha Plus akinoa panga kwa ajili ya kujiandaa kwenda kukata miti kwa ajili ya kujenga nyumba zao za kuishi ambapo kila nyumba moja watakuwa wanaishi washiriki watatu.
  Baadhi ya Mizigo ya washiriki baada ya kuwasili katika kijiji cha Maisha Plus
  Washiriki wa Shindano la Maisha Plus wakiwa wameanza kuandaa makazi yao
  Kazi Ikiendelea ya Kuandaa sehemu ya Kuishi
  Hapa kazi tuu yani kila mtu yupo na yake alimradi tuu wapate kujenga nyumba za kuishi katika kijiji hicho cha Maisha Plus.
  Kulikuwa hakuna namna lazima kila mmoja afanye kazi ili wapate sehemu ya kulala
  Wakati wenzake wamekwenda tafuta Miti ya Kujengea nyumba yeye alikuwa anatengeneza mpini
  Babu wa Kijiji cha Maisha Plus akiwa anatoa maelekezo na kutoa vipimo vya jinsi watakavyokujenga nyumba zao
  Kila mshiriki akiwa ameshika nyenzo yake kwa ajili ya kujenga nyumba zao zakuishi
  Kazi zinaendelea hapa na sasa ilikuwa ni mwendo wa kukata miti ili kuwahi kumaliza kujenga nyumba na kuanza kuishi.
  Babu wa Maisha Plus akiwa anafatilia jambo kijijini hapo.
  Bila kuchakalika na kazi ya kujiandaa kutafuta miti na kujenga nyumba unaweza kujikuta unalala nje
  Baadhi yao walikuwa wamesha anza kuweka nguzo za nyumba zao
  Akionekana akikomaa kuchimba kitu kabla hajawekea mpini
  Ukiwa katika kijiji cha Maisha Plus  lazima upate na ubunifu sana .. hawa jamaa washiriki wa Shindano la Maisha plus msimu wa 5 2016 wakiwa wanakata miti kwa ajili ya kujenga nyumba ambapo wataishi kwa wiki 8
  Pori kwa pori
  Kazi kwa kwenda mbele 

  MAISHA PLUS EAST AFRICA 2016 itakuwa ikionyeshwa na AZAM Two Chaneli 102 
  #HapaKaziTuu
  #VijanaNdioNgazi

  0 0

   Bw. Harusi Abraham Mossi na Mkewe Bi. Rachel Kissui wakiingia Kanisani tayari kwa Ibada ya Ndoa yao iliyofungwa katika Kanisa la Katoriki la Mtakatifu Isidori Bakanja, Parokia ya Boko Jijini Dar es salaam, mwishoni mwa wiki.ia kanisani.
   Maharusi na wapambe wao.
   Ibada kabla ya ndoa.
   Wadau.
   "Abraham Mossi umekubali kumuoa Rachel Kissui?"
  "Rachel Kissui umekubali kuolewa na Abraham Mossi?"
   Bw. Harusi akimvisha pete mkewe.
   Mke akimvisha pete mumewe.
  "Sasa ni mwili mmoja" Abraham na Rachel mwanzo mwisho....
   Tabasamu la nguvu baada ya kumamilisha tendo muhimu katika maisha.
   Hapo viti??
   Bw. Harusi Abraham Mossi akimwaga wino, kwa muongozo wa Padri humu mamsapu wake akimshuhudia.
   Bi. Harusi Rachel Kissui akimwaga wino pia.
   "Unajua nini My Wife, leo ni bonge la siku kwetu"
   Kicheki cha kiaina.
   Maharusi na Familia zao.

   Kamati maalum iliyosimamia vitengo vyote katika harusi hiyo


  0 0
  SIMU.tv: Naibu Spika wa bunge Dkt. Tulia Akson ataka wizara na kamati za kisekta zishirikishwe katika mafunzo ya bajeti; https://youtu.be/7QdpdfnQCoQ
   SIMU.tv: Baadhi ya wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi katika shule ya sekondari Longido mkoani Arusha waiomba serikali msaada wa vifaa vya kukinga ngozi zao;https://youtu.be/XBnctM5_ovk
   SIMU.tv: Mkuu wa mkoa wa Kigoma Brigedia  Jeneral mstaafu Emmanuel Maganga amesema serikali itafanya uchunguzi juu ya vifo vya watoto 7 walioteketea kwa moto ;https://youtu.be/ThRCj-3CRTI
   SIMU.tv: Serikali mkoani Lindi yapiga marufuku manunuzi ya Korosho kwa kangomba ili kuwawezesha wakulima kunufaika na kilimo cha korosho;https://youtu.be/3l3MbplGEso
   SIMU.tv: Mamlaka ya mapato Tanzania TRA yatenga eneo la kibiashara la kariakoo la jijini Dar es Salaam kuwa mkoa maalum wa kodi; https://youtu.be/gfh_bgY6sU0
   SIMU.tv: Wafanyabiashara wa soko la Tarakea wilayani Rombo mkaoni Kilimanjaro wasusia kufanyabiashara katika soko hilo kutokana na kuwa chini ya kiwango;https://youtu.be/iYiIJUdtkcI
   SIMU.tv: Jeshi la kujenga taifa JKT lawataka wahitimu wa mafunzo ya JKT mkoani Kigoma kuwa mstari mbele katika kudumisha maadili; https://youtu.be/PA_dj662mlc
   SIMU.tv: Baadhi ya wakazi wa Zanzibar wampongeza Rais Magufuli kwa kutoa hotuba safi inayosadifu hali ya maisha ya watanzania; https://youtu.be/R6dag5B_X2I
   SIMU.tv: Chama Cha Mapinduzi CCM kimesema hotuba za Rais Magufuli alizozitoa wakati wa ziara yake visiwani Zanzibar ni dira ya kuelekea Tanzania ya viwanda;https://youtu.be/UEWTtg8iB24
   SIMU.tv: Timu ya stand united imeibuka kidedea  katika mchezo wa ligi kuu Tanzania bara baada ya kuitandika Toto African goli moja kwa sifuri:https://youtu.be/rkz0X0HZPow
   SIMU.tv: Baadhi ya vilabu hapa nchini vitalazimika kubadilisha  mifumo yao ya uendeshaji kutoka sports klabu na kuwa football klabu: https://youtu.be/pYyqpNB86C8
   SIMU.tv: Kocha wa timu ya soka ya  wanawake Tanzania bara, amesema timu yake ipo tayari  kwa michuano ya challenge itakayofanyika nchini Uganda; https://youtu.be/JBN-2ucPugQ

  0 0

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dk. Augustine Mahiga akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Shelisheli, Alix Michel.
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dk. Augustine Mahiga akimtambulisha Balozi Innocent Shiyo kwa Rais wa Shelisheli, Alix Michel
  Rais wa Shelisheli, Alix Michel akiwa kwenye kikao na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Baloz Dk. Augustine Mahiga nchini Shelisheli.

  Waangalizi wa uchaguzi wa wabunge wa Shelisheli katika picha ya pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dk. Augustine Mahiga na Balozi Innocent Shiyo. (Picha kwa hisani ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki).
  .
  Tanzania ilikabidhiwa nafasi ya uenyekiti wa kuongoza Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC Organ), katika Mkutano wa 36 wa Wakuu wa Nchi na Serikali uliofanyika huko Mbabane, Swaziland tarehe 29 – 31 Agosti, 2016. 

  Mara baada ya kukamilika kwa Mkutano huo, Mheshimiwa Dkt. Augustine P. Mahiga (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki alielekea Jamhuri ya Shelisheli kwa lengo la kumwakilisha Mheshimiwa Dkt. John P. Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuongoza ujumbe wa Waangalizi wa SADC katika Uchaguzi wa Shelisheli utaofanyika tarehe 8 - 10 Septemba, 2016.

  Wajibu huu wa Tanzania katika kuongoza misheni hiyo ya waangalizi wa uchaguzi imetokana na misingi na muongozo wa chaguzi za kidemokrasia katika Kanda ya SADC. Akiwa nchini Shelisheli, Mheshiwa Mahiga (Mb), alizindua  rasmi misheni hiyo tarehe 2 Septemba, 2016 kwa niaba ya Mheshimiwa Rais Magufuli. Misheni hiyo ya waangalizi itakua na waangalizi kutoka nchi  za SADC .

  Wakati akiwa nchIni Shelisheli, Mheshimiwa Waziri Mahiga alipata fursa ya kukutana na kufanya mazungumzo na Mhe. James Alix  Michel Rais wa Sheliseli .
   Pia Mheshimia Waziri Mahiga aliweza kufanya mazungumzo na Mhe. Joel Morgan,  Waziri wa Mambo ya Nje wa Seychels na kukutana  na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Seychels.

  Imetolewa na :

  BALOZI  INNOCENT E. SHIYO

  0 0


  0 0
  Na Dotto Mwaibale

  MATAIFA 54 ya Barani Ulaya siku ya Jumapili hii yatashuka dimbani katika harakati za kuwania nafasi ya kufuzu ili kuungana na mwenyeji nchi ya Urusi katika michuano ya kombe la dunia itakayofanyika nchini humo mwaka 2018.

  Akitoa taarifa hiyo ya kusisimua kwa mashabiki wa soka nchini Makamu wa Rais wa StarTimes Tanzania, Zuhura Hanif amesema kuwa hii ni habari njema kwa wateja wetu na watanzania kwani wataweza kufuatilia kwa ukaribu kabisa mechi zote moja kwa moja kwenye runinga zao.

  “Michuano ya kuwania tiketi ya kufuzu kwenye kombe la dunia itakayofanyika nchini Urusi mwaka 2018 kwa nchi za Ulaya itakuwa ni yenye ushindani mkubwa ukizingatia ubora wa timu na wachezaji wake. Kwenye michuano hii mashabiki wataweza kujionea moja kwa moja mabingwa watetezi Ujerumani watakapoanza safari yao ya kulitetea kombe hilo kwa kuvaana na Norway.

  Pia macho ya wapenzi wengi wa soka watapenda kuiona Uingereza ikiwa chini ya kocha wake mpya Sam Allardyce watakaposhuka dimbani kucheza na Slovakia.” Alisema Hanif

  “StarTimes inayofuraha kuwataarifu watanzania kwamba mechi zote za michuano hii zitaonekana moja kwa moja kupitia chaneli zetu mahususi kabisa za michezo ambazo ni Sports Focus, Sport Arena, World Football, Sport Arena na Sport Premium.

  Tunafahamu ya kwamba soka ni mchezo unaopendwa sana hapa nchini, na sisi tupo katika kuhakikisha kuwa hilo linawezekana kwa gharama nafuu kabisa.” Aliongezea Hanif

  Mabingwa wa kombe la EURO mwaka 2016 timu ya Ureno nayo itashuka dimbani siku ya Jumatatu ya Septemba 5 kwenye mchezo wa kundi B dhidi ya Uswisi jijini Basel bila ya nahodha wake Christiano Ronaldo ambaye bado anauguza jeraha la goti ambalo lilimfanya atolewe kwenye kipindi cha kwanza kwenye fainali za EURO zilizofanyika nchini Ufaransa.

  “Michezo na burudani ni maudhui ambayo tunayatilia sana maanani StarTimes na ndiyo maana kila kukicha tunazidi kuongeza zaidi. Wateja wetu kwa malipo ya gharama nafuu kabisa ya mwezi wataweza kutazama mechi zote za michuano hii moja kwa moja kwenye chaneli tano tulizonazo mahususi kwa michezo pekee.

  Ninawaomba watanzania kuichangamkia hii fursa kwa kujiunga nasi na kufurahia kwa pamoja mchezo wa soka kupitia visimbuzi vyetu.” Alihitimisha Hanif

  Ratiba ya michezo itakayopigwa siku ya Jumapili ya Septemba 4 ni: San Marino na Azerbaijan (saa 1:00 usiku chaneli ya Sports Focus), Slovakia na Uingereza (saa 1:00 usiku chaneli ya World Football), Lituania na Slovenia (saa 1:00 usiku chaneli ya Sports Life), Denmark na Armenia (saa 1:00 usiku chaneli ya Sports Arena), Kazakhstan na Poland (saa 1:00 usiku chaneli ya Sports Premium), Romania na Montenegro (saa 3:45 usiku chaneli ya Sports Life), Jamuhuri ya Czech na Northen Ireland (saa 3:45 usiku chaneli ya Sports Premium), Norway na Ujerumani (saa 3:45 usiku chaneli ya World Football) na Malta na Scotland (saa 3:45 usiku chaneli ya Sports Arena).

  Michezo ya siku za Jumatatu ya Septemba 5 ni: Georgia na Austria (saa 1:00 usiku chaneli ya World Football), Croatia na Uturuki (saa 3:45 usiku chaneli ya Sports Life), Ukraine na Iceland (saa 3:45 usiku chaneli ya Sports Focus), Wales na Moldova (saa 3:45 usiku chaneli ya Sports Premium), Hispania na Liechtenstein (saa 3:45 usiku chaneli ya Sports Arena), na Israeli na Italia (saa 3:45 usiku chaneli ya World Football).

  Na michezo ya siku ya Jumanne ya Septemba 6 ni: Uswizi na Ureno (saa 3:45 usiku chaneli ya World Football), Bulgaria na Luxembourg (saa 3:45 usiku chaneli ya Sports Focus), Sweden na Uholanzi (saa 3:45 usiku chaneli ya Sports Premium), Belarus na Ufaransa (saa 3:45 usiku chaneli ya Sports Arena), na Cyprus na Ubelgiji (saa 3:45 usiku chaneli ya Sports Life).

  Michuao hii ya kuwania kufuzu kwenye kombe la dunia nchini Urusi mwaka 2018 inaundwa na makundi tisa ambayo ni:

  Kundi A ni: Netherlands, France, Sweden, Bulgaria, Belarus na Luxembourg; Kundi B ni: Portugal, Switzerland, Hungary, Faroe Islands, Latvia, na Andorra; Kundi C ni: Germany, Czech Republic, Northern Ireland, Norway, Azerbaijan, na San Marino; Kundi D ni: Wales, Austria, Serbia, Republic of Ireland, Moldova, na Georgia; Kundi E: ni Romania, Denmark, Poland, Montenegro, Armenia, na Kazakhstan; Kundi F ni: England, Slovakia, Scotland, Slovenia, Lithuania, na Malta; Kundi G ni: Spain, Italy, Albania, Israel, FYR Macedonia, na Liechtenstein; Kundi H ni: Belgium, Gibraltar, Bosnia and Herzegovina, Greece, Estonia, na Cyprus; Kundi I ni: Croatia, Kosovo, Iceland, Ukraine, Turkey na Finland.

  0 0

   Walimu wa Home Gym wakikata keki ya maadhimisho ya miaka 18 kwa pamoja katika sherehe zilizofanyika fukwe za Escape One mwishoni mwa wiki.
   Keki maalum.

   Wanachama wa Home Gym Wakiwa katika mazoezi mbalimbali
   Mazoezi yakiendelea kuadhimisha siku hiyo
   Wanachama wa Home Gym Wakiwa katika mazoezi mbalimbali
  Wanachama wa Home Gym Wakiwa katika mazoezi mbalimbali
  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

  MKURUGENZI wa Kituo cha kufanyia mazoezi ya viungo Home Gym, Andrew Mangomango amesema kuwa kwa mwaka huu maadhimisho ya miaka 18 toka kuanzishwa kwake yatazunguka katika baadhi ya mikoa.

  Akizungumza wakati wa maadhimishi hayo yaliyifanyika Katika fukwe za Escape One mwishoni mwa wiki, Mangomango amesema kuwa ndani ya miaka 18 ameweza kupata wanachama wa kudumu takribani 200 na ameweza kuwasaidia watu mbalimbali kufahamu jinsi gani ya kufanya mazoezi.

  Mangomango amesema kuwa, maadhimisho haya ni ya tano mfululizo na kwa mwaka wameamua kutembelea baadhi ya mikoa ikiwemo Tanga, Arusha na Mwanza ambapo baadhi ya wanachama wake wa siku nyingi wapo kule na watatumia fursa hiyo kuhamasisha watu mbalimbali kufanya mazoezi kwa afya.

  "Na katika kuendeleza michezo, Kituo cha Home Gym kimeweza kutoa walimu takribani nane ambao wote wameshafungua Gym zao mikoa mbalimbali, hii ni moja ya mafanikio tuliyoyapata na zaidi bado tunashirikiana nao na hata leo kwenye maadhimisho haya wapo wote wamekuja kuunga mkono jitihada za Home Gym,"amesema Mangomango.

  Katika maadhimisho yaliyohudhuriwa na baadhi ya wadau wa michezo ikiwemo Mkurugenzi wa Kampuni ya EAG, Imani Kajura, waandishi wa habari mbalimbali na taasisi zingine wameonyesha muitikio mkubwa wa kufanya mazoezi na kuhamasisha watu wajitokeze kwani Michezo ni Afya.

  Kwa mwaka huu, Mangomango amesema kuwa mwaka huu watafanya maadhimisho yao sambamba na Kumbukumbu ya Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Oktoba 14, mkoani Arusha.

  0 0  0 0

  Waziri Nape

  Anitha Jonas – WHUSM

  04/09/2016

  DAR ES SALAAM.

  Muswada wa Huduma za Vyombo vya Habari kusomwa kwa mara ya kwanza Bungeni Septemba hii na kujadiliwa Desemba Mwaka huu. .

  Kauli hiyo ilitolewa leo na Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye alipokuwa akizungumza katika kipindi cha TUNATEKELEZA kilichorushwa na TBC 1,chenye lengo la Mawaziri kueleza umma namna wanavyotekeleza majukumu.

  “Muswada huu mzuri na utasaida kuleta suluhishi la malalamiko ya kuwepo kwa sheria kandamizi,pia itasaidia kukuza tansia ya habari pamoja na kuifanya tasnia ya habari kuheshimiwa kama tansia nyingine”,alisema Waziri Nnauye.

  Waziri Nnauye alisisitiza kuwa uandaaji wa Muswada ulishirikisha wadau mbalimbali na kuzingatia maoni yao na serikali itaendelea kupokea maoni ya wadau hata mara baada ya kusomwa kwake.

  Pamoja na hayo Waziri huyo mwenye dhamana na sekta ya habari nchini kupitishwa kwa Muswada huo kutasaidia kutoa suluhisho la kuwepo na changamoto katika sekta ya utangazaji ambayo kwa sasa inaonekana kupoteza mulekeo.

  Aidha,Waziri Nnauye alisema kuwa serikali inataka kuipeleka tansia ya habari mbali na kupitia Muswada huo utasaidia kufanikisha hilo kwani umeeleza kuwa mwandishi anahitajika kuwa na digrii na hii ni kwalengo la kuweka heshima ya taaluma kama ilivyokwa taaluma nyingine mfano sheria.

  Halikadhalika Waziri huyo alizungumzia kuwepo na changamoto katika Sheria ya Utangazaji kwani imekuwa haionyeshi Mtangazaji anaporusha kipindi hewani kilicho kinyume na maadili ni adhabu gani apewe,

  “Tungependa sheria ijayo iweze kumbana mwandishi pale anapokosa maadili na kumchukulia hatua kama ilivyo kwa tansia nyingine kama uhandisi na sheria kufikia hatua kufutiwa utoaji wa huduma hiyo”,alisisitiza Mhe.Nnauye.

  Akizungumza kuhusu changamoto ya upatikanaji wa taarifa kutoka kwa wasemaji wa taasisi za Serikali Waziri Nape alisema tayari ametoa agizo kwa watendaji kuwashirikisha wasemaji katika vikao vya maamuzi ili waweze kuwa na taarifa za pamoja na kuwapa nafasi ya kusema ikiwa na sehemu ya kazi yao.

  Hata hivyo Mheshimiwa Waziri ameliahidi Shirika la Utangazaji nchi kulisaidia kutatua changamoto zinazolikabili ikiwemo uhaba wa vifaa,pamoja na kuboresha maslai ya watumishi wake.Pia ameeleza Bodi mpya ya TBC 1 iliyoundwa imepitia mkataba wa TBC 1 na STARTIMES kwa lengo la kutaka kuiboreshea mazingira shirika hilo na tayari imekwisha maliza kazi na kuwasilisha mapendekezo.

  0 0

  Mechi mbalimbali zikiwa zinaendelea katika Bonanza hilo ambalo lilikuwa na lengo la kuhamasisha Michezo, usafi na Afya Bora.
  Baadhi ya watu wadogo kwa wakubwa wakiendelea kufuatilia Bonanza hilo kwa makini 
  MC Fadhili Nandonde akiendelea kutoa utaratibu wa Mechi mbalimbali zilizokuwa zikicheza katika Bonanza hilo.
  Mgeni Rasmi katika Bonanza hilo Albert Kimaro ambaye ni Mkufunzi Mwandamizi Idara ya Michezo Chuo Kikuu cha Dar es salaam akikagua moja ya Timu hizo katika Bonanza hilo.
  Mgeni Rasmi katika Bonanza hilo Albert Kimaro ambaye ni Mkufunzi Mwandamizi Idara ya Michezo Chuo Kikuu cha Dar es salaam akizungumza na watu waliofika katika bonanza hilo na kuwapongeza waandaaji kwa kuona umuhimu wa Mazoezi, usafi na Afya Bora pia amewasihi watu wawe na utaratiu wa kufanya Mazoezi.
  Mwakilishi Kutoka Benki ya NMB ambao walikuwa ni moja ya wadhamini 
  wa Bonanza hilo Frank Rwamugira akiwasihi watu kuwa na utaratibu wa kujiwekea akiba 
  Watu mbalimbali wakiendelea kufuatilia Michezo hiyo , hata Boda boda nao walikuwa bize na Bonanza hilo.
  Mbuzi huyu ndio ilikuwa zawadi ya Mshindi katika Bonanza hilo lililoandaliwa na Songas Football Club.
  Rais wa Songas Football Club Ismail Sheha ambao ndio walioandaa Bonanza hilo akitoa neno la shukurani kwa wote ambao walihudhulia katika Bonanza na kusisitiza kuwa huo haukuwa mwisho wataendelea zaidi kuhamasisha Michezo, usafi na Afya Bora.
  Watu mbalimbali wakiwa katika Banda la NMB kwa ajili ya kufungua akaunti ya Chapchap ambapo Mteja anaipata papo hapo na kupata maelezo ya huduma mbalimbali zinazotolewa na Benki hiyo.
  Moja ya timu ikiwa imefungwa goli la kizembe huku goli kipa asijue cha kufanya na wachezaji wengine kukimbia kwa ajili ya kujipanga zaidi.
  Mpira ukiendelea huku watu mbalimbali wakifuatilia Burudani hiyo kwa makini.

  Picha na Fredy Njeje/Blogs za Mikoa.

  0 0  Mechi mbalimbali zikiwa zinaendelea katika Bonanza hilo ambalo lilikuwa na lengo la kuhamasisha Michezo, usafi na Afya Bora
  Baadhi ya watu wadogo kwa wakubwa wakiendelea kufuatilia Bonanza hilo kwa makini
  MC Fadhili Nandonde akiendelea kutoa utaratibu wa Mechi mbalimbali zilizokuwa zikicheza katika Bonanza hilo
  Mgeni Rasmi katika Bonanza hilo Albert Kimaro ambaye ni Mkufunzi Mwandamizi Idara ya Michezo Chuo Kikuu cha Dar es salaam akikagua moja ya Timu hizo katika Bonanza hilo
  Mgeni Rasmi katika Bonanza hilo Albert Kimaro ambaye ni Mkufunzi Mwandamizi Idara ya Michezo Chuo Kikuu cha Dar es salaam akizungumza na watu waliofika katika bonanza hilo na kuwapongeza waandaaji kwa kuona umuhimu wa Mazoezi, usafi na Afya Bora pia amewasihi watu wawe na utaratiu wa kufanya Mazoezi
  Mwakilishi Kutoka Benki ya NMB ambao walikuwa ni moja ya wadhamini wa Bonanza hilo Frank Rwamugira akiwasihi watu kuwa na utaratibu wa kujiwekea akiba

  Watu mbalimbali wakiendelea kufuatilia Michezo hiyo , hata Boda boda nao walikuwa bize na Bonanza hilo

  Mbuzi huyu ndio ilikuwa zawadi ya Mshindi katika Bonanza hilo lililoandaliwa na Songas Football Club
  Rais wa Songas Football Club Ismail Sheha ambao ndio walioandaa Bonanza hilo akitoa neno la shukurani kwa wote ambao walihudhulia katika Bonanza na kusisitiza kuwa huo haukuwa mwisho wataendelea zaidi kuhamasisha Michezo, usafi na Afya Bora.
  Watu mbalimbali wakiwa katika Banda la NMB kwa ajili ya kufungua akaunti ya Chapchap ambapo Mteja anaipata papo hapo na kupata maelezo ya huduma mbalimbali zinazotolewa na Benki hiyo.
  Moja ya timu ikiwa imefungwa goli la kizembe huku goli kipa asijue cha kufanya na wachezaji wengine kukimbia kwa ajili ya kujipanga zaidi
  Mpira ukiendelea huku watu mbalimbali wakifuatilia Burudani hiyo kwa makini


  Picha na Fredy Njeje/Blogs za Mikoa

  0 0

  0 0

  Mkurugenzi Msaidizi Utekelezaji wa Katiba kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Bw. Kamana Stanley akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu kuanza kutekelezwa kwa Sheria ya Kuwalinda Watoa Taarifa za Uhalifu na Mashahidi ya mwaka 2016 inayolenga kuimarisha utawala bora na mapambano dhidi ya uhalifu nchini. Kulia kwake ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa wizara hiyo Sheiba Bullu.


  Na. Fatma Salum – Dar es salaam.

  Serikali imeanza kutekeleza Sheria ya Kuwalinda Watoa Taarifa za Uhalifu na Mashahidi ya mwaka 2016 (The Whistleblower and Witness Protection Act. 2016) ili kuimarisha utawala bora na mapambano dhidi ya uhalifu nchini.

  Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Msaidizi Utekelezaji wa Katiba kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Bw. Kamana Stanley wakati akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu kuanza kutumika kwa sheria hiyo.

  Stanley amesema kuwa  kuwepo kwa sheria hiyo kutasaidia kuwapatia ulinzi wa kisheria wale wote wanaotoa taarifa za uhalifu wa makosa ya aina mbalimbali wanayoshuhudia yakitendeka. Vilevile itarahisisha utoaji na upatikanaji wa taarifa za uhalifu kwani sasa taarifa hizo zitatolewa na kupokelewa sio tu kwenye vyombo vya dola pekee bali pia kupitia vyombo vya habari na vyanzo vingine vinavyobainishwa katika sheria hiyo.

  “Wananchi wasiwe na woga kujitokeza kutoa taarifa za uhalifu na matendo ya aina zote yanayofanywa kinyume cha sheria kwani taarifa hizo zitakuwa siri na zitafanyiwa kazi bila ya kuwataja watoa taarifa. Pia mashahidi wanapotakiwa kufika mahakamani wasiogope kwani sheria hii inawalinda” amesema Stanley. 

  Amefafanua kuwa wahusika watakaoshindwa kushughulikia vyema taarifa zinazotolewa kwao na kuruhusu watoa taarifa na mashahidi kupata madhara, sheria hiyo imeweka utaratibu wa namna ya kushughulika nao.

  Aidha, Stanley ameeleza kuwa katika sheria hiyo wale ambao taarifa zao zitafanikisha kuokoa mali ya umma, kupatikana kwa wahalifu na kulinda mazingira na maisha ya binadamu kutokana na uhalifu uliopangwa kufanyika, wamewekewa utaratibu wa kupatiwa motisha ikiwa ni pamoja na kuwafidia wale ambao wataathirika kutokana na taarifa walizotoa.

  Stanley ameongeza kuwa Serikali inatarajia kwamba kutungwa kwa sheria hii kutaleta matokeo chanya katika kupambana na uhalifu wa aina zote hivyo kukuza ari ya wananchi kusimamia wenyewe juhudi za kujiletea maendeleo.

  “Masuala ya usimamizi wa utawala wa sheria yataimarika kutokana na kuwepo kwa utayari wa wananchi kushiriki katika mapambano dhidi ya uhalifu kwa kufika katika vyombo vya sheria kutoa ushahidi. Pia ushiriki wao katika kufichua maovu yakiwemo yanayosababisha hasara kwa taifa utasaidia kuinua uchumi ukizingatia kwamba sasahivi Serikali inapambana sana na mafisadi” ameeleza Stanley.

  Sheria ya Kuwalinda Watoa Taarifa za Uhalifu na Mashahidi ya mwaka 2016 (The Whistleblower and Witness Protection Act. 2016)imeanza rasmi kutumika Julai Mosi mwaka huu baada ya kuidhinishwa na Waziri mwenye dhamana ya usimamizi wa sheria Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe.

  0 0

   Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Benoit Janin akimkabidhi Mbuzi mwakilishi wa Kituo cha Kulelea watoto yatima na wanaoishi kwenye mazingira magumu cha Kurasini National Childrens Home, Silas Kusewa Kurasini jijini Dar es Salaam leo.
   Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Benoit Janin akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa kuzindua ofa maalumu kwa wateja wanaotumia mtandao wa simu za Mkononi wa Zantel ofa ya shinda mbuzi, pamoja na kutoa mbuzi kwa Vituo 50 vya kulelea watoto yatima jijini Dar es Salaam.
   Meneja huduma na bidhaa wa Zantel, Ernest sengeu akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo mara baada ya Mkurugenzi Mkuu wa Zantel Tanzania kuzindua Ofa maalumu kwa wateja wa nzantel ambapo wateja watajiunga kwa kubonyeza *149*15# ili kushiriki ofa hiyo ambayo mwisho nwake ni sikukuu ya Idd ya Kuchinja amayo itakuwa Septemba 13. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Benoit Janin.
   Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Benoit Janin akimkabidhi Mbuzi mwakilishi wa Kituo cha Kulelea watoto yatima na wanaoishi kwenye mazingira magumu cha Tanzania Mitindo House Klichopo Kiamboni, Khadija Mwanamboka mara baada ya Mkurugenzi huyo kuzindua Ofa maalumu kwa wateja wake ya shinda mbuzi.
  Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Benoit Janin akimkabidhi Mbuzi mwakilishi wa Kituo cha Kulelea watoto yatima na wanaoishi kwenye mazingira magumu cha Help2kids.Org, Leah Mchomvu Kituo kilichopo Mbezi Beach jijini Dar es Salaam leo.

  KAMPUNI ya Simu za Mkononi Zantel imezindua Kampeni ya Jibwage na Mbuzi katika kusherehekea Sikukuu ya Idd el Adha, ikitambulika pia kama 'Sherehe ya Kuchinja' kwa kutoa mbuzi 500 kwa wateja wake wenye matumizi ya  zaidi huku mbuzi 100 wakigawiwa katika vituo mbalimbali vya watoto yatima nchini.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Benoit Janin amesema "Hii ni sehemu ya kuwashukuru wateja wetu na kusherehekea pamoja nao Sikukuu ya Idd. Imekuwa ni utamaduni wetu kurudisha katika jamii kupitia kampeni na miradi mbalimbali, hivyo kwa leo Zantel inatoa mbuzi 500 katika kusherehekea Sikukuu hii ya Kuchinja.”

  Idd el –Adha ni moja ya sikukuu mbili muhimu za Kiislamu ambayo waumini wa dini ya kiislamu huiadhimisha kwa kuonyesha umuhimu wa kutoa sadaka kwa kuchinja na ibada.

  Mbuzi 400 watatolewa kwa wateja wa Zantel wenye matumizi zaidi kuliko wengine na ambao watakuwa wamejisajili katika kampeni kwa kupitia *149*15# na kuchagua  “Jibwage na Mbuzi”. Kujisajili katika promosheni hii ni bure kwa wateja wote wa Zantel. Kila siku wateja 40 watakaokuwa wametumia muda zaidi watajizawadia mbuzi.

   “Hii si bahati nasibu, wale wateja wa juu watakaokuwa wametumia dakika nyingi bila kuchezeshwa mchezo wa bahati watakuwa wamejizawadia moja kwa moja hivyo natumia fursa hii kuwahamasisha wateja wetu kujisajili ili kupata mbuzi na kusambaza furaha ya Eid katika familia zao” alisema  Benoit

  Mbuzi 100 wanaobaki watatolewa msaada kwa  vituo vya watoto yatima vilivyochaguliwa katika mikoa mbalimbali. 

  “ Pia tunatumia nafasi hiyo hiyo kusaidia watoto yatima na wale wasioweza kufanikisha sadaka hii ya kuchinja ili nao wafurahi pamoja na wengine na kushiriki upendo unaotokana na Idd”,  ameongeza.

  Miongoni mwa miradi ambayo Zantel imetoa misaada ni mradi wa kina mama wanaozalisha zao la mwani Unguja, huduma za maktaba Zanzibar –Zanzibar Library Services, vile vile kompyuta na internet ya bure kwa kikundi cha wasanii cha Mkubwa na Wanawe na vituo mbali mbali vya walimu Zanzibar.

  0 0

   Mkurungenzi wa maendeleo ya soka la wanawake Tanzania Amina Karuma akiongea na waandishi wa habari wakati wa kuchezesha droo ya michuano ya vijana chini ya umri 17 ya Airtel Rising Stars ngazi ya taifa. Katikati ni Mkurungenzi wa Ufundi TFF na kulia Afisa Uhusiano Airtel Tanzania Jana Matinde.
   Afisa Uhusiano Airtel Tanzania Jane Matinde akiongea wakati wa kuchezesha droo ya fainali za taifa ya michuano ya vijana chini ya umri 17 ya Airtel Rising Stars. Kushoto ni Mkurungenzi wa maendeleo ya soka la wanawake TFF Amina Karuma na katikati Mkurugenzi wa Ufundi TFF Salum Madadi. Mkurugenzi wa Ufundi TFF Salum Madadi.
  Mkurungenzi wa Ufundi TFF Salum Madadi akiongea na waandishi wa habari wakati wa kuchezesha droo ya michuano ya vijana chini ya umri 17 ya Airtel Rising Stars ngazi ya Taifa. Kushoto ni Mkurungenzi wa maendeleo ya soka la wanawake Tanzania Amina Karuma.

  TIMU za soka za wasichana za Lindi na Arusha zimepangwa kukutana katika mechi ya fungua dimba ya mashindano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Statrs ngazi ya taifa katika uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, jijini Dar es Salaam, Jumanne, Septemba 6, 2016.

  Mashindano hayo yanayojumuisha timu za wasichana na wavulana yatafunguliwa rasmi siku hiyo ya Jumanne mchana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Paul Makonda ambaye atashuhudia mechi ngumu ya wavulana kati ya Mwanza na Ilala.

  Timu nyingine zinazoshiriki katika michuano hiyo yenye lengo la kuibua vipaji ni Temeke, Kinondoni, Morogoro, Arusha, Mbeya, Lindi na Zanzibar. Tayari timu zimeshawasili na kupiga kambi katika shule ya Filbert Bayi iliyoko Kibaha.

  Akizungumza wakati wa hafla ya kupanga makundi iliyofanyika katika ofisi za shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF), Mkurungenzi wa Ufundi Mwalimu Salum Madadi alisema kuwa maandalizi yote ya mashindano hayo ngazi ya taifa yamekamilika.

  Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na mkurengenzi wa maendeleo ya soka la wanawake nchini Bi Amina Karuma ambaye aliyaelezea mashindano ya Airtel Rising Stars kuwa ni chemchem ya wanasoka chipukizi wasichana kwa wavulana.

  “Mashindano ya Airtel Rising Stars yametusaidia kupata wachezaji wenye vipaji vya ajabu ambao wanaunda timu za Serengeti Boys na timu ya taifa ya wanawake yaani Twiga Stars”, alisema na kuwashukuru Airtel Tanzania kwa kuendelea kudhamini mashindano hayo.

  Kwa upande wake, Ofisa Uhusiano wa Airtel Tanzania Jane Matinde alisema kuwa kampuni yake inajivunia kuweza kutoa mchango katika soka la Tanzania. “Airtel Rising Stars imekuwa chanzo cha kutumainiwa kwa klabu na timu za Taifa kupata vijana chipukizi wenye vipaji. Tunaona fahari kuweza kupata fursa ya kudhamini soka nchini Tanzania“alisema Matinde.

  Michuano ya Airtel Rising Stars ngazi ya Taifa inatarajia kufikia tamati siku ya Jumapili, Septemba 11, 2016 ambapo bingwa kwa upande wa wasichana na wavulana watapatikana na kukanidhiwa vikombe vya ubingwa.

  Vilevile TFF itatangaza wachezaji nyota kwa wasichana na wavulana wataochaguliwa kuunda timu ya Airtel Rising Stars mwaka 2016.

  0 0

   ashiriki wakiwa katika picha ya pamoja baada ya ufunguzi wa mafunzo. 
   Baadhi ya washiriki wakijadiliana jambo baada ya kupata mafunzo juu ya uwekezaji katika miradi ya umma.
   Naibu Katibu Mtendaji –Uchumi jumla kutoka Tume ya Mipango Bi. Lorah Madete, akiwaonyesha maafisa mipango kutoka mikoa ya Arusha, Tanga, na Kilimanjaro mwongozo wa kusimamia uwekezaji wa miradi ya Umma.
   aibu Katibu Mtendaji –Uchumi jumla kutoka Tume ya Mipango Bi. Lorah Madete, akiwaonyesha maafisa mipango kutoka mikoa ya Arusha, Tanga, na Kilimanjaro mwongozo wa kusimamia uwekezaji wa miradi ya Umma.
   Mhandisi. Arnold Masaki moja ya wakufunzi akieleza jambo kwa washikiri wa mafunzo ya Uwekezaji katika miradi ya umma.
  Washikiri wa mafunzo ya Uwekezaji katika miradi ya umma wakifuatilia kwa makini mafunzo. 

  Na Oyuke Phostine
  Wizara ya Fedha na Mipango – Tume ya Mipango inatoa mafunzo kwa maafisa mipango kutoka mikoa ya Arusha, Tanga na Kilimanjaro ili kuwawezesha kuchambua na kuchagua miradi itakayoleta tija kwa taifa na inayoendana na Mpango wa Pili wa Maendeleo ya Miaka Mitano.

  Akizindua mafunzo hayo yatakayofanyika kwa siku tani katika kanda ya kaskazini jiijjini Arusha, Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango anayeshuhghulika na Biashara za Kimataifa Bw. Paul Sangawe alibainisha kuwa lengo kuu la mafunzo haya limejikita katika kuimarisha uwezo wa maafisa mipango ili waweze kuibua miradi inayotekelezeka kwa urahisi na ufanisi.

  Uwepo wa mwongozo huu katika uwekezaji wa miradi ya umma utasaidia kuboresha usimamizi na utekelezaji wa miradi ya umma kwa kuonyesha taratibu za kuzingatiwa ili kuhakikisha miradi iliyochaguliwa inaendana na bajeti ya maendeloa ya taifa.

   “Baada ya mafunzo haya, ni mategemeo yetu kuwa mwongozo huu utawasaidia maafisa mipango kufanya upembuzi makini na uliyo sahihi ili kuja na miradi bora itakayotuepusha na matumizi mabaya ya fedha za umma saula ambalo kwa kipindi cha nyuma limekuwa likijitokeza huko nyuma. Hivyo jitihada hizi ni vema zikazaa matunda chanya” alisema Bw. Sangawe.

  Kutokana na kutokuwepo kwa mwongozo wa kupembua na kuchagua miradi ya uwekezaji katika sekta ya umma Tume ya Mipango imeandaa Mwongozo kwa maafisa mipango wote nchini. Mwongozo huu utasadia kwa kuelekeza taratibu na kanuni zitakazotumika kataka kuchagua, kufadhili, kutekeleza na hata kuperemba na kutathimini miradi ya umma.

  Ili kufikia malengo ya kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025, uchambuzi wa kitaalamu katika masuala ya fedha, athari za kiuchumi  na kijamii katika miradi tajwa inapaswa kusimamiwa vema ili kuleta uwiano sawia kati ya miradi hiyo iliyochaguliwa na bajeti ya taifa ya miradi ya maendeleo.

   “Lengo hilo linabeba matarajio ya wananchi wengi, japokuwa si suala ambalo ni rahisi kutekeleza bila kuwa na nidhamu katika uchaguzi wa miradi. Namana pekee ya kulifikia hii ndoto ni kwa kuhakikisha kidogo tulichonacho tunakitumia katika vipaumbele vya msingi vya taifa na inatumika ipasavyo” aliongeza Bw. Sangawe.

  Mwongozo huu katika uwekezaji wa umma unakuwa ni muhimili mkubwa katika utelezaji wa miradi ya maendeleo iliyopendekezwa katika Mpango wa Pili wa Miaka Mitano wa Maendeleo ya Taifa ambao umelenga kutumia kiasi cha trilioni 11.8 kila mwaka ndani ya mwika mitano ijayo. Hivyo kiwango hiki kikubwa cha fedha ni lazima kifadhili miradi muhimu ya miundombinu na rasilimali watu. 

  0 0


  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) January Makamba akiongea na Balozi wa Sweden Nchini Tanzania Bi. Katarina Rangnitt. Balozi huyo aliambatana na Kamati ya Mazingira na Kilimo ya Bunge la Sweden.

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) January Makamba (Kulia) akifurahia jambo na mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Mazingira na Kilimo kutoka Sweden walipomtembelea Ofisini kwake Mtaa wa Luthuli Jjijni Dar es Salaam leo.
  Sehemu ya wabunge kutoka Sweden wakifuatilia mazungumzo baina ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) January Makamba. Ujumbe huo wa Wabunge ulimtembelea Mh. Waziri na kujadili masuala ya Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira.

  0 0

  Mgeni Rasmi ambaye alimwakilisha mkuu wa wilaya ya Arusha.Afisa Tarafa wa jiji la Arusha Felician Rutahengerwa akisoma hotuba hiyo mbele ya wadau wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira jijini Arusha leo kushoto ni mwenye miwani ni Mkurugenzi wa Auwsa Ruth Koya na kulia ni Mwenyekiti wa bodi ya Auwsa Job Laizer na mjumbe wa bodi hiyo wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi kwenye mkutano wa Maboresho ya rasimu ya mkataba wa huduma za mteja,picha zote na mahmoud ahmad wa michuzi blog arusha

  Wadau mbali mbali waliopata nafasi ya kushiriki katika mkutano wa maboresho ya huduma kwa mteja wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi hayupo pichani katika viwanja vya makumbusho jijini Arusha leo

  Mkurugenzi wa Auwsa Ruth Koya akiongea na kujibu maswali ya wadau wa mamlaka hiyo na wakazi wa jiji la Arusha juu ya maboresho ya rasimu ya huduma kwa mteja leo jijini Arusha picha na mahmoud Ahmad wa michuzi blog Arusha

  Baadhi ya wadau na wakazi wa jiji la Arusha wakifuatilia majibu ya mkurugenzi juu ya uboreshaji wa huduma kwa mteja kwenye viwanja vya makumbusho jijini Arusha
  Maafisa wa kitengo cha Mawasiliano na uhusiano wa Mamlaka hiyo wakiwa wanaratibu shughuli hiyo kama walivyokuwatwa na kamera ya matukio ya michuzi blog jijini Arusha leo

  Maafisa wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira wakiandika maelezo na malalamiko mbali mbali yaliotolewa na wadau wa Auwsa pamoja na wakazi wa jiji la Arusha

  Wakazi mbali mbali wa jiji la Arusha walioshiriki mkutano huo wa maboresho ya rasimu ya huduma kwa mteja picha juu na chini

  WAfanyakazi wakiwa kazini kuratibu shughuli hiyo ya maboresho ya rasimu ya huduma kwa mteja picha zote na mahmoud ahmad wa Michuzi blog Arusha.

  ………………………………………………………
  Na Mahmoud Ahmad -Arusha

  Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingiza imewataka wakazi wa jiji la Arusha kukaa mkao wa kula kwani wapo katika wakati wa kuboresha huduma zake kwenye kipindi cha miaka miwili na nusu iliyobakia katika uboresha wa miundombinu na utafutaji wa vyanzo vipya vya maji na kuwa tatizo la maji litakuwa historia.

  Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa AUWSA Ruth Koya wakati akijibu maswali ya wadau mbali mbali walioshiriki kwenye Mkutano wa maboresho ya mkataba wa huduma kwa wateja jijini Arusha.

  Alisema kuwa kumekuwa na matatizo ya upungufu wa maji kwa mda mrefu na serikali imeliona hilo ndio maana ikatenga kiasi cha tsh,476 bilion za uboreshaji wa huduma mbali mbali za mamlaka hiyo hivyo suala hilo linafanyiwa kazi kuanzia mwaka huu hadi mwaka 2018 litakapokamilika.

  “Tuwe na subra maradi huu kwa sasa una mda wa miezi nane tangia uanze na mkandarasi wa utafutaji wa vyanzo vya maji yupo kazi akishakamilisha tutaanza maboresho ya miundombinu yetu ilkuweza kuwafikishia maji kwa wateja wetu wote”alisema Koya

  Kwa upande wake kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Arusha Afisa tarafa wa jiji la Arusha Felician Rutehengerwa aliitaka Auwsa kuwabainisha wezi wote wa maji ilikuweza kuwafisha katika mikono ya kisheria kwani suala hilo pia linachangia wananchi kukosa huduma ya maji safi na upotevu wa maji.

  Alisema kuwa kumekuwapo na vyanzo vingi vya maji zaidi ya 19 na vingine vimeanzishwa na viwanda ambavyo vimekuwa vikiikosesha Auwsa mapato ikiwemo kiwanda cha A to Z ambacho kimekuwa kikigawa maji bure
  huku wakitambua kuwa wao hawana mamlaka ya kisheria ya usimamizi wa maji hivyo ni mteja mkubwa mnampoteza kulipa huduma za maji.

  0 0


  Kaimu Mkuu wa kitengo cha habari, elimu na mawasiliano kutoka Mpango wa Taifa wa kudhibiti Ukimwi, Eddah Katikiro (katikati), akizungumza kwenye semina elekezi kuhusu uzinduzi wa Kondom mpya ya Zana itakayokuwa ikitolewa bure na serikali kwa wananchi, iliyofanyika Jijini Mwanza leo.

  Na BMG

  Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, imewahimiza wananchi kuzingatia matumizi sahihi na endelevu ya kondomu ili kujiepusha na mimba zisizotarajiwa pamoja na magongwa ya kuambukiza ikiwemo virusi vya Ukimwi.

  Kaimu Mkuu wa kitengo cha habari, elimu na mawasiliano kutoka Mpango wa Taifa wa kudhibiti Ukimwi, Eddah Katikiro, ametoa rai hiyo hii leo Jijini Mwanza, kwenye semina elekezi kuhusu uzinduzi wa Kondom mpya ya Zana itakayokuwa ikitolewa bure na serikali kwa wananchi.

  Katikiro amesisitiza matumizi sahihi na endelevu ya kondom ya Zana kwa wananchi walio kwenye mahusiano ya kimapenzi, yatasaidia kupunguza maambukizi ya magonjwa ya zinaa kama virusi vya Ukimwi pamoja na mimba zisizotarajiwa na kwamba aina hiyo ya kondom ni imara na yenye ubora.

  Mratibu wa mpango wa Taifa wa kudhibiti Ukimwi, mkoani Mwanza, Geofrey Mabu, amesema mkoa wa Mwanza umejipanga vyema ili kuhakikisha kondom za Zana zinawafikiwa walengwa hususani kupatikana bure katika maeneo mbalimbali ikiwemo kwenye vituo vyote vya afya, maeneo ya starehe pamoja na kwenye ofisi za serikali na binafsi.

  Uzinduzi wa Zana Kondom kitaifa ulifanyika mkoani Mbeya wiki iliyopita ambapo kwa mkoa wa Mwanza uzinduzi utafanyika kesho Jijini Mwanza ambapo aina hiyo ya kondomu itakuwa mbadala wa kondom za MSD zilizokuwa zikitolewa pia bure na Serikali lengo likiwa ni kuhakikisha mapambano dhidi ya Ukimwi yanafanikiwa.
  Washirki wa semina hiyo
  Wanasemina
  Wanasemina
  Mmoja wa washiriki wa semina akihojiwa na wanahabari
  Mmoja wa washiriki wa semina akihojiwa na wanahabari
  Picha ya pamoja

  Bonyeza HAPA Kujua Zaidi

older | 1 | .... | 961 | 962 | (Page 963) | 964 | 965 | .... | 1904 | newer