Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46339 articles
Browse latest View live

BALOZI WILSON MASILINGI ATEMBELEA CHUO CHA MTANZANIA WINSTON SALEM, NC.

$
0
0

Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Mhe. Wilson Masilingi akitia saidi kitabu cha wageni katika chuo kinachomilikiwa na Mtanzania Dr. Lucas Shallua kilichopo Winston Salem, North Carolina siku ya Ijumaa Septemba 2, 2016.

Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Mhe. Wilson Masilingi akifanya mazungumuzo na mmiliki wa chuo cha Mount Eagle College &University Dr. Lucas Shallua siku ya Ijumaa Septemba 3, 2016 Balozi Wilson Masilingi alipotembelea chuo hicho kilichopo Winston Salem, North Carolina.
 Mazungumuzo yakiendelea, wengine katika kufuatilia mazungumuzo hayo kutoka kushoto ni ni Afisa Uhamiaji wa Ubalozi Bwn. Abbas Missana, Dr. Dorothy Edward Shallua (mke wa Dr. Lucas Shallua), Mke wa Balozi Marystela Masilingi, na mwenyeiki wa Umoja wa Watanzania North Carolina, Bi. Gloria Alex.
 Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Mhe. Wilson Masilingi akimsikiliza Dr. Lucas Shallua alipokua akimwonyesha moja ya darasa linalotumia kurekodia masomo ya matandaoni.
 Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Mhe. Wilson Masilingi akimsikiliza Dr. Lucas Shallua (kulia) alipokua amkitembeza na kumwonyesha chuo cha Mount Eagle College & University kilichopo mji wa Winston Salem, North Carolina. Wengine katika picha kutoka kushoto ni mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Watanzania North Carolina, Bi. Gloria Alex, Mke wa Balozi Bi. Marystela Masilingi, nyuma ya Balozi asiyeonekana ni Afisa Uhamiaji wa Ubalozi Bwn. Abbas Missana na Mke wa Shallua, Dr. Dorothy Edward Shallua.
 Moja ya madarasa chuoni hapo.
 kutoka kushoto ni Afisa Uhamiaji wa Ubalozi Bwn. Abbas Missana, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Watanzania North Carolina, Bi. Gloria Alex, nyuma ya Mhe. Balozi ni mkewe Marystela Masilingi, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Mhe. Wilson Masilingi, mke wa Shallua, Dr. Dorothy Edward Shallua na Dr. Lucas Shallua ambaye akitoa maelezo kwa Mhe. Balozi wakati akimtembeza na kumwonyesha chuo hicho.
 Mke wa Dr. Shallua, Dr. Dorothy Edward Shallua (kulia) akimuelezea Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Mhe. Wilson Masilingi kuhusiana na kampuni yake ya Mount Eagle Health Care ambayo ofisi zake pia zipo kwenye jengo la ofisi za chuo hicho.
 Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Mhe. Wilson Masilingi akisikiliza maelezo kutoka mmoja ya walimu wa darasa la utgawaji utumiaji wa dawa kwa mgonjwa chuoni hapo Mwl. Allen Greene (kushoto) kati ni Dr. Lucas Shallua akifuatilia kwa makini muzungumuzo hayo.
 Wapili toka kushoto ni Mkuu wa chuo Bi. Denese Methews akitoa maelezo kwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Mhe. Wilson Masilingi (watano toka kushoto) kuhusiana na chuo hicho wengine wanao msikiliza kutoka kushoto ni mke wa Dr. Shallua, Dr. Dorothy Edward Shallua, mwenyeki wa Jumuiya ya Umoja wa Watanzania North Carolina, mke wa Balozi, Marystela Masilingi na Dr. Lucas Shallua.
 Kutoka kushoto ni Ted, mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Watanzania North Carolina Bi. Gloria Alex, Mke wa Balozi Marystela Masilingi, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Mhe. Wilson Masilingi, Dr. Lucas Shallua, mke wa Dr. Shallua, Dr. Dorothy Edward Shallua na Afisa Uhamijai wa Ubalozi, Bwn. Abbas Missana.
Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Mhe. Wilson Masilingi na mkewe wakipokea zawadi kutoka mke wa Dr. Shallua, Dr. Dorothy Edward Shallua na Dr. Lucas Shallua.

Chuo cha Mount Eagle kinatoa unafuu kwa Mtanzania anayetaka kujiunga katika masomo ya Unesi na ugawaji dawa na chuo hicho kwa kukuwezesha wewe kufanyakazi hospitanini au kwenye maduka ya dawa pia wanamsomo ya mtandaoni kwa bei nafuu. Kwa maelezo zaidi usisite kuwasiliana na Dr. Lucas Shallua barua pepe Lshallua@mounteag.com 

RAIS DKT. MAGUFULI ALIVYOWAHUTUBIA WANANCHI WA UNGUJA JIONI HII

$
0
0
 Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiwapungia wananchi na wanaCCM wa Zanzibar jioni hii wakati akiwasili kwenye Uwanja Uwanja wa Kibandamaiti katika mkutano maalum wa kuwashukuru wananchi wa Mikoa mitatu ya Unguja leo.


  Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanznia Dkt.John Pombe Magufuli akihutubia wananchi katika uwanja wa Kibandamaiti Mjini Unguja katika mkutano maalum wa kuwashukuru wananchi wa Mikoa mitatu(3) ya Unguja
 Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanznia Dkt.John Pombe Magufuli akihutubia wananchi katika uwanja wa Kibandamaiti Mjini Unguja katika mkutano maalum wa kuwashukuru wananchi wa Mikoa mitatu ya Unguja 




Sehemu ya maelfu ya wananchi na wana-CCM wa Zanzibar wakiwa wamefurika kwa wingi kwenye Uwanja Uwanja wa Demokrasia uliopo eneo la Kibanda Maiti, Mjini Unguja Zanzibar kunafanyika Mkutano wa hadhara.

Rais Dkt. Magufuli arejea jijini Dar es Salaam akitokea Zanzibar

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere akitokea Zanzibar jioni hii ya Septemba 3, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda mara baada ya kurejea jijini Dar es Salaam akitokea Zanzibar. PICHA NA IKULU

Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira yafanya ziara Bandari ya Dar es Salaam

$
0
0

 Mwenyekiti wa Kamati ya  Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira Mhe. Dkt. Dalaly Peter Kafumu Mbunge wa Igunga akizungumza na wadau wa biashara walipokutana kujadili masuala mbalimbali ya kibiashara katika Bandari za Tanzania leo Septemba 3, 2016.
 Mwenyekiti wa Kamati ya  Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira Mhe. Dkt Dalaly Peter Kafumu Mbunge wa Igunga akizungumza na uongozi wa Bandari na watendaji wa Wizara husika walipokutana kujadili masuala mbalimbali ya kibiashara katika Bandari za Tanzania leo Septemba 3, 2016.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania Mhandisi Deusdedit Kakoko(kushoto) akifafanua jambo mbele ya Kamati ya  Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira kuhusu masuala mbalimbali ya kibiashara katika Bandari za Tanzania leo Septemba 3, 2016 kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya  Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira Mhe. Dkt Dalaly Peter Kafumu Mbunge wa Igunga.
 Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira Mhe. Anatropia Theonest Mbunge wa Viti maalum (Chadema) akichangia hoja katika kikao baina ya wadau wa biashara na Kamati hiyo walipokutana kujadili masuala mbalimbali ya kibiashara katika Bandari za Tanzania leo Septemba 3, 2016.
 Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira Mhe. Khatib Said Haji Mbunge wa Konde akichangia hoja katika kikao baina ya wadau wa biashara na Kamati hiyo walipokutana kujadili masuala mbalimbali ya kibiashara katika Bandari za Tanzania leo Septemba 3,2016.
 
 Baadhi ya wadau wa biashara, watendaji kutoka Wizara husika za kamati hiyo wakimsikiliza Mwenyekiti wa Kamati ya  Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira Mhe. Dkt. Dalaly Peter Kafumu Mbunge wa Igunga (hayupo pichani) wakati akizungumza na wadau hao walipokutana kujadili masuala mbalimbali ya kibiashara katika Bandari za Tanzania leo Septemba 3, 2016.





 Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini TAFF Bw. Otieno Ogobo akitoa maoni yake kwa Kamati ya  Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira walipokutana kujadili masuala mbalimbali ya kibiashara katika Bandari za Tanzania leo Septemba 3, 2016.

 Kamishna wa Forodha na Ushuru wa Bidhaa kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Jocktan Kyamuhanga akifafanua jambo mbele ya Kamati ya  Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira kuhusu masuala mbalimbali ya ukusanyaji mapato katika Bandari za Tanzania leo Septemba 3,2016 .
 Kaimu Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam Bw. Nelson Mlela akifafanua jambo kwa Kamati ya  Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira walipotembelea kuangalia utendaji kazi wa Bandari ya Dar es Salaam leo Septemba 3,2016 . (Picha zote na Ofisi ya Bunge)

UCHAMBUZI WA MAGAZETI

SIMIYU YAJIPANGA KUANZA KUTENGENEZA CHAKI

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (kushoto) akionesha aina tofauti za maboksi yatakayotumika kufungashia chaki nyeupe na za rangi ambazo zinatarajiwa kuanza kuzalishwa na Vijana wa Wilaya ya Maswa, Mkoani humo wakati alipohitimisha Mafunzo ya Teknolojia ya Utengenezaji wa Chaki kwa vijana hao, (katikati) Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Mhe. Seif Shekalaghe (kulia) Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Maswa, Mhe. Peter Bunyongoli.
Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Mhe. Seif Shekalaghe akizungumza na vijana na wadau wengine wakati wa kuhitimisha mafunzoTeknolojia ya utengenezaji chaki yaliyotolewa na Shirika la Viwanda Vidogo vidogo SIDO kwa Vijana wajasiriamali wa Wilaya ya Maswa, katika ukumbi mdogo wa Halmashauri ya Wilaya hiyo.
Meneja wa Shirika la Viwanda Vidogo vidogo (SIDO) Mkoa wa Shinyanga, Athanas Moshi (aliyesimama) akizungumza navijana na wadau wengine wakati wa kuhitimisha mafunzo yaTeknolojia ya utengenezaji chaki yaliyotolewa na Shirika hilo  kwa Vijana wajasiriamali wa Wilaya ya Maswa.
Baadhi ya Vijana wajasiriamali wa Wilaya ya Maswa wakiangalia sampuli za maboksi yaliyopendekezwa kutumika kufungashia chaki pindi uzalishaji utakapoanza wakati Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka (hayupo pichani) akihitimisha mafunzo ya Teknolojia ya utengenezaji chaki yaliyotolewa na SIDO kwa vijana hao, wilayani humo
Vijana wajasiriamali wa Wilaya ya Maswa wakiweka chaki walizotengeneza wakati wa mafunzo ya Teknolojia ya utengenezaji chaki yaliyotolewa na SIDO katika maboksi mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu (hayupo pichani) kabla ya Mkuu huyo wa mkoa  kuhitimisha mafunzo hayo.   
 
                                   Na Stella Kalinga, Simiyu
Serikali Mkoani Simiyu imetangaza azma yake ya  kuanza kutengeneza Chaki ambazo zitauzwa katika Wilaya za Mkoa huo na nchi nzima kabla ya Oktoba 14 mwaka huu.


Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Anthony John Mtaka wakati alipohitimisha mafunzo ya Teknolojia ya utengenezaji wa Chaki kwa vikundi vya vijana Wajasiriamali wilayani Maswa, yaliyotolewa na Shirika la Viwanda Vidogo vidogo (SIDO) Mkoa wa Shinyanga.


Mtaka amesema shule zote za Msingi na Sekondari za Serikali Mkoani humo  zinatumia jumla ya katoni 1200 za chaki ambazo zinagharimu shilingi 25,000,000 kwa kila mwezi, hivyo kama Vijana wa Wilaya ya Maswa wakizalisha Chaki na kusambaza katika mkoa mzima watajipatia kipato na kuondokana na umaskini.


Mkuu huyo wa Mkoa amesema katika kutekeleza azma ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kuwa na  Tanzania ya Viwanda, Mkoa huo umejipanga kuimarisha uwekezaji katika viwanda vidogo vidogo ambavyo vitazalisha mahitaji ya kila siku ya wananchi, hivyo wamedhamiria kuwa na uzalishaji wa bidhaa moja kwa kila wilaya ( one district  one product), ambapo Wilaya ya Maswa itakuwa ikizalisha chaki.


“ Wilaya ya Maswa imepokea shilingi 38,000,000  Meatu 31,000,000 kwa ajili ya vijana kutoka Wizara yenye dhamana na Vijana, sasa hivi  tumepeleka maombi ya wilaya zilizobaki. Tumedhamiria kuutambulisha Mkoa kwa kuzalisha bidhaa zetu wenyewe, tumeanza na Chaki wilaya ya Maswa, Wilaya ya Meatu wao watazalisha maziwa,  tutaendelea kutengeza utambulisho(brand) wa wilaya nyingine kwa kuzalisha bidhaa zinazoendana na malighafi zilizopo” alisema Mtaka.


Akizungumza katika hitimisho la Mafunzo hayo kwa Vijana, Meneja wa Shirika la Viwanda vidogo (SIDO) Mkoa wa Shinyanga, Athanas Moshi ametoa wito kwa vikundi vya vijana kuwa na mipango itakayowasaidia kutangaza bidhaa zao na kupata soko la bidhaa hizo ndani na nje ya Mkoa ili kujiongezea kipato.


“Mtakapoanza kuzalisha chaki, kulingana na tathmini iliyofanyika kama mtauza kwa Mkoa wa Simiyu tu mtakuwa na uwezo wa kutengeneza faida ya shilingi 8,000,000 kila mwezi, hiyo si fedha ndogo mkiwa na mipango thabiti mkazalisha chaki bora mtaweza kuuza chaki zenu nchi nzima na hata nje ya nchi” alisema Moshi. 


Naye mmoja wa vijana waliopata mafunzo ya utengenezaji wa chaki, Kelvin Steven ametoa wito kwa Wananchi wa  Simiyu na Watanzania kwa ujumla,  kuunga mkono juhudi za Vijana Wajasiriamali na kuthamini bidhaa zinazozalishwa hapa nchini ili kuinua uchumi wa Vijana hao na Taifa kwa jumla.


Aidha, Bi. Specioza Fundikira ambaye pia amepata mafunzo hayo amesema matarajio ya Vijana waliopata mafunzo ni kuwa uzalishaji wa chaki utakapoanza kutakuwa na soko la uhakika kwa Shule zote za Msingi na Sekondari za Serikali mkoani humo na mikoa ya jirani, vijana watapata ajira na kuachana na shughuli zisizo halali kama wizi na ulevi.


Kwa Mujibu wa Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Mhe. Seif Shekalaghe vijana kutoka vikundi 8 vya Wajasiriamali ambao wameunda kikundi kimoja cha ‘Maswa Youth Enteprises’ wamepatiwa mafunzo ya Teknolojia ya utengenezaji wa chaki na Shirika la Viwanda Vidogo vidogo (SIDO) Mkoa wa Shinyanga kuanzia tarehe 29/08/2016 hadi tarehe 03/09/2016.


Waziri Mahiga aongoza Timu ya Waangalizi wa Uchaguzi ya SADC Uchaguzi wa Jamhuri ya Shelisheli

$
0
0
 Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustino Mahiga akifungua Misheni ya timu ya Uangalizi wa Uchaguzi wa Wabunge tarehe 2 Septemba, 2016, Mahe Seychelles. Mhe Waziri anamuawakilisha Mhe. Rais John pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ni Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC.
Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika picha ya pamoja na  Misheni ya timu ya Uangalizi wa Uchaguzi wa Wabunge tarehe 2 Septemba, 2016 huko Mahe, Seychelles.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Augustine P. Mahiga (Mb.), jana tarehe 2 Septemba, amezindua Misheni ya Waangalizi wa Uchaguzi wa SADC kwenye uchaguzi wa Jamhuri ya Shelisheli kwa niaba ya Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika -SADC Organ. 
Misheni hiyo ya waangalizi wa uchaguzi itakayojumuisha waangalizi kutoka nchi za SADC, itashiriki kwenye uangalizi katika vituo vyote 25 vya upigaji kura nchini Shelisheli. 

Pamoja na kuongoza misheni hiyo, Tanzania kama Mwenyekiti wa SADC Organ itaongoza timu za uandishi wa taarifa ya SADC pamoja na ufuatiliaji wa taarifa za vyombo vya habari kuhusu mwenendo mzima wa uchaguzi nchini humo unaotarajiwa kufanyika tarehe 8-10 Septemba, 2016. 

Tanzania ilikabidhiwa nafasi ya uenyekiti wa kuongoza asasi hii muhimu ya Jumuiya, wakati wa Mkutano wa 36 wa Wakuu wa Nchi na Serikali uliofanyika huko Mbabane, Swaziland tarehe 29 – 31 Agosti, 2016. 
Mara baada ya kukamilika kwa Mkutano huo, Mhe. Dkt. Mahiga, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki alielekea Jamhuri ya Shelisheli kumwakilisha Mhe. Dkt. Magufuli, katika kuongoza ujumbe wa Waangalizi wa SADC. 

Wajibu wa Tanzania kuongoza Misheni hya Waangalizi wa Uchaguzi imetokana na misingi na muongozo wa Jumuiya ya SADC ya kuwa na chaguzi za kidemokrasia katika nchi wanachama wa Jumuiya hiyo ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika. Waziri Mahiga anatarajiwa kutoa taarifa ya awali ya Misheni hiyo ya waangalizi wa SADC Septemba 12, 2016.

Mkubwa Fella alivyozitambulisha Nyumba alizowajengea Yamoto Band


Asha Baraka ampongeza Mkubwa Fella kwa Nyumba za Yamoto Band

NI LEO JIONI

KIKOSI KAZI CHA TANESCO CHAANZA KUBADILISHA MIUNDOMBINU YA UMEME JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0


Meneja Mwandamizi wa Usambazaji Umeme wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), ambaye pia ndiye Meneja wa Mradi wa kuimarisha miundombinu ya Umeme, Injinia Theodory Bayona.(katikati), akisimamia kazi hiyo leo Septemba 3, 2016
Kaimu Meneja Uhusiano wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), Leila Muhaji, akizungumza na waandishi wa habari kwenye eneo la mradi


NA K-VIS MEDIA/KHALFAN SAID

WAHANDISI, na mafundi wa Shirika la Umeme Nchini Tanzania, (TANESCO), kwa kushirikia na wale wa kampuni za Kijapani za Yachiyo Engineering Co Limited, Takaoka na National Construction Co. Limited, wameanza kazi ya uboreshaji miundombinu ya umeme kwenye kituo kikubwa cha kupooza na kusambaza umeme cha Ubungo jijini Dar es Salaam, imeanza leo Septemba 3, 2016.

Kazi kubwa inayofanyika hivi sasa ni kubadilisha laini kutoka umeme mdogo kwenda umeme mkubwa, lakini pia kubadilisha vifaa vingine muhimu ili kuwezesha usafirishaji umeme uweze kuwafikia watumiaji katika ubora ulio juu.

“Ikumbukwe kwamba, hapa tulikuwa na laini mbili (waya mbili) zilizokuwa na uwezo wa kusafirisha umeme kiasi cha Megawati 120 kila moja, kutoka hapa Ubungo kwenda kituo cha Ilala, lakini kazi inayofanyika sasa, ni kubadili njia hizo (waya za umeme), ambazo zitakuwa na uwezo wa kupitisha kiasi cha umeme wenye Megawati 220 kila moja,” Alifafanua Meneja Muandamizi wa Usambazaji Umeme wa Shirika hilo, ambaye pia ndiye Meneja wa wa Mradi wa kuimarisha miundombinu ya Umeme, Injinia Theodory Bayona.

Kwa mantiki hiyo, kazi inayofanyika leo hii itawezesha umeme utakaokuwa ukisafirishwa kutoka hapa Ubungo kwenda Ilala, kuwa na jumla ya Megawati 440 kwa laini zote mbili, tofauti na hapo awali ambapo uwezo wa kusafirisha umeme ulikuwa Megawati 240 tu,” Alisema.

Kazi ikikamilika wakazi wa jiji la Dar es Salaam, watakuwa wakipata umeme wa uhakika, na ulio bora, alifafanua Injinia Bayona

Naye Kaimu Meneja Uhusiano wa Shirika la Umeme Nchini Tanzania, (TANESCO), Leila Muhaji, amewaomba wananchi kuwa wavumilivu katika kipindi hiki ambapo Shirika linafanya juhudi kubwa za kuwapatia umeme wa uhakika wananchi kwa kuimarisha miundombinu yake,.

“Ili kuwawezesha mafundi wetu kufanya kazi katika mazingira salama, tutakuwa tukikata umeme kuanzia leo hii Septemba 3 na umeme utakuwa ukikatika kuanzia saa 2 asubuhi na kurejea saa 11 jioni kwa utaratibu na tarehe kama ifuatavyo; Septemba 3-4, Septemba 10-11, Septemba 17-18, na Septemba 24-25, 2016.” Alifafanua Leila, na kuwaomba wananc hi kuwa wavumilivu katika kipindi hiki.

Mradi huu ulioanza Februari 2015 na unaotarajiwa kukamilika Juni 2017 unatekelezwa na Serikali kupitia TANESCO kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Japan (JICA) .
Tsutomu Sato, wa kampuni ya Takaoka ya Japan, akiwa kazini
Mafundi wa TANESCO, wakitayarisha nyaya hizo mpya
Fundi wa TANESCO, akifunga kikombe wakati wa kazi ya kubadilisha miundombinu ya kusafirisha umeme kwenye kituo kikuu cha kupooza na kusambaza umeme cha Ubungo, jijini Dar es Salaam
Raphael Mjata, Msimamizi Mkuu wa Njia Kuu za Umeme, akionyesha uwezo wa kituo cha Ubungo cha kupooza umeme wenye kilovolti 132
Mafunzi wa TANESCO na kampuni ya National Construction Company Limited, wakivuta nyaya hizo mpya
Hizi ndio nyaya zitakazofungwa kwenye laini mbili za kusafirisha umeme kutoka kituo cha kupooza na kusafirisha umeme cha Ubungo

Mhandishi Bayona, akielezea waandishi wa habari mwenendo wa kazi hiyo
Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO makao makuu, Leila Muhaji, na Afia Uhusiano wa Shirika hilo, Henry Kilasila, wakiwa kazini



Mhandisi Bayona (kulia), akijadiliana jambo na Wahandisi wenzake, Yasutaka Osawa, (kushoto), ambaye ni mwakilishi katika mradi wa kuboresha umeme jiji la Dar es Salaam, kutoka kampuni ya Takaoka Engineering Co Ltd, na Mhandisi Ahmed Mmingwa, ambaye ni Msimamizi wa Mradi kutoka TANESCO
Fundi wa TANESCO, akiwa kazini leo Septemba 3, 2016
Tamai Masayuki, Mwakilishi wa kampuni ya Kijapani ya Yachiyo Engineering Co. Limited, akizungumza na waandishi wa habari kuhsuu maendeleo ya uboreshaji huo
Wahandisi wakijadiliana jambo
Fundi wa TANESCO akiwa kazini
Kazi inaendelea
Meneja Mwandamizi wa Usambazaji Umeme wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), ambaye pia ndiye Meneja wa Mradi wa kuimarisha miundombinu ya Umeme, Injinia Theodory Bayona.(katikati), Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Leila Muhaji, (kulia) na Afisa Habari wa Shirika hilo makao makuu, Henry Kilasila, (wakwanza kushoto) na waandishi wa habari, wakitembelea eneo la mradi mapema leo asubuhi Septemba 3, 2016 ambapo kazi ilianza kwa kasi

Wafanyakazi wa TANESCO chumba cha ufuatiliaji mwenendo wa umeme (control room) wakiwa akzini
Chumba cha kufutialia mwenendo wa umeme jijini Dar es Salaam, (Control room), cha TANESCO-Ubungo sub station)

Serikali imeimarisha sekta ya Mahakama nchini

$
0
0
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe 
 
 
Na Immaculate Makilika- MAELEZO

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amesema kuwa serikali imeimarisha sekta ya Mahakama nchini ambapo imeanzisha kamati ya maadili ya mahakama katika kila wilaya nchi nzima ili kusimamia upotofu wa maadili katika mahakama hizo.

Dkt. Mwakyembe amesema hayo leo wakati wa kipindi cha TUNATEKELEZA kinachoandaliwa na Idara ya Habari-MAELEZO kwa kushirikiana na TBC 1 ambapo alisema Serikali imeamua kuanzisha kamati hizo ili zipokee upotofu wa maadili unaofanywa na baadhi ya watumishi wa mahakama ambao sio waaminifu hali ambayo inaharibu sifa ya chombo hicho cha kutoa haki.

“Tumeanzisha kamati hizi katika kila wilaya ili zipokea upotofu wa maadili kwa upande wa mahakama, sasa wananchi wanaweza kwenda kutoa malalamiko yao kwenye kamati hizo ili yaweze kufanyiwa kazi na hatua zitachukuliwa kwa wale watakaokutwa na makosa”.

“Kamati hizo zinazoongozwa na wakuu wa wilaya zinaundwa na wajumbe mbalimbali wakiwemo viongozi wa dini ili kuwapa wananchi fursa nzuri ya kuweza kutoa malalamiko yao”. Alisema Dkt. Mwakyembe.

Aidha, Dkt. Mwakyembe alisema kuwa kwa sasa Serikali imeendelea kuwa na mikakati kadhaa ya kuimarisha sekta ya Mahakama nchini, ambapo inaendelea kukamilisha maandalizi ya mfumo wa divisheni ya mahakama ya rushwa na ufisadi ili itakapoanza iweze kufanyakazi bila matatizo.

“Tunaendelea kujiandaa na idara zote zinazohusika katika mahakama hiyo, ili ziweze kufanya kazi vizuri, tumeweka vigezo vya kesi zitakazosikilizwa huko na hakutakua na kesi za mwaka juzi au muda mrefu kwa kuwa zitasikilizwa kwa wakati”. Alisisitiza Dkt. Mwakyembe.

Akizungumzia wananchi wanaoshindwa kumudu gharama za huduma za kisheria zinazotozwa na mawakili au wanasheria mbalimbali, Dkt. Mwakyembe alisema kuwa Serikali imeandaa mswaada ambao utapelekwa Bungeni ili kutunga Sheria itakayosaidia kutatua changamoto hiyo.

Dkt. Mwakyembe aliongeza kuwa serikali imeendelea kushirikiana na vikundi vya harakati na asasi za kirai zaidi ya 290 vyenye wataalamu wa sheria 2500 nchi nzima ili kupanua wigo wa masuala ya sheria, pamoja na kuandaa mfumo wenye tija kwa taifa utakaosaidia kuwafikia na kuwasaidia wananchi wengi hasa waliopo maeneo ya vijijini ili kupata msaada wa kisheria kuhusu masuala mbalimbali hasa mirathi ya ndoa na ardhi.

Serikali ya Awamu ya Tano imeendelea kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta hiyo ikiwa ni pamoja na ujenzi wa Mahakama kwa wingi kwa ngazi mbalimbali pamoja na kuwaandaa vijana wengi kutoka vyuo vikuu kila mwaka ambao watafanyakazi katika mahakama mbalimbali nchini.

HIVI NDIVYO RAIS DKT MAGUFULI ALIVYOHITIMISHA ZIARA YAK YA KIKAZI ALIPOHUTUBIA WANANCHI UWANJA WA DEMOKRASIA ZANZIBAR JUMAMOSI

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akilakiwa na Mstahiki Meya wa Mji wa Zanzibar Mhe Khatib Abdurahaman Khatib alipowasili   kuhutubia mkutano wa hadhara katika uwanja wa Demokrasia mjini Unguja Jumamosi Agosti 3, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri wa Kazi,Uwezeshaji Wananchi Uchumi na Ushiriuka.Mhe Haroun Ali Suleiman  kuhutubia mkutano wa hadhara katika uwanja wa Demokrasia mjini Unguja Jumamosi Agosti 3, 2016.
Viongozi mbalimbali wakiwa wamejipanga kumsubiri Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kuhutubia mkutano wa hadhara katika uwanja wa Demokrasia mjini Unguja Jumamosi Agosti 3, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Makamu wa Rais wa Chama cha Siasa ADA-TADEA  Mhe. Juma Ali Khatib  kabla ya kuhutubia mkutano wa hadhara katika uwanja wa Demokrasia mjini Unguja Jumamosi Agosti 3, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akilakiwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Prof. Makame Mbarawa kabla  kuhutubia mkutano wa hadhara katika uwanja wa Demokrasia mjini Unguja Jumamosi Agosti 3, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Balozi Ali Karume
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli  akisalimiana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba   kabla ya kuhutubia mkutano wa hadhara katika uwanja wa Demokrasia mjini Unguja Jumamosi Agosti 3, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akilakiwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt Hussein Mwinyi kabla ya kuhutubia mkutano wa hadhara katika uwanja wa Demokrasia mjini Unguja Jumamosi Agosti 3, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akioungia umati kabla ya kuhutubia mkutano wa hadhara katika uwanja wa Demokrasia mjini Unguja Jumamosi Agosti 3, 2016
Mafundi mitambo wa AZAM TV  wakiongozwa  na Mehboub Al Hadad wakiwa tayari kurusha live mkutano wa hadhara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli katika uwanja wa Demokrasia mjini Unguja Jumamosi Agosti 3, 2016
Shekhe akitoa mawaidha kabla Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kuhutubia mkutano wa hadhara katika uwanja wa Demokrasia mjini Unguja Jumamosi Agosti 3, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na viongozi wengine wakiwa  katika uwanja wa Demokrasia mjini Unguja Jumamosi Agosti 3, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimshukuru Shekhe wakati wa mkutano wa hadhara katika uwanja wa Demokrasia mjini Unguja Jumamosi Agosti 3, 2016
Shekhe akipongezwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira na Muungano) Mhe.  January Makamba na waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt Hussein Mwinyi
Jukwaa kuu
Wasomautenzi walisisimua umati
Wasoma utenzi wakipongezwa jukwaa kuu
Sehemu ya viongozi mbalimbali wakifuatilia mkutano
Sehemu ya viongozi mbalimbali wakifuatilia mkutano
Sehemu ya viongozi mbalimbali wakifuatilia mkutano
Sehemu ya viongozi mbalimbali wakifuatilia mkutano
Sehemu ya viongozi mbalimbali wakifuatilia mkutano
Jukwaa kuu
Risala 
Pongezi kwa msoma risala
Bendi ya vijana
Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Ayoub Mohammed Mahmoud akisoma muhtasari wa shughuli na kutambulisha wageni
Sehemu ya umati mkubwa uliojitokeza
Umati
Nyomi
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akitambulishwa
Mke wa Rais wa Zanzibara Mama Mwanamema Shein akitambulishwa
 Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Zuberi Ali Maulid akitambulishwa
Mawaziri wakitambulishwa
Viongozi wa vyama mbalimbali wakitambulishwa
Bw. Hafidh Ameir, mume wa Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akitambulishwa
Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dk. Abdulhamid Yahya Mzee akitambulishwa
Viongozi wa vyama mbalimbali vya siasa wakitambulishwa
Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Ayoub Mohammed Mahmoud akisoma muhtasari wa shughuli na kutambulisha wageni
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha akisalimia viongozi
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha akitambulishwa jukwaani
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein wakiongea
Mama Fatma Karume akitambulishwa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein wakiongea, Kushoto ni  Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Mhe Vuai Ali Vuai 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akisalimia
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt Hussein Mwinyi akisalimia wananchi
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ, Mhe. Haji Omar Kheri akisalimia
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Mhe Vuai Ali Vuai akisalimia
Umati ukshangilia
Furaha
Makamu wa Rais wa Chama cha Siasa ADA-TADEA  Mhe. Juma Ali Khatib  akisalimia
Makamu wa Rais wa Chama cha Siasa ADA-TADEA  Mhe. Juma Ali Khatib  akipongezwa 

Mwananchi akifurahia hotuba
Umati ukifuatilia hotuba
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein akihutubia mkutano wa hadhara katika uwanja wa Demokrasia mjini Unguja Jumamosi Agosti 3, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akikaribishwa na Rais wa Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein kuhutubianmkutano wa hadhara katika uwanja wa Demokrasia mjini Unguja Jumamosi Agosti 3, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akihutubia mkutano wa hadhara katika uwanja wa Demokrasia mjini Unguja Jumamosi Agosti 3, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akihutubia mkutano wa hadhara katika uwanja wa Demokrasia mjini Unguja Jumamosi Agosti 3, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akihutubia mkutano wa hadhara katika uwanja wa Demokrasia mjini Unguja Jumamosi Agosti 3, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akihutubia mkutano wa hadhara katika uwanja wa Demokrasia mjini Unguja Jumamosi Agosti 3, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akihutubia mkutano wa hadhara katika uwanja wa Demokrasia mjini Unguja Jumamosi Agosti 3, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akihutubia mkutano wa hadhara katika uwanja wa Demokrasia mjini Unguja Jumamosi Agosti 3, 2016
Jukwaa kuu wakifurahia jambo wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe akihutubia Magufuli mkutano wa hadhara katika uwanja wa Demokrasia mjini Unguja Jumamosi Agosti 3, 2016 
Jukwaa kuu likifurahia hotuba
Viongozi wakifurahia
Umati wa wnanchi  ukimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akihutubia mkutano wa hadhara katika uwanja wa Demokrasia mjini Unguja Jumamosi Agosti 3, 2016
Umati ukisikiliza kwa makini hotuba hiyo
Umati ukifurahia
Umati ukilipuka kwa nderemo wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akihutubia mkutano wa hadhara katika uwanja wa Demokrasia mjini Unguja Jumamosi Agosti 3, 2016
Umati ukilipuka kwa nderemo
Nderemo uwanja mzima
Umati ukishangilia kwa nguvu
"....Sema baba semaaaaaaa....."
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akihutubia mkutano wa hadhara katika uwanja wa Demokrasia mjini Unguja Jumamosi Agosti 3, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akihutubia mkutano wa hadhara katika uwanja wa Demokrasia mjini Unguja Jumamosi Agosti 3, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akihutubia mkutano wa hadhara katika uwanja wa Demokrasia mjini Unguja Jumamosi Agosti 3, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akihutubia mkutano wa hadhara katika uwanja wa Demokrasia mjini Unguja Jumamosi Agosti 3, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akihutubia mkutano wa hadhara katika uwanja wa Demokrasia mjini Unguja Jumamosi Agosti 3, 2016
Nderemo na vifijo
"....Tuko pamoja babaaaaa...."
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akihutubia mkutano wa hadhara katika uwanja wa Demokrasia mjini Unguja Jumamosi Agosti 3, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiaga baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara katika uwanja wa Demokrasia mjini Unguja Jumamosi Agosti 3, 2016
akimpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwa hotuba nzuri
Dua ikisomwa baada ya mkutano kumalizika
Umati ukiitikia dua 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein akimpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwa hotuba nzuri
Spika wa Baraza la Wawakilishi Mstaafu Mhe. Pandu Ameir Kificho akimpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwa hotuba nzuri
Mama Fatma Karume akimpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwa hotuba nzuri

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipongezwa kwa hotuba nzuri
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiagana na makamanda wa FFU

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisindikizwa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Mhe Vuai Ali Vuai na Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Ayoub Mohammed Mahmoud
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisubiriwa kuagwa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiagana na viongozi mbalimbali
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiagana na viongozi mbalimbali
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiagana na viongozi mbalimbali
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiagana na viongozi mbalimbali
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiagana na viongozi mbalimbali
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiagana na viongozi mbalimbali
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiagana na viongozi mbalimbali
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiagana na viongozi mbalimbali
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiagana na Kada mashuhuri wa CCM Visiwani Zanzibar Mzee Borafia 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiagana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Magharibi Yussuf Mohammed Yussuf
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiagana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ, Mhe. Haji Omar Kheri 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiagana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Mhe Vuai Ali Vuai 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiagana  na Mstahiki Meya wa Mji wa Zanzibar Mhe Khatib Abdurahaman Khatib
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiagana makamanda
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiagana na Kamishna Mkuu  wa Idara ya Uhamiaji zanzibar, Johari Sururu 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiagana na makamanda 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiagana na Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar, Hamdan Omar Makame

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akioungia mkono kuaga katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Abeid Manai Karume baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara katika uwanja wa Demokrasia mjini Unguja Jumamosi Agosti 3, 2016
Akiaga kwa unyenyekevu

SERIKALI ITAWACHUKULIA HATUA WATAKAOBAINIKA KUHUSIKA NA MATUKIO YA MOTO MKOANI ARUSHA

$
0
0
Mkurugenzi wa Elimu ya Msingi katika Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Sarah Mlaki, akimkabidhi cheti cha kumaliza darasa la saba mhitimu Mercygracious Tolla wa Shule ya Msingi ya Macedonia kwenye mahafali ya tano ya shule hiyo iliyoko Tabata Segerea jijini Dar es Salaam.

……………………………..

Hussein Makame-MAELEZO

SERIKALI imesema itawachukulia hatua stahiki wale wote watakaobainika kwa sababu moja au nyingine kuhusika na matukio ya moto yaliyotokea mkoani Arusha hivi karibuni.

Hayo yamesema na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Simon Msanjila katika mahafali ya tano ya Shule ya Msingi ya Macedonia iliyopo Tabata Segerea jijini Dar es Salaam yaliyofanyika mwishoni mwa wiki.

Akizungumza kwa niaba ya Prof. Msanjila ambaye alialikwa kuwa mgeni rasmi, Mkurugenzi wa Elimu ya Msingi wa wizara hiyo Sarah Mlaki alikuwa akijibu kilio cha Mkuu wa shule hiyo aliyelaani matukio hayo ya moto kuendelea kujitokeza huko mkoani Arusha na maeneo mengine.

Alisema mbali na kuwachukulia hatua wahusika, Serikali imechukua hatua mbalimbali kudhibiti majanga ya moto katika shule zetu za sekondari za bweni nchini.

“Serikali imechukua hatua mbalimbali kudhibiti majanga ya moto katika shule zetu za sekondari za bweni.Tutachukua hatua stahiki kwa wale ambao watabainika kwa sababu moja au nyingine wanahusika na majanga hayo”, alisema Mkurugenzi Mlaki.

Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa Serikali pia imejipanga kuboresha miundombinu ya shule zake ili watoto Watanzania wapate haki yao ya msingi ya kupata elimu.

Kwa upande mwingine, Mkurugenzi Mlaki alisema soko la vitabu vya kiada vinavyotumika katika shule za msingi nchini limevamiwa na watu mbalimbali na Serikali inafahamu kuwa kuna vitabu vingine havina ubora unaostahili kwa matumizi ya shule.

Hata hivyo, Mkurugenzi Mlaki alisema Serikali kupitia Taasisi ya Elimu Tanzania (TEA) imepewa dhamana ya kuandaa vitabu vya kiada ili wanafunzi wote kutumie vitabu hivyo bila ya kuwa na tofauti katika elimu inayotolewa.

“Kwa kweli soko la vitabu limevamiwa na watu mbalimbali na tunafahamu kuna vitabu vingine havina ubora stahiki, lakini Serikali kupitia Taasisi ya Elimu Tanzania (TEA) imepewa dhamana ya kuandaa vitabu vya kiada (text book) ili wanafunzi wote waweze kutumia vitabu hivi pasiwe na tofauti katika elimu inayotolewa” alisema Mkurugenzi Mlaki.

Aliongeza kuwa anaamini kwamba tatiz hilo litatatuliwa kadri siku zinavyokwenda kwa kuwa taasisi husika tayari inalishughulikia suala hilo kulingana na uzito wake.

Katika mahafali hayo jumla ya wanafunzi 53 wa shule hiyo walihitimu na wanatarajia kufanya mitihani ya taifa ya darasa la saba mwaka huu, wakiwemo wanafunzi 24 wanaume na wanawake 29.

Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Shukuru Mbwire alisema shule hiyo iliyoanzishwa mwaka 2009, imekuwa ikifanya vizuri katika mitihani ya darasa la saba na la nne ambapo ilianza na wanafunzi 70 lakini hadi sasa ina wafanuzi 782.

Alisema katika matokeo ya mitihani ya kitaifa ya darasa la saba shule hiyo imekuwa ikifanya vizuri mwaka hadi mwaka ambapo katika mitihani ya mwaka 2015 shule hiyo ilipata wastani wa daraja A na kushika nafasi ya 3 kati ya shule 56 kiwilaya, nafasi ya 28 kati ya shule 534 kimkoa na kitaifa ilishika nafasi ya 219 kati ya shule 16,096.

“Kwa miaka yote hiyo shule ilifaulisha wanafunzi kwa asilimia 100 ambapo watoto wote walifanikiwa kujiunga na shule za Sekondari za vipaji maalum na zile za kawaida” alisema Mbwire.

Katika risala ya wanafunzi wa shule hiyo, wahitimu walitangaza kumuunga mkono kaulimbiu ya Rais John Pombe Magufuli ya Hapa Kazi Tu na kuwataka Watanzania wafanye kazi kwa bidii ili kulikomboa Taifa na umasikini.

TRA YAJIWEKEA MIKAKATI MIZITO NA ENDELEVU YA KUKUSANYA MAPATO MWAKA WA- 2016/17

$
0
0
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu ya Mlipakodi TRA,Bw Richard Kayombo akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za makao makuu ya Mamlaka hiyo jijini Dar es salaam leo kuhusu mikakati hiyo ya harakati za kuhakikisha kuwa Mapato yote stahiki yanakusanywa ipasavyo na kwa Wakati.
 Mkurugenzi wa Huduma na Elimu ya Mlipakodi TRA,
Bw Richard Kayombo  akisisitiza jambo katika mkutano huo wakati akizungumza na waandishi wa habari.

…………………………………………………………………………

Katika harakati za kuhakikisha kuwa Mapato yote stahiki yanakusanywa ipasavyo na kwa Wakati, Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA imejiwekea mikakati mbalimbali ya kuongeza wigo wa vyanzo vya Mapato pamoja na kukusanya Mapato kikamilifu.

Mikakati hiyo ni kama ifuatavyo;

Kulifanya eneo la Kariakoo kuwa Mkoa Maalumu wa Kodi kutokana na eneo hilo kuwa kitovu cha biashara hapa nchini na kuhakikisha kila mfanyabiashara anakuwa na Mashine ya Kielektroniki ya kodi (EFDs) na kuitumia ipasavyo.

Katika kutekeleza hilo Mawakala wote wa EFDs wamefungua ofisi ya pamoja katika jengo la Al-Falah Towers lililopo mtaa wa Msimbazi Kariakoo ili kurahisisha upatikanaji wa mashine hizo na kutatua changamoto zinazowakabili wafanyabiashara katika matumizi ya mashine hizo.

Aidha Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa kodi TRA Bw. Richard Kayombo ametoa wito kwa wananachi na wafanyabiashara kujitokeza kuhakiki taarifa zao za usajili wa TIN kabla ya Tarehe 15 Oktoba 2016 katika vituo vifuatavyo kwaajili ya zoezi hilo kwani muda hautaongezwa baada ya tarehe hiyo maana baada ya tarehe hiyo zoezi hili litahamia mikoa mingine;

Vituo hivyo vya uhakiki ni pamoja na:
Mkoa wa Kodi Ilala: Jengo la Mariam Tower (Shaurimoyo) na 14Rays (Kariakoo-Gerezani)
Mkoa wa Kodi Kinondoni: Jengo la LAPF (Kijitonyama) na Kibo Complex (Tegeta) na ofisi za TRA Kimara
Mkoa wa Kodi Temeke: Uwanja wa Taifa na Ofisi za TRA Mbagala- Zakiemu
Wilaya ya Kigamboni – Ofisi za TRA Kigamboni

Pamoja na kuhakiki taarifa zao, wafanyabiashara wote ambao hawana TIN nchini wanaombwa kufika katika ofisi ya TRA iliyoko karibu nao ili kujisajili kuepuka kukumbwa na msako unaondelea hivi sasa nchi nzima pamoja na uhamasishaji

Wakati huo huo Bw. Kayombo amewahimiza wamiliki wa vituo vya mafuta kutekeleza agizo la Serikali la kufunga mashine za EFDs kabla au ifikapo tarehe 30 Septemba 2016 kwani kinyume na hapo ukaguzi utaanza kufanyika kuanzia tarehe 1 oktoba na hatua za kisheria zitachukuliwa kwa wale wote watakaobainika kukiuka agizo hilo.

Katika kuhakikisha kwamba kodi ya ongezeko la thamani VAT inakusanyawa kwa Wakati Mamlaka inawakumbusha walipakodi wote waliosajiliwa na Kodi ya Ongezeko la Thamani -VAT kuwasilisha ritani ya kila mwezi kabla au tarehe 20 ya kila mwezi badala ya tarehe 27 iliyokuwepo kabla ya mwaka hu wa fedha.

Kwa upande wa walipa kodi zaa makadirio na kodi za makampuni (Corpoaration Tax) wanakumbushwa kulipa kodi zao mapema mwezi hu wa tisa badala ya kusubiri msongamano mwisho wa mwezi ambao unaweza kuwasababishia usumbufu

Hivyo hivyo walipakodi wote wanaodaiwa madeni ya kodi za nyuma au malimbikizo wanakumbushwa kutembelea Mameneja wa mikoa, Wilaya na ofisi mbali mabli za TRA zinazowahudumia ili kujadiliana namna ya kulipa madeni hayo.

Kutokana na mikakti mizuri iliyowekwa na uiongozi wa TRA na serikali Mpaka sasa baadhi ya mikakati hiyo imeanza kuonyesha mafanikio na mwelekeo mzuri wa makusanyo ambapo kwa kipindi cha mwezi Agosti 2016 TRA imekusanya Trillioni 1.158 ikilinganishwa na lengo la Trillion 1.152 ambayo ni asilimia 100.57. ambapo Mwezi Agosti Mwaka 2015 TRA ilikusanya Billion 923.

Wito wetu kwa wanahabari na wananchi kwa ujumla ni kuendelea kutuunga mkono kwa kuhimiza kutoa risiti pamoja na kudai risiti katika kila manunuzi pamoja na kutoa taarifa za dalili za ukwepaji wa kodi wa aina yoyote mahali popote nchini

‘Pamoja Tunajenga Taifa Letu’

Richard Kayombo

MKURUGENZI WA HUDUMA NA ELIMU KWA MLIPAKODI

RC SHIGELLA MGENI RASMI UZINDUZI WA BODI YA TANGA UWASA KESHO

$
0
0

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga(Tanga Uwasa)Mhandisi,Joshua Mgeyekwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na uzinduzi wa bodi mpya.kesho

Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira leo itazindua bodi mpya yake iliyoteuliwa na Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge Julai Mosi mwaka huu baada ya ile ya awali kumaliza muda wake ambayo ilidumu kwa kipindi cha miaka mitatu.

Katika uzinduzi huo Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigella anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika hafla ambayo inatarajiwa kuanza asubuhi.

Akizungumza jana,Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga(Tanga Uwasa)Mhandisi Joshua Mgeyekwa aliwaambia waandishi wa habari kuwa halfa hiyo pia itatumika kutambua na kupongeza juhudi zinazofanywa na bodi,menejimeni na wafanyakazi wa mamlaka hiyo.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga(Tanga Uwasa)Mhandisi,Joshua Mgeyekwa kushoto aliyesimama na PRO wa Mamlaka hiyo

Alisema licha ya wafanyakazi hao lakini pia wateja wao kwa kuiwezesha mamlaka hiyo kuwa bora kwa utoaji wa huduma za maji safi miongoni mwa mamlaka 23 za maji safi na usafi wa mazingira hapa nchini kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo tokea mwaka 2012/2013.

Aidha alisema pia mamlaka hiyo imepata leseni ya daraja la kwanza baada ya kukithi vigezo vya mdhibiti wa huduma za nishati na maji hivyo kuwa mamlaka ya kwanza ya maji safi na usafi wa mazingira hapa nchini kufikia hatua hiyo ya juu katika ufanisi wa utendaji wa mamlaka.

“Waandishi wa habari kama mnavyojua mamlaka yetu ina cheti cha ithibati ya Ubora (ISO 9001) ambacho imekipata tangu mwaka 2007 tokea kipindi hicho mamlaka imekuwa ikifanya kazi zake kwa viwango vya kimataifa katika usimamizi wa mfumo wa kumhudumia mteja kwa kufuata vigezo vya ubora “Alisema.

Waandishi wa habari mkoani Tanga wakifuatilia hotuba ya mkurugenzi huyo

“Lakini pia cheti hiki huuishwa kila baada ya miaka mitatu kwa kukidhi vigezo vya utoaji wa huduma vinazohitajika ,uhuishaji ulifanyika miaka 2010 na 2013 kwa kupata ISO 9001:2008 na mwaka huu Tanga Uwasa imekuwa taasisi ya kwanza nchini chini ya kampuni ya Ithibati ya SGS Tanzania kupata cheti cha Ithibati cha 9001:20015.

Aidha aliongeza kuwa mafanikio makubwa sana ambayo hayo yametokana na juhudi za pamoja kati ya bodi ya wakurugenzi, menejimenti,wafanyakazi,wateja na wadau wa Tanga Uwasa.

Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AWASILI MKOANI DODOMA KWA AJILI YA BUNGE

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jordan Lugimbana  baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma Septemba 4, 2016 kwa ajili ya vikao vya Bunge vinavyotarajiwa kuanza Septemba 6, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu,  Kassim Majaliwa akisalimiana Septemba 4, 2016  na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma kwa ajili ya vikao vya Bunge vinavyotarajiwa kuanza Septemba 6, 2016. .

TAZAMA VIDEO YA NDOA YA MUIGIZAJI WA FILAMU HAPA NCHINI SHAMSA FORD NA MFANYABIASHARA CHIDI MAPENZI

SHIRIKA LA NDEGE LA ETIHAD LASAIDIA KITUO CHA MICHEZO SOKOINE JOGGING CLUB TANZANIA

$
0
0
 Watoto wa kituo cha michezo cha Sokoine jogging club Tanzania kilichopo Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam, wakiwa kwenye picha ya pamoja kabla ya kushiriki michezo ya kirafiki kwa udhamini wa Shirika la ndege la Etihad iliyofanyika kwenye uwanja wa Uhuru, jijini Dar es salaam mwishoni mwa juma.
 Mwanafunzi kutoka shule ya Msingi Madenge iliyopo Temeke jijini Dar es salaam Mselemu Omary akigombania mpira na Sultan Said wa Shule ya Msingi Kibasila katika mchezo wa kirafiki uliofanyika katika Uwanja wa Taifa wa Uhuru mwishoni mwa juma.
 Mratibu wa Masoko wa Shirika la Ndege la Etihad Tanzania, Grace Kijo akigawa viburudisho kwa watoto wa kituo cha michezo cha Sokoine jogging club Tanzania kilichopo Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam,mara baada ya watoto hao kushiriki michezo ya kirafiki iliyofanyika kwenye uwanja wa Uhuru, jijini Dar es salaam mwishoni mwa juma.
Afisa Mauzo wa Shirika la Ndege la Etihad Tanzania, Bhavin Sonegra akigawa keki kwa watoto wa kituo cha michezo cha Sokoine jogging club Tanzania kilichopo Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam,mara baada ya watoto hao kushiriki michezo ya kirafiki iliyofanyika kwenye uwanja wa Uhuru, jijini Dar es salaam mwishoni mwa juma.

Shirika la Ndege la Etihad lenye makao yake makuu katika nchi za Falme za Kiarabu mwishoni mwa wiki iliyopita lilimesaidia Kituo cha michezo cha Sokoine jogging club Tanzania kilichopo Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam, hapa nchini.

Shirika hilo lililojinyakulia tuzo tatu za ubora wa huduma za anga kwa mwaka huu, limetoa vifaa vya shule na michezo pamoja na viburudisho mbalimbali baada ya watoto wa kituo cha michezo cha Sokoine kushiriki mechi ya kirafiki na michezo mbalimbali iliyofanyika kwenye uwanja wa Uhuru, jijini Dar es salaam.

Zaidi ya watoto 90 wa kituo hicho wengi wao kuanzia umri kati ya miaka 10-14 walijumuika kushiriki michezo  hiyo ya kirafiki iliyohusisha michezo ya mpira wa miguu kwa wavulana na netiboli kwa wasichana.

Bonanza hilo lililenga kuimarisha umoja na afya kwa vijana. Kituo cha Michezo cha Sokoine jogging club kilianzishwa 20 Agosti, 2014 kwa lengo la kusaidia vijana wa umri wa miaka 7-15 kunufaika kwa kupitia michezo na mazoezi ya kukimbia ( jogging).

Akilishukuru Shirika la Ndege la Etihad, mwanzilishi wa kituo hicho cha michezo, Bwana Felix Kauta Massawe (38) alisema,” Tunashukuru sana kwa kupokea msaada huu mkubwa kutoka Shirika la Ndege la Etihad. Vifaa hivi vitatusaidia kwenye shughuli zetu za kila siku hapa kituoni.”

 “Kituo chetu cha michezo kina takriban wanafunzi 120 ambao wanahitaji vifaa muhimu kwenye mafunzo tunayowapa, hili siyo tu tunawasaidia kupata elimu ya michezo bali pia inawaimarisha kiafya kupitia michezo na mazoezi wanayopata."

Mratibu wa Masoko wa Shirika la Ndege la Etihad nchini, Grace Kijo alisema, “Tunaamini kwamba kwa kuwasaidia vijana hawa tunaandaa taifa la vijana wenye nguvu na afya huku dhumuni lete likiwa kudhamini zaidi kwenye vituo vya michezo na matukio mengine kama haya kwa siku za karibuni.”

 “Shirika la Ndege la Etihad limedhamiria kusaidia na kuleta mabadiliko kwenye jamii ambako linafanya shughuli zake. Mchango wetu wa dhati wa shirikia hili ni kuhakikisha linasaidia juhudi zilizoanzishwa za kuleta maendeleo endelevu kwenye jamii na kuboresha maisha ya jamii ikiwamo elimu kwa watoto na kuwezesha maisha yao,” alisema Kijo.

DKT INTERNATIONAL TANZANIA YAZINDUA ‘TRUST COMMUNITY MATERNITY HOMES

$
0
0
 Meneja Masoko wa DKT international Tanzania Sialouise Shayo akizungumza na wageni mbalimbali waliofika kujionea Kliniki mpya na ya kisasa iliyozinduliwa katika makao makuu ya Shirika hilo hivi karibuni Masaki, jijini Dar es salaam kwa ajili ya Afya ya uzazi kwa kina mama.
 Meneja Mradi wa programu ya Trust community maternity homes kutoka DKT International Tanzania Carol Francis Mango akifafanua jambo kwa waandishi wa habari katika hafla ya uzinduzi wa kliniki hizo mpya zilizotengenezwa maalumu kwaajili ya kukidhi mahitaji ya afya ya uzazi na uzazi wa mpango kwa wanawake wanaoishi kwenye miji midogo katika jamii yetu. Uzinduzi wa kliniki hizo ulifanyika jana katika makao makuu ya Shirika hilo jijini Dar es salaam.
 Mkunga kutoka DKT International Tanzania Adella Hugo akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na huduma mbalimbali zinazopatikana kwenye Kliniki mpya ya uzazi wa Mpango iliyozinduliwa jana katika Makao makuu ya Shirika hilo Masaki, jijini Dar es salaam. Kliniki hiyo ni maalumu kwaajili ya kukidhi mahitaji ya afya ya uzazi na uzazi wa mpango. 
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la DKT International Tanzania Raphael da Silva akizungumza na vyombo mbalimbali vya habari wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kliniki mpya za Shirika hilo zijulikanazo kama “Trust community maternity homes”. Kliniki hizo mpya ni maalumu kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya afya ya uzazi na uzazi wa mpango kwa wanawake wanaoishi kwenye miji midogo katika jamii yetu. Uzinduzi huo ulifanyika jana katika Makao makuu ya Shirika hilo Masaki, jijini Dar es salaam.
Meneja Masoko wa DKT International Tanzania Sialouise Shayo akionyesha baadhi ya bidhaa kwa waandishi wa habari zinazopatikana kwenye Kliniki mpya ya uzazi wa Mpango iliyozinduliwa jana katika Makao makuu ya Shirika hilo Masaki, jijini Dar es salaam. Kliniki hiyo ni maalumu kwaajili ya kukidhi mahitaji ya afya ya uzazi na uzazi wa mpango.

SHIRIKA lisilo la kiserikali la DKT International Tanzania limezindua mfano wa Kliniki mpya ziitwazo “Trust community maternity homes kwa ajili ya wananchi wa kipato cha kawaida zinazoendeshwa na wakunga mbalimbali.

“Trust Community Maternity Homes” – Ni kliniki zinazojitosheleza zilizotengenezwa kwa ubunifu kwa kutumia kontena ya kusafirishia mizigo, kliniki hizi zimetengenezwa maalumu kwaajili ya kukidhi mahitaji ya afya ya uzazi na uzazi wa mpango kwa wanawake wanaoishi kwenye miji midogo katika jamii yetu.

Kiliniki za “Trust Community Maternity Homes”  zilizinduliwa kwa umma  wakati wa uzinduzi wa kliniki ya “Trust Health & Wellness Clinic “ ya Dar Es Salaam na ofisi  mpya za DKT International Tanzania  mnamo tarehe mbili September, 2016

“Kila mwaka, wanawake milioni moja hapa Tanzania ambao hawakukusudia kupata ujauzito hupata ujauzito” alisema mkurugenzi mkuu wa DKT international, Raphael da Silva.

“Hali hii si tu kuwa ina athiri wanawake hawa kifedha, afya zao binafsi na hali ya kiuchumi ya familia zao, lakini pia zinapelekea kuongeza uhitaji wa Serikali kutoa huduma za kiafya pamoja na elimu kwa watoto hawa .Kama tunaweza kufanikisha kutoa huduma zenye ubora wa hali ya juu za afya ya uzazi na uzazi wa mpango kwa jamii katika miji midogo na wanajamii ambao hawapati huduma hizi kiurahisi, tutafanikiwa kuleta mabadiliko chanya katika maisha ya wanawake hawa” alisema.

“Trust Community Maternity Homes ni kliniki zinazojitosheleza ndani ya kontena la kusafirishia mizigo, zinazoendeshwa na wakunga wataalamu na wenye uzoefu wa muda mrefu kama washirika chini ya kliniki mama za “Trust health and wellness clinics” .  Alisema meneja mradi, Karoli Mango.

“Kliniki hizi zinatoa ubora ule ule wa huduma , usiri na msaada  sawa sawa na Kliniki zetu nyingine za Trust  zinazopatikana mikoani hapa nchini .Kliniki yetu ya kwanza ya “ Trust community maternity homes” ya mjini  Kahama iko katika hatua za mwisho za  maandalizi kabla ya ufunguzi” aliongeza.

Trust ina mpango wa kuingia mikataba yenye masharti mepesi na wakunga wazoefu ambayo itawawezesha kukodisha na baadae kuzi miliki kliniki hizi.  Wakunga wanaotoa huduma hizi watatumia kliniki hizi ambazo ziko ndani ya kontena ambazo zinatumia umeme wa sola , zenye uwezo wa kutoa huduma kamili za afya ya uzazi na uzazi wa mpango, pamoja na huduma nyingine za afya kwa jamii. Wakunga hawa watajipatia kipato kwa kutoza kiasi kidogo cha fedha kwa huduma na bidhaa zitakazo tolewa katika kliniki hizi. 

Kwa sasa , kuna “ Trust health and wellness  clinic” nne  ambazo ziko Dar es Salaam, Dodoma, Mbeya and Mwanza  na pia kuna kliniki  na hospitali washirika  30  ambazo zinatoa huduma kwa kutumia chapa ya Trust. 

Kliniki ya Msasani peninsula ya Dar Es Salaam ilifunguliwa mapema mwezi Julai.
Viewing all 46339 articles
Browse latest View live


Latest Images