Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 959 | 960 | (Page 961) | 962 | 963 | .... | 1897 | newer

  0 0


  Mhandisi wa Mkongo wa Taifa kutoka Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nsaji Mwamukonda (kushoto) akizungumza na mmoja wa wakandarasi kwenye banda la maonesho ya bidhaa na huduma za TTCL, kwenye Mkutano Mkuu wa 14 wa Wahandisi jijini Dar es Salaam Mhandisi Mratibu wa Huduma Mpya za TTCL, Yonah Kulanga (wa kwanza kushoto) akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa 14 wa Wahandisi jijini Dar es Salaam


   KAMPUNI ya Simu Tanzania (TTCL) imesema inamajibu ya mawasiliano ya uhakika kwa wahandisi wanaofanya kazi zao maeneo yasio na mawasiliano na sasa imeanza kutoa huduma hiyo kwa wahandisi hao ili waweze kutekeleza kazi zao kwa ufanisi. Kauli hiyo imetolewa na Mhandisi Mratibu wa Huduma Mpya za TTCL, Yonah Kulanga akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa 14 wa Wahandisi jijini Dar es Salaam ambapo kampuni hiyo imewahakikishia wakandalasi hao kuwa ipo tayari kusaidia kutoa mawasiliano hata maeneo yasio na mifumo ya kawaida ya mawasiliano nchini. 

  Alisema mawasiliano ni miongoni mwa nyenzo muhimu kwa makampuni hayo hivyo TTCL inamajibu ya kutoa mawasiliano hata kwa maeneo ambayo hayana mfumo wa mawasiliano wa kawaida kwa kufunga vifaa maalumu ambavyo vinasaidia kampuni hizo kufanya mawasiliano yao wakiwa kwenye maeneo ya kazi. Alisema wahandisi wanafanya tafiti na mawasiliano nje na ndani ya nchi hivyo kuhitaji mawasiliano ya uhakika wakati wote wawapo kazini. 

  Aliongeza kuwa wakandarasi wamekuwa wakifanya kazi maeneo ya porini sehemu ambazo hazina mawasiliano ya mkongo, wala kopa na hata mawasiliano ya redio jambo ambalo TTCL imeleta mapinduzi kwa wakandarasi hao ili kuweza kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na bila vikwazo vya mawasiliano. "...Kwa maeneo kama haya ambayo hayana mawasiliano TTCL tumekuja na majibu kwa wahandisi katika maeneo kama haya tunaweza kuwapatia wahandisi mawasiliano ya intaneti kwa kutumia mawasiliano ya sateliti, yaani tunafunga vifaa maalumu vinavyo saidia kupata mawasiliano eneo husika...," alisema Kulanga. 

  Alisema kwa sasa maeneo yote ya Tanzania TTCL inaweza kutoa huduma hizo kwa wahandisi watakao hitaji Aidha alisema huduma hii imesha tolewa, yataja maeneo ambayo wamesha toa huduma hizo kuwa ni pamoja na Rukwa kwa baadhi ya mbuga, Lindi Londo Forest, Mbuga ya Serengeti maeneo ya utafiti, Kituo cha Tawiri, Kituo cha Utafiti Makutupora Dodoma, Maeneo ya Ufugaji Kongwa, mbayo hayana mawasiliano kama wakanda. Kwa upande wake, Mhandisi wa Mkongo wa Taifa, Nsaji Mwamukonda alisema wahandisi wanapewa fursa kubwa ya kutumia mkongo pamoja na faida zake kwenye shughuli zao hivyo kuwataka pia kutumia kituo mahiri cha kutunzia taarifa (Data Centre) kinachoendeshwa na TTCL katika kuhifadhi taarifa zao kwa usalama. 

  Alisema wahandisi wana taarifa muhimu ambavyo hutumika kwa shughuli mbalimbali hivyo hazina budi kuhifadhiwa sehemu salama na ya uhakika hivyo kuwaomba wajitokeze kukitumia kituo hicho cha kuhifadhi taarifa. "...Wahandisi wetu wanataarifa muhimu katika kazi zao na nyingine wamekuwa wakizitegemea kwenye tafiti hivyo nashauri makampuni haya kukitumia kituo chetu kuhifadhi taarifa zao kiusalama," alisema Mwamukonda. 

  Mkutano Mkuu wa 14 wa Wahandisi unafanyika kwa siku mbili jijini Dar es Salaam Septemba 1 na 2, 2016 katika viwanja vya Mlimani City ambapo makampuni na taasisi mbalimbali wadau wa wahandisi ikiwemo TTCL zimeshiriki kufanya maonesho juu ya huduma na bidhaa anuai kwa wajumbe kwenye mkutano huo.

  0 0


  Mkuu wa Idara ya Rasilimawatu kiwanda cha Sauji cha Simba Cement cha Tanga, Diana Malambugi, akimkabidhi mifuko ya saruji 400 yenye thamani zaidi ya milioni 4.8 kwa mwalimu mkuu shule ya Sekondari ya Ilboru ya Arusha, Julias Shulla ikiwa ni ujenzi wa vyumba vya madarasa.nyuma kulia ni Mkuu wa fedha Pieter Jaggar na kushoto ni Emmanuel Jonas mhasibu.
  Tangakumekuchablog

  Tanga, KIWANDA Cha Saruji Cha Simba (Simba Cement) cha Tanga, kimeipa shule ya Sekondari ya Ilboru Secondary School ya Arusha mifuko 400 ya saruji yenye thamani zaidi ya milioni 4.8 kwa ujenzi wa vymba vya madarasa.

  Akizungumza wakati wa halfa fupi ya makabidhiano leo, Mkuu wa Idara ya Rasilimaliwatu kiwanda cha Saruji cha Simba Cement, Diana Malambugi, alisema msaada huo umetolewa ili kupunguza changamoto za vyumba vya madarasa kwa shule hiyo.

  Alisema msaada huo utapunguza uhaba wa vyumba vya madarasa na kutoa wito kutumika kama ilivyokusudiwa na kuiagiza kamati ya shule kuhakikisha mifuko hiyo inatumika ipasavyo.

  ‘Mifuko hii ya saruji itapunguza changamoto inayoikabili shule yako ikiwemo vyumba vya madarasa na ujenzi wa nyumba za walimu, sera yetu moja wapo ni hii ya elimu” alisema Malambugi

  Alimtaka mwalimu huyo na kamati yake ya shule kuitunza mifuko hiyo ya saruji na kumhakikishia kuisaidia pale ambapo kutakuwa na uhitaji na kuwataka wadau wengine wa elimu kusaidia sekta ya elimu zikiwemo kuondosha changamoto za uhaba wa madawati na vyumba vya madarasa.

  Kwa upande wake, mwalimu mkuu wa shule ya Ilboru sekondari school , Julias Shulla, alikishukuru kiwanda hicho na kusema kuwa msaada huo utatumika kama ilivyoombwa.

  Alisema shule yake inakabiliana na changamoto nyingi zikiwemo uhaba wa vyumba vya madarasa pamoja uhaba wa vifaa vya maabara hivyo kuwataka wadau wa elimu kuisaidia.

  ‘Tunakishukuru kiwanda cha saruji cha simba kwa moyo wao waliounyesha kwetu, kwa fadhila hii tunawaahidi kuwa tutaitumia saruji kama tulivyoiomba” alisema Shulla

  Alisema mifuko hiyo itapunguza kwa kiasi kikubwa changamoto ambazo shule yake inakabiliana nazo na kusema kuwa msaada huo ni faraja kwao na wanafunzi wa shule yake.


  Mhasibu wa kiwanda cha Saruji cha Simba Cement, Emmanuel Jonas, akimkabidhi mwalimu mkuu wa shule ya Sekondari ya Iboru ya Arusha, Julias Shulla mifuko ya saruji 400 yenye thamani zaidi ya shilingi milioni 4.8 kwa ajili ya ujenzi wa vymba vya madarasa, nyuma ni mkuu wa fedha, Pieter Jaggar.

  Afisa Uhusiano kiwanda cha Saruji cha Simba Cement cha Tanga, Mtanga Nnour, akimkabidhi mifuko ya saruji 400 yenye thamani zaidi ya shlingi milioni 4.8 kwa mwalimu mkuu wa shule ya sekondari ya Ilboru ya Arusha, Julias Shulla, ikiwa ni kusaidia ujenzi wa vyumba vya madarasa. Nyuma ni mkuu wa fedha, Pietre Jaggar.


  Mkuu wa fedha kiwanda cha saruji cha Simba Cement, Pieter Jaggar, akimabidhi mifuko ya saruji 400 yenye thamani zaidi ya shilingi milioni 4.8 mwalimu mkuu wa shule ya sekondari ya Ilboru ya Arusha, Julias Shulla ikiwa ni kusaidia ujenzi wa vyumba vya madarasa, kulia ni meneja usambazaji na ugawaji, Samwel Shoo, nyuma kulia ni Afisa Uhusiano , Nour Mtanga na mkuu wa Idara ya Rasilimawatu, Diana Malambugi.
  Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Kumekucha. 0655902929

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dkt. Charles Kimei  amefanya ziara katika baadhi ya matawi ya Benki hiyo yaliyopo jijini Dar es Salaam kujionea utendaji kazi na kukabiliana na changamoto zilizopo. 
  Katika ziara hiyo pamoja na kukagua utendaji kazi, Dk. Kimei pia alitumia fursa hiyo kukutana na kuzungumza na wateja.

  Dk. Kimei pia alitembelea ATM za Benki hiyo zilipozo maeneo ya Namanga-Msasani, Mikocheni, Tegeta, Mbezi na Millennium Tower na kuahidi kuwa Benki hiyo imejipanga kuhakikisha kuwa huduma hiyo inaendelea kuboreshwa ili kufikia mahitaji ya wateja. "Hivi sasa tuna zaidi ya ATMs 400 na tunajipanga kufikisha ATM 500 ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.

  Pia aliongeza kuwa "Tumeweka mikakati ya kuhakikisha kuwa ATM zetu zinajazwa pesa kwa wakati ili kuondoa usumbufu wowote kwa wateja wetu" alisema Dk. Kimei.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kabla ya kuanza kwa ziara yake katika baadhi ya matawi ili kujionea utendaji kazi pamoaja na kutembelea ATM za benki hiyo.
  Dk. Charles Kimei akitoa fedha katika mashine ya ATM ya eneo la Namanga jijini Dar es Salaam, baada ya kufanya ziara ya kuangalia utendaji kazi wa baadhi ya matawi ya jijini Dar es Salaam. 
  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akizungumza na Mkurugenzi wa Benki ya CRDB, tawi la Tegeta, Richard Mkakala (kushoto), wakati alipofanya ziara kuangalia utendaji kazi katika baadhi ya matawi ya benki hiyo jijini Dar es Salaam. 
  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (kulia), akizungumza na wateja wa benki hiyo katika tawi la Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.
   Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akifafanua jambo wakati alipofanya ziara ya kuangalia utendaji kazi katika tawi la Mbezi Beach jijini Dar es Salaam. Katikati ni Meneja wa tawi hilo, Wemaeli Msechu na kulia ni Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa benki hiyo, Tully Mwambapa.

  0 0


  Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na uhamasishaji wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bi. Sarah Kibonde Msika (katikati) na Bw. Kenneth Batanyita (kushoto), wakitoa maelezo kuhusu Hifadhi ya Jamii kwa mgeni aliyetembelea banda la SSRA, wakati wa maonesho ya Wiki ya Fedha, viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
  Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Uhamasishaji wa SSRA, Bi. Sarah Kibonde Msika akitoa maelezo na kugawa vijarida kuhusu hifadhi ya Jamii kwa baadhi ya wageni waliotembelea banda la SSRA katika maonesho ya Wiki ya Fedha, viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
  Afisa wa SSRA, Bi. Amina Ally akitoa mada katika Semina ya uhamasishaji wa Hifadhi ya Jamii kwa wajasiriamali wadogo walioshiriki katika mafunzo yaliyokuwa yakitolewa katika Wiki ya Fedha yaliyofanyika viwanja vya Mnazi Mmoja hivi karibuni.
  Maofisa wa Mamlaka, Bi. Imani Masebu (kushoto) na Bi. Agnes Lubuva (kulia) wakitoa maelezo kuhusu umuhimu wa Hifadhi ya Jamii kwa wajasiriamali wadogo waliotembelea banda la SSRA katika maonesho ya wiki ya Fedha hivi karibuni.
  Afisa wa Mamlaka Bw. Athumani Juma akigawa vipeperushi na vijarida vya uhamasishaji wa umuhimu wa kujiunga na Hifadhi ya Jamii kwa wajasiriamali wadogo waliotembelea banda la SSRA katika maonesho hayo, hivi karibuni.
  Afisa wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bw. Ally Masaninga akitoa maelezo kuhusu kazi mbalimbali zinazofanywa na Mamlaka pamoja na kugawa vipeperushi kwa washiriki waliotembelea Banda la SSRA katika maonesho ya wiki ya Fedha, viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

  Afisa wa SSRA, Bw. Frank Kilimba akitoa maelekezo kuhusu Sekta ya Hifadhi ya Jamii kwa wageni waliotembelea banda la Mamlaka hiyo, katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini.
  Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama (wa pili kushoto), katika meza kuu akiwa na viongozi wa maonesho ya wiki ya Fedha pamoja na wawakilishi wa Mashirika na Taasisi mbalimbali ikiwemo SSRA, wakifuatilia kwa makini risala toka kwa wajasiriamali (hawapo pichani), katika siku ya kilele cha maonesho ya Fedha, viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam hivi karibuni.

  0 0

  Mbunge,Mh.Venance Mwamoto


  Na Matukiodaima Blog

  KOCHA wa timu ya Bunge Venance Mwamoto ametoa mwaliko kwa timu ya Bodaboda kilolo kwenda bungeni kucheza mchezo wa kirafiki na wabunge 

  Mwamoto ambae ni mbunge wa Kilolo mkoani Iringa alitoa mwaliko huo wakati wa kikao chake na vijana hao wa bodaboda mjini Ilula Jana.

  Alisema kuwa kabla ya kwenda bungeni vijana hao watashindana kupata bingwa wa mashindano hayo ambaye atakwenda Dodoma kucheza na wabunge.Hivyo alisema lazima kujipanga vema kwa kujiandaa ili kuepuka aibu ya kichapo kutoka kwa wabunge. 

  "Nawaomba timu itakayoshinda iwe bungeni kutangaza wilaya getu ya Kilolo kisoka pia kuanza rasmi kwa mashindano ya Mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdalah na mimi mbunge wenu nitadhamini "

  Hata hivyo alisema kabla ya mashindano hayo atatoa vifaa vya michezo kwa timu zote shiriki kama njia ya kuondoka kero ya vifaa vya michezo. Mwamoto alisema lango ni kuona vijana Kilolo wanakuwa na timu na kupitia michezo wanapata ajira kwa kuchezea timu mbali mbali kubwa nchini.

  0 0


  0 0


  Usajili wa MeTL Career Fair (Job Bonanza) kufungwa leo jumamosi changamkia fursa.

  Kama wewe ni mhitimu katika Uhandisi au Utawala (Masoko, Mahusiano, Fedha) na una ari ya kujifunza, ukiwa na mtazamo chanya wa mafanikio na mfuatiliaji wa maadili katika kazi, njoo ujiunge nasi katika bonanza hili la uchambuzi wa ajira.
  Rasilimali Watu
  Mauzo
  Uhasibu
  Masoko
  Uhandisi
  Kilimo
  Nguo
  Kwani unaweza ukawa mmoja kati ya watu 25 tutakao wachagua kwa ajili ya kujiunga kwenye programu ya uendelezaji wa wahitimu wa vyuo vikuu.Na ukibahatika kuwa mmoja wapo kati ya hao utapata nafasi ya kujifunza kwa vitendo katika viwanda vyetu vilivyopo maeneo mbalimbali.Pia utapata nafasi ya kufundishwa mifumo ya uendeshaji wa viwanda vya kisasa.     
                  
  Utakuwa chini ya wakufunzi waliobobea katika kazi zao duniani ambao  watakuwezesha wewe kukua katika kazi na kushika nyadhifa kwenye kazi yako.
  Zaidi ya yote hayo utakayofanyiwa pia utalipwa ili kujifunza
  Kwa taarifa zaidi tazama vipeperushi vyetu:


  0 0  0 0


  Afisa Tawala Wilaya ya Nyamagana, Kombe Danty (wa pili kushoto), akizungumza kwenye ungaji wa Mafunzo/Semina ya Utetezi wa Haki za Binadamu katika Sekta ya Madini nchini hii leo jijni Mwanza.

  Na George Binagi-GB Pazzo

  Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, Mary Tesha, amesema Serikali itaendelea kushirikiana na Watetezi wa Haki za Binadamu nchini ikiwemo kuweka mazingira salama katika utendaji wao wa kazi.

  Tesha ameyasema hayo hii leo Jijini Mwanza, katika hotuba yake iliyosomwa na Afisa Tawala Wilaya ya Nyamagana, Kombe Danty, kwenye ungaji wa Mafunzo/Semina ya Utetezi wa Haki za Binadamu katika Sekta ya Madini nchini.

  Naye Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu nchini, Onesmo Olengurumwa, amesema mtandao huo umekuwa ukitoa semna kwa watetezi mbalimbali wa haki za binadamu ili kuwajengea uwezo wa kufanya kazi bila migogoro yoyote na serikali.


  Kutoka ni Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Nyamagana, Heri Nkoromo, Afisa Tawala Wilaya ya Nyamagana, Kombe Danty, Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu nchini, Onesmo Olengurumwa na Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu mikoa ya Mara, Mwanza na Simiyu, Antony Mayunga.
  Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Nyamagana, Heri Nkoromo, akizungumza kwa niaba ya mbunge huyo, ambapo amewasihi washiriki wa mafunzo hayo kufikisha elimu waliyoipata kwa watetezi wengine ambao hawakubahatika kuhudhuria semina hiyo.
  Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu nchini, Onesmo Olengurumwa (kulia), anasema wakati mwingine Watetezi wa Haki za Binadamu wamekuwa wakichukuliwa kama wachochezi kwenye jamii jambo ambalo si sahihi.
  Washiriki wa Semina hiyo ya siku tatu, iliyoanza Agosti 31,2016 wamepatiwa vyeti vya ushiriki ambapo pichani ni Jimmy Luhende kutoka taasisi ya Utawala Bora nchini, akipokea cheti cha ushiriki.
  Angel Benedict kutoka Shirika la Kutetea Wafanyakazi wa Majumbani, Wote Sawa, la Jijini Mwanza, akipokea cheti cha Ushiriki.
  Mwanahabari na Mwendeshaji wa Mtandao wa Mabadiliko Forums, akipokea Cheti cha Ushiriki.
  Mshiriki akipokea cheti cha Ushiriki
  Mshiriki akipokea cheti cha Ushiriki
  Mshiriki akipokea cheti cha Ushiriki
  Mshiriki akipokea cheti cha Ushiriki
  Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu nchini (THRD) unajumuisha Watetezi/Watu wanaotetea haki mbalimbali katika jamii ikiwemo kwa makundi ya Wakulima, Wafugaji, Waandishi wa Habari, Wanasheria, Katiba, Utawala Bora, Watoto, Wanawake miongoni mwa makundi mengi katika jamii.

  Bonyeza HAPA Kujua Zaidi

  0 0

  Kaimu Katibu Mkuu wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) Dkt .Adolf Rutayuga(Kushoto) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam ( hawapo pichani) kuhusiana na matapeli wanaowaomba fedha au rushwa wakuu wa vyuo hasa vilivyopewa notisi na Baraza hilo,kushoto kwake ni Mkuu wa Kitengo cha Udahili wa baraza hilo, Seremani Majindo.  Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) linatoa tahadhari kwa Wamiliki na Wakuu wote wa Vyuo vya Elimu ya Ufundi nchini kuwa kumeibuka matapeli wanaowaomba fedha au rushwa wakuu wa vyuo hasa vilivyopewa notisi na Baraza ya kushushwa hadhi au kufungiwa ili kuweza kuwasaidia kutatua matatizo yao kupitia namba mbalimbali za simu wanazozitoa.

  Baraza linaendelea na kuwatahadharisha wateja wetu kuwa msikubali kupokea simu zenye kuwaomba fedha au kutoa kitu chochote wakati mnapotekeleza maelekezo ya Baraza au hata baada ya kutekeleza maelekezo hayo.

  Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Dkt. Adolf Rutayuga anatoa tahadhari hii baada ya ofisi yake kupokea malalamiko hivi karibuni kutoka kwa baadhi ya Wakuu wa Vyuo na Wamiliki ambao wamedai kupigiwa simu na watu wanaojitambulisha kuwa Maafisa wa NACTE na kuwadai kiasi cha fedha kama masharti ya kutatuliwa matatizo yao. Pia Baraza limepokea taarifa kutoka kwa Wadau wanaolalamika kuwa kuna kundi watu wanaodai kupewa fedha ili wasaidiwe kupangiwa vyuo fulani vya ufundi kwa masomo mbali mbali.

  Baraza halina utaratibu wa kuomba fedha au zawadi ya aina yeyote kwa Mkuu wa Chuo au Mtu yoyote kama sharti la kupata huduma/msaada fulani.

  Ni imani yetu kwamba wakati Baraza likiendelea na uchunguzi wa kuwabaini matapeli hao ili kuwachukulia hatua za kisheria, Wadau wetu wataongeza umakini na kuchukua tahadhari binafsi na watu wa namna hiyo.

  Imetolewa na
  Ofisi ya Katibu Mtendaji – NACTE
  01 Septemba, 2016.

  0 0

  Malkia wa Kinondoni 2016 Diana Edward ndiye huyu hapa.
  Lete Raha Miss Kinondoni 2016, Diana Edward (katikati), akipunga mkono baada ya kutangazwa kuwa mshindi Dar es Salaam jana. Kulia ni mshindi wa pili Regina Ndimbo na kushoto ni mshindi wa tatu, Sia Pius.
  Warembo hao wakiserebuka wakati wakijitambulisha.
  Wadau wakifuatilia kwa karibu shindano hilo. 
  Washiriki wa shindano hilo wakiwa katika vazi la ubunifu. Kutoka kushoto ni Catherine Liston, Hafsa Mahamoud na Mariana Charles.
  Washiriki hao waliofanikiwa kuingia 10 bora.
  Washiriki waliofanikiwa kuingia tano bora. Kutoka kulia ni Hafsa Mahamoud, Diana Edward ambaye ndiye Miss Kinondoni 2016. Regina Ndimbo, Sia Pius na Jackline Kimambo.
  Majaji wa shindano hilo wakiwa kazini. 
  Mgeni rasmi wa shindano hilo, Gift Msuya (kulia), akiwa katika picha ya pamoja na washindi wa shindano hilo.
  Hapa ni sebene kwa kwenda mbele.
  Wakina mama wakimtuza mwanamuziki Christian Bella wakati akiimba wimbo wa Nani kama mama.
  Mgeni rasmi wa shindano hilo, Katibu Tawala wa Wilaya ya Kinondoni, Gift Msuya (katikati), akikabidhi zawadi.


  Na Dotto Mwaibale

  KAMATI ya maandalizi ya shindano la Lete Raha Miss Kinondoni 2016 imemtangaza Diana Edward kuwa mlimbwende wa wilaya hiyo baada ya kuibuka mshindi katika shindano lililofanyika Hoteli ya Denfrances iliyopo Sinza jijini Dar es Salaam jana.

  Edward aliibuka mshindi baada ya kuwabwaga washiriki wenzake 20 waliokuwa wakiwania taji hilo ambapo nafasi ya pili ilichukuliwa na Regina Ndimbo huku ya tatu ikichukuliwa na Sia Pius ambapo Happyness Munisi akishinda nafasi ya utanashati.

  Akizungumza wakati wa mchakato wa kutoa zawadi Mratibu wa shindano hilo, Rhamat George alisema asilimia 10 ya mapato yaliyopatikana katika shindano hilo yatakwenda Wilaya ya Kinondoni kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa madarasa ikiwa ni kumuunga mkono Rais Dk. John Magufuli ya kuhakikisha kila mwanafunzi anapata elimu bure katika mazingira bora.

  Katika shindano hilo washindi waliofanikiwa kuingia tano bora wataingia moja kwa moja katika kinyang'anyiro cha kumsaka mlimbwende wa Tanzania.

  Shindano hilo lilidhaminiwa na Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Ltd kupitia bia ya Windhoek Lager na Draught pamoja na Gazeti la Lete Raha na wadhamini wengine.

  Katibu Tawala wa Wilaya ya Kinondoni, Gift Msuya alisema Serikali itaendelea kuunga mkono mashindano hayo ambayo yamekuwa yakitoa ajira na kuibua vipaji vya watoto wa kike.

  Shindano hilo lilipambwa na burudani kutoka kwa mwanamuziki wa muziki wa dansi Christian Bella na kundi la sanaa la Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Ltd.

  0 0

  Mazungumuzo yakiendelea wengine katika mazungumuzo hayo kutoka kushoto kwa mzunguko wa meza ni Afisa Uhamiaji wa Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani, Bwn. Abbas Missana, Brady Surles ambaye ni Mkurugenzi mtendaji wa Sister Cities ya Durham yenye mashirikiano na mji wa Arusha, Tony Nturu, Dorothy Borden ambaye ndie mwanzilishi wa Sister Cities na Mwenyekiti wa Umoja wa Watanzania North Carolina, Bi. Gloria Alex,
  Mazungumuzo yakiendelea.
  Mwenyekiti wa Umoja wa Watanzania North Carolina akiongea na Mayor William V"Bill Bell" na kumkaribisha kwenye mkutano wa Mhe. Balozi Wilson Masilingi atakapokutana na Watanzania wa Nortrha Carolina utakaofanyika leo Jumamosi Septemba 3, 2016 katika hotel ya Comfort Suites RDU iliyopo 5219 Page Road, Durham, NC 27703 kuanzia saa 12 jioni kwa saa za Marekani Mashariki(ET)
  Mayor William V" Bill Bell" na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Mhe. Wilson Masilingi katika picha ya pamoja.
  Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Watanzania North Carolina (UTNC) Bi. Gloria Alex akimpokea na kukaribisha North Carolina Balozi wa Jamhuri wa Muungano ya Tanzania nchini Marekani na Mexico, Mhe. Wilson Masilingi siku ya Ujumaa Septemba 2, 2016 City Hall mjini Durham, Northa Carolina katika ofisi ya Mayor ambapo Mhe. Balozi alikwenda kukutana na kufanya mazungumuzo na Mayor wa mji wa Durham Mayor William V." Bill Bell" (hayupo pichani,
  Kushoto ni Mayor William V" Bill Bell" Mayor wa mji wa Durham akisalimiana na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Mhe. Wilson Masilingi ofisini kwake siku ya Alhamisi Septemba 3, 2016 Mhe, Balozi alipokwenda kumtembelea na kufanyanae mazungumuzo.
  Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Mhe. Wilson Masilingi akifanya mazungumuzo na Mayor wa mji wa Durham Mayor William"Bill Bell"
  Na mwandishi wetu, Durham, NC

  Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Mhe. Wilson Masilingi siku ya Ijumaa Septemba 2, 2016 alimtembelea na kufanya mazungumuzo na Mayor wa mji wa Durham, North Carolina, Mayor William V. "Bill Bell".

  Katika mazungumuzo hayo yaliyofanyika ofisi ya Mayor iliyopo City Hall, Mhe. Balozi Wilson Masilingi alimweleza Mayor William "Bill Bell" nia yake ya kutafuta wawekezaji watakaosaidia kukuza uchumi wa Tanzania kupitia seka mbalimbali huku akimweleza juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Magufuli za kufufua na kujenga viwanda,

  Mhe. Balozi Wilson Masilingi alimhakikishia Mayor William "Bill Bell" wawekezaji watakaokua tayari kuwekeza Tanzania watafanyia taratibu zote na kwa haraka zaidi na bila kuwa na usumbufu huku Mayor William "Bill Bell" akimuahidi Mhe. Balozi William Masilingi kutoa ushirikiano wa karibu na kuhakikisha anamkutanisha na wawekezaji wa Durham, North Carolina watakaokua tayari kuwekeza nchini Tanzania.

  0 0

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano), Prof. Faustin Kamuzora akizungumza wakati akifunga warsha ya wadau na wataalamu kutoka Shirika la Mawasiliano la Jumuiya ya Madola (hawapo pichani) kuhusu uandaaji wa Mkakati wa Kitaifa wa Usalama katika Mitandao nchini.
  Afisa Mwandamizi wa ufundi na ushauri wa Shirika la Mawasiliano la Jumuiya ya madola Bw. Fargani Tambeayuk akitoa shukurani kwa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano pamoja na wadau wengine baada ya kumalizika kwa warsha ya uandaaji wa Mkakati wa Kitaifa wa Usalama katika Mitandao.
  Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya TEHAMA wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Dkt. Shabani Pazi akizungumza wakati akimkaribisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano), Prof. Faustin Kamuzora (hayupo pichani) wakati wa kufunga Semina ya Uuandaaji wa Mkakati wa Kitaifa wa Usalama katika Mitandao leo. Jijini Dar es Salaam.
  Wadau wa Sekta ya Mawasiliano wanaoandaa Mkakati wa Kitaifa wa Usalama kwenye Mtandao wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano), Prof. Faustin Kamuzora (hayupo pichani) wakati wa kufunga warsha ya wadau na wataalamu kutoka Shirika la Mawasiliano la Jumuiya ya Madola wanaoandaa mkakati huo.

  Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano ( Sekta ya Mawasiliano), Prof. Faustin Kamuzora ametoa wito kwa vyuo vyote nchini kuanzisha mitaala inayohusu usalama wa mitandao ya mawasiliano ili kukabiliana na matumizi mabaya ya mitandao hiyo.

  Kauli hiyo imetolewa Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu huyo alipokuwa akifunga warsha ya siku ya wadau na wataalamu kutoka Shirika la Mawasiliano la Jumuiya ya Madola iliyohusu Uandaaji wa Mkakati wa Kitaifa wa Usalama wa Mitandao iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania.

  Prof. Kamuzora amesema kuwa moja ya vitu vilivyoelezewa katika Sera ya Tehama iliyotolewa mwezi Mei mwaka huu ni kuhakikisha mitandao ya mawasiliano inakuwa salama hivyo kila mwananchi anawajibu wa kulinda mitandao hiyo.

  “Suala la usalama wa mitandao ya mawasiliano linapelekea kuwepo kwa fursa nyingi za ajira hivyo, napenda kutoa wito kwa vyuo mbalimbali nchini kuanzisha mitaala mipya itakayohusu masuala haya kwa sababu watu watatakiwa wajikite kwenye masomo yanayohusiana na mitandao”, alisema Prof.Kamuzora.

  Ameongeza kuwa kwa mujibu wa ripoti za hivi karibuni zimebainisha kuwa dunia nzima inapoteza jumla ya dola bilioni 400 kwa mwaka kwa njia ya wizi wa mitandaoni hivyo kushindwa kulinda mitandao ya mawasiliano kunapelekea hasara kubwa kwa Taifa na Dunia kwa ujumla.

  Naye Afisa Mwandamizi wa ufundi na ushauri wa Shirika la Mawasiliano la Jumuiya ya madola , Fargani Tambeayuk amesema kuwa Jumuiya hiyo inawasaidia nchi wanachama katika kudhibiti usalama wa mitandao ili kusaidia nchi hizo kupata maendeleo kwa kutumia mitandao pamoja ma kuepukana na uhalifu.

  Kwa upande wake Mratibu Mwandamizi wa Jeshi la Polisi, Kitengo cha Makosa ya mitandao, Joshua Mwangasa amesisitiza suala la kutolewa kwa elimu ya usalama wa mitandao liwe endelevu akiamini kuwa elimu hiyo itawasaidia wananchi kuepuka kutumia vibaya mitandao ya mawasiliano.

  Aidha, ameusifia mpango huo kwani utawasaidia Jeshi la Polisi kuweza kukabiliana kirahisi na wananchi wanaofanya makosa kwenye mitandao pia amesisitiza kuwa makosa ya kimtandao ni kama makosa mengine hivyo taratibu za kuripoti makosa hayo ni zile zile za kawaida.

  0 0

  Taasisi mbalimbali zikiwemo za Serikali na binafsi kutoka ndani na nje ya nchi zimeshiriki Maonesho ya Biashara ya Afrika Mashariki, yanayofanyika viwanja vya Rock City Mall Jijini Mwanza. Maonesho hayo huandaliwa na Chama cha Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo nchini, TCCIA.

  Taasisi mbalimbali za Wajasiriamali, Wafanyabiashara na Viwanda hutumia Maonesho hayo kukutana na wateja wapya, kutangaza na hata kuuza bidhaa zake. Mbali na hilo taasisi mbalimbali hutumia fursa hiyo kukutana na wananchi na kufikisha elimu husika.

  Jeshi la Polisi mkoani Mwanza kwa kujumuisha vitengo vyake ikiwemo Kikosi cha Usalama barabarani na dawati la jinsia, limetumia maonesho hayo kufikisha elimu mbalimbali kwa wananchi na hata kupokea maoni kutoka kwa wananchi.

  Na BMG
  Banda la Jeshi la Polisi mkoani Mwanza, Kitengo cha dawati la jinsia
  Banda la Jeshi la polisi mkoani Mwanza, kitengo cha Usalama barabarani
  Maonesho hayo yalianza Agosti 26,2016 na ufungi rasmi kufanyika Agosti 30,2016 ambapo Mkuu wa Wilaya ya Ilemela alifungua Maonesho hayo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kama picha inavyoonekana mgeni rasmi akiwa kwenye banda la jeshi la polisi mkoani Mwanza.

  Endelea kutazama picha, Mgeni rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza, akikagua mabanda ya washiriki mbalimbali


  Soma zaidi HAPA

  0 0

   Wajumbe wa Bodi ya wakurugenzi wakimsikiliza Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwigaje, wakati wa uzinduzi wa Bodi hiyo, Leo Jijini Dar es Salaam.
   aziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwigaje akiongea na wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Taifa la Maendeleo  (NDC) wakati akiizindua leo Jijini Dar es Salaam, ambapo ameitaka bodi hiyo kushika miradi mikubwa ya uwekezaji na kuhakikisha inairudisha katika hali yake ili kuiwezesha nchi kufikia uchumi wa kati kupitia uanzishwaji na uendelezaji wa viwanda.

   Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwigaje(kulia) akimkabidhi Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Taifa Maendeleo (NDC) Dkt. Samweli Nyantahe nyaraka mbalimbali zitakazomuongoza katika utendaji kazi.
   Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwigaje akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi ya wakurugenzi ya Shirika la Taifa la Maendeleo  (NDC) mara baada ya kuizindua leo Jijini Dar Es Salaam.
  PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO.

  0 0


  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (Mb) akifuatilia maelezo ya ramani ya Makazi Mapya ya Mhe. Waziri Mkuu Majaliwa Kassim kutoka kwa Wataalam wa maswala ya Ujenzi kulia kwake ni Mhandisi Joseph Muhamba na wa kwanza kushoto ni Bw. Keffa Chana wakati wa Ziara yake katika makazi hayo Septemba 2, 2016 Mlimwa Dodoma.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagam (katikati) akipata maelezo ya eneo la Makazi Mapya ya Mhe. Waziri Mkuu Majaliwa Kassim kutoka kwa Mtaalam wa Masuala ya Ujenzi Bw. Keffa Chana alipofanya ziara ya kukagua makazi haya Septemba 02, 2016 Mlimwa Dodoma.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagam (katikati) akipata maelezo ya eneo la Makazi Mapya ya Mhe. Waziri Mkuu Majaliwa Kassim kutoka kwa Mtaalam wa Masuala ya Ujenzi Bw. Keffa Chana alipofanya ziara ya kukagua makazi haya Septemba 02, 2016 Mlimwa Dodoma.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagam (katikati) akipata maelezo ya eneo la Makazi Mapya ya Mhe. Waziri Mkuu Majaliwa Kassim kutoka kwa Mtaalam wa Masuala ya Ujenzi Bw. Keffa Chana alipofanya ziara ya kukagua makazi haya Septemba 02, 2016 Mlimwa Dodoma.


  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (mb) amesisitiza kuwa dhamira ya Serikali kuhamia Dodoma ipo palepale ndani ya kipindi cha miaka minne hatua kwa hatua.

  Akizungumza na waandishi wa habari Septemba 2, 2016 wakati wa ziara yake eneo la Makazi Mapya ya Mhe. Waziri Mkuu Majaliwa Kassim yaliyopo Mlimwa Dodoma, Waziri Mhagama alisema “Watanzania wawe na amani, dhamira yetu iko vizuri na kama Mhe. Rais alivyosema na tunawahakikishia kwamba ndani ya kipindi hicho sisi tumeshajipanga kuhamamia mkoani Dodoma hatua kwa hatua”.

  Waziri Mhagama alieleza kuwa shughuli za maendeleo hazitosimama kwa kuzingatia mipango iliyopo na bajeti ya Serikali, “Niwatoe wasiwasi kwamba mipango yote ya maendeleo haitosimama na shughuli zote za maendeleo hazitozuiwa na ujio wa Serikali mkoani Dodoma zitafanyika kama zilivyopangwa na tutaendelea kuyafanya hayo kwa kuzingatia Ilani ya uchaguzi ya mwaka 2015 Ibara ya 151 tumesema tunahamia Dodoma na tutafanya hivyo”.Alisisitiza Mhagama

  Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana ameahidi kutekeleza usimamizi wa maagizo ya Waziri ili kukamilisha ujenzi wa barabara kwa wakati “kwa upande wa mkoa kazi iliyobaki ni kuhakikisha kuwa ujenzi wa barabara unakamilika na tutakutana na Wakala wa Barabara (TANROADS), Mamlaka ya Ustawishaji Mji (CDA) na Manispaa ili kuona shughuli hii tunaifanyeje kwa kutekeleza maagizo hayo ikiwa ni sehemu ya majukumu ya mkoa.”

  Aidha, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jordan Rugimbana alimshukuru Waziri Mhagama kwa kutembelea maeneo ya makazi mapya ya Mhe. Waziri Mkuu na Jengo la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,”Namshukuru Mhe. Waziri Mhagama, Manaibu Waziri na Ofisi yote ya Waziri Mkuu kwa ziara hii na kukamilisha awamu ya kwanza ya ujenzi wa Makazi Mapya ya Mhe. Waziri Mkuu.”

  0 0

  Waziri Muhongo.

  Na Georgina Misama-MAELEZO

  Mpaka kufikia 2021 serikali imeahidi kusambaza umeme wa kutosha na wa uhakika katika vijiji vyote nchini ili kuendana na dhamira ya kuelekea katika uchumi wa kati kupitia viwanda.

  Hayo yamesemwa na Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo wakati wa kipindi cha TUNATEKELEZA kinachorushwa na Televisheni ya Taifa ya TBC1 kwa ushirikiano na Idara ya Habari-MAELEZO.

  Prof. Muhongo alisema kuwa kukamilika kwa miradi ya kuzalisha nishati ya umeme ikiwemo Mradi wa Kinyerezi 1 unaozalisha megawati 150 kwa siku umesaidia kuongeza upatikanaji wa huduma ya umeme wa kutosha mijini na baadhi ya vijiji.

  “serikali sasa ipo katika kutekeleza miradi mikubwa ya nishati za umeme na gesi ikiwa ni jitihada za kuhakikisha mpaka kufikia 2021 vijiji vyote nchini viwe vimepata huduma ya nishati ya umeme”. Alisema Prof. Muhongo

  Aidha, Prof. Muhongo alisema kuwa utekelezaji wa Miradi hiyo unaenda sambamba na lengo la Serikali ya awamu ya Tano ya kuwa na uchumi wa kati kupitia viwanda ifikapo 2025.

  Akizungumzia kuhusu mikakati ya kuthibiti utoroshaji wa madini nchini Prof. Muhongo alisema kuwa serikali inaendelea kuweka mikakati ya kuwakamata watoroshaji wa madini hasa katika maeneo ya mipakani na viwanja vya ndege.

  Prof. Muhungo alisema kuwa kuanzia mwaka 2012 wamekamata madini ya aina mbalimbali zaidi ya Tani 10 yaliyokuwa yanatoroshwa kutoka nchini kwenda nchi mbalimbali.

  Prof. Muhongo amewataka watanzania kutumia fursa mbalimbali zitakazotokana na utekelezaji wa miradi katika sekta ya gesi na mafuta ili kujiongezea kipato na kuiwezesha nchi kutimiza malengo yake kuelekea kuwa nchi ya uchumi wa kati.

  0 0


   Nahodha wa timu ya Super Girls Tatu Makota akipokea kombe la ubingwa wa michuano ya Airtel Rising Stars mkoa wa Lindi kutoka kwa Katibu Tawala wa wilaya ya Nachingwea Hadja Sekibo baada ya kuifunga VC Vito Malaika 4-1 katika fainali iliyochezwa kwenye uwanja wa Sokoine, Nachingwea.
   Katibu Tawala wa Wilaya ya Nachingwea Hadja Sekibo akikagua timu wakati wa fainali za michuano ya Airtel Rising Stars mkoa wa Lindi zilizofanyika kwenye uwanja wa Sokoine, Nachingwea. Super Girls ilishinda 4-1 dhidi ya VC Vito Malaika.
  Wachezaji wa timu ya Super Girls wakishangalia ubingwa wa michuano ya Airtel Rising Stars mkoa wa Lindi baada ya kuifunga VC Vito Malaika 4-1 katika fainali iliyochezwa kwenye uwanja wa Sokoine, Nachingwea.

  TIMU ya wasichana ya Super Girls imetwaa ubingwa wa michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars Mkoa wa Lindi baada ya kuichapa FC Vito Malaika 4-1 katika fainali iliyochezwa kwenye uwanja wa Sokoine mjini Nachingwea. Katika michuano hiyo, Mpiruka Queens iliweza kuibuka mshindi wa tatu baada ya kuifunga Kipara Queens 2-1.

  Katika mchezo wa fainali, Super Girls walianza kwa kasi na kuliandama lango la wapinzani wao tangu dakika za mwanzo lakini ilibidi kusuburi hadi dakika ya 15 ili kuandika goli la kwanza. Goli hilo lilofungwa kwa ustadi na mchezaji Ashura Mfaume baada kungongeana vizuri na Tatu Makota. 

  Baada ya bao hilo, Super Girls waliendelea kutandaza kandanda safi na kufanikiwa kufunga bao la pili dakika ya 18 lilifungwa tena na Ashura Mfaume baada ya kuwalamba chenga mabeki watatu wa FC Vito Malaika. Bao la tatu lilifungwa na Alia Fikiri mnamo dakika ya 22 baada ya mabeki wa FC Vito kushindwa kuokoa mpira wa kona.

  Timu ya FC Vito Malaika walipata bao lao pekee katika dakika ya 27 baada ya mchezaji Sarah Isaac kuachia shuti kali na mpira kujaa moja kwa moja wavuni. Hadi mapumziko, Super Girls 3 FC Vito Malaika 1.

  Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku kila timu ikasaka bao lakini ilikuwa ni Super Girls waliopata goli dakika ya 63 baada ya mchezaji Tatu Makota kufunga kwa penati baada ya beki wa FC Vito Malaika kunawa mpira kwenye eneo ya hatari.

   Akiongea kwenye fainali wa michuano hiyo,mgeni rasmi Hadja Sekibo ambaye ni Katibu Tawala wa mkoa wa Nachingwea aliwapongeza kampuni ya Airtel kwa kuwekeza kwenye soka la wanawake nchini. ‘Nachukua nafasi ya kuwapongeza wenzetu wa Airtel kwa kuona umuhimu wa kuwekeza kwenye soka vijana wetu sana sana kwa wasichana. 

  Tunatambua soka ni ajira, lakini kuwapa hawa vijana wetu wa kike nafasi ya kuonyesha vipaji vyao, mnawafungulia milango ya kuonekana nchini nzima na pia kunawafanya kutoweza kujiingiza kwenye makundi yenye malengo mabaya kwani muda wao wa ziada wanatumia kucheza mpira. Kwa hivyo wanapongeza kwa kuweza kuunga mkono jitihada za serikali za kuwawezesha vijana kujiajiri’, alisema Sekibo.

  Naye Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha Mpira wa Miguu mkoani Lindi Ally Mkadeba alisema michuano ya Airtel Rising Stars imewawezesha kupanua wingo wa kutafuta vipaji vya soka mkoani na kufikia maeneo mengi ambayo bila Airtel Rising Stars wasingeweza kufika. Mkadeba aliongeza kuwa wakati wa michuano hiyo, makocha waliweza kuchangua wachezaji 16 ambao hana uhakika kuwa watawakilisha vyema Mkoa wa Lindi kwenye fainali za michuano hiyo ambazo zitafanyika Dar es Salaam kuanzia Septemba 6-11.

  0 0

  Fundi wa TANESCO, akiwa kazini leo Septemba 3, 2016.
  Meneja Mwandamizi wa Usambazaji Umeme wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), ambaye pia ndiye Meneja wa Mradi wa kuimarisha miundombinu ya Umeme, Injinia Theodory Bayona.(katikati), akisimamia kazi hiyo leo Septemba 3, 2016.
  Kaimu Meneja Uhusiano wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), Leila Muhaji, akizungumza na waandishi wa habari kwenye eneo la mradi 

  NA K-VIS MEDIA/KHALFAN SAID
  WAHANDISI, na mafundi wa Shirika la Umeme Nchini Tanzania, (TANESCO), kwa kushirikia na wale wa kampuni za Kijapani za Yachiyo Engineering Co Limited, Takaoka na National Construction Co. Limited, wameanza kazi ya uboreshaji miundombinu ya umeme kwenye kituo kikubwa cha kupooza na kusambaza umeme cha Ubungo jijini Dar es Salaam, imeanza leo Septemba 3, 2016.

  Kazi kubwa inayofanyika hivi sasa ni kubadilisha laini kutoka umeme mdogo kwenda umeme mkubwa, lakini pia kubadilisha vifaa vingine muhimu ili kuwezesha usafirishaji umeme uweze kuwafikia watumiaji katika ubora ulio juu.

  “Ikumbukwe kwamba, hapa tulikuwa na laini mbili (waya mbili) zilizokuwa na uwezo wa kusafirisha umeme kiasi cha Megawati 120 kila moja, kutoka hapa Ubungo kwenda kituo cha Ilala, lakini kazi inayofanyika sasa, ni kubadili njia hizo (waya za umeme), ambazo zitakuwa na uwezo wa kupitisha kiasi cha umeme wenye Megawati 220 kila moja,” Alifafanua Meneja Muandamizi wa Usambazaji Umeme wa Shirika hilo, ambaye pia ndiye Meneja wa wa Mradi wa kuimarisha miundombinu ya Umeme, Injinia Theodory Bayona.

  Kwa mantiki hiyo, kazi inayofanyika leo hii itawezesha umeme utakaokuwa ukisafirishwa kutoka hapa Ubungo kwenda Ilala, kuwa na jumla ya Megawati 440 kwa laini zote mbili, tofauti na hapo awali ambapo uwezo wa kusafirisha umeme ulikuwa Megawati 240 tu,” Alisema.

  Kazi ikikamilika wakazi wa jiji la Dar es Salaam, watakuwa wakipata umeme wa uhakika, na ulio bora, alifafanua Injinia Bayona.

  Naye Kaimu Meneja Uhusiano wa Shirika la Umeme Nchini Tanzania, (TANESCO), Leila Muhaji, amewaomba wananchi kuwa wavumilivu katika kipindi hiki ambapo Shirika linafanya juhudi kubwa za kuwapatia umeme wa uhakika wananchi kwa kuimarisha miundombinu yake,.

  “Ili kuwawezesha mafundi wetu kufanya kazi katika mazingira salama, tutakuwa tukikata umeme kuanzia leo hii Septemba 3 na umeme utakuwa ukikatika kuanzia saa 2 asubuhi na kurejea saa 11 jioni kwa utaratibu na tarehe kama ifuatavyo; Septemba 3-4, Septemba 10-11, Septemba 17-18, na Septemba 24-25, 2016.” Alifafanua Leila, na kuwaomba wananc hi kuwa wavumilivu katika kipindi hiki.

  Mradi huu ulioanza Februari 2015 na unaotarajiwa kukamilika Juni 2017 unatekelezwa na Serikali kupitia TANESCO kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Japan (JICA) .
  Tsutomu Sato, wa kampuni ya Takaoka ya Japan, akiwa kazini
  Mafundi wa TANESCO, wakitayarisha nyaya hizo mpya
  Fundi wa TANESCO, akifunga kikombe wakati wa kazi ya kubadilisha miundombinu ya kusafirisha umeme kwenye kituo kikuu cha kupooza na kusambaza umeme cha Ubungo, jijini Dar es Salaam
  Raphael Mjata, Msimamizi Mkuu wa Njia Kuu za Umeme, akionyesha uwezo wa kituo cha Ubungo cha kupooza umeme wenye kilovolti 132.
  Mafundi wa TANESCO na kampuni ya National Construction Company Limited, wakivuta nyaya hizo mpya
  Hizi ndio nyaya zitakazofungwa kwenye laini mbili za kusafirisha umeme kutoka kituo cha kupooza na kusafirisha umeme cha Ubungo.
  Mhandisi Bayona, akielezea waandishi wa habari mwenendo wa kazi hiyo
  Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO makao makuu, Leila Muhaji, na Afisa Uhusiano wa Shirika hilo, Henry Kilasila, wakiwa kazini.
  Mhandisi Bayona (kulia), akijadiliana jambo na Wahandisi wenzake, Yasutaka Osawa, (kushoto), ambaye ni mwakilishi katika mradi wa kuboresha umeme jiji la Dar es Salaam, kutoka kampuni ya Takaoka Engineering Co Ltd, na Mhandisi Ahmed Mmingwa, ambaye ni Msimamizi wa Mradi kutoka TANESCO.
   Mwakilishi wa kampuni ya Kijapani ya Yachiyo Engineering Co. Limited, Tamai Masayuki,akizungumza na waandishi wa habari kuhsuu maendeleo ya uboreshaji huo


  Wahandisi wakijadiliana jambo
  Fundi wa TANESCO akiwa kazini.
  Kazi inaendelea 
  Meneja Mwandamizi wa Usambazaji Umeme wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), ambaye pia ndiye Meneja wa Mradi wa kuimarisha miundombinu ya Umeme, Injinia Theodory Bayona.(katikati), Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Leila Muhaji, (kulia) na Afisa Habari wa Shirika hilo makao makuu, Henry Kilasila, (wakwanza kushoto) na waandishi wa habari, wakitembelea eneo la mradi mapema leo asubuhi Septemba 3, 2016 ambapo kazi ilianza kwa kasi 
  Wafanyakazi wa TANESCO chumba cha ufuatiliaji mwenendo wa umeme (control room) wakiwa akzini.
  Chumba cha kufutialia mwenendo wa umeme jijini Dar es Salaam, (Control room), cha TANESCO-Ubungo sub station)

  0 0


   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Joseph Pombe Magufuli akiweka shada la maua kwenye kaburi la Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume katika ofisi Kuu ya CCM Makao Kisiwandui mjini Zanzibar leo Agosti 3, 2016.
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Joseph Pombe Magufuli akitoa heshima zake baada ya akiweka shada la maua kwenye kaburi la Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume katika ofisi Kuu ya CCM Makao Kisiwandui mjini Zanzibar leo Agosti 3, 2016.
   Mama Janeth Magufuli, Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Joseph Pombe Magufuli,  akiweka shada la maua kwenye kaburi la Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume katika ofisi Kuu ya CCM Makao Kisiwandui mjini Zanzibar leo Agosti 3, 2016.
   Mama Janeth Magufuli, Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Joseph Pombe Magufuli,  akitoa heshima baada ya kuweka shada la maua kwenye kaburi la Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume katika ofisi Kuu ya CCM Makao Kisiwandui mjini Zanzibar leo Agosti 3, 2016.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Joseph Pombe Magufuli,  na viongozi wengine wakiomba dua bada ya kuweka shada la maua kwenye kaburi la Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume katika ofisi Kuu ya CCM Makao Kisiwandui mjini Zanzibar leo Agosti 3, 2016.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Joseph Pombe Magufuli,  na viongozi wengine wakiomba dua bada ya kuweka shada la maua kwenye kaburi la Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume katika ofisi Kuu ya CCM Makao Kisiwandui mjini Zanzibar leo Agosti 3, 2016.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Joseph Pombe Magufuli,  akiwa na Mama Fatma Karume baada ya kuweka shada la maua kwenye kaburi la Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume katika ofisi Kuu ya CCM Makao Kisiwandui mjini Zanzibar leo Agosti 3, 2016.

  PICHA NA IKULU
   ais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Joseph Pombe Magufuli,  akiwa na Mama Fatma Karume baada ya kuweka shada la maua kwenye kaburi la Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume katika ofisi Kuu ya CCM Makao Kisiwandui mjini Zanzibar leo Agosti 3, 2016.

  PICHA NA IKULU
  ais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Joseph Pombe Magufuli,  akiwa na Mama Fatma Karume baada ya kuweka shada la maua kwenye kaburi la Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume katika ofisi Kuu ya CCM Makao Kisiwandui mjini Zanzibar leo Agosti 3, 2016.

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Joseph Pombe Magufuli akitoka katika ofisi Kuu ya CCM Makao Kisiwandui mjini Zanzibar leo Agosti 3, 2016 baada ya kuweka saini kitabu cha wageni kabla ya kuzuru na kuweka shada la maua kwenye kaburi la Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume.
  PICHA NA IKULU

older | 1 | .... | 959 | 960 | (Page 961) | 962 | 963 | .... | 1897 | newer