Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live

Mwanadiplomasia: Hakuna sababu ya maandamano

$
0
0
Na Beatrice Lyimo-MAELEZO

Dar es salaam

Tofauti za kisiasa zilizopo nchini zisivuruge nuru ya amani iliyojengwa tangu enzi za Serikali ya Awamu ya Kwanza ambapo siasa za nchi zililenga katika umoja, amani na ujenzi wa Taifa imara, anaonyesha mmoja wa walimu wa diplomasia nchini.

Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Mkuu wa Chuo cha Diplomasia nchini (CFR), Dkt. Bernard Achiula wakati wa mahojiano na Mwandishi wa habari hii kuhusu hali ya siasa nchini kwa sasa na ushiriki wa watanzania kwa ujumla katika kuiunga mkono Serikali ya Awamu ya Tano katika utatuzi wa changamoto za kimaendeleo badala ya kuanzisha tabia za vurugu na maandamano.

Dkt. Achiula amesema kuwa uwepo wa amani nchini unachangia katika kuvutia wawekezaji  nchini, kukuza utalii wa ndani, kuvutia wahisani kutoa misaada kwa kuchangia katika uanzishaji na uendelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo hivyo kila raia nchini bila kujali itikadi yake ya dini wala chama ana budi kuilinda amani iliyopo.

“Tofauti za kisiasa zipo katika kila nchi kulingana na mitazamo tofauti iliyopo ila kinachotakiwa ni kuweka taifa mbele kwa manufaa ya nchi, watanzania tunatakiwa kuwa wazalendo ili kuimarisha umoja na amani iliyopo kwani vitu hivi vinategemeana na hatimaye kuiwezesha Serikali ya awamu ya tano kuwatumikia wananchi kwa kuwaletea maendeleo.

“Tofauti hizo zisiwe chachu ya kuvuruga amani tuliyonayo bali watanzania kwa ujumla tunatakiwa kuitunza amani hii iliyojengwa tangu enzi za Mwalimu Julius Nyerere ili kuweza kuvutia wawekezaji na  utalii katika nchi yetu” alifafanua Dkt Achiula.

Alisema kuwa haoni sababu kwa vyama vya siasa nchini kuandaa maandamano yanayolenga kuvuruga amani iliyopo kwani kikubwa kinachotakiwa kwa wananchi ni misingi mikuu ya maendeleo ikiwemo elimu, afya na huduma bora mbalimbali  ambapo Rais Magufuli ameanza kuvifanyiakazi. 

Akizungumza kuhusu Balozi zetu nje ya nchi Dkt Achiula aliwashauri mabalozi hao kuzidi kuitanganza nchi yetu ya Tanzania ili kuweza kuvutia wawekezaji, utalii na biashara ili kusaidia katika ukuuaji wa sekta ya viwanda ambapo Serikali ya Awamu ya Tano imejipanga kuipeleka nchi katika uchumi wa viwanda.

Akizungumzia utendaji wa Serikali ya Awamu ya Tano Dkt Achiula amesema kuwa Rais Dkt. Magufuli amejikita katika kutatua changamoto zinazolikabili taifa kwa muda mrefu ikiwemo kupiga vita rushwa, kuongeza ukusanyaji mapato kwa kuwabana wakwepa kodi, kubana matumizi ikiwa nia ni kuimarisha uchumi wa nchi na kuipeleka nchi kwenye uchumi wa Kati.

VIJUSO VYA BAADHI YA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI AGOSTI 28

DC MTATURU AWATAKA WANANCHI WALIOVAMIA ENEO LA HIFADHI KUHAMA NDANI YA MWEZI MMOJA

$
0
0
Baadhi ya wananchi wakimsikiliza kwa Makini Mkuu wa Wilaya ya ikungi.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi mhe Miraji Jumanne Mtaturu akisikiliza Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Kaugere Beatus Kapatya akitoa taarifa juu ya kusimama kwa ujenzi wa Zahanati hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi mhe Miraji Jumanne Mtaturu akimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa Kijiji cha Kaugeri wakati akitoa maelezo wakati wa kikao cha serikali ya kijiji.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi mhe Miraji Jumanne Mtaturu akitoa ufafanuzi wa mambo mbalimbali wakati wa ziara yake Wilayani humo
Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Kaugere Beatus Kapatya akitoa ufafanuzi mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu
Umakini wa wananchi ukiwa umetawala wakati wa Mkutano wa Kijiji, Wilayani ikungi

Na Mathias Canal, Singida

Serikali ilitangaza eneo la Hifadhi ya msitu wa wananchi waliomo ndani mwaka 2003 ambao kutangazwa huko kuliashiria wananchi kuhama katika maeneo hayo ili kutoa fursa kwa serikali kusimamia kwa karibu eneo hilo lakini wananchi hao mpaka sasa hawajahama kwa kukaidi agizo hilo.

Jambo hili limemsukuma Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu kufanya ziara na kuzungumza na wananchi wa maeneo hayo kwa lengo la kuwaelemisha juu ya uvunjaji sheria za nchi kwa kuendelea kusalia katika maeneo ambao wametakiwa kuhama jambo ambalo kama watashindwa kulitekeleza serikali itawatoa kwa nguvu kwani kwa kiasi kikubwa wanaharibu mazingira.

Akizungumza na Wananchi hao katika Kijiji cha Kaugeri Kata ya Mwaru Wilayani hapa Dc Mtaturu ametoa mwezi mmoja kwa wananchi hao kuhama haraka iwezekanavyo ili kupisha eneo hilo la Hifadhi ya msitu kufanya Kazi iliyokusudiwa kwa zaidi ya miaka kumi sasa.

Mtaturu amesema kuwa Kwa mujibu wa sheria Kijiji kinapaswa kutoa Ardhi hekari zisizozidi hamsini kwa mwekezaji lakini uongozi wa Kijiji hicho umegawa kwa mwekezaji hekta 150 hadi 200 kinyume kabisa na taratibu za kiutendaji ukiwa ni pamoja na kuingia mikataba ya kinyonyaji.

Pamoja na hayo pia viongozi hao wametoa Ardhi hiyo bila kushirikisha wananchi jambo ambalo limeibua hisia Kali kwa wananchi ambao wanatambua uporwaji huo wa maeneo yao.

Kufuatia kadhia hiyo ya viongozi hao kugawaji Ardhi kinyume na taratibu Dc Mtaturu amewaweka lumande Mwenyekiti wa Kijiji cha Kaugeri Mange Nkuba, Aliyekuwa Kaimu Afisa Mtendaji Laurent Bomba, na mjumbe wa serikali ya Kijiji Paul Kilo huku Amani Clement ambaye alitoweka kabla Ya mkutano kumalizika anaendelea kutafutwa mpaka apatikane.

Katika hatua nyingine Dc Mtaturu ameagiza mkandarasi Samwel John kukamatwa na kuhojiwa kwa kushindwa kukamilisha ujenzi wa zahanati ya kijiji tangu Mwaka 2013 ambapo tayari alishapewa kitita cha shilingi milioni 19 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi huo.

Hata hivyo pamoja na mkandarasi kukabidhiwa fedha hizo alianza ujenzi lakini jengo hilo halijafika hata kwenye Renta huku likiwa limejengwa chini kiwango.

Sambamba na hayo pia Mkuu huyo wa Wilaya ya Ikungi amemuagiza mkurugenzi wa Halamashauri ya Wilaya hiyo kupitia idara ya ujenzi kutoa taarifa kwanini hawakushiriki kutoa huduma za kiutaalamu katika kusimamia jengo hilo la umma kabla na wakati ujenzi unaanza.

MBUNGE WA ILEJE JANET MBENE AKABIDHI VIFAA VYA KAZI KWA JESHI A POLISI WILAYA YA ILEJE

$
0
0

Mbunge wa Ileje Mh Janet Mbeneakipokea Risala kutoka kwa Ocd Wilaya Ileje
Mbunge wa Ileje Mh Janet Mbene, akikabidhi Laptop kwa OCD wa Wilaya ya Ileje kw ajaili ya kusaidia kazi katika Wilaya hiyo
Mbunge wa Ieje , Mh Janet Mbene, akikabidhi Matairi kwa Katibu wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Ileje Hamida Mbogo
Mbunge wa Ileje Mh Janet Mbene akipokea mkono wa shukrani kwa Mkuu wa Wilaya ya Ileje Joseph Mkude mara baada ya kukabidhi laptop, Photocopy Mashine, Matairi na lim tano.

KIFAHAMU KIPINDI KIPYA CHA 'CHUKUA HATUA' KINACHOHUSU VIJANA MKOANI DODOMA

$
0
0
Watangazaji wa kipindi kipya cha CHUKUA HATUA Happy Balisidya na Mohammed Hammie, siku ya kwanza walipokutana wakati wa maandalizi ya kutengeneza kipindi hicho.


Chukua Hatua ni kipindi kipya cha radio kitakachowashirikisha vijana, wakizungumza na kujadili kwa pamoja masuala yanayowahusu hasa ya kujikwamua na maendeleo mkoani Dodoma na maeneo jirani.

Hiki ni kipindi ambacho kinatarajiwa kujadili kwa kina changamoto za ajira kwa vijana kupata mwelekeo wa maendeleo kwa vijana wa kike na kiume.

Lengo kuu la kipindi hiki ni kutoa taarifa muhimu ambazo zitasaidia vijana kuondokana na ukosefu wa ajira na changamoto wanazokutana nazo katika mihangaiko yao, kipindi kitapaza sauti za vijana ambazo hazikupata nafasi ya kusikika hapo kabla.

Si kipindi tu, bali pia ni jukwaa kwa ajili ya kubadilishana ujuzi, mawazo, uzoefu na pia kujifunza kutoka kwa wengine, ni mahala pekee ambapo kijana atayaona matarajio na uzoefu kutoka fani na taaluma mbalimbali.

Kipindi pia kinatarajiwa kuimarisha ujuzi na kuelekeza upya akili za vijana kufanya kazi na kuchangamkia fursa za ajira kwa ujasiriamali, kujiajiri na kuukwepa umaskini uliokithiri miongoni mwao.

Kipindi kitaanza kuruka hewani siku ya Alhamisi ya tarehe 01/09/2016 kupitia kituo cha RASI FM RADIO inayopatika masafa ya 103.7 Dodoma.

Pia kipindi kitakuwa kinapatikana kupitia mtandao wa Youtube ukurasa wa CHUKUA HATUA, pia mijadala itakuwa inaendelea kupitia ukurasa wetu wa facebook ambao ni CHUKUA HATUA, Instagram ni KIJANA CHUKUA HATUA, na Twitter ni CHUKUA HATUA1

PEACOCK HOTEL YAZINDUA RASMI MTANDAO WAKE WA KIJAMII UNAOLENGA KUTANGAZA CHAKULA CHA ASILI CHA MTANZANIA.

$
0
0

Mmoja kati ya Wakurugenzi wa Peacock Hotel,Daniel Mfugale akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya uzinduazi wa mtanao wa kijaamii unaolenga kutangaza chakula cha asili cha Mtanzania leo jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya wafanyakazi wa hotel hiyo waliofika kwenye uzinduzi huo leo jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii).

Uongozi wa Peacock Hotel umezindua rasmi mtandao wake wa kijaamii unaolenga kutangaza chakula cha asili cha Mtanzania.

Mmoja kati ya Wakurugenzi wa Hotel hiyo Daniel Mfugale alisema kuwa uamuzi huo umefanyika baada ya kuona mitandao ya kijamii sasa inasambaza taarifa haraka na kuwafikia watu wengi nje na nchi hivyo itasaidia kuongeza utalii Nchini.

“Kwa sasa mitandao ya kijamii ndiyo imeshika hatamu kwa usambazaji wa taarifa hivyo huduma yetu iitwayo Usiku wa Mtanzania ambayo ni maalumu kwa chakula cha asili cha makabila yote nchini itakua inatangazwa katika kurasa zetu za facebook na Instagram tulizozifungua leo”, alisema Mfugale.

WAZIRI MKUU: SEKTA BINAFSI NI MUHIMU KTK UJENZI WA UCHUMI

$
0
0
*Shinzo Abe aahidi $ bilioni 10 kwa miaka mitatu

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema mabadiliko ya mifumo ya ujenzi wa uchumi wa viwanda hayawezi kuletwa na Serikali peke yake bali ni lazima yahusishe pia wadau kutoka sekta binafsi.

“Tunahitaji kushirikiana na sekta binafsi ili tuweze kufanikisha ajenda zetu za maendeleo ziwe za kitaifa, kikanda au za bara zima la Afrika. Ushirikiano huu utasaidia kuleta mabadiliko dhahiri ya kiuchumi na kukuza ustawi wa jamii zetu,” alisema.

Ametoa kauli hiyo jana (Jumamosi, Agosti 27, 2016) wakati akichangia mjadala kuhusu TICAD na umuhimu wake kwa maendeleo ya Afrika mara baada ya ufunguzi wa Mkutano wa Sita wa Kimataifa wa Tokyo kuhusu Maendeleo ya Bara la Afrika (TICAD VI) uliofanyika katika kituo cha Mikutano ya Kimataifa cha Jomo Kenyatta (JICC) jijini Nairobi, Kenya.

“Wakati Serikali zinaweka mazingira wezeshi ya kufanya biashara na uwekezaji, jukumu kubwa la sekta binafsi ni kuleta mageuzi ya kiuchumi na kujenga uchumi wa viwanda ambao ndio tunakusudia kuufikia,” alisema.

Waziri Mkuu ambaye anahudhuria mkutano huo wa siku mbili kwa niaba ya Rais, Dk. John Pombe Magufuli, alisema Tanzania inawakaribisha wawekezaji wa sekta binafsi kutoka Japan waje kujenga viwanda vya kusindika gesi asilia, kutengeneza mbolea na kemikali mbalimbali, vyuma, nguo, bidhaa za ngozi na usindikaji wa mazao.

Alisema ili kufikia uchumi wa viwanda na maendeleo endelevu, ni lazima nchi za Afrika na wabia wa TICAD wawekeze kwa pamoja na washirikiane kujenga uwezo wa rasilimali watu, kwa kuwa ndio nguzo muhimu ya kuleta ushindani wenye tija katika sekta ya viwanda.

Akizungumzia mpango wa mafunzo kwa vijana wa Kiafrika katika masuala ya biashara (African Business Education Initiative for Youth–ABE), Waziri Mkuu alisema: “Huwezi kuzungumzia mabadiliko ya mfumo wa uchumi wa viwanda bila kujenga uwezo wa watu wetu ambao hasa ndiyo watekelezaji wa mabadiliko hayo. Ni lazima pia tuangalie vipaumbele vya kidemografia kama kweli tunataka kukuza uchumi kwa kujenga tabaka la watu wenye ujuzi.”

Mapema, Waziri Mkuu wa Japan, Bw. Shinzo Abe aliwaahidi viongozi wa nchi za Afrika kwamba nchi yake itatoa kiasi cha dola za marekani bilioni 10 katika kipindi cha miaka mitatu kwa ajili ya kuendeleza miundombinu barani humo na kwamba sehemu ya fedha hizo itatolewa kwa kushirikiana na Benki ya Benki ya Maendeleo ya Afrika (AFDB).

“Ahadi hii ina nia ya kuendeleza miundombinu ya barabara, bandari na nishati jadidifu hasa ya nishati ya jotoardhi kwani bara hili lina uwezo mkubwa wa kuzalisha nishati hiyo kwa wingi,” alisema.

“Uzalishaji wa umeme barani Afrika, unatarajiwa kuongezeka kwa kiwango cha megawati 2,000. Nishati ya jotoardhi itaboreshwa kwa kutumia yeknolojia za Kiajapan. Na kutokana na mradi huo, utazalishwa umeme wa kutosha kuhudumia nyumba zaidi ya milioni tatu ifikapo mwaka 2022,” alisema.

Hii ni mara ya kwanza kwa mkutano wa TICAD kufanyika barani Afrika tangu mikutano hii ianze mwaka 1993. Mkutano huo, unahudhuriwa na washiriki zaidi ya 6,000 kutoka bara la Afrika na Japan.

Mkutano huo uliofunguliwa kwa pamoja na Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta na Waziri Mkuu wa Japan, Shinzo Abe, umehudhuriwa na marais 34 kutoka nchi za Afrika, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bw. Ban Ki-Moon na Marais wa Benki ya Dunia na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AFDB).


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAPILI, AGOSTI 28, 2016.

UZINDUZI WA DKT.AMON MKOGA FOUNDATION SOUTHERN SUN HOTEL TAREHE 25/8/2016

$
0
0

Mwenyekiti wa Dr.Amon Mkoga Foundation na Bw.Habibu Msammy(Mwenye miwani)mwakilishi wa Katibu mkuu wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo pembeni ni Bw.Basel Haydar Meneja wa shirika la Ndege la Qatar nchini Tanzania ambao ni wadhamini wa kuu wa mradi wa madawati uitwao Simama kaa desk campaign ambao unaendeshwa na Taasisi hiyo.

Mradi huo mwenye lengo la kupunguza uhaba wa madawati unadhaminiwa pia na Halotel,Empress Furniture,TIRA,CBA Bank,Insignia,tayari mikoa ya Tabora na Pwani wameanza kufaidi matunda ya mradi huo.

DC IKUNGI AWASWEKA RUMANDE VIONGOZI WANNE WA KIJIJI CHA KAUGERI

$
0
0
 
 Mkuu wa wilaya Ikungi, Miraji Mtaturu, akikagua ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Kaugeri wilayani humo ambayo mkandarasi ametoweka bila kukamilisha ujenzi.

MKUU wa wilaya ya Ikungi mkoani Singida, Miraji Mtaturu, ameamuru kuwekwa ndani kwa viongozi wanne wa kijiji cha Kaugeri kilichopo katika wilaya hiyo kwa kosa la kuuza ardhi bila ya kufuata kanuni na taratibu zilizopo.

Aidha ameagiza kutafutwa mkandarasi Samweli John na kuwekwa rumande kutokana na kutokamilisha ujenzi wa Zahanati ya kijiji hicho wakati alishalipwa shilingi milioni 19.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara kijijini hapo, Mtaturu amesema watendaji hao wamegawa ardhi kwa mwekezaji zaidi ya hekta 150 na kuingia mikataba ya kiunyonyaji wakati kisheria kijiji hakitakiwi kutoa ardhi zaidi ya hekta 50 hivyo wamewekwa ndani mpaka jumatatu ili wahojiwe na kutoa maelezo na hatimaye maamuzi yafuate.

Amewataja waliosekwa rumande kuwa ni mwenyekiti wa kijiji cha Kaugeri Mange Nkuba, ,aliyekuwa kaimu mtendaji wa kijiji, Laurent Komba, na wajumbe wawili wa serikali ya kijiji, Paul Kilo na Aman Clement ambaye anaendelea kutafutwa baada ya kutoroka kabla ya mkutano kufanyika.

Kuhusu ujenzi wa Zahanati hiyo ya Kijiji hicho, Mtaturu amesema mkandarasi huyo alitoweka toka mwaka 2013 na hivyo kufanya ujenzi huo kusimama wakati fedha alishachukua.

Kadhalika, ametoa muda wa mwezi mmoja kwa wananchi walio katika eneo la msitu uliotangazwa kuwa hifadhi toka mwaka 2003 kuondoka wenyewe katika eneo hilo kabla hawajatolewa kwa nguvu kutokana na kuharibu mazingira.

Amewaasa wananchi kushirikiana kwa pamoja katika kutii maelekezo na maagizo yanayotolewa na serikali ili kuifanya Ikungi isonge mbele kimaendeleo.

USIKOSE KUTAZAMA KIPINDI CHA 'TUNATEKELEZA'

NAIBU WAZIRI JAFO AFANYA ZIARA YA SIKU MBILI MKOA WA SHINYANGA NA GEITA

$
0
0

Naibu waziri Ofisi ya rais, Tamisemi, Selemani Jafo, akizungumza na wananchi nje ya kiwanda cha kukamulia alizeti mjini Chato.
Naibu waziri Ofisi ya rais, Tamisemi, Selemani Jafo, akikagua mashine za kukamulia mafuta ya alizeti mjini Chato.
Mkurugenzi wa mji wa Kahama, Andason Msumba akitoa maelezo kwa Naibu waziri Ofisi ya rais, Tamisemi, Selemani Jafo kuhusu mgogoro wa soko wanalolitaka wananchi kutumika kwa maslahi ya wananchi wa mji huo. 
Naibu waziri Ofisi ya rais, Tamisemi, Selemani Jafo, akikagua mradi wa maji kijiji cha Chankorongo wilayani Geita uliohujumiwa na watendaji na kumuagiza Katibu tawala wa mkoa wa Geita kuunda timu ya uchunguzi.

Naibu waziri Ofisi ya rais, Tamisemi, Selemani Jafo, akiwa katika harambe ya kuchangia madawati mkoani Geita, kulia kwake ni Mkuu wa mkoa huo Meja jenerali mstaafu Ezekiel Kiunga pamoja na Mwenyekiti wa harambee hiyo, Ignas Inyasi.
Naibu waziri Ofisi ya rais, Tamisemi, Selemani Jafo, akizungumza katika harambe ya kuchangia madawati mkoani Geita, ambayo alikuwa akimwakilisha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
NAIBU Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za mikoa na serikali za mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo amefanya ziara ya Siku mbili katika mikoa ya Shinyanga na Geita na kukagua miradi mbalimbali.

Akiwa Mkoani Shinyanga, Jafo alitembelea Hospitali ya Wilaya ya Kahama ambapo alijionea changamoto mbali mbali ikiwepo ya Jengo dogo linalotumiwa na kinamama wakati wakujifungua kutokana na hospitali hiyo kuzidiwa uwezo.

Kufuatia hali hiyo, Jafo amemuagiza Injinia wa Wilaya kuhakikisha wanaharakisha ujenzi wa Jengo kubwa la kisasa la kinamama kwani fedha zipo za Ujenzi huo ili wagonjwa wasiendelee kupata mateso kwa michakato ya Ujenzi mirefu isiyo na tija.

Kadhalika, akiwa wilayani Kahama, Naibu Waziri Jafo ametembelea Mradi wa Soko na kumuagiza Mkurugenzi wa Wilaya, Andason Msumba, kuhakikisha anakaa na timu yake ya Wataalamu ili kutatua mgogoro wa Soko hilo kwa Maslahi mapana ya wananchi wa Mji wa Kahama.

Amehitimisha Ziara yake mkoani Shinyanga kwa kuzungumza na Watumishi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama na Halmashauri ya Msalala ambapo amewataka Watumishi kufanya kazi kwa kujituma huku wakiepuka Uzembe kazini,upendeleo, kupigana majungu, na kuchukiana.

Katika mkoa wa Geita, Jafo amekagua mradi wa Maji na Kiwanda cha kukamua mafuta ya Alizeti wilayani Chato huku akimuagiza Mhandisi wa Maji wa Wilaya hiyo kuhakikisha mradi unakamilika mapema kabla ya Mwezi wa 10 ili kuweza kusaidia kutatua changamoto ya Maji.

Amesema wananchi hawawezi kuwa na Upungufu wa Maji wakati kuna maji mengi ya Ziwa Victoria. Akikagua Mradi wa kiwanda cha kukamua Mafuta ya Alizeti, Jafo alimwagiza Mkurugenzi kuhakikisha anashirikiana na Sido ili kuweza kuukamilisha mradi huo haraka.

Akiwa njiani kuelekea Geita mjini, Jafo alipita Jimbo la Busanda wilaya ya Geita Vijijini na Kukagua Mradi wa Maji uliokamilika Kijijini Makondeko kisha Safari ikaelekea Kijiji cha Chankorongo ambapo kuna Mradi wa Maji wa muda mrefu usio kamilika ambapo mpaka sasa umetumia zaidi ya Bilioni moja na dalili za kukamilika bado.

Kufuatia hali hiyo, Naibu Waziri huyo amemwagiza Katibu tawala wa Mkoa wa Geita Selestine Gesimba kuunda tume maalum ya kuchunguza sakata la mradi huo wa maji wa Chankorongo ambapo wamepewa mwezi mmoja kukamilisha uchunguzi huo.

Alimwagiza Katibu Tawala Mkoa akishirikiana na Wakurugenzi wote kuhakikisha suara la Oprass linapewa kipaumbele kwa watumishi na linafanyika kwa wakati na ipasavyo. Naibu Waziri aliwahakikishia watumishi kuwa serikali inafuatilia changamoto mbalimbali zinazowakabili na kuwataka wawe na Subra.


Wakati huo huo, akiwa Mkoani Geita Jafo alimwakilisha Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa katika Harambee ya ya kuchangia Madawati.

Katika harambe hiyo Jafo alihamasisha na kuweza kukusanywa kiasi cha Shilingi Bilioni Moja, mia saba arobaini Milioni , laki tano na elfu tisini na saba (1,740,597,000) Kiasi ambacho kilimfanya Mkuu wa Mkoa huo Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga kumshukuru sana Naibu waziri huyo kwani hakutegemea kiasi hicho kikubwa cha Fedha kuweza kupatikana.

MATUKIO YA MKUTANO WA WAFANYABIASHARA KIGOMA NA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO

$
0
0
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (kushoto) akimsikiliza kwa makini Bi. Rehema Kabuye (katikati) aliyekua akilia kwa uchungu, akimsihi Waziri huyo wa Fedha na Mipango, amsaidie ili mume wake ambaye ni Nahodha wa meli ya MV Liemba pamoja na wafanyakazi wengine wa Mamlaka ya Huduma za meli mkoani Kigoma, walipwe mishahara yao ya miezi nane ili kuwaondolea adha ya maisha inayowakabili wao na familia zao
Bi. Rehema Kabuye, (Katikati) ambaye ni mke wa Nahodha wa Meli ya Mv Liemba, inayotoa huduma zake Ziwa Tanganyika, akimwonesha Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), picha za mtoto wake ambaye ana matatizo ya kiafya, akimsihi Waziri huyo amsaidie yeye pamoja na wenzake ili waume zao walipwe mishahara yao ya miezi 8 wanayomdai mwajiri wao, Mamlaka ya Huduma za Meli mkoani Kigoma.
Katibu wa Waziri wa Fedha na Mipango, Edwin Makamba (Kulia), akichukua maelezo ya kina kutoka kwa Bi. Rehema Kabuye, Mkazi wa Kigoma, ambaye amemwomba Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), aingilie kati sakata la waume zao wanaofanya kazi kwenye mamlaka ya huduma za meli mkoani Kigoma, ambao hawajalipwa mishahara yao kwa muda mrefu.
Baadhi ya wafanyabiasha wa Kigoma Mjini, wakimsikiliza kwa makini waziri wa fedha na Mipango, Mhe. Dkt Philip Mpango (Mb) (hayupo pichani), wakati wa mkutano na Waziri huyo kuhusu masuala mbalimbali ya biashara na ulipaji kodi, mkutano uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa NSSF, mjini Kigoma.
Baadhi ya wafanyabiasha wa Kigoma Mjini, wakimsikiliza kwa makini waziri wa fedha na Mipango, Mhe. Dkt Philip Mpango (Mb), wakati wa mkutano na Waziri huyo kuhusu masuala mbalimbali ya biashara na ulipaji kodi, mkutano uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa NSSF, mjini Kigoma.

Baadhi ya maofisa wa Wizara ya Fedha na Mipango, wakifuatilia kwa makini hotuba ya Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), wakati wa mkutano wake na wafanyabiashara wa Kigoma Mjini, mkutano uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa NSSF, mjini Kigoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), aliyesimama kushoto, akiwahutubia wafanyabiasha wa Kigoma Mjini, kuhusu masuala mbalimbali ya biashara na ulipaji kodi, mkutano uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa NSSF, mjini Kigoma.
Katibu wa Jumuiya ya Wafanyabiashara mkoa wa Kigoma Bw. Raymond Ndabiyegetse (katikati) akichangia hoja katika kikao na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (hayupo pichani) ambaye alipongeza juhudi zinazofanya na Serikali katika kutengeneza mazingira mazuri ya biashara zao.
Mkurugenzi wa kampuni ya Aifola ya Mjini Kigoma, Bw. Zubery Mabie, akiongea kwa hisia kali akishutumu TRA na maafisa wengine wa serikali katika kituo kidogo cha Forodha cha Manyovu kilichoko mpakani mwa Tanzania na Burundi, kujihusisha na rushwa kwa kupitisha maroli yakiwa na mizigo, ikiwemo chokaa anayozalisha, bila kulipia kodi. Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), ameahidi kulifanyiakazi suala hilo.
Mmoja wa wafanyabiashara wa Mjini Kigoma akichangia hoja katika mkutano ulioitishwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), kuhimiza ulipaji kodi, matumizi adili ya fedha za umma, matumizi ya Mashine za Kieletroniki na utoaji wa risiti, mkutano uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa NSSF, mjini Kigoma.

Askofu Mstaafu wa Kanisa la Anglican, Dkt. Gerard Mpango, akitoa mchango wake wa mawazo ambapo ameitaka serikali kutoa elimu ya kutosha ya biashara na ujasiriamali kwa wafanyabiashara nchini ili waweze kutumia fursa zilizopo katika soko la Afrika Mashariki, kukuza mitaji na biashara zao, wakati wa mkutano wa wafanyabiashara na Waziri wa fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), hayupo pichani, uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa NSSF, mjini Kigoma

Kamisha Msaidizi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, anayeshughulikia masuala ya kodi, Bw. Shogholo Msangi akifafanua kuhusu kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwa wafanyabiashara wa Kigoma Mjini wakati wa mkutano na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (mb).
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dokta Philip Mpango (Mb), akizungumza na wafanyabiashara wa Kigoma Mjini, kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo umuhimu wa kulipa kodi na matumizi ya mashine za kieletroniki pamoja na kuwasisitizia kutoa risiti kwa wateja wao. kushoto kwake ni Kamishna Msaidizi anayeshughulikia masuala ya kodi, Wizara ya Fedha na Mipango, Shogholo Msangi, mkutano uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa NSSF, mjini Kigoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), akionesha rundo la makaratasi yaliyoandikwa hoja na kero mbalimbali za wafanyabiashara wa mjini Kigoma, wakati wa mkutano kati yake na wafanyabiashara hao, uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa NSSF, mjini Kigoma
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Askofu Dkt. Gerard Mpango, baada ya kumalizika kwa mkutano wake na wafanyabiashara wa Mkoa wa Mjini Kigoma, uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa NSSF, mjini Kigoma.

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (kushoto) akifurahia jambo pamoja na Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini, Mhe. Zitto Kabwe, wakati wakitoka nje ya ukumbi wa mikutano wa NSSF, ulipofanyika mkutano kati ya Waziri wa Fedha na Mipango na wafanyabiashara wa mjini Kigoma.


Mbunge wa Kigoma Mjini, Mhe. Zitto Kabwe (kushoto), akisisitiza jambo wakati akizungumza na Waziri wa Fedha na Mipango,Dkt. Philip Mpango (Mb), baada ya kumalizika kwa mkutano kati yake na wafanyabiashara wa mjini Kigoma, uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa NSSF, mjini Kigoma.




Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), (kushoto) akipeana mkono na Mbunge wa Kigoma Mjini Mhe. Zitto Kabwe, mara baada ya kumalizika kwa mkutano kati ya Waziri huyo na wafanyabiashara wa Mkoa wa Kigoma uliofanyika katika ukumbi wa NSSF, mjini Kigoma.

Watanzania waaswa kuhifadhi lugha za asili ili kuongeza misamiati ya Kiswahili.

$
0
0

Na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Dar es Salaam 

Serikali inathamini jitihada za wadau katika kuhifadhi, kutunza na kusambaza lugha za makabila mbalimbali nchini ambazo ndio msingi wa lugha aushi ya Kiswahili ambayo ni lugha ya taifa. 

Hayo yamesemwa mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam na Mhariri Mkuu wa Bazara la Kiswahili la Taifa (BAKITA) Richard Mtambi alipokuwa akisoma hotuba ya Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel wakati wa uzinduzi wa kitabu cha Historian a Mila za Kabila la Wasukuma, Wasilanga wa Nasa wa mkoani Simiyu. 

Akisoma hotuba ya Katibu Mkuu huyo, Mtambi alisema kuwa mwandishi wa kitabu hicho pamoja na ushirikiano wa Wasilanga wa Nasa wameongeza hazina kubwa kwa taifa ya kukusanya, kuhifaadhi na kusambaza mila na desturi za moja ya makabila zaidi ya 120 ya Tanzania. 

Katika hotuba hiyo, Profesa Gabriel amewaasa makabila mengine nchini waige mfano wa Wasukuma wa Nasa wa kutunza na kuhifadhi mila na desturi zao kwa manufaa ya taifa ili kuhakikisha utamaduni wa Mtanzania unatunzwa, kuhifadhiwa na kuendelezwa kwa vizazi vya sasa na vijavyo.
Aidha, Mkambi amesema kuwa BAKITA inathamini juhudi zinazofanywa na makabila mbalimbali nchini za kuhifadhi lugha zao maana lugha hizo zinasaidia kutengeneza na kuendeleza misamiati ya Kiswahili. 

Kwa upande wake Mtemi wa Masanza, Magu Mkoani Mwanza Frederick Ntobi amesema uzinduzi wa kitabu hicho umekuwa chachu kwa utamaduni wa kuhifadhi historia, masimulizi, mafundisho na elimu mbalimbali katika kuendeleza utamaduni wa Mtanzania. 

Ntobi ameyataja mambo ya msingi yanayopaswa kuzingatiwa katika kuendeleza utamaduni wa Mtanzania yakiwemo kukusanya vitu vya kale na kusaidia kutunza kumbukumbu vitu vilivyofanyika wakati uliopita kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo ili kusaidia kutunza historia kwa wakiongozwa na uzalendo miongoni mwa jamii na taifa, na amewaonya watu wasiwe na tamaa ya kuuza kumbukumbu hizo kwa watu wa nje kwa maslahi binafsi. 

Ntobi ameongeza kuwa mambo mengine ya kuzingatia katika kuendeleza utamaduni ni kutunza sanaa za kijadi ikiwemo michoro, mapishi ya kiasili ambayo yana manufaa kwa afya za walaji kwa kuhusisha siku ya kujifunza namna bora mapishi, kutunza maeneo ya matambiko ya kimila, kutunza lugha za asili pamoja na kutunza Ikulu za Kimila hatua ambayo itasaidia kukuza uchumi wa jamii husika na kuwa vyanzo vya mapato kwa Serikali. 

Kuhusu Sera ya Taifa ya Utamaduni, Ntobi amesema kuwa Umoja wa Machifu nchini wapo tayari kutoa maoni yao ili waweze kusaidia kupatikana Sera bora kwa manufaa ya taifa na kuifanya sekta ya utamaduni iweze kuchangia katika pato la taifa kwa njia ya utalii na kukuza uchumi wa nchi.
Naye mtunzi wa kitabu hicho Mratibu wa Mila na Desturi wa Nasa Busega Johnson Rollas Gervas ameishukuru Serikali kwa kutahamini na kuunga mkono juhudi za kuhifadhi utamaduni kwa kuzingatia mila na desturi ambazo ndio utambulisho wa taifa. 

Katika kuhakikisha amani ya nchi inaendelea kudumishwa, Johnson amesema kuwa watatumia ngoma, nyimbo na matamasha ambayo ni moja ya kazi ya sanaa ili kuweza kuunga juhudi za Serikali ya Awamu wa Tano kwa kushirikiana na Waziri mwenye dhamana ya utamaduni Mhe. Nape Nnauye na kuahidi kuwa wapo mstari wa mbele katika kuimarisha na kusimamia utamaduni wa Mtanzania. 

Akitoa neno la shukrani kwa Mgeni Rasmi mara baada ya uzinduzi wa kitabu hicho, Felister Mayala Bwana amesema kuwa Busega wataendelea kuunga mkono juhudi za Serikali katika kusimamia na kuendeleza utamaduni kwa kujenga na kuboresha kituo cha mila na desturi cha jamii ya kabila la Wasukuma wa Busega ili kuendelea kuitangaza Tanzania miongoni mwa mataifa kupitia sekta ya utamaduni.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AKUTANA NA RAIS UHURU KENYATTA JIJINI NAIROBI

$
0
0

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta katika Mkutano wa TICAD 6  kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Kenyatta (KICC) jijini Nairobi Agosti 28, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wakuu wa nchi mbalimbali wanaoshiriki katika Mkutano wa TICAD 6 kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Kenyeatta (KICC) jijini Nairobi Agosti 28, 2016.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WASOMI: JPM NA LOWASSA WAMEONYESHA KUWA MAZUNGUMZO YATALETA MUAFAKA.

$
0
0
Waziri Mkuu wa zamani Mh.Edward Lowassa akisalimiana na Rais Dkt John Pombe Magufuli


Na Tiganya Vincent, MAELEZO- Dar es salaam

Wasomi na Wanazuoni mbalimbali wamepongeza hatua ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na Waziri Mkuu zamani Edward Lowassa kushikana mikono na kusalimiana wakati wa Jubilei ya dhahabu ya miaka 50 ya ndoa ya Rais Mstaafu Benjamin William Mkapa na Anna Mkapa.

Wanazuoni hao wametoa kauli hiyo leo katika mahojiano maalum na Idara ya Habari iliyokuwa ikitaka kupata maoni yao kuhusu kitendo kilichoonyeshwa na viongozi hao kwa jamii.Profesa Kitila Mkumbo wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam amesema kuwa hatua hiyo imeonyesha kuwa huo ndio Utanzania ulivyo wa kutofautiana bila kugombana.

Amesema kuwa kitendo hicho kimewaonyesha wananchi kuwa mazungumzo yana nafasi kubwa ya kuondoa tofauti zilizopo kuliko kutumia njia nyingine kama vile maandamano na mabavu katika kutafuta ufumbuzi wa baadhi ya matatizo.“Kukutana kwa viongozi hao na kupeana mikono wakati wa kusalimiana kunakumbusha utamaduni wetu uliojingekea toka siku nyingi wa kutatua matatizo yetu kwa mazungumzo bila kugombana au kutumia mabavu,”alisema Profesa Mkumbo.

Kwa upande wa Profesa Joseph Semboja amesema kuwa amefurahishwa sana na kitendo kilichoonyeshwa na viongozi hao kwani kimeuonyesha ulimwengu kuwa Watanzania ni watu wenye Amani na upendo.Amesema kuwa hatua hiyo imeonyesha kuwa Watanzania wanaweza kuwa na tofauti lakini wakaendelea kuishi pamoja na kushirikiana katika mambo mbalimbali ya kijamii kwa ajili ya maendeleo yao na Taifa lao.

Profesa Semboja amewataka wananchi kujifunza kutokana na kitendo kilichoonyeshwa na viongozi hao ambao wameonyesha kuwa ni lazima wakae pamoja kwa ajili kushughulikia mambo muhimu ya maendeleo ya wananchi badala kuendeleza tofauti ambazo hazina manufaa kwa Watanzania.

Amesema kuwa ipo haja ya kwenda zaidi ya hapo kwa kuweka utaratibu wa kukaa pamoja na kujadiliana ili kutatua vyanzo vya migogoro kwa ajili ya mustakabali mzuri wa Taifa hili.Profesa amesema kuwa sio sahihi kutumia mfumo wa jino kwa jino kwani utaratibu huo ndio unaoweza kusababisha kukua zaidi kwa migogoro na wakati mwingine unasababisha umaskini kwa wananchi na Taifa kwa ujumla kwani muda mwingi wananchi hawana muda wa kushiriki katika shughuli za maendeleo kwa sababu ya migogoro.

Naye Profesa Samwel Wangwe amesema kuwa hatua ya viongozi hao kukutana na kupeana mikonop ni ishara kwa Watanzania kujifunza kuwa mazungumzo yana nafasi kubwa katika kuleta muafaka mgogoro wowote kuliko kutunishiana misuli.

Amesema kuwa mazungumzo yana nguvu kubwa katika kultea upatanishi katika migogoro mbalimbali inatokea katika jamii kuliko kutumia njia nyingine ambazo zinaweza kusababisha vurugu na uharibifu wa mali za watu na upotevu wa maisha ya watu.

MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AWASILI NCHINI SWAZILAND,KUMUWAKILISHA RAIS MKUTANO WA 36 WA SADC

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania SAMIA SULUHU HASSAN amewasili mjini Mbabane - Swaziland leo kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa 36 wa Wakuu wa nchi na serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika- SADC-.

Makamu wa Rais SAMIA SULUHU HASSAN atamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Dakta JOHN MAGUFULI katika mkutano huo ambao utafanyika tarehe 29 Agosti 2016 ambapo Tanzania inatarajiwa kukabidhiwa nafasi ya Uenyekiti wa Jumuiya hiyo.

Mkutano huo wa 36 wa SADC ni maalum kwa wakuu wa nchi na serikali wanaounda Kamati ya siasa,ulinzi na usalama ambao watajadili kwa kina hali ya siasa na usalama, demokrasia na maombi ya Burundi na Comoro kwa ajili ya kujiunga na SADC.

Makamu wa Rais SAMIA SULUHU HASSAN katika msafara wake amefuatana na Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Kikanda na Kimataifa Augustine Mahiga, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji John Mwijage na Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Amina Salum Ali.

Imetolewa na

Ofisi ya Makamu wa Rais

Mbabane – SWAZILAND.

TAZAMA HAFLA NZIMA YA RAIS DKT MAGUFULI KUHUDHURIA MISA YA JUBILEI YA DHAHABU (MIAKA 50) YA NDOA YA RAIS MSTAAFU BENJAMIN MKAPA NA ANNA MKAPA

$
0
0
 Rais Dkt John Pombe Magufuli akilakiwa na Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Petro  Fr. Stephano Kaombwe wakati akiwasili kuhudhuria  Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa ya Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016
 "Maharusi" Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa wakiingia kanisani  tayari kwa  Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa yao katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016
 "Maharusi" Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa wakiingia kanisani  tayari kwa  Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa yao katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016
 Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa  wakiwa tayari kwa  Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa yao katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016
  Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa  na wageni waalikwa akiwemo Rais Dkt John Pombe Magufuli na mkewe mama Janeth Magufuli  katika  Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa yao katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016
 Sehemu ya wanafamilia wa Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa    katika  Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa yao katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016
 MC Mavunde akipiga kinanda wakati wa  Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa hiyo katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016

  Sehemu ya wanafamilia wa Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa    katika  Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa yao katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016
 Sehemu ya waumini na wageni waalikwa   katika  Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa hiyo  katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016
  Sehemu ya waumini na wageni waalikwa   katika  Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa hiyo  katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016
  Sehemu ya waumini na wageni waalikwa   katika  Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa hiyo  katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016
  Sehemu ya waumini na wageni waalikwa   katika  Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa hiyo  katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016
  Sehemu ya waumini na wageni waalikwa   katika  Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa hiyo  katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016
  Sehemu ya waumini na wageni waalikwa   katika  Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa hiyo  katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016

  Sehemu ya waumini na wageni waalikwa   katika  Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa hiyo  katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016
  Sehemu ya waumini na wageni waalikwa   katika  Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa hiyo  katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016
  Wanakwaya katika  Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa hiyo  katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016
 Kiongozi wa kwaya  katika  Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa hiyo  katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016
  Sehemu ya wanafamilia wa Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa    katika  Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa hiyo  katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016
  Bw. Nicholaus Mkapa, mtoto wa Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa  akisoma somo la kwanza   katika  Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa hiyo katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016
  Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Arusha Josephat Lebulu akiongea na wana familia, waumini na wageni waalikwa katika  Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa hiyo katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016
 Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Petro  Fr. Stephano Kaombwe akiongoza Ibada ya ukumbusho wa ahadi za ndoa wakati wa Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa ya Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016
 Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Petro  Fr. Stephano Kaombwe akiongoza Ibada ya ukumbusho wa ahadi za ndoa wakati wa Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa ya Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016
 Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Petro  Fr. Stephano Kaombwe akiongoza Ibada ya ukumbusho wa ahadi za ndoa wakati wa Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa ya Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016
 Rais Dkt Magufuli, mkewe Mama Janeth Magufuli, Mama Maria Nyerere, Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa na waumini na wageni waalikwa  wakiwa katika Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa ya Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016
 Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Petro  Fr. Stephano Kaombwe akiongoza Ibada ya ukumbusho wa ahadi za ndoa wakati wa Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa ya Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016
 Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa akimvisha pete Mama Anna Mkapa katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016
 Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa akivishwa pete na Mama Anna Mkapa katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016
 Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa wakifurahia jambo baada ya zoezi hilo
 Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Petro  Fr. Stephano Kaombwe akitoa neno kwa "maharusi" hao wenye furaha 
  Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Petro  Fr. Stephano Kaombwe akitoa neno kwa "maharusi" . Kulia ni  Balozi Anthony Nyaki aliyesimamia harusi yao siku kama ya leo miaka 50 iliyopita. Matron alikuwa Marehemu Lucy Lameck.
  "Maharusi" Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa wanaketi baada ya ukumbusho wa viapo vya ndoa yao katika  kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016

 Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa akiongea na kadamnasi 

  Rais Dkt Magufuli, mkewe Mama Janeth Magufuli, Mama Maria Nyerere, Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa na waumini na wageni wakiendelea na misa
 Mawaziri wakuu wastaafu walikuwepo. Kutoka kushoto ni Jaji Joseph Sinde Warioba na mkewe Evelyn Warioba. Mzee Cleopa Msuya, Mama Amne Salim na mumewe Dkt. Salim Ahmed Salim na Mhe Edward Lowasssa na mkewe mama Regina Lowassa
 Sir Andy Chande akiungana na waalikwa katika misa hiyo
 Mohamed Dewji na mkewe wakiwa katika misa hiyo
 Mstari wa mbele
 Makamu Mwenyekiti wa CCM Ndg Philip Mangula na mkewe pamoja na wageni wengine
 Mawaziri wakuu wastaafu walikuwepo. Kutoka kushoto ni Jaji Joseph Sinde Warioba na mkewe Evelyn Warioba. Mzee Cleopa Msuya, Mama Amne Salim na mumewe Dkt. Salim Ahmed Salim na Mhe Edward Lowasssa na mkewe mama Regina Lowassa
 Katibu Mkuu Kiongozi Eng. John Kijazi, Maspika wastafu Mzee Pius Msekwa na Mama Anne makinda na Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu Balozi Ombeni Sefue
 Sehemu ya waalikwa
 Jaji Mkuu mstaafu Mhe. Barnabas Samatta na mkewe pamoja na waalikwa wengine
 Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu Mhe. Marten Lumbanga na mkewe pamoja na Waziri mstaafu Profesa Philemon Sarungi na mkewe Mama Sarungi
 Waalikwa
 Wageni waalikwa 
 Waalikwa
 Sehemu ya waalikwa
 Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa wakiongoza wana familia kupeleka matolea altereni
 Kwaya 
 Sehemu ya waalikwa
 Waalikwa
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Arusha Josephat Lebulu akiongoza misa 
 Misa ikiendelea
 Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Arusha Josephat Lebulu akiongoza misa 
 Misa ikendelea
 Rais Dkt John Pombe Magufuli akimtakia amani Mama Anna Mkapa
Mama Janeth Magufuli na Mama Maria Nyerere wakiwatakia amani Mzee Mkapa na Mama Anna Mkapa
 Rais Dkt John Pombe Magufuli akimtakia amani Mhe. Edward Lowassa

 Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa wakipokea hati malumu ya ndoa kutoka Vatican kwa Baba Mtakatifu Papa Francis kutoka kwa Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo
 Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa wakipongezwa na Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo
 Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa wakionesha hati yao  maalumu kutoka  Vatican
Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa na hati yao kutoka Vatican
Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo akiongea 
 Kila mtu anafurahia mafundisho ya Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo
 Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa wakipokea zawadi kutoka Paroko ya Upanga ya Mt. Imakulata 
 Rais Dkt John Pombe Magufuli akisalimia na kuwapongeza Mzee Mkapa ma mkewe
 Rais Dkt John Pombe Magufuli akifurahiajambo
 Wote wanafurahia hotuba ya Rais Dkt John Pombe Magufuli 
Rais Dkt John Pombe Magufuli  
 Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Dk. Martin Shoo akitambulishwa kanisani hapo
 Ni wakati wa kupata picha za kumbukumbu ambapo Mzee Mkapa na Mama Anna Mkapa wanaanza na Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo na  Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Arusha Josephat Lebulu 
 Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Dk. Martin Shoo akimpongeza Mama Anna Mkapa
 Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Dk. Martin Shoo Mhe Benjamin William Mkapa
 Picha na viongozi wastaafu na wana familia 
 Picha na waliosoma na Mzee Mkapa
 Picha na kamati ya maandalizi

 Picha na viongozi wastaafu
 Picha na viongozi wastaafu na walio kazini
 Picha na watoto wa kutoka Kituo cha Kulea Watoto Yatima cha Kibaha (Kibaha The EOTF Orpham Centre) 
Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa wakipozi na Sir Andy Chande 
 Ukumbi wa sherehe
 Msafara ukielekea ukumbini
 Viongozi waalikwa
 Viongozi wastaafu
 MC Angela Bondo kazini
 Sehemu ya waalikwa
 Taswira ya mbele
 Meza ya wana familia
 Burudani ya muziki
wakielekea jukwaani kukata keki
 Ni wakati wa keki
 Wakikata keki
 Wakilishana keki huku wakishuhudiwa na msimamizi wa ndoa yao miaka 50 iliyopita Balozi  Anthony Nyaki
 Wajukuu, watoto, wakwe wakilishwa keki
 Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Mama Maria Nyerere na Mama Shadya Karume
 Wanafamilia wakijadiliana jambo
 Taswira ya ukumbi
 Bw. Nicholaus Mkapa akimimina champagne isiyo na kilevi  meza kuu
 Bw. Nicholaus Mkapa akijianda kumimina champagne isiyo na kilevi  kwa Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho kikwete na Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdulrahman Kinana
 Katibu Mkuu Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma) Mstaafu Mhe.  Joseph Rugumyamheto akiwatakia wote maisha marefu kwa kuongoza toast
  Meza kuu wakigonganishiana glasi na Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa
 Meza kuu wakigonganishiana glasi na Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa
 Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa akigongesha glasi na Mama Maria Nyerere, Mama Shadya Karume na Mama Salma Kikwete
   Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa akigongesha glasi na Katibu Mkuu Kiongozi Eng. John Kijazi na Jaji Mkuu Mhe Mohamed Chande Othman
  Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa wakigongesha glasi na Katibu Mkuu Kiongozi Eng. John Kijazi, Jaji Mkuu Mhe Mohamed Chande Othman, Spika Mstaafu Mamam Anne Makinda
  Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa wakigongesha glasi viongozi  wastaafu na Makamu Mwenyekiti wa CCM na katibu Mkuu wake
 Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa wakigongesha glasi viongozi  wastaafu na Makamu Mwenyekiti wa CCM na katibu Mkuu wake
 Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa wakigongesha glasi viongozi  wastaafu
Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa wakigongesha glasi na mawaziri wakuu wastaafu
 Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa wakipongezwa na MKUU wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) mstaafu, Jenerali George Mwita Waitara na mkewe Mama Waitara
 Rais Dkt. Magufuli akisaini kitabu cha sherehe hizo
 Katibu Mkuu wa CCM Ndg Abdulrahaman Kinana akisalimiana na Waziri mkuu wa zamani Mhe. Edward Lowassa
 Mama Salma Kikwete akisalimiana na Waziri wa zamani wa Nishati na Madini, Mhe. Alnoor Kassum    na mkewe Mama Kassum
 Watoto kutoka Kituo cha Kulea Watoto Yatima cha Kibaha (Kibaha The EOTF Orpham Centre) wakiwaimbia babu na bibi Mkapa
 Brigedia Jenerali  mstaafu Francis Mbena akikabidhi zawadi yake
 Brigedia Jenerali  mstaafu Francis Mbena akikabidhi kadi maalumu aliyotengeneza
 Brigedia Jenerali  mstaafu Francis Mbena akikabidhi kwa Nicholaus Mkapa na mkewe zawadi yake
 Bw. Kambona aliyesoma darasa moja na Mzee Mkapa akionesha zawadi ambao baadhi ya waliosoma naye waliileta kumkabidhi
 Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na mkewe Mama Anna Mkapa wakipokea zawadi ya waliosoma na Mzee Mkapa
 Msemaji wa familia ya Mzee Mkapa Bw. William Erio akitoa shukurani kwa wote waliofika na pia waliofanikisha sherehe hizo

 Sheikh wa mkowa wa Dar es salaam Ahaj Alhad Mussa Salum akisema machache
 Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwapongeza Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na mkewe Mama Anna Mkapa 
  Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa akitoa shukurani zake kwa wote waliohudhuria na waliofanikisha sherehe hizo
 Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa akitoa shukurani zake kwa wote waliohudhuria na waliofanikisha sherehe hizo
 Rais Dkt. Magufuli na mkewa Mama Janeth Magufuli wakiwapongeza Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na mkewe Mama Anna Mkapa 
  Rais Dkt. Magufuli na mkewa Mama Janeth Magufuli wakiwapongeza Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na mkewe Mama Anna Mkapa 
  Rais Dkt. Magufuli na mkewa Mama Janeth Magufuli wakiwakabidhi zawadi Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na mkewe Mama Anna Mkapa 
 Rais Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu wa zamani Mhe. Edward Lowassa. Kushoto ni Mama Regina Lowassa

  Rais Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na  Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Bishop Eusebius Nzigilwa
 Rais Dkt John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakipozi na viongozi wa dini. Kutoka kushoto ni Sheikh Alhad Mussa Salum, Shekhe wa mkoa wa Dar es salaam, Rais Magufuli, Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Dk. Martin Shoo, Mama Janeth Shoo na Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Bishop Eusebius Nzigilwa
 Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa pamoja na Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho kikwete  wakipozi na wajukuu wa Mzee Mkapa
 Rais Dkt John Pombe Magufuli akiongea na Mama Maria Nyerere

Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa pamoja na Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho kikwete na Mama Salma Kikwete wakipozi na wajukuu wa Mzee Mkapa. Picha zote na IKULU

SIKILIZA HAPA ALICHOKISEMA RAIS DKT JOHN POMBE MAGUFULI BAADA YA KUKUTANA USO KWA USO NA MH.LOWASSA

ATOWEKA KATIKA MAZINGIRA YA KUTATANISHA

$
0
0
MKAZI wa kijiji cha Kabare kata ya Uwarama wilaya ya Kakonke, Robent Laurent (35) ametoweka nyumbani kwake Dodoma Makulu katika mazingira ya kutatanisha.

kwa mujibu wa Shemeji yake, Mchungaji Philip Kayanda, amesema kuwa Laurent alikuwa ametokea Zanzibar na kuelekea Kahama lakini alipofika hapa Dodoma aliteremka na kuelekea nyumbani kwao eneo la Dodoma makulu ambako alitoweka kusikojulikana.

Mchungaji Kayanda alisema kuwa shemeji yake huyo ana matatizo ya akili.

Laurent ambaye rangi yake maji ya kunde amesema kabla ya kujachanganyikiwa akili ,alikuwa anafanya kazi ya uchungaji katika kanisa la FPCT huko kijijini kwao Kabare mkoa wa Kigoma ikiwemo na Zanzibar.

Amesema jitihada za kumtafuta kwa ndugu, jamaa na marafiki zimefanyika bila mafanikio na tayari wametoa taarifa kituo cha polisi kati cha Dodoma na kufungua jalada namba RB/DOM/8409/2016.

Ameomba kwa yeyote atakayemuona atoe taarifa katika kituo chochote cha polisi kilichopo karibu ama apige simu namba 0688 - 688229,0788 – 669300 au 0655 – 090820

WEKEZA KWENYE MWANZO MZURI WA ELIMU YA MTOTO WAKO, BEGINNERS FOUNDATION CENTER WAMEANZA KUANDIKISHA WANAFUNZI WAPYA

$
0
0
Je una mtoto wa miezi 3 mpaka miaka 5? Wekeza sasa kwenye msingi bora wa elimu yake kwa kuchagua elimu bora; Mwandikishe mwanao sasa Beginners Foundation Center iliyopo Sinza Mori.

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi 0745 793 916





Viewing all 46343 articles
Browse latest View live




Latest Images