Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live

MWANDISHI WA HABARI MARY LYIMO KUZIKWA LEO

$
0
0

Mwandishi wa Habari Mary Jovian Lyimo amefariki dunia Agosti 23 baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa Kansa ya Ini, kwa mujibu wa Dada wa marehemu, Liliani Jovian Lyimo amesema kuwa marehemu enzi za uhai wake aliwahi kufanya kazi katika Shirika la Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASCO), kama Ofisa habari wa shirika hilo, pia alifanya kazi katika Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).

Marehemu atazikwa leo Agosti 27 saa nane katika makaburi ya Kondo Kunduchi jijini Dar es Salaam. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi amani.

TPDC KIMENUKA,WAKURUGENZI WATANO WASIMAMISHWA KAZI KUPISHA UCHUNGUZI

NMB TAWI LA NELSON MANDELA WASHIRIKI ZOEZI LA USAFI MJINI MOSHI LEO.

$
0
0

Meneja wa NMB tawi la Neslon Mandela Emanuel Kishosha akiwa amebeba taka mara baada ya kumaliza kuzikusanya wakati wa zoezi hilo la usafi.
Hivi ndivyo yalivyooonekana maeneo ambayo wafanyakazi wa Benki ya NMB tawi la Moshi walishiriki kuyafanyia usafi  mjini Moshi hii leo.Wafanyakazi wa Benki ya NMB tawi la Nelson Mandela mjini Moshi wakiwa wamebeba vifaa kwa ajili ya kufanya usafi katika eneo la njia mbili maarufu kama Double Road mjini Moshi leo.
Wafanyakazi wa Benki ya NMB tawi la Moshi wakivuka barabara tayari kuanza zoezi la kufanya usafi katika eneo la Double Road mjini Moshi leo.
Wafanyakazi wa Benki ya NMB tawi la Moshi wakifanya usafi katika maeneo ya maduka yaliyopo eneo la Double Road mjini Moshi.
Meneja wa Benki ya NMB tawi la Nelson Mandela mjini Moshi Emanuel Kishosha akiowaongoza wafanyakazi wenzake katika zoezi la kufanya usafi .
Wafanyakazi wa Benki ya NMB tawi la Moshi wakiokota taka zilizokusanywa wakati wa zoezi la usafi lilofanyika katika eneo la Double Road mjini Moshi.
Wafanyakazi wa NMB tawi la Nelson Mandela mjini Moshi wakiwa na taka zilizokusanywa wakienda kuzitupa katika eneo la kusanyia takataka.
Wafanyakazi wa Benki ya NMB tawi la Nelson Mandela mjini Moshi wakiendelea na usafi katikati ya barabara.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini .

MKUTANO WA MAWAZIRI WA TICAD WAFANYIKA JIJINI NAIROBI

$
0
0

Sehemu ya Wajumbe waliohudhuria mkutano huo
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Susan Kolimba akiongoza ujumbe wa Tanzania kwenye kikao cha Mawaziri wa Mkutano wa Sita wa Kimataifa kuhusu Ushirikiano wa Maendeleo kati ya Japan na Afrika (Tokyo International Conference on African Development-TICAD VI) uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kenyatta (KICC) tarehe 26 Agosti, 2016. Kulia ni Waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Khalid Salum Mohammed na kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbelwa Kairuki.
Balozi Mbelwa akitoa ufafanuzi kwa Mhe. Naibu Waziri kuhusu masuala yatakayojadiliwa kwenye Mkutano huo.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kenya, Mhe. Amina Mohammed akizungumza wakati wa Mkutano huo.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan, Mhe. Fumio Kishida nae akizungumza wakati wa mkutano wa Mawaziri.
Sehemu nyingine ya wajumbe
Picha ya pamoja ya meza kuu.


Kikao cha Mawaziri kuandaa Mkutano wa Kilele wa Sita wa Kimataifa kuhusu Ushirikiano wa Maendeleo kati ya Japan na Afrika (Tokyo International Conference on African Development-TICAD VI) kimemalizika Jijini Nairobi leo ambapo Mawaziri hao wameikubali kwa kauli moja Rasimu ya Azimio la Nairobi na Mpango Kazi wake tayari kwa kuwasilishwa kwa Wakuu wa Nchi na Serikali kwa ajili ya kupitishwa.



Akihitimisha Mkutano huo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya, Mhe. Amina Mohammed amewashukuru Mawaziri wenzake, waandaaji wa kikao hicho na washiriki wote kwa kikao chenye mafanikio na kueleza kuwa ana matumaini makubwa kuwa agenda zilizojadiliwa zitapitishwa na Wakuu wa Nchi na Serikali kwenye Mkutano wao.



Aidha, alisema kuwa Rasimu hiyo ya Azimio ambalo linazungumzia agenda muhimu tatu ambazo ni Kuhamasisha mageuzi ya kiuchumi kupitia uendelezaji wa viwanda; Kuboresha sekta ya Afya kwa maisha bora na Kusaidia jitihada za kudumisha amani na utulivu katika jamii linalenga kutatua changamoto mbalimbali na kuiwezesha Afrika kufikia maendeleo endelevu.



Pia, aliishukuru Serikali ya Japan kwa kuendelea kuiunga mkono Afrika katika kukamilisha malengo yake ya maendeleo na kwamba mkutano huu wa 6 utaendelea kuimarisha na kudumisha ushirikiano uliopo kati ya nchi za Afrika na Japan.



“Mkutano huu una lengo kubwa moja la kuiwezesha Afrika kufikia maendeleo endelevu kwa kushirikiana na Japan. Hivyo nawapongeza waandaaji na washiriki wote kwa kufanikisha rasimu ya Azimio la Nairobi na ni imani yangu kuwa Azimio hili litapitishwa na Wakuu wa Nchi na Serikali katika mkutano wao” alisema Mhe. Mohammed.



Awali akizungumza wakati wa mkutano huo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan, Mhe. Fumio Kishida alisema kuwa Afrika imeendelea kuwa mdau muhimu katika ushirikiano na Japan na kwamba nchi yake inaona fahari kuendeleza ushirikian huo ili kuziwezesha nchi za Afrika kufikia maendeleo endelevu. Pia aliishukuru Serikali ya Kenya kwa kuwa mwenyeji wa mkutano wa TICAD VI na ana matarajio makubwa kuwa utakuwa na tija.



Pia aliongeza kuwa Mikutano ya TICAD ni jukwaa muhimu linaloziwezesha nchi za Afrika na Japan kuangalia vipaumbele mbalimbali katika ushirikiano ili hatimaye kufikia malengo yaliyokusudiwa ikiwemo kuinua uchumi na kuboresha sekta mbalimbali ikiwemo afya.



Naye Waziri wa Uchumi na Mipango wa Chad, Mhe. Mariam Mahamat Nour ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Umoja wa Afrika alisema kuwa mkutano wa 6 wa TICAD utatoa mwanga kwa changamoto mbalimbali zinazolikabili Bara la Afrika kupitia Azimio la Nairobi mara litakapotishwa na kuanza kutekelezwa.



Kwa upande wa Tanzania Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika, Mhe. Dkt. Susan Kolimba aliongoza ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano huo wa Mawaziri. Wajumbe wengine waliohudhuria ni Waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Dkt. Khalid Salum Mohammed na Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia, Balozi Mbelwa Kairuki.



Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali unatarajiwa kufanyika tarehe 27 na 28 Agosti, 2016 ambapo moja ya agenda ni kupitisha Azimio la Nairobi. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa atamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Magufuli kwenye mkutano huo.



Mkutano wa Sita wa TICAD unalenga kuiwezesha Afrika katika sekta ya uchumi na uwekezaji ambapo utawashirikisha pia wadau kutoka sekta binafsi zikiwemo Kampuni binafsi zaidi ya 300 kutoka Japan ili kufikia lengo hilo.

WAKALA WA VIPIMO NA VIPIMO

$
0
0
 WAKULIMA WA KOROSHO KATIKA MKOA WA RUVUMA WAKIPATA ELIMU KUPITIA VIPEPERUSHI VILIVYO ANDALIWA NA WAKALA WA VIPIMO WAKATI WA ZOEZI LA UTOAJI ELIMU.
 MENEJA WA WAKALA WA VIPIMO MKOANI MTWARA AUGUSTINE MAZIKU AKIWAONESHA WAKULIMA WA KOROSHO, MKOANI HUMO KUSOMA KWA USAHIHI MIZANI ILIYO HAKIKIWA NA WAKALA WA VIPIMO

 ALFA MTUI AFISA VIPIMO MWANDAMIZI, AKITOA ELIMU KWA WAKULIMA WA KOROSHO MKOANI RUVUMA NAMNA YAKUTAMBUA MIZANI  ILIYO HAKIKIWA NA KURUHUSIWA KUTUMIKA NA WAKALA WA VIPIMO.
 MENEJA WA WAKALA WA VIPIMO MKOANI MTWARA BWANA AUGUSTINE MAZIKU AKIJIBU MASWALI KUTOKA KWA WAKULIMA WALIOKUWA WAMEFIKA KUPATIWA ELIMU YA MATUMIZI SAHIHI YA MIZANI ILIYO HAKIKIWA NA WAKALA WA VIPIMO KABLA YA MSIMU WA UNUNUZI WA KOROSHO KUANZA.
MENEJA WA WAKALA WA VIPIMO MKOANI RUVUMA BW.  HALLET HASSAN  AKITOA ELIMU KWA WAKULIMA WA KOROSHO  MKOANI HUMO KABLA YA MSIMU KUANZA  ILI KUEPUSHA KUZULUMIWA NA WANUNUZI WASIO WAAMINIFU. (Picha zote na Iren John).

Uchambuzi wa kina kuhusu Dkt Magufuli kumtia Dkt Kipilimba kuwa DG wa Idara ya Usalama wa Taifa

$
0
0
Tarehe 24 mwezi huu, Rais Dokta John Magufuli alimteua Dokta Modestus Kipilimba kuwa Mkurugenzi Mkuu (DGIS) wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS). Uteuzi huo umefanyika kufuatia kustaafu kwa mkurugenzi aliyemaliza muda wake, Othman Rashid.

Makala hii inajikita katika uchambuzi wa uteuzi huo kwa kuangalia changamoto na fursa zinazomkabili kiongozi huyo mkuu wa taasisi hiyo nyeti kabisa. Kwa mtizamo wangu, kama kuna kitu ambacho kinaweza kuzua maswali kuhusu uteuzi huo basi ni wadhifa wa Director of Risk Management alioshikilia Dokta Kipilimba huko nyuma alipokuwa mtumishi wa Benki Kuu ya Tanzania.

Sote twafahamu jinsi Benki Kuu yetu imekuwa ikiandamwa na matukio mfululizo ya ufisadi, kuanzia EPA hadi Tegeta Escrow. Kwa wadhifa wake katika taasisi hiyo, kuna uwezekano wa bosi huyo mpya wa mashushushu kuonekana ‘sehemu ya mfumo ulioshindwa kudhibiti ufisadi.’ Hata hivyo, utetezi unaweza kuwa huenda yeye alitekeleza majukumu yake vema lakini walio juu yake hawakuchukua hatua stahili.

Kadhalika, huko mtandaoni kuna ‘tuhuma’ kadhaa kuhusu Dokta Kipilimba, lakini itakuwa sio kumtendea haki yeye, blogu hii na mie mwenyewe kujadili tuhuma ambazo hazina ushahidi wowote. Ni muhimu kutambua kuwa Tanzania yetu licha ya kuwa kisiwa cha amani pia ni kisiwa cha majungu, uzandiki, fitna, umbeya na uzushi.

Changamoto kubwa kwa Dokta Kipilimba ni pamoja na kurejesha hadhi na heshima ya Idara ya Usalama wa Taifa. Katika miaka ya hivi karibuni, taasisi hiyo muhimu kabisa imekuwa ikishutumiwa kuwa inachangia ustawi wa ufisadi, ujangili, biashara ya madawa ya kulevya, nk.

Wanaoilaumu taasisi hiyo hawamaanishi kuwa watumishi wake wanahusika katika matukio hayo ya kihalifu as such bali kushindwa kwa Idara hiyo kukabiliana na kushamiri kwa matendo hayo ya kihalifu, ambayo kimsingi ni matishio kwa usalama wa taifa, na kazi kuu ya Idara hiyo ni kukabiliana na matishio kwa usalama wa taifa la Tanzania.

Ninaamini kuwa Dokta Kipilimba anafahamu kanuni muhimu kuhusu ufanisi au mapungufu ya idara ya usalama wa taifa popote pale duniani, kwamba “kushamiri kwa vitendo vinavyotishia usalama wa taifa lolote lile ni kisheria cha mapungufu ya idara ya usalama wa taifa ya nchi husika, na kudhibitiwa kwa vitendo vinavyotishia usalama wa taifa popote pale duniani ni kiashiria cha uimara wa idara ya usalama wa taifa ya nchi husika.”

Kwahiyo, kwa kuzingatia kanuni hiyo, kushamiri kwa biashara ya madawa ya kulevya, ujangili, rushwa, na ufisadi mwingine ni viashiria vya mapungufu ya Idara yetu ya Usalama wa Taifa.

Changamoto nyingine kwa Dokta Kipilimba ni tuhuma za mara kwa mara dhidi taasisi hiyo muhimu kabisa kuwa katika utendaji kazi wake imegeuka kuwa kama ‘kitengo cha usalama cha chama tawala CCM.’ Idara hiyo imekuwa ikituhumiwa kuwa kwa kiasi kikubwa imeweka kando taaluma ya ushushushu (tradecraft) na kutekeleza majukumu yake kisiasa.

Madhara ya muda mfupi ya kasoro hiyo ni taasisi hiyo kujenga uhasama na vyama vya upinzani na kwa namna flani kupoteza heshima na uhalali wake. Lakini la kuogofya zaidi ni madhara ya muda mrefu, ambapo watu wanaoweza kuwa ni matishio kwa usalama wa taifa letu wanaweza kutumia ‘urafiki’ unaodaiwa kuwepo kati ya Idara ya Usalama wa Taifa na CCM, wakitambua bayana kuwa ‘Idara haina muda na makada wa chama tawala,’ na hatimaye kufanikiwa kutimiza azma zao ovu.

Baadhi ya watumishi wa zamani wa taasisi hiyo walijikuta matatizoni kwa vile tu walitekeleza majukumu yao dhidi ya wanasiasa wa chama tawala, na wakaishia kuonekana kama wahaini.

Changamoto nyingine kwa Dokta Kipilimba ni tuhuma zinazoikabili taasisi hiyo kuhusu mfumo wa ajira ambapo inadaiwa kuwa zimekuwa zikitolewa kwa upendeleo kwa ndugu na jamaa za ‘vigogo.’ Tatizo kubwa hapa ni kwamba utiifu wa ‘ndugu na jamaa hao wa vigogo’ haupo kwa taifa bali kwa vigogo hao waliowaingiza Idarani. Pengine sio vibaya kufikiria ‘utaratibu wa wazi’ katika ‘recruitment’ kama inavyofanywa na wenzetu wa CIA, NSA, MI5, MI6, HGCQ, nk wanaotangaza nafasi za ajira kwenye vyombo vya habari.

Pia kuna tatizo la baadhi ya maafisa usalama wa taifa ‘kujiumbua’ kwa makusudi kwa sababu wanazojua wao wenyewe, kubwa ikiwa kutaka sifa tu, au waogopwe ‘mtaani.’ Hii inaathiri sana ufanisi wa maafisa wa aina hiyo kwani ni vigumu kutekeleza majukumu yao ipasavyo pasi usiri.

Sambamba na hilo ni kasumba ya muda mrefu ambapo baadhi ya maafisa wa Idara hiyo waliopo kwenye vitengo mbalimbali kuwepo huko kwa muda mrefu mno kiasi cha kuathiri utendaji wao. Miongoni mwa maeneo hayo ni pamoja na ‘vituo muhimu’ na kwenye ofisi za balozi zetu nje ya nchi. Ikumbukwe kuwa unless afisa ametengeneza deep cover, uwepo wake kwa muda mrefu katika sehemu aliyokuwa ‘penetrated’ au kituo chake cha kazi kwingineko (mfano ubalozini) unaweza kupelekea ‘akaungua’ (burned).

Changamoto nyingine kubwa ni uwepo wa majasusi kibao nchini mwetu, hususan kutoka nchi moja jirani, huku wengi wa majasusi hao wakiwa wameajiriwa katika taasisi za umma na binafsi. Hili ni tishio kubwa kwa usalama wa taifa wa Tanzania yetu.

Kwa upande fursa kwa Dokta Kipilimba, licha ya kuwa ‘mwenyeji’ katika taasisi hiyo muhimu, wasifu wake kitaaluma unamweka katika nafasi nzuri sana kukabiliana na changamoto za karne ya 21 ambayo imetawaliwa zaidi na teknolojia ya kisasa.

Dokta Kipilimba ni msomi aliyebobea kwenye teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) na yayumkinika kuamini kuwa anaweza kutumia usomi wake kuibadilisha Idara yetu ya Usalama wa Taifa kwenda na wakati, kufanya kazi kama taasisi ya kishushushu ya karne ya 21, ambayo licha ya kutegemea HUMINT inaweza pia kutumia njia nyingine za kukusanya taarifa za kiusalama kwa kutumia teknolojia (GEOINT, MASINT, SIGINT, CYBINT, FININT na TECHINT kwa ujumla.

Fursa nyingine kwa Dokta Kipilimba ni matarajio ya sapoti ya kutosha kutoka kwa Rais Dokta Magufuli ambaye kama alivyoahidi wakati wa kampeni za kuwania urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka jana, mapambano dhidi ya ufisadi yamepewa kipaumbe cha hali ya juu kabisa. Kama ‘sponsor’ na ‘consumer’ wa taarifa za kila siku usalama, inatarajiwa kuwa Dokta Magufuli atatekeleza ushauri wa Idara katika kukabiliana na matishio mbalimbali ya usalama wa taifa letu.

Dokta Kipilimba ana fursa ya kuleta mageuzi kwa Idara ya Usalama wa Taifa kwa kuangalia uwezekano wa kuwafikia watu walio nje ya taasisi hiyo, hasa pale uwezo wa Idara yetu unapokuwa limited. Nitoe mfano. Katika kupata taarifa mwafaka wa kudumu kuhusu, kwa mfano, mgogoro wa kisiasa huko Zanzibar, Idara inaweza ku-reach out wanazuoni wa historia ya taifa letu walipo ndani na nje ya nchi yetu.

Ikumbukwe kuwa sio rahisi kwa taasisi hiyo kuwa na maafisa au watoa habari katika kila eneo. Wenzetu wa nchi za Magharibi wamekuwa wakikabiliana na hali hiyo kwa kufanya kazi na ‘makandarasi’ (contractors), ambao of course, wamekidhi taratibu kama vile vetting.

Sambamba na hilo ni Idara hiyo kuangalia uwezekano wa kutumia hazina kubwa tu ya maafisa wake wa zamani, hususan wastaafu Ikumbukwe kuwa wengi wao ni watu wanaowindwa na ‘subjects’ mbalimbali wanaolenga kulihujumu taifa letu.

Nimalizie makala hii kwa kutoa pongezi za dhati kwa Dokta Kipilimba na Naibu wake (DDGIS) Robert Msalika, sambamba na kumtakia mapumziko mema Mkurugenzi mstaafu Othman, na kumkaribisha ‘uraiani.’


MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI IDARA YETU YA USALAMA WA TAIFA

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AKUTANA NA OFISA MTENDAJI MKUU WA GLOBAL FUND

$
0
0
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Global Fund, Mark Dybul  (kulia  kwake)  kwenye hoteli ya Windsor Agosti 26,2016.Kushoto kwake ni Balozi wa Tanzania nchini Japan, Mathias Chikawe.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Global Fund, Mark Dybul    kwenye hoteli ya Windsor Agosti 26,2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Global Fund, Mark Dybul   kabla ya mazungumzo yao kwenye hoteli ya Windsor jijini Nairobi, Agosti 26,2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA ASHIKIRI MKUTANO WA APRM NAIROBI

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Tanzania iko tayari kujifunza kutoka kwa nchi nyingine ambazo ni wanachama wa Mpango wa Kujitathmni Kiutawala Bora barani Afrika (APRM) ili iweze kuboresha hatua ilizofikia kwenye mpango huo.

Ametoa kauli hiyo jana jioni (Ijumaa, Agosti 26, 2016) wakati akichangia mada katika Mkutano wa 25 wa Wakuu wa Nchi wanachama wa Mpango wa Kujitathmni Kiutawala Bora barani Afrika (APRM Forum) uliofanyika kwenye hoteli ya InterContinental jijini Nairobi, Kenya.

“Nitumie fursa hii kukiarifu kikao chako kwamba Tanzania imeshaanza kutekeleza mpango kazi wa Kitaifa ambao umejikita kutatua changamoto katika sekta za maji, elimu, kilimo, nishati na miundombinu kama zilivyoainishwa kwenye kikao cha APRM,” alisema.

“Ili kuhakikisha kuwa zinafanyiwa kazi haraka, changamoto hizi za kisekta zimepewa kipaumbele kwenye Mpango wetu wa Pili wa Taifa wa Maendeleo wa miaka mitano wa 2016-2021 ambao umejikita zaidi kwenye viwanda,” aliongeza.

Tanzania ilifanyiwa tathmini yake Januari, 2013 kwenye kikao cha Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika kilichofanyika Addis Ababa, Ethiopia.

Mapema, akifungua mkutano huo, Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya alisema viongozi wa Afrika hawana budi kukubaliana na kuungana kutafuta suluhisho katika ushindani wa kibiashara.

Alisema nchi wanachama wa mpango huo hawana budi kujenga umoja kama njia ya muafaka ya kufikia makubaliano hayo.

Wakati huohuo, Rais Yoweri Museveni wa Uganda alisema bara la Afrika linakabiliwa na changamoto 11 (strategic bottlenecks) ambazo zinakwamisha maendeleo ya bara hilo na akataka zitafutiwe ufumbuzi ili kuzisaidia nchi nyingi barani humo.  

Akiwasilisha mada binafsi katika mkutano huo, Rais Museveni alisema kwa zaidi ya miaka 50, amekuwa kiongozi katika sehemu kadhaa na kwamba amebaini kuwa changamoto hizo zimezuia ukuaji wa uchumi barani Afrika pamoja na mabadiliko ya kiuchumi na kijamii.
Alisema asilimia kubwa ya changamoto hizo haikupata ufumbuzi hata wakati malengo ya maendeleo ya milenia (MDGs) yalipokuwa yanatekelezwa.

Alizitaja changamoto hizo kuwa ni mikanganyiko ya kiitikadi ambayo huzaa ubinafsi na maslahi binafsi; kuwepo kwa mataifa dhaifu (weak states); nguvukazi duni (kitaaluma na kiafya), uduni wa miundombinu (barabara, maji, umeme, tehama) ambao unashindwa kuvutia uwekezaji; uhaba wa viwanda unaolazimisha nchi kusafirisha mali ghafi na uhaba wa masoko ya bidhaa zinazozalishwa barani Afrika.

Changamoto nyingine ni uduni wa huduma za kijamii unaosababisha huduma mbovu kwenye maeneo ya utalii, mabenki na mahoteli; kilimo duni kisichotumia mbolea, dawa za kuua wadudu, mbegu za kisasa au njia za umwagiliaji; makosa ya kisera kama vile ubinafishaji au utaifishaji mali zinazomilikiwa na sekta binafsi; ukandamijazi wa demokrasia na ukosefu wa maadili miongoni mwa watumishi wa umma.

Naye Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini alisema kwa vile changamoto hizo zinagusa nchi nyingi za Afrika, ni vema iundwe timu ya wataalamu watakazipitia zote na kuainisha zipi zinafaa kufanyiwa kazi na kisha taarifa yao iwasilishwe kwenye kikao kijacho cha Wakuu wa Nchi wanachama.

Akifunga mkutano huo, Rais Kenyatta aliitaka sekretarieti ya APRM ipitie changaoto hizo na kuziwakilisha kwenye kikao chao kijacho ambacho alisema kitafanyika Januari 2017, mjini Addis Ababa, Ethiopia katika tarehe itakayopangwa baadaye.

(mwisho)

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAMOSI, AGOSTI 27, 2016.

DC DEO NDEJEMBI AWATIA NDANI VIONGOZI WA CHAMA CHA CARGO POTTERS WA SOKO LA KIMATAIFA LA MAZAO KIBAIGWA KWA UFISADI.

$
0
0



Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mh Deo Ndejembi Siku 14 zilizopita alitembelea Soko la Mazao la Kimataifa lililopo Mji Mdogo wa Kibaigwa Wilayani Kongwa, katika ziara hiyo aliagiza kusimamishwa shughuli zote za madalali katika soko hilo baada ya Kubaini Madalali huwanyonya Wakulima wanapokwenda Sokoni hapo kuuza Mazao.

Agizo hilo lilipaswa liwe limetekelezwa ndani ya siku 14 na Ndipo DC akajerea na kuwaita Viongozi ili Kujadili.

Baada ya Hapo DC Aliombwa Kikao na Viongozi hao na ndipo DC kaita BODI ya Soko la Kibaigwa, Uwongozi wa CARGO Potters, Meneja wa Soko Kuu la Kimataifa la Kibaigwa, Lengo Kuu nikujadili hali ya Soko na Wafanyabiashara wa Sokoni hapo na Zaidi hao Madalali ambao kwa Kiwango Kikubwa Wamekuwa wakijikusanyia Mapato kinyume cha Sheria na Taratibu.

Wakati kikao kinaendelea kwa majadiliano ndipo DC alipobaini UFISADI Mkubwa ndani ya soko hilo na uwovu unaofanywa na Viongozi hao ndani ya Soko.

DC Alijilidhisha kwa kikao nakubaini haina haja ya kuendelea na Majadiliano bali Viongozi wa CARGO Potters kwa Kuwa Wamekuwa WAKIFISADI ikiwemo kukusanya Mapato kinyume cha Sheria na taratibu tulizojiwekea.Lakini pia wanakusanya Mapato ambayo hayana maelezo yamatumizi yake.

Lakini Pia Viongozi hawa Wamezuia Wafanyabiashara kufanya Biashara zao jambo ambalo Mh DC limemchukiza sana kwani Limefanya Wakulima Washindwe kuuza Mazao yao kwa Amani.Kulingana na Ufisadi huo DC aliamuru kukamatwa kwa Viongozi hao na kumuagiza OCD Kufuata Taratibu za Kisheria ili Wahojiwe na hatua za Kisheria zichukuliwe kulingana na makosa yao hayo yakifisadi.

DC Kawaeleza Wanakongwa kuwa, Yuko kongwa kwa ajili ya kuijenga Kongwa na kuhakikisha Haki na kila namna ya Uwazi inafanyika pasipokuwa na Upindishaji wa Haki zozote, Sheria, Kanuni na Haki zitafuatwa ili Kutenda Haki kwa Kila Jambo. Lakini Kama Ni Majipu Yatatumbuliwa bila Uwoga kwa Maslai ya Kongwa na Taifa kwa Ujumla.

MKURUGENZI WA JIJI LA ARUSHA AMSIMAMISHA KAZI AFISA MAENDELEO YA JAMII WA JIJI KWA KUSHINDWA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAKE

$
0
0


Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Ndg. Athumani J. Kihamia amempuzisha kutekeleza majukumu yake Afisa Maendeleo ya Jamii wa Jiji Bi. Mwantumu Dosi kwa tuhuma za kushindwa kutekeleza majukumu yake hivyo kukiuka kanuni za Utumishi wa Umma za mwaka 2003.

Mkurugenzi Kihamia ametoa taarifa hiyo leo tarehe 27.08.2016 baada ya kukamilisha mbio za Mwenge wa Uhuru na kufanya tathmini ya miradi iliyopitiwa na Mwenge na kugundulika kwa dosari zilizojitokeza katika moja ya mradi ambao uko chini ya Idara hii.

Mradi huo ni kikundi cha vijana wanaojishughulisha na Uselemara pamoja na Uchomeleaji kinachojulikana kama Mbeshere Umoja Group kilichopo Kata ya Olorieni kiligundulika kuwa na wananchama waliovuka umri wa miaka 35 ambao hawastahili kunufaika  na Mikopo ya Vijana kwa mujibu wa Sera.

Mwenge wa Uhuru katika Jiji la Arusha ulikimbizwa tarehe 24.08.2016 na Kikundi hicho kilikua ni miongoni mwa miradi iliyokua inapitiwa na Mwenge wa Uhuru ambapo wanachama wake hawakizi vigezo. Wanachama hao walikua wameandaliwa kupewa Hundi ya TSH Milioni tano kama ishara ya kuunga mkono jitihada zao zakuboresha maisha.  Mkimbiza Mbio za Mwenge Kitaifa Ndg. George Jackson Mbijima alisitisha zoezi hilo baada ya kugundua dosari za umri kwa baadhi ya wanachama.

Kupumzishwa kutekeleza majukumu ya Mkuu wa Idara hii kunafuatana na masharti ya kukabidhi Ofisi kwa Mratibu wa Tasaf Bi. Tajiel Mahega ambaye kwa sasa atakua Kaimu Mkuu  wa Idara  hii mpaka pale uchunguzi utakapokamilika.

Nteghenjwa Hosseah
Afisa Habari, Halmashauri ya Jiji
Arusha.
27  Agosti,2016 


HATIMAYE LOWASSA USO KWA USO NA JPM LEO KWENYE SHEREHE YA MIAKA 50 YA NDOA YA MZEE MKAPA

$
0
0

 Waziri Mkuu wa Zamani na aliyekuwa Mgombea Urais wa chama cha CHADEMA,Mh.Edward Lowassa akijadiliana jambo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,awamu ya tano,Dk John Pombe Magufuli,mapema leo walipkwenda kushiriki misa ya Jubilei ya Dhahabu ya ndoa ya Rais Mstaafu awamu ya tatu,Mh Benjamin William Mkapa na Mkewe Mama Anna Mkapa jijini Dar leo
 Picha ya pamoja mara baada ya misa hiyo
  Rais Mstaafu awamu ya tatu,Mh Benjamin William Mkapa na Mkewe Mama Anna Mkapa wakifurahia  Jubilei ya Dhahabu ya ndoa jijini Dar leo

HATIMAYE LOWASSA USO KWA USO NA JPM LEO KWENYE SHEREHE YA MIAKA 50 YA NDOA YA MZEE MKAPA

$
0
0

 Waziri Mkuu wa Zamani na aliyekuwa Mgombea Urais wa chama cha CHADEMA,Mh.Edward Lowassa akijadiliana jambo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,awamu ya tano,Dk John Pombe Magufuli,mapema leo walipkwenda kushiriki misa ya Jubilei ya Dhahabu ya ndoa ya Rais Mstaafu awamu ya tatu,Mh Benjamin William Mkapa na Mkewe Mama Anna Mkapa jijini Dar leo
 Picha ya pamoja mara baada ya misa hiyo
  Rais Mstaafu awamu ya tatu,Mh Benjamin William Mkapa na Mkewe Mama Anna Mkapa wakifurahia  Jubilei ya Dhahabu ya ndoa jijini Dar leo

JWTZ KUADHIMISHA MIAKA 52 SEPTEMBA MOSI 2016 KWA KUFANYA USAFI NCHI NZIMA

$
0
0
Jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) limepanga kuadhimisha miaka 52 ya kuanzishwa kwake, kwa kufanya usafi katika maeneo mbalimbali, siku ya maadhimisho hayo Septemba Mosi, 2016.

Habari iliyorushwa na mtandao wa Dar24, imemnukuu msemaji wa JWTZ Kanali Ngemela Lubinga akisema kuwa Jeshi hilo litasherehekea bila kufanya maandamano ya aina yoyote na kwamba linafahamu kuwa Serikali imeshapiga marufuku maandamano siku hiyo.

“Ratiba yetu ni kusherehekea, tunajua serikali imeshapiga marufuku maandamano, lakini sisi kama wanajeshi tutafanya shughuli zetu kamazilivyopangwa”, alisema Lubinga.

JWTZ liliundwa Septemba Mwana 2064baada ya kuvunjwa rasmi kwa jeshi lilorithiwa kutokakwa wakoloni la Tanganyika Rifles.

Taamko hilo la JWTZ imekuja wakati ambapo kumekuwepo na mvutano wa kufanyika akwa maanadamano ya Operesheni ya UKUTA iliyoandaliwa na Chama cha CHADEMA ambayo serikali imeyapiga marufuku.
 

WAZIRI LUKUVI AZINDUA MIRADI YA UPATIKANAJI WA PICHA ZA ANGA

$
0
0

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akizindua miradi ya upatikanaji wa picha za anga na mfumo unganishi wa menegiment ya taarifa za umma (ILMIS) jijini Dar es Salaam jana. Kutoka (kushoto) ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, George Simbachawene, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Yamungu Kayandabila.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akiongea wakati wa uzindua wa miradi ya upatikanaji wa picha za anga na mfumo unganishi wa menegiment ya taarifa za umma (ILMIS) jijini Dar es Salaam jana.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akizindua miradi ya upatikanaji wa picha za anga na mfumo unganishi wa menegiment ya taarifa za umma (ILMIS) jijini Dar es Salaam jana. Kutoka (kushoto) ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, George Simbachawene, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Yamungu Kayandabila.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akijadiliana jambo na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Yamungu Kayandabila (kulia) wakati wa hafla ya uzinduzi huo. Katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Faustine Kamuzora.

Baadhi ya waheshimiwa wabunge na wageni waalikwa waliohudhuria hafla hiyo wakifuatilia uznduzi wa huo.

Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria hafla hiyo wakifuatilia uznduzi wa huo.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akifafanua jambo wakati wa uzindua wa miradi ya upatikanaji wa picha za anga na mfumo unganishi wa menegiment ya taarifa za umma (ILMIS) jijini Dar es Salaam jana.
Baadhi ya waheshimiwa wabunge na wageni waalikwa waliohudhuria hafla hiyo wakifuatilia uznduzi wa huo.
Baadhi ya waheshimiwa wabunge na wageni waalikwa waliohudhuria hafla hiyo wakifuatilia uznduzi wa huo.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, George Simbachawene akisalimiana na Mbunge wa Mpanda Mjini, Sebastian Kapufi na baadhi ya wabunge walihudhuria hafla hiyo. (Imeandaliwa na Robert Okanda blogspot)

KAMANDA SIRRO ATANGAZA KIAMA KWA WANANCHI WATAKAO ANDAMANA SEPTEMBA MOSI JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna wa Polisi (CP), Simon Sirro akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam leo, wakati akitangaza kiama kwa mwananchi yeyote atakayefanya maandamano Septemba Mosi ya kupinga udikiteta Tanzania yaliyoandaliwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Kamanda Sirro akisisitiza jambo kwenye mkutano huo.
Magari ya polisi yenye zaidi ya askari 80 yakiondoka Kituo cha Polisi cha Kati, yakielekea Vikindu kwa ajili ya Operesheni saka majambazi.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Askari wa kikosi maalumu cha kupambana na uhalifu wakiondoka Kituo Kikuu cha Polisi cha Kati kuelekea Vikindu kwa operesheni maalumu ya kuwasaka watu wanaotuhumiwa kwa ujambazi.


Na Dotto Mwaibale

KAMANDA wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna wa Polisi (CP), Simon Sirro ametangaza kiama kwa mwananchi yeyote atakayefanya maandamano Septemba Mosi ya kupinga udikiteta Tanzania yaliyoandaliwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)

“Jeshi la polisi mkoa wa Dar es Salaam tumejipanga vizuri siku hiyo nawaomba wananchi wasidhubuti kujitokeza kuandamana siku hiyo kwani watakiona cha moto” alisema CP Sirro.Sirro alisema tayari jeshi hilo lina taarifa za kiinteligensia kuwa kuna vijana wanapewa fedha kwa ajili ya kuandamana na kufanya fujo Septemba mosi.

Aliwasihi wananchi hasa vijana kutoingia barabarani Septemba mosi na kuwaachia wachache wenye nia ya kuletafujo.“Ni rai yangu wale wananchi wazalendo wan chi hii wasiopenda kupambana na jeshi lao la polisi ambalo linawalinda na kulinda mali zao siku hiyo wasiingie barabarani,” alisema.

Aliwakaribisha wanao taka kuingia barabarani na kupambana na jeshi hilo na kuwa watakamatwa na kufikishwa kwenye mkono wa sheria.“Sisi tupo vizuri na tupo imara hasa kwa wale wanaopenda kuvunja sheria kwa makusudi wata wajibika kwa mujibu wa sheria, hivyo suala la utiiwa sheria bila shuruti ni la msingi sana,” alisema Sirro.

Alisema jeshi hilo limejiandaa kwa wananchi wachache ambapo alibainisha wananchi wengine hawana haja na maandamano hayo huku akibainisha vijana wachache wenye shida kupewa fedha na viongozi kwa lengo la kuandamana.“Jiulize hiyo 40,000 unayo pewa kuingia barabarani na matokeo yake ukavunji kama mguu hiyo 40,000 ina thamani gani kwani… kwa hiyo mimi kama kiongozi wenu wa jeshi la polisi na sisitiza na ninaelekeza tuwaache wale wenye sababu zao binafsi waingie barabarani,” alisema.

Katika hatua nyingine Kamanda Sirro alisema askari zaidi ya 80 wa kikosi maalumu cha kupambana na uhalifu wameondoka kwenda vikindu na maeneo mengine wilayani Mkuranga mkoani Pwani kufanya operesheni ya kuwasaka watu wanaodhaniwa kujihusisha na ujambazi.

WIZARA YA ELIMU SAYANSI NA TEKNOLOJIA YAELEKEZA NGUVU YA UFUNDISHAJI MTAALA WA KKK.

$
0
0


Na Chalila Kibuda. Globu ya Jamii.

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imewajengea uwezo wathibiti ubora wa shule 1,469 ili wapate umahiri wa kusimamia kwa ufanisi ufundishaji na ujifunzaji bora unaozingatia umahiri wa Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK).

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Idara ya uthibiti ubora wa shule nchini, Marystella Wasena alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya mikakati ya Idara hiyo katika kukagua na kusimamia utekelezaji wa ufundishaji wa kusoma , kuandika na kuhesabu katika shule za awali na msingi nchini.

“Kipindi cha mwaka wa fedha 2015/2016 Idara ilifanya tathmini ya mafanikio ya utekelezaji wa mtaala ambapo shule za Msingi 6,831 zilikaguliwa na ilibainika kuwepo kwa wanafunzi 10,273 (wakiume 5,010 na wakike 5,263) wasiojua kusoma wala kuandika katika shule za Msingi 515,” alifafanua Wasena.

Marystella amesema tathmini hiyo imebainisha sababu zinazotokana na wanafunzi wenyewe kushindwa kumudu kujifunza kwa umahiri husika na sababu zinazotokana na utekelezaji wa mtaala ikiwemo ukosefu wa walimu wa kufundisha KKK.

Amesema ili kuondokana na tatizo la wanafunzi kutojua kusoma na kuandika, kila kanda na kila wilaya zimeteua shule mbili za mfano zikiwemo za Serikali na Binafsi ili kuhakikisha wathibiti ubora wa shule wanafanya ufuatiliaji wa KKK katika shule hizo kwa kutoa msaada wa kitaalamu kwa walimu kuhusiana na changamoto za ufundishaji na ujifunzaji mahiri wa KKK.

Aidha Marystella amefafanua kuwa, Idara kupitia mpango wa LANES imeongeza idadi ya magari katika wilaya 38 yatakayotumika kwa ajili ya ukaguzi wa shule za awali, Msingi na Sekondari ambapo idara hiyo imepanga kukagua shule 8426 za awali na Msingi na Sekondari shule 2392 ili kuona utekelezaji wa KKK pamoja na kutoa msaada kwa walimu kufundisha kwa ufasaha kulingana na malengo ya Mtaala husika.

Hata hivyo Idara hiyo ina mkakati wa kufanya tafiti mbalimbali katika shule za Awali, Msingi na Sekondari kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ili kuona utekelezaji wa Mtaala wa KKK na kutoa mapendekezo sahihi ya kuondoa changamoto na kutoa ushauri kwa Walimu, Wakuu wa Shule, Maafisa Elimu, wamiliki wa Shule, Kamishna wa Elimu na Wadau wa Elimu.

RAIS DKT MAGUFULI AHUDHURIA MISA YA JUBILEI YA DHAHABU YA NDOA YA RAIS MSTAAFU BENJAMIN MKAPA NA ANNA MKAPA

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu wa zamani Mhe Edward Lowassa wakati wa Misa ya Jubilei ya Dhahabu ya ndoa ya Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016 Misa ya Jubilei ya Dhahabu ya ndoa ya Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016
LO2
LO3
Paroko  akisimamia ukumbusho wa ahadi za ndoa wakati wa Misa ya Jubilei ya Dhahabu ya ndoa ya Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016
LO4
Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa wakipokea hati maalumu ya ndoa toka kwa   ASKOFU Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo  wakati wa Misa ya Jubilei ya Dhahabu ya ndoa ya Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016
LO5
Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa akitoa shukurani  wakati wa Misa ya Jubilei ya Dhahabu ya ndoa yake na  na Mama Anna Mkapa katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016
LO6
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akitoa salamu zake za pongezi  wakati wa Misa ya Jubilei ya Dhahabu ya ndoa ya Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016
LO7
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli katika picha ya pamoja viongozi wa dini na viongozi wastaafu na wake zao  wakati wa Misa ya Jubilei ya Dhahabu ya ndoa ya Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016
LO8
LO9
Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa  wakikata keki  katika hafla ya chakula cha mchana waliyoandaa baada ya Misa ya Jubilei ya Dhahabu ya ndoa yao  katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016
LO10
Katibu Mkuu wa CCM Ndg Abdulrahman Kinana akiteta jambo na Waziri Mkuu wa zamani Mhe Edward Lowassa wakati wa hafla ya chakula cha mchana baada ya Misa ya Jubilei ya Dhahabu ya ndoa ya Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndg Abdulrahman Kinana akimueleza jambo Waziri Mkuu wa zamani Mhe Edward Lowassa wakati wa hafla ya chakula cha mchana baada ya Misa ya Jubilei ya Dhahabu ya ndoa ya Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndg Abdulrahman Kinana akimsikiliza Waziri Mkuu wa zamani Mhe Edward Lowassa wakati wa hafla ya chakula cha mchana baada ya Misa ya Jubilei ya Dhahabu ya ndoa ya Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016.

=======  =====  ========
RAIS MSTAAFU BENJAMIN WILLIAM MKAPA AADHIMISHA JUBILEI YA MIAKA 50 YA NDOA.

Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa leo tarehe 27 Agosti, 2016 ameadhimisha Jubilei ya Dhahabu ya Miaka 50 ya Ndoa yake na Mama Anna Mkapa katika kanisa la Mtakatifu Petro lililopo Oysterbay Jijini Dar es Salaam.

Hafla ya Jubilei hiyo imefanyika nyakati za mchana katika ukumbi wa Kardinali Rugambwa uliopo kando ya kanisa la Mtakatifu Petro-Oysterbay na imetanguliwa na Misa ya shukrani iliyofanyika katika kanisa hilo majira ya asubuhi.

Jubilei hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli, Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu wa Awamu ya Sita wa Zanzibar Dkt. Amani Abeid Karume, Mke wa Baba wa Taifa Mama Maria Nyerere, Mawaziri Wakuu Wastaafu Mhe. Cleopa Msuya, Dkt. Salim Ahmed Salim, Jaji Joseph Warioba na Mhe. Edward Lowassa.

Misa Takatifu ya Shukrani imeongozwa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Arusha Mhashamu Askofu Josephat Lebulu na kuhudhuriwa na Maaskofu na Maaskofu Wakuu saba akiwemo Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo.

Akizungumza baada ya kumalizika kwa Misa Takatifu Rais Magufuli amempongeza Rais Mstaafu Benjamin William Mkapa kwa kutimiza miaka 50 ya ndoa na ameeleza kuwa ndoa hiyo iliyowaunganisha wanandoa wanaotoka katika madhehebu tofauti ya Kikristo imetoa fundisho kubwa kuwa binadamu wanapaswa kuwa wamoja hata kama wana tofauti mbalimbali zikiwemo za kimadhehebu ya dini, siasa na kanda.

Rais Magufuli amesema miaka 50 ya ndoa ya Mhe. Benjamin William Mkapa ambaye ni Muumini wa Kanisa Katoliki na Mkewe Mama Anna Mkapa ambaye ni Muumini wa Kanisa la Kilutheri inawafundisha watanzania wote hususani wanasiasa kuishi kwa upendo na kuilinda amani waliyonayo na ametoa wito kwa viongozi dini kuendeleza juhudi zao za kuliombea taifa na kuwaunganisha wananchi licha ya tofauti walizo nazo.

Kwa upande wake Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa pamoja na kuwashukuru Viongozi wote, ndugu, jamaa na marafiki waliohudhuria Misa ya Shukrani na Jubilei hiyo ya miaka 50 ya ndoa yake amemshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuijaalia ndoa yake umri mrefu.

Rais Mstaafu Mkapa pia ametoa wito kwa watanzania kupenda na kushirikiana huku akibainisha mafunzo aliyoyapata kutoka kwa viongozi wa dini kuwa "Kila mmoja ni zawadi kwa mwenzake"

Nae Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo amempongeza Rais Mstaafu Mkapa na Mkewe Mama Anna Mkapa kwa kuadhimisha miaka 50 ya ndoa na amewasihi watanzania kuiga mfano mwema uliooneshwa na wana ndoa hao ambao wamedumu katika imani bila kuyumba.

Kardinali Pengo amesema ndoa ya Rais Mstaafu Mkapa anaifundisha jamii kuwa tunaweza kuishi kwa imani zetu bila kubadili dini.

TAARIFA YA MSIBA WA HANIFA SEKIBO

$
0
0
 Familia ya Marehemu Mossey Abdulsalim Sekibo,  Wa Motel Villa, Kijitonyama,  Inasikitika kutangaza kifo cha Binti yao Hanifa Sekibo,  Kilichotokea jana katika Hospitali ya Temeke. 

Ratiba ya Leo. 

Saa 4:00-Mwili kuwasili nyumbani  kwa Mama  wa Marehemu, Bi Gile, Mbezi Makabe.
Saa 5:00-Kusomewa Dua
Saa 6:00-Chakula 
Saa 7:00- Marehemu ataswaliwa Msikiti wa Mangara Baada ya Swalat Adhuhuri. 
Saa 8:00- Msafara kuelekea Bagamoyo. 
Saa 10:00-Maziko Makaburi ya Familia ya Sekibo, Kiromo Shule, Bagamoyo.
Saa 11:00- Msafara kurejea kwa Tanga Ndugu.

Marehemu ameacha mtoto mmoja, Grace-Linda Pascal Mayalla na mjukuu mmoja Sarrah-Patricia. 
Innalilah Wainnailaih Rajiun.

 Kufika  msibani kutokea Mbezi mwisho Stendi Mpya. Fuata njia ya Makabe Msakuzi mpaka njiapanda ya Makabe.  Ulizia Msikitini kwa Mangara.

Kwa kuanzia Bagamoyo Rd. Njia ya Goba hadi njia panda ya Makabe .
 
Kwa Maelezo zaidi
Contact 
1.Kaka wa Marehemu-Haji Sekibo -0713 866 480
2. Dada wa Marehemu -Masha Sekibo 0719226422.

MUNGUA AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI  PEMA PEPONI-AMIN

JWTZ YAKABIDHI VIKOMBE KWA MKUU WA MAJESHI

$
0
0

Brigedia Jenerali Alfred kapinga kwa niaba ya Mkuuu wa majeshi Akipokea bendera toka kwa mkurugenzi wa michezo kutoka makao makuu ya JWTZ ikiwa ni ishara ya kurejea baada ya kumalizika Mashindano ya majeshi kwa Nchi za Afrika mashariki yaliyofanyika Rwanda Hivi karibuni, zoezi la kukabidhi vikombe na bendera ilifanyika katika ukumbi wa Twalipo Mgulani Jijini Dar es Salaam. 

Brigedia Jenerali Alfred kapinga akipokea kikombe kwa niaba ya Mkuu wa Majeshi toka kwa Nahodha wa Timu ya Soka Koplo Stanslaus Mwakitosi walichoshinda katika Mashindano ya majeshi kwa Nchi za Afrika mashariki yaliyofanyika Rwanda Hivi karibuni, zoezi la kukabidhi vikombe na bendera ilifanyika katika ukumbi wa Twalipo Mgulani Jijini Dar es Salaam. 
Brigedia Jenerali Alfred kapinga akiongea na wanamichezo wakati wa hafla ya kukabidhi vikombe na bendera mara baada ya kumalizika Mashindano ya majeshi kwa Nchi za Afrika mashariki yaliyofanyika Rwanda Hivi karibuni, zoezi la kukabidhi vikombe na bendera ilifanyika katika ukumbi wa Twalipo Mgulani Jijini Dar es Salaam.
Brigedia Jenerali Alfred kapinga akipokea kikombe kwa niaba ya Mkuu wa Majeshi toka kwa Nahodha wa Timu ya Netball Dorita Mbunda walichoshinda katika Mashindano ya majeshi kwa Nchi za Afrika mashariki yaliyofanyika Rwanda Hivi karibuni, zoezi la kukabidhi vikombe na bendera ilifanyika katika ukumbi wa Twalipo Mgulani Jijini Dar es Salaam.
Brigedia Jenerali Alfred kapinga kwa niaba ya Mkuuu wa majeshi Akipokea bendera toka kwa mkurugenzi wa michezo kutoka makao makuu ya JWTZ ikiwa ni ishara ya kurejea baada ya kumalizika Mashindano ya majeshi kwa Nchi za Afrika mashariki yaliyofanyika Rwanda Hivi karibuni, zoezi la kukabidhi vikombe na bendera ilifanyika katika ukumbi wa Twalipo Mgulani Jijini Dar es Salaam. 
Baadhi ya Wachezaji wa Timu teule za jeshi walioshiriki Mashindano ya majeshi kwa Nchi za Afrika mashariki yaliyofanyika Rwanda Hivi karibuni, wakimsikiliza Brigedia jenerali Alfred kapinga (hayuko Pichani) wakati wa zoezi la kukabidhi vikombe na bendera ilifanyika katika ukumbi wa Twalipo Mgulani Jijini Dar es Salaam
Baadhi ya Wachezaji wa Timu teule za jeshi walioshiriki Mashindano ya majeshi kwa Nchi za Afrika mashariki yaliyofanyika Rwanda Hivi karibuni, wakimsikiliza Brigedia jenerali Alfred kapinga (hayuko Pichani) wakati wa zoezi la kukabidhi vikombe na bendera ilifanyika katika ukumbi wa Twalipo Mgulani Jijini Dar es Salaam. picha na Luteni Selemani Semunyu) 


Na Luteni Selemani Semunyu JWTZ .

Timu teule za Jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania zilizowakilisha nchi katika mashindano ya majeshi kwa nchi za Afrika Mashariki zimekabidhi kwa bendera na Vikombe ilivyonyakua wakati wa mashindano yaliyofanyika  Kigali nchini Rwanda. 

Akipokea Bendera na Vikombe kwa Niaba ya Mkuu wa majeshi ya ulinzi Brigedia Jenerali Alfred Kapinga alisema ushindi uliopatika ni faraja kwa watanazania na jeshi hivyo ni vyema kwa wanamichezo kujipongeza hasa ukizingatia ushindani mkubwa . 

“Ushindi ni Ushindi hivyo hakuna budi kujipongeza kwa kuwa washindi kwani vikombe vitat u vilivyopatika ni faraja na hasa kikombe cha Mpira wa pete ambacho tulikipoteza mwaka jana na kuchukuliwa na Uganda”,Alisema Brigedia kapinga. Pia alizitaka Timu kuanza maandalizi kwa ajili ya mashindano yajayo lakini pia kujiweka sawa kwa mashindano yatakayoshirikisha vyombo vya ulinzi na usalama ili kuibuka na ushindi zaidi ya ilivyokuwa sasa. 

Aliongeza kuwa hakika jeshi limeamua kurejesha heshima yake kama ambavyo mkuu wa majeshi aliagiza katika michuano hiyo. Pia aliwapongeza waandishi wa habari wa kushirikiana na JWTZ na kuwataka kuendeleza ushirikiano huo kwani JWTZ ni timu ya Ushindi hivyo nao ni washindi na vivyo hivyo kwa wadhamini ambao amewaomba kuendeleza ushirikiano wao katika kuchangia mafanikio ya michezo kwa jeshi. 

Kwa upande wake Mkurugenzi wa michezo kutoka makao makuu ya JWTZ Brigedia Jenerali martin Busungu ameshukuru kwa ushirikiano na kuwapongeza wote waliofanikisha ushiriki wa JWTZ katika mashindano hayo na kuahidi kufanya vizuri zaidi katika mashindano yajayo. 

Alisema katika mashindano hayo waliyoshiriki michezo mitano ambAYO NI Riadha mpira wa Miguu, mpira wa pete ,mpira wa mikono na mpira wa kikapu ambapo katika mpiwa wa miguu JWTZ imeshika nafasi ya tatu, Riadha Wanawwake nafasi ya tatu na Mpira wa pete nafasi ya kwanza na mchezaji Bora ambaye alikuwa na Nasra Suleiman. 

Mbali na zoezi la kukabidhi vikombe pia bendera iliyokabidhiwa kwa wanamichezo hao imerejeshwa kuashiriia mwisho wa jukumu hilo walilokabidhiwa la kupeperusha vyema bendera ya taifa .

WAZIRI LUKUVI: SERIKALI TUMEDHAMIRIA KUMALIZA MIGOGORO YA ARDHI

$
0
0
Na Sheila Simba- MAELEZO

Waziri wa Aridhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amesema kuwa Serikali imeanza kazi ya kupima ardhi  nchi nzima kuanzia mkoani Morogoro.

Akizungumza  katika kipindi kipya cha "TUNATEKELEZA" kinachoandaliwa na Idara ya Habari-MAELEZO na TBC1 ,alisema utekelezaji wa zoezi hilo umeanzia mkoani humo ili kupima maeneo ya wakulima na wafugaji na kutatua migogoro ya ardhi Mkoani humo.

“Serikali tumedhamiria kumaliza migogoro ya ardhi, kutimiza ndoto ya Rais Magufuli ya kuondokana na migogoro ya ardhi isiyo na tija inayosababisha watu kupoteza maisha’’Alisema Lukuvi

 Ameongeza kuwa katika upimaji huo wa ardhi serikali inashirikiana na kampuni binafsi zilizosajiliwa ili kumuwezesha mwananchi anayemiliki shamba,kiwanda ,mkulima na mfugaji mwenye eneo  kupimiwa na kuongezewa thamani.

 “Nakuhakikishia katika kipindi cha miaka 10 kila kipande cha ardhi Tanzania kitakuwa kimepangwa na kupimwa utaratibu mzuri utakao mwezesha kila mtumiaji wa ardhi kutumia eneo lake”alifafanua Lukuvi.

Pia ameeleza suala la kuthibiti bei ya kupima ardhi kwa kushirikiana na wapimaji binafsi katika kumfanya kila mtanzania alipe bei halali ya kupima ardhi.Aidha amesme kuwa Serikali itaweka ukomo wa kumiliki ardhi ili kuondoa tabia za watu kumiliki eneo kubwa la ardhi bila ya kuliemdeleza kwa muda mrefu.

“serikali itaweka muda wa mtu kumiliki ardhi, haiwezekani mtu mmoja amiliki eneo hata bila kulitumia, tabia hii itafika mwisho.”Akizungumzia suala la wageni kumiliki ardhi alisema kuwa ni marufuku kwa wageni na wawekezaji kununua ardhi vijijini bila kupitia wizara inayohusika.

“Ni marufuku kwa mgeni au mwekezaji kwenda kijijini kununua ardhi bila kuja kwangu au Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC),wakifanya hivyo tutawapa ardhi wawekeze, Pia mtu yeyote anayetaka kujenga kiwanda popote afike ofisini kwangu nitampatia ardhi ndani ya siku saba.”alisema Lukuvi

Ameongeza kuwa  Wizara imetenga viwanja 240 kwa ajili ya Viwanda eneo la Kigamboni ili kutimiza lengo la Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa viwanda.Mbali na hayo Waziri Lukuvi alisema  wananchi wote waliodhulumiwa viwanja Jijini Dar es Salaam kwa makosa ya watendaji wa Serikali wameanza kupewa  viwanja vingine mbadala.

“Naagiza Halmashauri zote ziwapatie viwanja mbadala wananchi ambao walidhulimiwa viwanja vyao kwa makosa ya watendaji.”
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live




Latest Images