Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live

GAZETI LA MTANDAONI LA NCHI YETU


PSPF YAKABIDHI VIFAA VYA MICHEZO KWA JESHI LA MAGEREZA UKONGA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0

Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Abdul Njaidi, (kushoto), akimkabidhi sehemu ya vifaa vya michezo, Mkuu wa Kikosi Maalum cha Jeshi la Magereza Ukonga jijini Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Rajabu Nyange Bakari, Agosti 25, 2016. Vifaa hovyo ni vya michezo ya ngumi, mpira wa miguu na mpira wa pete.

Afisa Masoko wa PSPF, Magira Werema, (kushoto), akimkabidhi sehemu ya vifaa hivyo, Mkuu wa Kikosi Maalum cha Jeshi la Magereza Ukonga jijini Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Rajabu Nyange Bakari.

NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID

MFUKO wa Pensheni wa PSPF, umekabidhi vifaa vya michezo kwa wanamichezo wa Jeshi la Magereza Ukonga jijini Dar es Salaam na kasha kufuatiwa na PSPF bonanza la michezo ya mpira wa miguu, mpira wa pete, Ngumi na Judo.

Akikabidhi vifaa hivyo vya michezo Agosti 25, 2016, Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Abdul Njaidi, alisema, PSPF imeamua kutoa vifaa hivyo ili kuunga mkono juhudi za serikali katika kuinua michezo nchini.

“Nyinyi mkiwa kama sehemu kubwa ya wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, tunayo furaha kutoa vifaa hivi vya michezo kwani baada ya kutekeleza majukumu mazito ya kitaifa mnahitaji kushiriki michezo ili kujenga afya lakini pia kuinua vipaji vyenu,” alisema na kuongeza,

“Nichukue fursa hii kuwahamasisha mjiunge na PSPF kwani kuna faida nyingi mtapata kutokana na kutoa mafao mbalimbali yatakayoboresha maisha yenu kama ambavyo kauli mbiu yetu inavyosema, PSPF ni chaguo lako sahihi na kamwe hutajutia uamuzi wako wa kujiunga na Mfuko huu.” Alisisitiza Njaidi.

Akipokea vifaa hivyo kwa niaba ya wanamichezo hao, Mkuu wa Kikosi Maalum cha Magereza-Ukonga, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Rajabu Nyange Bakari, aliishukuru PSPF kwa msaada huo wa vifaa vya michezo kwani vitawawezesha wanamichezo hao kushiriki michezo katika mazingira bora ya kiuanamichezo. Baada ya makabidhiano hayo, wanamichezo hao walionyesha uwezo wao katika michezo ya mpira wa miguu, ngumi, mpira wa pete, na judo.
Afisa Matekelezo (Compliance), wa PSPF, George Mnasizu, (kushoto), akigawa vipeperushi vyenye maelezo ya kina ya huduma zitolewazo na Mfuko huo kwa baadhi ya wanamichezo wa Jeshi la Magereza
Njaidi akiwa na Mkuu wa Kikosi hicho, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Kikosi Maalum cha Magereza Ukonga jijini Dar es Salaam, Rajabu Nyange Bakari, na wacheza judo wa kikosi hicho wakiwa katika picha ya pamoja na vipeperushi vya PSPF.
Njaidi akimkabidhi sehemu ya vifaa hicho, Nahodha wa timu ya mpira wa pete (Netball), wa timu ya Magereza Ukonga, Pili Enzi
Werema akimkabidhi sehemu ya vifaa hivyo kocha wa soka wa timu ya Magereza, Sajenti Hassan Mulego
Njaidi akikagua timu ya soka ya Magereza Ukonga, ambayo ilimenyana na Kikosi Maalum cha Magereza Dar es Salaam, wakati wa bonanza hilo la michezo
Soka likiendelea baina ya Kikosi Maalum na timu ya Magereza

Soka likiendelea baina ya Kikosi Maalum na timu ya Magereza



Soka likiendelea baina ya Kikosi Maalum na timu ya Magereza


Hizi ndio Gloves na flana zilizotolewa kwa wana masumbwi (ngumi)
Pambano la masumbwi likiendelea
Pambano la masumbwi likiendelea
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Abdul Njaidi, akiwa na Mkuu wa Kikosi Maalum cha Magereza jijini Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Rajabu Nyange Bakari, wakati akitoa nasaha kwa wanamichezo kabla ya kuanza kwa bonanza hilo

Nasaha za mgeni rasmi kwa wanamichezo
Wanamichezo wakishangilia hotuba
Onyesho la Judo
Werema akimkabidhi sehemu ya vifaa hivyo vya michezo, Kocha na Afisa Michezo wa Kikosi Maalum cha Magereza Dar es Salaam, Inspekta Francis Tabu
Soka likiendelea baina ya Kikosi Maalum na timu ya Magereza
Mkuu wa Kikosi Maalum cha Jeshi la Magereza Ukonga jijini Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Rajabu Nyange Bakari.
Picha ya pamoja

WATANZANIA TUPAZE SAUTI KUKATAA MAANDAMANO YA SEPTEMBA MOSI-CHEYO

$
0
0
Mwenyekiti wa UDP Mh. John Cheyo akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani)kwenye ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO mapema leo jijini Dar,akiwaomba viongozi wa chama cha CHADEMA,Kusitisha maandamano yao waliyoyapa jina la UKUTA,wanayotarajia kuyafanya Septemba Mosi nchi nzima,Mh Cheyo amekiomba chama hicho kutofanya maandamano hayo kwa lazima na badala yake watumie njia ilio sahihi ambayo ni ya mazungumzo ya mezani na kuendelea kuitunza amani ya nchi iliopo,pia amewaomba Watanzania kupaza sauti zao kuyakataa maandamano hayo yanayoweza kuharibu amani na utulivu wa nchi yetu.Pichani kulia ni Kaimu Katibu MKuu wa chama hicho Mh,Goodluck Ole Medeye.

"Ukitaka kufanya maandamano,vyombo vya usalama vikikukatalia,basi usitumie nguvu,jaribu kutafauta njia nyingine ambayo itakuwa ya amani zaidi kuliko kulazimisha,jambo ukililazimisha bila kufuata taratibu na sheria za nchi,matokeo yake hayatakuwa mazuri,yataleta machafuko na kutia doa amani ya nchi yetu ambayo tumekuwa tukijivunia,hivyo nawasihii ndugu zangu wa CHADEMA bado kuna njia nzuri za kufuata na kufikia muafaka wa jambo hilo bila kusumbua amani ya nchi yetu iliopo kwa sasa" alisema Mh Cheyo.
Mh,Cheyo akisitiza jambo wakati alipokuwa akijiabu maswali mbalimbali ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo wa kukitaka chama cha CHADEMA kusitisha maandamano yake,kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari MAELEZO,Vicent Tinganya.PICHA NA MICHUZI JR.


Na: Lilian Lundo-MAELEZO
Dar Es Salaam

Mwenyekiti wa Chama cha UDP John Cheyo amewataka Watanzania kupaza sauti na kukataa maandamano ya Septemba Mosi mwaka huu ambayo yameandaliwa na Chama cha Demokrasia (CHADEMA).

Cheyo ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusu msimamo wake juu ya maandamano hayo.

“Watanzania wenzangu jambo la kuwaacha watoto wetu kwenda kupambana na Polisi si jambo zuri, wote tupaze sauti zetu na kusema hapana kwa maandamano ya Septemba Mosi,” alisisitiza Cheyo.

Alisema kuwa, ziko njia mbalimbali ambazo Chadema wanaweza kuzitumia kutatua migogoro, kama vile meza ya mazungumzo na kuachana na maandamano ambayo yanachochea vurugu na hata kutishia amani ya nchi.

Aliongeza kuwa Jeshi la Polisi linapotoa katazo la maandamano ni lazima utii uwepo, kwani Polisi wapo kwa mujibu wa Sheria na Katiba. Ikiwa Chama hicho hakikuridhika na katazo hilo basi wanatakiwa kuonana na Waziri anayehusika na Jeshi la Polisi.

Akifafanua zaidi alisema kuwa Rais Magufuli amekuwa akichukua hatua za makusudi za kutatua matatizo mbalimbali kama vile kupambana na ufisadi, ambapo viongozi wengi wa Serikali wamesimamishwa kazi au kufukuzwa kutokana na kujihusisha na masuala ya rushwa.

Mwenyekiti huyo wa UDP amewataka watanzania kumuunga mkono Mhe. Rais Magufuli ili aweze kutimiza ndoto zake na yale ambayo ameyaahidi kwa ajili ya nchi ya Tanzania.

Aidha Cheyo aliwasifu viongozi wa Dini ambao walikaa na Viongozi wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) na kukubali kurudi bungeni bila pingamizi lolote. Amewataka viongozi hao wa dini kuendelea kuzungumzia suala la amani kwa Watanzania na Viongozi wa kiasa ili kudumisha amani ya nchi.

Tahadhari ya msanii nguli wa Bongo movies, GABO ZIGAMBA, kuhusu matapeli wanaotumia jina lake

$
0
0
Msanii nguli wa Bongo Movies, Gabo Zigamba, anatoa tahadhari kuhusu matapeli mbalimbali wanaotumia jina lake. Awali, msanii huyo alipoteza simu mbili za mkononi, ambazo baadaye zilikuwa zikitumiwa na matapeli hao kuomba misaada kwa watu mbalimbali wakijifanya kuwa wao ndio Gabo.
Kadhalika, majuzi, akaunti ya Facebook ya msanii huyo ilidukuliwa na ikatumika kwa muda na matapeli hao kwa kujifanya wao ndio msanii huyo. Hatimaye alifanikiwa kuirejesha akaunti hiyo katika himaya yake.
Gabo ameeleza kuwa anahisi kuwa yeye ndio msanii anayeongoza kwa jina lake kutumiwa na matapeli kwa sababu amekuwa akipata taarifa mbalimbali kuhusu watu wanaotumia jina lake, kwa mfano binti mmoja aliyejifanya ndiye Gabo na amekuwa akitapeli kwa kudai anauza mabegi.

Msanii huyo ametoa wito kwa Watanzania kuwa makini na watu wanaotumia majina ya watu wengine, hususan watu maarufu, kwa minajili ya kutapeli. Amesema kuwa yupo katika mchakato wa uzinduzi mpya wa akaunti zake mbalimbali za mitandao ya kijamii ili, pamoja na sababu nyingine, iwe rahisi kwa watu kuwasiliana nae pindi wanapokumbana na matapeli hao wanaotumia jina lake.

Balozi Mpya wa Uingereza nchini awasili Jijini Dar

$
0
0
Bibi Sarah Cooke, Balozi mpya (Mteule) wa Uingereza nchini Tanzania amewasili jana 25 Agosti, 2016 Dar es Salaam.

Bi. Cooke amechukua nafasi iliyoachwa wazi na Bi.Dianna Melrose (ambaye amestaafu) na ni mwanamke wa tatu kushika nyadhifa ya ubalozi kuiwakilisha Uingereza nchini Tanzania.

Bi Cooke alijiunga na Utumishi Uingereza mnamo mwaka 2002. Alifanya kazi kadha wa kadha katika idara za Serikali ya Uingereza ikiwemo Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Uingereza (DFID), Wizara ya Mambo ya Nje na Kitengo cha Mikakati cha Waziri Mkuu katika Ofisi ya Baraza la Mawaziri. Pia alipata kuhudumu kama Makamu Mkuu wa Tume ya Sekretariati ya Africa. 

Hivi karibuni, alikuwa ndiye Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo (DFID) nchini Bangladesh. Kabla ya kujiunga Utumishi katika Serikali ya Uingereza, alipata kufanya kazi kama Mchumi jijini London, Guyana na visiwa vya Solomoni.

Juu ya uteuzi wake, Bi.Cooke alisema; “Nimefurahi na ni heshima kubwa kwangu kupewa jukumu hili jipya kama Balozi wa Uingereza nchini Tanzania. Uingereza na Tanzania inafurahia mahusiano na ushirikiano wa muda mrefu na kufanya kazi kwa karibu katika maeneo mengi ambayo tunashabihiana katika vipaumbele ikiwemo biashara, uwekezaji, maendeleo na usalama. Nina dhamiria kuimarisha ushirikiano huu bora zaidi na nina taraji kuijua vyema Tanzania na watu wake”

Waziri Lukuvi afanya ziara eneo la Pugu jijini Dar es Salaam

$
0
0
Afisa Tarafa wa Ukonga Bw. Jeremiah Makorere akifafanua jambo kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi wakati wa ziara ya waziri huyo kubaini migogoro mbalimbali ya ardhi katika eneo la Pugu Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akizungumza na wananchi wa Mtaa wa Guluka Kwalala kata ya Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam ambao wamevamia eneo la Kilichokuwa kiwanda cha nguo cha KiliTex.

Mmoja ya Fundi gereji katika Mtaa wa Guluka Kwalala kata ya Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam Bw. Mohamed Ali akielezea sababu za wao kuvamia eneo la Kilichokuwa kiwanda cha nguo cha KiliTex kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi (hayupo pichani).
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akimsikiliza kwa makini Afisa Ardhi toka Manispaa ya Ilala Bw. Furaha Mwakapalila akielezea historia ya eneo la Kilichokuwa kiwanda cha nguo cha KiliTex ambalo kwa sasa limevamiwa na mafundi magari wa kata ya Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam.

MAKABIDHIANO YA UWANJA WA UHURU-DAR ES SALAAM

UHALIFU MTANDAO NA ATHARI KIUCHUMI

$
0
0

Yapo maeneo mengine ambayo yanaweza kuathiriwa vibaya na uhalifu mtandao – UCHUMI, ni moja ya eneo muhimu ambalo wahalifu mtandao wanaweza kuliletea athari. Aidha, Unapotazama kinacho wapelekea wahalifu mtandao kufanya uhalifu moja wapo ni kujipatia fedha.

Ni wazi kua Raisi wa awamu ya Tano ana pambana kwa dhati kuhakiki wa Tanzania wanaondokana na umasikini ulio kithiri ambapo anaendelea kuchukua jitihada na hatua mbali mbali hadi sasa.

Mfano: Kumekua na uhimizaji mkubwa wa ukusanyaji wa kodi ki elektriniki – Kwa njia ya mtandao ambapo amesisitiza anataka aone TEHAMA inatumiwa vizuri katika eneo hili ili kuhaliki hakuna upotevu wa pesa katika ukusanyaji wa kodi Nchini.

Aidha, Mabenki yameendelea kuboresha mifumo ya Kimtandao kuhakiki miamala inafanyika zaidi kupitia mtandao na nikitolea mfano, mabenki Nchini yamekua yaki hamasisha huduma mtandao kama vile (Huduma za kifedha kupitia simu, kutumia kadi zetu kufanya manunuzi pamoja na matumizi ya mashine za kutolea fedha “ATM”)


Makampuni ya simu nayo hayajakubali kubaki nyuma – Yame hakiki yanaingiza huduma inayoshika kasi zaidi Nchini ya kuweza kufanikisha miamala ya kifedha kupitia simu zetu (Mobile money) ambapo wana nchi wengi wameendelea kuona huduma hizi ni rahisi na wengi wanazitumia.

Maeneo mengine nayo yameona huu ndio muelekeo – Mabasi ya mwendo kasi yamehamasisha miamala kufanyika kwa kadi, huku ulipaji wa bili mbali mbali nao kuendelea kufanyika kupitia mitandao.

Hali hii ni nzuri sana – Kitendo cha mtu kuweza kufanya miamala ya kifedha bila kuhangaika kutoka shemu moja kwenda nyingine kunapelekea uokoaji wa muda na kuongeza ufanisi kwa tunayo yafanya. LAKINI – Je, Upande wa pili wa shilingi, kuna jitihada zozote tumechukua kuangazia? Hapa nazungumzia wahalifu mtandao ambao pia wana uwezo mkubwa wa kupelekea upotevu mkubwa wa pesa tunazozizungusha mitandaoni.

Ni mara ngapi tumekua tukiathirika kimtandao kunapo pelekea kupoteza pesa zetu, bila kujadiliwa kwa sura ya kipekee? Kuna wanao lalama bila kufata taratibu juu ya kupotelewa kwa fedha, na kuna wanao potelewa bila kujua na pia kuna wanao dai wametoa taarifa lakini hakuna matokeo chanya.

Taasisi za kifedha nazo si kweli kua hazi kubwi na kadhia ya upotelewaji wa fedha kupitia mitandao, Lakini ni Aghalab kusikia haya yakizungumzwa na kujadiliwa kwa kina. 
 

NMB YAWAKUTANISHA KATIKA SIKU YA WAALIMU 'TEACHERS DAY' JIJINI DAR LEO.

$
0
0

Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mbando ambaye ni mgeni rasmi akizungumza na walimu wanachama wa Chama cha Walimu Tanzania jijini Dar es Salaam katika maadhimisho ya siku ya walimu 'Teachers Day', Benki ya NMB imewakutanisha walimu katika maadhimisho hayo na kuwapa semina ya masuala anuai ya kibenki.Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mbando (wa tatu kushoto) pamoja na Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam na Zanzibar, Bi. Vicky Bishubo (wa pili kulia) wakionesha ujumbe wa maadhimisho mara baada ya kuzindua hafla ya maadhimisho ya siku ya walimu 'Teachers Day'. Benki ya NMB imewakutanisha walimu katika maadhimisho hayo na kuwapa semina ya masuala anuai ya kibenki.Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mbando (wa tatu kushoto) pamoja na Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam na Zanzibar, Bi. Vicky Bishubo (wa pili kulia) wakionesha ujumbe wa maadhimisho mara baada ya kuzindua hafla ya maadhimisho ya siku ya walimu 'Teachers Day'. Benki ya NMB imewakutanisha walimu katika maadhimisho hayo na kuwapa semina ya masuala anuai ya kibenki.Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mbando ambaye ni mgeni rasmi akizungumza na walimu wanachama wa Chama cha Walimu Tanzania jijini Dar es Salaam katika maadhimisho ya siku ya walimu 'Teachers Day', Benki ya NMB imewakutanisha walimu katika maadhimisho hayo na kuwapa semina ya masuala anuai ya kibenki.Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mbando ambaye ni mgeni rasmi akizungumza na walimu wanachama wa Chama cha Walimu Tanzania jijini Dar es Salaam katika maadhimisho ya siku ya walimu 'Teachers Day', Benki ya NMB imewakutanisha walimu katika maadhimisho hayo na kuwapa semina ya masuala anuai ya kibenki.Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam na Zanzibar, Bi. Vicky Bishubo akizungumza na walimu wanachama wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) jijini Dar es Salaam katika maadhimisho ya siku ya walimu 'Teachers Day', Benki ya NMB imewakutanisha walimu katika maadhimisho hayo na kuwapa semina ya masuala anuai ya kibenki.Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam na Zanzibar, Bi. Vicky Bishubo akizungumza na walimu wanachama wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) jijini Dar es Salaam katika maadhimisho ya siku ya walimu 'Teachers Day', Benki ya NMB imewakutanisha walimu katika maadhimisho hayo na kuwapa semina ya masuala anuai ya kibenki.[/caption]   [caption id="attachment_74342" align="alignnone" width="800"]Augustino Mbogela Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani wa Benki ya NMB akizungumza na walimu wanachama wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) jijini Dar es Salaam katika maadhimisho ya siku ya walimu 'Teachers Day', Benki ya NMB imewakutanisha walimu katika maadhimisho hayo na kuwapa semina ya masuala anuai ya kibenki.Augustino Mbogela Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani wa Benki ya NMB akizungumza na walimu wanachama wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) jijini Dar es Salaam katika maadhimisho ya siku ya walimu 'Teachers Day', Benki ya NMB imewakutanisha walimu katika maadhimisho hayo na kuwapa semina ya masuala anuai ya kibenki.Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mbando (mwenye gauni jeusi) ambaye ni mgeni rasmi katika shughuli hiyo akipiga picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi na viongozi wa NMB kwenye maadhimisho ya siku ya walimu 'Teachers Day'. Benki ya NMB imewakutanisha walimu katika maadhimisho hayo na kuwapa semina ya masuala anuai ya kibenki.Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mbando (mwenye gauni jeusi) ambaye ni mgeni rasmi katika shughuli hiyo akipiga picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi na viongozi wa NMB kwenye maadhimisho ya siku ya walimu 'Teachers Day'. Benki ya NMB imewakutanisha walimu katika maadhimisho hayo na kuwapa semina ya masuala anuai ya kibenki.Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mbando akiagana na baadhi ya viongozi wa UWT na NMB mara baada ya kuzindua hafla hiyo ya 'Teachers Day'.Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mbando akiagana na baadhi ya viongozi wa UWT na NMB mara baada ya kuzindua hafla hiyo ya 'Teachers Day'.Baadhi ya walimu wanachama wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) jijini Dar es Salaam wakiwa katika maadhimisho ya siku ya walimu 'Teachers Day'. Benki ya NMB imewakutanisha walimu katika maadhimisho hayo na kuwapa semina ya masuala anuai ya kibenki.Baadhi ya walimu wanachama wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) jijini Dar es Salaam na maofisa wa NMB wakiwa katika maadhimisho ya siku ya walimu 'Teachers Day'. Benki ya NMB imewakutanisha walimu katika maadhimisho hayo na kuwapa semina ya masuala anuai ya kibenki.

Wizara za Nishati Zanzibar, Bara Zajadili Utafutaji Mafuta na Gesi Asilia Bahari ya Hindi

$
0
0
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (katikati) akiongoza kikao baina ya Watendaji kutoka Wizara ya Nishati na Madini na Wizara ya Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira ya Zanzibar. Kikao hicho pia kimehudhuriwa na Wataalam kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania TPDC, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) na Mamlaka ya Udhibiti wa shughuli za Mkondo wa Juu wa Mafuta (PURA).
Meneja Mkuu wa Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) Hassan Mbarouk, akiongea jambo wakati wa kikao baina ya Wizara ya Nishati na Madini na baadhi ya Taasisi na Wizara ya Maji, Ardhi, Nishati na Mazingira kilichojadili Utafutaji wa Mafuta na Gesi kwenye maeneo ya Bahari ya Hindi.
Wajumbe wa kikao wakifuatilia kikao baina ya Wizara ya Nishati na Madini na Viongozi Waandamizi kutoka Wizara ya Maji, Ardhi, Nishati na Mazingira ya Zanzibar. Wa kwanza kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Ardhi, Nishati na Mazingira Zanzibar. Katikati ni Mkurugenzi wa Idara ya Nishati Zanzibar, Wizara ya Maji, Ardhi, Nishati na Mazingira Zanzibar.
Mtaalam kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzani, akiwaonesha wajumbe wa kikao ramani inayoonesha maeneo ya shughuli za Utafiti wa Mafuta na Gesi nchini.

………………………

Watendaji kutoka Wizara ya Nishati na Madini na Wizara ya Maji, Ardhi, Nishati na Mazingira ya Zanzibar, wamekutana katika kikao kilichojadili Utafutaji wa Mafuta na Gesi Asilia kwenye maeneo ya Bahari ya Hindi.

Kikao hicho kimejadili kuhusu umuhimu wa kuimarisha mahusiano na ushirikiano zaidi katika sekta ya nishati ambayo ina mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi.

Pia, mbali na kujadili suala la utafiti wa Mafuta na Gesi asilia, kikao hicho kimejadili masuala ya nishati ya umeme kwa upande wa Tanzania Bara na Zanzibar. Aidha, Taasisi nyingine zilizoshiriki katika kikao hicho ni Watendaji kutoka Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO), Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na Mamlaka ya Udhibiti wa shughuli za Mkondo wa Juu wa Mafuta (PURA)

Programu ya LTSP kuvipatia Hatimiliki ya Ardhi Vijiji 37 vya MALINYI, KILOMBERO na ULANGA mkoani Morogoro

$
0
0

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa tume ya taifa ya Matumizi Bora ya Ardhi Dkt Stephen Nindi ( Kulia ), akikabidhi Mpango wa miaka 20 wa Matumizi Bora ya Ardhi wa Watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga, Mpango huo umelenga kutunza mazingira na Bio anuai Zilizopo nchini pamoja na kumnufaish Mwananchi wa Kipato cha kawaida.

Kiongozi wa Urasimishaji kupitia Programu ya LTSP, iliyo Chini ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi SAGWILE MSANANGA akitoa maelezo kuhusu Mradi wa kuwezesha Umilikishaji Ardhi kwa Wananchi pamoja na Vijiji Vilivyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga Mkoani MOROGORO.

Mratibu wa Programu ya Kuwezesha Umilikishaji Ardhi katika Wilaya za MALINYI, KILOMBERO na ULANG, Godfrey Machabe aliyevaa Tai Shingoni, akimsikiliza kwa Umakini Kiongozi wa Urasimishaji ndugu Sagwile Msananga alipokuwa akielezea kuhusu Programu ya LTSP, kwa Washiriki wa Mafunzo ya Kuwezesha Umilikishaji wa Ardhi katika Wilaya ya Ulanga Mkoani MOROGORO.

Kaimu kamishna wa Ardhi nchini Bi Mary Makondo ( katikati), akimsikiliza Katibu tawala wa Wilaya ya ULANGA mkoani Morogoro Ndugu Abraham Mwaivile aliyevaa Koti la Rangi ya Kijivu akisisitiza Jambo kwa Washiriki wa mafunzo ya kuwezesha Umilikishaji Ardhi katika Halmashauri hiyo, ambapo zoezi la Upimaji Mipaka ya Vijiji na Utoaji hatimiliki za Ardhi litafanyika.




Kiongozi wa Urasimishaji Sagwile Msananga kupitia Programu ya LTSP chini ya Wizara ya Ardhi inayoendelea katika Wilaya za MALINYI, KILOMBERO na ULANGA mkoani Morogoro akitoa Semina elekezi Juu ya Mradi huo, wenye lengo la Kutoa Kupika mipaka ya Vijiji na kutoka hatimiliki pamoja na kuhamasisha Ujenzi wa Masjala za Ardhi kwenye Vijiji.

Kiongozi wa Urasimishaji kupitia Programu ya LTSP, iliyo Chini ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi SAGWILE MSANANGA akitoa maelezo kuhusu Mradi wa kuwezesha Umilikishaji Ardhi kwa Wananchi pamoja na Vijiji Vilivyopo wilayani Kilombero Mkoani MOROGORO.

Picha zote na Hannah Mwandoloma



MWANAMUZIKI WA NIGERIA, KISS DANIEL KUTUMBUIZA KATIKA UZINDUZI WA MONTE CARLO JIJINI DAR KESHO.

$
0
0
  (Kutoka kulia) Mkurugenzi wa Stra8up Vibes, Sniper Mantana ambao ni waandaaji wa Tamasha la “Monte Carlo Classic’ akizungumza na waandishi wa habari (hawapo) pichani wakati wa kumtambulisha Msanii maarufu kutoka Nigeria Anidugbe Oluwatobiloba Daniel almaarufu kama ‘Kiss Daniel’atakayepamba uzinduzi wa Tamasha hilo litakalofanyika kesho katika ukumbi wa Akemi ulipo katika jengo la Golden Jubilee Towers, Posta jijini Dar es salaam. Pamoja nae ni Meneja Masoko wa benki ya Barclays Joe Bendera, Msanii kutoka Nigeria Kiss Daniel, mbia wa Tamasha hilo kutoka Malaysia DeJurist Global na Meneja wa Msanii huyo Louiza Williams.
 Meneja Masoko wa benki ya Barclays Joe Bendera akizunguzmza katika mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kumtambulisha Msanii kutoka Nigeria Kiss Daniel atakayepamba uzinduzi wa Tamasha la “Monte Carlo Classic” litakalofanyika kesho katika ukumbi wa Akemi ulipo katika jengo la Golden Jubilee Towers, Posta jijini Dar es salaam. Benki ya Barclays ni wadhamini rasmi wa Tamasha hilo ambalo limezinduliwa kwa mara ya kwanza nchini Tanzania.
 Mmoja wa washiriki katika uandaaji wa Tamasha la Monte Carlo Classic DeJurist Global kutoka Malaysia akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika hafla ya kumtambulisha msanii kutoka Nigeria Kiss Daniel ambaye yupo nchini kwa ajili ya kupamba uzinduzi wa Tamasha hilo litakalofanyika kesho katika ukumbi wa Akemi ulipo katika jengo la Golden Jubilee Towers, Posta jijini Dar es salaam. Pamoja na kulia ni Msanii kutoka Nigeria Kiss Daniel, Meneja masoko wa benki ya Barclays, Joe Bendera na Mkurugenzi wa Sta8up Vibes, waandaji wa Tamasha Sniper Montana. Benki ya Barclays ni wadhamini rasmi wa Tamasha hilo ambalo limezinduliwa kwa mara ya kwanza nchini Tanzania.
 Msanii maarufu kutoka Nigeria Anidugbe Oluwatobiloba Daniel almaarufu kama Kiss Daniel akionesha albamu yake kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kumaliza mkutano wa kutambulisha uwepo wake katika Tamasha linalozinduliwa jijini Dar es salaam siku ya kesho katika ukumbi wa Akemi ulipo katika jengo la Golden Jubilee, Posta jijini Dar es salaam.
 Msanii maarufu kutoka Nigeria Anidugbe Oluwatobiloba Daniel almaarufu kama Kiss Daniel akifurahia jambo na Meneja Masoko wa benki ya Barclays Joe Bendera (kushoto) sambamba na Mkurugenzi wa Stra8up Vibes Sniper Mantana (katikati) mara baada ya kumaliza mkutano na waandishi wa habari wa kumtambulisha msanii huyo atakayepamba uzinduzi wa Tamasha jipya nchini la “Monte Carlo Classic” litakalofanyika kesho kwenye ukumbi wa Akemi uliopo Golden Jubilee Towers, Posta jijini Dar es salaam.

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
Mwanamuziki maarufu wa Nigeria Anidugbe Oluwatobiloba Daniel anayefahamika kwa jina la kisanii Kiss Daniel aliyetamba hasa kwa kibao cha ‘Woju’ kwenye anga za muziki,  ametua jijini Dar es Salaam kwa ajili ya uzinduzi wa Monte Carlo Classic tukio lililoandaliwa na Str8up Vibes wakishirikiana na DeJurist Global kwa udhamini wa Benki ya Barclays Tanzania.

Mwimbaji huyo wa Nigeria aliyejizolea mashabiki wengi tangu alipoachia kibao chake cha ‘Woju’, ataongoza uzinduzi wa tukio hilo Jumamosi hii jijini Dar es Salaam katika Mgahawa wa Akemi uliopo kwenye jengo la Jubilee Towers, Mtaa wa Ohio.

Akizungumza mapema hii leo kwenye mkutano na waandishi wa habari, Mkurugenzi Mtendaji wa Str8up Vibes, Sniper Mantana alithibitisha mbele ya waandishi kwamba maandalizi ya tukio hilo yamekamilika na kuwasihi Watanzania kujitokeza kwa wingi ili kujumuika na msanii huyo maarufu.
Aliongeza kwamba kabla ya tukio hilo tiketi zitauzwa kwa shilingi 25,000 na itakapo timu usiku tiketi zitauzwa kwa shilingi 35,000.

Alisema tukio la the Monte Carlo Classic limelenga kubadilishana uzoefu baina ya Watanzania hususani kwenye sekta ya burdani.

“Kwenye miji kama vile;-Monte Carlo, New York, Los Angeles (L.A), Paris watu maarufu hushiriki kwa kupamba matukio kama haya. Hii ni sawa na ambavyo sisi tumelenga kuliimarisha tamasha la Monte-Carlo Classic jijini Dar es Salaam, ambapo kwa usiku mmoja kila mtu anakuwa mtu wa hadhi ya juu, huku akisherehekea na mtu maarufu aliyeteuliwa na kwenye eneo lenye hadhi ambalo limeandaliwa na waandaaji,” alisema.

Nae Meneja Masoko wa Benki ya Bacrays Tanzania, Joe Bendera, alisema benki hiyo imekuwa ikidhamini ligi kubwa ya soka ulimwenguni jambo ambalo limeifanya kuisogeza karibu na jamii benki hiyo. Tunayofuraha kuwa sehemu ya uzinduzi wa tukio hili kubwa jambo ambalo litatuwezesha kukutana na wageni waalikwa mbalimbali na wateja wetu.

"Tukio hili linatupa fursa ya kutoa elimu kuhusu matumizi ya kadi zetu na kuhamasisha matumizi yake sehemu mbalimbali kwenye mashine za mauzo maeneo mbalimbali nchini. 

Mwezi uliopita Benki ya Bacrays ilitunukiwa cheti cha ubora cha Mtoaji wa Kadi Bora za Visa nchini Tanzania. Kubeba fedha taslimu kuna kiwango maalumu hivyo tunapenda kuwahamasisha kadi zetu za Debit na Cretid kwenye tukio hili," alisema.
Kwa upande wake msanii huyo alisema alishtuka alipopata mwaliko kutoka kwa Str8up Vibes na kumchague yeye kuwa mgeni rasmi kwenye tukio hilo, na kwa mara ya kwanza kuja hapa nchini kama msanii.

 “Nimefuarahi sana kualikwa kwenye tukio la Monte Carlo Classic hapa jijini Dar es Salaam, ninashukuru kwa nafasi hii na ninapenda kuwashukuru waandaji kwa kutambua umuhimu wangu.”

Msanii huyo aliongeza kwamba, amekuja nchini kufurahia na kujumuika na watu hadhi tofauti, wasanii wa muziki pamoja na mashabiki zake na kuwaomba wakazi wa Jiji la Dar es Salaam kufika kwa wingi siku ya Jumamosi kwenye tukio hili.

Kwa hivi sasa amejiunga na lebo ya G-Worldwide Entertainment iliyomwezesha kurekodi nyimbo zake tatu; Woju, Mama na aliouachia hivi karibuni wa Jombo.

MKUTANO WA VYAMA VYA SIASA WAPIGWA KALENDA

$
0
0
Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Mstaafu Francis Mutungia akisisitiza juu ya umuhimu wa mkutano wa vyama vya siasa utaofanyika Septemba 3 hadi 4 kwaka huu jijini Dar es Salaam mkutano uliofanyika katika Ofisi Msajili wa Vyama vya Siasa leo jijini Dar es Salaam.
Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa,Vuai Ali Vuai akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya kusogeza mkutano wa vyama vya siasa leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni Mjumbe na Mwenyekiti wa kamati ya fedha ya baraza la vyama vya siasa, Constatine Akitanda.

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

BARAZA la vyama vya Siasa nchini limesogeza mbele mkutano wa kujadili sintofahamu iliyojitokeza kwa baadhi ya vyama vya siasa na kusababisha kuwepo kwa hofu, na taharuki kwa wananchi.

Mkutano huo ulitangazwa kufanyika Agosti 29 hadi 30 na kusogezwa kufanyika Septemba 3 hadi 4 jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi habari jijini Dar es Salaam, Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa, Vuai Ali Vuai amesema kusogeza mbele kwa mkutano huo kumetokana na kutaka kutoa muda kwa wadau ili waweze kujiandaa.

Amesema kuwa mkutano huo ni muhimu sana kwa wadau kukutana na kujadili mambo yaliyojitokeza na kuweka sawa kwa mstakabali wa taifa.

jukwaa la viongozi wa kitaifa wa vyama vya siasa kukutana mara kwa mara kujadiliana masuala yanayohusu demokrasia ya vyama vingi na siasa hapa nchini kwetu.

Amsema kila chama cha siasa kinawakilishwa na viongozi wawili wa ngazi kitaifa katika Baraza la Vyama vya Siasa, ambapo kiongozi mmoja anapaswa kutoka Tanzania Bara na mwingine Zanzibar.

Mwenyekiti na Makamu mwenyekiti wa Baraza huchaguliwa miongoni mwa wajumbe wa Baraza. Baraza la Vyama vya linaendeshwa kwa mujibu wa kanuni za zilizotungwa na Baraza.

Baraza la vyama vya siasa lina majukumu ya  kuishauri msajili wa vyama vya siasa kuhusu migogoro baina ya vyama vya siasa,kumshauri Msajili wa vyama vya siasa kuhusu masuala yenye masilahi ya kitaifa yanayohusu vyama vya siasa na hali ya siasa nchini.

Aidha amesema kazi ya baraza hilo kuishauri Serikali kupitia Msajili wa Vyama vya Siasa kuhusu kutungwa, marekebisho na utekelezaji wa sheria ya vyama vya siasa na sheria nyingine zinazohusu vyama vya siasa,kushauri kuhusu uratibu wa shughuli za vyama vya siasa.

Baraza hilo linaweza kumtaarifu Msajili wa Vyama vya Siasa kuhusu masuala yoyote yanayohusu utendaji wa chama chochote cha siasaKamati ya uongozi ya Baraza la Vyama vya Siasa inaundwa na Mwenyekiti wa Baraza, Makamu Mwenyekiti wa Baraza, wenyeviti wa kamati nne za Baraza na katibu wa Baraza.

RAIS WA ZANZIBAR DK. SHEIN AKUTANA NA BALOZI MDOGO WA CHINA

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia)akisalimiana na Mgeni wake Balozi mdogo wa Jamhuri ya Watu wa China anayefanyia kazi Zanzibar Mhe,Xie XiaowuTek Chand Barupai alipofika Ikulu Mjini Unguja leo,
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto)akizungumza na Mgeni wake Balozi mdogo wa Jamhuri ya Watu wa China anayefanyia kazi Zanzibar Mhe,Xie XiaowuTek Chand Barupai alipofika Ikulu Mjini Unguja leo,[Picha na Ikulu.]26/08/2016.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto)akiagana na Mgeni wake Balozi mdogo wa Jamhuri ya Watu wa China anayefanyia kazi Zanzibar Mhe,Xie XiaowuTek Chand Barupai alipofika Ikulu Mjini Unguja leo baada ya mazungumzo yao,[Picha na Ikulu.]26/08/2016.

MWENGE WA UHURU WAZINDUA MIRADI YENYE THAMANI YA ZAIDI YA SH.3 BILIONI HALMASHAURI YA ARUSHA DC WILAYANI ARUMERU

$
0
0

Mkimbiza Mwenge wa Uhuru kitaifa akiwaongoza Askari wa Kikosi cha Kutulia Ghasia(FFU)kuingia katika halmashauri ya wilaya ya Arusha DC baada ya kumaliza mbizo zake halmashauri ya wilaya ya Meru zote zikiwa katika wilaya ya Arumeru mkoa wa Arusha .
Kiongozi wa Mbio za Mwenge  kitaifa mwaka 2016,George Mbijima akivalishwa Skafu na kijana wa Scout wakati wa kuanza kukimbiza Mwenge wa Uhuru katika halmashauri ya wilaya ya Arusha DC.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge kitaifa mwaka 2016,George Mbijima akisalimiana na watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Arusha DC kabla ya kuanza kuweka Mawe ya Msingi na kuzindua miradi yenye thamani ya zaidi ya Sh 3 bilioni.
Mkurugenzi wa New Age Company Ltd,Godson Ngomuo akimwonyesha Samani zinazotengenezwa na kuuzwa na kampuni yake na kusaidia kutengeneza ajira kwa vijana wazawa.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge kitaifa mwaka 2016,George Mbijimaakizungumza na maafisa wa taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa wilaya ya Arumeru wanaotoa elimu dhidi ya Rushwa.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge kitaifa mwaka 2016,George Mbijima  akijiandaa kukabidhi hundi yenye thamani ya Sh 3 milioni kwa kikundi cha Vijana waliopata mikopo yenye riba nafuu,kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Arumeru,Alexander Mnyeti.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge kitaifa mwaka 2016,George Mbijima akiwakabidhi  hundi yenye thamani ya Sh 3 milioni kikundi cha Wanawake  waliopata mikopo yenye riba nafuu,kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Arumeru,Alexander Mnyeti.
Vijana wa JKT Oljoro na Scout wakiserebuka kushangilia Mwenge wa Uhuru.
Moja ya mradi wa maji uliozinduliwa katika Kijiji cha Lekamba.

WASANII WA TANZANIA UGHAIBUNI WAPAZA SAUTI KUPINGA MAANDAMANO YA UKUTA,

$
0
0

Wanachi Tusikubali kufanywa chambo cha kuvunja amani tuliyoijenga

Wasanii wa kitanzania wanaoishi na kufanyia kazi zao nje ya nchi au ughaibuni,wametoa wito kwa wananchi wa Tanzania walio nyumbani na nje
kupinga kwa nguvu zote maandamano yaliyopewa na jina la UKUTA yalipangwa kufanyika siku 1 september 2016. 
 
Wasanii hao wakikaliliwa na
na vyombo vya habari walisema maandamano hayo hayana tija kwa watanzania na zaidi yataleta mpasuko katika jamii. baadhi ya wasanii hao
ni mwanamuziki Saidi Kanda anayeishi nchi uingerea alisema " Hakuna haja ya Kuunga mokono maandamano yatakayo lisababishia taifa uvunjifu wa amani" baadala yake wanasiasa watuache wananchi tufanye shughuli zetu na kufurahia maisha- Alisema mwanamuziki Saidi Kanda kiongozi wa Mvula-Mandondo Band ya Uingereza.

Kule Ujerumani nako Kiongozi wa Ngoma Africa band mwanamuziki maarufu Kamanda Ras Makunja alikuwa akiongea na vyombo vya habari kwa niaba ya wasanii waishio ujerumani,mtazamo wa Kamanda Ras Makunja una hoja nzito kuhusu maandamano ya UKUTA alikaliliwa akisema" Watanzania tusikubali kufanywa mtaji au chanzo cha vurugu na uvunjivu wa Amani ambayo kwa miaka tumeijenga,kwani hatuoni sababu yeyote ya msingi ya kuunga mkono maandamano ya UKUTA, sisi watanzania ndio tuliopiga kula kuiweka serekali ya awamu ya tano,leo hii
heti tuende mtaani kuandamana kuipinga !? kwa sababu ya watu wanajiita UKUTA kwa kweli itakuwa sawa na watoto walio juu ya tawi la mti na kuanza kulikata tawi walio kalia kwa shoka ni sawa Ukichaa- Ras Makunja alihoji.

Mwanamuziki huyo nguli alizidi kuhoji hivi wanasiasa si tuliwapa muda wa kutushawishi kuwapigia kula katika kampeni zao na sasa uchaguzi umepita
sasa kuna haja gani tena sisi raia tushawishiwe kuandamana maandamano ambayo tafasiri yake UKUTA kisheria hayakubaliki ,yaani ukiyatazama kwa upana haya nia ya AMANI ! yaani mfano wake yawe maandamano kama ya
IRANI yalioshawishiwa kumtoa Shah ? lakini Tanzania sio Irani kwa sababu serekali ya Tanzania imechaguliwa na wananchi kihalali sasa leo sisi wapiga kura tena tuende mtaani kupinga kitu ambacho tumekichagua kihalali..? 
 
SHAH wa Iran alikuwa mfalme sio kiongozi wa kuchaguliwa ndio maana Khomen alishawishi wanafunzi waanze kuandamana, Maandamano ya India 1947 yakiongozwa na Ghandi yalikuwa ya kumuondoa mkoloni mwingereza,Sasa haya ya UKUTA na tafisiri yake ipo wazi ni yanini? 
 
kwa faida zipi za taifa letu,TUNAWAOMBA WANANCHI TUSIKUBALI KABISA KUUNGA MKONO MAANDAMANO YA UKUTA,tusikubali kushawishiwa kuandamana kwa madai yasiyoleta maandeleo kwa taifa, tusikubali kila siku
baadhi ya wanasiasa wanatuendesha mara tususie kupiga kura,mara tuandamane UKUTA ,wakati nchi jirani wanachapa kazi sisi tupo katika siasa kila kukicha ?! Ras Makunja alisisitiza kuwa anayo haki ya kutoa maoni yake kwani yeye bado raia halali wa Tanzania.

WATANZANIA WALIOSOMA CHINA kupata uongozi mpya

$
0
0



By LEAH MUSHI

Chama cha watanzania waliosoma China- CHINA ALLUMNI ASSOCIATION OF TANZANIA (CAAT) hii leo tarehe 27 August, 2016 kinatarajia kufanya uchaguzi mkuu kwa ajili ya kupata viongozi wake wapya.

Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika katika ukumbi wa Rombo Green views Hotel sinza Dar es salaam kuanzia saa saba kamili mchana nakufuatiwa na sherehe ya kuwapongeza viongozi wapya na kuwaaga viongozi waliomaliza muda wao.

Kwa mujibu wa mwenyekiti wa uchaguzi wa chama hicho GUSTAV SANGA uchaguzi huo utawaweka madarakani viongozi hao miaka mitatu kwa mujibu wa katiba ya chama hicho.

Nafasi zinazogombewa katika uchaguzi huo ni Chairperson, Secretary, Treasurer, Director of Statistics, media and information, director of Art, culture and heritage pamoja na Director of Education, Science and Technology

SANGA pia amewakaribisha watanzania wote waliomaliza China kujiunga katika chama hicho ili kuweza kutimiza malengo mbalimbali waliyojiwekea ikiwemo kuishauri serikali masuala yahusuyo TANZANIA- CHINA.

Chama hicho cha watanzania waliosoma China kina miaka sita tangu kuanzishwa kwake na kina wanachama tangu waliosoma china miaka ya1980 kwa ngazi ya shahada , astashahada na shahada ya uzamivu.

Mafundi wa TEMESA washauriwa kutumia mafunzo waliyoyapata kuendana na mabadiliko ya teknolojia.

$
0
0

Mjumbe wa Bodi ya TEMESA Brigedia Jenerali Msataafu Mhandisi Mabula Mashauri(katikati aliyesimama) akizungumza na mafundi wa TEMESA wakati akifunga mafunzo ya mafundi wa Wakala hao iliyofanyika katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Agosti 26,2016.
Kaimu Mtendaji TEMESA Mhandisi Manase Ole Kujan(kulia) akitoa neno kwa mafundi wa TEMESA wakati wa hafla ya kuhitimisha mafunzo kwa mafundi hao iliyofanyika katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Agosti 26,2016 kushoto ni Mjumbe wa Bodi ya TEMESA Brigedia Jenerali Msataafu Mhandisi Mabula Mashauri .
Mjumbe wa Bodi ya TEMESA Brigedia Jenerali Msataafu Mhandisi Mabula Mashauri akionesha moja ya vifaa vilivyokabidhiwa na mafundi wa TEMESA kwa ajili ya karakana zao wakati wa hafla ya kuhitimisha mafunzo kwa mafundi hao iliyofanyika katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Agosti 26,2016.

Mjumbe wa Bodi ya TEMESA Brigedia Jenerali Msataafu Mhandisi Mabula Mashauri akikabidhi cheti kwa mmoja wa mafundi Bw.Saidi Waziri kutoka Arusha wakati wa hafla ya kuhitimisha mafunzo kwa mafundi hao iliyofanyika katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Agosti 26,2016.

Mjumbe wa Bodi ya TEMESA Brigedia Jenerali Msataafu Mhandisi Mabula Mashauri akikabidhi moja ya vifaa vilivyotolewa kwa ajili ya karakana za TEMESA kwa Bw. Japhet Mwita mmoja wa washiriki wa mafunzo yaliyofanyika hivi karibuni katika hafla ya kuhitimisha mafunzo hayo iliyofanyika katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Agosti 26,2016.

Baadhi wa mafundi wa Temesa kutoka mikoa mbalimbali nchini wakimsikiliza mgeni rasmi (hayupo pichani) wakati wa hafla ya kuhitimisha mafunzo kwa mafundi hao iliyofanyika katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Agosti 26,2016.


Picha/Habari na Theresia Mwami TEMESA

Mafundi wa TEMESA wameshauriwa kutumia mafunzo waliyoyapata kuendana na mabadiliko ya teknolojia katika utengenezaji magari na vifaa vya umeme. Ushauri huo umetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Mjumbe wa Bodi ya Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Brigedia Jenerali Msataafu Mhandisi Mabula Mashauri wakati wa hafla ya kuhitimisha mafunzo kwa mafundi Wakala hao iliyofanyika katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT). 

Brigedia Jenerali Msataafu Mhandisi Mabula Mashauri amesema kuwa Serikali kupitia Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA imedhamiria na kuhakikisha kuwa magari na mitambo yote ya Serikali inatengenezwa kitaalam ili kuleta tija na thamani halisi ya fedha iliyokusudiwa pamoja na kukidhi kiu na matarajio ya wateja.

”Napenda kuwakumbusha kwamba mnayo dhamana kubwa ya kutengeneza magari ya Serikali hivyo kwa mafunzo mliyoyapata ninaamini mmejenga uwezo wa kutosha wa kuhudumia magari na vifaa vya umeme kwa kutumia mfumo wa kisasa” alisema Mhandisi Mashauri.

Ameongeza kuwa ni fursa pekee kwa mafundi waliopata mafunzo hayo kwenda kuwafundisha wenzao ambao hawakuweza kupata mafunzo hayo ili kuongeza kasi ya kutengenza magari na vifaa vya umeme na kupunguza changamoto zilizopo katika utengenezaji magari kwa kutumia mfumo wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).

Aidha Kaimu Mtendaji wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Mhandisi Manase Ole Kujan amewashukuru washirika wa TEMESA wakiwemo Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) na kampuni ya Superdoll kwa kuwezesha kufanyika kwa mafunzo hayo ambayo yataleta chachu ya utendaji kazi wa mafundi na karakana za TEMESA zilizopo nchini nzima.

Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA kwa kushirikiana na Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) na kampuni ya Superdoll waliandaa mafunzo ya siku 14 yaliyoanza Agosti 9 na kumalizika Agosti 26, 2016 yaliyoshirikisha jumla ya mafundi 25 kutoka mikoa mbalimbali ili kuwapa uwezo wa kutengeneza magari kwa kutumia mifumo ya kisasa.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aongoza ujumbe wa Tanzania kwenye kikao cha 25 cha Wakuu wa Nchi wanaoshiriki kwenye mchakato wa APRM

$
0
0
Mheshimiwa Kasim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano Tanzania, aliongoza ujumbe wa Tanzania kwenye kikao cha 25 cha Wakuu wa Nchi wanaoshiriki kwenye mchakato wa APRM. Pia walikuwepo Mheshimiwa Dkt Susan Kolimba, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mheshimiwa Dkt. Khalid S. Mohamed, Waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. 
Kikao hicho kilifanyika mjini Nairobi, Kenya; kuanzia tarehe 21-26 Agosti 2016 na kilihudhuriwa na jumla ya Wakuu wa Nchi 22.

APRM ni Mpango wa Kujitathmini Ki-Utawala Bora uliobuniwa na Wakuu wa Nchi za Kiafrika mwanzoni mwa miaka ya 2000, ili kutatua changamoto za utawala bora zinazolikabili bara la Afrika. Tanzania ni miongoni mwa nchi 35 zinazoshiriki kwenye Mpango huu.

Kauli mbiu ya kikao hiki ni “kuwa na APRM Imara itakayosaidia kuleta Mabadiliko katika Uongozi barani Afrika” na hivyo kuendelea kuwa chombo kitakachosaidia katika kufikiwa kwa malengo ya Umoja wa Afrika (Agenda 2063) na Malengo Endelevu ya Maendeleo ya Umoja wa mataifa.

Kwa mara ya kwanza katika historia ya kuanzishwa kwa Mpango huu, APRM ilipata muda wa siku takriban sita za kuangazia kwa kina masuala mbalimbali ambayo ni pamoja na Ripoti za Tathmini za nchi za Djibouti na Chad, Ripoti ya utekelezaji wa Mpango kazi wa Nchi ya Msumbiji, Mpango Mkakati wa APRM 2016-2020, Mpango Kazi na Bajeti kwa mwaka 2016/17, Masuala mbalimbali yanayohusu utendaji wa Jopo la Watu Mashuhuri, Hati ya Kuinganisha APRM kama Taasisi ndani ya Umoja wa nchi huru za Kiafrika, Taarifa ya Mkaguzi wa Mahesabu ya APRM, Vianzio vya Fedha na Maeneo ya changamoto yanayopendekezwa kuingizwa kwenye Hojaji Kuu ya APRM pamoja na kuzingatiwa kwenye mbinu za tathmini y utawala bora kwa vipindi vijavyo.


Maeneo mtambuka katika Afrika yaliyoonekana kuhitaji mikakati endelevu ya pamoja katika kuyatafutia ufumbuzi ni pamoja na; Minyukano ya kimtazamo hasa juu ya itikadi, sekta binafsi kutowezeshwa vya kutosha, miundo mbinu duni ikiwa nia pamoja na nishati, barabara, reli, simu, mitandao ya mawasiliano n.k, dola zisizokuwa imara, changamoto zihusuzo masoko, ukosefu wa viwanda pamoja na usindikaji wa bidhaa usiyoridhisha, uhaba wa wataalam, maendeleo duni katika sekta ya kilimo, maendeleo duni katika sekta ya huduma ikiwa ni pamoja na benki, bima, utalii n.k, udhaifu kwenye mifumo ya kidemokrasia na udhaifu wa uwajibikaji katika sekta ya umma. Baada ya mjadala wa kina kuhusu maeneo yaliyotajwa hapo juu, ilikubalika kuwa, Hojaji Kuu ya APRM pamoja na mbinu za tathmini zifanyiwe marekebisho ili kulenga zaidi mambo hayo muhimu na hatimaye kuungezea mchakato wa APRM thamani zaidi.

Tanzania inaendelea kutekeleza Mpango kazi wa APRM kwa kushirikiana na Wizara, Idara na Wakala za Serikali, pamoja na kuishirikisha Sekta Binafsi.

VIJUSO VYA BAADHI YA MAGAZETI YA LEO AGOSTI 27,NDANI NA NJE YA NCHI

Viewing all 46343 articles
Browse latest View live


Latest Images