Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live

DED Bunda amsimamisha kazi Mthamini

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya mji wa Bunda mkoani Mara, Bibi. Janeth Mayanja akiwa ofisini kwake.


Na. Immaculate Makilika- MAELEZO.
 
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya mji wa Bunda mkoani Mara, Bibi. Janeth Mayanja amemsimamisha kazi mtumishi wa Idara ya Ardhi na Mipango Miji kwa kosa la kujipatia fedha kinyume na taratibu za utumishi wa umma.

Akizungumza leo mjini Bunda wakati wa tukio hilo, Bibi. Mayanja alisema kuwa ameamua kumsimamisha kazi kwa muda, Bw.Eliudi Haonga ambaye ni mtumishi wa Idara ya Ardhi na Mipango Miji pia ni Mthamini wa Halmashauri hiyo ili kupisha uchunguzi kwa kosa la kujipatia fedha kinyume na taratibu za utumishi wa umma.

“Tarehe 28 mwezi Juni mwaka huu Bw.Eliudi Haonga alipokea fedha kiasi cha shilingi milioni saba kutoka kiwanda cha Olam ikiwa ni kodi ya pango kwa mwaka kodi 2015/2016, lakini mtumishi huyo alihifadhi kwenye akaunti ya Halmashauri ya mji yaani ‘own source’ fedha kiasi cha shilingi milioni mbili tu, na kiasi kilichobaki yaani milioni tano alizitumia kwa masuala binafsi kinyume na taratibu za utumishi wa umma” alisema Bibi Mayanja

Aliongeza kuwa Bw. Haonga aligushi risiti ya Halmashauri ya Mji na ambayo aliikabidhi katika kiwanda cha Olam baada ya kupokea fedha hizo.
Alisisitiza kuwa mtumishi huyo amesimamishwa kazi kwa mujibu wa kifungu namba 38 (1) cha kanuni za utumishi wa umma za mwaka 2003.

Aidha, Bibi Mayanja amewaasa watumishi wa umma wanaofanyakazi katika Halmashauri hiyo kuwa waadilifu kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu za nchi. Vile vile ameonya kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa yeyote atakayekiuka.

WATAALAMU WA TEHAMA WATAKIWA KUWA NA MAADILI.

$
0
0
 Naibu Waziri  Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani  akiongea na wataalam wa Tehama wakati wa uzinduzi wa mkutano wa siku moja wa wataalamu hao uliofanyika jijini Dar es Salaam leo.
 Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia Sekta ya Mawasiliano Prof. Faustine Kamuzora  akiongea na wataalam wa Tehama wakati wa uzinduzi wa mkutano wa siku moja wa wataalamu hao uliofanyika jijini Dar es Salaam leo.
 Naibu Waziri  Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani  akiongea na wanahabari  hawapo pichani wakati wa uzinduzi wa mkutano wa siku moja wa wataalamu hao uliofanyika jijini Dar es Salaam leo. (Picha zote na Benjamin Sawe).

Na abushehe Nondo,MAELEZO.

Naibu Waziri wa Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani ameiagiza Tume ya Teknolojia ya Habari na  Mawasiliano nchini kuhakikisha wanatengeneza misingi ya uadilifu wa kitaaluma na misingi hiyo itumike kuwadhibiti wale ambao wanatumia utaalamu huo kwa nia ovu.

Mhandisi Ngonyani aliyasema hayo  wakati akizindua mkutano wa kwanza ambao umeandaliwa ma Tume mpya ya Teknolojia Habari na Mawasiliano (TEHAMA) uliofanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa  Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

Alisema Mkutano huo una lengo la kuwakutanisha wataalamu wa TEHAMA kutoka katika sekta za umma na sekta binafsi ili kuweza kujadiliana ni kwa namna gani taaluma hiyo inavyoweza kutumika zaidi kwa faida ya ukuaji wa uchumi nchini Tanzania.

“Wapo baadhi ya watu wanatumia taaluma ya TEHAMA kwa manufaa mbalimbali ya kujenga uchumi na maendeleo, lakini wapo wachache ambao wanatumia utaalamu wao kwa manufaa  binafsi ikiwemo kuwadhalilisha watu wengine na kuwaibia fedha zao katika mitandao” Alisema Mhandisi Ngonyani.

Alisema Tume hiyo ya Teknolojia ya Habari na  Mawasiliano inatakiwa  kuja na sheria kali ambazo zitawabana wale wote ambao wamekua na tabia ya kutumia mitandao katika kufanya vitendo viovu badala ya kutumia katika kujiletea maendeleo.

Awali akizungumza katika mkutano huo,  Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano upande wa sekta ya Mawasiliano Prof. Faustin Kamuzora alisema uanzishwaji wa Tume ya Teknolojia ya Habari na  Mawasiliano nchini ni jitihada za makusudi za serikali  katika kukuza Mawasiliano .

Prof,Kamuzora alisema kuwa tume hiyo ina mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa Taifa na hivyo kuwasihi watendaji hao kuwaelimisha zaidi wananchi  kujikita zaidi katika kufuata maadili ya taaluma hiyo ili kulifikisha Taifa katika mafanikio ya sekta  ya mawasiliano.

Alisema Tume ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano itasaidia kukuza uchumi wa Taifa kutokana na kukua kwa sekta ya TEHAMA na kuchochea uzalishaji ,ukuaji wa sekta zingine kiuchumi na usambazaji wa huduma za jamii.

MAJALIWA: WAKURUGENZI WAHAMASISHENI WALIMU KUJIENDELEZA KIELIMU

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Wakurugenzi wa halmashauri na Maofisa Elimu nchini kutowaondoa katika nyadhifa zao Waratibu wa Elimu Kata na Wakuu wa shule za sekondari wasiokuwa na shahada, walimu wakuu wa shule za msingi wasiokuwa na diploma badala yake wawahamasishe kwenda kusoma.

“Maofisa Elimu na Wakurugenzi msije mkawaondoa wale walimu wakuu kwa zile sifa nilizosema bado muda ukifika tutatangaza.Msije mkawakurupusha sasa hivi waacheni waendelee na kazi zao tutatoa muda ili wajipange viziri,” aliema.

Agosti 20 mwaka huu Waziri Mkuu alisema Waratibu wa Elimu katika ngazi ya Kata na Wakuu wa shule za sekondari wanatakiwa kuwa na shahada huku walimu wakuu kwenye shule wanatakiwa kuwa na diploma.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo jana jioni (Jumatano, Agosti 24, 2016) wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kiwanja cha Mandela katika jimbo la Sumbawanga mjini. Alisema Mratibu wa Elimu katika ngazi ya Kata ni lazima awe na shahada ili aweze kutekeleza majukumu yake ya kusimamia utolewaji wa elimu katika shule za sekondari na msingi.

“Wakuu wa shule za sekondari na waratibu wa elimu kata wasiokuwa na shahada wasiondolewe katika nafasi zao kabla ya kupewa nafasi ya kwenda kujiendeleza kwa masomo ili waweze kuwa na vigezo vya kuendelea kushika nyadhifa hizo,” alisema.

Alisema katika kuboresha maslahi ya walimu Serikali imetenga zaidi ya sh. bilioni tano kwa mwezi ambazo ni posho ya madaraka. Waratibu Elimu Kata wanapewa sh 250,000 kwa mwezi huku Wakuu wa shule za sekondari na walimu wakuu katika shule za msingi wanapewa sh. 200,000.

Waziri Mkuu alisema badala ya kuwaondoa kwenye nyadhifa hizo ni vema Wakurugenzi wakawahamasisha walimu hao kwenda kusoma ili na wao wanufaike na posho ya madaraka iliyoanza kutolewa na Serikali hivi karibuni.

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu amewataka wazazi na walezi kwenda kuwaandisha watoto wenye umri wa miaka mitano katika shule za awali ambapo watapata fursa ya kujengewa msingi mzuri wa masomo kabla ya kuanza darasa la kwanza.


Pia aliagiza shule zote za msingi nchini zisizokuwa na madarasa ya awali kuhakikisha waanzisha madarasa hayo haraka na kuanza kutoa elimu hiyo.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
ALHAMIS, AGOSTI 25, 2016

Balozi wa Palestina Achangia Damu katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili leo.

$
0
0
 Balozi wa Palestina nchini Tanzania, Hazem Shabati akichangia damu leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH). Kulia ni mtaalamu kwa kutoa damu katika hospitali hiyo, Sabastian Magulu. 
 Mkuu wa Idara ya Maabara Mkuu katika hospitali  hiyo, Alex Magesa akijadiliana jambo na Balozi huyo baada ya kumaliza kuchangia damu leo.

Balozi wa Palestina nchini Tanzania, Hazem Shabati akijisajili kabla ya kuchangia damu leo katika hospitali hiyo. Kushoto ni Msajili wa damu, Titus Mhokole. Picha na John Stephen, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)

Balozi wa Palestina nchini Tanzania, Hazem Shabati amewataka Watanzania kuwa na tabia ya kuchangia damu ili kuokoa maisha ya wagonjwa wanaohitaji damu.

Balozi Shabati amefika leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa ajili kuchangia damu na kuwahamasisha watu wajitokeze kwa wingi ili kuchangia damu.

Amesema kila mtu ana wajibu wa kuchangia damu kwa kuwa ni muhimu kwa maisha ya wagonjwa wenye matatizo mbalimbali ya kiafya.

Pia, Balozi Shabati amesema lengo la kuchangia damu ni kudumisha uhusiano kati ya Tanzania na nchi yake ambao ni wa muda mrefu na wa kihistoria.

 Katika hatua nyingine, Ofisa Uhusiano wa hospitali hiyo, Neema Mwangomo amesema kwa wastani hospitali hiyo inakusanya chupa 40 hadi 50 kwa siku, lakini mahitaji kwa siku ni chupa 80 hadi 100.

Amesema makundi makubwa yanayohitaji damu kina mama wajawazito, watoto wenye saratani, majeruhi wa ajali na wagonjwa wanaotakiwa kufanyiwa upasuaji.

Mwangomo amesema mwanaume mwenye umri wa miaka 18 hadi 65 ndiye anapaswa kuchangia damu wakati mwanamke ni miaka 18 hadi 62.

Amesema kigezo cha pili ni mtu anayechangia damu anapaswa kuwa na uzito wa kilo 50 na kuendelea na kwamba mtu anapaswa kuwa na wingi wa damu kuanzia asilimia 85.

Mwanamke anaweza kuchangia damu mara tatu kila baada ya miezi minne wakati mwaume mara nne kila baada ya miezi mitatu.

Umoja wa Wanawake Viongozi wa Vyama vya Siasa Tanzania wapinga maandamano ya kuvunja amani

$
0
0

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Viongozi wa Vyama vya Siasa Tanzania (UWASATA), Cecilia Augustino akifafanua jambo wakati alipozungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, kupinga maandamano ya UKUTA. Kulia ni Katibu wa umoja huo Mwajuma Naty na Makamu Mwenyekiti Zaitun Hokororo.

Hussein Makame-MAELEZO

Umoja wa Wanawake Viongozi wa Vyama vya Siasa Tanzania (UWASATA), umepinga maandamano yasiyo na ukomo yaliyotanganzwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa kuwa hayana tija kwa wananchi na Tifa kwa ujumla.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mwenyekiti wa umoja huo Cecilia Augustino, alisema maandamano hayo yanaashiria uvunjifu wa amani ambayo ni urithi wa Taifa la Tanzania. Alisema wamefikisha tamko lao kwa Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Francis Mutungi na kumtaka msajili kutoacha chokochocko hizo ziendelee kwani zitasababisha kutoweka kwa amani nchini.

“Sisi wanawake viongozi wa vyama vya Siasa Tanzania tunapinga azimio la maandamano yasiyo na kikomo yanayoandaliwa na chama cha Chadema, hakika maandamano hayo hayana tija kwa wananchi na Taifa kwa ujumla” alisema Hokororo na kuongeza:

“Mheshimiwa Msajili, chokochocko hizi zinazofanywa na baadhi ya viongozi wa kisiasa zikiachwa tu bila ya kukemewa tunaamini tunu yetu ya amani ambayo ni urithi wetu tulioachiwa na waasisi wetu itatoweka” .Aliongeza kuwa hatma ya maandamano hayo ni kuingia kwenye machafuko na hatimaye mauaji na mateso kwa wanawake, watoto na walemavu, mambo ambayo hawatakubali yatokee.

Alibainisha kuwa wanawake viongozi wa vyama vya siasa wanaamini kuwa siasa ni kushindana kwa hoja na si uvunjifu wa sheria kwa njia ya maandamano yasiyo na tija kwa wananchi na Taifa. Aliliomba Baraza la Vyama vya Siasa kuhakikisha linawajibika katika kulinda demokrasia, amani na ustawi wa jamii nzima ya Watanzania. Katika hatua nyingine, umoja huo unaojumuisha wanawake viongozi wa vyama 22 vya siasa nchini, umeomba kufanya kongamano la amani lenye lengo la kuhamasisha amani na utulivu nchini.

Hivyo, Hokororo aliwaomba viongozi wakuu wa nchi kuanzia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, wadau wa amani na mashirika binafsi kushirikiana na umoja huo kufanikisha kongamano hilo. “Hakika tunaumia wanasiasa wanapokuwa chanzo cha migogoro na vurugu kwa Taifa letu.Hivyo tunamuomba Rais wetu tunajua ni msikivu aweze kuona namna nzuri ya kutafuta suluhu ya mgogoro huu wa kisiasa” alisema Mwenyekiti Cecilia Hokororo.

Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, tayari ameitisha Baraza la Vyama vya Siasa Agost 31, mwaka huu ili kutoa fursa kwa pande vyama husika kukaa meza moja na kujadili tofauti zilizopo na kuzipatia ufumbuzi.

Naye Makamu Mwenyekiti wa umoja huo Ziada Athumani alisema wanaunga mkono hatua hiyo kwani ndio njia muwafaka ya pande husika ili kufikia muwafaka kwa njia ya amani.

Katika mkutano huo na waandishi wa habari, wanawake viongozi wa vyama vya siasa waliwakilishwa na wenzao kutoka vyama vya Demokrasi Makini, ADA TADEA na Chama cha Umoja wa Demokrasi ya Vyama Vingi (UMD).

WATANZANIA WATAKIWA KUMUENZI BABA WA TAIFA KWA KUFANYA KAZI KWA BIDII NA KUEPUKA VITENDO VINAVYOCHOCHEA VURUGU NA UVUNJIFU WA AMANI.

$
0
0


 Mzee Said Maohamed Mannoro, Mkazi wa wilaya ya Kilwa - Kivinje akitoa ufafanuzi kuhusu nafasi ya wazee na mchango wao katika maendeleo ya Taifa.

Na. Aron Msigwa – Dar es salaam
 
Watanzania hususan vijana wametakiwa kumuenzi Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa vitendo kwa kufanya kazi kwa bidi, kulinda na kudumisha amani iliyopo na kufanya matendo yenye tija na manufaa kwa Taifa.

Wito huo umetolewa leo jijini Dar es salaam na Mzee Said Maohamed Mannoro, Mkazi wa wilaya ya Kilwa - Kivinje wakati akizungumza katika mahojiano maalum na mwandishi wa habari hii kuhusu nafasi ya wazee na mchango wao katika maendeleo ya Taifa.

Amesema yeye kama mzee anao wajibu wa kuwaeleza na kuwashauri vijana  kuepuka kutumika kama chanzo cha kufanya vitendo vinavyochochea vurugu na kusababisha uvunjifu wa amani iliyopo. 

“Mahali ambapo panahatarisha amani hakuna mjadala, suala la amani linapewa nafasi ya kwanza mambo mengine yanafuata, hata kama kungekuwa na jambo zuri namna gani linalotaka kufanyika linapohatarisha amani kwa upande mmoja au mwingine ni afadhali kuliacha” Amesisitiza mzee Monnoro.

Amesema kuwa maandamano yaliyopangwa kufanywa na baadhi ya vyama vya Siasa Septemba mosi hayana sababu ya kufanyika kwa kuwa yana ajenda ya kukosa uvumilivu kuhusu usahihi wa uongozi wa nchi hivyo ni vyema wananchi wakayaepuka kwa kuendelea na shughuli zao za kujiingizia kipato kwa kuwa amani haina mjadala.

Amesisitiza kuwa ni vyema viongozi wa vyama vya hivyo wakatumia njia zinazostahili kutafuta ufumbuzi wa kero zao kupitia mazungumzo ili kupata haki kuliko kuwahamasisha wananchi kuandamana na kupambana na vyombo vya dola na jambo ambalo mwisho wake ni kuleta vurugu zisizo na maana.Aidha, amewaomba viongozi hao wawe na busara na waheshimu maisha ya watu wanaowaongoza pia waepuke kuwa na kiburi cha kujiona wao ni bora kuliko wanachama wao.

“Mimi nayezungumza hapa niko upande wa upinzani, yanapokuja mambo ya kitaifa hayanizuii kuzungumza kwa kuwa yana manufaa kwa taifa, nasema kiongozi yeyote anayewashawishi wafuasi wake waandamane bila sababu za msingi ni kosa na jambo hili ni kupungukiwa na busara” Amesema mzee Mannoro.

Amebainisha kuwa kiongozi asiyeheshimu wala kujali maisha ya wananchi wake na kujiona anajua kuliko wao hafai, anapoteza sifa za kuwa kiongozi akisisitiza kuwa watanzania wanayo fursa nzuri ya kuchagua mustakabali mwema wa Taifa lao kwa kuwa amani ya Tanzania haina mbadala.

Akifafanua kuhusu utendaji wa viongozi wa Serikali katika ngazi mbalimbali za Serikali kuanzia kijiji hadi Taifa amesema kuwa katika nafasi zao wanao wajibu wa kulisaidia Taifa kwa kuwa wasimamizi wa utekelezaji wa malengo ya Serikali yaliyopangwa.

 “Sote tunafahamu Serikali imekuwa ikitekeleza mipango mbalimbali ya maendeleo ikiwemo suala la utoaji wa elimu bure haya ndiyo mambo ya msingi ya kufuatilia na kusimamia kwa kila kiongozi katika nafasi yake, tunapaswa kumsaidia Rais wetu kutekeleza malengo ya nchi” Amesisitiza.

Kuhusu maboresho ya sekta ya elimu ameishauri Serikali na wadau mbalimbali kuendelea kuwekeza katika miundombinu ya elimu hasa ujenzi wa madarasa na mabweni ili kuwawezesha wanafunzi wanaokaa mbali na shule hususani eneo analotoka la wilaya ya Kilwa Kivinje ili waweze kuondokana na tatizo la kutembea umbali mrefu.

 Ametoa wito kwa watanzania hususan vijana kujikita katika shughuli za kilimo na shughuli nyingine zinazoweza kuwaongezea kipato badala ya kupoteza muda mwingi katika masuala yasiyo na tija kwa maendeleo yao binafsi na taifa.

Amesisitiza kuwa Kilimo sio adhabu kwa kuwa yeye mwenyewe pamoja na uzee wake shughuli za kilimo zimemsaidia kujenga familia imara na kuendesha maisha yake akiamini kuwa utajiri wa kweli uko kwenye ardhi.

 “Kinachonigusa mimi ni maisha ya watu, nawaomba watumishi wa Serikali waliosomea mambo ya kilimo wafanye kazi kwa bidi, wawasimamie vijana wetu wanaolalamika mitaani kuwa hawana cha kufanya, tukiwajenga na kuwasimamia vijana wetu katika misingi ya uwajibikaji na kufanya kazi kwa bidii umasikini utaondoka” 

Waziri wa Afya Mh. Ummy Mwalimu awasilisha Muswada wa kutunga sheria ya wanataaluma wa Kemia kwa Kamati Dodoma

$
0
0

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya kudumu ya Maendeleo ya Jamii, Mh. Peter Serukamba (MB) akitoa miongozo kwenye mkutano huo wa Kamati mjini Dodoma .

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu amewasilisha muswada wa kutunga Sheria ya wanataaluma wa kemia mbele ya kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii mapema jana tarehe 24 Agosti 2016 katika ukumbi wa mdhibiti na mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali mjini Dodoma zinakoendelea Kamati mbalimbali za Bunge.

Kamati hiyo ya Bunge ya kudumu ya Maendeleo ya Jamii inaongozwa na Mwenyekiti wake Mh. Peter Serukamba (MB).Muswada huo unatarajiwa kuwasilishwa kwenye mkutano wa nne wa Bunge utakaoanza tarehe 6 September 2016.
Baadhi ya wajumbe wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii katika mkutano huo

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu akiongoza mkutano huo wa Kamati wakati wa kuwasilisha muswada wa kutunga Sheria ya wanataaluma wa kemia mbele ya kamati ya Kudumu ya Bunge.

Mkemia Mkuu wa Serikali Prof. Samwel V. Manyele (Katikati) akifuatilia mkutano huo wa Kamati mjini Dodoma


Baadhi ya wajumbe wa Kamati wakijadiliana jambo wakati wa mapunziko ya kamati hiyo ya Huduma za Maendeleo ya Jamii.

Wanafunzi wa Ualimu waliokosa UDOM wapangiwa vyuo vya ualimu vya serikali.

$
0
0
Na: Lilian Lundo - MAELEZO

Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imewapangia vyuo wanafunzi wa programu maalum ya ualimu chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) ambao hawakupata nafasi ya vyuo katika awamu ya kwanza, walioagizwa kuomba mafunzo kulingana na sifa zao kupitia Baraza la Taifa la Mafunzo ya Ufundi (NACTE).

Hayo yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Leonard Akwilapo leo, jijini Dar es Salaam alipokuwa akitoa taarifa kuhusu wanafunzi wanaosoma stashahada maalum ya ualimu wa sayansi chuo kikuu cha Dodoma.

“Mtakumbuka tuliagiza kwamba wanafunzi ambao walikosa sifa za kujiunga na ualimu wa sayansi waliombwa kuomba mafunzo yanayolingana na ufaulu wao kupitia NACTE, Lakini baada ya taarifa hiyo tulipokea maombi mengi kutoka kwa vijana hawa wakiomba kupangiwa vyuo moja kwa moja na Wizara, wizara imetafakari na kuamua nao wapangiwe vyuo vya Serikali,” alifafanua Dkt. Akwilapo.

Aliendelea kusema kuwa, wanafunzi ambao waliachwa awamu ya kwanza na kupangiwa katika awamu ya pili ni wanafunzi 290 ambao walikuwa wakisomea programu ya stashahada ya ualimu wa sekondari na wanafunzi 1,181 ambao walikuwa wakisomea stashahada ya ualimu wa msingi.Dkt. Akwilapo amesema kuwa Wizara imeamua kuwapangia wanafunzi hao vyuo kutokana na kuonyesha nia ya dhati ya kusomea ualimu ambapo wanafunzi hao wamepangiwa vyuo vya ualimu vya Marangu na Tabora.

Aidha, Dkt. Akwilapo ameeleza kuwa wanafunzi hao watajigharamia masomo yao kulingana na viwango vya ada vilivyowekwa na Serikali. Pia amewataka kutembelea tovuti ya wizara ya hiyo ambayo ni www.moe.go.tz ili kuona vyuo walivyopangiwa.

Mnamo tarehe Mei 28, 2016 Serikali iliwarejesha nyumbani wanafunzi 7,805 waliokuwa wanasoma Stashahada Maalum ya Ualimu wa Sayansi na Hisabati katika Chuo Kikuu cha Dodoma. Katika mchujo wa awamu ya kwanza wanafunzi 382 ndio waliokuwa na sifa ya kuendelea na masomo chuo kikuu cha UDOM na wengine 4,586 walipangiwa vyuo vya ualimu vya Serikali

Temeke yaandaa operesheni kabambe Stendi ya Mbagala

$
0
0

Na Jacquiline Mrisho - MAELEZO

Halmashauri ya Manispaa ya Temeke imeandaa operesheni kabambe katika stendi ya Mbagala ili kuhakikisha biashara zote zinafanyika katika maeneo yaliyotengwa na yasiyohatarisha afya ya jamii.Hatua hiyo imefikiwa baada ya kuongezeka kwa malalamiko kutoka kwa wananchi wa eneo hilo juu ya wafanyabiashara mbalimbali waliovamia eneo hilo na kulifanya kuwa la biashara.

Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Nassib Mbaga na kuwataka wafanyabiashara wanaofanya biashara zao katika mazingira yasiyo rasmi kuacha mara moja kwani ni kinyume cha sheria na taratibu.

“Tumeandaa operesheni kabambe ya kuondoa Kero zilizogundulika katika stendi ya Mbagala ili kuhakikisha kwamba biashara zote zinafanyika katika maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya shughuli hizo” alisema Mbaga.

Aliongeza kwa kuwataka watu wote wanaofanya biashara bila kibali katika maeneo ya stendi hiyo waondoke kabla ya zoezi la kusafisha halijaanza na kwa wale watakaokaidi, hatua za kisheria zitachukulia dhidi yao.

Aidha Mbaga alieleza kuwa kumekuwepo na jitihada za wazi za kuiweka Halmashauri katika hali ya usafi ikiwemo kutoa elimu kwa umma pamoja na kuhamasisha wananchi kuweka mazingira katika hali ya usafi na kuzuia unywaji wa maji ya kwenye vifuko vya plastiki yajulikanayo kama viroba/Kandoro kwa kuwa hayana viwango vya ubora.

Vilevile Halmashauri hiyo itaendelea kuwakamata wale wote wanaofanya biashara hiyo na kuteketeza mali zao kisha kuwafikisha Mahakamani au kuwalipisha faini. Mkurugenzi huyo ameyataja maeneo matano ambayo yametengwa rasmi kwa ajili ya biashara yakiwemo soko la Toangoma, Kilamba, Makangarawe, Sigara na Kiponza ambapo maeneo hayo yana huduma zote za jamii ikiwemo vyoo bora.

Maeneo mengine yaliyotengwa na Halmashauri kwa ajili ya Masoko ni pamoja na Temeke Stereo, Vetenari Tazara, Madenge, Tandika Kuu, Tandika Kampochea, Keko Magurumbasi, Temeke Mwisho, Bulyaga, Kizuiani, Zakhem, Mbagala Rangi tatu, Kampochea Mbagala, Mtoni Mtongani, Lumo, Urassa,Feri, Maguruwe, Limboa na Kabuma.

Mkurugenzi Mbaga ametoa rai kwa wananchi wanaohitaji kupata nafasi za kufanyia biashara katika maeneo mbalimbali ya Halmashauri hiyo kufanya mawasiliano na Ofisi yake ili kupatiwa maeneo rasmi kwa ajili ya shughuli hizo

MIILI YA ASKARI WALIOUAWA NA MAJAMBAZI YAAGWA LEO JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Waziri wa  Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, akipita kutoa heshima za mwisho mbele ya majeneza yaliyobeba  miili ya askari waliouawa baada ya kuvamiwa na majambazi    katika eneo la Mbande, Temeke ,bada hiyo ya kuaga miili ilifanyika katika viwanja vya polisi  vilivyopo barabara ya Kilwa,jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa  Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, akitoa mkono wa pole kwa mmoja wa ndugu wa  askari waliouawa baada ya kuvamiwa na majambazi  katika eneo la Mbande, Temeke ibada hiyo ya kuaga miili  ilifanyika katika viwanja vya  polisi vilivyopo barabara ya Kilwa,jijini Dar es Salaam.
 Naibu Waziri wa   Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni , akitoa mkono wa pole kwa mmoja wa ndugu wa  askari waliouawa baada ya kuvamiwa na majambazi  katika eneo la Mbande, Temeke ,ibada hiyo ya kuaga miili  ilifanyika katika Viwanja vya Kambi Kuu ya Polisi iliyopo barabara ya Kilwa,jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Wizara ya  Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, akizungumza wakati wa  kuaga miili ya askari waliouawa katika eneo la Mbande, Temeke baada ya kuvamiwa na majambazi .Ibada hiyo ya kuaga  ilifanyika katika Viwanja vya  Polisi  vilivyopo  barabara ya Kilwa,jijini Dar es Salaam
 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Ernest Mangu, akizungumza wakati wa maombolezo na kuaga miili ya askari waliouawa katika eneo la Mbande, Temeke baada ya kuvamiwa na majambazi.Ibada hiyo ya kuaga  ilifanyika katika Viwanja vya  polisi vilivyopo barabara ya Kilwa,jijini Dar es Salaam.

MIILI YA ASKARI WALIOUAWA NA MAJAMBAZI YAAGWA LEO KUPELEKWA MIKOANI KWA MAZISHI.

$
0
0
 Waziri wa Wizara ya  Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, akizungumza wakati wa  kuaga miili ya askari waliouawa katika eneo la Mbande, Temeke baada ya kuvamiwa na majambazi .Ibada hiyo ya kuaga  ilifanyika katika Viwanja vya  Polisi  vilivyopo  barabara ya Kilwa,jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Ernest Mangu, akizungumza wakati wa maombolezo na kuaga miili ya askari waliouawa katika eneo la Mbande, Temeke baada ya kuvamiwa na majambazi.Ibada hiyo ya kuaga  ilifanyika katika Viwanja vya  polisi vilivyopo barabara ya Kilwa,jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa  Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, akipita kutoa heshima za mwisho mbele ya majeneza yaliyobeba  miili ya askari waliouawa baada ya kuvamiwa na majambazi    katika eneo la Mbande, Temeke ,bada hiyo ya kuaga miili ilifanyika katika viwanja vya polisi  vilivyopo barabara ya Kilwa,jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa  Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, akitoa mkono wa pole kwa mmoja wa ndugu wa  askari waliouawa baada ya kuvamiwa na majambazi  katika eneo la Mbande, Temeke ibada hiyo ya kuaga miili  ilifanyika katika viwanja vya  polisi vilivyopo barabara ya Kilwa,jijini Dar es Salaam.
 Naibu Waziri wa   Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni , akitoa mkono wa pole kwa mmoja wa ndugu wa  askari waliouawa baada ya kuvamiwa na majambazi  katika eneo la Mbande, Temeke ,ibada hiyo ya kuaga miili  ilifanyika katika Viwanja vya Kambi Kuu ya Polisi iliyopo barabara ya Kilwa,jijini Dar es Salaam.
Askari wakimsaidia mzazi wa mmoja wa askari waliouawa baada ya kuvamiwa na majambazi  katika eneo la Mbande, Temeke, ibada hiyo ya kuaga miili  ilifanyika katika viwanja vya  polisi vilivyopo barabara ya Kilwa,jijini Dar es Salaam.
(Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

WABUNGE WA VYAMA VINNE WAKUBALI USHAURI WA VIONGOZI WA DINI.

$
0
0
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
VYAMA vinne vyenye uwakilishi bungeni vimesema kuwa watarejea bunge lijalo kutokana na ushauri wa viongozi wa dini waliokaa kujadili sintofahamu kwa vyama hivyo.

 Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa NCCR-MAGEUZI, James Mbatia amesema viongozi wa dini wamefanya kazi kubwa katika majadiliano hayo kwa kuweka masilahi mapana ya taifa.

Amesema kuwa kurudi katika bunge lijalo mpaka wabunge wote wa vyama wakutane na kuweza kufikia mwafaka huo kutokana na ushauri wa viongozi hao.

Mbatia amesema kuwa kuna vitu vingine huwezi kuangalia katika katiba huvyo unahitaji busara zaidi kwa kuangalia masilahi mpana ya taifa.

Amesema kuwa NaibuSpika , Dk.Tulia Ackson anatakiwa kuweka busara katika kuongoza bunge na kuacha taratibu kanuni za bunge pamoja na katiba.

Aidha amesema kuwa viongozi wa dini wameshauri vyama kurejea bungeni na kutaka masuala yao wanayoyataka kikatiba yatatuliwe.
.
Waandishi wakimsikiliza Mwenyekiti wa NCCR-MAGEUZI, James Mbatia leo Makuu ya chama NCCR -MAGEUZI jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa NCCR-MAGEUZI, James Mbatia akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani juu ya vyama vinne vyenye uwakilishi bungeni  vitarejea bunge lijalo kutokana na ushauri wa viongozi wa dini waliokaa kujadili sintofahamu kwa vyama hivyo katika mkutano uliofanyika leo Makao Makuu ya chama NCCR -MAGEUZI jijini Dar es Salaam.
 Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Zanzibar, Said Issa Mohamed akizungumza na waandishi habari juu ya maazimio ya viongozi wa dini jana katika mkutano uliofanyika leo Makao Makuu ya chama NCCR -MAGEUZI.(Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii.)

HAKUNA MWANASIASA ATAKAYERUHUSIWA KUVURUGA AMANI-MAJALIWA.

ZINGATIENI AMRI HALALI YA JESHI LA POLISI- MWAKYEMBE

$
0
0
Dkt. Mwakyembe Waziri wa Katiba na Sheria leo amezungumza maalum na TBC1 kuhusiana na kauli ya jeshi la Polisi . TBC1 walikuja kupata ufafanuzi juu ya uhalali wa kauli ya kuzuia mikutano iliyotolewa na jeshi la polisi leo.

WAZIRI wa Mambo ya  Katiba na Sheria Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe  amesema amri ya Jeshi la Polisi ya kuzuia mikutano ya nje na ndani ya vyama vya siasa ni halali ambayo kila Mtanzania na mwanachama wa chama chochote cha siasa anapaswa kuitii na kuizingatia na kwamba kutokufanya hivyo ni kuvunja sheria za nchi.

Amesema amri hiyo ni ya kudumu ambayo imelenga kuangalia na kufanya tathmini ya hali ya nchi kutokana na viashiria mbalimbali vya uvunjifu wa amani nchini ambavyo vimeanza kuonekana.

Dkt Mwakyembe alikuwa akijibu swali kutoka kwa Kituo cha Televisheni cha Taifa TBC 1 ambacho kilitaka kupata ufafanuzi  kuhusiana na uhalali wa kauli ya Jeshi la Polisi ya kuzuia mikutano ya ndani na ya hadhara kwa vyama vya siasa nchini. 

“Jeshi  la Polisi ni chombo halali cha cha dola kilichoanzishwa kisheria chenye wajibu wa kulinda usalama wa raia na mali zake ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na kuongeza kuwa  uamuzi huo una lengo la kulinda amani ya nchi na endapo kutakuwa na viashiria vya kutishia amani ya nchi yetu lazima hatua za kisheria na kinidhamu zichukuliwe. Ni amri halali na kila Mtanzania na mwanachama wa chama chochote nchini anapaswa kuitii na kuizingatia na kwamba kwenda kinyume ni  kukiuka sheria, ” alisisitiza Mhe. Mwakyembe.

Mhe. Waziri amesema ni haki ya vyama vya siasa kufanya mikutano ila wanatakiwa kutoa taarifa Polisi ili waweze kutoa ulinzi wakati wa mkutano huo na kuongeza kuwa Jeshi la Polisi linaweza kuzuia mikutano hiyo kwa sababu za kiusalama.

Mhe. Waziri pia alisema sio kweli kuwa Mhe. Rais amezuia mikutano ya siasa, bali alichofanya ni kudhibiti uendeshaji wa holela au huria wa shughuli za siasa nje ya maeneo ya uchaguzi ya wanasiasa na kuongeza kuwa Mhe. Rais amefanya hivyo kutokana na kiapo chake cha kuilinda, kuihifadhi  na kuitetea Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Taifa kwa ujumla.

“Mhe. Rais hajapiga marufuku siasa, alichofanya ni kudhibiti uendeshaji holela au huria wa shughuli za siasa nje ya maeneo ya uchaguzi ya wanasiasa husika kuepusha shari na chuki na amefanya hivyo kutokana na kiapo chake cha kuilinda, kuihifadhi na kuitetea Katiba ya Tanzania na taifa kwa ujumla wake. Kwa hatua hiyo Mhe. Rais hajafunga milango ya majadiliano. Milango iko wazi na tulitegemea wenzetu wangekuja na njia mbadala na kulizungumzia hilo badala ya kuitisha maandamano ya nchi nzima, alisema.

Mhe Mhe. Waziri amevitaka vyama vya upinzani nchini kukaa na kuzungumza na Serikali na kuacha kufanya vitendo vya kutishia uvunjifu wa amani kama kuitisha maandamano kwa nchi nzima. “Njooni tukae tuzungumze tupime ushauri wenu, hili ni taifa letu sote na milango iko wazi, tuache kuchochea vitendo vya uvunjifu wa amani kama ambavyo inavyoonekana nchini hivi sasa,” alisisitiza.

Amasema Sheria ya Vyama vya siasa hairuhusu kufanyika kwa maandamano kwa nchi nzima, kufanya hivyo ni kuchochea wananchi kuasi “civil disobedience” ni kinyume cha sheria na serikali haiwezi kuivumilia hali hiyo.  Mhe. Waziri ametoa wito kwa Watanzania wote kutoshiriki maandamano ya Ukuta ambayo alisema hayatakuwa na tija kwa nchi bali kuleta vurugu katika jamii.

WASANII WAPENDA AMANI WAUNGANA KUPINGA MAANDAMANO YA UKUTA.

$
0
0
 Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wasanii wapenda Amani nchini, Asha Baraka akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya tamko lao la kuungana pamoja kupinga Maandamano ya UKUTA, Septemba 1.  
Mwenyekiti wa Umoja huo, Steven Mengere (Steve Nyerere) akizungumza juu ya kupinga maandamano ya UKUTA yanayotarajiwa kufanyika  Septemba Mosi kote nchini.
Mwanamziki na Malkia wa Nyimbo za Taarab, Khadija Kopa akizungumza katika mkuatano wa Kupinga maandamano ya UKUTA jijini Dar es Salaam leo.
Mwanamuziki wa Bendi ya Twanga Pepeta, Ally Choki akizungumza katika Mkutano wa Kupinga maandamano ya UKUTA jijini Dar es Salaam leo.

WASANII mbalimbali wanaopenda amani wameungana kwa pamoja kupinga maandamano ya UKUTA yanayotarajiwa kufanyika Septemba Mosi, mwaka huu.

Akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari, Mwenyekiti wa Wasanii hao wapenda amani, Steve Nyerere amesema hamna haja ya maandamano bali tunahaja ya kufanya kazi hususan kwa vijana.

"Vijana ndio muhimili mkubwa kulinda amani ya nchi,tusiwaze maandamano bali tuwaze je Akinamama na Watoto wanapata huduma hospitali"alihoji Steve Nyerere

Kwa Upande wa Makamu Mwenyekiti wa Wasanii hao, Asha Baraka amesema wameamua kupaza sauti zao kwa niaba ya Wasanii wote wanaopenda amani.

Amesema Tanzania ni nchi ya Amani sio nchi ya vita hivyo wanapofanya shughuli za UKUTA shughuli zote za kijamii zitasimama.

Hatahivyo ameomba Septemba 1,  UKUTA wasimamishe maandamano hayo, pia watafute njia muafaka ya kuweza kuongea Vyama kwa Vyama na wakapata muafaka ili nchi iweze kwenda mbele. 

KATIBU MKUU WA MALIASILI NA UTALII, MAJ. GEN. GAUDENCE MILANZI AMEWATAKA MAJANGILI WATAFUTE KAZI NYINGINE

$
0
0
    Askari wanyamapori wakionesha kwa vitendo wakati wa kuhitimu mafunzo maalumu  yaliyofanyika katika Pori la Akiba la Rungwa  Mkoani Singida yaliyohitimishwa jana wakionesha namna ya kujificha wanapomkaribia jangili ili waweze kukamata. ( Picha na Lusungu Helela- MNRT)
1Askari wanyamapori wakionesha kwa vitendo wakati wa kuhitimu mafunzo maalumu  yaliyofanyika katika Pori la Akiba la Rungwa  Mkoani Singida yaliyohitimishwa jana wakionesha namna ya kupambana na majangili  wakati  wakiwakamata majangili ( Picha na Lusungu Helela- MNRT)
    Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudence Milanzi akifunga mafunzo maalum ya kupambana  na ujangili kwa Askari wanyamapori katika Pori la Akiba la Rungwa mkoani Singida jana. Mafunzo hayo yatawasaidia Askari wanyamapori kupata taarifa za kitenteligensia kwa ustadi wa hali ya juu katika kupambana na kukabiliana na  majangili. ( Picha na Lusungu Helela- MNRT)

 .   Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa wanyamapori Tanzania ( TAWA) Childress akizungumza wakati wa kufunga mafunzo maalumu ya ya kupambana  na ujangili kwa Askari wanyamapori katika Pori la Akiba la Rungwa mkoani Singida jana. Mafunzo hayo yatawasaidia Askari wanyamapori kupata taarifa za kitenteligensia kwa ustadi wa hali ya juu katika kupambana na kukabiliana na  majangili. ( Picha na Lusungu Helela- MNRT)
 Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Mark Childress akizungumza wakati wa kufunga mafunzo maalumu ya ya kupambana  na ujangili kwa Askari wanyamapori katika Pori la Akiba la Rungwa mkoani Singida jana. Mafunzo hayo yatawasaidia Askari wanyamapori kupata taarifa za kitenteligensia kwa ustadi wa hali ya juu katika kupambana na kukabiliana na  majangili. ( Picha na Lusungu Helela- MNRT)

Mitihani ya Taifa Darasa la 4 na Kidato cha 2 kufanyika kama kawaida

$
0
0
Na: Lilian Lundo - MAELEZO

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inaukumbusha Umma kuwa mitihani ya Taifa ya Darasa la 4 na Kidato cha 2 itaendelea kuwepo na mwaka huu itafanyika kama kawaida.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Leonard Akwilapo ameyasema hayo leo, jijini Dar es Salaam alipokuwa akikanusha taarifa za kutokuwepo kwa mitihani hiyo kwa mwaka 2016.

“Napenda niukumbushe Umma kuwa mitihani hii ni muhimu sana katika ufuatiliji wa maendeleo ya wanafunzi wetu. Kwa hiyo mitihani yote miwili itaendelea kuwepo na mwaka huu itafanyika kama kawaida. Kama kuna watu wanawaambia kuwa haitafanyika wawapuuze kabisa,” alifafanua Dkt. Akwilapo

Dkt. Akwilapo aliendelea kwa kusema kuwa, mitihani hiyo ina umuhimu mkubwa katika kupima maendeleo ya mwanafunzi kwa lengo la kufanya maendeleo ya kitaaluma. Aidha kwa wanafunzi ambao watakuwa hawajafikia viwango vya ufaulu vilivyowekwa watatakiwa kukariri darasa au kidato. 
 
Amebainisha kuwa Baraza la Mitihani ndilo lenye jukumu la kushughulikia maandalizi ya mitihani hiyo ikiwa ni pamoja na utungaji, uchapaji, ufungaji na usafirishaji hadi ngazi ya Mkoa na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) ikiwa na majukumu ya kuhakikisha kuwa uendeshaji na usahihishaji wa mitihani hiyo unafanyika kikamilifu

Madiwani kutoka Uganda wafanya ziara ya mafunzo Jijini Dar es Salaam

$
0
0
Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Mhe. Isaya Mwita Charles akipokea zawadi kutoka kwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Koboko, na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mamlaka za Miji nchini Uganda (UAAU) Mhe. Sanya Wilson(kushoto) wakati wa ziara ya Madiwani kutoka nchini Uganda leo Jijini Dar es Salaam. Anayeshuhudia ni Kaimu ya Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jiji la Dar es Salaam, Phillip Mwakyusa.
Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Mhe. Isaya Mwita Charles akimkabidhi zawadi Mstahiki Meya wa Manispaa ya Koboko, na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mamlaka za Miji nchini Uganda (UAAU) Mhe. Sanya Wilson(kushoto) wakati wa ziara ya Madiwani kutoka nchini Uganda leo Jijini Dar es Salaam. Anayeshuhudia ni Kaimu ya Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jiji la Dar es Salaam, Phillip Mwakyusa.




Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Mhe. Isaya Mwita Charles akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano baina ya Wataalamu kutoka Jijini la Dar es Salaam na Madiwani kutoka baadhi ya Halmashauri za Uganda Magharibi na Kaskazini wakati wa ziara yao ya kujifunza masuala mbalimbali leo Jijini Dar es Salaam.Kutoka kulia ni Mratibu wa Taifa wa Mtandao wa Majiji Tanzania (TACINE) Bw. Philotheusy Mbogoro, Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jiji la Dar es Salaam, Phillip Mwakyusa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Koboko, na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mamlaka ya Miji nchini Uganda (UAAU) Mhe. Sanya Wilson.
Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jiji la Dar es Salaam, Phillip Mwakyusa akielezea jambo wakati wa ufunguzi wa mkutano baina ya Wataalamu kutoka Jijini hilo na baadhi ya Madiwani kutkoka Halmashauri za Miji nchini Uganda wakati wa ziara yao ya kujifunza masuala mbalimbali leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Koboko, na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mamlaka ya Miji nchini Uganda (UAAU) Mhe. Sanya Wilson na Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Mhe. Isaya Mwita Charles
Afisa Uhusiano na Itifaki wa Jiji la Dar es Salaam Gaston Mwakwembe akielezea jambo wakati wa mkutano uliowakutanisha baadhi ya viongozi wa Halmashauri ya Jiji na baadhi ya Madiwani kutoka nchini Uganda leo Jijini Dar es Salaam. Madiwani hao wapo katika ziara ya kujifunza mambo mbalimbali ikiwemo Menejimenti ya Usafiri, Uchafu, Maji, Rasilimali watu, Fedha na namna ya kuongoza mabaraza ya Madiwani.
Mhandisi wa Barabara wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Swalehe Nyenye akiwasilisha maada kuhusu mkakati wa kuboresha usafiri katika Jiji la Dar es Salaam leo wakati wa ziara ya baadhi ya Madiwani kutoka Uganda walipo nchini kwa ajili ya kujifunza mambo mbalimbali ikiwemo Menejimenti ya Usafiri, Uchafu, Maji, Rasilimali watu, Fedha,Kilimo cha mjini,na namna ya kuongoza mabaraza ya Madiwani.
Afisa Utumishi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Godhelp Ringo akifafanua maada kuhusu muundo wa Jiji la Dar es Salaam wakati wa ziara ya baadhi ya Madiwani kutoka Uganda waliopo nchini kwa ajili ya kujifunza mambo mbalimbali ikiwemo Menejimenti ya Usafiri, Uchafu, Maji, Rasilimali watu, Fedha,Kilimo cha mjini,na namna ya kuongoza mabaraza ya Madiwani.
Baadhi ya Madiwani kutoka nchini Uganda wakifuatilia mada kutoka kwa wataalamu wa Jiji la Dar es Salaam wakati wa ziara kwa ajili ya kujifunza mambo mbalimbali ikiwemo Barabara na Mitaa, Menejimenti ya Usafiri, Uchafu, Maji, Rasilimali watu, Fedha,Kilimo cha mjini,na namna ya kuongoza mabaraza ya Madiwani.
Baadhi ya Madiwani kutoka nchini Uganda wakifuatilia mada kutoka kwa wataalamu wa Jiji la Dar es Salaam wakati wa ziara kwa ajili ya kujifunza mambo mbalimbali ikiwemo Barabara na Mitaa, Menejimenti ya Usafiri, Uchafu, Maji, Rasilimali watu, Fedha,Kilimo cha mjini,na namna ya kuongoza mabaraza ya Madiwani.
Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Mhe. Isaya Mwita Charles akimkabidhi zawadi Mstahiki Meya wa Manispaa ya Koboko, na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mamlaka za Miji nchini Uganda (UAAU) Mhe. Sanya Wilson(kushoto) wakati wa ziara ya Madiwani kutoka nchini Uganda leo Jijini Dar es Salaam. Anayeshuhudia ni Kaimu ya Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jiji la Dar es Salaam, Phillip Mwakyusa.
Picha na Frank Shija, MAELEZO.

JACQUELINE MENGI AUNGA MKONO JUHUDI ZA JPM KWA KUKARABATI NA KUNUNUA VITABU VYA MAKTABA

$
0
0

Mkurugenzi wa Dr.Ntuyabaliwe Foundation na Miss Tanzania 2000, Bi. Jacqueline Mengi (wa pili kushoto) akiwa ameongoza na Afisa Elimu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Raymond Mapunda (kushoto), Diwani wa Kata ya Mwananyamala, Songoro Mnyonge (wa tatu kushoto) pamoja na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kinondoni, Emmanuel Ntenga mara baada ya kuwasili shuleni hapo.
Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation na Miss Tanzania 2000, Bi. Jacqueline Mengi akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Msingi Kinondoni ambapo aliwahimiza kusoma kwa bidii vitabu hivyo ili kupanua ufahamu wao zaidi na hata kimasomo pia vitasaidia kuinua viwango vyao vya ufaulu.

Mkurugenzi wa Dr.Ntuyabaliwe Foundation na Miss Tanzania 2000, Bi. Jacqueline Mengi na uongozi wa shule hiyo kwa pamoja wakiimba na wanafunzi wa shule ya Msingi Kinondoni.
Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation na Miss Tanzania 2000, Bi. Jacqueline Mengi akizungumza na waandishi wa habari kwenye hafla ya uzinduzi wa maktaba ya vitabu aliyoipa jina la Dr. Ntuyabaliwe Foundation katika hatua za kumuenzi marehemu baba yake ambaye aliyemjengea misingi mizuri ya usomaji wa vitabu wakati wa makuzi yake
Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation na Miss Tanzania 2000, Bi. Jacqueline Mengi akionyesha wageni waalikwa picha mbalimbali za awali kabla ya kukarabati maktaba hiyo.

Afisa Elimu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Raymond Mapunda akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa maktaba ya Shule ya Msingi Kinondoni jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Miss Tanzania 2000, Bi. Jacqueline Mengi (katikati) pamoja na Diwani wa Kata ya Mwananyamala, Songoro Mnyonge.
Afisa Elimu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Raymond Mapunda na Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation, Miss Tanzania 2000, Bi. Jacqueline Mengi kwa pamoja wakizundua nembo ya taasisi hiyo.
Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation, Miss Tanzania 2000, Bi. Jacqueline Mengi wakipeana mikono na Afisa Elimu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Raymond Mapunda.



Miss Tanzania 2000, Bi. Jacqueline Mengi akimwonyesha baadhi ya vitabu Afisa Elimu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Raymond Mapunda vinavyopatikana katika maktaba hiyo.
Miss Tanzania 2000, Bi. Jacqueline Mengi akifurahi katika picha ya pamoja na baadhi ya walimu wa shule hiyo wakati akiondoka shuleni hapo.



Kwa kutambua umuhimu wa elimu kwa kizazi cha sasa na baadae, Jacqueline Mengi kupitia Taasisi yake ya Dk. Ntuyabaliwe ameamua kuunganisha nguvu kwa serikali ya awamu ya tano iliyo chini ya Rais Magufuli kwa kusaidia kuboresha upatikanaji wa elimu bora kwa kufanya marekebisho ya maktaba katika shule ya msingi Kinondoni.

Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo ambao uliambatana na uzinduzi wa Taasisi ya Dk. Ntuyabaliwe, Jacqueline amesaidia kufanya ukukarabati wa maktaba katika shule hiyo na kuweka vitabu ikiwa ni sehemu ya kumkumbuka baba yake Dk. Ntuyabaliwe kutokana na kupenda kwake kusoma vitabu.

Alisema baba yake alikuwa akiamini zaidi katika vitabu hivyo alipenda hata watoto wake wasome vitabu na anachokifanya yeye kwa sasa ni kuendeleza juhudi ambazo alikuwa akiifanya baba yake ya kuona watu wakisoma vitabu na matarajio yake ni kuona vitabu hivyo vikiwasaidia wanafunzi wa shule hiyo kuwaongezea uwezo wa kufaulu katika masomo yao ya darasani.

"Ndoto yangu ya muda mrefu leo imetimia, kila mtu ambaye alikuwa akimfahamu baba yangu Dk. Ntuyabaliwe alikuwa akifahamu kuwa alikuwa anapenda vitabu na hata sisi alituzoesha kusoma vitabu na hata kuanzishwa kwa taasisi hii ni sehemu ya kumkumbuka yeye,

"Naamini kuwa usomaji wa vitabu unaweza kumsaidia mtu kufika mbali hata kama sio katika elimu unaweza kumsaidia kwa jambo lingine hata katika maisha ... ndoto yangu ni kuona watanzania wote wanapenda kusoma kama baba yangu alivyokuwa anapenda kusoma vitabu," alisema Jacqueline.

Nae mgeni rasmi katika shughuli hiyo, Afisa Elimu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Raymond Mapunda alisema sio jambo rahisi serikali kuweza kumaliza changamoto zote zilizopo na kupitia watu wenye moyo kama wa Jacqueline ambao wanaunga mkono juhudi za serikali kunaweza saidia upatikanaji wa elimu bora.

Alisema kupitia maktaba hiyo anaamini ipo siku kutatokea mtu ambaye atakuwa na msaada kwa Tanzania ambaye wakati akisoma alikuwa akitumia maktaba ambayo imefanyiwa ukarabati na Jacqueline Mengi.

"Nimeona hali ambayo ilikuwa awali katika eneo hili na niseme tu Jacqueline atakuwa na yeye aliguswa na hali hiyo na nitumie fursa hii kumshukuru sana kwa msaada ambao ameutoa, shule inatakiwa kutoa elimu bora lakini ili kufikia malengo hayo kunahitajika kuwe na nyenzo za kutosha ambazo zitasaidia malengo ya kielimu kufikiwa," alisema Mapunda.

Kwa upande wa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kinondoni, Emmanuel Ntenga alimshukuru Jacqueline Mengi kwa msadaa wa kukarabati maktaba ya vitabu ili wanafunzi kujisomea, maktaba ambayo awali hawakuwahi kuwa nayo.

"Tunakushukuru sana kwa maktaba hii sasa wanafunzi wataweza kujisomea, tunafahamu juhudi za Dk. Mengi katika kusaidia elimu kwa kutoa madawati sasa na wewe umemuunga mkono tunawashukuru kwa hilo," alisema Ntenga.

GLOBAL EDUCATION LINK YAWANOA WANAFUNZI WANAOKWENDA KUSOMA VYUO VYA NJE

$
0
0
MKURUGENZI wa Kampuni ya Global Education Link (GEL) abdulmalik mollel amesema wanafunzi wanaokwenda vyuo vya nje ya nchi ni 350 kwa masomo ya utabibu, uhandisi, pamoja na biashara.

Akizungumza na wazazi na wanafunzi jana katika ukumbi wa mwalimu nyerere jijini dar es salaam, juu safari hiyo ,Mollel amesema kila kitu kifanyike kwa utaratibu ili kuondoa usumbufu wakati safari hiyo kwa wanafunzi hao.

Amesema wanafunzi hao wanakwenda huku tume ya vyuo vikuu nchini (TCU), ikiwa inatambua vyuo hivyo na kuwataka wazazi kuondoa hofu juu ya vyuo wanavyokwenda kusoma.

Aidha amesema Global Education Link (GEL), iko tayari kuhakikisha nchi inapata vijana wanapata elimu bora katika vyuo vya nje.

Amesema kuwa kusoma nje sio anasa kutokana na mahitaji yaliyopo vijana wanatakiwa kupata utaalam tofauti tofauti ili kuweza kufikia uchumi wa kati was viwanda.
Sehemu ya wazazi na wanafunzi na wazazi wakimsikiliza Mkurugenzi wa Global Education Link (GEL), Abdulmalik Mollel hayupo pichani katika mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam.


Sehemu ya wafanyakazi Global Education Link (GEL), wakiwa katika mkutano huo uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Global Education Link (GEL), Abdulmalik Mollel akizungumza na wazazi pamoja na wanafunzi juu ya safari wanafunzi wanaokwenda kusoma katika vyuo vya nje ya nchi katika mkutano uliyofanyika jijini Dar es salaam.
Mbunge wa Mfindi Kusini, Meadrad Kigola akichangia katika mkutano huo uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live




Latest Images