Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46362 articles
Browse latest View live

Shindano la kumtafuta mrembo wa mkoa wa Mwanza kufanyika june 14

$
0
0
Shindano la kumtafuta mrembo wa mkoa wa Mwanza, linatarajiwa kufanyika June 14 katika viwanja vya Yatch Club jijini Mwanza. 
Warembo 18 kutoka wilaya mbalimbali za mkoa wa Mwanza wamejitokeza kushiriki shindano hilo la aina yake huku....Burudani inayosubiriwa kwa hamu kubwa ni Mh. Mbunge Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu atakapo panda jukwaani kukumbushia enzi hizo...akishindikizwa na mkali mwingine Chege Chigunda kutoka TMK. 

Warembo wote wanatarajiwa kuanza kabi rasmi Jumanne hii katika moja ya hoteli maarufu jijini humo. Itakumbukwa mkoa wa Mwanza tayari ulishatoa Mrembo wa Tanzania, ambaye ni Nasreem Karim 2009 na Miriam Gerald 2010. 

Pamoja na mchakato wa shindano la urembo kuendelea kwa hivi sasa nchini, macho na masikio yapo mkoani Mwanza, ambako kumekua kukileta changamoto na upinzani mkali wa warembo kila Mwaka.


BASATA YAOMBOLEZA KIFO CHA MSANII ALBERT MANGWEA

$
0
0
Baraza la Sanaa la Taifa limepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za msiba wa msanii wa tasnia ya Muziki nchini Albert Mangwea a.k.a Ngwair.

“ Baraza limestushwa na kuhuzunishwa sana kutokana na taarifa ya kifo hiki cha Ngwair ambaye mchango wake unahitajika sana katika tasnia ya sanaa, pengo aliloliacha ni kubwa kwani ubunifu wao bado unahitajika katika tasnia hii.” Baraza linatoa pole kwa familia ya marehemu na wasanii wote nchini, aidha linawatakia moyo wa subira katika wakati huu wa majonzi ya kuondokewa na mpendwa wetu.

Tunaomba mwenyezi Mungu aipumzishe mahala pema peponi roho ya marehemu. Baraza liko pamoja na familia ya marehemu katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo, tutambue kuwa haya ni mapenzi ya Mungu.

Imetolewa na
Ghonche materego
Katibu Mtendaji
Baraza la Sanaa la taifa.

TANZANIA OIL AND GAS SUPPLIERS CONFERENCE 26th July 2013, HYATT REGENCY KILIMANJARO

$
0
0

Tanzania Oil and Gas Suppliers Conference (TOGSC) is a conference cum exhibition that will bring together key players from the supply chain together with stakeholders from the government and the oil and gas industry to discuss and engage on the different opportunities and challenges within the East Africa Scenario particularly Tanzania.

This conference that will incorporate suppliers within the oil and gas industry is a strategic event that has come at the right time considering the recent large and world class deposits of oil and gas in Mtwara and Lindi with potential for more to be discovered.

Within this new burgeoning oil and gas industry there is a need to bridge the gap of the supply chain between the suppliers/ service providers and the oil and gas industry Stakeholders. The conference will give suppliers especially the local Tanzanian suppliers the channels and means to harness and cater for this massive industry. 

Rais Kikwete ahudhuria ufunguzi wa mkutano wa TICAD V Yokohama

$
0
0
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe , Katibu Mkuu wa umoja wa Mataifa Ban-Ki Moon akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wengine wa Afrika wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa tano wa TICAD jijini Yokohama leo asubuhi.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa tano wa TICAD unaofanyika Mjini Yokohama, Japan, leo. Picha na Freddy Maro

SALAAM ZA RAMBI RAMBI KUFUATIA KIFO CHA MSANII ALBERT MANGWEA.

$
0
0
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO

 

               SALAAM ZA RAMBIRAMBI KUTOKANA NA KIFO CHA
BW. ALBERT MANGWEHA, (Man Ngwair)

1/06/2013.


Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, imepokea kwa mshituko na masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha msanii wa muziki wa kizazi kipya (Bongo fleva) Albert Mangwea, aliyefariki huko Afrika  Kusini katika hospitali ya St. Hellen akiwa katika shughuli za muziki, Jumanne  tarehe 28 Mei, 2013. 

Kifo cha Albert Mangwea ni pigo kubwa kwa fani ya muziki hapa nchini, na pia kimataifa. Na kutokana na umahiri wake katika fani hiyo ya muziki wa kizazi kipya hususan aina yake ya uimbaji ya “Free Style” alikonga mioyo ya wapenzi wake hasa vijana ndani na nje ya nchi.  Albert Mangwea atakumbukwa na wasanii na wapenzi wa muziki  kwa kipaji na juhudi zake za kukuza muziki hapa nchini. 

Serikali inawapa pole ndugu na jamaa wote  na kuwaomba wawe na uvumilivu na subira katika kipindi cha msiba.  Wito wa Serikali kwa wasanii na wananchi kwa ujumla ni kuendelea kumuenzi kwa  yale yote mazuri aliyoyafanya wakati wa uhai wake.

“Mwenyenzi Mungu ailaze roho yaAlbert Mangwea mahala pema peponi.”

 

 

Imetolewa na Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara

LOOKING FOR SPONSORSHIP/DONATION FOR TRANSPORT FAIR AND SPORTS EQUIPMENTS

$
0
0



LOOKING FOR SPONSORSHIP/DONATION FOR TRANSPORT FAIR AND SPORTS EQUIPMENTS


Kindly refer to the heading above concern.

We have the pleasure to write to you in order to request your support on different materials assistance for our Participating in the East Africa Cup June 25th to 30th 2013 in Moshi.The Organization is a registered national non-profit making and nongovernmental organization, it was registered on the 30th October, 2010 and registration number is No. 4047.Acot aims at supporting long-term socio-economic development projects which encourage self sufficiency for disadvantaged youth and community in Tanzania. In Rural and Urban in general.

Will offers an excellent opportunity to increase visibility of your organization with a prominent presence your company logo will be printed on the Jezzy, Tshirts, balls and Player bags will reach a thousand people of East Africa Cup participants of Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi and other Tanzanian throughout Moshi area. The flyer will also be posted on ACOT website and ACOT BlogSpot for duration of Six months.

If your interest please send us your email address to acottz@acottz.org , We will send to you annexed/attached Invitation letter, Summary Budget describing the basic needs in matter for Bus Fair and other equipments alike, Profile, Certificate.

Thank you in advance for your assistance and we are looking forward to receive your possible and positive response.


                                                Yours Faithfully
                                               Emmanuel Mwampishi
                                                  Director.
                                                Mobile:+255713 544271
                                                Email: acottz@acottz.org

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA MAJADILIANO YA KITAIFA YA USHIRIKIANO KWA MANUFAA YA WOTE JIJINI DAR LEO

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwahutubia washiriki wa Majadiliano ya Kitaifa ya Ushirikiano kwa manufaa ya Wote, wakati akifungua rasmi Majadiliano hayo yaliyoanza leo Juni 1, 2013 kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue, akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Waziri wa Viwanda na Biashara, Mary Nagu, kumkaribisha Mhe. Makamu wa Rais.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu ( Uwekezaji na Uwezeshaji) Dkt. Mary Nagu, akisoma Hotuba yake kabla ya kumkaribisha Makamu wa Rais kufungua Majadiliano hayo.

Sehemu ya washiriki wa Majadiliano hayo, wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati akisoma hotuba yake ya ufunguzi wa majadiliano hayo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Majadiliano ya Kimataifa ya Ushirikiano kwa Manufaa ya wote, baada ya kufungua majadiliano hayo leo. Picha na OMR.

Miss Kigamboni 2013 kujulikana juni 7

$
0
0
  kamati ya  miss Tanzania ilitembelea Miss kigamboni 2013 hivi karibuni wakiwa kwenye kambi yao ya mazoe na kutoa maelekezo kadhaa kwa washiriki wa shindano hilo.Shindano hilo linatarajiwa kufanyika juni 7 2013 katika ukumbi wa Navy Beach.

AAR WITH THE MINISTER OF INFORMATION, CULTURE ANS SPORTS DR. FENELLE MKUNGARA TO SUPPORT TLGU

$
0
0

The Minister of Information,Culture and sports Dr. Fenella Mkakangara handling the national flag to TLGU at the prss conference
AAR The Marketing Manager Tabia Masuddi handling Golf items to the Minister of Information,Culture and sports Dr. Fenella Mkangara at the Press conference held in Gold tower.
AAR Marketing Manager Tabia Masuddi speaking to the media on the reasons of AAR to sponsor TLGU for East and Central Africa Challenge Trophy, at the Press conference held in Gold tower
The Minister of Information,Culture and sports Dr. Fenella Mkakangara congratulating and providing her blessings to TLGU who are living today for East and Central Africa Golf Challenge Trophy in Lusaka, Zambia

kinana ahitimisha ziara yake mkoani njombe,avuna wanachama 160

$
0
0

Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwa katika picha a pamoja na baadhi ya washiriki walikuwa wakila kiapo mara baada ya kukabidhiwa kadi zao za uanachama

 Katibu Mkuu wa chama cha CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wakazi wa Mji wa Makambako mapema leo jioni wakati alipohitimisha ziara yake ya siku saba mkoani Njombe.Katika hitimisho hilo Ndugu Kinana ametembelea na kukagua miradi ya maendeleo katika wilaya zote za mkoa huo katika kuimarisha chama,aidha ziara hiyo ilikwenda sambamba na kuangalia utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya chama hicho cha CCM.Mkutano huo umefanyika katika uwanja wa Polisi mjini Makambako.Katika mkutano huo Kinana alikabidhi kadi kwa wanachama wapya wapatao 160 walioujiunga na chama hicho.
Katibu Mkuu wa chama cha CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akikata utepe kuashiria uzinduzi wa ofisi ya chama hicho katika tawi la Mizani mapme leo jioni.
Katibu wa NEC,Itikadi na Unezi,Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa Mji wa Makambako mapema leo jioni wakati wa hitimisho la ziara ya CCM mkoani Njombe,ikiwa ni siku ya siku saba.
Wadau wakifuatilia mkutano huo.
Ndugu Kinana akipata maelezo mafupi kutoka kwa mmoja wa kikundi cha Wajasiliamali  kutoka kata ya Mjimwema
Baadhi ya Wakazi wa Makambabo wakiwa wamekusanyika kwenye uwanja wa polisi,wakifuatilia kwa makini yaliyokuwa yakijiri uwanjani hapo.

TBL YAKABIDHI KISIMA CHA SH. MIL. 41 MBARALI,MBEYA

$
0
0

 Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Stephen Kilindo (kulia) akiwa na wafanyakazi wenzake  wakifurahia maji yanayotoka katika kisima walichosaidia kijijini isnura, wilayani Mbarali, katika hafla iliyofanyika hivi karibuni kijijini hapo.
Sehemuambapo kisima kimechimbwa

Kisima chenyewe kinavyoonekana

Kilindo (kulia) akizungumza na baadhi ya wanakijiji pamoja na wafanyakazi wa TBL wakati wa makabidhiano ya kisima hicho.

Mmoja wa viongozi wa kijij cha Isnura akitoa shukrani kwa TBL kwa kuwapatia msaada huo muhimu.

Baadhi ya wanakijiji wakishuhudia makabidhiano hayo.
Mkurugenzi waUhusiano na Sheria wa Kampuni ya Tbl, Stephen Kilindo akizungumza na wakazi wa kijiji cha Isnura alipokuwa ametembelea maendeleo ya ujenzi huo ambao umekamilika kwa asilimia Tisini aliwaasa Wananchi kuutunza mradi huo ili uweze kudumu milele.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Isnura Josphine Ndimilage amesema tatizo la maji lilianza mwaka 2008 baada ya idadi kubwa ya watu kuongezeka katika Mji wa Rujewa na kufanya maji yaliyokuwa yameletwa na kampuni ya Danida kupungua.


BAADA ya Wananchi wa Kijiji cha Isnura kata ya Mawindi Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya kuteseka kwa zaidiya miaka mitano kutokana na ukosefu wa maji safi na salama hatimaye neema yawaangukia baada ya kujengewa kisima kitakachozalisha maji miaka yote.
  
Akizungumzia adha ya Maji iliyokuwa ikiwasumbua wananchi hao, Mwenyekiti wa Kijiji hicho Josphine Ndimilage alisema tatizo hilo lilianza mwaka 2008 baada ya idadi kubwa ya watu kuongezeka katika Mji wa Rujewa na kufanya maji yaliyokuwa yameletwa na kampuni ya Danida kupungua.

Alisema baada ya watu kuongezeka maji yalianza kusumbua na kufikia hatua ya kugawana maji ambapo kijiji hicho kilikuwa kikipata mara moja kwa wiki hivyo kluwalazimu wananchi kutumia maji machafu yaliyotwama makorongoni maji ambayo yalikuwa yakitumiwa na mifugo.
  
Uchimbaji wa kisima katika Kijiji hicho umefadhiliwa na Kampuni ya Vinywaji ya Tbl kwa gharama ya Shilingi milion 41  ikiwa ni pamoja na Jenereta ndogo kwa ajili ya kupandisha maji katika Tanki kubwa lenye ujazo wa Lita 45,000.

Mkurugenzi wa Mawasiliano na Sheria wa Kampuni ya Tbl, Stephen Kilindo akizungumza na wakazi wa kijiji cha Isnura alipokuwa ametembelea maendeleo ya ujenzi huo ambao umekamilika kwa asilimia Tisini aliwaasa Wananchi kuutunza mradi huo ili uweze kudumu milele.
  
Alisema Kampuni yake imechimba kisima hicho kutokana na Maombi ya wananchi wa eneo husika yatokanayo na mahitaji ya maji, uwepo wa magonjwa, idadi ya watu na mwitikio wa wananchi wa kupokea mradi tangu katika hatua za awali jambo ambalo liliitikiwa vizuri na wakazi wa kijiji cha Isnura.
  
Alisema kutokana na mradi huo ambao utawanufaisha zaidi ya wakazi 4000 unakabiliwa na changamoto ya Nishati kwa ajili ya kupandisha maji kutoka chini hadi kwenye tanki ambapo Mkurugenzi aliwataka wanakijiji hicho kuchukua jukumuhilo na siyo kutegea ili wafadhili wafanye wao wenyewe.
  
Kilindo alisema Kampuni inafanya kazi ya kutoa misaada  ili kuisaidia Serikali kupunguza matatizo yanayowakabili wananchi ikiwa ni pamoja na kurudisha shukrani kwa kile kinachovunwa katika rasilimali za nchi kwa kutoa misaada mbali mbali katika jamii.
  
Aliongeza kuwa mradi huo haupo kisiasa na kuwaomba wananchi wamwandae kiongozi wa kuzindua mradi huo ambye hatakuwa mwanasiasa wa chama chochote cha Siasa uzinduzi ambo utafanyika Juni 27, Mwaka huu baada ya kukamilika kabisa.

Kwa upande wake Mkandarasi anayejenga kisima hicho Moses Francis Lujaji kutoka kampuni ya Water Family Co.Ltd  alisema tangu mradi huo uanze haujachukua muda mrefu kutokana na wananchi kuonesha ushirikiano na msaada kwa mafundi.

Aidha aliongeza kuwa baada ya kufanikiwa kuchimba kisima hicho chenye urefu wa Mita 80 walikuta maji mengi ambayo yakitumiwa vizuri hayataweza kukauka milele yote na kuongeza kuwa tayari Maabara ya Serikali  imeshaidhinisha maji hayo kuwa yanafaa kwa matumizi ya binadamu baada ya kupimwa.

Article 7

CUF YAFANYA MKUTANO MKUBWA VIWANJA VYA KIBANDA MAITI MJINI ZANZIBAR.

$
0
0
 Makamo Mwenyekiti wa kamati ya maridhiano Eddi Riami, akitoa nasaha zake kwa wazanzibari, huko katika Mkutano wa CUF ulifanyika kibanda maiti, nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
  Waandishi wa habari wa vyombo tofauti Nchini wakihakikisha wanapata matokeo mbalimbali yaliojiri katika Mkuto wa CUF uliofanyika kibanda maiti.
 Sehemu ya umati uliojitokeza leo Kibanda Maiti
 Katibu Mkuu wa CUF Taifa ambae pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamadi, akihutubia maelfu ya wananchi waliofika kiwanjani hapo leo jun 06 2013.
Msanii Talinyo na wenzake wa kikundi cha Full Matatizo cha  Bulioni Mjini Unguja wakitoa burudani katika Mkutano wa CUF ulifanyika kibanda maiti, nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar

Mabadiliko ya kuwasili kwa mwili wa Ndugu yetu Albert Mangweah

$
0
0
Kamati ya msiba tunaomba kutoa ya taarifa kwamba mwili wa Ndugu  yetu Albert Mangwea hautoweza kufika siku ya jumapili ya tarehe 2/ 06/2013 kama ilivyo taarifa hapo awali, hii ni kutokana na sababu  zilizokuwa nje ya uwezo wetu.

Kwa sasa tunasubiri taarifa kamili kutoka kwa wenzetu/wawakilishi  wetu waliopo nchini Afrika Kusini, mara tutakapopata taarifa hizo  tutawafahamisha zaidi.

Tunaomba radhi watanzania wote kwa usumbufu wote  uliojitokeza  tushirikiane na uvumilivu kwa hili.

Asante
Mwenyekiti wa Kamati
Kenneth Mangweha
…………………………………
Msemaji wa Kamati
Adam Juma


Kinana aibana Serikali,aitaka itatue kero za watanzania ikiwemo tatizo la mbolea na bei ya korosho.

$
0
0
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM), Abdulrahman Kinana akiwasili mapema leo kwenye uwanja wa Maji maji huku akiwasalimia wananchi mbambali waliofika kwenye mkutano wa ndani uliohusu mabalozi na wenyeviti wa chama hicho,katika mchanganuo wa kutekeleza Ilani ya chama cha CCM.

======   ========  ===== 

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM), Abdulrahman Kinana aimeitaka  Serikali kutatua kero za Watanzania ikiwemo ya tatizo la mbolea na bei ya korosho.


Akizungumza na viongozi wa ngazi mbalimbali na wanachama wa chama hicho mkoani hapa, Kinana alisema kuwa kuna mambo ambayo yamekuwa kero  kwa muda mrefu, hivyo lazima Serikali itafute majibu ili kutatua kero hizo.


Alisema kuwa amefanya ziara katika maeneo mbalimbali yakiwemo ya Mkoa  wa Njombe na kubwa ambalo amebaini licha ya juhudi ambazo Serikali inafanya katika kutafuta ufumbuzi wa kero za   wananchi bado kuna haja ya kuongeza kasi ya kushughulikia.  


"Hakuna sababu ya kila siku kuzungumzia matatizo hayo hayo, ndio maana   baadhi ya kero tayari CC imeagiza Serikali kuandaa taarifa ya namna   ambavyo imejipanga kutafuta ufumbuzi wake.


Hivyo   kikao kinachokuja CC itapewa majibu na kuona nini kinafanyika kumaliza   matatizo ya Watanzania,"alisema Kinana.   Kinana aliamua kutoa ufafanuzi huo baada ya viongozi wa Moa wa Ruvuma   kutoa kilio cha wananchi wa mkoa huo wanalalamikia bei ndogo ya   korosho, pembejeo za kilimo na hasa mbolea pamoja na migogoro ya ardhi ambapo wananchi wanadai fidia lakini hawalipwi. 


Kutokana na malalamiko hayo, Kinana alisema CCM ipo makini katika  kushughulikia matatizo ya wananchi na tayari imeshatoa maagizo kwa Serikali kutafuta suluhu ya matatizo hayo. Wakati huo huo, Kinana alisisitiza umuhimu wa viongozi wa CCM kwenda kwa wananchi kusikiliza matatizo yao badala ya kukaa kimya kwani  katika uchaguzi mkuu ujao kunaweza kuwa na maswali  mengi ambayo yanapaswa kujibiwa sasa. 


Alisema hakuna sababu ya viongozi kushindwa kusikiliza wananchi kwani nafasi ambazo wameomba hasa zile za kuchaguliwa waliomba wenyewe, hivyo hawana sababu ya kutowasikiliza wananchi.   Pia aliwataka viongozi kwenda kwenye mashina na mabalozi wa CCM kwani huo ndio msingi wa uwepo wa chama hicho na moja ya kazi ambayo amekuwa  akiifanya katika ziara yake ni pamoja na  kuwatembelea mabalozi na kusikiliza maoni na ushauri wao kwa kuwa wao ndio wapo karibu na wananchi.   

Kinana alitumia nafasi hiyo, kuweka wazi kuwa viongozi wa CCM  

wanatakiwa kutambua kuwa huu si wakati wa kubembelezana bali kila   kiongozi kwa nafasi yake atimize wajibu wake wa kuwatumikia  
wananchi huku akisisitiza hakuna sababu ya kuitana waheshimiwa bali viongozi waitane ndugu ili kuondoa ukuta kati ya wananchi.  
Pia aliwataka watendaji wa ngazi mbalimbali wa CCM kuacha tabia ya kuwa makawala wa kuchagua viongozi maana hiyo si kazi yao huku akitawaka wachape kazi kwa bidii na kutenda haki.

Alisema inasikitisha kuona baadhi ya watendaji wanakuwa na kazi ya kuwa mawaka kwa viongozi wanaotaka nafasi ndani ya chama hicho na matokeo yake hata wale wenye sifa wanakosa nafasi    jambo ambao sasa amesema hapana na kutaka haki itendeke kwa ngazi zote.

Alitumia nafasi hiyo kuweka wazi  wana-CCM wanatakiwa kuwa wamoja na kuwakumbusha heri wakabi wachache waadilifu badala ya kuwa na wanachama wengi ambao tabia zao ni za hovyo na hawana msaada wa kukisaidia chama chao kufanikisha utekelezaji wa Ilani ya CCM,

Akizungumza na viongozi wa mablozi wa CCM katika Uwanja wa Maji Maji mjini hapa Kinana aliwahakikishia kuwa ahadi zote za CCM zitatekelezwa lakini alitumia nafasi hiyo kmpongeza Waziri wa

Mambo ya Ndani ya Nchi Dk.Emmanuel Nchimbi kwa kazi nzuri ambayo amekuwa akiifanya ya kutekeleza ahadi za CCM katika jimbo lake lakini pia hata kazi kubwa anayofanya katika kulitumikia taifa kwa nafasi yake ya uwaziri wa Serikali ya Awamu ya Nnne. 

NSSF All Media Stars yavunja rekodi ya Bunge FC, Yaichapa bao 1-0

$
0
0
TIMU inayoundwa na wachezaji kutoka vyombo vya habari mbali mbali vilivyoshiriki katika michuano ya NSSF “NSSF Media All Stars” imevunja mwiko wa timu ya Bunge FC ya kutofungwa kwa miaka tisa baada ya kuichapa kwa bao 1-0.
Katika mchezo huo uliofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri na kuhudhuliwa na watazamaji wengi katika historia ya uwanja wa Jamhuri, ulikuwa mkali na wa kusisimua na timu zote zilishambuliana kwa zamu.
NSSF All Media ilianza mchezo huo kwa kasi kufanya mashambulizi makali katika dakika 10 za kwanza. Julius Kihampa alikosa bao la wazi katika dakika ya pili baada  ya pasi safi kutoka kwa Mbozi Katala ambaye alishirikiana vyema na Maulid Kitenge, Wilbert Molandi na Emmanuel China.
Dakika ya saba, shuti la faulo iliyopigwa na nahodha wa timu hiyo, Majuto “Ronaldo” Omary iligonga mwamba baada ya kumshinda kipa wa Bunge FC Idd Azzan ambaye hakuweza kufanya lolote.
NSSF All Media ilisheherekea bao lake pekee katika dakika ya tisa kwa kichwa kufuatia kazi nzuri iliyofanywa na Majuto ambaye aliwatoka walinzi wawili kutoka upande wa kulia na kupiga krisi safi.
 Bunge FC ilijikuta ikiutafuta mpira kwa tochi muda mwingi, ilishindwa kufanya mashambulizi ya kina karibu  dakika 70 na kuifanya NSSF All Media Stars iliyokuwa chini ya kocha wake, mchezaji wa zamani wa mabingwa wa soka nchini Yanga, Sanifu Lazaro ilitawala muda mwingi.
Baada ya goli hilo Bunge FC walijitahidi kushambulia lakini ngome ya NSSF Media Cup Stars FC chini ya kipa Said Ambua ilikuwa imara kuokoa hatari zote langoni.
Katika mechi ya wanawake, Bunge Quuens iliyokuwa ikiongozwa na Halima Mdee (GK) na Esta Bulaya (WD) ilitoka kifua mbele kwa magoli 31 kwa 18 ya NSSF Media Cup Stars Queens.
Katika mechi hiyo iliyoshuhudiwa na mawaziri mbalimbali pamoja na huku  mgeni rasmi akiwa  pamoja na Naibu Spika wa Bunge. Bunge Queens ilikuwa ikiongoza kwa magoli 17-10.
Magoli ya NSSF Media Cup Stars Queens yalifungwa na Lulu Habib na Imani Makongoro (GS) aliyemtoa jasho halima Mdee (GK).
Baada ya mechi hiyo Naibu Spika, Job Ndugai  alizipongeza timu za kombaini za NSSF hasa ya soka ambayo imeweka rekodi mpya kwa kuwafunga wabunge kwenye uwanja wao.
“ Mmeonyesha uwezo mzuri lakini pia mmeonyesha kweli nyie ni wachezaji makini kwani mara kwa mara wabunge hawafungwi hapa Dodoma lakini nyinyi mmekuwa wa kwanza hongereni sana," alisema Ndungai ambaye ndiye alikabidhi vikombe kwa washindi kwa kushirikiana na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, DK Ramadhan Dau.

FM ACADEMIA KUTUMBUIZA MISS KIGAMBONI 2013

$
0
0
BENDI ya FM Academia maarufu Ngwasuma wanatarajia kutoa burudani katika shindano la kumsaka malkia wa kitongoji cha Kigamboni 'Redd's Miss Kigamboni 2013' litakalofanyika Ijumaa Juni 7 kwenye ukumbi wa Navy Beach.

Mratibu wa shindano hilo, Somoe Ng'itu alisema jana kuwa maandalizi ya shindano hilo yako katika hatua za mwisho na wanamuziki wa bendi hiyo wameahidi kuonyesha burudani nzuri.  Alisema kuwa Ngwasuma wanatarajia kutumia shindano la Redd's Miss Kigamboni kutambulisha nyimbo zake mbili mpya ziitwazo Chuki ya Nini na mwingine uitwao Fataki.

Aliongeza kuwa warembo wanaendelea na mazoezi katika hatua za mwisho na wameahidi kutoa ushindani kwenye mashindano ya ngazi ya kanda ya Temeke baadaye mwezi ujao.  Alisema kwamba wanawashukuru wadau wote waliojitokeza kudhamini shindano hilo na kuongeza kuwa warembo 13 watapanda jukwaani kuwania taji hilo.


Taji la Redd's Miss Kigamboni linashikiliwa na Edda Sylivester ambaye alishika nafasi ya tatu katika shindano la Miss Tanzania mwaka jana. Katika kuwaanda washiriki wa shindano hilo, kamati ya Miss Tanzania chini ya Hashim Lundenga na mrembo wa nchi wa mwaka 1999, Hoyce Temu, walitembelea kambi hiyo ili kuwafunda warembo wawe tayari na uelewa wa sanaa ya urembo.


MABORESHO YANAYOENDELEA KATIKA USAFIRI WA BANDARI NA RELI YALETA NEEMA

$
0
0
 Rais wa Chama cha Wakala wa Forodha na Uondoshaji wa Shehena Tanzania (TAFFA) Bw. Stephen Ngatunga  wakati akitoa ufafanuzi  kuhusu mkutano wa Kimataifa wa Wakala wa Forodha katika nchi za Afrika na Mashariki ya kati  (RAME 2013) utakaofanyika jijini Dar es salaam kuanzia  Juni 19. Kushoto ni Mkurugenzi mshauri wa TAFFA.
 Rais wa Chama cha Wakala wa Forodha na Uondoshaji wa Shehena Tanzania (TAFFA) Bw. Stephen Ngatunga akisisitiza kuhusu serikali kulifanyia kazi suala uundaji wa mkakati wa kutangaza bandari zetu nje ya nchi kwa kufungua ofisi katika nchi zinazotuzunguka kwa lengo la kuongeza watumiaji wa bandari . Kushoto ni Mkurugenzi mshauri wa TAFFA na Bw. Jimmy Mwalugerwa (Mkurugenzi TAFFA).
 Viongozi wa Chama cha Wakala wa Forodha na Uondoshaji wa Shehena Tanzania (TAFFA). Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.





=======  ======= ========

MABORESHO YANAYOENDELEA KATIKA USAFIRI WA BANDARI NA  RELI YALETA NEEMA, TANZANIA KUWA MWENYEJI WA MKUTANO WA KIMATAIFA WA FORODHA.

Na. Aron Msigwa – MAELEZO.
2/6/2013, Dar es salaam.

Imeelezwa kuwa Tanzania itanufaika zaidi kibiashara kupitia bandari ya Dar es salaam, Mtwara na Tanga kutokana na serikali kuamua kufanya maboresho  makubwa katika sekta ya usafiri wa Bandari na  reli.
Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es salaam na Rais wa Chama cha Wakala wa Forodha na Uondoshaji wa Shehena Tanzania (TAFFA) Bw. Stephen Ngatunga  wakati akitoa ufafanuzi  kuhusu mkutano wa Kimataifa wa Wakala wa Forodha katika nchi za Afrika na Mashariki ya kati  (RAME 2013) utakaofanyika jijini Dar es salaam kuanzia  Juni 19.
Amesema Tanzania kupitia Chama cha Wakala wa Forodha na Uondoshaji Shehena Tanzania (TAFFA) itakuwa mwenyeji wa mkutano huo  utakaowashirikisha mawakala 300 wa makampuni ya usafirishaji na upokeaji wa mizigo , wafanyabiashara, maafisa wa serikali na mabalozi mbalimbali kutoka nchi za Mashariki ya kati.
Amesema mkutano huo wa siku 3 utakuwa na manufaa makubwa kwa wafanyabishara kutoka Tanzania kujenga mahusiano na kunufaika na fursa mbalimbali zilizo katika eneo zima la Afrika na Mashariki ya kati ,kuitangaza Bandari ya Dar es salaam, Tanga na Mtwara pamoja na kukuza utalii nchini.
Amefafanua kuwa Tanzania kupitia TAFFA  inakuwa mwenyeji wa mkutano huo kutokana na pendekezo lililopitishwa katika  mkutano mkuu wa dunia wa mwaka 2012 uliofanyika mjini Los Angeles, Marekani.


Ameongeza  kuwa katika mkutano huo wa Juni 19, rais wa Shirikisho la Kimataifa la Wakala wa Forodha na Uondoshaji wa Shehena (FIATA) Bw. Stanley Lim pamoja na wajumbe waandamizi wa shirikisho hilo kutoka nchi wanazoziwakilisha watajadili mambo mbalimbali ya kuboresha biashara katika ukanda wa nchi za Afrika na Mashariki ya Kati (RAME).
Katika hatua nyingine  Bw. Ngatunga  amefafanua kuwa  maboresho yanayoendelea hususan katika bandari ya Dar es salaam yanaifanya Tanzania kuwa katika nafasi nzuri ya kupanua wigo wa kunufaika na ongezeko la fursa za biashara  kwa nchi zisizo na ukanda wa bahari  zikiwemo Burundi, Rwanda , Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Uganda, Zambia na Malawi  kuendelea kutumia usafiri wa reli na Bandari za Tanzania kusafirisha mizigo.
Amesema kitendo cha serikali kufanya maboresho makubwa ya kiutendaji katika bandari na reli kimesaidia kuendelea kuleta imani kwa wafanyabishara kutoka nchi mbalimbali zisizo za ukanda wa Bahari kupitisha mizigo yao na kuongeza kuwa matatizo mbalimbali yaliyokuwa yakikwamisha uondoshaji wa shehena bandarini yamefanyiwa kazi.
Ameeleza kuwa serikali kukubali kulifanyia kazi suala la ukusanyaji wa mapato ya Bandari na kuagiza lifanyike  kupitia benki badala ya utaratibu wa awali wa kulipa fedha moja kwa moja bandarini limepunguza urasimu na kuongeza uwajibikaji na ukusanyaji wa mapato katika sekta hiyo.
“Kwanza suala la ukusanyaji wa mapato bandarini  lilisababisha usumbufu mkubwa, waziri wa uchukuzi alivyoingia tulimweleza na tukamwomba alifanyie kazi na jambo hilo likatekelezwa sambamba na uboreshaji wa huduma za usafiri wa reli ili kupunguza mrundikano wa makontena bandarini kanma ilivyoainishwa katika bajeti ya uchukuzi ya 2013/2014 limetufariji sana” ameeleza Bw.Ngatunga.
Aidha ameiomba serikali kulifanyia kazi suala uundaji wa mkakati wa kutangaza bandari zetu nje ya nchi kwa kufungua ofisi katika nchi zinazotuzunguka kwa lengo la kuongeza watumiaji wa bandari na kukabiliana na ushindani pamoja na kuwachulia hatua za kisheria wale wote watakaokwamisha ufanisi wa shughuli za bandari nchini.

Majadiliano ya Ushirikiano kwa wote ni kwa faida ya watanzania—Dkt. Nagu

$
0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwezeshaji, Dkt. Mary Nagu akisisitiza jambo wakati  wa mkutano wa kitaifa wa Majadiliano kwa manufaa ya wote jana jijini Dar es Salaam.  Wengine  katika picha ni Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue (kushoto) na Mkuu wa Jeshi la Polisi  nchini, Saidi Mwema.
=========  =======  =======
Majadiliano ya Ushirikiano kwa wote ni kwa faida ya watanzania—Dkt. Nagu

Serikali imesema Majadiliano ya Ushirikiano kwa Manufaa ya wote yanalenga kuwawezesha  watanzania kumiliki uchumi wao na nchi kufikia uchumi wa kati kufikia mwaka 2025.  Akiongea na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam wakati wa siku ya pili ya mkutano wa  Majadiliano ya Ushirikiano kwa Manufaa ya wote Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji  na Uwezeshaji, Dkt. Mary Nagu alisema serikali imejipanga kuona majadiliano hayo yanaleta mapinduzi  ya kiuchumi na kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha uchumi wa viwanda katika eneo hili la Afrika.

“Serikali imedhamiria kuhakikisha majadiliano haya yanaleta manufaa kwa wananchi wake na  majadiliano haya yanatoa msukumo wa kipekee kufanikisha hili,” alisema. Dkt. Nagu ambaye alikuwa Mwenyekiti wa mkutano huo kwa niaba ya ya Makamu wa Rais, Dkt. Ghalib  Bilal alisema serikali inataka kuona takwimu za kukua kwa uchumi wa nchi unaendana na maendeleo ya  watu wake katika kila pembe ya nchi na kwa kila mtu.

Mkutano huu wa siku mbili uliomalizika jana ni matayarisho ya mkutano wa kimataifa wa  Majadiliano ya Ushirikiano kwa Manufaa ya wote au “Smart Partnership Dialogue Global 2013”   unaotarajiwa kufanyika mwezi Julai mwaka huu hapa Tanzania. Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) kama taasisi ya serikali ilipewa jukumu la kuratibu  majadiliano haya kitaifa.  

Akiwasilisha mada katika mkutano huo, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Bw. Lucas  Kusima alisema usalama wa nchi ni mtaji wa maendeleo hivyo kila mtu hana budi kulinda  usalama wa nchi ili kufikia maendeleo ya kweli.

“Kama usalama haupo hakuna wawekezaji wala watalii watakaokuja,” alisema na kuongeza  kuwa usalama ni muhimu katika kukuza ushirikiano wa kimataifa. Alisema dalili za usalama kutoweka hapa nchini kama migogoro ya kidini, kisiasa, kugombea   ardhi kati ya wafugaji na wakulima haina budi kutafutiwa suluhisho la kudumu kwa faida ya  wananchi.


“Kuna umuhimu wa vyombo vya usalama kushirikiana na wananchi kuimarisha usalama wa taifa  zima kama kweli tunataka majadiliano haya yalete manufaa,” alisema. Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Saidi Mwema alisema wakati umefika wa makundi  mbalimbali nchini kuunda kamati za ulinzi katika maeneo yao ili kujihakikishia usalama.

Akitoa mfano alisema maeneo ya ibada kama makanisa, misikiti, maeneo ya kazi, na majirani   wanaweza kuunda kamati za ulinzi na jeshi la polisi liko tayari kuwawezesha mbinu mbalimbali   za ulinzi katika maeneo yao. “Jeshi la polisi linahitaji sana ushirikiano wa karibu na wananchi ili kufikia malengo ya usalama,”  alisema. 

Awali akifungua mkutano huo, Dkt.  Bilal alipendekeza majadiliano hayo kuanza kufanyika kila  mwaka hapa nchini ili kuharakisha maendeleo. 
Dkt. Bilal alisema kwenye ngazi ya mikoa na wilaya majadiliano hayo yafanyike kila mwaka  wakitumia mabaraza yao ya biashara ngazi husika kabla ya majadiliano ya kitaifa.

“Mabaraza ya biashara ya mikoa na wilaya yatasimamia utekelezaji wa mambo yaliyokubalika  ngazi husika na kufanyiwa tathmini kila mwaka,” alisema. Makamu wa Rais alisema kuwa majadiliano haya yanatoa fursa kwa viongozi wa serikali  kukutana na kada mbalimba za wananchi ili kujadiliana na kuelewa mambo yanayochangia   upatikanaji maendeleo endelevu.

Alieleza kuwa uzoefu unaonesha kuwa, mtu mmoja mmoja au makundi ya watu,  wakishirikishwa na kuhamasishwa katika jambo lolote, na wakiliamini na kulikubali; utekelezaji   wake huwa rahisi. “Azma hii itatusaidia katika utekelezaji wa mipango yetu ya maendeleo ya miakamitano na dira  ya maendeleo ya taifa ya 2025,” alisema.

Alitaja misingi ya majadiliano ambayo huleta maendeleo endelevu kama kuamini kwamba  jirani wa mtu akiendelea basin a watu wote wanaendelea na kwamba maendeleo hayaji kwa  kukwamishana na kulumbana bali kwa kushirikiana. Alitaja msingi mwingine kuwa ni watu wote ni sawa bila kujali nyadhifa zao kwenye jumuia  wanazoishi.

“Kila mtu anao mchango mkubwa katika kuleta maendeleo katika jumuiya anayoishi,” alisema. Alisema kuna umuhimu wa kuachana na dhana potofu ambayo viongozi wa juu hutoa maagizo  ngazi ya chini kwa utekelezaji na kuwa viongozi wakubali kupokea na kuthamini ushauri toka  chini kwenda juu kwa utekelezaji.

Alitaja msingi mwingine kama ni kuwa na muono wa pamoja na utekelezaji wa nidhamu wa hali  ya juu. Kabla ya majadiliano haya TNBC iliendesha mikutano ya kuelimisha wananchi kupitia makundi   mbalimbali kupitia  katika jumla ya kanda 11; tisa Tanzania bara na mbili Tanzania visiwani   
mmoja Pemba na mwingine Unguja.  

Mkutano huo ulihudhuriwa na watu zaidi ya 500 wakiwemo viongozi wa serikali toka mikoa  yote, vikundi mbalimbali na sekta binafsi.

Mwili wa Marehemu Mzee Felician Makwaia wasafirishwa leo kwenda Bukoba kwa Mazishi

$
0
0
  Picha ya Marehemu Mzee Felician M. Makwaia enzi za uhai wake.
 Watoto wa Marehemi Mzee Felician Makwaia,Christopher Makwaia ambaye ni mmoja wa Wakurugenzi wa Michuzi Media Group (wa kwanza kulia,waliovalia fulana zenye picha),Frank Makwaia,Robert Makwaia pamoja na Stella Makwaia wakiwa wamesimama pembeni ya Jeneza lenye mwili wa Marehem baba yao.Mwili wa Mzee Makwaia umesafirishwa leo kwenda kijijini kwake huko Bukoba mkoani Kagera kwa mazishi
 Mjane wa Marehemu Mzee Makwaia,Mama Makwaia (wa pili kulia).
 Katekist wa Kanisa Katoliki Mwenge,akiongoza ibada ya kuaga mwili wa Marehemu Mzee Felician Makwaia.
 Neno la Mungu likisomwa.
 Wasifu wa Marehemu Ukisomwa.
 Waombolezaji waliofika kuaga mwili wa Marehemu Mzee Felician Makwaia nyumbani kwa Familia Sinza Mori,jijini Dar es Salaam leo.Mwili wa Mzee Makwaia umesafirishwa leo kwenye Bukoba kwa mazishi. 
 Watoto wa Marehemu,kutoka kulia ni Frank Makwaia,Robert pamoja na Christopher Makwaia ambaye ni mmoja wa Wakurugenzi wa Michuzi Media Group.
 Waombolezaji wakiacha mwili.
 Mtoto wa Mwisho wa Marehemu Mzee Makwaia,Christopher Makwaia ambaye ni mmoja wa Wakurugenzi wa Michuzi Media Group akiuaga mwili wa Baba yake.
 Mjane wa Marehemu akiaga.
 Safari imeanza. 
Viewing all 46362 articles
Browse latest View live




Latest Images