Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live

Tume ya Mipango yakamilisha Mafunzo ya Wataalamu wa kufundisha Usimamizi na Utayarishaji wa Miradi ya Umma

$
0
0
Mchumi Mwandamizi kutoka Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Bi. Sauda Ponda akitoa neno la shukrani kwa uongozi wa Tume ya Mipango kwa niaba ya wahitimu.
Naibu Katibu Mtendaji kutoka Tume ya Mipango anayesimamia Klasta ya Biashara za Kimataifa na Mahusiano ya Uchumi, Bw. Paul Sangawe akifunga mafunzo ya kuandaa wataalamu wa kufundisha masuala ya Usimamizi na Utayarishaji wa Miradi ya Uwekezaji katika sekta ya Umma, pembeni yake ni Kaimu Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango anayesimamia Klasta ya Uchumi Jumla, Dkt. Lorah Madete.
Wajumbe wa mafunzo wakimsikiliza Naibu Katibu Mtendaji kutoka Tume ya Mipango anayesimamia Klasta ya Biashara za Kimataifa na Mahusiano ya Uchumi, Bw. Paul Sangawe wakati wa kufunga mafunzo hayo.

…………………………………………………………………..

Na Adili Mhina
Tume ya Mipango imekamilisha zoezi la kuandaa wataalamu wanaotarajiwa kutoa mafunzo juu ya usimamizi na utayarishaji wa miradi ya uwekezaji katika sekta ya umma kwa maofisa wa serikali walio chini ya Idara za Sera na Mipango na zile za Uwekezaji katika Wizara, Mikoa, Halmashauri, Mashirika pamoja na Taasisi mabalimbali za Umma hapa nchini.

Akifunga mafunzo hayo mwishoni mwa juma, Naibu Katibu Mtendaji kutoka Tume ya Mipango anayesimamia Klasta ya Biashara za Kimataifa na Mahusiano ya Uchumi, Bw. Paul Sangawe alisema kuwa katika awamu hii ambapo Shilingi trilioni 59 kati ya trilioni 107 zinatarajiwa kutolewa na Serikali pekee katika kutekeleza Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano, Serikali imeamua kujipanga upya ili kuhakikisha miradi yote itakayoanzishwa inaleta tija kwa wananchi.

“Tumeamua kujiandaa mapema kwa sababu tunatarajia miradi mingi mikubwa itaanzishwa katika kipindi hiki cha utekelezaji wa Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (FYDP II). Hivyo, ni muhimu huko mtakapoelekea kutoa mafunzo mhakikishe mnatoa mbinu sahihi za kukabili changamoto zinazojitokeza katika kutayarisha, kutekeleza na kusimamia miradi ya maendeleo”, Alisema Bw. Sangawe.

Sangawe aliongeza kuwa baada ya mafunzo hayo kuwafikia walengwa wote hakutakuwa na sababu kwa maofisa wa serikali kushindwa kuandaa, kutekeleza, kusimamia au kutoa ushauri sahihi pale serikali inapofanya uwekezaji kwa ajili ya miradi ya maendeleo.

Akitoa neno la shukrani kwa uongozi wa Tume ya Mipango kwa niaba ya wahitimu wote, Mchumi Mwandamizi kutoka Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Bi. Sauda Ponda alisema kuwa wahitimu wote walipata fursa ya kujadili, kuuliza na kufanya mazoezi mbalimbali katika vikundi kwa lengo la kuongeza uelewa na kuimarisha uwezo kwa ajili ya kwenda kutoa mafunzo kwa wahusika.

“Kwa niaba ya wenzangu wote napenda kutoa shukrani za pekee kwa Tume ya Mipango kwa kuandaa mafunzo haya, waalimu wetu kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wametufundisha vizuri na wametupa mazoezi ya kutosha na sote tuko tayari kwenda kutoa elimu hii kwa wenzetu,”. Alisema Bi. Ponda.

Wataalamu hao waliotumia siku tano kuchambua kwa kina Mwongozo wa Usimamizi na Utayarishaji wa Miradi ya Uwekezaji katika sekta ya Umma ambao ndio unaopaswa kufuatwa katika kutekeleza miradi yote ya serikali, wanatarajiwa kugawanyika katika makundi mbalimbali yatakayotoa mafunzo kikanda ambapo zoezi hilo litaanza tarehe 22 mwezi huu.

MAJALIWA: TUTAWANYANG’ANYA URAIA TULIOTOA KWA WAKIMBIZI WATAKAOBAINIKA KUTUUMIA VIBAYA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema kuwa wakimbizi waliopewa uraia wa Tanzania na kuitumia vibaya nafasi hiyo kwa kuingiza watu wengine kinyume cha sheria watanyang’anywa na kurudishwa walikotoka.

Aidha, Waziri Mkuu amewaomba viongozi wa dini wawe wanawaelimisha waumuni wao umuhimu wa kulinda amani na kuishi kwa kufuata sheria na taratibu za nchi husika.

Kauli hiyo imetolewa leo (Jumapili, Agosti 20, 2016) na Waziri Mkuu wakati akizungumza na waliokuwa wakimbizi wa Burundi ambao kwa sasa wamepewa uraia wa Tanzania wanaoishi katika Kata ya Katumba, Halmashauri ya Nsimbo wilayani Mpanda.

“Wakimbizi waliopewa uraia wameendelea kuingiza ndugu zao. Naagiza kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa ifanye ukaguzi katika kambi zote kwa sababu zimegeuzwa kuwa maficho ya kuwahifadhi watu wanaoingia nchini bila ya vibali,” amesema.

“Hakikisheni mnachukua hatua kwa wote watakaoingiza watu kinyemela katika kambi za wakimbizi za Mishamo na Katumba. Pia msiruhusu watu kuleta silaha kwenye maeneo haya. Tanzania watu wanaoruhusiwa kutembea na silaha ni askari tu,” amesisitiza.

Waziri Mkuu amesema lazima ulinzi uimarishwe katika maeneo ya mipakani na wasipofanya hivyo watu wengi wataingia nchini bila ya kuwa na vibali hivyo kusababisha ongezeko kubwa la idadi ya watu.

Wakati huo huo Waziri Mkuu ameuagiza uongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Mpanda wasiwaudhi wakulima na wafanyabiashara wadogo kwa kuwatoza ushuru kwenye mazao wanapotoka shambani kama debe moja la nafaka na wanaouza bidhaa ndogo ndogo.

“Mkulima ametoka shambani na debe moja la mahindi unamtoza ushuru maana yake nini? Halmashauri tusitafute mgogoro katika hili. Tafuteni biashara za kutoza ushuru, mkulima anatoka kijiji cha Kanoge anakwenda kijiji cha Ikongo ushuru wa nini? Waziri Mkuu amehoji.

Waziri Mkuu amesema “Tumewasisitiza mkusanye kodi lakini siyo hivyo. Mkiendelea kutoza ushuru kwa wakulima wanaotoka shambani na mahindi kidogo mtasababisha wakate tamaa ya kulima,”.

Akisoma taarifa ya maendeleo ya mkoa wa Katavi jana jioni (Jumamosi, Agosti 20, 2016) mara baada ya Waziri Mkuu kuwasili mkoani hapa Mkuu wa mkoa, Meja Jenerali (Mstaafu) Raphael Muhuga alisema mkoa una jumla ya wakimbizi 6,918 wanaoishi katika kambi za Mishamo na Katumba ambapo kati yake wakimbizi 2,150 waliomba uraia wa Tanzania na kunyimwa.

Alisema wakimbizi 2,489 walichagua kurejea nchini kwao Burundi ila bado wapo katika kambi hizo huku wengine 653 waliomba uraia lakini majina yao hayakuonekana kwenye orodha ya waliokubaliwa wala kukataliwa uraia hivyo mkoa unaendelea kufuatilia ili kujua hatma yao.

Mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa wakimbizi wengine sita walichagua kubaki nchini lakini hawakuomba uraia, 398 waliomba uraia ila fomu zao hazikukamilika,249 waliomba uraia ila majina yao hayakurudi huku wengine 973 hawakusajiliwa walipoingia nchini mwaka 2007/.2008.


IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAPILI, AGOSTI 21, 2016.

Rio2016: Mkenya Eliud Kipchoge ashinda mbio za marathon

$
0
0
 
Mkenya Eliud Kipchoge aliwaacha wenzake wakimfuata nyuma kwa kipindi kirefu na kufanikiwa kushinda medali ya dhahabu katika mbio za marathon upande wa wanaume katika michezo ya Olimpiki ya Rio de Janeiro.

Kipchoge mwenye umri wa miaka 31 ambaye alishinda mbio za London Marathon mnamo mwezi Aprili alitawala mbio hizo na kumaliza katika muda wa saa mbili,dakika nane na sekunde 44.

Feyisa Lilesa wa Ethiopia alimaliza wa pili akiwa nyuma ya Kipchoge kwa sekunde 70 ili kushinda fedha naye raia wa Marekani Galen Rupp akimaliza wa tatu na kujishindia medali ya shaba.Ushindi huo sasa unaipatia kenya medali yake ya sita kabla ya kukamilika kwa michezo hiyo siku ya Jumapili. 

Kenya pia ilijishindia medali ya dhahabu katika mbio za marathon upande wa wanawake katika siku ya kwanza ya mashindano hayo ambapo Jemimah Sumgong aliibuka mshindi.

BEI YA SAMAKI YAPANDA MNADA WA SAMAKI KAWE

$
0
0
Baadhi ya Samaki waliopatikana leo,walipokuwa wakiuzwa kwenye mnada wa samaki katika ufukwe wa Kawe,jijini Dar leo.Baadhi ya Wanunuzi wa samaki waliokuwepo kwenye mnada huo wamelalamikia bei ya samaki hao kuwa juu,ambapo nao wauza samaki wameeleza kuwa upatikanaji wa samaki hao kwa sasa umekuwa mgumu kutokana na hali ya hewa ya bahari,na kwamba samaki wamekuwa wakipatikana mbali,kufuatia hali hiyo samaki ni lazima bei yake iwe juu.

HUYU HAPA NDIYE MKUU MPYA WA WILAYA YA ARUSHA ALIETEULIWA LEO NA RAIS DKT JOHN POMBE MAGUFULI

$
0
0

 
Mkuu wa Wilaya ya Arusha mteule Bw. Gabriel Fabian Dagarro




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 21 Agosti, 2016 amemteua Bw. Gabriel Fabian Daqarro kuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha.

Bw. Gabriel Fabian Daqarro anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Mrisho Mashaka Gambo ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha.

Uteuzi wa Bw. Gabriel Fabian Daqarro unaanza mara moja.


Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es Salaam
21 Agosti, 2016

Wakili Ringia akanusha taarifa iliyotolewa na vyombo vya habari kuhusu Dk. Mengi kupandishwa kizimbani

$
0
0

Mkurugenzi wa Makampuni ya IPP, Dk. Reginald Mengi.

Kufuatia vyombo vya habari mbalimbali nchini kutoa habari ambayo inamhusu Mkurugenzi wa Makampuni ya IPP, Dk. Reginald Mengi kuwa anatakiwa kufika mahakamani Agosti, 24 mwaka huu kujieleza kwanini asifungwe kwa kushindwa kutekeleza hukumu ya kulipa Dola 598,750 (Bil. 1.20), wakili wa Dk. Mengi, Deogratias Ringia amekanusha habari hiyo.

Katika taarifa ambayo imetolewa na wakili Ringia, amesema kuwa akiulizwa na watu mbalimbali kama ni kweli kuna hati imetolewa na Mahakama Kuu ikimtaka mteja wake Dk. Mengi kufika mahakamani kujieleza kwanini asifungwe baada ya vyombo mbalimbali kuripoti kuwa anatakiwa kufika mahakamani lakini jambo hilo halina ukweli.

"Mhusika mkuu katika kesi hiyo ni kampuni nayoitwa KM Prospecting Limited ambayo Dk. Mengi siyo mwanahisa wala mkurugenzi katika kampuni hiyo. Kampuni hiyo ndiyo iliingia kwenye mkataba na wadai iliyopelekea kesi hiyo ya madai," alisema Ringia.

Ringia alisema hatua ya kumuunganisha Dk. Mengi katika kesi hiyo lilikuja baada ya mahakama kuamua hoja mbili zinazohusu kesi hiyo ndipo wadai ambao ni wafanyabiashara Muganyizi Lutagwaba, Eric Mshauri na Charles Mgweo kumuingiza Dk. Mengi katika kesi licha ya kuwa hausiki.

Baadhi ya vyombo vya habari vilivyoandika habari hiyo ni pamoja na gazeti la Jambo Leo, Daily News, The Citizen na mtandao wa Habari Leo Online.
Jambo Leo
Barua ya Mwanasheria wa Mengi 21-Aug-2016 14-39-27-page-001

TAASISI YA THE HOPE CAMPAIGN YATOA MSAADA KWA WATOTO YATIMA CHAMAZI JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0

Mratibu wa Taasisi ya The Hope Campaign, Mpelo Kapama (kushoto), akiwaelekeza maofisa wenzake kabla ya kwenda kukabidhi msaada huo.
Mizigo ikitolewa kwenye gari.
Aman Issaya wa taasisi hiyo akiwa na kiroba cha sukari akielekea eneo la makabidhiano.


Mratibu wa Taasisi ya The Hope Campaign, Mpelo Kapama, akiwa amebeba kiroba cha sukari wakati taasisi hiyo ilipotoa msaada wa vyakula na vifaa vya shuleni kwa Kituo cha Yatima Group Trust Fund cha Chamazi Temekie jijini Dar es Salaam leo.




Vifaa hivyo viwekwa sawa kabla ya kukabidhi.




Aman Issaya wa taasisi hiyo (kushoto), akimkabidhi Katibu Mkuu wa Kituo hicho, msaada huo. Kulia ni Mratibu wa Taasisi ya The Hope Campaign, Mpelo Kapama na Furaha Kapama.



Furaha Kapama (kushoto), akimkabidhi msaada Katibu Mkuu wa Kituo hicho, Fred George.





Upendo Kapama akikabidhi msaada huo.



Thomas Anzuluni akimkabidhi Katibu wa kituo hicho, Fred George msaada wa mafuta ya kula.




Mwakilishi wa Taasisi ya The Hope Campaign, Stela Mpelo (kushoto), akiwakabidhi vifaa vya shule watoto Yatima wa Kituo cha Yatima Group Trust Fund cha Chamazi Temeke jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Ofisa wa taasisi hiyo, Thomas Anzuluni na Katibu wa kituo hicho, Fred George.



Aman Issaya wa taasisi hiyo (kushoto), na Katibu Mkuu wa Kituo hicho wakiwa wameshika mipira iliyotolewa na taasisi hiyo kwa watoto wa kituo hicho.




Hapa ni kikosi kamili cha taasisi hiyo kabla ya kukabidhi msaada huo.


Ni pozi la kukata na shoka na vipeperushi mkononi.


Na Dotto Mwaibale

TAASISI ya The Hope Campaign imetoa msaada wa vyakula na vifaa vya shuleni kwa Kituo cha Yatima Group Trust Fund cha Chamazi Temeke jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kukabidhi msaada huo kituoni hapo Dar es Salaam leo asubuhi , Mratibu wa Taasisi hiyo Mpelo Kapama alisema msaada huo umelenga kuwasaidia watoto hao kwa ajili ya chakula na vifaa vya kusomea.

"Taasisi yetu kupitia kwa mwezeshaji wetu mkuu John Amigo imejijengea utamaduni wa kusaidia makundi mbalimbali yenye uhitaji kama watoto hao na kambi za ukimbizi na mara nyingi tumekuwa tukisaidia kituo hiki" alisema Kapama.

Katibu wa Kituo hicho cha Yatima, Fred George alisema ni muhimu kwa jamii kujitokeza kusaidia Yatima na kuwafariji kama ilivyofanya taasisi hiyo.

Alisema kituo hicho chenye watoto zaidi ya 150 kimekuwa na changamoto ya chakula, fedha za kuwalipa wafanyakazi pamoja na ujenzi wa uzio kwa ajili ya usalama.

MAWAKALA WA AIRTEL MONEY KUPATIWA MAFUNZO KUKUZA BIASHARA ZAO.

$
0
0
 Baadhi ya mawakala wa Airtel Money jijini Dar es Saalam wakifatilia kwa makini maelezo juu ya huduma ya Airtel Timiza yaliyotolewa kwenye semina ya mafunzo inayoshirikisha kampuni ya simu ya Airtel na washirika wake Jumo Tanzania.
Meneja wa Jumo Tanzania, Rwebu Mutahaba akiongea na mawakala wa Airtel (hawapo pichani) wakati wa semina ya uzinduzi wa mpango utakaowawezesha mawakala wa Airtel Money katika mikoa mbalimbali kupata elimu ya huduma ya Airtel  Timiza Wakala itakayowasaidia kupata mikopo isiyo na dhamana ili kukuza biashara zao . Semina ya mawakala iliyofanyika jijini Dar es saalam mwishoni mwa wiki.
 Wakala wa Airtel Money wa maeneo ya msimbazi kariakoo bwana Maneno George akiuliza swali wakati wa semina ya uzinduzi wa mpango utakaowawezesha mawakala wa Airtel Money katika mikoa mbalimbali kupata elimu ya huduma ya Timiza itakayowasaidia kupata mikopo isiyo na dhamana ili kukuza biashara zao . Semina ya mawakala iliyofanyika jijini Dar es saalam mwishoni mwa wiki.

Mawakala wa Airtel Money kupatiwa mafunzo kukuza Biashara zao
Airtel Tanzania inatangaza uzinduzi wa mpango wake utakaowawezesha mawakala wa Airtel Money katika mikoa mbalimbali kupata elimu zaidi kuhusu fursa zinazopatikana  katika bidhaa na huduma zake  ikiwemo  huduma ya Airtel Timiza wakala inayowawezesha mawakala kupata mikopo isiyo na masharti na kusaidia kukuza mitaji na biashara zao

Mafunzo hayo, ambayo yatawasilishwa kwa mawakala zaidi ya  1000 katika mikoa ya Dar es Salaam,Arusha, Mwanza Morogoro na Dodoma yameanza mwishoni mwa wiki katika mkoa wa Dar es salaam na yanategemea kumalizika agost 28 katika mkoani Morogoro .

Jackson Mmbando, Meneja wa Uhusiano wa Airtel Tanzania anasema, “Kusaidia biashara zistawi ni sehemu muhimu ya biashara ya Airtel na tuna shauku ya kuanzisha bidhaa za kibunifu zenye faida kwa jamii na wateja wetu wenye lengo la kuinua uchumi wao kote nchini. Mafanikio ya huduma ya mikopo ya Airtel Timiza yanatokana moja kwa moja na mtandao wetu mpana wa mawakala.  tunaamini mafunzo haya yataongeza uelewa mkubwa zaidi wa huduma za kifedha zinazopatikana kwa mawakala wa Airtel Money.”

Timiza Wakala,ni huduma inayowawezesha mawakala wetu nchi nzima kupataa mtaji wa kufanyia kazi  kupitia simu zao za mkononi,huduma hii  iliyozinduliwa mwaka mmoja uliopita, kwa sasa mtandao wa mawakala  50,000 wa Airtel Money nchini Tanzania wanaweza kutumia huduma hii. Theluthi moja ya mawakala wote wa Airtel Money hutumia Timiza, na baadhi ya mawakala sasa hivi wanakidhi vigezo vya kupata mikopo hadi Shilingi milioni moja.

Akizungumzia kuhusu jinsi Mawakala wanavyonufaika na Timiza Wakala, Mmbando anasema “Utafiti wetu unaonyesha kwamba mawakala wengi hutumia Timiza wakala  kuendesha biashara yao ya uwakala kwa kuweka pesa kwenye akaunti zao za Airtel Money kwaajili ya kufanya miamala na kuhudumia wateja.  Wakala anaamua kiasi cha pesa wanachotaka kukopa pia na masharti ya marejesho, hivyo kuwapa udhibiti wa fedha zao”

Mmbando alisema Katika kipindi cha mwaka jana Timiza imekuaa  kwa kiasi kikubwa na wateja wanathamini jinsi huduma hii inavyobadili maisha yao “Uhusiano kwa misingi ya kuaminiana umejengeka ambao unaturuhusu kutoa mikopo isiyo na dhamana kwa urahisi, wakati wowote mteja anapohitaji.  Sambamba na hilo wateja wetu wanaelewa kwamba kuzingatia masharti ya mkopo ili kupata mikopo mikubwa na kutumia huduma ya Timiza kama benki”.

Tunayo mabadiliko tuliyoyafanya katika kuboresha huduma hii ya   Timiza Wakala ikiwa nia pamoja na  kuwapatia mawakala uwezo zaidi wa kuchagua jinsi ya kulipa mikopo mapema kwa mafungu na kupata mikopo mikubwa, lengo la semina za mafunzo haya ni kuwaelimisha mawakala ili kupata uelewa zaidi kulinganisha na ilivyo sasa. Huduma ya Airtel Timiza pia inawawezesha wateja wetu kupata mikopo isiyo ya dhamana ya hadi shillingi laki tano, mawakala na wateja nchi nzima  kwa ujumla wanafaidia na huduma hii aliiongeza Mmbando

“Huduma ya Airtel Timiza imeendele kuungwa mkono na serikali na Benki kuu , na kuiwezesha Tanzania kuweka rekodi nzuri  katika kuwapatia wananchi wake mazingira wezeshi yanayowanufaisha kifedha.  Sisi Kama mtandao mkubwa zaidi wa simu nchini, tunajivunia mafanikio haya na  kuendeleza dhamira yetu ya  kutoa huduma za kibunifu za  kifedha kwa wateja nchi nzima,” anahitimisha Mmbando.

JUBILEE INSURANCE & AGA KHAN LAUNCHES JILINDE AFYA PRODUCT

$
0
0
Jubilee Insurance Tanzania CEO, George Allande officiate the product during the launch ceremony at Serena Hotel in Dar Es Salaam recently.

EFM KUZINDUA TAMASHA LA MUZIKI MNENE AGOSTI 28 MWAKA HUU KATIKA ENEO LA BOKO JIJINI DAR

$
0
0
 Meneja Mkuu wa Efm, Denis  Ssebo akizungumza leo na waandishi wa habari (hapo pichani) juu ya tamasha la kila mwaka lijulikanalo kama muziki mnene ambalo litaanza rasmi Agosti 28  mwaka huu katika eneo la Boko  jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa kitengo cha masoko na mawasiliano Vodacom, Nandi Mwiyombella akizungumza leo na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya kuidhamini Efm kwa sababu ni sehemu ya kuwafikishia muziki wateja wa vodacon  jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii).

REDIO ya burudani ya Efm imezindua tamasha la kila mwaka lijulikanalo kwa jina la MUZIKI MNENE,ambalo linatarajia kuanza rasmi Agosti 28  mwaka huu katika eneo la Boko.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Meneja Mkuu wa Efm, Denis  Ssebo amesema tamasha hilo litafanyika kwa kipindi cha wiki 12 sawa na miezi mitatu ambapo muziki utapigwa  katika bar 12 za vijijini vya Dar es Salaam na  Pwani ikiwa na kauli mbiu isemayo 'Tunasepa na kijiji '.

Alisema mziki mnene mwaka huu itaenda sambamba na kampeni ya nje ndani ambapo vipindi vinne vitarushwa moja kwa moja katika mtaa husika kwa siku nne mfululizo.

Ssebo alivitaja vipindi hivyo kuwa ni Uhondo ambacho kitafanyika siku ya jumatano, Sports headquarters siku ya Alhamisi, joto la asubuhi siku ya Ijumaa na Funga mtaa siku ya jumamosi ,ambapo pia utapigwa muziki wenye ladha ya singeli kwa lengo la kutafuta vipaji vya wasanii wa muziki huo.

Mkuu wa kitengo cha masoko na mawasiliano vodacom Nandi Mwiyombella alisema wanafurahi kuidhamini Efm kwa sababu ni sehemu ya kuwafikishia muziki wateja wa vodacon."Burudani ndio sehemu ya maisha ya kila mtu na lengo ni kuhakikisha kwamba wateja wetu anapata burudani ya muziki kupitia Efm,"amesema Nandi.

Dawasco Kanda ya Tabata yaendelea kutoa Vifaa kwa ajili ya wateja wanaunganishiwa huduma za maji

$
0
0

Na: Frank Shija, MAELEZO.

Huduma za uunganishaji wa mabomba ya maji kupitia program ya kuunganishwa bila ya kuwepo kwa gharama za awali kwa Wateja wa Dawasco Kanda ya Tabata waendelea kushika kasi kutokana na muitikio mkubwa wa wananchi wanaoishi maeneo hayo.

Hayo yamesemwa na Afisa Uhusiano wa Dawasco Makao Makuu Joseph Mkonya alipokuwa akijibu malalamiko ya mmoja wa wakazi wa Mtaa wa Tabata Segerea jana Jijini Dar es Salaam.

Mkonya alisemakuwa tangu zoezi hilo kuzinduliwa wananchi waliitikia kwa kiasi ambacho ilisababisha kujitokeza kwa changamoto ya uhaba wa vifaa kwa ajili ya shughuli hiyo na kupelekea waombaji wengi kuendelea kusubiri huduma hiyo muhimu.

“Kutokana na huduma hiyo kuwa ya bure muitikio umekuwa mkubwa hivyo kusababisha kuwepo na changamoto ya vifaa, hata hivyo suala hilo limekwishapatiwa ufumbuzi na tayari vifaa vimenunuliwa na kuanza kugaiwa kwa wananchi waliojaza fomu za maombi ya huduma hiyo”. Alisema Mkonya.

Kwa upande wake Meneja wa Dawasco Kanda ya Tabata Bi. Victoria Masele amesema kuwa katika kanda yake zoezi linaendelea ambapo takribani wiki moja sasa wateja wamekuwa wakipatiwa vifaa kwa ajili ya zoezi la kuunganisha mabomba ya maji katika maeneo yao.

“Mapaka sasa wateja wa Kanda ya Tabata tumeshawapa taarifa juu ya ujio wa vifaa ili waje kuvichukua kwa ajili ya kuvifanyia kazi” Alisema Victoria.

Aliongeza kuwa tangu zoezi hili liratibiwe jumla ya wateja 1500 wamekwishaunganishwa na huduma za maji katika maeneo mbalimbali ya Kanda ya Tabata inayojumuisha maeneo ya Mabibo hadi Vingunguti.

Kampuni ya Dawasco ambayo ndiyo msambazaji wa huduma za maji Safi Dar es Salaam, imeanzisha program ya kuhakikisha wananchi wengi zaidi wanafikiwa na huduma hiyo muhimu kwa kuwawezesha kuwaunganisha na huduma hiyo bila ya gharama za awali na baadaye mteja ataanza kulipia huduma hiyo kwa malipo ya Ankara ya matumizi.

Hakuna mvutano wowote kati ya Bandari na wamiliki wa Bandari Kavu

$
0
0

Benjamin Sawe-Maelezo

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) inapenda kutoa ufafanuzi juu ya habari iliyoandikwa na Gazeti la Mwanahalisi Toleo Na. 353 la Agosti 22-28, 2016 kama ifuatavyo;

Hakuna mvutano wowote ambao umetokea kati ya Mamlaka na Wamiliki wa Bandari Kavu nchini juu ya kuhifadhi mizigo inayopakuliwa bandarini. Mnamo mwaka 2008/2009 bandari ya Dar es Salaam ilikuwa inakabiliwa na shehena kubwa kuliko uwezo wake na hivyo kusababisha mlundikano wa mizigo bandarini hali ambayo ingeachwa kuendelea ingesababisha ufanisi kushuka.

Kutokana na hali hiyo wadau wa bandari walikubaliana kuanzishwa kwa bandari kavu ambazo zitafanya kazi kama ‘extension of the port’ ikiwa na maana kwamba mzigo utapelekwa katika bandari hizo na kuhudumiwa kama ambavyo ungehudumiwa ndani ya bandari.

Wadau waliingia mikataba ya jinsi ya kuhudumia shehena ya magari na makontena inayopitia bandari ya Dar es salaam.

Bandari ya Dar es Salaam ina uwezo wa kuhudumia magari 3650 ndani ya bandari kwa wakati mmoja na katika kipindi cha kuanzia Juni magari yote ambayo yalikuwa ya napelekekwa kwenye bandari kavu sasa yanahudumiwa bandarini kwa kasi na ufanisi mkubwa.

Kasi ya utoaji magari bandarini imepanda na wateja wanaridhishwa na tunawataka wateja kutoa taarifa endapo itachukua zaidi ya saa 48 kabla mteja hajatoa gari ndani ya bandari tofauti na ilivyokuwa awali ambapo mteja alikuwa analazamika kulipia gharama za storage. Ujio wa meli unaongezeka kila siku hivi sasa kuna wastani wa meli 5 kila siku zinazokuja na kutoka bandarini.

Ufanisi umepanda baada ya changamoto ambazo zilikuwepo kati ya Dec-June kufanyiwa marekebisho mbalimbali na Serikali. Mapato yameongezeka kufikia shs 662.000 bilioni 2015/2016 kiasi ambacho hakijawahi kukusanywa. Lengo tulilowekewa na Serikali ni kukusanya Trilioni moja ambalo tutalifikia.

Kushuka kwa shehena kwa kiasi kikubwa kunachangiwa na kushuka kwa kiasi cha uagizaji kutoka China ambayo inatumia sana shaba kutoka Zambia na DRC na utafiti unaonyesha kwamba siyo bandari za Tanzania tu ambazo zimeathirika bali ni bandari karibu zote Afrika Mashariki na Kusini.
Mamlaka inasisitiza ushirikiano na wadau katika kuhakikisha shehena inaongezeka na bandari inafanya kazi kwa ufanisi.

Mamlaka inaamini katika kuongeza ufanisi, kukusanya mapato na ushirikiano na wadau ili bandari ziweze kutoa mchango unaokusudiwa na Serikali katika kukuza uchumi wa Tanzania na jirani zinazotegemea bandari zetu.

Mfumo wa tiketi za Elektroniki Uwanja wa Taifa kuongeza mapato ya Serikali

$
0
0

Eneo lililowekwa mageti kwa ajili ya mashine za mfumo wa tiketi za eletroniki katika Uwanja wa Taifa.Picha na Genofeva Matemu - WHUSM
Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (kulia) akitoa maelekezo ya namna ya kutumia mfumo wa tiketi za eletroniki kwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye alipokuwa akikagua vifaa vya mfumo huo katika Uwanja wa Taifa leo Jijini Dar es Salaam Agosti 22,2016.
Kaimu Meneja wa Uwanja wa Taifa Bw. Julius Mgaya(katikati) akimuonesha moja ya mashine ya tiketi za kieletroniki Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye katika Uwanja wa Taifa leo Jijini Dar es Salaam Agosti 22,2016.

Na: Genofeva Matemu – WHUSM .

Serikali inatarajia kuongeza mapato katika Uwanja wa Taifa kwa kutumia mfumo wa tiketi za elektroniki ambapo wateja watahitajika kuwa na kadi za e-wallet pamoja na kufanya malipo kwa njia ya mtandao ili kuingia uwanjani.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye alipokua akikagua vifaa vya mfumo huo leo jijini Dar es Salaam katika uwanja wa Taifa.

Mhe. Nnauye amesema kuwa Mfumo wa elektroniki unatumia umeme na una UPS inayohifadhi umeme kwa masaa matatu hivyo wananchi wasiwe na wasiwasi kuhusiana na mfumo huo kwani unatarajiwa kukidhi huduma kwa wananchi wote watakaotumia uwanja wa taifa katika matukio mbalimbali.

“Ni vema wananchi mkajenga utamaduni wa kuwahi uwanjani wakati wa mechi ili kurahisisha na kutumia kwa makini mfumo wa elektroniki katika uwanja wa taifa unaotarajiwa kakabidhiwa rasmi tarehe 4 Septemba mwaka huu kwa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo” alisema Mhe. Nnauye

Naye Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Pro. Elisante Ole Gabriel amesema kuwa mfumo huo wa elektroniki katika uwanja wa taifa ni wa kisasa na utawawezesha watu wote kuingia uwanjani ndani ya dakika 180 hivyo kuokoa muda wakati wa kuingia uwanjani.

Prof.Gabriel amesema kuwa kila mashine itatumia sekunde mbili kumruhusu mteja kuingia uwanjani tofauti na awali ambapo ilimlazimu mteja kupanga foleni kwa kutumia tiketi za kawaida wakati wa kuingia uwanjani.

Aidha Kaimu Mkurugenzi Maendeleo ya Michezo Bw. Makoye Nkenyenge amesema kuwa mradi wa mfumo wa elektroniki katika uwanja wa taifa unaendelea vizuri ambapo hadi sasa mashine 20 za mfumo wa elektroniki zimeshawasili na ujenzi wa sehemu ya miundombinu kwa ajili ya mashine hizo umeshakamilika.

Vyama vya Michezo nchini vyashauriwa kujenga ofisi zao ndani ya Uwanja wa Uhuru.

$
0
0
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akiongozana na baadhi ya viongozi wa Wizara na Uwanja wa Uhuru mara baada ya kuwasili katika makabidhiano ya Uwanja wa Uhuru leo 22 Agosti 2016.
  Mhandisi Mshauri Bw Aloyce Moshi(Kulia) akitoa ufafanuzi kwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye(katikati)  kuhusu matengenezo yaliyofanyika katika Uwanja wa Uhuru , kushoto kwake ni  katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel.
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akijadiliana jambo na katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel wakati alipokuwa akikagua matengenezo ya Uwanja wa Uhuru leo Agosti 22 , 2016 kulia ni Mhandisi Mshauri Bw Aloyce Moshi  
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (katikati) akiangalia eneo ambalo limetengwa kwa ajili ya ujenzi wa ofisi  mbalimbali   kulia ni katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel  na kushoto ni Mhandisi Mshauri Bw Aloyce Moshi.

 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na waandishi wa habari wakati wa makabidhiano ya Uwanja wa Uhuru leo Agosti 22,2016 . 
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akiangalia nyasi za Uwanja wa Uhuru mara baada ya kukabidhiwa uwanaja huo baada ya matengenezo leo Agosti 22,2016 .
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye(katikati)  akijadiliana jambo na katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel (wa pili kulia) wakati alipokuwa akikagua matengenezo ya Uwanja wa Uhuru leo Agosti 22 , 2016 kulia ni Mhandisi Mshauri Bw Aloyce Moshi.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel akiweka saini makabidhano ya Uwanja wa Uhuru  kati ya Serikali na Kampuni ya BCEG ya China leo Agosti 22,2016.
   
 Meneja wa kampuni  BCEG Bw. Cheng Longhai akiweka saini makabidhano ya Uwanja wa Uhuru  kati ya Serikali na Kampuni yake ya  BCEG leo Agosti 22,2016.    
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel(kulia) akibadilishana hati za makabidhiano ya Uwanja wa Uhuru mara baada ya kumalizika kwa matengenezo leo Agosti 22,2016.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel(kulia) akionesha  hati ya makabidhiano ya Uwanja wa Uhuru kwa waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa matengenezo ya uwanja huo leo Agosti 22,2016 (katikati ) ni Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye.
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na waandishi wa habari na wadau wa michezo mara baada ya makabidhiano ya Uwanja wa Uhuru leo Agosti 22,2016.
 Muonekano wa Uwanja wa Uhuru mara baada ya matengenezo.
 Picha zote na Raymond Mushumbusi WHUSM
Vyama vya michezo nchini vimeshauriwa kujenga ofisi zao ndani ya uwanja wa Uhuru kuepukana na gharama za kukodi ofisi katika maeneo mengine.

Ushauri huo umetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye wakati akipokea Uwanja wa Uhuru uliokuwa unafanyiwa  matengenezo na  kampuni ya CBG.

Mhe. Nape Moses Nnauye amesema kuwa mpaka sasa michoro kwa ajili ya majengo ndani ya Uwanja huo ipo tayari na vyama vya michezo vinakaribishwa kuanza kujenga ofisi zao.

“Kama kuna vyama vya michezo vyenye uwezo binafsi au kama wanaweza kupata ufadhili wa kuja kujenga ofisi zao humu michoro ipo tayari na eneo lipo tayari ata kesho waje wajenge ” alisema Mhe. Nape.

Mhe. Nape amesisitiza kuwa zoezi hili litaratibiwa na Serikali moja kwa moja na kutoa nafasi kwa vyama vyenye uwezo kujitokeza na kuchangamkia fursa hiyo ambapo  ramani,michoro na eneo lipo tayari kwa ajili ya zoezi hilo.

Aidha Serikali imewaalika wadau mbalimbali kuwekeza katika michezo kwa kujenga miundombinu itakayosaidia kukuza vipaji kwa wanamichezo mbalimbali na kusukuma gurudumu la  maendeleo ya sekta ya michezo nchini.

Kwa upande wake katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel amevishauri vyama vya michezo nchini kuchangamkia fursa iliyotolewa na Serikali ya kujenga ofisi za vyama vyao ndani ya Uwanja wa Uhuru na kushauri wadau wa michezo kuwekeza zaidi katika michezo hasa kwa vijana.

“ Wadau kimbilieni fursa ndio hii ya kuwekeza katika michezo pamoja na vyama vya michezo kujenga ofisi zao ndani ya Uwanja wa Uhuru kwa ajili ya maendeleo yao na michezo nchini” alisema Prof Gabriel.

WAZIRI MKUU MAJALIWA ATEMBELEA ENEO LA INYONGA WILAYANI MLELE, KATAVI

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa wodi katika zahanati ya Inyonga wilayani Mlele amabayo inatarajiwa kupandishwa hadhi na kuwa hospitali ya wilaya . Alikuwa katika ziara ya mkoa wa Katavi Agosti22, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakiwapungia wananchi wa Inyonga baada ya waziri Mkuu kutawazwa kuwa Chief wa Wakonongo na kupewa jina la Chief Kayamba wa Kwanza katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Inyonga Agosti 22, 2016. Kulia ni Cheif wa Wakonongo, Kayamba wa Pili.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji ambaye pia ni Mbunge wa Katavi, Mhandisi Isaack Kamwelwe katika mkutano wa hadhara aliouhutubia kwenye uwanja wa shule ya msingi ya Inyonga wilayani Mlelele Agosti 22, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia Mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Shule ya Msingi ya Inyonga wilayani Mlele Agosti 22, 2016.

MBUNGE WA ILEJE,MH JANET MBENE AKABIDHI MIFUKO 50 YA SARUJI ILEJE SEKONDARI

$
0
0
 Mbunge wa Ileje , Mh Janet Mbene,akikabidhi mifuko 50 ya Saruji kwa Mkuu wa shule ya Sekondari ya Ileje Agrey Mwahihojo kwa ajaili ya ukarabati wa madarasa

 Mbunge wa Ileje Mh Janet Mbene akikagua Mabweni ya Wasichana  ya shule ya Sekondari ya Ileje
 Mbunge wa Ileje ,Janet Mbene akisalimiana na Makamu mkuu wa Shule ya Sekondari ya Ileje , Hamidu Mwabulanga

MARUFUKU 'UKUTA' JIJINI DAR

$
0
0
 Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro akionyesha site Mirror zilizoibwa katika magari leo jijini Dar es Salaam.
 Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro akizungumza na waandishi habari juu ya Operesheni mbalimbali za kanda hiyo pamoja na kuzuia maandamano ya UKUTA, jijini Dar es Salaam leo.
 Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro akionyesha magazine ya kuwekea risasi zilizokamatwa jijini Dar es Salaam.
 Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro akioyesha bastola aina ya Browning yenye  risasi sita iliyokamatwa jijini Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro akionyesha flana rangi mbalimbali zilizokamatwa. 
(Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii).

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limepiga marufuku maandamano ya Chama cha Demokrasia Maendeleo (CHADEMA) yanayopangwa  kufanyika Septemba 1 mwaka huu. Maandamano hayo  yamepewa jina la UKUTA ambapo wanachama wake wanataka kuingia mitaani kupinga kile wanachokiita ukandamizaji wa demokrasia.
 Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro amesema leo kwamba maandamano hayo hayatafanyika na jeshi la polisi limejipanga kuzuia maandamano hayo.
Kamanda Sirro amesema kuwa hakuna habari ya Ukuta na hakuna mtu atakayedhubutu kuingia barabarani kutokana jeshi lilivyojipanga kuhakikisha wananchi wanafanya shughuli zao bila kuingiliwa na kitu chochote.
Amesema kuwa utaratibu wa kufanya mikutano ya siasa umeelezwa hivyo kufanya mikutano bila kufuata utaratibu hautaruhusiwa.
Kamishina Sirro amesema kuwa kikundi/watu  wanaotaka kutumia siasa katika kuvunja Amani kwa Dar es Salaam hakuna kitu chochote kitafanyika kutokana na jeshi la polisi lilivyojipanga.
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, Agasti 20 majira ya saa 12:00 jioni lilipata taarifa toka kwa raia wema kuwa maeneo ya mtaa wa Ufipa Kinondoni kuna duka linauza flana rangi mbalimbali zenye maneno ya uchochezi yaliyoandikwa ‘’TUJIPANGE TUKATAE UDIKITETA UCHWARA’’ rangi nyeupe idadi yake 28, rangi nyekundu fulana 18 zenye  maneno ‘UKUTA’ fulana 6  za Kakhi zenye maneno ‘’UKUTA’ Na fulana zingine rangi nyeusi 23 zenye maneno ’’UKUTA’’. 
Aidha Polisi baada ya kupata taarifa hizo walifika eneo la tukio na kumkamata mtuhumiwa Yoram Sethy Mbyelllah (42) mfanyabiashara, mkazi wa Mburahati akiwa anauza fulana hizo dukani kwake. Mtuhumiwa anaendelea kuhojiwa na baada ya upelelezi kukamilika atafikishwa mahakamani.

Rais wa zamani Kenya Mwai Kibaki alazwa Afrika Kusini

$
0
0
 
Aliyekuwa Rais wa Kenya Mwai Kibaki, 84, amelazwa hospitalini nchini Afrika Kusini akipokea matibabu maalum baada ya kuugua mwishoni mwa wiki.

Kiongozi huyo wa zamani aliugua akiwa nyumbani kwake na akapelekwa hospitalini Karen, Nairobi Jumamosi jioni kabla ya kusafirishwa Afrika Kusini Jumapili.

"Aliandamana na daktari wake. Tunamtarajia arejee nyumbani hivi karibuni, na Wakenya watafahamishwa kuhusu hali yake wakati mwafaka," taarifa iliyotolewa na familia yake ilisema.

Desemba mwaka 2002, Bw Kibaki aliumia baada ya kuhusika katika ajali ya barabarani wakati wa kampeni na akapelekwa Uingereza kwa matibabu.
Aliapishwa kuwa rais muhula wake wa kwanza akiwa kwenye kiti cha magurudumu.

chanzo BBC

Rais Magufuli apokea taarifa ya ujenzi wa Kiwanda cha gesi asilia (LNG)

$
0
0
 Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwakilishi wa Kampuni ya Mafuta ya Stat Oil ya Norway, Bw. Oystein Michelsen kabla ya kupokea taarifa ya maendeleo ya mradi mkubwa wa ujenzi wa kiwanda cha kusindika gesi asili (LNG Plant) kinachotarajiwa kujengwa katika eneo la Likon'go, Mchinga Mkoani Lindi.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Meneja Biashara wa Kampuni ya Stat Oil ya Norway Oivind Holm Karlsen (watatu) kutoka kushoto mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. Wapili kutoka kushoto ni Mwakilishi wa Kampuni hiyo, Bw. Oystein Michelsen. PICHA NA IKULU



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 22 Agosti, 2016 amepokea taarifa ya maendeleo ya mradi mkubwa wa ujenzi wa kiwanda cha kusindika gesi asili (LNG Plant) kinachotarajiwa kujengwa katika eneo la Likon'go, Mchinga Mkoani Lindi.

Mwakilishi Mkazi wa Kampuni ya Statoil ya nchini Norway ambayo ni moja ya Kampuni zitakazowekeza katika mradi huo Bw. Oystein Michelsen amemueleza Rais Magufuli kuwa ujenzi wa kiwanda hicho unatarajiwa kugharimu Dola za Kimarekani Bilioni 30 sawa na zaidi ya Shilingi Trilion 65 za Kitanzania na kwamba uzalishaji unatarajiwa kuchukua muda wa zaidi ya miaka 40 baada ya kuanza.

Bw. Oystein Michelsen amebainisha kuwa Serikali ya Norway ina dhamira ya dhati ya kuhakikisha mradi huo unatekelezwa kwa manufaa ya pande zote na ameomba Serikali ya Tanzania iendelee kutoa ushirikiano ili kufanikisha ujenzi wa kiwanda hicho.

Kwa upande wake Rais Magufuli amemuhakikishia Mwakilishi huyo wa kampuni ya Statoil kuwa Serikali ya Tanzania ipo tayari kuhakikisha mradi unafanikiwa na ameitaka Wizara ya Nishati na Madini kupitia Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC) kushirikiana na wadau kutoka Wizara nyingine kuharakisha mchakato wa kuanza kwa ujenzi wa kiwanda hicho.
"Nataka kuona mradi huu unaanza kujengwa, tunachukua muda mrefu mno, kamilisheni mambo yaliyobaki ili wawekezaji waanze kazi mara moja" Amesema Rais Magufuli.

Dkt. Magufuli amesema mradi huo unatarajiwa kuzalisha ajira kwa idadi kubwa ya watanzania na utaiwezesha serikali kupata mapato kupitia tozo mbalimbali, na hivyo kutumika kuimaisha huduma za kijamii zikiwemo elimu, afya, maji na miundombinu.
Pamoja na Statoil kampuni nyingine zinazoshiriki katika uwekezaji wa mradi huu ni Shell, Exxon Mobil, Pavillion na Ophir.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es Salaam
22 Agosti, 2016.

BANK OF AFRICA WAFUNGUA TAWI JIPYA BABATI MKOANI MANYARA

$
0
0
Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Manyara Bw. Longino Kazimoto akikata utepe kuashiria kufunguliwa kwa tawi jipya la Bank of Africa mjini Babati.

Mwakilishi wa Mkuu wa mkoa Bw Longino Kazimoto, mkurugenzi mtendaji wa Bank of Africa Ammishaddai Owusu-Amoah na Meneja wa Tawi jipya la Babati Bw Goodluck Mwasa katika picha ya pamoja.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Bank of Africa Bw. Ammishaddai Owusu-Amoah akitoa hotuba fupi kwenye hafla ya uzinduzi wa Tawi la Benki hiyo huko Babati

Meneja wa Tawi jipya la Babati Bw Goodluck Mwasa

Meneja wa Tawi la Benki ya Bank of Africa Babati akifafanua kitu kwa Bw. Longino Kazimoto na Kamishna wa Polisi wa Mkoa wa Manyara Bw. Francis Massawe.

Waliokaa kutoka kushoto ni Bw. Samson Ntunga, akimuwakilisha Katibu Tawala (Manyara)Mkurugenzi Mtendaji wa wa Bank of Africa Bw. Ammishaddai Owusu-Amoah akiwa na mgeni rasmi Bw. Longino Kazimoto na RPC Mkoa wa Manyara Kamishna wa Polisi Bw. Francis Massawe.

Viewing all 46343 articles
Browse latest View live


Latest Images