Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46206 articles
Browse latest View live

Article 4

0
0


DC MTATURU AKEMEA SIASA TAKA ZINAZOCHANGIA KURUDISHA NYUMA MAENDELEO YA WANANCHI

0
0

Baadhi ya wagonjwa wakiwa katika hali ya ahueni mara baada ya kulazwa katika Hospitali ya Malkia wa Ulimwengu iliyopo katika Kijiji cha Puma
Dc Mtaturu Mtaturu akiwasisitiza watumishi wa Hospitali ya Malkia wa Ulimwengu kujiunga na mfuko wa Bima ya Afya ili wawe mabalozi katika kuwashawishi wananchi nao kujiunga katika mfuko huo
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu akiwa katika picha ya pamoja na watumishi ngazi ya juu katika Hospitali ya teule ya Makiungu pamoja na baadhi ya wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya
Dc Mtaturu akisisitiza jambo kuhusu utoaji bora wa huduma za afya
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu akiwasalimu baadhi ya wagonjwa ambao wamefikakupatiwa tiba hospitalini
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika ofisi za Mganga Mkuu wa Hospitali Teuli ya Makiungu
Baadhi ya watumishi wakisikiliza kwa makini hotuba ya Mkuu wa Wilaya ya Ikungi
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu akiwasisitiza wanawake wajawazito kuhudhuria Kliniki wiki 12 za mwanzo mara baada ya kuhisi kuwa ni wajawazito sawia na kuwashauri kufika Hospitalini wakiwa wameambatana na waume zao


Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza na watumishi wa Hospitali ya Malkia wa Ulimwengu iliyopo Kijiji na Kata ya Puma
Dc Mtaturu akizungumza na viongozi wa ngazi ya juu katika Hospitali Teule ya Wilaya ya ikungi Makiungu mara baada ya kuwasili katika Hospitali hiyo
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu akikagua jengo jipya linalojengwa kwa ajili ya wodi na baadhi ya Ofisi za Hospitali ya Malkia wa ulimwengu
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Hospitali ya Malkia wa ulimwengu, Na baadhi ya wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama Wilaya
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu akikagua Mtambo wa oxygen jinsi unavyofanya kazi mara baada ya kuzuru katika Hospitali Teuli ya Wilaya


Na Mathias Canal, Singida
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu ametoa onyo kwa wanasiasa wanaotumia vibaya madaraka yao kwa kushindwa kuwaelimisha wananchi juu ya umuhimu wa uchangiaji huduma za afya na badala yake kuwafanya kudumaa kifikra na hatimaye kushindwa kufika hospitalini kupatiwa matibabu hivyo kupelekea vifo vya baadhi ya wananchi ambao wameamini maneno ya kisiasa kuliko kauli za watendaji za kufika Hospitalini kwa ajili ya matibabu.

Ametoa onyo hilo hii leo wakati alipotembelea na kuzungumza na watumishi wa Hospitali teuli ya Makiungu Wilaya ya Ikungi, Mkoani Singida pamoja na Hospitali ya Misheni Cathoric Malkia wa Ulimwengu inayomilikiwa na Shirika la Mothers of the Holy Cross an Missionaries of the Holy Cross.

Mtaturu amesema kuwa serikali inatambua umuhimu na huduma bora zinazotolewa na taasisi za dini katika Wilaya ya Ikungi kwani sekta ya afya ni sehemu muhimu kusukuma maendeleo ya nchi endapo wananchi watakuwa na afya bora itakuwa nguzo yao ya kufanya kazi na kuendana na falsafa ya Serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais Dkt John Pombe Magufuli ya Hapa Kazi Tu.

Kauli ya watumishi wa umma ambao wanatumia vyeo vyao vibaya ikiwemo kuzuia wananchi kuchangia shughuli za maendeleo kama vile ujenzi wa Vituo vya afya na Dispensari jambo ambalo linajikita zaidi katika kudhoofisha afya za watanzania waishio katika maeneo ambayo hayana huduma za afya karibu.
Mtaturu amesema kuwa serikali kwa kushirikiana na hospitali hizo ili kuhakikisha kuwa changamoto mbalimbali zinatatuliwa ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa vifaa tiba, uwepo wa madaktari bingwa lakini ni muhimu wananchi kuchangia huduma za kijamii hususani sekta ya afya ili kuimarisha afya zao na kupunguza vifo visivyokuwa vya lazima.

Hospitali ya Makiungu ilianzishwa na Masista Wamisionari wa huduma ya tiba mnamo mwaka 1954 kwa mwaliko wa Baba Askofu Winters aliyekuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Singida wakati ule na ndio ilikuwa Taasisi ya kwanza kutoa huduma za afya katika Mkoa wa Singida.

Pamoja na huduma za tiba katika Hospitali ya Makiungu pia inatoa huduma za kinga kwa vijiji vilivyo karibu na hospitali katika vituo vitano kwa njia ya kiliniki tembezi walengwa wakuu wakiwa ni wajawazito na watoto wenye umri chini ya Miaka mitano.

Dc Mtaturu amesema kuwa katika Wilaya ya Ikungi kuna jumla ya Zahanati 34 katika Vijiji 34 pekee kati ya Vijiji 101 vilivyopo Wilayani humo kinyume kabisa na sera ya Taifa inavyoelekeza ya kuwa na Zahanati kwa kila Kijiji ili kupunguza kadhia wanazokumbana nazo madaktari bingwa kwa kuwahudumia wagonjwa wenye mafua badala ya magonjwa sugu na makubwa.

Amesema kuwa uchache na kusuasua kwa ujenzi na upatikanaji wa huduma za afya umechagizwa na kauli za kisiasa za kuzuia wananchi kuchangia shughuli za maendeleo jambo ambalo linazidi kurudisha nyuma maendeleo ya Vijiji, Tarafa, Wilaya, Mkoa na Taifa kwa ujumla.

Hospitali ya Malkia wa Ulimwengu inahudumia wagonjwa wa ndani ya Wilaya ya Ikungi na Wilaya nyingine za Mkoa wa Singida na hata nje ya Mkoa wa Singida kama Shinyanga, Manyara, Tanga, Dodoma, Mwanza, Arusha na hata nchi jirani kama vile Kenya na Malawi.

"Changamoto zote mlizo nazo tumezichukua na serikali itazifanyia kazi haraka iwezekanavyo ili kuinua huduma za afya na kuokoa vifo vya wananchi kisa matamko ya kisiasa, Lakini pia nataka niwakumbushe kuwa siasa zilishamalizika Tarehe 25 mwezi Octoba mwaka jana baada ya wananchi kufanya maamuzi yao kwenye uchaguzi Mkuu hivyo huu ni muda wa kufanya kazi kama ambavyo tumekuwa tukimsikia Rais akisema, Kwahiyo kuanzia leo sitaki siasa taka zenye kurudisha nyuma shughuli za maendeleo" Alisema Mtaturu

Aidha Dc Mtaturu amewapongeza watumishi wote katika Hospitali hizo mbili kwa jinsi ambavyo wanawahudumia wananchi kwa moyo mkunjufu pamoja na uchache wa vifaa tiba pamoja na uchache wa madaktari na Wauguzi lakini ameziomba Hospitali hizo kupunguza gharama za Dawa kwani kumekuwa na malalamiko kutoka kwa wananchi juu ya gharama kubwa zinazotakiwa baada ya matibabu sawia na kuwataka watumishi wote kutumia lugha nzuri kwa wagonjwa ili wagonjwa hao kupata tiba kwa amani na upendo.

Akisoma risala kwa mgeni rasmi kwa ajili ya Hospitali Teule ya Wilaya ya Makiungu Afisa utumishi katika hospitali hiyo, Mary Shirima ameiomba serikali kusaidia upatikanaji wa gari la wagonjwa katika Hospitali hiyo ambalo litafanya kazi masaa 24 ili kusaidia kupunguza vifo vya akina mama wajawazito ambao wengi wao wanaathirika kutokana na umbali wanaotoka kwa ajili ya kufika hospitalini kupatiwa tiba.

Shirima alisema kuwa mbali na gari la kubeba wagonjwa pia Hospitali hiyo inaidai serikali jumla ya shilingi milioni 466,072,500/= ikiwa ni fedha za serikali na baadhi ya watumishi ambao serikali imeshindwa kuwalipa watumishi katika kipindi cha mwaka mzima baada ya kusaini mkataba na Askofu wa Jimbo katoliki la Singida wa Hospitali ya Makiungu kuwa teule mwaka 2008.

Kwa upande wake Diwani wa Viti maalumu Tarafa ya Ihanja Rabeka Ntandu Chaimbo Amempongeza Mkuu huyo wa Wilaya kwa kuzuru katika Taasisi hizo zinazotoa huduma za afya kwa wananchi kwani zimekuwa msaada mkubwa kwa Wilaya ya Ikungi sambamba na Wilaya na Mikoa mingine nchini.

Naye Mkurugenzi wa Hospitali ya Malkia wa Ulimwengu Padri Manoel Tsino amesema kuwa wananchi wanapaswa kujiunga na Mfuko wa Bima ya Afya (CHF) ili kuwa na uhakika wa huduma bora ili pindi wanapoenda kupatiwa matibabu iwe rahisi kwao.

Sawia na ushauri huo kwa wanachi Padri Tsino pia amewashauri watumishi wote wa Hospitali hiyo kujiunga na mfuko wa Bima ya Afya kufikia mwishoni mwa mwezi huu ili kuwa mfano bora kwa wananchi ambao hawajajiunga na mfuko huo.

Ziara ya Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu hii leo ni ziara ya kwanza kuzitembelea Taasisi hizo tangu alipoteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya hiyo.

KUNDI LA ORIGINAL COMEDY LAINGIA MATATANI KWA KUVAA SARE ZA POLISI KWENYE HARUSI YA MASANJA MKANDAMIZAJI

0
0
Katika siku za hivi karibuni, kumejitokeza  tabia kwa baadhi ya watu wakiwemo wasanii watu wengine mmoja mmoja kutumia mavazi yanayofanana na sare za Majeshi ya Ulinzi na usalama hapa nchini likiwemo Jeshi la Polisi katika shughuli zao za kisanii au katika kazi mbalimbali, Jambo ambalo ni kinyume cha sheria, kanuni na taratibu za Nchi. 
Kwa mujibu wa Sheria ya kanuni za makosa ya Jinai, sura ya 16 na  marejeo yake ya mwaka 2002,  kifungu cha 178 (1) na  (2) kinachozungumzia makosa dhidi ya sare za majeshi ya ulinzi na usalama,  kinabainisha wazi kuwa ni kosa kisheria kwa mtu yeyote ambaye siyo mtumishi wa majeshi ya ulinzi na usalama kuvaa mavazi yanayotumiwa au kushabihiana na sare za majeshi hayo  bila kibali kutoka kwa  Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kufuatia  kitendo kilichofanywa na kundi la kisanii la “ Original Comedy” kuvaa mavazi yanayoshabihiana na sare za Jeshi la Polisi, Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar Es Salaam linachukua  hatua za kisheria dhidi ya wasanii hao.

Aidha Jeshi la Polisi nchini, linatoa onyo kali kwa mtu ama kikundi chochote kuacha kutumia  mavazi yanayofanana na sare zinazovaliwa na  majeshi ya ulinzi na usalama hapa nchini na atakayebainika hatutasita kuchukua hatua kali za kisheria dhidi yake.

Jeshi la Polisi linatoa rai kwa wale wote wenye mavazi yanayoshabihiana na sare za majeshi ya ulinzi na usalama  kuzisalimisha mara moja katika vituo vya Polisi vilivyokaribu nao.


 Imetolewa na:

Advera John  Bulimba – Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP)

Msemaji wa Jeshi la Polisi.
Makao Makuu ya Polisi.         

WAKUU WA WILAYA WASTAAFU WAUNDA SACCOS, WAJIPANGA KUWEKEZA DODOMA

0
0
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, (TAMISEMI), George Simbachawene, (watatu waliokaa), Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashantu Kijaji, (wapili waliokaa), Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya PSPF, George Yambesi, (wapili kulia), Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu, (wakwanza kushoto waliokaa) na Mwenyekiti wa Wakuu hao wa Wilaya wastaafu, Ramadhan Maneno, (wakwanza kulia waliokaa) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wastaafu hao
 Mgeni rasmi na wakuu hao wa wilaya wastaafu
 Mgeni rasmi na wakuu hao wa wilaya wastaafu
 Mkuu wa Wilaya Mstaafu, Erasto Sima
 Mkuu wa Wilaya mstaafu, Christopher Kangoye
 Shigongo, akisalimiana na Mkuu wa wilaya mstaafu, Mwalimu Zainabu R.M. Mbussi
 Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu, akifunga mafunzo hayo Agosti 16, 2016

 Meneja wa PSPF, anayeshughulikia Mpango wa Uchangiaji wa Hiari, (PSS), Mwanjaa Sembe, akitoa mada kuhusu faida za kujiunga na mpango huo
 Kaimu Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, (NHIF), Mkoa wa Ilala, Hipoliti Lello, akitoa mada kuhusu huduma zitolewazo na Mfuko huo hususan ushirikiano wa Mfuko huo na PSPF, katoa bima ya afya kwa wanachama wa PSPF
 Mkuu wa Wilaya Mstaafu, Betty Mkwasa, akifuatilia kwa makini mada zilizokuwa zikitolewa kwenye mafunzo hayo
  Mkuu wa Wilaya Mstaafu, Manzie Manguchie, akifuatilia kwa makini mada zilizokuwa zikitolewa kwenye mafunzo hayo
 Mwenyekiti wa Wakuu wa Wilaya Wastaafu, Ramadhan Maneno, (kushoto), akizungumza jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publisher, Eric Shigongo
 Mkuu wa Wilaya Mstaafu, Makunga, akitoa maoni yake kuhusu uanzishwaji wa SACCOS hiyo
 Meneja wa PSS, Mwanjaa Sembe, akimsikiliza Mkuu wa wilaya mstaafu, Erasto Sima
 Shigongo akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wakuu wa wilaya wastaafu, baada ya kuwapa elimu juu ya ujasiriamali
 Shigongo akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa PSPF
 Shigongo akisikiliza maswali ya wakuu wa wilaya wastaafu baada ya kutoa mada yake, iliyowavutia wengi
 Kaimu Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, (NHIF), Mkoa wa Ilala, Hipoliti Lello, (kushoto), akizungumza jambo na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Abdul Njaidi, (kulia) na Mtafiti wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Mapesi Maagi
 Shigongo aiasikiliza wakuu wa wilaya wastaafu baada ya kutoa mada yake juu ya ujasiriamali
 Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu, (wapili kushoto), akipokewa na Mwenyekiti wa Wakuu wa wilaya wastaafu, Ramadhan Maneno, (watatu kushoto), Katibu wa wakuu hao, Betty Mkwasa, (kushoto) na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo Abdul Njaidi wakati akielekea ukumbini kufunga mafunzo hayo Agosti 16, 2016
Shigongo akitoa mada yake.


NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
WAKUU wa wilaya wastaafu, wameunda Ushirika wa Kuweka na Kukopa, (SACCOS), ikiwa ni moja ya maazimio waliyotoka nay oleo Agosti 16, 2016, baada ya semina ya mafunzo ya siku mbili, iliyolenga kuwaelimisha namna bora ya kuwa wajasiriamali.
Akitangaza azimio hilo, mwishoni mwa mafuno hayo yaliyofadhiliwa na Mfuko wa Pensheni wa PSPF, na kufanyika makao makuu ya Mfuko huo jijini Dar es Salaam, Mjumbe wa Sekretariati ya wakuu hao wastaafu, Crispin Meela, alisema, wajumbe 10 wamechaguliwa na wana semina hao ili kushughulikia utaratibu mzima wa kuanzishwa kwa SACCOS hiyo haraka iwezekanavyo.
Wajumbe wa Kamati ya muda ya kusimamia mambo hayo ni pamoja na Ramadhan Maneno (Mwenyekiti), Betty Mkwasa (Katibu), Crispin Meela, Erasto Sima, Geogina Bundala, Farida Mgomi, Said Amanzi, Fatma Ally, Muhingo Rweyemamu na Manzie Mangochie.
Kwenye mafunzo hayo Wakuu hao wa wilaya wastaafu, waliweza kupata elimu kutoka kwa wataalamu mbalimbali wakiwemo Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Beng’ Issa, na wataalamu wa Saikolojia, na Wajasiriamali wenyewe kama vile Eric Shigongo.
Akifunga mafunzo hayo Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu, ametoa changamoto kwa wakuu hao wanaokadiriwa kufikia 100 na ambao wamejiunga uanachama wa Mfuko huo kupitia mpango wa uchangiaji wa Hiari, (PSS), kuwa uamuzi wao utawakwamua kiuchumi na wanachotakiwa ni kuwa na mpango kamambe utakaoweza kutekelezeka kwa ufanisi mkubwa.
“PSPF kama shirika lingine lolote lile la kutoa huduma za Pensehni na za kifedha, umoja huo ni fursa kubwa kwa Mfuko na ndio maana umeamua kuwaunga mkono  ili mmfikie azma yenu ya kuanzisha SACCOS hiyo”. Alisema.


Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Global Publishers, Eric Shigongo, akitoa mada juu ya ujasiriamali kwa Wakuu wa Wilaya wastaafu, wakati wa semina ya mafunzo ya ujasiriamali yaliyofadhiliwa na Mfuko wa Pensheni wa PSPF, na kufanyika makao makuu ya Mfuko huo jijini Dar es Salaam, Agosti 16, 2016.
 Mwenyekiti wa Wakuu wa wilaya wastaafu, Ramadhan Maneno

WAHARIRI WA HABARI WAPEWA SOMO KUHUSIANA NA MASUALA MBALIMBALI YA UWEKEZAJI NCHINI

0
0
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha Uwekezaji (TIC), Clifford Tandari akifafanua jambo wakati wa Kangamano la pili la Wahariri wa Habari lililofanyika mapema leo kwenye Makao makuu ya Ofisi hizo jijini Dar.PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI.

Bw. Tandari alieleleza lengo kubwa la kukutana na Wahariri na wanahabari kutoka vyombo mbalimbali ni kuwaeleza na kuwafanya watambue fursa na mchango wa Kituo cha Uwekezaji wa kunadi miradi ya uwekezaji, Kuishauri Serikali kuhusiana na masuala mazima yanayohusu uwekezaji na kuwahudumia wawekezaji kwa mtindo wa “One Stop Centre”. 

"Kama sote tunavyofahamu uwekezaji nchini umechangia kwa kiasi kikubwa sana kukuwa kwa uchumi wetu. Nchi ambayo haivutii wawekezaji na kutengeneza mazingira mazuri ya biashara kamwe haiwezi kufanikiwa katika uchumi wake. Kubwa zaidi ni kwamba Tanzania inashindana na nchi zingine zote duniani katika kuvutia wawekezaji hao hao, hali ambayo inatuhitaji kuwa makini zaidi na jinsi tunavyowahudumia wawekezaji wa ndani na wale wa nje wanaotaka kuja kuwekeza nchini mwetu" alisema Bw. Tandari.

Bw. Tandari alisema kuwa TIC kwa sasa imejipanga katika kuandaa mpango mkakati ambao utaweza kurahisisha Utekelezaji wa majukumu ya Kituo na kusimamia utekelezaji wa maagizo na malengo yake, Alisema kuwa wanaamini mpango mkakati huo utarahisisha Usimamiaji wa shughuli na mipango yao na kwamba wanategemea mpango mkakati huo utaweza kusaidia Kituo kuhakikisha Utekelezaji wa Majukumu yao unaendana na mahitaji ya Mpango Mkakati wa Miaka Mitano. 
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha Uwekezaji (TIC).Clifford Tandari akifafanua mambo mbalimbali kuhusiana na sula zima la uwekezaji hapa nchini wakati wa Kangamano la pili la Wahariri wa Habari lililofanyika mapema leo jijini Dar.

Bw. Tandari alieleza kuwa Kituo cha Uwekezaji kina mkakati maalumu wa kuhakikisha upatikanaji wa Sera na Sheria Mpya ya Uwekezaji kwani ile ya awali imepitwa na wakati. "Sera yetu ya Uwekezaji pamoja na Sheria vimepitwa na wakati na haviendani na mazingira ya sasa na tupo kwenye taratibu za kufanyia marekebisho sera na sheria ili kuhakikisha vinakidhi mahitaji ya sasa na ya baadaye ya nchi yetu katika masuala yanayohusu Uwekezaji"alisema Bw. Tandari.

Alisema kuwa Vivutio vingi wanavyopewa wawekezaji vinalenga kuwapa nafasi ya kuanza kuzalisha bidhaa zao mapema na hivyo kuwa na uwezo wa kulipa kodi katika muda mfupi zaidi. "Kwa misingi hii kivutio kikubwa kuliko vyote ni huduma wanayoipata kutoka serikalini kuwa bora, ya haraka na isiyo na ukiritimba unaozaa usumbufu mkubwa kwa wawekezaji. 

"Mkakati wa Serikali ni kukiwezesha Kituo chetu kuboresha huduma bora chini ya “One Stop Shop” kwani ni muhimu sana katika kuondoa usumbufu kwa wawekezaji na kujenga mazingira bora ya uwekezaji kwa wote. Mwekezaji hana haja ya kuzunguka ili kupata vibali mbalimbali. Badala yake Anapata huduma ya vibali hivi kupitia Kituo Cha Uwekezaji" alisema Bwa.Tandari .
Meneja Mahusiano wa Kituo cha Uwekezaji (TIC) Pendo Gondwe akiratibu mijadala iliokuwa ikiendelea wakati wa Kangamano la pili la Wahariri wa Habari.lililofanyika mapema leo makao makuu ya ofisi hizo jijini Dar.
Baadhi ya Makaimu Wakurugenzi wa TIC wakifuatilia yaliyokuwa yakijadiliwa kwenye wakati wa Kangamano la pili la Wahariri wa Habari.lililofanyika mapema leo makao makuu ya ofisi hizo jijini Dar.

Waziri wa Viwanda Mh Charles Mwijage azindua Upanuzi wa kiwanda cha saruji TANGA

0
0

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage, akizindua rasmi upanuzi wa kiwanda cha saruji Tanga (Tanga Cement Company Ltd.) upanuzi huo umehusisha kuongeza Tanuri no. 2 (Kiln no. 2) ambapo uzalishaji utaongeza hadi kufikia tani mil. 1.25 kwa mwaka, kiwanda kimewekeza dola za kimarekani mil. 152 katika kufanikisha upanuzi huo.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage, akihutubia mara baada ya upanuzi wa kiwanda cha saruji Tanga (Tanga Cement Company Ltd.), shughuli hii ilihudhuriwa na Viongozi, Wabunge wa Mkoa wa Tanga, Wafanyakazi wa Kiwanda na Uongozi wa Kiwanda.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage, akizungumza na Mwenyekiti wa Bodi ya Kiwanda cha saruji cha Tanga Bw. Lawrence Masha.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage, akikata utepe kuashilia uzinduzi rasmi wa upanuzi wa kiwanda.
Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa katika uzinduzi huo
Mkurugenzi mtendaji wa Kiwanda cha saruji cha Tanga Ndugu. Reinhardt Swart akihutubia wakati wa mkutano huo.
Mku wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Ndugu, Martin Shigella Akihutubia katika uzinduzi huo.

WAZIRI WA AFYA MHE.UMMY MWALIMU AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA ISRAEL NCHINI.

0
0



Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akizungumza na Balozi wa Israel nchini Tanzania anayezihudumia pia nchi Afrika Mashariki za Kenya na Uganda Mhe. Yahel Vilan (kulia) Ofisini kwake leo jijini Dar es salaam. Pamoja na mambo mengine viongozi hao wamejadili kuhusu uanzishwaji wa ushirikiano katika maeneo mbalimbali yatayoinufaisha Tanzania na Israel kwenye sekta ya Afya.

Balozi wa Israel nchini Tanzania anayezihudumia pia nchi Afrika Mashariki za Kenya na Uganda Mhe. Yahel Vilan (kulia)akimweleza jambo Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu mara baada ya kumtembelea Ofisini kwake leo jijini Dar es salaam.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu (katikati) akifurahia jambo mara baada ya kumalizika kwa mazungumzo baina yake na Balozi wa Israel nchini Tanzania anayezihudumia pia nchi Afrika Mashariki za Kenya na Uganda Mhe. Yahel Vilan (kulia) Ofisini kwake leo jijini Dar es salaam. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mafunzo ya Wizara hiyo, Agnes Kimemo.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akiagana na Balozi wa Israel nchini Tanzania anayezihudumia pia nchi Afrika Mashariki za Kenya na Uganda Mhe. Yahel Vilan (kulia) mara baada ya mazungumzo Ofisini kwake leo jijini Dar es salaam.Picha na Aron Msigwa –MAELEZO.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Israel nchini Tanzania Mhe. Yahel Vilan ambapo pamoja na mambo mengine viongozi hao wamekubaliana kuanzisha ushirikiano katika maeneo mbalimbali ambayo yatazinufaisha Tanzania na Israel katika sekta ya Afya.

Balozi huyo anayezihudumia nchi za Afrika mashariki zikiwemo Kenya na Uganda katika mazungumzo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu ameyataja baadhi ya mambo ambayo Israel imekuawa ikishirikiana na Tanzania kuwa ni pamoja na utaratibu wa kuleta madaktari wa kutoa huduma kwa wagonjwa pamoja na ujuzi kwa wataalaam.

Balozi Yahel amesema Israel imekua ikitoa mafunzo ya muda mfupi kwa wataalam hususani madaktari na Wauguzi kutoka Tanzania na kuongeza kuwa wanao mpango wa kusaidia uanzishwaji wa chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) katika eneo ambalo serikali ya Tanzania itapenda kuboresha huduma hiyo.

Akitoa shukrani zake kwa niaba ya Serikali kwa misaada hiyo na mashirikiano mapya yatakayoanza kati ya Israel na Tanzania kwenye sekta ya Afya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu amesema anaishukuru Serikali ya Israel kwa misaada mikubwa inayotoa katika eneo la tiba hasa matibabu ya wagonjwa wa moyo katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya kikwete.

Amesema madaktari bingwa wanaotoka katika nchi mbali mbali ikiwemo Israel wamekuwa wakitoa huma ya upasuaji katika taasisi hiyo na kuisaidia Serikali kuokoa kiasi kikubwa cha fedha ambazo zingetumika kuwapeleka wagonjwa hao nje ya nchi kwa ajili ya matibabu.

“Hadi sasa kati ya wagonjwa 400 waliokuwa wanasubiri kupelekwa nje ya nchi kwa matibabu nusu yao wamepatiwa matibabu kupitia mashirikiano haya” Amesema Mhe. Ummy.

Kwa upande wa mafunzo Mhe. Ummy Mwalimu ameshauri yatolewe kwa kada nyingi zaidi ikiwemo wataalam wa maabara,wauguzi, madaktari na kadhalika ili kuhakikisha lengo la serikali la kupunguza vifo vya akina mama vitokanavyo na uzazi linafanikiwa.

Akizungumzia ombi la balozi huyo la Israel kutaka kusaidia ujenzi wa chumba cha wagonjwa mahututi, hapa nchini Mhe.Ummy amependekeza chumba hicho kijengwe Dodoma katika Hospitali ya Benjamin Mkapa.

Amesema sababu za mapendekezo hayo zimetokana na uamuzi wa serikali wa kuhamia Dodoma ambao unakwenda sambamba na maboresho makubwa ya utoaji wa huduma za afya kwa watu watakaohamia Dodoma.

Aidha, amefafanua kuwa wataalam kwa ajili ujenźi wa chumba hicho wanatarajia kufika nchini mwezi septemba kwa ajili ya kuendelea na utekelezaji wa ahadi ya balozi huyo.

Tume ya Mipango yaendesha Mafunzo ya Usimamizi wa Uwekezaji wa Umma

0
0

Kaimu Naibu katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Bi. Lorah Madete Akionesha kitabu cha Mwongozo wa Usimamizi na Utayarishaji wa Miradi ya Uwekezaji katika sekta ya Umma kwa wajumbe wa mafunzo (hawapo pichani), pembeni yake ni Kaimu katibu Mtendani wa Tume ya Mipango Bibi Florence Mwanri.

Wakufunzi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (wenye kompyuta mpakato), wa kwaza kutoka kushoto ni Dkt. Kenneth Mdadila, Katikati ni Dkt. John Mduma, na kulia (mwenye tai) ni Dkt. Jehovaness Aikaeli.
Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri akifungua mafunzo juu ya Mwongozo wa Usimamizi na Utayarishaji wa Miradi ya Uwekezaji katika sekta ya Umma, pembeni yake ni Kanimu Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Bi. Lorah Madete.
Baadhi ya wajumbe Wakifuatilia kinachoendelea wakati wa mafunzo.

Baadhi ya wajumbe Wakifuatilia kinachoendelea wakati wa mafunzo.
Mjumbe akitoa machango wake wakati wa mjadala.
Mjumbe akitoa uchambuzi kutoka kwenye kitabu cha Mwongozo wa Usimamizi na Utayarishaji wa Miradi ya Uwekezaji katika sekta ya Umma ambacho ndicho kinachotumika kutolea mafunzo.
Wajumbe Wakifuatilia kinachoendelea wakati wa mafunzo.


Na Adili Mhina

Tume ya Mipango imeanza zoezi la kuwajengea uwezo wataalamu katika kuandaa na kutekeleza miradi ya maendeleo inayotumia fedha za serikali au kwa kushirikiana na Sekta binafsi kwa lengo la kuongeza nidhamu na weledi katika matumizi ya rasilimali za Umma.

Mafunzo hayo yanayoendelea katika moja ya kumbi za ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es salaam na kuendeshwa na wataalamu elekezi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yanalenga kuanda wataalamu ambao watakwenda kutoa mafunzo kwa maofisa wa Serikali walio chini ya idara za Sera na Mipango na zile za uwekezaji katika Wizara, Mikoa, Halmashauri, pamoja na mashirika na taasisi mbalimbali za umma hapa nchini.

Akifungua mafunzo hayo mwanzoni mwa Juma, Kaimu Katibu Mtendani kutoka Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri alieleza kuwa mafunzo hayo yatasaidia kuimarisha utendaji, uwajibikaji na kuleta ufanisi katika matumizi ya rasilimali za umma zinazoelekezwa katika miradi ya maendeleo.

“Shabaha kuu ya mafunzo haya ni kutoa maelekezo ya mchakato na hatua zinazohitajika kufuatwa katika kutayarisha na kutekeleza miradi yote inayotumia fedha za umma au kwa kushirikiana na sekta binafsi,” Alisema Bibi Mwanri.

Kamu Katibu Mtendaji huyo alieleza kuwa kutokana na kukithiri kwa kasoro katika miradi ya maendeleo inayotumia fedha za umma, Serikali kupitia Tume ya Mipango ililazimika kuandaa Mwongozo wa Usimamizi na Utayarishaji wa Miradi ya Uwekezaji katika sekta ya Umma (Public Investment Management Operational Manual) ambao utatumika katika kuandaa, kutekeleza na kusimamia miradi yote inayotumia fedha za umma au kwa kushirikiana na sekta binafsi.

Bibi Mwari alieleza kuwa katika awamu hii ambayo Serikali imejikita katika kujenga uchumi wa viwanda miradi mingi ya maendeleo inatarajiwa kuanzishwa. Hivyo, bila kuwa na uelewa wa pamoja moingoni mwa wadau wanaohusika katika kuandaa, kutekeleza na kusimamia miradi hiyo malengo ya Mpango wa Pili wa Maendeleo hayatafikiwa kama inavyotarajiwa.

“Katika kipindi hiki ambapo bajeti ya maendeleo imeongezeka na kufikia asilimia arobaini ni wazi kuwa miradi mingi ya maendeleo inaanzishwa, hivyo ni lazima kila mtaalamu aelewe kuwa tunawajibu wa kuandaa miradi bora, yenye tija kwa wananchi na inayoendanda na thamani ya fedha zinazotumika,” Alisisitiza Bibi Mwanri.

Bibi Mwanri aliwataka wajumbe wote kuhakikisha wanatumia mafunzo hayo vizuri ili kupata uelewa wa kutosha juu ya mwongozo huo.

Mafunzo hayo ya siku tano yamehudhuriwa na wajumbe kutoka Wizara, Taasisi za Serikali, Wadau wa Maendeleo, Asasi za Kiraia pamoja na Sekta binafsi na yanatarajiwa kuandaa wataalamu bora watakaokwenda katika kanda mbalimbali nchini kutoa mafunzo tarajiwa kwa walengwa.

Rasimu ya Taarifa ya Utafiti kuhusu hali ya maadili ya viongozi wa umma nchini yazinduliwa Jijini Dar es Salaam.

0
0

Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angela Kairuki akizungumza wakati wa uzinduzi wa warsha ya kujadili rasimu ya Taarifa ya Utafiti kuhusu hali ya maadili ya viongozi wa umma nchini leo Jijini Dar es Salaam. Warsha hiyo imeratibiwa na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

Kamishina wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Salome Kaganda akizungumza wakati wa uzinduzi wa warsha ya kujadili rasimu ya Taarifa ya Utafiti kuhusu hali ya maadili ya viongozi wa umma nchini leo Jijini Dar es Salaam. Warsha hiyo imeratibiwa na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma.Kutoka kulia ni Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angela Kairuki na Profesa John Kessy kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo (SUA) ambaye ndiye aliyefanikisha utafiti huo.

Katibu wa Maadili ya Viongozi – Siasa, Waziri Kipacha akielezea jambo wakati wa warsha ya kujadili rasimu ya Taarifa ya Utafiti kuhusu hali ya maadili ya viongozi wa umma nchini leo Jijini Dar es Salaam. Warsha hiyo imeratibiwa na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma.Kutoka kulia ni Kamishina wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Salome Kaganda, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angela Kairuki na Profesa John Kessy kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo (SUA) ambaye ndiye aliyefanikisha utafiti huo.

Profesa John Kessy kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo (SUA) akiwasilisha rasimu ya Taarifa ya Utafiti kuhusu hali ya maadili ya viongozi wa umma katika warsha iliyoandaliwa na Sekrtetarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma leo Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angela Kairuki (wapili kutoka kulia) na Kamishina wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Salome Kaganda (kushoto) wakifuatilia uwasilishwaji wa rasimu ya Taarifa ya Utafiti kuhusu hali ya maadili ya viongozi wa umma nchini katika warsha warsha ya kujadili rasimu hiyo leo Jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya washiriki wa warsha ya kujadili Taarifa ya rasimu ya Utafiti kuhusu hali ya maadili ya viongozi wa umma nchini wakifuatilia uwasilishwaji wa rasimu hiyo leo Jijini Dar es Salaam.

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Phillip Mangula akiteta jambo na Kaimu Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi – CUF Twaha Tasrima walipokuta katika warsha ya kujadili Taarifa ya rasimu ya Utafiti kuhusu hali ya maadili ya viongozi wa umma nchini leo Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angela Kairuki akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Dini pamoja na Vyama vya Siasa nchini mara baada ya uzinduzi wa warsha ya kujadili rasimu ya Taarifa ya Utafiti kuhusu hali ya maadili ya viongozi wa umma nchini leo Jijini Dar es Salaam.Kutoka kulia ni Kaimu Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi – CUF Twaha Tasrima, : Kamishina wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Salome Kaganda, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Phillip Mangula .Picha na Frank Shija

BREAKING NEWZZZZZZZ;ALIYEKUWA MKURUGENZI WA VITAMBULISHO VYA TAIFA (NIDA) NA WENZAKE NANE WAFIKISHWA MAHAKAMANI

0
0

 
Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya vitambulisho vya taifa-NIDA- Dickson Maimu (wa tatu kushoto) na viongozi wengine  nane wa taasisi hiyo wamefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi kisutu mapema leo.Habari zaidi tutawaletea.

Mnamo mwezi January 2016, Rais Magufuli aliamua kutengua uteuzi wa Mkurugenzi wa mamlaka ya vitambulisho vya taifa (NIDA) Bwana Dickson Maimu na kumsimamisha kazi yeye na wafanyakazi wengine ili kupisha uchunguzi wa namna ilivyotumika kiasi cha shilingi bilioni 179.6 katika zoezi la upatikanaji wa vitambulisho vya taifa wakati bado kuna malalamiko kwamba watu wengi hawajapata vitambulisho hivyo. .

TANGA YAANZA MAANDALIZI MRADI WA BOMBA LA MAFUTA

0
0

 Mkurugenzi wa Sheria, Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Ibrahim Ngabo, akizungumza na waandishi wa Habari wakati Mkuu wa Mkoa wa Tanga alipotembelea eneo la Chongoleani itakapojengwa gati itakayotumika kupakua mafuta ghafi.
 Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigella, akiongea jambo mara baada ya kutembelea eneo la Chongoleani Mkoani Tanga, itakapojengwa Gati itakayotumika kupakua mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda.
 Mkuu wa Mkoa wa Tanga , Martine Shigella ( Wa tano kutoka kulia), katika picha ya pamoja  na  Wawakilishi kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Mamlaka ya Bandari Tanga . Pia yupo Meya wa Jiji la Tanga na Mkurugenzi wa Jiji la Tanga.
Maandalizi ya awali ya kuandaa eneo itakapojengwa Gati itakayotumika kupakua mafuta ghafi ya kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga yakiendelea.
Picha kwa Hisani ya www.tangaraha.tz.blogspot.com

Na Asteria Muhozya, Tanga.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigella amesema, tayari Mkoa huo umeanza maandalizi ya awali ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP), kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga.

Shigella aliyasema hayo mwanzoni mwa juma alipotembelea eneo la Chongoleani Tanga itakapojegwa gati ya kushusha mafuta ili kuona maandalizi yanavyoendelea na kuongeza kuwa, Mkoa huo unaandaa mazingira ya kutekeleza mradi husika ambapo tayari barabara ya kuelea eneo hilo imekwishachongwa.

“Tunajenga mazingira ya kutekeleza mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi, lakini pia tunao wajibu wa kuboresha Bandari yetu kwa ajili ya utekelezaji huo. Yale tunayoweza kufanya sisi kama Serikali tayari tunaanza wakati tukisubiri Marais na Mawaziri wa nchi husika kusema ni lini ujenzi huu utaanza rasmi. Kwetu ni fursa na tunataka maendeleo.”

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Bandari ya Tanga, Henry Arika alisema kuwa, katika maandalizi ya mradi huo, Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) imetenga jumla ya Shilingi bilioni 9.2 kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya bandari hiyo ili kuwezesha mapokezi ya vifaa vya mradi husika.

Aliongeza kuwa, mbali na kuboresha miundombinu, fedha hizo pia zitatumika kuongeza kina cha gati ili kuwezesha Meli kubwa zitakazobeba vifaa vya ujenzi kuweza kutia nanga kwa urahisi.

“TPA inatarajia kupokea wastani wa tani 250,000 za shehena za vifaa kupitia Bandari yetu wakati wa maandalizi na ujenzi wa bomba hilo, hivyo maboresho kwetu ni muhimu sana. Tunajua kazi kubwa iliyo mbele yetu, tunajipanga na tunajiandaa kuhakikisha kwamba mizigo inapita kwa ufanisi na usalama,” alisema Arika.

Alifafanua kuwa, ili kuimarisha usalama na kupanua wigo wa eneo la kuhifadhi mizigo, tayari Mamlaka hiyo imetenga eneo la ukubwa wa kilomita za mraba 2,600 litakalotumika kwa shughuli za kuhifadhia shehena ya mizigo kabla ya kusafirishwa, ikiwemo pia maandalizi ya ujenzi wa mashine maalum ya ukaguzi (scanner) kwa ajili ya kukagulia mizigo ili kuimarisha usalama.

Naye, Mkurugenzi wa Sheria kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Ibrahim Ngabo alisema kuwa, majadiliano ya mfumo wa Kisheria kuhusu mradi kati ya nchi za Tanzania na Uganda yamekwishaanza na yanaendelea vizuri.

Kwa upande wake, Kaimu Kamishna wa Nishati anayeshughulikia masuala ya Petroli, Wizara ya Nishati na Madini, Mwanamani Kidaya, alisema kuwa, amefurahishwa na namna Mkoa huo ulivyoanza maandalizi ya utekelezaji wa mradi husika na hivyo kuwataka wananchi kuwa tayari kuupokea mradi huo ikiwemo kutumia fursa zitakazojitokeza kupitia mradi husika.

Katika ziara ya kutembelea eneo hilo, Mkuu wa Mkoa alifuatana na Uongozi wa Mkoa akiwemo Meya  na Mkurugenzi wa Jiji hilo, Uwakilishi kutoka Wizara ya Nishati na Madini, TPDC na TPA.

KISOMO CHA KHITMA NA DUA YA HAYATI MZEE ABOUD JUMBE

0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) pamoja na Viongozi na waumini wa Dini ya kiislamuwakisoma Khitma ya kumuombea Dua Marehemu Rais wa Awamu ya Pili wa Zanzibar Mzee Aboud Jumbe Mwinyi katika msikiti wa Mwushawal Mwembe Shauri Mjini Unguja leo jioni
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) pamoja na Viongozi na waumini wa Dini ya kiislamu wakisoma Khitma ya kumuombea Dua Marehemu Rais wa Awamu ya Pili wa Zanzibar Mzee Aboud Jumbe Mwinyi katika msikiti wa Mwushawal Mwembe Shauri Mjini Unguja leo jioni
 Viongozi mbali mbali waliojumuika katika Kisomo cha Dua ya Khitma ya kumuombea Dua Marehemu Rais wa Awamu ya Pili wa Zanzibar Mzee Aboud Jumbe Mwinyi katika msikiti wa Mwushawal Mwembe Shauri Mjini Unguja leo jioni
 Miongoni mwa Waumini wa Dini ya Kiislamu walioshiriki katika msikiti wa Mushwawal Mwembe Shauri Mjini Unguja wakisoma dua ya Khitma leo ya kumuonbea Dua Marehemu Rais wa Awamu ya Pili wa Zanzibar Mzee Aboud Jumbe Mwinyi aliyezikwa juzi nyumbani kwake Migombani
Mustafa Aboud Jumbe Mwinyi  akitoa shukurani kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein  pamoja na Viongozi na Wananchi na waislamu walioshiriki katika Khitmaya Dua ya kumuombea  Rais mstaafu wa Awamu ya Pili wa Zanzibar Marehemu Mzee Aboud Jumbe Mwinyi,Iliyosomwa leo katika Msikiti wa Mushawala Mwembe shauri Mjini Unguja. Picha na Ikulu Zanzibar

MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA UJUMBE WA SHIRIKA LA GLOBAL COMMUNITIES NA UJUMBE WA MER GROUP JIJINI DAR ES SALAAM

0
0

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (wa pili kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja wa ujumbe wa Shirika la Kimataifa lisilo la Kiserikali la Global Communities uliomtembelea leo ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam wengine pichani ni kutoka kushoto ni Meneja wa Biashara Ndugu Lucas Mazige,Meneja wa Shirika hilo Ndugu Mwita Mchuni , kulia ni Meneja wa Mikopo wa Shirika hilo Ndugu Victor Anthony .

..........................................
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ameutaka uongozi wa Shirika la Kimataifa lisilo la Kiserikali la Global Communities uhakikishe unaweka utaratibu bora wa kupata taarifa muhimu kuhusu masuala ya kilimo kutoka kwa wakulima wenyewe hatua ambayo itasaidia serikali, wafadhili na wadau wengine wa maendeleo kukipa msukumo wa kipekee kilimo ili kiweze kuwa na tija nchini.

Makamu wa Rais ametoa kauli hiyo 17-Aug-16 alipokutana na ujumbe wa watu watatu wa shirika hilo ukiongozwa na Programu Meneja Mwita Mchumi ambao ulimtembelea ofisini kwake Ikulu kwa ajili ya kujitambulisha na kuelezea shughuli zinazofanywa shirika hilo nchini.

Makamu wa Rais amesisitiza kuwa kama wakulima wakipata taarifa sahihi kuhusu masuala ya kilimo na masoko wataweza kuongeza uzalishaji wa mazao na hivyo kuleta mapinduzi makubwa ya kilimo kwa kujiongezea kipato na la taifa kwa ujumla.

"Changamoto kubwa katika kilimo ni hii ya kukosekana kwa taarifa kutoka kwa wakulima wenyewe. Nyinyi kama shirika wekeni kama mradi hivi, mnaenda mfano Singida mnaongea na wakulima wenyewe aina ya mazao ya biashara yanayolimwa pale, pembejeo wanapata kwa wakati na inakidhi haja vitu kama hivyo. Taarifa hizo zitaisadia serikali, wafadhili kukiwezesha kilimo kuwa na tija," alisema Mheshimiwa Samia.

Katika mazungumzo hayo Mwita Mchumi aliiomba serikali iangalie uwezekano wa kupunguza riba ili kuwawezesha wafanyabiashara na wakulima kukopa kwenye mabenki jambo ambalo Makamu wa Rais alisema serikali inalifanyia kazi.

Shirika la Global Communities lenye makao yake makuu Washington, Marekani tangu lilipoanza kazi rasmi hapa nchini mwezi Februari mwaka huu limeweza kuwaunganisha wauzaji na wanunuzi wadogo na wa kati wa biashara za kilimo ambao wameweza kufanya biashara ya takribani Dola za Kimarekani milioni 150.

Shirika hilo limeweza pia kufundisha mabenki umuhimu wa mfumo wa kuuza mazao kupitia stakabadhi ghalani na kuifanya Benki ya Afrika (BOA) kutenga shilingi milioni 500 kwa ajili ya kuwakopesha wakulima wadogo wadogo wanaojishughulisha kuuza mazao kupitia stakadhi ghalani katika mkoa wa mbeya

Kwa mujibu wa Mwita Mchumi hivi sasa kuna mafunzo yanaendelea ngazi ya cheti katika kuwajengea uwezo wataalam wa benki katika biashara za kilimo ili waweze kutoa huduma stahiki katika sekta ya kilimo.

Mwita Mchumi amesema shirika hilo ambalo limeanzishwa mwaka jana linajishughulisha zaidi na masuala ya kilimo hasa biashara za kilimo katika minyororo ya thamani ya mazao ya nafaka, jamii ya mikunde, bustani, mifugo na mazao ya mafuta kama alizeti na ufuta.

Shirika hilo pia linatumia njia za tehama katika kupata taarifa za masoko na kuwakutanisha wauzaji kwa ajili ya kuingia biashara na kujenga uwezo kwa wafanyabiashara wa kati na wadogo pamoja na wakopeshaji ambao ni taasisi za kifedha kama mabenki.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (wa pili kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na ujumbe kutoka kampuni ya MER GROUP,wa kwanza kushoto ni Meneja wa Kampuni hiyo Bw. Dov Aronovich, wengine ni Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo Bw. Omer Leviv na Meneja wa Biashara Bw. Mohammed Magori, Ujumbe huu ulimtembelea Makamu wa Rais Ikulu jijini Dar es Salaam na kutambulisha shughuli wanazofanya nchini.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Mabalozi waendelea kutoa salamu za pole kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Awamu ya Pili wa Zanzibar Mzee Aboud Jumbe Mwinyi

0
0
 Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Bw.  Jassem Al Najem ni miongoni mwa mabalozi waliotembelea Ofisi ya Makamu wa Rais leo na kutoa salamu za pole kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Awamu ya Pili wa Zanzibar.
Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Bw.  Jassem Al Najem ni miongoni mwa mabalozi waliotembelea Ofisi ya Makamu wa Rais leo na kutoa salamu za pole kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Awamu ya Pili wa Zanzibar. Picha zote na Ofisi ya Makamu wa Rais
 Balozi wa Uganda nchini Tanzania Bi. Dorothy Samali Hyuha akisaini kitabu cha maombolezo na kutoa salamu za rambirambi kufuatia kifo cha aliyekua Rais wa Pili wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mzee Aboud Jumbe Mwinyi.
 Mwakilishi wa Ubalozi wa Nigeria nchini Bi. Abiola Sherif Deluya akitoa salamu za pole katika kitabu maalumu kilichopo katika Ofisi ya Makamu wa Rais Mtaa wa Luthuli, Jijini Dar es Salaam leo.

SHIRIKISHO LA VYUO VYA ELIMU YA JUU-CCM, LATOA TAMKO RASMI KUMUUNGA MKONO RAIS DK. JOHN MAGUFULI

0
0

Katibu wa Shirikisho la Vyuo vya Elimu ya Juu-CCM, Siraji Madebe

Shirikisho la vyuo vya Elimu ya Juu CCM katika kikao chake cha kazi cha Agosti 11, 2016, pamoja na mambo mengine.

Kimeazimia yafuatayo:-

Kuunga mkono utekelezaji wa ilani ya CCM kwa vitendo kwa kuelimisha wananchi kumuunga mkono Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM taifa Dk. John Pombe Magufuli, kuhusu umuhimu wa kila mwananchi kudai risiti na muuzaji kutoa risti katika kila manunuzi, kwa lengo la kuwezesha serikali kupata fedha kupitia kodi, kutoa elimu kwa jamii na uelewa wa Tanzania yenye viwanda ikiendana na uwanzishaji wa mashamba darasa ya shirikisho na viwanda vya kati vya kusindika mazao.

Vilevile Shirikisho la vyuo vya Elimu ya juu - CCM, tunafungua milango kwa vijana mbali mbali wenye lengo la kuunda vikundi vyenye dhamira ya kujikwamua kiuchumi na kutaka kujiajili, kufika kwenye ofisi zetu za Shirikisho zilizopo mikoani na Makao Makuu, mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam, ili kupata ushauri wakitaalamu na kusaidiwa kuandika maandiko yatakayo waongoza kwenye uanzishwaji wa miradi itakayo saidia kutoa fursa za ajira kwa vijana.

Pia Shirikisho la vyuo vya Elimu ya juu - CCM, linamuomba Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli, kuwashughulikia kikamilifu wale wote waliohujumu mali za CCM, kwani vitendo hivyo vinadhoohofisha nguvu ya chama na wakati mwingine kuwafanya wanachama kuwa wanyonge kwenye Chama chao.

Shirikisho la vyuo vya Elimu ya juu - CCM, kwa kumuunga mkono Mwenyekiti wa CCM, kwa kuhamia Dodoma, tumeazimia kuwa Ofisi ya Makao Makuu ya Shirikisho nayo itahamia Dodoma rasmi hivi karbuni, baada ya taratibu za upatikanaji wa Ofisi kukamiliaka.

Mwisho, Shirikisho la Vyuo vya Elimu ya Juu-CCM, linapenda kuwaomba Watanzania kuendelea kumuunga mkono na kumuamini kwa dhati kabisa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Dk. John Pombe Magufuli kwani dhamira yake ni kuitumikia jamii ya Watanzania na si kufanya siasa kwenye maisha ya watu wenye shida.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

Imetolewa na:-
Idara ya Habari na Mawasiliano
Shirikisho Makao Makuu

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA APOKEA MSAADA WA SH. MILIONI 12 KUTOKA KUWAIT

0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al Najem wakiwa wamekalia madawati mawili kati ya 50 yaliyotolewa na Kuwait na kukabidhiwa kwake na balozi huyo jijini Dar es salaam Agosti 17, 2016.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepokea msaada wa sh. milioni 12 kutoka mashirika ya misaada ya Kuwait kwa ajili ya kununulia madawati ili kupunguza tatizo hilo nchini. Pia amepokea madawati 100 kutoka ubalozi wa Kuwait na taasisi ya Direct Aid ya nchi hiyo.

Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo leo (Jumatano, Agosti 17, 2016), Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Bw. Jasem Al Najem amesema msaada huo ni michango kutoka mashirika ya misaada ya nchi yake ambayo yanatoa huduma mbalimbali hapa nchini.

“Tumejipanga kukamilisha ahadi ya madawati 600, tunaendelea kuwasiliana na wenzetu wa Kuwait Fund, na mashirika mengine. Kwa sasa tunachangia madawati, baadaye tutakwenda kwenye ujenzi wa madarasa, hata ikibidi tutaenda kwenye ujenzi wa shule,” alisema.

Balozi Najem amesema wanatoa misaada hiyo ili kuunga mkono juhudi za Mhe. Rais Dkt. John Magufuli za kutaka wanafunzi wote wakae kwenye madawati.

Akitoa shukrani mara baada ya kupokea msaada huo, Waziri Mkuu alimshukuru Balozi wa Kuwait kwa moyo wao wa kujitolea ikizingatia kuwa ni wiki tatu tu zilizopita alikwishatoa msaada mwingine wa madawati kwenye shule ya msingi Chamazi, wilayani Temeke jijini Dar es Salaam.

Aliyashukuru pia mashirika ya misaada kupitia Ubalozi huo, ambao wametoa fedha kwa ajili ya ununuzi wa madawati. Ametoa wito kwa mabalozi wengine, sekta binafsi na wadau wa maendeleo watoe michango zaidi ili yapatikane madawati ya kutosha.

Mashirika yaliyotoa michango hiyo ni African Relief Organisation (hundi ya sh. milioni 6), Al Furqaan Islamic Centre (hundi ya sh. milioni 6), Taasisi ya Direct Aid (madawati 50 ya shule za Msingi) na ubalozi wa Kuwait (madawati 50 ya shule za sekondari).

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S.  L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM.

JUMATANO, AGOSTI 17, 2016.

Rais Magufuli akutana na Kiongozi Mkuu wa Bohra na pokea ujumbe wa Rais wa Saharawi

0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha  Kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Bohora Duniani Mtukufu Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin Ikulu jijini Dar es Salaam. 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Bohora Duniani Mtukufu Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin wakwanza kushoto.(Katikati ni mkalimani)
 Kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Bohora Duniani Mtukufu Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin akimuombea dua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Bohora Duniani Mtukufu Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin mara baada ya kuchangia madawati kwa kutoa hundi yenye thamni ya dola za Kimarekani (USD 53,000) kwa ajili ya utengenezwaji wa madawati.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Bohora Duniani Mtukufu Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin mara baada ya kuchangia madawati kwa kutoa hundi yenye thamni ya dola za Kimarekani (USD 53,000) kwa ajili ya utengeezwaji wa madawati. Wengine katika picha ni Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeir watatu kutoka kushoto na Sheikh mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Alhadi Mussa Salum wa kwanza kushoto.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na  Kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Bohora Duniani Mtukufu Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin wengine katika picha ni Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeir pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Augustine Mahiga.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na  Kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Bohora Duniani Mtukufu Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin wengine katika picha ni Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeir,  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Augustine Mahiga pamoja na viongozi wengine wa BAKWATA na wa madhehebu ya Bohora.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na  Kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Bohora Duniani Mtukufu Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin wengine katika picha ni Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeir pamoja na viongozi wengine wa Madhehebu ya Bohora.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Bohora Duniani Mtukufu Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin kabla ya kuondoka Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Bohora Duniani Mtukufu Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeir Ikulu jijini Dar es Salaam mara baada ya kuagana na  mgeni wake Kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Bohora Duniani Mtukufu Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Bohora Duniani Mtukufu Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Bohora Duniani Mtukufu Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin aliyeambatana na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais Dkt. John Pombe Magufuli akipokea ujumbe uliotoka kwa Rais wa Saharawi na kuwasilishwa kwake na Mjumbe Maalum Bachir Moustapha Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU.

 



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 17 Agosti, 2016 amekutana na kufanya mazungumzo na Kiongozi Mkuu wa Jumuiya ya Dawoodi Bohra Duniani Mtukufu Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin Saheb(TUS) Ikulu Jijini Dar es Salaam.


Mazungumzo hayo yamehudhuriwa na Mufti wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeir Ali na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga ambapo Rais Magufuli ameipongeza Jumuiya ya Dawoodi Bohra kwa juhudi kubwa inazofanya katika kutoa huduma za kiroho na pia kushiriki katika maendeleo.

Dkt. Magufuli amewakaribisha wana Jumuiya hiyo kuwekeza hapa nchini hususani katika sekta ya viwanda na pia amewakaribisha katika Maadhimisho ya Jumuiya ya Dawoodi Bohra duniani yanayotarajiwa kufanyika Jijini Dar es Salaam Mwezi Oktoba 2016.

"Tanzania ni nchi nzuri, tumekuwa na ushirikiano mzuri sana na wenzetu wa Jumuiya ya Bohra, hivyo njooni mfanye biashara na Tanzania,  tumepanga katika kipindi cha mwaka 2016/2017 hadi 2020/2021 Tanzania iwe nchi ya viwanda, kwa hiyo tunawakaribisha kuja kuanzisha viwanda vya kutosha" Amesema Rais Magufuli.


Kwa upande wake Kiongozi Mkuu wa Jumuiya ya Dawoodi Bohra Mtukufu Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin Saheb amempongeza Rais Magufuli kwa kazi nzuri inayofanywa na Serikali yake ya awamu ya Tano, na pia ameahidi kuwa Jumuiya ya Dawoodi Bohra ipo tayari kushirikiana na Tanzania katika maendeleo.


Aidha, Mtukufu Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin Saheb amemkabidhi Rais Magufuli hundi ya Dola la Marekani Elfu Hamsini na Tatu (USD-53,000) sawa na Shilingi Milioni 116 za Kitanzania kwa ajili ya kuchangia utengenezaji wa madawati ya wanafunzi kwa shule mbalimbali hapa nchini na pia amekabidhi hundi ya Dola za Marekani Elfu Ishirini na Moja (USD-21,000) sawa na Shilingi Milioni 46 kwa ajili ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA).


Katika hatua nyingine, Rais Magufuli amepokea barua kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Kiarabu ya Saharawi Mhe. Brahim Ghali iliyowasilishwa na Mjumbe Maalum wa Rais huyo ambaye ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mhe. Bachir Moustapha Sayed.Pamoja na kupokea barua hiyo Rais Magufuli amesema Serikali yake ya Awamu ya Tano itaendeleza na kuimarisha zaidi ushirikiano wake na Jamhuri ya Kiarabu ya Saharawi na pia itaendelea kuunga mkono juhudi za wananchi wa Saharawi kupata haki ya kuamua hatma yao.





Gerson Msigwa

Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

Dar es Salaam

17 Agosti, 2016.

WAZIRI MWIGULU AKUTANA NA BALOZI WA ISRAEL NCHINI, JIJINI DAR ES SALAAM LEO.

0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (katikati) akimkaribisha Balozi wa Israeli nchini, Yahel Vilan (kushoto), ofisini kwake jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujadiliana masuala mbalimbali ya ushirikiano kati Israel na Tanzania. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (katikati) akizungumza na Balozi wa Israeli nchini, Yahel Vilan (kulia) masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Israel na Tanzania. Mazungumzo hayo yalifanyika katika ofisi ya Waziri Mwigulu, jijini Dar es Salaam leo.  Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (kushoto) akimsikiliza Balozi wa Israeli nchini, Yahel Vilan alipokuwa akizungumza masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya nchi yake na Tanzania. Mazungumzo hayo yalifanyika katika ofisi ya Waziri Mwigulu, jijini Dar es Salaam leo.  Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

AZAM FC WATWAA NGAO YA JAMII, WAITANDIKA YANGA BAO 4-1 (PENATI)

0
0
 Wachezaji wa Timu ya Azam pamoja na viongozi wao wakishangilia baada ya kutwaa Ngao ya Jamii, kwa kuifunga Yanga kwa mikwaju ya penati 4-1, kufuatia mchezo wao kumalizika kwa sare ya bao 2-2.
Mgeni Rasmi katika Mtanganye wa kuwania Ngao ya Jamii uliozikutanisha Timu ya Azam na Yanga, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akikabidhi Ngao hiyo kwa Nahodha wa Timu ya Azam, John Boko 'Adebayour', baada ya kuifunga Yanga kwa mikwaju ya penati 4-1, kufuatia mchezo wao kumalizika kwa sare ya bao 2-2.
 Beki wa Timu ya Azam FC, David Mwantika akizua mpira kwa umaridadi mkubwa huku akimdhibiti Mshambuliaji machachari wa Yanga, Donald Ngoma katika mchezo wa Ngao ya Jamii ikiwa ni sehemu ya ufunguzi wa Ligi kuu Tanzania bara, uliopigwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam. Dakika 90 zilimalizika kwa timu hizo kulingana 2-2, na kupelekea kuamuliwa kupigwa mikwaju ya penati iliyoipa ushindi timu ya Azam kwa mabao 4-1.
 Mshambuliaji wa Yanga, Amisi Tambwe akitaka kuzuia shuti la Beki wa Azam, Shomari Kapombe.
 Kipa wa Azam akiwa chini huku mpira ukiwa wavuni, baada ya kupelekwa markiti na Mshambuliaji wa Yanga, Donald Ngoma kwa mkwaju wa penati.
 Beki wa Yanga, Hassan Kessy akiutuliza mpira kwa ustadi mbele ya Benchi la Wapinzani wake.

Pangani nzima kupatiwa umeme ifikapo 2018 : Kuwa wilaya ya mfano Tanzania kwa vijiji vyote kuunganishiwa na umeme

0
0

Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mkaramo kilichopo wilayani Pangani mkoani Tanga. Waziri Muhongo yupo mkoani Tanga kwa ajili ya kukagua miradi ya kusambaza umeme vijijini inayotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) pamoja na kuzungumza na wananchi.
Wananchi wa kijiji cha Sakula kilichopo wilayani Pangani mkoani Tanga wakionyesha mabango yenye jumbe tofauti mbele ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (hayupo pichani) walipomsimamisha njiani kwa lengo la kuwasilisha kero mbalimbali wakati akielekea katika kijiji cha Mkaramo kwa ajili ya kuhutubia wananchi
Mkuu wa Wilaya ya Pangani, Zainab Abdallah Issa (kushoto) akiwasilisha mahitaji ya umeme katika wilaya ya Pangani
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akisisitiza jambo wakati alipokuwa akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Mkaramo kilichopo wilayani Pangani mkoani Tanga (hawapo pichani)
Waziri wa Nishati na Madini (kulia) akipokea kero mbalimbali kutoka kwa wananchi wa kijiji cha Mkaramo

………………………………………………………………………..

Na Greyson Mwase, Pangani

Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo amesema kuwa Serikali ina mpango wa kusambaza nishati ya umeme katika wilaya nzima ya Pangani na kuifanya kuwa wilaya ya mfano ndani ya kipindi cha miaka miwili.

Profesa Muhongo aliyasema hayo alipokuwa akihutubia katika kijiji cha Mkaramo kilichopo wilayani Pangani mkoani Tanga. Profesa Muhongo yupo mkoani Tanga kwa ajili ya kukagua miradi ya usambazaji wa umeme vijijini inayotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA).

Kabla ya kuwasili katika kijiji hicho msafara wa Profesa Muhongo ulisimamishwa na wananchi wa kijiji cha Sakura kilichopo wilayani Pangani mkoani Tanga waliokuwa na mabango wakiomba kupatiwa umeme katika kijiji chao.

Akizugumza kwa niaba ya wanakijiji wenzake, Boga Mbega alisema kuwa kijiji hicho kimekuwa gizani kwa muda wa miaka mingi hali inayopelekea uchumi katika kijiji hicho kudumaa.

Aliongeza kuwa kutokana na ukosefu wa umeme katika kijiji hicho wamekuwa wakifuata huduma za jamii kama vile matibabu na maji katika vijiji vya mbali na hivyo kuhisi kama wako kwenye kisiwa cha giza.

Mara baada ya Waziri Muhongo kuwasili katika kijiji cha Mkaramo na kuanza kuhutubia alisema kuwa kutokana na wilaya ya Pangani kuwa nyuma kimaendeleo kuliko wilaya nyingine nchini, Serikali imepanga mikakati ya kuhakikisha kuwa wilaya nzima ya Pangani pamoja na vijiji vyake vyote inapata nishati ya umeme ndani ya kipindi cha miaka miwili.

Akielezea malengo ya kuipa kipaumbele wilaya ya Pangani kwenye mpango wa usambazaji wa umeme vijijini chini ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Profesa Muhongo alieleza kuwa ni kufuta umasikini kupitia uboreshaji wa huduma za jamii kama shule, zahanati, pamoja na kuzalisha ajira na kupunguza wimbi la vijana kukimbilia mjini kutafuta ajira.

Alisema katika utekelezaji wa mradi wa REA Awamu ya tatu katika wilaya ya Pangani, maeneo yatakayopewa kipaumbele cha kwanza ni pamoja na shule, zahanati, vyuo, makanisani na misikitini.

Aliwataka wananchi wa wilaya ya Pangani kujiandaa na mradi huo kwa kubuni fursa mbalimbali kama vile kuanzisha vikundi vidogo vidogo kwa ajili ya kuanzisha viwanda, ukulima na ufugaji wa kisasa ili kujipatia maendeleo.

Alifafanua kuwa ni wakati wa wakinamama wa wilaya ya Pangani kuachana na matumizi ya kuni na kutumia majiko ya umeme na gesi.

Profesa Muhongo aliendelea kusema kuwa miradi ya umeme haihitaji siasa na kuwataka wananchi kuweka nguvu zaidi kwenye uchumi kwa kutumia nishati ya umeme badala ya kupoteza muda kwenye siasa.

Naye Mbunge wa Pangani Jumaa Hamidu Aweso (CCM) aliishukuru serikali kwa kuipa kipaumbele wilaya ya Pangani na kusisitiza kuwa wataanza kufanya uhamasishaji kwa wananchi wote wa Pangani .

Aliwataka wananchi kuachana na maandamano ya siasa na badala yake waweke nguvu kwenye shughuli za kiuchumi zitakazowapatia maendeleo.

Alisema kuwa mara baada ya umeme katika wilaya nzima ya Pangani kupatikana, wawekezaji watajitokeza kuwekeza kwenye viwanda vya korosho na kuongezeka mapato katika halmashauri ya Pangani.
Viewing all 46206 articles
Browse latest View live




Latest Images