Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 933 | 934 | (Page 935) | 936 | 937 | .... | 1897 | newer

  0 0


  Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya TEHAMA, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. Arnold Mathoyo akieleza utaratibu wa mafunzo ya TEHAMA kwa washiriki wanaosimamia miradi ya TEHAMA chini ya Mradi wa Miundombinu ya Mawasiliano (RCIP) Tanzania katika ukumbi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Dodoma.
  Washiriki wa mafunzo kuhusu TEHAMA wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bi. Susan Mlawi (hayupo pichani).
  Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bi. Susan Mlawi akisisitiza jambo wakati akifungua mafunzo kwa wataalam wa TEHAMA wanaosimamia miradi chini ya Mradi wa Miundombinu ya Mawasiliano (RCIP) Tanzania katika ukumbi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Dodoma.

  0 0
 • 08/10/16--07:56: UMLEAMVYO NDIVYO AKUAVYO
 • Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Mhe. Freeman Mbowe akiwa amemba mtoto (Jina limehifadhiwa) aliyetaka kumsalimia baada ya kumuona katika viwanja vya maonyesho ya wakulima Nane Nane, Themi Njiro jijini Arusha, Jumanne 9/8/2016.

  0 0


  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei (kushoto), akimkabidhi tiketi ya ndege ya kwenda Nairobi Kenya, Mwandishi wa Habari wa gazeti la The Guardian Finnigan Simbeye.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei (kushoto), akimkabidhi tiketi ya ndege ya kwenda Nairobi Kenya, Mwandishi wa Habari wa gazeti la Daily News, Abduel Elinaza.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei (kushoto), akimkabidhi tiketi ya ndege ya kwenda Nairobi Kenya, Mwandishi wa Habari wa gazeti la Citizen, Samuel Kamndaya.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (wa pili kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa habari za Biashara na Masuala ya Fedha walipota udhamini wa benki hiyo.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei akifafanua jambo wakati wa hafla ya kukabidhi tiketi za ndege kwa waandishi wa habari wa watatu waliopata udhamini wa benki hiyo kwenda Nairobi Kenya kuhudhuria mafunzo ya biashara na masuala ya fedha. Waandishi waliopata ufadhili huo ni Finnigan Simbeye (The Guardian, Abduel Elinaza (Daily News) na Samuel Kamndaya (The Citizen). Hafla hiyo ilifanyika Makao Makuu ya Benki hiyo jijini Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande)
  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi tiketi za ndege kwa waandishi wa habari wa watatu.
  Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa akuzungumza katika hafla hiyo.

  0 0

   Naibu Waziri  wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(wa pili kulia), akishirikiana na viongozi wengine akiwemo Mbunge wa Jimbo la Segerea,Mheshimiwa  Bonnah Kaluwa(wa kwanza kushoto),kuzindua   ujenzi wa kituo cha polisi kinachojengwa katika Jimbo la Segerea ikiwa ni mkakati wa kupambana na uhalifu katika jimbo hilo.
   Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akishiriki ujenzi wa awali wa kituo cha polisi kinachojengwa katika Jimbo la Segerea ikiwa ni mkakati wa Mbunge wa jimbo hilo  kupambana na vitendo ya uhalifu katika jimbo hilo.
   Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(suti nyeusi), akisikiliza maelezo kutoka kwa mmoja wa wajumbe wa kamati ya Ujenzi wa Kituo cha Polisi .Naibu Waziri huyo pia aliongoza Harambee ya Ujenzi wa kituo hicho ikiwa ni mkakati wa  Mbunge wa Jimbo hilo Bonnah Kaluwa, kupambana  na matukio ya uhalifu.Naibu Waziri huyo aliongoza
   Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza wakati wa Harambee ya Ujenzi wa Kituo cha Polisi .Wa kwanza kulia ni Mbunge wa Jimbo la Segerea,Mheshimiwa  Bonnah Kaluwa. Ujenzi wa kituo hicho ni mkakati wa kupambana na matukio ya uhalifu yanayotokea katika jimbo hilo.
   Mbunge wa Jimbo la Segerea la Segerea, Bonnah Kaluwa, akimuongoza Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(suti nyeusi) na viongozi wengine kwenda kutembelea eneo ambapo ujenzi  wa kituo cha polisi katika jimbo hilo umeanza ikiwa ni mkakati wa kupambana na matukio ya uhalifu jimboni hapo.
  Wananchi wa Jimbo la Segerea, wakimsikiliza Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(hayupo pichani), wakati wa Harambee ya  Ujenzi wa Kituo cha Polisi ikiwa ni mkakati wa Mbunge wa Jimbo hilo, Bonnah Kaluwa, kupambana na matukio ya uhalifu katika jimbo hilo.(Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)

  IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI-WIZARA YA         MAMBO YA NDANI YA NCHI

  0 0  Kiungo mshambuliaji wa Simba Queens Zainabu Mohammed (nyeupe) akichuana na mabeki wa Msimbazi Queens wakati wa michuano ya vijana chini ya umri 17 ya Airtel Rising Stars mkoa wa Ilala. Simba Queens ilishinda 3-0.


  Mshambuliaji wa Simba Queens Zainabu Mohammed (nyeupe) akichuana na beki wa Msimbazi Queens Fatuma Shabaan wakati wa michuano ya vijana chini ya umri 17 ya Airtel Rising Stars mkoa wa Ilala. Simba Queens ilishinda 3-0.
  Mshambuliaji wa Simba Queens Zainabu Mohammed (nyeupe) akichuana na mabeki wa Msimbazi Queens wakati wa michuano ya vijana chini ya umri 17 ya Airtel Rising Stars mkoa wa Ilala. Simba Queens ilishinda 3-0. 
   
  Timu ya Simba Queens jana iliweza kuwaadhibu wapinzani wao Msimbazi Queens kwa 3-0 katika muendelezo wa mashindano ya soka kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars katika mkoa wa Ilala mchezo amba ulichezwa kwenye uwanja wa Karume.

  Katika mchezo huo ambao ulianza huo ambao ulikuwa na kasi sana, timu ya Msimbazi Queens ndio walikuwa wa kwanza kufika langoni la wapinzani wao baada ya mshambuaji wake Rosemary Renatus kuwalamba chenga mabeki wawili wa Simba Queens na kuachia shuti dhaifu liliokolewa na kipa wa Simba Queens kwenye dakika ya 4 ya mchezo.

  Msimbazi Queens waliendelea kusakama lango la wapinzani wao lakini hali ilibadilika kwenye dakika ya 17 baada ya Simba Queens kumtoa Zainabu Said na kumuingiza Eva Charles ambaye kwa kiasi kikubwa alibadilisha hali ya mchezo.

  Hata hivyo, Simba Queens walibidi kusubiri mpaka dakika ya 36 kuandika mbao la kwanza. Ilikuwa Diani Hussein ambaye alichukua mpira katika ya uwanja na kutoa fursa murua kwa Zainabu Mohammed na kuandika mbao la kwanza.

  Baada ya mbao hilo, Msimbazi Queens walionekana kuchanganyikiwa kitu ambacho kilitoa nafasi kwa Simba Queens kuandika mbao. Mbao hilo lilitokana na beki wa Msimbazi Fatuma Shabaan kushindwa kucheza mpira uliorudishwa kwake na beki mwenzake Salma Masoud na kusababisha mshambualiaji wa Simba Queens Zainabu Mrisho kuifungia timu yake mbao la pili kwenye dakika ya 38 ya mchezo.

  Simba Queens waliendelea kutawala mchezo na mnamo dakika ya 48, mchezaji ambaye aling’ara katika mchezo huo Zainabu Mohammed alishirikiana vema na mshambuaji mwenzake Eva Charles na kutoa pasi kwa Sarah Ramadhan aliweza kuifungia timu yake goli ya tatu.

  Katika mchezo mwingine uliochezwa katika uwanja huo Ilala Queens waliibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Ukonga Queens, bao ambalo lilipatikana katika dakika ya 17 ya mchezo mfungaji akiwa ni Jane Claus.

  0 0

  Waziri wa mambo ya ndani ya Nchi Mh Mwigulu Nchemba akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa wilaya ya Buhigwe(kushoto) Col.Marko Elisha Gaguti na Mkuu wa wilaya ya Kasulu(kulia) Col.Martin Mkisi.mara baada ya kuwasili mkoani Kigoma mapema leo kuendelea na ziara yake ya kikazi

  0 0


  0 0

  Rais Mstaafu wa Awamu ya pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Ally Hassan Mwinyi ametoa wito kwa watanzania kuongeza juhudi katika kupiga vita dhidi ya ujangili nchini.

  Wito huo umetolewa leo jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa kitabu cha “Tembo-Faru wana haki ya kuishi Tanzania” kilichoandaliwa na Kamati ya Amani ya Viongozi wa Dini Mkoa wa Dar es salaam.

  Rais mstaafu huyo, amesema kumekuwa na tatizo la kutowalinda na kuwatunza wanyama hao kwani kuwauwa ni dhambi na kinyume na kusudio la Mungu kwa kuwa wanyama hao wana haki ya kuishi kama viumbe wengine.

  “ kumekuwa na matukio mengi ya uuaji wa wanyama wakiwemo tembo na faru na hivyo kupunguza rasilimali ya taifa kwa vizazi vijavyo na pia kitendo hicho ni kinyume na kusudio la Mungu hivyo ni vizuri kuwatunza, kuwapenda, kuwaendeleza na kuwalinda wanyama hao kwani ni moja ya vivutio vinavyochangia pato la Taifa” aliongeza Rais Mstaafu Mwinyi.

  Kwa upande wake Waziri wa Maliasili na Utalii Prof Jumanne Maghembe amesema kuwa Tanzania ni nchi ya pili kwa kuwa na mbuga nzuri duniani hivyo ni budi kushirikiana katika kupambana dhidi ya ujangili ndani ya nchi yetu.

  Ameongeza kuwa jumuiya ya ujangili ni kubwa ambayo inahusisha mifumo mbalimbali ikiwemo watengenezaji wa silaha za kuua tembo, waagizaji wa meno ya tembo, wasambazaji na watu mashuhuri ambao wanatumia nyumba zao kuhifadhi meno ya tembo.

  Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya WILDAID Peter Knights ambao ni wadhamini wa kitabu hicho, ameipongeza Serikali ya China kwa jitihada zake za kupiga marufuku biashara ya uuzaji wa meno ya Tembo hatua hiyo imesaidia kulinda wanyama hao.

  Kitabu cha Tembo-Faru wana haki ya kuishi Tanzania kimetayarishwa na kamati ya Amani ya Viongozi wa Dini Mkoa wa Dar es salaam kikiwa na lengo la kudumisha amani kwa binadamu na Wanyama ili wasiweze kupoteza uhai wao
   
  Na Jovina Bujulu-MAELEZO
  10/08/2016
  DAR es Salaam

  0 0

  Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe ametoa wito kwa viongozi wa dini nchini kupitia mahubiri na dua kufikisha ujumbe kwa jamii juu ya kupambana na ujangili nchini.

  Wito huo umetolewa leo jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa kitabu cha “Tembo-Faru wana haki ya kuishi Tanzania” kilichoandaliwa na Kamati ya Amani ya Viongozi wa Dini Mkoa wa Dar es salaam.

  Waziri Maghembe amesema kuwa Viongozi wa dini wakiongeza neno juu ya ujangili wa wanyama hao itasaidia roho za waumini kujua umuhimu wa wanyama hao na kuwatendea mema kwani nao wana haki ya kuishi kama viumbe wengine.

  “Katika ibada zetu za jumapili na ijumaa tujitahidi kutoa mahubiri na dua kwa jamii ili kufikisha ujumbe juu ya kuwalinda wanyama hawa na kupambana na ujangili ndani ya nchi yetu”, amesema Waziri huyo.

  Aidha amesema kuwa idadi ya tembo mwaka 1990 hadi 1994 walikuwa takribani laki tatu na nusu(350,000), mwaka 2009 walikuwa 45,000 na mwaka jana idadi ya tembo hao walikuwa 55,000 hivyo jamii kwa ujumla imetakiwa kuwalinda wanyama hao.

  Mbali na hayo Waziri Maghembe alizitaja faida za wanyama kuwa ni pamoja na kuongeza pato la taifa kwa asilimia 15.5 na kuweza kutoa ajira takribani Watanzania milioni moja katika Sekta ya Utalii na kusaidia katika mzunguko wa uotaji wa baadhi ya mbegu.

  Kwa upande wake Mwandishi wa Kitabu hicho Mchungaji Christosiler Kalata amesema kuwa lengo la kuandaa kitabu hicho ni kuwaelemisha na kuitaka jamii kutunza uumbaji wa Mwenyezi Mungu wakiwemo wanyama.

  Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya WILDAID Peter Knights ambao ni wadhamini wa kitabu hicho, ameipongeza Serikali ya China kwa jitihada zake za kupiga marufuku biashara ya uuzaji wa meno ya Tembo hatua hiyo imesaidia kulinda wanyama hao. 
   
  Na Beatrice Lyimo-MAELEZO
  10/08/2016
  Dar es Salaam 

  0 0


  aziri wa Nchi, Kazi na Mambo ya Jamii kutoka nchini Bavaria Emilie Müller (kulia) akifurahia picha ya kuchorwa aliyokabidhiwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (katikati) jana jijini Dar es salaam wakati wa hafla fupi iliyoandaliwa na Mfuko wa Hanns Seidel Foundation unaojihusisha na masuala ya uwezeshaji wa wanawake katika Nyanja za uongozi, usawa kijinsia na masuala ya siasa katika nchi mbalimbali duniani. Kushoto ni Prof.Ursula Mannle, Mwenyekiti wa Mfuko wa Hanns Seidel Foundation wenye makao yake nchini Ujerumani.
  Wageni mbalimbali waliohudhuria hafla fupi iliyoandaliwa na Mfuko wa Hanns Seidel Foundation unaojihusisha na masuala ya uwezeshaji wa wanawake katika Nyanja za uongozi, usawa kijinsia na masuala ya siasa katika nchi mbalimbali duniani, jana jijini Dar es salaam.


  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza na wageni mbalimbali waliohudhuria hafla fupi iliyoandaliwa na Mfuko wa Hanns Seidel Foundation unaojihusisha na masuala ya uwezeshaji wa wanawake katika Nyanja za uongozi, usawa kijinsia na masuala ya siasa katika nchi mbalimbali duniani. Kwa mujibu wa Hanns Seidel Foundation, Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazofanya vizuri katika uwezeshaji wa wanawake.
  Waziri wa Nchi, Kazi na Mambo ya Jamii kutoka nchini Bavaria Emilie Müller akitoa uzoefu wa nchi ya Bavaria katika kushughulikia masuala ya wanawake kupitia Sera zilizopo nchini humo wakati wa hafla fupi iliyoandaliwa na Mfuko wa Hanns Seidel Foundation unaojihusisha na masuala ya uwezeshaji wa wanawake katika Nyanja za uongozi, usawa kijinsia na masuala ya siasa katika nchi mbalimbali duniani jijini Dar es salaam.
  Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angelina Mabula (kushoto) ambaye ni miongoni mwa wanawake viongozi wa Tanzania walionufaika na Mfuko wa Hanns Seidel Foundation akizungumza jambo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa hafla fupi ya Tathmini ya Mafanikio ya Mfuko wa Hanns Seidel Foundation nchini Tanzania, jana usiku jijini Dar es salaam.
  Prof.Ursula Mannle, Mwenyekiti wa Mfuko wa Hanns Seidel Foundation wenye makao yake nchini Ujerumani unaojihusisha na masuala ya uwezeshaji wa wanawake katika Nyanja za uongozi, usawa kijinsia na masuala ya siasa katika nchi mbalimbali duniani akizungumza wakati wa hafla fupi iliyoandaliwa na Mfuko huo jijini Dar es salaam. Kwa mujibu wa Hanns Seidel Foundation, Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazofanya vizuri katika uwezeshaji wa wanawake.

  Na.Aron Msigwa – Dar es salaam.

  Mfuko wa Hanns Seidel Foundation (HSF) unaojihusisha na uwezeshaji wa wanawake katika nyanja za uongozi, usawa kijinsia na masuala ya siasa katika nchi mbalimbali umeitaja Tanzania kuwa miongoni mwa nchi zinazofanya vizuri katika uwezeshaji wa wanawake duniani.

  Mwenyekiti wa Mfuko huo ambao makao yake yako nchini Ujerumani Prof. Prof.Ursula Mannle ameyasema hayo jijini Dar es salaam wakati hafla fupi iliyoandaliwa na mfuko huo kwa lengo la kufanya tathmini ya mchango wa HSF nchini Tanzania katika kuwajengea uwezo wanawake vijana katika Nyanja za uongozi, usawa kijinsia na masuala ya siasa.

  Prof. Ursula amesema kuwa HSF imekuwa ikitekeleza program mbalimbali za uwezeshaji kwa wanawake kisiasa, kuwaandaa na kuwajengea uwezo wa kuwa viongozi mahiri katika nchi wanazotoka.

  Amesema HCF imeamua kuanzisha programu maalumu nchini Tanzania kwa ajili ya kuwaangalia wanawake wanaojitokeza kugombea katika nafasi mbalimbali za uongozi ili kuwawezesha kuwa viongozi katika nafasi mbalimbali serikalini pia kuziba pengo lililopo la uwakilishi katika nafasi za kisiasa.

  Ameeleza kuwa Hanns Seidel Foundation itaendelea kuwaunga mkono wanawake wa Tanzania wanaojitokeza kuwania nafasi mbalimbali za kisiasa nchini Tanzania kupitia program mbalimbali za ufadhili ili kuwawezesha kumudu gharama na kuwajengea uwezo wa kushindana katika majukwaa ya Siasa.

  Waziri Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto kutoka Tanzania Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza wakati wa hafla hiyo amesema kuwa Serikali ya Tanzania imeendelea kutoa kipaumbele katika nafasi za uongozi kwa wanawake.

  Amesema licha ya kuwepo kwa changamoto mbalimbali zinazowakabili wanawake vijana wa Kitanzania zikiwemo za kijamii na kimila pia ndoa na mimba za utotoni zinazochangia vijana wanafunzi wa kike kuacha masomo yao, Serikali ya awamu ya Tano imeamua kuja na Sera ya Elimu bure kuwawezesha vijana wa kike wa kitanzania kupata elimu.

  Amesema Tanzania imeendelea kuwathamini wanawake katika uteuzi wa ngazi mbalimbali za uongozi Serikalini kuanzia wakuu wa Wilaya, Mikoa, Wakurugenzi, Mawaziri na Naibu Mawaziri pia uwepo wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye ni alama ya hamasa na ushindi katika uongozi kwa wanawake wengine Tanzania.

  Mhe. Mwalimu ameushukuru Mfuko huo kwa mchango wake katika kuwainua wanawake wa Tanzania pia program mbalimbali zilizoanzishwa na mfuko huo kwa lengo la kuwawezesha wanawake nchini.

  Kwa Upande wake Waziri wa Nchi, Kazi na Mambo ya Jamii kutoka nchini Bavaria Emilie Müller akitoa uzoefu wa nchi ya Bavaria katika kushughulikia masuala ya wanawake amesema kuwa kupitia Sera zinazosimamia masuala ya wanawake mambo mengi yameweza kufanyika.

  Ametoa wito kwa Tanzania kuendelea kuzishughulikia changamoto mbalimbali ambazo zimekuwa kikwazo kwa wanawake wa Tanzania kufika mbali na kuwazuia wasiweze kusimama wenyewe katika masuala ya Siasa.

  Naye Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Mbunge wa jimbo la Ilemela Mhe. Angelina Mabula ambaye ni miongoni mwa wanawake wa Tanzania walionufaika kutokana na HSF amesema kuwa alianza harakati za siasa mwaka 2004 licha ya kuwepo kwa changamoto mbalimbali.

  Amesema kuwa ipo haja ya wagombea wanawake vijana wanaoingia katika ulingo wa siasa kusaidiwa kifedha na mfuko huo pamoja na vyama vyao vya siasa wanavyoviwakilisha pindi wanapogombea nafasi mbalimbali za uongozi na kuongeza kuwa wakati umefika kwa wanawake wanaoingia katika siasa kusimama wenyewe kwenye majimbo ya uchaguzi.

  Ametoa wito kwa HSF kuendelea kuwasaidia wanawake vijana wanaoingia kwa mara ya kwanza katika masuala ya siasa kwenye chaguzi zinazokuja ili kuwawekea mazingira mazuri ya kukabiliana na changamoto zinazowakabili.

  0 0  Rahma Moyo Mwanafunzi wa mafunzo kwa vitendo kutoka chuo cha Mt. Agustine Mwanza anayejifunza katika Kitengo cha Mawasiliano wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na maendeleo ya Makazi, akibandika stika kwenye gari la mmoja wa wakazi wa Dar es Salaam, wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya uhamasishaji kulipa kodi ya pango la ardhi itakayoendelea nchi nzima. Kampeni hiyo ilizinduliwa katika uwanja wa Mbagala Zakhem leo. (Imeandaliwa Okanda Blogspot)


  Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mboza Lwandiko akiwagawia vipeperushi wakazi wa Dar es Salaam leo, katika uwanja wa Zakhem Mbagala, wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya uhamasishaji kulipa kodi ya pango la ardhi itakayoendelea nchi nzima.

  Rahma Moyo Mwanafunzi wa mafunzo kwa vitendo kutoka chuo cha Mt. Agustine Mwanza anayejifunza katika Kitengo cha Mawasiliano wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na maendeleo ya Makazi, akimpa vipeperushi mfanyabiashara wa Dar es Salaam, wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya uhamasishaji kulipa kodi ya pango la ardhi itakayoendelea nchi nzima. Kampeni hiyo ilizinduliwa katika uwanja wa Mbagala Zakhem leo.

  Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na maendeleo ya Makazi, Mboza Lwandiko akiwagawia vipeperushi wakazi wa Dar es Salaam leo, katika uwanja wa Zakhem Mbagala, wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya uhamasishaji kulipa kodi ya pango la ardhi itakayoendelea nchi nzima.

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akitembelea Kituo kikuu Ubungo cha Mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani, leo.
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akizungumza na sehemu ya Wananchi waliokuwepo kwenye Kituo Kikuu cha Ubungo, Jijini Dar es salaam leo.
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akiwasalimia wananchi.

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amemtaka Mkurugenzi wa jiji kuanza  mchakato wa kuhamisha kituo kikuu cha mabasi ya mkoani cha ubungo  kuhamia Mbezi mwisho 

  Makonda ameyasema hayo leo wakati alipotembelea  kituo hicho leo, amesema kituo hicho kimeelemewa na idadi ya kubwa ya wasafiri huku miundombinu haiendani na utoaji wa huduma kwa wasafiri wanaotumia kituo hicho.

  Makonda  amesema kuwa baada ya kituo hicho kuhama panatakiwa kufanyika  uwekezaji wa soko kubwa  ili kupunguza msongamano wa watu katika soko la Kariakoo.

  Aidha Makonda amesema kuwa uamuzi huo umetokana na kuonekana kwa kituo hicho kuwa kidogo na kushindwa kutoa huduma ya usafirishaji ya abiria wanaoingia na kutoka katika mikoa mbalimbali.

  Makonda ameutaka uongozi wa kituo hicho  kufunga taa maeneo yote kutokana na kutawala kwa giza nyakati za  usiku,ambapo ni  hatari kwa usalama wa abiria  wanaoshuka  nyakati hizo.

  RC Makonda pia amepiga marufuku kukamata magari kwa kigezo cha maegesho, wakati hakuna alama zinazoonyesha sehemu ya kuegesha magari.


  0 0


  0 0

  0 0  Picha ya pamoja ya Baadhi ya Washiriki wa Mdahalo huo


  wakilishi Mkazi msaidizi kutoka UNFPA Bi. Christine Mwanukuzi akifungua mdahalo huo, kuwashukuru vijana kwa kujumuika pamoja na kuwapongeza kwa kufanikisha mdahalo huo kuelekea katika siku ya vijana duniani siku ya tarehe 12.08.2016
  Bw. Badru Juma Rajabu akielezea historia ya siku ya vijana ilipoanzia na kusisitiza kuwa vijana wanatakiwa kutambulika na wasisahau kuchukua fursa pale wanapowezeshwa
  Oscar Kimario muwezeshaji kutoka Restless Development akielezea baadhi ya ripoti juu ya vijana na kuwasihi vijana kuwa ndio watakuwa mstari wa mbele katika maendeleo endelevu hivyo wanapaswa kujituma na kufanya kazi kwa bidii
  Vijana wakiendelea kufuatilia mdahalo huo kwa makini
  Mwakilishi kutoka Shirika la Kazi la Umoja wa Mataifa ILO Nancy Lazaro akizungumzia ajira zenye staha ,alisema kuwa vijana wengi wameajiriwa lakini katika ajira zisizo na staha na kusisitiza ifike kipindi sasa vijana waajiliwe na kazi zenye Staha.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Msichana Initiatives Rebeca Gyumi akijibu maswali mbalimbali ambayo waliuliza vijana waliofika katika kongamano hilo na kusema kwamba sio kweli kwamba wanafunzi waliomaliza elimu ya vyuo ni vilaza
  Vijana wakiendelea kufuatilia wajibu maswali wakijibu yale waliyo yauliza
  Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya St.Josephs Veronica Shayo kidato cha tano akisisitiza vijana kuwa na tabia za kuweka akiba kwa kile wanachopata ili kije kuwasaidia pindi watakapo kuwa wakubwa.
  Muwezeshaji wakati wa kongamano hilo la vijana ambalo kauli mbiu yake inasema Sepesha Umasikini kwa Michongo Endelevu na yenye tija Bw. Lawrence Ambokile akiendelea kutoa mwongozo
  Noreen Toroka akijibu baadhi ya maswali lakini pamoja na hayo amewasisitiza vijana kuto kutumia kipato wanacho kipata bila tija na wawe na utaratibu wa kuhifadhi kwa ajili ya maendeleo baadae, pia aliongeza kuwa vijana wasilazie damu fursa mbalimbali zinazotolewa kwa ajili yao
  Baadhi ya vijana kutoka Restless Development na wanafunzi pamoja na wadau wakendelea kufuatilia mdahalo
  Mwanzilishi wa Malkia Investment Bi. Jenipher Shigoli akichangia jambo katika mdahalo huo
  Albert Kutoka ILO akichangia na kujibu maswali ya vijana mbalimbali katika mdahalo huo ambapo alisisitiza vijana kujituma
  Mwanzilishi wa Charity Movement Sophia Mbeyela akitoa ushuhuda wake wa jinsi alivyo anza ujasiliamali tangia akiwa mdogo na kusisitiza kwamba vijana haijalishi ni mzima au ana ulemavu wa viungo vya mwili wake wote wanatakiwa kujumuika pamoja na kufanya kazi kwa bidii ili kuleta maendeleo ya Taifa
  Kijana Onesmo akiwaeleza vijana wenzake kuwa kama wao walemavu wavioungo wanaweza kufanya mambo makubwa iwaje vijana wazima wasiweze hii ilikuwa ni changamoto


  Picha na Fredy Njeje wa Blogs za Mikoa

  0 0
 • 08/10/16--14:36: TAARIFA KWA UMMA


 • 0 0

   Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi katikati ya jiji la Mwanza.
    Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiendelea kuzungumza na wananchi katikati ya jiji la Mwanza.
    Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi katikati ya jiji la Mwanza.
   Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiaga baada ya kuzungumza na wananchi baada ya kuwasili katikati ya jiji la Mwanza. 

   Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na baadhi ya wanahabari baada ya kuhutubia maeneo mbalimbali akiwa njiani kuelekea jijini Mwanza
    Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na baadhi ya wanahabari baada ya kuhutubia maeneo mbalimbali akiwa njiani kuelekea jijini Mwanza

    Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongela akitoa taarifa fupi kwaRais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kabla kumualika kuongea na wakazi wa Sengerema akiwa njiani kuelekea jijini Mwanza
   Dkt. Charles John Tizeba ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Buchosa na  Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi akisalimia wananchi mjini Sengerema kabla Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli hajaongea
    Mbunge wa Sengerema Mhe. William Ngeleja akiwashukuru wananchi wa jimbo lake kwa kujitokeza kwa wingi kumpokea Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli jimboni mwake  akiwa njiani kuelekea jijini Mwanza
   Wakazi wa Sengerema wakimshangilia  Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipozungumza nao  akiwa njiani kuelekea jijini Mwanza
   Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wakazi wa Sengerema akiwa njiani kuelekea jijini Mwanza
   Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wakazi na wasafiri mbalimbali wa eneo la Busisi kabla ya kuvuka na kuelekea Mwanza mjini.
   Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu Bw. Gerson Msigwa akimsaidia mwanahabari wa ITV kuripoti ziara ya Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa akizungumza na wakazi na wasafiri mbalimbali wa eneo la Busisi kabla ya kuvuka na kuelekea Mwanza mjini.
   Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mbunge wa Misungwe Mhe. Charles Kitwanga baada ya kuzungumza na wakazi na wasafiri eneo la Busisi kabla ya kuvuka na kuelekea Mwanza mjini.
   Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na mwalimu Mstaafu Mama Zena Seif (61) ambaye alimfundisha darasa la tatu wakati akisoma shule ya msingi ya Chato. Hii ni baada ya kuzungumza na wakazi na wasafiri mbalimbali wa eneo la Busisi kabla ya kuvuka na kuelekea Mwanza mjini. 

   Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na wabunge na baadhi ya viongozi wa mkoa wa Mwanza akiwa katika pantoni MV Misungwi wakati akivuka kuelekea Mwanza mjini.
   Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na wabunge na baadhi ya viongozi wa mkoa wa Mwanza akitoka kwenye  pantoni MV Misungwi wakati akivuka kuelekea Mwanza mjini.
   Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na  wananchi eneo la  Kigongo mara baada ya kuvuka upande wa pili kutokea Busisi.
    Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimia wananchi eneo la  Kigongo mara baada ya kuvuka upande wa pili kutokea Busisi.

    Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimia mtoto na mama yake baada ya kuongea na wananchi eneo la  Kigongo mara baada ya kuvuka upande wa pili kutokea Busisi.
   Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia wananchi mbalimbali wa Kigongo mara baada ya kuvuka upande wa pili kutokea Busisi. 
   Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Mbunge wa Misungwe Mhe. Charles Kitwanga akimtajia badhi ya changamoto jimboni kwake mbele ya  wakazi  wa Usagara katika jimbo la Misungwi mkoani Mwanza.
   Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Mkuu wa Wilaya Mstaafu wa Biharamulo akiongea na kumkaribisha  mbele ya  wakazi  wa Usagara katika jimbo la Misungwi mkoani Mwanza.
   Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na  Mkuu wa Wilaya Mstaafu wa Biharamulo  eneo la Usagara katika jimbo la Misungwi mkoani Mwanza.
   Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na wakazi mbalimbali wa Usagara
   Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wakazi mbalimbali wa Usagara
   Wakazi wa Usagara wakimuaga Rais
   Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono kuwaaga wakazi mbalimbali wa Usagara
   Sehemu nyingi alikuta wananchi wametanda barabarani wakimtaka awasalimu na kuongea nao
   Mbunge wa Nyamagana Mhe. Stanslaus Mabula akiongea na wananchi waliokuwa wametanda barabarani kutaka kumsikia Rais
   Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi wa Buhongwa nje kidogo ya jiji la Mwanza
    Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na mamia ya wananchi wa Mwanza waliofurika barabarani kumsubiri
   Palikuwa hapatoshi
   Wananchi wa Mwanza wakimshangilia  Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli 
   Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli anawaambia wananchi kwamba yeye ni Rais wa kila mtu nchini na atawatumikia wote bila kuwabagua
    Wananchi wa Mwanza wakimshangilia  Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli huku wakimtaka aendelee kuongea nao
    
    Wananchi wa Mwanza wakimshangilia  Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli 
    Wananchi wa Mwanza wakimshangilia  Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli 
   Kila mtu alikuwa na shauku yakumuona na kumsikia Rais
   Wengi walitumia simu zao za mkononi kunasa kila alichokisema
    Wananchi wa Mwanza wakimshangilia  Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli 
    Wananchi wa Mwanza wakimshangilia  Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli 
    Wananchi wa Mwanza wakimshangilia  Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli 
    Wananchi wa Mwanza wakimshangilia  Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli 
   Wananchi wameziba njia ili kumtaka Rais asiwapite bila kuongea nao
    Wananchi wa Mwanza wakimshangilia  Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli 
   Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiendelea kuongea na wananchi wa Mwanza 
   Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahakikishia wananchi wa Mwanza kwamba atawatumikia wote bila kujali dini zao, makabila yao wala  itikadi zao za kisiasa
    Wananchi wa Mwanza wakimshangilia  Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli 
    Wananchi wa Mwanza wakimshangilia  Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli 
   Msafara unapokaribia katikati ya jiji la Mwanza unakutana na umati mkubwa wa wananchi
   Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli anajikuta hana jinsi bali kuzungumza nao
  PICHA ZOTE NA IKULU


  0 0

  Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetengua uamuzi uliotolewa na Hakimu Mkazi Mkuu Emmilius Mchauru wa kufuta shtaka la kutakatisha Dola Milioni 6 za Kimarekani baada ya kuona liliondolewa kinyume cha sheria!
  Kesi hiyo inayomkabili aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) (pichani kati) Harry Kitilya na wenzake dhidi ya mashtaka manane ikiwamo la kutakatisha fedha na walipandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza Aprili Mosi Mwaka huu.  

  Akisoma uamuzi huo Jaji Edson Mkasimongwa alisema baada ya kupitia hoja za pande zote mbili mahakama yake imeona Hakimu Mchauru wa Mahakama ya Kisutu alikosema kuliondoa shtaka hilo na kwamba shtaka la kutakatisha fedha litabaki kama lilivyofunguliwa katika hati ya mashtaka.

  "mahakama ya Kisutu ilikosea kisheria kulifuta shtaka la 8 na ninaamuru kurejesha kumbukumbuku ya jalada la kesi hii kwa ajili ya kuendelea kusikilozwa" alisema Jaji Mkasimongwa.

  Mbali na Kitilya washtakiwa wengine ni Miss Tanzania 1996 Shose Sinare na Sioi Solomon ambao walisomewa mashtaka yao mbele ya Hakimu Mkazi Mchauru.

  Hata hivyo jopo la mawakili wa utetezi liliwasilisha maombi ya kuliondoa shtaka la nane ya kutakatisha fedha na mahaka?a ya Kisutu ilikubali na kuliondoa.Upande wa Jamhuri ukiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu Osward Tibabyekomya ulowasilisha nia ya kukata rufaa kupinga uamuzi huo.

  Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Dar es Salaam alitupolia mbali rufaa hiyo baada ya kusikiloza hoja za pande zote mbili kwamba mahakama yake haina mamlaka ya kusikiliza rufaa ya kuondolewa shtaka la kutakatisha fedha.

  Upande wa Jamhuri ulikata rufani katika Mahakama ya Rufani Tanzania.

  Mahakama hiyo iliyoketi chini ya Jopo la Majaji watatu ikiongozwa na Bernad Luanda,Salum Masati na Aristoclas Kaijage liliamuru jalada la kesi hiyo kurejeshwa mahakama kuu na  kupangiwa jaji mwingine wa kusikiliza rufaa ya Jamhuri.

  Jalada hilo lilipangwa kusikilizwa mbele ya Jaji Mkasimongwa.

  0 0


   Mkurugenzi wa Huduma za Kinga wa Wizara hiyo Dk. Neema Rusimabayila akitoa ufafanuzi kuhusu Chanjo ya Homa ya Manjano na vitendo vya baadhi ya watumishi wa afya   wasiowaaminifu  ambao hulipwa fedha ili waweze kuwatengenezea wasafiri kadi za Chanjo ya Homa ya Manjano na kisha kuzitumia nje ya nchi jambo ambalo kinyume cha sheria  na hatari kwa usalama wa Afya zao.
   Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Mohamed Mohamed akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari juu ya hatua iliyochukuliwa na Serikali kuagiza na kusambaza dozi mbalimbali za chanjo kupitia mpango Serikali wa kukabiliana na changamoto ya upungufu wa chanjo uliojitokeza nchini.
   Meneja Mpango wa Taifa wa Chanjo wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Dafrosa Lyimo akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa Habari kuhusu mpango wa utoaji wa chanjo  zilizokuwa na upungufu zikiwemo za kifua Kikuu, Polio, Surua na Lubela ambazo MSD wamekwisaha anza kuzisambaza.

  Na. Aron Msigwa – Dar es salaam.
  Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kupitia Bohari Kuu ya Dawa (MSD) inatarajia kupokea dozi 14,000 za chanjo ya homa ya manjano mwanzoni mwa mwezi Septemba, 2016 ili kutosheleza mahitaji ya wasafiri watakaohitaji huduma hiyo kwa kipindi cha mwaka mzima.


  Aidha, Wizara hiyo imekwisha nunua dozi za chanjo ya Kifua Kikuu na Polio 739,700 na kusambaza dozi zipatazo milioni  7 kwenye mikoa ya Morogoro, Singida, Dodoma, Tabora na Kigoma.


  Akizungumza leo jijini Dar es salaam Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Mohamed Mohamed amesema kuwa uagizaji na usambazaji wa dozi hizo ni mpango Serikali wa kukabiliana na changamoto ya upungufu wa chanjo uliojitokeza nchini.


  Akifafanua kuhusu kukosekana kwa baadhi ya chanjo ikiwemo ya Homa ya Manjano amesema hali hiyo imetokana na kutokea kwa mlipuko wa homa hiyo katika nchi za jirani ikiwemo Angola jambo lililosababisha akiba ya chanjo hiyo dunia nzima kupelekwa kwenye nchi zenye mlipuko wa ugonjwa huo kwa lengo la kuwachanja wananchi wote ili kuzuia ugonjwa huo kusambaa.


  Amesema kutokana na hali hiyo akiba iliyokuwa imewekwa kwa ajili ya kuzigawia nchi nyingine hasa matumizi kwa ajili ya wasafiri ilibidi ipelekwe katika maeneo yaliyokuwa na upungufu wa dozi hizo kutokana na uharaka na uhitaji wa chanjo hizo.


  Amesema wizara kwa kushirikiana na Shirika la Afya Duniani (WHO) inatekeleza mradi wa majaribio wa kutokomeza kichaa cha mbwa kwenye mikoa ya Lindi, Mtwara, Morogoro, Pwani na Dar es salaam ambayo sasa ina chanjo za kichaa cha mbwa.


  Amebainisha kuwa jijini Dar es salaam chanjo hizo zinapatikana katika hospitali ya wilaya ya Temeke, Kituo cha Afya Magomeni.

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma za Kinga wa Wizara hiyo Dk. Neema Rusimabayila akitoa ufafanuzi kuhusu baadhi ya watoto waliokosa chanjo katika awamu tofauti amesema kuwa wote waliokosa chanjo kuhakikisha kuwa wanamaliza chanjo zao kwa mujibu wa idadi ya chanjo walizopangiwa pindi zitakapopatikana.


  Ametoa wito kwa wataalam wa afya wanaohusika na utoaji wa chanjo kuwapatia taarifa wazazi wenye watoto ambao walihudhuria vituo vya afya kisha kukosa chanjo hizo, kuhakikisha kuwa wanarudi katika vituo vya afya ili waweze kumalizia idadi ya chanjo walizotakiwa kupata pindi zitakapofikishwa kwenye vituo vyao.


   Kuhusu Mradi wa majaribio wa kipindi cha miaka 5 wa chanjo ya kichaa cha mbwa wenye lengo la kuondoa kichaa cha mbwa amesema kuwa unalenga kupunguza idadi ya wagonjwa na vifo vya watu vinavyotokana na kichaa cha mbwa.


  Naye Meneja Mpango wa Taifa wa Chanjo wa Wizara hiyo Dk. Dafrosa Lyimo akifafanua kuhusu mpango wa utoaji wa chanjo  zilizokuwa na upungufu hizo amesema kuwa mpaka sasa utaratibu wa kupokea chanjo zaidi  zikiwemo za kifua` Kikuu, Polio, Surua na Lubela ambapo MSD wamekwisaha anza kuzisambaza.


  Ametoa wito kwa wazazi wenye watoto waliokosa chanjo kuwasiliana na vituo husika ili waweze kupangiwa ratiba ya kupatiwa chanjo hizo kwenye vituo vya kutolea huduma vya serikali ndani ya umri wa miaka 5.

  0 0

  Mwenyekiti wa Bodi wa Shule za Feza, Habib Miradj akizungumza na waandishi wa habari juu kuhusiana na taarifa zinazozagaa za kufungwa kwa shule za Feza leo jijini Dar es Salaam,kushoto ni mkuu wa shule wa Feza, kadri dalcicea


  Na Dotto Mwaibale

  UONGOZI wa Shule za Feza nchini umeibuka na kukanusha taarifa zilizozagaa kwenye mitandao ya kijamii, kuwa wao hawana uhusiano na Fethullah Gulen wala serikali ya Uturuki kwa vile hawajawahi kupokea misaada toka pande hizo mbili za uendeshaji na kuwa shule hizo hazitafungwa.

  Kauli hiyo imetolewa baada ya hivi karibuni kuenea kwa uvumi kuwa shule za Feza zipo hatarini kufungwa kwa madai kuwa mmiliki wake ni yule aliyejihusisha na jaribio la kuipindua serikani nchini Uturuki.

  Mwenyekiti wa Bodi wa Shule hizo, Habibu Miradji aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na wanahabari Kawe jijini Dar es Salaam leo asubuhi.Alisema Watanzania wanapaswa kufahamu kuwa Shule za Feza ni kama asasi zingine zilizosajiliwa kishera na serikali, hivyo ni mali ya watanzania.

  “Shule za Feza zitabaki kuwa kiwanda cha kuzalisha wazalendo wa kitanzania na raia bora wa duniani, hivyo wazazi wanapaswa kuondoa hofu,” alisema.Alisema toka mwaka 1995 shule hiyo imepata mafanikio ya kujenga shule za awali tatu, shule za msingi mbili, sekondari tatu na shule ya kimataifa moja.

  Aliongeza kuwa huo ni uwekezaji wenye mchango katika kukuza pato la taifa, kutoka awamu ya pili, tatu, nne hadi awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli.\Alisema shule ya Feza ni hazina kwa Tanzania kwani shule zake zimekuwa zikishika nafasi ya 10 bora toka mwaka 2004 hadi leo.

  Alisema wanatoa wito kwa wazazi kuwasiliana na uongozi wa shule hiyo kujua kinachoendelea kwenye shule husika kwa manufaa ya wanafunzi wetu na taifa bila kusikiliza uvumi huo unaoenezwa na watu wasiopenda maendeleo ya shule hizo.

older | 1 | .... | 933 | 934 | (Page 935) | 936 | 937 | .... | 1897 | newer