Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 929 | 930 | (Page 931) | 932 | 933 | .... | 1898 | newer

  0 0  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Askofu Josephat Gwajima wa Kanisa la Uzima na Ufufuo katika hafla ya harusi ya Naibu Katibu Mkuui wa Sheria na Katiba Amon Mpanju na mkewe Analises iliyofanyiak kwenye ukumbi wa jeshi wa Lugalo jijini Dar es salaam Agosti 6, 2016.
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Sheria na Katiba, Amon Mpanju akilishwa keki na mkewe , Analises katika tafrija ya harusi yao iliyofanyika kwenye ukumbi wa Jeshi Lugalo jijini Dar es salaam Agosti 6, 2016. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary walihudhuria katika tafrija hiyo.
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Sheria na Katiba, Amon Mpanju akimlisha keki mkewe , Analises katika tafrija ya harusi yao iliyofanyika kwenye ukumbi wa Jeshi Lugalo jijini Dar es salaam Agosti 6, 2016. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary Walihudhuria katika tafrija hiyo.

  0 0


  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mstahiki Meya wa Lindi mjini Ndugu Mohamed Liumbwe mara baada ya kuwasili mkoani Lindi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akivishwa skafu wakati wa mapokezi na Vijana wa mkoa wa Lindi .(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
  Wakina Mama wa mkoa wa Lindi wakimuimbia nyimbo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa mapokezi mkoani hapo.
  Wakina Mama wa mkoa wa Lindi wakimuimbia nyimbo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa mapokezi mkoani hapo.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kwenye Ikulu ndogo mkoani Lindi.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisaini kitabu mara baada ya kuwasili kwene Ikulu ndogo mkoani Lindi wengine pichani ni Waziri wa Kilimo Maliasili na Uvuvi wa Zanzibar Mhe.Hamad Rashidi (kulia) na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Lindi Mzee Ally Mtopa.

  ......................................

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewasili mjini Lindi mchana huu akitokea mkoa wa Dar es Salaam kwa njia ya barabara ambapo hapo kesho anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kilele cha Sikukuu ya Wakulima Nanenane kitaifa kwenye viwanja wa Ngongo katika Manispaa ya Lindi.

  Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kufunga maonyesho hayo ya Nane nane hapo kesho kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta John Pombe Magufuli.Alipowasili ikulu ndogo mjini Lindi Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amepokelewa na Mkuu wa mkoa wa LINDI Godfrey Zambi pamoja na Viongozi mbalimbali wa Serikali na wa vyama vya siasa.

  Katika Msafara wake, Makamu wa Rais ameambatana na Waziri wa Kilimo, Maliasili na Uvuvi wa Zanzibar Mhe. Hamad Rashid.

  0 0  Shekhe wa Bakwata Wilaya ya Chato Hassan Issa Mnubi akiongoza dua ya Kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Mkewe Mama Janeth Magufuli nje ya Msikiti wa Omar Bin-L-Khattab Chato Mkoani Geita. PICHA NA IKULU

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mke wake Mama Janeth Magufuli wakisali katika ibada ya Jumapili katika Kanisa la Bikira Maria Parokia ya Chato mkoani Geita.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na waumini wa kanisa Katoliki wa Parokia ya Chato mara baada ya Ibada katika kanisa hilo Chato Mkoani Geita.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihamasisha mchango wa ujenzi wa Kanisa jipya la la Bikira Maria Parokia ya Chato mkoani Geita.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Padre wa Kanisa la Bikira Maria Parokia ya Chato Henry Mulinganisa mara baada ya kushiriki Ibada katika Kanisa hilo.
  Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akisalimiana na na Padre wa Kanisa la Bikira Maria Parokia ya Chato Henry Mulinganisa mara baada ya kuwasili kwenye kanisa hilo.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono waamini wa Kanisa Katoliki Kanisa la Bikira Maria Parokia ya Chato mkoani Geita hawapo pichani mara baada ya kushiriki Ibada katika kanisa hilo.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Mama Janeth Magufuli wakimsikiliza Mchungaji wa Kanisa la Anglikana Chato Zacharia Samson mara baada ya kuwasili katika kanisa hilo la Anglikana Chato Mkoani Geita.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiimba wimbo wa Amani pamoja na Kwaya ya Kanisa la African Inland Church la Chato Mkoani Geita mara baada ya kuwasili katika kanisa hilo.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Mama Janeth Magufuli wakimsikiliza Mchungaji wa Kanisa la Anglikana Chato Zacharia Samson mara baada ya kuwasili katika kanisa hilo la Anglikana Chato Mkoani Geita.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsalimia Mwalimu wake wa zamani wa Shule ya Msingi Chato Mkoani GeitaMwalimu Mkuu Mstaafu Jackson Nyamwaga mara baada ya kumuona wakati akitoka katika Kanisa la African Inland Church la Chato Mkoani Geita.

  Shekhe wa Bakwata Wilaya ya Chato Hassan Issa Mnubi akiongoza dua ya Kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Mkewe Mama Janeth Magufuli nje ya Msikiti wa Omar Bin-L-Khattab Chato Mkoani Geita. PICHA NA IKULU


  0 0


  Vikombe Vya washindi wa Nyimbo na Kwaya katika Jimbo la Musoma Vijijini. Mashindano hayo yameandaliwa na Waziri wa Nishati na Madini Prof Muhongo Kwa ajili ya kusheherekea sherehe za NANE NANE katika Jimbo hilo. Mashindano hayo yanezinduliwa Leo Tarehe 7/8 kwa Nyimbo za Kwaya na Kumalizika Kesho Kwa Ngoma za utamaduni. Washindi wa kwanza hadi 3 watapewa Kombe na Fedha Taslimu (Mshindi wa kwanza 1,000,000, wa Pili 600,000 na wa tatu 400,000).


  0 0


  Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano wa Kampuni ya Uwekezaji ya UTT AMIS ndugu Daudi Mbaga akitoa elimu kwa wananchi kwenye viwanja vya Nane Nane Arusha.
  Bi Ashura Kassim wa UTT AMIS akiwasaidia wananchi wa mkoa wa Arusha kujiunga katika uwekezaji wa pamoja

  0 0


  Mmoja wa akinamama anaenyonyesha watoto wake maziwa pekee miezi sita ya mwanzo Raya Khamis akitoa ushuhuda na mafanikio anayopata kwenye kilele cha maadhimisho hayo.
  Afisa Lishe, UNICEF Dar es salaam Elizabeth Macha akitoa salamu za Shirika hilo katika maadhimisho ya kilele cha wiki ya unyonyeshaji duniani yaliyofanyika kitaifa Mwera Wilaya ya Kati Mkoa Kusini Unguja.
  Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya Zanzibar Dkt. Fadhil Mohd Abdalla akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika Mwera Wilaya ya Kati Unguja.
  Naibu Waziri wa Afya Arusi Said Suleiman wa kwanza (kulia) akizungumza na akinamama waliohudhuria maadhimisho ya kilele cha wiki ya unyonyeshaji duniani katika kijiji cha Mwera Wilaya ya Kati Unguja.

  Mkuu wa Kitengo cha Lishe Wizara ya Afya Zanzibar Asha Hassan akizungumzia umuhimu wa kunyonyesha maziwa ya mama pekee katika miezi sita ya mwanzo kama Lishe bora zaidi katika makuzi ya mtoto wakati wa kilele cha maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji yaliyofanyika Mwera Wilaya ya Kati Unguja.

  NaRamadhani Ali/Maelezo Zanzibar 7.8.2016

  Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto (UNICEF) limesisitiza umuhimu kwa Tanzania kuongeza juhudi katika kuweka mikakati ya kuboresha unyonyeshaji wa watoto mara tu baada ya kuzaliwa hadi kufikia miaka miwili.

  Akitoa salamau za kilele cha wiki ya unyonyeshaji duniani iliyoadhimishwa katika kijiji cha Mwera Wilaya ya kati Unguja, Afisa Lishe kutoka UNICEF Dar es Salam, Elizabeth Macha alisema utafiti wa 2014 unaonyesha ni mtoto mmoja kati ya wawili wenye umri hadi kufiki miezi 23 wanaonyonyeshwa mara baada ya kuzaliwa kwa Tanzania.

  Alisema kwa Zanzibar ni asilimia 61 tu ya watoto wenye umri kati ya miaka 0-23 wanaonyonyeshwa katika muda wa nusu saa baada ya kuzaliwa na Mkoa wa Kusini Pemba upo nyuma zaidi ukiwa na asilimia 52.

  Aliongeza kusema kuwa watoto wakicheleweshwa kunyonyeshwa kwa masaa 2 hadi 23 baada ya kuzaliwa inaongeza hatari ya kufa katika siku 28 za kwanza za maisha ya mtoto kwa asilimia 40.

  Alisisitiza watoto kunyonyeshwa maziwa ya mama kwa kipindi cha miezi sita ya mwanzo bila kupewa chakula chengine kwa vile yanamsaidia kukua vizuri kiakili na kimwili.Alisema watoto wanaonyonyeshwa maziwa ya mama pekee kwa Zanzibar ni asilimia 20 wakati Pemba ina asilimia 10.

  Afisa Lishe wa UNICEF alisema kunyonyesha ni moja ya uwekezaji muhimu ambayo nchi inaweza kufanya kwa ajili ya ustawi wa wananchi wake."Tunaweza kupata maendeleo ya haraka katika maendeleo yetu endelevu kwa kukuza, kulinda na kusaidia unyonyeshaji," alikumbusha afisa Lishe wa UNICEF.

  Alisema iwapo mipango mizuri ya kuboresha unyonyeshaji na kutekeleza kwa vitendo Tanzania inaweza kufanya unyonyeshaji kuwa sehemu ya mwanzo katika kuimarisha afya kwa kila mtoto na jamii kwa jumla.

  Mkurugenzi wa Kinga na Elimu ya Afya Zanzibar Dkt. Fadhil Mohd Abdalla akimkaribisha mgeni rasmi katika sherehe hizo alisema asilimia kubwa ya wanawake wananyonyesha watoto lakini kasoro iliyopo ni kuwachelewa kuwanyonyesha, kuwalisha vyakula vyengine wakiwa chini ya miezi sita na kuwaachisha maziwa kabla ya miaka miwili.

  Naibu Waziri wa Afya ambae alikuwa mgeni rasmi katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji duniani Arusi Said Suleiman aliwahimiza akinamama kuwanyonyesha watoto wao maziwa pekee katika kipindi cha miezi sita ya mwanzo kwani ni kinga bora kwa afya zao.

  Kauli mbiu ya maadhimisho hayo "Unyonyeshaji ni kichocheo cha Maendeleo endelevu. Dumisha unyonyeshaji kwa maslahi ya wote".

  0 0

   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Amos Makalla baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Songwe, Mbeya Agosti 7, 2016 ambako Agosti 8, 2016 atahitimisha maonyesho ya wakulima Nanenane
     Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakipokea heshima kutoka kwa Skauti wa Mbeya baada ya kuwasili kwenye uwanja wa  Songwe Agosti 7, 2016 ambako Agosti nane atahitimisha maonyesho ya wakulima Nanenane. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary wakifurahia ngoma baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Songwe, Mbeya Agosti 7, 2016 ambako  Agosti 8, 2016 Mheshimiwa Majaliwa atahitimisha maonyesho ya wakulima Nanenane. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makla. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0
 • 08/07/16--08:38: katuni


 • 0 0


  Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Bi. Anastazia Wambura (kushoto) pamoja na Makamu wa Rais wa StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif (kulia) wakiwa wamekaa kwenye madawati hayo.
  Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Bi. Anastazia Wambura (kulia) , akizungumza wakati wa kupokea madawati hayo. Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Mh. Dkt. Khatib Malimi Kazungu
  Makamu wa Rais wa StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif (kushoto), akizungumza wakati wa kukabidhi madawati hayo.


  Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Bi. Anastazia Wambura (kushoto) pamoja na Makamu wa Rais wa StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif (kulia) wakiwa kwenye baadhi ya madawati yaliyochangiwa na kampuni hiyo ikiwa ni jitihada za kuunga mkono kampeni ya kuchangia madawati nchi nzima iliyoanzishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt. John Pombe Magufuli. Zoezi hio la uchangiaji wa madawati lilifanyika katika ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Mtwara mwishoni mwa wiki hii.
   
   Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Bi. Anastazia Wambura amepokea madawati hamsini yenye thamani ya shilingi milioni tano kutoka kwa kampuni ya matangazo ya dijitali ya StarTimes ikiwa ni jitihada za kuunga mkono kampeni ya kuchangia madawati iliyoanzishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt. John Pombe Magufuli.

  Akizungumza mara baada ya hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika mwishoni mwa wiki moani Mtwara, Mh. Bi. Wambura amebainisha kuwa zoezi la kuchangia madawati ili kuwawezesha wanafunzi kusoma katika mazingira mazuri linawahusu watu wote na sio serikali pekee.

  “Ningependa kuchukua fursa hii kuzipongeza taasisi za umma na sekta binafsi kwa mwitikio wao mkubwa wa kumuunga mkono Mheshimiwa Rais katika kampeni ya kuchangia madawati. Wote tunafahamu ni kwa kiasi gani shule nyingi nchini zinavyokabiliwa na uhaba wa madawati jambo linalopelekea mazingira magumu ya kufundishia na kujinzia. 
  Lakini kwangu mimi suala la wanafunzi kuongezeka sioni kama ni tatizo bali ni changamoto kwa serikali yetu na jamii kwa ujumla kuendana na mwamko mkubwa wa wazazi na walezi kuwapeleka watoto wao shule. Kwa muda mrefu sana serikali imekuwa ikiwahamasisha wananchi wake wawapeleke watoto shule na wakafanya hivyo, sasa suala hilo tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa na vivyo jinsi walivyoitikia mwamko huo basi waitikie na wa huu wa kuchangia madawati.” Alisema Mh. Bi. Wambura

  Naibu Waziri huyo aliendelea kwa kuelezea kuwa serikali ina wajibu wa kuhamasisha maendelea kwa wananchi wake kwa njia mbalimbali ikiwemo hii ya kuwasilisha maeneo ambayo yanapaswa kupewa kipaumbele kama vile suala la elimu nchini.

  “Elimu ndio suala la msingi katika taifa lolote duniani iwe lililoendelea au linaloendelea na ndio maana kwa nchi za wenzetu wanawekeza fedha nyingi katika sekta hii. Nchi yoyote yenye wasomi wengi lazima itakuwa na maendeleo makubwa kutokana na raia wake kuelimika lakini hayo yote haya hayatowezekana kama tusipowawekea mazingira mazuri wanafunzi wetu tangu ngazi ya msingi,” alisema Mh. Naibu Waziri na kumalizia, “Ningependa kumalizia kwa kuwapongeza na kuwashukuru wenzetu wa kampuni ya StarTimes kwa kuguswa na suala hili na kuamua kuja huku Mtwara kuchangia madawati kwani huku ndiko kwenye changamoto kubwa hasa kutokana na taasisi na makampuni mengi kuwepo sehemu za mijini. Tunawashukuru sana na tunawaomba muendelee na moyo huo huo na mfike sehemu nyingine amabko makampuni mengine hayafiki.”

  Kwa upande wake Makamu wa Rais wa StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif amesema kuwa kampuni hiyo imekuwa ni mdau mkubwa wa masuala ya kijamii hususani elimu kwa inafahamu umuhimu wake katika kuleta mapinduzi ya kimaendeleo.

  “StarTimes ni mdau mkubwa sana wa masuala ya elimu na kwa muda mrefu tumekuwa tukisaidia shule zenye wanafunzi wenye mahitaji maalumu. Uchangiaji wa madawati ni kampeni ya aina yake iliyoanzishwa na Mh. Rais Magufuli na inahitaji kuungwa mkono kwa nguvu zote kwani yeye aliamini kabisa watanzania tunao uwezo huo ila tulikosa tu uhamasishaji. 
   
   
  Na ni kweli uhamasishaji ndio uliokosekana kwani mara baada ya kutoa tamko hilo taasisi, makampuni, mashirikia, wananchi na watu binafsi wameonyesha mwitikio mkubwa. Hii ni dalili njema kwamba watanzania tunaweza kuleta maendeleo yetu wenyewe bila ya kungojea msaada kutoka kwa watu wa nje.” Alisema Bi. Hanif

  “Leo hii tumekuja huku Mtwara kuja kukabidhi madawati haya, tunafahamu kwamba ni machache lakini yatakuwa ni msaada mkubwa kwa watoto wetu kusoma katika mazingira mazuri. Wanafunzi wanaposoma katika mazingira mazuri hupelekea kuhudhuria vipindi, kuipenda shule, kuelewa vizuri na hatimaye kupelekea kufaulu masomo yao,” alisema na kuhitimisha Bi. Hanif kuwa, “Wananfunzi wanapowekewa mazingira mazuri ya kusomea pia hutoa hamasa kwa walimu kufanya kazi yao kwa ufanisi mkubwa kwani ufundishaji unakuwa ni rahisi na vivyo hivyo uelewa kwa wanafunzi.
   
   Hivyo basi, ningependa kutoa wito kwa wanafunzi wayatunze madawati haya ili yaje kuwanufaisha na wenzao watakaokuja siku za usoni na tunawaahidi kuwa tuko pamoja nao katika kutatua changamoto zinazowakabili.”

  0 0


  Wakazi wa manispaa ya kinondoni.

  Kuna karatasi linazunguka mitaani kuwa ni sheria mpya za halmashauri ya manispaa ya kinondoni, likionyesha tozo mbalimbali za uegeshaji magari kando ta barabara na gharama zake.

  Hiyo nyaraka si nyaraka halali wala rasmi ya manispaa ya kinondoni;

  • Haina afisa muidhinishaji, Kwa niaba au mkurugenzi na saini yake,pamoja na terehe ya kutolewa.

  •Hakuna mkataba mpaka sasa ulioingiwa na manispaa wala kikao kilicho kaa kupitisha jambo hilo.

  Tunawaomba mpuuzie na msiwe na hofu na jambo hilo kwa maana sio halali mpaka mtakapo julishwa rasmi kama lipo.

  Watu wenye nia ovu na taswira ya manispaa ya kinondoni huenda wana ajenda wanayoijua, bali si mamlaka halali.

  Mstahiki Meya, Manispaa ya Kinondoni
  Boniface Jacob

  0 0


  Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu akikagua kuku waliofungwa kisasa ambapo jogoo mmoja aliyefikisha umri wa mwaka mmoja anauzwa shilingi 20,000
  Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu akinunua Asali kwa ajili ya matumizi yake baada ya kuvutiwa na asali hiyo iliyopo kwenye banda la Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
  Dc Mtaturu akikagua chakula cha kuku kinachotengenezwa na Uyanjo Vicoba Group ya Wilayani Ikungi
  Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu (mwenye suti), Kulia kwake ni mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ikungi Hassan Tati, kushoto kwake ni Ally Mwanga ambaye ni Mwenyekiti wa Halmshauri ya Wilayaya Ikungi, Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya yaikungi, na Wajasiriamali kutoka katika Halmashauri ya Wilaya hiyo 
   
  Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika banda la maonesho ya Nanenane la Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
  Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu akisikiliza kwa makini maelekezo kutoka kwa Rehema F. Malila kutoka Kijiji cha Unyangwe, Kata ya Iseke ya namna usindikaji unavyofanyika Wilayani humo
  Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu akipata ufafanuzi kutoka kwa Mratibu wa Mfuko wa Afya ya jamii (CHF) Edward Bulilo Maselo alipotembelea banda la maonesho la Halmashauri ya Wilaya ya Singida juu ya umuhimu wa jamii kujiunga na mfuko huo
  Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu akipata maelekezo ya ufugaji wa kisasa wa kuku kutoka kwa mfugaji aliyefanikiwa katika ufugaji Madai Njou anayetokea Kijiji cha Nyangwe, Kata ya Iseke baada ya kupatiwa mafunzo kutoka Idara ya Kilimo na ufugaji ya Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
  Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu akikagua Tomato Saurce inayotengenezwa na mjasiriamali Rehema F. Maliwa na nyanya aina ya Tanya

  Na Mathias Canal, Dodoma

  Wananchi wametakiwa kujihusisha na ufugaji wa kuku kwa njia za kisasa ili waweze kujipatia kipato kupitia mayai ama kuuza kuku mwenyewe ili kuondokana na dhana ya kuishi na kuku ilihali wanajigamba kama wafugaji wazuri.

  Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Mkoani Singida Miraji Jumanne Mtaturu alipotembelea banda la Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi katika maonesho ya Nane nane yanayofanyika katika Uwanja wa Nzuguni Kanda ya Kati Dodoma ambayo yanataraji kufikia kilele hapo kesho.

  Mtaturu amesema kuwa asilimia kubwa ya wananchi Wilayani humo na Taifa kwa ujumla wanajihusisha na shughuli za Kilimo na ufugaji lakini aina ya ufugaji wanayoitumia ni ile iliyopitwa na wakati na kuishi na mifugo ndani badala ya kuijengea eneo la banda ambalo ni pana na maalumu kwa ajili ya ufugaji.

  Dc Mtaturu amewataka wataalamu wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi katika idara ya kilimo kutoa elimu kwa wananchi juu ya mazao makuu ya biashara yanayostahimili mvua ili kupata mazao ya kutosha na kuyauza kwa wakati tofauti na mazao mengine ambayo yanalimwa kila maeneo hivyo kupunguza gharama halisi ya bei.

  Amewataka pia wataalamu hao kuhakikisha elimu wanayoitoa kwa wananchi inakuwa sambamba na kuwashauri wananchi kulima zao la mtama wa muda mfupi aina ya Hakina na Macia.

  Kwa upande wake Afisa Kilimo wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ayoub Yusuph amesema kuwa ofisi yake itatekeleza maagizo yote yaliyotolewa na mkuu wa Wilaya hiyo ili kuwainua zaidi wananchi ambao wanalima na kufuga lakini sio kilimo na ufugaji wa kisasa jambo ambalo linawarudisha nyuma kimaendeleo.

  Yusuph alisema kuwa katika maonesho hayo wamewaalika wakulima na wafugaji ambao wamefanikiwa katika kilimo na ufugaji wao baada ya kupata mafunzo kutoka katika ofisi yake ili kushuhudia na kuelezea mbinu walizopatiwa na namna zilivyowasaidia.

  0 0

  0 0

  Mmoja wa washiriki wa timu ya Lugalo Golf Club Noel Mheni akiwa mwenye furaha mara baada ya kuibuka washindi wa mashindano ya Golf yaliyojulikana kwa jina la MOSHI OPEN,yaliyofanyika mkoani Kilimanjaro mwishoni mwa wiki.Timu hiyo ya golf ya Jeshi ya Lugalo imewapa raha wanachama wake akiwemo Mlezi wa Klabu hiyo ambaye ni Mkuu wa majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange kwa kurejesha Ubingwa wa mashindano ya Moshi Open .
  Mmoja wa wacehezaji wa timu ya Lugalo Golf Club,Nicholaus Chitanda akionesha makombe waliyoyanyakuwa mara baada ya timu yao kuibuka washindi wa mashindano ya Golf yaliyojulikana kwa jina la MOSHI OPEN,yaliyofanyika mkoani Kilimanjaro mwishoni mwa wiki.Timu hiyo ya golf ya Jeshi ya Lugalo imewapa raha wanachama wake akiwemo Mlezi wa Klabu hiyo ambaye ni Mkuu wa majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange kwa kurejesha Ubingwa wa mashindano ya MOSHI OPEN.Timu hiyo ya Golf  imeirejesha heshima yake kwa wanachama na wapenzi wake kwa kuibuka na vikombe,ambapo mara ya mwisho klabu hiyo kuibuka na ushindi ilikuwa ni mwaka 2014.
  Timu ya Lugalo Golf Club wakiwa katika picha ya pamoja mara baada
  ya kuibuka washindi wa mashindano ya Golf yaliyojulikana kwa jina la MOSHI OPEN,yaliyofanyika mkoani Kilimanjaro mwishoni mwa wiki,Mashindano hayo yalizishirikisha timu ya Ghymkana,timu ya Golf Moshi pamoja na timu ya Gofu ya jijini Arusha.

  0 0

  Picha ya pamoja.
  Mamaa wa mitindo Asya Idarous Khamsini akipata picha ya kumbukumbu baada ya siku ya Jumamosi Aug 6, 2016 kufanya kweli kwenye kenya Women Reunion iliyoyanyika katika hotel ya Hilton Garden Inn  iliyopo mtaa wa State Highway Dallas, Texas nchini Marekani.
  Mlimbwende wa mitindo akiwa kwenye kivazi kilichowavutia wengi kutoka kwa mama mitindo Asya Idarous Khamsini alipofanya kweli siku ya Jumamosi Aug 6, 2016  kwenye kenya Women Reunion iliyoyanyika katika hotel ya  Hilton Garden Inn  iliyopo mtaa wa State Highway Dallas, Texas nchini Marekani.
  Mlimbwende akiwa katika pozi na kivazi cha mama mitindo Asya Idarous Khamsini.
  Ni Kivazi kingine kutoka kwa mama mitindo Asya Idarous Khamsini.
  Mlimbwende katika picha.
  Mlibwende katika picha akiwa na kivazi kutoka kwa mama mitindo Asya Idarous Khamsini.
  Asya Idarous Khamsini ni Balaa tupu.
  Mlimbwende akiwa ametokelezea kweli na kivazi kutoka kwa mama mitindo Asya Idarous Khamsini.
   

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia Wajasiriamali wa mkoa wa Lindi kwenye ukumbi wa Kanisa Katoliki la Mtakatifu Kagwa.

  Mkuu wa mkoa wa Lindi Ndugu Godfrey Zambi akisoma taarifa ya mkoa wakati wa mkutano uliowakutanisha Makamuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Wajasiriamali wa mkoa wa Lindi katika ukumbi wa Kanisa Katoliki la Mtakatifu Andrea Kagwa.

  Wajasiriamali wa mkoa wa Lindi waliohudhuria mkutano wao na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
                                                
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewahimiza viongozi wa mkoa wa Lindi wasimamie kikamilifu zoezi la utengenezaji wa madawati ili kuhakikisha madawati yanayotengenezwa yanakuwa na ubora na yanakidhi viwango vinavyotakiwa.

  Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo mjini Lindi Tarehe  7-Aug-2016 katika mkutano wake na wajasiriamali wa mkoa Lindi pamoja na viongozi mbalimbali wa mkoa huo.


  Makamu wa Rais amesema msukumo mkubwa wa serikali uliopo kwa sasa unalenga kuhakikisha madawati yanayotengenezwa kote nchini yanakuwa imara  huku akipongeza  jitihada kubwa zinazofanywa na serikali ya mkoa wa Lindi ya utengenezaji wa madawati ambapo mpaka sasa mkoa huo umebakisha asilimia Moja tu ya utengenezaji wa madawati hayo ili kukamilisha zoezi hilo.


  Kuhusu mikopo kwa wajasiriamali, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa serikali italifanyia kazi ombi la wajasiriamali wa mkoa wa Lindi ambao wameiomba serikali ifanye mazungumzo na watendaji wa taasisi za kifedha nchini ili waweze kupunguza riba kwenye mikopo wanayopata kama hatua ya kuongeza hamasa kwa wananchi wengi zaidi kukopa fedha kwa ajili ya kuimarisha shughuli ujasiriamali.


  Makamu wa Rais pia amezitaka halmashauri zote nchi kutekeleza kwa vitendo mkakati wa kutenga asilimia TANO ya makusanyo ya mapato yake na kutoa fedha hiyo kwa wanawake na vijana kwenye halmashauri hizo ili waweze kuanzisha na kuendeleza miradi yao ya kiuchumi kwenye maeneo yao.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0


  Meneja wa Bayport Financial Services, Kanda ya Kaskazini, Emmanuel Nzutu, kulia, akipeana mikono na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Bumbuli, Peter Nyalali kushoto baada ya kumkabidhi msaada wa jenereta kutoka kwenye taasisi yao ya Bayport kwa ajili ya ofisi ya Halmashauri ya Bumbuli ili iweze kujiendesha vizuri kutokana na ukosefu wa umeme kwenye majengo yao ya ofisi. Nyuma ya Nzutu ni Meneja wa Bayport wilaya ya Lushoto Consolata Thomas, akifuatiwa na Afisa Utumishi wa Bumbuli, Fatma Mrope. Picha na Mpiga picha wetu Bumbuli.

  Na Mwandishi Wetu, Bumbuli.

  KUTOKANA na kukosa umeme katika ofisi za Halmashauri ya Bumbuli, Taasisi ya kifedha ya Bayport Financial Services, imemkabidhi jenereta Mkurugenzi wa halmashauri hiyo ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi na kufanikisha maendeleo kwa wakazi na wananchi wa Bumbuli, mkoani Tanga.

  Makabidhiano hayo yamefanyika mwishoni mwa wiki iliyopita yakiongozwa na Meneja wa Bayport Kanda ya Kaskazini, Emmanuel Nzutu, Meneja wa Bayport, wilayani Lushoto mkoani Tanga, Consolata Thomas, Mkurugenzi Mtendaji Bumbuli Peter Nyalali, Afisa Utumishi wa Bumbuli Fatma Mrope na baadhi ya watumishi wengine wa halmashauri hiyo.

  Akizungumza katika makabidhiano hayo, Meneja wa Bayport Kanda ya Kusini, Nzutu, alisema kwamba taasisi yao imeona ikabidhi msaada wa jenereta kwa mkurugenzi wa Bumbuli ili watumishi kwenye ofisi hiyo watoe huduma bora na kwa wakati ili kuharakisha maendeleo katika serikali ya Hapa Kazi Tu, inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dr John Pombe Magufuli.

  Bayport ni taasisi inayotoa huduma za mikopo huku tukifanya kazi kwa karibu na watumishi wengi nchini Tanzania, hivyo baada ya kuona ofisi za Halmashauri Bumbuli hazina umeme na wafanyakazi wanapata tabu, tukaona tuje kuwakomboa kwa kuwapa jenereta.

  “Tunaamini sasa wana Bumbuli watahudumiwa vizuri na kwa wakati, maana awali mtu anaweza kukosa huduma pale inapohitaji kifaa kinachoendeshwa na umeme, hivyo Bayport tunaamini tutaendelea kufanya kazi kwa karibu na kushirikiana na viongozi wote ili kuhakikisha kwamba nchi yetu inasonga mbele,” Alisema.

  Meneja wa Bayport Financial Services, Kanda ya Kaskazini, Emmanuel Nzutu, kulia, akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Bumbuli, Peter Nyalali kushoto baada ya kumkabidhi msaada wa jenereta kutoka kwenye taasisi yao ya Bayport kwa ajili ya ofisi ya Halmashauri ya Bumbuli ili iweze kujiendesha vizuri kutokana na ukosefu wa umeme kwenye majengo yao ya ofisi. Nyuma ya Nzutu ni Meneja wa Bayport wilaya ya Lushoto Consolata Thomas, akifuatiwa na Afisa Utumishi wa Bumbuli, Fatma Mrope.

  Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo ya Bumbuli, Nyalali, aliwashukuru Bayport Financial Services kwa kuwakomboa baada ya kuwapa msaada wa jenereta litakalowezesha utoaji huduma bora pamoja na ukusanyaji wa mapato na rekodi kwa ofisi muhimu za halmashauri yao.

  “Kukosekana umeme kwa ofisi nyeti za halmashauri ni jambo linaloweza kuwafanya watumishi wafanye kazi chini ya kiwango pamoja na kushindwa kukusanya mapato ya serikali kwa wakati kwa sababu kuna vifaa ili vijiendeshe lazima umeme uwepo,” Alisema Mkurugenzi huyo ambaye ameripoti kazini kwa mara ya kwanza tangu alipoteuliwa kuongoza halmashauri hiyo.

  Afisa Utumishi wa Bumbuli, Fatma Mrope aliwashukuru Bayport huku akisema kupata jenereta kutawafanya watumishi wote wakose visingizio vya umeme hivyo kufanya kazi kwa nguvu zote za kuwatumikia wana Bumbuli na Watanzania kwa ujumla.

  Mwandishi wa Star Tv mkoani Tanga, Mbonea Herman akiwajibika katika tukio la Bayport Financial Services kukabidhi jenereta kwa ofisi ya Halmashauri ya Bumbuli, mwishoni mwa wiki.

  “Ofisi za Halmashauri yetu ya Bumbuli ilikuwa na changamoto kubwa ya kukosa umeme, hivyo ingawa tunaendelea na juhudi za kupata umeme kutoka Mamlaka ya Umeme Vijijini (REA), tunafurahia sana msaada huu kutoka kwa watu wa Bayport, maana utakuwa mkombozi kwa kiasi kikubwa mno kwa sababu nikiwa kama Afisa Utumishi naifahamu adha tuliyokuwa tunaipata,” alisema Fatma.

  Mbali na kutoa mikopo ya fedha taslimu, Bayport pia inatoa huduma ya mikopo ya viwanja katika maeneo mbalimbali kama vile Kibaha, Chalinze, Bagamoyo, Kigamboni na Kilwa, huku ikifanikiwa kuwa na ofisi katika mikoa yote ya Tanzania Bara na wilaya mbalimbali kwa ajili ya kusogeza huduma zao karibu na wananchi.

  0 0


  Kaimu Mkurugenzi wa utafiti na Uchimbaji wa Shirika la Madini (STAMICO) Alex Rutagwelela (Katikati) akiongea na waandishi wa Habari (Hawapo pichani) wakati wa maonyesho ya Nane nane Viwanya vya Ngongo - Lindi.

   
  Katika kuhakikisha wachimbaji wadogo wananufaika na kazi zao na kuepuka kuondolewa na wachimbaji wakubwa wameshauriwa kuchukua leseni ndogo za awali za uchimbaji.
   
  Wito huo kwa wachimbaji umetolewa na kaimu mkurugenzi wa utafiti na uchimbaji wa shirika la madini (STAMICO) Alex Rutagwelela alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari katika viwanja vya ngongo Manispaa ya Lindi yanapofanyika maonyesho ya nane nane kitaifa.

  Rutagwelela alisema wachimbaji wadogo wanatakiwa kuwa na leseni za awali zitakazowafanya wawe na haki kwenye maeneo wanayochimba. hivyo kuwa na uhakika wa kuto ondolewa bila taratibu na wachimbaji wakubwa kwenye maeneo wanayochimba.
  Wananchi wakisikiliza maelekezo kutoka kwa Maafisa wa STAMICO walipotembelea Banda lao katika Maonyesho ya Nane nane yanayoendelea Mkoani Lindi katika viwanja vya Ngongo.

  Aliwahakikishia wanahabari na wananchi shirika hilo linania ya kuwainua wachimbaji wadogo kwa kufanyia tathimini maeneo wanayochimba ili waweze kujua kiasi cha madini na mashapo yaliyopo katika maeneo hayo.

  Alisema wachimbaji wanaweza kupata fursa ya mafunzo ili waweze kupata ujuzi wa kuyafahamu mambo ya kijiolojia, vilevile watakuwa na uwezo wa kupata mikopo. Hata hivyo alitahadharisha kwamba wanaweza kunufaika na fursa hizo ni wachimbaji wenye leseni.

  "Wachimbaji wenye leseni nilazima wainuliwe, wengi wao hawana mitaji wanachimba kipindi cha masika kwenye makorongo na kiasi wanachopata ni kidogo sana, kwamfano wilaya ya Ruangwa na mkoa huu unamadini ya aina nyingi na mengi wakiwezeshwa watanufaika," alisema Rutagwelela.
  Akibainisha wachimbaji wadogo wanachimba kwa kubahatisha, hivyo shirika hilo lipotayari kuwasaidia kufanya tathimini na kuwaonesha kiasi cha mashapo yaliyopo katika maeneo wanayochimba.

  Huku akitoa wito wawe tayari kwa uchangiaji kiasi kidogo cha fedha ambacho ni rafiki kwa wachimbaji wadogo kwa ajili ya gharama ya uendeshaji mitambo wakati wa kuchoronga, ikiwamo mafuta.

  Akiongeza kusema STAMICO kwa niaba ya serikali imejipanga kuwasaidia kufikia malengo yao ya kiuchumi na kimaendeleo.

  0 0


  Baadhi ya Wananchi wakijaza Fomu ya Kujiunga na WOTE SCHEME katika Banda la PPF Viwanja vya Nane Nane Ngongo Kama Picha Inavyoonekana Afisa Uhusiano Mwandamizi, Janet Ezekiel akitoa maelekezo ya Jinsi ya Kujaza Fomu Hizo.
  Wananchi waliotembelea Banda la PPF, wakimsikiliza kwa Makini Afisa Masoko PPF Wakati akitoa Elimu Juu ya Mfumo wa WOTE SCHEME.
  Baadhi ya Wananchi wakijaza Fomu ya Kujiunga na WOTE SCHEME katika Banda la PPF Viwanja vya Nane Nane Ngongo Kama Picha Inavyoonekana Afisa Uhusiano Mwandamizi, Janet Ezekiel na Afisa Masoko PPF, Wakitoa maelekezo ya Jinsi ya Kujaza Fomu Hizo
  Afisa Uhusiano Mwandamizi, Janet Ezekiel akimkabidhi kadi ya WOTE SCHEME kwa mwananchi aliyejiunga na Mfuko huo.

  Mfuko wa Pensheni wa PPF upo katika Viwanja vya Ngongo Manispaa ya Lindi katika Maonesho ya Nane nane ili Kutoa Elimu kwa Wananchi juu ya Mfumo wa WOTE SCHEME kwa Sekta Binafsi kama Vile Wakulima,Wafugaji, Mama Lishe, Madereva Bodaboda na Wajasilamali mbalimbali ili waweze kujiwekea Akiba wakati huohuo wakinufaika na Bima ya Afya, Mikopo kwa Ajili ya Kujiendeleza Kielimu, Kuongeza Mtaji na Kunufaika na Pensheni za kila Mwezi.

  Akiongea na Lindiyetu.com Bi Janeth ametoa wito kwa wadau mbalimbali kutembelea Banda hilo la PPF kwa ajili kupata elimu na kujiunga na mfuko huo na kufaidika na fursa zinazotolewa na PPF.

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu , Mhe. Anthon Mtaka akimkabidhi fedha Bw. Methesela Mrobi wakati wa zoezi la uhawilishaji fedha za ruzuku kwa wanufaika wa Mpango wa kunusuru kaya maskini TASAF III ,katika kijiji cha Mwamgoba, Wilaya ya Busega Mkoani humo.
  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu , Mhe. Anthon Mtaka akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Mwamgoba wilayani Busega (hawapo pichani) kabla ya zoezi la uhawilishaji fedha za ruzuku kwa wanufaika wa Mpango wa kunusuru kaya maskini TASAF III kijijini hapo, Wilayani Busega Mkoani humo. Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akifafanua jambo kwa wakazi wa Kijiji cha Mwamgoba wilayani Busega (hawapo pichani) kabla ya zoezi la uhawilishaji fedha za ruzuku kwa wanufaika wa Mpango wa kunusuru kaya maskini TASAF III kijijini hapo, Wilayani Busega Mkoani humo. Baadhi ya wanufaika wa Mpango wa kunusuru kaya maskini TASAF III katika kijiji cha Mwamgoba Wilayani Busega, wakiwasikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka na katibu tawala Jumanne Sagini (hawapo pichani), walipozungumza nao kabla ya zoezi la uhawilishaji wa fedha za ruzuku kwa ajili ya mpango huo. Bw. Methesela Mrobi akimuonesha Mkuu wa Mkoa wa Simiyu na viongozi wengine wa Mkoa na Wilaya(hawapo pichani) Bwawa dogo alilochimba kwa kutumia fedha za ruzuku za Mpango wa kunusuru kaya maskini TASAF III, ambalo analitumia kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji Mkuu wa Wilaya ya Busega , Mhe. Tano Mwera (katikati) na Katibu Tawala Wilaya ya Busega, Bw. Sebastian Masanja (kulia) wakizungumza jambo kabla ya zoezi la uhawilishaji fedha za ruzuku kwa wanufaika wa Mpango wa kunusuru kaya maskini TASAF III kijiji cha Mwamgoba, Wilayani Busega (kushoto) Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini
   
    Na Stella Kalinga (Ofisi ya Mkoa wa Simiyu)

  Mkuu wa mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka amewataka viongozi wa kata na vijiji kuwabaini wanufaika wa Mpango wa kunusuru kaya TASAF III(PSSN) wanaojihusisha na ulevi na kuwaondoa katika orodha ya wanufaika wa mpango huo.

  Mtaka ametoa agizo hilo wakati alipozungumza na wananchi wa kijiji cha Mwamgoba wilayani Busega katika zoezi la uhawilishaji fedha za TASAF III PSSN, ambapo jumla ya shilingi 2,976,000 zimegawiwa kwa wanufaika 82 kijijini hapo.

  Mtaka amesema lengo la mpango wa TASAF III ni kuwatoa watanzania katika hali ya umaskini kwa kuwapa ruzuku itakayowasadia kupata huduma muhimu ikiwa ni pamoja huduma za afya, kuwasaidia watoto wao waweze kwenda shule lakini baadhi ya wanufaika wamekuwa wakitumia fedha hizo kulewa badala ya kuanzisha miradi midogo midogo kama ufugaji wa kuku, mbuzi na kondoo pamoja na kilimo ili miradi hiyo iwasaidie kuwaongezea kipato.

  “Hatuwezi kuleta fedha tukifikiri zitawasaidia kujikwamua katika Umaskini lakini mnashinda baa na vilabuni kulewa , wengine mnaongeza wake, tukiwabaini mtaondolewa kwenye huu mpango” , alisema Mtaka.

  Mtaka amewataka wanufaika hao kujishugulisha na kilimo na ufugaji na kuondokana na dhana ya kuwa watakuwa wanufaika wa mpango huo siku zote, ambapo alieleza azma ya Serikali ya awamu ya tano ya kuwatoa wananchi katika umaskini na kuwaondolea changamoto mbalimbali kama kutoa elimu ya bila malipo na kuanzisha Mfuko wa Huduma ya Afya Watanzania wasio na uwezo waweze kupata matibabu kwa gharama nafuu na akatoa wito kwa wanufaika hao kujiunga na Mfuko wa Huduma ya Afya ya Jamii (CHF)ambao utawasaidia wao wenyewe pamoja na wategemezi wao kupata huduma za Afya katika Vituo vya kutolea huduma za Afya.

  Aidha, ametoa wito kwa wazazi kuwakumbusha watoto wao wajibu wa kuwatunza kwa sababu kumekuwa na baadhi ya wazee ambao wametambuliwa kuwa ni maskini, wakati wana watoto wenye nguvu na uwezo wa kuwasaidia lakini hawatimizi wajibu wao kuwatunza kwa kuwapa mahitaji muhimu.

  Akizungumza baada ya kukabidhiwa fedha hizo Bibi. Christina Robert ambaye ni mnufaika wa mpango wa TASAF amesema mpango huo umemsaidia kuondokana na kuishi katika nyumba ya nyasi na matope na kumuwezesha kujenga nyumba ya matofali na bati.

  “Naishukuru TASAF maana imenisaidia sana, ruzuku niliyopewa mara ya kwanza ilinisaidia kutibiwa nilipofanyiwa upasuaji, mara ya pili nilitumia tena kwenye matibabu, mara ya tatu nilinunua kuku na bata, mara ya nne nikanunua bati nikajenga nyumba ya vyumba viwili”, alisema Christina.

  Pamoja na kusisitiza juu ya matumizi sahihi ya fedha za ruzuku za TASAF Mtaka amewataka wananchi wa Busega na Mkoa wa Simiyu kwa ujumla kuongeza juhudi katika kilimo cha mazao ya mikunde kwa kuwa tayari Serikali ya India imekubali kununua zaidi ya tani milioni sita ya choroko, dengu na mbaazi kutoka Tanzania, hivyo wakati utekelezaji wa makubaliano hayo utakapoanza wananchi walime kwa wingi mazao hayo kwa kuwa kutakuwa na soko la uhakika.

  Jumla ya kaya 4260 zilibainishwa katika vijiji 41 vya wilaya ya Busega ambapo kaya 53 ziliondolewa katika mpango wa TASAF III PSSN baada ya uhakiki na kubaini kuwa hazikukidhi vigezo.

older | 1 | .... | 929 | 930 | (Page 931) | 932 | 933 | .... | 1898 | newer