More Channels
Showcase
Articles on this Page
(showing articles 18581 to 18600 of 37921)
- 08/05/16--14:05: _WAZIRI NCHEMBA AAGI...
- 08/05/16--14:13: _JE UMEZAA MTOTO N...
- 08/05/16--23:46: _VIJUSO VYA BAADHI Y...
- 08/06/16--05:21: _JE WAJUA UMUHIMU WA...
- 08/06/16--06:14: _RC ZAMBI AISHAURI W...
- 08/06/16--06:28: _DKT. KIGWANGALA ATO...
- 08/06/16--06:31: _LHRC YAMPA MAPOKEZI...
- 08/06/16--06:34: _DAS ILALA, EDWARD M...
- 08/06/16--07:05: _N/WAZIRI JAFO: WATA...
- 08/06/16--07:18: _ BRAZIL YAONESHA N...
- 08/06/16--07:54: _NAIBU WAZIRI MAMBO ...
- 08/06/16--12:53: _UVCCM ARUSHA YATOA ...
- 08/06/16--12:57: _MSHINDI WA AIRTEL T...
- 08/06/16--13:03: _KAMPUNI YA BRITAM Y...
- 08/06/16--13:06: _WANANCHI WAZIDI KUF...
- 08/06/16--13:39: _HIVI KAMA WEWE UNGE...
- 08/06/16--13:43: _WAKIHAMIA DODOMA SI...
- 08/07/16--01:52: _MKURUGENZI WA UTAWA...
- 08/07/16--02:03: _TUWATAKIE JUMAPILI ...
- 08/07/16--04:39: _MASHINDANO YA MAJES...
(showing articles 18581 to 18600 of 37921)
Channel Description:
Karibuni Jamvini Wanajamii
Waziri Nchemba akitembelea eneo la Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa
Mganga mkuu wa mkoa wa Iringa Dr Salmu Robart akimwonyesha waziri Nchemba ufinyu wa eneo la Hospitali hiyo ya rufaa ya mkoa wa Iringa
Na MatukiodaimaBlog
WAZIRI wa mambo ya ndani ya nchi Bw Mwigulu Nchemba ameagiza uongozi wa Magereza ya mkoa wa Iringa kuanza mchakato wa kuhamisha magereza ya Manispaa ya Iringa ili eneo hilo kutumika kupanua Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Iringa.
Bw Nchemba ametoa agizo hilo leo baada ya kutembelea eneo hilo ambalo limekuwa likiombwa kwa muda mrefu na viongozi wa serikali ya mkoa wa Iringa ili litumike kwa ajili ya matumizi ya Hospitali hiyo ya Rufaa ya mkoa wa Iringa .
Akizungumza baada ya kutembelea eneo hilo lililopo eneo la Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa alisema kuwa amekubaliana na maombi ya viongozi wa mkoa wa Iringa ya kuomba gereza hilo kuhamishiwa katika eneo la Mlolo nje kidogo na Manispaa ya Iringa huku eneo hilo la Magereza litumike kupanua majengo ya Hospitali hiyo ya Rufaa ya mkoa wa Iringa.
“ Kwa kawaida kati ya Hospitali na magereza kinachotakiwa kuwepo mjini ni Hospitali na sio magereza hivyo hivyo kati ya mgonjwa na mfungwa ama mahabusu anayeweza kufanya kazi ya kufyatua tofari za ujenzi ni mahabusu ama mfungwa na sio mgonjwa ……hivyo naagiza mtaalam wa ujenzi wa magereza kuanza kuandaa vifaa vya kufyatualia tofari na kwa kufuata taratibu za magereza waorodheshwe wale ambao watakuwa tayari kujitolea kufanya kazi ya ujenzi ili kazi hiyo ianze”
Hata hivyo waziri huyo alisema kuwa kuanzia leo jioni anataka kupata orodha ya wafungwa waliopo gerezani hapo ambao wanauwezo wa kufanya kazi.
Pia alisema suala la kuhamishwa kwa gereza hilo litafanyika kwa awamu na kuwa wakati gereza linajengwa na baadhi ya nyumba za watumishi bado askari wataendelea kuishi katika eneo hilo huku majengo yao likiwemo jengo la Ghorofa utawekwa utaratibu wa kujengewa jingine ili hilo linalotumiwa na magereza litumike kwa ajili ya madaktari .
waziri wa mambo ya ndani ya nchi Bw Mwigulu Nchemba akisalimiana na waziri wa nyumba na maendeleo ya makazi Bw Wiliam Lukuvi (kuli) leo baada ya kukutana ofisi ya mkuu wa mkoa wa Iringa
Waziri Lukuvi katikati akimtambulisha mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela kwa waziri Nchemba leo
Waziri Nchemba akisikiliza jambo kutoka kwa waziri Lukuvi
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Bw Peter Kakamba akisalimiana na waziri wa mambo ya ndani ya nchi Bw Nchemba
Mbunge Msigwa akisalimiana na waziri wa mambo ya ndani ya nchi Bw Mwigulu Nchemba
Mbunge wa Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa wa pili kushoto wakisalimiana kwa furaha na mwenyekiti wa CCM Iringa mjini Abeid Kiponza huku waziri wa mambo ya ndani ya nchi Bw Mwigulu Nchemba na mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela (kushoto) wakiangua kicheko
0 |
|
0 |
|
Unao watoto wa namna mbalimbali. Unao uliowazaa ndani ya ndoa na wale uliowazaa nje ya ndoa. Unawapenda sana wote kwa usawa kwasababu wote ni watoto wako. Kuna suala la kifo na ungependa baada ya kifo chako watoto wako wote wafaidi kidogo ulichochuma. Lakini je hilo umelijengea mazingira.
Ni muhimu sana ujue kuwa suala la watoto wako kufaidi ulichonacho halitokani na matakwa yako, laa hasha bali linatokana na matakwa ya sheria. Wewe waweza kuamua watoto wako wote wa nje ya ndoa na wale wa ndani ya ndoa wapate mali lakini baadhi wakakosa kutokana na msimamo wa sheria.
Ni hapo unapotakiwa kuandaa mazingira yanayoendana na matakwa ya sheria ili watoto wako wote waweze kufaidi machumo yako.
1.FANYA HAYA ILI KUWAWEZESHA WATOTO WA NJE YA NDOA KURITHI.
a. KWA WAISLAMU.
Kama wewe ni muislam na una mtoto/watoto nje ya ndoa hakikisha unaandika wosia ambao utampatia mali hata huyo mtoto wa nje ya ndoa. Lakini lazima ujue kuwa mali yako yote uliyonayo ni 3/3 = (100%). Hivyo 2/3 ya mali yote ni lazima iende kwa warithi halali ambamo mtoto wa nje ya ndoa hataingia kabisa. Katika mali hiyo ya 2/3 wala haihitaji wosia kwakuwa tayari sheria ya kiislam imeeleza vipi hiyo mali igawanywe.
Uhuru wako wa kugawa mali kwa wosia upo katika 1/3 basi na si vinginevyo. Na ni kusema kuwa mtoto/watoto wa nje ya ndoa haki yao ipo katika 1/3 tu. Ikiwa utampatia mali zaidi ya 1/3 basi anaweza kunyanganywa . Kwahiyo uelewe kuwa wosia utakaoandika unahusu 1/3 ya mali tu.
Zingatia kuwa usipoandika wosia kugawa 1/3 yote au sehemu yake kwa mtoto/watoto uliowazaa nje ya ndoa basi hawatapata mali kabisa baada ya kifo chako. Na hii ni kwasababu watoto hao hawaruhusiwi kurithi kisheria. Kwahiyo utaona kuwa unachotakiwa kufanya ili hao watoto wasikose ni kupiga hesabu ili kupata 1/3 ya mali yako na kuwapa yote au sehemu yake.
KUSOMA ZAIDI sheriayakub.blogspot.com
Na Khadija Khamis – Maelezo .
Mtaalamu wa kitengo cha lishe kutoka Wizara ya Afya Zanzibar Mariyam Amir amesema kunyonyesha mtoto maziwa ya mama mara tu anapozaliwa hadi kufikia miaka miwili humjenga kukuwa mwili na kiakili pamoja na kumuepushia utapiamlo na maradhi nyemelezi.
Aliyasema hayo leo katika Shehia ya Muungano wakati akitoa elimu kwa wananchi wa shehia hiyo katika siku ya kwanza ya wiki ya unyonyeshaji wa maziwa ya mama kwa watoto wenye umri wa siku ziro hadi miaka miwili .
Alisema kinga bora kwa watoto ni maziwa ya mama katika kuwaepusha na maradhi mbali mbali iwapo wazazi watawanyonyesha watoto wao kwa mujibu inavyotakiwa .
“Kunyonyesha maziwa ya mama ni njia inayomsaidia mtoto kukua vizuri na kumuepushia mzazi kupata ujauzito katika kipindi cha miezi sita ya mwanzo,”alisema mtaalamu huyo .
Alifahamisha kuwa maziwa ya kifua hupatikana muda wote na pahala popote na ni safi na salama pia yanavirutubisho vya kutosha na joto linalohitajika kwa kumjenga mtoto.
Aliongeza kuwa maziwa ya mama hupunguza vifo vya watoto kwa asilimia kubwa iwapo mtoto atanyonyeshwa maziwa pekee kwa miezi sita ya mwanzo
Wiki ya unyonyeshaji huanzia wiki ya kwanza ya mwezi wa nane kila mwaka na tarehe nane huwa ni kilele cha siku hiyo na kaulimbiu ya mwaka huu ni UNYONYESHAJI NA KAZI HAKIKISHA INAWEZEKANA .
Akizungumzia unyonyeshaji kwa akinamama wanaofanyakazi ofisini, amewashauri kukamua maziwa katika chombo safi na kuyahifadhi katika jokofu na kupewa mtoto mara kwa mara kwani yanauwezo kukaa hadi saa nane bila kuharibika.
KUTOKA HABARI MAELEZO ZANZIBAR
0 |
|
0 |
|
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi akisoma kipeperushi cha Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Miaka Mitano alipotembelea banda la Wizara ya Fedha na Mipango katika Maonesho ya Wakulima Nanenane Mkoani Lindi.
Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo (wa pili kushoto) na Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Kikwete, Mama Salma Kikwete (wa pili kulia) wakipata maelezo kutoka kwa mtaalamu wa Kilimo walipotembelea banda la Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) katika Maonesho ya wakulima (Nanenane) katika viwanja vya Ngongo-Lindi.
Wananchi kutoka mikoa ya Lindi na Mtwara wakifuatilia kwa makini maelezo kuhusu maonesho ya Nane Nane yanayoendelea katika viwanja vya Ngongo mkoani Lindi
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Godfrey Zambi (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa mtaalamu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Alexander Lweikiza, alipotembelea banda la Wizara hiyo katika Maonesho ya Wakulima Nane nane Mkoani Lindi.
Mkuu wa Hazina Ndogo Mkoani Lindi Bi. Pili Kamali (wa pili kulia) pamoja na wakazi wa mkoa wa Lindi wakipata maelezo kwa mtaalamu wa Taasisi iliyochini ya Wizara ya Fedha na Mipango katika Maonesho ya Wakulima Nane nane Mkoani Lindi.
Walimu wa Sekondari Mnolela iliyopo Mkoani Lindi wakipata maelezo katika Taasisi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Bima nchini (TIRA) walipotembelea katika banda la Wizara ya Fedha na Mipango katika Maonesho ya Wakulima ya Nanenane yanayoendelea katika viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi. Walimu na wanafunzi wa Sekondari ya Mnolela Mkoani Lindi wakipata maelezo kutoka kwa mtaalamu wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) walipotembelea katika banda la Wizara ya Fedha na Mipango katika Maonesho ya Wakulima ya Nanenane yanayoendelea katika viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.
Walimu na wanafunzi wa Sekondari ya Mnolela Mkoani Lindi wakipata maelezo kutoka kwa mtaalamu wa Wizara ya Fedha na Mipango kuhusu Hotuba ya Bajeti Kuu ya mwaka 2016/2017 walipotembelea katika banda la Wizara ya Fedha na Mipango katika Maonesho ya Wakulima ya Nanenane yanayoendelea katika viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.
RC ZAMBI AITAKA WIZARA YA FEDHA KUJENGA MIUNDOMBINU YA KUDUMU ENEO LA NANE NANE-NGONGO
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Godfrey Zambi ameishauri Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na Taasisi zake kujenga jengo la kudumu katika Viwanja vya maonesho ya Kitaifa ya Wakulima (Nanenane) mkoani Lindi katika viwanja vya Ngongo ili kupunguza gharama za kukodi maturubai wakati wa maonesho.
Alisema pamoja na kupunguza gharama, baada ya maonesho, jengo hilo linaweza kutumiwa katika shughuli nyingine na Halmashauri ya Wilaya hivyo kuiongezea Wizara kipato.
Mhe. Zambi alitoa ushauri huo alipotembelea banda la Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na Taasisi zake katika viwanja vya Ngongo Lindi ambapo aliweza kuona shughuli mbalimbali zilizokuwa zikifanyika katika mabanda ya yanayotumiwa na Taasisi zilizoko chini ya Wizara hiyo.
Vilevile alizishauri Taasisi kujitangaza ili wananchi wengi waweze kufahamu huduma zinazotolewa na Taasisi hizo kwani huduma zao ni muhimu kwa Wananchi hususani wakulima.
"Wananchi wengi wanaoishi mikoani hususani Lindi, hawana uelewa wa kutosha kuhusu huduma zinazotolewa na Taasisi zilizo chini ya Wizara hasa huduma ya Bima na Mifuko ya uwekezaji"Alisema Zambi.
Alisema kuwa maonesho haya yanawawezesha Wananchi kuelewa pia namna ya utekelezaji wa bajeti na vipaumbele vyake kamavile kujenga miundombinu ya Barabara, Maji, Elimu na Afya.
Mhe. Zambi ameziomba Taasisi zinazoshughulika na utoaji mikopo kuwawezesha wananchi wa kipato cha chini hasa wakulima ili waweze kujiendeleza kiuchumi.
Pia aliipongeza Serikali kwa kuandaa Mpango wa Pili wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano ambao anaamini utakua chachu ya mapinduzi ya kiuchumi kwani mpango huo umelenga zaidi katika kukuza viwanda ambayo vitaongeza ajira kwa vijana.
Pia alitoa rai kwa Taasisi ambazo hazijashikiri maonesho hayo mwaka huu kujipanga kwa ajili ya mwakani kwani maonesho hayo ni muhimu kwao, Wananchi na Taifa kwa ujumla.
Imetolewa na:
Benny Mwaipaja
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Fedha na Mipango
0 |
|
0 |
|


Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla amefanya ziara ya ghafla katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kufuatia taarifa zilizoripotiwa kwenye mitandao ya Kijamii na baadhi ya Magazeti ya hapa Nchini juu ya kutelekezwa bila kupatiwa huduma kwa mgonjwa wa Sickle Cell (Selimundu) na Madaktari na manesi wa Hospitali hiyo.
Dk. Kigwangalla ameweza kufika kwenye Hospitali hiyo ya Muhimbili na kisha kwenda moja kwa moja kwa mgonjwa huyo ambaye awali picha yake ilisambazwa kwenye mitandao ya kijamii na ujumbe wa kutelekezwa iliyosambazwa na Wanaharakati wa Sickle Cell ambao waliomba Serikali ichukue hatua. (Kama walivyoandika kawenye ujumbe hapa chini).


Hata hivyo, Dk. Kigwangalla baada ya kujionea hali halisi ya tukio la mgonjwa huyo kupitia mitandao na magazeti aliamua kutembelea mwenyewe katika wodi ya magonjwa ya damu (Haematology) huku akiomba kuoitia nyaraka zake zote pamoja na kupatiwa taarifa za kutelekezwa mgonjwa huyo kama ilivyoripotiwa ambapo hata hivyo hali ilikuwa ni tofauti na ilivyoripotiwa.
“Nimekuja mwenyewe na wala sikutaka kutuma wasaidizi wangu. Nimemtembelea Mgonjwa ‘KK ‘ na kukuta hajatelekezwa wala kunyanyaswa. Hajalazwa chini. Ameonwa na jopo la Madaktari bingwa lililoongozwa na Dk. Stella, kwa siku mbili mfululizo tokea alipowasili wodini.
Mgonjwa alilazwa juzi. Ni kweli anaumwa Sickle Cell, yupo kwenye 'painful crisis', lakini amepewa Antipains zote anazopaswa kupewa ikiwemo kali kabisa ya aina ya 'Morphine'! Mgonjwa hana malalamiko. Mwanzoni hakujua mimi ni nani na nilikuwa peke yangu na hivyo hakuogopa kunipa taarifa yoyote ile. Pia nimekagua faili lake neno Kwa neno, nimeridhika ametibiwa ipasavyo.
Kuzusha taarifa za uongo, kutafuta 'sympathy' (huruma) Kwa kusingizia watu kunakatisha tamaa, Hivyo naagiza Hospitali zote nchini kudhibiti wageni kupiga picha wodini hii ni pamoja na kuzuia simu zote za camera kuingizwa mawodini pamoja na camera za aina yoyote ile na kwa atakayekihuka kuna sheria na kanuni zitafanya kazi” alieleza Dk. Kigwangalla.
Kwa upande wake mgonjwa huyo Mwanadada, K. Kasongo ambaye alikiri kufika hapo siku tatu zilizopita na kupokelewa vizuri na wahudumu pamoja na Madaktari ambapo na kupatiwa huduma stahiki.
Kwa hali hiyo, Dk. Kigwangalla aliomba jamii kuacha kuripoti mambo wasiyo yajua kwani yanaweza kuchangia upotevu wa amani.
“Nilisononeka sana awali wakati nimepata habari hizi. Bahati mbaya nilikuwa Jimboni, sikuwa na namna ya kufanya zaidi ya kurudi Ofisini kisha kufuatilia. Niliyoyakuta hayafanani hata chembe na kilichoandikwa hapa na wanaharakati hawa wa Sickle Cell (selimundu). Wakati tukihangaika kuboresha huduma za Afya nchini Kwa ajili ya watu wote, Wakati tukifanya kazi Kwa bidii zote, usiku na mchana, masaa ya ziada, Kila kona ya nchi, kutwa kucha barabarani, unakutana na watu wa aina hii, wanapotosha umma, wanaotafuta umaarufu wa taasisi yao kwa kutoa taarifa za uongo kwa umma juu ya mambo wasiyoyajua. Alieleza Dk. Kigwangalla.
Aidha, aliongeza kuwa: kutokana na hali hiyo ambayo imeonekana kukatisha sana tama, ametoa rai kwa Wanaharakati kutambua kuwa Serikali imewekwa madarakani na wananchi kwa kura na Kwa Msingi huo ina imani na Matumaini kamili ya wananchi, Na pia ina uchungu na huruma kwa wananchi walioipa mamlaka na si vinginevyo.
Na kwamba, hata siku moja wanaharakati wasidhani wanaweza kuwa mbadala kamili wa Serikali, wao ni wabia muhimu na wanaisaidia Serikali kuutumikia umma (complementary efforts) na Siyo mbadala (alternative) wa Serikali. Kama wabia wakuu wa Serikali, wanaharakati wana wajibu wa kusema ukweli bila kuegemea upande wowote ule ili kulinda heshima yao na kulinda 'relevance' yao kwenye mfumo wa uongozi na utawala wa nchi.


Geline Fuko (kushoto) akipokea maua kutoka kwa wafanyakazi wenzake wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC),ikiwa ni ishara ya kumpongeza baada ya kutua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam jana, akitokea Marekani alikokuwa akihudhuria mafunzo ya vijana wa kiafrika yaliyoandaliwa na
Raisi Obama.
Na Dotto Mwaibale
SHANGWE ilitawala wakati mtanzania Geline Fuko alipo wasili Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) majira ya saa nne usiku jana Agosti 5, 2016 akitokea nchini Marekani alikohudhuria mafunzo ya viongozi vijana kutoka Bara la Afrika.
Wafanyakaziwa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu ambao ni wafanyakazi wenzake wa Geline, familia ya Geline, ndugu na marafiki walitoa mapokezi ya kishujaa wa wanaharakati huyo aliyetajwa kuwa mfano wa kuigwa na Rais Obama.
Akizungumza na wanahabari, Geline alisema amefarijika na hakutarajia kama wazo lake la kuanzishwa kwa Kanzidata ya Katiba litakuwa wazo kubwa ambalolitakubalika mpaka na Rais Obama.
Hata hivyo Geline alisema amefurahishwa na program hiyo ya Mandela Washington Fellowship kwani imewawezesha washiri kikujifunza mambo mengi na kupata uono mpana zaidi wakufanya mambo.
Geline iliwahimiza watanzania kutembelea Kanzidata hiyo iliyopo mtandaoni (http://katiba.humanrights.or.tz/) ili kuweza kuijua katiba yao na kuweza kujua haki zao kama watanzania. Mwisho alishukuru wa mapokezi makubwa ambayo pia hakuyatarajia.
Akitoa neno la shukurani kwa Geline kwa niaba ya LHRC, Mkurugenzi wa Fedha naUtawala-LHRC, Ezekiel Masanja amempongeza Geline kwa kuitoa kimasomaso LHRC na Tanzania kwa ujumla.
Geline Fuko amepata kutambulika baada ya Rais Obama kumtaja kama mfano wa kuigwa wa wanaharakati wa haki za binadamu wakati akizungumza Jumatano Agosti 3, 2016 katika kilele cha mpango wake wa kuwawezesha vijana wakiafrika unaojulikana kama Mandela Washington Fellowship.
Raisi Obama alimsifu mwanasheria huyo kutoka LHRC ambaye ni moja ya vijana 1000 waliokuwa jijini Washington kwa lengo la kujengewa uwezo ili kuweza kusaidia Maendeleo katika Nyanja zote za maisha katika nchi zao.
RaisiObamaalisifujuhudizaGelinezakuibuawazo la kuanzishakwamaraya kwanza Kanzidata ya Katiba nchini Tanzania kwa kutekeleza wazo hilo chiniya LHRC. Raisi Obama alikaririwa akisema Marekani itaendelea kushikamana na wanaharakati kama Geline Fuko kutoka Tanzania.
GelinenimwanasherianamwanaharakatiwahakizabinadamuambayeamefanikishakuanzishwakwaKanzidatayaKatibaya kwanza nayapekeenchini Tanzania inayowawezesha watanzania kusoma Katiba kupitia simu zao za mkononi”.
Programu ya Mandela Washington Fellowship yenye lengo la kuwa wezesha vijana wa Kiafrika katika Nyanja za kiuchumi, kisiasa, kiteknolojia na kijamii ilianzishwa na Rais Obama mwaka 2014.
Programu hii hujumuisha vijana elfu moja (1000) kutoka nchi mbalimbali za Afrika ambao hugharamiwa na serikali ya Marekani kwenda jijini Washington kwa lengo la kujengewa uwezo zaidi.
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kilianzisha Kanzidata ya Katiba mwaka mmoja uliopita mnamo Julai 15, 2015.
Kupitia tovuti maalumu (http://katiba.humanrights.or.tz/) na simu za mkononi, watanzania wanaweza kusoma Katiba katika Kanzidata hiyo.
0 |
|
0 |
|

OfisaTawala wa wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam, Edward Mpogolo, akiwahutubia Vijana waalikuwa na wanachama wa Taasisi ya Vijana ya TYVA, wakati wa hafla maalum ya maadhimisho ya miaka 16 ya Taasisi hiyo, iliyofanyika leo katika ukumbi wa British Council jijini Dar es Salaam.
Na Bashir Nkoromo
Ofisa Tawala wa Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam, Edward Mpogolo, pamoja na mambo mengine, Mpogolo amewaasa Vijana wa Taasisi ya Vijana ya TYVA kuhakikisha mipango yao ya kushirikisha Vijana katika shughuli za kimaendeleo, inaendana na mipango ya serikali ili kuwezesha utekelezwaji usiokinzana.
Amesema, iwapo TYVA itapanga kwenye malengo yao mipango inayotofautiana na ile ya serikali kuhusu maendeleo ya vijana na mengineyo, basi utekelezwaji wake unaweza kuwa siyo rahisi kutokana na kukinzana kwa kuwa malengo ya serikali yatakuwa yanaelekeza vingine wakati na wao wamelenga vingine.
Pia aliwataka vijana wa TYVA na wengine kote nchini kuhakikisha wanailinda amani ya Tanzania kwa gharama na nguvu zao zote, akitahadharisha kwamba, amani ni tunu ambayo ikishapotea si rahisi kurejeshwa.
Ameitaka TYVA na Taasisi ngingine za Vijana popote zilipo, kuhakikisha wanakuwa makini dhidi ya watu wasioitakia mema Tanzania, akisema, wapo ndani na nje ya nchi ambao hutamani sana kuona amani ya Tanzania inapotea au inatetereka kwa namna yoyote, na kibaya zaidi kujaribu kujipenyeza kwa makundi ya vijana ili kufanikisha azima zao mbaya.
"Kitu kingine ninacho waasa wakati Taasisi yenu ya TYVA inatimiza miaka 16 sasa, waelimisheni vijana wenzangu, wajihadhari sana, wasije kutekwa na watu waliopo ndani na nje ya Tanzania ili kuwatumia kuharibu amani ya nchi yetu", alisema Mpogolo.
Baadaye Mpogolo alizindua Kitabu cha Mipangokazi au bajeti ya Taasisi hiyo na kukata keki kushiria TYVA kutimiza miaka 16 tangu ilipoanzishwa na kuendelea kwa mafanikio kufanya kazi zake katika nyanja mbalimbali ikiwemo kuhamasisha vijana kushiriki katika shughuli za ujenzi wa taifa.

OfisaTawala Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam, Edward Mpogolo akizindua mpangokazi au bajeti ya Taasisi ya Vijana ya TYVA, wakati wa maaldhimisho ya miaka 16 ya Taasisi hiyo yaliyofanyika leo katika ukumbi wa British Council Dar es Salaa.. Kushoto ni Mwenyekiti wa TYVA Nuria Mshale

Vijana wakiwa wamenyoosha miko yao wakati Ofisa Tawala wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo (aliyesimama) alipokuwa akiwapiga tafakuri kuhusu umuhimu wa Amani ya Tanzania, alipozungumza nao wakati wa maadhimisho ya miaka 16 ya TYVA yaliyofanyika leo katika ukumbi wa British Council jijini Dar es Salaam.

Ofisa wa TYVA Zuleikha akiwasilisha keki meza kuu kwa ajili ya mgeni rasmi, Osisa Tawala wa wilaya ya Ilala Edward Mpogolo (kulia) kuikata, kunogesha maadhimisho ya miaka 16 ya TYVA yaliyofanyika leo katika ukumbi wa British Council, Dar es Salaam.

Ofisa Tawala wa wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo akikata keki kunogesha maadhimisho ya miaka 16 ya Taasisi ya Vijana ya TYVA, yaliyofanyika katika ukumbi wa British Council, Dar es Salaam, leo. Kulia ni Ofisa Vijana mkoa wa Dar es Salaam, Masalida Sephania Njashi na kushoto ni Zuleikha wa TYVA na wapili ni Mwenyekiti wa TYVA Nuria Mshare

Keki baada ya kukatwa

Mwenyekiti wa TYVA Nuria Mshare akimlisha keki Ofisa Tawala wa wilaya ya Ilala Edward Mpogolo wakati wa hafla hiyo

Mwenyekiti wa TYVA Nuria Mshare akimlisha keki Ofisa Vijana Dar es Salaam, Masalida Njashi wakati wa hafla hiyo

Mpogolo akimlisha keki Mwenyekiti wa TYVA wakati wa hafla hiyo.

Mpogolo akimlisha keki Mkuu wa Idara ya Ushawishi na Utetezi ya TYVA, Makwita Abdul wakati wa hafla hiyo

Mpogolo akimlisha keki Zuleikha wa TYVA wakati wa hafla hiyo

Ofisa Tawala wa wilaya ya Ilala Edward Mpogolo akiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa juu wa Taasisi ya Vijana ya TYVA mwishoni mwa hafla ya TYVA kutimiza miaka 16 tangu kuanzishwa kwake. Kulia ni Ofisa Vijana wa mkoa wa Dar es Salaam. Masalida Njashi na aliyeketi kushoto ni Mwenyekiti wa TYVA Nuria Mshare. Picha zote na Bashir Nkoromo. PICHA KEM-KEM ZA BIRTHDAY HIYO YA TYVA TAFADHALI>>GONGA HAPA
0 |
|
0 |
|

Naibu waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI Jafo Suleiman Said akisikiliza maelezo ya namna ya kulima kilimo na ufugaji wa kisasa.

Naibu waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI Jafo Suleiman Said akizungumza na Luteni AJ Massawe Meneja wa banda la JKT

Naibu waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI Jafo Suleiman Said akipokea zawadi ya mafuta ya alizeti kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Deogratius Ndejembi

Naibu waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI Jafo Suleiman Said akiwa katika pichaya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya ikungi na Kongwa pamoja na watendaji Mfuko wa LAPF .

Naibu waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI Jafo Suleiman Said akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu mara baada ya kuwasili katika uwanja wa maonesho ya nane nane Nzuguni mjini Dododma

Naibu waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI Jafo Suleiman Said akisikiliza kwa makini maelezo ya kilimo cha mbogamboga yanayofanywa na Jeshi la kujenga Taifa JKT

Naibu waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI Jafo Suleiman Said akiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama mara baada ya kutembelea banda la Halmashauri hiyo

Naibu waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI Jafo Suleiman Said akisikiliza kwa makini maelezo ya awali kutoka kwa Mwenyeji wake katika Maonesho hayo ambaye ni mkuu wa Wilaya ya ikungi Miraji Jumanne Mtaturu

Naibu waziri TAMISEMI Jafo Suleiman Said akisaini kitabu cha wageni katika banda la Mwanzo Bora Nutrition Program
Na Mathias Canal, Dodoma
Watanzania wametakiwa kuthamini na kununua bidhaa zinazozalishwa nchini Tanzania hususani katika sekta ya Kilimo, Ufugaji na uvuvi kwani hakuna sababu ya kuagiza bidhaa kutoka nje ya nchi ilihali bidhaa hizo wanazoagiza zinazalishwa na watanzania wenzao.
Naibu waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI Jafo Suleiman Said ameyasema hayo mara baada ya kutembelea baadhi ya mabanda katika maonyesho ya wakulima Nane nane Kanda ya kati Dodoma yanayofanyika katika uwanja wa Nzuguni huku kauli mbiu ya mwaka huu ikiwa ni "Kilimo, Mifugo na Uvuvi ni nguzo ya maendeleo, Kijana shiriki kikamilifu (Hapa Kazi Tu).
Jaffo amesema kuwa asilimia kubwa ya watanzania wamekuwa watumwa wa mambo ya kigeni, kuiga tamaduni mbalimbali ikiwemo matumizi ya bidhaa zinazotoka nje ya nchi wakati pia bidhaa hizo zinazalishwa nchini, huku akitolea mfano wa manunuzi ya viatu kutoka nchi mbalimbali wakati hapa nchini Jeshi la Magereza linatengeneza viatu bora vya ngozi tena kwa bei nafuu.
Sambamba na hayo pia Naibu Waziri huyo ameiagiza Mamlaka ya Ustawishaji Makao makuu Dodoma kusimamia vyema na kwenda na kasi kubwa katika utengenezaji wa stendi kubwa na ya kisasa ili kufanana na mji wa Dodoma ambapo pia hivi karibuni makao makuu ya serikali yatahamia mjini hapo.
Aidha ameongeza kuwa Maonesho hayo ya
napaswa kuboreshwa ili maonyesho yajayo yawe ya kitaifa ambapo nchi mbalimbali zitapata fursa ya kutembelea na kuifanya Tanzania kujikomboa katika wimbi la umasikini.
Maonesho hayo yanahusisha Shughuli za wakulima, wafugaji wa mifugo, wafugaji wa nyuki, wavuvi, wana mazingira, wasindikaji wa bidhaa za mazao ya kilimo na mifugo, wizara taasisi/Makampuni ya umma, makampuni Binafsi, mabenki, taasisi za umma na za binafsi na mashirika yasiyo ya kiserikali.
Akitoa salamu za shukrani kwa niaba ya waandaaji wa Maonesho hayo Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Miraji Jumanne Mtaturu amesema kuwa maandalizi ya maonyesho hayo yametumia muda mfupi lakini kwa kiasi kikubwa yamekuwa bora na kuahidi kuwa na Maonesho yajayo kuwa bora zaidi katika kipindi kinachokuja.
Mtaturu amesema kuwa lengo mahususi la maonesho hayo ni utoaji wa elimu ya matumizi ya teknolojia mbalimbali kwa wadau wengi kwa muda mfupi ambapo watajifunza kwa njia ya kuona, kujadiliana na kuulizana maswali.
Ameongeza kuwa maeneo makuu ya mafunzo ni teknolojia za uzalishaji wenye tija wa mazao, mifugo na usindikaji wa bidhaa ili kuongeza thamani.
Dc Mtaturu amesema kuwa pia wadau watajionea na kujifunza huduma zitolewazo na serikali, Mashirika ya umma na binafsi, ambapo wafanya biashara wanayatumia maonesho hayo kwa kuuza bidhaa, kufahamiana na kuingia makubaliano.
Kwa upande wake Katibu wa maandalizi ya Maonesho hayo Aziza Rajabu Mumba amesema kuwa Wanatarajia kila mwananchi atakayetembelea maonesho hayo kwenda kutekeleza kwa vitendo anayojifunza katika eneo lake na kuwafundisha wengine ambao hawakupata fursa ya kuhudhuria kwenye Maonesho hayo.
Watanzania wametakiwa kuthamini na kununua bidhaa zinazozalishwa nchini Tanzania hususani katika sekta ya Kilimo, Ufugaji na uvuvi kwani hakuna sababu ya kuagiza bidhaa kutoka nje ya nchi ilihali bidhaa hizo wanazoagiza zinazalishwa na watanzania wenzao.
Naibu waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI Jafo Suleiman Said ameyasema hayo mara baada ya kutembelea baadhi ya mabanda katika maonyesho ya wakulima Nane nane Kanda ya kati Dodoma yanayofanyika katika uwanja wa Nzuguni huku kauli mbiu ya mwaka huu ikiwa ni "Kilimo, Mifugo na Uvuvi ni nguzo ya maendeleo, Kijana shiriki kikamilifu (Hapa Kazi Tu).
Jaffo amesema kuwa asilimia kubwa ya watanzania wamekuwa watumwa wa mambo ya kigeni, kuiga tamaduni mbalimbali ikiwemo matumizi ya bidhaa zinazotoka nje ya nchi wakati pia bidhaa hizo zinazalishwa nchini, huku akitolea mfano wa manunuzi ya viatu kutoka nchi mbalimbali wakati hapa nchini Jeshi la Magereza linatengeneza viatu bora vya ngozi tena kwa bei nafuu.
Sambamba na hayo pia Naibu Waziri huyo ameiagiza Mamlaka ya Ustawishaji Makao makuu Dodoma kusimamia vyema na kwenda na kasi kubwa katika utengenezaji wa stendi kubwa na ya kisasa ili kufanana na mji wa Dodoma ambapo pia hivi karibuni makao makuu ya serikali yatahamia mjini hapo.
Aidha ameongeza kuwa Maonesho hayo ya
napaswa kuboreshwa ili maonyesho yajayo yawe ya kitaifa ambapo nchi mbalimbali zitapata fursa ya kutembelea na kuifanya Tanzania kujikomboa katika wimbi la umasikini.
Maonesho hayo yanahusisha Shughuli za wakulima, wafugaji wa mifugo, wafugaji wa nyuki, wavuvi, wana mazingira, wasindikaji wa bidhaa za mazao ya kilimo na mifugo, wizara taasisi/Makampuni ya umma, makampuni Binafsi, mabenki, taasisi za umma na za binafsi na mashirika yasiyo ya kiserikali.
Akitoa salamu za shukrani kwa niaba ya waandaaji wa Maonesho hayo Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Miraji Jumanne Mtaturu amesema kuwa maandalizi ya maonyesho hayo yametumia muda mfupi lakini kwa kiasi kikubwa yamekuwa bora na kuahidi kuwa na Maonesho yajayo kuwa bora zaidi katika kipindi kinachokuja.
Mtaturu amesema kuwa lengo mahususi la maonesho hayo ni utoaji wa elimu ya matumizi ya teknolojia mbalimbali kwa wadau wengi kwa muda mfupi ambapo watajifunza kwa njia ya kuona, kujadiliana na kuulizana maswali.
Ameongeza kuwa maeneo makuu ya mafunzo ni teknolojia za uzalishaji wenye tija wa mazao, mifugo na usindikaji wa bidhaa ili kuongeza thamani.
Dc Mtaturu amesema kuwa pia wadau watajionea na kujifunza huduma zitolewazo na serikali, Mashirika ya umma na binafsi, ambapo wafanya biashara wanayatumia maonesho hayo kwa kuuza bidhaa, kufahamiana na kuingia makubaliano.
Kwa upande wake Katibu wa maandalizi ya Maonesho hayo Aziza Rajabu Mumba amesema kuwa Wanatarajia kila mwananchi atakayetembelea maonesho hayo kwenda kutekeleza kwa vitendo anayojifunza katika eneo lake na kuwafundisha wengine ambao hawakupata fursa ya kuhudhuria kwenye Maonesho hayo.
Aidha amesema Malengo ya muda mrefu ni kuendeleza uwanja wa Nzuguni ufikie ubora na hadhi ya viwanja vya maonesho ya Kilimo Kimataifa na kuendelea kushawishi wadau mbalimbali kuwekeza ili kuufanya uwanja wa Nzuguni uwe kituo cha huduma cha Maonesho ya Kilimo nchini kama ilivyo kwa uwanja wa Mwalimu Nyerere Dar es salaam kwa maonesho ya Biashara.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (Kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Brazil nchini Tanzania, Carlos Alfonso Puente, wakati Balozi huyo alipomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Balozi wa Brazil nchini Tanzania, Carlos Alfonso Puente (Kushoto), akisaini Kitabu cha Wageni ofisini kwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (Kulia), alipomtembelea Waziri na kufanya naye mazungumzo kuhusu ushirikiano baina ya nchi hizo mbili hususan katika uwekezaji kwenye sekta ya nishati.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (Kushoto), akimsikiliza kwa makini Balozi wa Brazil nchini Tanzania, Carlos Alfonso Puente (Kulia), wakati Balozi huyo alipomtembelea Waziri Ofisini kwake jijini Dar es Salaam hivi karibuni na kufanya mazungumzo naye kuhusu masuala ya uwekezaji katika sekta za nishati na madini. Wengine pichani ni Maafisa wa Wizara waliohudhuria mkutano huo.
Na Veronica Simba
Serikali ya Brazil imeonesha nia kuwekeza katika sekta ya nishati nchini hususan katika kuzalisha umeme kwa kutumia maji na mabaki ya miwa.
Hayo yameelezwa jana jijini Dar es Salaam na Balozi wa Brazil nchini Tanzania, Carlos Alfonso Puente, alipomtembelea Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo ofisini kwake na kufanya mazungumzo naye.
Balozi Puente alimweleza Profesa Muhongo kuwa nchi yake inao ujuzi na uzoefu wa kutosha katika uzalishaji wa umeme kwa kutumia vyanzo mbalimbali hususan maji.
Alisema, Brazil ingependa kuchangia kufanikisha azma ya Rais John Magufuli kuifanya Tanzania kuwa nchi ya Viwanda.
“Kutekeleza mchakato wa kuifanya nchi kuwa ya Viwanda, unahitaji umeme mwingi unaotokana na vyanzo mbalimbali. Ni bahati nzuri kwamba Tanzania inazo njia za kufanikisha azma hiyo,” alisema.
Alisema kuwa, nchini Brazil, kuna Kampuni kubwa zenye uzoefu wa muda mrefu unaofikia miaka 20 hadi 40 katika kazi hiyo, ambazo huzalisha umeme wa maji nchini mwao na hata nje ya nchi.
Pia, alitaja eneo jingine ambalo nchi yake ina nia ya kuwekeza kuwa ni uzalishaji wa umeme unaotumia mabaki ya miwa ambayo aliielezea kuwa chanzo kizuri cha nishati safi.
Balozi Puente alisisitiza kuwa, Brazil ikiwa ni nchi inayozalisha miwa kwa kiwango kikubwa duniani, itasaidia kuleta mabadiliko katika sekta ya nishati kwa kuzalisha umeme unaotokana na mabaki ya miwa kwa kutumia teknolojia za kisasa.
Kwa upande wake, Waziri Muhongo, akimjibu Balozi Puente, alikiri kuwa kuwa Brazil ina ujuzi, uzoefu na uwezo mkubwa hususan katika maeneo ambayo Balozi aliyataja na hivyo akamwambia nchi hiyo inakaribishwa kuwekeza Tanzania kwa kufuata masharti na utaratibu uliowekwa na Serikali.
Akizungumzia zaidi kuhusu utaratibu wa uwekezaji, Waziri Muhongo alieleza kwamba Serikali ya Tanzania, kupitia Wizara yake, inabadilisha utaratibu wa kupokea wawekezaji katika sekta husika.
Alisema, kunaandaliwa utaratibu maalum utakaokuwa wa wazi na kuruhusu ushindani kwa wenye nia ya kuwekeza kwa malengo ya kupunguza au kuondoa kabisa mazingira ya rushwa na muda mrefu unaotumika katika majadiliano pasipo sababu za msingi.
Profesa Muhongo alifafanua zaidi kwamba, Serikali itaweka mazingira mazuri zaidi ya ushindani kwa kuandaa maelezo ambayo pamoja na mambo mengine yatabainisha aina mbalimbali za vyanzo vya umeme vilivyopo nchini pamoja na maeneo vilipo.
Alisema, Kampuni zenye nia ya kuwekeza zitakaribishwa kupendekeza viwango vya bei vitakavyotumika kuuza umeme utakaozalishwa na zitashindanishwa, ambapo washindi wachache watachaguliwa kwa ajili ya majadiliano kabla ya kuingia mkataba wa uwekezaji husika.
“Kwa hivyo, tunaandaa kabrasha maalum litakalokuwa na maelezo husika na litakuwa tayari mwezi wa Septemba mwaka huu. Kabrasha hilo lenye maelezo litatumika kama mwongozo wa ushindanishaji maombi mbalimbali ya uwekezaji hususan katika kuzalisha umeme kwa kutumia vyanzo mbalimbali kwa uwazi,” alisisitiza.
Alivitaja vyanzo hivyo kuwa ni pamoja na gesi asilia, makaa ya mawe, maji, jua, upepo, jotoardhi, mawimbi ya bahari pamoja na nishati mbadala.
Waziri Muhongo alisema kuwa maelezo hayo maalum yatasambazwa kwa wadau mbalimbali wa sekta husika wakiwemo wale wote wenye nia ya kuwekeza ikiwa ni pamoja nan chi ya Brazil kupitia Ubalozi wake hapa nchini.
“Kwa kutumia Kabrasha hilo maalum lenye maelezo husika, wewe Balozi utaweza kuwashawishi wafanyabiashara kutoka nchini kwako kutoa mapendekezo ya uwekezaji ambayo yana vigezo vyote muhimu vinavyoshawishi wapate fursa husika za uwekezaji katika sekta ya nishati,” Profesa Muhongo alimweleza Balozi Puente.
Kuhusu Mradi mkubwa wa ujenzi wa Bomba la kusafirisha mafuta kutoka Uganda hadi Tanzania, ambao pia Brazil imeonesha nia kuwa ingependa kuwekeza kwa kushirikiana na Tanzania; Profesa Muhongo alisema Serikali itaweza kulisemea hilo baada ya kipindi cha miezi takribani 45 kupita, ambapo mambo yote ya kisheria kuhusu Mradi huo yanatarajiwa kuwa yamekamilika.
Aidha, Profesa Muhongo alitumia fursa hiyo kuomba nafasi za masomo nchini Brazil kwa wanafunzi wa kitanzania katika ngazi za Shahada za Uzamili na Uzamivu katika sekta ya Nishati hususan Mafuta na Gesi, kwa kuzingatia kuwa Brazil imeendelea sana katika sekta hiyo.
“Ninyi mnazo Taasisi bora kabisa za Utafiti duniani. Mnafanya vizuri sana katika maeneo mbalimbali.”
Kwa mujibu wa Profesa Muhongo, Brazil ni miongoni mwa nchi Tano (5) bora duniani zinazozalisha umeme kwa kutumia nishati jadidifu kwa sababu umeme mwingi wanaozalisha unatokana na maji, kutoka katika Mito mikubwa waliyonayo.
0 |
|
0 |
|

Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ambae pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na askari wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani(hawapo pichani) wakati wa mkutano na askari hao wakiwa ni wadau muhimu katika Mkakati wa Baraza wa kukabiliana na ajali za barabarani nchini, uliozinduliwa hivi karibuni na Baraza la Taifa la Usalama Barabarani. Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa Polisi Oysterbay, jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamanda Mohamed Mpinga, ambaye pia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, akizungumza na askari wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani(hawapo pichani) wakati wa mkutano na askari hao wakiwa ni wadau muhimu katika Mkakati wa Baraza wa kukabiliana na ajali za barabarani nchini, uliozinduliwa hivi karibuni na Baraza la Taifa la Usalama Barabarani. Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa Polisi Oysterbay, jijini Dar es Salaam.Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa Polisi Oysterbay, jijini Dar es Salaam.

Askari wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, akiuliza swali wakati wa mkutano ambao mgeni Rasmi alikuwa Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ambae pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni(hayupo pichani) .Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa Polisi Oysterbay, jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ambae pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni (katikati), akieleka ukumbi wa mkutano wakati wa kikao alichofanya na askari wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani.Kushoto ni Naibu Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi, Abdulrahman Kaniki na kulia ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamanda Mohamed Mpinga. Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa Polisi Oysterbay, jijini Dar es Salaam. Askari Polisi hao ni wadau muhimu katika kufanikisha Mkakati wa Baraza wa kukabiliana na ajali za barabarani nchini uliozinduliwa hivi karibuni na Baraza la Taifa la Usalama Barabarani

Askari wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, wakimsikiliza Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ambae pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni(hayupo pichani) wakiwa ni wadau muhimu katika Mkakati wa Baraza wa kukabiliana na ajali za barabarani nchini, uliozinduliwa hivi karibuni na Baraza la Taifa la Usalama Barabarani. Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa Polisi Oysterbay, jijini Dar es Salaam. (Picha Zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).

Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ambae pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni (katikati), akiwa amesimama wakati askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani(hwapo pichani), wakiimba wimbo wa maadili wa Jeshi la Polisi. Kushoto ni Naibu Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi, Abdulrahman Kaniki na kulia ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamanda Mohamed Mpinga. Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa Polisi Oysterbay, jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, ambae pia ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Edwin Ngonyani, akizungumza na askari wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani(hawapo pichani) wakati wa mkutano na askari hao wakiwa ni wadau muhimu katika Mkakati wa Baraza wa kukabiliana na ajali za barabarani nchini, uliozinduliwa hivi karibuni na Baraza la Taifa la Usalama Barabarani. Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa Polisi Oysterbay, jijini Dar es Salaam.Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa Polisi Oysterbay, jijini Dar es Salaam.
IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
0 |
|
0 |
|

Viongozi wa UVCCM mkoa wa Arusha wakiwa wanatembelea shule ya Sekondari ya Nanja ilioungua na moto Julai 2 mwaka huu

mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Arusha Sabaya Lengai wa pili kushoto akiwa anaangalia bweni la shule ya Nanja lililoungua na moto


Mwenyekiti wa UVCCM Arusha akiwa na wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Nanja ilioungua na moto hivi karibuni wakati alipoenda kutembelea shule hiyo na kutoa mifuko 100 ya simenti kwa ajili ya ujenzi wa bweni la shule hiyo lililoungua na moto




Na Woinde Shizza,Arusha
Umoja wa vijana Wa chama cha mapinduzi Mkoa wa Arusha wamehaidi mifuko 100 ya simenti kwa ajili ya ujenzi wa shule ya sekondari Nanja iliopo wilayani Monduli mkoani Arusha iliyounguliwa bweni na moto mapema july 2 mwaka huu
Akiongea na wanafunzi wa shule hiyo mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Arusha Sabaya Lengai alisema kuwa wao kama vijana wa ccm mkoani hapa wameguswa sana na tukio hilo ndio maana wakaamua kujikusanya na kwenda kutembelea shule hiyo pamoja na kuwapa mifuko 100 ya simenti kwa ajili ya ujenzi wa bweni ambalo limeungua.
Alisema kuwa wao kama vijana wanamoyo na wananguvu hivyo wako tayari kuwasaidia wadogo zao ambao wapo mashuleni na ndio maana wameamua kutoa mifuko hiyo.
"unajua atuna ela nyingi lakini tumeamua kuwapa msaada hawa wadogo zetu ili wasome kwa raha na wasiwe na mawazo kabisa kuhusia na tatizolililo wakuta na ndio maana wameamua kuwapa msaada huo"alisema Sabaya
Alisema kuwa mchawi hatoki mbali ivyo ni wajibu wa kila mwanafunzi kufanya uchunguzi na iwapo ata jua nani alisababisha bweni hilo likaungua watoe taarifa katika ngazi usika.
Aliwatoa hofu wanafunzi hao kwa kuwasihi wasiwe na wasiwasi wa kuishi shuleni hapo kwani serekali ya chama cha mapinduzi chini ya Rais wake John Magufuli ipo makini katika swala zima la ulinzi na imeimarisha ulinzi shuleni hapo hivyo wasome wakiwa na amani kabisa wakijua kuwa kunawatu wanawalainda.
Kwa upande wake katibu wa UVCCM wilaya ya Arusha Ezekiel Molel aliwasihi wanafunzi hao kuzingatia masomo kwani amna urithi wowote wanaoweza kupewa na walimu wao zaidi ya elimu
Aliongeza kuha haya yanayotokea ni matatizo ya kawaida ivyo wasiyaweke akilini bali waangalie swala la kusoma na fate sana elimu maana bila elimu amna kitu chochote ambacho wanawezakukipata katika miaka hii .
"serekali ya sasa hivi aina mambo ya kona kona hivyo wadogo zangu naomba niwasihi msome sana mzingatie elimu maana bila elimu hamna kitu chochote kinachoweza kufanyika kwanielimu ni kila kitu kwa kipindi hata mnavyotuona sisi hapa sisi wenyewe tumesoma na tunakazi na ndio maana leo hii tumeweza kuja kuwapa pole na kuchangia hiyo mifuko 100 tungekuwa atuna elimu hata kuja hapa au kufanya hizi kazi tusingeweza "alisema Molell
Aliwaambia kuwa ata vitabu vya dini vimeaandika waishikilie sana elimu na wasiiacha iende zake hivyo ni wajibu wao kuweka akili zao katika swala zima la elimu na sio kungine ,aliongeza kuwa sasa ivi kuna gonjwa hatari la ukimwi hivyo ni wajibu wao wanafunzi ambao ni taifa la kesho kuhakikisha wanaepuka vishawishi mbalimbali ambavyo vinaweza jitokeza
Star wa Airtel Trace Music 2015, Mayunga Andrew Nalimi-MAYUNGA, akizungumza na #BMG kuhusiana na project yake ambayo anaifanya na star M-Rap.
Na George Binagi-GB Pazzo
Project inaitwa Across Lovers and Friend Music Tour ambayo Mayunga anaitumia kukutana na mashabiki zake na kuwapa burudani ikizingatiwa tangu atoke Marekani hakuwahi kufanya tour kama hiyo kwa ajili ya mashabiki zake.
Mayunga amesema Project hiyo imeanzia Mwanza na itaendelea katika mikoa mingine na hata nje ya nchi kama vile Kenya, Uganda, Malawi na Afrika Kusini.Usiku huu anapiga show Jembe Beach Jijini Mwanza.
Awali Mayunga pamoja na M-Rap kwa kushirikiana na Star Foundation na Kwanza Online na timu nzima ya Trace Music, waliweza kukutana na vijana Jijini Mwanza kwa ajili ya kuzungumza nao kuwahamasisha kutumia vipaji vyao ili kujikwamua kimaisha.
Mayunga akizungumza na BMG
Stella Mutta ambaye ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Star Foundation ya Jijini Mwanza, akizungumza na BMG
Petro Malongo ambaye ni mmoja wa Vijana waliohudhuria Inspiration Event ya hii leo
Mkurugenzi wa Star Foundation akizungumza na Vijana Jijini Mwanza
Mmoja wa viongozi wa Star Foundation akizungumza na Vijana Jijini Mwanza
Baadhi ya Viajana Jijini Mwanza waliohudhuria event hiyo
Mkurugenzi wa Star Foundation
Mayunga (Kushoto) na M-Rap (Kulia)
Vijana katika picha ya pamoja
Picha ya pamoja
GB (L) with Mayunga (R).
Bonyeza HAPA Kusikiliza Mahojiano. Au bonyeza Play hapo chini
Soma zaidi Hapa
Katikati ni Mgeni rasmi mkuu wa Wilaya ya Arusha Mjini Mh.Mrisho Gambo ambaye alikuwa akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mh.Daudi Ntibenda, akipongezana na Mkurugenzi wa Masoko BRITAM Kenya huku miale ya baruti ikihanikiza ishara ya uzinduzi wa shughuli zitakazokuwa zikifanywa na BRITAM katika jiji la Arusha wakati wa hafla hiyo katika hoteli ya Mount Meru
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mjini Mh.Mrisho Gambo akihutubia wageni katika hafla hiyo
Kulia ni Mgeni rasmi mkuu wa Wilaya ya Arusha Mjini Mh.Mrisho Gambo ambaye alikuwa akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mh.Daudi Ntibenda, akifungua pazia ishara ya uzinduzi wa shughuli zitakazokuwa zikifanywa na BRITAM katika jiji la Arusha wakati wa hafla hiyo katika hoteli ya Mount Meru
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mjini Mh.Mrisho Gambo akipeana mikono na Mwenyekiti wa Bodi BRITAM Tanzania Bw.Michael Laizer ishara ya pongezi mara baada ya ufunguzi
Mkurugenzi mtendaji BRITAM Tanzania Bw.Stephen Lokonyo akitoa historia ya utendaji wa kampuni kuhusu kampuni yao wakati wa hafla hiyo katika hoteli ya Mount Meru (picha zote na Dickson Mulashani)
Mgeni rasmi mkuu wa Wilaya ya Arusha Mjini Mh.Mrisho Gambo ambaye alikuwa akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mh.Daudi Ntibenda, akiefuatilia shughuli zilizokuwa zikiendelea wakati wa hafla hiyo katika hoteli ya Mount Meru
Kutoka kulia ni Afisa Mkuu wa Uendeshaji BRITAM Bw.Sodson Manatsa akiwa na Meneja Masoko BRITAM Tanzania Bw.Godfrey Mzee wakifuatilia kwa makini hafla hiyo
Meza Kuu ambapo wageni rasmi waliketi katika hafla hiyo
Meneja BRITAM Tanzania tawi la Arusha Bi. Loisi Yatera akizungumza wakati wa ufunguzi wa hafla hiyo
Kutoka kushoto ni Mbunge wa zamani wa jimbo la Arusha Mjini Mh.Felix Mrema, katikati ni Mkurugenzi wa Masoko BRITAM Kenya na mwisho ni Mkurugenzi BRITAM Kenya Bw.Stephen Wandera
Meneja BRITAM Tanzania tawi la Arusha Bi. Loisi Yatera akiwatambulisha baadhi ya watendaji wa Kampuni hiyo mbele ya wageni waliohudhuria katika hafla hiyo
Sehemu ya wageni waliohudhuria hafla hiyo katika hoteli ya Mount Meru
Mbunge wa Arusha Mjini Mh.Godbless Lema pamoja na mke wake wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri katika hafla hiyo ndani ya Hoteli ya Mount Meru jijini Arusha
Mkurugenzi BRITAM Kenya Bw.Stephen Wandera akimsikiliza kwa makini mgeni rasmi wakati akihutubia wageni katika hafla hiyo
Habari na Woinde Shizza,Arusha.
Kampuni ya Bima ya Britam imeadhimisha miaka 50 ya kutoa huduma za bima nchini Tanzania huku ikiongoza katika utoaji wa huduma bora za bima za magari,nyumba ,mali pamoja na afya.
Sherehe za Maadhimisho hayo zimefanyika katika Hotel ya Mount Meru iliyoko jijini Arusha na kuudhuriwa na Viongozi wa kiserikali pamoja na Wadau wa Bima.Afisa Mkuu wa Kampuni hiyo nchini Tanzania Stephen Lokonyo amesema kuwa kampuni hiyo imejipanga vizuri kuwahudumia watanzania na kuwafikia watu wengi zaidi ili waweze kunufaika na huduma za bima .
Aliongeza kuwa wao kama kampuni ya bima ya Britam wamejipanga kuwasaidia wananchi mbalimbali wakiwemo wa juu pamoja na wachini kwakuanzisha bima za aina mbalimbali ikiwemo ya mali zao kama nyumba ,bima za afya pamoja bima ya kilimo kwa ajili ya wakulima pamoja na wafugaji.
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mrisho Gambo aliwataka mashirika ya bima kuwafikiria pia madereva bodaboda kwa kuwaanzishia bima za afya pamoja na bima za vyombo vyao ili pale wanapopata matatizo kama ya kuunguliwa na piki piki zao pamoja na kupata ajali waweze kusaidika kwa uraisi matibabu na kufidiwa pindi wanapopata ajali.
Alisema kuwa kumekuwa na pikipiki nyingi sana hivyo iwapo wataanzisha bima kwa ajili ya pikipiki wataweza kuwasaidia sana vijana pia wataweza kupata wateja wengi waotumia vyombo hivi.
Aidha mkuu huyo wa wilaya alihiasa kampuni ya bima ya Britam pamoja na kampuni zingine za bima kujikita zaidi kwa watu wenye kipato cha chini.

Mmoja wa wananchi waliotembelea maonesho ya Kilimo na Mifugo ya Nanenane Kanda ya Kaskazini yanayofanyika kwenye uwanja wa Taso Themi akipata maelezo kwenye banda la kampuni ya Simba Cement

Meneja Mauzo wa Simba Cement mkoa wa Arusha,Christopher Mgonja(kulia)akimkabidhi mmoja wa wananchi waliotembelea banda hilo,Thomas Mollel kofia na tisheti .

Bwana Shamba wa kampuni ya mbegu ya Seed Co,Lukinga Miho akizungumzia kampuni hiyo kuanza kuzalisha mbegu za mbogamboga ambazo zina soko kubwa ndani na nje ya nchi.

Wananchi wakipata maelezo ya kilimo cha Mbogamboga na Matunda kwenye banda la taasisi ya TAHA inayojihusisha na kuhamasisha wakulima kuzalisha kwa wingi kwaajili ya soko la ndani na masoko ya Ulaya .

Wananchi wakipata elimu ya kilimo kwenye uwanja wa maonesho ya Wakuma na wafugaji Kanda ya Kaskazini uwanja Taso, Themi mkoani Arusha.

Wajasiriamali hawakua nyuma kwenye banda la Halmashauri ya Jiji la Arusha kuonyesha bidhaa zao kwa wananchi waliotembelea maonesho ya mwaka huu.

Wanafunzi nao ni sehemu ya wananchi wanaotembelea maonesho ya Wakulima na Wafugaji ya Nanenane pamoja na mambo mengine hujifunza mambo mengi yanaendana na masomo yao kwa vitendo.

Maafisa wa Benki ya NMB mjini Arusha wakitoa huduma kwa wananchi wanaofika kwenye banda lao.
Mkurugenzi Mstaafu wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Said Msambachi na Mama Msambachi wakikata Keki ya kuagwa waliyoandaliwa na watumishi wa Wizara hiyo.
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi (kushoto) akizungumza katika hafla fupi iliyoandaliwa na watumishi wa Wizara hiyo kumuaga aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Utumishi, Said Msambachi (kulia) aliyestaafu rasmi kwa mujibu wa sheria tarehe 16 Juni, 2016. Hafla hiyo ilifanyika juzi tarehe 05 Agosti, 2016 katika ukumbi wa mikutano wa Selous, Makao Makuu wa Wizara hiyo, Jengo la Mpingo, jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mstaafu wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Said Msambachi (kulia) akitoa nasaha zake kwa watumishi wa Wizara hiyo katika hafla fupi ya kumuaga iliyoandaliwa na watumishi hao tarehe 05 Agosti, 2016. Aliwaasa watumishi hao kutekeleza majukumu yao kwa kufanya kazi kwa bidii, uadilifu na uaminifu kama chachu ya maendeleo yao kazini. Aliwataka pia kufanya kazi kwa ushirikiano kujiepusha na majungu, vitendo vya rushwa na ubaguzi pahala pa kazi. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Maj. Gen. Gaudence Milanzi.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Utumishi, Ziana Mlawa (kushoto) akitoa shukurani kwa niaba ya watumishi wote kwa ushirikiano walioupata kutoka kwa Bw. Said Msambachi (kulia) katika kipindi chote cha miaka mitano alichofanya kazi katika Wizara hiyo.
Mkurugenzi Msaidizi wa Rasilimali Watu, Idara ya Utawala na Utumishi, Aurelia Matagi, akitoa ufafanuzi wa ratiba na kuongoza utambulisho katika hafla hiyo.
Baadhi ya watumishi wa Wizara hiyo katika hafla hiyo.
Baadhi ya watumishi wa Wizara walioshiriki hafla hiyo.
Baadhi ya watumishi wa Wizara katika hafla hiyo.
Sehemu ya watumishi katika hafla hiyo.
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi (kushoto) akizungumza na watumishi walihudhuria hafla hiyo.
Picha ya pamoja kati ya Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi (wa pili kushoto, msatari wa mbele), Mkurugenzi Mstaafu wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu, Said Msambachi (wa tatu kushoto), Mkurugenzi anayekaimu nafasi yake kwa sasa ambaye pia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala, Ziana Mlawa (kulia), Mkurugenzi Msaidizi wa Rasilimali Watu, Aurelia Matagi na Watumishi wa Wizara walioshiriki hafla hiyo (mstari wa pili na wa tatu nyuma) .
(Picha na Hamza Temba - WMU)
0 |
|
0 |
|
Mkuu wa Majeshi ya Rwanda (CDS) Jenerali Patrick Nyamvumba (Kushoto)akiongea na Waandishi habari Hawapo Pichani katika Ukumbi wa Uwanja wa Amahoro Juu ya maandalizi ya mashindano ya majeshi kwa Nchi za Afrika mashariki yanayotarajia kufungulia Kesho(Leo Jumatatu Agosti 8)Kulia ni Mwenyekiti wa kamati ya Mandalizi Brigedia Jenerali martin Kemwanga wa JWTZ.
Mwenyekiti wa kamati ya Mandalizi ya Mashindano ya 10 ya Majeshi kwa Nchi za Afrika mashariki Brigedia Jenerali Martin Kemwanga wa JWTZ akifafanua jambo Mbele ya Waandishi wa habari (Hawapo Pichani)Mjini Kigali kuhusu Maandalizi ya mashindano hayo kushoto ni Mkuu wa Majeshi wa Rwanda (CDS) Jenerali Patrick Nyamvuba ).
Baadhi ya Viongozi na Wachezaji wa Timu za Jeshi wanaoshikiri Michuano ya Kumi ya Majeshi kwa Nchi za Afrika mashariki yanayotaraji kufunguliwa Kesho (Leo) katika Uwanja Wa Amahoro Mara walipowasili katika Mji wa KigalI Nchini Rwanda .(Picha na Selemani Semunyu).
Na Selemani Semunyu, JWTZ
Timu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzani limewasili Salama katika Mji wa Kigali Nchini Rwanda kuungana na Wanajeshi wa Nchi Za Afrika Masahariki katika Mashindano ya majeshi kwa nchi hizo yanayotajiwa kufunguliwa Rasmi kesho.
Kiongozi wa Msafara wa Timu hiyo Brigedia Jenerali Jairos Mwaseba Alisema muda mfupi baada ya Timu hiyo kuwasili kuwa Timu iko salama na Wameanza mazoezi mepesi kwa Ajili ya Kujiandaa na Michuano hiyo sambamba na kuzoea hali ya hewa.
“Timun yetu iko vizuri kilizhobaki watanzania waendelee kuiombea Timu yetu kwani maombi yao yakichanganyika na jitihada za Timu basi ushindi utapatikana na ni vema Watanzania walioko Rwanda kujitokeza kushangilia Timu zao,Alisema Brigedia Jenerali mwaseba.
Wakati huo huo Mkuu wa majeshi wa Rwanda Jenerali Patrick Nyamvumba akizungumza Na Waandishi wa Habari alisema Maandalizi yote yamekamilika na kinachosubiriwa ni kuanza kwa Michezo hiyo huku Timu zikimalizia hatua za Mwisho za Usajili kwa ajili ya Michuano hiyo
Alisema Wanajeshi 500 kutoka katika Majeshi ya Nchi Nne za Tanzania,Rwanda,Uganda, na Kenya wanatarajiwa kushiriiki katika Mashindano ya Kumi ya Majeshi ya Nchi za Afrika Mashariki huku Burundi ikiwa imeshindwa kushiriki kutokana na hali ilivyo katika Nchi yake.
Jenerali Nyamvumba alisema anamatumani makubwa na mazungumzo yanayoendelea kuhusu Burundi hivyo Matarajio yake yataifikisha Burundi katika Hatua Nzuri na Hivyo kushiriki katika Michezo hiyo ambayo aliita Muhumi kwa Ushirikiano.
“Michezo hii ni Muhimu kwa Ushirikiano wetu kwani hakuna Mshindi mwisho wa mashindano sote tunakuwa washindi kutokan na kufanikisha kuwa pamoja,Urafiki kama kamajeshi yaliyo katika Ukanda wa Afrika Mashariki,” Alisema Jenerali Nyamvumba.
Kwa Upande Wake Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi kutoka Tanzania Brigedia Jenerali Martin Kemwanga amesema kama kamati waliridhia kuwepo kwa Michezo Mitano ambayo ni Mpira wa miguu,Kikapu,Pete,Mikono na Mbio za Nyika.