Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live

WIKEND YA BURUDANI KUTOKA KWA MALIJENDALI WA MUZIKI NCHINI


KUMEKUCHA KWA WALA RUSHWA NA WAUHUJUMU UCHUMI

Serikali yapokea msaada wa Bilioni 142.23 kuinua vituo vya afya Nchini.

$
0
0
Wafanyakazi wa Common Wealth war Graves Commision wakisafisha sanamu la askari liliopo katikati ya mji wa Dar es salaam ili kuwaenzi mashujaa waliopigana vita kuiletea Uhuru nchi yetu.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisabisya akiongea na wadau wa Nchi washiriki kutoka Canada,Uswizi, Denmark na Korea kusini hawapo pichani wakati wa kusaini msaada wa Bilioni 142.23 kwa ajili ya kuinua vituo vya afya nchini.
 Wadau wa Nchi washiriki kutoka Canada,Uswizi, Denmark na Korea kusini wakiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisabisya katikati mara baada ya kusaini msaada wa Bilioni 142.23 kwa ajili ya kuinua vituo vya afya nchini.Picha Na Ally Daud-Maelezo.
 
Na Ally Daud-Maelezo

Serikali chini ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto imepokea msaada wa shilingi bilioni 142.23 kutoka nchi washiriki Canada, Denmark, Uswizi na Korea Kusini ili kusaidia kuinua vituo vya afya nchini.

Akizungumza mara baada ya kusaini msaada huo Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisabisya amesema kuwa msaada huo wataupeleka moja kwa moja katika Zahanati za vijiji,Hospitali za Wilaya na mkoa ikiwa pamoja na vituo vya afya nchi nzima.

“Tumepokea msaada huo kwa furaha kubwa na kuhaidi kupeleka fedha hizo hizo mahali panapohitajika kwa matumizi ya kukuza na kuboresha vituo vya afya katika zahanati na hospitali nchi nzima ili kuokoa maisha ya watanzania” alisema Dkt. Ulisabisya.

Aidha Dkt. Ulisabisya anaishukuru Benki ya Dunia kwa kuimarisha na kusaidia mfuko wa maendeleo ya afya nchini kwa kuwakutanisha na wahisani kutoka nchi mbalimbali.

Mbali na hayo Dkt.Ulisabisya amewaomba Benki ya Dunia na nchi wahisani wasichoke na kushindwa kuisaidia Tanzania katika sekta ya Afya ili kutokomeza maradhi kwa kiwango kikubwa na kupambana kwa ajili ya kukuza uchumi wan chi.
 

WALIMBWENDE 11 KUPANDA JUKWAANI KUWANIA TAJI LA MISS KANDA YA MASHARIKI 2016

$
0
0

WANYANGE 11 watakao panda katika jukwaa la Nashera Hotel mjini Morogoro kesho kuwania taji la Miss Kanda ya Mashariki 2016 wakiwa katika pozi tofauti katika kambi yao mjini Morogoro. Warembo hao ni kutoka mikoa ya Pwani, Lindi, Mtwara na Morogoro.

HABARI NJEMA HII:TRA yavuka lengo la ukusanyaji kodi mwezi Julai

$
0
0

 Na Jacquiline Mrisho - MAELEZO

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imevuka lengo la ukusanyaji wa kodi wajumla ya kiasi cha shilingi trilioni 1 sawa na asilimia 95.6 tofauti na lengo lililokuwa limekusudiwa la kukusanya trilioni 1.1 kwa mwezi Julai 2016.

Kiasi hicho ni sawa na ongezeko la asilimia 15.43 ukilinganisha na makusanyo ya awali ya mwaka 2015 ambapo mamlaka hiyo ilikusanya jumla ya kiasi cha shilingi Bilioni 914.

Takwimu hizo zimetolewa na Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA, Richard Kayombo wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jjijini Dar es Salaam.

“Kwa mwezi Julai mwaka huu makusanyo yameongezeka kwa asilimia 15.43 ukilinganisha na kipindi cha mwezi Julai 2015 ambapo tulikusanya shilingi Bilioni 914” alisema Kayombo.

Aidha aliongeza kuwa mamlaka imeweka mikakati thabiti ya kuhakikisha kuwa inafikia au inavuka lengo la Serikali la kukusanya shilingi trilioni 15.1 kwa mwaka wa fedha 2016/2017 huku mkakati mmoja wapo ukiwa ni kuhakikisha kuwa walipa kodi wapya wanasajiliwa zaidi.

Bw. Kayombo aliongeza kuwa mkakati mwingine ni kuhuisha taarifa za walipa kodi kwa kuhakikisha kwamba namba za utambulisho wa mlipa kodi (TIN) zisizotumika zinafutwa katika mfumo wa TRA.

Pia amefafanua kuwa maandalizi ya kuhuisha taarifa za walipa kodi yapo katika hatua za mwisho ikiwemo upigaji picha,uchukuaji wa alama za vidole pamoja na vielelezo muhimu.

TRA inawakumbusha wananchi kuhakikisha wanakagua tiketi/ risiti zao za manunuzi na kuangalia usahihi wa pesa walizolipa na uhalali wa risiti yenyewe.

KIONGOZI NI KUONESHA MFANO,KAMA HUU WA MBUNGE WA MKURANGA,MH ULEGA.

NYOSHI EL SADAT AHIDI KUWAPAGAWISHA WAKAZI WA JIJI LA ARUSHA ONESHO LA KUMSAKA MISS KANDA YA KASKAZINI KESHO

$
0
0
Na Woinde Shizza ,Arusha.
 
  Rais Wa bendi ya FM Academia Nyoshi El Sadat amewahidi wakazi Wa jiji la Arusha kuwapa burudani ya nguvu katika onyesho la kumsaka Miss Kanda ya kaskazini.

Akiongea na waandishi Wa habari jijini hapa, Mwanamuziki huyo alisema kuwa bendi hiyo imejipanga vya kutosha kuwapa burudana wapenzi na mashabiki wake.Alisema kuwa katika shoo hiyo ya Usiku Wa kumpata mrembo Wa kanda ya kaskazini amekuja na wanamuziki wote pamoja na wacheza show wa bendi ya Fm Academia .

"Tunawapa burudani ya kufa mtu tunamastaili mapya ,pia yule mnenguaji ambae walimmiss kwa muda mrefu Qeen Suzy atakuwepo katika onyesho hilo"alisema Nyoshi .

Naye mwandaaji wa onyesho hilo Faustine Mwandago alisema kuwa katika show hii atahakikisha washabiki wote wanaifurahia show hiyo . Alisema show hiyo itafanyika kesho jumamosi July sita itaanza kuanzia tatu kamili Usiku na kiingilio kawaida itakuwa kawaida 10000 huku V.I.P 30000.

Picha ikionyesha warembo wanaoshiriki shindano la miss kanda ya kaskazini wakiwa wanafanya mazoezi kwa ajili ya shindano linalofanyika jumamosi hii July 6 katika viwanja vya ukumbi Wa triple A .

TUMEKATA RUFAA ILI KUPATA MAAMUZI KUTOKA CHOMBO CHA JUU YATAKAYOKUWA KAMA SHERIA

$
0
0

Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akipokea vitabu na vipeperushi mbalimbali kutoka kwa mjumbe wa Chama cha Wanasheria Wanawake (TAWLA) baada ya kumaliza mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe katika ukumbi wa mikutano wa Wizara jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome akipokea vitabu na vipeperushi mbalimbali kutoka kwa mjumbe wa Chama cha Wanasheria Wanawake (TAWLA) baada ya mkutano na Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe katika ukumbi wa mikutano wa Wizara jijini Dar es salaam.



Mwenyekiti wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) Bi. Anastazia Soka (mwenye miwani) akiongea katika ukumbi wa mikutano ghorofa ya Nane wakati wa mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe jijini Dar es Salaam.



Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria akiongea na wanawake wa Chama cha Wanawake Wanasheria Tanzania (TAWLA) walipomtembelea kubadilishana mawazo mbalimbali kuhusu masuala mbalimbali ya kisheria hasa kwa upande wa Wanawake katika Ukumbi wa mikutano ghorofa ya Nane jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria.


Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Dkt Harrison Mwakyembe amesema Serikali imeamua kukata rufaa Mahakama ya Rufani dhidi ya uamuzi wa Mahakama Kuu uliosema kipengele cha umri wa mtoto wa kike kuolewa kinakiuka Katiba ili kuweza kupata maamuzi ya chombo cha juu cha Mahakama ambayo hayatweza badilishwa na hivyo kuwa kama Sheria .

Amesema sio kama Serikali inapingana na uamuzi wa Mahakama Kuu, ila kinachofanyika ni utaratibu wa kawaida ambao utaiwezesha Serikaki kuwa na maamuzi kutoka katika Chombo cha Juu Kabisa cha Mahakama nchini na hivyo maamuzi hayo hayataweza kutenguliwa na mtu au chombo chochote na kuongeza kuwa ukibaki uamuzi huo pekee inaweza ikatokea siku nyingine Jaji mwingine akatoa maamuzi tofauti na hayo.

“Jamani , nimesikia mengi, Sio kama Serikali inapingana na uamuzi wa Mahakama Kuu, ila kinachofanyika ni sasa ni utaratibu wa kawaida ambao utaiwezesha Serikali kupata maamuzi kutoka katika Chombo cha Juu Kabisa cha Mahakama nchini, maamuzi hayo yakitolewa hakutakuwa na mtu au chombo kingine kitakachokuwa na mamlaka ya kutoa maamuzi mengine juu ya suala hilo alisema na kuongeza kuwa tumefanya hivyo ili Mahakama ya Juu kabisa ithibitishe juu ya suala hilo ili ijulikane moja, alisema Dkt Mwakyembe.

Amewasihi wanasheria wanawake na wanaharakati wengine wanaoshughulikia haki za wanawake na watoto nchini kufahamu kuwa Serikali ina nia njema na inaliona suala la mtoto kuolewa kabla ya kufikisha miaka 18 kama miongoni mwa changamoto nyingi inazozikabiliana nazo na ndio maana hata ikapitisha sheria inayosema atakayemuoa mwanafunzi atachukuliwa hatua kali.

Amesema kitendo cha kuoa watoto wakiwa shuleni au hata chini ya miaka 18 ni cha hatari sana hasa ikizingatiwa kuwa watoto wa kike wanakosa fursa ya kuendelea na masomo ikiwa ni pamoja na kupata madhara mbali mbali ya kiafya.

“Hakuna anepinga tunapishana tu njia za kuhakikisha haki hii ya mtoto wa kike inalindwa, na niwahakikishie hapa kuwa njia hii ya kulipeleka suala hili katika mahakama ya Rufani ni njia bora kabisa kwani maamuzi yake yatasimama na hayatatenguliwa na yeyote” alisema dkt Mwakyembe.

Waziri Dkt Mwakyembe amesema hayo leo jijini Dar es Salaam alipokutana na Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania ( TAWLA) ambao walimtembelea ofisini kwake na kuongelea vitu kadhaa likiwemo suala hilo la serikali kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo.

SHEHENA YA MADAWATI KUTOKA JAMUHURI YA MUUNGANO TANZANIA YAWASILI ZANZIBAR.

$
0
0
 
Wafanyakazi wa bandari ya Zanzibar wakishusha madeski yaliyotolewa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ajili ya wanafunzi wa Zanzibar.
 akamu Mwenyekiti wa Bunge la Tanzania Salim Hassan Turky akimkabidhi sehemu ya madeski hayo Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya kuchangia madeski Zanzibar Haroun Ali Suleiman Bandarini Zanzibar.
 Makamu Mwenyekiti wa Bunge la Tanzania Salim Hassan Turky akizungumza na waandishi wa habari kuhusu madawati hayo wakati wa makabidhiano bandarini Zanzibar.PICHA na Mkame Mshenga -Maelezo Zanzibar.

Na Mwashungi Tahir         Maelezo Zanzibar   5-08-2016.

Jumla ya madawati  5,500 ikiwa ni mgao wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kutoka  Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  yamewasili  Zanzibar  kwa ajili ya matumizi ya wanafunzi wa skuli za Unguja na Pemba.

Akipokea madawati hayo  bandarini  Zanzibar, Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya madawati  Zanzibar  Haroun Ali Suleiman alisema mgao huo utapunguza tatizo kubwa la madawati linalozikabili skuli nyingi hapa nchini.

Alisema kupatikana kwa madawati hayo  kutaleta faraja kwa wanafunzi na kuongeza hamasa na ari katika kujipatia elimu.

“Msaada huu utapunguza usumbufu wa wanafunzi kukaa chini kwa muda mrefu na utaongeza ufanisi kwa walimu na wanafunzi katika kusomesha na kujifunza, “alisema Mwenyekiti huyo.

Nae  Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Riziki  Pembe Juma aliwashukuru Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kusimamia kupatikana madawati hayo na ameeleza matumaini yake ya kupatikana msaada zaidi wa madeski.

 Amewaomba wasamaria wema kujitokeza kuunga mkono juhudi za Serikali katika kukabiliana na tatizo la madawati kwa kutoa michango yao kupitia Kamati ya Taifa ya Madawati ya Zanzibar.  

Aidha  amewaomba walimu wakuu wa skuli zitakazopata madeski hayo kuwapa elimu wanafunzi  jinsi ya kuyatunza  ili yaweze kudumu kwa muda mrefu.

Sambamba na hayo Spika wa Baraza la Wawakilishi  Zuberi Ali Maulid alisema kupatikana kwa madeski hayo  ni faraja  kwa baraza hilo kwani suala hilo linazungumzwa sana na tumeanza kuona mafanikio  yake.

Alisema kupatikana kwa msaada huo ni jambo la kupigiwa mfano kwa wabunge kwani wabunge  waliopita  hawajawahi kufanya jambo kama hilo. 

Makamo Mwenyekiti wa wa Bunge Salim Hassan Turky ambae ni Mbunge wa Jimbo la Mpendae kwa niaba ya wabunge wenziwe amesema  madawati hayo ni mchango   wa bunge  uliotokana na pesa za bajeti zilizobakia katika  bajeti iliyopita.

Jumla ya shilingi billion sita zimetumika kununulia madawati hayo  ambayo ni kila jimbo lilitarajiwa  kupata  madeski 300 na  kwa kuanzia kila jimbo limetapatiwa madeski 100 na mengine yatafuatia baadae.

Aidha amemshukuru Rais  wa Jamhuri ya Muungano Mh. John Pombe Magufuli kwa kutoa wazo la kutumia fedha zilizobaki za bunge  bajeti iliyopita kwa kununulia madeski hayo.

BWENI LA SHULE YA LONGIDO SEKONDARI LIMETEKETEA KWA MOTO USIKU HUU

$
0
0
Picha ya bweni hilo lionekanavyo usiku huu.
 Bweni la shule ya Longido sekondari wilayani Longido mkani Arusha,limeteketea kwa moto usiku huu,kama lionekanavyo pichani,taarifa kamili ya chanzo cha moto huo bado hakijajulikana,hivyo tutazidi waletea taarifa kadiri ya zitakavyokuwa zikipatikana.

RC MAKONDA AKUTANA NA KIKOSI CHA KUTULIZA GHASIA (FFU) UKONGA JIJINI DAR LEO

$
0
0

-Awapongeza kwa Uzalendo wao Kwa Taifa letu .
-Awaahidi kuwapatia Ambulance
-Awataka Waifanye Dar Kama Dubai Kiulinzi.

Mkuu wa Mkoa wa Dar Mh.Paul Makonda Leo amekutana na kikosi cha kutuliza ghasia(FFU)ukonga Jijini Dar na amezungumza mengi moja kubwa nao ni Mhe. Makonda amewaeleza kuwa hakuna wafanyakazi wazalendo kama Askari kwani wao wako tayari kufa ili taifa letu Liwe salama. 

Makonda aliongezea kwakusema uzalendo wao hauko kwenye mshahara bali utaifa kwani hakuna mshahara unaoweza kununua uhai wa mtu.Rc Makonda amewaahidi kuendelea kuwa pamoja nao na kuwaomba wafanye dar iwe kama dubai ambapo mtu anaweza kuacha mzigo wake na kesho akaukuta. Rc.Makonda anaamini dar inapaswa kuwa salama zaidi ili watu wafanye kazi bila hofu na hata majumba yasiwekewe mageti endapo tu usalama utakuwa mkubwa. 

Mwisho Mh.Makonda amewahakikishia askari hao wa FFU ukonga kuwapatia gari la wagonjwa ili liwasaidie askari katika hospitali yao huku akiahidi kufatilia ombi lake alilolitoa siku ya uzinduzi wa huduma ya polisi kwa wananchi pale viwanja vya Biafra mbele ya Mhe Rais Dkt.John Magufuli, ombi la Makonda lilikua juu ya asilimia 20% ya faini zinazotozwa na trafiki zibaki kwa askari ili kuboresha utendaji ikiwa pamoja na ukarabati wa Magari ya askari sambamba na mafuta ili polisi watakapohitajika wawe wanafika bila kuchelewa.
 
 
 
 

Samata A - KODO ( Official HD Video)

JE UNAZIJUA KAZI ZA WANASHERIA WA TAASISI YA MANUNUZI YA UMMA,HIZI HAPA ZISOME.

$
0
0
Jacquiline Mrisho-MAELEZO

MOJA kati ya sekta ambazo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amezizungumza sana katika hotuba zake ni sekta ya Manunuzi ya Umma ambayo ameonesha wasiwasi kuwa sekta hiyo ina mianya inayopoteza fedha za Umma.

Sheria ya Ununuzi wa Umma ya Mwaka 2011 na Kanuni zake imeweka bayana taratibu za kufuata hadi Mkataba kukamilika katika kufanya manunuzi ya Umma.Katika hatua hiyo Mwanasheria Mkuu wa Serikali imepewa nguvu kupitia Kifungu cha 60 cha Sheria hiyo na Kanuni ya 59 ya Kanuni za Ununuzi wa Umma za Mwaka 2013.

Katika kusisitiza hilo, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Benno Sanga anasema kuwa msingi mkubwa wa sheria hiyo ni ushindanishwaji wa wazabuni unaoweza kuiletea Serikali thamani ya fedha.“Kila taasisi ya Serikali lazima ifuate Sheria ya Manunuzi ya Umma kwa manunuzi mbalimbali ya vifaa vya ofisi, sheria hii imeweka utaratibu wa kuhakikisha fedha iliyotumiwa inalingana na huduma inayopatikana”,anasema Sanga.

Hapo awali Kanuni ya 59 ya Kanuni za Ununuzi wa Umma za Mwaka 2013 ilikuwa inaelekeza kwamba mikataba yote ya ununuzi wa umma ambayo thamani yake inafikia shilingi milioni hamsini au zaidi ifanyiwe uhakiki na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kabla ya kusainiwa lakini kwa sasa kanuni hizo zimerekebishwa kupitia Marekebisho ya Kanuni za Ununuzi wa Umma za Mwaka 2016 na sasa mikataba ya ununuzi ambayo inatakiwa kuhakikiwa na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa mujibu wa Kanuni 59(1) ya Kanuni hizo ni ile yenye thamani ya kuanzia shilingi bilioni moja au zaidi na mikataba ya ununuzi inayohusu ushindani wa zabuni ya kimataifa.

Kwa mujibu wa Kanuni ya 59(2) ya Kanuni za Ununuzi wa Umma, mkataba wowote wa aina hiyo ambao haukufanyiwa uhakiki na Mwanasheria Mkuu utakuwa batili.Aidha, Kanuni ya 59(5) inaelekeza kuwa Afisa Masuhuli anapaswa kuhakikisha kuwa ushauri wa kisheria uliotolewa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali wakati akihakiki mkataba husika umezingatiwa ipasavyo na kuingizwa katika rasimu ya mkataba.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju amefafanua kuwa kwa mikataba ambayo iko chini ya thamani ya shilingi bilioni moja inafanyiwa upekuzi na Afisa Sheria wa Taasisi ya Manunuzi husika kama inavyoelezwa katika Kanuni ya 60(1).

”Hata hivyo, kwa mujibu wa Kanuni ya 60(4) ya Kanuni za Ununuzi wa Umma, Taasisi ya Manunuzi haizuiwi kuomba ushauri wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa jambo lolote linalohusu mkataba unaoweza kuhakikiwa na Afisa Sheria (Legal Officer) wa taasisi husika”, anasema Masaju.

Divisheni ya mikataba ni moja ya ofisi zilizoko chini ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali inayojumuisha wanasheria wa taasisi ya manunuzi ya umma ambayo inashughulikia masuala yote ya kuhakiki mikataba kwa makini ili kufahamu kama taratibu za manunuzi zimefuatwa pamoja na kutoa ushauri wa mikataba ya manunuzi ya umma kwa taasisi mbalimbali za Serikali.

Divisheni hiyo ya Mikataba ina jukumu la kutoa ushauri wa kisheria kwa taasisi za Serikali kwa uadilifu na uweledi wa hali ya juu, kushiriki majadiliano kwa nia ya kuingia makubaliano na nchi moja au zaidi ya moja.Pia kushiriki katika kazi mbalimbali za Serikali ambazo zinahitaji muongozo wa kisheria pamoja na upekuzi wa mikataba ihusuyo Serikali ikiwemo ya hati za makubaliano, mikataba ya upangaji, mikopo, madini, mafuta na gesi, ununuzi wa umeme, utekelezaji wa miradi, mikataba itokanayo na zabuni.

Jukumu lingine ni kuangalia ibara mbalimbali za mkataba kama zimewekwa sahihi ili kuondoa uwezekano wa athari hasi kwa Serikali na kujiridhisha kama mikataba husika inakidhi au kuzingatia maslahi ya Umma au Taifa. Hata hivyo, “chochote kizuri huwa hakikosi kasoro”, majukumu hayo yanaingiwa na changamoto nyingi kwa kuwa Divisheni ya Mikataba iko katika Makao Makuu ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali pekee.

Hivyo, mikataba hiyo imekuwa ikipelekwa Dar es Salaam kwa ajili ya kuhakikiwa, hatua ambayo imekuwa ikisababisha wadau wa masuala hayo hasa Halmashauri za Wilaya, Miji, Manispaa, Jiji na wengine walioko mikoani kusafiri na kupeleka mikataba Dar es Salaam kwa ajili ya uhakiki. Mbali na kuongeza gharama kwa halmashauri na wadau wengine, utaratibu huo unaweza kuchelewesha mradi kuanza mapema.

Kutokana na changamoto hiyo, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali inaona umuhimu wa kuwajengea uwezo Mawakili wa Serikali waliopo katika ofisi zao za Mikoani ili baadhi ya Mikataba iwe inahakikiwa na ofisi hizo.

Akifungua semina ya mafunzo ya Mawakili wa Serikali yanayohusu Sheria ya Manunuzi ya Umma, Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju anasema kuwa "Kutokana na changamoto hiyo, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali inaona umuhimu wa kuwajengea uwezo Mawakili wa Serikali wa Ofisi za Mwanasheria Mkuu wa Serikali zilizoko mikoani ili hatimaye baadhi ya mikataba kutoka kwa wadau walioko wilayani na mikoani iwe inapelekwa katika Ofisi za Mwanasheria Mkuu wa Serikali zilizoko mikoani".

Masaju anaongeza kuwa kutokana na kuongezeka kwa thamani ya mikataba inayohakikiwa na Wanasheria wa Taasisi ya Manunuzi ni wazi kwamba wanasheria hao wanatakiwa kujengewa uwezo kuhusu uhakiki wa mikataba kwani iwapo watashindwa kutekeleza wajibu huo ipasavyo watawajibishwa kwa kuchukuliwa hatua stahiki za kinidhamu au kisheria.

Naye Mkurugenzi Msaidizi wa Mikataba (Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali) Bi.Monica Otaru anasema kuwa mafunzo hayo yatawasaidia mawakili kufanya upekuzi wa mikataba kwa makini na uhakika zaidi.“Pamoja na kuwa kazi ya kupekua mikataba ni sehemu ndogo ya kazi zetu lakini inachukua muda mwingi, hivyo mafunzo haya yatawaandaa Mawakili wa Serikali walioko katika Ofisi za Kanda kuweza kufanya upekuzi wa mikataba kwa umakini na uhakika zaidi”,alisema Bi. Otaru.

Ili Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali itekeleze wajibu huo wa kuhakiki mikataba kwa ufanisi ipasavyo, Wizara, Taasisi na Idara za Serikali zinazopeleka Mikataba katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali zinakumbushwa kuzingatia mambo ya msingi.

Mambo hayo ni masharti ya kifungu cha 22 cha Sheria ya Utekelezaji wa Majukumu ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, 2005, Kanuni ya 13(1) ya Kanuni za Utekelezaji wa Majukumu ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya mwaka 2006 inayoelekeza namna ya kupata ushauri katika Ofisi hiyo kwa kuainisha maelezo muhimu kuhusu mkataba husika.Pia kuandika barua ya kuiomba Ofisi kuhakiki mkataba husika ili Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali itoe ushauri wake ikiwa inaelewa vizuri yaliyomo katika mkataba husika.

Wakati wa mafunzo hayo, Wakili wa Serikali Mwandamizi Divisheni ya Mikataba, Said Kalunde anaelezea juu ya mambo muhimu ya kuzingatia katika kufanya upekuzi wa mikataba ya ununuzi ikiwemo ya ujazaji wa fomu mbalimbali zinazotumika katika uhakiki wa mikataba hiyo kwa mujibu wa Sheria ya Manunuzi ya Umma.

“Ni muhimu sana kwa wakili kujiridhisha kama taratibu za ujazaji wa fomu zimefuatwa na fomu zimejazwa kwa usahihi, endapo wakili hatojiridhisha kwa kuhakiki fomu hizo huenda akapatwa na matatizo makubwa ya kiutendaji”,alisema Kalunde.

“Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali inapenda kuzikumbusha Wizara, Idara na Taasisi za Serikali kuzingatia ipasavyo masharti ya kifungu cha 20(1) cha Sheria ya Utekelezaji wa Majukumu ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali cha mwaka 2005 kinachoelezea kuhusu mambo muhimu ya kuzingatia pale wizara na taasisi zinapohitaji huduma za kisheria kutoka nje ya Ofisi ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.”anasema Kalunde.

Anafafanua kuwa kifungu hicho kinaelekeza kuwa," Mkataba wa utoaji huduma ya kisheria kwa Wizara au Taasisi ya Serikali uingiwe baada ya kupata kibali kwa maandishi kutoka kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali".

KAMPUNI YA POWER MACHINES KUTOKA URUSI YAONESHA NIA YA KUWEKEZA KWENYE UZALISHAJI WA UMEME KWA MAKAA YA MAWE

$
0
0

Mkurugenzi wa Masoko kutoka Kampuni ya Power Machines kutoka nchini Urusi (kulia) akielezea uwezo wa kampuni yake katika uwekezaji kwenye miradi ya makaa yam awe. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya Nishati. Dk. Juliana Pallangyo.
Watendaji kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) wakifuatilia mada zilizokuwa zinawasilishwa katika kikao hicho.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya Nishati. Dk. Juliana Pallangyo akifuatilia maelezo yaliyokuwa yanatolewa na Dk. Gachao Kiuna kutoka kampuni ya Aqua Power katika kikao hicho.
Dk. Gachao Kiuna kutoka kampuni ya Aqua Power (kushoto) akifafanua jambo katika kikao hicho. Kulia ni Sergey Livinskg kutoka Kampuni ya Power Machines kutoka nchini Urusi. 



Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya Nishati. Dk. Juliana Pallangyo akielezea fursa za uwekezaji kwenye kikao chake na kampuni ya Power Machines kutoka nchini Urusi. Kikao hicho pia kilishirikisha watendaji kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO)

CHAMA CHA WAFANYAKAZI COTWU (T) KANDA YA DAR ES SALAAM CHAFANYA MKUTANO WAKE MKUU HOTELI YA VILA JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0

Kaimu Mkurugenzi, Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA), Shanes Nungu (katikati), akihutubia wakati akifungua mkutano mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Sekta ya Mawasiliano na Uchukuzi Tanzania COTWU (T), Kanda ya Dar es Salaam leo asubuhi. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Mussa Mwakalinga na Mwenyekiti wa chama hicho Kanda ya Dar es Salaam, George Faustine.
Wanawake waliochaguliwa kushika nafasi mbalimbali katika chama hicho wakiwa katika picha ya pamoja.
Wanawake wajumbe wa chama hicho Kanda ya Dar es Salaam wakiwa katika picha ya pamoja kwenye mkutano huo.
Vigogo wa chama hicho wakiteta jambo kabla ya kuanza kwa mkutano huo. Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa chama hicho Kanda ya Dar es Salaam, George Faustine, Katibu wa chama hicho Kanda ya Dar es Salaam, Elisa Luvigo na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Kanda ya Dar es Salaam, Mussa Mwakalinga.
Wajumbe wakiwa kwenye mkutano huo.
Baadhi ya wajumbe wa Chama cha Wafanyakazi wa Sekta ya Mawasiliano na Uchukuzi Tanzania COTWU (T), Kanda ya Dar es Salaam wakiimba wimbo wa mshikamano katika mkutano mkuu wa chama hicho uliofanyika Dar es Salaam leo asubuhi.
Wajumbe wakionesha mshikamano wao wakati wakiimba wimbo maalumu wa mshikamano.
Katibu wa chama hicho Kanda ya Dar es Salaam, Elisa Luvigo akizungumza katika mkutano huo.
Makatibu wa matawi wa chama hicho wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi Tanzania (CMA), Shanes Nungu (wa tatu kushoto).
Mwenyekiti wa chama hicho Kanda ya Dar es Salaam, George Faustine (kulia), akizungumza wakati akimkaribisha mgeni rasmi.

DC IKUNGI AFUNGUA MAFUNZO YA MGAMBO

$
0
0

Kundi la vijana wa Mgambo kutoka Kijiji cha Ighombwe, Jerumani, na Mahonda wakimsikiliza mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa mafunzo hayo katika Tarafa ya Sepuka .


Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa Wilaya ya ikungi ambaye ni Mkuu wa Wilaya Miraji Jumanne Mtaturu akikagua vijana wa mafunzo ya Mgambo kutoka vijiji vitano vya Dung’unyi, Munkinya, Kipumbuiko, Samaka na Damankiya vinavyounda Kata ya Dung’unyi katika Tarafa ya Ikungi
Kundi la vijana wa Mgambo kutoka Kijiji cha Ighombwe, Jerumani, na Mahonda wakionyesha umahiri wao katika mafunzo waliyoyapata mbele ya mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa mafunzo hayo katika Tarafa ya Sepuka
Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa Wilaya ya ikungi ambaye ni Mkuu wa Wilaya Miraji Jumanne Mtaturu akiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya Ikungi 


Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa Wilaya ya ikungi ambaye ni Mkuu wa Wilaya Miraji Jumanne Mtaturu akijadili jambo na Mshauri wa Mgambo Wilaya ya Ikungi Fortunatus Ndalama
Mkuu wa Wilaya Miraji Jumanne Mtaturua akizungumza na watendaji Kata, na viongozi wa vijiji mara baada ya ufunguzi wa mafunzo ya mgambo yatakayodumu kwa wiki 16.
Na Mathias Canal, Singida

Wiki 16, Miezi minne itatosha kuwakutanisha pamoja vijana wa kata mbalimbali Wilayani Ikungi kwa pamoja wakipatiwa mafunzo ya Mgambo hususani kujifunza uzalendo, Mbinu za medani za kupambana na uhalifu, Kuimarisha nidhamu na kujituma.

Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na Usalama ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu wakati akifungua rasmi mafunzo hayo yatakayojikita pia katika kuimarisha utu na uadilifu.

Mtaturu amesema kuwa vijana wote walioamua kujitolea katika mafunzo hayo kwa ridhaa yao watapaswa kuwekwa katika kumbukumbu ya vijana ambao baada ya kumaliza mafunzo wataanzishiwa vikundi vya ujasiriamali ambavyo vitasimamiwa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya.

"Tanzania ina wimbi la vijana wengi ambao wanajiamulia maisha wenyewe kutokana na wazazi wao kuyakimbia majukumu yao ya kuwalea watoto wao katika maadili mema ya kumjua Mungu na nidhamu kwa kila mtu kwenye jamii hivyo sisi kama serikali ngazi ya Wilaya tutahakikisha Vijana hawa wanaimarika katika maadili mema" Alisema Mtaturu

Dc Mtaturu amesema kuwa mara baada ya kumalizika kwa mafunzo hayo vijana hao watapaswa kuamua wanataka kujishughulisha na nini kati ya ufugaji na kilimo cha kisasa ambapo ofisi ya mkuu wa Wilaya itasimamia kuhakikisha wanafanikiwa katika malengo yao.

Sambamba na hayo amewaeleza vijana hao kuwa serikali ina mamlaka ya kuwasaidia watanzania kujikwamua katika wimbi kubwa la umasikini lakini pia vijana na watanzania kwa ujumla wanapaswa kutumia muda wao mwingi kujishughulisha na shughuli za uzalishaji mali kwa kufanya kazi sio kucheza bao, kujihusisha na vikundi ovu, kunywa pombe, Ngono zembe ama kucheza Pool Table wakati wa kazi.

Dc Mtaturu amewapongeza vijana hao kwa kujitolea kwa moyo mmoja kushiriki katika mafunzo hayo ambapo amesema kuwa mafunzo wanayoyapata sio mateso ila ni sehemu ya kuwaimarisha kimwili na kiakili, Kujifunza maadili mema, ili kuwa na uchungu na nchi yetu.

Mafunzo ya mgambo yaliyofunguliwa na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu yanahusisha Tarafa mbili ya Ikungi na Sepuka ambapo katika Tarafa ya Ikungi vijana wa kiume waliojitokeza ni 138 huku wanawake wakiwa 6.

Kwa upande wa Tarafa ya Sepuka kuna jumla ya vijana 210 ambapo vijana wa kiume ni 206 na wanawake ni wa 4. Katika ufunguzi wa Mafunzo hayo katika Tarafa hizo mbili Mkuu huyo wa Wilaya ya Ikungi aliambatana na Wajumbe wa kamati ya Ulinzi na usalama ya Wilaya.

Dc Mtaturu amesisitiza kuwa mgambo wanajulikana kama jeshi la akiba ambapo wajibu wao Mkubwa ni kushirikiana na jeshi la pol
isi na Jamii katika kuimarisha ulinzi wa watu na Mali zao.


 

DIWANI WA CHADEMA ASWEKWA NDANI KWA KUKIUKA MAAZIMIO YA BARAZA LA MADIWANI WILAYANI IKUNGI

$
0
0




Kutoka Kushoto ni Eng Sadick Chakka Mhandisi wa Maji Wilaya ya Ikungi, Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji jumanne Mtaturu, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Rustika Turuka, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ally J. Mwanga, na Kulia ni Abel Suri Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi.


Na Mathias Canal, Singida

Jeshi la polisi Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida limemtia nguvuni Diwani wa Kata ya Iseke kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Emmanuely Njingu kwa kosa la kukwamisha shughuli za serikali kwa kuzuia watendaji wa serikali kufanya kazi yao ikiwemo ukusanyaji wa mapato.

Njingu ambaye alikuwa mjumbe wa kamati ya fedha awali kabla ya kuwekwa nguvuni na jeshi la polisi alivuliwa ujumbe wa kamati hiyo kutokana na kukiuka taratibu na makubaliano ya baraza la madiwani jambo ambalo limepelekea kuhamishiwa katikakamati nyingine.

Akitoa taarifa ya kukamatwa kwa diwani huyo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi ambaye ni Diwani wa Kata ya Irisia Ally Juma Mwanga amesema kuwa Diwani huyo amekamatwa kwa mujibu wa sheria hivyo yeye kama mwenyekiti hawezi kuingilia taratibu, sheria,na kanuni za serikali.

Mwanga amesema kuwa tarehe 19 mwezi Julai moja ya maadhimio ya kamati ya fedha na vikao vya baraza ilikuwa ni kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri lakini diwani huyo amekiuka makubaliano hayo kwa kung’oa mageti ya vizuizi vya barabarani kwa ajili ya ukaguzi wa mazao jambo ambalo limepelekea kuzorota kwa ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri.

Ameongeza kuwa Mjumbe yeyote anayekiuka maazimio wanayokubaliana na kutoa siri za kamati adhabu yake kisheriani kupoteza sifa ya kuwa mjumbe wa kamati husika.

Amesema diwani huyo ameondoshwa katika nafasi hiyo baada ya maridhiano ya kamati hiyo na kukubaliana kumuhamishia katika kamati nyingine ya huduma za uchumi.

“Jambo mkishakubaliana kisheria tena kwenye vikao vya kisheria maana yake linakuwa ni sheria hivyo kwa kiongozi yeyote akikiuka taratibu za kisheria zinachukua mkondo wake, kanuni za Halmashauri ni za watu wote hazichagui upande mmoja” Alisema Mwanga

Hapo jana Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu alihutubia Baraza la madiwani wa Halmashauri ya Wilaya hiyo ikiwa ni mara yake ya mwanzo kabisa tangu alipochaguliwa na Rais John Magufuli kuwa Mkuu wa Wilaya hiyo ambapo pamoja na kuzungumzia kuwepo kwa changemoto ya uhaba wa maabara, afya duni na miundombinu pia alizungumzia kuhusu ukusanyaji hafifu wa mapato jambo ambalo linairudisha nyuma Halmashauri ya Wilaya hiyo.

Bajeti ya Wilaya ya Ikungi kwa Mwaka 2013/2014 ilikuwa na Shilingi 509,701,044 namakusanyoyakeyakawa ni 338,325,000 ambapo hata hivyo mwaka ulimalizika kwa kuwa na upungufuwa shilingi 171,376,044.

Mwaka 2014/2015 ilipangwa bajeti ya shilingi 631,455,000 lakini makusanyo yake yakawa ni shilingi 457,555,172 ambapo mwaka ulimalizika kwa kukusanya 173,899,828.

Mwaka wa bajeti 2015/2016 bajeti ya Halmashauri iliyopangwa ilikuwa ni shilingi 1,127,030,000 makusanyo yalikuwa ni 679,283,000 ambapo hata hivyo mwaka ulimalizika kwa kwa kuwa na upungufu wa shilingi 450,747,000 hivyo kwa miaka mitatu Halmashauri hiyo imeshindwa kufikia malengo ya ukusanyaji.

Mwanga amesema kuwa Kutofikiwa malengo hayo kumesababishwa na kutopewa ushirikiano watendaji katika ukusanyaji wa mapato hii ikiwa ni kufuatia kauli za mazuio zinazotolewa na baadhi ya wanasiasa.

Hata hivyo ametoa Mwito kwa viongozi wa serikali, wanasiasa, taasisi za dini na wananchi kushirikiana kwa pamoja ili kufikia malengo ya kuifanya Ikungi kukua kiuchumi .

Kampuni ya Yono Auction Mart yamuunga mkono Rais Magufuli katika jitihada za kuleta maendeleo ya nchi.

$
0
0


Mwenyekiti wa Yono Auction Mart & Co Ltd Bw. Stanley Kivela akielezea jambo kuhusu Tuzo ya Almas ya Ubora, Uwajibikaji na Ufanisi (The Diamond Eye Award for Quality Commitment and Excellence) iliyotolewa na Rais wa Asasi ya Otherways Management & Consulting ya Paris Ufaransa ambapo takribani nchi 49 dunia zilishiriki mchakato huo huku Tanzania ikiwakilishwa na taasisi mbili ambazo ni Mamlaka ya Angaa (TCAA) kwa upande wa Serikali na Yono Auction Mart kwa upande wa Sekta binafsi.
Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Kampuni ya Udalai ya Yono Auction Mart na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Bibi. Scholastica Kevela wakiwa wameshika Tuzo na Cheti walivyopewa kutokana na kutoa huduma kwa viwango na ufanisi.Tuzo hiyo inajulikana kwa jina la The Diamond Eye Award for Quality Commitment and Excellence) imetolewa tarehe 25, Julai 2016 Jijini Rome Italia na Rais wa Asasi ya Otherways Management & Consulting ya Paris Ufaransa.
Mwenyekiti wa Yono Auction Mart & Co Ltd Bw. Stanley Kivela(katikati) akifafanua jambo kupitia picha za matukio yaliyofanyika wakati wa hafla ya kukabidhi The Diamond Eye Award for Quality Commitment and Excellence iliyotolewa na Rais wa Asasi ya Otherways Management & Consulting ya Paris Ufaransa ambapo takribani nchi 49 dunia zilishiriki mchakato huo huku Tanzania ikiwakilishwa na taasisi mbili ambazo ni Mamlaka ya Angaa (TCAA) kwa upande wa Serikali na Yono Auction Mart kwa upande wa Sekta binafsi. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Yono Auction Mart Bibi. Scholastica Kevela.
Mkurugenzi Mtendaji wa Yono Auction Mart Bibi. Scholastica Kevela akiwa ameshika Tuzo waliyopewa kutokana na kutoa huduma kwa viwango na ufanisi.Tuzo hiyo inajulikana kwa jina la The Diamond Eye Award for Quality Commitment and Excellence imetolewa tarehe 25, Julai 2016 Jijini Rome Italia na Rais wa Asasi ya Otherways Management & Consulting ya Paris Ufaransa.


Na: Frank Shija, MAELEZO.

Serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais Magufuli imeendelea kuungwa mkono na wadau mbalimbali kutokana na jitihada zake za kurejesha heshima na uadilifu miongoni mwa jamii ya Watanzania.

Haya yamebainishwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Udalali ya Yono Auction Mart & Co Ltd Bw. Stanley J. Kevela aliokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Tuzo iliyopata leo Jijini Dar es Salaam.

Kevela ameseme kuwa wao binafsi kama kampuni inayoaminiwa na Serikali na taasisi zake wanayosababu ya kuunga jitihada zinazoonyeshwa na Serikali katika kupigania maendeleo ya watu wake kwa kutekeleza majukumu yake kwa uadilifu, ubunifu na ufanisi unaostahili.

“Tunatoa Tuzo hii muhimu kwetu kwa Mhe. Dkt. Magufuli kama ishara ya kuheshimu mchango wake katika kuliletea taifa letu maendeleo na kuhakikisha mambo yanafanywa kwa ufanisi na viwango vyenye ubora wa hali ya juu”. Alisema Kavela.

Amesema kuwa tokea Rais Magufuli aingie madarakani mambo mengi yamekuwa yakienda vizuri hivyo ikiwemo suala la ukusanyaji wa Kodi kazi ambayo wamekuwa wakiisaidia Serikali kwa muda mrefu sasa.

Aliongeza kuwa Kampuni yake imekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha inatoa huduma zenye viwango tena kwa uadilifu na uwajibikaji usiotiliwa shaka ndiyo maana wanamuunga mkono Mhe. Rais kwakuwa naye ni muunini wa falsafa ya uwajibikaji, uadilifu na ubunifu.

Aidha Mwenyekiti huyo amesema kuwa katika kuendeleza jitahada za Serikali katika kukuza ajira wameajiri zaidi ya vijana 200 ambao wako mtaani wakifanya kazi ya ukusanyaji wa Kodi kwa niaba ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Yono Auction Marts &Co Ltd Bibi. Scholastica Kevela ametoa rai kwa wadau mbalimbali kuendelea kuiamini Kampuni hiyo kwa kupata huduma zao zikiwemo wakala wa Udalali wa Mahakama na Ukusanyaji wa Mapato ya Serikali kwa niaba ya TRA.

Yono Auction Mart imekuwa ikifanya kazi na Serikali katika Nyanja mbalimba ikiwemo ukusanyaji wa Kodi kwa niaba ya TRA, udalali wa Mahakama, Uuzaji wa viwanja vya Serikali na mambio mengine yanayohusu ukusanyaji wa Kodi za Serikali.

Kampuni ya Yono Auction Marts &Co Ltd ilipata fursa ya kushiriki katika hafla ya ugawaji wa Tuzo za Diamondo Eye kutokana na Ubora, Uwajibikaji na Ufanisi (The Diamond Eye Award for Quality Commitment and Excellence) iliyotolewa tarehe 25 Julai 2016 Jijini Rome, Italy iliyotolewa na Rais wa Asasi ya Otherways Management & Consulting ya Paris Ufaransa ambapo takribani nchi 49 dunia zilishiriki mchakato huo huku Tanzania ikiwakilishwa na taasisi mbili ambazo ni Mamlaka ya Angaa (TCAA) kwa upande wa Serikali na Yono Auction Mart kwa upande wa Sekta binafsi.

NEWS ALERT: TUNDU LISSU APANDISHWA KIZIMBANI KWA MASHITAKA MATATU,AACHIWA KWA DHAMANA

$
0
0
Na Mwene Saidi wa Globu ya Jamii.

Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu  (pichani) ambaye leo amefikishwa mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam na kupandishwa kizimbani dhidi ya mashtaka matatu ikiwamo kuidharau mahakama na kusababisha chuki kwa watanzania dhidi ya Rais John Magufuli na serikali yake ameachiwa kwa dhamana.

Lissu alipandishwa kizimbani  na kusomewa mashtaka matatu mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Cyprian Mkeha, katika kesi iliyoanza saa 9.26 mchana hadi saa 2.25 usiku. Hakimu alitupilia mbali kiapo cha Jamhuri cha pingamizi la dhamana kwa kuwa hakikuonesha tarehe iliyotolewa. 

Kisha Hakimu akamtaka mshtakiwa kujidhamini mwenyewe kwa kusaini hati ya dhamana ya shilingi milioni 10. Akafanya hivyona kuachiwa.
Upande wa Jamhuri uliongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu Faraja Nchimbi, akisaidiana na Wakili Serikali Mwandamizi Mutalemwa Kishenyi, Mawakili wa Serikali Simon Wankyo na Paul Kadushi.

Wakili Kadushi alidai kuwa Agost 2,2016 akiwa na nia ya kujenga chuki dhidi ya Rais Dk John Magufuli kwamba ni dikteta uchwara. 
Katika shtaka la pili ilidaiwa kuwa siku na eneo la tukio la kwanza mshtakiwa akiwa na nia ya kuleta dharau katika mfumo wa mahakama nchini alitamka kwam a "Kesi    ya kipuuzi na mashtaka yamekaa kimagufuligufuli "alinukuliwa mshtakiwa.

Shitaka la tatu linadai kuwa siku na eneo la tukio la kwanza mshtakiwa baada ya kutoka kusikiliza kesi zake mbili tofauti zinazomkabili katika mahakama hiyo akiwa na lengo la kudharau mahakama alitamka "Siwezi kufungwa mashtaka yenyewe ya kipuuzi yamekaa kimagufuligufuli" alinukuu Wakili Kadushi.

Lissu alidai kuwa maneno anayodaiwa kuyatamka katika hati ya mashtaka ni ya kweli lakini siyo ya uchochezi hivyo alikana mashtaka hayo.
Hata hivyo Wakili Nchimbi alidai kuwa upande waJamhuri unapinga dhamana dhidi ya mshtakiwa kupitia hati ya kiapo iliyowasilishwa na Mkuu wa upelelezi wa Mkoa wa Kipolisi Ilala ( RCO) kwamba mshtakiwa akipewa dhamana atarudia kufanya makosa hayo kinyume cha sheria.

Pia Wakili Nchimbi aliwasilisha pingamizi la kumkataa wakili kiongozi wa utetezi Peter Kibatala kwamba ametoa maelezo polisi na kwamba anatarajiwa kuwa shahidi wa Jamhuri dhidi ya mshtakiwa.
kuhusu uwakili Kibatala alidai kuwa hakuna sheria inayomzuia kumtetea mteja wake na kwamba ni njama za upande wa Jamhuri kwa kuwa wanamhofia.

Kutokana na pingamizi la dhamana, Lissu alilazimika kujibu hoja mwenyewe baada ya upande wa Jamhuri kusisitiza kwamba Kibatala haruhusiwi kumtetea mshtakiwa hadi mahakama itakapoamua vinginevyo.
Alidai kuwa hoja za Jamhuri hazina mashiko ya kuzuia dhamana yake kwa kuwa hajatiwa hatiani na kwamba chini ya kifungu cha 148 kidogo cha (5)a hakijaanisha sababu zilizotolewa na Jamhuri kuzuia dhamana yake.

DK. KIGWANGALA ALIAGIZA JESHI LA POLISI KUMKAMATA NA KUMFIKISHA MAHAKAMANI JUMA MWAKA WA FOREPLAN (T) LIMITED KWA KUKIUKA SHERIA ZA NCHI

$
0
0
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamis Kigwangalla (kulia) akiongea na waandishi na wananchi waliojitokeza kumsikiliza Naibu Waziri wa Afya Dkt. Hamis Kigwangala alipokuwa akitoa msimamo wa Serikali wa kumchukulia hatua kali za kisheria Tabibu Juma Mwaka wa kituo cha Tiba Asili na Tiba Mbadala cha FOREPLAN (T) LIMITED kwa kutoa huduma kinyume cha sheria. 
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kumsikiliza Naibu Waziri wa Afya Dkt. Hamis Kigwangala alipokuwa akitoa msimamo wa Serikali wa kumchukulia hatua kali za kisheria Tabibu Juma Mwaka wa kituo cha Tiba Asili na Tiba Mbadala cha FOREPLAN (T) LIMITED kwa kutoa huduma kinyume cha sheria. Picha/ARON MSIGWA -MAELEZO. 

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamis Kigwangalla (kulia) akiwa nje ya Jengo la Kituo cha Tiba Asili na Tiba Mbadala cha FOREPLAN (T) LIMITED mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza kufuatia mmiliki wa kituo hicho Tabibu Juma Mwaka kuendelea kutoa matibabu kwa wagonjwa kwa siri pia kujitangaza kwenye vyombo vya habari licha ya agizo la Serikali la Julai 11, 2016 la kumtaka asitishe kutoa huduma zake kutokana na kukosa vigezo vya kisheria vya kumruhusu kutoa tiba nchini. 
Baadhi ya Wagonjwa waliokutwa wakisubiri Tiba katika kituo cha Tiba Asili na Tiba Mbadala cha FOREPLAN (T) LIMITED kilichopigwa marufuku na Serikali kutoa huduma zake nchini.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamis Kigwangalla (kulia) akizungumzwa na baadhi ya wafanyakazi wa kituo cha Tiba Asili na Tiba Mbadala cha FOREPLAN (T) LIMITED waliokuwa wakitoa huduma licha ya kituo hicho kupigwa marufuku na Serikali kutoa huduma zake nchini.Kufuatia hali hiyo Naibu Waziri Dkt. Hamis Kigwangalla ameliagiza Jeshi la Polisi kumkamata ndani ya saa 24 na kumfikisha Mahakamani Mmiliki wa Kituo hicho tabibu Juma Mwaka kwa kukiuka agizo la Serikali na kutoa huduma kinyume cha Sheria. 
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamis Kigwangalla (kulia), Mrakibu wa Polisi Ilala, E.M .Swebe (katikati) na Mwenyekiti wa Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala Dk. Paulo Mhame (mwenye suti kushoto) kwa pamoja wakipitia kwa makini baadhi ya nyaraka zilizokutwa ndani ya kituo cha Tiba Asili na Tiba Mbadala cha FOREPLAN (T) LIMITED kilichopo ilala Bungoni kufuatia upekuzi uliokuwa ukifanywa na Jeshi la Polisi leo jijini Dar es salaam kwa lengo la kuchukua vielelezo kama ushahidi wa Tabibu Mwaka kuendelea kutoa huduma kinyume na sheria. 
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamis Kigwangalla (kulia), Mrakibu wa Polisi Ilala, E.M .Swebe (katikati) na Mwenyekiti wa Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala Dk. Paulo Mhame (mwenye suti kushoto) na Mkaguzi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini (TFDA) Dk. Itikija Mwanga wakiangalia baadhi ya dawa zilizokutwa ndani ya kituo cha Tiba Asili na Tiba Mbadala cha FOREPLAN (T) LIMITED kilichopo ilala Bungoni kufuatia upekuzi uliokuwa ukifanywa na Jeshi la Polisi leo jijini Dar es salaam kwa lengo la kuchukua vielelezo kama ushahidi wa Tabibu Mwaka kuendelea kutoa huduma kinyume na sheria. 
Daftari la lenye orodha ya mahudhurio ya wagonjwa lililokutwa dani ya kituo cha Tiba Asili na Tiba Mbadala cha FOREPLAN (T) LIMITED kilichopo ilala Bungoni kufuatia upekuzi uliokuwa ukifanywa na Jeshi la Polisi leo jijini Dar es salaam

Viewing all 46373 articles
Browse latest View live




Latest Images