Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 926 | 927 | (Page 928) | 929 | 930 | .... | 1897 | newer

  0 0


  Stanley Magesa (mjasiriamali) akifafanua jambo ndani ya studio kuhusu YALI 2016

  Aug 3, 2016 tulipata fursa ya kutembelewa na kuhojiana na baadhi ya Watanzania wanaowakilisha kwenye mkutano wa Mandela Washington Fellowship - Young African Leaders Initiative (YALI) 2016 waliomaliza mkutano wao hapa Washington DC

  Walikuwa wakarimu sana kujiunga nasi Studio na kuzungumza nasi kuhusu mambo mbalimbali

  Karibu uwasikilize

  Heri Emmanuel (kati kutoka Mwanza) akieleza jambo huku Tusekile Mwakalundwa ( Mhadhiri na Mwanasheria kutoka Arusha) akisikiliza kwa makini. Kulia ni Mubelwa Bandio wa Kwanza Production na Vijimambo Radio
  Baadhi ya wawakilishi wa YALI 2016 kutoka Tanzania, wajasiriamali Stanyey Magesa (Mwanza), Simon Malugu (Morogoro) na Lusajo Mwaisaka (Dar) wakiwa kwenye mahojiano Kilimanjaro Studio
  Mshiriki wa YALI 2016 Heri Emmanuel (Mwanza) kulia akaifafanua jambo huku akisikilizwa na mshiriki mwenzake ambaye pia ni Mhadhiri na Mwanasheria Tusekile Mwakalundwa (Arusha) na mjasiriamali na Lusajo Mwaisaka (kutoka Dar)


  0 0

  Na Zainab Nyamka.

  KAMANDA  wa polisi Mkoa wa kipolisi Kinondoni, ACP Christopher Fuime amethibitisha kumshikilia rais wa klabu ya Simba na alipoulizwa ni tuhuma gani zinazomkabili kiongozi huyo wa juu kabisa wa wekundu wa Msimbazi alisema ni vizuri swali hilo wakiulizwa TAKUKURU. Tumemshikilia toka juzi jioni na juhudi za kupatiwa dhamana zimeshindikana mpaka dakika hii kwani sisi kazi yetu ni kumshikilia tu ila mamlaka zaidi yapo TAKUKURU.

  Aveva anashikiliwa na polisi kwa kibali cha Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU lakini bado haijafahamika moja kwa moja anakabiliwa na tuhuma gani huku baadhi ya watu wakidai ni matumizi mabaya ya fedha walizolipwa kutoka Etoile Du Sahel juu ya malipo ya Emanul Okwi pamoja na za Mbwana Samatta ambazo anadaiwa kuzihamisha kutoka kwenye akaunti ya klabu ya Simba.

  “Kwa upande wangu siwezi kujua ila kwa maelezo zaidi  TAKUKURU wanaweza wakajua na ni lini huo uchunguzi  utakamilika na kumpeleka mahakamani. Sisi tunamshikilia kwasababu TAKUKURU hawana mahabusu binafsi,  na maswali yote  wangejibu sababu hasa ya kushikiliwa kwa Evance Aveva,” amesema Fuime

  Kwa upande wa TAKUKURU kupitia afisa habari Musa Misalaba amesema kuwa Aveva yupo kwenye mikono salama na wanamshikilia kwa uchunguzi, kwa sasa wanaendelea na uchunguzi kwani sheria inaturuhusu kufanya uchunguzi  na pia tunaruhusiwa kukamata, kupekuwa kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu.

  0 0

  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kuzindua Mkakati wa Baraza wa Kukabiliana na Ajali za Barabarani nchini. Mkakati huo wa miezi Sita ambao unalenga kukabiliana na ajali umenza mwezi huu Agosti na unatarajiwa kumalizika mwezi Februari 2017 ambapo tathmini itatolewa. Kulia meza kuu ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, ambaye pia ni Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Kamanda Mohammed Mpinga. Uzinduzi huo umefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara, jijini Dar es Salaam. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
   Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kuzindua Mkakati wa Baraza wa Kukabiliana na Ajali za Barabarani nchini. Mkakati huo wa miezi Sita ambao unalenga kukabiliana na ajali umenza mwezi huu Agosti na unatarajiwa kumalizika mwezi Februari 2017 ambapo tathmini itatolewa. Baadhi ya mambo yaliyolengwa katika mkakati huo ni pamoja na udhibiti wa madereva walevi na kuendesha kwa uzembe, udhibiti wa mwendokasi kwa madereva na wamiliki wa magari pamoja na kuanza utaratibu wa Mfumo Nukta (point system) kwenye leseni za udereva ambapo dereva akifanya makosa kadhaa atanyang’anywa leseni na kutokuruhusiwa kuendesha gari tena.  Uzinduzi huo umefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara, jijini Dar es Salaam.

  0 0

  In a recent live interview conducted at the Pan African Parliament in Midrand South Africa by Channel Africa which is an International broadcast service of the SABC, Hon.Stephen Julius Masele (MP) and a member of Pan African Parliament,  spoke about the new President of Tanzania and gave his opinion on current affairs and globe issues.

  Q1. Asked about Tanzanian President HE Dr John P. Magufuli Presidency and Leadership: Having been worked with him in the previous government, what is your opinion?

  "Yeah! I think (He),H.E Dr Magufuli is among the great leader this country has ever produced in recent years in my opinion. His qualities,strong character and mental strength add to his clear vision and knowledge for sustainable development, he is a great leader for me to take our country to the next level, I think our country needs him much than he needs the job".Stephen J. Masele(MP).

  Q2.  You have been a pioneer of Youth movements around the globe  and  involved and engaged in many International Youth platforms. As Young leader at the highest body of the African Union (Pan African Parliament)what is your opinion and advice to the African young leaders?

  Answer SM: First, They should always think positive with self determination, commitment and persistence, this is very important. Never let turbulances get you away, or trying not to get carried away with early success. They should  always stay focused,calm with great desire and hunger for success with a lot of torelence.

  "If you work hard enough and you're not afraid to dream then you're not afraid to fail.I'm not afraid to fail. Everybody fails. I have had more success than I've had failure."

  Q3. This is your second term with Pan African Parliament, does this mean anything in your future career as a Young parliamentarian and  upcoming diplomat.

  SM: Aaah haaah!  I was born a diplomat,joke. diplomacy? it is in my DNA, I have passion and love for diplomacy, I think I have the potential of becoming a great diplomat in the future given time and opportunity to develop my career in this field.I believe in my ability.I have got the right knowledge and trained at highest level and I am luck to have great mentors who  works hard  to guide me  and develop my raw talent and skills and install experience.

   Pan African Parliament is a huge platform to practice and gain knowledge and experiences at the highest level, its among the most important organ of the Africa Union.I have been actively engaged in various joint AU-PAP fact finding mission, peace keeping negotiations and participate at  international conferences around the globe. 

  It is always a dream for me to one day work as a top diplomat in my country and continent and  I know I can only achieve that by working hard and improve my skills and knowledge and gather enough experiences.I thank you my leaders who groomed me and raised me  within the ranks of  my Party youth system to government.I see and believe the future is wide open and the sky is the limit with the help of God.
   
   See: "Asked about Tanzanian President HE Dr John P. Magufuli Presidency and Leadership: Having been worked with him in the previous government, what is your opinion?

  "Yeah! I think (He),H.E Dr Magufuli is among the great leader this country has ever produced in recent years in my opinion. His qualities,strong character and mental strength add to his clear vision and knowledge for sustainable development, he is a great leader for me to take our country to the next level, I think our country needs him much than he needs the job".Stephen J. Masele(MP).

  0 0

   Mwenyekiti wa Klabu ya Golf ya Lugalo Brigedia Jenerali Michael Luwongo akiongea na Wapiga gofu wa klabu hiyo walioondoka Leo (jana) Jijini Dar es salaam wakati akiwatakia heri katika mashindano ya Moshi open na Tanzania Open yanayotarajiwa kufanyika hivi karibuni Mkoani Kilimanjaro na Arusha.
   Mwenyekiti wa Klabu ya Golf ya Lugalo Brigedia Jenerali Michael Luwongo akiwapa mkono wa heri Wapiga gofu wa klabu hiyo walioondoka Leo (jana) Jijini Dar es salaam kuelekea katika mashindano ya Moshi open na Tanzania Open yanayatarajiwa kuanza hivi karibuni Mkoani Kilimanjaro na Jijini Arusha. 
   Wapiga golf wa Klabu ya Lugalo wakifanya mazoezi ya Mwisho  kabla ya kuondoka Leo (jana) Jijini Dar es salaam kuelekea katika  mashindano ya Moshi open na Tanzania Open yanayotarajiwa kufanyika hivi Karibuni Mkoani Kilimanjaro na Arusha.

  Na Selemani Semunyu,JWTZ
  Timu ya golf ya Jeshi ya Lugalo imetakiwa kuhakikisha inawapa raha wanachama wake akiwemo  Mlezi wa Klabu hiyo ambaye ni Mkuu wa majeshi ya Ulinzi Jenerali davis Mwamunyange kwa kurejesha Ubingwa wa mashindano ya Moshi Open mashindano yanayotarajiwa kufanyika Mkoani Kilimanjaro.

  Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Klabu hiyo Brigedia Jenerali Michael Luwongo wakati akiongea na Wachezaji hao katika mazoezi yao ya Mwisho katika Klabu ya Lugalo Jijini  Dar es Salaam  kabla ya Kuondoka kuelekea Moshi.

  "Hakuna sababu kwa Timu ya Jeshi iliyofanya mazoezi kwa muda  Mrefu ikashindwa kirahisi katika Mashindano kama haya ambayo tuliwahi kuchukua ubingwa kiukweli wapeni raha wanachama wenu" Alisema Brigedia Jenerali Luwongo.

  Aliongeza kuwa Wanachama wa Lugalo akiwemo Mkuu wa Majeshi Mstaafu George Waitara hawahitaji kitu kingine zaidi ya Furaha ya Ushindi ambayo watakuwa wanaifuatilia hivyo ni Jukumu la wachezaji hao kuhakikisha wanakamilisha Furaha hiyo.

  Pia aliwataka wanachama wa Golf kuhakikisha wanamtuma kazi ili kuhakikisha mafaninio makubwa yanapatikana ikiwemo kuboresha Uwanja wa Golf wa Lugalo ambao ni Uwanja uliojengwa na wazalendo kuwa Bora na kuhamasisha Mashindano mengi ya Kimataifa kuandaliwa katika Uwanja huo.

  Mwenyekiti huyo ambaye ameteuliwa hivi karibuni aliahidi kuboresha Klabu hiyo na kuifanya kuwa ya kisasa zaidi na Kuwa kiwanja bora Afrika Mashariki na kuwataka watu wote kujitokeza kushiriki katika mchezo huo kwani ni mchezo unaokubalika kwa rika zote.

  Kwa upande wake Kapteni wa Timu hiyo Kapten Kassim Usitambe alisema Mara baada ya Mashindano hayo watakayoshiriki wakiwa ni wachezaji Tisa kutoka klabu ya Lugalo wataelekea Mkoani Arusha kwa mashindano ya Tanzania Open.

  Kwa upande wake mmoja wa wapiga Gofu hao Amina Hamisi aliahidi kurejea na ushindi katioka mashindano hayo ili kutoa zawadio kwa mwenyekiti mpya ikiwa ni siku chache tu baada ya kuteuliwa kushika madaraka hayo.

  Timu hiyo ya Golf iliyoondoka leo (Agosti Nne) itashiriki Mashindano hayo ya Moshi Open ambayo Klabu hiyo Mwaka 2014 walichukua kikombe yatashirikisha Wachezaji wote wakiwemo wa Nje sambamba na ya Tanzania open ambayo wapiga Gofu kutoka Nje ya Tanzania.    

  0 0

  Mwanamitindo mstaafu wa kimataifa Tausi Likokola, ambaye yupo hapa nchini,akifafanua jambo mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani) mapema leo jijini Dar,kuhusiana na uzinduzi kipindi chake cha Television, chenye malengo ya kuwainua wasichana na wanamitindo kwa jumla kwa kutumia ulimbwende, fasheni na uanamitindo kama mwamvuli kitakachojulikana kwa jina la ‘TAUSI LIKOKOLA’S AFRICAN PRINCESS MODEL SEARCH’. PICHA NA MICHUZI JR.

  Tausi ambaye amekuwa mstari wa mbele katika kukuza vipawa vya wasichana ulimwenguni kote kwa kutumia uzoefu wake katika fasheni, mitindo uandishi wa vitabu na ujasiriamali, anasema ni wakati sasa wa kufanya hayo hapa nyumbani kwao mwenyewe. Amesema kuwa kipindi hicho kimetokana na wazo lililobebwa katika vitabu vyake viwili, T’he African Princess’ na kingine cha ‘Beautiful You’."Lakini pia kipindi hicho cha kwanza na cha aina yake, kitaanza kurushwa katika kituo cha televisheni cha TV1 kuanzia Ijumaa ya Agosti 5, 2016 saa 10:00 jioni na kurejewa tena Jumapili asubuhi"amesema Likokola.

  Tausi anasema kuwa wasichana wanahitaji kufundishwa na kutiwa moyo kuelekea katika ndoto zao,hivyo kipindi hicho kitaonesha vipengele tofauti tofauti katika maisha kuanzia maadili, ulimbwende, nidhamu na mambo mengine, hiki ni kipindi kwa familia nzima,huku akibainisha lengo kuu la Tausi Likokola’s African Princess Model Search ni kukuza na kuongeza uwezo wa msichana mmoja mmoja katika stadi za uongozi na uwezo katika kujitambua, kujikubali, kujiamini na kuwa na mawazo chanya na kujifunza stadi za mawasiliano mazuri ambayo hatimaye yatafanya washindani kufanikiwa sana katika maisha yao ya baadaye katika ulimwengu wa ushindani wa fasheni.
  Tausi aliyezindua bidhaa kadhaa za urembo na maisha kupitia kampuni yake iliopo Tanzania,ijulikanayo kama ‘Tausi Dreams Ltd ambaye bado anayeishi Marekani,akionesha nywele zake ikiwa ni moja ya bidhaa ilioko kwenye miradi yake mbalimbali ikiwepo pafyumu yake inayoitwa Tausi Dreams,nywele za binadamu zinazoitwa Tausi Beautiful You Hair.Pichani kushoto ni Muwakilishi wa Tausi hapa nchin,Bi. Margaret Bitungwa na kulia ni Mmoja wa Wakilishi wa Tv1 kutoka kitengo cha Masoko,Edgar Wilson.
  Mmoja wa Wakilishi wa Tv1 kutoka kitengo cha Masoko,Edgar Wilson akifafanua zaidi kuhusiana na muda na mambo mbalimbali yatakayokuwa yakirushwa hewani kupitia kipindi hicho kitakachojulikana kwa jina la ‘TAUSI LIKOKOLA’S AFRICAN PRINCESS MODEL SEARCH’
  Tausi Likokola akionesha moja ya kitabu kati ya viwili ambavyo aliviandika The African Princess’ na kingine cha ‘Beautiful You’.

  Tausi aliyekulia katika ulimwengu wa fasheni kimataifa katika miaka ya 90, amefanya kazi na makampuni makubwa ya mitindo kama Gucci, Christian Dior, Issey Miyake, Tommy Hillfger, Escada na wengine wengi, na sura na kazi zake kupamba kurasa za mbele na za ndani katika magazeti na majarida kadhaa ya mitindo na maisha ya kimataifa na hapa nyumbani, amekuwa akiwatia moyo wanamitindo wengi hapa nchini na wengine duniani kote.

  Tausi amefanikiwa sana kulitumia jina na kipawa chake kuwasaidia watu wake wa Tanzania katika elimu, kutambua UKIMWI, mahitaji ya jamii, na ameweza kuchangia katika kukua kwa utalii katika nchi yake ya kuzaliwa (Tanzania), kibiashara na kukuza maliasili. Tausi ana mpango wa kusimamia kazi kadhaa za kujitolea kupitia kampuni yake ya ‘Tausi and Friends for Life’

  Tausi alipumzika kujitokeza katika uanamitindo ili kupata muda mzuri wa kukaa na familia. Wakati wa kazi za mitindo Tausi ametembelea nchini nyingi za Afrika, Ulaya, Asia, Australia na kwa sasa akiwa anaishi Marekani. Tausi ameandika vitabu vinne hadi sasa akitumia uzoefu wake uliopata toka mataifa mbalimbali akifanya kazi na wasichana toka ulimwenguni kote kuwasaidia kwa hali na mali. Vitabu alivyotoa hadi sasa ni; The Art of the Beauty and Health’, The African Princess,’ ‘The Touch of an Angel’ na ‘Beautiful You’.

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony J. Mtaka (Katikati) akizungumza na Viongozi wa Mkoa huo na Wajumbe wa Kamati za Fedha, Mipango na Uongozi kutoka katika Halmashauri za Mkoa huo katika kikao kilichofanyika Mjini Bariadi, kujadili mikakati ya ujenzi wa vyumba vya madarasa, (kushoto) Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Jumanne A. Sagini na (kulia) Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, mhe. Festo S. Kiswaga

  Wakuu wa Wilaya wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu (hayupo pichani) katika kikao cha kujadili mikakati ya ujenzi wa vyumba vya madarasa mkoani humo, mstari wa kwanza kutoka kushoto, Mhe. Benson Kilangi (Itilima), Joseph Chilongani (Meatu), Seif Shekalaghe, Tano Mwera (Busega) na mstari wa pili, kutoka kushoto, Mhe. Stanslaus Nyongo(Mbunge Maswa Mashariki), Mhe. Mashimba Ndaki (Mbunge Maswa Magharibi). Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Jumanne A. Sagini akizungumza kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony J. Mtaka (kulia) ili azungumze na Viongozi wa Mkoa huo na Wajumbe wa Kamati za Fedha, Mipango na Uongozi kutoka katika Halmashauri za Mkoa huo, katika kikao kilichofanyika Mjini Bariadi, kujadili mikakati ya ujenzi wa vyumba vya madarasa.
  Viongozi na baadhi Wajumbe wa Kamati za Fedha, Mipango na Uongozi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu (hayupo pichani) katika kikao cha kujadili mikakati ya ujenzi wa vyumba vya madarasa mkoani humo kilichofanyika Mjini Bariadi.
  Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Maswa, Mhe. Dila Mayeka akitoa mchango wake wa mawazo katika kikao cha kujadili mikakati ya ujenzi wa vyumba vya madarasa mkoani humo, kilichofanyika Mjini Bariadi

  Na Stella Kalinga

  Serikali Mkoani Simiyu imesema asilimia mbili ya ushuru wa zao la pamba inayopatikana katika Halmashauri zote za Mkoa wa Simiyu ielekezwe katika ujenzi wa Miundombinu ya elimu ya msingi na sekondari,hususani vyumba vya madarasa.

  Uamuzi huo umefikiwa kufuatia majadiliano ya pamoja kati ya Uongozi wa Mkoa na Halmashauri zote katika kikao kilichoongozwa na Mkuu wa mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony J. Mtaka akiwa na Wakuu wa Wilaya, Wenyeviti wa Halmashauri, Wakurugenzi wa Halmashauri, Makatibu Tawala Wilaya na Wajumbe wa Kamati za Fedha za Halmashauri ili kujadili mstakabali wa ujenzi wa vyumba vya madarasa katika mkoa huo.

  Mtaka amewaelekeza Wakurugezi wote wakafanye uhakiki na kuainisha takwimu sahihi za mahitaji ya vyumba vya madarasa ili kupata uhakika wa vyumba vinavyohitajika katika mkoa mzima na kupanga mkakati wa namna vyumba hivyo vitakavyojengwa ikiwa ni pamoja na teknolojia itakayotumika katika kufyatua matofali pamoja na gharama zake na kuwasilisha taarifa katika Ofisi yake tarehe 9 Agosti, 2016, ambapo baada ya kupata taarifa hiyo na kujiridhisha zoezi la ufyatuaji matofali kimkoa litazinduliwa rasmi Wilayani Maswa tarehe itakayopangwa na mkoa.

  “ Sina uhakika sana na takwimu hizi, niwaagize tena Wakurugenzi wote mkafanye mapitio upya na uhakiki wa kina katika maeneo yenu juu ya idadi ya vyumba vya madarasa vinavyohitajika kwa Elimu ya Msingi na Sekondari. Mkae na wataalam wenu wa ujenzi mfanye tathmini ya namna mtakavyojenga kama mtatumia matofali ya kuchoma, matofali ya block au matofali yakufungamana (interlocking blocks) yanayofyatuliwa na vijana waliopewa mafunzo na Shirika la Nyumba la Taifa,ambao wako katika kila halmashauri pamoja na gharama zitakazotumika”, alisema Mtaka.

  Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Jumanne Sagini amewataka Wakurugenzi kufanya utaratibu wa kubadilisha matumizi ya fedha haraka pale inapobidi kwa kufuata sheria kanuni na taratibu kufanikisha zoezi la ujenzi wa vyumba vya madarasa ili kuwatengenezea wanafunzi mazingira mazuri ya kujifunzia na kuwezesha madawati yaliyotengenezwa ambayo hayana mahali pa kuwekwa yasiharibike kwa kupigwa na jua na kunyeshewa na mvua.

  Pamoja na kutenga asilimia mbili ya ushuru wa pamba, Mtaka amesema Mkoa unakusudia kufanya Harambee kubwa itakayowashirikisha viongozi na wadau wengine muhimu kutoka ndani na nje ya mkoa ambao watachangia kwa kuunga mkono jitihada za Serikali Mkoani humo, katika kuondoa tatizo la upungufu wa vyumba vya madarasa kwa Mkoa wa Simiyu.

  Akichangia hoja hiyo ya harambee Mbunge wa Jimbo la Maswa Magharibi , Mhe.Mashimba Ndaki amesema, hiyo itakuwa ni fursa kwa wenyeji wa Mkoa wa Simiyu walo ndani na nje kuchangia maendeleo ya Mkoa wao na akasisisitiza fedha zitakazokusanywa zisimamiwe vizuri na viongozi.

  Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa wa Simiyu amekabidhi simu tano kwa Wakuu wa Wilaya tano za Mkoa huo zilizotolewa na idara ya mahakama kwa lengo la kutekeleza mpango wa mapambano dhidi ya rushwa na vitendo vinavyokwenda kinyume na maadili ya Utumishi wa Umma katika utoaji wa huduma za Mahakama, ambazo zitagawanywa kwa maafisa wa dawati la malalamiko kwa kila Ofisi ya Mkuu wa Wilaya na akaelekeza zitumike kwa malengo yaliyokusudiwa.

  Aidha, Mtaka amewataka Wakuu wa Wilaya kutenga siku maalum ya kusikiliza kero za wananchi ambayo Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi wa Halmashauri watakaa kuwasilikiliza wananchi na kuwapatia ufumbuzi na pale inaposhindikana masuala yao yapelekwe Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa ajili ya hatua zaidi.

  0 0

   
  \Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara(TanTrade) Bw Edwin Rutageruka akipata naelezo kutoka kwa Bw John Julius juu ya uzalishaji wa mafuta ya ufuta katika banda la halmashauri ya Masasi kwenye maonesho ya 88 mkoani Lindi. Mafuta ya ufuta yanasoko kubwa sana nje ya Afrika hasa nchi ya Japan na ni mafuta ya pili yenye ubora baada ya olive oil. 

  Lengo kuu tasisi hii kushiriki maonesho haya ni kuunganisha wazalishaji na masoko ya ndani na nje ya nchi. Hivo imekuwa ikipita kwa wazalishaji mbalimbali kuangalia fursa za kuwaungaisha na masoko mbalimbali ili kukuza uchumi wa nchi yetu na pia kualika wawekezaji katika nchi yetu na kuifanya Tanzania yenye viwanda. 

  Tantrade imeshiriki katika maonesho haya maarufu kama 88 kwenye kanda tano ambazo ni Lindi, Morogoro, Mwanza, Mbeya na Arusha na kila mkoa wazalishaji hutofautiana kutokana na aina za uzalishaji wa bidhaa za kila mkoa.

  0 0


  Afisa uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde pamoja na Meneja wa kitengo cha ujasiriamali na kozi fupi wa VETA Mwanza , Peter Mlacha wakitoa elimu ya VSOMO kwa mafundi magari na pikipiki mkoani mwanza wakati Airtel na VETA ilipotembelea vijiwe vya mafundi ili kutoa ufafanuzi wa jinsi ya kusoma kozi za ufundi za VETA kupitia simu za mkononi za Airtel . akishuhudia ni Afisa masoko wa Airtel kanda ya ziwa, Emmanuel Raphael
  Afisa uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde akiwaonyesha mafundi magari na pikipiki mkoani mwanza jinsi ya kupakua application ya VSOMO na kusoma kozi za ufundi za VETA kupitia simu zao za mkononi na kupata ujuzi zaidi utakao ongeza tija kwenye shughuli zao.
  Meneja wa kitengo cha ujasiriamali na kozi fupi wa VETA Mwanza, Peter Mlacha akitoa elimu kwa mafundi magari na pikipiki mkoani mwanza juu VSOMO mpango unaowawezesha watanzania kusoma kozi za ufundi za VETA kupitia simu zao za mkononi za Airtel . akishuhudia ni Afisa masoko wa Airtel kanda ya ziwa, Emmanuel Raphael (kushoto) na Afisa uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde
  Meneja wa kitengo cha ujasiriamali na kozi fupi wa VETA Mwanza, Peter Mlacha akitoa elimu juu ya VSOMO kwa mafundi wa kuchomea vyuma mkoani mwanza wakati Airtel na VETA ilipotembelea vijiwe vya mafundi ili kutoa ufafanuzi wa jinsi ya kusoma kozi za ufundi za VETA kupitia simu za mkononi za Airtel. akishuhudia ni Afisa masoko wa Airtel kanda ya ziwa, Emmanuel Raphael (kushoto) na Afisa uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde
  Afisa masoko wa Airtel kanda ya ziwa, Emmanuel Raphael akifafanua jinsi ya kupata masomo ya VETA kupitia simu ya mkononi ya Airtel kwa mafundi wa kuchomea vyuma mkoani mwanza wakati Airtel na VETA ilipotembelea mitaa ya mwanza kutoa elimu juu ya VSOMO

  0 0

  Katibu wa Kamati ya Amani Mkoa wa Dar es Salaam na kiongozi wa Kanisa la Anglikana, Mchungaji,John Solom(aliyeshika kipaza Sauti) akisali kuombea uwanja wa ndege wa Terminal III unaoendelea kujengwa leo jijini Dar es Salaam uliopo katika Uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. 
  Mkurugenzi wa Mradi wa Mamlaka ya Anga Tanzania (TAA), Mhandisi, Mohamed Milanga akitoa maelekezo kwa viongozi mbalimbali wa dini jijini Dar es Salaam leo walipotembelea na kuombea uwanja mpya wa ndege unaoendelea kujengwa wa Teminal III uliopo katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere. 
  Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhadi Mussa Salum akiomba dua  kuombea uwanja wa ndege wa Terminal III unaoendelea kujengwa leo jijini Dar es Salaam uliopo katika Uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Wengine ni Viongozi mbalimbali wa Dini.
    Katibu Mkuu wa Kampuni wa Mamlaka ya Anga Tanzania, Jaji Ramdhan Maleta(Mwenye tai Nyekundu) akitoa neno la Shukrani mara baada ya kumaliza ziara ya viongozi mbalimbali wa dini waliotembelea katika uwanja wa ndege unaoendelea kugengwa wa Terminal III jijini Dar es Salaam leo.
  Picha na Yasir Adam, Globu ya Jamii.

  0 0


  Na Saleh Masoud, BAGAMOYO

  Kikundi cha wakulima wa zao la miwa kilichopo Kiwangwa Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani, wameiomba Serikali ya awamu ya tano kuruhus Mradi wa ECO ENERGY utakaowezesha kujengwa kwa kiwanda cha sukari maeneo hayo.

  Katika Kikao cha Wadau wa Zao hilo Wakulima hao, wametilia Shaka kusuasua kwa Ujenzi wa Kiwanda hicho cha kuzalisha sukari, ambapo wamesema kukawia kwa Mradi wa ECO ENERGY kutazidi kuwadidimiza Kimaisha na kurudisha nyuma maendeleo yao Kiuchumi.

  Wamesema Tumaini walilonalo kwa sasa kuona mradi wa ECO ENERGY ukianza kufanya Kazi mara moja, ambapo watakuwa na fursa pana ya kuuza zao la Miwa kwa mwekezaji atakayejenga kiwanda cha zao hilo katika Wilaya ya BAGAMOYO.
  Mwenyekiti wa Kikundi cha CHUHA Bi PILI ALLY akielezea Changamoto zinazowapata wakulima Wadogo wa zao la Miwa Wilayani Bagamoyo, baada ya Kuchelewa kuanza kwa Mradi wa ECO ENERGY utaowezesha Kujengwa kwa Kiwanda cha Sukari Katika Wilaya Hiyo.

  Kuhusu tuhuma zinazotolewa na Wadau wa masuala ya Mazingira kuhusu Kilimo cha Miwa kwenye Ukanda huo, wameiomba Serikali iliyo chini ya Rais Dkt JOHN MAGUFULI kutuma wachunguzi ambao wamebobea kwenye suala la Mazingira ili kujiridhisha na kutoa Baraka za kuanza kwa Mradi wa ECO ENERGY.

  Kwa Upande wake mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Kiwangwa akizungumzia juu ya tatizo hilo amesema vilio vya wakulima katika eneo lake ni vyema vikatafutuwa ufumbuzi wa haraka.

  Amesema kushughulikia mapema mgogoro huo kutawasaidia Wakulima hao wadogo waliokopa fedha kwenye taasisi za Kibenki kurejesha mikopo hiyo baada ya kuuza zao Miwa kwa mwekezaji wa Kiwanda kitakachojengwa baada ya Kuanza kwa Mradi wa ECO ENERGY.

  Wakati malalamiko hayo ya wakulima yakitolewa uongozi wa mradi wa ECO ENERGY unaosimamia mradi huo, Umesema tayari wameanza kupata hasara ya Kutupa Miwa ambayo imevunwa lakini hakuna sehem ya kuipeleka kwa sababu ya kukosekana kwa Kiwanda kutokana na kusuasua kwa mradi huo.

  0 0


  Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella akikagua timu wakati wa ufunguzi wa Airtel Rising Stars mkoani humo. Ameambatana na mwenyekiti wa chama cha soka mkoani Mwanza (MZFA) Jackson Songora.

  Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella akipiga penati kufungua rasmi michuano ya Airtel Rissing Stars mkoani humo
   
  Mwanza,

  Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mheshimiwa John Mongella leo amefungua mashindano ya soka kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars mkoani humo na kuwataka vijana kuzingatia nidhamu na taratibu zinazoongoza mchezo huo maarufu duniani.

  “Hata ukiwa na kipaji cha aina gani bila kuwa na nidhamu kamwe huwezi kutimiza ndoto yako ya kuwa mchezaji nyota wa mpira wa miguu kwa sababu, kama ilivyo kwenye nyanja nyingine yoyote, mchezo wa soka unaongozwa na kanuni na sheria ambazo kila mchezaji lazima azifuate”, alisema.

  Alisema kuwa binafsi anaifurahia sana programu ya Airtel Rising Stars kwa kuwa inakwenda sanjali na mikakati ya serikali ya kuwawezesha vijana. “Wote tunafahamu kuwa mchezo wa mpira wa miguu ni chanzo cha ajira ya kuaminika kwa vijana duniani. Mnaweza kupata kipato na kuboresha maisha yenu kupitia mpira”, alisema Mongella na kuipongeza kampuni ya Airtel Tanzania kwa kuwekeza katika soka kupitia programu hii ya vijana.

  Alisema michuano ya Airtel Rising Stars inasaidia kubaini wachezaji wenye vipaji kutoka sehemu mbalimbali ambao bila mashindano haya wangeweza kupotea hivi hivi. Aliwataka viongozi wa soka mkoa humo kushirikiana na shirikisho la soka nchini (TFF) kuwalea na kuwaendeleza vijana wanaopatikana kupitia Airtel Rising Stars.

  Akiongea katika hafla hiyo ya ufunguzi, Mwenyekiti wa Chama cha Soka mkoani Mwanza (MZFA) Jackson Songora alisema kuwa Airtel Rising Stars imetoa hamasa kwa vijana wengi mkoani Mwanza kucheza soka na kuonyesha vipaji vyao. “Tunajivunia kuweza kutoa mfungaji bora na mchezaji bora katika fainali za mwaka jana. Aliwataja wachezaji hao kuwa ni David Richard na Cypria Mtesigwa.

  Songora pia alisema kuwa mkoa wa Mwanza umetoa wachezaji wa kutegemea katika timu ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Serengeti Boys. Aliwataja wachezaji hao walioibuliwa kupitia Airtel Rising Stars kuwa ni Arish Suleiman, Cypria Mtesigwa, Ally Ng’anzi na Ally Hussein Msengi.

  Kwa upande wake, Meneja wa kanda ya ziwa wa Airtel Tanzania Emmanuel Raphael alisema kuwa kampuni yake inajivunia kuweza kutoa mchango katika soka la Tanzania. “Airtel Rising Stars imekuwa chanzo cha kutumainiwa kwa klabu na timu za Taifa kupata vijana chipukizi wenye vipaji. Tunaona fahari kuweza kupata fursa ya kudhamini soka nchini Tanzania“alisema Raphael.

  Hafla hiyo ya ufunguzi ilishuhudia mchezo wa ufunguzi kati ya Barass Sports Centre na Alliance Academy ambapo Barass Sports Centre waliwaduwaza wapinzani wao kwa kuwatandika 4-1. Mshambuliaji Frank Osoro alikuwa moto wa kuotea mbali na kufanikiwa kufunga magoli huku goli la nne likifungwa na mlinzi wa Alliance aliyejifunga mwenyewe katika juhudi za kuutoa mpira katika hatari. Alliance Sports walipata goli la kufutia machozi kwa njia ya penati iliyofungwa na Rashid Hamis

  0 0


  Mkuu wa wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema akizungumza kwa unyenyekevu mbele ya Wazee wa CCM wilaya ya Ilala wakati alipokutana nao ili kujitambulisha na kufahamiana nao baada ya kuanza kazi kama mkuu wa wilaya hiyo, Aliwaomba wazee hao kushirikiana naye bega kwa bega na kumpa ushauri wa kila mara ili aweze kutekeleza majukumbu yake ya kuwaletea maendeleo wananchi wa wilaya hiyo na kufanikisha mipango ya Rais Mh. Dk John Pombe Magufuli ili kutekeleza kwa ufanisi ilani ya uchaguzi ya CCM, Katika picha kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala Ndugu Asaa Simba , Mkutano huo ulifanyika kwenye ofisi za CCM wilaya ya Ilala.
  Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala Ndugu Asaa Simba akimkaribisha mkuu wa wilaya ya Temeke Mh. Sophia Mjema ili kuongea na wazee wa CCM wilaya ya Ilala.
  Mkuu wa wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema akimsikiliza Katibu wa CCwilaya ya Ilala Bw. Kafuge Joel alipokuwa akizungumza mambo kadhaa kabla ya umkaribisha mwenyekiti wake ili kumkaribisha mkuu wa wilaya.
  Baadhi ya wazee wa CCM wilaya ya Ilala wakiwa katika mkutano huo uliowakutanisha na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema.
  Baadhi ya wazee wa CCM wilaya ya Ilala wakiwa katika mkutano huo uliowakutanisha na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema.

  0 0

  Na Ally Daud-Maelezo

  Serikali imetenga milioni 900 ili kuzalisha dawa za binadamu katika viwanda vya ndani ili kufanya asilimia 80 ya dawa zinazoagizwa nje zipatikane nchini.

  Akizungumza hayo wakati wa Uzinduzi wa Bodi mpya ya ushauri kutoka Mamlaka ya Chakula na dawa nchini (TFDA), Waziri wa Afya Waziri wa Afya ,Maendeleo ya jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amesema kuwa Serikali imetenga fedha hizo kuhakikisha viwanda vya ndani vinatengeneza dawa hapa nchini na kupiga hatua katika uchumi wa viwanda.

  “Serikali kupitia wizara yangu tumetenga milioni 900 ili kuzalisha dawa za binadamu katika viwanda vya ndani ili kufika uchumi wa kati kwa kutumia viwanda”.alisema Mhe. Ummy. Aidha Mhe. Ummy amesema kuwa TFDA kwa kushirikiana na Serikali wanapaswa kuhakikisha viwanda vya ndani vinatengeneza dawa zenye ubora kwa matumizi ya binadamu ili kupunguza magonjwa yanayotokana na sumu za kemikali zitokananzo na dawa hizo.

  Mhe. Ummy ameongeza kuwa TFDA inatakiwa ishirikiane na Taasisi ya viwango nchini (TBS) ili kuzuia na kupiga marufuku bidhaa zisizokizi viwango na ubora unaopaswa kutumiwa na Watanzania. Aidha Waziri Ummy amesema kuwa TFDA inatakiwa kutoa elimu ya kutosha kwa umma ili kuwawezesha watanzania kuepuka kutumia bidhaa zisizo na ubora kwa matumizi ya binadamu .

  Mbali na hayo Mhe. Ummy amesema kuwa TFDA inatakiwa ikusanye mapato kwa wingi zaidi ili kuendana na kasi ya Rais Magufuli na kupiga hatua kiuchumi ili isaidie wananchi katika shughuli za maendeleo. Kwa upande wa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri TFDA Balozi Dkt.Ben Moses amesema kuwa wamepokea maagizo yote yaliyotolewa na Mhe. Waziri na watayafanyia kazi kwa haraka na ufanisi ili kuendana na kasi ya “HAPA KAZI TU”.

  “Tumepokea maagizo ya Mhe. Waziri na nataka kumuhakikishia kwamba tutaendelea na kasi yetu ili kuifikisha nchi yetu kwenye kilele cha maendeleo na Afya bora” alisisitiza Dkt. Moses. 

  Waziri wa Afya ,Maendeleo ya jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiongea mbele ya Viongozi na watumishi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini(TFDA) hawapo pichani wakati wa Uzinduzi wa Bodi ya ushauri ya mamlaka hiyo leo jijini Dar es salaam.
  Waziri wa Afya ,Maendeleo ya jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wa kwanza kulia akimkabidhi nyenzo za kazi Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Ushauri TFDA Balozi Dkt. Ben Moses kushoto wakati wa Uzinduzi wa hiyo leo jijini Dar es salaam.
  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa Nchini(TFDA) Bw. Hiiti Sillo wa pili kushoto akifafanua jambo kwa Waziri wa Afya ,Maendeleo ya jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wa kwanza kulia wakati wa Uzinduzi wa Bodi ya ushauri ya mamlaka hiyo leo jijini Dar es salaam.
  Waziri wa Afya ,Maendeleo ya jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akipata maelekezo kutoka kwa wataalamu wa maabara za Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini (TFDA )wakati wa Uzinduzi wa Bodi ya ushauri ya mamlaka hiyo leo jijini Dar es salaam.
   

  0 0


  Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dk. Medard Kalemani akisisitiza jambo katika moja ya vikao vyake.

  Na Greyson Mwase, Shinyanga

  Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani ameitaka kampuni ya Pangea Minerals Ltd ya Canada inayofanya shughuli za utafutaji wa madini ya dhahabu katika kijiji cha Mwakitolyo Mkoani Shinyanga kuachia sehemu ya Leseni yake ili eneo hilo litengwe na kumilikishwa Wachimbaji Wadogo.

  Akizungumza na uongozi wa Mkoa wa Shinyanga pamoja na Wawakilishi wa Wachimbaji Wadogo pamoja na Uongozi wa Kampuni ya Pangea Minerals Ltd mkoani Shinyanga, aliitaka kampuni hiyo ambayo imeanza mazungumzo ya kuuza eneo hilo kwa kampuni ya Busolwa Mining Ltd, kuachia sehemu ya leseni yake yenye namba PL 5044/2008 ambayo kwa sasa wananchi wanaokadiriwa kufikia 3000 wanajishughulisha na uchimbaji mdogo wa dhahabu katika eneo hilo tangu mwaka 2011.

  Alifafanua kuwa ili kuepuka mgogoro huo ambao umedumu kwa muda mrefu kati ya kampuni hiyo na wananchi hao, ni vyema kampuni hiyo itoe ushirikiano kwa kijiji hicho kwa kuachia sehemu ya leseni yake ili wananchi nao wapate maeneo ya kufanyia shughuli za uchimbaji wa madini.

  Dk. Kalemani aliitaka kampuni hiyo kuachia eneo hilo kwa Kamishna wa Madini ifikapo Agosti 17, 2016 ambapo eneo hilo litaanza kugawanywa kwa wananchi kuanzia Septemba 2, 2016. Wakati huohuo Naibu Waziri Kalemani aliwataka wachimbaji wadogo kuheshimu sheria za nchi na kukubali kuhamia eneo litakalotengwa kwa ajili yao ifikapo tarehe 2 Septemba, 2016.

  Naye Mwakilishi na Mkurugenzi kutoka kampuni ya Pangea Minerals Limited Ltd, Deo Mwanyika alikubali maamuzi hayo na kueleza kuwa kampuni ipo tayari kukabidhi sehemu ya leseni hiyo ili iweze kutumiwa na wananchi. Naye Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga aliipongeza serikali kwa mikakati yake ya kusaidia wachimbaji wadogo kwa kuwapatia maeneo ya kujiajiri kwa ajili ya kujiongezea kipato.

  Aliwataka Wachimbaji Wadogo kutojihusisha na vitendo vya kiharakati na kuwarubuni baadhi ya wachimbaji na kupinga juhudi za Serikali kwa kuchochea vurugu migodini badala yake wayatumie maeneo hayo waliyotengewa kwa shughuli za kiuchumi. Eneo la Mwakitolyo ni kati ya maeneo yenge utajiri wa dhahabu hapa nchini yanayomilikiwa na kampuni ya Acacia kupitia kampuni yake tanzu ya Pangea Minerals Ltd.

  0 0

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof.Makame Mbarawa amemsimamisha kazi Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), Captain Johnson Mfinanga na Mkurugenzi wa Uendeshaji, Captain Sadick Muze kwa kosa la  kuchagua rubani mmoja ambaye hajakidhi vigezo anavyotakiwa kuwa navyo marubani wanaotarajia kuondoka kesho kuelekea nchini Canada kwa  ajili ya mafunzo  ya kurusha ndege mpya mbili zinazotarajiwa kuwasili nchini katikati ya mwezi Septemba.

  Akizungumza na waandishi wa habari wilayani Kyela, Mkoani Mbeya Prof. Mbarawa amesema baada ya kukamilisha malipo ya awali ya ununuzi wa ndege mbili mpya kwa ajili ya ATCL  alitoa maelekezo kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu huyo kuwachagua marubani watano wenye vigezo ambavyo vinahitajika kwa ajili ya mafunzo hayo jambo ambalo amebaini mmojawapo wa waliochaguliwa hajatimiza vigezo na hivyo kuamua kumsimamisha kazi kwa kosa la uzembe.

  Waziri  Mbarawa amesisitiza kuwa msimamo wa serikali ni kuhakikisha kila mtumishi  wa umma anatekeleza wajibu  wake kwa kufuata sheria kanuni na taratibu hivyo atakaye kiuka msimamo huo Serikali haitasita kumchukulia hatua za kinidhamu.

  Shirika la Ndege Tanzania katika mwaka huu wa fedha Serikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni 500 kwa ajili ya ununuzi wa ndege tatu.

  0 0
  0 0


  Muonekano wa Kivuko cha MV Tanga, kitakachotoa huduma ya usafirishaji katika Wilaya ya Pangani mkoani Tanga ambacho ukarabati wake umekamilika tayari kwa kuanza kazi.
  Muonekano wa Kivuko cha MV Magogoni ambacho ukarabati wake upo katika hatua za mwisho chenye uwezo wa kubeba tani mia tano, abiria elfu mbili na magari sitini, kivuko hicho kitaanza kutoa huduma kati ya Magogoni na Kigamboni katikati ya mwezi huu
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamhanga, amekagua na kuridhika na hatua ya ujenzi na ukarabati wa vivuko vitatu na tishari moja unaoendelea Jijini Dar es Salaam.

  Akizungumza mara baada ya kukagua ukarabati wa kivuko cha MV Magogoni, MV Tanga, New MV Magogoni na Tishari litakalotumiwa na Kivuko cha MV Dar es Salaam Eng. Nyamhanga amewapongeza mafundi wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) na kampuni ya M/S Songoro Marine Transport Boat Yard Ltd kwa kufanya kazi kwa kasi na ubora unaotakiwa.

  “kazi yenu ya ujenzi na ukarabati wa kivuko cha MV Magogoni, MV Tanga, Kivuko kipya cha Magogoni na Tishari inafanyika kwa viwango vinavyokubalika na hivyo baadae mwezi huu, vivuko vya MV Tanga na MV Magogoni vitaanza kazi, Hongereni”, amesema Eng. Nyamhanga.

  Eng. Nyamhanga amesisitiza nia ya Serikali kuhakikisha Ujenzi na Ukarabati wa vivuko unafanyika hapa nchini ili kuzipa nguvu kampuni za kizalendo na kupunguza gharama za utengenezaji na ukarabati nje ya Nchi.

  Kukamilika kwa Kivuko cha MV Magogoni chenye uwezo wa kubeba abiria 2000 na magari 60 kutapunguza msongamano katika kivuko cha Kigamboni na kuimarisha huduma ya usafiri kati ya Kigamboni na Magogoni.

  “Hakikisheni ujenzi wa Tishari na Kivuko kipya cha Magogoni unakwenda kwa kasi, ili kukamilisha mkakati wa Serikali wa kuhuisha usafiri wa majini hapa nchini.” Amesisitiza Eng. Nyamhanga.

  Naye Kaimu Mtendaji Mkuu wa TEMESA Eng. Manase Ole Kujan amemhakikishia Katibu Mkuu sekta ya ujenzi kuwa, ushirikiano kati ya TEMESA na kampuni ya Songoro, katika ujenzi na ukarabati wa Vivuko na Tishari ni mzuri na utakamilika kwa wakati.

  Kukamilika kwa Kivuko kipya cha Magogoni kunafanya TEMESA kuwa na vivuko 30 vinavyotoa huduma katika maeneo mbalilmbali nchini kote.

  Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.


  Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Eng. Joseph Nyamhanga akikagua michoro ya vivuko vitatu na Tishari Moja ambavyo ujenzi wake upo katika hatua za mwisho za kukamilika jijini Dar es Salaam, katikati ni Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Eng. Manase Ole Kujan.
  Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Eng. Joseph Nyamhanga akipata ufafanuzi kuhusu hatua za mwisho za ukarabati wa Kivuko cha Mv Magogoni kutoka kwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Eng. Manase Ole Kujan.
  Nahodha wa Kivuko cha Mv Tanga Bw. Gervas Mahai (katikati), akitoa maelezo kuhusu mfumo wa uendeshaji wa kivuko hicho ambacho ukarabati wake umekamilika kwa Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Eng. Joseph Nyamhanga alipokagua kivuko hicho jijini Dar esSalaam Kivuko hicho kitapelekwa Pangani wakati wowote kuanzia sasa.

  Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamhanga wa tano kutoka kushoto waliosimama akiwa na wajenzi wa Kivuko cha Mv Tanga na Mv Magogoni kutoka TEMESA na Kampuni ya M/s Songoro Marine Transport Boat Yard Ltd.

  0 0


  0 0older | 1 | .... | 926 | 927 | (Page 928) | 929 | 930 | .... | 1897 | newer