Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 925 | 926 | (Page 927) | 928 | 929 | .... | 1898 | newer

  0 0

   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe  Mary wakiteremka kuelekea eneo la kuchinjia ng'ombe katika kiwanda cha nyama Ngulu Hills Ranch kilichopo Morogoro wakati walipokitembelea kiwanda hicho Agosti 3, 2016. 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary (kulia) wakikagua eneo la kuchinjia ng'ombe katika kiwanda cha nyama cha Nguru Hills Ranch cha Morogoro Agosti 3, 2016. Kushoto ni Mkurugenzi na Mshauri wa Kiwanda hicho, Danstan Mrutu.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary wakizingumza na Mkurugenzi na mshauri wa kiwanda cha nyama cha Ngulu Hills Ranch cha Morogoro , Dunstan Mrutu (kulia kwa Waziri mkuu) ) wakati walipokitembelea kiwanda hicho Agosti 3, 2016
  Watoto na wananchi wa kijiji cha Majichumvi  wilayani Mvomero wakionyesha mabango wakati WaziriMkuu,Kassim Majaliwa aliposimama kijijini kwao kuwasikiliza Agosti 3, 2016.
   Waziri mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Bibi Halima Mwishehe alipouliza swali wakati Waziri Mkuu alipozungumza na Wananchi kwenye stendi mpya ya Msamvu Morogoro baada ya kukagua ujenzi wake Agosti 3, 2016.  Kulia ni Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dkt. Stephene Kebwe. 
  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).


  0 0  Serikali ya Tanzania inadhamini mchango mkubwa unaotolewa na Serikali ya Japani kupitia Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japani (JICA) ambalo limekuwa likishirikiana na Serikali katika kazi mbalimbali za maendeleo hapa nchini.

  Naibu Katibu Mkuu , Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bi. Susan Mlawi alisema hayo mapema leo katika ukumbi wa mikutano wa Utumishi wakati wa hafla fupi ya kuwakaribisha watalaam wa kujitolea kutoka Japani.

  “Tangu mwaka 1967 hadi sasa zaidi ya vijana wa Japani 1,500 wameshafika nchini na kufanya kazi za kujitolea katika maeneo mbalimbali hata katika mazingira magumu” Bi. Mlawi alisema na kuongeza kuwa kunufaika huko kwa Tanzania kunatokana na ushirikano baina ya Serikali ya Japani na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  Alisema Tanzania itaendelea kudumisha ushirikiano huo na Japani ili kuendelea kunufaika hasa katika suala zima la kujengewa uwezo katika sekta ya elimu na maendeleo ya jamii , sekta ambazo pia zimepewa kipaumbele katika Awamu ya Pili ya Mpango wa Serikali wa miaka Mitano (5) wa Maendeleo inayoanza mwaka 2016/17 na kumalizika mwaka 2021 /22.

  Kwa upande wake, mwakilishi mkuu wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo Japani (JICA) nchini Tanzania Bw. Toshio Nagase alisema wataalam hao ambao wako sita (6) watafanyakazi ya kujitolea katika sekta ya elimu kwa miaka miwili na kwa kipindi hicho wanaamini Watanzania watakuwa wamenufaika na ujuzi toka kwa vijana hao.

  Alisema watajitolea kufundisha masomo ya Sayansi, Hisabati, Masuala ya Maendeleo ya Jamii na Michezo katika shule za Sekondari , Shule za Msingi na Ofisi za Maendeleo ya Jamii katika Mikoa ya Morogoro, Pwani , Mtwara , Dodoma na Dar es salaam.

  0 0  Zoezi la uchangiaji Damu likiendelea katika makao makuu ya TAZARA ambapo wafanyakazi mbalimbali wa Shirika hilo na watanzania wengine wamejitokeza kucnagia damu

  Wakati Mamlaka ya Reli Tanzania na Zambia TAZARA wakiadhimisha miaka 40 ya uwepo wake nchini Tanzania maadhimisho hayo yameenda sambamba na zoezi maalum la kuchangia damu zoezi ambalo limefanyika makao makuu ya TAZARA Dar es salaam Tanzania ambapo wafanyakazi wake wameitumia siku ya leo kuchangia damu zoezi ambalo liliongozwa na mpango wa Taifa wa damu salama Tanzania.
  Akizungumza na wanahabari wakati wa zoezi hilo Mkurugenzi mtendaji wa Tazara ENG BRUNO TANDU CHINGANDU amesema kutokana na uhitaji mkubwa wa Damu uliopo Tanzania wao kama TAZARA wameamua kusitisha shughuli za leo kwa ajili ya kufanya zoezi moja la kuchagia damu zoezi ambalo linaenda sambamba na maadhimisho ya miaka 40 ya kuanzishwa kwake.
  Mkurugenzi mtendaji wa Tazara ENG BRUNO TANDU CHINGANDU akizngumza na wanahabari wakati wakiendelea na zoezi la ucnagiaji wa Damu .Amesema kuwa zoezi hilo linaonyesha ni jinsi gani wafanyakazi wa TAZARA wamekuwa wakiguswa na maswala mbalimbali ya kijamii hususani swala la ukosefu wa Damu mahospitalini huku akiyataka mashirika mengine na watu mbalimbali kuhakikisha kuwa wanachangia damu mara kwa mara wawezavyo kwa lengo la kuokoa maisha ya watanzania wamaopoteza maisha yao kwa kukosa Damu.

  Aidha mmoja kati ya wahamashishaji kutoka mpango wa taifa wa Damu salama Tanzania Bi Mariam Juma amesema kuwa Tanzania imekuwa na uhitaji mkubwa damu kutokana na kuongezeka kwa maswala mbalimbali yakiwemo ya ajali,vifo vya mama na watoto wakati wa kujifungua wanaofariki kwa kukosa damu,na magonjwa mengine mengi hivyo akawataka watanzania kujitahidi na kuhakikisha kuwa angalau wanachangia damu kwa mwaka japo mara mbili ili kuokoa maisha ya watanzania wenzao.

  Mmoja kati ya wahamashishaji kutoka mpango wa Taifa wa Damu salama Tanzania Bi Mariam Juma akifafanua jambo juu ya umuhimu wa kucnagia Damu kwa watanzania

  Mwandishi wa mtandao huu wa HABARI24 BLOG alishuhudia wafanyakazi wa TAZARA wakijitokeza kwa wingi kuchangia Damu ambapo walimueleza mwandishi wetu kuwa ni swala la kizalendo na utu kwa mtanzania kujali na kusaidia watanzania wengine ambao wana uhitaji mkubwa wa damu nchini.  0 0


  warembo wanaoshiriki shindano la miss kanda ya kaskazini kutoka katika mikoa ya Arusha,Manyara,Tanga na Kilimanjaro wakiwa nje ya hotel ya Clous view sehemu ambayo wanafanyia mazoezi kwa ajili ya shindano hilo linalofanyika july 6 katika viwanja vya ukumbi wa Triple A fm

  warembo hao wakiwa katika pozi .

  Na Woinde Shizza,Arusha

  Jamii imetakiwa kuwapa ushirikiano wa kutosha wasichana wanaoshiriki mashindano ya urembo kwani mashindano hayo ni kazi kama vile kazi zingine.

  Hayo yamebainishwa na baadhi ya warembo wanaoshiriki shindano la kumsaka mrembo wa kanda ya kaskazini (Miss Kanda ya kaskazini )wakati walipokuwa wakiongea kwa nyakati tofauti na mwanandisi wa habari hizi ndani ya hotel ambayo warembo hao wameweka kambi kwa ajii ya shindano hilo linalotarajiwa kufanyika mapema jumamosi July 6 katika ukumbi wa Triple A uliopo jijini Arusha

  MMoja wa washiriki hao aliyejitambulisha kwa jina la Mariamu Mohmed (18) Mshiriki kutoka mkoa wa Manyara alisema kuwa wazazi wengi hususa ni ndugu wamekuwa wakichukulia shindano hili kama ni sehemu ya uhuni kitu ambacho sio cha kweli

  Alibainisha kuwa shindano hili ni zuri na linatoa ajira kwa vijana wengi na mbali na ajira pia linasaidia vijana wengi ambao ni wasichana kujiajiri wenyewe na wengine kuajiriwa katika sehemu mbalimbali.

  Kwa upande wake mshiriki kutoka mkoani Tanga Rukaiya Hassan (20) alisema kuwa kuingia katika urembo sio uhuni wala umalaya kwani ,mtu kuwa na tabia chafu kama izi ni hulka yake mwenyewe na sio mashindano haya ndio yanasababisha mshiriki au mshindi kuwa muhuni

  Aidha mshiriki kutoka mkoani Arusha Maurine Ayubu (20) alisema kuwa baadhi ya ndugu wa karibu wamekua wakiwakatisha tamaa washiriki wengine wakiwatenga kutokana na kile wanachodai kuwa ndugu aliyeshiriki shindano hili ni malaya kitu ambacho sio cha kweli na kinawakatisha tamaa warembo wengi ambao walikuwa na ndoto ya kushiriki mashindano hayo.

  "unajua mimi naona kila mtu na tabia yake ambayo anayo lakini swala la kusema kuwa kushiriki shindano hili ni umalaya sio la kweli nanaomba ndugu a ambao wananduguzao wanashiriki mashindano ya umiss wawape ushirikiano wa kutosha kwani hii ni kazi kama kazi zingine"alisema mshiriki kutoka mkoani Kilimanjaro Navia Samwel.

  Aidha pia aliongeza kuwa kwa upande wake anaamini kabisa atashinda katika kinyaganyiro hicho kwani anajiamini na aliwasihi wenzake iwapo itatokea mtuakitolewa nje asibaatike kuingia katika hatua yatano bora asikate tamaa kwani anaweza pia kushiriki katika mambo mengine ikiwa ni pamoja na uwana mitindo.

  Kwa upande wake muaandaaji wa shindano hilo mkurugenzi wa mwandago ivestiment Faustine Mwandago alisema kuwa maandalizi ya shindano hilo yameshakamilika wanasubiri tu siku ya tukio ifike kwani warembo wamepikwa wakapikia vya kutosha .

  0 0

   
  Mkuu wa Mafunzo na Utendaji Kivita, Meja Generali Issa Nassoro (kushoto) akimkabiodhi Bendera Mkuu wa Msafara wa timu teule za jeshi, Brigedia Generali, Jairos Mwaseba, timu zinatarajia kushiriki mashindano ya Afrika Mashariki yanayoanza Agosti 5 hadi 18 Kigali Rwanda. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam Agosti 3. 2016. (Picha na Seleman Semunyu, JWTZ)

  0 0

  Na Dotto Mwaibale

  KITUO cha Televisheni cha TV1 Tanzania kinatarajia kuanza kurusha matangazo ya moja kwa moja ya mpira wa miguu ya ligi kuu soka ya Uingereza EPL matangazo ambayo yanatarajia kurushwa kuanzia Agosti 13 mwaka huu.

  Ligi kuu soka nchini Uingereza ndio ligi maarufu zaidi duniani na hii ni kutokana na kushirikisha timu kongwe zenye ubora na mashabiki dunia nzima ikiundwa na timu maarufu duniani kama vile Manchester United,Liverpool, Arsenal pamoja na Chelsea.

  TV1 Tanzania ndio kitakuwa kituo pekee cha runinga hapa nchini kupewa haki za kurusha matangazo haya yatakayokujia moja kwa moja yaani Live yakihusisha pia uchambuzi wa ligi hiyo ambapo kutakuwa na vipindi vya kabla ya mechi na baada ya mechi husika.

  Kwa upande Mkuu wa Kituo cha TV 1 Tanzania Joseph Sayi alisema hii ni fursa kubwa kwa wadau wa soka hapa nchini kuishuhudia ligi hiyo moja kwa moja, Mkuu wa kitengo cha masoko wa TV1 Gillian Rugumamu alisema lengo ni kuwapelekea watazamaji wao wa Tanzania ligi kuu England ambayo ni ligi inayopendwa na kufuatiliwa na Watanzania.

  Baadhi ya watangazaji na wachambuzi watakaokuwa wakishiriki katika urushaji wa matangazo hayo na uchambuzi ni Ally Kashushu na Dkt. Leakey Abdallah ambaye ni mchambuzi mwenye uzoefu wa miaka 20 kwenye tasnia ya michezo husasani uchambuzi.

  Mchambuzi wa Michezo Dk. Leakey alisema watanzania wategemee uhondo wa ligi hiyo kutokana na uwepo wa wachezaji nyota na makocha mahiri kama Antonio Conte,Arsene Wenger,Jurgen Klopp na makocha hasimu Jose Mourinho wa Manchester United na Pep Guardiola wa Manchester City.

  Tv1 Tanzania ni kituo cha runinga kilianza mwaka 2013 ambapo kilianza kurusha matangazo yake rasmi Januari 2014 ambapo kimekuwa kikiandaa na kurushwa vipindi vyenye ubora wa hali ya juu ambapo TV 1 inapatikana kupitia ving’amuzi vya Startimes namba 103,Azam 119 na Ting 36.  Mkuu wa TV 1, Joseph Sayi (katikati),akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu ,Kituo cha Televisheni cha TV1 Tanzania kuanza kurusha matangazo ya moja kwa moja ya mpira wa miguu ya ligi kuu soka ya Uingereza EPL matangazo ambayo yanatarajia kurushwa kuanzia Agosti 13 mwaka huu. Kulia ni Meneja Masoko wa TV 1, Gillian Rugumamu na Meneja Masoko Startimes, kushoto ni Felix Awino  Meneja Masoko wa TV 1, Gillian Rugumamu (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu ,Kituo cha Televisheni cha TV1 Tanzania kuanza kurusha matangazo ya moja kwa moja ya mpira wa miguu ya ligi kuu soka ya Uingereza EPL matangazo ambayo yanatarajia kurushwa kuanzia Agosti 13 mwaka huu. Kushoto ni Mkuu wa TV 1, Joseph Sayi na kulia ni Mchambuzi wa Michezo Dk. Leakey Abdallah.
  Mchambuzi wa Michezo Dk. Leakey Abdallah (katikati), akizungumzia masuala ya mpira katika mkutano huo.
  Production Meneja wa TV 1, Mukhsin Khalfan Mambo akizungumza katika mkutano huo.
  Mkutano ukiendelea.
  Wanahabari wakiwa kazini.
  Taswira ya meza kuu katika mkutano huo.
  Mchambuzi wa michezo, Ally Kashushu (kushoto), akizungumza katika mkutano huo.


  Mmiliki wa Blog ya Kajuna Son, Cathibert Kajuna (kulia), akiuliza swali katika mkutano huo.
  Wapiga picha za habari wakiwa kazini.


  Baadhi ya wafanyakazi wa TV 1 wakiwa wakifuatilia matukio mbalimbali ya mkutano.
  Mkutano ukiendelea.

  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wafugaji wenye mifugo mingi nchini kujiweka tayari kwa ajili ya kuhamia kwenye maeneo yatakayotengwa na Serikali katika ranchi mbalimbali nchini ili waweze kufuga kisasa.

  Pia aliwataka wafugaji hao kushirikiana na Serikali katika kuboresha miundombinu ya maeneo hayo ikiwemo ujenzi wa visima vya maji na majosho ili ufugaji wao uwe na tija.

  Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumatano, Agosti 03, 2016) wakati alipotembelea kiwanda cha kusindika nyama cha Nguru Hills Ranch kilichoko wilayani Movomero.

  Hata hivyo Waziri Mkuu alisema kitendo cha wafugaji hao kuhamia katika ranchi kitawezesha mifugo yao kuwa na ubora kwa sababu aina ya ufugaji wa sasa ya kutembeza mifugo umbali mrefu inasababisha ufugaji wao kuwa na tija ndogo.

  Akizungumzia kuhusu uwepo wa kiwanda cha kuchakata nyama wilayani Mvomero Waziri Mkuu alisema kitamaliza mgogoro wa muda mrefu kati ya wakulima na wafugaji kwa kuwa wafugaji watapata fursa ya kuuza mifugo yao kiwandani hapo.

  “Uwepo wa viwanda katika maeneo yetu utatuwezesha kupunguza matatizo tuliyonayo katika maeneo yetu ikiwemo suala la migogoro kati ya wafugaji na wakulima. Viwanda ndiyo vitakavyotuondoa kutoka katika uchumi wa chini hadi wa kati,” alisema.

  Kwa upande wake Mkurugenzi na Mshauri wa kiwanda cha Nguru Hills Ranch, Dunstan Mrutu alisema kiwanda hicho chenye uwezo wa kuchinja ng’ombe 300, mbuzi na kondoo 1,500 kwa siku kinatarajiwa kufunguliwa mwezi Desemba mwaka huu.

  Mkurugenzi huyo alisema takriban asilimia 80 ya nyama itafungashwa na kuuzwa nje ya nchi hasa Uarabuni kwa sababu nyama ya mbuzi ya Tanzania imebainika kuwa na mvuto maalum katika nchi hizo.

  “Mbali na uwekezaji huu wa kiwanda cha nyama pia tunatazamia kuwekeza katika mnyororo wa thamani kuanzia kusindika ngozi inayotoka kiwandani hadi kuzalisha viatu, mikanda na bidhaa zote za ngozi na kupunguza uagizaji wa bidhaa hizo kutoka nje ya nchi,” alisema.

  Mrutu alisema nia yao ni kuitikia wito wa Rais Dk. John Magufuli wa kutaka viwanda vizalishe viatu nchini kuanzia vya majeshi na wananchi wote ambapo wamepanga kuanzia mwakani wataanza kuuza bidhaa hizo.

  Aliongeza kuwa uwepo wa kiwanda hicho utatoa fursa kwa wafugaji na wakulima kuuza majani, mifugo na mazao ya chakula kama mtama, mahindi, ambapo tayari wameanza kuhamasisha jamii za wafugaji na wakulima wa Mvomero, Ngerengere na sehemu zinazozunguka eneo la kiwanda kuchangamkia fursa hiyo.

  Katika hatua nyingine Waziri Mkuu ameuagiza uongozi wa wilaya ya Mvomero kufanya mapitio ya mashamba ili kujua wamiliki wake na kama hawajayaendeleza wachukue uamuzi wa haraka wa kuyatwaa na kuyarudisha mikononi mwa Serikali.

  Waziri Mkuu alitoa agizo hilo wakati akijibu ujumbe uliokuwa katika mabango yaliyobebwa na wananchi wa kijiji cha Maji ya Chumvi wilayani Mvomero waliosimamisha msafara wakati ukitokea kwenye kiwanda cha nyama.

  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU, JUMANNE, AGOSTI 02, 2016.

  0 0  Muwakilishi wa Balozi wa China nchini Tanzania,Gou Haodong akimkabidhi moja ya dawati kati ya 100 yaliyotolewa na Wafanyabiashara wa Karikoo wenye asili ya China ,kwa Mkuu wa Wa Wilaya ya Ilala,Mh Sophia Mjema mapema leo jijini Dar.
  Mkuu wa Wilaya ya Ilala,Mh Sophia Mjema akizungumza kwenye hafla fupi ya kukabidhiwa madawati 200 kutoka kwa Wafanyabiashara wa Kariakoo wenye asili ya China leo jijini Dar,kwa ajili ya shule ya msingi Maghorofani iliyopo Gongolamboto,jijini Dar Es Salaam.Wafanyabiashara hao waliahidi kumkabidhi Mh.DC Mjema Madawati 200 lakini leo wamekabidhi nusu ya madawati hayo (100),huku mengine yakiendelea kutengenezwa.Shule hiyo ya Maghorofani ilikuwa na uhitaji wa madawati 525,yakapatikana madawati 250 na kupungukiwa madawati 275.
  Muwakilishi wa Balozi wa China nchini Tanzania,Gou Haodong akizungumza kwa ufupi mbele ya Waalimu,wageni waalikwa mbalimbali (hawapo pichani),kabla ya kukabidhi madawati 100 yaliyotolewa na Wafanyabiashara wa Kariako wenye asili ya China jijini Dar,pichani kulia ni Mkuu wa Wa Wilaya ya Ilala,Mh Sophia Mjema. 
  Baadhi ya Wanafunzi wa shule hiyo ya Maghorofani wakiwa wamekalia baadhi ya madawati yaliyotolewa na Wafanyabiashara wa Kariakoo wenye asili ya China jijini Dar. 
  Wakiwa katika picha ya pamoja .PICHA NA MICHUZI JR.

  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa siku moja kwa uongozi wa Manispaa ya Morogoro kutenga maeneo maalumu kwa ajili ya wafanyabiashara wadogo na kuyatangaza kesho.

  “Mbali na kutenga maeneo pia nawaagiza muwasaidie wafanyabiashara hawa kuunda vikundi kulingana na aina ya biashara wanazozifanya ili kuwawezesha kupata mikopo kwa urahisi kutoka katika taasisi za fedha” alisema.

  Waziri Mkuu alitoa agizo hilo leo (Jumatano, Agosti 03, 2016) wakati alipotembelea mradi wa ujenzi wa kituo cha mabasi Msamvu unaojengwa kwa ubia kati ya Manispaa ya Morogoro na Mfuko wa Pensheni wa LAPF.

  Awamu ya kwanza ya mradi huo inatarajiwa kufunguliwa Agosti 12 mwaka huu utakuwa ni kituo cha mabasi cha kwanza cha kisasa Tanzania ambapo Waziri Mkuu amezitaka halmashauri zote zilizoko makao makuu ya mikoa nchini kuiga mfano huo.

  Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kulipongeza Baraza la Madiwani la Manispaa ya Morogoro na LAPF kwa kubuni mradi huo wa kisasa utawezesha abiria kupata taarifa ya basi lilipo na muda litakapowasili kituoni hapo hivyo kupunguza udanganyifu kutoka kwa mawakala wasiokuwa waaminifu.

  Kwa upande wake Meneja wa mradi huo Stanley Mhapa alisema mradi huo umegharimu sh. bilioni 40 ambapo Manispaa inamiliki asilimia 40 ya hisa na mfuko wa LAPF unamiliki asilimia 60.

  “Mafanikio ya mradi huu ni pamoja na kuiwezesha Manispaa kuongeza ukusanyaji wa mapato kutoka sh 350,000 kwa siku hadi kufikia sh. milioni 1.7 kwa siku,” alisema.

  Mhapa alisema mradi huo utakapokamilika utatoa huduma mbalimbali ikiwa ni pamoja na huduma za kibenki, vibanda vya biashara, sehemu za chakula, ofisi na sehemu ya mapumziko ya abiria na vibanda vya kukatia tiketi.

  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU, JUMATANO, AGOSTI 03, 2016.

  0 0


  Mshiriki Mkuu wa Shindano la Kanumba Star Search, Florence Mutegoa (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Kampuni ya AM Arts Promotion pamoja na Mdhamini wa Shindano la “Kanumba Star Search” kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) leo tarehe 03.08.2016 Jijini Dar es Salaam,
   
  Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO

  Mshiriki Mkuu wa Shindano la Kanumba Star Search, Florence Mutegoa (Mama Kanumba) amezindua shindano la kusaka vipaji vya waigizaji watakaoigiza filamu itakayoenzi maisha ya Marehemu Steven Kanumba.

  Uzinduzi huo umefanywa leo Jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) ambapo Mshiriki Mkuu wa Shindano hilo ametoa rai kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kudhamini shindano hilo litakaloibua vipaji vipya vya uigizaji.

  “Tunatambua thamani ya maigizo ndio sababu tumeamua kuanzisha shindano hili ili kuibua vipaji vilivyojificha, hivyo tunawakaribisha wananchi wote wenye uwezo wa kuigiza waje washiriki kwenye mashindano yetu pia tunaomba wadhamini kujitokeza zaidi ili watusaidie kufanikisha shindano hili”, alisema Mutegoa. Mutegoa amefafanua kuwa shindano hilo limeandaliwa kwa ushirikiano wa Kampuni ya Kanumba the Great Film na Kampuni ya AM Arts Promotion ambapo hadi sasa shindano hilo lina mdhamini mmoja kutoka Kampuni ya simu za mkononi za KZG – Tanzania.

  Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya AM Arts Promotion, James Mwombeki amesema kuwa marehemu Kanumba alikuwa na mchango mkubwa katika kuitangaza nchi kimataifa pamoja na kuibua vipaji vya wasanii wa maigizo hivyo hatuna budi kumuenzi kwa kuiendeleza Sanaa ya uigizaji. “Sisi kama AM Arts Promotion tumeamua kushirikiana kwa pamoja na Mama Kanumba kufanya shindano hili kwa nia ya kuendeleza tasnia ya filamu nchini kama vile marehemu Kanumba alivyokua akijitahidi kuwapa fursa ya uigizaji watu wa kila rika”, alisema Mwombeki.

  Naye, Msanii wa filamu, Mayasa Mrisho amewasisitiza wananchi kushiriki kwa wingi kwenye mashindano hayo kwani Sanaa ya uigizaji ni njia mojawapo ya kujipatia kipato na kuinua maisha ya mtu binafsi na Taifa kwa ujumla. Aidha, Mkurugenzi wa Kampuni ya Simu za Mkononi za KZG – Tanzania, Raymond Kalikawe amesema kuwa wamekubali kuwa wadhamini wa shindano hilo kwa kuwa ukuzaji wa vipaji vya wasanii wa maigizo ni jambo muhimu pia amewaomba wadhamini wengine kujitokeza zaidi kusaidia shindano hilo.

  Shindano hilo linatarajiwa kuanza mwezi Septemba mwaka huu, litaanzia Mikoa ya Kanda ya ziwa na baadae kuendelea katika Mikoa mingine.Washindi wataigiza filamu ya kumuenzi marehemu Kanumba itakayojulikana kama “Maisha ya Kanumba.

  0 0


  Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, Abdulrahman Kaniki akizungumza na Washiriki wa Mkutano wa kutathmini mradi wa kupambana na ukimwi na kifua kikuu unaotekelezwa na Jeshi la Polisi katika vituo vyake vya Afya kumi na tano hapa nchini kwa ufadhili wa shirika lisilo la kiserikali la JSI-AIDS Free tawi la Tanzania.Mkutano huo wa siku tatu unafanyika mkoani Dodoma.(Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi)

  Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, Abdulrahman Kaniki akizungumza na Washiriki wa Mkutano wa kutathmini mradi wa kupambana na ukimwi na kifua kikuu unaotekelezwa na Jeshi la Polisi katika vituo vyake vya Afya kumi na tano hapa nchini kwa ufadhili wa shirika lisilo la kiserikali la JSI-AIDS Free tawi la Tanzania.Mkutano huo wa siku tatu unafanyika mkoani Dodoma.Kulia ni Mganga mkuu wa Polisi Dk.Janda Lushina na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, SACP Lazaro Mambosasa (Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi)
  Baadhi ya Maofisa wa Polisi ambao ni Washiriki wa Mkutano wa kutathmini mradi wa kupambana na ukimwi na kifua kikuu ndani ya Jeshi la Polisi wakifurahia jambo wakati wa ufunguzi wa mkutano huo mkoani Dodoma.Mradi huo unaotekelezwa na Jeshi la Polisi katika vituo vyake vya Afya kumi na tano hapa nchini kwa ufadhili wa shirika lisilo la kiserikali la JSI-AIDS Free tawi la Tanzania. (Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi


  Na Frank Geofray-Jeshi la Polisi, Dodoma .

  Jeshi la Polisi nchini litaendelea kuboresha vituo vyake vya afya ili kuwawezesha Askari kupata huduma zilizo bora jambo ambalo litawawezesha kufanya kazi wakiwa na afya pamoja na morali katika kupambana na uhalifu nchini. 

  Hayo yamesemwa na Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, Abdulrahman Kaniki Mkoani Dodoma wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa kutathmini mradi wa kupambana na ukimwi na kifua kikuu unaotekelezwa na Jeshi la Polisi katika vituo vyake vya Afya kumi na tano hapa nchini kwa ufadhili wa shirika lisilo la kiserikali la JSI-AIDS Free tawi la Tanzania. 

  Kaniki alizitaja juhudi zinazoendelea kuchukuliwa kuwa ni pamoja na kuboresha majengo, kutoa mafunzo kwa watendaji pamoja na kuhakikisha kuwa hospitali za Polisi zinakuwa na vifaa bora kwa mujibu wa viwango vilivyowekwa na Wizara ya Afya .
  Aidha alitoa wito kwa Shirika la JSI-AIDS Free kuongeza wigo wa huduma zake katika vituo vngine ambavyo havijafikiwa na mradi huo hapa nchini ili kuhakikisha kuwa kila mahali palipo na kituo cha Afya cha Polisi kunakuwepo na mradi huo ambao umesaidia sana askari na watumiaji wengine wa huduma hizo. 

  Kwa upande wake Mwakilishi mkazi wa Shirika hilo kwa upande wa Tanzania Dk.Beati Mboya alisema lengo la mkutano huo ni kufanya tathmini ili kubaini mafanikio na changamoto zinazovikabili vituo vinavyotekeleza mradi huo ilikuzipatia ufumbuzi.
  Alisema wanatarajia kufanya tathmini hiyo kila baada ya miezi mitatu ili kuhakikisha hakuna ucheleweshaji katika kutoa huduma baada ya kubaini changamoto na kuzifanyia kazi kwa haraka. 

  Naye Kamanda wa Kikosi cha Afya cha Jeshi la Polisi, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Paul Kasabago alisema kikosi hicho kitaendelea kutoa huduma zilizobora ili kuimarisha afya za Askari na familia zao kote nchini licha ya kukabiliwa na upungufu wa wahudumu wa Afya.

  0 0


  Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Mhe.Anthony Mavunde akiongea na waandishi wa Habari leo Jijijni Dar es salaam kuhusu maadhimisho ya siku ya Vijana Duniani inayoadhimishwa Kitaifa tarehe 14/10/2016,Mkoani Simiyu ambapo vijana wametakiwa kutumia fursa zilizopo kujiletea maendeleo ya kiuchumi na kijamii.Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Habari Maelezo Bi Zamaradi Kawawa na Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Vijana Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajiara na Wenye Ulemavu.
  Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Mhe.Anthony Mavunde akisisitiza umuhimu wa wa wadau mbalimbali kujitokeza kusaidia jitihada za Serikali kuwawezesha Vijana kiuchumi. Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Vijana Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajiara na Wenye Ulemavu.
  Baadhi ya Waandishi wa habari wakifuatilia mkutano wa Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Mhe.Anthony Mavunde na waandishi wa Habari leo Jijijni Dar es salaam kuhusu maadhimisho ya siku ya Vijana Duniani itakayoadhimishwa Kitaifa tarehe 14/10/2016,Mkoani Simiyu. (Picha na Frank Mvungi-Maelezo

  Frank Mvungi-Maelezo

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa Mgeni rasmi siku ya Kilele cha maadhimisho ya siku ya Vijana Kitaifa yatakayofanyika Mkoani Simiyu Oktoba 14 mwaka huu.

  Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Antony Mavunde wakati wa mkutano na waandishi wa Habari. Mhe Mavunde amebainisha kuwa Kauli mbiu ya Siku ya Vijana mwaka huu ni “Tokomeza umasikini kwa uzalishaji endelevu na matumizi yenye tija”.

  Akifafanua kuhusu kauli mbiu hiyo Mhe. Mavunde amesema lengo la kauli mbiu hii ni kuzihimiza nchi wanachama wa umoja wa mataifa kushirikisha kikamilifu Vijana katika shughuli za uzalishaji na kuhakikisha kuwa panakuwepo na matumizi sahihi ya rasilimali za nchi kama vile ardhi,maji,madini na Nishati ili kufikia shabaha ya kuwa na maendeleo endelevu ifikapo 20130.

  Akizungumzia maadhimisho hayo Kitaifa Mhe . Mavunde amesema kuwa vijana watapata fursa ya kushiriki shughuli mbalimbali kama makongamano,matamasha,michezo,maonnyesho ya Kazi za Vijana,Shughuli za kujitolea na maandamano ya amani.

  “Tanzania tutasherekea siku ya Vijana Duniani Kitaifa kuanzia tarehe 8/10/2016 na kilele kitakuwa tarehe 14/10/2016 Mkoani Simiyu ambapo Sherehe hii itaenda sambamba na Maadhimisho ya kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere, Wiki ya Vijana Kitaifa na kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2016.” Alisisitiza Mhe. Mavunde.

  Wazo la kuwa na siku ya Vijana Duniani lilitolewa katika Mkutano wa Vijana wa Kimataifa mwaka 1991 Mjini Vienna Australia kwa madhumuni ya kutafuta njia ya kuchangisha fedha za kusaidia mifuko ya Taifa ya Vijana ambapo mwaka 2000 nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa ikiwemo Tanzania zilianza kuadhimisha siku ya Vijana Duniani kulingana na mazingira yake kwa kuzingatia kauli mbiu ambayo huandaliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.

  0 0

  Na Rahma Khamis Maelezo -Zanzibar

  Wananchi wa Zanzibar wametakiwa kulipia huduma ya maji kwa wakati ili kuweza kupata huduma hiyo kwa ufanisi zaidi na kuepukana na usumbufu unaoweza kujitokeza.

  Wito huo umetolewa na Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA) Zahour Suleiman Ofisini kwake Msikiti Mabuluu Mjini Zanzibar wakati akitoa maelezo kuhusiana na ulipaji wa huduma ya maji.

  Amesema maji ni moja ya huduma muhimu katika maisha ya wananchi hivyo ni muhimu kuhakikisha yanapatikana muda wote na suala la kulipia huduma hiyo ili iwe endelevu ni jambo la msingi.

  Afisa huyo amefahamisha kuwa badhi ya wananchi wamekuwa na mwamko mdogo katika kulipia huduma ya maji na kusababisha Mamlaka kukosa uwezo wa kutoa huduma hiyo kwa ufanisi.

  Aidha amesema kuwa kwa sasa huduma hiyo inaelekea kuzidiwa kutokana na kukuwa kwa harakati za kimaendeleo hasa kwa matumizi ya kilimo ambacho kinatumia maji mengi ukilinganisha na matumizi ya majumbani.

  Afisa huyo amefahamisha kuwa wameanzisha utaratibu wa kupita katika maeneo kwa lengo la kutoa elimu kuhusiana na umuhimu wa kulipia maji na wale watakaoshindwa kuufahamu mpango huo Mamlaka huwapa onyo na baadae kusitishwa kupata huduma.

  Sambamba na hayo Zahour amewashauri wanajamii kufuata sheria bila ya kushurutishwa kwa kulipia maji kwa wakati ili kuipa uwezo Mmlaka ya maji kutekeleza wajibu wake wa kuwapatia wananchi huduma hiyo kama kawaida.

  0 0

  Na Mathias Canal, Dodoma

  Ufunguzi wa siku kuu ya wakulima Nane nane Kanda ya kati Dodoma mwaka 2016 umefanyika leo katika Uwanja wa Maonyesho ya kilimo Nzuguni Mkoani Dodoma huku kauli mbiu ya mwaka huu ikiwa ni “Kilimo, Ufugaji na Uvuvi ni nguzo ya maendeleo, Kijana shiriki kikamilifu (Hapa Kazi Tu).

  Maonyesho haya yanahusisha shughuli za wakulima, wafugaji wa mifugo, wafugaji wa nyuki, wavuvi, wanamazingira, wasindikaji wa bidhaa za mazao ya kilimo na mifugo, wizara taasisi/makampuni ya umma, makampuni binafsi, mabenki, taasisi za umma na za binafsi na mashirika yasiyo ya kiserikali.

  Akizungumza katika ufunguzi huo Mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew Mtigumwe amesema kuwa sekta ya kilimo bado ni mhimili wa uchumi wa Tanzania kwa sababu inaajiri zaidi ya asilimia takribani 80 ya watanzania na kwa kuzingatia malengo ya maendeleo ya Taifa ya kuwa nchi yenye uchumi wa kati unaotegemea viwanda hivyo kilimo kikiboreshwa viwanda vitapata malighafi ya uhakika na kuimarisha masoko kwa wakulima hivyo kuwepo na ajira ya kuaminika kwa vijana na watanzania kwa ujumla.

  Rc Mtigumwe amesema kuwa wastani wa ukuaji wa sekta ya kilimo unabadilika mwaka hadi mwaka kutokana na kilimo kwa kiwango kikubwa kutegemea mvua ambazo zimekuwa zikinyesha kwa viwango na mtawanyiko unaotofautiana kila mwaka ambapo kwa mwaka 2010 sekta ya kilimo ilikuwa kwa asilimia 4 ikilinganishwa na asilimia 6.5 ya mwaka 2015.

  “Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali zinaonyesha kuwa kanda ya kati ina rasilimali ya maji yakutosha ya chini ya ardhi hivyo kuendelea kuitamka kama kanda kame hakuna usahihi wa jambo hilo ipo haja ya kuona kuwa rasilimali hiyo inapatikana kwa ajili ya kuendeleza kilimo cha umwagiliaji hivyo kupunguza kilimo cha kutegemea mvua” Alisema Mtigumwe


  Baadhi ya Wakuu wa Wilaya za Dodoma na Singida wakiongozwa na Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Singida Mathew Mtigumwe wakikagua eneo la maonyesho ya mboga mboga
  Baadhi ya Wakuu wa Wilaya za Dodoma na Singida wakiongozwa na Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Singida Mathew Mtigumwe wakikagua eneo la maonyesho ya bwawa la samaki lenye samaki aina ya perege, kambare na kamongo liloandaliwa na Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba .
  Zoezi la kutembelea mabanda ya maonyesho likiwa linaendelea .


  Mkuu wa Mkoa wa wa Singida Mhandisi Mathew Mtigumwe (Kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya Nane Nane katika uwanja wa maonyesho ya kilimo Nzuguni Mkoani Dodoma
  Viongozi wa Mkoa wa Dodoma na Singida wakitembelea baadhi ya vibanda vya maonyesho wakati wa ufunguzi wa Maonyesho ya Nane Nane
  Mgeni rasmi alipotembelea banda la dawa za kilimo, uvuvi na ufugaji Farmer Centre and Farm base
  Baadhi ya Wakuu wa Wilaya za Dodoma na Singida wakiongozwa na Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Singida Mathew Mtigumwe wakikagua eneo la maonyesho ya kilimo cha zao la zabibu 
  Mkuu huyo wa Mkoa wa Singida kabla ya kuwahutubia wananchi waliojitokeza katika ufunguzi huo alitembelea baadhi ya mabanda ya maonesho na kuona shughuli mbalimbali za uzalishaji wa mazao, ufugaji, uvuvi, usindikaji na wauzaji wa zana na pembejeo za kilimo ambapo amejionea matokeo ya juhudi mbalimbali zilizofanywa na serikali ya awamu ya tano katika kuinua ukuaji wa sekta ya kilimo ambapo juhudi hizo zinajumuisha uzalishaji wa mbegu mbalimbali zinazostahimili hali ya hewa ya maeneo ya kanda ya kati.

  “Natoa wito maalumu kwa wakulima, wafugaji, wavuvi, wajasiriamali na wadau wa sekta zingine kuhakikisha kuwa bidhaa zenu zinafikia ubora wa hali ya juu kuanzia shambani zinakozalishwa, zinakosindikwa na kuhifadhiwa na hadi kumfikia mlaji, ikumbukwe kwamba kwa kuzalisha bidhaa zenye ubora wa hali ya juu kutawezesha bidhaa zetu kuhimili ushindani wa hapa nchini na nje ya nchi na kuuzwa kwa bei nzuri” Alisema Mtigumwe

  Akitoa neno la shukrani kwa niaba ya waandaaji wa maonyesho ya Kilimo, Mifugo na sherehe za nane nane, Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Miraji Jumanne Mtaturu amesema kuwa hotuba ya Mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Singida itakuwa ya mazingatio ili kurahisisha na kuendeleza kasi ya serikali ya awamu ya Tano kwa vitendo hususani katika kuakisi na kuwasaidia wananchi ambao ni wakulima na wafugaji kupata mbinu bora za kufuga na kulima kisasa ili kupata mazao kwa wingi.

  Hata hivyo Dc Mtaturu amesema kuwa ana imani thabiti kuwa baada ya kumalizika kwa maonyesho hayo wakulima, wafugaji na wananchi washiriki watakuwa wamejifunza vyema mbinu bora za kukabiliana na changamoto za kilimo na ufugaji hivyo kujikita zaidi katika mbinu bora na za kisasa za kilimo na ufugaji pia.

  Dc Mtaturu amesema kuwa shughuli kuu ya wakazi wa kanda ya kati inayoundwa na mikoa miwili ya Singida na Dodoma yenye jumla ya Wilaya kumi na mbili na Halmashauri 15 shughuli zao kuu ni kilimo na ufugaji.

  0 0

  Na Ally Daud-Maelezo.

  Serikali chini ya Wizara ya Afya ,Maendeleo ya jamii, Jinsia , Wazee na Watoto imeitaka Taasisi ya Mifupa Muhimbili(MOI) kuhudumia wagonjwa haraka iwezekanavyo ili kuondoa msongamano wa wagonjwa hospitalini hapo na kuwaruhusu wakaendelee na shughuli za kujenga taifa.

  Akizungumza hayo alipotembelea wagonjwa  MOI Waziri wa  Afya ,Maendeleo ya jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu aliwataka watumishi wa taasisi hiyo kuwahudumia wagonjwa haraka iwezekanavyo ili kuwapa fursa ya kwenda kufanya shughuli za kimaendeleo kwa ajili ya taifa.

  “Mnatakiwa kuhudumia wagonjwa kwa haraka na ufanisi mkubwa ili kuwasaidia watanzania kutotumia muda mwingi wakiwa hospitalina na badala yake wapone waende wakaendelee na shughuli zao za kujenga taifa kwa maendeleo ya Nchi yetu”alisema Mhe. Ummy
  Aidha Mhe. Ummy ameongeza kuwa licha ya kuwa na changamoto zinazojitokeza hospitalini hapo Wizara ipo bega kwa began a Taasisi hiyo  kuhakikisha huduma bora zinatolewa kwa wananchi chini ya kitengo hiko ili kufikia malengo ya milenia.

   Waziri wa  Afya ,Maendeleo ya jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wa pili kushoto akitoa maagizo kwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) Dkt. Samuel Swai  wa kwanza kulia wakati alipotembelea  wagonjwa katika hospitali hiyo leo jijini Dar es salaam.
   Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) Dkt. Samuel Swai  wa kwanza kulia akifafanua jambo kwa Waziri wa  Afya ,Maendeleo ya jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu katikati alipotembelea  wagonjwa katika hospitali hiyo leo jijini Dar es salaam.
   Waziri wa  Afya ,Maendeleo ya jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiwajulia hali baadhi ya wagonjwa waliopo katika taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI)alipotembelea  wagonjwa katika hospitali hiyo leo jijini Dar es salaam.
  Waziri wa  Afya ,Maendeleo ya jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu katikati akimfariji mtoto Rahel Razaro wa kwanza kushoto aliyelazwa katika Taasisi ya Mifupa Muhimbili(MOI) alipotembelea  wagonjwa katika hospitali hiyo leo jijini Dar es salaam na wa kwanza kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Taasisi hiyo Dkt. Samuel Swai.

  “Nafahamu kama kuna changamoto zinazoikabili taasisi hii kama mlivyonieleza lakini tupo pamoja katika kuziondoa na nyinyi hakikisheni mnafanya kazi kwa bidii ili kuondoa  malalamiko ya wananchi na kuleta huduma bora na kwa wakati” alisisitiza Mhe. Ummy.

  Mbali na hayo Mhe. Ummy ameitaka taasisi hiyo kurudisha huduma ya kufanya upasuaji kwa wagonjwa siku za jumamosi bila ya kukosa tena kwa haraka ili kupunguza mlundikano wa wagonjwa kwenye taasisi hiyo.
  Kwa upande wa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji MOI Dkt. Samuel Swai amesema kuwa wamepokea agizo hilo na wapo tayari kufanya kazi kwa bidii ili kuokoa maisha ya watanzania kwa haraka na ubora zaidi.

  “Tupo tayari kutekeleza agizo la Mheshimiwa Waziri la kufanya kazi kwa bidii ili kuokoa maisha ya watanzania kwa haraka na ataona matokeo mazuri kuanzia leo hii” alisisitiza Dkt. Swai.
  Mwisho.

  0 0

  Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE), Mhandisi Steven Mlote(kushoto)akifafanua jambo kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam,wakati wa alipokuwa akitoa tamko la baraza hilo juu ya kuvifutia Usajili baadhi ya vyuo ambapo kati ya 175 vimepewa notisi ya kushushwa hadhi na 5 vimefutiwa Usajili na 41 vimetakiwa kujisajili mara moja ,ikiwa katika jitihada za kuboresha elimu ya ufundi nchini,Katikati Kaimu wa baraza hilo Dkt. Adolf Rutayuga na Mkurugenzi wa Udhibiti,Ufuatiliaji na Tathimini Bi. Agness Ponera.
  Baadhi ya wafanyakazi wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) wakiwa kwenye mkutano wakati Mwenyekiti wa Baraza hilo Mhandisi Steven Mlote(hayupo pichani)alipokuwa akiongea na waandishi habari jijini Dar es Salaam kuhusiana na tamko la baraza hilo kuvifutia Usajili baadhi ya vyuo ambapo kati hivyo 175 vimepewa notisi ya kushushwa hadhi na 5 vimefutiwa Usajili na 41 vimetakiwa kujisajili mara moja,ikiwa katika jitihada za kuboresha elimu ya ufundi nchini. 

  Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) limetangaza kuwa vyuo 5 vimefungwa kuendesha mafunzo na kufutwa kwenye rejista ya vyuo vya ufundi nchini.Pia Baraza limetangaza kuwa vyuo 41 vinavyotoa elimu ya ufundi bila kusajiliwa kwa mujibu wa sheria vimepewa muda wa wiki mbili na kutakiwa vijisajili mara moja kwenye Baraza hilo kabla ya kuchukuliwa hatua kali za kisheria.

  Vilevile, vibali vya  usajili wa vyuo 112 vya kutoa elimu ya ufundi vimefikia ukomo hivyo vinapaswa kutekeleza masharti ya Usajili; wakati  vyuo 57 vimefikia ukomo wa ithibati, hivyo inapaswa kutekeleza masharti ya ithibati, imetangazwa jana.

  Akiongea katika mkutano na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Baraza (NACTE), Mhandisi Steven Mlote, amesema Baraza limetoa muda wa mwezi mmoja kwa vyuo 112 kutekeleza masharti ya usajili na vyuo 52 kutekeleza masharti ya ithibati kwa mujibu wa sheria za uendeshaji vyuo vya ufundi nchini, na vyuo vitakavyoshindwa kutekeleza agizo hili vitafungiwa mara moja.

  0 0


  Na Mathias Canal, Singida


  Mkuu wa wilaya ya Ikungi Mh. Miraji Jumanne Mtaturu amsema hakuna demokrasia yoyote duniani inayohubiri wananchi kutoshiriki shughuli za maendeleo hivyo mwananchi anapaswakushirikishwa katika kuchagua viongozi wake, kukaa na viongozi wake kupanga miradi ya maendeleo kama vile kuchangia ujenzi wa shule, zahanati na maabara na maendeleo mengine.
  Ushiriki wa wananchi katika shughuli za maendeleo kwa kutumia nguvu na akili katika kukamilisha na kumiliki miradi ya kijamii ni njia mojawapo itakayowafanya wananchi kuwa na uchungu na mali pamoja na maendeleo katika jamii husika.

  Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu amesema kuwa kumekuwa na matumizi mabaya ya demokrasia katika Wilaya hiyo hususani katika shughuli za kijamii kama vile kuchangia ujenzi wa maabara jambo lililopelekea Wilaya hiyo kuwa ya mwisho katika ujenzi wa maabara kwa ajili ya shule za sekondari zilizopo katika Wilaya ya Ikungi. 

  “Wataalamu wa Sayansi na viongozi mashuhuri wamewahi kusema Demokrasia bila maendeleo sio demokrasia, Hayati Mwalimu julius Kambarage Nyerere na Profesa Issa Shivji waliwahi kuandika kuwa demokrasia ya kweli ni ile inayowasaidia wananchi kutoka katika hali moja kwenda kwenye hali nyingine ambayo ni bora zaidi kuliko ile waliyo nayo, hivyo tukiongelea kuwashirikisha wananchi katika mipango na mikakati ya kuondokana na umasiki na si vinginevyo” Alisema Mtaturu

  Dc Mtaturu amesema kuwa kuwa mwenyekiti wa Kijiji kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM), CHADEMA, ACT WAZALENDO, CUF au chama chochote hapaswi kuongoza wananchi kwa matakwa yake binafsi bali ni lazima kufuata taratibu, kanuni, sheria na taratibu zinazowaongoza katika kutekeleza majukumu yao.

  Ameyasema hayo wakati wa kikao cha kazi kati ya Mkuu waWilaya Wakuu wa idara na vitengo, Maafisa Tarafa, Weneyeviti wa Vijiji naWatendaji wa Kata na Vijiji katika mafunzo yaliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo.

  Amewaelekeza wenyeviti wa Vijiji kuwa majukumu yao ni kuongoza vikao vya Halmashauri ya Kijiji na kuongoza mkutano mkuu wa Kijiji sio kuuza ardhi ya kijiji kiholela, Kumnyang’anya mtu ardhi au kupiga faini yoyote wanayojisikia na ndio maana kunakuwa na watendaji wa Vijiji ambao ni wataalamu hivyo wana majukumu muhimu katika kuwashauri wenyeviti wa Vijiji.

  Dc Mtaturu pia amewataka viongozi hao kutambua kuwa uchaguzi ulimalizika Octoba mwaka jana na chama kilichoshika dola ni Chama Cha Mapinduzi(CCM) hivyo kutokana na uchaguzi huo Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilipewa ridhaa ya kuongoza Tanzania kwa kipindi cha miaka mitano 2015-2020 hivyo ilani inayotekelezwa na serikali ya awamu ya Tano ni ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) hivyo kwa vile kila kiongozi wa Kijiji yupo ndani ya serikali anapaswa kutelekeza ilani ya CCM kwani huo ni utaratibu wa vyama vinavyoshinda popote dunia.

  Baadhi ya watendaji wa Kata, Wenyeviti wa Vijiji, na baadhi ya watendaji wa Vijiji Wilayani Ikungi hawajawahi kupatiwa mafunzo ya muongozo wa kiutendaji hali iliyopelekea baadhi yao kutotimiza wajibu wao na wengine kufanya kazi nje ya mipaka yao.

  “ Kupitia kikao/mafunzo haya Uonevu wowote, kosa lolote, matumizi mabaya ya madaraka yatakayofanywa aidha na Mtendaji wa Kata,Mwenyekiti wa Kijiji, Mtendaji wa Kijiji sitalifumbia macho nitakuchukulia hatua kwa mujibu wa sheria, kanuni, tulizowekeana kama serikali” Alisema Mtaturu

  Sambama na hayo Dc Mtaturu amewasihi viongozi hao kuwaunga mkono askari polisi katika kuimarisha ulinzi na usalama kwani bila usalama na amani katika jamii inayotuzunguka hakuwezi kuwa na maendeleo.

  0 0

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amesema kuwa Serikali haitaendelea na ujenzi wa jengo la pili la abiria katika uwanja wa ndege wa Songwe uliopo mkoani Mbeya mpaka tume ya watalamu iliyoundwa kuchunguza ili kujiridhisha kama utaratibu ulizingatiwa kabla ya kuaza ujenzi huo.Prof. Mbarawa ametoa kauli hiyo mara baada ya kukagua jengo hilo linalojengwa na mkandarasi wa Kampuni ya Db Shapriya ya Tanzania ambapo amesema hadhi ya jengo hilo hairidhishi hivyo ipo haja ya kujiridhisha kama taratibu zote zilifuatwa kabla ya ujenzi.

  Amebainisha kazi ya tume hiyo ya wataalamu ni kuhakiki namna utaratibu wa kumpata mkandarasi ulivyofanywa, gharama halisi za mradi na fedha iliyolipwa kwa mkandarasi kama inaendana na thamani ya jengo hilo. “Serikali haiwezi kutoa fedha ya kumalizia jengo hili kabla ya kujiridhisha ili kuhakikisha fedha tutakazozitoa zitatumika kulingana na ilivyopangwa na thamani ya fedha inaendana na jengo lenyewe”, amesema Waziri Prof. Mbarawa.

  Aidha Waziri Prof. Mbarawa ameeleza ili kuwa na miundombinu imara na ya kudumu ni lazima kuhakikisha miradi ya ujenzi wa miundombinu inasimamiwa vizuri na taratibu za kupata mkandarasi bora zinafuatwa. “Kutokuwa na miundombinu isiyo imara ni sababu ya wahusika kuweka mbele maslahi binafsi na siyo ya Taifa”, amesisitiza Waziri Prof. Mbarawa

  Pia ameutaka uongozi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) kuhakikisha makosa yaliyojitokezo kwenye ujenzi wa jengo la abiria katika uwanja wa ndege wa Mwanza hayajirudii katika kiwanja hiki. Kwa upande wake Meneja wa Uwanja wa Ndege wa Songwe Bw. Hamisi Amiri amemhakikishia Waziri Mbarawa kusimamia ujenzi uliobaki kwa kuzingatia taratibu na makubaliano yaliyowekwa ili jengo hilo lidumu kwa manufaa ya Taifa na Mkoa.

  Uwanja wa Songwe ni kiungo muhimu kwa wananchi wa mikoa ya Katavi, Rukwa, Njombe na Ruvuma na katika mwaka huu wa fedha umetengewa kiasi cha shilingi bilioni 10 kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa jengo la abiria na taa uwanjani hapo.

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akipata ufafanuzi wa michoro ya ujenzi wa jengo la abiria kutoka kwa Mhandisi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA) wakati alipokagua Uwanja wa Ndege wa Songwe, Mkoani Mbeya.

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa Mhandisi wa Mamlaka ya Viwanja vya ndege (TAA) kuhusu ujenzi wa jengo la pili la abiria katika Uwanja wa Ndege wa Songwe, wakati alipokagua uwanja huo Mkoani Mbeya.


  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kulia), akipata maelezo ya mfumo wa utabiri wa hali ya hewa katika Uwanja wa Kimataifa wa Songwe (SIA) kutoka kwa Mtaalam wa masuala ya hali ya hewa uwanjani hapo, Wakati alipokagua uwanja huo mkoani Mbeya.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kulia), akipata maelezo kutoka kwa Bw. Baraka Mwambipile kuhusu namna ndege zinavyoongozwa wakati wa kuruka na kutua katika Uwanja wa Kimataifa wa Songwe, Wakati alipokagua uwanja huo mkoani Mbeya.

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa pili kulia) akiendelea na ukaguzi wa jengo la pili la abiria katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Songwe, Mkoani Mbeya.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akiendelea na ukaguzi wa wa Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Songwe , Mkoani Mbeya.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kulia) akitoa maelekezo kwa Mkandarasi wa kampuni ya Shapriya Co Ltd anayejenga jengo la pili la abiria wakati alipokagua uwanja wa kimataifa wa Songwe, Mkoani Mbeya. 

  0 0

  BBALOZI wa Japan nchini Tanzania, Masaharn Yoshida amemtembelea Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na kuzungumzia masuala mbalimbali ya ushirikiano baina ya nchi zao hususan katika sekta ya nishati.

  Balozi Yoshida, aliyeambatana na Ujumbe wa baadhi ya maofisa kutoka Ubalozini na wataalam kadhaa kutoka Shirika la Japan Oil, Gas and Metals National Corporation (JOGMEC), alimtembelea Prof Muhongo Agosti 3 mwaka huu ofisini kwake, jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (wa tatu kutoka kulia) akizungumza na Balozi wa Japan nchini Tanzania, Masaharn Yoshida (Kulia kwa Waziri) na Ujumbe wake, walipomtembelea Waziri ofisini kwake jijini Dar es Salaam hivi karibuni. 
   Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Japan nchini Tanzania, Masaharn Yoshida (kushoto) na Mtaalam kutoka Shirika la Japan Oil, Gas and Metals National Corporation (JOGMEC) la nchini Japan, walipomtembelea Waziri hivi karibuni.
   Kutoka kushoto ni Bwana Hitoshi Suzuki (Ofisa kutoka Ubalozi wa Japan nchini Tanzania), Bibi Sakura Nishioka (Mtaalam kutoka Shirika la Japan Oil, Gas and Metals National Corporation (JOGMEC), Masaharn Yoshida (Balozi wa Japan nchini Tanzania), Profesa Sospeter Muhongo (Waziri wa Nishati na Madini), Bwana Yoshiaki Igarashi (JOGMEC), Bibi Ayumi Kosug (JOGMEC) na Tamiko Hirata (Ofisa kutoka Ubalozini). Balozi Yoshida na Ujumbe wake walimtembelea Waziri Muhongo ofisini kwake jijini Dar es Salaam hivi karibuni.

  0 0


  Meneja Rasilimali watu Kutoka Benki ya NMB Dada Edith Mwiyomela akitoa Mada kwa Wanawake Wa Mkoa wa Dar es Salaam walionufaika na Mradi Kutoka Taasisi ya Manjano waliokutana kujadili na Kuangalia namna ya Kutatua changamoto wanazokutana nazo kwenye Biashara yao ya Upambaji na Uuzaji wa Vipodozi, Ambapo wameaswa Kuwafanya Kazi kwa Bidii,kuwa na Nidhamu na Pia kuweka akiba Pamoja na Kuwa na uvumilivu kwenye kazi zao za kila siku ili kuweza Kufikia Malengo waliyojiwekea.
  Washiriki wakisikiliza kwa makini mada mbalimbali kwenye mkutano huo
  Afisa Mtendaji Mkuu wa wa Shear Illusions na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Manjano Foundation Mama Shekha Nasser (kushoto) Akimsiliza Mmoja wa Wanawake aliyekuwa akieleza namna anavyopambana na Changamoto zinzowakabili Wanawake wengi kwenye Biashara zao.Kwa Upande Mwingine Mama Shekha Nasser Amawataka Wanawake waliohudhuria namna gani ya kuweza kutofautisha faida na mtaji. 
   
  Biashara nyingi za kina mama hufa baada ya mwaka mmoja tu kwa sababu wanawake wengi hawana nidhamu ya kutunza pesa. Hivyo tutaona matokeo ya 'Savings Club' zitakavyo wawezesha kusave pesa ili wasiweze kula mitaji na faida yote kwa pamoja
  Washiriki wakisiliza kwa Makini Namna ya Kupambana Changamoto mBalimbali zilizowsilishwa kwenye Mkutano huo

older | 1 | .... | 925 | 926 | (Page 927) | 928 | 929 | .... | 1898 | newer