Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live

Mpango wa Urasimishaji Makazi Holela Jijini Dar waanza kutekelezwa

$
0
0
Fatma Salum-Maelezo

Serikali imeanza kutekeleza mpango wa kutambua, kupanga na kupima vipande vya ardhi na kuweka huduma za jamii kama miundombinu ya barabara na mitaro ya maji ya mvua ili kuboresha mazingira ya makazi na kuongeza usalama wa miliki kwa kutoa hatimiliki.

Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Dar es salaam na Kaimu Mkurugenzi wa Urasimishaji Makazi Holela kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bibi. Bertha Mlonda wakati wa mkutano na vyombo vya habari.

Akifafanua Mlonda alisema kuwa mpango huo unatekezwa kwa kushirikiana na Halmashuri zote za Jiji la Dar es salaam na tayari zoezi limeanza katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni ambapo wananchi wameonyesha mwitikio mkubwa kwa kuunga mkono juhudi hizo za Serikali .

Akizungumzia vigezo vinavyofuatwa katika urasimishaji makazi yaliyojengwa kiholela, Mlonda alibainisha kuwa ni pamoja na eneo husika liwe limetengwa kwa ajili ya matumizi ya makazi katika Mpango wa Jumla wa Jiji (Master Plan).

“Mpango huu ni shirikishi, wananchi wanatakiwa kuwa mstari wa mbele kushirikiana na wataalamu kubainisha mahitaji ya huduma za jamii na miundombinu na siyo makazi holela yote yana sifa ya kurasimishwa. “Alisisitiza Mlonda.

Aidha, alisema kuwa eneo husika ni lazima liwe na idadi kubwa ya watu wanaoishi katika eneo hilo ambao hawana uthibitisho wa uhalali wa kumiliki ardhi hata kama wanalipia ada. Kigezo kingine ni kuwepo kwa ongezeko kubwa la ujenzi wa nyumba katika eneo husika na idadi kubwa ya wakazi ambao wameishi katika eneo hilo kwa kipindi kirefu.


Kaimu Mkurugenzi wa Urasimishaji makazi holela toka Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bibi Betha Mlonda akifafanua kwa waandishi wa Habari kuhusu mpango wa urasimishaji makazi yaliyojengwa kiholea katika Jiji la Dar es saaam ambao umeanza kutekelzwa katika eneo la Kimara Jijini humo .kulia ni Afisa Habari wa Idara ya Habari- Maelezo Bi Fatma Salum na kushoto ni Afisa Habari wa Wizara hiyo Bw. Hassan Mabuye.
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Vyombo vya Habari leo Jijini Dar es salaam.
Moja ya eneo lenye makazi holela katika Jiji la Dar es salaam.
Mmoja wa Wataalamu wa upimaji Ardhi akiweka alama katika eneo lililorasimishwa. 

“Kuna maeneo mengi ambayo wamiliki wanaendelea kuuza mashamba au viwanja vyao na ujenzi wa nyumba mpya kwa ajili ya makazi na biashara unaendelea kwa kasi kubwa; ndio maana tumeona ni vyema tukaanza utaratibu huu wa kurasimisha ili watu wamiliki hayo maeneo kihalali.” Alifafanua Mlonda.

Pia idadi kubwa ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam na Asasi za Kijamii wamehamasika na wako tayari kushiriki katika mipango ya urasimishaji kwa kuchangia gharama za kupanga, kupima na kumilikisha.

Mlonda alitoa wito kwa wananchi kushirikiana na viongozi wao wa Serikali za Mitaa kutatua migogoro ya mipaka na kutoa ardhi kwa ajili ya barabara kwani ndio msingi wa ufanisi katika zoezi la urasimishaji makazi.

Makazi holela ni makazi ambayo yamejengwa bila kufuata Sheria, kanuni na taratibu za Mipangomiji. Ujenzi mijini unaongozwa na Sheria ya Mipangomiji namba 8 ya mwaka 2007 na ile ya Serikali za Mitaa sehemu ya mamlaka za miji ya mwaka 1982. ambazo zinaelekeza kupata kibali cha ujenzi kabla ya kujenga nyumba.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AKATAA KUPOKEA MADAWATI YALIYOTOLEWA NA TFS

$
0
0
Asema huu si wakati wa kupokea vitu vibovu

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekataa kupokea msaada wa madawati uliotolewa na Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) baada ya kubaini yametengenezwa chini ya kiwango.

“Ofisa Elimu njoo kagua haya madawati yaliyo mazuri nitayapokea na yaliyobaki yarudishwe karakana yakatengenezwe upya huu si wakati wa kupokea vitu vibovu,“ amesema.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumanne, Agosti 02, 2016) wakati alipowasili katika kiwanja cha Mabau, Mtibwa kwa ajili ya kuzungumza na wananchi ambapo alikabidhiwa madawati hayo na Meneja wa TFS

Alisema anatambua dhamira ya TFS ya kuunga mkono jitihada za Serikali za kumaliza tatizo la upungufu wa madawati lakini hawezi kupokea kupokea madawati yaliyotengenezwa chini ya kiwango.

Baada ya Ofisa Elimu (Msingi) wa Wilaya ya Mvomero, Michael Ligola kukagua madawati 102 yaliyoletwa uwanjani hapo madawati 84 yalibainika kuwa ni mabovu na 14 tu ndiyo yalikuwa mazima.

Waziri Mkuu alisema hawezi kupokea madawati hayo yaliyotolewa na Meneja wa Msitu wa Mtibwa, Hamza Kateti na kuuagiza uongozi wa wilaya ufuatilie suala hilo kwa kuwa walitakiwa kuyakagua kabla ya yeye kukabidhiwa.

Katika hatua nyingine aliwasisitiza wazazi na walezi wa wilaya hiyo kuhakikisha wanawapeleka watoto wao shule na atakayeshindwa atachukuliwa hatua kali za kisheria.

“Serikali imewapunguzia mzigo kwa kuwaondolea michango na ada hivyo tumieni fursa hiyo kwa kuwapeleka shule watoto wote waliofikia umri wa kwenda shule na wasimamie masomo yao,” alisema.

Awali mbunge wa jimbo la Mvomero, Saddiq Murad alisema miongoni mwa changamoto kubwa inayoikabili wilaya hiyo ni pamoja na wafugaji kuingiza mifugo katika mashamba hivyo amemuomba Waziri Mkuu kuingilia kati suala hilo.

Akizungumzia namna Serikali ilivyojipanga kutatua changamoto ya migogoro baina ya wafugaji na wakulima Waziri Mkuu alisema wafugaji wenye mifugo mingi watahamishiwa katika vitalu vinavyomilikiwa na ranchi za Taifa na wenye mifugo michache watatengewa maeneo katika vijiji.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMANNE, AGOSTI 02, 2016.

WAZIRI MKUU MAJALIWA AVITAKA VIWANDA VYA SUKARI KUZALISHA ASILIMIA 100 YA MAHITAJI IFIKAPO 2020

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amevitaka viwanda vya sukari nchini kuongeza mikakati ya uzalishaji zaidi ili mwaka 2020 Tanzania iwe imefikia kiwango cha kuzalisha asilimia 100 ya mahitaji yake.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumanne, Agosti 02, 2016) wakati alipotembelea kiwanda cha sukari cha Mtibwa kilichoko mkoani Morogoro ambapo amesisitiza viwanda vya ndani vizalishe zaidi ili kupunguza uagizaji wa bidhaa hiyo kutoka nje ya nchi.

Amesema Serikali imejikita katika kuimarisha na kulinda viwanda vya ndani nchini hivyo ni vema viwanda vya sukari vikaweka mikakati ya kuzalisha kwa wingi ili kuondokana na uagizaji wa bidhaa hiyo kutoka nje.

“Kiwango cha mahitaji ya sukari nchini ni zaidi ya tani 400,000, nimeiagiza Bodi ya Sukari kukaa na wataalamu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na kufanya utafiti ili tujue mahitaji halisi ya sukari,” alisema.

Waziri Mkuu amesema Serikali imeweka mkakati wa kulinda viwanda vya ndani kwa kuziongezea kodi bidhaa zinazotoka nje ambazo zinazalishwa na viwanda vya ndani ikiwemo sukari hivyo wenye viwanda hawana budi kuzalisha kwa wingi zaidi.

Hata hivyo Waziri Mkuu amewataka wamiliki wa viwanda vya sukari nchini kutoa motisha kwa wakulima wa nje kwa kununua miwa yao kwa bei nzuri na kuwalipa kwa wakati ili nao wanufaike na uwepo wa viwanda hivyo na kuwa walinzi wa uwekezaji huo.

Kwa upande wake Meneja Uhusiano Mwandamizi wa kiwanda hicho, Ibrahim Juma amesema kwa sasa kiwanda kinazalisha tani 20,000 kwa mwaka na wanatarajia kuongeza uzalishaji hadi kufikia tani 70,000 ifikapo mwaka 2021.

Juma alisema uzalishaji wa sukari kiwandani hapo ulipungua kutokana na uingizwaji wa sukari kutoka nje hivyo aliipongeza serikali kwa kudhibiti uingizwaji holela wa sukari kutoka nje jambo litakalosaidia ukuzaji wa viwanda vya ndani.

Meneja huyo alisema kuwa kwa sasa wameanza upanuzi wa mashamba kiwandani hapo ambapo wanatarajia kuongeza hekta 400,000 lengo likiwa ni kutimiza ndoto ya Serikali ya kuifanya Tanzania ijitosheleze katika uzalishaji wa sukari.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU, JUMANNE, AGOSTI 02, 2016

TPA YATAKIWA KUPUNGUZA VIKAO

$
0
0

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akikagua nondo zilizosukwa kwa ajili ya ujenzi wa Daraja la Kalambo lililopo katika barabara ya Sumbawanga-Matai-Kasanga yenye urefu wa KM 112, Mkoani Rukwa. 

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa Meneja wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Mkoa wa Rukwa Arch. Deocles Alphonce wakati alipokagua ujenzi wa ofisi za Bonde la Ziwa Rukwa na Maabara zake zilizopo Sumbawanga Mjini. 

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akiendelea na ukaguzi wa ujenzi wa barabara ya Sumbawanga-Matai-Kasanga yenye urefu wa KM 112, Mkoani Rukwa.

Mhandisi Mshauri wa Kampuni ya Nicholas O’Dwyer Eng. Farley Vicente akitoa taarifa kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa kuhusu ujenzi wa barabara ya Sumbawanga-Matai-Kasanga yenye urefu wa KM 112, Mkoani Rukwa.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa Mkandarasi wa China Railway 15 Bureau Group Corporation kutoka China Zhang Tonggang (mwenye sweta nyekundu) inayojenga barabara ya Sumbawanga-Matai-Kasanga yenye urefu wa KM 112 kwa kiwango cha lami, Mkoani Rukwa.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akihakiki taarifa za mapato katika Bandari ya Kasanga iliyopo Mkoani Rukwa. Katikati ni Msimamizi wa bandari hiyo Bw. Seleman Kalugendo.
Meneja wa Shirika la Posta Tanzania Bi. Zahara Sukeiman akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa kuhusu huduma ya kutuma na kupokea Vifurushi wakati Waziri alipotembelea ofisini hapo.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa Maelekezo kwa Meneja wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) nyanda za juu kusini Bw. Peter Kaguru wakati alipotembelea ofisi hizo Mkoani Rukwa.

……………………………………………………………………………………………………..

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), kupunguza idadi ya vikao vya baraza visivyo na ulazima ili kuondokana na matumizi mabaya ya fedha na badala yake fedha hizo zielekezwe kwenye uendelezaji wa miundombinu ya bandari za maziwa.

Ametoa agizo hilo mara baada ya kukagua shughuli za utendaji wa bandari ya Kasanga iliyopo mkoani Rukwa inayohudumia mkoa wa Kigoma, nchi ya Burundi na Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo (DRC) ambapo amebaini mapungufu ya kiutendaji ikiwemo malipo yasiyotumia njia za kielektroniki na miundombinu isiyo rafiki katika kukidhi ushindani wa kibiashara katika bandari hiyo.

Waziri Mbarawa ameitaka TPA kuweka mfumo wa uendeshaji vikao kwa njia ya kieletroniki (video conference) kwa lengo la kudhibiti matumizi ya fedha nyingi zilizokuwa zikitumika katika uendeshaji wa vikao hivyo.

“Nataka TPA muanze kutumia video Conference katika vikao vyenu ili fedha zilizokuwa zikitumika zifanyie kazi nyingine za maendeleo ya Taifa”, amesema Waziri Prof. Mbarawa.

Ameongeza kuwa TPA imekuwa na wajibu mkubwa wa kuchangia pato la Taifa kupitia huduma za upakiaji na upakuaji wa mizigo hivyo wanapaswa kuanza kutumia mfumo wa kielekroniki katika ukusanyaji wa mapato katika bandari zote nchini ili kudhibiti upotevu wa mapato.

“Tukianzisha mfumo wa kielekroniki katika bandari hii tutakuwa na uwezo wa kufuatilia mapato yanayopatikana katika utoaji wa huduma na kujua kama malengo yamefikiwa”, amesema Prof. Mbarawa

Katika Hatua nyingine Profesa Mbarawa amekagua barabara ya Sumbawanga-Matai-Kasanga Port yenye urefu wa KM 112 inayojengwa kwa kiwango cha Lami na kumtaka Mkandarasi wa barabara hiyo China Railway 15 Bureau Group Corporation kukamilisha ujenzi huo ifikapo Julai mwakani.

Amesema kukamilika kwa barabara hiyo kutaunganisha mji wa Sumbawanga na Bandari ya Kasanga na hivyo kurahisisha shughuli za usafirishaji wa abiria na mizigo kutoka bandarini hapo na hivyo kuwa kichocheo cha ukuaji wa uchumi katika Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini.

“Kukamilika kwa barabara hii kutawawezesha wananchi kusafirisha bidhaa zao, kutoka sehemu moja hadi nyingine na hivyo kukuza uchumi wao na kuongeza pato la Taifa”, amesisitiza Prof. Mbarawa.

Aidha Waziri Mbarawa amemuhimiza Mkandarasi huyo kujenga barabara hiyo kwa viwango vilivyopo katika mkataba na kuzingatia thamani ya fedha katika ujenzi huo ili kuwezesha barabara hiyo kudumu kwa muda mrefu.

Naye Meneja wa Wakala wa Barabara Nchini, Mkoa wa Rukwa Eng. Masuka Mkina amesema kuwa ujenzi wa barabara hiyo umekamilika kwa asilimia 62 ambapo kukamilika kwa ujenzi huo utatagharimu kiasi cha zaidi ya shilingi Bilioni 133.

“Mpaka sasa Mkandarasi ameweza kukamilisha kujenga makalvati makubwa 11 kati ya 13, na makalvati ya kawaida 169 kati ya 241”, amesema Eng Mkina.

Waziri Prof. Mbarawa yupo katika ziara ya kukagua miradi ya miundombinu na kuangalia utendaji kazi wa taasisi zilizopo katika Mkoa wa Rukwa.

MAKALA KUHUSU FALSAFA, DHANA NA UMUHIMU WA MBIO ZA MWENGE WA UHURU

$
0
0
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA WAZIRI MKUU
SERA, BUNGE, KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVUFalsafa ya Mwenge wa Uhuru
Historia ya nchi yetu ni pana na ya kuvutia kwa namna ya pekee ukilinganisha na nchi nyingi za Afrika na Duniani kote. Upekee huu unatokana na uwezo wa kujenga hoja na uadilifu wa viongozi wetu, hasa mwasisi wa Taifa letu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alipochaguliwa kuwa mjumbe kwenye Baraza la kikoloni la kutunga Sheria (Tanganyika Legislative Council) mwaka 1958.

Kwa kuwa Mwalimu alikuwa na ndoto ya kuiona Tanganyika na Afrika iliyo huru, mwaka 1958 katika hotuba yake ya kwanza alitamka maneno ya kifalsafa kwa wajumbe na Spika wa Baraza la kikoloni la kutunga Sheria kwa kusema “Sisi tunataka Uhuru wa Tanganyika, Mkitupatia tutauwasha Mwenge wa Uhuru na kuuweka juu ya Mlima Kilimanjaro, umulike ndani na nje na mipaka yetu, ulete tumaini pale ambapo hakuna matumaini, upendo mahali palipo na chuki na heshima palipojaa dharau”.  
Maneno haya aliyarudia tena mwaka 1959 alipohutubia kikao cha 35 cha Baraza la Umoja wa Mataifa kama Mbunge mwakilishi pekee wa Tanganyika.

Falsafa hiyo ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ilikuwa ni kiashiria kikubwa kwa Waingereza kwamba watu wa Tanganyika wamechoka kutawaliwa. Siku Tanganyika ilipopata Uhuru tarehe 09 Desemba, 1961. Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliuwasha Mwenge wa Uhuru na akamkabidhi Luteni Alexander Ngwebe Nyirenda na kikosi cha Vijana wenzake wakaupeleka Mwenge wa Uhuru juu ya Mlima Kilimanjaro.

Mwalimu wakati akitoa hotuba ya siku ya Uhuru; aliwatangazia Watanganyika, Afrika na Dunia kwa ujumla kwa kusema “Sisi tumekwisha uwasha Mwenge wa Uhuru na kuuweka juu ya Mlima Kilimanjaro, umulike ndani na nje ya mipaka yetu, ulete matumaini pale ambapo hakuna matumaini, ulete upendo mahali penye chuki na heshima mahali palipo jaa dharau”

Luteni Alexander Nyirenda akipandisha Bendera na Mwenge wa uhuru juu ya mlima Kilimanjaro usiku wa kuamkia tarehe 9 december, 1961

Baada ya Uhuru wa Tanganyika na kuwashwa kwa Mwenge wa Uhuru, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na viongozi wenzake wa awamu ya kwanza walielekeza juhudi zao katika kuwaunganisha Watanzania na kuweka misingi imara ya kulijenga taifa huru la Tanganyika; kudumisha amani, upendo, umoja, mshikamano na kuweka sera za kukabili maadui ujinga, umaskini na maradhi.

Awamu hii ilitafsiri falsafa ya Mwalimu aliyoijenga katika Mwenge wa Uhuru kwa kuweka misingi madhubuti ya uhusiano wa nje, sera ya kutofungamana na siasa za upande wowote, na kuweka msisitizo mkubwa katika ukombozi wa Bara la Afrika na mapambano dhidi ya ubeberu na vibaraka wao. Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Azimio la Arusha lililosisitiza siasa ya Ujamaa na Kujitegemea, na kuundwa kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki ni matunda ya utelekezaji wa Falsafa ya Mwenge wa Uhuru.

Mara baada ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya tarehe 12 Januari mwaka 1964, Tanganyika iliungana na Zanzibar na kupata Taifa moja la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Haya ni mafanikio makubwa katika kutekeleza falsafa ya Mwenge wa Uhuru kwani Wazanzibar walirejeshewa matumaini yaliyokuwa yametoweka chini ya utawala wa Kisultani.

Hata baada ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar wa mwaka 1964, falsafa yaMwenge wa Uhuru iliendelezwa kwa kuukimbiza Mwenge wa Uhuru katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa lengo la kujenga na kuimairisha misingi ya amani, umoja, uzalendo, upendo, mshikamano na kuhamasisha shughuli za maendeleo katika jamii zetu na kupeleka kwa Watanzania wote ujumbe maalum uliokusudiwa na Serikali kila mwaka. Aidha, Mwenge wa Uhuru ni chombo pekee tulichonacho kama taifa cha kuwaunganisha Watanzania na kuwa wamoja kwani haufungamani na itikadi za kisiasa, makabila yetu wala Dini zetu. Mwenge wa Uhuru ni mali ya Watanzania wote.

Kwa nini Mwenge wa Uhuru husimamiwa na Serikali

Hadi mwaka 1992, Mbio za Mwenge wa Uhuru zilikuwa zikisimamiwa na kuratibiwa na Chama Tawala. Baada ya nchi yetu kuingia katika mfumo wa vyama vingi vya siasa mwaka 1992; mwaka 1993 Mbio za Mwenge wa Uhuru zilianza kusimamiwa na Serikali chini ya Wizara yenye dhamana na Maendeleo ya Vijana. Mabadiliko hayo yalikuwa ni kiashiria kikubwa kwa watanzania wote kwamba Mwenge wa Uhuru hauna Chama, hauna kabila na hauna dini isipokuwa ni kwa ajili ya kujenga na kudumisha umoja wa kitaifa. Kwa sasa Mbio za Mwenge wa Uhuru zinaratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu kwa kushirikiana na Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Vijana, Wazee, Wanawake na Watoto Zanzibar. Aidha, rasilimali fedha kwa ajili ya uendeshaji wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa hutolewa na Serikali na hutengwa na Wizara zenye dhama na kupitishwa na Bunge la bajeti la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mwaka wa fedha husika.

Tangu Mbio za Mwenge wa Uhuru ziasisiwe hadi leo, misingi na madhumuni ya Mwenge wa Uhuru na Mbio zake zimeendelea kuwa zenye manufaa makubwa na zitaendelea kurithishwa vizazi hadi vizazi katika taifa letu.

Rais wa awamu ya nne Dkt Jakaya Mrisho kikwete akiwa kwenye picha ya pamoja na wawakilishi kutoka chama cha upinzani cha Chadema siku ya kilele cha mbio za mwenge wa uhuru mwaka 2013, sherehe zilizofanyika mkoani Iringa.

Faida na Mafanikio ya Mwenge wa Uhuru Kitaifa na Kimataifa.
Mwenge wa Uhuru umekuwa ni chombo muhimu cha kujenga undugu, umoja, mshikamano na kudumisha amani pote unapopita bila kujali itikadi zetu za kisiasa, dini wala makabila yetu. Umuhimu huu unatokana na ukweli kwamba, leo hii tunahitaji kujenga Taifa lenye amani, umoja, upendo na mshikamano wa kitaifa kuliko wakati wowote ule ikiwa ni pamoja na kujenga taifa lisilokuwa na dhuluma, unyonge, rushwa, ubaguzi, ukabila, udini wala vitendo vya kifisadi.
Mbio za Mwenge wa Uhuru zimeendelea kuhamasisha wananchi kwa kushirikiana na Serikali yao katika kubuni na kutekeleza shughuli mbalimbali za maendeleo katika nyanja za kilimo, ufugaji, Uvuvi endelevu, uboreshaji na ujenzi wa miundombinu ya barabara, afya, elimu, maji, umeme na huduma za jamii katika maeneo yote nchini na hasa katika maeneo yasiyofikika kiurahisi. Kwa mfano, kwa mwaka 2015 pekee, miradi 1,342 yenye thamani ya Tshs. 463,519,966,467.77 ilizinduliwa na kuwekewa mawe ya msingi. Kati ya fedha hizo, Tshs. 73,462,492,473. 62 zilitokana na nguvu za wananchi. Hata hivyo, michango yote inayotolewa na wananchi ni ya hiari na hutolewa baada ya wananchi kuhamasishwa na kufahamu umuhimu na matumizi yake ambayo ni kugharamia kwa miradi yao wenyewe.
Mbio za Mwenge wa Uhuru zimekuwa zikitumika kuelimisha wananchi katika maeneo yote nchini jinsi ya kupambana na maradhi yanayotishia ustawi wa watu wetu kama vile UKIMWI, Malaria na kupambana na matumizi ya Dawa za kulevya. Pamoja na njia nyingine tunazotumia kuwahamasisha wananchi wetu. Bado Mbio za Mwenge wa Uhuru zimekuwa ni njia sahihi ya kufikisha taarifa na elimu sahihi ya changomoto hizi kwa watanzania wote.
Mbio za Mwenge wa Uhuru pia, zimeendelea kuhamasisha na kuimarisha umuhimu wa Muungano kwa watanzania wa pande zote mbili za nchi yetu.
Kimataifa, Mwenge wa Uhuru umeendelea kusimamia dhana ya na maudhui yake ya kumulika hata nje ya mipaka yetu. Kwani umeendelea kuhamasisha amani ndani ya Afrika Mashariki, Kusini mwa Jangwa la Sahara Afrika na Duniani kwa ujumla. Tanzania imeendelea kuwa msuluhishi wa Amani Afrika na mfano wa kuigwa kwa mataifa mengine Duniani kote na imeshiriki ukombozi wa Bara la Afrika hasa kusini mwa Afrika na kusisitiza juu ya umoja, mshikamano, upendo na amani kwa mataifa hayo.
Mwenge wa uhuru umeendeleza falsafa ya kumulika ndani ya mipaka ya taifa letu kwa kumulika uovu katika jamii ikiwemo uzembe, kutowajibika, vitendo vya rushwa na ufisadi katika miradi mbalimbali ya maendeleo na huduma za kijamii nchini.
Mbio za Mwenge wa Uhuru pia hutumika katika kuratibu na kutathimini shughuli mbambali za maendeleo zinazofanywa na wadau wa maendeleo na kukusanya taarifa zinazohusu kero za wananchi ambazo husaidia Serikali katika upangaji na utelezaji wa mipango ya maendeleo kwa wananchi wake.

Dhana Potofu dhidi ya Mwenge wa Uhuru.

Pamoja na maono ya Baba wa Taifa, falsafa ya Mwenge wa Uhuru , faida na umuhimu wa Mwenge wa Uhuru ambao umeelezwa hapo juu, wapo watu wachache ambao huenda kwa sababu zao za kisiasa au maslahi yao binafsi wameamua kutumia nafasi zao na ushawishi wao kuupotosha umma wa Watanzania kwamba Mwenge wa Uhuru haufai kwa kutoa hoja nyepesi (Cheap arguments). Hoja hizo hizo ni pamoja na:-

(i) Falsafa ya Mwenge wa Uhuru haihitajiki sasa kwa Watanzania

Serikali kama ilivyoeleza hapo juu, inaendelea kusisitiza kuwa falsafa ya Mwenge wa Uhuru na maono ya Baba wa Taifa juu ya taifa hili bado yanaendelea kuishi japo yeye hatupo naye tena kwani ni dhahiri kuwa chombo hiki kinasaidia sana katika jitihada za kuwaunganisha Watanzania, kujenga umoja wa kitaifa, upendo, mshikamano, amani, uzalendo na kuchochea shughuli za maendeleo kote nchini. Kwa sasa Mbio za Mwenge wa Uhuru zinahitajika zaidi kwa lengo la kuhamasisha watu wetu kufanya kazi na kujiletea Maendeleo kama silaha ya kupambana na adui ujinga na umaskini.

 
Picha ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akiwa anapokea Mwenge wa Uhuru

(ii) Michango wakati wa Mbio za Mwenge wa Uhuru.

Serikali ingependa ifahamike kwa wananchi kuwa, Mbio za Mwenge wa Uhuru zinaendeshwa kwa rasilimali fedha za serikali zinazopitishwa na Bunge. Aidha, pale inapohitajika, wadau kwa hiari yao, husaidia katika kugharamia machapisho ya ujumbe wa Mbio za Mwenge wa Uhuru uliokusudiwa kama jitihada zao katika kuisaidia Serikali kufikisha ujumbe kwa wananchi wengi zaidi.

Mbio hizi pamoja na dhana nyingine zilizofafanuliwa hapo awali, unawahamasisha wadau mbalimbali kushiriki na kuchangia kwa hiari shughuli za Maendeleo katika maeneo yao. Michango ya wadau katika Halmashauri zetu hujumuisha nguvu za wananchi, Vifaa na fedha taslimu ambazo hutumika katika miradi wanayoibuni na kuitekeleza wenyewe. Lengo la kuwashirikisha wananchi katika miradi yao ya maendeleo ni kujenga moyo wa kujitolea, uzalendo na utaifa kwa wananchi wetu ili waweze kumiliki miradi inayoanzishwa na kujenga misingi ya uendelevu wa Miradi hiyo. Mara nyingi, asilimia ishirini ya kila mradi unaowekewa jiwe la msingi, kuzinduliwa, au kufunguliwa na Mbio za Mwenge wa Uhuru ni sharti itokane na nguvu za wananchi. Serikali inaendelea kusisitiza kuwa, michango hiyo ni ya hiari na matumizi yake huwekwa wazi kwa wanachi kila mradi wakati wa kuzinduliwa au kuwekewa jiwe la msingi.

(iii) Mikesha ya Mbio za Mwenge wa Uhuru na maambukizi ya VVU/UKIMWI

Baadhi ya watu wachache wamekuwa wakidai kuwa, mikesha ya Mbio za Mwenge wa Uhuru inachochea vitendo vya ngono zembe vinavyopelekea maambukizi mapya ya VVU/UKIMWI katika maeneo mbalimbali nchini. Serikali inapenda kufafanua jambo hili kuwa, Suala la mapambano dhidi ya ugonjwa wa UKIMWI ni jambo linalopewa kipaumbele kikubwa katika Mbio za Mwenge wa Uhuru.

Tangu mwaka 2000 hadi sasa, ujumbe wa mapambano dhidi ya UKIMWI umefanywa kuwa ujumbe wa kudumu na uandaliwa kwa kushirikiana na Tume ya taifa ya kuthibiti UKIMWI (TACAIDS) na kisha kutolewa kwa ufasaha na vijana wakimbiza Mwenge wa Uhuru kitaifa kila mwaka katika Halmashauri za Wilaya zote zote nchini. Lengo likiwa ni kuhakikisha maambukizi mapya ya VVU yanafikia asilimia sifuri katika jamii yetu. Katika kufanikisha azma hii, Mbio za Mwenge wa Uhuru huwafikishia wananchi wote nchini, taarifa sahihi kukusu VVU/UKIMWI kwa njia ya machapisho, sanaa kama vile maigizo, mashahiri na nyimbo, ushuhuda (testimony) kutoka kwa waathirika na hotuba za wakimbiza Mwenge kitaifa ambao huandaliwa na mamlaka husika kabla ya kunza mbio hizi. Mbio za Mwenge wa Uhuru pia huhamasisha wananchi kupima VVU kwa hiari na kila siku, wastani wa watu 200 hadi 600 hujitokeza kupima VVU jambo ambalo ni nadra sana kutokea kwa watu wengi kujitokeza kupima VVU kwa wingi katika program nyingine zinazolenga kuhamasisha upimaji wa VVU. Mbio za Mwenge wa Uhuru pia hukemea tabia za unyanyapaa katika jamii, huhamasisha juu ya matumizi sahihi ya ARVs na kuwaelekeza wananchi jinsi ya kujikinga na maabukizi ya VVU. Hivyo siyo kweli kuwa mikesha ya Mbio za Mwenge wa Uhuru inachangia katika maambukizi ya VVU. Ni vyema tukafahamu kuwa UKIMWI upo na tabia zetu hatarishi hasa za kufanya ngono zembe ndizo changamoto kubwa tunayotakiwa kuijadili kama Watanzania katika kupambana na ugonjwa huu wa UKIMWI na sio Mwenge wa Uhuru. Mwenge huu unatusaidia kupambana na tabia zetu hatarishi ambazo ndizo zimekuwa kikwazo kikubwa katika jitihada za Serikali za kupambana na VVU/UKIMWI.

Kutokana na umuhimu, dhana na falsafa ya Mwenge wa Uhuru kama ilivyoelezwa :-
Serikali itaendelea kujenga mshikamano, umoja, upendo na kudumisha amani miongoni mwa Watanzania kupitia Mbio za Mwenge wa Uhuru.Serikali itaendelea kuutumia Mwenge wa Uhuru kuwahamasisha wananchi kupambana na maadui ujinga, maradhi na umaskini kwa watu wetu.Serikali itaendelea kuutumia Mwenge wa Uhuru kumulika, kufichua na kuchukua hatua dhidi ya watu au kundi la watu wanaojihusisha na vitendo vyote vinavyolihujumu Taifa ikiwa ni pamaoja na vitendo vya kibaguzi, rushwa, ufisadi, ubadhirifu, uzembe na chuki.

Serikali inapenda kutumia nafasi hii kuwaomba watanzania wote kutambua kuwa, kila taifa lina chimbuko lake, utamaduni wake, na taratibu zake. Mwenge wa Uhuru utabaki kuwa ni chombo muhimu na alama ya Taifa letu. Kama Taifa tutaendelea kushirikiana na kuenzi kazi na fikra za waasisi wa Taifa hili. Tushiriki katika shughuli za maendeleo kupitia Mbio za Mwenge wa Uhuru, tuusikilize ujumbe wa Mbio za Mwenge wa Uhuru unapopita katika maeneo yetu, tuutafakari na kuufanyia kazi kwa vitendo kwa maendeleo ya Taifa letu. 
 
Tujiepushe na biashara na matumizi ya Dawa za kulevya, vitendo vinavyosababisha maambukizi ya Virusi vya UKIMWI na tufanye kazi kwa bidii huku tukiendeleza mshikamo, umoja, upendo, amani na undugu wetu. Serikali inatoa wito kwa Vijana ambao ndiyo nguzo ya Taifa, kudumisha chombo hiki kwa faida yetu sote na vizazi vijavyo. Hapa Kazi tu.

Mungu Ibariki Afrika, Mungu Ibariki Tanzania.

Makala hii, imetolewa na:

Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu.

JOKATE AJENGA UWANJA WA NETIBOLI NA KIKAPU SHULE YA JANGWANI JIJINI DAR

MKANDARASI APEWA WIKI MBILI KURUDISHA VIFAA NA KUENDELEA NA UJENZI

$
0
0

Mbunge wa Jimbo la Nkasi kaskazini Mhe. Ally Kessy (mwenye kofia) akieleza jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa wakati alipokagua miundombinu ya Bandari ya Kipili, Mkoa wa Rukwa.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa Afisa Uendeshaji wa Bandari ya Kipili Bw. Hamis Msellem wakati alipokagua miundombinu ya bandari hiyo wilaya ya Nkasi, Mkoani Rukwa. Kulia kwake ni Mbunge wa Jimbo la Nkasi kaskazini Mhe. Ally Kessy.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akifafanua jambo kwa Mbunge wa Jimbo la Nkasi Kaskazini Mhe. Ally Kessy wakati alipokagua miundombinu ya bandari hiyo, Mkoani Rukwa.
Mkandarasi anayejenga barabara ya Kanazi-Kizi-Kibaoni yenye urefu wa KM 76.6 akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa wakati alipokagua ujenzi huo. Katikati ni Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Mkoa wa Rukwa Eng. Masuka Mkina. 
Mbunge wa Jimbo la Nkasi kaskazini Mhe. Ally Kessy akiteta jambo na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa wakati alipotembelea Jimboni kwake.


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (Kulia) akitoa maelekezo kwa Meneja wa kiwanja cha ndege cha Rukwa Bw. Sandali Kaisi (kushoto) kuhusu uboreshwaji wa kiwanja hicho wakati alipotembelea kiwanja hicho.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa pili Kulia) akitoa maelekezo kwa Meneja wa kiwanja cha ndege cha Rukwa Bw. Sandali Kaisi (wa kwanza kushoto) wakati alipokagua kiwanja hicho.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa Mkandarasi anayejenga barabara ya Sumbawanga Mjini-Chala- Kanazi yenye urefu wa KM 75 alipokagua ujenzi wa barabara hiyo.
 …………………………………………………………………………………………….

Mkandarasi Jianx-Geo Engineering Group Corporation kutoka China anayejenga sehemu ya barabara ya Sumbawanga Mjini-Chala-Kanazi kwa kiwango cha lami amepewa wiki mbili kurejesha vifaa vya ujenzi katika eneo la kazi ili kuongeza kasi ya ujenzi wa barabara hiyo ambao umeonekana kusuasua kutokana na ukosefu wa vifaa vya kutosha.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, wakati alipokagua mradi wa ujenzi wa barabara ya Sumbawanga-Namanyere-Mpanda Mkoani Rukwa.

Waziri Prof. Mbarawa amesema barabara hiyo imegawanywa katika sehemu mbili ambazo ni Sumbawanga Mjini-Chala-Kanazi KM 75 na Kanazi-Kizi-Kibaoni KM 76.6 ili kuhakikisha barabara hiyo inakamilika kwa wakati na viwango kulingana na mkataba.

“Hakikisheni baada ya wiki mbili vifaa vinakuwepo katika eneo la kazi na mnatekeleza wajibu wenu kukamilisha barabara hii kwa wakati tuliokubaliana ili ianze kutumiwa na wananchi”, amesema Prof. Mbarawa.

Waziri Prof. Mbarawa ameongeza kuwa wananchi wanamatarajio makubwa na barabara hiyo kwa muda mrefu hivyo Mkandarasi ahakikishe kazi ya ujenzi katika kipande kilichobaki kwa kiwango cha lami inamalizika ifikapo mwezi Julai mwakani ili kuharakisha shughuli za kimaendeleo mkoani hapo.

Aidha, amemtaka mkandarasi huyo kukamilisha mzani wa kupima uzito wa magari katika kijiji cha Kanondo KM 5 kutoka Sumbawanga mjini ifikapo mwezi Agosti mwaka huu kwa lengo la kudhibiti uzito wa magari yanayofanya shughuli za kusafirisha mizigo na abiria katika barabara hiyo.

Kwa upande wake Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Rukwa, Eng. Masuka Mkina amemuhakikishia Waziri Mbarawa kuwa ujenzi wa barabara zote utazingatia viwango na utakamilika kwa wakati.

“Nikuhakikishie kuwa tutasimamia na kuzingatia viwango vilivyowekwa katika mradi wa ujenzi huu ili wananchi wanufaike na kuongeza uchumi wa mkoa “,amesema Eng. Mhina. Ujenzi wa barabara ya Sumbawanga-Namanyere-Mpanda kwa kiwango cha lami unagharamiwa na Serikali ya Tanzania kwa jumla ya kiasi cha Shilingi bilioni 150.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

MADIWANI MKURANGA WAMUOMBA RAIS KUFUTA HATI MILIKI YA SHAMBA LA SOAP & ALLIED INDUSTRIES LTD KUFUATIA KUIBUKA KWA MGOGORO MKUBWA NA WANANCHI

$
0
0

Madiwani wa kimsikiliza Kwa makini Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Abdallah Ulega katika kikao cha halmashauri ya wilaya ya Mkuranga.Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Mkuranga Kwa kauli moja wamepitisha maadhimio ya kuunda kamati itakayokwenda Kwa Waziri Mkuu ili kumuomba rais afute hati miliki ya shamba namba 271, linalomilikiwa na mwekezaji, Hamidu Balma. 
 
Shamba hilo ambalo lenye hekari 1750 ambalo lipo katika kata ya Mwandege limeingia katika mgogoro mkubwa na wananchi wa kijiji cha kazole, hadi kufikia hatua ya wananchi hao kulala mahabusu Mara kadhaa kwasababu ya wanakijiji hao kuingia katika shamba hilo ambalo limekaa zaidi ya miaka 28 bila kuendelezwa.(Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii).
Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Abdallah Ulega akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya wilaya hiyo, katika kikao chao madiwani ,ambapo katika kikao hicho waliadhimia kwa kauli moja kumuomba Rais kufuta hati miliki ya shamba la Soap and Allied industries limited ambalo linamilikiwa na Hamidu Balma lililopo mkoani Pwani kwa kushindwa kuliendeleza.
Mkuu wa wilaya ya Mkuranga,filbarto Sanga akizungumza katika mkutano wa baraza la madiwani katika halmashauri ya wilaya ya Mkuranga ,ambapo kikubwa alizungumzia suala la uimarishaji wa ulinzi na usalama ndani ya wilaya hiyo,kulia ni Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Abdallah Ulega

Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Mkuranga Juma Abeid (alie simama) akizungumza katika kikao hicho cha baraza la madiwani lililofanyika jana

Diwani wa Kata ya Mwandege Adolph Edward akichangia hoja katika kikao hicho cha Baraza la madiwani katika Halmashauri ya wilaya hiyo ambapo ziliibuka hoja mbalimbali ikiwamo ya mwekezaji Hamidu Balma aliyeshindwa kuendeleza shamba namba 271,lililopo katika kataka ya Mwandege

BAADA YA MO DEWJI KUMWAGA ML 100,HAYA NDIO MANENO YA ALIYOONGEA RAIS WA SIMBA,EVANS AVEVA

WANAFUNZI WANUSURIKA KUTEKETEA KWA MOTO SHULE YA SEKONDARI SADANI MUFINDI

$
0
0

Mkuu wa Wilaya mbunge na mwenyekiti wa Halmashauri wakiangalia bweni lililo ungua.
Mkuu wa wilaya ya mufindi akikabidhi kwa mwanafunzi godoro alipo wasili na viongozi wa halmashauri shuleni saadani usiku wa agosti 01

Jumla ya wanafunzi 50 wa shule ya Sekondari Sadani iliyopo halmashauri ya wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa, wamenusurika kuteketea kwa moto baada ya moja kati ya mabweni ya wasichana wa shule hiyo kushika moto na kuteketeza mali zote zilizokuwa ndani ya bweni hilo.

Taarifa ya iliyotolewa na kitengo cha habari na mawasiliano cha halmashauri ya Wilaya ya Mufindi, imeeleza kuwa moto ambao chanzo chake hakijafahamika mara moja uliibuka ghafla julai 31 majira ya saa moja na nusu usiku na kuteketeza vitu mbalimbali vyenye thamani ya zaidi ya Sh. Milioni 09 na laki 06.

Taarifa hiyo imebainisha baadhi ya vitu hivyo kuwa ni pamoja na vitanda, magodoro, blanketi na mabati na kuongeza kuwa hakuna mwanafunzi yeyote aliyepoteza maisha na tayari vyombo vya usalama vimeanza uchunguzi ili kubaini chanzo cha moto huo.

Aidha, uongozi wa halmashauri ya Wilaya ukiongozwa na Mkuu wa wilaya ya Mufindi Jamuhuri William, Mwenyekiti wa Halmashauri Festo Mgina na Mbunge wa jimbo la Mufindi kasikazini Mahamudu Mgimwa, ulifika shuleni hapo mapema agasti moja kutoa pole na kukabidhi mahitaji muhimu ya wanafunzi yenye thamani ya Shilingi milioni 06 kisha wakazungumza na wanafunzi.

Hii ni ajali nyingine ya moto katika mabweni ya wasichana Mkoani Iringa kwani manamo mwaka 2009 ajali mbaya zaidi ilitokea katika shule ya sekondari Idodi Wilayani Iringa na kusababisha vifo vya wanafunzi 12 .

KITUO CHA WATOTO WACHANGA YATIMA NJOMBE CHAOMBA MSAADA WA MASHINE YA KUFULIA.

$
0
0
Baadhi ya wafanyakazi wa kituo cha kulelea watoto wachanga Yatima na lishe cha kipengere Mkoani Njombe wakifua nguo za watoto kwa mikono baada ya mashine walizokuwa wakizitumia kuharibika, Picha na James Festo.

Na James Festo, Njombe.

KITUO cha kulelea watoto yatima na lishe cha Kipengere kinachopatikana wilayani Wanging'ombe Mkoani Njombe ambacho huwahumia watoto wachanga yatima wenye umri wa miaka 0 hadi mitano kimewaomba wadau kusaidia kununua na kutengeneza mashine ya kufulia kutokana na zilizokuwapo kuharibika baada ya kutumika muda mrefu.

Msimamizi wa kituo hicho ambacho kwa sasa kinawahudumia watoto 51 miongoni mwa 220 ambao waliwahi kuhudumiwa na kituo hicho, Sister Nivardina Mbifile aliliambia gazeti hili mwishoni mwa juma kwamba kwa sasa hulazimika kuamka saa kumi na moja asubuhi kufua nguo za watoto tofauti na hapo kabla.

""tunachangamoto kubwa sana ya mashine ya kufulia, tulikuwa nazo zimezeeka zimeharibika sasa tunafua nguo kwa mikono sasa watoto ni wengi tunaamka saa 10 kufua nguo za watoto hadi jioni tulionao ni wachanga ...hapo mwanzo tulikuwa na mashine hata wafuaji walikuwa wanapata nafuu...sasa hivi mikono inachubuka kwa sasa" alisema Sister Mbifile.

Aliongeza kuwa "mashine hizi mbili zilishawahi kusumbua na tulisubiri wataalamu kutoka nje ya nchi wakaja kututengenezea zikaendelea kufanya kazi na sasa hatuwezi kutengeneza tena...na hii moja haina mda mrefu tumeacha kuitumia kwa sababu ilianza kuleta maneno ya kichina hivyo tunasubiri wataalamu kutoka nje wakiwahi watakuwa wametusaidia sana ila tunaomba mwenye uwezo wa kutusaidia atusaidie.

Umoja wa wananchi wa Njombe Magharibi waishio jijini Dar es salaam UWENDE ni miongoni mwa waliofika kutoa msaada ya vyakula na mahitaji muhimu kwa watoto yatima katika kituo hicho wakiongozwa na Pascal Ngilangwa wenye thamani ya shilingi milioni 1.08 wakizungumza baada ya kuzungumza na wafuaji wa Nguo za watoto ambao wengi ni wachanga walisema msaada wa mapema unahitajika.

"kufua kwa mkono nguo za watoto ambao baada ya saa moja huwa hazitazamiki kama nepi ni jambo linalohitaji moyo tena si kidogo tunaomba wadau wengine wasaidie kupatikana kwa mashine ya kufulia... hata viongozi wa serikali wasaidie hadi Rais wangu Magufuli mimi namlilia aje asaidie kutengeneza mashine au kununua mashine ya kufulia" alisema Ngilangwa.

Aliongeza kuwa "sisi tumeamua kujitolea msaada ni jadi yetu tumekuwa tukisaidia kwenye upande wa elimu, kilimo, afya na mazingira sisi huchangishana na kutoa misaada hii kila mwaka katika maeneo mbalimbali.

Kulingana na Sister Mbifile sehemu kubwa ya watoto ambao hulelewa kituoni hapo wamewapoteza wazazi wao kutokana na ugonjwa wa ukimwi pamoja na matatizo ya uzazi wakati wanapojifungua na asilimia kubwa ni kutoka wilaya za Makete, Njombe na Wanging'ombe. Itakumbukwa Mkoa wa Njombe kwa sasa ndio unaongoza kwa kuwa na kiwango kikubwa cha maambukizi ya virusi vya Ukimwi kinachofikia asilimia 14.8 kulingana na utafiti wa Tume ya kudhibiti ugonjwa wa Ukimwi humu Nchini TACAIDS iliyotolewa mwanzoni mwa muongo wa pili wa karne ya 21

VYUO 5 VYAFUTIWA USAJILI, 175 VYAPEWA NOTISI YA KUSHUSHWA HADHI.

$
0
0
BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI
Description: Description: small_emblem
·        41  Vyapewa muda wa wiki mbili kujisajili mara moja

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) limetangaza kuwa vyuo 5 vimefungwa kuendesha mafunzo na kufutwa kwenye rejista ya vyuo vya ufundi nchini.
Pia Baraza limetangaza kuwa vyuo 41 vinavyotoa elimu ya ufundi bila kusajiliwa kwa mujibu wa sheria vimepewa muda wa wiki mbili na kutakiwa vijisajili mara moja kwenye Baraza hilo kabla ya kuchukuliwa hatua kali za kisheria.
Vilevile, vibali vya  usajili wa vyuo 112 vya kutoa elimu ya ufundi vimefikia ukomo hivyo vinapaswa kutekeleza masharti ya Usajili; wakati  vyuo 57 vimefikia ukomo wa ithibati, hivyo inapaswa kutekeleza masharti ya ithibati, imetangazwa jana.
Akiongea katika mkutano na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Baraza (NACTE), Mhandisi Steven Mlote, amesema Baraza limetoa muda wa mwezi mmoja kwa vyuo 112 kutekeleza masharti ya usajili na vyuo 52 kutekeleza masharti ya ithibati kwa mujibu wa sheria za uendeshaji vyuo vya ufundi nchini, na vyuo vitakavyoshindwa kutekeleza agizo hili vitafungiwa mara moja.
Mhandisi Mlote pia alitoa onyo akisema “vyuo 41 vinavyotoa elimu ya ufundi bila kusajiliwa kwa mujibu wa sheria nimevipa muda wa wiki mbili na navitaka vijisajili mara moja kwenye Baraza kabla ya kuchukuliwa hatua kali za kisheria”.
Mhandisi Mlote alivitaja vyuo vyote vyenye matatizo kama ifuatavyo:
Jedwali I: Vyuo vya Ufundi Vilivyofutiwa Usajili
NA.
CHUO
State College of Health and Allied Sciences - Dar es Salaam
Zoom Polytechnic College - Dar es Salaam
Tabitha College – Dar es Salaam (formerly: Thabita Vocational Training College - Dar es Salaam)
Financial Training Centre - Dar es Salaam
TMBI College of Business and Finance - Dar es Salaam

Jedwali II: Vyuo ambavyo Havijasajiliwa na vinavyoendesha Programu zisizo na Kibali cha Baraza

NA.
CHUO
1.      
King Solomoni College - Arusha
2.      
Avocet College of  Hotel Management - Arusha
3.      
Kewovac Nursing Training Centre - Mbagala, Dar es Salaam
4.      
St. Family Health Training Institute - Mbagala, Dar es Salaam
5.      
Bethesda Montessori Teachers Training College - Arusha
6.      
Green Themi Teacher’s College & Green Themi Institute of Tourism
7.      
Mainland Institute of Professionals - Arusha
8.      
St. David College of Health - Dar es Salaam
9.      
Islamic Culture School - Dar es Salaam
10.  
Tanzania Education College - Dar es Salaam
11.  
Macmillan Training College - Dar es Salaam
12.  
Tanzania International University (TIU) - Dar es Salaam
13.  
Dodoma College of Business Management - Dodoma
14.  
Faraja Health and Emergencies - Mbeya
15.  
St. Joseph College - Mbeya
16.  
St. Peter Health Management - Mbeya
17.  
Kapombe Nursing School - Mbeya
18.  
Uyole Health Institute - Mbeya
19.  
Josephine Health Institute - Mbeya
20.  
Institute of Public Administration - Chake chake Pemba
21.  
Dar es Salaam College of Hotel and Business Studies - Vuga, Unguja, Zanzibar and Chake Chake, Pemba, Zanzibar
22.  
Zanzibar Training Institute, the Professional College of Information Technology, Languages and Business Studies - Mwera Meli Sita Unguja  Zanzibar
23.  
Azania College of Management - Raha Leo, Zanzibar
24.  
Time School of Journalism - Chakechake, Pemba
25.  
Residence Professional College - Mombasa, Zanzibar  
26.  
Mkolani Foundation Organisation - Mwanza
27.  
Kahama College of Health Sciences - Kahama
28.  
Institute of Adult Education-Mwanza Campus - Luchelele Site
29.  
Zoom Polytechnic - Bukoba
30.  
Johrow Star Training College - Shinyanga
31.  
St. Thomas Training College – Shinyanga
32.  
Dar es Salaam School of Journalism and Mass Communication DMSJ - Bukoba
33.  
Dar es Salaam School of Journalism and Mass Communication (DMSJ - Mwanza
34.  
Dar es Salaam School of Journalism and Mass Communication (DMSJ - Geita 
35.  
Dar es Salaam School of Journalism and Mass Communication (DMSJ - Simiyu
36.  
Harvest Institute of Health Sciences - Mwanza
37.  
Singin International - Bukoba
38.  
College of Business Management - Mombasa, Zanzibar
39.  
Tanzania Star Teachers College - Chakechake, Pemba, Zanzibar
40.  
Tanzania Star Teachers College - Unguja, Zanzibar
41.  
St. Mary's International School of Business - Sumbawanga


Jedwali III: Vyuo Vilivyosajiliwa lakini Vinatoa Programu zisizo na Kibali cha Baraza
NA.
CHUO
PROGRAMU
1.
AP and Prime College of Business Studies - Dar es Salaam
Medical Attendant
Nursing Assistant
2.
Universal College of Africa - Dar es Salaam
Banking and Finance
Business Administration
Clearing and Forwarding
Airfares
Information and Communication Technology
Nursing
Hotel Management
Secretarial Course
Procurement and Supplies
3.
Professional Skills Development International  (PSDI-CENTRE) Centre - Bagamoyo
Offering Non-NTA programmes (Various Short Courses)
4.
Ruter Institute of Financial Management - Mwanza
Accountancy
Procurement and Supply
Banking and Finance
ICT
  5.
Mwanza Polytechnic College - Maswa
Ordinary Diploma in Early Childhood Education
      6.

Royal College of Tanzania - Dar es Salaam
Law
  7.
Belvedere Business and Technology College - Mwanza
Accountancy
  8.
Chato College of Health Sciences and Technology - Chato
Pharmacy
9
St. Glory College of Health and Allied Sciences - Dar es Salaam
Medical Attendant

10.
Zoom Polytechnic College - Dar es Salaam
Computer Science

11.
Zanzibar Technology College - Zanzibar
Computer Science
Business Information System

Jendwali IV: Vyuo vyenye Hadhi ya Usajili Iliyokwisha Muda wake
NA.
CHUO
Mteule Training College - Morogoro
Favre Language and Communication Institute - Dar es Salaam
Eagle Wings Training College - Dar-es-Salaam
The Sinon College - Dar es Salaam
Green Hill Institute (GHI) - Mbeya
Institute of Business Management (IBM) - Morogoro
Modern Commercial Institute (MCI) - Dar es Salaam
Evin School of Management - Dar es Salaam
SAMFELIS College of Business Studies - Dar es Salaam
Agape College - Dar es Salaam
Belvedere Business and Technology College - Mwanza
Dar es Salaam Institute of Business Management - Dar es Salaam
Ellys Institute of Technology - Bunda
Tanzania Institute of Chartered Secretaries and Administrators (TICSA) - Arusha
Msakamali Institute of Business Studies and Technology (MIBST) - Msata
Cum Laude College - Njombe
Tarime Institute of Business Management (formerly Tarime Business Training Institute) - Tarime
Dar es Salaam College of Hotel and Business Studies - Dar es Salaam
Institute of Management and Development Studies - Iringa (Formerly: Sophist  Tanzania College - Iringa)
Greenbelt Polytechnic College - Morogoro
Zanzibar Institute of Journalism and Mass Communication (ZIJMC) - Zanzibar
Habari Media Training Centre (HAMETC) - Dar es Salaam
City Media College - Arusha
Arusha East African Training Institute - Arusha
AP and Prime College of Business Studies – Dar es Salaam
DayStar Training College - Dar es Salaam
Emmanuel Community College - Kibaha
Victoria Institute of Tourism and Hotel Management  - Mwanza
Zanzibar Professional Training Institute (ZPTI) - Zanzibar
Rungwe International College of Business and Entrepreneurship - Mbeya
Mbengwenya College of Business and Information Technology  -  Mbinga
Musoma Utalii College - Shinyanga
Dar es Salaam Institute of Journalism and Mass Communication (DIJMC) - Dar es Salaam
Ubuntu Institute of Social Justice (UISJ) - Mwanza
Institute of Skills Development (ISD) - Morogoro formerly: RK Institute of Innovations (RKII) - Morogoro)
Mbeya Training College (MTC) - Mbeya
Media and Values Training Institute (MEVATI) - Dar es Salaam
Marian College of Law (MCL) - Dar es Salaam
PCTL Training Institute (PTI) - Dar es Salaam
KAPS Community Development Institute - Mafinga, Iringa
Professional Skills Development International  (PSDI-CENTRE) Centre - Bagamoyo
East African Institute of Entrepreneurship and Financial Management (EAIEFM) - Arusha
New Focus College - Mbeya
Northern Peaks Business College (NPBC) - Arusha
Mbalizi Polytechnic College - Mbeya
Genesis School of Information Technology and Journalism - Dar es Salaam
1.      
Kiteto School of Nursing - Kibaya
2.      
Kunduchi Nursing School – Dar es Salaam
3.      
Wisdom Medical laboratory Training and Research Centre - Dodoma
4.      
Global Community College - Geita
5.      
KCMC School of Assistant Medical Officers (Radiology) - Moshi
...

[Message clipped]  View entire message
9 Attachments
 
 
 

Yahoo Mail issamichuzi@gmail.com

Attachments13:55 (39 minutes ago)
to Pamoja
NA.
CHUO
Mteule Training College - Morogoro
Favre Language and Communication Institute - Dar es Salaam
Eagle Wings Training College - Dar-es-Salaam
The Sinon College - Dar es Salaam
Green Hill Institute (GHI) - Mbeya
Institute of Business Management (IBM) - Morogoro
Modern Commercial Institute (MCI) - Dar es Salaam
Evin School of Management - Dar es Salaam
SAMFELIS College of Business Studies - Dar es Salaam
Agape College - Dar es Salaam
Belvedere Business and Technology College - Mwanza
Dar es Salaam Institute of Business Management - Dar es Salaam
Ellys Institute of Technology - Bunda
Tanzania Institute of Chartered Secretaries and Administrators (TICSA) - Arusha
Msakamali Institute of Business Studies and Technology (MIBST) - Msata
Cum Laude College - Njombe
Tarime Institute of Business Management (formerly Tarime Business Training Institute) - Tarime
Dar es Salaam College of Hotel and Business Studies - Dar es Salaam
Institute of Management and Development Studies - Iringa (Formerly: Sophist  Tanzania College - Iringa)
Greenbelt Polytechnic College - Morogoro
Zanzibar Institute of Journalism and Mass Communication (ZIJMC) - Zanzibar
Habari Media Training Centre (HAMETC) - Dar es Salaam
City Media College - Arusha
Arusha East African Training Institute - Arusha
AP and Prime College of Business Studies – Dar es Salaam
DayStar Training College - Dar es Salaam
Emmanuel Community College - Kibaha
Victoria Institute of Tourism and Hotel Management  - Mwanza
Zanzibar Professional Training Institute (ZPTI) - Zanzibar
Rungwe International College of Business and Entrepreneurship - Mbeya
Mbengwenya College of Business and Information Technology  -  Mbinga
Musoma Utalii College - Shinyanga
Dar es Salaam Institute of Journalism and Mass Communication (DIJMC) - Dar es Salaam
Ubuntu Institute of Social Justice (UISJ) - Mwanza
Institute of Skills Development (ISD) - Morogoro formerly: RK Institute of Innovations (RKII) - Morogoro)
Mbeya Training College (MTC) - Mbeya
Media and Values Training Institute (MEVATI) - Dar es Salaam
Marian College of Law (MCL) - Dar es Salaam
PCTL Training Institute (PTI) - Dar es Salaam
KAPS Community Development Institute - Mafinga, Iringa
Professional Skills Development International  (PSDI-CENTRE) Centre - Bagamoyo
East African Institute of Entrepreneurship and Financial Management (EAIEFM) - Arusha
New Focus College - Mbeya
Northern Peaks Business College (NPBC) - Arusha
Mbalizi Polytechnic College - Mbeya
Genesis School of Information Technology and Journalism - Dar es Salaam
1.      
Kiteto School of Nursing - Kibaya
2.      
Kunduchi Nursing School – Dar es Salaam
3.      
Wisdom Medical laboratory Training and Research Centre - Dodoma
4.      
Global Community College - Geita
5.      
KCMC School of Assistant Medical Officers (Radiology) - Moshi
6.      
School of Physiotherapy - Moshi
7.      
Advanced Paediatric Nursing School - Moshi
8.      
KCMC Assistant Medical Officers’ Ophthalmology School - Moshi
9.      
Advanced Ophthalmic Nursing School - Moshi
10.  
Nicodemus Hhando School of Health Sciences - Manyara
11.  
Litembo Health Laboratory Sciences School - Mbinga
12.  

WATANZANIA WATAKIWA KUTHAMINI BIDHAA ZA NDANI.

$
0
0

Afisa Mipango wa Kampuni Old East International Ephrahim Moses Mwano akiwa anaonyesha Aina ya Wino wa Crown ambao wanatengeneza hapa nchini,Katika maonyesho ya wakulima na wafugaji Katika viwanja vya nanenane Njiro Jijini Arusha.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Old East International Moses Mwano akiwa anazungumza na wateja waliotembelea banda hilo katika Maonyesho yanayoendelea katika Viwanja vya Taso nanenane Njiro Jijini Arusha.
Meneja mauzo wa Kampuni Old East International akiwa anamfafanulia mteja juu ya Crown Cartridge,katika maonyesho yanayoendelea katika viwanja vya Taso nanenane.
Na Woinde Shizza,Arusha.
Wito umetolewa kwa Watanzania watumie na kuthamini bidhaa zinazotengenezwa na kupatikana ndani ya nchi badala ya kuzipa kipaumbele bidhaa za nje ya nchi.

Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi wa Old East International ndugu Moses Mwano ,katika maonyesho yanayoendelea katika viwanja vya Taso nanenane njiro Jijini Arusha.

Mwao amesema kuwa Watanzania wengi wanathamini bidhaa zinazoingia nchini kutoka nje ya nchi,ambazo baadhi hazina kiwango cha ubora unaotakiwa kwa mtumiaji.

Mkurugenzi huyo wa Kampuni ya Old East International amesema kuwa kampuni hiyo ni ya Kitanzania ,imesajiliwa na ipo chini ya Shirika la uwekezaji Tanzania wao ni wawekezaji wa ndani,wanahusika kutengeneza wino wa kuchapia unaofahamika kwa jina la Crown Cartridge.

Kwa upande wake Mwano amewataka Watanzania kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Tanzania Dokta John Magufuli,katika jitihada zake za kuifanya Nchi kuwa ya Viwanda.


Sambamba na hayo amewaasa Watanzania watengeneze na kuingiza Bidhaa zenye kukidhi ubora na viwango ,huku akimalizia na msemo usemao " kizuri cha jiuza kibaya chajitembeza akimaanisha kuwa ukitengeneza bidhaa nzuri yenye kukidhi viwango na ubora unaohitajika wateja watafurahiwa nayo.

Usajili Rock City Marathon waanza; RC Mongella awa wa kwanza kujisajili

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Mwanza ndg John Mongella jana alikuwa mtu wa kwanza kujisajili kushiriki Rock City Marathon inayotarajiwa kufanyika September 25 mwaka huu katika viwanja vya CCM Kirumba jijini humo.

Akizungumza kwenye hafla fupi ya uzinduzi wa mbio hizo mkoani humo Bw Mongella aliekuwa ameambatana na Rais wa Chama cha Riadha Tanzania ambae pia ni mkuu wa Mkoa wa Simiyu Bw Anthony Mtaka, pamoja na viongozi wengine wa mchezo huo alitoa pia aliahidi kukimbia mbio za kilomita 21 ili kuonyesha nia ya dhati katika kuinua mchezo huo uliolipa taifa heshima miaka ya nyuma.

“Nitamke rasmi kwamba kwa sasa Rock City Marathon ni agenda ya mkoa na hivyo basi nitahakikisha kwamba mbio hizi zinapata washikiriki wa kutosha sambamba na wadhamini kutoka mkoa huu. Haiwezekani mbio za mkoa wa Mwanza zitegemee wadhamini wengi kutoka Dar es Salaam huku Mwanza kukiwa na makampuni na mashirika yenye uwezo wa kuusaidia mkoa wao,’’ alisema.

Kwa mujibu wa Bw Mongella msukumo wake huo kwenye ushiriki wa mbio hizo unatokana na si tu nia ya kuinua mchezo huo mkoani mwake bali pia malengo ya mbio hizo ya kutangaza utalii wa ndani wa mkoa huo pamoja na kupinga vita ujangili hususani mauaji ya tembo.

Kwa upande wake Bw Mtaka mbali na kuwapongeza wadhamini wa mbio hizo yakiwemo mashirika ya Freidkin Conservation Fund na African Wildlife Trust pia alitoa wito kwa makampuni mengine ya hifadhi na kitalii yafikirie kutumia fursa hiyo kutangaza utalii wa ndani.

“Pamoja na kuwapongeza waandaaji wa mbio hizi pia yaani kampuni ya Capital Plus International naomba nitoe wito kwao kuhakikisha wanaandaa utaratibu wa kuwaandaa washiriki wa mbio hizo miezi mitatu kabla kwa kuhakikisha wanapata mazoezi ya kutosha ili kama taifa tuwe na matokeo mazuri dhidi ya washiri kutoka mataifa ya nje,’’ alisisitiza.

Akizungumzia mbio hizo, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya mbio hizo Bw Zenno Ngowi alisema Mbio hizi zinafanyika kwa mara ya nane mfululizo tangu zianze mwaka 2009 zikiwa na lengo la kusaidia utambuzi, uhamasishaji na uibuaji wa vipaji vya riadha nchini kuanzia umri mdogo kabisa sambamba na kutangaza utalii wa ndani kupitia michezo.

Zaidi Bw Ngowi aliwashukuru wadau mbalimbali wa michezo hapa nchini zikiwemo kampuni za Freidkin Conservation Fund, African Wildlife Trust, Mwanza Hotel, Nyanza Bottlers Limited, Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),na kampuni ya ujenzi kutoka China ya CRJE na kampuni ya Real PR Solutions kwa kudhamini mbio hizo.


Mkuu wa mkoa wa Mwanza ndg John Mongella (alievaa kofia nyeusi) sambamba na Rais wa Chama cha Riadha Tanzania ambae pia ni mkuu wa Mkoa wa Simiyu Bw Anthony Mtaka ( wa kwanza kulia) wakisaini fomu za ushiriki wa Rock City Marathon inayotarajiwa kufanyika September 25 mwaka huu katika viwanja vya CCM Kirumba jijini Mwanza. Anaeshuhudia ni Makamu Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi yam bio hizo Bw Zenno Ngowi (wa tatu kulia)
ais wa Chama cha Riadha Tanzania ambae pia ni mkuu wa Mkoa wa Simiyu Bw Anthony Mtaka (kulia) akimkabidhi Makamu Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mbio hizo Bw Zenno Ngowi (kushoto) fomu za ushiriki wa Rock City Marathon inayotarajiwa kufanyika September 25 mwaka huu katika viwanja vya CCM Kirumba jijini Mwanza baada ya kusaini ili kuthibitisha ushiriki wake kwenye mbio hizo. Anaeshuhudia (katikati) ni Mkuu wa mkoa wa Mwanza ndg John Mongella.
Meneja Mkuu wa Mwanza Hotel Bw Senthil Kumar (wa pili kulia)ambaye ni moja wa wadhamini wa mbio hizo akiwa na baadhi ya wageni waalikwa wakifuatilia kwa umakini hotuba ya mgeni rasmi.


Makamu Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mbio hizo Bw Zenno Ngowi akitoa taarifa fupi kuhusu mbio hizo mbele ya mgeni rasmi na wageni waalikwa.
Rais wa Chama cha Riadha Tanzania ambae pia ni mkuu wa Mkoa wa Simiyu Bw Anthony Mtaka akizungumza kuhusu mbio hizo wakati hafla hiyo.
Mgeni rasmi ambae ni Mkuu wa mkoa wa Mwanza ndg John Mongella akizungumza kwenye hafla hiyo. Pamoja na mambo mengine Bw Mongella alielezea adhma yake ya kushirikia mbio za kilomita 21 kwenye Rock City Marathon.
Mgeni rasmi ambae ni Mkuu wa mkoa wa Mwanza ndg John Mongella ( mwenye kofia nyeusi) pamoja na Rais wa Chama cha Riadha Tanzania ambae pia ni mkuu wa Mkoa wa Simiyu Bw Anthony Mtaka (watatu kushoto) wakiwa kwenye picha ya pamoja na waandaaji wa Rock City Marathon, wadhamini na maofisa wa michezo kutoka mkoa wa Mwanza.
Kwa upande wake Mratibu wa Mbio hizo kutoka kampuni ya Capital Plus Bw Mathew Kasonta alisema Rock City Marathon zitahusisha makundi matano yaani mbio za kilomita 21 kwa wanaume na wanawake, kilomita 5 kwa ngazi ya ‘corporate’, kilomita 3 kwa ajili ya walemavu na zile za wazee umri zaidi miaka 55 na kuendelea pamoja na kilomita 2 kwa ajili ya watoto umri kati ya miaka 7 hadi 19.

Pia litoa wito kwa wakazi wa jiji la Mwanza na mikoa jirani kujisajili kwa kuchukua fomu katika ofisi za michezo kwenye mikoa na wilaya zote za mkoa huo.

“Kwa upande wa Dar es Salaam Fomu za ushiriki pia zinapatikana katika ofisi za Kampuni ya Capital Plus International zilizopo ghorofa ya tatu jengo la ATC, jijini Dar es, Salaam na vituo vingine vitatangazwa hivi karibuni,” alihitimisha.

MTOTO ATOA MSAADA WA MADAWATI DODOMA

$
0
0

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Christina Mndeme (kushoto) akimshukuru mtoto Aisha Mshantu kwa Msaada wa madawati 50 yenye thamani ya shilingi milioni 5.2 aliyoyatoa katika shule ya Msingi Mwenge iliyopo Kata ya Mbabala Manispaa ya Dodoma. .
Mtoto Aisha Mshantu (kulia )akimkabidhi madawati 50 yenye thamani ya shilingi milioni 5.2 Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Christina Mndeme aliyoyatoa katika shule ya Msingi Mwenge iliyopo Kata ya Mbabala Manispaa ya Dodoma.
Mtoto Aisha Mshantu na wazazi wake Mzee Mshantu (wa kwanza kulia) na Bi Rehema (wa pili kulia) wakiwa amekaa katika madawati aliyoyatoa mtoto huyo kama msaada katika shule ya Msingi Mwenge iliyopo Kata ya Mbabala Manispaa ya Dodoma. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Christina Mndeme. PICHA KWA HISANI YA OFISI YA MKURUGENZI WA MANISPAA

MAADHIMISHO YA SIKU YA WAKULIMA KATIKA VIWANJA VYA NANE NANE NJIRO JIJINI ARUSHA

$
0
0

Mkulima wa zao la viazi vitamu akionesha namna viazi vinavyoweza kutengeneza bidhaa zaidi ya moja ikiwemo "tambi" na "crips"

Mboga aina ya kabichi zikiwa katika ubora wa hali ya juu .
Hakika kilimo kinapendeza .

Baadhi ya vijana waliofika katika banda la wizara ya Kilimo na Mifugo wakipata maelezo juu ya ufagaji wa ng'ombe wa kisasa maalumu kwa ajili ya maziwa Dkt John Mpinga kutoka Luti Campus Tengeru . PICHA NA GADIOLA EMANUEL

Na Dickson Mulashani

Vijana nchini wamehimizwa kushiriki kikamilifu katika shughuli za kimaendeleo ikiwemo kilimo ikiwa ni sehemu ya kujikwamua na kuliletea Taifa maendeleo sambamba na kumuunga mkono Rais kwa kauli mbiu yake ya HAPA KAZI TU!.

Hamasa hiyo inadhihirika wazi kupitia kauli mbiu ya maadhimisho ya siku ya wakulima maarufu zaidi kama nanenane mwaka 2016 inayosema KILIMO MIFUGO NA UVUVI NI NGUZO YA MAENDELEO, VIJANA SHIRIKI KIKAMILIFU “HAPA KAZI TU” ambapo kitaifa yataadhimishwa mkoani Morogoro.


Ikiwa ni siku za mwanzo,mwitikio wa wananchi unaonekana kuwa mzuri .Picha hizi ni kutoka viwanja vya nane nane vilivyopo Njiro mkoani Arusha .
Afisa wa kampuni inayojishughulisha na utengenezaji wa nishati kwa ajili ya matumizi ya nyumbani akielekeza namna mkaa unaotengenezwa kutumia pumba unavyofanya kazi .
Mmoja wa waliotembelea banda la TAHA akiangalia kwa makini zao la Hoho iliyonona vyema ambayo ni sehemu ya mradi wa TAHA .
Sehemu ya mabanda ya maonesho yalivyotawala katika viwanja vya nanenane Njiro mkoani Arusha
Wizara ya Maliasili na Utalii nao tayari wamepiga kambi katika viwanja hivyo

CHUO CHA UONGOZI WA FEDHA ZANZIBAR CHAANZISHA MPANGO WA KUWAPELEKA WANAFUNZI WAKE KUFANYA MAZOEZI YA VITENDO KATIKA TAASISI ZA KIJAMII

$
0
0

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto Mauwa Makame Rajab akifunga mafunzo elekezi ya wanafunzi wa Chuo cha Uongozi wa Fedha Zanzibar watakaoshiriki mazoezi ya vitendo katika vikundi vya kijamii (kushoto) Mkurugenzi wa Vyama vya Ushirika Zanzibar Khamis Simba na (kulia) Kaimu Mkuu wa Chuo Dkt. Iddi.



Baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha Uongozi wa Fedha Zanzibar wakifuatilia ufungaji wa mafunzo elekezi yaliyofanyika katika Chuo chao Chwaka Mkoa Kusini Unguja.
Mratibu wa mafunzo elekezi ya wanafunzi wa Chuo cha Uongozi wa Fedha Zanzibar Said Mohd Khamis akieleza lengo la Chuo kuanzisha mpango wa wanafunzi kufanya mazoezi ya vitendo katika taasisi za kijamii.PICHA NA RAMADHANI ALI/HABARI MAELEZO ZANZIBAR.

Na Ramadhani Ali/Maelezo Zanzibar 3.8.2016

CHUO cha Uongozi wa Fedha Zanzibar (ZIFA) kimeanzisha mpango wa kuwapeleka wanafunzi wa Chuo hicho kufanya mazoezi ya vitendo katika vikundi vya Kijamii (SACCOS) kuanzia mwaka huu. 

Uamuzi huo unafuatia muongozo uliotolewa na Baraza la Chuo baada ya kubaini kuwa wanafunzi wengi wanapokuwa katika mazoezi ya vitendo katika Mawizara, Maidara na Taasisi za Umma wanakaa maofisini bila ya kufanya kazi yoyote na kutofaidika na mazoezi yao.

Jumla ya wanafunzi 130 wa mwaka wa pili shahada ya kwanza wanaosoma fani ya Uhasibu, Manunuzi na Tehama wataanza mazoezi ya vitendo katika SACCOS za Unguja na Pemba baada ya kupatiwa mafunzo elekezi ya siku tatu yaliyotolewa na Idara ya Vyama vya Ushirika kwa kushirikiana na ZIFA.

Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo, Mhadhiri wa Chuo cha Uongozi wa Fedha Maalim Said Mohd Khamis alisema lengo la mpango huo ni kuwawezesha wanafunzi kutoa elimu kwa jamii baada ya masomo yao.

Amesema vyama vingi vya ushirika vinakabiliwa na matatizo hasa katika masuala ya uhasibu, manunuzi na matumizi ya Tehama hivyo wanafunzi wao watakwenda kusaidia katika kutoa elimu kwa wanachama wa vikundi hivyo.‘’Wanafunzi wetu watakwenda kufundisha matumizi ya Teknolojia ya kisasa, utaratibu mzuri wa manunuzi na masuala ya uhasibu”, alisisitiza Maalim Said.

Ameongeza kuwa mtazamo wa Chuo ni kutoa huduma na fursa zinazopatikana chuoni hapo kwa jamii ili kuisaidia Serikali katika juhudi zake za kuwapunguzia wananchi hali ngumu ya maisha.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto Mauwa Makame Rajab amewaeleza wanafunzi hao kuwa baadhi ya SACCOS wanachama wake hawana taaluma kubwa katika masuala ya ushirika hivyo mchango wao utasaidia sana katika kuviimarisha vikundi hivyo.

Amewataka vijana hao kuitumia elimu waliyonayo na fursa waliyopata ya kufanyakazi katika vikundi vya kijamii vijijini kujiajiri kwa kuanzisha SACCOS ama kuongoza ziliopo katika kukabiliana na tatizo kubwa la ajira liliopo.Amewashauri wanafunzi hao kuwa mabalozi wazuri katika sehemu watakazokwenda kupinga vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia vinavyozidi kuongozeka katika maeneo mbali mbali ya Unguja na Pemba.

Aidha amevishauri vyuo vyengine viliopo Zanzibar na Tanzania kwa jumla kuiga mfano ulioonyeshwa na ZIFA kuwapeleka wanafunzi wao kufanya mazoezi ya vitendo katika vikundi vya kijamii kusaidia masuala mbali mbali ikiwemo sheria, uongozi demokrasia ndani ya vikundi vyao.

Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo cha Uongozi wa Fedha Zanzibar amesema wameupokea mpango wa Chuo kwenda kusaidia vikundi vya ushirika vijijini kwa moyo safi na ameahidi watatoa mchango mkubwa.

Amesema wanauchukulia mpango huo kama ni majaribio kwao na watajitahidi kuweka mazingira mazuri na kuwa mfano wa kuigwa na wanafunzi wenzao watakaofuata hapo baadae.

Wekeza kwenye mwanzo mzuri wa elimu ya Mtoto wako, Beginners Foundation Center ndio chaguo sahihi.

$
0
0
Welcome to Beginner's Foundation Center on 6th August 2016 open from 10.00 am to 4.30 pm, (Come in! Sit down, stay and see how we spend our day.) 

Plot 4, Sinza Mori behind Wanyama Hotel










MBOWE AMTEMBELEA SPIKA WA BUNGE NDUGAI NYUMBANI KWAKE JIJINI DAR LEO

$
0
0

Kiongozi wa Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni Mhe Freeman Mbowe akisalimiana na Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai alipomtembelea nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam.Spika wa Bunge amerejea nchini hivi karibuni kutoka nchini India alipokwenda kwa ajili ya uchunguzi wa afya yake.
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akizungumza na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya upinzani Bungeni Mhe Freeman Mbowe aliyemtembelea Nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam.
iongozi wa Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni Mhe Freeman Mbowe akizungumza na Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai alipomtembelea Nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam.(Picha na Ofisi ya Bunge)

BANDA LA NSSF LAVUTIA WENGI KWENYE MAONESHO YA NANENANE LINDI

$
0
0
Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) linashiriki kwenye maonesho ya nanenane ambayo yanafanyika kitaifa katika viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.

Katika maonesho hayo NSSF inatoa huduma mbalimali zikiwemo kutoa taarifa za michango za wanachama, kuandikisha wanachama wapya na kutoa kadi mpya kwa wanachama wa zamani, kutoa maelezo juu ya uuzaji wa nyumba za mtoni kijichi phase 3 na Viwanja vya Kiluvya na pia kutoa elimu ya mafao na huduma mbalimbali zitolewazo na NSSF.NSSF inapenda kuwakaribisha wananchi wa Lindi na Mtwara kutembelea banda lao lililopo kwenye viwanja hivyo vya Ngongo.
Afisa wa NSSF mkoa wa Lindi, Saad Juma akitoa maelezo kwa wananchi wa Mkoa wa Lindi waliotembelea banda la NSSF kwenye maonesho ya Nanenane mkoani humo.
Afisa Matekelezo wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), mkoa wa Lindi, Adam Mbena akimwandikisha kujiunga na NSSF mmoja wa wakazi wa Lindi aliyetembelea kwenye maonesho ya Nanenane.
Afisa Masoko Muandamizi Amina Mmbaga akiwapa maelezo wakazi wa Lindi waliotembelea banda la NSSF kwenye maonesho ya nanenane anayoendelea mkoani Lindi.
Wakazi wa Mkoani Lindi wakiingia kwenye banda la NSSF ili kupata taarifa mbalambali kwenye maonesho ya nanenane yanayoendelea kwenye viwanda vya ngongo Mkoani Lindi.
Wakazi wa Mkoani Lindi wakiingia kwenye banda la NSSF ili kupata taarifa mbalambali kwenye maonesho ya nanenane yanayoendelea kwenye viwanda vya ngongo Mkoani Lindi.

Afisa Mifumo ya Kompyuta Rukia Penza akimuelezea mwanachama taarifa yake ya Michango alipotembelea banda la NSSF kwenye maonesho ya nanenane Lindi
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live




Latest Images