Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46201 articles
Browse latest View live

WADAU WA SEKTA YA AFYA KANDA YA KASKAZINI WAKUBALIANA KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA.

0
0
  Meneja Masoko wa AAR Insurance Tanzania, Tabia Masoud akiongea machache.
  Meneja Masoko wa AAR Insurance Tanzania, Tabia Masoud akitambulisha wafanyakazi wenzake kwa wadau wa sekta ya afya wa mkoa kanda ya Kaskazini wakati wa mkutano wa kampuni hiyo na wadau hao kujadiliana namna ya kuboresha huduma za afya jana jijini Arusha.
  Meneja Maendeleo ya Biashara wa AAR Insurance Tanzania, Hamida Nassor akijadiliana jambo na wadau mbalimbali waliohudhuria mkutano kati ya kampuni hiyo na wadau wa sekta ya afya kanda ya kaskazini kujadiliana namna ya kuboresha huduma za afya jana jijini Arusha
Wadau wa sekta yaw a kanda ya kaskazini wakijadiliana wakati wa mkutano kati yao na kampuni ya bima ya afya ya AAR Insurance Tanzania juu ya namna ya kuboresha huduma za afya jana jijini Arusha.
 Wadau wakijiandikisha.


 Wadau wakiwa katika picha ya pamoja. 

Ikiwa ni sehemu ya jitihada zake kuimarisha utoaji huduma za afya nchini, kampuni ya bima ya AAR Insurance Tanzania pamoja na wadau wake waliopo Kanda ya Kaskazini wamekubaliana kuhakikisha huduma zitolewazo kwa wateja wake zinakuwa za ubora wa hali ya juu na za kuridhisha. Maazimio hayo yamefikiwa baada ya wadau hao kukutana jijini Arusha mwishoni mwa wiki ambapo walijadiliana mikakati na changamoto za kiutendaji zinazokabili utoaji huduma za afya.

Akiongea katika mkusanyiko huo uliojumuisha wadau kutoka hospitali mbalimbali, vituo vya afya, zahanati, kliniki na maduka ya dawa kutoka mikoa ya kanda ya kaskazini, Mkuu wa Operesheni wa AAR Insurance Tanzania, Wilfred Rono alisema ubora wa huduma ya afya unaweza kuboreshwa na uongozi bora, kuwa na mipango mizuri, elimu na mafunzo, upatikanaji wa rasilimali, menejimenti thabiti ya rasilimali, wafanyakazi, na ushirikiano miongoni mwa wadau na akaongeza kuwa ni muhimu kwa wadau hao kukutana na kuweka mikakati.

Wilfred Rono pia aliongeza kwamba dhumuni la tukio hilo lilikuwa ni kuimarisha uhusiano kati ya kampuni hiyo kubwa zaidi ya bima ya afya na wadau wake huku na kuongeza kuwa mkutano huo umetumika kuelimisha wadau juu ya bidhaa na huduma za bima ya afya.

AAR Insurance Tanzania ni sehemu ya AAR Insurance Holdings ambayo ndio kampuni kubwa zaidi ya bima za afya kwenye ukanda wa Afrika Mashariki.

Haki Madini waendesha mdahalo wa maendeleo ya uchumi na uwekezaji kwenye madini Simanjiro.

0
0

Mkurugenzi wa Shirika la Haki Madini, Amani Mustafa Mhinda akizungumzia juu ya ugatuzi na ugatuaji wa madaraka kwa wadau wa madini ya Tanzanite wa Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, katika mdahalo wa siku mbili wa maendeleo ya uchumi na uwekezaji kwenye madini unaofanyika Mirerani na kuandaliwa na shirika hilo.
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Albert Msole (katikati), Diwani wa Kata ya Mirerani Yohana Onyango, (kushoto) na Mwenyekiti wa mtaa wa Twiga Anthony Musiba, wakifuatilia mdahalo siku mbili wa wa maendeleo ya uchumi na uwekezaji kwenye madini, juu ya mpango wa uhamasishaji na uwazi katika katika mapato ya madini, gesi asilia na mafuta unaonyika Mji mdogo wa Mirerani na kuandaliwa na shirika la Haki Madini.Wadau wa madini ya Tanzanite wa Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, wakifuatili mdahalo wa siku mbili wa maendeleo ya uchumi na uwekezaji kwenye madini uliondaliwa na shirika la Haki Madini.

Rais Magufuli akamilisha ziara ya siku nne Singida, Tabora, Shinyanga na Geita atoa maagizo Elimu

0
0



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewaagiza viongozi wote wa kuanzia ngazi ya Mkoa hadi Kitongoji hapa nchini kufuatilia matumizi ya fedha zinazotolewa na Serikali kwa ajili ya kutoa elimu bila malipo kwa lengo la kudhibiti mianya ya matumizi mabaya ya fedha hizo.

Rais Magufuli ametoa maagizo hayo leo tarehe 01 Agosti, 2016 katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Mnadani na kuwajumuisha wananchi wa Katoro na Buseresere Mkoani Geita.Katika agizo hilo Dkt. Magufuli amewaonya walimu ambao wameanza kufanya udanganyifu kwa kuandikisha idadi kubwa ya wanafunzi kuliko idadi halisi kwa lengo la kupata mgao mkubwa wa fedha za ruzuku na amesema Serikali itachukua hatua kali dhidi ya yeyote atakayebainika kufanya hivyo.

"Ninafahamu mgao wa fedha hizo hutolewa kulingana na idadi ya wanafunzi waliopo, wapo baadhi ya walimu ambao wameanza kuandika wanafunzi hewa katika shule zao, ili kusudi aletewe hela nyingi kuliko idadi ya wanafunzi waliopo, wanafunzi kama wapo laki nne yeye anasema shule yangu hii ina wanafunzi laki tano, ili kusudi hela zikija za wanafunzi laki tano, za wanafunzi laki moja wagawane."Napenda nitoe wito kwa walimu Tanzania nzima, mnatafuta matatizo, narudia mnatafuta matatizo, msijaribu kula hela ya Serikali" Amesema Rais Magufuli.

Pamoja na agizo hilo, Rais Magufuli pia ametaka viongozi wa ngazi zote katika Mikoa kuhakikisha wana takwimu za idadi ya wanafunzi katika shule zote zilizopo katika maeneo yao ili kurahisisha ufuatiliaji wa fedha hizo na amesema kuwa kuanzia sasa ataanza kutembelea shule kwa kushitukiza na kwamba kiongozi atakayeonekana kutojua takwimu itakuwa ni uthibitisho kuwa hatoshi kuendelea na wadhifa alionao.

"Na nitoe wito kwa viongozi wa Mikoa, Mkuu wa Mkoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi, Makatibu Tarafa, Watendaji wa Kata, Wenyeviti wa Vijiji, kila mmoja awe na idadi ya wanafunzi waliopo katika shule zao, hatutaki kuwapunja wanafunzi hela ambayo wanatakiwa kupata, lakini pia hatutaki kutoa hela ambayo haitakiwi"Amesisitiza Rais Magufuli.

Mhe. Rais Magufuli ambaye ametumia mkutano huo kueleza juhudi mbalimbali zilizofanywa na Serikali yake ya Awamu ya Tano, kutekeleza ahadi yake ya kujenga Tanzania Mpya pia amewataka viongozi na watendaji wa Serikali kutekeleza wajibu wao kwa kutembelea wananchi wanaowaongoza badala ya kukaa muda mwingi ofisini huku akisisitiza ofisi hizo kuwepo katika maeneo yenye shughuli husika.

Aidha, Dkt. Magufuli amekosoa utaratibu unaotumiwa na Halmashauri nyingi za Majiji, Manispaa, Miji na Wilaya kutumia mawakala katika ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri akisema mawakala hao wamekuwa wakitumia utaratibu huo kukusanya fedha nyingi na kisha kuwasilisha kiasi kidogo katika Halmashauri husika.

"Hivi kwa nini Halmashauri msingekuwa na maafisa wenu wazuri na mkawa na mashine za kielektroni kwa ajili ya kukusanya fedha? Amehoji Dkt. Magufuli na kuongeza kuwa "tena mawakala wengine ndio hao hao wamekuwa wakikusanya kodi hata kwa wananchi wanyonge wenye vibiashara vidogo vya kuuza mchicha bila hata kuwaonea huruma"

Rais Magufuli ambaye ameongozana na Mkewe Mama Janeth Magufuli amemaliza ziara yake ya siku nne katika Mikoa ya Singida, Tabora, Shinyanga na Geita na yupo nyumbani kwake Chato Mkoani Geita kwa mapumziko mafupi.


Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Chato
01 Agosti, 2016

KAPUMZIKE KWA AMANI MPIGANAJI MWENZETU JOSEPH SENGA

0
0
Waombolezaji wakilishusha jeneza lenye mwili wa marehemu Joseph Senga, aliyekuwa mpiga picha mkuu wa gazeti la Tanzania Daima, wakati wa mazishi yake yaliyofanyika Mchana wa leo kwenye Makaburi ya Kijijini kwao, Shushu wilayani Kwimba mkoani Mwanza. Marehemu Senga alifariki wiki iliyopita nchini India alikokuwa akipatiwa matibabu ya moyo. Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi AMIN.
Mjane wa Marehemu Joseph Senga, Bi. Winfrida Senga akiweka shada la maua kwenye Kaburi la Mumewe, wakati wa mazishi yaliyofanyika Mchana wa leo kwenye Makaburi ya Kijijini kwao, Shushu Kwimba, Jijini Mwanza.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe akiweka shada la maua katika kaburi la aliyekuwa Mpigapicha Mkuu wa gazeti hili, marehemu Joseph Senga wakati wa mazishi yake yaliyofanyika katika Kijiji cha Shushi Wilaya ya Kwimba, Mwanza. 
Mbunge wa Jimbo la Sumve, Richard Ndassa akiweka shada la Maua.
Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe, ambaye pia ni Mmiliki wa Kampuni ya FreeMedia wachapishaji wa Gazeti la Tanzania Daima alikokuwa akifanya Kazi Marehemu Joseph Senga, akitoa salamu za Rambirambi, wakati wa Mazishi yaliyofanyika Mchana wa leo kwenye Makaburi ya Kijijini kwao, Shushu Kwimba, Jijini Mwanza.
Ibada ya Mazishi ikiendelea.
Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Tanzania Daima, Neville Meena akiweka shada la maua kaburini.

Njoo Uzijue Siri za Kufanikiwa Kwenye Hali Ngumu ya Uchumi

0
0
semina

JIACHIE NA NGOMA HII: Rogers Lucas feat Josee Mtambo - siri ya maumivu

0
0

MO DEWJI AMWAGA MILIONI 100 ZA USAJILI SIMBA SC JIJINI DAR LEO

0
0
Mfanyabiashara maarufu nchini, Mohammed Dewji ameanza kuinufaisha klabu ya Simba baada ya kuipatia sh milioni 100 kwa ajili ya kusaidia zoezi la usajili. 

Dewji alikabidhi fedha hizo kwa Rais wa klabu ya Simba, Evans Aveva katika hafla fupi iliyofanyika makao makuu ya kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited zilizopo jengo la Golden Jubilee,jijini Dar. Akizungumza katika makabidhiano hayo, Dewji alisema kuwa fedha hizo ni mchango wake kwa timu hiyo ili kusajili wachezaji ambao imepanga kuwaongeza katika zoezi ambalo litaisha Agosti 6. 

Dewji alisema kuwa amefurahishwa sana na hatua ya uongozi na wanachama wa klabu hiyo kubariki mabadiliko ya uendeshaji na kuingia katika mfumo wa hisa. “Huu ni mchango wangu kama mwanachama wa klabu, nina mambo mengi mazuri yanakuja wakati wa kufanya mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa klabu,” alisema Dewji. 

“Simba SC ni timu kubwa sana, ina wanachama na mashabiki wengi, inahitaji kuwa na hadhi ya pekee kabisa, naamini kwa mchango huu, uongozi utaweza kumsajili mchezaji kutoka Ivory Coast ambaye kwa sasa anasubiri fedha ili aweze kusaini,” alisema. 

Rais wa Simba, Evans Aveva alimshukuru Dewji kwa msaada huo ambao utawawezesha kumsajili mchezaji, Frederick Blagnon. Alisema kuwa kwa sasa klabu yao inahitaji Sh milioni 320 ili kukamilisha usajili na kuwaomba wadau wengine kumuunga mkono Dewji.

Mfanyabiashara maarufu nchini Mohamed Dewji akimkabidhi mfano wa hundi sh. milioni 100 Rais wa Simba SC, Evans Aveva kama mchango wake katika usajili wa klabu hiyo leo ofisini kwake,jijini Dar es salaam.
Mfanyabiashara maarufu nchini Mohamed Dewji a.k.a Mo Dewji akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari mapema leo jijini Dar,alipokuwa akikabidhi mfano wa hundi ya sh. milioni 100 kwa Rais wa simba sc,(pichani kushoto) Evans Aveva kama mchango wake katika usajili wa klabu hiyo.
Baadhi ya Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakisikiliza yaliyokuwa yakijiri ukumbini humo.

MHE. KAIRUKI KATIKA KIKAO KAZI WATUMISHI KUJADILI MATUMIZI YA TEHAMA SERIKALI

0
0

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) (kulia) akimsikiliza Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Utumishi, Dkt. Laurean Ndumbaro (aliyeinua mkono) alipokuwa akifafanua jambo wakati wa kikao kazi na baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Rais- Utumishi kuhusu utoaji huduma na matumizi ya TEHAMA katika Utumishi wa Umma kilichofanyika katika ukumbi wa utumishi leo, wa tatu kulia (mstari wa mbele) ni Naibu Katibu Mkuu Utumishi na Utawala Bora, Bi. Susan Mlawi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akielekeza jambo kwa baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Rais Utumishi wakati wa kikao kazi kuhusu utoaji huduma na matumizi ya TEHAMA kilichofanyika katika ukumbi wa utumishi leo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akimsikiliza Mkurugenzi wa TEHAMA katika Utumishi wa Umma, Bw. Priscus Kiwango wakati wa kikao kazi kuhusu utoaji huduma na matumizi ya TEHAMA katika Utumishi wa Umma kilichofanyika katika ukumbi wa utumishi leo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) na baadhi ya Watumishi wa Ofisi ya Rais-Utumishi wakijadili kuhusu matumizi ya TEHAMA katika utoaji huduma Serikalini wakati wa kikao kazi kilichofanyika katika ukumbi wa utumishi leo.

TIMU TEULE ZA JESHI KUKABIDHIWA BENDERA KWA AJILI YA KUELEKEA RWANDA KESHO(LEO)

0
0
Wanariadha wa Timu Teule ya JWTZ wakifanya mazoezi katika Kambi iliyoko Mbulu Mkoani Manyara.Picha na Maktaba

Na mwandishi wetu JWTZ.

Timu teule za Jeshi la wananchi wa Tanazania zinazotarajiwa kushiriki mashindani ya majeshi kwa nchi za Afrika mashariki zinatarajiwa kukabidhiwa bendera ya Taifa Kesho(Leo) tayari kuelekea Kigali chini Rwanda kwa ajili ya mashindano hayo. 

Kwa Mijubu wa Afisa habari wa Michezo Kutoka makao Makuu ya Jeshi Luteni Selemani Semunyu alisema mkuu wa Operesheni na mafunzo Meja Jenerali Issa Nassoro ndiye anayetarajiwa kukabidhi bendera hiyo kwa Niaba ya Mkuu wa majeshi Jenerali Davis Mwamunyange.

Luteni Semunyu alisema kuwa Hatua hiyo inafikiwa baada ya Timu hizo kuweka kambio katika Visiwa vya Zanziba kwa Michezo minne huku Riadha wakiweka kambi Arusha kabla ya kambi hiyo kuhamishiwa mbulu Mkoani Manyara kutokan na haliya hewa. 

Aliitaja Michezo hiyo kuwa mpira wa miguu,pete,Mikono,Kikapu na Riadha ambapo wachezaji wako katia ari ya hali ya juu kutokana na wito wa mkuu wa majeshi kuwatak kurejesha hshima ya JWTZ katika Michezo.
ASlifafanua kuwa QWachezaji wa Timu hizo teule walipatikana baada ya kupitia hatua mbali mbali za mcvhujo kwa kuanzi na kombe la Mkuu wa majeshi ambalo lilishirikisha kuanzia ngazi ya Viko mpaka kamandi na hivyo kuibua vipaji. 

Michezo ya majeshi kwa Nchi za Afrika Mashariki imekuwa ikifanyika kila mwaka kwa kuhama nchi wenyeji kutoka na utarativbu waliojipangia nchi wananchama ndio maan mwaka huu yanafanyika nchini Rwanda na Mwakani yatahamia katika nchi nyingine amabayo itatangazwa baada ya kumalizika mashindano haya. 

Timu teule za Jeshi zinatarajia kuanza safari kuelekea Kigali nchini Rwanda Agosti nne siku moja baada ya kukabidhiwa bendera ili kuwahi ratiba ya kuanza mashindano hayo yanayotarajia kuanza Agosti saba na Kumalaizika Agosti 17.

WAKUU WA IDARA WILAYANI IKUNGI, MAAFISA TARAFA, WATENDAJI WA KATA, VIJIJI NA WENYEVITI WA VIJIJI WAFUNDWA.

0
0
 Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu akisisitiza umuhimu wa kuchangia maabara kwa ajili ya kuwanusuru wanafunzi wanaotaka kusoma masomo ya sayansi lakini kikwaza inakuwa maabara
 Kutoka Kushoto ni Mustafa Mtopo kaimu Afisa usalama wa Taifa Wilaya ya Ikungi, Fortunatus Ndalama Mshauri wa Mgambo Wilaya ya Ikungi, Dijovson Ntangeki Kaimu Katibu Tawala Wilaya ya Ikungi, Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu, Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya ikungi Rustika Turuka, na Mkuu wa poiisi Wilaya ya Ikungi Milton Nkyalu wakifatilia mafunzo kutoka kwa wawasilishaji waliotoka ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya hiyo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya ikungi Rustika Turuka aliyesimama akizungumza na Wakuu wa Idara na vitengo, Maafisa Tarafa, Watendaji wa Kata, Vijiji, na Wenyeviti wa Vijiji wakati wa kikao hicho cha kazi.
 Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu akiwasilisha mtazamo wa namna ambavyo anataka Wilayahiyo iwe.

 Wakuu wa Idara na vitengo, Maafisa Tarafa, Watendaji wa Kata, Vijiji, na Wenyeviti wa Vijiji wakifatilia mafunzo kutoka kwa wawasilishaji
 Afisa utumishi wa Wilaya ya Ikungi Evodius Buberwa akifafanua na kutofautisha majukumu ya watendaji wote ngazi ya Wilaya, Tarafa, Kata na Vijiji
 Afisa utumishi wa Wilaya ya Ikungi Ahmed Mussa akiwasilisha madawakati wa mafunzo hayo.
Kaimu katibu Tawala wa Wilaya ya Ikungi Dijovson Ntangeki akielezea ratiba ilivyo ya mafunzo hayo

Na Mathias Canal, Singida
Wakuu wa Idara na vitengo, Maafisa Tarafa, Watendaji wa Kata, Watendaji wa vijiji na wenyeviti wa vijiji 101 vilivyopo Wilayani Ikungi Mkoani Singida hii leo wamepatiwa mafunzo ya kutambua mipaka ya majukumu yao kiutendaji katika kikao cha kazi kilichofanyika katika ukumbi wa shule ya sekondari Ikungi.

Mafunzo hayo yameandaliwa na uongozi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo kutokana na kubainika kuwa asilimia kubwa ya watendaji hususani wenyeviti wa vijiji na vitongoji wamekuwa wakiingilia katika majukumu ya kiutendaji.

Akifungua mafunzo hayo yaliyodumu kwa zaidi ya masaa matano yaliyojikita zaidi kutoa ufafanuzi juu ya majukumu ya watendaji wa Kata, Wenyeviti wa Vijiji na Watendaji wa Vijiji, Mkuu wa Wilaya hiyo Miraji Jumanne Mtaturu amebainisha kuwa pamoja na mafunzo kwa ajili ya ufahamu wa majukumu ya watendaji hao lakini amesema kuwa Wilaya ya Ikungi ipo nyuma kielimu kutokana na shule kuwa mbali na maeneo ya watu, wanafunzi wa kike kuachishwa shule na kuolewa, baadhi ya viongozi na wataalamu kutotimiza wajibu wao na wakati mwingine uzembe wa baadhi ya watumishi wa serikali katika kutatua kadhia za wananchi.

Pamoja na hayo pia DC Mtaturu amesema kuwa kuna baaadhi ya maeneo kuna shule ambazo zina majengo mazuri na Hosteli kwa ajili ya wanafunzi lakini wazazi wanakataa kuwapeleka wanafunzi shuleni ikiwa ni pamoja na shule ya Sekondari Mkinya iliyopo Kata ya Dung’unyi, Shule ya Sekondari Mtunduru, Shule ya Sekondari Mwaru na Wembere , huku shule ya Sekondari Issuna ikiwa na Majengo na Hosteli nzuri lakini wanafunzi wanaosoma hapo ni wale wanaotoka Wilaya nyingine huku wenyeji wakiwa wamejichimbia ndani. 

Dc Mtaturu amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya hiyo kwa kushirikiana na Polisi kufanya uchunguzi na kuwachukulia hatua baadhi ya Watendaji wa Kata, Waratibu wa elimu wa Kata, Wenyeviti wa Vijiji na Watendaji wa Vijiji wanaoshirikiana na baadhi ya wazazi kuwaachisha wanafunzi shule ili wakaolewe ambapo amebaini kuwa katika Kata ya Mwaru na baadhi ya Kata zinazozunguka katika Kata hiyo viongozi wake kwa kushirikiana na Waratibu elimu Kata wamekuwa wakifanya biashara ya kuruhusu wanafunzi kuolewa kwa kupewa Ng’ombe.

Hata hivyo pia amewaagiza Watendaji wa Kata ya Makilawa na Iyumbu kumpatia taarifa ya kamati ya maendeleo ya Kata (WDC) ili kubaini mpango wa mikakati katika kujenga shule za Sekondari katika Kata hizo mbili ambazo zimesalia ilihali Kata 28 tayari zina shule za sekondari kati ya Kata 30 zilizopo katika Wilaya hiyo.

Katika shule 28 ni shule 3 tu zenye maabara, shule ya Sekondari ya Puma na Wembere ambao nao walijenga maabara baada ya kupata msaada kutoka Benki ya dunia Mwaka 2013, shule ya Sekondari Mkinya ina maabara 2 ambazo zilijengwa kwa msaada wa SADC mwaka 2009 hivyo kupelekea Wilaya nzima ya Ikungi kuwa na Maabara 4 pekee zilizojengwa kwa msaada wa wahisani ambapo hakuna hata maabara moja iliyojengwa na wananchi ikakamilika kutokana na zuio la kuchangia walilolipata wananchi kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki Tundu Lissu.

Sawia na hayo pia Mkuu huyo wa Wilaya amewaagiza Watendaji wa Kata na Vijiji kwa kushirikiana na Wabunge, Madiwani na Wenyeviti wa Vijiji kuwaelimisha wananchi kukaa vikao na kupitisha maadhimio ya kuendelea kuchangisha michango ya ujenzi wa maabara kwa mujibu wa waraka wa Elimu namba 6 wa mwaka 2015 wa elimu msingi bila malipo.

Hata hivyo agizo limetolewa pia kwa Wazazi/Walezi pamoja na wanafunzi wenyewe kuchukuliwa hatua kali za kisheria kutokana na utoro wa wanafunzi shuleni jambo ambalo linapelekea kuwa na ufaulu duni wa wanafunzi Wilayani humo.

Dc Mtaturu pia amemuagiza Afisa Mtendaji wa Katana Afisa Mtendaji wa Tarafa kutumia siku 14 kuhakikisha madawati yanafika katika shule zenye uhaba wa madawati ili kuondokana na adha ambayo inaendelea kuwakumba wanafunzi shuleni ilihali madawati tayari yamepatikana.
Aidha ndani ya siku tano viongozi hao wameagizwa kuhakikisha kuwa Masoko pamoja na stendi zinaenda katika maeneo yaliyopangiwa ili ushuru upatikane kwa wakati na kwa kiasi kilichokusudiwa.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Rustika Turuka amewashukuru Watendaji wa Kata, Wenyeviti wa Vijiji na Watendaji wa Vijiji kwa kujitokeza kwa wingi katika mafunzo hayo jambo ambalo limeonyesha kuwa wananchi hao wana imani na serikali ya awamu ya nne hivyo amewaomba kuachana na siasa na kufanya kazi kwa moyo na nguvu zaidi.
Amewataka viongozi wote wa ngazi ya Wilaya, Tarafa, Kata, Vijiji na vitongoji kutekeleza maagizo yote yanayotolewa na serikali kwa haraka na kwa ukamilifu.

Turuka amesema kuwa kila kiongozi anapaswa Kutatua kero za wananchi kwa kutenda haki, kutofanya kazi kwa mazoea, kutoa majawabu sahihi ya wananchi na kama hawafahamu wanapaswa kuuliza sehemu husika ili kutozungumza jambo wasilokuwa na uhakika nalo.

Kupitia kikao hicho kilichoitishwa na mkuu huyo wa Wilaya kilichokuwa na dhumuni la kufahamiana na kukumbushana majukumu na wajibu wa viongozi na kueleza mtazamo wa Ikungi mpya inavyotakiwa kuwa Afisa utumishi wa Wilaya sawia na Mkuu wa Polisi Wilaya wamepewa nafasi ya kuelezea majukumu na wajibu wa kila mmoja katika maeneo yao.

Kwa upande wao baadhi ya Watendaji wa Kata, Vijiji na wenyeviti wa vijiji 101 vilivyopo Wilayani humo wamesema kuwa mafunzo waliyoyapata watayatumia vyema kuwa mabalozi wazuri kwa wananchi na kuwaelimisha zaidi ili kutambua mipaka yao na majukumu yao katika kuishauri serikali.
Aidha Maafisa Tarafa, Watendaji wa Kata, Watendaji wa vijiji na wenyeviti wa vijiji wote ambao hawajahudhuria kikao hicho cha kazi wametakiwa kuandika barua za maelezo kwanini wameshindwa kuhudhuria na zimetakiwa kupitia kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Ikungi hadi kufikia tarehe 10 ya mwezi huu wa nane.

MAREKANI YAIPIGA JEKI TANZANIA SHILINGI BILIONI 895

0
0
Mkurugenzi wa Shirika la Misaada la Maendeleo la Marekani, USAID, Bi. Sharon Cromer, na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile, wakitia saini Hati ya makubaliano ya msaada wa Zaidi ya shilingi Bilioni 895, kwaajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo hapa nchini katika kipindi cha miaka mitano ijayo kuanzia mwaka wa fedha 2016/2020, Jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Shirika la Misaada la Maendeleo la Marekani, USAID, Bi. Sharon Cromer (Kushoto), na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile, wakitia saini Hati ya makubaliano ya msaada wa Zaidi ya shilingi Bilioni 895, kwaajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo hapa nchini katika kipindi cha miaka mitano ijayo kuanzia mwaka wa fedha 2016/2020, Jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Shirika la Misaada la Maendeleo la Marekani, USAID, Bi. Sharon Cromer (Kushoto), na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile, wakibadilishana Hati za makubaliano ya msaada wa Zaidi ya shilingi Bilioni 895, kwaajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo hapa nchini katika kipindi cha miaka mitano ijayo kuanzia mwaka wa fedha 2016/2020, Jijini Dar es salaam
Kaimu Kamishna wa Fedha za Nje, Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Mamelta Mutagwaba, wakiteta jambo na Mkurugenzi wa Shirika la Misaada la Maendeleo la Marekani, USAID, Bi. Sharon Cromer (Katikati), baada ya kukamilika kwa tukio la utiwaji saini makubaliano ya msaada wa zaidi ya shilingi Bilioni 895, kwaajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo hapa nchini katika kipindi cha miaka mitano ijayo kuanzia mwaka wa fedha 2016/2020, Jijini Dar es salaam. Mkurugenzi wa Shirika la Misaada la Maendeleo la Marekani, USAID, Bi. Sharon Cromer (Kushoto), na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile, wakiwa wameshika Hati za makubaliano baada ya kukamilika kwa tukio la utiwaji saini makubaliano ya msaada wa Zaidi ya shilingi Bilioni 895, kwaajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo hapa nchini katika kipindi cha miaka mitano ijayo kuanzia mwaka wa fedha 2016/2020, Jijini Dar es salaam


Na Benny Mwaipaja, MoFP, Dar es salaam

SERIKALI ya Marekani, kupitia shirika lake la Misaada ya Maendeleo USAID, imeipatia Tanzania msaada wa dola Milioni 407 sawa na zaidi ya shilingi Bilioni 895 zitakazotumika kwaajili ya kuendeleza sekta za Kilimo, Afya, Nishati ya Umeme, Elimu na Utawala Bora, katika kipindi cha miaka mitano ijayo kuanzia mwaka 2016/2020.

Hati za Makubaliano hayo zimetiwa saini Jijini Dar es salaam, kati ya Mkurugenzi wa Shirika la USAID, Bi. Sharon Cromer, na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile.

Msaada huo ni sehemu ya dola Milioni 800, sawa na zaidi ya shilingi Trilion 1.76 ambazo serikali ya Marekani kupitia USAID, imepanga kuipatia Tanzania ili kufanikisha Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa katika kipindi cha miaka mitano ijayo, wenye lengo la kuiwezesha Tanzania kufikia uchumi wa kati kupitia sekta ya viwanda ifikapo mwaka 2025.

Kiasi hicho cha fedha kitatumika na serikali ya Tanzania kupitia mfuko mkuu moja kwa moja wakati kiasi kingine kitatumiwa na Taasisi zisizokuwa za kiserikali zinazofanya shughuli zake hapa nchini kufanikisha malengo ya msaada huo.

Miradi iliyopewa kipaumbele ni pamoja na kupambana na UKIMWI na Kifua Kikuu, Uzazi wa Mpango, Kupunguza vifo vya mama na mtoto, kukuza utawala wa kidemokrasia, Usimamizi wa Rasilimali za Taifa, na kuwekeza kwenye sekta ya umeme ili kuimarisha sekta ya viwanda na uzalishaji mali.

MAMLAKA YA USIMAMIZI NA UDHIBITI WA SEKTA YA HIFADHI YA JAMII (SSRA) KATIKA MADHIMISHO YA SIKUKUU YA WAKULIMA YANAYOFANYIKA KATIKA VIWANJA VYA NGONGO MKOANI LINDI

0
0

Mkuu wa Kitengocha uhusino na Uhamasishaji wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bi. Sarah Kibonde Msika (katikati) akigawa baadhi ya vifaa vya uhamasishaji kwa wadau waliotembelea banda la SSRA katika maonesho ya sherehe za Wakulima katika viwanja vya Ngongo mkoani Lindi jana. Maadhimisho ya sikukuu hiyo, yatafanyika Agost 8, 2016.
Bi. Sarah Kibonde Msika (kulia) na Bw. Mathayo Mihayo (Kushoto) wakitoa maelezo mbalimbali ya Hifadhi ya Jamii kwa wananchi waliotembelea banda la SSRA katika viwanja vya Ngongo mkoani Lindi katika maonesho ya Nane nane.
Wananchi mbalimbali wakipata maelezo ya Sekta ya Hifadhi ya Jamii kutoka kwa Wafanyakazi wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Hifadhi ya Jamii (SSRA) katika maonesho ya Nane nane.
Wananchi mbalimbali wakipata maelezo ya Sekta ya Hifadhi ya Jamii kutoka kwa Wafanyakazi wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Hifadhi ya Jamii (SSRA) katika maonesho ya Nane nane mjini Lindi jana.


Mkulima akipokea vipeperushi na maelezo toka kwa Afisa wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bw. David Mathayo katika maonesho ya wakulima Nane nane mkoani Lindi jana.
Afisa Uhusiano na Uhamasishaji Bi. Agnes Lubuva akitoa malezo na vipeperushi kwa wageni waliotembelea banda la SSRA katika Viwanja vya Ngongo mkoani Lindi wakati wa maonesho ya Wakulima jana.

MSANII PATORANKING AANZA ZIARA YA UZINDUZI WA ALBAMU YAKE NCHINI TANZANIA

0
0
 Mwanamuziki maaarufu anaetambulika zaidi kwa miondoko ya dancehall na reggae kutoka nchini Nigeria Patrick Nnaemeka Okorie aka Patoranking akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika ziara yake ya siku moja jijini Dar es salaam ya kuitambulisha album yake mpya inayokwenda kwa jina la “God over everything”. Pamoja nae ni Meneja Mkuu Masoko wa kampuni ya Spice Africa Joan Nkuzi ambapo kupitia programu yao ya Mziiki wanajishughulisha na uendelezaji wa kazi za wasanii mbalimbali nchini Tanzania na Afrika kwa ujumla.
 Mwanamuziki maaarufu anaetambulika zaidi kwa miondoko ya dancehall na reggae kutoka nchini Nigeria Patrick Nnaemeka Okorie aka Patoranking alipowasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) siku ya jana jioni kwa ziara yake ya siku moja tu jijini Dar es salaam ya kuitambulisha albamu yake mpya aliyoipa jina la “God over everything” kwa mashabiki wake nchini Tanzania.
Toka kushoto ni Meneja Mkuu Masoko wa kampuni ya Spice Africa Joan Nkuzi, Mwanamuziki maaarufu anaetambulika zaidi kwa miondoko ya dancehall na reggae kutoka nchini Nigeria Patrick Nnaemeka Okorie a.k.a Patoranking, Meneja bidhaa wa Spice Africa Mariam Nnauye pamoja na Meneja wa Msanii huyo nchini Tanzania Tom Raymond kwenye picha ya pamoja mara baada ya kumaliza shughuli ya utambulisho wa album ya msanii huyo kwa waandsihi wa habari katika hafla iliyofanyika jana usiku ndani ya ukumbi wa Paparazzi jijini Dar es salaam. Msanii huyo alikuwa nchini kwa ziara ya siku moja kuitambulisha albamu yake ya “God over everything” kwa mashabiki wake nchini Tanzania.

Albamu iliyokuwa ikisubiriwa kwa muda mrefu inayoitwa“God over Everthing” (GOE) kutoka kwa nyota wa mtindo wa reggae/dancehall wa kinigeria Patrick Nnaemeka Okorie a.k.a Patoranking hatimaye imekemilika.

Mara baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa mwalimu nyerere (JNIA) jana jioni, msanii huyo wa miondoko ya reggae pamoja na timu yake iliyopokelewa na Spice Africa, kampuni ambayo inayofanya kazi na Patoranking katika kutangaza mziki wake na usambazaji wa albamu mpya ya msanii huyo kwa nchini Tanzania.

Akizungumza kwenye mkutano wa vyombo vya habari uliofanyika katika ukumbi wa Paparazi-Slipway jioni hiyo hiyo, msanii huyo alitambulisha baadhi ya vibao/nyimbo zake ambazo ziko katika albamu hiyo, baadhi ambazo tayri zinafanya vizuri katia anga za kimataifa kama “Girlie O”, “My woman”, “Make Am”, “Another Level”, “Alubarika” na wimbo wake mpya wa hivi karibuni “No Kissing Baby”aliomshirikisha msanii Sarkodie kutoka Ghana. Albamu hiyo imebeba nyimbo zilizotengenezwa katika label yake ya VP records yenye idadi ya zaidi ya nyimbo 16.

“Albamu hii ni ya kipekee; ina nyimbo kwaajili ya kila mtu, kwa watu wenye umri wowote na kila kona ya Afrika. Nilitaka kulipa fadhila/Heshima kwa asili yangu na pia kukumbatia mfumo mpya wa muziki wa kiafrika ambao unashika kasi Ulimwenguni kwa sasa. Nina furaha sana kuitambulisha albamu yangu kwa mara ya kwanza duniani kwa mashabiki wangu waTanzania”….alisema Patoranking.

Msanii huyo pia alitumia muda huo kufafanua kwanini alichagua Dar es salaam kama Jiji la kwanza kuitambulisha albamu yake mpya, “watanzania ni watu wazuri sana, nimeona wasanii wengi kutoka Nigeria na mataifa mengine wakija kufanya shoo hapa jinsi wanavyopokelewa vizuri na upendo mkubwa”. Aliwataja baadhi ya wasanii  wa Kitanzania ambao nyota huyu anapanga kufanya nao kazi akiwemo: Navy Kenzo na Vanessa Mdee a.k.a  V-Money ambao kwa maelezo yake ni kama wanafamilia.

Aliwashukuru mashabiki wake na vyombo vya habari vya Tanzania kwa kuunga mkono mziki wake  kabla  hajabainisha kuwa atatembelea Nairobi, Kampala na Accra-Ghana kuitambulisha albamu hiyo kabla ya kurudi nyumbani.

Patoranking pia aliendelea kutaja siri ya kuwa ameanzisha lebo ya kurekodi /studio aliyoiita “his baby”, ambayo msanii wa kwanza ametokea kutoka hapa hapa Tanzania, “Jina lake ni Walid, mnaweza msimfahamu kwa sasa, lakini mtamfahamu, huyu amekusudiwa kufanya mambo makubwa” alisema Patoranking

Kwa upande wake Meneja wa Masoko wa Spice Africa Joan Nkuzi amesema, ni heshima kubwa sana kwa Msani  nyota wa Nigeria kutambulisha albamu yake kwa mara ya kwanza hapa Tanzania na ndio maana hawakusitasita kuunga mkono juhudi zake. Jukumu kubwa lab Spice Africa kupitia application yake ya Mziiki ni kupeleka muziki wa Kiafrika duniani kote kama wakusanyaji na wasambazaji walioko katika masoko zaidi ya 12 ndani ya Afrika, walitoa uhakika sio tu kufanya kazi na wasanii wenye vipaji, bali pia wasanii ambao ni wanyenyekevu na ambao wanajua malengo yao – ambapo mmoja wao ni Patoranking.

WAKUU WA IDARA WILAYANI IKUNGI, MAAFISA TARAFA, WATENDAJI WA KATA, VIJIJI NA WENYEVITI WA VIJIJI WAFUNDWA

0
0

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu akiwasilisha mtazamo wa namna ambavyo anataka Wilaya hiyo iwe. Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya ikungi Rustika Turuka aliyesimama akizungumza na Wakuu wa Idara na vitengo, Maafisa Tarafa, Watendaji wa Kata, Vijiji, na Wenyeviti wa Vijiji wakati wa kikao hicho cha kazi.
Wakuu wa Idara na vitengo, Maafisa Tarafa, Watendaji wa Kata, Vijiji, na Wenyeviti wa Vijiji wakifatilia mafunzo kutoka kwa wawasilishaji
Kutoka Kushoto ni Mustafa Mtopo kaimu Afisa usalama wa Taifa Wilaya ya Ikungi, Fortunatus Ndalama Mshauri wa Mgambo Wilaya ya Ikungi, Dijovson Ntangeki Kaimu Katibu Tawala Wilaya ya Ikungi, Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu, Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya ikungi Rustika Turuka, na Mkuu wa poiisi Wilaya ya Ikungi Milton Nkyalu wakifatilia mafunzo kutoka kwa wawasilishaji waliotoka ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya hiyo.

…………………………………………………………………………………………..

Na Mathias Canal, Singida

Wakuu wa Idara na vitengo, Maafisa Tarafa, Watendaji wa Kata, Watendaji wa vijiji na wenyeviti wa vijiji 101 vilivyopo Wilayani Ikungi Mkoani Singida hii leo wamepatiwa mafunzo ya kutambua mipaka ya majukumu yao kiutendaji katika kikao cha kazi kilichofanyika katika ukumbi wa shule ya sekondari Ikungi.

Mafunzo hayo yameandaliwa na uongozi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo kutokana na kubainika kuwa asilimia kubwa ya watendaji hususani wenyeviti wa vijiji na vitongoji wamekuwa wakiingilia katika majukumu ya kiutendaji.

Akifungua mafunzo hayo yaliyodumu kwa zaidi ya masaa matano yaliyojikita zaidi kutoa ufafanuzi juu ya majukumu ya watendaji wa Kata, Wenyeviti wa Vijiji na Watendaji wa Vijiji, Mkuu wa Wilaya hiyo Miraji Jumanne Mtaturu amebainisha kuwa pamoja na mafunzo kwa ajili ya ufahamu wa majukumu ya watendaji hao lakini amesema kuwa Wilaya ya Ikungi ipo nyuma kielimu kutokana na shule kuwa mbali na maeneo ya watu, wanafunzi wa kike kuachishwa shule na kuolewa, baadhi ya viongozi na wataalamu kutotimiza wajibu wao na wakati mwingine uzembe wa baadhi ya watumishi wa serikali katika kutatua kadhia za wananchi.

Pamoja na hayo pia DC Mtaturu amesema kuwa kuna baaadhi ya maeneo kuna shule ambazo zina majengo mazuri na Hosteli kwa ajili ya wanafunzi lakini wazazi wanakataa kuwapeleka wanafunzi shuleni ikiwa ni pamoja na shule ya Sekondari Mkinya iliyopo Kata ya Dung’unyi, Shule ya Sekondari Mtunduru, Shule ya Sekondari Mwaru na Wembere , huku shule ya Sekondari Issuna ikiwa na Majengo na Hosteli nzuri lakini wanafunzi wanaosoma hapo ni wale wanaotoka Wilaya nyingine huku wenyeji wakiwa wamejichimbia ndani.

Dc Mtaturu amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya hiyo kwa kushirikiana na Polisi kufanya uchunguzi na kuwachukulia hatua baadhi ya Watendaji wa Kata, Waratibu wa elimu wa Kata, Wenyeviti wa Vijiji na Watendaji wa Vijiji wanaoshirikiana na baadhi ya wazazi kuwaachisha wanafunzi shule ili wakaolewe ambapo amebaini kuwa katika Kata ya Mwaru na baadhi ya Kata zinazozunguka katika Kata hiyo viongozi wake kwa kushirikiana na Waratibu elimu Kata wamekuwa wakifanya biashara ya kuruhusu wanafunzi kuolewa kwa kupewa Ng’ombe.

Hata hivyo pia amewaagiza Watendaji wa Kata ya Makilawa na Iyumbu kumpatia taarifa ya kamati ya maendeleo ya Kata (WDC) ili kubaini mpango wa mikakati katika kujenga shule za Sekondari katika Kata hizo mbili ambazo zimesalia ilihali Kata 28 tayari zina shule za sekondari kati ya Kata 30 zilizopo katika Wilaya hiyo.

Katika shule 28 ni shule 3 tu zenye maabara, shule ya Sekondari ya Puma na Wembere ambao nao walijenga maabara baada ya kupata msaada kutoka Benki ya dunia Mwaka 2013, shule ya Sekondari Mkinya ina maabara 2 ambazo zilijengwa kwa msaada wa SADC mwaka 2009 hivyo kupelekea Wilaya nzima ya Ikungi kuwa na Maabara 4 pekee zilizojengwa kwa msaada wa wahisani ambapo hakuna hata maabara moja iliyojengwa na wananchi ikakamilika kutokana na zuio la kuchangia walilolipata wananchi kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki Tundu Lissu.

Sawia na hayo pia Mkuu huyo wa Wilaya amewaagiza Watendaji wa Kata na Vijiji kwa kushirikiana na Wabunge, Madiwani na Wenyeviti wa Vijiji kuwaelimisha wananchi kukaa vikao na kupitisha maadhimio ya kuendelea kuchangisha michango ya ujenzi wa maabara kwa mujibu wa waraka wa Elimu namba 6 wa mwaka 2015 wa elimu msingi bila malipo.

Hata hivyo agizo limetolewa pia kwa Wazazi/Walezi pamoja na wanafunzi wenyewe kuchukuliwa hatua kali za kisheria kutokana na utoro wa wanafunzi shuleni jambo ambalo linapelekea kuwa na ufaulu duni wa wanafunzi Wilayani humo.

Dc Mtaturu pia amemuagiza Afisa Mtendaji wa Katana Afisa Mtendaji wa Tarafa kutumia siku 14 kuhakikisha madawati yanafika katika shule zenye uhaba wa madawati ili kuondokana na adha ambayo inaendelea kuwakumba wanafunzi shuleni ilihali madawati tayari yamepatikana.

Aidha ndani ya siku tano viongozi hao wameagizwa kuhakikisha kuwa Masoko pamoja na stendi zinaenda katika maeneo yaliyopangiwa ili ushuru upatikane kwa wakati na kwa kiasi kilichokusudiwa.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Rustika Turuka amewashukuru Watendaji wa Kata, Wenyeviti wa Vijiji na Watendaji wa Vijiji kwa kujitokeza kwa wingi katika mafunzo hayo jambo ambalo limeonyesha kuwa wananchi hao wana imani na serikali ya awamu ya nne hivyo amewaomba kuachana na siasa na kufanya kazi kwa moyo na nguvu zaidi.

Amewataka viongozi wote wa ngazi ya Wilaya, Tarafa, Kata, Vijiji na vitongoji kutekeleza maagizo yote yanayotolewa na serikali kwa haraka na kwa ukamilifu.

Turuka amesema kuwa kila kiongozi anapaswa Kutatua kero za wananchi kwa kutenda haki, kutofanya kazi kwa mazoea, kutoa majawabu sahihi ya wananchi na kama hawafahamu wanapaswa kuuliza sehemu husika ili kutozungumza jambo wasilokuwa na uhakika nalo.

Kupitia kikao hicho kilichoitishwa na mkuu huyo wa Wilaya kilichokuwa na dhumuni la kufahamiana na kukumbushana majukumu na wajibu wa viongozi na kueleza mtazamo wa Ikungi mpya inavyotakiwa kuwa Afisa utumishi wa Wilaya sawia na Mkuu wa Polisi Wilaya wamepewa nafasi ya kuelezea majukumu na wajibu wa kila mmoja katika maeneo yao.

Kwa upande wao baadhi ya Watendaji wa Kata, Vijiji na wenyeviti wa vijiji 101 vilivyopo Wilayani humo wamesema kuwa mafunzo waliyoyapata watayatumia vyema kuwa mabalozi wazuri kwa wananchi na kuwaelimisha zaidi ili kutambua mipaka yao na majukumu yao katika kuishauri serikali.

Aidha Maafisa Tarafa, Watendaji wa Kata, Watendaji wa vijiji na wenyeviti wa vijiji wote ambao hawajahudhuria kikao hicho cha kazi wametakiwa kuandika barua za maelezo kwanini wameshindwa kuhudhuria na zimetakiwa kupitia kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Ikungi hadi kufikia tarehe 10 ya mwezi huu wa nane.

BancABC YAZINDUA HUDUMA MPYA YA “MKOPORAHISI”, MTEJA ANACHUKUA PESA NDANI YA SAA 48

0
0

Mkuu wa Kitengo cha Mikopo Rahisi, (Easy Banking), wa BancABC,Thompson Mwasikili, (kushoto), akiwa na Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara cha benki hiyo, Joyce Malai, wakati akizindua huduma mpya ya “Mkoporahisi”, makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam, Agosti 2, 2016. BancABC, ambayo ni sehemu ya Atlas Mara, imerahisisha upatikanaji wa mikopo kwa wateja wake ambapo mteja wa benki hiyo ambaye ni mtumishi wa serikali anaweza kupatiwa mkopo ndani ya masaa 48.

BANCABC ambayo ni sehemu ya Atlas Mara imerahisisha upatikanaji wa mikopo kwa wateja wake kwani imeanza kutoa mikopo ndani ya saa 48 kupitia huduma mpya ya ‘mkoporahisi’.

Akizungumza na waandishi wa habari Agosti 1, 2016, makao makuu ya benki hiyo, kwenye jingo la Uhuru Hights jijini Dares Salaam, Mkuu wa kitengo cha Easy Banking wa BancABC, Thomson Mwasikili, (pichani juu), alisema.wameamua kuanzisha huduma hiyo ili kuwavutia wateja wengi zaidi kutoka sekta mbalimbali ikiwemo serekalini ili kuhakikisha wanapata huduma hii kwa haraka.

“Kwa kupitia huduma hii ya mkoporahisi tutahakikisha kuwa wateja wetu ambao ni waajiriwa wa Serikali, wanapata mikopo yao ndani ya saa 48 kuanzia muda ambao maombi yaliwasilishwa..tutalisimamia hili na kuhakikisha linatekelezeka,” alisema Mwasikili.  Bw. Mwasikili alisema benki yake inatoa mikopo ya hadi Tsh milioni 40 kwa riba ya kiwango cha chini hadi asilimia 1.6 kwa mwezi ambayo ni miongoni mwa riba za chini kabisa katika soko la sasa.

“Waombaji wataweza kulipa mikopo yao kwa muda mrefu wa hadi miaka 6 na hakuna pingamizi kuhusu lini unaweza kuongeza mkopo wako,” alisema na kuongeza kuwa muombaji ana uhuru wa kupata mkopo wa muda mfupi hata wa mwezi mmoja. Kwa mujibu wa Mwasikili, tofauti na mikopo mingine, waombaji wana uhuru wa kuchagua matumizi ya fedha kwa mfano kulipia ada, kununua gari, kukarabati nyumba, kulipia kodi na kumaliza ujenzi na benki haitamlazimisha mkopaji matumizi ya mkopo wake.

Waombaji pia watapata fursa ya kuchanganya mikopo yao yote na kuwa na mkopo mmoja kwani BancABC inaweza kununua mikopo yote hiyo na kumpunguzia mteja usumbufu. “Endapo muombaji wa mkopo atafariki, mkopo utafidiwa kupitia bima ya mikopo na fedha kiasi cha Tsh 500,000 taslimu zitatolewa kugharamia mazishi,” alisema

“Tunatoa rai kwa wateja wetu wote na pia wale ambao hawana akaunti na benki yetu kuchangamkia huduma hii ya mkoporahisi kwani hii ndio benki pekee ambayo inakusogeza karibu na ndoto zako , pata
mikopo ndani ya saa 48,” alisema.

Atlas Mara iliorodheshwa katika soko la hisa la London Disemba 2013. Atlas Mara ina lengo la kujitanua na kuwa kinara katika masuala ya kifedha katika ukanda wa sub sahara kwa kutumia uzoefu wake  na uwezo wa kukuza mitaji. Malengo yake ni kuunganisha na kukuza uwezo wa taasisi za kifedha na pia kuendeleza uchumi katika nchi ambazo inafanya shughuli zake.

BENKI YA CRDB YADHAMINI BONANZA LA MPIRA WA KIKAPU

0
0
WAZAZI wameshauliwa kuwapa nafasi ya kushiriki michezo watoto wao ili kuwajengea utumilifu wa akili kwenye masomo yao.Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa wateja wa CRDB, Tully Esther Mwambapa kwenye bonanza la mpira wa kikapu lililofanyika jana kwenye viwanja vya Gymkhana Dar es Salaam.

Tully, alisema kuwa kwa kutambua umuhimu wa michezo katika kuboresha afya Benki ya CRDB imetenga kiasi cha asilimia moja ya faida yake kurudisha kwa jamii kupitia huduma mbalimbali za kijamii ikiwemo michezo.

"Ni vizuri tukawahusisha watoto katika michezo, itawajenga kiakili na kuwa katika nafasi ya kufanya vizuri, si vyema kuwafungia ndani na kutowapa nafasi ya kushiriki michezo na wenzao," alisema Tully.Bonanza hilo lilishirikisha wachezaji mbalimbali wa mpira wa kikapu wakiwemo watoto ambapo timu za Libeneke, Chang'ombe, Old Guards pamoja na Pazi.

Katika hatua nyingine, Tully alitoa mchango wa Sh. Milioni mbili kwa ajili ya kusaidia kukarabati viwanja vya mchezo huo vya Gymkhana.
Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa wateja wa CRDB, Tully Esther Mwambapa akizungumza wakati wa uzinduzi wa Bonza la Mpira wa Kikapu kwenye viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam na kudhaminiwa na Benki ya CRDB. (Picha na Francis Dande)
Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa, akifunga goli kuashiria uzinduzi wa bonanza la mpira wa kikapu lililofanyika kwenye viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam. Bonanza hilo lilidhaminiwa na benki hiyo.
Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa wateja wa CRDB, Tully Esther Mwambapa, akikagua timu katika bonanza la mpira wa kikapu lililofanyika kwenye viwanja vya Gymkhana Dar es Salaam.
Mchezaji wa Kikapu wa timu ya Libeneke, Edion Brighton (kushoto), akitafuta mbinu za kumtoka mchezaji wa timu ya Old Guards, John Tungaraza, katika bonanza la mpira wa kikapu lililofanyika kwenye viwanja vya Gymkhana Dar es Salaam na kudhaminiwa na Benki hiyo.
Mchezaji wa timu ya mpira wa Kikapu ya Old Guards, Godwin Semunyu, akizongwa na mchezaji wa timu ya Libeneke, Joseph Iyaka katika bonanza la mpira wa kikapu lililofanyika kwenye viwanja vya Gymkhana Dar es Salaam na kudhaminiwa na Benki hiyo.
 

WAUMINI WA KKKT MTAA WA KULASI WILAYANI KOROGWE WAJENGEWA KANISA JIPYA.

0
0
Muonekano wa Jengo la Kanisa lililokuwa likitumiwa na Waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Mashariki mtaa wa Kulasi wilayani Korogwe .
Muonekano wa Jengo jipya la Kanisa linalotumiwa na Waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Mashariki mtaa wa Kulasi wilayani Korogwe . Waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Mashariki mtaa wa Kulasi wilayani Korogwe wakiandamana wakati wa sherehe ya ufunguzi wa jengo jipya la kanisa lililojengwa na wazawa wa kijiji hicho waishio maeneo mbalimbali nchini.

Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Dkt Stephen Munga (wa kwanza kushoto) akiongoza wachungaji wa kanisa hilo kupokea waumini wakati wa ibada ya ufunguzi wa jengo jipya la kanisa la mtaa wa Kulasi wilayani Korogwe.

Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Dkt Stephen Munga akiongoza ibada ya ufunguzi wa jengo jipya la kanisa la mtaa wa Kulasi wilayani Korogwe.



Baadhi ya Waumini wa kanisa hilo wakiimba nyimbo wakati wa ibada ya ufunguzi wa jengo jipya la kanisa la mtaa wa Kulasi wilayani Korogwe.





Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Dkt Stephen Munga akikata utepe kufungua rasmi jengo jipya la kanisa la mtaa wa Kulasi wilayani Korogwe.

Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Dkt Stephen Munga akifungua mlango wa kanisa ili waumini wapate kuingia ndani.

Muonekano wa ndani wa jengo jipya la Kanisa la KKKT mtaa wa kulasi.

Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Dkt Stephen Munga akisoma neno mara baada ya waumini kuingia ndani ya kanisa hilo.



Waumini wa kanisa la Mtaa wa Kulasi wakiwa wameshika kuta za kanisa hilo wakati wa sala ya kubariki jengo la kanisa.



Baadhi ya waumini wa kanisa la mtaa wa Kulasi wakiwa katika ibada hiyo .



Kwaya Walawi ya jijini Arusha ikiimba nyimbo za kusifu kwa watu waliojitoa kwa ajili ya ujenzi wa kanisa hilo.

Mchungaji Kiongozi .........akitoa salamu kwa wauimini waliohudhuria ibada hiyo maalumu ya ufunguzi wa kanisa hilo.



Kwaya ya watoto wa kanisa la mtaa wa Kulasi wakiiiomba nyimbo wakati wa ibada hiyo.

Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Dkt Stephen Munga akitoa mahubiri katika ibada ya ufunguzi wa jengo jipya la kanisa la mtaa wa Kulasi.



Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Dkt Stephen Munga akimpa mkono Sayuni Shelutete kwa kushiriki katika utoaji wa msaada wa ujenzi wa kanisa hilo.

Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Dkt Stephen Munga akimpa mkono Pascal Shelutete kwa kushiriki katika utoaji wa msaada wa ujenzi wa kanisa hilo.

Waumini wa kanisa la mtaa wa Kulasi wilayani Korogwe wakitoa zawadi kwa familia ya Pascal Shelutete kwa msaada waliotoa kwa ajili ya kufanikisha kazi ya ujenzi wa kanisa la mtaa wa Kulasi.

Kiongozi wa familia ya Mzee Shelutete,Bwana Nicolaus Kingazi akizungumza kwa niaba ya familia hiyo wakati wa ibada ya ufunguzi wa jengo jipya la kanisa la mtaa wa Kulasi.



Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Dkt Stephen Munga akihitimisha ibada ya ufunguzi wa kanisa la mtaa wa Kulasi wilayani Korogwe.

Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Dkt Stephen Munga akipeana mikono na wachungaji mara baada ya kumaliza ibada ya ufunguzi wa jengo la kanisa.





Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Dkt Stephen Munga akisaidiana na Pascal Shelutete kuotesha mti wa kumbukumbu katika viunga vya kanisa hilo.

Bwana,Pascal Shelutete (Kushoto) na Bibi Sayuni Shelutete (kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Dkt Stephen Munga mara baada ya kukamilika kwa ibada ya ufunguzi wa kanisa jipya la mtaa wa Kulasi.




Na Dixon Busagaga wa Michuzi Blog,Kanda ya Kaskazini.

KATIBU MKUU WIZARA YA NCHI OFISI YA RAIS AZUNGUMZA NA WAANDHISHI WA VYOMBO VYA FM

0
0

Katibu Mkuu Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Nd,Salum Maulid Salum (katikati) akizungumza na waandishi wa Habari wa vyombo mbali mbali vya Redio za FM kuhusu kongamano la Watanzania wanaoishi Nje ya Nchi (Diaspora) linalotarajiwa kufanyika Agosti 24 mwaka huu.
Katibu Mkuu Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Nd,Salum Maulid Salum (wa pili kulia) alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbali mbali vya Redio za FM kuhusu kongamano la Watanzania wanaoishi Nje ya Nchi (Diaspora) linalotarajiwa kufanyika Agosti 24 mwaka huu (kushoto) Naibu Katibu wa Rais Nd,Marium Haji Mrisho na Mkurugenzi wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Silima Kombo Haji.
Katibu Mkuu Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Nd,Salum Maulid Salum (kulia) alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbali mbali vya Redioza FM kuhusu kongamano la Watanzania wanaoishi Nje ya Nchi (Diaspora) linalotarajiwa kufanyika Agosti 24 mwaka huu (kushoto) Mkurugenzi wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Silima Kombo Haji.

[Picha na Ikulu.]

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa atembelea Bandari ya Dar es Salaam

0
0
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa, Mhe. Jean-Marc Ayrault (watatu kulia) na ugeni wake wakisikiliza maelezo kuhusu Bandari ya Dar es Salaam kutoka kwa Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dk. Leornard Chamuriho (kushoto). Kulia ni Kaimu Meneja Bandari ya Dar es Salaam, Bw. Habel Mhanga.
Baadhi ya Maafisa kutoka nchini Ufaransa ambao waliongozana na Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo kutembelea Bandari ya Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dk. Leornard Chamuriho (kushoto) akifafanua jambo kwa mmoja wa waandishi wa habari  kutoka nchini Ufaransa wakati wa ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi  hiyo katika Bandari ya Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Deusdedit Kakoko (kulia) akifurahia jambo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dk. Leornard Chamuriho (wapili kulia) na baadhi ya Maafisa wa Serikali waliofanikisha ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa kutembelea Bandari ya Dar es Salaam.

TUHUMA KUHUSU NGOs KUHAMASISHA VITENDO VYA USHOGA

0
0
 
Siku za hivi karibuni kumekuwepo na tuhuma za kuwepo kwa baadhi ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs) yanayojihusisha na kuhamasisha vitendo vya ushoga nchini. Tunapenda kuujulisha umma kuwa NGOs zinasajiliwa kutekeleza majukumu yanayokubalika kisheria na kwamba vitendo vya kuhamasisha ushoga si majukumu halali yanayopaswa kutekelezwa na NGOs. 
 
Tunazitaka NGOs kutekeleza majukumu yaliyo ndani ya usajili wao na kuepuka vitendo vya uvunjifu wa sheria. Aidha, tunazidi kusisitiza kuwa vitendo vya ushoga havikubaliki nchini kwani ni kinyume na mila, desturi na sheria za nchi. Ofisi ya Msajili inaomba wadau na umma kwa ujumla kutoa taarifa zitakazowezesha kuthibitisha tuhuma tajwa ili hatua stahiki dhidi ya NGOs husika zichukuliwe. Taarifa zinaweza kutolewa kupitia namba zifuatazo: 022 2110714/0222123143/ 0754391942/0715391942.

M.S.Katemba

MSAJILI WA NGOs

WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO

01 Agosti, 2016
Viewing all 46201 articles
Browse latest View live




Latest Images