Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46202 articles
Browse latest View live

Radio Maria waiomba Serikali kurekebisha Sheria ya leseni ya redio za jamii

0
0
Na Jacquiline Mrisho - MAELEZO

Rais wa Redio Maria Tanzania, Humphrey Kira ameiomba Serikali kurekebisha Sheria ya leseni ya redio za jamii ili ziweze kuwa na vituo vingi vya kurushia matangazo yake.

Hayo yamesemwa leo na Rais huyo wakati alipokuwa akisoma risala kwenye sherehe za kilele cha maadhimisho ya miaka 20 ya redio hiyo yaliyofanyika kwenye viwanja vya Msimbazi Centre, Jijini Dar es Salaam.

Kira amefafanua kuwa redio za kijamii hasa zilizojikita katika nyanja za kiimani zinasaidia kufundisha maadili na kufanya wananchi wakomae kiimani, hivyo angefurahi sana kuona redio za aina hiyo zinapewa leseni za kurusha matangazo yake nchi nzima.

“Ndugu mgeni rasmi, redio yetu inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na ufinyu wa sehemu za usikivu (coverage areas) ambapo tatizo hili linatokana na sheria ya leseni za redio ambayo hairuhusu redio za aina hiyo kuwa na vituo zaidi ya kumi nchini nzima, tunaomba serikali itusaidie kuiboresha sheria hii ili tuongeze vituo vya matangazo ya dini”, alisema Kira.

Rais huyo ameongeza kuwa majimbo yote yanahitaji kufikiwa na huduma za maombi, hivyo anawashauri wasikilizaji wote kuendelea kuisikiliza redio hiyo kwa njia ya mitandao ikiwemo simu za mkononi kwani hivi sasa huduma hiyo inapatika nchi nzima.


Mwashamu Askofu wa Jimbo Katoliki la Mtwara akikata keki wakati wa sherehe za kilele cha maadhimisho ya miaka 20 ya Redio Maria Tanzania leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anne Makinda, katikati ni Mkurugenzi wa Redio Maria Tanzania (RMTZ) Padre John Maendeleo.
Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anne Makinda akikata keki wakati wa sherehe za kilele cha maadhimisho ya miaka 20 ya Redio Maria Tanzania leo Jijini Dar es Salaam yaliyoanza rasmi tangu April 26 mwaka huu. Katikati ni Mwashamu Baba Askofu wa Jimbo Katoliki la Mtwara Titus Mdoe,kutoka kulia ni Mhamasishaji Mkuu wa Redio Maria Tanzania Bi. Veronica Mwita na wapili kushoto ni Mkurugenzi wa Redio Maria Tanzania (RMTZ) Padre John Maendeleo.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Benjamin William Mkapa akisalimiana na Baba Askofu wa Jimbo Katoliki la Mtwara Mwashamu Askofu Titus Mdoe wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 20 ya Redio Maria Tanzania leo Jijini Dar es Salaam.Katikati ni Mkurugenzi wa Redio Maria Tanzania Padre. John Maendeleo.
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Saalam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo akizungumza na wadau na marafiki wa Redio Maria Tanzania leo Jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 20 tokea kuanzishwa kwa Redio hiyo.
Mkurugenzi wa Redio Maria Tanzania Padre John Maendeleo akizungumza na wadau na marafiki wa Radio Maria Tanzania leo Jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 20 tokea kuanzishwa kwa Redio hiyo.
Rais wa Redio Maria Tanzania Humphrey Julius Kira akizungumza na wadau na marafiki wa Radio Maria Tanzania leo Jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 20 tokea kuanzishwa kwa Redio hiyo.
Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anne Makinda akipokea risala kutoka kwa Rais wa Redio Maria Tanzania Humphrey Julius Kira(Kulia) wakati wa sherehe za kilele cha maadhimisho ya miaka 20 ya Redio Maria Tanzania leo Jijini Dar es Salaam.
Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anne Makinda akipeana mkono na baadhi ya marafiki wa Redio Maria Tanzania waliofika kuchangia Redio hiyo katika harambee iliyofanyika ikiambatana na sherehe za maadhimisho ya miaka 20 ya Redio Maria Tanzania leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Rais wa Redio Maria Tanzania Bw. Humphrey Julius Kira.
Baadhi ya waumini wa Roman Katoliki wakifurahi wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 20 ya Redio Maria Tanzania (RMTZ). Picha zote na Frank Shija, MAELEZO.
Kwa upande wake Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo ametoa rai kwa uongozi wa redio hiyo kutobadilisha maudhui wala kuweka vipindi visivyokuwa vya dini ili iendelee kuunganisha familia na sio kuzigawa familia.

“Tunasema kuwa redio Maria ni sauti ya kikristu nyumbani mwako lakini mimi nasema ni sauti ya Mungu ndani ya familia kwa kuwa inafanya kazi ya kuunganisha familia, vyombo vingine vya habari vinafanya kazi kubwa ya kuigawa familia lakini Redio Maria ni tofauti”, alisema Pengo.

Askofu Pengo amewashukuru wananchi wote waliohudhuria kwenye maadhimisho hayo kwa kuwa kufanya hivyo ni njia moja wapo ya kumuenzi na kumpa heshima Mama Bikira Maria.

Nchini Tanzania, Redio Maria ilianzishwa Aprili 26 mwaka 1996 katika Jimbo Kuu Katoliki la Songea ikiwa na lengo la kumsaidia Mama Bikira Maria katika kazi yake ya kumtangaza Yesu Kristo kwa watu wote. Mpaka sasa ina vituo 10 Tanzania Bara na viwili Zanzibar.

Kampuni ya Off Grid yajibadili jina la biashara na kufungua maduka mapya Tanzania na Rwanda

0
0
Arusha, Tanzania (July 28, 2016) Kampuni ya Off Grid Electric, inayomiliki kampuni ya umeme wa jua ya M-POWER ya Tanzania, imetangaza rasmi leo kubadilisha jina la biashara (brand name) na ufunguzi wa duka lake la mauzo ya bidha zake kwa rejareja hapa nchini.

Ufunguzi huo utawasaidia Watanzania kupata umeme wa jua wenye uhakika kwa bei nafuu kwa matumizi ya majumbani  na katika biashara zao.Wakati ikiendelea na kujipanua, Off Grid sasa inabadilisha jina la biashara kutoka M-POWER na kwamba kwa sasa itajiuza kwa jina la Zola.

Jina hili la biashara linabeba dhana nzima ya kwamba kampuni hii ina mizizi yake hapa Afrika Mashariki. Neno Zola limetoholewa kutoka katika neno la Kiswahili la Solar (Sola) na hivyo litatumika kama jina la biashara la kampuni ya Off-Grid katika mataifa ya Tanzania na Rwanda wakati kampuni ikijidhatiti kujipanua zaidi barani Afrika.

Hata hivyo, kampuni itaendelea kujulikana kwa jina la Off Grid Electric. 
“Kutokana na azma yetu ya kukua zaidi na kufika katika nchi nyingi zaidi hapa barani Afrika, tunahitaji jina la biashara litakalofanya kazi ndani na nje ya jiografia ya Afrika ili kuonyesha mtazamo wetu wa mabadiliko katika utendaji,” alisema mwanzilishi mwenza wa Off-Grid Electric, Bwana Erica Mackey na kuongeza: “Tunaijenga Zola ili iwe kampuni ya umeme wa nguvu ya Sola kwa Afrika nzima”.Jina ya biashara la Zola litazinduliwa rasmi leo (July 28, 2016) kwa ufunguzi rasmi wa maduka ya mauzo ya bidhaa za Zola Tanzania na Rwanda.

Akizungumza katika uzinduzi huo, mkuu wa ubia wa Zola, Bwana Godfrey Kakembo alisema: “Maduka ya Zola yatawasaidia wateja kujionea jinsi ambavyo bidhaa zetu zinavyfanya kazi na pia kuweza kuagiza ili waweze kufungiwa sola majumbani mwao. Kwa njia hiyo, wateja wataweza kutoa Zawadi ya kudumu kwa ndugu, jamaa na marafiki zao waishio vijijini”.

Katika maduka ya Zola, wateja wataweza kulipa papo hapo na pia wataruhusiwa kuingia makubaliano ya kulipa kidogo kidogo.
Wahudumu kwa wateja watakuwepo muda wote ili kujibu maswali yote yatakayoulizwa na wateja kuhusiana na bidhaa za Zola.

Waanzilishi wa kampuni na wajumbe wa bodi nao pia watakuwepo ili kushuhudia ukataji utepe utakaoashiria ufunguzi rasmi wa duka la Zola jijini Arusha.Mwezi uliopita, kampuni ya Off Grid Electric ilizindua mpango maalum wa kusaidia kufikisha umeme wa sola unaofaa kwa matumizi ya wajasiliamali wa vijijini. Mpango huo ulizinduliwa huko California katika mkutano wa kilele uliohudhuriwa na Rais wa Marekani Barak Obama.

Mpango huo unajulikana kwa jina la “Kazi na Zola” na unatoa umeme wa kutosha kwa wafanyabiashara chipukizi kutoka Tanzania na Rwanda kuweza kufanya biashara zao bila shida, iwe ni biashara ya kinyozi, kuchaji simu, bar na mgahawa kwa kutumia umeme wa jua.

MADIWANI NA WATENDAJI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MKURANGA WAMESHAURIWA KUACHA SIASA NA BADALA YAKE WACHAPE KAZI.

0
0
MBUNGE wa Jimbo la Mkuranga, Abdallah Ulega amewataka madiwani na watendaji kufanya kazi kwa bidii kwa lengo la kuwaletea maendeleo wananchi wa jimbo hilo na kwamba muda wa kufanya siasa umemalizika na kilichobaki ni kuchapa kazi kama Rais Dkt. John Magufuli anavyohamasisha kwamba watu wafanye kazi.

Ulega ametoa kauli hiyo leo katika semina ya madiwani na watendaji kata pamoja na wataalamu wa afya kutoka halmashauri juu ya masuala mazima ya  usafi wa mazingira na matumizi ya vyoo na kudai kuwa wilaya ya Mkuranga kuna changamoto ya watu  tabia ya kutumia vyoo hali inayojenga taswira mbaya wilayani humo.

Alisema kuwa wilaya hiyo inachangamoto kubwa ya watu kushindwa kutumia vyoo na kujenga taswira mbaya katika jamii hivyo lazima watu wajenge tamaduni ya matumizi ya vyoo nakutoa elimu hiyo kuazia  utotoni ili hata mtoto anapokuwa anakuwa tayari na uelewa juu ya matumizi ya vyoo.

Injia wa Maji ndani ya Halmashauri ya wilaya ya mkuranga Leonard Baseke akitoa ufafanuzi juu ya matumizi bora ya vyoo kwa wananchi wa wilaya hiyo katika semina iliyoshirikisha madiwani na watendaji kata wa wilaya ya mkuranga leo mkoani Pwani.
 Mbunge wa Jimbo la Mkuranga, Abdallah Ulega  akiwa katika picha ya pamoja na madiwani pamoja na watendaji kata ndani ya wilaya ya Mkuranga mara baada ya kutoka kwenye semina ya uhamasishaji wa usafi hususani baada ya kutoka chooni.

 Mbunge wa jimbo  la Mkuranga, Abdallah Ulega akizungumza  katika semina ya iliyoshilikisha madiwani wa Halmashauri ya  wilaya hiyo ambapo pamoja na mambo mengine aliwataka  madiwani hao na watendaji kata ndani ya wilaya hiyo  kufanya kazi nakuacha siasa kwani muda wake umekwisha leo mkoani Pwani.
 Madiwani wa halmashauri hiyo na watendaji kata kwa pamoja wakimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Abdalla Ulega wakati akizungumza katika semina ya  kuhamasisha masuala ya usafi na matumizi ya vyoo ikiwa pamoja na kujenga tabia ya kunawa mikono baada ya kutoka chooni leo mkoani Pwani.
Picha na Emmanuel massaka, Globu ya Jamii, Mkuranga.

Zantel commits to empower women by using Mobile Financial service

0
0

Zanzibar’s leading mobile operator, Zantel, has today announced its commitments to economically empower women by using Mobile Financial service.

By closing the mobile gender gap, women will ultimately have more economic and social opportunities on how they conduct their lives. The commitments were made by Zantel’s Chief Executive Officer, Benoit Janin during the Mobile 360 - Africa Conference, taking place at the Julius Nyerere International Convention Centre in Dar es Salaam.

‘We at Zantel understand that by closing the mobile gender gap will create economic opportunities for women and we are able to generate growth and advancement for the communities that surround us’ said Mr Janin.

Zantel have also committed to grow the women percentage of its active base using Ezypesa from the current 27% to 40% by 2020. ‘Zantel already has projects that are underway with various women groups such as Nia ni Umoja in Pemba and Association of Seaweed Farmers in Unguja. Our intention is to train over 2000 women on the use of Ezypesa’ said Mr Janin.

Mr Janin also said in its bid to unlock potential women and other underserved groups, Zantel has doubled its reach. In the mainland it covers 80% of the population, while in Zanzibar, Zantel has the widest network.

‘In Zanzibar for instance, where Zantel has almost 70% market share, we will be partnering with Zanzibar Social Security Fund (ZSSF). This is to ensure that its members, of which 60% are women, contribute their donations through Ezypesa’.

Benoit also urged stakeholders and operators to work together in ensuring end users benefit from Mobile Financial Services. He also pointed out the critical role mobile communications plays in the social and national development.

‘Operators and stakeholders should work together to ensure barriers such as access to Internet, connectivity, digital literacy are resolved’ said Mr Janin.

Airtel Money yaingia ubia na NMB bank kuongeza ufanisi kwa wakala wake.

0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Bwana Sunil Colasso akiongea wakati wa kutambulisha kuhusu Money airtel kuingia ushirikiano na NMB banki ili banki ya NMB ihudumie wakala wa Airtel Money
Wakala wa Airtel kupata Airtel Money salio kwenye benki ya NMB popote.

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kupitia huduma yake inayokuwa kwa kasi ya Airtel Money imeingia ubia na Benki ya NMB ili kutoa huduma kwa wakala wake wanaotoa huduma za Airtel Money kujipatia huduma ya salio na pesa taslim katika matawi ya benki hiyo popote nchini.

Akiongelea ubia huo, Mkurugenzi wa Airtel Bw, Sunil Colaso alisema “tunachofanya Airtel na benki ya NMB ni mundelezo wa mikakati tuliyojiwekea ya kuhakikisha tunaleta maendeleo katika huduma za kifedha nchini ili wateja wetu wapate huduma za uhakika na nafuu. Pia kuwepo kwa sera bora za udhibiti na uwekezaji itachochea wawekezaji kuendelea kuboresha na kuweka miundombinu bora zaidi ya huduma ili kugusa mahitaji ya wateja wengi”

Tunajisikia fahari kuona NMB banki anakuwa nguzo muhimu ya kutoa huduma za Airtel Money kwa kuwafikishia wakala wetu salio kila walipo ili waweze kuhudumia wateja wetu, hii inaonyesha dhairi huduma za kifedha kwa mtandao zinazidi kupanuka kutokana na jitihada na ubunifu wa watoa huduma kwa lengo la kuwahakikishia wateja usalama na unafuu katika kufanya malipo, Nina uhakika Tanzania itaendelea kukua katika swala la huduma za fedha endapo tu kutakuwa na mahusiano ya wadau kibiashara kama haya ya Airtel Money na Banki ya NMB”

“NMB itahudumia wakala wetu zaidi ya 45,000 ili kuweka na kutoa salio la Airtel Money wakati wowote katika matawi yao 160 nchi nzima, haya ni maendeleo makubwa sana hata kwa biashara yetu”. alieleza Colaso

NMB na Airtel inaingia Ubia kipindi ambacho Airtel Money pia imezindua kampeni yake kabambe ya Mr Money kwa lengo la kuwafikishia wateja wake taarifa za uhakika na unafuu katika huduma za Airtel Money. Airtel Money imefanikiwa pia kuleta huduma pekee za mikopo isiyokuwa na maharti magumu ya TIMIZA ambapo inawawezesha wateja na mawakala wake zaidi ya milioni 2 kujipatia mikopo kila wakati.

MRI, CT-SCAN ZAPIGA MZIGO SAA 24 MUHIMBILI, WAGONJWA 41,101 WAPIMWA.

0
0
Na John Stephen, MNH
 HOSPITALI ya Taifa Muhimbili (MNH) inaendelea kutoa huduma bora hasa ya vipimo kwa wagonjwa mbalimbali na kufanikiwa kupima wagonjwa 41,101 katika mwaka 2015/2016 kutoka wagonjwa 32,010 waliopimwa mwaka wa fedha 2014/2015.

Taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma na Huduma kwa Wateja, Aminiel Buberwa Aligaesha imeeleza kwamba mashine zinafanya kazi vizuri na kwamba hakuna mashine mbovu hadi kusababisha wagonjwa kukosa huduma za vipimo.

“Hospitali inahakikisha kila mgonjwa anayehitaji vipimo anapata na kwa gharama nafuu. Kama mashine ilisimama kufanya kazi tangu Januari hadu Juni, 2016 ni kwa muda wa kati ya siku moja hadi mbili kupisha matengenezo kinga,” amesema Bwana Aligaesha katika taarifa yake aliyoitoa leo kwa vyombo vya habari.

 Mkuu wa Idara ya Mionzi katika Hospitali Ya Taifa Muhimbili (MNH), Dk. Flora Lwakatare akifuatilia mgonjwa anavyochukuliwa vipimo leo mchana katika hospitali hiyo.
 Mgonjwa akiwa katika mashine ya MRI LEO katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH). Pembeni ya mgonjwa ni Mtaalamu wa Mionzi, Medard Mallya akimsaidia mgonjwa kukaa vizuri kwenye mashine hiyo.
Picha na John Stephen, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).

TIMU ZA OLIMPIKI ZAKABIDHIWA BENDERA, DSTV WAIPA SHAVU.

0
0

 Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Annastazia Wambura akiwakabidhi wachezaji bendera ya Taifa kwaajili ya kwenda kupeperusha huko Rio De Jeneiro nchini Brazil wanaokwenda kushiriki mashindano Olimpiki.
 Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania, Filbert Bayi akizungumza kabla ya kukabidhi bendera na kuwaaga  kwa wanaokwenda katika mashindano ya Olimpiki Rio De Jeneiro nchini Brazil.
Baadhi ya wadau wa michezo mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja jijini Dar es Salaam leo.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Annastazia Wambura  akiwa katika Picha ya Pamoja na washiriki wa mashindano ya Olimpiki wanaoenda nchini Brazil

Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii.
NAIBU Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Annastazia Wambura amewataka washiriki wanaoenda kuwakilisha nchi kwenye mashindano ya Olimpiki mwaka huu Rio De Jeneiro nchini Brazil kujituma na kuhakikisha wanafanya vizuri ili kurudi na medali, hayo ameyasema wakati wa kukabidhi bendera kwa timu za kuogelea, judo na riadha leo Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam.

Wambura amesema kuwa wanapokwenda kuiwakilisha waamini kuwa macho na masikio ya watanzania wote yapo kwao kwahiyo wajitahidi kadri ya uwezo wao kuweza kuhakikisha watakapokuwa wanarejea basi waje wakiwa wamevaa medali zao. " Mnakwenda katika mashindano ya Olimpiki na macho yote ya watanzania yapo kwenu tunategemea mkiwa mnarudi basi tutakuja kuwapokea mkiwa na medali zeni kifuani na hilo linawezekana kama mtajituma mkiwa na ari ya ushindi".

Akiwa anawakabidhi bendera hiyo, Wambura amewaasa wanamichezo hao kutumia fursa nyingine ya kujifunza zaidi kwani kama wataenda kukutana na mataifa mengine mbalimbali. Naye moja ya wadhamini wa safaru hiyo kampuni ya Multichoice Africa, imewataka washiriki hao kujituma zaidi kwani watanzania wote watakuwa wanawaangalia kupitia chaneli zao zinazopatikana kwenye kisimbuzi cha DSTV.

Mkurugenzi wa Multichoice Maharage Chande amesema mwaka huu mashindano yote yatakuwa yanakuja moja kwa moja kupitia channeli za Super Sport na itawapa fursa watanzania kuwashuhudia.wawakilishi wao kwenye mashindano hayo makubwa duniani. Mbali na hilo watakapokuwa huko waitangaze nchi yetu kwa vivutio vilivyopo nchini ili kuzidi kupata watalii mbalimbali kutoka.kote duniani hayo yamesemwa na Godfrey Tengeneza mkurugenzi wa utalii nchini.

Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania , Filbert Bayi amesema kuwa kwa mwaka huu washiriki wamekaa kambi katika sehemu tofauti nchini na wengine wakiwa nje ya nchi na hilo.limefanikisha kuweza kujifua vyema ili kuweza kurejesha ushindi nyumbani. Hilal ameweza kuweka kambi nchini Dubai, Magdalena alikuwa nchini Australia. Andrew aliweka kambi chuo cha polisi Moshi na wanariadha waliweka kambi mkoa wa Arusha.

Washiriki kwa upande wa riadha ni Alphonce Simbu, Said Makula l, Fabian Naasi na Sarah Makela. Timu ya kuogelea inawakilishwa na Hilal Hilal na Magdalena Moshi na Judo ni Andrew Mlungu. Huku timu ya kwanza ikitarajiwa kuondoka alfajiri ya leo wakiambatana na daktari wa timu Nasoro Matuzya.

PINK RIBBON ITASHIRIKIANA NA SERIKALI KUFANYA UCHUNGUZI NA TIBA YA SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI

0
0

Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiongea na Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Pink Red Ribbon toka nchini Marekani Bi.Celina Schocken,shirika hilo limeahidi kushirikiana na Tanzania kwenye masuala mazima ya saratani ya matiti na mlango wa kizazi ili kuwezesha huduma kuwa endelevu,kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa UNAIDS Dkt.Warren Naamara
Waziri Ummy Mwalimu akizungumza kwenye kikao hicho,kushoto ni mkurugenzi msaidizi wa kitengo cha afya na mtoto-wizara ya afya dkt.Georgina Msemo .
Waziri Ummy Mwalimu akiongea na Mkurugenzi Mtendaji wa Pink Ribon Red Itinerary Bi. Celina Schocken

Watu 14 wafariki kwa ugonjwa unaosababishwa na sumukuvu

0
0
Hussein Makame-MAELEZO

Watu 14 wamefariki dunia katika wilaya za Chemba mkoani Dodoma na Kiteto mkoani Manyara kutokana na ugonjwa unaojulikana kitaalamu kama ‘Aflatoxicosis’ unaosababishwa na sumu kuvu (Aflatoxins) kwenye nafaka iliyoharibika.

Hayo yamesema na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari juu ya magonjwa ya milipuko na magonjwa mengine leo jijini Dar es Salaam.

“Ugonjwa uliosababishwa na sumu kuvu (Aflatoxins) uliripotiwa kwa mara ya kwanza tarehe 13 Juni, 2016 katika wilaya za Chemba mkoani Dodoma na baadaye mkoani Manyara katika wilaya ya Kiteteo” alisema Waziri Ummy na kuongeza kuwa:

“Wagonjwa walikuwa na dalili za kuumwa tumbo, kuharisha, kutapika, tumbo kuvimba na kuwa manjano sehemu mbalimbali za mwili ambayo inaashiria kuathirika kwa ini”

Alisema mbali na vifo hivyo, hadi kufikia Julai 31 mwaka huu wagonjwa 54 waliripotiwa kuugua ugonjwa hu huku wagonjwa wanne wakilazwa kutokana na kuugua. “Hadi kufikia tarehe 31, Juni 2016 kulikuwa na wagonjwa 54 na watu 14 walipoteza maisha kutokana na ugonjwa huo.Aidha katika wiki iliyopita aliripotiwa mgonjwa mmoja mpya kutoka wilaya ya Kondoa” alisema Waziri Ummy na kufafanua kuwa:

“Jumla ya wagonjwa waliolazwa wodini ni wanne kati yao mmoja yupo Hospitali ya Rufaa ya Dodoma na watatu wapo katika Hospitali ya Kondoa”
Waziri Ummy alitaja wilaya zilizoripoti wagonjwa hao na idadi ya wagonjwa kuwa ni wilaya ya Chemba wagonjwa 38, Kondoa wagonjwa tisa , Kiteto wagonjwa watatu, Chamwino wagonjwa wawili na Dodoma Manispaa mgonjwa mmoja.

“Vijiji vilivyoathirika zaidi na ugonjwa huo ni kutoka wilaya ya Chemba ambavyo ni Kinkima, Itolwa, Mwailanje na katika wilaya ya Kondoa ni kijijini cha Ubembeni” alisema Waziri Ummy. Hivyo, aliitoa hofu familia iliyopoteza watu wanne katika kijiji cha Mwaikuzabe na kusema vifo hivyo havihusiani na uchawi au kuwekewa sumu bali ni chakula cha siku ile kilithibitika kwamba kilikuwa na sumukuvu.

Kufuatia athari hizo Serikali itafanya uchunguzi wa kina katika wilaya kumi za Chemba, Kondoa, Chamwino na Kiteto na wilaya nyingine za mikoa ya Sindida, Dodoma na Manyara zinazopakana na wilaya hizo. Alisema uchunguzi huo unalenga kubaini hali ya usalama wa vyakula vinavyotumiwa na jamii ili kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo na kuwaathiri wananchi wengi zaidi wanaoishi katika wilaya hizo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taifa wa Afya wa Wizara hiyo Dkt. Fausta Mosha alisema wizara imeandaa vipepereshi vyenye maelekezo yanayotoa elimu juu ya kijikinga kwa kuandaa chakula kuanzia hatua ya uvunaji shambani hadi wakati wa kula. Naye Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Otilia Gowelle alisema njia bora ya kupambana na ugonjwa huo ni kuukinga kwa kuhakikisha sumu kuvu haizalishwi kutoka kwenye nafaka.

Akifafanua kuhusu udhibiti, Waziri Ummy alisema wanashirikiana na Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi kutoa elimu kwa wananchi juu ya njia sahihi ya uhifadhi na uandaaji wa chakula utakaosaidia kupunguza kiasi cha sumukuvu kwa nafaka ambazo hazijaharibika sana. “Njia hizi ni pamoja na kuhifadhi nafaka zilizokauka vizuri na kuchambua nafaka zilizoharibika (zilizooza, kuvunjika, zilizobadilika rangi), kukoboa mahindi kabla ya kusaga au kuacha kutumia nafaka zitakazoonekana kuharibika rangi” alisema.

Waziri Ummy alisisitiza Serikali kuendelea kuimarisha mikakati ya kitaifa ya kupunguza uchafuzi wa sumukuvu katika vyakula, ikiwa ni pamoja na kujenga uwezo wa kupima sumukuvu katika damu na choo kidogo miongoni mwa taasisi za ndani ya nchi. Inaelezwa kuwa ugojwa wa‘Aflatoxicosis’unaosababishwa na sumu kuvu (Aflatoxins) kwenye nafaka uliwahi kutokea nchini Kenya mwaka 2004 na kusababisha vifo vya zaida ya watu 100 huku wengine 200 waliathirika.

RAIS DKT MAGUFULI AHITIMISHA ZIARA YA SIKU NNE MIKOA YA SINGIDA, TABORA NA SHINYANGA

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akihutubia wananchi wa Katoro na Buseresere wakati akielekea nyumbani kwake Chato mkoani Geita leo Agosti 1, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Mbunge wa Chato na Naibu Waziri wa Nishati na Mdini Mhe. Dkt Medard Kalemani baada ya kuhutubia wananchi wa Katoro na Buseresere wakati akielekea nyumbani kwake Chato mkoani Geita leo Agosti 1, 2016.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli katika picha ya pamoja na madiwani na viongozi wa Katoro na Buseresere baada ya kuhutubia wananchi wakati akielekea nyumbani kwake Chato mkoani Geita leo Agosti 1, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimsabahi mtoto Shabani Kalemani (miezi 8) na mama yake Asha Simon baada ya kuhutubia wananchi wa Katoro na Buseresere wakati akielekea nyumbani kwake Chato mkoani Geita leo Agosti 1, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akilakiwa kwa furaha kijijini Bwanga wakati akielekea nyumbani kwake Chato mkoani Geita leo Agosti 1, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimia wananchi kijijini Bwanga wakati akielekea nyumbani kwake Chato mkoani Geita leo Agosti 1, 2016

SERIKALI YATOA SIKU 30 KWA GGM

0
0

Afisa Madini wa Geita, Fabian Mshai (aliyesimama) akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt Medard Kalemani (katikati), namna ambavyo Ofisi yake ilitekeleza maagizo aliyoyatoa kwao kuhusu malalamiko ya baadhi ya wananchi wanaoishi karibu na Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) likiwemo suala la mipasuko ya nyumba zao. Wengine pichani ni maafisa kutoka Wizarani.
Baadhi ya Maafisa kutoka Wizara ya Nishati na Madini wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt Medard Kalemani (hayupo pichani), wakati alipokuwa akizungumza na uongozi wa Mkoa wa Geita na wawakilishi wa wananchi kuhusu ripoti ya wataalam wa mipasuko kutoka Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) juu ya chanzo cha mipasuko ya baadhi ya nyumba na majengo yaliyo karibu na Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM).
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt Medard Kalemani akizungumza na wawakilishi wa wananchi wa Geita wakiwamo wabunge na madiwani kuhusu uamuzi wa Serikali kufuatia malalamiko mbalimbali yaliyotolewa na baadhi ya wananchi wanaoishi jirani na Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) kuwa shughuli zinazoendeshwa na Mgodi huo zinawaathiri kwa namna 
 
 

Na Veronica Simba - GEITA

Serikali imetoa siku 30 kwa Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) kuwalipa fidia wananchi wanaoishi ndani ya eneo la leseni ya Mgodi huo au kuwaruhusu rasmi waendelee kuishi humo na kufanya shughuli za kiuchumi.

Sambamba na agizo hilo, pia Serikali imeupa Mgodi huo siku 14 kuziba Tuta lililopasuka ambalo huzuia maji machafu kutoka Mgodini yasiende katika makazi ya wananchi.

Aidha, kufuatia taarifa iliyowasilishwa na timu ya wataalam wa mitetemo kutoka Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST), baada ya kukamilisha kazi waliyopewa kutafiti chanzo cha mipasuko ya baadhi ya nyumba za wananchi na majengo mbalimbali yaliyo jirani na Mgodi wa GGM, Serikali imeagiza timu hiyo kufanya tathmini maalum ya idadi ya waathirika.

Iliagizwa kazi hiyo ifanyike kwa kushirikiana na Ofisi ya Makamu wa Rais, Kitengo cha Maafa na Kitengo cha Mazingira pamoja na uongozi kuanzia ngazi za vijiji mpaka madiwani na wabunge husika kwa muda wa siku Saba tu kuanzia tarehe 29 mwezi huu na kuiwasilisha serikalini ili hatua stahiki zichukuliwe.

Maagizo hayo yalitolewa hivi karibuni mjini Geita na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt Medard Kalemani katika kikao chake kilichomshirikisha Mkuu wa Mkoa wa Geita na wawakilishi wa wananchi wa Geita wakiwamo wabunge na madiwani.

Dkt Kalemani alisema kuwa maagizo hayo ni kufuatia maelekezo aliyoyatoa mapema mwezi Februari mwaka huu alipotembelea mkoani humo na kusikiliza kero za wananchi wa vitongoji vya Katoma na Nyamalembo. Alisema maagizo hayo yasipotekelezwa ipasavyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa, chini ya sheria ya madini na sheria nyingine za nchi. 
mbalimbali.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST), Prof Abdulkarim Mruma akiwaeleza wawakilishi wa wananchi wa Geita (hawapo pichani) namna wataalam wa mitetemo kutoka Ofisi yake walivyofanya utafiti kuhusu chanzo cha mipasuko ya baadhi ya nyumba za wakazi wanaoishi karibu na Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM).
Mbunge wa Viti Maalum Geita (CHADEMA), Upendo Peneza, akizungumza wakati wa kikao baina ya Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt Medard Kalemani na wawakilishi wa wananchi wa Geita wakiwamo wabunge na madiwani husika kuhusu malalamiko mbalimbali kutoka kwa baadhi ya wananchi wanaoishi jirani na Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) kwamba shughuli zinazofanywa na Mgodi huo zinawaathiri kwa namna mbalimbali.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt Medard Kalemani (katikati) akitoa maagizo mbalimbali kwa Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) kuhusu malalamiko ya baadhi ya wananchi wanaoishi jirani na Mgodi huo kuwa shughuli zinazofanywa na Mgodi zinawaathiri kwa namna mbalimbali. Waliokaa Kulia ni viongozi kutoka GGM. Kushoto ni baadhi ya wawakilishi wa wananchi wa Geita wakiwamo wabunge na madiwani na Maafisa wa Wizara ya Nishati na Madini. 
 


SERIKALI YATOA SIKU 30 KWA GGM KUTOA UAMUZI
Akifafanua zaidi kuhusu masuala hayo yaliyosababisha Serikali kufikia hatua husika, Naibu Waziri alisema kuwa mwezi Februari alipotembelea Geita, wananchi walieleza kero kubwa walizokuwa nazo kuwa ni baadhi ya nyumba zao kupasuka kiasi cha kutoweza kukalika na nyingine kukalika lakini zimeharibika kutokana na ulipuaji wa baruti (blasting) wa Mgodi wa GGM.

Malalamiko mengine yalihusu wananchi ambao wanaendelea kuwa na makazi ndani ya eneo la leseni ya GGM, ambayo ina ukubwa wa kilomita za mraba 196. 7 ambao walikuwa wanadai fidia ili waondoke katika eneo husika au waendelee kubaki na kufanya shughuli zao za maendeleo.

Pia, baadhi ya wananchi wanaoishi karibu na Mgodi na hasa maeneo ya chini ya Mgodi, walilalamikia maji machafu ambayo yalikuwa yanakingwa na tuta ambalo lilikuwa limebomoka na kuruhusu maji kutiririka kuelekea kwenye makazi yao na hivyo kuwepo uwezekano wa kuathiri afya zao. Walitaka hatua madhubuti zichukuliwe kuzuia mtiririko huo wa maji.

Alisema kuwa, baada ya kusikiliza maelezo ya pande zote mbili, kwa suala la mipasuko, aliunda timu ya wataalam wa Serikali kutoka GST na kuiagiza kufanya utafiti wa kisayansi ili kubaini chanzo cha mipasuko husika kwa kushirikiana na wawakilishi wa wananchi wa maeneo hayo.

Timu hiyo ilikamilisha kazi hiyo na kukabidhi taarifa yake kwa Serikali mwezi Julai mwaka huu ambapo ilibainisha vyanzo vikuu viwili vya mipasuko hiyo kuwa ni udhaifu wa majengo yaliyoathirika lakini pia milipuko inayofanywa na GGM hasa ya miaka ya nyuma hususan kuanzia mwaka 2007 hadi 2010 ambayo ilikuwa na kipimo cha juu cha mitetemo kinachofikia 57.

Kuhusu wananchi wanaoishi kwenye eneo la leseni, Dkt Kalemani alisema kuwa alimwagiza Afisa Madini wa Geita kuwaandikia GGM ili wathibitishe kwa maandishi kati ya kuwaondoa wananchi wale kwa kuwafidia kama eneo hilo lilivyo kwenye leseni yao au kuwaruhusu waendelee kuishi na kufanya shughuli za maendeleo, jambo ambalo Mgodi haukutekeleza badala yake walisema wananchi hao ni wavamizi.

Aidha, kuhusu suala la Tuta, Naibu Waziri alieleza kuwa, aliagiza lizibwe mara moja ili kuepusha madhara ambayo yangeweza kujitokeza kama maji yangeendelea kutiririka kuelekea kwenye makazi ya wananchi, ambalo pia halijatekelezwa hadi sasa.

“Ni kutokana na hali hiyo, sasa Serikali tumeona tutoe maagizo ya mwisho ili yatekelezwe na yasipotekelezwa, hatua kali za kisheria zitachukuliwa.” Naibu Waziri alisema kuwa Serikali haina nia mbaya kwa Mgodi husika isipokuwa ni wajibu wa Serikali kuhakikisha pia sheria zinafuatwa ili pande zote zipate haki stahiki.

“Tunapenda sana wawekezaji muwekeze kwa sababu ndiyo mnatupa ajira, mnalipa mirabaha na kodi lakini lazima tuzingatie sheria.” Dkt Kalemani alizitaka Mamlaka zinazohusika kusimamia zoezi hilo kikamilifu.

KATIBU MKUU WIZARA YA UJENZI NA BALOZI WA ITALIA WAKIKAGUA RAMANI YA BARABARA

0
0
BEN2 
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia masuala ya Ujenzi Injinia Joseph Nyamhanga  akimuonyesha Balozi wa Italia Bwana Roberto Mengoni( kulia) baadhi ya barabara ambazo zimependekezwa kuombewa mkopo wa masharti nafuu kutoka serikali ya Italia, kushoto ni Mkurugenzi wa barabara nchini Injinia Ven Ndiyamukama
BEN3 
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia masuala ya Ujenzi Injinia Joseph Nyamhanga  akimuonyesha Balozi wa Italia Bwana Roberto Mengoni( kulia) baadhi ya barabara ambazo zimependekezwa kuombewa mkopo wa masharti nafuu kutoka serikali ya Italia, kushoto ni Mkurugenzi wa barabara nchini Injinia Ven Ndiyamukama
BEN4 
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia masuala ya Ujenzi Injinia Joseph Nyamhanga  akimuonyesha Balozi wa Italia Bwana Roberto Mengoni( kulia) baadhi ya barabara ambazo zimependekezwa kuombewa mkopo wa masharti nafuu kutoka serikali ya Italia, kushoto ni Mkurugenzi wa barabara nchini Injinia Ven Ndiyamukama.
BEN1 
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia masuala ya Ujenzi Injinia Joseph Nyamhanga kushoto  akimuonyesha Balozi wa Italia Bwana Roberto Mengoni baadhi ya barabara ambazo zimependekezwa kuombewa mkopo wa masharti nafuu kutoka serikali ya Italia.

WAZIRI MKUU AITAKA WIZARA KUWEKA MIKAKATI YA KUENDELEZA UVUVI KATIKA KINA KIREFU CHA BAHARI

0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameitaka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kuweka mikakati endelevu ya kuwawezesha wananchi kuvua katika maji ya kina kirefu cha bahari kwa kutumia meli kubwa na za kisasa ili Taifa liweze kunufaika na rasilimali hiyo ambayo imekuwa ikichukuliwa na wavuvi wenye vyombo vya kisasa kutoka nje ya nchi.

Aidha, amezitaka halmashauri zote nchini ziweke mikakati na mipango ya kuifanya mito na maziwa mbalimbali nchini kuwa na uvuvi endelevu kwa kufuatilia kwa karibu shughuli za wavuvi na kuwaadhibu wote watakaovua kinyume na sheria.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumatatu, Agosti 01, 2016) wakati akifungua maadhimisho ya 23 ya sherehe za maonesho ya wakulima Kanda ya Mashariki katika Uwanja wa Mwalimu J.K Nyerere yanayofanyika katika mkoa wa Morogoro ambapo amesema bado nchi haijaweza kutumia rasilimali hiyo kikamilifu.

Amesema halmashauri zinatakiwa zihamasishe vijana kuunda vikundi vya kuanzisha miradi ya kufuga samaki katika maeneo yao na wewezeshwe kupata teknolojia ya ufugaji huo. Akizungumzia vikundi vya wajasiariamali wanaovua katika maeneo ya bahari na maziwa alishauri waelimishwe kuhusu namna ya kupata mikopo ya kununulia zana bora za kisasa za uvuvi ili shughuli zao ziwe na tija.

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu amesema wakulima wanatakiwa kuzingatia matumizi ya kanuni bora za kilimo ikiwemo matumizi sahihi ya zana za kisasa, pembejeo na viuatilifu vilivyopendekezwa na wataalam ili kufanikisha mapinduzi ya kilimo kuelekea kilimo cha biashara.

Akizungumzia kuhusu suala la usindikaji alisema wakati anatembelea mabanda mbalimbali alipata fursa ya kuona teknolojia zinazoweza kutumiwa na wakulima, wafugaji na wavuvi katika kuongeza uzalishaji bora wenye tija. Amesema amefurahi kuona wakulima, wafugaji na wafanyabiashara wa mazao, pembejeo na zana za kilimo wana ari kubwa ya kushiriki katika kuleta mapinduzi katika sekta ya kilimo ili kwenda sambamba na kasi ya Serikali ya kuifanya nchi kujitosheleza kwa chakula na kuendeleza uchumi wa viwanda.

“Naamini kuwa pamoja na lengo la kujitosheleza kwa chakula, wakulima, wafugaji na wavuvi wataongeza ari ya uzalishaji kwa kushirikiana na sekta za umma na binafsi katika kuvipatia viwanda vyetu malighafi na kuongeza thamani ya mazao,” alisema.

Kufuatia hatua hiyo Waziri Mkuu aliziagiza halmashauri zote kuhamasisha uanzishaji na uendelezaji wa viwanda vidogo vya kusindika mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi kwa kushirikisha taasisi za umma na binafsi, mashirika na vikundi vya ujasiriamali katika maeneo yao.

Akizungumzia namna Serikali ilivyojipanga kutatua changamoto ya migogoro baina ya wafugaji na wakulima Waziri Mkuu alisema wafugaji wenye mifugo mingi watahamishiwa katika vitalu vinavyomilikiwa na ranchi za Taifa na wenye mifugo michache watatengewa maeneo katika vijiji.

Awali Waziri Mkuu alitembelea baadhi ya mabanda na maeneo ya vipando vya mazao mbali mbali yaliyoko katika viwanja hivyo ambapo alisema ameridhishwa na juhudi zilizofanyika katika maandalizi ya maonesho ya mwaka huu ikiwa ni pamoja na uendelezaji wa uwanja huo.

“Napenda kutoa pongezi za dhati kwa kujenga miundombinu na nyumba za kudumu za kufanyia maonesho. Aidha, natoa shukrani za pekee kwa Halmashauri zetu, Mashirika yetu ya Umma na binafsi; na watu binafsi ambao wamejenga na wanaendelea kujenga majengo mazuri na ya kudumu,” alisema.

Pia alizindua jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Temeke na kusema kuwa uboreshaji wa viwanja hivyo unaonesha jinsi wadau wote katika sekta ya kilimo, mifugo, uvuvi na ushirika wanavyotambua umuhimu wa maonesho hayo kama njia ya kuongeza maarifa na kumuenzi mkulima, mfugaji na mvuvi kwa kutambua mchango wao katika uchumi wa Taifa.


Kauli mbiu ya maonyesho hayo kwa mwaka huu ni kilimo, mifugo na uvuvi ni nguzo ya maendeleo: vijana shiriki kikamilifu (“HAPA KAZI TU”)


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU, JUMATATU, AGOSTI 01, 2016.

JPM amaliza mgogoro wa makazi Magomeni Kota

0
0
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi akiongea na wakazi wa Magomeni Kota kuhusu kumalizika kwa mgogoro wa makazi leo jijini Dar es Salaam. Kushoto Ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angelina Mabula na Kulia ni Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Yamungu Kayandabila.
Wakazi wa Magomeni Kota wakimsikiliza Waziri Lukuvi akitoa taarifa ya kumalizika kwa mgogoro wa makazi ya eneo hilo leo jijini Dar es Salaam.


Na Jonas Kamaleki, MAELEZO

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imemaliza mgogoro wa makazi wa Magomeni Kota uliodumu kwa kipindi kirefu.Hayo yamesbainishwa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi wakati akiongea na Kamati ya Mgogoro wa Makazi ya Magomeni Kota mbele ya waandishi wa habari.

“Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli amefuta hati na mikataba yote inayohusiana na ardhi ya yaliyokuwa makazi ya Magomeni Kota, Dar es Salaam”,alisema Lukuvi.

Kwa mujibu wa Lukuvi Rais ameondoa umiliki wa eneo hilo toka Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na kumilikisha Serikali Kuu ambayo ndiyo itakayosimamia ujenzi wa nyumba 644 ambazo zitauzwa kwa bei nafuu kwa waliokuwa wakazi wa Magomeni Kota.

“Tutajenga nyumba 644 na kuwauzia kwa bei ya jengo na siyo ya ardhi ili kuwapeni unafuu katika kununua,”alisema Lukuvi huku akishangiliwa na baadhi ya wakazi wa Magomeni.Aidha, Lukuvi amesema kuwa anampongeza Mhe. Rais Magufuli kwa kumaliza mgogoro huu ambao umedumu kwa muda mrefu na kuongeza kuwa ameagiza timu ya wataalamu wa Wizara kupima na kuchora michoro kwa ajili ya ujenzi.

Lukuvi amesema katika eneo hilo zitajengwa nyumba za heshima ambazo kila moja itakuwa na vyumba vitatu ili kukidhi mahitaji ya kifamilia kwani watu hawa wamekaa kwa miaka takribani 50 hadi wameshapata wajukuu. Ameongeza kuwa kila mmiliki wa nyumba hiyo atapewa hati yake hata kama nyumba hiyo itakuwa kwenye ghorofa.

Lukuvi amesema kuwa Rais ameagiza maeneo kama ya Magomeni Kota katika mikoa ishirini ya Tanzania Bara nayo yatakuwa katika mfumo huo wa Magomeni. Kwa mujibu wa Lukuvi wazee ambao wanakaa kwenye nyumba kama hizo sehemu nyingine wasiondolewe kwani hao walikuwa watumishi wa umma hivyo Rais amesema wasibughudhiwe.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Mgogoro wa Makazi Magomeni Kota, George Abel ameshukur Mhe Rais Magufuli na Wazir Lukuvi kwa kutatua mgogoro huo ambao anadai umewasumbua sana.

Ameahidi kutoa ushirikiana kwa Serikali pindi suala la ujenzi litakapokuwa linaendelea ili kuhakikishaujenzi unaenda haraka.Naye Wakili ambaye alikuwa akiendesha kesi hiyo kabla ya Mhe. Rais kuingilia kati, Mhe. Twaha Tasilima ameonyesha kuridhishwa na utendaji wa Rais Magufuli.

“Rais Dkt Magufuli na Mhe. Waziri Lukuvi ni watu wa vitendo na si maneno na kweli wanawajali wanyonge, nawashukuru sana,”alisema Tasilima.

Uamuzi wa kurudisha eneo hilo kwenye Serikali Kuu umetolewa na Rais Magufuli tarehe 10/7/ 2016.

Serikali yawashukuru wadau wa michezo kwa kushiriki katika maendeleo ya michezo nchini.

0
0

Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akiongea na wanamichezo na wadau wa michezo katika hafla ya kuwaaga wanamichezo wanaokwenda kuiwakilisha Tanzania nchini Brazil katika mashindano ya Olimpiki kwa mwaka 2016 leo Agosti 1, 2016.



Picha/Habari na Raymond Mushumbusi.

Serikali imewashukuru wadau wa michezo nchini kwa kujitokeza na kuwa mstari wa mbele kushiriki na kudhamini michezo mbalimbali nchini.

Shukrani hizo zimetolewa leo na Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura alipokuwa akizungumza na wanamichezo wanaokwenda kushiriki mashindano ya Olimpiki kwa mwaka 2016 yanayofanyika Jijini Rio dejaneiro nchini Brazil.

Mhe. Anastazia Wambura amesema kuwa wadau wa michezo wamekuwa wakishirikiana na Serikali sio katika suala la michezo pekee hata katika habari na Sanaa na amewapongeza kampuni ya ving’amuzi ya Multichoice Tanzania (DSTV) na Bodi ya Utalii katika azma yao ya kuunga mkono maendeleo ya sera ya michezo nchini.

“Napenda kuwashukuru wadau wetu Dstv na Bodi ya Utalii, nawapongeza kwa kuona fursa hii muhimu na kuitumia kuwatia moyo wawakilishi wa nchi yetu katika michezo ya Olimpiki kwa mwaka 2016 mueendelee kuiunga mkono Serikali katika kutekeleza sera ya maendeleo ya Michezo ili kufikia malengo” alisema Mhe. Anastazia.

Aidha amewataka wawakilishi wa Olimpiki kutumia fursa hii ya wadau wa michezo waliojitokeza kuwaunga mkono ikiwemo Bodi ya Utalii kutangaza utalii wa Tanzania kwa mataifa mengine watakayo kutana nayo katika mashindano ya Olimpiki nchini Brazil.

Kwa upande wake Mkurungezi Mkuu wa Multichoice Tanzania Bw.Maharage Chande ameishukuru Serikali kwa kuwapa fursa ya kushirikiana na timu ya Olimpiki kuitangaza michezo na kuitangaza Tanzania kimataifa na kuahidi kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuendeleza michezo nchini.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA MAJALIWA AFUNGUA MAONYESHO YA NANENANE MOROROGORO

0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizindua Banda la Maonyesho la wilaya ya Temeke kwenye maonyesho ya wakulima Nanenane mjini Morogoro Agosti 1, 2016. Kulia kwake ni mkewe Mary na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam , Paul Makonda. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama bidha mbalimbali zinazotokana na zao la mronge zikiwema, dawa, mafuta na sabuni wakati alipoembelea meza ya Bibi Salome Kaiza (kulia) kwenye banda la wilaya ya Tameke katika  maonyesho ya wakulima Nanenane mjini Morogoro, Agosti, 1, 2016. Kulia kwake ni Mkewe Mary.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakitazama matikiti maji wakati walipotembelea meza ya Bwana Diocresty Theonesy kwenye banda la wilaya ya Temeke katika maonyesho ya wakulima Nanenane mjini Morogoro Agost 1, 2016. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisikiliza Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Damian Lubuva wakati alipotembelea Banda la Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika Monyesho ya Wakulima Nane mjini Morogoro Agosti 1, 2016, Kushoto ni mkewe Mary. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary (kulia kwake)wakitazama kilimo cha mbogamboga kwa mtindo wa kilimo kichuguu wakati walipotembelea banda la Chuo Kikuucha Kilimo cha Sokoine (SUA) kwenye maonyeshoya Nanenane mjini Morogoro Agosti 1, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakitazama viatu vilivyotengenezwa katika gereza la Karanga mkoani Kilimanjaro wakati alipotembelea banda la Magereza katika maonyesho ya wakulima Nanenane mjini Morogoroo Agosti 1, 2016, kulia ni Mratibu wa Magereza wa maonyesho hayo na Mkuu wa Gereza la Mtego wa Simba, Oman Msekwa. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary (Kulia kwake) wakatazama bwawa la samaki na banda la kufugia bata wakati alipotembelea banda la Magereza katika monyesho ya wakulima Nanenane mjini Morogoro Agosti 1, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary wakitazama mboga zilizokaushwa na mtambo wa kukaushia mboga hizo katika katika maonyesho ya wakulima Nanene nane mjini Morogoro Agosti 1, 2016
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary wakipokezana tikiti maji wakiwa kwenye meza ya Bwana Diocresty Theonesy kwenye banda la Wilaya ya Temeke katika Maonyesho ya wakulima Nanenane mjini Morogoro Agost 1, 2016. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakikagua mtama uliopandwa kwenye eneo la Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) katika maonyesho ya wakulima Nanenane mjini Morogoro Agost 1, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizindua Banda la Maonyesho la wilaya ya Temeke kwenye maonyesho ya wakulima Nanenane mjini Morogoro Agosti 1, 2016. Kushoto ni mkewe Mary.
 

Mrema akutana na Madereva Bodaboda wa Kinondoni.

0
0

Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole Mhe. Augustine Mrema (katikati)akisitiza jambo kwa madereva wa pikipiki toka Wilaya ya kinondoni wakati alipokutana nao ili kusikiliza kero mbalimbali wanazokutana nazo wakiwa katika kazi zao mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni Mwenekiti wa Waendesha Bodaboda na Bajaj wilaya ya Kinondoni Bw. Almano Mdede na kushoto ni Katibu wake Bw. George Mbwale.
Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole Mhe. Augustine Mrema ( Mwenye Kofia Katikati) akisisitiza jambo kwa madereva wa pikipiki toka Wilaya ya kinondoni wakati alipokutana nao ili kusikiliza kero mbalimbali wanazokutana nazo wakiwa katika kazi zao mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Madereva wa pikpiki Wilaya ya Kinondoni Bw. Almano Mdede akifafanua jambo kwa madereva pikipiki wa Wilaya ya Kinondoni wa Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole Mhe. Augustine Mrema (katikati) alipowatembelea madereva hao na kusikiliza kero mbalimbali wanazokutana nazo wakiwa katika kazi zao mapema hii leo jijini Dar es Salaam,kushoto ni Katibu wa Madereva Pikipiki Wilaya hiyo Bw. George Mbwale.
Baadhi ya madereva Pikipiki wa Wilaya ya Kinondoni wakimsikiliza Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole Mhe. Augustine Mrema (hayupo pichani) alipokutana nao ili kusikiliza kero mbalimbali wanazokutana nazo wakiwa katika kazi zao mapema hii leo jijini Dar es Salaam. Picha na Eliphace Marwa.Picha zote na Eliphace Marwa -Maelezo

Ilala yawataka wafanyabiashara kuzingatia muda wa usafi

0
0
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO

Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jijini Dar es Salaaam imewataka wafanyabiashara kuzingatia muda uliopangwa na Serikali kwa ajili ya usafi wa mazingira katika maeneo yao ya kazi unaofanywa kila ifikapo siku ya jumamosi.

Muda uliowekwa kwa ajili ya zoezi hilo ni kuanzia saa 12:00 asubuhi hadi saa 3:30 asubuhi, ambapo wafanyabiashara wote watapaswa kufungua maduka na masoko yao mara baada ya zoezi hilo kukamilika.

Hayo yamesemwa leo na Afisa wa Manispaa hiyo, David Langa wakati alipokuwa akiongea na mwandishi wa habari hii kuhusu mwitikio wa wananchi juu ya zoezi la usafi wa mazingira unaofanyika kila jumamosi na kila mwisho wa mwezi.

“Nawaomba Wafanyabiashara wenye tabia ya kujichelewesha ili wafike baada ya muda wa usafi pamoja na wale wanaofungua biashara kabla ya muda uliopangwa na Serikali kuacha mara moja kwani lengo la kubadili muda wa kufungua biashara ni kwa ajili ya kufanya usafi” alisema Langa.

Akifafanua zaidi Langa aliwatahadharisha wananchi wanaopenda kutupa taka hovyo kuacha mara moja kwani sheria ya afya na sheria ya mazingira inapinga suala hilo na kwa mujibu wa sheria hizo adhabu yake ni faini ya shilingi milioni moja au kifungo kisichozidi miaka 6.

Kwa mujibu wa Langa alisema kuwa, suala la usafi sio suala la Serikali pekee bali wananchi wanatakiwa walifanye kuwa ni sehemu ya kulinda afya zao, hivyo kila mmoja anapaswa kuzingatia usafi kwenye maeneo yanayomzunguka. Aidha Langa alisema kila mwananchi anapaswa kuwa mlinzi wa mwenzie kwani zoezi la kulipishwa faini bado ni endelevu, mtu atakaemkamata mwenzie anatupa taka atapewa shilingi elfu 20 na aliyekamatwa atatoa faini ya shilingi elfu 70

Naibu Waziri Anastazia Wambura akagua eneo la ujenzi wa mageti ya kieletroniki katika Uwanja wa Taifa Leo Jijini Dar es Salaam.

0
0

Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel (kulia) akimuonesha Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura eneo eneo la ujenzi wa mageti ya kieletroniki katika Uwanja wa Taifa leo Agosti 1, 2016 Jijini Dar es Salaam.

Kaimu Meneja wa Uwanja wa Taifa Bw.Julius Mgaya (kulia) akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura na Katibu Mkuu Wizara ya hiyo Prof Elisante Ole Gabriel kuhusu ujenzi wa mageti ya kieletroniki katika Uwanja wa Taifa leo Agosti 1, 2016 Jijini Dar es Salaam.

Picha zote na Raymond Mushumbusi WHUSM

MBUNGE ULEGA AKUTANA NA WANANCHI WAKE VIJIWE VYA KAHAWA

0
0

Mbunge wa Jimbo la Mkuranga, Abdallah Ulega wa tatu kutoka kushoto akiwa sambamba na Wazee wa Mkuranga katika eneo la stendi kwenye kijiwe cha kahawa akipata kikombe cha kahawa pamoja ambapo pia walibadilishana mawazo juu ya maendeleo ya wilaya yao leo mkoani Mpwani. Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya jamii.
Viewing all 46202 articles
Browse latest View live




Latest Images