Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI NCHI MH:MWIGULU NCHEMBA ATUA MGODI WA NYAMHUNA UNAODAIWA KUTESA NA KUUA MTANZANIA MMOJA,AWAKAMATA WAHUSIKA(WACHINA NA WATANZANIA) WANAOSADIKIKA KUHUSIKA.

$
0
0
Waziri wa mambo ya ndani ya nchi,Mwigulu Nchemba hii leo amewasili mkoa wa Geita kwa ziara ya kikazi kubwa ikiwa ni kufuatia taarifa za mateso na mauaji yaliyofanywa na raia wa china wanaomiliki sehemu ya mgodi wa Nyamhuna uliopo Katoro-Geita dhidi ya wafanyakazi/vibarua ambao ni watanzania.

Takribani wiki moja sasa kumekuwa hali ya sintofahamu dhidi ya picha zinazoenezwa mitandaoni na kwenye vyombo vya habari zikionesha raia wa tanzania anayefanya kazi kwenye mgodi tajwa akiteswa na kufanyiwa vitendo vya kinyama na mwajili wake ambaye ni raia wa china.

Imemlazimu waziri mwenye dhamana na usalama wa raia na mali zao kupitia wizara ya mambo ya ndani kufika eneo la mgodi kujiridhisha kwa taarifa zilizotapakaa na kubeba simanzi kwa watanzania.

Mwigulu Nchemba amejiridhisha kuwa kulikuwepo na tukio hilo la mtanzania kuteswa na huyo mwajili wake kipigo kilichopelekea kupoteza fahamu na sio kifo.Hatua za awali mwigulu alizozifanya ni kwenda gereza la Geita mjini alikohifadhiwa kijana huyo kwa madai ameshitakiwa na mwajili wake kwa kosa la wizi lililopelekea yeye kupigwa.Katika mahojiano ya waziri Mwigulu Nchemba na kijana huyo,Mwigulu alibaini kuwa kijana huyo aliyepo gerezani ndiye mhanga wa tukio lile kwa uthibitisho wa makovu yaliyopo mwili mwake na mavazi aliyovalia wakati anateswa na wakati yupo hapo gerezani.
Katika hali hiyo ilimlazimi Mh.Mwigulu kwenda mgodini akiwa ameambatana na kijana huyo kwaajili ya kutambua waliofanya vitendo hivyo vya kinyama.Katika oparesheni hiyo, kijana aliyeteswa na kujeruhiwa aliwabaini watanzania 5 ambao ni walinzi wa eneo hilo na mchina mmoja walioshirikiana kumpiga,kumtesa na kumjeruhi.Kufuatia utambuzi huo na maelezo ya wahusika,Nchemba akaagiza wahusika wakamatwe mara moja na ameondoka nao kwa hatua zaidi za kisheria.

Katika hali nyingine ya kusikitisha,Mwigulu amebaini uwepo wa wahamiaji haramu raia wa china katika mgodi huo ambapo nyaraka za uhamiaji mkoa wa geita zinainesha raia 28 wenye vibali ndio waliruhusiwa kukaa kwenye mgodi huo,lakini katika operasheni ya kushitukiza aliyoifanya Mh.Mwigulu nchemba amebaini uwepo wa raia wa china zaidi ya 50 wanaoishi katika mgodi huo kinyume na sheria.Hivyo amemuagiza mkuu wa mkoa na timu yake ya uhamiaji kuhakikisha wote wasio na vibali wanakamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria.



 


 

MWENYEKITI WA CCM RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA SEKRETARIETI NA WAFANYAKAZI WA CHAMA DODOMA MJINI DODOMA

$
0
0

Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akilakiwa mara baada ya kuwasili makao makuu ya chama hicho mjini Dodoma leo
Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akijiandaa kuongea na sekretarieti ya CCM kwa mara ya kwanza katika makuu ya chama hicho mjini Dodoma leo .

Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiongea na wafanyakazi wa makao makuu ya chama hicho mjini Dodoma leo
Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Waziri Mkuu Ndg. Kassim Majaliwa katika picha ya pamoja na Secretarieti ya CCM makao makuu ya chama hicho mjini Dodoma leo
:Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Waziri Mkuu Ndg. Kassim Majaliwa katika picha ya pamoja na Sekretarieti ya CCm na wafanyakazi wa makao makuu ya chama hicho mjini Dodoma leo
Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiaga baada ya kupata picha ya pamoja na Sekretarieti ya CCm na wafanyakazi wa makao makuu ya chama hicho mjini Dodoma leo
Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiwa na Katibu Mkuu wa CCM Ndg Abdulrahman Kinana akisikiliza maoni na changamoto toka kwa wafanyakazi wa makao makuu ya chama hicho mjini Dodoma leo.PICHA NA IKULU.

Ofisi ya Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali yawataka wananchi kuheshimu tunu za Taifa

$
0
0

Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali Bw. Kassian Chibogoyo (kulia) akionesha kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) rangi sahihi zinazotakiwa kutumika katika bendera ya Taifa wakati akielezea umuhimu wa wananchi kutumia vielelezo sahihi vya Taifa na kuachana na vile vya kughushi, kulia ni Afisa Habari toka Idara ya Habari (Maelezo) Bw. Frank Shija.

Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali Bw. Kassian Chibogoyo (kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu umuhimu wa wananchi kutumia vielelezo sahihi vya Taifa na kuachana na vile vya kughushi, kushoto ni Afisa Habari toka Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Nyamagori Omari
Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali Bw. Kassian Chibogoyo (katikati) akionesha kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) baadhi ya vielelezo sahihi vya Taifa vinavyotakiwa kutumiwa na wananchi wakati alipokuwa akielezea umuhimu wa wananchi kutumia vielelezo sahihi vya Taifa na kuachana na vile vya kughushi mapema hii leo Jijini Dare s Salaam kulia ni Afisa Habari toka Idara ya Habari (Maelezo) Bw. Frank Shija na kushoto ni Afisa Habari toka Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Nyamagori Omari.Picha zote na Eliphace Marwa - Maelezo


Na: Frank Shija, MAELEZO

Katika kuhakikisha heshima , hadhi na maadili miongoni mwa jamii ya Watanzania Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi mahiri wa Rais John Pombe Magufuli imewakumbusha wananchi kuheshimu na kuzingatia matumizi sahihi ya Vielelezo vya Taifa.

Haya yamebainishwa na Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali Cassian Chibogoyo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika Kipindi chake cha ‘Tujikumbushe’’ Sehemu ya Pili kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam.

Chibogoyo amesema amesema kuwa wakati sasa umefika kwa jamii kuendeleza utamaduni uliokuwapo wa kuheshimu na kufuata desturi zilizowekwa katika kuendeleza umoja, amani na mshikamano. ‘Natoa wito kwa watanzania wote, katika kufanya maboresho ya kurejesha hadhi ya taifa tunapaswa kuheshimu sana Vielelezo vya Taifa letu, hapa na maanisha tuheshimu wimbo wa taifa na Nembo ya Taifa.’

Amesema kuwa katika kuhakikisha vielelezo hivyo vinaheshimiwa Ofisi yake imejipanga kufuatilia kwa karibu wale wote watakao kiuka matumizi sahihi ya Vielelezo vya Taifa ikiwemo Nembo, Bendera na Wimbo wa Taifa.

Aliongeza kuwa kuanzia sasa matumizi ya Bendera ya Taifa yatakwenda sambamba na matumizi ya Bendera ya Jumuiya ya Afrika Mashariki hivyo amezitaka Ofisi zote za Serikali pamoja na Taasisi zake waanze utaratibu wa kupandisha pia bendera hiyo kwani Tanzania tunaamini katika ushirikiano huo.

Katika hatua nyingine uongozi wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu (TUGHE) Tawi la Ofisi ya Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali wamekanusha tuhuma zilizoandikwa na moja ya gazeti hapa nchini(Jina limehifadhiwa) zikimtuhumu Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali kuwa na kusema kuwa tuhuma zilizoandikwa katika Gazeti hilo siyo zakweli na ata wao kama wafanyakazi wameshangazwa

Katibu wa TUGHE Tawi la Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali amesema kuwa ni vyema waandishi wakafanya kazi zao kwa weledi kuliko kuandika taarifa zizizosahihi kwani kufanya hivyo kuta waingiza matatizoni. Nilitegemea kabla mwandishi hajachapisha habari ile angetafuta ukweli kutoka upande wa pili ikiwemo kuhusishwa kwa uongozi wa Chama cha Wafanyakazi kwani ndiyo wenye mamlaka yakutoa taarifa katika ngazi husika kwa tupo kwa ajili ya kuwawakilisha na kuwatetea wafanyakazi.

Kipindi cha Tujikumbushe kimekuwa kikionyeshwa na TBC1 ambapo lengo lake kuu ni kutoa elimu kwa jamiii juu ya matumizi sahihi na umuhimu wa kutunza nyaraka na tunu za Taifa, ambapo Sehemu ya Kwanza ya kipindi hicho kilihusu Nyaraka za Serikali. Kipindi kinachofuata kitahusu Historia ya kuwepo kwa Katiba na Katiba inayopendekezwa.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya atembelea chuo cha maendeleo ya wananchi kilichopo nzega mkoani tabora.

$
0
0


Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga akisaini kitabu cha wageni alipotembelea Chuo cha aendeleo ya Wananchi kilichopo Nzega Mkoani Tabora.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga (katikati) akiangalia chumba kwa ajili ya mafunzo ya Komputa alipotembelea Chuo cha Maendeleo ya Wananchi kilichopo Nzega Mkoani Tabora.Kulia ni Mkuu wa Chuo hicho Bw. Bw. Eustaki Shirima na Kushoto ni Mkurugenzi Idara ya Ununuzi na Ugavi kutoka Wizara hiyo Bw. Richard Mallya.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga (katikati) akiangalia karakana inayotumika kwa mafunzo katika chuo hicho, Kushoto ni Mkuu wa Chuo hicho Bw. Eustaki Shirima
Jengo la Karakana katika chuo hicho.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga akiongea na watumishi katika chuo hicho mapema leo alipotembelea kuona utendaji chuoni hapo.


Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga akijadiliana jambo na Mkurugenzi Idara ya Ununuzi na Ugavi kutoka Wizara hiyo Bw. Richard Mallya (katikati) na Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Bw. Eustaki Shirima kilichopo Nzega Mkoani Tabora alipokitembelea chuo hicho mapema leo.

PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO

Wizara ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu, Bunge na Watu wenye Ulemavu kuhamia Dodoma wiki ijayo

$
0
0
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu, Bunge, Kazi,Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (Kushoto) akiongea leo jijini Dar es Salaam na Watendaji Wakuu na Watumishi wa Wizara na Taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu kuhusu utekelezaji wa kuhamia Dodoma, Kulia ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu), Dr. Abdallah Possi.
 Mkurugenzi wa Utawala na Raslimaliwatu Ofisi ya Waziri Mkuu, Issa Nchasi akifafanua jambo wakati wa kikao cha Waziri Jenista Mhagama na Watendaji Wakuu na Watumishi wa Wizara na Taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu kuhusu utekelezaji wa kuhamia Dodoma (Kulia kwake ni Mkurugenzi Msaidizi-Utawala, Samwel Mwashambwa).
Baadhi ya Watendaji Wakuu na Watumishi wa Wizara na Taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu wakimsikiliza Waziri Jenista Mhagama wakati wa kikao kuhusu utekelezaji wa kuhamia Dodoma.


Na Jonas Kamaleki, MAELEZO

Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu,Bunge, Kazi, Ajira na Watu Wenye Ulemavu itahamia Dodoma juma lijalo kufuatia agizo la Mhe. Rais John Pombe Magufuli la Serikali kuhamia Dodoma.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu, Bunge, Kazi ,Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Jenista Mhagama wakati akiongea na watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu na Taasisi zilizoko chini ya ofisi hiyo.

“Mchakato wa kuhamia Dodoma umekwisha kilichobaki kwa sasa ni utekelezaji, mimi na manaibu mawaziri wangu tunahamia juma lijalo ili tukamkaribishe Mhe. Waziri Mkuu anayehamia Septemba mwaka huu,” alisema Mhagama.

Mhagama amesema kuwa kila kiongozi anayehamia Dodoma inabidi awakute walio chini yake tayari wamekwishahamia ili kumpokea, hivyo akawataka na watendaji ambao wako chini yake watangulie kwa ajili ya kumpokea yeye na viongozi wenzake. Aidha, Waziri huyo amesema kwa sasa hakuna mjadala wa kuhamia Dodoma lilobaki ni utekelezaji tu wa kuhamia Makao Makuu.

Mhagama amesema kama kuna Taasisi chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu imetenga fedha kwenye bajeti kwa ajili ya ujenzi, shughuli hiyo ikafanyike Dodoma ambako Serikali inahamia. Kwa kusema hivyo kadhalika na ofisi au Wizara nyingine za serikali ambazo zimetenga fedha ya ujenzi wakajenge Dodoma.

Suala la kuhamia Dodoma sio geni bali limekewepo kwa kipindi kirefu ila utekelzaji wake ndio ulikuwa bado; pia katika Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015 suala hili lipo, alisema Mhagama na kuongeza kuwa kipindi cha nyuma Wizara saba (7) ziliwahi kuhamia Dodoma na kwa sasa Wizara inayoshughulikia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) iko Dodoma.

Waziri Mhagama ameipongeza Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa kuanza ujenzi wa jengo lake mjini Dodoma na kusisitiza kuwa Wizara na Taasisi nyingine za Serikali kuiga mfano huo kwa kujenga ofisi zao Dodoma.

“Kwa kuwa sisi ni waratibu wa wizara zote inabidi tuunde kikosi kazi kitakachofanya kazi ya uratibu wa kuhama kikiwa Dodoma ili kuwawezesha na watumishi wenzetu kutekeleza agizo la Mhe. Rais la serikali nzima kuhamia huko,”alisema Mhagama.

Mhagama amesema kuwa Mamlaka ya Ustawishaji wa Makao Makuu Dodoma (CDA) wameshafanya kazi nzuri ya upimaji eneo la serikali ambalo litatumika kwa ajili ya ofisi. “Tumefika mwisho wa mchakato sasa ni utekelezaji na tunataka watumishi walielewe vizuri suala hili na wawe tayari kulipokea,”alisisitiza Mhagama.

Kuhamia Dodoma katika kipindi hiki kunatokana na agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli alillolitoa tarehe 27 Julai, 2016 mjini Dodoma kwenye Mkutano Mkuu Maalum wa CCM ambo ulimchagua kuwa Mwenyekiti wa tano wa chama hicho tawala.

MARAIS WASTAAFU NCHI ZA AFRIKA WAWASILI JIJINI DAR KUHUDHURIA MKUTANO MKUU WA UONGOZI WA MWAKA 2016

$
0
0

Rais mstaafu wa Afrika Kusini Mheshimiwa Thabo Mbeki (pichani kulia) akiwasili leo jijini Dar Es Salaam akiwa na Mwenyeji wake Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya UONGOZI Profesa Joseph Semboja,kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Uongozi wa mwaka 2016 utakoanza kesho hapa jijini Dar Es Salaam katika Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro.Mkutano huo utakaodumu kwa siku mbili utawajumuisha wadau mbalimbali.PICHA NA MICHUZI JR.MMG.
Raisi mstaafu wa Afrika Kusini Mheshimiwa Thabo Mbeki akisalimiana na Balozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania Mh. Thamsanga Dennis Msekelu baada ya kuwasili jijini Dar Es Salaam kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Uongozi wa mwaka 2016 utakoanza kesho hapa jijini Dar Es Salaam katika Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro wa siku mbili.Pichani kati ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya UONGOZI Profesa Joseph Semboja .
Raisi mstaafu wa Afrika Kusini Mheshimiwa Thabo Mbeki akizungumza na Balozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania Thamsanga Dennis Msekelu baada ya kuwasili jijini Dar Es Salaam kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Uongozi wa mwaka 2016 utakoanza kesho hapa jijini Dar Es Salaam katika Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro.
Rais mstaafu wa Msumbiji, Armando Emilio Guebuza akikaribishwa na baadhi ya wafanyakazi wa taasisi ya UONGOZI mara baada ya kuwasili jijini Dar Es Salaam kuhudhuria mkutano Mkuu wa Uongozi wa mwaka 2016 unaotarajiwa kuanza hapo kesho jijini Dar Es Salaam katika Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro kwa siku mbili.

Rais mstaafu wa Msumbiji, Armando Emilio Guebuza akikaribishwa na baadhi ya wafanyakazi wa taasisi ya UONGOZI mara baada ya kuwasili jioni ya leo jijini Dar Es Salaam kuhudhuria mkutano Mkuu wa Uongozi wa mwaka 2016 unaotarajiwa kuanza hapo kesho jijini Dar Es Salaam katika Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro kwa siku mbili.
Rais Mstaafu wa Msumbiji Joachim Chissano akikaribishwa na baadhi ya wafanyakazi wa taasisi ya UONGOZI mara baada ya kuwasili jijini Dar Es Salaam jioni ya leo kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Uongozi wa mwaka 2016 wa siku mbili,utakoanza hapo kesho jijini Dar Es Salaam katika Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro.Pichani shoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya UONGOZI Profesa Joseph Semboja .

Serikali yapongeza mpango wa Airtel FURSA,

$
0
0
 Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (kushoto) akikabidhi msaada wa mashine ya kutengeneza sabuni na vifungashio vyenye thamani ya zaidi ya milioni 10/- kupitia mpango wa Airtel FURSA ‘Tunakuwezesha’ kwa Mwenyekiti wa Kikundi cha Tupendane cha Tandika, Nasra Haji  katika hafla iliyofanyika kituoni hapo Manispaa ya  Temeke jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Afisa Maendeleo ya Vijana wa Manispaa hiyo, Anna Marika. 
Afisa Maendeleo ya Vijana wa Manispaa ya Temeke, Anna Marika (kushoto) akikabidhi kwa niaba ya Airtel msaada wa na vifungashio vya sabuni  baada ya kampuni hiyo kukabidhi  mashine ya kutengeneza sabuni vyenye thamani ya zaidi ya milioni 10/- kupitia mpango wa Airtel FURSA ‘Tunakuwezesha’ kwa Mwenyekiti wa Kikundi cha Tupendane cha Tandika, Nasra Haji  katika hafla iliyofanyika kituoni hapo jijini Dar es Salaam jana.  Wa (pili kushoto) ni Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi.

Kufatia mchango wake katika maendeleo ya miradi ya vijana Serikali imeupongeza mpango wa Airtel FURSA kwa kuwawezesha vijana nchi nzima kukuza uchumi wao.

Hayo yamesemwa na Afisa maendeleo ya vijana wa wilaya ya Temeke , Bi Anna Marica wakati Airtel kupitia mpango wake wa Airtel FURSA ilipotoa msaada wenye thamani ya shilingi milioni 10  kwa kikundi kilichoundwa na wanawake 12 cha Tupendane kilichopo Temeke jijini Dar es salaam

Alisema”  kupitia mradi wa Aritel FURSA, Airtel Tanzania imekuwa mstari wa mbele katika kuwasaidia vijana nchini na kupongeza kikundi cha Tupendane kwa kuwa moja kati ya vikundi vilivyofikiwa na Airtel FURSA

“Kikundi cha Tupendane kimeonyesha mfano mzuri hususani kwa vijana wakike na napenda kuwahasa muongeze hari na kufanyakazi kwa bidii zaidi ili kuongeza uzalishaji na kutengeneza ajira kwa vijana waishio jijini Dar es salaam.” Alisema Marica

Msaada wa vifaa uliotolewa kwa kikundi hicho ni pamoja na mashine mpya ya kutengenezea sabuni, vifungashio pamoja na kuboreshewa mazingira ya ofisi ya kufanyia kazi.

Kwa upande wake Meneja huduma kwa jamii, Bi Hawa Bayumi alisema“  tunatambua juhudi na ubunifu mkubwa unaofanywa na kikundi hiki na tunaamini msaada huu utasaidia kuinua mapato yao  kwa ujumla.

 “Huu ni msimu wa pili wa mradi wetu wa Airtel FURSA ambapo mpaka sasa tumeweza kuwafikia vijana wajasiriamali 20, makundi ya wajasiriamali 30 pamoja na kutoa mafunzo ya ujasiriamali kwa zaidi ya vijana 3000 nchini. leo tunajisikia furaha kukiwezesha kikundi hiki cha Tupendane kwani tunatambua kwa kuwawezesha vijana hawa 12 tutaweza kuziwezesha familia zao na jamii kiuchumi kwa namna moja au nyingine“ alisema Bayumi

 Mwenyekiti wa kikundi cha Tupendane Nasa Hija Siri aliwashukuru Airtel kwa kuwafikia vijana wengi na kutatua changamoto zao na kuahidi kutumia msaada huo kuongeza uzalishaji

 “ kupitia msaada huu tunauhakika wa kuongeza kiwango cha uzalishaji wa bidhaa zetu kwani kwa sasa tunatengeneza lita 20 kwa siku, na kwa msaada huu sasa tutazalisha hadi lita 100 kwa siku  haya kwetu sisi ni mafanikio makubwa na tunawashukuru sana Airtel”alisema Nasa

 Kikundi cha tupendane kilianza biashara zake kwa kuuza vitenge na kukopesa kwa wateja, biashara hii haikuwa ya mafanikio kwani wateja walishindwa kulipa madeni yao kwa wakati ndipo walipoamua kuanzisha biashara ya kutengeneza na kusambaza sabuni za maji na shampoo za nywele

Wagonjwa 45,000 wa saratani hugundulika tanzania kila mwaka

$
0
0

Mhe Ummy Mwalimu akiwa na waziri wa afya (Uganda) Mhe .Sara Opendi na Mhe Omar Sey Waziri wa Afya wa Gambia.
Waziri wa afya Ummy Mwalimu akifuatilia mkutano huo
.Picha ya pamoja ya wake wa marais na mawaziri wa afya wa afrika,waliohudhuria mkutano wa 10 wa kupambana na saratani ya shingo ya Kizazi,matiti na tezi dume (picha/habari na wizara ya afya)

Na.Mwandishi wetu,Addis Ababa

Ugonjwa wa saratani nchini Tanzania ni chanzo cha magonjwa na vifo,hivyo inakadiriwa Takribani wagonjwa wapya wa saratani 45,000 hugundulika kila mwaka.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu katika Mkutano wa 10 wa kupambana na ugonjwa wa saratani ya shingo ya kizazi, matiti na tezi dume barani Afrika unaofanyika nchini hapa.

Waziri Ummy amesema kati ya wagonjwa hao asilimia 38 ni wa saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake, asilimia 14 saratani ya ngozi, asilimia 10 saratani ya matiti na saratani ya tezi ni asilimia 4 . Hatahivyo,takribani watu 35,000 hufariki kila mwaka kutokana na magonjwa ya Saratani.

Licha ya changamoto mbalimbali zinazokwamisha jitihada za kukabiliana na magonjwa hayo ikiwemo uhaba wa Miundombinu ya kutolea huduma za afya, vifaa tiba, Uhaba wa Watumishi wa Afya, rasilimali fedha na gharama kubwa za dawa za matibabu ya saratani,Waziri Ummy amesema Serikali ya Tanzania imepitisha Sera za Kitaifa na Miongozo mbalimbali ya Kupambana na Saratani, kutoe Elimu kwa jamii na watoa huduma za afya nchini kuhusu Saratani.

Aidha, kuanzishwa kwa huduma za upimaji wa saratani katika Hospitali na vituo vya afya zaidi ya 300 nchini na huduma za Tiba kupitia Hospitali ya Saratani ya Ocean Road.

“Serikali itapanua wigo wa matibabu ya saratani katika Hospitali ya Bugando Mwanza na KCMC, Kilimanjaro. Mipango ya baadae ni huduma hizo pia kutolewa ktk Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya.”hii itapunguza wagonjwa kufuata huduma kwenye hospitali ya saratani ya Ocean Road

Mkutano wa 10 wa Saratani ya shingo ya kizazi, matiti na tezi dume barani Afrika unafanyika kwa kuasisiwa kwa juhudi za wake za Marais wa bara la Afrika. Mkutano huu unahudhuriwa na Wake wa Marais wa Afrika, Mawaziri wa Afya wa Afrika, Wanataaluma na Wadau wa Maendeleo. Lengo kuu ni kufanya mapitio ya hatua zilizochukuliwa na nchi za Afrika, changamoto zilizopo na kuweka mikakati ya pamoja na ya nchi katika kukabiliana na saratani.

Wakati wa kukabidhiwa uenyekiti wa Umoja wa Wake wa Marais wa Afrika wa Kupambana na saratani ya Shingo ya Kizazi, Matiti na Tezi Dume kutoka kwa Mwenyekiti anaemaliza muda wake, mke wa Rais wa Kenya mama Magreth Kenyatta, Mke wa Waziri Mkuu wa Ethiopia mama Roman Tesfaye Abneh ameleeza masikitiko yake kwa jinsi ambavyo ugonjwa wa saratani unavyoua kuliko hata ugonjwa wa UKIMWI na kifua kikuu. 
 
Hivyo ameziomba nchi za Afrika kuongeza uwekezaji katika eneo hili hasa kwa kuhakikisha dawa zinakuwepo za kutosha, kuboresha utoaji wa huduma za afya ikiwemo upimàji na tiba, kuhakikisha nchi zinatoa mafunzo ya Kutosha kwa watumishi wa afya katika fani hii

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII,MHANDISI MAKANI AFANYA KIKAO NA VIONGOZI WA HIFADHI YA TAIFA YA KISIWA CHA RUBONDO.

$
0
0
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii ,Mhandisi Ramo Makani akizungumza na viongozi wa serikali ikiwemo kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Geita pamoja na viongozi wa Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo alipokutana nao katika Hoteli ya Asilia Lodge.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani akizungumza na mmoja wa wageni katika Hoteli ya Asilia Lodge iliyopo katika Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo.
Ugeni wa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani ukipunga mikono kuaga wenyeji wao katika Hoteli ya Asilia Lodge ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo.
Naibu Waziri wa Maliasilili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani ,akiviishwa vazi maalum (Boya) ambalo hutumika kujiokoa wakati uafiri wa maji unatumika.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii ,Mhandisi Ramo Makani akiingia kwenye Boti kwa ajili ya kutembelea vivutio mbalimbali vya Utalii katika Hifadhi ya Taifa ya Rubondo.
Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo,Misana Mwishawa akimueleza jambo Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani wakati akitembelea vivutio mbalimbali vya utalii katika hifadhi hiyo.
Mamba ni moja ya vivutio katika Hifadhi ya Taifa ya Rubondo ambayo Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani alivutiwa kuwatizama.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani akitizama vivutio mbalimbali wakati akizunguka na boti maalumu katika visiwa vilivyoko Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo.
Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo,Missana Mwishawa akimuonesha Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani eneo ambalo ni makazi na mazalia ya ndege katika moja ya visiwa vilivyoko katika Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo.
Mkuu wa wilaya ya Geita,Herman Kapufi alikuwa ni mmoja wa viongozi walioongozana na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhandisi Ramo Makani kazika ziara hiyo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani akizunbgumza jambo mara baada ya kupata maelezo mbalimbali kutoka kwa Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo,Misana Mwishawa
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani akitia saini katika kitabu cha wageni baada ya kuwasili katika hoteli ya Asilia Lodge iliyopo ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo.
Mkurugenzi wa Utalii na Masoko wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Ibrahim Musa akizungumza wakati wa kikao kifupi cha Naibu Waziri wa Utalii na Maliasili ,Mhandisi Ramo Makani na viongozi wa Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo.
Mbunge wa Jimbo la Geita Vijijini,Joseph Kasheku (Msukuma) akizungumza wakati wa kikao hicho.
Mkuu wa wilaya ya Geita,Herman Kapufi akizungumza katika kikao hicho.
Na Dixon Busagaga wa Michuzi Blog,Kanda ya Kaskazini.

WAZIRI MBARAWA ATEMBELEA OFISI ZA TTCL.

$
0
0

 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akiongea na Uongozi wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) wakati alipotembelea kampuni hiyo, Jijini Dar es salaam.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya simu Tanzania (TTCL), jinsi ya mfumo wa kutoa taarifa kwa wafanyakazi unavyofanya kazi wakati alipotembelea ofisini hiyo jijini Dar es salaam.
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni  ya Simu Tanzania (TTCL) Dkt . Kamugisha Kazaura akisoma taarifa ya utendaji kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (Hayupo pichani) wakati alipoongea na uongozi wa kampuni hiyo, jijini Dar es salaam.
 Mwenyekiti wa bodi ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) Profesa Tolly Mbwete akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (hayupo pichani) wakati Waziri alipotembelea ofisi hiyo, jijini Dar es salaam.
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni  ya Simu Tanzania (TTCL) Dkt . Kamugisha Kazaura akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa wakati alipofanya mazungumzo na wafanyakazi wa kampuni hiyo,jijini Dar es salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akiongea na wafanyakazi wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL),Jijini Dar es salaam.
PICHA ZOTE NA BENJAMINI SAWE -MAELEZO.

TAARIFA KWA UMMA, WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA

NAIBU WAZIRI WA AFYA DK. HAMISI KIGWANGALLA AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA UJUMBE WA VIONGOZI WA MFUKO WA ABBOTT (ABBOTT FUND) KUTOKA MAREKANI

$
0
0

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla (kushoto) akizungumza na viongozi wa mfuko wa Abbott (Abbott Fund) kutoka nchini Marekani na wale wa Tanzania waliomtembelea Ofisini kwake jijini Dar es salaam kuzungumza naye kuhusu masuala mbalimbali ya uboreshaji wa huduma za Afya na Elimu kupitia program mbalimbali zinazofanywa na Mfuko huo nchini. Kutoka Kulia ni Makamu Mtendaji wa Rais wa Mfuko wa Abbott, Stephen Fussell na Makamu wa Rais Mwandamizi wa Mfuko wa Abbott (Abbott Fund Bi.Elaine Leavenworth (katikati).
Makamu wa Rais Mwandamizi wa Mfuko wa Abbott (Abbott Fund) Bi.Elaine Leavenworth (kulia) akimweleza Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla (kushoto) juu ya namna Mfuko wa Abbott ulivyojipanga kuendelea kutekeleza Program mbalimbali nchini Tanzania zikiwemo za Matumizi ya Teknolojia ya kisasa katika utoaji wa Tiba, maabara za kisasa, dawa na vifaa vya mafunzo kwa wanafunzi wa masomo ya Sayansi.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla (kushoto) akifurahia jambo na Makamu wa Rais Mwandamizi wa Mfuko wa Abbott (Abbott Fund) Bi.Elaine Leavenworth (kushoto) mara baada ya ujumbe wa viongozi wa mfuko huo kutoka nchini Marekani kumtembelea Ofisini kwake jijini Dar es salaam.
Ujumbe wa viongozi wa mfuko wa Abbott (Abbott Fund) kutoka Marekani ukimsikiliza Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla mara baada ya kumtembelea Ofisini kwake leo jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Mfuko wa Abbott (Abbot Fund) nchini Tanzania Andy Wilson akielezea utayari wa Mfuko huo katika kuzitafutia ufumbuzi changamoto zinazoikabili sekta ya Afya na Elimu nchini kupitia ufadhili wa Programu mbalimbali zinazofanywa na Mfuko huo kwa niaba ya Watu wa Marekani. Picha/ Aron Msigwa –MAELEZO.

Marais Wastaafu wa Afrika washirki Mkutano Mkuu wa Uongozi wa mwaka 2016 ( African Leadership Forum) jijini Dar leo

$
0
0
Baadhi ya Marais Wastaafu wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na Wadau mbalimbali kwenye mkutano huo Mkuu wa Uongozi wa mwaka 2016 ( African Leadership Forum) ulioanza leo jijini Dar Es Salaam katika Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro.Mkutano huo utakaodumu kwa siku mbili umewajumuisha wadau mbalimbali wakiwemo Mabalozi wa nchi mbalimbali.
Mtoa mada mkuu wa mkutano wa 'African Leadership Forum' Bw. Sipho Nkosi, ambaye ni mfanyabiashara maarufu na Mwenyekiti Mstaafu wa Chemba ya Madini kutoka Afrika Kusini akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo. Bw, Nkosi ni bilionea watatu mweusi anayeongoza kwa utajiri Afrika Kusini.
Rais mstaafu wa Afrika Kusini Mheshimiwa Thabo Mbeki akichangia moja ya mada katika Mkutano Mkuu wa Uongozi wa mwaka 2016  ( African Leadership Forum)  ulio anza leo jijini Dar Es Salaam katika Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro.Mkutano huo utakaodumu kwa siku mbili utawajumuisha wadau mbalimbali wakiwemo Mabalozi wa nchi mbalimbali.
 Rais Mstaafu wa Msumbiji Joachim Chissano akichangia moja ya mada mbalimbali zilizokuwa zikijadiliwa katika mkutano huo Mkuu wa Uongozi wa mwaka 2016  ( African Leadership Forum) wa siku mbili,unaondelea hivi sasa katika hoteli Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro,ambapo Mabalozi kutoka nchi mbalimbali pamoja na Wadau wengine wameshiriki.
Waziri wakuu wa Wastaafu katika awamu mbalimbali nchni Tanzania,pichani kulia ni Mh David Cleopa Msuya,Mh John Samuel Malecela pamoja na Mh.Salim,Ahmed Salim wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye  mkutano  Mkuu wa Uongozi wa mwaka 2016 ( African Leadership Forum) ulioanza leo jijini Dar Es Salaam katika Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro.Mkutano huo utakaodumu kwa siku mbili umewajumuisha wadau mbalimbali wakiwemo Mabalozi wa nchi mbalimbali.
Baadhi ya wafanyakazi wa taasisi ya UONGOZI walioandaa Mkutano MKuu wa UONGOZI wa 2016 sambamba na Waratibu wa Mkutano huo Kampuni ya MONTAGE wakiwa katika picha ya pamoja mapema leo asubuhi ndani ya hoteli ya Hyatt Kilimanjaro ambako ndiko mkutano huo unafanyika.
Mkutano ukiendelea
Baadhi ya Mabalozi na Wadau wengine wakifuatilia yanayojiri katika mkutano huo unaoendelea hivi sasa ndnai ya hoteli ya Hyatt Kilimanjaro,jijni Dar
Baadhi ya Wadau mbalimbali wakifuatilia yanayojiri kwenye mkutano huo.

MRADI WA HARAMBEE NI MKOMBOZI WA WANANCHI WA KIJIJI CHA CHOLE, MAFIA - PWANI

$
0
0
 Mkazi wa kijiji cha Chole, Bi. Riziki Hassan Selenge ambaye anasomeshewa watoto wake wawili na Mfuko wa maendeleo wa Harambee. 
Mwenyekiti wa Kijiji cha Chole, Shehari Ahmadi akielezea waandishi wa habari maendeleo ya kijiji cha Chole ikiwa ni pamoja na kutolea ufafanuzi suala la kauli iliyoleta mkanganyiko hivi karibuni ya kuwa mwekezaji amemilikishwa mapango ya kale kinyume cha sheria jambo ambalo si halina ukweli wowote kwa vile linachafua sura ya kijiji chao. Picha zote na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.


 Na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog - CHOLE, MAFIA. Wananchi wa kijiji cha Chole, wilayani Mafia - Pwani wameusifia mradi wa Harambee unaowapatia elimu watoto wao. Wakizungumza kwa nyakati tofauti na Kajunason Blog iliyoweka kambi kijijini hapo kujionea hali halisi ya kisiwa hicho, wananchi hao walisema ujio wa mwekezaji umekuwa mkombozi wa wanachi kwa vile ni mambo mengi waliyofaidika kwa muda wote ambao amekuwepo mwekezaji kijijini hapo. Akizungumza Mwenyekiti wa Kamati ya Harambee, Hamis Musa Athuman alisema mpaka sasa zaidi ya Sh. milioni 500 zimetumika kugharimia ada na mahitaji muhimu ya wanafunzi shuleni wa kijiji cha Chole, kupitia mradi huo. Aliongeza kuwa pesa hiyo imeweza kuwafikia jumla ya wanafunzi wapatao 300.
Mwenyekiti mstaafu wa kijiji cha Chole (kulia) ambaye alianza kazi yake 1999 - 2014, Bw. Maburuki Sadiki aliishukuru kampuni ya Chole Mjini Conservation and Development kwa kuweza kuwaletea maendeleo ya kweli kwa kuwajengea shule ya msingi, Zahanati, shule ya ChekeChea, Darasa la watu wazima kujifunza kingereza, watoto kwenda sekondari na mengine mengi. Pembeni ni mwenyekiti wa sasa Shehari Ahmadi.   Mkazi wa Chole, Bw. Johari Rajabu Fadhil ambaye ndiye mmoja ya waasisi waliompokea mwekezaji, na aliweza kupata ufadhili wa kwenda kusoma masomo ya kufundisha watoto ya miaka 2.
 Mkazi wa kwanza wa kijiji cha Chole wilayani Mafia kijiji cha Chole Mjini kupata digrii ya chuo kikuu, Zubeda Bhai akiwaelezea waandishi wa habari abato Kasika na Florence Mugarula waliotembelea eneo hilo la kihistoria jinsi ambavyo taasisi ya Chole Mjini Conservation and Development ilivyomsaidia gharama zote za kupata elimu ya juu.

 Alisema kuwa miaka ya nyuma wakazi wa Chole hawakuwa na mwamko wa elimu, lakini baadaye wakapata mwekezaji ambaye amechangia shughuli mbalimbali za maendeleo na kuwafanya wakazi wa kisiwa hicho kuwa nma mwamko wa elimu. "Tuna mwekezaji ambaye ni kampuni ya Chole Conservation & Development inayosimamia na kutunza magofu ya Kijerumani, ametusaidia sana kutuamsha na sasa hapa Chole kuna mwamko mkubwa wa elimu," alisema Kingi. 

Alisema kuwa mwekezaji huyo aliwahamasisha kuanzia kamati hiyo ndipo ufaulu wa wanafunzi wa darasa la saba ukaanza kuongezeka kuanzia mwaka 2007 na umekuwa ukizidi kupanda kadri miaka inavyokwenda.
 Wanafunzi wa Chekechea wakifundishwa.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari wanaonufaika na mfuko wa maendeleo wa Harambee. wakiwa pamoja na mkurugenzi wa Kampuni ya Chole Mjini Conservation and Development Bi. Anne K. de Villiers.
Moja ya usafiri wa boti unaotumika kuwavusha wakazi wa Chole kwenda Mafia Mjini.
Wageni waliofika kutembelea kisiwa cha Chole kujionea majumba ya kizamani yenye histori za mababu zetu.
Mwenyekiti wa Kamati ya Harambee, Hamis Musa Athuman akielezea maendeleo ya kijiji cha Chole katika upande wa elimu akiwa na  katibu wa kamati hiyo Mohamed Kingi (kulia).

Shule ya msingi ya Chole iliyojengwa na Mwekezaji wa Kampuni ya Chole Mjini Conservation and Development. 

Majengo ya kale yanayosimamiwa na kampuni ya Chole Mjini Conservation and Development yakionekana katika sura nzuri ya utunzaji wa hali ya juu.  Mkazi wa Kijiji Cha Chole Mjini kilichopo Mafia mkoani Pwani, Faharani Shomari, akiwaonyesha picha ya magofu ya kihistoria yalivyokuwa yameharibika na yalivyo sasa baada ya kufanyiwa ukarabati na kampuni ya  Chole Mjini Conservation & Development wakati waandishi hao walipoenda kutembelea eneo hilo. 

Picha zikionyesha jinsi majengo ya kale yalivyoonekana kabla hayajakarabatiwa na kufanyiwa usafi.
Katibu wa Harambee wa Kijiji Cha Chole Mjini kilichopo Mafia Mkoa wa Pwani, Mohammed Kingi akiwafundisha wanafunzi wa Shule ya Msingi Chole. Shule hiyo pamoja na masomo hayo yanafadhiliwa na kampuni ya Chole Conservation and Development

Kituo cha elimu ya watu wazima, hapa ndipo hujifunza kingereza.

 Kwa upande wake Mkurugenzi wa kampuni ya Chole Mjini Conservation & Development, Anne K. de Villiers, alisema kuwa wafadhili wa Kamati ya Harambee wako nchini Uingereza. Alisema kuwa aliwatafuta baada ya kubaini kwamba wakazi wa kijiji hicho hawana mwamko wa elimu na wamekuwa wakifadhili hata ujenzi wa vyumba vya madarasa, ujenzi wa nyumba za walimu na mambo mengine ya muhimu kwa ajili ya elimu. 

"Mbali na hilo kwa sasa tuna shule ya chekechea, kituo cha wanawake cha kujufunza kusoma, kituo cha kujifunza kompyuta na kituo cha wanafunzi na watu wengine kujifunza lugha ya Kiingereza na maktaba," alisema mkurugenzi huyo na kuendelea: 

Mwenyekiti wa Kijiji cha Chole, Shehari Ahmad alisema kuwa serikali imekuwa ikifaidika kwa kupata dola 10 kwa kila mgeni anayeingia na kulala katika hoteli ya Chole mjini inayosimamiwa na kampuni ya Chole Mjini Conservation and Development sambamba na dola 5 kwa kila mgeni anayetembelea majengo ya kale ya mapango ya Chole ambayo yakikuwa yakitumika katika biashara ya watumwa. 

Nae Bi. Riziki Hassan Selenge alisema kuwa hapo mwanzo mambo yalikuwa magumu tokea kuingia kwa mwekezaji huyo ndiye amekuwa mwasisi wa maendeleo kijijini kwao kwa vile asilimia 99 wakazi wa Chole hali zao ni masikini na hawakuweza kupeleka shule watoto wao. Upande wake Mwenyekiti mstaafu, 1999 - 2014, Bw. Maburuki Sadiki aliishukuru kampuni ya Chole Mjini Conservation and Development kwa kuweza kuwaletea maendeleo ya kweli kwa kuwajengea shule ya msingi, Zahanati, shule ya ChekeChea, Darasa la watu wazima kujifunza kingereza, watoto kwenda sekondari na mengine mengi.

 Akitoa historia fupi Bw. Sadiki alisema mchakato wa kumpokea mwekezaji huyo ulifanyika Desemba 4, 1993 kwa kueleza dhamila yake na tulimkubalia kwa kufuata sheria zote na makubaliano tuliwekeana nae tokea kipindi hicho ambapo tokea ameingia mwekezaji huyo amekuwa akitekeleza mkataba aliyopewa na kijiji.  

HOMA YA INI B NA C KUTOKOMEZWA IFIKAPO MWAKA 2030.

$
0
0
 Maandamano yakiendelea kuelekea viwanja vya Mwembe Yanga. Katikati ni Mratibu wa Mtandao wa Watu Wanaotumia Dawa za Kulevya (TANPUD), Happy Assan.
 Vijana waliopo kwenye mtandao wa kupinga matumizi ya dawa za kulevya wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
Mratibu wa Mtandao wa Watu Wanaotumia Dawa za Kulevya (TANPUD), Happy Assan, akizungumza kwenye maadhimisho hayo.
 Mwenyekiti wa TanPud Tanzania, Godfrey Ten, akizungumza katika maadhimisho hayo.
 Ofisa Maendeleo ya Jamii, Mratibu wa Asasi za Kiraia kutoka Tume ya Kuratibu Udhibiti wa Dawa za Kulevya Tanzania, Salome Mbonile, akizungumza kwenye maadhimisho hayo.
 Mwakilishi wa Taasisi ya Pasada, akizungumza kwenye maadhimisho hayo.
 Mratibu wa Afya- Dawa za kulevya wa Manispaa ya Temeke, Mwajuma Mwihumbo akizungumza kwenye maadhimisho hayo kwa niaba ya Meya wa Manispaa hiyo.

 Maadhimisho yakiendelea.
 Vijana waathirika na dawa za kulevya wakicheza kwenye maadhimisho hayo.
 Meneja wa Afya  Madaktari wa Dunia Dk. Faith Aikaeli kutoka Taasisi ya Medicins Du Monde akizungumza kuhusu ugonjwa huo.
Wageni waalikwa katika picha ya pamoja.

Dotto Mwaibale

UGONJWA wa homa ini umepangwa kutokomezwa ifika mwaka 2030 imefahamika ambapo watu wapatao  milioni 1.4 upoteza maisha ulimwenguni kutokana na maambuki ya ugonjwa huo ulimwenguni hasa kwa wale wanaotumia mihadarati kwa njia ya kujidunga.

Hayo yalibainishwa na Mratibu wa Afya- Dawa za kulevya wa Manispaa ya Temeke, Mwajuma Mwihumbo kwa niaba ya Meya wa Manispaa hiyo ambaye alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya homa ya ini yaliyofanyika viwanja vya Mwembe Yanga Dar es Salaam jana.

Alisema kuna umuhimu mkubwa wa kuongeza ufahamu kuhusu na kuungana na juhudi za ulimwengu za kutokomeza homa ya ini.

Alisema mada ya kampeni ya kimataifa ya homa ya ini ya mwaka huu ni utokomezaji ambao ni mwaka muhimu kwa homa ya ini.

Alisema lengo la maadhimisho hayo yaliyoandaliwa na asasi za kiraia, wafanyakazi wa huduma za afya, taasisi na vikundi vya utetezi na ushawishi ni kuongeza ufahamu wa homa ya ini B na C hasa kwa makundi hatarishi kama watumiaji wa mihadarati wanaojidunga.

Meneja wa Afya  Madaktari wa Dunia Dk. Faith Aikaeli kutoka Taasisi ya Medicins Du Monde alisema katika mkutano mkuu wa 69 wa Shirika la Afya Duniani (WHO) ni serikali zote ziliazimia kwa pamoja kuidhinisha mkakati wa ulimwengu wa utokomezaji wa homa ya ini.

Alisema hadi Februari 2016 nchi 36 zilikuwa zina mipango ya kitaifa ya utokomezaji wa homa ya ini na nchi 33 zipo katika mikakati ya kuandaa mipango hiyo.

"Mkakati unalenga kutokomeza homa ya ini B na C ifikapo mwaka 2030 ambapo unahusisha malengo ya tiba ambayo iwapo yatafikiwa yatapunguza vifo vinavyosababishwa na homa ya ini kwa asilimia 65 na kuongeza huduma ya tiba kwa asilimia 80 hivyo kuokoa maisha ya watu milioni 7.1 ifikapo mwaka 2030" alisema Dk.  Aikaeli
(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com.

KITENGO CHA SELIMUNDO”SICKLE CELL”HOSPITALI YA MUHIMBILI CHAPOKEA MSAADA WA SIMU 130 TOKA VODACOM TANZANIA.

$
0
0

 Balozi wa Ugonjwa wa Selimundo”Sickle cell” wa hospitali ya Taifa Muhimbili, Khadija Abdallah(kulia) Mtafiti wa magonjwa ya binadamu wa muhimbili University, Dkt.Mariam Ngaeje(katikati)wakiwaonyesha waandishi wa habari(hawapo pichani)baadhi ya simu kati ya 130 walizokabidhiwa na Mkuu wa kitengo cha Vodacom Tanzania Foundation,Renatus Rwehikiza(kushoto)zitakazotumika  kwa ajili ya utafiti wa utumiaji wa dawa za ugonjwa wa Selimundo”Sickle cell”.
 Balozi wa Ugonjwa wa Selimundo”Sickle cell” wa hospitali ya Taifa Muhimbili, Khadija Abdallah (kushoto), Mkuu wa kitengo cha Vodacom Tanzania Foundation, Renatus Rwehikiza (katikati) wakimsikiliza mtafiti wa magonjwa ya binadamu wa muhimbili University, Dkt.Mariam Ngaeje alipokuwa akiongea na waandishi wa habari (hawapo picha) wakati wa hafla ya kupokea simu 130 zilizotolewa msaada na Vodacom Tanzania Foundation kwa ajili ya utafiti wa utumiaji wa dawa za ugonjwa wa Selimundo”Sickle cell” Hafla hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa kitengo cha Vodacom Tanzania Foundation, Renatus Rwehikiza (kushoto)akimkabidhi baadhi ya simu kati ya 130,Balozi wa Ugonjwa wa Selimundo”Sickle cell” wa hospitali ya Taifa Muhimbili, Khadija Abdallah wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya simu hizo zilizotolewa na mfuko wa kampuni hiyo wa kusaidia jamii kwa ajili ya utafiti wa utumiaji wa dawa za ugonjwa wa Selimundo”Sickle cell”anayeshuhudia katikati ni mtafiti wa magonjwa ya binadamu wa muhimbili University, Dkt.Mariam Ngaeje.Hafla hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa kitengo cha Vodacom Tanzania Foundation, Renatus Rwehikiza (kushoto)akifungua moja ya simu kati ya 130 zilizotolewa msaada na mfuko wa kusaidia jamii wa kampuni hiyo, kwa ajili ya utafiti wa utumiaji wa dawa za ugonjwa wa Selimundo”Sickle cell”.wakati wa hafla ya kuzikabidhi simu hizo iliyofanyika jijini Dar e Salaam,Katikati ni mtafiti wa magonjwa ya binadamu wa muhimbili University, Dkt.Mariam Ngaeje na Balozi wa Ugonjwa wa Selimundo”Sickle cell” wa hospitali ya Taifa Muhimbili, Khadija Abdallah.

BURIANI MPIGANAJI MWENZETU JOSEPH SENGA

$
0
0
Mpiga picha Mkuu wa Gazeti la TanzaniaDaima, Mzee Joseph Senga amefariki Dunia huko nchini India alikokuwa akitibiwa usiku wa kuamkia leo. 

 inaelezwa kuwa alishapatiwa matibabu na kuruhusiwa kutoka hospitalini hivyo akaenda hotelini kwa mapumjziko na kujiandaa kwa safari ya kutoka huko Tarehe 5/8/2016 na angefika Tanzania tarehe 6/8/2016.  Kwamba leo hii akiwa hotelini alizungumza na mke wake akamwarifu kuwa anaendelea vizuri na anatarajia kuanza safari ya  kurejea nyumbani nchini tarehe 5 na angefika tarehe 6 mwezi ujao.

 Baadaye aliomba apelekwe bafuni kwa sababu mkono wake mmoja ulikuwa haujiwezi kujikunja kwa sababu ya oparesheni aliyofanyiwa. Aliogeshwa kisha baadaye akaomba apewe chakula na matunda bila kuchanganywa pilipili na akapewa akala. 

Alianza kujisikia vibaya baadaye kati ya saa 12 na saa 1 jioni jana, akaomba arudishwe hospitalini. Wakati anafuatwa dereva tax chini ya gorofa mbili alimokuwa akiishi Mwalimu Senga, walirudi wakamkuta hali yake imeanza kubadirika. 

Walimuwahisha hospitalini, kwamba kadri wanavyozidi kupunguza umbali ili hospitali alipokuwa akitibiwa ndivyo hali yake ilivyokuwa ikizidi kubadilika. 

Walipofika hospitalini, madaktari walimpima na kukuta Mwalimu Joseph Senga amefariki dunia. Mungu acha aitwe Mungu. Mwalimu Joseph Senga, tunakulilia, Mungu akupokee upumuzike kwa amani

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA MAJALIWA ATAKA MABARAZA YA MADIWANI KUFANYA MAPITIO YA UPUNGUFU VYA VYUMBA VYA MADARAKA KATIKA HALMASHAURI NCHINI.

$
0
0

Na Beatrice Lyimo-MAELEZO

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa ametoa maagizo kwa Mabaraza ya Madiwani nchini kufanya mapitio katika shule zote za Halmashauri ili kujua upungufu wa madarasa na kuanza mkakati wa utekelezaji wa ujenzi wake.

Aliyasema hayo leo wakati akipokea mchango wa madawati kwa shule ya msingi Chamazi kutoka Wizara Ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais la upatikanaji wa madawati katika shule za msingi na sekondari nchini.

Mhe. Majaliwa alisema suala la upatikanaji wa madawati linakwenda sambamba na ujenzi wa madarasa hivyo ni wajibu wa kila halmashauri kuweka mkakati wa ujenzi wa vyumba vya madarasa kwani elimu bora ni pamoja na kuwa na mazingira rafiki ya kusomea.

‘Mbali na utekelezaji wa agizo la Rais juu ya mkakati wa upatikanaji wa madawati, suala hili linakwenda sambamba na ujenzi wa madarasa hivyo Serikali imeanza utekelezaji wa ujenzi huo kwa maeneo machache hivyo ni jukumu la halmashauri kuhakikisha mnaandaa mikakati ya kuongeza vyumba vya madarasa’ alisema Majaliwa.

Aidha Waziri Mkuu Majaliwa alisema kuwa Serikali imeanza mkakati wa utekelezaji wa mpango wa kutumia mfumo mpya wa upandishaji madaraja walimu kwa kuwa mfumo wa uliuotumika awali haukuwa na tija kwa maslahi ya walimu nchini.

Akipokea madawati hayo Waziri mkuu alisema kuwa anajua shida iliyopo ya upungufu wa madawati katika wilaya ya Temeke hivyo na kugawa madawati hayo katika shule tatu zilizopo katika Wilaya hiyo ikiwemo shule ya msingi Chamazi, shule ya msingi Mbande pamoja na shule ya msingi Majimatitu .

Kwa upande wake Waziri wa Wizara Ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Augustine Mahiga alisema wizara yake ina jukumu la kuhakikisha inaitangaza nchi ili kuvutia wawekezaji na kukuza uchumi wa nchi, na kuongeza kuwa elimu bora ni msingi imara katika kufanikisha hilo.

Waziri Mahiga alisema Ubalozi wa Kuwait nchini pamoja na Jumuiya ya Mabohora wameikabidhi Serikali jumla 405 ili kuunga mkono jitihada za Rais ikiwemo .“Serikali ya Kuwait kupitia Ubalozi wake hapa nchini wametoa madawati 300 na kuahidi kutoa mengine 300 na Jumuiya ya Mabohora nao wamechangia madawati 105” alisema Balozi Mahiga.

Kwa mujibu wa Waziri Mahiga alisema watumishi wa Wizara yake walichanga kiasi cha Tsh. Milioni 100 ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha umma ili kuhamasisha umma kuhusu zoezi la upatikanaji wa madawati katika shule za msingi na Sekondari nchini.

BALOZI WA CANADA NCHINI AAGANA NA WAZIRI WA NISHATI NA MADINI PROFESA SOSPETER MUHONGO

$
0
0

Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kulia) na Balozi wa Canada Nchini Tanzania, Alexandre Lévêque (kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja.
Balozi wa Canada Nchini Tanzania, Alexandre Lévêque akisaini kitabu cha wageni kwenye Ofisi ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo. Balozi huyo alimtembelea Profesa Muhongo kwa ajili ya kumuaga mara baada ya muda wake kumalizika hapa nchini.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akimweleza Balozi wa Canada Nchini Tanzania, Alexandre Lévêque (kushoto) mikakati ya Serikali katika uboreshaji wa sekta ya nishati nchini .
Naibu Katibu Mkuu wa Nishati na Madini anayeshughulikia Madini Prof. James Mdoe (kushoto) na Naibu Katibu Mkuu wa Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati Dk. Juliana Pallangyo (kulia) wakifuatilia mazungumzo kati ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo na Balozi wa Canada Nchini Tanzania, Alexandre Lévêque (hawapo pichani)

TUNAZISUBIRI NEC NA ZEC KUIPIGIA KURA YA MAONI KATIBA INAYOPENDEKEZWA

$
0
0
 waziri wa Mambo ya Katiba na sheria Dkt Harrison Mwakyembe akizungumza na Kikosi cha Kupambana na Haki za Mirathi  (KIKUHAMI ) chini ya WiLDAF uliomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam
 Mwenyekiti wa  Kikosi cha Kupambana na Haki za Mirathi  (KIKUHAMI ) chini ya WiLDAF  Bibi Thabita Siwale akizungumza kumshukuru Waziri wa Mambo ya Katiba na sheria Dkt Harrison Mwakyembe walipokutana nae Ofisini kwake jijini Dar es salaam
Uongozi  wa Kikosi cha Kupambana na Haki za Mirathi  (KIKUHAMI ) chini ya WiLDAF  katika picha ya pamoja na  Waziri wa Mambo ya Katiba na sheria Dkt Harrison Mwakyembe  na katibi Mkuu Prof Sifuni Mchome walipokutana nao Wizarani jijini Dar es salam.

Waziri wa Katiba na Sheria Dkt Harrison Mwakyembe amesema Serikali inazisubiri Tume ya Uchaguzi nchini (NEC) na Tume ya Uchaguzi Zanziba (ZEC) zimalize majadiliano yao ili mchakato wa kuipigia kura ya maoni Katiba Inayopendekezwa ufanyike.

Mhe. Mwakyembe ametoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam alipokutana na uongozi wa Kikosi cha Kupambana na Haki za Mirathi (KIKUHAMI ) kilichoko chini ya Chama cha Wanawake katika Sheria na Maendeleo Afrika – WiLDAF.

Amesema zoezi hilo lingekuwa limeshakamilika ila Tume za Uchaguzi ziliona ni bora liahirishwe kwanza ili kupisha zoezi la Kikatiba lililokuwa likiikabili nchi la Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana likamilike na kwamba kukamilika kwa zoezi hilo kunatoa fursa kwa Serikali kuendelea na mpango wake wa kuendesha kura ya maoni juu ya Katiba Inayopendekezwa ili kupata Katiba Mpya ya Tanzania.

Aliongeza kuwa Katiba Inayopendekezwa ina vitu vingi sana ambavyo vitasaidia upatikanaji wa haki za wanawake na kuondoa uonevu dhidi yao na hivyo kufanikisha harakati ambazo wadau mbalimbali wa wanawake nchini wamekuwa wakizipigania na hivyo kukamilika wakati Katiba mpya itakapokuwa imepatikana.

Aidha Mhe. Waziri ameutaka uongozi huo wa KIKUHAMI kupitia WiLDAF kuwasilisha Wizarani mapendekezo yao juu ya mabadiliko ya sheria mbalimbali za Mirathi nchini wanazoziona zinawakandamiza wanawake ili ziweze kufanyiwa marekebisho na ziendane na wakati uliopo.

“si mnataka sheria mbalimbali za mirathi zibadilishwe?, leteni mapendekezo yenu , hili ni jukumu letu sote, sisi tupo na hapa wizarani tunao wataalamu watazipitia na kuona namna ya kuzifanyia kazi, ili ziendane na wakati uliopo sasa, alisema na kuongeza kuwa ndio maana amesema Katiba Inayopendekezwa ina vipengele vingi ambavyo vitasaidia kuondoa uonevu kwa wanawake nchini itakapopitishwa na wananchi kupitia kura ya maoni.”

KIKUHAMI chini ya Uongozi wa Bibi Thabita Siwale ulimuomba Waziiri wa Katiba na Sheria Dkt Mwakyembe kuangalia uwezekano wa kuondoa sheria zinazowakandamiza wanawake hasa zile za mirathi kwani zinawafanya wanawake hasa wajane kunyanyasika katika nchi yao.
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live




Latest Images