Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46202 articles
Browse latest View live

NAIBU WAZIRI MALIASILI NA UTALII, ENG. RAMO MAKANI ATAKA JAMII ZINAZOZUNGUKA MAENEO YA HIFADHI NCHINI ZISHIRIKISHWE KULINDA MALIASILI ZA TAIFA

0
0
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani (wa kwanza kulia) akizungumza na Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo, Massana Mwishawa (wa pili kulia) alipotembelea hifadhi hiyo tarehe 21 Julai, 2016 kwa ajili ya kujionea kero mbalimbali na kuzitafutia ufumbuzi. Kushoto aliyesimama na Mbunge wa Jimbo la Geita Vijijini, Joseph Kasheku maarufu kwa jina la Msukuma.
  Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo, Massana Mwishawa (wa pili kulia) akimuonesha Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani (wa kwanza kulia) sehemu ya fukwe za hifadhi hiyo ambazo ni makazi ya Mamba na Ndege wa aina mbali mbali alipotembelea hifadhi hiyo tarehe 21 Julai, 2016 kwa ajili ya kujionea kero mbalimbali na kuzitafutia ufumbuzi. Kushoto aliyesimama na Mbunge wa Jimbo la Geita Vijijini, Joseph Kasheku maarufu kwa jina la Msukuma. 
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani (wa pili kulia) akiteta jambo na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mwl. Herman Kapufi (kulia) katika fukwe ya Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo alipotembelea hifadhi hiyo tarehe 21 Julai, 2016 kwa ajili ya kujionea kero mbalimbali na kuzitafutia ufumbuzi. Kushoto anaesaini kitabu cha wageni ni Mbunge wa Jimbo la Geita Vijijini, Joseph Kasheku maarufu kwa jina la Msukuma. 
Picha ya pamoja kati ya Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani (katikati waliokaa), Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mwl. Herman Kapufi (wa tatu kushoto waliokaa), Mbunge wa Jimbo la Geita Vijijini, Joseph Kasheku maarufu kwa jina la Msukuma (wa tatu kulia waliokaa), Kaimu Mkurugenzi Mkuu TANAPA, Ibrahim Mussa (wa pili kushoto waliokaa) na baadhi ya Watumishi wa Hifadhi ya Taifa Kisiwa cha Rubondo hifadhini hapo tarehe 21 Julai, 2016
Mamba katika Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo.

 Moja ya Fukwe katika Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo.
 Huduma za malazi katika Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo.
Huduma bora ya vyumba inapatikana katika Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo.
Huduma za usafiri wa boti zinapatikana katika Hifadhi ya Taifa ya Rubondo.

NA HAMZA TEMBA - WIZARA YA MALIASILI NA UTALII 
____________________________________________________________

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani ameitaka Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kuzishirikisha jamii zinazozunguka maeneo ya hifadhi hapa nchini kutambua umuhimu wa kuhifadhi maeneo hayo ili kutoa ulinzi shirikishi katika kupambana na Ujangili.


Eng. Makani amesema hayo jana wakati akizungumza na viongozi pamoja na watumishi wa Mamlaka hiyo akiwa ziarani Mkoani Geita katika Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo.


“Wananchi waoishi jirani na maeneo haya ya hifadhi ni muhimu wakaelimishwa juu ya faida za uhifadhi kiikolojia na kiuchumi kwenye maisha yao ambapo itawapa msukumo wa kuyatunza na kuyalinda” Alisema Eng. Makani.


Aliongeza kuwa vita dhidi ya Ujangili hapa nchini haiwezi kufanikiwa kirahisi iwapo jamii inayozunguka maeneo ya Hifadhi haitatoa ushirikiano kwa Serikali katika kulinda na kuhifadhi Maliasili zilizopo.


“Pamoja na mbinu nyingine, washirikisheni wananchi watusaidie kupambana na ujangili ili fedha ambayo ingetumiwa na Serikali kwa kazi hiyo itumike kuendeleza hifadhi zetu pamoja na kutoa huduma nyingine za kijamii” Alisema Eng. Makani.


Akizungumzia faida za uhifadhi kiuchumi hapa nchini alisema kuwa, Sekta ya utalii ndio sekta pekee inayoongoza kwa kuliingizia taifa mapato mengi ya nje (foreign currency) ambayo ni asilimia 25 ya mapato yote. Sekta hiyo pia inachangia pato la taifa kwa asilimia 17.2.


Eng. Makani aliongeza kuwa “Serikali ya awamu ya tano ina mpango wa kuboresha sekta ya utalii ili iweze kuiingizia zaidi mapato, katika kufanikisha hilo tumeweka mkakati wa kuboresha ofisi zetu za utalii za Kanda ili ziweze kutangaza na kukuza zaidi utalii wa ndani”.


Kwa upande wa hoteli zinazotoa huduma ya kitalii hapa nchini alisema kuwa ifikapo mwezi Septemba mwaka huu, Serikali itaanza rasmi zoezi la kuorodhesha hoteli zote zinazotoa huduma hiyo na kuzipanga kwenye makundi ya ubora ambapo zile zitakazoonekana hazina hadhi kabisa zitaondolewa katika mtandao wa kutoa huduma hiyo. Alisema zoezi hilo litaboresha huduma za kitalii nchini na kusaidia watalii kufikia hoteli wanazozihitaji na kupata huduma stahiki .


Katika kushirikisha sekta binafsi kwenye kukuza utalii nchini, amewaomba watoa huduma za ndege kuangalia upya viwango vya gharama zao za usafiri ili wananchi wengi zaidi waweze kumudu na kunufaika na huduma hiyo.


Wakati huo huo aliwaasa watumishi wa Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo kufanya kazi kwa bidii, kuwa na maadili mema na uadilifu kazini. Aliwataka pia kuwa mstari wa mbele kupiga vita ujangili, kuboresha ukusanyaji wa mapato na kushirikisha wananchi kwenye uhifadhi.


Hapo awali akiwasilisha taarifa ya hifadhi hiyo kwa Naibu Waziri wa Maliasili, Eng. Ramo Makani, Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo, Massana Mwishawa alisema kuwa changamoto kubwa inayoikabili hifadhi hiyo ni ujangili na upatikanaji mdogo wa mapato ambao hauwiani na mahitaji ya hifadhi hiyo.


Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Geita Vijijini, Joseph Luiza Kasheku maarufu kama Msukuma, alimuomba Naibu Waziri huyo wa Maliasili kuboresha Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo ambayo ipo Jimboni kwake iweze kupata mapato ya kutosha na kujiendesha yenyewe. Hifadhi hiyo kwa sasa inategemea mapato kutoka kwenye hifadhi nyingine kujiendesha.


Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo iliyopo Mkoani Geita ni moja ya sehemu pekee na muhimu katika uzalishaji wa mazalia ya samaki katika ziwa Victoria. Sehemu nyingine ni Hifadhi ya Kisiwa cha Saanane iliyopo Mkoani Mwanza. Hifadhi hizi zina umuhimu mkubwa katika upatikanaji wa samaki katika Ziwa Victoria.

Ziara ya Rais wa Benki ya Exim kwenye kituo cha kuhifadhia kumbukumbu.

0
0

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (wa kwanza kulia) akizungumza kumshukuru Rais wa Benki ya Exim ya nchini China Bw, Liu Lian’ge (hayupo pichani) mara baada ya kukagua kituo mahiri cha kutunza kumbukumbu (Internet Data centre) kilichopo eneo la kijitonyama Dsm.


Rais wa Benki ya Exim ya nchini China Bw, Liu Lian’ge (wa kwanza kushoto) akizungumza mara baada ya kukagua kituo mahiri cha kuhifadhia kumbukumbu ambacho kilijengwa kwa ufadhili wa Benki ya Exim ya nchini china.
Rais wa Banki ya Exim ya nchini China Bw, Liu Lian’ge (wa pili kutoka kulia) akizungumza na Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (wa kwanza kulia) wakati wakikagua kituo mahiri cha kuhifadhi kumbukumbu (Internet Data centre) kilichopo eneo la kijitonyama Dsm.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (wa kwanza kushoto) akishuka ngazi wakati wa kukagua kituo mahiri cha kutunzia kumbukumbu (Internet Data centre) kilichopo eneo la kijitonyama, (wa kwanza kulia) ni Rais wa Benki ya Exim ya nchini China Bw. Liu Lian’ge.

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AFANYA MAZUNGUMZO NA WAJUMBE WANAWAKE WA HALMASHAURI KUU YA CCM TAIFA

0
0

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ambapo aliwaambia umoja na mshikamano ni nguzo muhimu kwa wanawake .Aliwataka kutumia fursa zinazopatikana mjini na kujiunga na Majukwaa ya Wanawake.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kutoka Wilaya ya Uvinza ,Asha Baraka akichangia jambo wakati wa Mazungumzo na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
Sehemu ya Wajumbe wakifuatilia mazungumzo baina yao na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Samia Suluhu Hassan.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

KIKWETE AONGOZA KIKAO CHA HALMASHAURI KUU YA TAIFA YA CCM MJINI DODODMA LEO

0
0
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete akifungua Mkutano wa Halmashauri Kuu ya taifa ya CCM mjini Dodoma Julai 21, 2016. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mtarajiwa, Rais John Pombe Magufuli na Wapili kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM, Zanzibar, Rais wa Zanzibar Dkt, Ali Mohamed Shein . Kulia ni Makamu Mwenye kiti wa CCM, Bara, Philip Mangula na wapili kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.
  Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete akisisitiza jambo mbele ya Wajumbe wa Mutano wa Halmashauri Kuu ya taifa ya CCM mjini Dodoma Julai 21, 2016.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimkaribisha  Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete kufungua Mkutano wa Halmashauri Kuu ya taifa ya CCM mjini Dodomam leo Julai 21, 2016. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mtarajiwa, Rais John Pombe Magufuli na Wapili kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM, Zanzibar, Rais wa Zanzibar Dkt, Ali Mohamed Shein . Kulia ni Makamu Mwenye kiti wa CCM, Bara, Philip Mangula . 
 Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Makamu wa Rais, Samia Suluhu na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakiimba  wimbo wa CCM katika kikao cha  Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM kilichofanyika mjini Dodoma Julai 21, 2016.
  Baadhi ya Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM wakiwakaribisha viongozi wa Meza Kuu,mara walipokuwa wakiingia ukumbini wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete 
 Baadhi ya Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM wakimsikiliza Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete wakati alipofungua mkutano wao mjini Dodoma Julai 21, 2016.
  Baadhi ya Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM wakimsikiliza Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete wakati alipofungua mkutano wao mjini Dodoma Julai 21, 2016.PICHA NA MICHUZI JR-DODOMA

DTK TULIA AONGOZA MBIO ZA TULIA MARATHON KM 5 MJINI DODOMA LEO

0
0
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt Tulia Ackson (wa nne kulia),akiongoza mbio za Tulia Marathon KM 5 akiwa sambamba na baadhi ya Wabunge mbalimbali vikiwemo na vikundi vya kuhamasisha mbio hizo zilizoanzia geti la Bunge na baadae kuishi katika viwanja vya Nyerere Skwea mjini Dodoma.Dkt Tulia na washiriki wa mbio hizo. Baada ya mbio hizo walikwenda kutoa msaada wa vitu mbalimbali katika kituo cha Watoto Yatima kiitwacho kijiji cha Matumaini kilichopo nje kidogo ya mji wa Dodoma.Wakati wa kutoa msaada huo Dkt Tulia alisema kuwa ni vvema kila Mkoa vikawa na vikundi mbalimbali kikiwemo cha Wazalendo wakafanya shughuli za Kijamii kusaidia makundi mbalimbali.PICHA NA MICHUZI JR-MMG DODOMA.
Dkt Tulia akishirikia na Wabunge na vikundi mbalimbali wakifurahia kumaliza mbio hizo za kuhamasisha jamii kusaidia watoto Yatima na waishio katika Mazingira Magumu.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt Tulia Ackson (wa tatu kulia),akiwa ameongoza na Wabunge mbalimbali vikiwemo na vikundi vya kuhamasisha mbio hizo zilizoanzia geti la Bunge na baadae kuishi katika viwanja vya Vya Nyerere Skwea mjini Dodoma.
Baadhi ya Wabunge wakishiriki mbio za Tulia Marathon KM 5 mapema leo,ambapo mbio hizo zilikomea katika viwanja vya Nyerere Skwea.

Vikundi mbalimbali vikiunga mkono mbio za Tulia Marathon KM 5 mapema leo asubuhi.
Baadhi ya vikundi mbalimbali vikisubiri kuanza mbio za Tulia Marathon KM 5 zikiwa ni sehemu ya kuhamasisha jamii kusaidia watoto Yatima na waishio katika Mazingira Magumu,ambapo baada ya mbio hizo walikwenda kutoa msaada wa vitu mbalimbali katika kituo cha Watoto Yatima kiitwacho kijiji cha Matumaini kilichopo nje kidogo ya mji wa Dodoma.Wakati wa kutoa msaada huo Dkt Tulia alisema kuwa ni vvema kila Mkoa vikawa na vikundi mbalimbali kikiwemo cha Wazalendo wakafanya shughuli za Kijamii kusaidia makundi mbalimbali.PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

WASIFU WA DKT. JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI

0
0
MGOMBEA NAFASI YA MWENYEKITI WA CCM

1.0.  MAISHA YAKE

Ndugu John Pombe Joseph Magufuli alizaliwa Oktoba 29, mwaka 1959 katika kijiji cha Chato, Wilayani Biharamulo katika Mkoa wa Kagera. Hivi sasa Chato ni Wilaya katika Mkoa wa Geita. Ndugu Magufuli ni Daktari wa Falsafa (PhD) ya Kemia. Ana mke  na watoto saba.  Alichaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwezi Oktoba, 2015 kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (C.C.M). Aliapishwa na kuanza rasmi majukumu yake ya kuiongoza Tanzania tarehe 5 Novemba, 2015.

Tangu ameingia madarakani, Rais Dkt. Magufuli, ameonesha kuwa ana sifa zote muhimu za uongozi. Ana dira, maono na malengo kuhusu anakotaka Taifa liende. Ana mikakati ya kutekeleza dira na maono yake. Haogopi kufanya maamuzi makini. Ana kiu ya kuona Taifa linapata maendeleo. Amejipambanua kuwa yeye ni mtetezi wa wanyonge na dhamira yake kubwa ni kuona wananchi wanapata huduma bora  za jamii na kero zao zinaondoka.

2.0.  ELIMU NA MAFUNZO

Rais Dkt. Magufuli alianza elimu ya msingi katika Shule ya msingi Chato mwaka 1967 na kumaliza mwaka 1974. Mwaka 1975 alianza masomo ya sekondari katika Shule ya Seminari ya Katoke Mkoani Kagera.  Mwaka 1977 alihamia shule ya sekondari ya Lake iliyopo Mkoani Mwanza  na kuhitimu kidato cha Nne mwaka 1978. Kuanzia mwaka 1979 hadi 1981 alifanya masomo ya kidato cha Tano na  Sita katika shule ya Sekondari ya Mkwawa Mkoa wa Iringa  .

Mwaka 1981 hadi 1982 alisoma Chuo cha Ualimu Mkwawa na kuhitimu Stashahada ya Ualimu ya Masomo ya Kemia na Hisabati.  Mwezi Julai hadi Disemba mwaka 1983, Dkt. Magufuli alipata mafunzo ya kijeshi  katika Jeshi la  kujenga Taifa kikosi cha Makutupora mkoa wa Dodoma. Mwezi Januari hadi Machi 1984 alihamishiwa kikosi cha mafunzo Jeshi la Kujenga Taifa Makuyuni, Arusha.  Mwezi huo wa Machi alihamia kikosi cha Jeshi la Kujenga Taifa Mpwapwa Dodoma na kumaliza mafunzo mwezi Juni 1984.

Mwaka 1985 alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es salaam kusoma Shahada ya kwanza ya Sayansi na Ualimu akijikita katika masomo ya Kemia na Hisabati. Alitunukiwa Shahada hiyo mwaka 1988.  Mwaka 1991 hadi 1994 alisoma na kutunukiwa Shahada ya Uzamili katika fani ya Kemia iliyotolewa na Chuo Kikuu cha Dar es salaam na Chuo Kikuu cha Salford cha Uingereza. Mwaka 2006 alijiunga na  Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa ajili ya Shahada ya Uzamivu katika Fani ya Kemia na kufanikiwa kuhitimu mwaka 2009.

3.0.  UZOEFU WA NDANI YA  SERIKALI

Baada ya kuhitimu masomo yake ya Stashahada ya Ualimu, mwaka 1982 hadi 1983 Dkt. Magufuli alikuwa Mwalimu katika shule ya Sekondari ya Sengerema iliyopo Mkoani Mwanza akifundisha masomo ya Kemia na Hisabati.  Mwaka 1989 alijiunga na Chama Cha Ushirika cha Nyanza Mkoani Mwanza, ambapo alifanya kazi kama Mkemia Mkuu  hadi mwaka  1995.

Mwaka 1995 alichaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Biharamulo Mashariki Mkoa wa Kagera.  Baada ya Uchaguzi, Rais wa Awamu ya Tatu, Mheshimiwa Benjamin William Mkapa alimteua kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi nafasi ambayo aliitumikia  hadi mwaka 2000.  Mwaka 2000 alichaguliwa kwa mara ya pili kuwa Mbunge wa Jimbo la Biharamulo Mashariki lakini mara hii akipita bila kupingwa.  Mwaka huo huo aliteuliwa kuwa Waziri kamili wa Wizara ya Ujenzi hadi mwaka 2005. 

Mwaka 2005 Rais Dkt. Magufuli alichaguliwa kwa mara ya tatu kuwa mbunge wa jimbo la Biharamulo Mashariki, kwa mara nyingine akipita bila kupingwa.   Baada ya uchaguzi, Rais wa Awamu ya Nne, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete alimteua kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuanzia mwaka 2005 hadi mwaka 2008 ambapo alihamishiwa Wizara ya   Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi hadi hadi mwaka 2010.

Mwaka 2010 Dkt. Magufuli alichaguliwa kwa mara ya nne  kuwa  Mbunge lakini, kufuatia mgawanyo wa majimbo uliofanyika, mara hii katika Jimbo jipya la Chato.  Baada ya uchaguzi, aliteuliwa kuwa Waziri wa Ujenzi kuanzia mwaka 2010 hadi mwaka 2015.

Wakati akiwa Mbunge na Waziri, Dkt. Magufuli amefanya shughuli na kushika nyadhifa kadhaa ndani na nje ya nchi. Mwaka 2014, Dkt. Magufuli alishiriki katika Bunge Maalum la Kutunga Katiba Mpya akiwa  ni Mjumbe wa Bunge hilo. Aidha, wakati akiwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi aliweza kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti Mwenza (Co-Chair) wa Mkutano wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Makazi (UN-Habitat).

Tarehe 25 Oktoba, 2015 Dkt. John Pombe Joseph Magufuli alichaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na tarehe 5 Novemba, 2015 aliapishwa kushika rasmi wadhifa huo.

4.0.  UZOEFU WA UONGOZI NDANI YA CHAMA

Rais Dkt. Magufuli alijiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) mwaka 1977. Amekuwa Mwanachama mwaminifu na ameshika nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya Chama. Nafasi alizowahi kushika ni pamoja na kuwa Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Wilaya, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya, Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Wilaya, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Mkoa, Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Mkoa na Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa. 

Sambamba na kushika nafasi mbalimbali za uongozi, Dkt. Magufuli mara zote alijitoa kukitetea Chama na kuhakikisha kinapata ushindi. Alishiriki kikamilifu kuwafanyia kampeni wagombea wa CCM katika Chaguzi Ndogo zilizofayika katika majimbo ya Busanda, Biharamulo Magharibi na Igunga na kupata ushindi.  Katika Mkutano Mkuu wa CCM wa tarehe 11 – 12 Novemba mwaka 2012, Dkt. Magufuli alikuwa miongoni mwa Mawaziri wachache waliopata fursa ya kuelezea mafanikio ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama ya Mwaka 2010 – 2015. Alielezea mafanikio ya utekelezaji wa Ilani, hususan katika sekta ya miundombinu.

Tarehe 11 mwezi Julai, 2015 Mkutano Mkuu wa Taifa wa CCM ulimchagua na kumteua Dkt. Magufuli kuwa mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.  Aliinadi vyema Ilani ya uchaguzi ya CCM (2015) na kukiwezesha Chama kupata ushindi mkubwa. Tarehe 25 Oktoba, 2015 alichaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.  Nafasi hiyo imemwezesha kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa.

5.0.  UFANISI KATIKA UONGOZI

Dkt. Magufuli ni kiongozi mnyenyekevu, aliye na hofu ya Mungu, mkweli, mtekelezaji wa ahadi, mwadilifu, shupavu, mahiri, mbunifu, mtafiti, mchapakazi na mtetezi wa wanyonge. Ni kiongozi mpenda haki na mchukia dhuluma, rushwa, ufisadi na ubaguzi wa aina yoyote ile.  Ni kiongozi mwenye msimamo na mtetezi wa yale anayoyaamini. 

Katika nyadhifa zote alizopata kutumikia alifanya kazi kwa uadilifu na umahiri mkubwa. Amejidhihirisha na kujipambanua kuwa ni mfuatiliaji na msimamizi wa sheria. Akiwa Mwalimu Sengerema Sekondari aliwezesha wanafunzi wote wa darasa lake kufaulu masomo ya Hesabu na Kemia aliyokuwa akiyafundisha. Akiwa Mkemia Mkuu wa Chama cha Ushirika cha Nyanza alisimamia vyema ubora wa uzalishaji wa mafuta ya Pamba na kuifanya Kampuni ya Nyanza kuwa mzalishaji mzuri wa mafuta ya Pamba. 

Akiwa Waziri wa Ujenzi anakumbukwa kwa kubuni na kusanifu miradi ya ujenzi wa barabara, kusimamia vizuri matumizi ya fedha na kuhakikisha miradi hiyo inatekelezwa kwa viwango na kwa wakati uliopangwa. Uwezo wake katika kubuni na kusanifu miradi ya barabara uliigwa na nchi majirani, ikiwemo Kenya. Ameondoka Wizara ya Ujenzi akiwa amesimamia ujenzi wa zaidi ya Kilometa 17,000 za barabara za lami, madaraja makubwa zaidi ya 14 na madaraja madogo madogo zaidi ya 7,000 na vivuko. Aidha, alisimamia vizuri taasisi mbalimbali za Makandarasi, Wahandisi, Wabunifu na Wakadiriaji Majengo.

Dkt. Magufuli pia anasifika kwa uwezo wake mkubwa wa kuweka kumbukumbu ya kazi zake.  Akiwa Wizara ya Ujenzi aliweza kutaja majina ya barabara zilizojengwa au zilizokuwa katika hatua za ujenzi, urefu wake, majina ya wakandarasi pamoja na gharama za ujenzi bila kusoma mahali popote.  Wakati wa Rais Mstaafu Benjamini William Mkapa alimwita “Askari wa Mwavuli”.  

Akiwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi alisimamia upimaji wa ardhi za vijiji na viwanja vya makazi, na kushughulikia migogoro mingi ya ardhi iliyowahusu wananchi wa maisha ya chini. Wakati  akiwa Waziri wa Wizara ya Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi alikuwa maarufu wa kutambua na kutaja idadi ya mifugo,  kama vile samaki,  ngómbe, mbuzi, kondoo, kuku, mbwa n.k. Kitendo cha kukamata meli ya kichina iliyokuwa ikivua samaki kwa wizi ndani ya Bahari Kuu ya Hindi eneo la Tanzania kilidhihirisha uzalendo kwa Taifa lake.  Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Kikwete alimpachika jina maarufu la “Tingatinga”. 

Sifa hizi nzuri ameendelea nazo hata baada ya kuchaguliwa kuwa Rais. Katika miezi michache ya uongozi wake amethibitisha anatekeleza ahadi. Aliahidi kutoa elimu bila malipo na kuanzisha Mahakama ya Mafisadi. Ameweza kusimamia nidhamu kwenye utumishi wa umma kwa kuondoa watumishi hewa na kuchukua hatua dhidi ya watumishi wa umma wasio waaminifu, wala rushwa, wazembe na wanaoshindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo. Ameweza kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za umma na kuongeza ukusanyaji wa mapato ya Serikali. Kwa hakika Dkt. Magufuli anaakisi uongozi bora unaopaswa kuigwa na viongozi wengi Barani Afrika na Dunia.

6.0. DHIMA YA UONGOZI WA SERIKALI YA AWAMU YA TANO 2015 – 2020) NA MALENGO YAKE MAHSUSI

Ilani ya uchaguzi ya CCM  ya Mwaka 2015 – 2020 inazielekeza serikali zake kutumia nguvu zake zote kuendelea kupambana na changamoto kubwa nne;- Kwanza kuondoa umaskini, Pili, kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira hasa kwa vijana, Tatu, kuendeleza vita dhidi ya adui rushwa na ubadhirifu wa mali ya umma, na Nne, kuendelea kudumisha amani, ulinzi na usalama wa maisha ya Watanzania na mali zao.

Sambamba na kutekeleza mambo hayo makubwa manne, kipindi cha Kampeni na wakati akizindua Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 20 Novemba, 2015 Rais Dkt. Magufuli alitaja malengo mahsusi ya Serikali ya Awamu ya Tano. Malengo hayo ni haya yafuatayo:

·    Kudumisha Muungano, Amani na Umoja wa Tanzania. Serikali haitamwonea aibu mtu mwenye nia ya kuvunja Muungano na kuvuruga amani na mshikamano katika nchi. Hili alilidhihirisha vizuri wakati wa uchaguzi wa marudio huko Zanzibar, kwani Uchaguzi ulifanyika kwa amani na utulivu.

·    Kujenga Uchumi wa Viwanda ili kufikia azma ya kuwa nchi ya  uchumi wa kati kulingana na malengo ya Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025.  Viwanda vinalengwa ni vyenye kutumia nguvu kazi kubwa, malighafi za ndani ya nchi, kuzalisha bidhaa kwa ajili ya soko la ndani na nje ya nchi. Nia ni kukabiliana na tatizo la ajira na umasikini;

·     Kuongeza kasi ya ujenzi wa miundombinu ya kiuchumi, hususan miundombinu ya usafiri na nishati;

·     Kuimarisha huduma za jamii, hususan elimu, Afya na Maji. Lengo ni kuhakikisha huduma hizo zinapatakana sio tu kwa urahisi bali pia kwa ubora unaostahili ili kukabiliana na maadui ujinga, umaskini na maradhi;

·     Kusimamia uwajibikaji wa utumishi wa umma na kuondoa urasimu ndani ya Serikali. Lengo ni kuhakikisha watumishi wa umma wanafanya kazi kwa ueledi, uadilifu na kujituma ili kuwawezesha wananchi kupata huduma kwa wakati;

·      Kuimarisha usimamizi wa rasilimali za nchi, ikiwemo kuhifadhi mazingira na kuzidisha vita dhidi ya ujangili. Lengo ni kuhakikisha rasilimali za nchi zinawanufaisha watu wote wa kizazi cha sasa na kijacho. Aidha, ukusanyaji wa mapato ya Serikali na udhibiti wa matumizi ya Serikali nao utaimarishwa;

·      Kusimamia utawala bora unaozingatia sheria na haki za binadamu. Jitihada za makusudi zitaelekezwa katika kuzidisha mapambano dhidi ya rushwa, ufisadi, dhuluma na uonevu wa aina yoyote. Aidha, maslahi ya makundi mbalimbali katika jamii, ikiwemo wanawake, wazee, watu wenye ulemavu na watoto yatalindwa. Kwa upande mwingine, wananchi watahimizwa kuheshimu na kufuata sheria za nchi;

·       Kulinda usalama wa raia na mali zao kwa kupambana na uhalifu, ikiwemo wizi, ujambazi, tatizo la dawa za kulevya n.k.

·       Kudumisha na kuendeleza ujirani mwema, mahusiano mema na Mataifa mengine duniani pamoja na Mashirika ya Kimataifa na Kikanda;

·       Kuendeleza na kusimamia vizuri shughuli za michezo, sanaa, burudani na utamaduni, ikiwemo kukuza lugha ya Kiswahili.

HITIMISHO
Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Dkt. John Pombe Joseph Magufuli imedhamiria kuongeza kasi ya ukuaji wa maendeleo ya kiuchumi na kuwataka watanzania  washiriki kufanya kazi kwa bidii na maarifa  ndani ya falsafa ya HAPA KAZI TU. Dhamira hii inakusudia kuwezesha Taifa letu kufikia Uchumi wa Kati uaoongozwa na Viwanda ili kutimiza malengo ya Dira ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2025.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI ALIPOTEMBELEA CHUO CHA USAFIRISHAJI

0
0

 Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani akitoa maelekezo kwa  Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Prof. Zacharia Mganilwa kuhusu namna nzuri ya kukiwezesha Chuo hicho kujiendesha kwa faida na kuboresha miundombinu yake.
 Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Prof. Zacharia Mganilwa akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani alipotembelea Chuo hicho kukagua miundombinu yake.
 Mkuu wa Kitengo cha Uhandisi wa anga katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji NIT Eng. Azizi Mdimi akimuonesha Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani injini ya ndege inayotumia kwa mafunzo wakati alipokagua Hanga katika chuo hicho.
 Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani akikagua ndege inayotumiwa kufundishia wanafunzi wanaosomea utengenezaji wa ndege na urubani alipotembelea Chuo cha Usafirishaji NIT.
 Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Prof. Zacharia Mganilwa akimuonesha  Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani moja ya kitabu kinachotumiwa kufundishia marubani na wahandisi wa ndege alipotembelea maktaba ya chuo hicho.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani akikagua mtambo unaopima magari ili kujua ubora wake kabla ya kuanza kutumika hapa nchini alipotembelea Chuo cha Taifa cha Usafirishaji NIT. (Picha na Benjamin Sawe-Maelezo)

TBL YAZINDUA BIA MPYA YA NDOVU RED MALT JIJINI DAR ES SALAAM

0
0
 Mkurugenzi wa Masoko TBL, Kushila Thomas (wa kwanza kushoto) akijadiliana jambo na Meneja wa Bia ya Ndovu Red Malt, Nicolas John (katikati) pamoja na mgeni mwaliko aliyefika katika uzinduzi wa bia ya Ndovu Red Malt uliofanyika mgahawa wa 305 The Boks uliopo Kinondoni jijini Dar e Salaam.  Meneja wa Bia ya Ndovu Red Malt, Nicolas John (wa kwanza kushoto) akifuatiwa na Mkurugenzi wa Masoko TBL Kushila Thomas pamoja na Meneja Masoko wa vinywaji wa kampuni ya TBL Vimal Vaghmaria (wa kwanza kulia) wakionyesha kinywaji cha Ndovu Red Malt mara baada ya kuzindua kinywaji hicho jana katika mgahawa wa 305 The Boks uliopo Kinondoni jijini Dar e Salaam ambapo wateja zaidi ya 50 walihudhuria katika hafla ya uzinduzi wake. Picha zote na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.  Meneja wa Bia ya Ndovu Red Malt, Nicolas John akiongea wakati wa Uzinduzi wa bia ya Ndovu Red Malt uliofanyika jana katika mgahawa wa 305 The Boks uliopo Kinondoni jijini Dar e Salaam ambapo wateja zaidi ya 50 walihudhuria katika hafla ya uzinduzi wake.  Meneja Masoko wa vinywaji wa kampuni ya TBL Vimal Vaghmaria amesema: “Ubunifu wa kila bidhaa yetu unalenga kukidhi matakwa ya watumiaji wake ambao ni wateja wetu ambao wanahitaji kutumia bia zilizo bora na zinazokwenda na wakati katika soko”. 
 Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya, Damian Soul akitoa burudani katika uzinduzi wa bia ya Ndovu Red Malt uliofanyika jana katika mgahawa wa 305 The Boks uliopo Kinondoni jijini Dar e Salaam.   Wageni waalikwa wakijipatia bia ya Ndovu Red Malt.  Wageni waaalikwa wakibadilisha nawazo huku wakijipatia kinywaji cha Ndovu Red Malt.  Wageni waliohudhuria uzinduzi wa bia ya Ndovu Red Malt uliofanyika mgahawa wa 305 The Boks uliopo Kinondoni jijini Dar e Salaam.  Kinywaji cha Ndovu Red Malt.  Meneja wa Bia ya Ndovu Red Malt, Nicolas John(kushoto) akiwa na Msanii wa Kuchora Picha Bwana Lute (katikati) wakionyesha furaha yao mara baada ya uzinduzi wa bia hiyo.  Maua yaliyohudumia tukio hilo.
 Katika mkakati wake wa kuendelea kuwaletea wateja wake bidhaa zenye bora wa hali ya juu, kampuni ya Tanzania Breweries Limited (TBL) imezindua bia mpya inayojulikana kama Ndovu Red Malt, bia ambayo imetengenezwa kwa kimea kwa asilimia 100 na ikiwa ni mwendelezo wa ubunifu wenye ubora wa bia ya Ndovu Special Malt inayoongoza kwa ubora na bia pendwa kwa watumiaji wengi wa bia nchini. 

 Bia ya Ndovu Red Malt imegundulika na kutengenezwa hapa nchini Tanzania ili kukidhi ladha ya wanywaji wa bia ikiwa na ubora wa kiwango cha juu na yenye ladha ya pekee kwa kulinganisha na aina nyinginezo za bia zilizopo kwenye soko. Uzinduzi wa bia ya Ndovu Red Malt umefanyika katika mgahawa wa 305 The Boks uliopo Kinondoni jijini Dar e Salaam Julai 20 mwaka huu ambapo wateja zaidi ya 50 walihudhuria katika hafla ya uzinduzi wake. 

 Mbali na kuwa na ladha ya aina yake inayoleta burudani kwa watumiaji wake kutokana na kutengenezwa kwa Shahiri kwa asilimia kubwa pia bia ya Ndovu Red Malt inavutia kwa mwonekano wake wa rangi kuwa na rangi ya uwekundu kwa mbali. Meneja Masoko wa vinywaji wa kampuni ya TBL Vimal Vaghmaria amesema: “Ubunifu wa kila bidhaa yetu unalenga kukidhi matakwa ya watumiaji wake ambao ni wateja wetu ambao wanahitaji kutumia bia zilizo bora na zinazokwenda na wakati katika soko”. 

 Alisema utengenezwaji wa bia ya Ndovu Red Malt kwa kutumia Shahiri kwa asilimia asilimia100 kunaleta upekee wa bia hii kwa kulinganisha na bia zingine kwenye soko na ina ladha tamu na mwonekano wake wa kuvutia ambao unaiongezea thamani. Kwa upande wake, Mpishi Mkuu wa Bia wa Kiwanda cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Cavin Nkya, alisema kuwa bia hii mpya ya Ndovu Red Malt inazinduliwa ikiwa ni uthibitisho wa uwezo wa kampuni katika kuwapatia watanzania kinywaji chenye kiwango cha kimataifa na chenye ubora wa hali ya juu.

 “Ndovu Red Malt ni bia ya daraja la kwanza inayodhihirisha dhamira yetu ya kuwapatia wateja kinywaji ambacho daima wametamani kukipata kikiwa kimesheheni radha murua nay a kipekee,” alisema Nkya. Nkya alimalizia kwa kusema kwamba matokeo mazuri katika utayarishaji kinywaji hiki ni kutokana na uchanganyaji mahiri na wa umakini wa nafaka bora zinazozalisha hapa nchini ambazo zinazotumika kutengeneza bia Ndovu Red Malt. 

 Bia hii ina kiasi cha kilevi cha asilimia asilimia 4 na inapatikana katika chupa zenye muundo maridhawa zenye ujazo wa mililita 375 ,kama zilivyo aina nyingi za bia zinazozalishwa na kampuni ya TBL zilizopo sokoni. Sasa, bia ya Ndovu Red Malt itaanza kupatikana sehemu zote nchini ambako kampuni inasambaza bidhaa zake kuanzia wiki hii kwa gharama ya shilingi 2,000/ kwa bei ya reja reja.

UTIAJI SAINI MAKUBALIANO YA AWALI YA UJENZI WA RELI YA KATI (STANDARD GAUGE)

0
0
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servaciaus Likwelile akitiliana saini na Naibu Meneja Mikopo Nafuu wa Benki ya Exim ya China Bw. Zhu Ying kuhusu makubaliano ya awali ya ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kisasa (Standard Gauge), jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servaciaus Likwelile akibadilishana hati ya makubaliano na Naibu Meneja Mikopo Nafuu wa Benki ya Exim ya China Bw. Zhu Ying mara baada ya kusaini makubaliano ya awali ya ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kisasa (Standard Gauge), jijini Dar es Salaam.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo imetiliana saini na Benki ya Exim ya China makubaliano ya awali ya ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kisasa (Standard Gauge).

Makubaliano hayo ya awali yamefanywa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servaciaus Likwelile kwa niaba ya Tanzania na Naibu Meneja Mikopo Nafuu wa Benki ya Exim ya China Bw. Zhu Ying.

Akizungumza katika hafla hiyo ya utiliaji saini Dkt. Likwelile amesema hatua hiyo inawezesha hatua za upembuzi yakinifu, usanifu na uundwaji wa timu za pamoja kuanza kuanisha mahitaji halisi ya ujenzi wa mradi huo.

Zaidi ya Shilingi Trilioni 16 za Tanzania zinatarajiwa kutumika katika ujenzi wa mradi wa reli ya kati yenye urefu wa Kilometa 2,190 ambapo Benki hiyo itashirikiana na Serikali ya Tanzania katika ujenzi wake.

Mradi wa ujenzi wa reli ya kati utahusisha ujenzi wa reli kwa kiwango cha kisasa kutoka Dar es Salaam-Tabora-Isaka-Mwanza na Tabora-Mpanda-Kalemela-Uvinza-Kigoma-Isaka-Keza hadi Msongati.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

EALA EULOGISES HON HAFSA MOSSI AT SPECIAL SITTING.

0
0
East African Legislative Assembly
 The Speaker, Rt Hon Daniel F. Kidega communicates to the Assembly at the start of the Special Sitting. In the foreground is Clerk, Kenneth Madete (left) and Senior Clerk Assistant, Stephen Mugume.
 Hon Peter Mathuki, the mover of the Resolution condemning the killing of the late Hon Hafsa Mossi
 A bird’s eye view of the Assembly at the Special Sitting yesterday
 Hon Dora Byamukama pays tribute to the late Hon Hafsa Mossi
 A section of Members at the tree-planting ceremony in honour of the late Hon Hafsa Mossi.

…Condemns killing, asks for speedy investigations
East African Legislative Assembly, Arusha, Tanzania: July 22, 2016: It was an emotional send-off for the late Hon Hafsa Mossi at a one-day Special Sitting held in Arusha yesterday with EALA legislators condemning in the strongest terms possible, the despicable, brutal and dastardly murder.   With that, the Assembly underscored the need for instituting independent investigations by credible organization(s) to unearth the killers of the late Hon Mossi, while remaining resolute that peace, security and stability should be immediately restored in Burundi.

The Resolution which condemned the killing of the fallen legislator while paying special tribute to her, was moved by the Chair of the Committee on Legal Rules Privileges, Hon Peter Mathuki, seconded by Hon Dora Byamukama and supported by the entire House.

In the foregoing, the Assembly urged the Summit of EAC Heads of State to ensure the on-going mediation deliberations are taken seriously by all parties.

“The Assembly calls upon the Summit of the East African Community Heads of State to reign in their powers and authority and take such stern measures as to ensure that both sides in Burundi take the ongoing mediation efforts seriously so that peace, security and stability are restored in the said country in shortest time possible”, a section of the Resolution read.

The House was unanimous that the use of political assassinations or murder as a tool to settle political differences was not only myopic, cowardly and despicable but that it had no place in the political dispensation of the modern world of democracy, freedom of expression and association.

In the regard, EALA underscored the need for the Government of Burundi to put in place security measures that ensure safety of lives and property of all people irrespective of their political leanings.

The Resolution notes with deep concern that a spate of targeted murders of political leaders and politically active citizens have been realized on both sides of the political divide since the country plunged into a political crisis resultant from the controversial Presidential elections held in July 2015.

The Resolution further calls upon the EAC Secretariat to monitor, assess and report to this Assembly at its next Plenary Sitting in August, on the safety and security situation in Burundi.

Hon Hafsa Mossi was gunned down by unknown assailants a week ago in Bujumbura, Burundi.  She is survived by three daughters, Nahimana Astona, Nahimana Dada and Semanyenzi Ummu-Aiman.

Hon Mossi was elected as a Member of EALA in 2012. At time of death, the late Hafsa Mossi was the Chapter Chair of Members of Burundi and Chairperson of the Assembly’s Women’s caucus.Prior to her election, the late Hafsa Mossi, then Minister for EAC Affairs in the Republic of Burundi since 2010, had played a critical role in Burundi’s integration into the EAC.

The late Mossi joined Government in 2007 then as Minister for Information, Communication, Relations with Parliament and Government Spokesperson.  She was also a politician and a Member of the CNDD-FDD party in Burundi.

She is a former journalist and national correspondent broadcasting for the British Broadcasting Corporation Swahili Service, having had stints in Bujumbura and in London.

During debate, the entire House eulogized Hon Mossi as a peace maker and said her death was a big blow to Burundi, the Assembly and the EAC in totality.

The Minister for EAC, Burundi, Hon Leontine Nzeyimana assured the House the Government of Burundi was investigating the matter and appealed to the Assembly not to isolate the country.

The Speaker of EALA called for the meeting in accordance with Rule 10 (2) of the Rules of Procedure of the House.

WATUHUMIWA 1,065 WAKAMATWA KATIKA OPERESHENI JIJINI DAR ES SALAAM.

0
0
 Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limefanikiwa kukamata watuhumiwa 1,065 kwa makosa mbalimbali yakiwemo makosa ya unyang’anyi kwa kutumia nguvu.

Watuhumiwa hao  ni wapiga debe katika sehemu mbalimbali za vituo vya daladala, watengenezaji pombe haramu ya Gongo waliokamatwa na lita 952 ikiwemo na mitambo mitatu ya kutengezea pombe hiyo, Kikosi cha mbwa mwitu 10, wauzaji na wavutaji bhangi puli 277, Kete 210, misokoto 144, pamoja na  wacheza kamari.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Polisi Kanda Maalum, Simon Sirro amesema kuwa watuhumiwa 1,065 walikamatwa katika operesheni inayofanywa na jeshi hilo.

Amesema katika operesheni Julai  21 wameweza kufanikiwa kupata silaha aina ya gobore yenye namba za usajili HD 201-2014 kutoka kwa watuhumiwa wanaotumia silaha katika matukio ya uhalifu iliyotelekezwa na watu wasiofahamika baada ya raia wema kuhisi kuna mtu anamiliki silaha na msako ukaendelea.

 Aidha amesema mnamo Juni 16 hadi 19  Polisi wamemkamata lita 952 za Gongo katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam kati ya lita hizo 420 zilikamatwa katika maeneo ya Kinzudi Wazo Hill kutoka kwa watu sita, mitambo mitatu ya kutengeneza pombe haramu ya Gongo pamoja na kukamata sukari kilo 100.

 Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro akionesha  waandishi wa habari  vitu mbalimbali leo jijini Dar es Salaam

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro akionesha simu zilizoibwa na majambazi mbalimbali jijini Dar es Salaam waandishi wa habari.
 
 Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro  akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam, juu ya  operesheni walioifanya na kufanikiwa kukamata watuhumiwa sugu 1,065 wa makossa mbalimbali  jijini Dar es Salaam.
(Picha na Emmanuel Massa,Globu ya jamii).

JESHI LA POLISI MKOA WA DAR ES SALAAM LAINGIZA SH.MILIONI 198 KATIKA ZOEZI LA KUHAKIKI SILAHA 14107

0
0
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna, Simon Sirro, akisisitiza jambo wakati akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Ofisini kwake Dar es Salaam leo mchana alipokuwa akitoa taarifa ya matukio mbalimbali ya uhalifu pamoja na mchakato wa uhakiki wa silaha.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna, Simon Sirro, akiwaonesha waandishi wa habari bunduki aina ya gobore walioikamata kabla ya kutumika kwa ujambazi wakati akitoa taarifa ya matukio mbalimbali ya uharifu pamoja na mchakato wa uhakiki wa silaha mkoani humo leo mchana.
Kamanda Sirro akionesha simu walizokutwa nazo watu wanaodaiwa vinara wa kupora simu kwa kutumia pikipiki katika maeneo mbalimbali ya jijini.

Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakichukua taarifa hiyo.


Na Dotto Mwaibale

JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limefanikiwa

kuliingia mapato taifa ya sh.milioni 198 kutokana na zoezi la uhakiki wa silaha lililofanyika mapema mwaka huu.

Jeshi hilo limefanikiwa kuhakiki jumla ya silaha 14,107 kwa kipindi cha kuanzia Machi Mosi hadi Juni 30 mwaka huu, vile vile Jeshi hilo limefanikiwa kuwakamata jumla ya watuhumiwa sugu 1,065.

Hayo yameelezwa leo na Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Simon Sirro wakati akitoa taarifa za matukio mbalimbali ya uhalifu pamoja na zoezi la kuhakiki wa silaha hizo.Alisema zoezi la uhakiki wa silaha lilihusisha mikoa ya kipolisi ya Temeke, Ilala na Kinondoni."Idadi ya watu waliojitokeza kuhakiki silaha kwa mikoa yote ni 11,602, na silaha zilizohakikiwa ni pistol 5,073, shotgun 4,707 na rifle 2,974," alisema.

Kamishna Sirro alisema dosari ndogo ndogo zilizojitokeza katika zoezi hilo ni kama vile wamiliki wa silaha kuwa na umri mkubwa zaidi ya miaka 70, na wengine kumili silaha za marehemu kinyume na taratibu."Hawa kwa kweli hatukuwaruhusu waendelee kumiliki hizo silaha, hivyo tulibaki nazo na wale walioshindwa kuzilipia silaha zao kwa muda mrefu pia tulibaki nazo," alisema.

Kamishna Sirro alisema kutokana na sababu hizo jumla ya silaha 66 walibaki nazo (kusalimishwa), ikiwa ni shotgun 36, rifle 10 na pistol 20.Katika operesheni maalumu iliyowezesha kukumata watuhumiwa sugu 1,065, Kamishna Sirro alisema watuhumiwa hawo walikatwa kwa makosa mbali mbali yakiwemo ya makosa ya unyang'anyi wa kutumia nguvu.

"katika hawa tumefakiwa kuwakamata watengenezaji wa pombe haramu ya gongo wakiwa na lita 952 pamoja na mitambo mitatu, vile vile kuna wavutaji wa bangi na puli zao 277."Matukio mengine ni pamoja na kukamatwa kwa kete 210, misokoto 144, pamoja na wacheza kamari," alisema.

Katika hatua nyingine Jeshi hilo limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa watatu kwa makosa ya uporaji wa simu katika maeneo mbali mbali ya kinondoni, mtuhumiwa wa kwanza ni Richard Augustino 18 aliyekamatwa Julai 11 mwaka huu maeneo ya Coco Beach akiwa na sumsung yenye thamani ya sh. 500,000.

"Wengine ni Abdalah Chande 36 aliyekematwa Julai 11 mwaka huu maeneo ya Magomeni Mapipa akiwa na simu 11 za wizi, na Abdalah Saidi 22 ambaye alikamatwa maeneo ya Mapipa julai 14 mwaka huu akiwa na pikipiki aina ya boxer ambayo ilikuwa ikitumika katika matukio ya ukuporaji simu," alisema.

Serikali kupima viwanja zaidi ya 25,000 jijini Dar es Salaam

0
0
Na Jonas Kamaleki, MAELEZO

SERIKALI iko mbioni kutoa hatimiliki zaidi ya 25,000 kwa wakazi wa kata za Kimara na Saranga zilizopo jijini Dar es Salaam ikiwa ni hatua ya kurasimisha makazi holela.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Mratibu wa Mradi wa urasimishaji wa makazi holela Kata za Kimara na Saranga, Bi Grace Masatu wakati wa zoezi la ukaguzi wa maeneo ya mradi. “Zoezi za la upimaji linaenda sanjari na utambuzi wa mipaka,ujazaji wa madodoso, uchoraji wa ramani za upimaji na mipangomiji,”alisema Masatu.

Viwanja zaidi ya 25,000 vinatarajiwa kupimwa katika kata za Kimara na Saranga ambapo hadi leo ramani za upimaji 14 na ramani sita (6) za mipangomiji zenye jumla ya viwanja1028 ziko tayari na zimeshawasilishwa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa ajli ya kupitishwa, alisema Masatu. Aidha, Masatu amesema kuwa malengo ya mradi huo ni kuongeza thamani ya makazi kwa kutoa hatimiliki na kutambua mipaka ya wakazi wa maeneo husika.

Kwa upande wake, Afisa Mipango miji Mkuu, Bi Anna Macha, alisema kuwa hadi sasa maeneo yaliyopimwa katika kata ya Kimara ni mtaa wa Kilungule A wote pamoja na viwanja 724 vya mtaa wa Kilungule B, ambavyo vimechukuliwa mahesabu ya upimaji kwa ajili kuandaa ramani.

Ameongeza kuwa umetengenezwa mfumo maalum ambao unachukua taarifa za madodoso zinazojazwa wakati wa utambuzi wa mipaka ya wamiliki wa maeneo husika. Mfumo huo utaunganishwa na mfumo wa Kamishna wa Ardhi (MOLIS) utakaorahisisha kufahamu idadi ya viwanja vilivyopimwa na kumilikishwa. Naye Mjumbe wa Mtaa wa Kilungule B, Bwana Claud Misri Silayo ameonyesha kuridhishwa na zoezi zima la utambuzi na upimaji wa maeneo.

“ Nimefurahishwa na zoezi la upimaji kwani nitamiliki ardhi kisheria, kihalali na nitafaidika na ardhi ninayomiliki kwa sababu mwisho wa zoezi hili nitapata hatimiliki ambayo itaniwezesha kupata mikopo kwenye taasisi za fedha,”alisema Silayo.

Urasimishaji ni mwendelezo wa utambuzi wa makazi holela katika jiji la Dar es Salaam unaotekelezwa chini ya Sheria ya Ardhi Na. 4 pamoja na Sheria ya Mipangomiji.

Wananchi wa bahi wahimizwa kujiunga na CHF

0
0

Waziri Ummy Mwalimu akiwasili kwenye kituo cha afya Mundemu wilayani Bahi.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu akisalimiana na watumishi wa kituo hicho cha afya.
Waziri wa afya akuongea na wagonjwa walifiks kituoni hapo kupata huduma(picha na Habari na wizara ya afya.
Mmoja wa watumishi wa kituo hicho akimsomea taarifa ya kituo hicho cha afya waziri wa afya(hayupo pichani).

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto, Ummy Mwalimu amewahimiza wananchi wa wilaya ya Bahi kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za afya.

Waziri Ummy alisema hayo leo wakati alipofanya ziara ya kikazi wilayani BAHI ambapo kwa kutembelea kituo cha Afya cha Mundemu.Akijibu maswali ya wananchi kuhusu kutopewa dawa licha ya wao kuwa na kadi za CHF, Waziri Ummy amewahakikishia wananchi wote kuwa, wizara yake kupitia Bohari ya Dawa(MSD) itahakikisha dawa za kutosha zinapatikana kwenye vituo vya kutolea huduma ili wananchi na wanachama wa CHF waweze kupata dawa wakati wote.”


kupitia CHF iliyoboreshwa mtaweza kupata huduma hizo hadi ngazi ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa”alisema.Katika ziara hilo,Waziri Ummy pia alitembelea mradi wa usafi wa mazingira mashuleni, katika jamii na maeneo ya kutolea huduma kwa jamii unaofadhiliwa na PLAN INTERNATIONAL

TTB AND TWO YOUTH ASSOCIATIONS FORGE PARTNERSHIP IN PROMOTING DESTINATION TANZANIA

0
0

The TTB’s Acting Director of Marketing Mr. Philip Chitaunga (left) talks with gesture to members of the youth associations on how the associations can closely work with TTB in promoting the country.
The TTB’s Acting Marketing Manager Mr. Vedastus Mwita (center) making elaborating something during a meeting with members of YLA and TYP. Others in a picture are Rossan Mduma (right) and Mr. Hoza Mbura (left)
Some members of YLA and TYP following with keen interest a brief presentation on the function and roles of TTB in promoting destination Tanzania..
Mr Rossan Mduma, Head TTB’s IT unit explaining to the members of youth associations (not in picture) how TTB uses an online destination Portal in promoting the country.
Mr. Philip Chitaunga who is the Acting Director of Marketing (center) pauses for group photo with members of the two youth .associations and some members of TTB staff.

…………………………

Tanzania Tourist Board (TTB) and Youth Light Africa (YLA) and Tanzania Youth Patriotism (TYP) have to join hands in promoting destination Tanzania within and outside the country by using social media.

The agreement reached today in a meeting held at TTB head office in Dar es salaam whereby TTB briefed members of the associations on TTB’s functions and roles as a national organ mandated for promoting Tanzania as a unique tourist destination worldwide. They were also briefed about the marketing strategy and different techniques applied in promoting destination Tanzania.

On their part members of the two associations commended TTB for their invaluable effort in promoting the country and vowed to give TTB a supporting hand.

Programu za vyuo vikuu ambazo hazijasajiliwa na TCU na NACTE kufutwa

0
0
Na: Lilian Lundo – MAELEZO

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Bi. Maimuna Tarishi ameitaka Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) kufuta programu zinazotolewa na vyuo vikuu hapa nchini ambazo hazijafanyiwa tathmini wala kusajiliwa.

Katibu Mkuu huyo ameyasema hayo leo alipokuwa akifunga maonyesho ya kumi na moja ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia yaliyoanza Julai 20 katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.

“Wakati mwingine najiuliza inakuwaje chuo kinafundisha programu ambayo haijatathminiwa wala kusajiliwa na TCU au NACTE, ni lazima tuwe makini kwani tunahitaji elimu bora katika vyuo vyote nchini bila kuangalia kama ni cha Serikali au ni Binafsi,” alifafanua Bi. Tarishi.

Aliendelea kwa kusema kuwa, TCU na NACTE wanajukumu ya kuzifuta programu hizo na kuanzisha programu zenye uhitaji mkubwa kama vile shahada ya mafuta na gesi, Kompyuta na Ualimu wa Sayansi ambapo wataalamu katika maeneo hayo wamekuwa wakihitajika zaidi katika kipindi hiki ambacho Serikali ya Awamu ya Tano inajikita zaidi katika uanzishwaji wa viwanda.

Aidha Bi. Tarishi amewataka TCU na NACTE kudahili wanafunzi wenye vigezo vinavyohitajika na kusisitiza kuwa ni bora kuwa na wanafunzi wachache katika vyuo vikuu kuliko kuwa na wanafunzi wengi ambao hawana sifa.

Wakati huo huo Mkuu wa Kitivo cha Biashara Chuo Kikuu cha Zanzibar Salehe Mwinyi amesema kuwa wanafunzi wengi wamejitokeza kutembelea banda la Chuo hicho kutaka kujua pogramu zinazotolewa na wengi wao wameonyesha nia ya kujiunga katika Chuo hiko.

Vile vile Mwinyi amesema kuwa mwaka huu idadi ya wanafunzi waliotembelea maonyesho hayo ni wengi zaidi kutokana na eneo lililochaguliwa kufikika kwa urahisi kutoka pande zote za jiji la Dar es Salaam ukilinganisha na mwaka jana ambapo yalifanyika viwanja vya Saba Saba na kutembelewa na idadi ndogo ya wanafunzi na wazazi.

Kwa upande wake, Fadia Suleiman mwanafunzi anayetegemea kujiunga na Chuo Kikuu mwaka huu, amesema kuwa maonyesho hayo yamemsaidia kwa kiasi kikubwa kujua ni programu gani asome kutokana na ufaulu wake wa kidato sita.

Maonyesho ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia ambayo huandaliwa na TCU hufanyika kila mwaka yakitoa fursa kwa Vyuo Vikuu vya ndani na nje ya nchi kutoa elimu kwa wazazi na wanafunzi wanaotegemea kujiunga na vyuo vikuu kwa mwaka husika juu ya programu zinazotolewa na vyuo hivyo pamoja na kutoa ushauri ni programu gani mwanafunzi asome kwa kuangalia ufaulu wake.

UTIAJI SAINI MAKUBALIANO YA AWALI YA UJENZI WA RELI YA KATI (STANDARD GAUGE)

0
0

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servaciaus Likwelile akitiliana saini na Naibu Meneja Mikopo Nafuu wa Benki ya Exim ya China Bw. Zhu Ying kuhusu makubaliano ya awali ya ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kisasa (Standard Gauge), jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servaciaus Likwelile akibadilishana hati ya makubaliano na Naibu Meneja Mikopo Nafuu wa Benki ya Exim ya China Bw. Zhu Ying mara baada ya kusaini makubaliano ya awali ya ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kisasa (Standard Gauge), jijini Dar es Salaam,

……………………………………….

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo imetiliana saini na Benki ya Exim ya China makubaliano ya awali ya ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kisasa (Standard Gauge).

Makubaliano hayo ya awali yamefanywa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servaciaus Likwelile kwa niaba ya Tanzania na Naibu Meneja Mikopo Nafuu wa Benki ya Exim ya China Bw. Zhu Ying.

Akizungumza katika hafla hiyo ya utiliaji saini Dkt. Likwelile amesema hatua hiyo inawezesha hatua za upembuzi yakinifu, usanifu na uundwaji wa timu za pamoja kuanza kuanisha mahitaji halisi ya ujenzi wa mradi huo.
 
Zaidi ya Shilingi Trilioni 16 za Tanzania zinatarajiwa kutumika katika ujenzi wa mradi wa reli ya kati yenye urefu wa Kilometa 2,190 ambapo Benki hiyo itashirikiana na Serikali ya Tanzania katika ujenzi wake.Mradi wa ujenzi wa reli ya kati utahusisha ujenzi wa reli kwa kiwango cha kisasa kutoka Dar es Salaam-Tabora-Isaka-Mwanza na Tabora-Mpanda-Kalemela-Uvinza-Kigoma-Isaka-Keza hadi Msongati.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI ATEMBELEA CHUO CHA USAFIRISHAJI

0
0
03 
Mkuu wa Kitengo cha Uhandisi wa anga katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji NIT Eng. Azizi Mdimi akimuonesha Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani injini ya ndege inayotumia kwa mafunzo wakati alipokagua Hanga katika chuo hicho.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani akikagua ndege inayotumiwa kufundishia wanafunzi wanaosomea utengenezaji wa ndege na urubani alipotembelea Chuo cha Usafirishaji NIT.
05 
Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Prof. Zacharia Mganilwa akimuonesha  Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani moja ya kitabu kinachotumiwa kufundishia marubani na wahandisi wa ndege alipotembelea maktaba ya chuo hicho.
06 
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani akikagua mtambo unaopima magari ili kujua ubora wake kabla ya kuanza kutumika hapa nchini alipotembelea Chuo cha Taifa cha Usafirishaji NIT.(Picha na Benjamin Sawe-Maelezo)
01 
Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Prof. Zacharia Mganilwa akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani alipotembelea Chuo hicho kukagua miundombinu yake.
02 
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani akitoa maelekezo kwa  Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Prof. Zacharia Mganilwa kuhusu namna nzuri ya kukiwezesha Chuo hicho kujiendesha kwa faida na kuboresha miundombinu yake.

UMMY MWALIMU AZINDUA UJENZI WA WODI YA WAZAZI KATIKA KITUO CHA AFYA CHA GAIRO

0
0

Waziri wa afya,Maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto Ummy Mwalimu akikata utepe kuashiria uzinduzi wa ujenzi ya wodi ya wazazi kwenye kituo cha afya Gairo.
Waziri Ummy Mwalimu akiwasikiliza watumishi wa kituo hicho cha afya(hawapo pichani),kushoto ni mbunge wa jimbo la Gairo Mhe.Ahmed Shabiby(wa kwanza kushoto)Mkuu wa Wilaya hiyo mhe.Siriel Mchembe(wa pili kulia) na wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa halmashauri bi.Agnes Mkandya
Waziri Ummy akimsikiliza mwananchi(hayupo pichani)kwenye kituo cha afya gairo mara baada ya kuzindua ujenzi wa wodi ya wazazi,kulia ni bi. Agnes Mkandya Mkurugenzi wa halmashauri hiyo
Waziri wa afya akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa halmashauri hiyo,mara baada ya kuzindua ujenzi wa wodi ya wazazi inayojengwa kwenye kituo cha afya gairo.
(picha na wizara ya afya)


Na.Catherine Sungura,Gairo

Halmashauri ya Wilaya ya Gairo wametakiwa kuweka kwenye mipango yake na kiwe kipaumbele chao ujenzi wa Hospitali ya wilaya.Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati akizindua ujenzi wa wodi ya wazazi inayojengwa kwenye kituo cha Afya mjini hapa inayodhaminiwa na mbunge Ahmed Shabiby.

Waziri Ummy amesema wodi hiyo ikikamilika itawasaidia akina mama wengi wa halmashauri Hiyo pamoja na vijiji vya jirani kufika kituoni hapo kujifungua”suala ya uzazi kwa mwanamke ni haki yake ya msingi,hivyo kuwa na wodi yao ni haki yao pia na kwa afya zao na za watoto wanaojifungua”

Aidha,amesisitiza juu ya utekelezwaji wa sera ya afya inayohusu matibabu bure kwa akina mama wajawazito,wazee na watoto chini ya miaka mitano.
“Nazikumbusha hospitali na vituo vya afya nchini kuwapa kipaumbele kwa kuwapatia matibabu makundi haya,pia muweke dirisha litakaowahudumia wazee,na hii ndio muhimu mlitekeleze”

Kwa upande wa watumishi,Waziri Ummy Karnataka waendelee kufanya kazi kwa uadilifu kwa mujibu wa sheria na taratibu Za taaluma zap na kuzingatia viapo vyao katika kuwahudumia wananchi ili kusiwepo na malalamiko yatakayoleta matatizo.miongoni mwao.

“Nakuagiza Mkurugenzi wa halmashauri uhakikishe unatatua changamoto za watumishi ikiwemo kuwalipa posho za sare za kazi, likizo na stahiki zao nyingine watumishi hawa”
Awali akisoma taarifa ya Wilaya,mkuu wa wilaya hiyo bi. Siriel Mchembe alitaja changamoto kubwa kwa upande wa huduma za afya ni kukosekana kwa hospitali ya Wilaya Mkuu wa wilaya ya Gairo juu ya hali ya huduma za afya wilayani humo, alieleza changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya afya ikiwemo ukosefu wa hospitali ya wilaya, gari la kubebea wagonjwa, upungufu wa watumishi pamoja na kutokuwepo kwa zahanati na vituo vya afya katika kata na vijiji hali inayopelekea wananchi kuzifuata huduma za afya umbali mrefu.

AMANA BANK TANZANIA WAZINDUA KITUO CHA HUDUMA KWA WATEJA

0
0

Juma Msabaha ambaye ni senior costomer service manager wa Bank Ya AMANA nchini Tanzania akifafanua jambo kwa wanahabari wakati Bank Hiyo ikizindua Rasmi Kituo cha Huduma kwa wateja ambacho ni mahsusi kwa kuwasaidia wateja wake kuzifikia na kuzipata Huduma Zao kiurahisi zaidi

Benki ya kwanza ya Kiislam nchini Tanzania Amana benki leo imezindua kituo chake cha huduma kwa wateja ambacho kitakuwa kikiwasaidia wateja wake kuweza kupata taarifa mbalimbali kuhusu huduma zao kama maulizo kuhusu bidhaa za amana, Atms,huduma za mitandao (simu banking) na amana banki mtaani n.k.

Kituo hicho kitakuwa kikifanya kazi kuanzia saa 2 asubuhi mpaka saa 4 na watakuwa wanapatikana kwa nambari 0657980000 ambapo amana Bank ni miongoni mwa benki zinazofanya vizuri kwa sasa wana matawi saba matano yakiwa Dar es salaam,Arusha,Mwanza na wanatarajia kufungua matawi mengine mikoa mingi zaidi ila waliyoipa kipaumbele zaidi ni Zanzibar na Tanga
Akizungumza na waadishi wa habari meneja mfawidhi na huduma kwa wateja Juma Msabaha Amesema kuwa utaratibu wanaotumia kuweza kuwapata mawakala ni kwamba wakala lazima awe na leseni ya biashara pia awe na tin namba ya biashara kuonyesha kuwa ni mlipa kodi pia awe amefanya kazi zaidi ya miaka miwili na pia anaweza kuomba uwakala kwa namba zao ambazo ni 0657980000 au info@ amanabank.co.tz na maombi yake yatapelekwa BOT kuweza kujadiliwa na kama amekidhi vigezo atapewa uwakala ambapo amesema kuwa kwa sasa wana mawakala kwa mikoa kama tabora ,bukoba,na mtwara na bado wanaendelea kupokea maombi kutoka kwa watu mbalimbali.

Munir Rajab – mkuu wa idarara ya biashara amana benki amisema kuanzishwa kituo hicho kuna lengo la kuhitaji kuwa karibu na na wateja wao huku akitanabaisha kuwa huduma za kibenki huwa zinafanana lakini kinachoweza kuwatofautisha ni ubora wa huduma kwa wateja na kwamba wao wamejipanga vizuri kuingia kwenye ushindani huo ambapo wameamua kuwa mwaka huu ni mwaka wa mawakala kwa sababu wanahitaji kuweza kuwafikia wateja wao mpaka mahali ambapo hakuna matawi na wataweza kutumia huduma za kibenki kupitia mawakala wao .
Mkuu wa biashara wa Bank ya AMANA nchini Tanzania Munir rajab akieleza mambo mbalimbali kwa wanahabari kuhusu huduma hiyo mpya kutoka kwao .

Bw. Juma Msabaha akijibu swali wa muandishi wa habari Alisema kuwa utaratibu wanaotumia kuweza kuwapata mawakala ni kwamba wakala lazima awe na leseni ya biashara pia awena tin namba ya biashara kuonyesha kuwa ni mlipa kodi pia aweamefanya kazi zaidi ya miaka miwili na pia anaweza kuomba uwakala kwa namba zao ambazo ni 0657980000 au info@ amanabank.co.tz na maombi yake yatapelekwa BOT kuweza kujadiliwa na kana amekidhi vigezo atapewa uwakala . na kwa sasa wana mawakala kwa mikoa kama Tabora ,Bukoba,na Mtwara na bado wanaendelea kupokea maombi kutoka kwa watu mbalimbali.
Viewing all 46202 articles
Browse latest View live




Latest Images