Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 912 | 913 | (Page 914) | 915 | 916 | .... | 1897 | newer

  0 0

   Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji,Dkt Adelhelm James Meru akizungumza na Wawekezaji mbalimbali wa Tanzania na Poland kuhusu uwekezaji baina ya nchi hizo mbili.
   Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji(TIC),Clifford Tandari(kulia) pamoja na  Mtendaji Mkuu wa Uwekezaji nchini Poland, Bartlomies Pawlak(kushoto) wakitia saini ya Makubaliano baina ya nchi mbili hususan katika Sekta ya Kilimo na kusaidia katika kuendeleza Uchumi wa Viwanda pamoja na Elimu hapa nchini.
   Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Nchini, Gedfrey Simbeye akizungumza na Wadau wa Sekta ya Uwekezaji wa Tanzania na Poland juu fursa ya Uwekezaji iliyopo hapa nchini.
   Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji(TIC),Clifford Tandari akiwasilisha mada katika mkutano huo uliowahusisha wadau wa Sekta ya uwekezaji wa Tanzania na Poland.
  Wadau mbalimbali wa Sekta ya Uwekezaji wakisikiliza baadhi ya mada zilizokuwa zinawasilishwa katika mkutano huo uliofanyika jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii).

  0 0  NA, MWANDISHI WETU TANGA

  MSANII wa Mziki wa Bongo Fleva nchini Tanzania Navy Kenzo anatarajiwa kutumbuiza kwenye shindano la kumtafuta malkia wa Mkoa wa Tanga Miss Tanga 2016 litakalofanyika Julai 29 mwaka huu kwenye ukumbi wa Hotel ya Tanga Beach Resort.

  Licha ya Navy Kenzo wasanii wengine ambao watasindikiza onyesho hilo kwa kutoa burudani ni kundi la mziki wa kizazi kipya mkoani Tanga,Wazenji Classic pamoja na Dances.

  Akizungumza jana,Mratibu wa Onyesho hilo, alisema kuwa maandalizi ya kuelekea shindano hilo yanaendelea vizuri ambapo tayari warembo watakaoshiriki wameanza kuingia kambini .

  Shindano hilo ambalo limeandaliwa na kituo cha Radio cha TK FM 88.5 kilichopo mjini Tanga kwa kushirikiana na Hotel ya Tanga Beach Resort wameelezea namna walivyo jipanga kuhakikisha onyesho hilo linakuwa na ushindani mkubwa kutokana na aina ya warembo waliopo .

  “Nisema tu tumejiandaa vizuri kuhakikisha shindano hilo linafanyika kwa umakini mkubwa ili kuwawezesha wadau wa tasnia ya urembo mkoani hapa kuweza kupata ladha halisi ya onyesho hilo kwani licha ya kuwaona warembo wakali wakini pia mzee wa kamatia chini atakuwepo kuwapagawisha “Alisema.

  Hata hivyo alisema kuwa mazoezi ya warembo watanaoshiriki onyesho hilo yanaendelea kwenye ukumbi wa New Hotel uliopo mjini hapa kuanzia saa kumi jioni.Aidha alisema kuwa kabla ya kufanyika shindano hilo warembo hao watapata fursa ya kutembelea maeneo mbalimbali ya vivutio vya utalii mkoani hapa ikiwemo Mapango ya Amboni na Hifadhi ya Taifa ya Saadani.

  Habari kwa hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

  0 0

   Naibu waziri anazindua kuanza kwa madarasa ya kidato cha 5-6
   Naibu waziri JOFO  alipowasili katika hospitali ya Wilaya Mafinga
  Naibu waziri nazungumza na umati wa wanafunzi na wazazi katilka shaule ya Sekondalri Mdabulo

  Na. Ofisi ya habari Mufindi.

  Naibu waziri Ofisi ya Rais tawala za Mikoa na serikali za mitaa (Tamisemi) Mh. SELEMAN JAFO, amewataka waalimu wenye tabia ya kujihusisha katika mahusiano ya kingono na wanafunzi wao, kuacha mara moja tabia hiyo kwani kwa kufanya hivyo watakuwa wanaatarisha ajira na maisha yao.

  Kauli hiyo ameitoa wakati akizindua madarasa ya kidato cha tano na sita (5 -6) katika shule kongwe ya Sekondari ya Mdabulo iliyopo katika kata ya Mdabulo Wilayani Mufindi Mkoani Iringa wakati wa ziara yake ya kikazi Mkoani humo.

  Mh. JAFO amesema, katika kipindi hiki cha Serikali ya awamu ya tano Mwalimu yeyote atakayebainika kujihusisha na vitendo hivyo atachukuliwa hatua kali za kinidhamu kwa kuzingatia taratibu za maadili ya mtumishi wa umma sanjari na kufikishwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria na kubainisha kuwa tayari zaidi ya Waalimu 10 wamebainika na kuadhibiwa.

  Aidha, Waziri JAFO ameuagiza uongozi wa halmashauri na Wilaya hiyo kusimamia haki na sitahiki za waalimu Wilayani huo ikiwepo kero sugu ya kutopandishwa madaraja inayolalamikiwa na waalimu nchini kote na kuangeza kuwa, kwa kutatua kero zao, itawajengea hali na shauku ya kufanya kazi kwa bidii hivyo kuinua kiwango cha elimu nchini.

  Shule ya Sekondari Mdabulo imeanza rasmi kutoa elimu ya juu ya sekondari kwa wanafunzi wa kike pekee wapatao 70 kupitia michepuo ya HGL na HKL.

  Pamoja na uzinduzi huo, naibu waziri JAFO alifanya ziara katika Zahanati ya Idunda, chamzo cha maji katika mji wa Mafinga, kukagua utoaji huduma na kuzindua ufanyaji kazi wa mashine mbili za Ultra sound katika Hospitali ya Mafinga kisha akahitimisha kwa kuzungumza na watumishi wa Halmshauri za Mufindi.

  0 0


  Sehemu ya wadau kutoka Idara na Taasisi mbalimbali za Serikali wakifuatilia Hotuba ya ufunguzi iliyotolewa na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (hayupo pichani) katika Warsha ya kupitia Rasimu ya Sera ya Taifa ya Mazingira.
  Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Mbaraka AbdulWakil akiteta jambo na Kaimu Mkurugenzi wa Mazingira Bw. Richard Muyungi (kushoto) mara baada ya kufungua Warsha ya kupitia Rasimu ya Sera ya Taifa ya Mazingira. Warsha hiyo imefanyika katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Bw. Deogratius Paul
  Wana warsha wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni Rasmi mara baada ya ufunguzi wa Warsha katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam

  0 0

  Wasanii Kala Jeremiah na Super Nyamwela wanatarajiwa kupamba msimu mpya wa programu ya Jukwaa la Sanaa ambayo imekuwa ikiendeshwa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kwa kushirikiana na chama cha waandishi wa habari za Sanaa na Utamaduni (CAJAtz) kwa miaka mitano sasa tangu mwaka 2011.

  Msimu mpya wa Jukwaa la Sanaa unatazamiwa kuzinduliwa rasmi Jumatatu ya tarehe 25/07/2015 kwenye Ukumbi wa BASATA ulioko Ilala Sharif Shamba jijini Dar es Salaam kuanzia saa saa 4:00 Asubuhi – 6:30 Mchana.

  Wasanii hawa wanatarajiwa kuupamba uzinduzi huo kwa kutoa burudani mbalimbali sambamba na kuongea na wasanii wachanga katika kuwahamasisha na kuwajengea uwezo juu ya namna wanaweza kutumia fursa mbalimbali za mashindano ya kukuza vipaji katika kujijenga kisanaa.

  BASATA linatambua kwamba kumekuwa na tatizo la wasanii katika kutambua na kuchangamkia fursa mbalimbali zilizoko katika sekta ya Sanaa hasa zile zilizomo kwenye mashindano mbalimbali ya kutafuta vipaji ambayo wasanii Kala Jeremiah na Super Nyamwela wamekuwa wakishiriki kikamilifu.

  Ushiriki wa wasanii hawa katika kuwajengea hamasa na kuwapa changamoto wasanii wachanga utasadia katika kuwajengea uwezo wa kutumia fursa hizo.

  Mbali na burudani na elimu hiyo, uzinduzi huu wa msimu wa mpya wa Jukwaa la Sanaa unaotarajiwa kuhudhuriwa na watu zaidi ya mia moja (100) utahusisha pia kongamano maalum ambalo litajikita katika kutoa elimu mbalimbali kuhusu sekta ya Sanaa kwa wadau watakaohudhuria.

  Jukwaa la Sanaa ni programu iliyobuniwa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kwa lengo la kutoa elimu kuhusu masuala mbalimbali yahusuyo sekta ya Sanaa lakini pia kusaidia waandishi wa habari kupata habari zihusuzo sekta ya Sanaa kutoka vyanzo mahsusi.

  Sanaa ni kazi, tuipende na kuithamini


  Imetolewa na Kitengo cha Habari
  Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA)

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mh. Dkt. ALI Mohamed Shein amefanya uteuzi wa viongozi katika Taasisi mbali mbali za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar Dkt. Abdulhamid Y. Mzee, katika Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Juma Yakout Juma ametuliwa kuwa Naibu Katibu Msaidizi Baraza la Mapinduzi (Sera, Ufuatiliaji na Tathmini).

  Mkurugenzi wa Idara ya Mipango, Sera na Utafiti ameteuliwa Nd. Mwadini Makame Haji.

  Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mkurugenzi wa Mipango, Sera na Utafiti Nd. Abdalla Issa Mgongo na Mkurugenzi wa Miundo ya Taasisi, Utumishi na Maslahi ya Watumishi Nd. Shaibu Ally Mwazema.

  Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara maalum za SMZ Mkurugenzi wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Nd. Khalid Omar Abdalla na Katibu wa Tawala wa Wilaya ya Magharibi ‘A’ Nd. Mashaka Hassan Mwita.

  Katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Nd. Issa Mlingoti Ally ameteuliwa kuwa Mratibu Mkuu wa Ofisi ya Uratibu wa Shughuli za SMZ, Dar es salaam.

  Mkurugenzi wa Idara ya Mipango, Sera na Utafiti Nd. AMEIR Makame Ussi

  Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa shughuli za Serikali Nd. Khalid Bakari Amran, Mkurugenzi wa Idara ya sherehe na Maadhimisho ya Kitaifa Nd. Riziki Daniel Yussuf na Ofisa Mdhamini wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Pemba Nd. Ali Salim Alim Matta.

  Wizara ya Afya Mkurugenzi wa Idara ya Mipango, Sera na Utafiti Nd. Ramadhan Khamis Juma na Ofisa Mdhamini wa Wizara ya Afya Pemba Nd. Ali Bakari Ali. Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na UvuviMkurugenzi wa Umwagiliaji Maji Nd. Haji Hamid Saleh.

  Wizara ya Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa na Sensa ya Filamu na Utamaduni Dkt. Omar Abdalla Adam.

  Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba Nd. Abdalla A. Mwinyigogo na Mkurugenzi wa Wakala wa Majengo Nd. Ramadhan Mussa Bakari.

  Katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Nd. Omar Ali Omar Bhai ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Uendeshaji na Utumishi.

  Wizara ya Ardhi, Mji, Nishati na Mazingira Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Nd. Tahir M. K. Abdalla na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Kudhibiti Huduma za Maji na Nishati (ZURA) Nd. Hemed Salim Hemed.

  WIZARA YA Biashara Viwanda na Masoko Mkurugenzi wa Mipango, sera na Utafiti Nd. Nana Mwanjisi.

  UTEUZI HUO UMEANZA TAREHE JULAI 20, 2016.

  IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO ZANZIBAR

  0 0

  Hamza Hemed kutoka Twalipo Youth Academy akijaza fomu ya usajili kwa ajili ya michuano ya Airtel Rising Stars 2016 huku akishuhudiwa na Katibu Mkuu wa Chama cha Mpira wa miguu wa mkoa wa soka wa Temeke Kassim Ally.
  Farid Ally kutoka Mbangala Youth Academy FC akijaza fomu ya usajili kwa ajili ya michuano ya Airtel Rising Stars 2016 huku akishuhudiwa na Katibu Mkuu wa Chama cha Mpira wa miguu wa mkoa wa soka wa Temeke Kassim Ally.
  Hamisi Nassoro kutoka Carpet FC akijaza fomu ya usajili kwa ajili ya michuano ya Airtel Rising Stars 2016 huku akishuhudiwa na Katibu Mkuu wa Chama cha Mpira wa miguu wa mkoa wa soka wa Temeke Kassim Ally.  Usajili wa wachezaji kwa ajili ya mashindano ya vijana chini ya umri 17 ya Airtel Rising Stars 2016 umeanza leo katika mikoa inayoshirikia michuano hiyo mwaka huu ambapo mashindano katika ngazi ya mkoa yamepangwa kuanza wiki ijayo Julai 30.

  Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Shirikisho la Mpira wa miguu nchi TFF, michuano hiyo ngazo ya mkoa inatarajiwa kumalizka Agosti 28 na kufuatiwa na mashindano ya taifa yatakayofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Septemba 6 hadi 11.

  Akiongea wakati wa usajili katika mkoa wa kisoka wa Temeke, Katibu Mkuu wa Chama Cha Mpira Temeke Kassim Mustafa alisema mkoa wake wamejiandaa vema kwa ajili ya kutetea ubingwa walioshinda mwaka jana. “Leo tumeanza usajili wa wachezaji kwa ajili ya michuano ya Airtel Rising Stars 2016. Napenda kuchukua fursa hii kuwashukuru Airtel kwa mradi wake huu wa kusaka na kukuza vipaji vya soka kwa vijana wetu. Temeke tunao vipaji vyingi na ndio sababu mkoa wetu uliweza kushinda taji la ARS 2015,” alisema Mustafa.

  Naye kocha mkuu wa Twalipo Youth Academy Neville Kanza alisema anafurahi ujio wa Airtel Rising Stars 2016 huku akisema vipaji vipo vingi na kutamba kuendelea kutoa vijana wengi kwenye kombaini timu ya mkoa. Mwaka jana Twalipo academy ilitoa wachezaji watano ambao waliunga timu ya taifa ya Airtel Rising Stars Dream Team.

  Kwa wake Ofisa Uhusiano Airtel Tanzania Jane Matinde alisema wanayo furaha kuona vijana wameweza kufanikisha ndoto zao kwa kupitia michuano ya Airtel Rising Stars. “Ni furaha kuona timu zetu za taifa zikiwa na wachezaji ambao wametoka na program hii ya Airtel Rising Stars,” alisema na kuongeza kuwa hii ni fursa nyingine kwa vijana kujitokeza kwenye usajili ambao utawawezesha kushiriki michuano hii na kuonyesha vipaji vyao.

  Alisema Airtel Rising Stars mwaka inafanyika chini ya mwanvuli wa kampeni ya Airtel RURSA iliyozinduliwa mwaka jana kwa lengo la kuwahamasisha vijana kutumia fursa mbalimbali walizonazo ili kujiendeleza kiuchumi. “Airtel Rising Stars yenyewe ni Airtel FURSA kwa kuwa inawawezesha vijana kutumia vipaji vyao kujikwamua kimaisha kupitia mpira. Mpira ni chano cha kipato cha kuaminika”, alisema.

  Mikoa inayoshirikia mwaka huu ni Ilala, Temeke, Kinondoni, Mwanza, Mbeya na Morogoro (wavulana) na Ilala, Kinondoni, Temeke, Arusha, Lindi na Zanzibar zikishirikisha wasichana.


  0 0
  Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana ,Ajira na Walemavu Bi. Jenista Mhagama akizungumza na wadau mbalimbali hawapo pichani wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Mashauriano ya ushiriki wa Watanzania katika uwekezaji uliofanyika leo jijini Dar es salaam.
  Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana ,Ajira na Walemavu Bi. Jenista Mhagama wa kwanza kulia akimkabidhi cheti cha pongezi kwa kuwa mdhamini wa Mkutano wa Mashauriano ya ushiriki wa Watanzania katika uwekezaji Mkurugenzi Mtendaji wa ARIS Bw. Sanjay Suchak wa kwanza kushoto wakati wa ufunguzi wa Mkutano huo leo jijini Dar es salaam.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel wa kwanza kushoto akibadilishana mawazo na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt.Hamis Mwinyimvua wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Mashauriano ya ushiriki wa Watanzania katika uwekezaji uliofanyika leo jijini Dar es salaam.
  Wadau kutoka wa uchumi kutoka taasisi mbalimbali nchini wakifuatilia kwa makini hotuba ya Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana ,Ajira na Walemavu Bi. Jenista Mhagama hayupo pichani wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Mashauriano ya ushiriki wa Watanzania katika uwekezaji uliofanyika leo jijini Dar es salaam.


  Na Ally Daud-Maelezo

  Serikali imetenga shilingi bilioni 15 kwa ajili ya kukuza ujuzi kwa vijana ili kuwawezesha kujikimu kimaisha na kuchangia kuinua uchumi wa nchi.

  Akizungumza kwa niaba ya Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Mashauriano ya ushiriki wa Watanzania katika uwekezaji Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana ,Ajira na Walemavu Bi. Jenista Mhagama amesema kuwa Serikali imetenga fedha hizo ili kukuza ujuzi wa vijana katika sekta mbalimbali kwa madhumuni ya kuwakwamua vijana katika uchumi.

  “Tunatambua vijana ni nguvu kazi ya Taifa na wana mchango mkubwa katika kuinua uchumi wan chi hapa tulipo mpaka kufika uchumi wa kati hivyo katika kila bajeti tutatenga bilioni 15 kuwawezesha vijana kiujuzi” alisema Bi. Mhagama.

  Aidha Mhe. Jenista ameongeza kuwa Serikali imeanza kupitia na kurekebisha upya sheria itakayowawezesha wafanya biashara kuweza kumiliki uchumi wa nchi ili kufikia malengo waliyojiwekea hadi kufikia 2020.

  Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni inayojihusisha na maswala ya Bima (ARIS) Bw. Sanjay Suchak amesema kuwa anashukuru kuona serikali imeweka mkakati wa kupitia upya na kurekebisha sheria itakayowaruhusu wafanya biashara kumiliki uchumi kwani kwa hali hiyo itawezesha kundi hilo kushiriki katika masuala ya ujenzi wa uchumi wa nchi.

  Naye Mwenyekiti wa Sekta binafsi Nchini (TPSF) Bw. Reginald Mengi amesema kuwa ipo haja ya watanzania hususani wakulima washirikishwe kwenye semina mbalimbali za kukuza uchumi wa nchi kwani asilimia 60 ya watanzania ni wakulima.

  Mkutano huo wa Mashauriano ya ushiriki wa Watanzania katika uwekezaji umeandaliwa na Baraza la Taifa la uwezeshaji wa Wananchi  iuchumi(NEEC) kwa lengo la kujadili jinsi ya kutumia fursa na kuwezesha nchi kukua kiuchumi limeanza Julai 21 na kumalizika 22 Julai mwaka huu.

  0 0


  Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi Dkt Jakaya Kikwete akiwa sambamba na Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye wakipita kukagua ndani ya ukumbi wa mikutano wa CCM, Dodoma Conversion Center uliopo nje kidogo ya mji wa Dodoma leo, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Mkutano Mkuu Maalum wa CCM utakaofanyika Julai 23, 2016.
  Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi Dkt Jakaya Kikwete akiwa sambamba na Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi (kushoto) na wajumbe wengine wakipita kukagua ukumbi wa mikutano wa CCM, Dodoma Conversion Center uliopo nje kidogo ya mji wa Dodoma, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Mkutano Mkuu Maalum wa CCM utakaofanyika Julai 23, 2016.
  Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi Dkt Jakaya Kikwete akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi walipokuwa wakipita kukagua ukumbi wa mikutano wa CCM, Dodoma Conversion Center uliopo nje kidogo ya mji wa Dodoma, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Mkutano Mkuu Maalum wa CCM utakaofanyika Julai 23, 2016.
  Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi CCM Dkt Jakaya Kikwete akitoa ufafanua wa jambo kwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi,anaefuta ni Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana
  Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana akimuonesha Mwenyekiti wa CCM Dkt Jakaya Kikwete moja ya alama ya wajumbe watakaokuwa wamefika kutoka mikoa mbalimbali.


  Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi Dkt Jakaya Kikwete akiwa sambamba na Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi wakiwasili kwenye ukumbi wa mikutano wa CCM, Dodoma Conversion Center uliopo nje kidogo ya mji wa Dodoma kuukagua leo Julai 21, 2016, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Mkutano Mkuu Maalum wa CCM utakaofanyika Julai 23, 2016.

  Baadhi ya Vyombo vya habari pia vitarusha matangazo ya moja kwa moja,likiwemo shirika la Utangazaji Taifa TBC,Azam TV kama ambavyo magari yake yaonekanavyo katika viunga vya ukumbi huo tayari kwa kwenda Live siku ya mkutano huo.PICHA NA MICHUZI JR-DODOMA.

  0 0

  Na. Aron Msigwa – Dar es salaam.

  Serikali imewataka wataalam wa vyuo Vikuu vinavyotoa mafunzo ya Usimamizi wa Ardhi waitumie taaluma yao katika kutafuta suluhisho la migogoro ya Ardhi inayowakumba wananchi katika maeneo mbalimbali nchini.

  Akizungumza kwa Niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Wanataaluma ya Usimamizi wa Ardhi Kanda ya Afrika Mashariki leo jijini Dar es salaam, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo (Sayansi) Prof. Simon Msanjila amesema kuwa wataalam hao wanalo jukumu la kufuatilia migogoro inayotokea nchini na kuhakikisha wanatoa ushauri wa kitaalam utakaotoa majibu ya utatuzi wa migogoro hiyo.

  “Ninyi kama watalaam wa sekta ya Ardhi lazima mtoe majibu kwa nini migogoro ya ardhi inaendelea kutokea katika maeneo mbalimbali licha kuwepo kwa kanuni, Sheria na taratibu zinazosimamia sekta ya Ardhi nchini” Amesema Prof.Msanjila.

  Ameeleza kuwa wao kama watalaam wa sekta hiyo wanatakiwa kwenda zaidi kwenye matatizo halisi na kuwawafikia wananchi wengi zaidi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ili kuondoa changamoto zao kuliko kucheza na vitabu na kuongea kwenye Ofisi.

  Amewataka wataalam hao hasa wale walioko nchini Tanzania kufika katika maeneo yenye migogoro ya Ardhi ikiwemo Morogoro na maeneo mengine ili kuangalia kwa nini wananchi wanaendelea na mapigano tunajua ipo migogoro ya Ardhi inayotokea katika mikoa ya Morogoro, Pwani na mikoa mingine.


  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo (Sayansi) Prof. Simon Msanjila Akizungumza kwa Niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Wanataaluma ya Usimamizi wa Ardhi Kanda ya Afrika Mashariki leo jijini Dar es salaam.
  Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi Prof. Idrissa Mshoro akizungumza na Mtandao wa Wanataaluma wa Vyuo Vikuu Vinavyotoa Mafunzo yahusuyo Usimamizi wa Ardhi Kanda ya Afrika Mashariki leo jijini Dar es salaam.

  Washiriki wa Mtandao wa Wanataaluma wa Vyuo Vikuu Vinavyotoa Mafunzo yahusuyo Usimamizi wa Ardhi Kanda ya Afrika Mashariki kutoka nchi 9 za Bara la Afrika wakifuatilia Mkutano wa mtandao huo leo jijini Dar es salaam.
  Washiriki wa Mtandao wa Wanataaluma wa Vyuo Vikuu Vinavyotoa Mafunzo yahusuyo Usimamizi wa Ardhi Kanda ya Afrika Mashariki kutoka nchi 9 za Bara la Afrika wakifuatilia Mkutano wa mtandao huo leo jijini Dar es salaam.
  Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi Prof. Idrissa Mshoro akizungumza na waandishi wa Habari leo jijini Dar es salaam mara baada ya Ufunguzi wa Mkutano wa Wanataaluma ya Usimamizi wa Ardhi Kanda ya Afrika Mashariki .
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Mozes Kusiluka akiwaeleza waandishi wa Habari kuhusu mpango wa Serikali wa kupima na kurasimisha maeneo yasiyopimwa katika jiji la Dar es salaam leo.
  Amesema kuwa kwa upande wa Serikali suala la ufumbuzi wa migogoro ya Ardhi linaendelea kupewa kipaumbele kwa kuhakikisha kuwa ardhi inaendelea kutolewa kwa kuzingatia sheria pia kushughulikia changamoto zote zinazokwamisha ustawi wa sekta ya ardhi hususan uondoaji kero zote zinazokwamisha matumizi bora ya ardhi kwa jamii.

  Akifafanua kuhusu nafasi ya Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi katika mkutano huo ameeleza kwamba kupitia mkutano huo wa kitaalam wa masuala ya Ardhi, Wizara hiyo inajifunza kuhusu changamoto zitakazojitokeza na kuibuliwa ili ziwekwe kwenye mitaala kwa lengo la kuwaandaa watalaam watakaokuwa na uwezo wa kusuluhisha matatizo yote yanayojitokeza kwenye sekta hiyo.

  Amesema kuwa Sekta ya Elimu kupitia mkutano huo itaboreshwa kwa kupata nyongeza ya utalaam kutoka kwa wataalam kutoka Vyuo vikuu vya nchi mbalimbali za Bara la Afrika waliohudhuria mkutano huo na kuongeza kuwa Chuo Kikuu Ardhi nchini Tanzania ambacho kimebobea kwenye masuala ya Ardhi kitapata taarifa zaidi katika uboreshaji wa mitaala na mafunzo ya Programu za Utawala wa Ardhi, Ugawaji wa Ardhi na Upimaji wa Ardhi”

  Kwa Upande wake Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi Prof. Idrissa Mshoro akizungumza mara baada katika mkutano huo amesema kuwa wataalam wa Ardhi nchini Tanzania bado wana umuhimu mkubwa katika maendeleo ya sekta ya Ardhi na kufafanua kuwa wao kama chuo kinachozalisha watalaam wa Ardhi wanalo jukumu kuzalisha watalaam watakaofanya usimamizi thabiti wa Ardhi kukabiliana na changamoto zilizopo.

  “Sisi nafasi yetu kama Chuo Kikuu Ardhi ni kujua ni namna gani tunavyoweza kuzalisha wataalam wa kutosha wenye weledi watakaoweza kukabiliana na changamoto mbalimbali zilizoko kwenye sekta ya Ardhi pia kuhakikisha wataalam tunaozalisha wanakidhi ubora na matarajio ya wananchi” Amesema Prof. Mshoro.

  Amesema kuwa wanataaluma kutoka Tanzania watanufaika kutokana na mkutano huo kwa kuwa unawajumuisha watalaam wa Ardhi kutoka takribani nchi 9 watakaobadilishana uzoefu kuhusu changamoto mbalimbali za ardhi zinazojitokeza katika maeneo yao na namna wanavyozitatua.

  Aidha, amesema kuwa Sekta ya Ardhi nchini Tanzania bado inakabiliwa na uhaba wa watalaam wa kutosha ambao wangeweza kusimamia maamuzi katika masuala ya Ardhi ngazi za chini na kuongeza kuwa ili kupata maamuzi na taarifa sahihi za ardhi ni lazima suala la uwepo wa watalaam hao liendelee kupewa kipaumbele.

  Kuhusu mchango wa watalaam hao katika utatuzi wa migogoro ya Ardhi amesema kuwa ipo haja ya watalaam waliopo kutumika ipasavyo kutatua migogoro inayojitokeza na kuwaletea manufaa wananchi ambao wanahitaji huduma za wataalam hao.

  Amesema kuwa kwa upande wa Serikali tayari watalaam wa sekta husika wamejipanga kuhakikisha kuwa wanapata suluhisho la mgogoro inayojitokeza kupitia sheria zilizopo.

  Mkutano huo unaohusisha Mtandao wa vyuo Vikuu ni wa nane tangu kuanzishwa Mtandao wa EALAN mwaka 2009 ambapo kwa mwaka huu Chuo Kikuu Ardhi, Tanzania kimekuwa mwenyeji wa Mkutano huo kufuatia kuteuliwa kuwa kituo Maalum Cha Mafunzo ya Usimamizi wa Ardhi Barani Afrika.

  0 0

   Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana ,Ajira na Walemavu Bi. Jenista Mhagama wa kwanza kulia akimkabidhi cheti cha pongezi kwa kuwa mdhamini wa Mkutano wa Mashauriano ya ushiriki wa Watanzania katika uwekezaji Mkurugenzi Mtendaji wa ARIS Bw. Sanjay Suchak wa kwanza kushoto wakati wa ufunguzi wa Mkutano huo leo jijini Dar es salaam.
   Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana ,Ajira na Walemavu Bi. Jenista Mhagama akizungumza na wadau mbalimbali hawapo pichani wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Mashauriano ya ushiriki wa Watanzania katika uwekezaji uliofanyika leo jijini Dar es salaam.
  Wadau kutoka wa uchumi kutoka taasisi mbalimbali nchini wakifuatilia kwa makini hotuba ya Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Bi. Jenista Mhagama hayupo pichani wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Mashauriano ya ushiriki wa Watanzania katika uwekezaji uliofanyika leo jijini Dar es salaam.

  Na Ally Daud-Maelezo
  Serikali imetenga shilingi bilioni 15 kwa ajili ya kukuza ujuzi kwa vijana ili kuwawezesha kujikimu kimaisha na kuchangia kuinua uchumi wa nchi.

  Akizungumza kwa niaba ya Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Mashauriano ya ushiriki wa Watanzania katika uwekezaji Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana ,Ajira na Walemavu Bi. Jenista Mhagama amesema kuwa Serikali imetenga fedha hizo ili kukuza ujuzi wa vijana katika sekta mbalimbali kwa madhumuni ya kuwakwamua vijana katika uchumi.

  “Tunatambua vijana ni nguvu kazi ya Taifa na wana mchango mkubwa katika kuinua uchumi wan chi hapa tulipo mpaka kufika uchumi wa kati hivyo katika kila bajeti tutatenga bilioni 15 kuwawezesha vijana kiujuzi” alisema Bi. Mhagama.

  Aidha Mhe. Jenista ameongeza kuwa Serikali imeanza kupitia na kurekebisha upya sheria itakayowawezesha  wafanya biashara kuweza kumiliki uchumi wa nchi ili kufikia malengo waliyojiwekea hadi kufikia 2020.

  Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni inayojihusisha na maswala ya Bima (ARIS) Bw. Sanjay Suchak amesema kuwa anashukuru kuona serikali imeweka mkakati wa kupitia upya na kurekebisha sheria itakayowaruhusu wafanya biashara kumiliki uchumi kwani kwa hali hiyo itawezesha kundi hilo kushiriki katika masuala ya ujenzi wa uchumi wa nchi.

  Naye Mwenyekiti wa Sekta binafsi Nchini (TPSF) Bw. Reginald Mengi amesema kuwa ipo haja ya  watanzania hususani wakulima washirikishwe kwenye semina mbalimbali za kukuza uchumi wa nchi kwani asilimia 60 ya watanzania ni wakulima.

  Mkutano huo wa Mashauriano ya ushiriki wa Watanzania katika uwekezaji umeandaliwa na Baraza la Taifa la uwezeshaji wa Wananchi Kiuchumi(NEEC) kwa lengo la kujadili jinsi ya kutumia fursa na kuwezesha nchi kukua kiuchumi limeanza Julai 21 na kumalizika 22 Julai mwaka huu.

  0 0

   Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi Prof. Idrissa Mshoro akizungumza na Mtandao wa Wanataaluma wa Vyuo Vikuu Vinavyotoa Mafunzo yahusuyo Usimamizi wa Ardhi Kanda ya Afrika Mashariki leo jijini Dar es salaam.

   Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo (Sayansi) Prof. Simon Msanjila Akizungumza kwa Niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Wanataaluma ya Usimamizi wa Ardhi Kanda ya Afrika Mashariki leo jijini Dar es salaam.
   Washiriki wa Mtandao wa Wanataaluma wa Vyuo Vikuu Vinavyotoa Mafunzo yahusuyo Usimamizi wa Ardhi Kanda ya Afrika Mashariki  kutoka nchi 9 za Bara la Afrika wakifuatilia Mkutano wa mtandao huo leo jijini Dar es salaam.
   Washiriki wa Mtandao wa Wanataaluma wa Vyuo Vikuu Vinavyotoa Mafunzo yahusuyo Usimamizi wa Ardhi Kanda ya Afrika Mashariki  kutoka nchi 9 za Bara la Afrika wakifuatilia Mkutano wa mtandao huo leo jijini Dar es salaam.
   Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi Prof. Idrissa Mshoro akizungumza na waandishi wa Habari leo jijini Dar es salaam mara baada ya Ufunguzi wa Mkutano wa Wanataaluma ya Usimamizi wa Ardhi Kanda ya Afrika Mashariki .
   Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Mozes Kusiluka akiwaeleza waandishi wa Habari kuhusu mpango wa Serikali wa kupima na kurasimisha maeneo yasiyopimwa katika jiji la Dar es salaam leo.

  Na. Aron Msigwa – Dar es salaam.
  Serikali imewataka wataalam wa vyuo Vikuu vinavyotoa mafunzo ya Usimamizi wa Ardhi waitumie taaluma yao katika kutafuta suluhisho la migogoro ya Ardhi inayowakumba wananchi katika maeneo mbalimbali nchini.


  Akizungumza kwa Niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Wanataaluma ya Usimamizi wa Ardhi Kanda ya Afrika Mashariki leo jijini Dar es salaam, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo (Sayansi) Prof. Simon Msanjila amesema kuwa wataalam hao wanalo jukumu la kufuatilia migogoro inayotokea nchini na kuhakikisha wanatoa ushauri wa kitaalam utakaotoa majibu ya utatuzi wa migogoro hiyo.


  “Ninyi kama watalaam wa sekta ya Ardhi lazima mtoe majibu kwa nini migogoro ya ardhi inaendelea kutokea katika maeneo mbalimbali licha kuwepo kwa kanuni, Sheria na taratibu zinazosimamia sekta ya Ardhi nchini” Amesema Prof.Msanjila.


  Ameeleza kuwa wao kama watalaam wa sekta hiyo wanatakiwa kwenda zaidi kwenye matatizo halisi na kuwawafikia wananchi wengi zaidi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ili  kuondoa changamoto zao kuliko kucheza na vitabu na kuongea kwenye Ofisi.


   Amewataka wataalam hao hasa wale walioko nchini Tanzania kufika katika maeneo yenye migogoro ya Ardhi ikiwemo Morogoro na maeneo mengine ili kuangalia kwa nini wananchi wanaendelea na mapigano tunajua ipo migogoro ya Ardhi inayotokea katika mikoa ya Morogoro, Pwani na mikoa mingine.


  Amesema kuwa kwa upande wa Serikali suala la ufumbuzi wa migogoro ya Ardhi linaendelea kupewa kipaumbele kwa kuhakikisha kuwa ardhi inaendelea kutolewa kwa kuzingatia sheria pia kushughulikia changamoto zote zinazokwamisha ustawi wa sekta ya ardhi hususan uondoaji kero zote zinazokwamisha matumizi bora ya ardhi kwa jamii.


  Akifafanua kuhusu nafasi ya Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi katika mkutano huo ameeleza kwamba kupitia mkutano huo wa kitaalam wa masuala ya Ardhi, Wizara hiyo inajifunza kuhusu  changamoto zitakazojitokeza na kuibuliwa ili ziwekwe kwenye mitaala kwa lengo la kuwaandaa watalaam watakaokuwa na uwezo wa kusuluhisha matatizo yote yanayojitokeza kwenye sekta hiyo.


  Amesema kuwa Sekta ya Elimu kupitia mkutano huo itaboreshwa kwa kupata nyongeza ya utalaam kutoka kwa wataalam kutoka Vyuo vikuu vya nchi mbalimbali za Bara la Afrika waliohudhuria mkutano huo na kuongeza kuwa Chuo Kikuu Ardhi nchini Tanzania ambacho kimebobea kwenye masuala ya Ardhi kitapata taarifa zaidi katika uboreshaji wa mitaala na mafunzo ya Programu za Utawala wa Ardhi, Ugawaji wa Ardhi na Upimaji wa Ardhi”


  Kwa Upande wake Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi Prof. Idrissa Mshoro akizungumza mara baada katika mkutano huo amesema kuwa wataalam wa Ardhi nchini Tanzania bado wana umuhimu mkubwa katika maendeleo ya sekta ya Ardhi na kufafanua kuwa wao kama chuo kinachozalisha watalaam wa Ardhi wanalo jukumu kuzalisha watalaam watakaofanya usimamizi thabiti wa Ardhi kukabiliana na changamoto zilizopo.


  “Sisi nafasi yetu kama Chuo Kikuu Ardhi ni kujua ni namna gani tunavyoweza kuzalisha wataalam wa kutosha wenye weledi watakaoweza kukabiliana na changamoto mbalimbali zilizoko kwenye sekta ya Ardhi pia kuhakikisha wataalam tunaozalisha wanakidhi ubora na matarajio ya wananchi” Amesema Prof. Mshoro.


  Amesema kuwa wanataaluma kutoka Tanzania watanufaika kutokana na mkutano huo kwa kuwa unawajumuisha watalaam wa Ardhi kutoka takribani nchi 9 watakaobadilishana uzoefu kuhusu changamoto mbalimbali za ardhi zinazojitokeza katika maeneo yao na namna wanavyozitatua.


  Aidha, amesema kuwa Sekta ya Ardhi nchini Tanzania bado inakabiliwa na uhaba wa watalaam wa kutosha  ambao wangeweza kusimamia maamuzi katika masuala ya Ardhi ngazi za chini na kuongeza kuwa ili kupata maamuzi na taarifa sahihi za ardhi ni lazima suala la uwepo wa watalaam hao liendelee kupewa kipaumbele.


  Kuhusu mchango wa watalaam hao katika utatuzi wa migogoro ya Ardhi amesema kuwa ipo haja ya watalaam waliopo kutumika ipasavyo kutatua migogoro inayojitokeza na kuwaletea manufaa wananchi ambao wanahitaji huduma za wataalam hao.


  Amesema kuwa kwa upande wa Serikali tayari watalaam wa sekta husika wamejipanga kuhakikisha kuwa wanapata suluhisho la mgogoro inayojitokeza kupitia sheria zilizopo.


  Mkutano huo unaohusisha Mtandao wa vyuo Vikuu ni wa nane  tangu kuanzishwa Mtandao wa EALAN mwaka 2009 ambapo kwa mwaka huu Chuo Kikuu Ardhi, Tanzania kimekuwa mwenyeji wa Mkutano huo kufuatia kuteuliwa kuwa kituo Maalum Cha Mafunzo ya Usimamizi wa Ardhi Barani Afrika.

  0 0

   Watetezi haki za watoto wakiwa katika picha ya pamoja baada katika mkutano wa kujadili juu ya kutaka sheria ya ndoa ya mwaka 1971 irekebishwe  uliofanyika jijini Dar es Salaam.
   Mkurgenzi wa Shirila Utu wa Mtoto, Koshuma Mtengeti akichangia maada katika mkutano wa kujadili ndoa za utotoni katika mkutano wadau wa masuala ya watoto uliofanyika jijini Dar es Salaam.
  Wadau wa masula ya watoto wakisikiliza maada katika mkutano wa kujadili ndoa za utotoni katika mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam.

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
  TAKWIMU zinaonyesha kwamba mimba za utotoni zimeongezeka kwa wastani wa asilimia nne kutoka asilimia 23 mwaka 2010,hadi kufikia asilimia 27,mwaka Jana kutokana na kukosa uwekezaji kwa watoto wa kike.

  Akizungumza kwenye mkutano wa Nijali Media Dialogue ulioandaliwa na Shirika la C-SEMA, Mwakilishi Mkazi Msaidizi wa Shirika la Umoja Wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu Duniani(UNFPA),Christina Kwayu, amesema wasichana wenye umri chini ya miaka  18 wamekuwa wakiolewa kwa idadi kubwa.

  Amesema ndoa hizo zinasababisha  kuwepo kwa mimba za utotoni na ndio nas kufanya wadau wa masuala ya watoto kupigia kelele juu ya sheria ya ndoa ya mwaka 1971 irekebishwe ili kuweza msichana kutimiza malengo yake.

  "Japo baadhi ya imani ya dini zinasema mtoto chini ya miaka 18 anaweza kuolewa lakini haijatoa nafasi ya kumlazimisha msichana kuolewa",amesema Kwayu.

  Naye Mkurugenzi Wa Shirika la Utu wa Mtoto, Koshuma Mtengeti, amesema kati ya watoto watano,watoto wawili wanaolewa hapa nchini.

  Amsema hukumu iliyoyolewa na mahakama kuu kuhusu umri wa mtu kuolewa kuwa ni miaka 18, itumiwe kama sehemu ya kuwashitaki wale wote wanaooa watoto.

  Mtengeti, mchakato wa kubadilisha sheria ya ndoa umefika katika hatua nzuri na kuwataka wadau wote kuwa na nguvu ya pamoja katika kumtetea msichana waTanzania.

  Amesema utekelezaji wa hilo litafanikiwa pale wadau wote wataposhinikiza wabunge kubadilisha sheria hiyo na kuwataka watunge Sera na sheria walichukue hilo na kulifanyia kazi.

  Kwa upande wake,Afisa Jinsia kutoka Shirika la Kimataifa  la Vijiji vya Watoto(SOs), Catherine Kasimbazi, alisema kubadilishwa kwa vipengele ambavyo vina mkandamiza mtoto ni hatua nzuri katika msichana kuweza kupata utu wake.

  Amesema dhamira ya Nijali ni kuwajali watoto na kwamba sheria ya ndoa ikibadilishwa usawa kati ya mtoto wa kike na wakiume utakuwepo.

  Mkutano huo ulioandaliwa na Csema kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Australia uliwashirikisha wadau mbalimbali wakiwemo wanachama wa Chama cha Waandishi wa Habari za watoto.

  0 0

   Mbunge wa jimbo la Ukonga, Mwita Waitara, akimkabidhi madawati mwalim Mkuu msaidizi wa Shule ya Msingi  Kerezange Dar es Salaam.
   Mbunge wa jimbo la Ukonga, Mwita Waitara, akimkabidhi mpira mwalimu wa michezo wa shule ya Msingi Kilimani, Abdull Mukhusini,  iliyopo Kipunguni wakati alipoenda kukabidhi madawati kwa shule tatu.
   Mbunge wa jimbo la Ukonga, Mwita Waitara akisalimiana na wanafunzi wa shule ya msingi  Kilimani  iliyopo Kipunguni wakati alipoenda kukabidhi  madawati kwa shule tatu za jimbo lake.
   Mbunge wa jimbo la Ukonga, Mwita Waitara akiongea na wanafunzi wa Shule ya msingi Kilimani iliyopo Kipunguni wakati alipoenda kukabidhi madawati kwa shule tatu za jimbo lake.
   Mbunge wa jimbo la Ukonga, Mwita Waitara, (kushoto) akimkabidhi madawati Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Serengeti, Marietha Mulalia iliyopo Kivule Dar es Salaam. 
  Mbunge wa jimbo la Ukonga, Mwita Waitara akiteta jambo na  wanafunzi wa Shule ya Msingi Kipunguni Dar es Salaam wakati alipokabidhi madawati kwa shule ya Msingi Kilimani.

  0 0

  Mwenyekiti wa CCM na Rais Mstaafu, Dkt Jakaya Kikwete akifungua Mkutano wa Kamati Kuu ya CCM kwenye ukumbi wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM mjini Dodoma Julai 21, 2016. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mtarajiwa, Rais John Magufuli, Wapili kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM , Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein, kuliani ni Makamu Mwenyekiti wa CCM , Bara, Philip Mangula na wapili kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana. 
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akimkaribisha Mwenyekiti wa CCM na Rais Mstaafu, Dkt Jakaya Kikwete kwa ajili ya kufungua Mkutano wa Kamati Kuu ya CCM kwenye ukumbi wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM mjini Dodoma Julai 21, 2016 pamoja na wajumbe wa mkutano huo. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mtarajiwa, Rais Dkt John Magufuli, Wapili kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM , Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein, kuliani ni Makamu Mwenyekiti wa CCM , Bara, Philip Mangula na wapili kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana. Kamati kuu hiyo ilikuwa ni kwa ajili ya kupendekeza jina la Dkt John Pombe Magufuli kuwa Mwenyekiti na baadae kuliwasilisha jina hilo kwenye Halmashauri kuu ya Taifa kwa ajili ya kupeleka kwenye mkutano unaotarajiwa kufanyika Julai 23,2016.
  Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo kabla ya kuanza kwa kikao chao kwenye ukumbi wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM mjini Dodoma.

  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akimkaribisha Mwenyekiti wa CCM Dkt Jakaya Kikwete
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akimpokea Makamu Mwenyekiti wa CCM , Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein pamoja na Mwenyekiti mtarajiwa,Rais Dkt Jonh Magufuli nje ya ukumbi wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM mjini Dodoma Julai 21, 2016.
  Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana kabla ya kuanza kwa kikao chao kwenye ukumbi wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM mjini Dodoma Julai 21, 2016.
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akimpokea Mwenyekiti Mtarajiwa wa CCM,Rais Dkt John Pombe Magufuli walipokuwa wakiwasili kwenye ukumbi wa Sekretarieti, katika jengo la White House, Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma, leo.Kamati kuu hiyo ilikuwa ni kwa ajili ya kupendekeza jina la Dkt Magufuli kuwa Mwenyekiti na baadae kuliwasilisha jina hilo kwenye Halmashauri kuu ya Taifa kwa ajili ya kupeleka kwenye mkutano.
  Mwenyekiti Mtarajiwa Dkt John Pombe Magufuli akiwasalimia baadhi ya wanachama na wafuasi wa chama cha CCM nje ya ukumbi wa ukumbi wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM mjini Dodoma Julai 21, 2016.
  Baadhi ya Wanahabari wakiwa kazini.

  Wajumbe wa mkutano huo wakijadiliana kabla ya kuaza Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM, kilichoongozwa na Mwenyekiti wa CCM, Dk Jakaya Kikwete katika jengo la White House, Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma, leo.Kamati kuu hiyo ilikuwa ni kwa ajili ya kupendekeza jina la Dkt Magufuli kuwa Mwenyekiti na baadae kuliwasilisha jina hilo kwenye Halmashauri kuu ya Taifa kwa ajili ya kupeleka kwenye mkutano.
   ajumbe wa mkutano huo wakijadiliana kabla ya kuaza Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM, kilichoongozwa na Mwenyekiti wa CCM, Dk Jakaya Kikwete katika jengo la White House, Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma, leo.Kamati kuu hiyo ilikuwa ni kwa ajili ya kupendekeza jina la Dkt Magufuli kuwa Mwenyekiti na baadae kuliwasilisha jina hilo kwenye Halmashauri kuu ya Taifa kwa ajili ya kupeleka kwenye mkutano.

     0 0


  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiongea na Mawaziri wanaoshiriki mkutano wa kumi wa Baraza la Mawaziri wa Maji wa nchi za Afrika (AMCOW) leo jijini Dar es slaam.
  Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge akimkaribisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akuongea na Mawaziri wanaoshiriki mkutano wa kumi wa Baraza la Mawaziri wa Maji wa nchi za Afrika (AMCOW) leo jijini Dar es slaam.
  Rais wa Baraza la Mawaziri wa Maji wa nchi za Afrika (AMCOW) ambaye pia ni Waziri wa Maji na Usafi wa Mazingira wa Senegal Amadou Mansour Faye akitoa hotuba ya baraza hilo kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan (hayupo pichani) leo jijini Dar es slaam.
  Mwenyekiti wa Maji na Uwezeshaji Afrika na Waziri wa Maji nchini Nigeria Mhandisi Suleiman Adamu akieleza hali ya maji ilivyo Afrika na namna ya kutumia maji kwa zaidi ya nchi moja ili kuwahudumia wananchi wa bara hilo wakati wa mkutano wa kumi wa Baraza la Mawaziri wa Maji wa nchi za Afrika (AMCOW) leo jijini Dar es slaam.
  Baadhi ya wajumbe wa mkutano wa 10 wa Baraza la Mawaziri wa Maji wa nchi za Afrika (AMCOW) wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan (hayupo pichani) leo jijini Dar es slaam.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan (wa nne kutoka kulia, walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na Mawaziri wanaoshiriki mkutano wa kumi wa Baraza la Mawaziri wa Maji wa nchi za Afrika (AMCOW) leo jijini Dar es slaam.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan (wa kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Mabalozi wanaowakilisha nchi mbalimbali nchini Tanzania wakati mkutano wa kumi wa Baraza la Mawaziri wa Maji wa nchi za Afrika (AMCOW) leo jijini Dar es slaam.

  (Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO)

  0 0


  Jengo la Ofisi Kuu ya Chama cha Ushirika KCU 1990 LTD Mkoani Kagera
  Kaimu Mrajisi wa Vyama Vya Ushirika Nchini Dkt. Audax Peter Rutabanzibwa (Kulia) Akiongea na Waandishi wa Habari Mkoani Kagera Mara Baada ya Kuwasilisha Uamuzi wa Serikali
  Kaimu Mrajisi wa Vyama Vya Ushirika Nchini Dkt. Audax Peter Rutabanzibwa.
   
  SERIKALI YAKINUSURU CHAMA KIKUU CHA USHIRIKA CHA KCU 1990 LTD MKOANI KAGERA.

  ·         Bodi na Meneja Mkuu wa KCU 1990 LTD Wasimamishwa Kazi Kuanzia Sasa
  ·         Nafasi ya Mrajisi Msaidizi Kagera yasitishwa na Kuteuliwa Mwingine.
  ·         Akaunti zote za KCU 1990 LTD Zasitishwa Kupisha Uchunguzi

  Bodi ya Chama Kikuu cha Ushirika Mkoani Kagera, Kagera Co operative Union 1990 LTD (KCU) pamoja na Meneja Mkuu wa Chama hicho na Mrajisi Masidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoani Kagera wamesimamishwa kazi kuanzia leo tarehe 21.07.2016 kwa tuhuma za ubadhilifu zaidi ya shilingi milioni 900 pamoja na kuingia mikataba yenye harufu ya rushwa iliyopelekea hasara kubwa kwa Chama hicho Kikuu cha Ushirika Mkoani Kagera.

  Kaimu Mrajisi wa Vyama vya Ushirika Nchini Dkt. Audax Peter Rutabanzibwa akitangza rasmi kusimamishwa kwa Bodi ya KCU pamoja na Meneja Mkuu wa Chama hicho cha Ushirika alisema kuwa Bodi hiyo ikishirikiana na Meneja Mkuu Bw. Vedastus Ngaiza walitoa taarifa za uongo katika Mkutano Mkuu wa Chama hicho wa mwezi Mei 2016 kuhusu deni wanalodaiwa na Benki ya CRDB.

  Dkt. Rutabanzibwa alisema baada ya kutuma wakaguzi kutoka ofisi ya Mrajisi wa Vyama vya Ushirika nchini, Wakaguzi hao walibaini kuwa taarifa waliyosomewa wananchama katika mkutano ilitaja kuwa deni lilikuwa Shilingi bilioni 2.8 kumbe haikuwa kweli kwani deni lilikuwa limepanda hadi shilinngi bilioni 3.15 Bodi na Meneja Mkuu walikuwa wamewadanganya wanachama wa chama hicho.

  Pili, Wakaguzi hao waligundua kuwa shilingi Milioni 124 zilitumika katika malipo na hakukuwa na maelezo ya kutosheleza kuhusu malipo ya fedha hizo. Tatu, KCU iliingia mikataba ya kukodisha majengo yake amabayo haikufuata bei ya soko kwa sasa, na mikataba hiyo ilifungwa kwa makubaliano ya miaka 10 jambo ambalo linapelekea Chama hicho kulipwa pango kwa bei ya chini kabisa isiyoendana na soko.

  Nne, Chama Kikuu cha Ushirika Mkoani Kagera KCU kimekuwa kikinunua kahawa ya kiwango cha chini kabisa na kusababisha hasara kubwa. Tano, Chama cha KCU kilijiingiza kataika miradi isiyokuwa na tija kama mradi wa kununua maharage ambao ulikisababishia hasara kubwa Chama hicho.

  Dkt. Rutabanzibwa alisema kuwa kutokana na sheria Na. 6 ya mwaka 2003 inayohusu usimamizi wa Vyama vya Ushirika nchini Bodi ya KCU hakufanya kazi yake ipasavyo ya kukisimamia vizuri chama hicho Aidha, Bodi hiyo ilifanya vikao 12 kwa mwaka jana 2015 vikao ambavyo vinaonekana havikuwa na tija kwani pamoja na vikao hivyo vya Bodi kufanyika bado kulikuwa na ubadhirifu mkubwa wa fedha.

  MAELEKEZO

  Dkt. Ruatabazibwa baada ya kutaja ubadhirifu uliofanyika katika Chama Kikuu cha Ushirika KCU alisema kuwa Serikali imeamua kuchuka hatua zifuatazo;

  1. Kufuta Bodi ya Chama Kikuu cha Ushirika Mkoani Kagera KCU iliyoteuliwa mwaka 2014

  2. Kusitisha ajira ya Meneja Mkuu wa KCU Bw. Vedastus Ngaiza mpaka hapo uchunguzi wa tuhuma za ubadhirifu wa fedha utakapokamilika.

  3. Kusitisha nafasi ya Mrajisi Msaidizi wa Mkoa wa Kagera Bw. Nestory Shorozi kwani ubadhirifu huo ulifanika yeye akiwepo bila kukishauri vizuri Chama hicho Kikuu cha Ushirika .

  4. Akaunti zote za Chama cha Ushirika KCU kusimamishwa mara moja mpaka hapo utaratiibu mzuri utakapokuwa umewekwa .  KUNUSURU CHAMA

  Dkt. Rutabanzibwa alisema kuwa katika kukinusuru Chama Kikuu cha KCU pia na kuendelea na Msimu wa manunuzi ya kahawa Serikali imefanya uteuzi mdogo wa Mrajisi Msaidizi Bw, Robert Makene Mtambo kutoka Ukerewe Mkoani Mwanza atakayeshikiria kwa muda nafasi ya Bw. Nestory Shorozi aliyekuwa Mrajisi Msaidizi wa Mkoa wa Kagera.

  Aidha mrajisi Msaidizi aliyeteuliwa Bw. Mtambo atakaimu nafasi ya Meneja Mkuu wa KCU iliyokuwa ikishikiliwa na Bw. Vedastus Ngaiza. Katika kukaimu nafasi hiyo Bw. Mtambo atatakiwa kuitisha Mkutano Mkuu wa wanachama wa KCU ndani ya mwezi mmoja na katika mkutano huo atateuliwa Mwenyekiti ambaye atatakiwa kusoma taarifa halisi ya KCU iliyotakiwa kusomwa mwezi Mei 2016 katika Mkutano Mkuu.

  Adha Dkt. Rutabanzibwa alisema Serikali haikukurupuka kuchukua hatua hiyo bali ilifanya uchunguzi wa kutosha ikiwa ni pamoja kuipa bodi nafasi ya kujieleza lakini haikutoa maelezo ya kutosha na badala ya kupunguza deni wao waliliongeza deni likapanda zaidi. Pia Dkt. Rutabanzibwa aliviagiza vyombo vya uchunguzi kama TAKUKURU, Polisi na Usalama kuanza kulifanyia kazi suala hilo mara moja.

  Kaimu Mrajisi wa Vyama Vya Ushirika Dkt. Audax Peter Rutabanzibwa alimalizia kwa kusema kuwa Serikali imeamua kulifanyia kazi suala la VyamaVikuu vya Ushirika nchini kwani vyama hivyo vimeonekana kuwa badala ya kuwasaidia wakulima vinawadidimiza ambapo alisema walianzia Mwanza, sasa Kagera, na wanaelekea Mikoa ya Geita, Simiyu, na Shinyanga.

   

  0 0


  Meneja wa kituo cha huduma kwa Wateja Bw.Juma Msabaha akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na uzinduzi wa kituo cha huduma kwa wateja kilichozinduliwa hii leo Makao makuu ya Benki hiyo,Golden Jubilee towers Daresalam. Sasa wateja na wasiokuwa wateja wa benki hiyo wataweza kupata maelezo kuhusiana na mikataba ya mikopo inayofuata mifumo ya kiislamu, kutoa msaada katika matumizi ya huduma zetu mbadala kama ATM, Internet Banking, Amana Bank Mtaani, Amana Mobile na huduma nyingine mbalimbali.
  Sehemu ya waandishi wa habari waliohudhuria Mkutano huo wakisikiliza kwa makini uzinduzi wa kituo hicho. Imeelezwa kuwa kituo hicho kitasaidia kusogeza huduma karibu na wananchi na kutatua baadhi ya kero ambazo wateja walikuwa wanakutana nazo.
  Mkuu wa biashara wa AMANA BENKI Bw. Munir Rajab akifafanua jambo kuhusu kituo hicho.


  NA SELEMANI MAGALI- DARESLAAM

  BENKI ya Kiislamu ya Amana imezindua kituo chake kipya cha huduma kwa wateja kwa njia ya mawasiliano ya simu ikiwa ni sehemu ya mkakati wao wa kuboresha huduma kupitia teknolojia ya mawasiliano
   
  Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam,Meneja Mwandamizi Huduma kwa wateja wa Benki hiyo Bw. Juma Msabaha alisema uzinduzi wa kituo hicho umelenga kuboresha mahusiano ya wateja pamoja na kusogeza huduma za kibenki karibu na wananchi.

  Akifafanua kuhusu kituo hicho, Bw. Msabaha alisema kituo hicho kitafanya kazi kwa masaa 15 kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa nne usiku ambapo wateja wa Amana na ambao bado hajabahatika kutumia huduma za benki hiyo watapata fursa ya kuuliza masuala mbalimbali kuhusu huduma zinazotolewa na Benki.

  “Tumejipanga vizuri, tunayo timu nzuri yenye uzoefu na masuala ya Kibenki ,watafafanua mambo mbalimbali kuhusu huduma za Amana benki kuanzia masuala ya akaunti,miamala ya kimtandao na huduma zinazotolewa na mawakala wetu kote nchini.Alisema Msabaha.

  Ameongeza kusema Kituo hicho kitafanya kazi siku saba katika wiki,pamoja na siku za siku kuu jambo ambalo wanaamini litasaidia kufafanua mambo mbalimbali yanayowahusu wateja.

  “Namba yetu ya huduma kwa mteja ni 0657 980 000, kupitia namba hiyo ni matarajio yetu kuwa wateja watafurahia zaidi huduma tuliyoizindua kwani ni rafiki kwa kila mmoja, imeandaliwa mahususi kabisa kuwapa uwezo wananchi kupiga simu,kutuma ujumbe mfupi pamoja na njia zingine za mitandao ya kijamii”.Alisema Msabaha

  Kwa mujibu wa Bw Msabaha kituo hicho kinatarajiwa kuleta mabadiliko kwenye biashara kupitia huduma za kibenki huku akiongeza: “Ni adhma yetu kuhakikisha kwamba tunapambana siku zote ili tu hali ya kiuchumi kwa wateja wetu iendelee kuwa bora na ni hicho tu ndio kimekuwa kikitusaidia kuwa na matokeo mazuri

  Alibainisha kuwa huduma hiyo ilibuniwa mahususi ili kuleta tija kwa wateja wa benki hiyo kwa kuwa inaenda sambamba na mahitaji yao, mfumo wao wa maisha pamoja na hadhi yao hatua aliyoilezea kuwa itaiongezea benki hiyo uaminifu miongoni mwa wateja wake

  Kwa upande wake Mkuu wa idara ya Biashara ya Amana Benki Bw. Rajab Munir amesema wateja wa Amana watapata fursa ya kuijua benki yao kwa undani kwani sasa wanaweza kuulizwa maswali yao na kujibiwa kwa wakati ndani ya masaa 15 katika wiki ikiwamo siku za siku kuu.

  Alisema hiyo ilikuwa dhamira yao ya muda mrefu na kuzinduliwa kwake imekuwa ni faraja kwa wateja ambao sasa watafaidika nayo.kwa kupata majibu ya papo kwa hapo kuhusiana na akaunti zao, miamala yao na misaada kuhusu kutumia huduma za kimtandao.

  katika kipindi kisichopungua miaka mitano Tayari Benki ya Amana kwa imefanikiwa kuwa na matawi saba matano yakiwa katika Jiji la Daresalaam na mengine mawili yakiwa katika Jiji la Mwanza na Arusha.

  Mipango ya Baadae ni kwamba Amana benki inatarajia kufungua matawi mengine si chini ya matatu kati ya Mkoa wa Tanga au Zanzibara kulingana na upembuzi yakinifu utakaofanywa na benki hiyo.

  0 0

  Ofisa Uchumi  wa Idara ya Afrika wa Nchi Zinazoendelea  kutoka Geneva (Unctad), Claudia Roethlisberger, akizungumza na wadau mbalimbali wa masuala ya uchumi wakati wa uzinduzi wa ripoti ya maendeleo ya kiuchumi barani Afrika iliyofanyika jijini Dar es Salaam,jana. Kulia ni Ofisa habari Umoja wa Mataifa Kitengo cha Mawasiliano (UNIC),Stellah Vuzo.
   Ofisa habari Umoja wa Mataifa Kitengo cha Mawasiliano (UNIC),Stellah Vuzo,akizungumza katika uzinduzi wa ripoti hiyo ya maendeleo ya kiuchumi barani afrika. Kushoto ni Ofisa Uchumi  wa Idara ya Afrika wa Nchi Zinazoendelea  kutoka Geneva (Unctad), Claudia Roethlisberger.
  Mtafiti wa Shirika linalojishughulisha na masuala ya utafiti wa masuala ya uchumi (REPOA),Stephen Mwombela,akichangia mada katika mkutano huo.
  Wadau mbalimbali wa masuala ya uchumi nchini wakifuatilia kwa makini uzinduzi wa ripoti hiyo .

  ………………
  NA ELISA SHUNDA

  SERIKALI za Afrika zimeshauriwa kuchukua hatua ya kuzuia ukuaji wa madeni ya mataifa yao ili kuepusha migogoro inayoweza kutokea kama iliyowahi kutokea miaka ya mwishoni mwa 1980 na 1990.Pia zimetakiwa kuongeza vyanzo vipya vya mapato kwaajili ya kugharamia maendeleo ya nchi zao.

  Kauli hiyo imetolewa jijini hapa jana na Ofisa Uchumi Idara ya Afrika,Nchi zinazoendelea ambaye ni mwakilishi kutoka Geniva, Claudia Reothlisberger, wakati alipokuwa akizindua Ripoti ya Maendeleo ya Kiuchumi Barani Afrika.“Ripoti hii ya UNCTAD inayozinduliwa leo(jana) inayohusu Maendeleo ya Uchumi barani Afrika, lakini tufahamu imekuwa ikichapishwa kila mwaka kuanzia mwaka 2000,lengo likiwa ni kuzisaidia nchi za Afrika kukabiliana na hasara ya uwezekano wa ushirikiano mkubwa wa kiuchumi na uchumi wa dunia kwa kufanya utafiti na uchambuzi sambamba na kujenga maridhiano na ushirikiano wa kiufundi,

  “Ripoti hii ambayo imezinduliwa chini ya Umoja wa Mataifa kuhusu Biashara na Maendeleo (UNCTAD), inasisitiza kuwa kukopa inaweza kuwa sehemu muhimu ya kuboresha maisha ya wananchi wa afrika lakini lazima kupata uwiano kati ya wakati wa sasa, na baadaye kwa sababu madeni ni hatari yanapokuwa sio endelevu” alisema.

  Aidha alisema kwa mujibu wa ripoti hiyo ilibaini kuwa angalau dola za kimarekani bilioni 600 zinahitajika kila mwaka ili kufikia Malengo ya Maendeleo endelevu(SDGs) barani Afrika.Alisema licha ya ripoti hiyo kubaini pia kwa sasa nchi nyingi za afrika zimeanza kuondokana na utegemezi wa misaada rasmi ya maendeleo kutokana na kutumia vyanzo vyake vipya vya fedha na vyenye ubunifu lakini zinapaswa kuangalia vyanzo vya mapato vya nyongeza ambavyo vitasaidia afrika kufikia malengo yake.

  “Ripoti hii ambayo pia imepewa kichwa kidogo kuwa Mienendo ya Madeni na Fedha za maendeleo barani afrika ilionyesha kuwa zipo nchi kadhaa za Afrika zilikopa sana katika masoko ya ndani, na nchi hizo ni Nigeria, Ghana, Kenya,Tanzania na Zambia” alisema.Kwa upande wake Mchumi kutoka Benki ya Maendeleoa ya Afrika(AfDB), Prosper Charles alisema kuwa ni wakati sasa serikali kuwa macho na hatari za kukopa kutokana na masharti magumu yaliyopo katika kipindi hiki.

  “Ili kufikia malengo endelevu ya  ya millennia ni lazima serikali ijizatiti kutekeleza miradi yake haswa mipango yake ambayo itasaida kuondokana na hatari ya deni la taifa”alisema.

  Imeandaliwa na Shunda blog/elisashunda@gmail.com/0719-976633.

  0 0


  Meneja wa Mtambo wa Ruvu Chini Mhandisi Emmanuel Makusa akiwaelezea baadhi ya Mawaziri wa Maji wa nchi za Afrika waliotembelea mtambo huo kujifunza namna Tanzania inavyojidhatiti kuwapatia maji wananchi wake.
  Baadhi ya Mawaziri wa Maji wa nchi za Afrika wakitembelea maeneo mbalimbali ya mtambo Ruvu Chini kujifunza namna Tanzania inavyojidhatiti kuwapatia maji wananchi wake.
  Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwewe akiwaeleza baadhi ya Mawaziri wa Maji wa nchi za Afrika namna mradi wa Ruvu Chini unavyowahudumia baadhi ya wakazi wa wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani na wakazi wa mkoa wa Dar es salaam.
  Mhifadhi wa Mji Mkongwe wa Bagamoyo Noel Laswai akiwaeleza baadhi ya Mawaziri wa Maji wa nchi za Afrika namna mji wa kale wa Kaole ulivyokuwa tangu karne ya 13.
  Mhifadhi wa Mji Mkongwe wa Bagamoyo Noel Laswai akiwaeleza baadhi ya Mawaziri wa Maji wa nchi za Afrika mti aina ya mpingo unaohifadhiwa katika eneo la Kaole namna unavyotumiwa ambao mti huo una zaidi ya miaka 30.
  Waziri wa Mji wa Namibia Anna Shiweda na Waziri wa kutoka nchini Libya Assayed Abdurrahaman Naji wakiangalia baadhi ya mabaki ya viumbe vinavyoishi baharini katika ufukwe wa Bagamoyo wakati wa ziara ya kujifunza namna Tanzania inavyotunza rasilimali zake kwa mnaufaa ya sasa na baadaye.
  Madhari za baadhi ya maeneo ya fukwe za wilaya ya Bagamoyo zinavyovutia kwa utalii na michezo mbalimbali. (Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO)

  Na Eleuteri Mangi-MAELEZO

  Mawaziri wanaoshiriki mkutano wa kumi wa Baraza la Mawaziri wa Maji wa nchi za Afrika wametembelea chanzo cha maji cha Ruvu Chini uliopo Bagamoyo Mkoani Pwani kwa lengo la kujionea namna Tanzania ilivyojizatiti katika kuhakikisha wananchi wanapata maji ya uhakika wakati wote.

  Akizungumzia ziara hiyo, Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwewe amesma kuwa mradi wa Ruvu Chini unahudumia baadhi ya wakazi wa wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani na wakazi wa mkoa wa Dar es salaam.

  Mhandisi Kamwewe aliwaambia Mwaziri hao kuwa chanzo hicho cha maji kinauwezo wa kuzalisha maji yapatayo lita milioni 275 kwa siku ambapo jiji la Dar es salaam peke yake wakazi wake wapatao zaidi ya milioni tano wanatumia maji kiasi cha lita milioni 450 kwa siku.

  Kiasi kingine cha maji mengine ambayo yanatumika jijini dare s salaam Mhandisi Kamwewe alisema kuwa yanazalishwa katika chanzo cha maji cha Ruvu Juu ambapo zinazalishwa lita milioni 186 kwa siku.

  Mhandisi Kamwewe aliongeza kuwa ili kuhakikisha wananchi wanapata maji ya uhakika kwa wakazi wa mikoa ya Pawani na Dar es salaam kwa manufaa ya maendeleo yao na kwa ujmla taifa.

  Aidha, Serikali inaendelea kuhakikisha miundombinu ya maji inakuwa imara na bora wakati wote ambapo kwa sasa uboreshaji wa mabomba unafanyika mara kwa mara ambapo mabomba ya zamani yanaendelea kubadilishwa na kuimarishwa matanki ya maji yaliyopo eneo la chuo kikuu cha Ardhi, Kimara na Kibamba.

  Kwa upande wake Mwakilishi wa Mawaziri wa Maji waliotembelea mradi huo wa Ruvu Chini Mhe. Anna Shiweda kutoka nchini Namibia amesema kuwa wamefurahishwa na Tanzania jinsi ilivyojipanga kuwahakikishia wananchi wake wanapata maji kwa maendeleo yao na wame wamevutiwa kwa jinsi chanzo hicho cha maji kilivyo na vifaa vya kisasa.

  Akizunguzia upatikanaji wa maji katika nchi yake, Mhe. Anna amesema kuwa nchi yao ni miongoni mwa nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara ambapo eneo kubwa linakabiliwa na ukame ambapo wakazi wa nchi hiyo maji hupatikana kwa zaidi ya kilometa 250.

  “Mkutano wetu umekuwa wa manufaa sana, tumefurahishwa na Tanzania kwa namna ilivyojidhatiti kuwapatia wananchi wake maji, tumejifunza na tunayachukua mawazo haya kwa manufaa ya nchi zetu” alisema Mhe. Anna.

  Mhe. Waziri Anna amesema kuwa Namibia ina changamoto ya kuwa na ukame ambao unalikumba taifa hilo lenye idadi ya watu zaidi ya milioni 2.3, kutoka Tanzania wamejifunza mambo muhimu kupitia mkutano huo na Namibia imejipanga kutumia teknolojia inayotumia Tanzania ili nao waweze kuwahudumia raia wake waweze kupata maji safi na salama.

  Maonesho ya wiki ya maji yanayofanyika Dar es salaam yanahudhuriwa na Mawaziri wa Maji kutoka nchi 38 zikiwemo Tanzania ambayo ni mwenyeji wa maonesho hayo, Sudan, Kongo, Lesotho,Madagaska, Burundi, Namibia, Nigeria, Rwanda, Senegal, Togo, Liberia, DRC na Zimbabwe.

  Nchi nyingine zilizoshiriki ni pamoja na Libya, Kenya, Misri, Ivory Coast, Cameroon, Msumbiji, Zambia, Sudan Kusini, Bukina Fasso, Afrika Kusini, Mali, Ethiopia, Benin, Mauritania, Uganda na Djibouti.

older | 1 | .... | 912 | 913 | (Page 914) | 915 | 916 | .... | 1897 | newer