Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 911 | 912 | (Page 913) | 914 | 915 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Mwakilishi Maalumu wa masuala ya maji kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Watu wa Kenya Mwai Kibaki ametembelea mabanda ya maonesho ya sita katika ya wiki ya maji Afrika yanayoendelea jijini Dar es salaam.

  Katika tukio hilo Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Mhandisi Emmanuel Kalobelo amimweleza Mwakilishi huyo kuwa Tanzania imejipanga kuhakikisha kuwa hadi ifikapo 2020 iweze kufikisha maji kwa wananchi wote kwa maendeleo yao na taifa kwa ujumla.

  Mhandisi Kalobelo aliongeza kuwa hatua hiyo itaifanya Tanzania kufikisha maji kwa wakazi wa mijini kwa asilimia 95 na kwa wakazi wa vijijini kw asilimia 85.

  Aidha, katika hatua nyingine, Mwakilishi huyo alitembelea barabara iliyopewa jina la Mwai Kibaki inayoanzia eneo la Morocco hadi njia panda ya Kawe jijini Dar es salaam pia alitembelea na daraja la Mwalimu Nyerere linalounganisha eneo la Kigamboni kupitia bahari ya Hindi na eneo la katikati ya jiji la Dar es salaam.

  Maonesho ya sita katika ya wiki ya maji Afrika mwaka huu yanayoendelea jijini Dar es salaam yanaongozwa na kaulimbiu inayosema “Kufikia lengo la Mendeleo Endelevu (SDGs) juu ya Usalama wa Maji na Usafi wa Mazingira”.

  Mwakilishi Maalumu wa masuala ya maji kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Watu wa Kenya Mwai Kibaki (kushoto) akisalimiana na Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya Maonesho ya Wiki ya Maji Afrika (Sylivester Matemu) wakati wa maonesho ya sita katika ya wiki ya maji Afrika yanayoendelea jijini Dar es salaam. Katikati ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Mhandisi Emmanuel Kalobelo.
  Mwakilishi Maalumu wa masuala ya maji kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Watu wa Kenya Mwai Kibaki akisalimia na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Mhandisi Emmanuel Kalobelo leo jiji Da es salaam.
  Katibu wa Mwakilishi Maalumu wa masuala ya maji kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Watu wa Kenya Mwai Kibaki (katikati), Profesa Nick Wanjohi akifafanua jambo kwa mwakilishi huyo alipotembelea na daraja la Mwalimu Nyerere linalounganisha eneo la Kigamboni kupitia bahari ya Hindi na eneo la katikati ya jiji la Dar es salaam. 
  Katibu wa Mwakilishi Maalumu wa masuala ya maji kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Watu wa Kenya Mwai Kibaki (katikati), Profesa Nick Wanjohi akifafanua jambo kwa mwakilishi huyo alipotembelea na daraja la Mwalimu Nyerere linalounganisha eneo la Kigamboni kupitia bahari ya Hindi na eneo la katikati ya jiji la Dar es salaam.

  0 0

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji - Dk. Adelhelm Meru (katikati) akipiga kengele kuashiria kuorosheshwa rasmi hati fungani za Benki ya NMB kiasi cha shilingi Bilioni 41.4 leo katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE). Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa NMB, Bi. Ineke Bussemaker pamoja na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), Moremi Marwa (Kulia). Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji - Dk. Adelhelm Meru (kulia) akimpongeza Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker (kushoto) mara baada ya tukio la Benki ya NMB kuoroshesha rasmi hati fungani kiasi cha shilingi bilioni 41.4 katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE). Ofisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), Moremi Marwa (Kushoto) akimpongeza Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker (kulia) mara baada ya tukio la Benki ya NMB kuoroshesha rasmi hati fungani kiasi cha shilingi bilioni 41.4 katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE). Mmoja wa maofisa waandamizi wa DSE (aliyeshika kengele) akiongoza hafla ya Benki ya NMB kuoroshesha rasmi hati fungani kiasi cha shilingi bilioni 41.4 katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE). Wengine kutoka kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa DSE, Moremi Marwa, Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dk. Meru na Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker wakishuhudia. Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker akizungumza katika hafla ya benki hiyo kuoroshesha rasmi hati fungani kiasi cha shilingi Bilioni 41.4 leo katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE). Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dk. Adelhelm Meru akizungumza katika hafla ya benki hiyo kuoroshesha rasmi hati fungani kiasi cha shilingi Bilioni 41.4 leo katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE).

  BENKI ya NMB leo imeorodhesha kiasi cha shilingi Bilioni 41.4 ilichokipata kutokana na mauzo ya hati fungani katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE). Tukio hilo limezinduliwa rasmi leo jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dk. Adelhelm Meru kwa ishara ya kupiga kengele kwenye ofisi za DSM. Akizungumza katika hafla hiyo Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji - Dk. Meru alipongeza hatua hiyo ya kuorodhesha hati fungani kwenye soko la hisa na kuongeza kuwa ni ya kizalendo na kuwataka wawekezaji katika sekta binafsi kushiriki kikamilifu. “Hati fungani hii inatarajiwa kuleta maendeleo katika soko la mitaji na inafungua njia kwa mashirika mengine binafsi, mashirika ya serikali na mamlaka za manispaa kutafuta njia mpya za kukuza mitaji na uwezeshaji” alisema Dk. Adelhelm.

  Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa NMB - Ineke Bussemaker alisema “Hati fungani hii ya miaka mitatu si tu imeleta msisimko chanya kwenye soko la mitaji bali hata katika soko la hisa, NMB inakuwa benki ya kwanza kupata Kiwango zaidi ya mara mbili ya Kiwango tulichoomba awali.” Bi Ineke aliongeza kuwa mwitikio chanya kwenye hati fungani ya NMB unatoa somo kuwa kuna umuhimu wa benki mbalimbali kuchangia kwa Kiwango kikubwa katika kuendeleza masoko ya mitaji na pia kupigania elimu ya fedha kwa jamii. Hati fungani inayoorodheshwa leo ina riba ya asilimia 13 kwa mwaka na iitakomaa baada ya miaka miatatu.

  Bi Ineke alisema Kutolewa kwa hati fungani ya NMB ni sehemu ya mkakati wa benki kutafuta njia mbadala za vyanzo vya fedha. Fedha zilizopatikana kwenye hati fungani zitatumika kwaajili ya kutoa mikopo kwa wateja, wateja watakaonufaika ni pamoja na wateja binafsi, wafanyabiashara wadogo, wa kati na wakubwa pamoja na taasisi za serikali. Akiongea kwenye hafla hiyo, Afisa Mtendaji Mkuu wa DSE - Moremi Marwa alisema “mafanikio ya Hati fungani ya NMB yanatuambia kuwa wawekezaji wanajua uwepo wa fursa zilizopo katika masoko ya mitaji na wana uwezo na hamu ya kusaidia wale walio na uhitaji wa kukuza mitaji yao.”

  Hati fungani ya NMB ilipata mwitikio chanya kutoka kwa wawekezaji na kupita Kiwango kilichopangwa awali kwa asilimia 107. Benki ilipata maombi 1,811 yenye thamani ya shilingi bilioni 41.4 huku maombi mengi yakirundikana wiki ya mwisho kabla ya kufunga upokeaji wa maombi. Kutokana na kuorodheshwa kwenye soko la hisa, wawekezaji wataweza kuuza hati fungani zao kupitia soko la hisa la Dar es Salaam – DSE. Stanbic Bank Tanzania Ltd. Ndio wawezeshaji wa hati fungani ya NMB huku makampuni ya Orbit Securities Ltd. na EA Capital Ltd wakiwa kama mawakala viongozi.

  0 0

  Naibu Waziri ofisi ya Makamu wa Raisi Mazingira Mheshimiwa Luhaga Mpina akiwasha mtambo wa kusafirisha majitaka kiwandani hapo mara baada ya kuzindua rasmi katika hafla iliyofanyika katika kiwanda hicho Temeke Jijini Dar es salaam. 
  Naibu Waziri ofisi ya Makamu wa Raisi Mazingira Mheshimiwa Luhaga Mpina akiongea na wafanyakazi wa kiwanda cha bia ya serengeti mara baada ya uzinduzi wa bomba la kudhibiti majitaka katika kiwanda hicho Jijini Dar es salaam. 
  Naibu Waziri ofisi ya Makamu wa Raisi Mazingira Mheshimiwa Luhaga Mpina , Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Helene Weesie na waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini jinsi mtambo wa kusafirisha majitaka unavyofanya kazi kutoka kwa mmoja wa wasimamizi wa mradi huo. 
  Naibu Waziri ofisi ya Makamu wa Raisi Mazingira Mheshimiwa Luhaga Mpina (katikati) akifurahi jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Helene Weesie mara baada ya kukata utepe katika mtambo kusafirisha majitaka katika hafla iliyofanyika mapema leo kiwandani hapo.


   Kampuni ya Bia ya Serengeti leo imezindua bomba la kudhibiti wa majitaka ambalo linalenga kuhakikisha kiwango cha juu kiafya kwa kampuni, mazingira na wakazi wa maeneo yaliyo karibu.

  Bomba hilo limejengwa chini ya usimamizi wa Kampuni ya Maji Safi na Taka  ya Dar es Salaam (Dawasco), Mamlaka ya Barabara (Tanroads) na Halmashauri ya Manispaa ya Temeke likihusisha takribani kilometa mbili kuanzia katika kiwanda cha bia cha Serengeti kilichpo Temeke hadi Kurasini ambako ndip ulipo mfumo wa majitaka wa Dawasco.

  Akizungumza wakati wa uzinduzi, huo Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Helene Weesie, alisema kwamba mradi huo wa aina yake na wa kwanza nchini unadhihirisha juhudi zisizo na ukomo za kampuni hiyo katika kuhifadhi mazingira.

  “Ubora wa maji ni jambo lililo mstari wa mbele katika utengenezaji wa bia lakini suala la usafi kutokana na kuzalishwa kwa majitaka ni sehemu kubwa inayotujengea hisia za kimazingira katika shughuli za kutengeneza bia. Kwa hiyo uzinduzi wa bomba hili ni moja ya hatua ya kusonga mbele katika kuhakikisha yanakuwepo mazingira safi kiafya,” alisema Weesie.

  Mkurugenzi Mtendaji huyo alibainisha kwamba majitaka yanayotolewa na bomba hilo yatakuwa yanafanyiwa tiba kwanza ili kuondoa aina yoyote ya sumu kabla ya kuachiwa ili kuingia katika mfumo wa majitaka wa Dawasco.

  Alisema kuwa uzinduzi huyo uko katika mkondo mmoja na sera ya Kampuni ya Serengeti ya kujikita katika ustawi wa jamii ambayo imeainishwa katika maeneo manne ya vipaumbele ambavyo vinajumuisha, Utoaji wa Stadi za Maisha, Uendelevu wa Mazingira na Kuboresha Unywaji wa Kistaarabu.

  Mgeni rasmi katika uzinduzi huo Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Masuala ya Muungano na Mazingira, Mh. Luhanga Mpina aliipongeza Serengeti kwa kuzindua bomba hilo akibainisha kwamba ujenzi unaendana na ajenda ya serikali ya uhifadhi wa mazingira.

  Mpina alibainisha kwamba uchafuzi wa mazingira katika miji na maeneo ya pembezoni unaathiri afya za watu wengi na kupunguza tija inayotokana na mazingira na kutoa wito kwa makampuni mengine kuiga kazi nzu 

  0 0

  Na Lydia Churi- Mahakama ya Tanzania 

  Mahakama ya Tanzania imeamua kuchukua juhudi za makusudi ili kubadilisha muonekano wake na kuwa chombo kitakachojibu maswali na kuondoa kiu ya watanzania katika kupata haki kwa wakati.

  Akifungua Mkutano wa Mahakama ya Tanzania na wadau wake wa kujadili utekelezaji wa Mpango Mkakati wa mhimili huo leo mjini Dodoma, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu kanda ya Dodoma Mheshimiwa Mwanaisha Kwariko amesema Mahakama ya Tanzania inakusudia kukibadilisha chombo hicho ili kiweze kutoa haki kwa wakati kwa mujibu wa jukumu ililopewa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 

  Alisema katika kufanikisha azma hiyo, Mahakama ya Tanzania inaendelea na mafunzo ya wiki mbili kwa watumishi wake yanayolenga kuuboresha Mpango Mkakati wake kwa kushirikiana na wadau ili kuhakikisha wananchi wanapata haki kwa wakati na taswira ya mahakama inakuwa chanya wakati wote.

  Jaji Kwariko amesema Mahakama imeamua kuwashirikisha wadau kwenye Mpango Mkakati wake kwa kuwa umuhimu na nguvu waliyonayo Sitasaidia kufanikisha utendaji wa Mahakama katika kuyafikia malengo ya kutoa huduma bora kwa wananchi.

  Aidha, Jaji Kwariko aliwataka watumishi wa Mahakama ya Tanzania kufanya kazi kwa bidii katika kuutekeleza Mpango Mkakati kwa kuwa utendaji kazi wao utapimwa kwa jinsi watakavyotekeleza majukumu yao kulingana na Mpango Mkakati huo. Aliongeza kuwa Mahakama ya Tanzania itaelekeza rasilimali zake zote kama vile watu, fedha na muda katika kuleta matokeo makubwa yanayotarajiwa.

  Alisema endapo watumishi hao watajikita katika kufanikisha uimara wa nguzo zote tatu za Mpango Mkakati huo, upatikanaji wa haki kwa wakati na uhusishwaji wa wadau na imani ya wananchi vitakifanya chombo hicho kutimiza ndoto yake na kuifikia dira yake. Nguzo tatu za Mpango Mkakati huo ni Utawala bora, Uwajibikaji na Usimamizi wa rasilimali.

  Naye Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mheshimiwa Katarina Revokati alisema baada ya Mpango Mkakati wa Mahakama kukamilika, watumishi watasaini kadi itakayokuwa ikionyesha namna ya utekelezaji wa Mpango Mkakati na kadi hiyo itaweka alama za kuonyesha ufaulu katika utekelezaji, endapo mtumishi atapata alama ndogo atachukuliwa hatua.

  Akizungumzia namna Mahakama inavyopambana na rushwa, Msajili huyo alisema Mahakama imeweka mazingira ya uwazi katika utoaji wa huduma zake pamoja na kuweka mifumo ya kielekitroniki na kuhusisha wadau wake katika utendaji kazi wake. 

  Mahakama ya Tanzania inaendelea na Mafunzo ya wiki mbili kwa watumishi wake kuhusu uandaaji na utekelezaji wa Mpango Mkakati wake ambapo leo ilikutana na wadau wake ili kujadili namna ya utekelezaji wa Mpango huo. 

  Wadau waliohudhuria, mafunzo hayo leo ni Wizara ya Katiba na Sheria, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Polisi Makao Makuu, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa-TAKUKURU na Wakala wa Majengo Tanzania-TBA.

  Wengine ni pamoja na Baraza la Habari Tanzania-MCT, Tume ya Kurekebisha Sheria, Tume ya Usuluhishi wa Migogoro, Ofisi ya Nyaraka za Taifa na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa-TAMISEMI.

  0 0


    Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (mwenye koti la Bluu) akizungumza na wananchi katika kijiji cha Matongo wilayani Tarime. Profesa Muhongo alifika kijijini hapo ili kuwaeleza wananchi, maamuzi ya Serikali yanayotokana na mapendekezo  ya Kamati iliyoundwa mwezi Februari mwaka huu ili kutathmini migogoro kati mgodi wa Acacia NorthMara na wananchi wanaozunguka mgodi huo.
  Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche (kushoto),  akizungumza na wananchi katika kijiji cha Matongo wilayani Tarime) wakati  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (mwenye koti la Bluu) alipofika kijijini hapo ili kuwaeleza wananchi, maamuzi ya Serikali yanayotokana na Mapendekezo ya  Kamati iliyoundwa mwezi Februari mwaka huu ili kutathmini migogoro kati mgodi wa Acacia NorthMara na wananchi wanaozunguka mgodi huo.
  Baadhi ya wananchi katika kijiji cha Nyabichune wilayani Tarime, wakimsikiliza Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (hayupo pichani) aliyefika kijijini hapo ili kuwaeleza wananchi, maamuzi ya Serikali yanayotokana na Mapendekezo ya  Kamati iliyoundwa mwezi Februari mwaka huu ili kutathmini migogoro kati mgodi wa Acacia NorthMara na wananchi wanaozunguka mgodi huo.
  Kaimu Kamishna wa Madini, Mhandisi Ally Samaje akisoma Ripoti kuhusu tathmini ya Mgogoro kati ya mgodi wa Acacia North Mara na Wananchi wanaozunguka mgodi huo. Ripoti hiyo aliisoma mbele ya  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (mwenye koti la Bluu) aliyefika katika kijiji cha Matongo ili kuwaeleza wananchi, maamuzi ya Serikali yanayotokana na Mapendekezo ya  Kamati iliyoundwa mwezi Februari mwaka huu ili kutathmini migogoro kati mgodi wa Acacia NorthMara na wananchi wanaozunguka mgodi huo.

  Na Teresia Mhagama.
  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo ametoa agizo   la kupimwa tena kwa maji yanayotoka katika vyanzo vinavyozunguka mgodi wa dhahabu wa Acacia North Mara ili kujiridhisha kuwa hayana athari kwa binadamu, mifugo na mazingira.

  Agizo hilo alilitoa wilayani Tarime wakati  akizungumza na wananchi katika vijiji vya Matongo, Nyabichune, Mrwambe na Nyakungulu ambavyo vinazunguka mgodi huo wa dhahabu.

  Profesa Muhongo alitoa agizo hilo baada ya Kamati iliyokuwa ikitathmini migogoro kati ya Mgodi huo na wananchi kueleza kuwa matokeo ya vipimo vya  maabara vinaonyesha kuwa maji hayo yana viwango vinavyokubalika kwa matumizi ya binadamu, mifugo na mazingira na kupendekeza kuwa wataalam wa afya na mifugo wafanye utafiti zaidi ya suala hilo ili kujiridhisha zaidi.

  “Viwango vinavyopaswa kutumika katika upimaji wa maji haya lazima viwe vya Shirika la Afya Duniani (WHO) hivyo zichukuliwe tena sampuli za maji wakati wa kiangazi na wakati wa mvua na zipimwe tena. Sampuli hizo zigaiwe kwa makundi mbalimbali ikiwemo wananchi, Mkuu wa wilaya, Kamati iliyofanya tathmini na mimi mwenyewe ili kila kundi lipeleke katika maabara inayoaminika na baadaye kuwasilisha majibu ya uchunguzi,” alisema Profesa Muhongo.

  Aidha alisema kuwa sampuli za maji atakazopatiwa yeye  atazipeleka katika nchi  mbalimbali duniani ikiwemo Ujerumani na Ubelgiji ambako kuna maabara za kisasa na zinazoaminika duniani.
  Aliongeza kuwa, vyanzo vya maji katika sehemu nyingi zenye uchimbaji mkubwa na mdogo duniani vimekuwa vikiathiriwa na shughuli za  migodi na kueleza kuwa atawasiliana na Mamlaka zinazosimamia Sekta ya Maji pamoja Mgodi ili kupata chanzo mbadala cha maji na hivyo kuondoa malalamiko ya wananchi wanaozunguka mgodi huo.

  Aidha aliagiza wataalam wa Wizara ya Nishati na Madini kuhakikisha kuwa kila baada ya miezi mitatu wanachukua sampuli za maji  katika vyanzo vinavyozunguka mgodi huo na kuzipima ili kujiridhisha kuwa maji hayo hayana madhara kwa binadamu, mifugo na mazingira.
  Naye Mbunge wa Tarime vijijini, John Heche alimshukuru Waziri wa Nishati na Madini kwa kuamua kuishughulikia changamoto hiyo ya maji kwa kutoa agizo kuwa upimaji wa maji hayo uwe endelevu na  kutafuta chanzo mbadala cha maji.

  Aidha Profesa Muhongo alitumia fursa hiyo kuwaasa Wachimbaji  wadogo kujiunga katika makundi ambayo yatawawezesha kufaidika na masuala mbalimbali  ikiwemo Ruzuku  inayotolewa na Serikali ambapo kwa mwaka huu, takribani Dola za Marekani milioni 400 zinatumika kuwaendeleza wachimbaji wadogo kupitia Ruzuku hiyo. 

  0 0

  Shirika la Hifadhi ya Taifa ya Jamii NSSF Makao Makuu ikishirikiana na Ofisi ya Mkoa wa Lindi Imechanga Jumla ya Shilingi Milioni 50 Kwa Ajili ya Kuchangia Harambee ya Kusaidia Ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Lindi Iliyoungua Moto Wiki iliyopita.

  Kwa Kutambua Umuhimu wa Elimu kwa Watoto Shirika Hilo Kupitia Mkurugenzi Mkuu Wake ,Aliewakilishwa na Meneja wa Mkoa Bi Nour Aziz Limetoa ahadi hiyo kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Majaliwa Kasim Majaliwa Alieongoza Harambee Hiyo Ambayo Ilihudhuriwa na Wadau Mbali mbali Akiwemo Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne,Mama Salma Kikwete.

  Katika Harambee Hiyo Jumla ya Shilingi Milioni 80 Taslimu zilichangwa Huku Ahadi na Vifaa vya Ujenzi zikifikia Shilingi Milioni 640 Ambapo Katika Ujenzi Mpya Waziri Mkuu Ameagiza Kujengwa Jengo la Ghorofa litakalokuwa na Ofisi na Madarasa.

  Katika Tukio Hilo la Moto,Jumla Ya Madarasa 9 na viti na Meza zaidi ya 300,Ofisi 4 na Vyoo Matundu 24 Viliteketea na Moto Uliotokana na hitilafu ya Umeme. (Picha na Abdulaziz Video, Lindi)
  Meneja wa NSSF Mkoa wa Lindi, Bi Nour Aziz akisalimiana na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Lindi wakati wa Harambee.
  Meneja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mkoa wa Lindi, Bi Nour Aziz (kulia) akiwasilisha ahadi ya shirika hilo ya kuchangia milion 50 katika harambee hiyo iliyoongozwa na Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa, mwishoni mwa wiki.
  Meneja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mkoa wa Lindi, Bi Nour Aziz akipeana mkono na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimshukuru Mkuu wa Kitengo cha Mafao NSSF, Bw Juma Namuna, baada ya shirika hilo kuahidi kuchangia Milioni 50.
  Waziri Mkuu akisalimiana na Mkuu wa Idara ya Uhasibu NSSF mkoa wa Lindi, Jumbe Dona. 
  Baadhi ya wafanyakazi wa NSSF-Lindi wakisalimiana ba Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
  Wafanyakazi wa NSSF Lindi wakiwa na nyuso za furaha baada ya kusalimiana na Waziri Mkuu.
  Wafanyakazi wa NSSF Lindi wakiongozwa na Meneja wa Mkoa wakiwa katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Lindi kwa ajili ya Harambee Hiyo iliyoendeshwa na Waziri Mkuu.
  Baadhi ya wafanyakazi wa NSSF wakiwa katika harambee hiyo.
  Baadhi ya wageni waalikwa na viongozi wakiwa meku kuu.
  Meza Kuu.
  Mama Salma Kikwete akiwa katika harambee hiyo.

  Mke wa Rais mstaafu wa awamu ya nne, Mama Salma Kikwete akiwasilisha mchango wake katika Harambee hiyo huku Taasisi ya WAMA ikitoa ahadi ya kuchangia vitabu vya Shule hiyo.

  0 0

  GGM Kili Challenge 2016 - Heroes Faces Day IV.
  Today’s images….What a positive sight despite the tiredness!!!!
  Former President of the United Republic of Tanzania HE. Dr Jakaya Mrisho Kikwete has flagged off the 2016 Kili Challenge at Machame Gate in Moshi marking its 15th year historical event!!. Government authorities and institution, United Nations Development Programme representatives in Tanzania, the general public and Strong 57 Kili climbers and 30 Cyclists were all there ready to mark the historical event.

  Speaking during the ceremony to start a 7 days double routes, President Kikwete commended GGM and its partnering stakeholders for the continued commitment to support government initiative in the fight against HIV and AIDS.

  “The initiative is now approaching to 1,000 people from all across the world participating in the Kilimanjaro Challenge and combined with  joint effort with other initiatives, the reduction of HIV infections has been reduced from a double digits to 5.1% nationalwide…this is commendable effort”.

  He added that Tanzania at that percentage, people must be proud of the hard work done by the government through TACAIDS and its associate partners such as GGM and this has been possible through these kind of innovative approaches.

  “I sincerely thank GGM and its partners for this noble undertaking. This is a positive corporate responsibility. I therefore ask other companies and even individuals to contribute to this course. Let us all rise up to join the fight against HIV & AIDS in order to make our Country the first in the world to get to 3 Zeros: Zero New Infections, Zero Stigma and Zero AIDS related deaths. "He said.
   the hungry Cycling team was enjoying a video clip while waiting for the lunch to be set on the “Road table”. 

  GGM Managing Director Mr. Terry Mulpeter appreciated the government support to the initiative. “Your presence here our Former President,  signifies your personal commitment to this noble fight and the government of Tanzania appreciations in supporting the joint efforts made by Private sector and Public Institution by working hand in hand to support government initiatives in the fight against HIV and AIDS in Tanzania”  He added that GGM in partnership with TACAIDS and other organizations, want to see a healthy and productive society. Mr. Terry said “this year, the heroic and determined climbers and cyclists are from Tanzania, Mali; South Africa, United States, United Kingdom and Australia together will be undertaking this Challenge for a good cause and for fulfilling the dreams.” He concluded.

  GGM Managing Director  jointly with Executive Director from TACAIDS handled over certificates of appreciations to HE. President Kikwete Ret. (1995 -2005) as well as HE President Ali Hassan Mwinyi-Ret. (1985-1995)

  Day IV:
  Climbing Updates
  GGM Kili Climb Lead Captain:  Kelvin Yasiwa
  Assistant Captain:  Japhet Kidende 

  It was 9:00am when a group of 57 Kili Challenge Climbing Heroes left Baranco Camp in deep silence despite the most fresh tasty breakfast they had with the famous cucumber soup. The walk today took the team 6hrs to Karanga Camp for an early rest before tomorrow where they will face the Great wall climbing famous as “Kissing rocks.” Tomorrows’ Challenge is not a cliff face and it is not a climb. It is mostly a  very steep path that requires the team to use their hands every now and then with a bit of a scramble in a couple of places.

  At Karanga, the team relaxed while looking at the beautiful sunset view from the far west high above the clouds.  Unfortunately, one hero who was so determined to make it to the top, tried and tried real hard, but the body could not take it further due to the altitude and acclimatization adaptation. He was advised by doctors not to continue with the Challenge. Therefore the number has come down from 57 to 56 climbers.

  There is symptoms of altitude sickness to almost everyone in the team today resulted by climbing on high altitude. However the level of effect differs from one individual to another. It is a tough call.

  Height: 13255 ft / 4040m
  Walking distance: 5.5 km/3.5 miles
  Walking time: 6 hours
  Altitude gain: 55 m/185 ft

  Cycling Updates:
  GGM Kili 360 Cycling Lead Captain: Andrew Austin

  Assistant Captain: Gordon Maclear.
  The team is currently going under the  “No network zone” Despite several communications  attempts made, we did not have further information apart from the last successful communication through Whatsapp by the captain when the team was taking lunch on the road at 1:27pm. We will inform you once the communication channel issues have been solved and secured.

  0 0

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
  SERIKALI imesema kuwa itaweka utashi wa kisiasa katika kupambana dhidi ya utapiamlo kwa kuongeza elimu hususani katika maeneo ya vijijini.

  Hayo ameyasema leo Makamu wa Rais, Samia Hassan Suluhu wakati wa uzinduzi wa ripoti ya Dunia iliyoandaliwa na Jukwa la Lishe Nchini (PANITA) , amesema kuwa suala la lishe likiwekewa utashi wa kisiasa litaweza kufanikiwa kutokana na jitihada ambazo zimeanza kuonekana kwa wadau.

  Amesema serikali inatambua kuwa mojawapo ya malengo ya Baraza la Afya Duniani ni kutokomeza utapiamlo ifikapo mwaka 2025 na lengo hilo linaweza lisifikiwe kama tutaendelea kutekeleza mipango yetu kwa mazoea.

  Makamu wa Rais Samia amesema kuwa serikali kwa kushirikiana na wadau wote kwa pamoja tuweze katika kutokomeza utapiamlo katika kufikia malengo ya Tanzania isiyo na Utapiamlo, Tanzania ya viwanda na yenye uchumi wa kati.

  Amesema malengo kupambana na utapiamlo yatawezekana kwa kuendeleza jitihada za kuongeza bajeti za lishe,kuongeza virutubishi katika vyakula , kutumia vyema wataalam wa lishe na kuhakikisha utekelezwaji wa afua za lishe kwa ufanisi zaidi.

  Makam wa Rais, Samia amesema kuwa ripoti imetilia mkazo suala la lishe kama msingi wa maendeleo hivyo kuzungumzia maendeleo inamaanisha afya,elimu ,ajira ,kuondoa umasikini na kuleta usawa.

  Amesema suala la usawa limewaangalia kuwajengea uwezo wakina mama kutokana na akina mama kuwa walezi wa jamii ,wazalishaji wakubwa katika sekta ya kilimo lakini wanaume wanawajibu wa kushiriki katika suala hilo.

  Nae Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto , Ummy Mwalimu amesema kama wizara inatambua tatizo la lishe na kusema kwa kiwango tulichofikia lazima kipungue.
  Makamu wa Rais, Samia Hassan Suluhu akizungumza na wadau wa lishe katika uzinduzi wa ripoti ya lishe ya dunia katika uzinduzi uliofanyika jijini Dar es Salaam leo.
  Makamu wa Rais, Samia Hassan Suluhu, Mkurugenzi wa Jukwaa la Lishe Tanzania (Panita), Tumaini Mikindo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy  Mwalimu wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa uzinduzi wa ripoti ya Dunia iliyoandaliwa na Jukwa la Lishe Nchini (PANITA) iliyozinduliwa jijini Dar es Salaam leo.
  Mkurugenzi wa Jukwaa la Lishe Tanzania (Panita), Tumaini Mikindo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kuzindua ripoti ya lishe ya Dunia.
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto , Ummy Mwalimu akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuzindua ripoti ya lishe ya dunia jijini Dar es Salaam leo.
  Makamu wa Rais, Samia Suluhu akigawa ripoti ya lishe ya dunia iliyozinduliwa leo jijini Dar es Salaam.

  Makamu wa Rais, Samia Hassan Suluhu akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa lishe mara baada ya kuzindua ripoti ya afya jijini Dar es Salaam leo.

  0 0


   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Rais wa Benki ya Exim ya China Liu Liang  mara baada ya kumaliza mazungumzo yao katika  Ikulu ndogo ya Chamwino mkoani Dodoma.
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Rais wa Benki ya Exim ya China Liu Liang katika Ikulu ndogo ya Chamwino mkoani Dodoma.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Rais wa Benki ya Exim ya China Liu Liang  wa kwanza kulia katika Ikulu ndogo ya Chamwino mkoani Dodoma. Wakwanza kushoto ni Balozi wa China hapa nchini Lu Youqing.
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza kikao cha pamoja na ujumbe wa Rais wa Benki ya Exim ya China Liu Liang katika Ikulu ndogo ya Chamwino mkoani Dodoma.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Benki ya Exim ya China Liu Liang  (watatu) kutoka kulia mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu ndogo ya Chamwino mkoani Dodoma. Wengine katika picha ni Balozi wa China hapa nchini Lu Youqing wakwanza kushoto, Waziri wa Fedha na Mipango Filipo Mpango, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Suzan Kolimba.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Benki ya Exim ya China Liu Liang watatu kutoka kulia mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu ndogo ya Chamwino mkoani Dodoma.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza kwa msisitizo mara baada ya kikao chake na ujumbe wa Rais wa Benki ya Exim ya China Liu Liang katika Ikulu ndogo ya Chamwino mkoani Dodoma.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Rais wa Benki ya Exim ya China Liu Liang katika Ikulu ndogo ya Chamwino mkoani Dodoma.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana kwa furaha na Rais wa Benki ya Exim ya China Liu Liang katika Ikulu ndogo ya Chamwino mkoani Dodoma. PICHA NA IKULU

  0 0

  Banda la Chuo cha Kiislamu cha Morogoro katika maonesho ya vyuo Vikuu yaliyoandaliwa na Taasisi ya Vyuo vikuu hapa nchini(TCU)yanayoendelea kufanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam Julai 20,21,22 mwaka huu.  

  Waziri wa Elimu,Sayansi,Teknolojia na Ufundi Prof.Joyce Ndalichako akitembelea katika banda la chuo cha Kiislamu cha(MUMO) yanayoendelea kufanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam Julai,20,21,n1 22 mwaka huu.
   Mkurugenzi wa kituo cha confucius wa  Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Morogoro,Sun Xiaofei akitoa maelekezo kwa baadhi ya wananchi waliotembelea banda la Chuo Kikuu cha Kiislamu  cha Morogoro yanayoendelea kufanyika katika viwanja vya karimjee jijini Dar es Salaam leo.
   Mwalimu wa Taasisi ya Confucius iliyopo katika chuo kikuu cha Kiislamu cha Morogoro, Chang Yue akitoa maelekezo yanayoendelea katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Hayo ameyasema mkurugenzi mtendaji, Abdulmalik Mollel wakati wa maonesho ya vyuo vikuu yanayoendelea katika viwanja vya karimjee jijini Dar es Salaam .

  Mollel amesema kuwa vyuo vya nje viko 100 ambavyo vimeshiriki maonesho hayo. Mkurugenzi huyo amesema kuwa bodi ya mikopo wanafunzi wanaweza kutumia kujua jinsi gani bodi

  inafanya ikiwa pamoja na udahili wa vyuo vya nje unafanywa katika maonesho hayo .Mollel amesema kuwa vyuo vya nje vilivyopo ni bora na vinaendana maisha ya watanzania kuweza kumudu gharama za vyuo hivyo

  0 0

  Rais wa Zanzibar na MakamU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Mh Jordan Rugimbana muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege mkoani Dodoma sambamba na wajumbe wake asubuhi hii,kushiriki mkutano maalum wa CCM unaotarajiwa kufanyika Julai 23,206 katika ukumbi wa mikutano wa CCM, Dodoma Conversion Center nje kidogo ya mji wa Dodoma.
  Rais wa Zanzibar na MakamU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na baadhi ya Wafanyakazi wa ndege ya shirika la Precision air muda mfupi baada ya kuwasili mkoani Dodoma sambamba na wajumbe wake asubuhi hii kushiriki mkutano maalum wa CCM unaotarajiwa kufanyika Julai 23,206 katika ukumbi wa mikutano wa CCM, Dodoma Conversion Center nje kidogo ya mji wa Dodoma.

  Pichaani ni baadhi ya Wajumbe mbalimbali kutoka Visiwani Zanzibar wakiwasili katika uwanja wa ndege mjini Dodoma asubuhi hii,kushiriki mkutano maalum wa CCM unaotarajiwa kufanyika Julai 23,206 katika ukumbi wa mikutano wa CCM, Dodoma Conversion Center nje kidogo ya mji wa Dodoma.

  0 0

  Msimu wa nane wa Rock City Marathon 2016 unatarajiwa kuzinduliwa Jumanne ya wiki ijayo jijini Dar es Salaam huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa ni Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye. Uzinduzi wa mbio hizo zinazoratibiwa na kampuni ya Capital Plus International utafuatiwa na uzinduzi mwingine utakaofanyika jijini Mwanza siku chache zijazo.

  Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mratibu wa mbio hizo Bi Elizabeth Riziki alisema maandalizi ya mbio hizo kwa kiasi kikubwa yameshakamilika na zinatarajia kufanyika Septemba 25 mwaka huu kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza zikihusisha wanariadha kutoka ndani na nje ya nchi ikiwemo baadhi ya nchi za Afrika, Ulaya na Marekani.

  Alisema mbio hizo zinazofanyika kwa mara ya nane mfululizo tangu zianze mwaka 2009 zina baraka zote kutoka Chama cha Riadha Tanzania (RT), pamoja na Chama cha Riadha Mkoa wa Mwanza (MRAA) kwa kuwa zinalenga kutambua na kuinua vipaji vya wanariadha nchini na pia kukuza utalii wa ndani kupitia sekta ya michezo. 

  “Mbio hizi zimekuwa zikionyesha mafanikio makubwa tangu kuanzishwa kwake, mafanikio ambayo kimsingi yamekuwa yakichagizwa na asili ya sehemu zinapofanyika. Jjiji la Mwanza limebarikiwa kuwa na vivutio mbalimbali vya utalii na sisi kama waandaaji wa mbio hizi tumekuwa tukitumia fursa hiyo kuendelea kumulika vivutio vya kipekee vinavyopatikana katika ukanda wa ziwa Victoria,” alisema.

  Alisema tayari baadhi ya makampuni yameshajitokeza kudhamini mbio hizo ikiwa ni pamoja na Freidkin Conservation Fund, African Wildlife Trust, Mwanza Hotel, Nyanza Bottlers Limited na kampuni ya Real PR Solution.

  “Tunawaalika wadhamini waendelee kujitokeza kwa wingi ili kuzifanya mbio za mwaka huu kuwa bora zaidi,” alisema. Pamoja na Waziri Nape, uzinduzi huo unatarajiwa kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa michezo ikiwa ni pamoja na viongozi wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), viongozi wa vyama vya riadha, wanariadha na wadau mbali mbali wa mchezo huo nchini.

  0 0


  Julai 15 mwaka huu, serikali ya Uturuki ilinusurika kupinduliwa katika jaribio la mapinduzi liliyodumu kwa chini ya masaa 12. Tayari watu zaidi ya 60,000 aidha wamekamatwa, wamesimamishwa au wamefukuzwa kazi kwa tuhuma za kuhusiana na jaribio hilo lililofeli.

  Jaribio la mapinduzi lilitokeje?

  Awali daraja kuu katika mkondo wa Bosphorous liliwekewa vizuizi na kundi la wanajeshi wakitumia vifaru, na wakati huohuo ndege za kivita zilikuwa zikiruka katika anga la mji mkuu wa nchi hiyo, Ankara, huku milio ya bunduki ikisikika sehemu mbalimbali.Baadaye, Waziri Mkuu Binali Yildrim, alitangaza kwamba kulikuwa na jaribio linaloendelea la kuipindua serikali.

  Muda mfupi baadaye, kikundi cha wanajeshi kilitangaza kupitia radio ya taifa kuwa jeshi limechukua madaraka kutoka kwa Rais Recep Tayyip Erdogan ili kulinda demokrasia.

  Kisha likafuatia tangazo la hali ya hatari (curfew), sheria za kijeshi (marshall law) na maandalizi ya katiba mpya.Rais Erdogan ambaye alikuwa likizoni alifanikiwa kuwasihi wananchi waingie mtaani kupinga mapinduzi hayo. Alitoa wito huo kwa kutumia app ya Facetime ya iPhone na kuonyeshwa live kama inavyoonekana pichani chini.
  Katika usiku huo, vituo vya televisheni vilivamiwa na wanajeshi, milipuko kadhaa ilisikika sehemu mbalimbali za Ankara na Istanbul, abaadhi ya waandamaji walishambuliwa na wanajeshi na kuuawa au kujeruhiwa, jengo la bunge na ikulu zilishambuliwa, helikopta ya jeshi ilitunguliwa, na mnadhimu wa jeshi kuchukuliwa mateka.

  Jaribio la mapinduzi liliishaje?

  Ili jaribio hilo la mapinduzi lifanikiwe, wahusika walihitaji sapoti ya sehemu kubwa zaidi ya jeshi badala ya kikundi kidogo tu, na sapoti ya wananchi mtaani. Yote mawili hayakutokea. Kana kwamba hiyo haikutosha, vyama vya upinzani navyo vilijitokeza kulaani jaribio hilo.

  Kufikia Jumamosi asubuhi - chini ya masaa 12 baada ya tangazo la mapinduzi - baadhi ya wanajeshi walioshiriki katika jaribio hilo walianza kujisalimisha.

  Kadhalika, polisi walifanikiwa kurejesha sehemu mbalimbali muhimu mikononi mwa dola kutoka kwa waasi. Kufikia Jumamosi mchana, mitaa ilikuwa imesheheni wananchi wakilaani jaribio hilo la mapinduzi na kuunga mkono serikali ya Erdogan.

  Kwanini jaribio hili la mapinduzi lilifeli?

  Kwanza, jaribio hilo halikuwa na sapoti ya kutosha ndani ya jeshi la nchi hiyo. Kilichoonekana ni kikundi kidogo tu cha wanajeshi kilichojumisha wanajeshi wapya, pasipo uwepo wa viongozi waandamizi wa jeshi la nchi hiyo.Pili, jaribio hilo halikuwa na spaoti ya wananchi. Mara baada ya Rais Erdogan kuwataka wananchi waingie mtaani kupambana na jaribio hilo, ikageuka kuwa mapambano kati ya wanajeshi na wananchi, kitu ambacho kwa vyovyote kingeathiri 'uhalali' wa mapinduzi hayo.

  Tatu, wahusika wa jaribio hilo la mapinduzi kushindwa kudhibiti njia zote za mawasiliano kati ya viongozi wakuu wa serikali na wananchi, kwa mfano vituo vya televisheni na redio. Mwelekeo wa jaribio hilo la mapinduzi ulibadilika kwa kiasi kikubwa baada ya Rais Erdogan kuonekana kwenye kituo kimoja cha televisheni akiwataka wananchi waingie mtaani.

  Nne, Uturuki ni taifa lenye asilimia kubwa ya watu wenye kipato cha kati na cha juu. Ni vigumu sana kwa taifa lenye wananchi wa aina hii kuunga mkono mapinduzi. Ni rahisi kwa mapinduzi kuungwa mkono katika nchi masikini ambapo mara nyingi 'chuki' dhidi ya serikali huwa kubwa.

  Jaribio hilo la mapinduzi lilionekana kufeli bayana baada ya Rais Erdogan kurejea Instanbul na kuhutubia katika uwanja wa ndege wa Ataturk.  Hali ikoje sasa?

  Idadi halisi ya waliokamatwa, kusimamishwa kazi au kutimuliwa kazi na hatua nyingine zilizochukuliwa ni kama ifuatavyo

  Watumishi 300 wa Wizara ya madini wametimuliwa.
  Watumishi 184 wa Wizara ya Forodha wametimuliwa.
  Waandamizi wanane wa Bunge wameondolewa.
  Waturuki wote wanapaswa kuwa na nyaraka za ziada wanapofanya safari nje ya nchi. 

  Watumishi 86 wa taasisi ya udhibiti na usimamizi wa mabenki wametimuliwa.
  Watumishi 51 wa Soko la Hisa wametimuliwa.
  Majaji 140 wa Mahakama Kuu wametumiwa hati za kukamatwa.
  Watumishi 15,200 wa Wizara ya Elimu wametimuliwa.
  Vyombo vya habari 24 vimefutiwa hati za usajili.
  Watu 429 wa taasisi ya umma ya masuala ya dini (Diyanet) wameondolewa.
  Walimu binafsi 21,000 wamefutiwa leseni zao.
  Watumishi 393 w Wizara ya Familia na Sera za Jamii wametimuliwa.
  Watumishi 257 katika ofisi ya Waziri Mkuu wametimuliwa.
  Wakuu (deans) 1577 wa vyuo vikuu wametakiwa kujiuzulu.
  Magavana 33 wametimuliwa.
  Watumishi 9,000 wa Wizara ya Mambo ya Ndani wametimuliwa.
  Maafisa Usalama wa Taifa 180 wamesimamishwa kazi
  Majaji 2,745wametimuliwa. 

  Watumishi wa umma milioni tatu wamezuwia kwenda likizo.
  Mjadala kuhusu kurejeshwa kwa hukumu ya kifo umeanza, na Rais Erdogan ametanabaisha kuwa pindi bunge likiridhia kurejeshwa kwa hukumu hiyo basi wote waliohusika na jaribio hilo la mapinduzi watahukumiwa kifo.
  Maafisa 1,500 wa Wizara ya Fedha wametimuliwa.
  Majenerali na maadmirali 85 ni miongoni mwa maelfu ya wanajeshi waliokwishakamatwa. Pia zaidi ya polisi 8,000 wamekamatwa, wametimuliwa au wamesismamishwa kazi.

  Mashushushu wa Uturuki walikuwa wapi wakati mapinduzi hayo ynaandaliwa na hadi yakakaribia kufanikiwa?

  Makala hii inahusu hasa swali hilo hapo juu, kwa moja ya kazi kuu za Idara ya Usalama ya taifa lolote lile ni kutambua, kuzuwia na kudhibiti matishio ya usalama wa taifa, ikiwa ni pamoja na mapinduzi. Sasa wakati serikali ya Uturuki ikionekana kuchukua hatua kali dhidi ya watumishi mbalimbali wa umma ikiwa ni pamoja na kuwakamata, kuwasimamisha kazi na kuwatimua, ni idadi ndogo tu ya maafisa usalama wa taifa waliochukuliwa hatua (angalia juu nilipoandika kwa maandishi mekundu).

  Lakini swali kubwa zaidi ni kwamba je Idara ya Usalama wa Taifa ya nchi hiyo, MIT, haikufahamu kuhusu mipango ya kufanyika kwa mapinduzi hayo, na kwanini?

  Turudi nyuma kidogo. Oktoba mwaka jana, mhadhiri wa chuo kikuu cha Haifa , Israel, Norman Bailey, alieleza kwa uhakika kuwa jeshi la Uturuki linaweza kuchukua madaraka ya nchi hiyo iwapo litaona nchi inaelekea kusikofaa.

  Kadhalika, Machi mwaka huu, wachunguzi wa masuala ya usalama wa Russia walionya kuwa jeshi la Uturuki lilikuwa likijiimarisha kisiasa, na hivyo kujenga msingi wa mapinduzi.

  Baadaye mwezi huohuo, Michael Rubin wa taasisi ya American Enterprise, aliuliza"je Uturuki itakumbwa na mapinduzi?" na akajibu kwamba "isiwe jambo la kushangaza iwapo jeshi la Uturuki litajaribu kumng'oa (Rais) Erdogan na kuwatupa jela watu wake wa karibu."

  Machi 30, jarida linaloheshimika la Foreign Affairs lilichapisha makala ya Gonul Tol, Mkurugenzi mwanzilishi wa Taasisi ya Mashariki ya Kati, kituo cha stadi za Uturuki, alieleza kuwa nchi hiyo ilikuwa ikikabiliwa na mapinduzi.

  Kadhalika, mwanzoni mwa mwezi huu, Joseph Fitsanakis wa tovuti ya IntelNews alizungumzia kuhusu hali tete iliyokuwa ikiikabili Uturuki na kutanabaisha kuwa hakuna nchi katika eneo hilo ambayo ilikuwa 'haijatulia' kama Uturuki.

  Pia, wachambuzi wa taarifa za kiusalama wa Marekani walikuwa wakihofia kitambo kuhusu hali ya usalama nchini Uturuki. Swali lilibaki kuwa lini kungetoa jaribio la mapinduzi na lingeongozwa na nani.

  Sasa, kama wataalamu hao mbalimbali wa masuala ya usalama waliokuwa wakitegemea 'vyanzo vya wazi vya taarifa za kishushushu' (open sources) waliweza kutoa tahadhari kuhusu uwezekano wa jaribio hilo la mapinduzi, inatarajiwa kuwa mashushushu wa Uturuki pia walikuwa na tahadhari hiyo.

  Kwa kuangalia 'sintofahamu' iliyoikumba serikali ya Rais Erdogan wakati wa jaribio hilo la mapinduzi, yayumkinika kuhisi kuwa idara ya ushushushu ya nchi hiyo nayo ilikuwa katika 'sintofahamu' pia.

  Na kuthibitisha kuwa taasisi hiyo haikuwa imejipanga vizuri, asuhuhi ya Julai 16 makao makuu yake yalishambuliwa na helikopta za jeshi pasipo upinzani wowote. Wakati serikali ikikabiliwa na jaribio la mapinduzi, mkuu wa idara ya ushushushu ya nchi hiyo, Hakan Fidan, alikuwa mafichoni.

  Kuna sababu kuu tatu zinazoweza kueleza kwanini idara ya ushushushu ya nchi hiy, MIT, ilionekana kutokuwa na taarifa kuhusu jaribio hilo la mapinduzi na kushindwa kwake kulizuwia.

  Kwanza, uwezo wa utendaji kazi wa taasisi hiyo ni duni, na kwa kiasi kikubwa umekuwa ukikuzwa na vyombo habari kuliko hali halisi. Taasisi hiyo inaelezwa kuwa yenyeurasimu mkubwa, yenye kutumia mbinu za kale, in uhaba mkubwa katika mtandao wake wa upatikanaji taarifa za kiusalama, sambamba na mapungufu katika uwezo wake kwenye uchambuzi wa taarifa za kiusalama.


  Pili, kuchanganya siasa na taaluma ya ushushushu. Awali, taasisi hiyo ilikuwa ikijitegemea na kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia taaluma na utaalam wa ushushushu. Hata hivyo, tangu Erdogan aingie madarakani mwaka 2003, taasisi hiyo imekuwa kama chobo cha kisiasa cha AKP, chama tawala chenye mrengo wa kulia kidogo kidini kinachoongozwa na Erdogan.

  Tatu, kwa takriban muongo mzima sasa, MIT imekuwa 'bize' zaidi na changamoto za matishio ya usalama kwa Uturuki kutoka nje, yaani tishio la kikundi cha kigaidi cha ISIS, harakati za uhuru za Wakurdi na wapiganaji wao wa PKK, kuibuka kwa taifa lisilo rasmi la Rajava huko Syria, na hali tete ya usalama huko Iraki na Syria kwa ujumla. Changamoto hizo zimepeleka taasisi hiyo kuwekeza nguvu nyingi katika kukabiliana na matishio kutoka nje badala ya matishio ya kiusalama ya ndani ya nchi.
  Kwa upande mwingine, kumekuwa na hisia kwamba huenda Erdogan alishirikiana na MIT kuruhusu wapinzani wa chama tawala na serikali ndani ya jeshi la nchi hiyo kufanya jaribio hilo la mapinduzi , lengo likiwa ni kuwa mapinduzi hayo yakishindikana (na lengo ni yashindikane) basi Erdogan awe na kila sababu na haki ya kuendesha taifa hilo kwa mkono wa chuma. Ikumbukwe kuwa kwa muda mrefu Erdogan amekuwa akifanya jitihada za kutaka taasisi ya urais wa nchi hiyo iwe ya kiutendaji kuliko sasa ambapo kinadharia mkuu wa serikali ni Waziri Mkuu.

  Nimalizie makala hii kwa kuahidi kufanya uchambuzi mwingine kadri taarifa mbalimbali zitakavyopatikana. Kwa habari zaidi kuhusu masuala ya ushushushu, bonyeza hapo juu palioandikwa 'INTELIJENSIA,' sambamba na kusoma habari nyingine katika blogu hii.

  0 0  Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia Wambura akizungumza na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Muziki Tanzania Bw.John Kitime mara baada ya kupokea taarifa ya mapendekezo ya kuboresha tasnia ya Muziki hapa nchini leo Julai 21 Jijini Dar es Salaam.

  Katibu Mkuu wa Shirikisho la Muziki Tanzania Bw.John Kitime akizungumza na Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia Wambura ofisini kwa Naibu Waziri wakati aki wasilisha taarifa ya mapendekezo ya kuboresha tasnia ya Muziki hapa nchini leo Julai 21 Jijini Dar es Salaam.
  Afisa Utamaduni kutoka Wizara ya Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Habibu Msammy akichangia mada wakati wa majadaliano kati ya na Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia Wambura na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Muziki Tanzania Bw.John Kitime kuhusu maboresho ya tasnia ya Muziki hapa nchini leo Julai 21 Jijini Dar es Salaam.


  Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia Wambura akipokea moja ya kazi ya muziki wa dansi alizowahi kufanya Mzee Kitime baba wa Katibu Mkuu wa Shirikisho la Muziki Tanzania Bw.John Kitime leo Julai 21 Jijini Dar es Salaam.
  Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia Wambura (wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Muziki Tanzania Bw.John Kitime(kulia), wa pili kushoto ni Afisa Utamaduni kutoka Wizara ya Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Habibu Msammy na kushoto katibu wa Naibu Waziri Bi. Anna Nkinda leo Julai 21 Jijini Dar es Salaam.

  Katibu Mkuu wa Shirikisho la Muziki Tanzania Bw.John Kitime akisaini kitabu cha wageni alipowasili ofisini kwa Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia Wambura kuwasilisha taarifa ya mapendekezo ya kuboresha tasnia ya Muziki hapa nchini leo Julai 21 Jijini Dar es Salaam.
  Picha na Shamimu Nyaki

  0 0

  Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla amemaliza ziara yake ya kuwashukuru Wanachi wa Jimbo hilo kwa kumchagua kuwa Mbunge wao huku akiwaahidi kuendelea kushirikiana nao katika shughuli za kimaendeleo kama alivyotoa ahadi katika uchaguzi uliopita.

  Katika ziara hiyo iliyoanza Julai 13 na kufikia tamati Julai 20, mwaka huu, Dk. Kigwangalla ameweza kuzunguka Vijiji mbalimbali vilivyo katika Kata 19 za Jimbo hilo ambapo amekutana na wananchi hao na kutoa shukrani zake.Dk. Kigwangalla katika ziara hiyo, amewaomba Wananchi wa Jimbo hilo waendelee kumuombea kwani kazi ndio imeanza na kuwataka wananchi hao kushirikiana nae bega kwa bega katika shughuli za kimaendeleo.

  “Kwanza nashukuru kwa kura zenu. Hakika zilitosha kuniwezesha mimi kuwa Mbunge. Kwa kura zenu nyingi pia zimewezesha kumpata Rais wetu Dk. Magufuli na Madiwani wengi katika Jimmbo hili. Nawashukuru sana Wana Nzega Vijijini” alieleza Dk. Kigwangalla.

  Aidha, Dk. Kigwangalla katika ziara hiyo, alipata wasaha wa kutembelea maeneo mbalimbali ikiwemo sehemu za shule, Vituo vya Afya ambapo alijioenea hali ilivyo huku akieleza kuwa ataendelea kushirikiana na Watendaji wote wa ngazi ya Kijiji, Kata na ngazi za juu.

  Dk. Kigwangalla pia aliweza kutoa misaada ya vifaa vya michezo kwa vijana mbalimbali ambapo awali aliwaahidi yeye mwenyewe.Kata zinazounda Jimbo hilo la Nzega Vijijini ni pamoja na Kata ya Puge, Ndala, Nata,, Sanzu, Lusu, Milambo Itobo, Magengati, Budushi, Nkiniziwa, Mbagwa, Mizibaziba, Utwigu, Muhugi, Mwantundu, Wela, Mwasala, Tongi, Ugembe na Mwakanshanhala.

  Aidha, Dk.Kigwangalla alipata wasaha wa kushiriki mazishi ya Kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Abdalla Simba ambaye alikuwa mwenyekiti wa CCM Kata wa Nzega Magharibi aliyefariki Julai 19 jioni.Marehemu Mzee Simba ambaye alikuwa mkongwe kwenye chama hicho tokea chama cha TANU ambapo aliwelezewa kuwa alikuwa mstari wa mbele katika kukiunganisha chama cha TANU na baadae CCM.

  Mpaka umahuti unamkuta alikuwa Mwenyekiti wa CCM wa tawi hilo. Dk. Kigwangalla pia alipata kutoa ubani na kuwajulia pole ndugu wa wafiwa.

  Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akipiga picha ya pamoja na vijana wa Sungusungu wa jadi waliokuwa wakitoa burudani.  Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akitoa vifaa vya michezo kwa mmoja wa viongozi wa timu ya Lusu (Kata ya Lusu)  Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akipata picha yaa pamoja  Vijana wa Sungusungu wakifanya mambo..

  Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na walimu katika shule ya Msingi Nata


  Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akisaini kitabu cha wageni cha shule ya Msingi Nata

  Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Nata


  Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akiwahutubia Wananchi wa Kata ya Nata.

  Vijana wa Sungusungu wakifuatilia mkutano huo wa Dk. Kigwangalla (hayupo pichani).


  Vijana wa Sungusungu wakitoa budani katika mkutano huo wa Dk. Kigwangalla (Hayupo pichani). Picha zote na Andrew Chale, Nzega).


  Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akiingia kucheza sambamba na vijana wa Sungusungu wa Jadi  Vijana wa Sungusungu wakicheza ngoma za jadi wakimuonyesha mgeni Dk. Kigwangalla ambaye ni Mbunge wa Jimbo hilo la Nzega Vijijini

  0 0


   Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (katikati) akimsikiliza na Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al Najem (kulia) wakati alipokuwa akizungumzia masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Kuwait na Tanzania. Mazungumzo hayo yalifanyika katika ofisi ya Waziri Mwigulu, jijini Dar es Salaam leo.  Wapili kushoto ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhandisi Hamad Masauni, kushoto ni Katibu Mkuu, Meja Jenerali Projest Rwegasira na Naibu Katibu Mkuu, Balozi Simba Yahya.
   Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (katikati) akizungumza na Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al Najem (kulia) masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Kuwait na Tanzania. Mazungumzo hayo yalifanyika katika ofisi ya Waziri Mwigulu, jijini Dar es Salaam leo.  Wapili kushoto ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhandisi Hamad Masauni, kushoto ni Katibu Mkuu, Meja Jenerali Projest Rwegasira na Naibu Katibu Mkuu, Balozi Simba Yahya.
   Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akizungumza na Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo nchini, Jean-Pierre Mutamba (kushoto) masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Kongo na Tanzania. Mazungumzo hayo yalifanyika katika ofisi ya Waziri Mwigulu, jijini Dar es Salaam leo.
   Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (katikati) akimsikiliza Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo nchini, Jean-Pierre Mutamba (kushoto) wakati alipokuwa akizungumzia masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Kongo na Tanzania. Mazungumzo hayo yalifanyika katika ofisi ya Waziri Mwigulu, jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Balozi Simba Yahya.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (kulia) akipokea zawadi ya Pambo kutoka kwa Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al Najem. Waziri Mwigulu alizungumza na Balozi huyo masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Kuwait na Tanzania. Mazungumzo hayo yalifanyika katika ofisi ya Waziri Mwigulu, jijini Dar es Salaam leo.  Katikati ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Simba Yahya. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

  0 0


  WAZIRI wa Habari, Utlii,Utamaduni na Michezo Zanzibar Rashid Ali Juma akipokea maonesho ya fensi mbali mbali ya Tamasha la 21 la Utamaduni wa Mzanzibari yaliyofanyika katika Mnara wa kumbumkumbu wa miaka 50 Mchenzani.
  WAJASIRIAMALI wakionesha bidhaa mbali mbali walizotengeza katika maonyesho ya Tamasha iliyofanyika katika Mnara wa kumbumkumbu wa miaka 50 Mchenzani. . (PICHA NA MIZA OTHMAN – HABARI MAELEZO –ZANZIBAR).

  MKURUGENZI Mipango, Sera na Utafiti Wizara ya Habari,Utalii, Utamaduni na Michezo Zanzibar Mahamoud Omar Hamad akimpa maelezo Balozi Mdogo wa India namna ya ubuyu wakizanzibari ulivyotengenezwa wakati alipokuwa maonyesho hayo katika Mnara wa kumbumkumbu wa miaka 50 Mchenzani.
  WANANCHI mbalimbali wakishuhudia moja kati ya kiburudisho katika fensi hiyo iliyofanyika katika Mnara wa kumbumkumbu wa miaka 50 Mchenzani.

  WASANII WA UTAMADUNI wakionyesha igizo la ung’owaji wa jino katika Tamasha la 21 Utamaduni wa Mzanzibari katika maonyesho yaliyofanyika katika Mnara wa kumbumkumbu wa miaka 50 Mchenzani.


  ICHA NO:0291: ZANa za Utmaduni zilizokuwa zikitumika kusagia nafaka mbalimbali kama zinvyoneshwa na wasanii wetu katika maonyesho ya Tamasha iliyofanyika katika Mnara wa kumbumkumbu wa miaka 50 Mchenzani.

  0 0


  Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu Dkt. Abdallah Possi akionyesha Ripoti ya Matokeo ya Utafiti wa Utumikishwaji wa Watoto Tanzania wa Mwaka 2014. Uzinduzi huu umefanyika leo jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango.
  ………………..

  Benjamin Sawe-Maelezo.

  Utumikishwaji wa watoto umekuwa ni tatizo kubwa duniani ambapo kutokana na tawkimu za makadirio za mwaka 2000-2012 za Shirika la Kazi Duniani asilimia 11 (watoto milioni 264) ya watoto wote duniani wenye umri wa miaka 5-17 wnatumikisahwa kwenye ajira za aina mbalimbali sawa na asilimia 11 ya watoto wenye umri huo.

  Kwa upande wa Tanzania, utumikishwaji wa watoto kwa mwaka 2014/15 matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa kati ya watoto milioni 15 wenye umri kati ya miaka 5 hadi 17 (watoto milioni 4.2) sawa na asilimia 28.8 wanatumikishwa katika kazi mbalimbali

  Takwimu hizo zinaonesha kuwa sekta za kilimo na uvuvi zimeendelea kuwa sekta zinazoajiri watoto wengi zaidi ikiwa ni kiwango cha asilimia 92.1 ya watoto wote wanaojihusisha na shughuli za kiuchumi na wengi wao wanaishi vijijini.

  Akizungumza katika uzinduzi wa ripoti ya matokeo ya utafiti wa utumikishwaji wa watoto Tanzania Bara wa mwaka 2014, Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa anasema matokeo ya utafiti huo yanaonesha kuwa watoto hutumia zaidi ya nusu ya muda wao wa siku ikiwa ni asilimia 58.8 kwa shughuli za kujihudumia na usafi huku wasichana wakionekana kutumia muda mrefu zaidi kwa shughuli hizo kwa kiwango cha asilimia 58.3.

  Ripoti hiyo inaendelea kuonesha shughuli za kujisomea kwa watoto zilichukua nafasi ya pili kwa matumizi ya muda kwa kiwango cha asilimia 15.5 ambapo wavulana wanatumia muda mrefu zaidi kwa shughuli za kujisomea ikiwani sawa ana asilimia 16.4 ikilinganishwa na wasichana waliotumia wastani wa asilimia 14.6

  Dkt Chuwa anasema matokea hayo yakilinganishwa na nchi nyingine za Afrika kama Ghana yanaonesha kuwa watoto wa Kighana wenye umri wa miaka 10 hadi 17 wanatumia muda mwingi (asilimia 60.9) kwa siku kwenye shughuli za kujihudumia, usafi binafsi na starehe kama kuangalia runinga ikilinganishwa na asilimia 23.4 ya muda wao kwa siku kwenye shughuli za kujisomea.

  Akizindua ripoti ya matokeo ya utafiti wa utumikishwaji wa watoto Tanzania Bara wa mwaka 2014, Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye ulemavu Mh. Dkt. Abdallah Possi (Mb) anasema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesharidhia mikataba mbalimbali ikiwemo ya kikanda na kimataifa inayohusiana na ustawi na haki za watoto

  Dkt. Possi anasema mikataba iliyoridhiwa ni pamoja na Mkataba Na. 138 wa Shirika la Kazi Duniani unaohusu umri wa chini unaoruhusiwa kujihusisha na ajira ya mwaka 1998 ambapo Mkataba na 182 wa utumikiswhaji wa watoto katika kazi hatarishi wa mwaka 2002 unatafsiri mtoto kama mtu mwenye umri chini ya miaka 18.

  Aidha Tanzania imeridhia Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa mwaka 1989 unaohusu Haki za Mtoto mwaka 1991, pia Serikali ilitunga Sheria ya Ajira na Mahusiano ya Kazi Na. 6 ya mwaka 2014 inayozuia kuajiri watoto wenye chini ya miaka 14 ambapo sheria hiyo inapiga marufuku kumfanyisha kazi mtot kwenye mazingira hatarishi yanayoweza kuidhuru afya yake.

  Kwa mujibu wa Shirika la Kazi Duniani, utumikishwaji wa watoto unatafsiriwa kama ushiriki wa watoto katika kazi zinazomnyima mtot haki yake ya utoto, utu na fursa ya kujiendeleza ambazo pia huathiri watoto kiafya, kiakili, kielimu na kijamii.

  Kama ilivyobainishwa katika Mkataba Na. 138 wa Shirika la Kazi Duniani, umri wa chini wa mtoto kujihusisha na ajira ni miaka 15 au 14 kutokana na muundo wa elimu ya msingi ya nchi husika

  Kwa mujibu wa Ripoti ya Shirika la Kazi Duniani (ILO) kuhusu makadirio ya mwenendo wa utumikishwaji wa watoto duniani ya mwaka 2000-2012 inaonesha karibu nusu ya watoto wote wanaotumikishwa kwenye kazi mbalimbali, watoto milioni 85 wanatumikishwa kwenye kazi hatarishi (Hazodous Works) ambazo zinaathiri afya zao, usalama pamoja na makuzi yao.

  Kutokana na tafiti hiyo utumikishwaji wa watoto wa mwaka 2014 Tanzania Bara umebaini kuwa, kuna idadi ya watoto milioni 15 wenye umri kati ya miaka 5-17 ambapo kati yao wavulana ni milioni 8 na wasichana ni milioni 7 na kundi kubwa la watoto ni wenye umri wa miaka 5-11 wakiwa ni asilimia 59.6 ya watoto wote ikifuatiwa na watoto wenye umri wa miaka 14-17 ambao ni asilimia 24.6.

  Mgawanyo wa kijinsia wa watoto wanaojihususha na ajira kwenye sekta ya kilimo unaonesha kuwa wavulana ni asilimia 94.3 ya wavulana wote na wasichana ni asilimia 89.6 ya wasichana wote.

  “Utumikishwaji wa watoto umekuwa ni tatizo kubwa duniani ambapo nchi mbalimbali ikiwemo Tanzania zinafanya jitiada za kutokomeza tazizo hili”Anasema Dtk. Possi.

  Aidha matokeo ya utafiti wa utumikishwaji wa watoto wa mwaka 2014 yanabainisha kuwa kati ya watoto milioni 15 wenye umri kati ya miaka 5-17, watoto milioni 4.2, sawa na asilimia 28.8 wanatumikishwa katika kazi mbalimbali za kiuchumi hapa nchini.

  Hata hivyo mwenendo wa utumikishwaji wa watoto umepungua kutoka asilimia 31.1 mwaka 2006 adi asilimia 28.8 mwaka 2014.

  Kutokana na takwimu utafiti huo matokeo yanaonesha kuwa hali ya utumikishwaji wa watoto imekuwa ikiongezeka kadri umri unavyoongezeka ambapo watoto wenye umri wa kati ya miaka 14 hadi 17 wameonesha kuwa na kiwango cha juu cha asilimia 40.7 ikifuatiwa na watoto wenye umri wa miaka 12-13 sawa na asilimia 36.0 na miaka 5-11 sawa na asilimia 22.1

  Kwa mgawanyiko wa kijiografia, matokeo yanaonesha kuwa tatizo la utumikishwaji wa watoto ni kubwa zaidi katika maeneo ya vijijini kwa asilimia 35.6 ikilinganishwa na maeneo ya miji mingine kwa asilimia 18.0 na Dar es Salaam kwa asilimia 3.6.

  Utafiti huo unebainisha kuwa jumla ya watoto milioni 10.2 wenye umri wa miaka 5 hadi 17 wanahudhuria masomo shuleni, miongoni mwao wavulana ni milioni 5.2 sawa na asilimia 50.9 na wasichana ni asilimia 5.0 sawa na asilimia 49.1

  Akizungumza hivi karibunu katika uzinduzi wa ripoti hiyo Dtk Possi anasema Serikali itaendelea kupambana vikali na kupinga utumikishwaji wa watoto nchini na kuhakikisha kuwa kiwango cha asilimia 28.8 kinapungua kwa kiasi kikubwa.

  Dtk Possi anasema moja ya jitihada zilizofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano kupambana na utumikishwaji wa watoto ni kuanzisha programu ya ELIMU BURE ili kuhamasisha mahudhurio ya watoto shuleni na kupunguza uwezekano wa watoto kujihusisha na ajira za utotoni.

  “Natoa wito kwa wazazi na walezi kutumia vyema fursa ya kuwapeleka watoto shule ili kuwaondoa katika janga la utumikishwaji wa kuzuia mimba za utotoni

  Aidha anawaomba Shirika la Kazi Duniani (ILO) kuendelea kushirikiana na Ofisi ya Taifa ya Takwimu kufanya uchambuzi zaidi wa kitaaluma ili kupata makadirio ya viwango vya utumikishwaji wa watoto katika ngazi za chini kama vile mkoa ili kudumusha hali halisi ya utumikishwaji wa watoto katika maeneo hayo.

  0 0

  SHINDANO la kumsaka mrembo wa kitongoji cha Tabata mwaka huu Miss Tabata 2016 linafanyika leo  Ijumaa kwenye Ukumbi wa Da West Park, Tabata jijini Dar es Salaam.

  Mratibu wa shindano hilo Joseph Kapinga alisema jana kuwa jumla ya warembo 16 wanatarajia kupanda jukwaani kuwania taji hilo linaloshikiliwa na Ambasia Mallya, ambaye alishinda taji hilo mwaka 2014.

  Mratibu huyo aliwataja warembo watakaoshiriki kuwa ni pamoja na Happiness Paul (21), Neema Makwaia (21), Rose Lucas (22), Mariam Maabadi 23), Sabrina Khalifa (20), Catherine Alex (22) na Grace Malikita (21).

  Warembo wengine ni Rachel George (21), Nasra Munna (23), Jackline Evarest (21), Flora Msigwa (21),  Noela Pastory (21), Neema Zablon (24) na Jesca Jackson (22).

  Aliongeza kuwa warembo watano watakaofanya vizuri katika shindano hilo, watapata tiketi ya kuiwakilisha Tabata katika shindano la Kanda ya Ilala baadaye mwaka huu.

  Alisema kuwa warembo watakaoingia tano bora kila moja atazawadiwa kusoma nafasi ya kusoma kozi yoyote katika Chuo cha DataStar Training College. Kila kozi itagharimu 1.8m/-
  Mshindi wa kwanza pia atapata fedha  taslimu Sh. 300,000 wakati mshindi wa pili ataondoka na Sh. 200,000 huku mrembo atakayeshika nafasi ya tatu atajinyakulia Sh. 150,000.

   Mshindi wan ne na watano kila mmoja atapata Sh. 100,000 huku kifuta jasho cha Sh. 50,000 kila m Wengine ni Rachel George (21), Nasra Munna (23), Jackline Evarest (21), Flora Msigwa (21),  Noela Pastory (21), Neema Zablon (24),  Narcisa Wilbert (19) na Jesca Jackson (22).
  moja kitatolewa kwa waliobakia.

  Bendi ya Twanga Pepeta itatumbuiza kwenye shindano hilo linaloandaliwa na Keen Arts na Bob Entertainment.
  Nae Mkurugenzi wa Miss Tabata ambae pia ni mkuu wa kambi Godfrey Kalinga alisema jana kuwa maandalizi ya shindano limekamilika.

  Miss Tabata inadhaminiwa na Lete Raha, DataStar College, Global Publishers, CXC Africa, Fredito Entertainment, Yono Auction Mart, Saluti5, Kitwe General Traders na Bob Entertainment.

older | 1 | .... | 911 | 912 | (Page 913) | 914 | 915 | .... | 1897 | newer