Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46371 articles
Browse latest View live

Hoyce temu awafunda miss kigamboni

$
0
0
Pichani ni washiriki wa Miss Kigamboni wakiwa na miss Tanzania mwaka 1999 Hoyce Temu aliyekuwa akiwafunda warembo wa miss kigamboni, amewaeleza mambo mbali mbali kuhusiana na masuala ya urembo likiwemo suala la nidhamu na kujitambua katika jamiii.

MAJANGA YA BODA BODA

$
0
0
 Pichani juu ni  Lori aina ya Fuso likiwa limeigonga pikipiki iliyokuwa inakatiza kwenye taa nyekundu leo kwenye njia panda ya Segerea,Dereva wa pikipiki akiugulia maumivu kabla ya kupatiwa msaada wa kukimbizwa hospitali.

MKUTANO WA VIONGOZI WA MATAWI YA VYUO YA CCM WAFANYIKA JIJINI DAR LEO.

$
0
0
 Kaimu Mwenyekti vyuo vikuu, wilaya ya Dar es salaam, Assenga Abubakar (Kushoto),Katibu Msaidizi Mkoa wa vyuo vikuu,anayeshughulikia  na mikoa ya Dar es salaam na Zanzibar na Kepteni mstaafu,Alhaji Mohamed Ligola wakiwa kwenye mkutano na viongozi wa matawi ya vyuo ya CCM DSM.
Baadhi ya viongozi wa matawi ya CCM ya vyuo vikuu mkoa wa Dar es salaam wakiwa kwenye mkutano wao ambao pamoja na kujadili masuala mbali mbali ya kisiasa na masaula ya gesi Mtwara pia walipata wasaa wa kupata Darasa la Itikadi.

RAIS KIKWETE KATIKA MKUTANO WA SHEREHE ZA MIAKA 50 YA AU JIJINI ADDIS ABABA LEO

$
0
0
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete Mkutano wa Sherehe za miaka 50 ya AU katika makao makuu ya umoja huo jijini Addis Ababa leo Mei 25, 2013. 
 Muono wa jicho la samaki katika Mkutano wa Sherehe za miaka 50 ya AU katika makao makuu ya umoja huo jijini Addis Ababa leo Mei 25, 2013 
 Marais Wastaafu wakiwa katika Mkutano wa Sherehe za miaka 50 ya AU katika makao makuu ya umoja huo jijini Addis Ababa leo Mei 25, 2013
 Viongoi AU wakiwakumbuka waliotangulia mbele ya haki.PICHA NA IKULU

Issere Sports yatoa jezi, mipira kwa vijana Kondoa

$
0
0

Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Isere Sports, Abbas Ally Isere (kulia) akimkabidhi jezi seti moja mwakilishi, Dige Shaaban Nkusa kwa ajili ya timu ya vijana wa kijiji cha Mwembeni wilayani Kondoa ili kuimarisha michezo vijijini.

 =======  =====  ======

KAMPUNI ya Isere Sports imetoa vifaa vya michezo vyenye thamani ya sh. mil. 1.7 kwa ajili ya kuendeleza vijana katika wilaya ya Kondoa.

Akikabidhi vifaa hivyo jana, Mkurugenzi wa Masoko wa Isere Sports, Abbas Isere alisema ametoa vifaa hivyo ili kuwasaidia vijana kupenda michezo ili kujenga afya na kujikinga na vitengo cha kihalifu.

Abbas alisema vifaa alivyotoa ni kwa ajili ya vijiji vya Changaa kwa Mafunchi ambako wamepewa jezi, mipira na soksi, katika kijiji cha Mwembeni kata ya Hondomairo wilayani Kondoa wamekabidhiwa vifaa kama hivyo.

Akipokea vifaa hivyo kwa niaba ya vijana wa Changaa, Issa Lubuva alisema umefika wakati kwa wananchi waishio mijini kuwakumbuka vijana waliobaki nyumbani kwa kuwapatia vifaa vya michezo.

Naye Dige Shaaban aliyepokea vifaa kwa niaba ya kijiji cha Mwembeni alisema wachezaji wengi wapo vijijini lakini hawajapata fursa ya kuonesha vipaji vyao hivyo vifaa hivyo vitasaidia kutoa wachezaji kutoka wilaya ya Kondoa.

Madabida mgeni rasmi Tamasha la wasanii chipukizi la Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA)

$
0
0
MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida atakuwa mgeni rasmi katika tamasha la Mastaa chipukizi zaidi ya 320 litafanyika Jumapili 26, 2013 katika ukumbi wa Starlight Hotel kuanzia saa 4 asubuhi.

 

Peter Mwenda

                             

Mwenyekiti wa Shiwata, Caasim Taalib alisema Madabida ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) atapata nafasi ya kuona vikundi mbalimbali vya sanaa kikiwepo kikundi cha  Kaole, Splendid, Super Shine Taarab pamoja na wasanii mbalimbali wa Bongo Flava, Maigizo,Ngoma, Dansi na Sarakasi nao wamethibitisha kushiriki.

Taalib alisema wasanii wakongwe wa bongo flava walioalikwa ni Stara Thomas, Safi Theatre Group, Ommy G na waigizaji wakongwe wa Kaole na Splendid wataonesha umahiri wao katika fani ya sanaa Kauli Mbiu ikiwa ni Kilio cha Msanii .

Vikundi vingine vitakavyonesha vipaji vyao ni Kepteni  Shaibu, Tanzania Disabled, Uyoga Boga Village, Ndafu Arts Group, CGC, Magengistar Crew, Dodo Arts Group, Culture Arts Group, Wachapa Kazi Academy, Soweto Picture, Shiwata Commedy, Mwavionelachi, Manuari Arts Group, Tandale Morden Taarab na Begeja Wushu,
 Taalib alisema tamasha hilo ambalo limepata kibali cha Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) pia wamealikwa Shirikisho la Sanaa za Maonesho Tanzania,Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF),Shirikisho la Muziki Tanzania na Shirikisho la Sanaa za maonesho Tanzania.
Mwenyekiti aliwaomba viongozi wengine wa bendi za muziki, taarab, vikundi vya sanaa,mapromota,maprodusa na wadau wote kushiriki katika tamasha hilo ili kujenga ushirikiano wa pamoja.

USAHIRI WA SHINDANO LA BIBI BOMBA WAFANYIKA LEO KWENYE VIWANJA VYA LEADERS CLUB, TAMASHA LA NYIMBO ZA MAKABILA LINAENDELEA

$
0
0
 Majaji wa Shindano la 'Bibi Bomba' kutoka (kushoto) Zamaradi Mketema, Babuu wa Kitaa, Regina Mwalekwa na Benny Kinyaiya, wakifuatilia washiriki wakati wakijieleza kuhusu ufahamu wa shindano hilo, lililoanza leo katika Viwanja vya Leaders Club Kinondoni, wakati wa Tamasha la Nyimbo za Makabila 'Tamadunika' linaloendelea hivi sasa viwanjani hapa.
 Mmoja kati wa washiriki 32, akijieleza wakati wa mahojiano rasmi viwanjani hapo....
  Mmoja kati wa washiriki 32, akijieleza wakati wa mahojiano rasmi viwanjani hapo....
 Baadhi ya wanacrew wasimamizi wa shoo hiyo, wakiwa eneo la tukio.....
 Babu wa Kitaa, (kushoto) akiburudika kwa miondoko ya sebene na mmoja wa washiriki wa shindano hilo.
 Sehemu ya washiriki waliojitokeza kushiriki shidano hilo...
 Mshiriki akijieleza......
 Watazamaji wakifuatilia shindano hilo......
Waongozaji wa Tamasha hilo, wasema lolote, Mbwiga Mbwiguke na Suzzy Bartazar, wakijiandaa kusherehesha Tamasha hilo la Nyimbo za Makabila.
 Benny Kinyaiya, akitoa maelezo mafupi kwa washiriki wa shindano la Bibi Bomba.......
 Gea Habib, akifafanua jambo kwa washiriki wa shindano hilo....
 Sehemu ya watazamaji......
Sehemu ya watazamaji waliojitokeza kushuhudia Tamasha hilo.....

TASWIRA MBALIMBALI ZA MAKAO MAKUU YA UMOJA WA AFRIKA JIJINI ADDIS ABABA WAKATI WA KUADHIMISHA MIAKA 50 YA UMOJA HUO

$
0
0
 Wajumbe, wageni waalikwa, wanahabari na wadau mbalimbali wakijichanganya nje ya ukumbi wa mkutano wakati wa mapumziko
  
 Viongozi wa nchi mbalimbali waliohudhuria 
 Mandhari za nje na ndani ya jengo la Makao Makuu ya Umoja wa Afrika jijini Addis Ababa, Ethiopia
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Mhe Ban Ki Moon akiwa meza kuu pamoja na Rais wa AU Mama Nkosazana Dlamini Zuma na Waziri Mkuu wa Ethiopia Mhe. Hailemariam Desalegn na viongozi wengine wa umoja huo

  
 Sehemu ya ukumbi wa mikutano kwa ndani.PICHA NA IKULU.


TASWIRA WAKATI WA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA AU JIJINI ADDIS ABABA, ETHIOPIA

$
0
0
 Marais wastaafu waliohudhuria maadhimisho ya miaka 50 ya AU katika makao makuu ya Umoja huo jijini Addid Ababa, Ethiopia. Kutoka kushoto ni Dkt Kenneth Kaunda (Zambia), Sam Nujoma (Namibia) na Mzee Festus Mogae (Botswana)

  Mama Salma Kikwete na wake wa marais wengine wakiwa katika mkutano wa maadhimisho ya miaka 50 ya AU katika makao makuu ya Umoja huo jijini Addid Ababa, Ethiopia

  Wapiga picha toka nchi mbalimbali wakiwa kazini wakati wa mkutano wa maadhimisho ya miaka 50 ya AU katika makao makuu ya Umoja huo jijini Addid Ababa, Ethiopia.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoka katika chumba cha mikutano baada ya kuhudhuria kikao cha 29 cha wakuu wa nchi za NEPAD pembeni ya mkutano wa maadhimisho ya miaka 50 ya AU katika makao makuu ya Umoja huo jijini Addid Ababa, Ethiopia.
Wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika na wageni mashuhuri walioalikwa wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa mkutano wa maadhimisho ya miaka 50 ya AU katika makao makuu ya Umoja huo jijini Addid Ababa, Ethiopia.PICHA NA IKULU

Tamasha la ngoma za kiasili lilivyorindima ndani ya viwanja vya lida club,jijini dar

A SNEAK PEEK INTO BIG BROTHER HOUSE!

$
0
0
The Countdown to the launch of Big Brother The Chase has begun! With just two days to go, many surprises await eagerly anticipating audiences across the continent, including the all important Big Brother house. A character in its own right, the house is always subject to interest and now AfricaMagic has unveiled a sneak peek in the Big Brother house.

Modern, trendy and contemporary are just some of the words that define the imagery of the house. This year’s look is definitely distinctive, featuring a solid use of bright colour with a sophisticated polish. The décor is fresh and airy with a cosmopolitan and yet youthful demeanor, dominated by straight lines and square finishes.

Audiences and housemates can also expect intriguing fixtures that will certainly create talkability. There are also unique accessories thoughout the house creating a cosy and homey ambiance. The house is also technically well equipped and Biggie can watch 24/7, thanks to 56 cameras and 137 microphones.

More of the house will be revealed on Sunday May 26 at 20:00 when audiences from over 50 African countries are introduced to the 28 housemates for the first time. Tune into the Big Brother live launch show on AfricaMagic, AfricaMagic Entertainment and AfricaMagic World, as well as on DStv channel 197 and 198. The launch will also stream live on the Big Brother website.
Big Brother The Chase is headline sponsored by Airtel and is produced by Endemol.

The excitement is building and audiences can also join the conversation on Facebook and Twitter. Africa biggest reality series will be screened live 24/7 on DStv channels 197 and 198.

Hafla ya Uzinduzi wa Big Brother The Chase 2013 wafana sana jijini Dar

$
0
0
Meneja Uhusiano wa MultiChoice Tanzania, Barbara Kambogi akizungumza maneno machache muda mfupi kabla ya kuanza kwa Show ya Big Brother The Chase 2013 usiku huu pale kwenye Kiota cha Maraha cha Samaki Samaki kilichopo maeneo ya katikati ya Jiji la Dar es salaam,ambapo wadau mbali mbali walihudhulia hafla hiyo.
 Kabla ya kuanza uzinduzi wa Show ya Big Brother The Chase 2013 usiku huu pale kwenye Kiota cha Maraha cha Samaki Samaki kilichopo maeneo ya katikati ya Jiji la Dar es salaam,ilichezeshwa bahati nasibu ndogo iliyompelekea mdau huyu (kushoto) kuibuka na Tablat mpya kabisa.kulia ni Mshereheshaji wa hafla hiyo,Millard Ayo.
Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya nchini,Ambwene Yessaya a.k.a AY akisoma kikaratasi wakati akimtaja mshindi wa bahati nasibu ya shilingi laki moja.
Wadau wakiwakilisha ndani ya Samaki Samaki,toka shoto ni Missie Populer,Othman,B12,Jimmy,Mdau pamoja na Kajunason.

Feza Kessy na Nando waiwakilisha Tanzania kwenye Shindano la Big Brother-The Chase 2013

$
0
0
IMG_0156
Kundi la Mafikizolo la nchini Afrika Kusini likitoa burudani wakati wa uzinduzi wa show ya Big Brother-The Chase iliyorushwa Live na Channel za DStv 197 na 198 jijini Johannesburg usiku huu. Shindano la Big Brother-The Chase limedhaminiwa na Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel.
IMG_0140
Baadhi ya wageni waalikwa wakiwemo waandishi wa habari kutoka nchin mbalimbali za Afrika kushuhudia Live uzinduzi huo.
IMG_0209
Mwakilishi kutoka Tanzania Nando akihojiwa na Mtangazaji wa kipindi hicho Ik wakati wa uzinduzi wa show hiyo.Kushoto patna wa Nando Mshiriki kutoka Namibia Cleo.
IMG_0226
Mwakilishi wa Tanzania Feza Kessy akiwasalimu mashabiki wake kwa kuwapungia bendera ya Tanzania. Kulia ni mtangazaji wa Shindano la Big Brother The Chase 2013 Ik.
IMG_0231
Mtangazaji IK akifanya mahojiano na Patna wa Mwakilishi wa Tanzania Mshiriki kutoka Ghana Elikem wakati wa uzinduzi wa Shindano la Big Brother The Chase lililozinduliwa rasmi leo jijini Johannesburg Afrika Kusini ambapo washiriki watakaa ndani ya jumba hilo kwa siku 90 na mshindi kujinyakulia kitita cha Usd 300,000. Kulia ni Feza Kessy mshiriki kutoka Tanzania.
IMG_0235
Mtangazaji IK akimtambulisha rasmi mshiriki kutoka Tanzania Feza Kessy kwa Patna wake Mshiriki kutoka Ghana Elikem wakati wa uzinduzi wa shindano hilo leo jijini Johannesburg.
IMG_0108
Baadhi ya waandishi wa habari kutoka nchi mbalimbali za Afrika waliopata  mwaliko wa kuhudhuria uzinduzi wa shindano hilo Live kutoka Kampuni ya Multichoice Africa. Wa pili kulia ni Operations Manager wa Mo Blog Zainul Mzige aliyeiwakilisha Tanzania.
IMG_0081
Kutoka kushoto ni Mwandishi wa habari kutoka Afrika Kusini Munya, Buhle na Thato kutoka Ofisi za Multichoice Afrika Kusini wakishow love back stage wakati wa uzinduzi wa shindano la Big Brother The Chase.
IMG_0083
Wageni waalikwa kutoka mataifa mbalimbali mbele ya camera yetu.
IMG_0098
Mini Bar iliyondaliwa maalum kwa wageni waalikwa.
IMG_0220
Msanii wa muziki wa Hip Hop kutoka nchini Kenya Stella Mwangi a.k.a STL akitoa burudani huku akipewa sapoti na Manager wake.Picha na Zeinul Mzige - Mo Blog
IMG_0218

NCHI 22 ZA AFRIKA ZAPATA DARASA JUU YA AMANI YA MTU BINAFSI JANA

$
0
0

Mtaalam na mkufunzi wa masuala ya amani ya mtu binafsi kwa njia ya kutafakari kutoka taasisi ya Art of Living, Chandrika Magaraja akitoa maelezo juu ya amani ya mtu binafsi inavyoweza kupatikana kwa kutafakari wakati wa kushiriki Mafunzo hayo yalifanyika jana kwa njia ya video na kufanyika kwa wakati mmoja kwa nchi 22 za Afrika na yaliongozwa na Kiongozi wa Art of Living Duniani ambaye pia ni Balozi wa Amani Sri Sri Ravi Shankar ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya Umoja wa Afrika (AU).


Baadhi ya wakazi wa Dar es Salaam walioshiriki katika katika kutafakari ambayo ni njia bora na yapekee ya kuleta amani ya mtu binafsi. Mafunzo hayo yalifanyika jana kwa njia ya video na kufanyika kwa wakati mmoja kwa nchi 22 za Afrika na yaliongozwa na Kiongozi wa Art of Living Duniani ambaye pia ni Balozi wa Amani Sri Sri Ravi Shankar ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya Umoja wa Afrika (AU). 

Balozi wa Jamhuri ya Djbout nchini Tanzania, Saidi Amin Shamo (kushoto) na Balozi wa India hapa nchini, Debnath Shaw wakishiriki katika kutafakari ambayo ni njia bora na yapekee ya kuleta amani ya mtu binafsi. Mafunzo hayo yalifanyika jana kwa njia ya video na kufanyika kwa wakati mmoja kwa nchi 22 za Afrika na yaliongozwa na Kiongozi wa Art of Living Duniani ambaye pia ni Balozi wa Amani Sri Sri Ravi Shankar ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya Umoja wa Afrika (AU). 
 Balozi wa Jamhuri ya Djbout nchini Tanzania, Saidi Amin Shamo (kushoto) Balozi wa India hapa nchini, Debnath Shaw (katikati) na Mwakilishi na Mtaalam na mkufunzi wa masuala ya Kutafakari kutoka Taasisi ya Art of Living, Chandrika Magaraja wakishiriki katika kutafakari ambayo ni njia bora na yapekee ya kuleta amani ya mtu binafsi. Mafunzo hayo yalifanyika jana kwa njia ya video na kufanyika kwa wakati mmoja kwa nchi 22 za Afrika na yaliongozwa na Kiongozi wa Art of Living Duniani ambaye pia ni Balozi wa Amani Sri Sri Ravi Shankar ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya Umoja wa Afrika (AU). 

Wageni maalum katika mafunzo maalum ya ya amani ya Mtu bianfsi kwa njia ya kutafakari kutoka kulia Mwakilishi na Mtaalam na mkufunzi wa masuala ya Kutafakari kutoka Taasisi ya Art of Living, Chandrika Magaraja,  Balozi wa India hapa nchini, Debnath Shaw, Balozi wa Jamhuri ya Djbout nchini, Saidi Amin Shamo, Mke wa Balozi Shamo, Mariam Shamo, Mke wa Mkurugenzi wa Kampuni ya Bia Serengeti (SBL) Theresa Gannon na Mkurugenzi wa SBL, Steven Gannon,  wakishiriki katika kutafakari ambayo ni njia bora na yapekee ya kuleta amani ya mtu binafsi. Mafunzo hayo yalifanyika jana kwa njia ya video na kufanyika kwa wakati mmoja kwa nchi 22 za Afrika na yaliongozwa na Kiongozi wa Art of Living Duniani ambaye pia ni Balozi wa Amani Sri Sri Ravi Shankar ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya Umoja wa Afrika (AU). 

MARTIN FUNDI NDIYE MSHINDI WA THE VODACOM MIC KING 2013

$
0
0
Meneja wa Mahusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu (kushoto) akimkabidhi ufunguo wa gari mshindi wa The Vodacom Mic King 2013, Martin Fundi. Katikati ni Meneja Matukio wa Dar Live, Abdallah Mrisho. Martin Fundi akifungia mlango wa gari lake.
...Akiingia.
...Akiliwasha gari lake.
Mashabiki wakiwa wamelizunguka gari la Martin Fundi.
Martin Fundi kutoka Kimara usiku wa kuamkia leo ameibuka kidedea katika shindano la The Vodacom Mic King 2013 na kujinyakulia gari jipya aina ya Toyota Funcargo (new model). Shindano hilo lililokuwa likidhaminiwa na Kampuni ya simu ya Vodacom lilidumu kwa takribani miezi sita na usiku wa kuamkia leo ndiyo limefika tamati.
(PICHA NA RICHARD BUKOS /GPL)

Miss Tabata waenda Mikumi

$
0
0

Redd’s Miss Tabata 2013 usiku wa kuamkia leo waliondoka kwenda kutembelea hifadhi ya taifa ya Mikumi. Mratibu wa shindano hilo Godfrey Kalinga alisema jana kuwa warembo hao waliondoka na gari ya aina ya Toyota Double Coaster ikiwa na warembo 20 pamoja na walimu na viongozi wao.  Kalinga alisema ziara hiyo ina lengo la kukuza utalii wa ndani na kujenga ushirikiano miongoni mwao.

Alisema kuwa warembo hao pia watapata fursa ya kutembelea vivutio mbalimbali vilivyomo kwenye mbuga hiyo iliyoko mkoani Morogoro. “Tutarudi Dar es Salaam Jumatatu kujiandaa na shindano letu litakalofanyika Ijumaa ijayo,” alisema Kalinga.  Kadhalika, Kalinga  alisema kuwa ziara hiyo imedhaminiwa na kampuni ya CXC Africa.  Shindano la kumsaka Miss Tabata  litafanyika Ijumaa ya Mei 31 katika ukumbi wa Da’ West Park, Tabata.

Wadhamini wa shindano hilo ni Nipashe, Redds, Dodoma Wine, Nipashe, Vayle Springs, Multichoice, Fredito Entertainment, Integrated Communications Limited, CXC Africa, Brake Point na Saluti5. Warembo hao ni Madgalena Bhoke (21), Kabula Juma Kibogoti (20), Upendo Dickson Lema (22),Hidaya David Mwenda (22), Aneth Ndumbalo (19),  Dorice Mollel (22), Eunice Nkoha (19), Kazunde Musa Kitereja (19),  Rehema Kihinja (20),  Pasilida Mandali (21), Brath Chambia (23), Joaniter Kabunga (21), Recho Mushi (20),Caroline Sadiki (20) na  Suzan Daniel (18).

Anayeshikilia taji la Miss Tabata kwa sasa ni Noela Michael ambaye pia ni Miss Ilala. Miss Tabata inaandaliwa na Bob Entertainment na Keen Arts.

Uzinduzi wa Big Brother The Chase 2013 ulinogaje sasa jijini Dar jana

$
0
0
 Big Brother The Chase imeanza sasa.
Meneja Uhusiano wa MultiChoice Tanzania, Barbara Kambogi akizungumza maneno machache muda mfupi kabla ya kuanza kwa Show ya Big Brother The Chase 2013 usiku huu pale kwenye Kiota cha Maraha cha Samaki Samaki kilichopo maeneo ya katikati ya Jiji la Dar es salaam,ambapo wadau mbali mbali walihudhulia hafla hiyo.
 Kabla ya kuanza uzinduzi wa Show ya Big Brother The Chase 2013 usiku huu pale kwenye Kiota cha Maraha cha Samaki Samaki kilichopo maeneo ya katikati ya Jiji la Dar es salaam,ilichezeshwa bahati nasibu ndogo iliyompelekea mdau huyu (kushoto) kuibuka na Tablat mpya kabisa.kulia ni Mshereheshaji wa hafla hiyo,Millard Ayo.
Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya nchini,Ambwene Yessaya a.k.a AY akisoma kikaratasi wakati akimtaja mshindi wa bahati nasibu ya shilingi laki moja.
Pongezi kwa mshindi wa kitita cha sh. laki moja.
bahati nasibu ikiendelea.
Wadau sie tukiwakilisha ndani ya Samaki Samaki,toka shoto ni Missie Populer,Mie,B12,Jimmy,Mdau pamoja na Kajunason.
Wadada wa Airtel,Dangio na Jannet.
Mdau Njedengwa akitafakari jambo.
Wadau.
mazungumzo ya hapa na pale kati ya Meneja Uhusiano wa MultiChoice Tanzania, Barbara Kambogi na MC Millard Ayo.
Mkuu wa Kitengo cha Masoko DStV,Dada Furaha Samalu akiwa na Mdau kwenye hafla hiyo.
Bahati nasibu ya kufungua box lenye zawadi huku kila mmoja akiwa na funguo yake.
Cathbert Angelo akizungusha mkono kwenye kindoo ili kuchagua jila la mshindi wa bahati nasibu.
Ni shangwe kwa kwenda mbele pale Mtanzania Feza Kessy alipoonekana ndani ya Jumba la Big Brother.
Wadau wakishoo lavu ndani ya Samaki Samaki.
Wengi walikuwa wakifuatilia kwa umakini zoezi hilo.

Exim Bank supports African Day Golden Jubilee celebrations

$
0
0
The African Development Bank (AfDB) Resident Representative in Tanzania, 
Tonia Kandiero (right) shares a light moment with the Exim Bank Tanzania 
Managing Director Anthony Grant (left) during Africa Day 2013-Golden Jubilee  celebrations held in Dar es Salaam at the weekend. The event was supported by Exim Bank. 
=======  ======  =========
Exim Bank supports African Day Golden Jubilee celebrations

THE African Development Bank (AfDB) Resident Representative in Tanzania, Tonia Kandiero has urged African countries including Tanzania to embark on intra-regional trade in a bid to achieve meaningful development within the next few years.

Speaking during the African Day Celebrations sponsored by Exim Bank Tanzania at the weekend, Kandiero said currently only 12% of Africa’s Trade is Intra-Regional adding that African states should now invest in infrastructural development to increase intra-regional trade.

Kandiero said AfDB has come up with the Africa’s Transformation Strategy 2013-2022 that seeks to support Africa’s economic development with Infrastructure development with five core operational priorities that include Regional integration, Private sector development, Governance and accountability and Skills/ technological development.

“Africa seeks to be competitive, diversified, integrated, prosperous, and a full participant in global trade and investment’ “This vision achievable because real GDP Growth and the number of FDI-financed greenfield projects in Africa are on a par with those in the BRICs,” she added.

Earlier, Foreign Affairs and International Cooperation Minister Bernard Membe noted that African states should now focus on economic empowerment in a bid to achieve increased economic development in years to come. “We can achieve fully   fledged integrated economies if we encourage intra-trade within our nations. This must go in line with developing good infrastructure networks,” Membe said

MARTHA GEWE AIBUKA KINARA REDD'S MISS UKONGA 2013

$
0
0
Mshindi wa Shindano la Redd’s Miss Ukonga 2013, Martha Gewe (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na mshindi wa pili, Diana Joachim (kushoto) pamoja na mrembo aliyeshika nafasi ya tatu, Natasha Mohamed mara baada ya warembo hao kutangazwa kuwa ndio washindi wa shindano hilo Usiku wa kuamkia jana katika shindano lililofanyika Ukumbi wa Wenge Garden Ukonga Mombasa jijini Dar es Salaam. Martha aliwashinda warembo wengine 12 katika shindano hilo.
Warembo waliofanikiwa kuingia hatua ya tano bora ya Redd’s Miss Ukonga 2013 wakiwa katika picha ya pamoja kutoka kushoto ni Vanesa Magile, Matha Gewe, Diana Joachim, Natasha Mohamed na Nancy Abasy shindano lilifanyika Ukumbi wa Wenge Garden Ukonga Mombasa jijini Dar es Salaam. Martha.
Baadhi ya washiriki wa Shindano la Redd’s Miss Ukonga 2013 wakicheza show ya ufunguzi wa shindano lao lililofanyika usiku wa kuamkia jana katika ukumbi wa Wenge Garden Ukonga jijini Dar es Salaam.

RAIS KIKWETE AKUTANA NA MARAIS WASTAAFU, AHUDHURIA KIKAIO CHA AMANI DRC CONGO

$
0
0
 Jakaya Mrisho Kikwete akizingumza na Marais Wastaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi, Mzee Benjamin Mkapa na Waziri Mkuu Mstaafu na Katibu Mkuu wa Umoja wa Afrika Mstaafu Dkt Salim Ahmed Salim kuhusiana na sherehe za miaka 50 ya AU alipokutana nao jijini Addis Ababa, Ethiopia, leo  Mei 26, 2013. Viongozi hao wastaafu ni miongoni mwa wageni mashuhuri walioaliokwa kwenye sherehe hizo.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na wanahabari baada ya kuhudhuria Mkutano wa Kanda wa Usimamizi wa Amani, Usalama na Ushirikiano katika DRC na nchi za Maziwa Makuu katika makao makuu ya Umoja wa Afrika leo Mei 26, 2013.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika  Mkutano wa Kanda wa Usimamizi wa Amani, Usalama na Ushirikiano katika DRC na nchi za Maziwa Makuu katika makao makuu ya Umoja wa Afrika leo Mei 26, 2013.PICHA NA IKULU.
Viewing all 46371 articles
Browse latest View live




Latest Images