Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 901 | 902 | (Page 903) | 904 | 905 | .... | 1898 | newer

  0 0


  Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali (Rt), Emmanuel Maganga akizindua mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) katika mkoa wake wa Kigoma leo. Mradi huo wa miaka mitano unafadhiliwa na Shirika la Misaada la Kimataifa la Marekani (USAID) na utatekelezwa katika mikoa 13 nchini na kushirikisha Halamashauri 93.
  Mkuu wa Mkoa aliwataka watendaji wa Halamashauri hizo kufanya kazi kwa bidii kuhakikisha mradi unaleta manufaa kwa jamii na mkoa.
  Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma Charles Pallangyo, akizungumza wakati wa uzinduzi huo. Wengine kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Mjini Samsoni Anga, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali (Rt), Emmanuel Maganga, Kiongozi wa Mradi wa PS3, Dk Conrad Mbuya na Mwakilishi kutoka Ofisi ya Rais Tamisemi.
  Kiongozi wa mradi wa PS3, Dk Conrad Mbuya akizungumza na kueleza dhumuni la mradi huo. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kigoma,Brigedia Jenerali (Rt), Emmanuel Maganga.
  Mwakilishi kutoka Tamisemi, Mrisho Mrisho akizungumza kuhusiana na mradi huo na namna ambavyo serikali imejipanga kuhakikisha utekelezaji wake unafanikiwa.
  Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Kigoma wakifuatilia kwa makini uzinduzi huo. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe, Kanali. Elisha Marco Gaguti, Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali.Hosea Malonda Ndagala na Mkuu wa Wilaya ya Kibondo Luis Peter Bura.
  Mkuu wa Wilaya Kasulu, Kanali. Martin Elia Mkisi akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Mwanamvua Hoza Mlindoko, wakifuatilia mada katika uzinduzi huo. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
  Msimamizi wa Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta ya Umma (PS3) Dk Conrad Mbuya akiwasilisha mada baada ya kufanyika kwa uzinduzi.  UZINDUZI wa kimkoa wa Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma, unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID), umefanyika mjini Kigoma siku ya Jumatatu na Jumanne, Julai 4-5, 2016. Mradi huo ujulikanao kwa Kiingereza kama Public Sector Systems Strengthening (PS3) ni wa miaka mitano, na utafanya kazi na Serikali Kuu pamoja na Halmashauri 93 katika mikoa 13 ya Tanzania bara.


  PS3 inalenga kuunda ushirikiano na Serikali ya Tanzania kwa ajili ya kuimarisha mifumo ya sekta za umma yakiwemo masuala ya utawala bora, rasilimali watu, fedha, utoaji wa taarifa, na tafiti tendaji. Ushirkiano huu wa PS3 katika ngazi ya Serikali kuu na Halmashauri, una nia ya kukuza utoaji, ubora, na matumizi ya huduma za umma, hususan kwa jamii ambazo hazijanufaika vya kutosha katika uzinduzi huo, mgeni rasmi alikuwa ni Mkuu wa Mkoa waKigoma, Mh. Brigedia Jenerali (Mstaafu) Emmanuel Maganga. Watu takribani 250 walihudhuria.


  Washiriki wa uzinduzi huo walikuwa ni: Katibu Tawala wa Mkoa (RAS), Wakuu wa Wilaya za Lindi, Wenyeviti wa Halmashauri, Wakurugenzi wa Halmashauri, Wajumbe wa Sekretarieti ya Mkoa, na Wajumbe wa Timu ya Mejenimenti kutoka kwenye Halmashauri. Mkoa wa Kigoma una Halmashauri nane, ambazo ni: Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma, Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma, Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu, Halmashauri ya Mji wa Kasulu, Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo, Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko, Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza, na Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe.


  PS3 ni mradi wa miaka mitano ambao umeandaliwa na USAID kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania, na unafadhiliwa na USAID. Unatekelezwa na mashirika saba yakiwepo ya kitaifa na kimataifa, ambayo ni: Abt Associates Inc., kama mtekelezaji mkuu, na watekelezaji wasaidizi ambao ni Taasisi ya Benjamin Mkapa (BMF), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo cha Mafunzi ya Serikali za Mitaa Hombolo (LGTI), Taasisi ya Ushauri Tanzania (TMA), Broad Branch Institute, Intra Health International, na Urban Institute. Mikoa 13 ya Tanzania Bara ambako mradi utatekelezwa ni: Iringa, Dodoma, Kagera, Kigoma, Lindi, Mara, Mbeya, Morogoro, Mtwara, Mwanza, Njombe, Rukwa, na Shinyanga.


  MIFUMO YA SEKTA ZA UMMA


  PS3 itaimarisha mifumo katika ngazi ya Taifa, Mkoa na Halmashauri. Mradi utahakikisha mifumo iliyopo katika ngazi ya Halmashauri inaimarishwa kupitia kitita cha afua zilizoundwa kwa ajili ya kuongeza ufanisi wa utoaji huduma kwa wananchi wa Tanzania. Mafanikio yanayotarajiwa ni pamoja na:


  Utawala Bora na Ushirikishwaji wa Raia: Uimarishaji wa utawala katika ngazi ya kitaifa na ya Mamlaka za Serikali za Mitaa, ili kuweza kutumia rasilimali kwa uwazi, kuwezesha ushiriki wa wananchi katika kupanga, kufuatilia, na kutoa matokeo katika kila sekta.


  Rasilimali Watu: Kuongezeka kwa usawa katika mgawanyo wa rasilimali watu kwa ajili ya utoaji wa huduma bora kwenye maeneo yenye uhitaji zaidi. Kuimarisha mfumo wa ajira pamoja na kudumu kwa watumishi katika ajira serikalini.


  Fedha: Ongezeko la pato la ndani kwa ajili ya huduma za umma, kuongeza ufanisi katika matumizi ya fedha za umma, na pia kuongeza uwiano kati ya kiasi cha fedha kilichotumika na mali iliyonunuliwa.


  Mifumo ya Mawasiliano: Kuimarisha mifumo ya utoaji taarifa iliyopo nchini, pamoja na matumizi ya takwimu kwa wadau.


  Utafiti Tendaji: Tafiti Tendaji muhimu zitakazosaidia mradi kujua changamoto na mikakati ya kuzishughulikia changamoto hizo. Tafiti hizi zitasaidia kugundua fursa zilizopo na kuzitumia kuweza kupata matokeo yanayotarajiwa. Pia tafiti hizo zitasaidia kuboresha maamuzi serikalini.
  Dk Gemin Mtei akiwasilisha mada kuhusiana na mikakati ya kufanikisha mradi huo.
  Aloyce Maziku kutoka PS3 akiwasilisha mada kuhusiana na Tafiti Tendaji.
  Mkuu wa Wilaya ya Uvinza, Mwanamvua Mlindoko akifuatilia mada hizo kwa makini.
  Washiriki wakifuatilia mada kwa umakini.
  Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe, Kanali. Elisha Marco Gaguti akisikiliza kwa makini.
  Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali.Hosea Malonda Ndagala akiwa makini kusikiliza mada zinazowasilishwa.
  Wakuu wa Wilaya na washiriki wengine wakifuatilia mada.
  Benchi la Ufundi la mradi wa PS3 wakiwa kazini.


  Washiriki wakiuliza maswali
  Matiko Machonchoryo akijibu moja ya maswali yaliyoulizwa.
  Mshauri wa Habari na Mawasiliano katika Mradi wa PS3, Leah Mwainyekule akielezea jambo.
  washiriki wakiwa mkutanoni.
  Mkuu wa Mkoa wa Kigoma (wapili kulia) akiagana na Msimamizi wa mradi wa PS3, Dk Conrad Mbuya baada ya uzinduzi. Kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma, Charles Pallangyo na kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kigoma mjini,Samsoni Anga.  Picha za pamoja na makundi mbalimbali.


  Picha ya pamoja kati ya viongozi na waratibu wa mradi wa PS3.

  0 0


  Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi (katikati), akikata utepe wakati wa uzinduzi rasmi wa Ofisi ya Tanapa jijini Dar es Salaam. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Allan Kijazi.
   
  Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi (katikati), akikata utepe wakati wa uzinduzi rasmi wa Ofisi ya Tanapa jijini Dar es Salaam.

  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Allan Kijazi akizungumza wakati wa ufunguzi wa Ofisi ya TANAPA jijini Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande)
  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Allan Kijazi akizungumza wakati wa uzinduzi wa Ofisi za TANAPA jijini Dar es Salaam.
  Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi (katikati), akikata utepe wakati wa uzinduzi rasmi wa Ofisi ya Tanapa jijini Dar es Salaam. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Allan Kijazi.
  Baadhi ya wadau wa sekta ya Utalii wakiwa katika hafla hiyo.

  Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi akiangalia ofisi mpya ya TANAPA iliyopo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Allan Kijazi.
  Kuangalia ofisi.
  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Allan Kijazi (kushoto), akifafanua jambo wakati Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi (kulia) alipokuwa akikagua Ofisi ya Tanapa zilizopo jijijini Dar es Salaam.
  Chumba cha mikutano.
  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Allan Kijazi (kulia), akifafanua jambo wakati Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi (kushoto).
  Jengo la Ofisi za TANAPA zilizopo Dar es Salaam.

  0 0

  Zikiwa zimesalia siku kadhaa kabla ya kusherekea sikukuu ya Eid El Fitri, Kampuni ya Multichoice Tanzania ambao ndiyo wasambazaji wa ving'amuzi vya DSTV nchini imetoa msaada wa vitu mbalimbali kwa watoto yatima ambao wanaishi katika kituo cha Al-Madina kilichopo Tandale kwa Tumbo, misaada ambayo kwa namna moja au nyingine inaweza kusaidia kubadilisha maisha ya watoto hao.

  Misaada ambayo imetolewa kwa watoto hao ni Cherehani 4, kapeti 12, vikombe 60, sahani 40, magodoro 11, shuka 40, tenga za nguo 3, jagi 6, beseni kubwa 3, sufuria 9, chupa za chai 4 na mikeka 6.Akizungumzia misaada hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania, Maharage Chande alisema msaada huo ni mwendelezo wa misaada ambayo Multichoice imekuwa ikitoa kwa kituo hicho kwa lengo la kuwasaidia kuishi maisha bora lakini pia kuwapatia msaada ambao unaweza kuwasaidia kuwa na uwezo wa kuingiza kipato.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania, Maharage Chande akizungumza kuhusu msaada ambao wameutoa kwa kituo cha Al--Madina.

  "Multichoice tumekuwa tukitoa misaada yetu kwa kituo hiki tangu 2009 na leo tumewaletea mwingine ikiwa ni kila mwaka tunafanya hivyi lakini kwa mwaka huu tumeleta pia Cherehani ambazo zitawasaidia kupata kipato,
  "Pamoja na hayo pia tumewafungia king'amuzi ambacho watoto watakuwa wakiangalia vipindi balimbali baada ya kurejea nyumbani na tuna chaneli mbalimbali za vipindi vya watoto na burudani kwahiyo tunaamini kuwa watoto watafurahi," alisema Chande.

  Nae mlezi wa kituo hicho, Bi. Kuruthum Yusuf aliwataja Multichoice kama kampuni ambayo imekuwa mstari wa mbele kuwapatia misaada na kuyaomba makampuni mengine kuwa na utaratibu kama wa Multichoice wa kuwasaidia misaada kutokana na kuwa na idadi kubwa ya watoto ambao wanahitaji misaada ili kuboresha maisha yao.

  Mlezi wa kituo cha watoto yatima cha Al-Madina akizungumza kuhusu msaada ambao wamepokea na jinsi ambavyo Multichoice Tanzania imekuwa ikiwapatia misaada. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania, Mharage Chande.

  "Tangu walipotufahamu wamekuwa wakitupatia misaada kila mwaka, niwashukuru sana kwa moyo wao na kutoa sio utajiri ila tu wana moyo wa kutoa na hata wenngine wanatakiwa kuwa na moyo kama wao (Multichoice) wa kusaidia," alisema Bi. Kuruthum.Pamoja na hayo pia, Bi. Kuruthum alieleza kuwa kwa sasa bado wanakabiliwa na changamoto ya vifaa vya shuleni kwa watoto ambao wanasoma.

  Kutokana na msaada ambao umetolewa na Multichoice kwa watoto wa kituo cha Al-Madina ambacho kina watoto 57, wasichana wakiwa ni 23 na wavulana ni 34 basi ni wazi kuwa kama wakitumia msaada huo vyema basi kwa namna moja au nyingine wanaweza kubadilisha maisha yao kwa hatua fulani ambayo awali hawakuwa nayo kama vile kutumia cherehani kwa kushona nguo na kujiongezea kipato.
  Meneja Uhusiano na Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Sumalu akitoa neno la ufunguzi kuhusu misaada ambayo imekuwa ikitolewa na Multichoice Tanzania pamoja na historia fupi ya kituo hicho.  Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania, Mharage Chande akimkabidhi Cherehani, mlezi wa kituo cha Al-Madina, Kuruthum Yusuf. Wa tatu kushoto ni Meneja Uhusiano na Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Samalu wakiwa na wafanyakazi wengine wa Multichoice Tanzania.

  Meneja Uhusiano na Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Samalu akimpongeza mlezi wa kituo cha Al-Madina, Kuruthum Yusuf baada ya kukabidhiwa misaada na Multichoice Tanzania.
  Wafanyakazi wa Multichoice Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na watoto yatima wanaoishi katika kituo cha Al-Madina.
  Meneja Uhusiano na Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Samalu akiwaelekeza jambo watoto wanaoishi katika kituo cha Al-Madina.
  Watoto yatima wanaoishi katika kituo cha Al-Madina wakiwa katika picha ya pamoja.
  Mwonekano wa vitu vilivyotolewa na Multichoice Tanzania kwa kituo cha kulelea watoto yatima cha Al-Madina.

  0 0

  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla amesema Serikali itaendelea kushirikiana na taasisi mbalimbali za watu binafsi zikiwemo zile za kidini na kijamii katika kufanikisha maendeleo ambapo amelipongeza Kanisa la Waadventista wa Sabato la Ilemela Jijini Mwanza kwa hatua yake kujenga Hospitali ya Kisasa ambayo itakuwa msaada katika Wilaya hiyo.

  Dk. Kigwangalla ambaye alikuwa mgeni rasmi katika tukio hilo la ufungaji wa sherehe za miaka 50 ya Jubilee ya kuanzishwa Utume wa Kanisa la Waadventista wa Sabato katika jiji la Mwanza tukio lililofanyika siku ya Julai 3.2016 kwenye uwanja wa CCM Kirumba.

  Akitoa hotuba za kufunga sherehe hizo, Dk. Kigwangalla amelipongeza kanisa la Kirumba kuwa na jubilee ya miaka 50 Lakini pia amelipongeza kwa huduma ya malezi ya vijana wa kanisa hilo wakingali wadogo na kwamba kwa kufanya hivo ni kuliandaa kanisa na Taifa kwa ujumla kuwa na viongozi waadilifu.Dk. Kigwangalla ameyataka madhehebu ya dini yawe mstari wa mbele katika kukemea maovu ili Taifa lidumu kuwa na Amani.

  “Uwepo wenu tunaupongeza kwani naamini mumekuwa mstari wa mbele katika kuliombea Amani Taifa hili na pia kuwaombea ulinzi watu mbalimbali pamoja na kutoa misaada, huduma za Afya na mambo mengine mbalimbali. Hii ni faraja sana na Serikali tutaendelea kuwaunga mkono.

  Aidha, katika hutuba hiyo, Dk. Kigwangalla aliwahakikishia uongozi wa kanisa hilo kuwa Hospitali yao mpya inayojengwa Serikali itakuwa nao bega kwa bega na kuaahidi kutoa ushirikiano katika suala hilo la ujenzi pamoja na uendeshaji wa Hospitali hiyo kwa lengo la kuboresha afya za Wananchi wote.Katika hatua nyingine, Dk. Kigwangalla alikemea vitendo vilivyoanza kushamili ikiwemo baadhi ya watu kushabikia masuala ya mapenzi ya jinsia moja ambapo ikiwemo suala la ushoga.

  “Serikali haipo tayari kuona vitendo vya ushoga vinafanyika kwa wananchi wake lakini pia kuzitangaza kwa jamii. Wizara yangu itakutana na NGOs, zote za Kijamii na taasisi zilizosajiliwa ambazo pia zingine zipo chini ya Wizara yetu kukaa nazo na kujua ni zipi zinajihusisha na masuala haya iwe kwa kutetea ushoga ama kubariki vitendo hivi, tutawachukulia hatua kali za kisheria na hata kuzifuta kabisa” alimalizia Dk. Kigwangalla.

  Aidha, katika tukio hilo, Dk. Kigwangalla alipata kutembelea ujenzi wa Hospitali hiyo mpya na ya kisasa inayotarajiwa kukamilika kwake hapo baadae na kisha kuwasili kwenye viwanja vya CCM Kirumba ambapo pia alipata kukagua gwaride la vijana wadogo, wa kati na wa kanisa hilo ambao ni pamoja na vijana waliopatiwa mafunzo ya Kiroho, Kimwili na Kikakamavu wakiwemo Wavumbuzi (adventure) Watafuta njia (path finder-Pf), Mabalozi na Kiongozi Mkuu (Master Guide)Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla (katikati mwenye suti ya bluu) akiwa katika jengo la kisasa linalojengwa kwa ajili ya Hospitali ya Kanisa la Waadventista wa Sabato Jijini Mwanza.
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla akitoa maelezo namna ya miundo ya Hospitali na viwango vyake..Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa kanisa hiloKituo cha Afya kilichopo kwa sasa kikiendelea na hudumaNaibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla wakitoka walipotembelea jengo hilo la Hospitali linalojengwa..

  Picha ya jengo hilo la Hospitali pindi litakapokamilikaMuonekano wa mbali katika jengo hilo la kanisa

  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla akivikwa skafu maalum wakati alipowasili kwenye uwanja wa CCM Kilumba katika sherehe za kufunga Jubilee ya miaka 50 ya kanisa hilo Jijini Mwanza.  Heshima zikitolewa kwa mgeni rasmi

  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla wakishuhudia matembezi ya sherehe hizo  Matembezi ya sherehe hiyo yakiendelea  Sehemu ya umati wa watu katika tukio hilo la Jubilee ya Miaka 50  Vikundi vya matembezi yakiendelea  Jukwaa kuu wakishuhudia matembezi hayo  Vijana wadogo wa Path Finde-(PF) wakipita mbele ya mgeni rasmi kutoa heshima zao.

  Vijana wadogo wa Path Finde-(PF) wakipita mbele ya mgeni rasmi kutoa heshima zao  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla akielekea kukagua gwaride la vijana hao

  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla akikagua gwaride hilo

  Sehemu ya wananchi wakishuhudia tukio hilo

  Vijana PF wakipita kwa mwendo wa haraka mbele ya mgeni rasmi (Hayupo pichani)  Jukwaa kuu wakishuhudia matembezi hayo  Mbunge wa Jimbo la Ilemela ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk. Angeline Mabula akitoa salamu katika tukio hilo  Vijana wakiwa katika hali ya ukakamavu katika tukio hilo Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla akihutubia katika tukio hilo

  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla akipokea vitabu kama kutoka kwa uongozi wa kanisa hilo vyenye mafunzo mbalimbali

  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla akishuka katika jukwaa kuu mara baada ya kumalizika kwa tukio hilo.

  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na Jaji Mkuu na Mwanasheria Mkuu Mstaafu, Mzee Mark Boman.

  Mzee Boman ni miongoni mwa Wazee waanzilishi wa kanisa hilo ambalo kwa sasa limetimiza Jubilee ya Miaka 50.

  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla ateta jambo na Jaji Mkuu na Mwanasheria Mkuu Mstaafu, Mzee Mark Boman ambaye ni Mzee wa kanisa hilo. (Picha zote na Andrew Chale,modewjiblog-Mwanza).

  0 0

  Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe Annastazia James Wambura akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Finland Tanzania Pekka Hukka wakati wa kukabidhi Bendera ya Taifa kwa timu ya mpira wa miguu ya wasichana ya Fc Vito Malaika inayoenda kushiriki mashindano ya Helsinki Cup nchini Finland Julai 8 mwaka huu. ( Picha zote na Raymond Mushumbusi WHUSM)
  Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe Annastazia James Wambura (wa pili kulia) akikabidhi Bendera ya Taifa kwa nahodha timu ya mpira wa miguu Fc Vito Malaika Alia Fikiri (kushoto) kwenda kushiriki mashindano ya Helsinki Cup nchini Finland Julai 8 mwaka huu.
  Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura akizungumza na timu ya mpira wa miguu ya wasichana ya umri wa miaka 11 Fc Vito Malaika na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika hafla ya kukabidhi Bendera ya Taifa kwa timu hiyo kwenda kushiriki mashindano ya mpira wa miguu ya Helsinki Cup nchini Finland Julai 8 mwaka huu kushoto Mwakilishi wa Sport Development Aid Bw. Chigogolo Mohamed.

  Na Raymond Mushumbusi WHUSM

  Serikali imeazimia kujenga na kuendeleza shule za michezo zilizopo katika mikoa yote nchini kwa kipindi hiki cha Serikali awamu ya tano.

  Azimio hilo limetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura wakati akizungumza na timu ya mpira ya miguu ya wasichana ya Fc Vito Malaika katika hafla ya kukabidhi Bendera ya Taifa kwa timu hiyo kwenda kushiriki mashindano ya mpira wa miguu ya Helsinki Cup yatakayofanyika nchini Finland Julai 8 mwaka huu.

  “Azima ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kuendeleza michezo nchini kwa kuibua vipaji vya michezo na kuviendeleza kuanzia wakiwa shule” Alisema Mhe. Annastazia.  Mhe Annastazia Wambura ameongeza kuwa Serikali ya Tanzania inashirikia na Serikali ya Finland katika kuendeleza michezo shuleni na zaidi ya shule 462 nchini zitafaidika na miradi ya michezo ya vijana inayofadhiliwa na Serikali ya Finland.

  Kwa upande wake Balozi wa Finland nchini Tanzania Pekka Hukka amesema kuwa wamedhamiria kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kuendeleza michezo nchini hasa kwa vijana ili kujenga timu nzuri za baadae, na kwa sasa wanapeleka timu za vijana kwenda kushiriki mashindano mbalimbali ya kimataifa ikwemo Helsinki Cup linalofanyika nchini finland Julai 8 mwaka huu.

  Naye Meneja wa Timu ya wasichana ya mpira wa miguu ya Fc Vito Malaika Bakari selemani ameipongeza Serikali kwa juhudi zake za kuendeleza michezo hasa kwa vijana kwa kushirikiana na Taasisi mbalimbali na ili kuendeleza michezo na kukuza vipaji kwa vijana Serikali na wadau wa michezo wametakiwa kuwekeza kwa vijana ili kujenga timu zenye kuleta ushindani katika mashindano ya kitaifa na kimataifa. 


  0 0


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kwa mamlaka  aliyonayo kwa mujibu wa kifungu cha 48 cha sheria ya tafsiri za sheria (Interpretation of Laws Act)  Sura 1, leo tarehe 5 Julai, 2016 ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Maendeleo ya TIB Prof. William Lyakurwa.  Kufuatia hatua hiyo, kwa mujibu wa mamlaka aliyonayo chini ya kifungu cha 9 (2) cha ya Sheria ya mashirika ya umma (Public Corporations Act) Sura 257, Mhe. Rais amemteua Prof. Palamagamba J. A. M. Kabudi kushika nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Maendeleo ya TIB kwa kipindi cha miaka mitatu.  Kufuatia mabadiliko hayo, Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango  kwa mamlaka aliyonayo kwa mujibu wa kifungu cha 48 cha sheria ya sheria ya tafsiri za sheria (Interpretation of Laws Act)  Sura 1,  ametengua uteuzi wa Wajumbe Bodi ya Benki ya Maendeleo ya TIB. Aidha,  kwa mujibu wa mamlaka aliyonayo chini ya kifungu cha 9 (1) cha ya Sheria ya mashirika ya umma (Public Corporations Act, Sura 257) Mhe. Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango ameteua wajumbe wapya wa Bodi wafuatao kwa kipindi cha miaka mitatu:  1.      Brig. Gen (Rtd) Mabula Mashauri

  2.      Dkt. Razack B. Lokina

  3.      Bi. Rose Aiko

  4.      Prof. Joseph Bwechweshaija

  5.      Bw. Said Seif Mzee

  6.      Dkt. Arnold M. Kihaule

  7.      Bw. Maduka Paul Kessy

  8.      Bw. Charles Singili  Uteuzi  wa Mwenyekiti na Wajumbe wapya wa Bodi unaanza tarehe leo 5 Julai, 2016.   Gerson Msigwa

  Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

  Dar es salaam

  05 Julai, 2016.

  0 0  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akifungua mkutano wa Uwezeshaji viwanda baina ya China na nchi za Afrika uliofanyika jijini Dar es Salaam leo (jana), wa pili kutoka kulia ni Balozi wa China nchini Dr.Lu Youqing.
  Baadhi ya Wajumbe wa mkutano wa Uwezeshaji viwanda baina ya China na nchi za Afrika wakifuatilia hotuba ya ufunguzi iliyotolewa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (hayupo pichani), katika mkutano wa Uwezeshaji viwanda baina ya China na nchi za Afrika.

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akizungumza jambo na Balozi wa China nchini Dr.Lu Youqing wakati wa mkutano wa Uwezeshaji viwanda baina ya China na nchi za Afrika uliofanyika jijini Dar es Salaam leo .
  Balozi wa China nchini Dr.Lu Youqing kulia akiongea na mmoja wa wajumbe wa mkutano huo Prof. Ibrahim Lipumba mara baada ya ufunguzi wa mkutano wa uwezeshaji viwanda baina ya China na nchi za Afrika uliofanyika jijini Dar es Salaam
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa kushoto akiongea na mjumbe wa mkutano huo mara baada ya ufunguzi wa mkutano wa Uwezeshaji viwanda baina ya China na nchi za Afrika uliofanyika jijini Dar es Salaam leo
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa kushoto akifurahia jambo na Prof. Ibrahimu Lipumba mjumbe wa mkutano wa Uwezeshaji viwanda baina ya China na nchi za Afrika uliofanyika jijini Dar es Salaam leo.katikati ni Balozi wa China nchini Dr.Lu Youqing.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (wa tano kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa mkutano wa Uwezeshaji viwanda baina ya China na nchi za Afrika.Picha na Benjamini Sawe-Maelezo.

  0 0

  MAMLAKA ya Mapato Tanzania(TRA) itaendelea kudhibiti na kupambana na biashara za magendo katika vituo mbalimbali ambavyo vinaendelea na vitendo vya magendo.

  Hayo yamesemwa na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Alphayo Kidata wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. 

  Amesema TRA itazidi kupambana na kuziba mianya yote ya  upotevu wa mapato hususani katika msisitizo wa matumizi wa Mashine za Kieletroniki za kodi za EFDs pamoja na ukaguzi wa mara kwa mara na kufuatilia madeni.

  Pia amesema kuwa TRA itaendelea kudhibiti wafanyabiashara wanaokwepa kutumia mashine za Kieletroniki za kodi za (EFDs) kwa kuwakamata na kuwatoza faini au kuwafikisha mahakamani na kuwachukulia hatua za kisheria ili kuhakikisha inafikia na kuvuka malengo.

  Amesema kuwa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) imeshagawa mashine za Kieletroniki za EFDs 1120 kwa wafanyabiashara wanaostahili kupata mashine hizo bure na ambao hawajachukua machine za kieletroniki za kodi za EFDs ili kuwezesha TRA kukusanya mapato ya Serikali.
  Kamishna wa mapato ya ndani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Elijah Mwandumbya akifafanua juu ya Operesheni ambayo itatumika katika makusanyo ya ndani ambapo watapita nyumba kwa nyumba na mtaa kwa mtaa na fremu kwa fremu katika kugawa Mashine za Kieletroniki za EFDs kwaajili ya Kukusanya kodi kwa kila Mfanyabiashara Kushoto ni  Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Alphayo Kidata.
   Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Alphayo Kidata(Kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) kuvuka lengo la makusanyo ya Kosi kwa mwaka 2015/2016.Kulia ni Kamishna wa mapato ya ndani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Elijah Mwandumbya.
  Kushoto ni Kamishna wa mapato ya ndani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Elijah Mwandumbya na Mkurugenzi wa Elimu na Huduma kwa Mlipa Kodi, Richard Kayombo wakiwa katika mkutano wa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Alphayo Kidata uliofanyika jijini Dar es Salaam leo.

  Baadhi ya  viongozi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) wakiwa katika mkutano wa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Alphayo Kidata uliofanyika jijini Dar es Salaam leo.
   Mtafiti Mwandamizi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Beldo Chaula akifafanua juu ya makato yanayokatwa kwenye taasisi za fedha hapa nchini kuwa zitatozwa kwa taasisi hizo za fedha kwenye Miamala na sio kwa kila mwananchi.
  Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

  0 0


  Na: Lilian Lundo – MAELEZO

  Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Polisi Awadhi Haji amesema kwamba Jeshi la Polisi linaendelea na msako wa madereva wa pikipiki (bodaboda) wanaokiuka sheria ya uvaaji wa kofia ngumu na sheria nyingine za barabarani.

  Kamanda Awadhi ameyasema hayo leo kwa njia ya simu alipokuwa akieleza namna ambavyo Jeshi la Polisi linakabiliana na ongezeko la ajali za bodaboda katika Jiji la Dar es Salaam.“Tumekuwa na operesheni ya kukamata waendesha bodaboda wanaovunja sheria za barabarani ikiwa pamoja na ukiukwaji wa uvaaji wa kofia ngumu kwa madereva na abiria wa bodaboda na wamekuwa wakilipishwa faini au kupelekwa mahakamani,” alifafanunua Kamanda Awadhi.

  Aliendelea kusema kuwa, kwa sasa mwitikio wa uvaaji wa kofia ngumu kwa madereva na abiria wa bodaboda ni mkubwa kwani wengi wao wanatii sheria hiyo na kwa wachache wanaokiuka huchukuliwa hatua kali.

  Mapema mwezi Juni, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda alilitaka Jeshi la Polisi kuwachukulia hatua kali madereva wa bodaboda na abiria wanaokiuka kuvaa kofia ngumu.Mhe. Makonda amesema kukiuka kuvaa kofia ngumu kwa dereva na abiria wa bodaboda ni tukio la kujaribu kujiua. Hii imetokana na ongezeko kubwa la ajali za bodaboda nchini ambazo zinakatiza maisha ya watanzania wengi.

  0 0


  Mtendaji Mkuu wa BMT Bw. Mohamed Kiganja (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkufunzi wa Mpira wa Meza wa Shirikisho la mchezo huo la dunia kutoka Egypty Ahmed Dawlatly (kushoto), Kaimu Mwenyekiti wa TTTA Athony Mutafurwa (kulia) baada ya ufunguzi.
  Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wakimsikiliza Mtendaji Mkuu wa Baraza Bw. Mohamed Kiganja hayupo pichani wakati akifungua mafunzo.
  . Mtendaji Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa Bw. Mohamed Kiganja akicheza mpira wa meza na Mkufunzi wa Shirikisho la Dunia kutoka Egypty Ahmed Dawlatly baada ya ufunguzi wa mafunzo hayo katika Shule ya Msingi Kisutu leo asubuhi.
  Mtendaji Mkuu wa Baraza Bw. Mohamed Kiganja akitoa maelekezo kwa Viongozi wa TTTA hawapo pichani juu ya kupanua wigo wa mchezo huo katika vituo vingine Mkoa wa Dar es salaam pamoja na mikoa mingine kushoto kwake ni Mkufunzi wa Mpira wa Meza wa Shirikisho la mchezo huo la dunia kutoka Egypty Ahmed Dawlatly.


  Kaimu Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Bw. Mohamed Kiganja ameitaka Kamati ya Oliympiki Tanzania (TOC) wajiulize na kujifunza jinsi nchi zingine zinavyokuza na kuendeleza michezo kupitia kamati hizo.

  Rai hiyo ameitoa leo wakati akifungua mafunzo ya Ualimu wa Mpira wa Meza yanayofanyika kwa siku nane kuanzia tarehe 4 hadi 11 Julai mwaka huu katika Shule ya Msingi Kisutu jijini Dar es salaam.

  Aidha, ameitaka Kamati hiyo kuweka wazi kwa vyama mambo wanayotakiwa kuyafanya kuendeleza michezo wanayoelekezwa na Kamati ya Olimpiki ya dunia. “TOC jengeni mahusiano yakaribu na muwe wawazi kwa vyama, mpo kwa ajili ya kuendeleza michezo, fanyeni vile mnavyoelekezwa na Kamati hii duniani”, alisema Kiganja.

  Katika hatua nyingine Kaimu Katibu Mkuu wa Baraza Bw. Mohamed Kiganja amekielekeza chama cha mchezo wa meza kupanua wigo kwa kuanzisha vituo vingine katika Manispaa za Kinondoni na Temeke na katika shule tofauti za Mkoa wa Dar es salaam na wasitegemee kituo kimoja cha shule ya Kisutu pekee.

  Aliendelea kuwa, chama hakina budi kwenda mbali zaidi katika Mikoa mingine ambapo, aliwahakikishia kuwa, Baraza liko tayari kuwasaidia kwa Makatibu Tawala ili kuona mchezo huo unakuwa katika Mikoa yote nchini. “Tuwatengenezee mazingira Walimu wanaopata mafunzo”, alieleza.

  Awali Kaimu Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Meza (TTTA) Bw. Athony Mutafurwa ameeleza changamoto zinazokikabili chama cha mpira wa meza ni pamoja na Uwanja na fedha ambapo ameeleza kuwa, TTTA inaishauri Serikali kurudisha mfumo wa kutoa ruzuku kwa vyama na kuongeza kuwa:

  Serikali ione umuhimu wa kujenga uwanja wa ndani wenye hadhi ya kimataifa katika awamu ya pili ya ujenzi wa uwanja wa Taifa ili Tanzania tuweze kuandaa mashindano ya kimataifa ambayo yamekewa yakishindikana kutokana na kukosekana kwa uwanja.

  0 0


  Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) akiangalia baadhi ya bidhaa zinazozalishwa na wajasiliamali wanawake wakati alipotembelea banda la Wanawake na Maendeleo (WIPE) katika Viwanja vya Maonesho ya Biashara mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kulia ni Mke wa Rais wa awamu ya tatu Mama Anna Mkapa.

  Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein (kushoto), akiangalia mafuta ya kula yanayotengenezwa na wajasiliamali , wakati alipotembelea banda la Wanawake na Maendeleo (WIPE), Viwanja vya Kimataifa vya Maonesho ya Biashara vya Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam leo.

  Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein akipata maelezo kuhusiana na uzazi wa mpango, wakati alipotembelea banda la Wanawake na Maendeleo (WIPE), Viwanja vya Kimataifa vya Maonesho ya Biashara vya Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam leo.
  Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein akipata maelezo toka kwa Mkurugenzi wa VETA kanda ya Dar es Salaam Bw. Habibu Bukko wakati alipotembelea banda la VETA katika Viwanja vya Kimataifa vya Maonesho ya Biashara vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam mapema hii leo.
  Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko wa Zanzibar Balozi Amina Salum Ali,wakati alipotembelea banda la Wanawake na Maendeleo (WIPE) katika Viwanja vya Kimataifa vya Maonesho ya Biashara vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam mapema hii leo.

  Picha na Eliphace Marwa - Maelezo

  0 0


  Afisa Usajili wa Dawa kutoka TFDA Dkt. Alex Nkyamba akionesha kwa waandishi wa habari fomu inayotakiwa kujazwa na wananchi pale wanapopata madhara yatokanayo na dawa Leo Jijini Dar es salaam wakati wa mkutano na vyombo vya habari.Kulia ni Afisa Uhusinao wa mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Bi. Gaudensia Simwanza

  Serikali imedhamiraia kuendelea kuwalinda wananchi dhidi ya madahara yatokanayo na Matumizi ya Dawa kwa lengo la Kulinda afya ya Jamii. Kauli hiyo imetolewa na Meneja Uhusiano wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Bi Gaudensia Simwanza wakati wa mkutano na Waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam.

  Akifafanua Simwanza amesema kuwa Mamlaka hiyo inao mfumo wa ufuatiliaji wa Usalama wa Dawa ambao Kitaalamu unajulikana kama (Pharmacovigince) unaojumuisha utambuzi,tathmini,uelewa na udhibiti 


  Meneja Uhusinao wa mamlaka ya Chakula naD awa (TFDA) Bi. Gaudensia Simwanza (kulia) akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu mkakati wa Mamlaka hiyo kudhibiti madahara ya Dawa ikiwa ni moja ya majukumu yake ili kuhakikisha kuwa wananchi wanakuwa Salama.kushoto ni Afisa Usajili wa Dawa kutoka TFDA Dkt. Alex Nkyamba.

  0 0  Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Prof. Justin Ntalikwa wa kwanza kulia, akifuatiwa na Kamishna Msaidizi anayeshughulikia masuala ya Petroli Mwanamani Kidaya (katikati) na Mratibu wa Mradi, Salum Mnuna (kushoto) wakifuatilia majadiliano wakati wa kikao cha Makatibu Wakuu wa nchi za Uganda na Tanzania, kilichohusu utekelezaji wa Mradi wa bomba la Mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga, Tanzania.

  Kikao hicho kilifanyika tarehe 04.07.2016, kabla ya kikao cha Mawaziri wan chi husika. Aidha, Wataalam wengine (hawapo pichani) waliohudhuria kikao hicho kwa upande wa Tanzania walitoka Wizara ya Nishati na Madini, Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA).

  Pia, kwa upande wa Uganda waliwakilishwa na Wizara ya Nishati na Maendeleo ya Madini, wadau wa sekta hizo kutoka idara mbali mbali za Serikali na wawekezaji kampuni za Total, CNOOC na Tullow.Vikao hivyo ni sehemu ya Maandalizi ya ripoti iliyowasilishwa katika kikao cha Mawaziri cha tarehe 5.07.201, Hoima nchini Uganda.

  Waziri wa Nishati na Madini (katikati mstari wa kwanza kulia) akiongoza Wataalam wa Watanzania katika kikao cha Mawaziri wa Tanzania na Uganda kujadili utekelezaji wa Mradi wa bomba la Mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga. Kikao cha Mawaziri kimefanyika tarehe 5.07.2016.

  0 0


  Kwa muda mrefu Tanzania imekuwa na urafiki na Korea na katika kulidumisha hilo, Balozi wa Korea nchini, Song Geum-young amemtembelea Naibu Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla na kuzungumza mambo mbalimbali kuhusu ushirikiano wa Korea na Tanzania zaidi katika sekta ya afya na jinsi Korea ambavyo imekuwa ikisaidia uboreshwaji wa huduma za kiafya nchini.

  Akizungumza na Mo Blog kuhusu ugeni huo, Dk. Kigwangalla alisema kuwa balozi Geum-young alitaka kujua kama naibu waziri anafahamu kuhusu ujenzi wa chuo na hospitali ya Mlonganzira ambapo alitaka kufahamu kama serikali itakuwa tayari kutoa watumishi wa afya 900 ambao watahudumia hospitali hiyo.

  Naibu Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na balozi wa Korea nchini, Song Geum-young kuhusu uhusiano wa Tanzania na Korea na jinsi ambavyo nchi hiyo imepanga kuendelea kuisaida Tanzania katika kuboresha huduma za kiafya nchini. (Picha zote na Rabi Hume, MO Blog)

  Katika hilo Dk. Kigwangalla alimuhakikishia balozi kuwa serikali ipo tayari kutoa wataalam wa afya ambao watakuwa wakitoa huduma katika hospitali ya Mlonganzira ambayo itakuwa na vifaa vya kisasa kutoka Korea na itakuwa na vitanda 600 ambavyo vitakuwa vinatumiwa na wagonjwa wanaofika kupata huduma.

  Naibu Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akifanya mazungumzo na balozi wa Korea nchini, Song Geum-young, alipofika ofisini kwake kwa ajili ya kuzungumza mambo yanayohusu mahusiano ya Tanzania na Korea.

  Jambo lingine ambalo walizungumza ni kuhusu msaada wa magari ya kutolea huduma za kiafya ambayo yanatembea 'mobile clinic' ambayo yatatolewa kwa kanda zote nchini na zaidi katika maeneo ambayo yanaonekana kuwa na ugumu kufikika na kuwa na vituo vya afya vichache.

  Naibu Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na balozi wa Korea nchini, Song Geum-young, wa kwanza kushoto ni Katibu wa Balozi wa Korea, Songwon Shin na wapili kulia ni Katibu wa Naibu Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Kulwa.

  "Amesema watatuletea convoy zaidi ya sita (kila moja ina magari 10) ambayo yatagawiwa kwa kila kanda nchini, magari haya kila gari linakuwa na mengine 10 ambayo yanakuwa na huduma mbalimbali za kiafya kama chumba cha upasuaji, store ya madawa, maji na mengine ambayo yanahitajika kutoa huduma kwa mgonjwa," alisema Dk. Kigwangalla.

  Naibu Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla na balozi wa Korea nchini, Song Geum-young wakipiga picha ya pamoja baada ya kumaliza mazungumzo.

  Aidha aliongeza kuwa magari hayo ya kutolea huduma za afya ambayo yanatembea 'mobile clinic' yanataraji kuletwa nchini mwakani mwezi Januari na kwasasa wizara imetakiwa kuandika andiko la mradi ili kuonyesha kuwa imekubali kuingia katika mradi huo ambao kwa kiasi kikubwa utaweza kurahisisha upatikanaji wa huduma za kiafya kwa maeneo ambayo yana vituo vichache vya afya.

  Na Rabi Hume, MO Blog

  Katibu wa Balozi wa Korea, Songwon Shin akibadilishana mawasiliano na Naibu Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla katikati ni balozi wa Korea nchini, Song Geum-young.

  Naibu Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akiagana na balozi wa Korea nchini, Song Geum-young baada ya kumaliza kufanya mazungumzo.

  0 0

  Mtoto Clara Damian mwanafunzi wa darasa la saba asiyeona akiwa darasani  akitumia mashine maalumu ya kuandikia na kusoma katika shule ya msingi  patandi iliyopo wilaya ya arumeru mkoani arusha shule hiyo inakabiliwa na upungufu wa walimu na vitabu.

  Na Woinde Shizza,Arusha.

  Wanafunzi wenye ulemavu katika shule ya msingi Patandi iliyopo wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha wamelalamikia tatizo la upungufu wa walimu,vitabu na vifaa vya kufundishia kwa wanafunzi hao wenye mahitaji maalumu hali inayokwamisha maendeleo ya kitaaluma hivyo wameiomba serikali na taasisi binafsi kutatua changamoto hiyo.

  Mwanafunzi asiyeona anayesoma darasa la saba Clara Damian ni alisema kuwa kumekua na uhaba wa vitabu kwa watoto wasioona na mashine za kuandikia maandishi yenye nundu ambazo ni chache na kwa sasa ni mashine tatu pekee zinafanya kazi ukilinganisha na idadi kubwa ya wanafunzi.

  Alisema kuwa miundombinu ya majengo ya madarasa pia yamekua si rafiki kwa watoto wenye ulemavu hivyo anashauri miundombinu ya majengo na shule iendane na mahitaji wa watoto hao.

  Mibaku Limba Mwanafunzi asiyesikia (kiziwi) alisema kuwa walimu walioko kwa sasa wanaofundishwa kwa lugha za alama ni wachache ukilinganisha na idadi ya masomo hali ambayo inachangia kuwarudisha nyuma.

  Mratibu wa Kitengo Cha Walemavu Mwalimu Anna Shayo Katika Shule hiyo Mwalimu Shayo alikiri kuwepo kwa upungufu wa walimu na vitabu kwa watoto wenye mahitaji maalumu na kuiomba jamii,taasisi na serikali kushiriki katika kuboresha maendeleo ya watoto hao ambao wakijengewa misingi bora ya elimu wanaweza kuwa na mchango kwa jamii badala ya kuwa tegemezi.

  Mwalimu Marko Alois Mamuya anayefundisha watoto viziwi ameiomba serikali itoe motisha kwa walimu wanaofundisha watoto wenye mahitaji maalumu ili kuongeza ari na hamasa itakayosaidia kupata idadi kubwa ya walimu.

  “Tunawaomba wazazi wasiwafiche watoto wenye ulemavu majumbani bali wawalete mashuleni huku waweze kupata elimu ,lishe na mazoezi badala ya kuwafungia nyumbani kwani wanazidi kuwa tatizo licha nya uwezo,vipaji na ubunifu walioanao ambao unaweza kuwasaidia wao na jamii yao” alisema Mwalimu Marko.

  0 0
  0 0


  Na Benedict Liwenga, WHUSM.

  Vyama vya Muziki nchini vimetakiwa kufuata, Sheria, Taratibu na Kanuni pindi Wanachama wake wanapopanga kukutana na baadhi ya Viongozi wa Serikali.

  Ushauri huo umetolewa leo jijini Dar es Salaam na Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa masuala ya Lugha, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi. Husna Kitogo ambaye alimwakilisha Mkurugenzi wa Sanaa Wizarani hapo wakati alipokutana na Mashirikisho ya Vyama vya Muziki nchini.

  Bi. Kitogo amesema kwamba kumekuwa na tabia kwa baadhi ya Wasanii Wanachama na wasio wanachama kukutana na baadhi ya Viongozi wa juu wa Serikali pasipo Wizara kupewa taarifa jambo ambalo ni kinyume na utaratibu na kuwataka kufuata Sheria na utaratibu mzuri wa kufanya mawasiliano na Wizara kabla ya kufanya hivyo.

  ‘’Msifanye kazi kwa mazoea, kwani mnapojiamulia kukutana na Viongozi wa Serikali pasipo kuijulisha Wizara mnakosea kwani Serikali inafanya kazi kwa kuzingatia Sheria, Taratibu na Kanuni, na baadhi ya watu wanaofanya hivi pindi wanapokwama utaona wanarudi kwetu, jitahidini kujenga utaratibu hata wakutuletea nakala ya barua ili sisi tuweze kuwasaidia katika kukutana nao hao viongozi’’, alisema Kitogo.

  Kwa upande wake Katibu Mkuu Taifa wa Chama cha Madj wa Muziki Tanzania (TDMA) Bw. Asanterabbi Mtaki ametaja baadhi ya changamoto zinazowakabili ni pamoja na Usajili wa Vikundi, vibali vya kufanyia kazi, masuala ya Haki Miliki (Copy rights), kodi za bidhaa za muziki pamoja na usimamizi wa mapato ya kazi za sanaa.

  Amesema kwamba, baadhi ya Wanamuziki nchini wamekuwa hawatambui umuhimu wa kujiunga na Mashirikisho pamoja na vyama mbalimbali hali ambayo inadidimiza tasnia ya sanaa kwani kunapelekea kukosekana kwa ushirikiano katika kujenga taifa, kutokana na hali hiyo ameishauri Serikali kuwasimamia wanamuziki ambao bado hawajajiandikisha katika Vyama kufanya hivyo ili kuleta nguvu ya pamoja katika kupigania haki za Wasanii nchini.

  ‘’Naishauri Serikali kuliangalia suala hili la baadhi ya wasanii kutojiandikisha katika vyama na ndiyo hawa wasanii ambao wamekuwa wakikutana kimya kimya na Viongozi wa juu wa Serikali na baadhi ya yao hawako katika Mashirikisho ama Vyama vya Wasanii, hii ni changamoto kwetu sisi, tunaiomba Serikali itusaidie kuwapa elimu hawa watu ili wajue faida na umuhimu wa kujiunga na vyama’’, alisema Mtaki.

  Naye Mwanamuziki Mkongwe na Makamu wa Rais wa Shirikisho la Muziki wa Dansi Tanzania (CHAMUDATA) maarufu kama Bw. Juma Ubao ameiomba Serikali kuendelea kuzisimamia haki za Wasanii nchini hususani katika suala zima la Haki Miliki zao kwani ndiyo kilio chao cha muda mrefu.

  ‘’Ushirikiano baina ya Serikali na Vyama vya Wanamuziki nchini uzidi kudumu na hivyo tunaiomba Serikali itusaidie katika kupunguza kodi kwa bidhaa za muziki kwani kwa kufanya hivyo kutatuondolea adha ya kununua vifaa visivyo na ubora, kwani tunajikuta tunanunua vifaa hivyo kutokana na kushindwa kununua vyenye ubora zaidi vitokavyo nje kutokana na kodi yake kuwa kubwa.

  Katika kikao hicho, baadhi ya mapendekezo waliyokubaliana ni pamoja na suala la usajili unaofanywa na Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) kutambua uwepo wa Shirikisho la Vyama vya Muziki Tanzania, uboreshaji wa Sheria pamoja na Sera ya Sanaa, Wasanii kulipwa kutokana na kazi zao zitumikazo katika baadhi ya Vyombo vya habari nchini pamoja na Wanafani wote nchini kupitia katika Vyama husika.

  Kikao hicho kilichoitishwa na Wizara kiliwakutanisha Wajumbe mbalimbali toka Chama cha Madj wa Muziki Tanzania (TDMA), Chama cha Muziki wa Dansi Tanzania (CHAMUDATA), Chama cha Taarab Tanzania (TTA), Chama cha Muziki wa Kizazi Kipya (TUMA), Chama cha Muziki wa Injili Tanzania pamoja na Vyama venginevyo lengo likiwa ni kutambua baadhi ya changamoto mbalimbali zinazoikabili vyama hivyo.

  0 0


  Waziri wa Michezo Tanzania Mhe Nape Mnauye akitowa nasaha zake kabla ya kuaza kwa mchezo wa kirafiki wa utangulizi wakati wa fainali ya Kombe la Ramadhani Masauni and Jazeera Cup zilizofanyika uwanja wa mnazi mmoja jana usiku
  .

  Timu za Baraza na Maveterani zikiingia uwanjani tayari kwa mchezo wao wa kirafiki uliofanyika wakati wa fainali hiyo Timu ya Maveterani wa Kikwajuni wakiongozwa na Mhe. Mbunge wa Kikwajuni na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Eng Hamad Yussuf Masauni kulia na Timu ya Baraza ikiongozwa na Mwakilishi wa Jimbo la Kikwajuni Mhe Nassor Salum Jazeera.
  Waziri wa Habari Michezo Mhe Nape akisalimiana na wachezaji wa timu ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar kabla ya kuaza kwa mchezo wao na maveterani wa kikwajuni Zanzibar

  Waziri Nape akisalimiana na wachezaji wa Timu ya Maveterani wa Jimbo la Kikwajuni kabla ya mchezo wao wa kirafiki na Timu ya Baraza la Wawakilishi ukiwa ni mchezo wa utangulizi wa Fainali ya Kombe la Ramadhani Masauni and Jazeera. mchezo uliofanyika uwanja wa mnazi mmoja jana usiku.
   

  Mchezaji wa Timu ya Maveterani wa Jimbo la Kikwajuni Zanzibar akimiliki mpira wakati wa mchezo wao wa kirafiki wa utangulizi wa ufunguzi wa mchezo wa Fainali kati ya Timu ya Kisimamanjongoo na Kilimani.

   
  .
  Waziri wa Habari Michezo Mhe Nape akisalimiana na wachezaji wa timu ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar kabla ya kuaza kwa mchezo wao na maveterani wa kikwajuni Zanzibar.
  Mhe Waziri wa Michezo Mhe Nape akisalimiana na Nahodha wa Timu ya Maveterani wa Jimbo la Kikwajuni Mbunge wa Jimbo hilo Mhe Hamad Masauni wakiwa na bashasha wakati wakisalimiana.
  Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo Zanzibar Mhe Rashid Ali Juma akizungumza wakati wa mchezo huo wa ufunguzi wa Fainali ya Kombe la Ramadhani Masauni and Jazeera Cup na kumkaribisha Waziri mwezake wa Michezo Mhe Nape Mnauye, akiwa kulia kwa waziri.
  Waziri wa Michezo Tanzania Mhe Nape Mnauye akitowa nasaha zake kabla ya kuaza kwa mchezo wa kirafiki wa utangulizi wakati wa fainali ya Kombe la Ramadhani Masauni and Jazeera Cup zilizofanyika uwanja wa mnazi mmoja jana usiku
  Wachezaji wa Timu ya Maveterani wa Jimbo la Kikwajuni wakimsikiliza Waziri wa Michezo Mhe Nape Mnauye akitowa nasaha zake kwa Wanamichezo waliohudhuria fainali hiyo na kuupongeza Uongozi wa Kamati ya Mashindano hayo Jimbo la Kikwajuni Zanzibar.
  Wachezaji wa Timu ya Maveterani wa Jimbo la Kikwajuni wakimsikiliza Waziri wa Michezo Mhe Nape Mnauye akitowa nasaha zake kwa Wanamichezo waliohudhuria fainali hiyo na kuupongeza Uongozi wa Kamati ya Mashindano hayo Jimbo la Kikwajuni Zanzibar.
  Nahodha wa Timu ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Nassor Salim Jazeera akiongoza wachezaji wake kusalimiana na Timu ya Maveterani wa Jimbo la Kikwajuni Zanzibar.
  Kikosi cha Timu ya Maveterani wa Jimbo la Kikwajuni. kilichotowa upinzani kwa Timu ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar na kulazimishwa kufungwa bao moja.
  Kikosi cha Timu ya Baraza la Wawakilishi kilichotoa kipigo cha bao moja dhidi ya Timu ya Maveterani wa Jimbo la Kikwajuni Zanzibar.
  Mchezaji wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar akimpita mchezaji wa Timu ya Maveterani wa Jimbo la Kikwajuni Zanzibar wakati wa mchezo wao wa kirafiki wa utangulizi wa ufunguzi wa mchezo wa Fainali kati ya Timu ya Kisimamanjongoo na Kilimani.
  Mchezaji wa Timu ya Maveterani wa Jimbo la Kikwajuni Zanzibar akimpita mchezaji wa Timu ya Baraza la Wawakilishi, wakati wa mchezo wao wa kirafiki wa utangulizi wa ufunguzi wa mchezo wa Fainali kati ya Timu ya Kisimamanjongoo na Kilimani.
  Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Mhe. Hamad Masauni akimiliki mpira akijiandaa kumpita mchezaji wa Timu ya Baraza la Wawakilishi wakati wa mchezo wao wa kirafiki.
  Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Mhe. Hamad Masauni akimiliki mpira akijiandaa kumpita mchezaji wa Timu ya Baraza la Wawakilishi wakati wa mchezo wao wa kirafiki.

  Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Mhe. Hamad Masauni akimiliki mpira akijiandaa kumpita mchezaji wa Timu ya Baraza la Wawakilishi wakati wa mchezo wao wa kirafiki.Imetayarishwa na OthmanMapara


  Waziri wa Habari Michezo Mhe Nape Moses Nnauye akisalimiana na Mwenyekiti wa Jumuiya ya TAYI Tanzania Ndh Abdalla Othman Miraji wakati akihudhuria fainali za Kombe la Masauni and Jazeera lililofanyika jana usiku katika viwanja vya Mnazi Mmoja kati ya Kilimani na Kisimamanjongoo, kabla ya mchezo huo kulikuwa na mchezo wa utangulizi kati ya Maveterani wa Kikwajuni na Timu ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar, katika mchezo huo timu ya Baraza imeshinda bao 1--0.

  Zanzinews.Blgospot.com.


  Email othmanmaulid@gmail.com.

  0 0

  Kutoka kushoto ni Naibu wa fedha mkuu wa Shirika la Ndege la Etihad, Adam Boukadida, Mkuu wa Idara ya Fedha wa Mashirikia ya Etihad,Ricky thirion wakiwa kwenye kupokea tuzo za Uhasibu za Adam Smith jijini London hivi karibuni.

  Shirika la Ndege la Etihad limeibuka mshindi katika tuzo za Treasury Today Adam Smith jijini London, Uingereza kutokana na ubora na ufanisi mkubwa kwenye masuala ya kifedha.

  Idara ya Fedha ya Shirika la Ndege la Etihad imenyakua tuzo hiyo ya juu kwa kuwa mshindi wa kwanza kwenye uongozi bora Idara ya Fedha kwa kuwa mshindi wa jumla. Pia, imeshinda tuzo kwa utoaji bora wa huduma za kifedha na utawala wa fedha.

  Kushinda tuzo ya jumla katika ushindani huo wa kimataifa, kumetokana na idara ya fedha ya Shirika la Ndege la Etihad kutambuliwa kutokana na  ubunifu wake katika teknolojia na kuwapo kwa mikakati endelevu ambayo imewezesha mchango mkubwa kwenye sekta ya anga.

  Akitangaza kwenye Ukumbi wa Gala, jijini London, Gibson Hall, tuzo za Etihad zilipokelewa na Mkuu wa Idara ya Fedha wa Shirika la Ndege la Etihad na msaidizi wake Adam Boukadida.

  Rais na Mtendaji Mkuu wa  Shirika la Ndege la Etihad alisema, “Ubunifu ndiyo msingi wa yale tunayoyafanya kwenye shirika letu. Tuzo hizi ni uthibithisho kwa kazi nzuri tunayoifanya kwenye uongozi masuala ya fedha. Mikakati yetu ipo wazi na ndiyo inayotuwezesha kufanya biashara kwa kisasa inayozingatia ukuaji na uwekezaji zaidi kwenye sekta ya anga ulimwenguni kote. Ushirikiano wetu umetunawezesha kufanya mambo makubwa miongoni mwa yale tuliyonayo ikiwamo, kushirikiana katika kuimarisha mapato, kupunguza gharama za uendeshaji na kuanzisha biashara mpya inayovutia.
  .
  Mkuu wa Idara ya Fedha wa mashirika ya Etihad alisema, “Utendaji wa wafanyakazi wetu kwa mwaka huu umetambulika. Tuzo hizi za juu hususani tuzo ya uongozi wa fedha, hakika tulishathili. Mafanikio tuliyopata ni chachu kwa mashirika yaliyopo chini ya Etihad kwa kuweka mipango mizuri zaidi katika ukuaji na uwekezaji.”

  Mwanzilishi wa tuzo hizo katika kampuni ya Treasury Today Group, Angela Berry alisema, “Tuzo za Adam Smith huangazia mafanikio yaliyofikiwa katika shirika kwenye masuala ya fedha. Tunaipongeza Shirika la Ndege Etihad kwa kupata tuzo nyingi kwa mwaka huu.”

  Tuzo ya Ubora Utawala wa Fedha ilitolewa kutambua Shirika la Ndege la Etihad kutokana na kuwekeza mtaji wa  dola 700 mwaka jana mpaka mwezi Septemba.

  Ilionekana kama ni mpango wa mara ya kwanza kwenye ushirikiano kifedha katika sekta ya anga, fedha hizo zililenga kupanua maeneo ya uwekezaj ikwenye mashirika ya Etihad.  Dola milioni 500 zaidi, zilitolewa katika awamu ya pili iliyoisha mwezi uliopita kwa kuzingatia soko la fedha jambo lililoimarisha Shirika la Ndege la Etihad na washirika wake.

  Katika utekelezaji kwenye kukuza mtaji maeneo mbalimbali ilipowekeza ulimwenguni, ilianzisha upunguzaji gharama za uendeshaji jambo lililowezesha shirika la ndege la Etihad kumudu kulisimamia shughuli zake, upatikanaji wa taarifa sahihi za fedha, jambo ambalo limepelekea kupata tuzo ya ubora kwenye usimamizi wa fedha. Jambo hilo ndilo lililotuwezesha kuimarika kiuchumi, kuongeza ufanisi wa uendasheaji, kuongezeka mapato na kukabiliana na utatuzi wa haraka kwenye mahitaji yanayoongezeka kwenye soko la usafiri wa anga ulimwenguni.

  0 0  Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kutoa zawadi za vitu mbalimbali kwa vituo 6 vya kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu jijini Dar es Salaam, leo ikiwa ni sehemu ya kusherehekea Sikukuu ya Eidd el Fitr. Zawadi hizo zimetokana na fedha zilizopatikana katika Tamash la Pasaka.
  Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama (kulia), akimkabidhi mlezi wa Kituo cha Kulelea watoto Yatima cha Irshaadi, Juma Kaseja, sehemu ya msaada wa vitu mbalimbali kwa ajili ya Sikukuu ya Eidd el Fitr, hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam
  Baadhi ya watoto waliohudhulia hafla hiyo.
  Msama akitoa zawadi za Sikukuu ya Eid el Fitr.

  Baadhi ya vitu mbalimbali vilivyotolewa na kampuni ya Msama Promotions Ltd,mapema leo jijini Dar katika vituo sita.
  Baadhi ya watoto waliohudhulia hafla hiyo.


  Msama akitoa zawadi za Sikukuu ya Eid el Fitr.
  Watoto wakipokea zawadi.
  Msama akigawa zawadi mbalimbali kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu.
  Msama akimkabidhi mtoto Fahari Haji vitu mbalimbali kwa ajili ya Sikukuu ya Eid el Fitr.

older | 1 | .... | 901 | 902 | (Page 903) | 904 | 905 | .... | 1898 | newer