Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 900 | 901 | (Page 902) | 903 | 904 | .... | 1896 | newer

  0 0


  Mkurugenzi wa TIB, Charles Singili akipewa maelezo na wafanyakazi wa kampuni ya Alko Vintages kuhusiana na mvinyo wa Dodoma. Katikakati ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano, Sarah Majengo akifuatiwa na Dr Hildebrand Shayo, Meneja wa Mipango na Utafiti.
  Afsa Mauzo wa kampuni ya Pipe Industries, Ignas Mafita (kushoto) akimpa maelekezo Mkurugenzi Mtendaji wa TIB, Charles Singili (kulia) juu ya bidhaa zinazozalishwa na kampuni hiyo. Anayetazama katikati ni afsa wa TIB.


  Benki ya TIB imepongezwa na wadau mbalimbali kwa jitihada zake kusaidia wajasiriamali wakati wa maonyesho ya kimataifa ya kibiashara yanayoendelea ya Saba Saba.

  Benki imetoa fursa kwa baadhi ya wateja wake kutangaza bidhaa na huduma zao katika banda la benki hiyo lilipo katika viwanja vya Sabasaba.Miongoni mwa wateja wake waliopata fursa ya kutangaza biashara katika banda la benki hiyo ni kampuni ya Pipe Industries ambao ni wazalishaji wa mabomba mbalimbali ya kilimo cha umwagiliaji, maji taka na gesi na kampuni ya Alko Vintages ambao ni wazalishaji maarufu wa mvinyo aina ya 'Dompo' .

  Benki ya TIB pia inatoa mafunzo ya bure kwa wajasiriamali katika banda lake katika maeneo ya usimamizi wa fedha, masoko, pamoja na utawala.Akizungumza katika banda la benki hiyo, Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa TIB, Bwana Charles Singili, alisema ushiriki wao katika maonyesho ya Sabasaba mwaka huu unaendana na kauli mbiu ya maonyesho ya Sabasaba ambayo yamelenga kuunganisha uzalishaji na masoko.

  'Kupitia huduma yetu ya mikopo ya viwanda tumeweza kusaidia makampuni na miradi mbalimbali ikiwemo miradi ya kusindika mazao, miradi ya madini, na ya viwanda, mfano mzuri ni haya makampuni yaliyopewa fursa ya kutangaza bidhaa zao kwenye banda letu la TIB’ alisema Singili.

  Akielezea zaidi ushiriki wa TIB, Singili alisema benki yake imejikita katika kusaidia ukuaji wa viwanda na kuwezesha viwanda vidogo vidogo na vya kati ili kuzalisha bidhaa bora zitakazowapatia soko la uhakika ili kusaidia kukuza uchumi wa nchi.

  0 0


  Jina: Philbart Patrick Gwagilo
  Umri miaka kwa sasa 29 alipotea akiwa na umri wa miaka 27.
  Kabila: Muha
  Dini: Mkristo
  Mkoa alipozaliwa: Kigoma Wilaya ya Kasuru.
  Maeneo anayopenda kutembelea: Sinza, Kibamba na Arusha.

  Alikuwa anafanya kazi ya uwakili wa kujitegemea katika kampuni ya Declam jijini Dar es Salaam.

  Mtajwa hapo juu anatafutwa na ndugu zake. Kwa mara ya mwisho alikuwa anaishi Sinza Lion jijini Dar es Salaam ilikuwa siku ya Jumamosi Machi 28, 2015.

  Wajihi (Rangi yake ni Mweusi) mrefu kiasi na mnene kiasi.
   Msamaria mwema yeyote mwenye taarifa zake au atakayemuona popote anaombwa kuwasiliana na ndugu zake kwa namba:-

  Peter P. Gwagilo: 0784390904
  Paul P.Gwagilo: 0659649891
  Yohanes  P.Gwagilo: 0714514103

  0 0


  Wakuu wa Wilaya wa Wilaya za Mkoa wa Kagera wakiwa katika picha ya pamoja na mkuu wa mkoa wa Kagera Meja jenerali Mstaafu Salimu Kijuu mara baada ya kula kiapo.Na Editha Karlo wa blog ya jamii-Kagera.
  Mkuu wa Wilaya ya Missenyi Mkoani Kagera Luteni kanali Denis Mwila akila kiapo mbele ya mkuu wa mkoa wa Kagera (hayupo pichani).
  Mkuu wa Wilaya ya Kywerwa Mkoa wa Kagera akila kiapo mbele ya mkuu wa mkoa wa Kagera Meja Jenerali mstaafu Salum Kijuu,(hayupo pichani).
  Mkuu wa Wilaya ya Biharamulo Saada Malunde akila kiapo cha utii na utumishi na kuilinda nchi mbele ya mkuu wa Mkoa wa Kagera.

  Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali mstaafu Salum Kijuu akimkabidhi vitendea kazi mkuu mpya wa Wilaya ya Bukoba mjini Deodatus Kinawilo.

  Baadhi ya wakuu wa Wilaya ya Mkoa wa Kagera Kabla ya kula viapo wakimpokea mgeni rasmi(ambaye hayupo pichani) wakati akiingia ukumbini

  0 0


  Producer nguli wa muziki nchini John Shariza a.k.a Mann Water (chini kushoto) akiweka saini kwenye hati ya mkataba wa lebo ya KOMBINENGA kurasimisha usimamizi wa kazi za msanii Abbas Hamisi Kinzasa almaarufu kama 20% (Twenty per Cent) akishuhudiwa na Wakili msomi Iddi M. Gogo wa Alpha Attorneys (juu kulia) aliyefanikisha zoezi hilo, pamoja na meneja uzalishaji wa Combination Sounds, Rowel Moses (juu kushoto) kwenye studio za Combination Sounds Kinondoni Studio jijini Dar es salaam.
  Producer nguli wa muziki nchini John Shariza a.k.a Mann Water (chini kushoto) baada ya kuweka saini kwenye hati ya mkataba wa lebo ya KOMBINENGA kurasimisha usimamizi wa kazi za msanii Abbas Hamisi Kinzasa almaarufu kama 20% (Twenty per Cent) wakisimamiwa na Wakili msomi Iddi M. Gogo wa Alpha Attorneys (juu kulia) aliyefanikisha zoezi hilo, pamoja na meneja uzalishaji wa Combination Sounds, Rowel Moses (juu kushoto) kwenye studio za Combination Sounds Kinondoni Studio jijini Dar es salaam.
  Msanii Abbas Hamisi Kinzasa almaarufu kama 20% (Twenty per Cent) akiweka saini kwenye hati ya mkataba wa lebo ya KOMBINENGA kurasimisha usimamizi wa kazi zake huku akishuhudiwa na Producer nguli wa muziki nchini John Shariza a.k.a Mann Water (chini kushoto), Wakili msomi Iddi M. Gogo wa Alpha Attorneys (juu kulia) aliyefanikisha zoezi hilo, pamoja na meneja uzalishaji wa Combination Sounds, Rowel Moses (juu kushoto) kwenye studio za Combination Sounds Kinondoni Studio jijini Dar es salaam.

  Msanii Abbas Hamisi Kinzasa almaarufu kama 20% (Twenty per Cent) wakipongezana na producer nguli wa muziki nchini John Shariza a.k.a Mann Water baada ya kuwekeana saini mkataba wa kufanya kazi pamoja chini ya lebo ya KOMBINENGA kwenye studio za Combination Sounds Kinondoni Studio jijini Dar es salaam.(Picha na Sultani Kipingo)

  Na Sultani Kipingo

  Mfalme wa Afro Pop nchini Abbas Hamisi Kinzasa almaarufu kama 20% (Twenty per Cent) anavunja ukimya na kurejea kwa kishindo kwenye anga ya muziki, huku akiwa msanii wa kwanza kusaini mkataba na lebo mpya ya KOMBINENGA inayoendeshwa na producer nguli John Shariza a.k.a Mann Water.

  Twenty Percent, ambaye mwaka 2011 alitwaa tuzo saba za Kilimanjaro Music Awards (KTMA) kwa mpigo, huku Mann Water akisomba tuzo mara mbili mfululizo za producer bora (mwaka 2013 na 2014), tayari amesharekodi vibao vitano na anatarajia kuachia ngoma moja mpya ya kwanza Julai 18, 2016, katika kuandaa albamu yake ya SAUTI YA GHARAMA.

  "Nimerudi kuwachinja tena" anasema Twenty Per cent, akiwa anakamilisha kurekodi katika studio za Combination Sounds iliyoko Kinondoni Mkwajuni jijini Dar es salaam. "Nimerudi kurudisha sauti ya gharama kwa jamii. Sauti inayofundisha. Sauti inayoonya. Sauti inayoburudisha. Sauti inayozengua kila mtu, " anaogeza.

  Tayari Tweny Per cent ameshasaini mkataba wa miaka mitano na lebo ya KOMBINENGA, katika hafla fupi iliyofanyika Jumapili katika ofisi za Combination Sounds. Kuanzia sasa shughuli zote za msanii huyu zitasimamiwa na lebo hiyo chini ya Producer Mann Water.

  Wakili msomi Iddi M. Gogo wa Alpha Attorneys ndiye aliyefanikisha zoezi hilo la kutiliana saini mkataba lililoshuhudiwa pia na meneja uzalishaji wa Combination Sounds, Rowel Moses.

  "Namkubali sana Twenty Pa kwani ni msanii aliyetimia na hutumii shuruba wakati wa kurekodi maana ana kipaji cha ajabu cha kutunga akiwa wima na kukariri hapohapo", anasema Mann Water, ambaye ameshafanya kazi na wasanii nyota kibao wakiwemo Lady Jay Dee, Ali Kiba, Ommy Dimpoz, Christian Bella, MB Dogg, Juma Nature, Mr Blue na wengine wengi.

  Twenty Percent alitamba sana tokea mwaka 2006 kwa wimbo wake wa "Manemane" uliomfanya ashinde tuzo ya KTM, kabla ya kuweka historia ya kusomba tuzo saba kwa mpigo mwaka 2011. wakati huo nyimbo zilizompandisha chati zilikuwa ni "Tamaa Mbaya" na "Ya nini Malumbano" na "Maisha ya Bongo"

  Mbali na Muziki Twenye Percent pia alitamba sana kwenye tasnia ya filamu ambapo alicheza kwenye mchezo uliofahamika kwa jina lake la 20%. Baada ya hapo akaamua kupumzika kwa muda na kujishugulisha na shughuli za kilimo. "Kilimo kinaendelea vyema na sasa nimeamua kurudi kwenye gemu ili kuwachinja tena" alimalizia, akiinuka kuelekea kwake Kimzichana, Mkuranga, Mkoa wa Pwani, anakoishi.

  0 0


  Rais wa Rwanda Paul Kagame, (wa pili kulia) akimkabidhi Mkuu wa Idara ya Masoko, Biashara ya Nje na Wateja, Bw. Zachy Irenus Mbena, Tuzo ya Mshindi wa Kwanza wa Maonesho ya Bidhaa Bora za Vyakula na Vinywaji 2016, wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya Biashara ya Kimataifa kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere Sabasaba jana Julai 2.

  Na Ripota wa Sufianimafoto, Dar

  KAMPUNI ya Kitanzania ya Afri Tea and Blrenders (1963) Ltd, inayozalisha bidhaa bora zinazotangaza vivutio mbalimbali na Uchumi wa Tanzania kama Majani ya Chai ya Green Label, African Pride Tea, Kilimanjaro Infusions, Simba Chai, Kahawa ya Africafe na Uji Bora, wameibuka kidedea katika Maonesho ya Biashara ya Kimataifa kwa kunyakua Tuzo ya Mshindi wa Kwanza wa Maonesho ya Bidhaa Bora za Vyakula na Vinywaji 2016.

  Akizungumza na Mtandao huu Mkuu wa Idara ya Masoko, Biashara ya Nje na Wateja, Bw. Zachy Irenus Mbena, alisema kuwa hii ni Tuzo ya tatu kwa mwaka wa tatu mfululizo kupata ambapo mwaka 2014 wapitwaa Tuzo ya mshindi wa kwanza, 2015 walipata Tuzo ya mshindi wa pili ya Wauzaji wa Bidhaa za Tanzania Nje ya Nchi (Best Exporting) na mwaka huu wamerejea katika nafasi ya kwanza.

  Aidha Mbena alisema kuwa anawashukuru waeteja na watumiaji wa bidhaa zao waliowafanya kuweza kutambulika Kimataifa kwa kutangaza Uchumi, Vivutio na Utalii wa Tanzania kupitia bidhaa zao kama Mlima Kilimanjaro, Wanyama, Khanga Vazi la asili ya Kimasai na Utamaduni wa Mtanzania kwa ujumla.Kampuni hiyo imezidi kujizolea sifaa kabambe kwa kuwa wabunifu katika kuzalisha Bidhaa zinazoendana na mahitaji halisi ya Watanzania.

  Aidha Kampuni hiyo imezalisha bidhaa pekee inayotangaza Kisiwa cha Zanzibar ‘Africafe Zanzibar Spice Coffee’ iliyochanganywa na Karafuu huku ikiwa katika muonekano wa kuvutia inajitangaza kimataifa, iliyohifadhiwa katika Kasha lililonakshiwa ramani ya Kisiwa cha Zanzibar na baadhi ya alama za Kisiwa hicho.

  ‘’Pamoja na hayo lakini pia tunashiriki katika maonesho mbalimbali ya Nje ya nchi yanayoandaliwa na Mabalozi wetu wa Tanzania nchi za Nje ‘Tanzania Day in Embasses’ ambapo mwezi uliopita tulialikwa kushiriki maonesho yaliyofanyika katika jiji la Antalya Uturuki, ambayo pia yalishafanyika Msumbiji, Uingereza, Ethiopia na Rusia’’.

  Alisema MbenaPia wamekuwa wakushirikiana na Mamlaka ya Usimamizi wa Maendeleo ya Biashara Tanzania ‘TAN TRADE’ katika maonesho mbalimbali ya Kimataifa.Kutokana na umuhimu na ubora wa bidhaa zao zinazotengenezwa kiasili, wamekuwa wakishiriki pia katika maonesho mbalimbali ya Sikukuu ya Wakulima Nane Nane katika Mikoa ya Mbeya, Arusha na Morogoro.

  Aidha Bw. Mbene aliwakaribisha Wanzania wote wanaofika katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere kutembelea Mabanda ya maonesho kufika katika Banda lao linalotoa huduma kufuturisha BURE kwa wafungaji mida ya jioni ambao hupewa fursa ya kuonja chai za aina zote pamoja na Chai, Uji ,Kahawa na Maji bila malipo yeyote.

  Pamoja na hayo pia wananchi wanaofika katika Banda hilo hupewa zawadi ya Pakiti moja Majani ya Chai yenye mchanganyiko wa radha tofauti tofauti za Green Tea, Hibiscus, Rooibos, Paper Minty, Camomile, Vanilla na Morocco Minty.
  Muonekano wa Banda la Maonesho la Afri Tea and Blrenders (1963) Ltd.
  Afisa Masoko na Mauzo wa Kampuni ya Afri Tea and Coffee (1963) Ltd, Sheila Manafi, akipozi na Tuzo waliyokabidhiwa na Rais Kagame.
  Baadhi ya Wananchi waliofika katika Banda hilo wakinunua na kuonja radha tofauti za Chai za Kampuni hiyo.

  Muonekano wa Mandhari ya banda hilo lililo katika maonesho hayo likiwa na baadhi ya vitu vyenye muonekano wa Tamaduni za Kitanzania.

  Baadhi ya Wananchi waliofika katika Banda hilo wakionja radha za Chai na Kahawa za Kampuni hiyo.
  Mfanyakazi wa Kampuni hiyo, Cecilia Mrema (kulia) akitoa maelezo kwa baadhi ya wateja katika Banda hilo.
  Mfanyakazi wa Kampuni hiyo, Ronne Zachy (kushoto) akifafanua jambo kwa baadhi ya wateja waliotembelea Banda hilo.
  Sheila akipanga bidhaa.
  Baadhi ya wateja wakipata maelezo kutoka kwa wahudumu wa Kampuni hiyo
  Mfanyakazi wa Kampuni hiyo, Cecilia Mrema (kulia) akitoa maelezo kwa baadhi ya wateja katika Banda hilo.
  Baadhi ya wananchi waliofika katika Banda hilo wakionja radha tofauti za Chai na Kahawa za Kampuni hiyo.
  KARIBU KATIKA BANDA LA MAONESHO LA KAMPUNI YA AFRI TEA AND COFFEE BLENDERS 1963 LTD KATIKA MAONESHO YA BIASHARA YA KIMATAIFA YA SABASABA 2016.

  0 0

   Mkuu wa Huduma za Kibenki zinazofuata kanuni na misngi ya kiislamu (Islamic Banking)  wa Benki ya NBC, Yassir Masoud (kushoto), akizungumza na baadhi ya wateja wa benki hiyo waliyohudhuria hafla ya futari waliyoiandaa mjini Dodoma hivi karibuni.
   Meneja Uendelezaji wa Biashara wa Benki ya NBC, Eddie Mhina (kulia), akizungumza na baadhi ya wateja wa benki hiyo katika hafla ya futari walitowaandalia wateja wao wa mjini Zanzibar hivi karibuni.
   Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Singida, Saidi Amanzi akikabidhi kitabu kwa Mwenyekiti wa BAKWATA Singida, Sheikh Hamis Mohamed Kituke (kulia) wakati wa  hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki ya NBC kwa wateja wake  mkoani Singida hivi karibuni. Kushoto ni Mkuu wa Huduma za Kibenki zinazofuata kanuni na misngi ya kiislamu (Islamic Banking)  wa Benki ya NBC, Yassir Masoud.

   Mkuu wa Huduma za Kibenki zinazofuata kanuni na misngi ya kiislamu (Islamic Banking)  wa Benki ya NBC, Yassir Masoud (kulia), akisalimiana na  Sheikh wa Mkoa wa Mtwara na Naibu Kadhi wa Mtwara, Nurdin Mangochi katika hafla ya  futari waliyoandaa kwa wateja wao mkoani humo hivi karibuni.
   Baadhi ya wateja wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) mjini Tanga,  wakishirki mlo wa futari ulioandaliwa na benki hiyo mkoani Tanga hivi karibuni.
   Mkuu wa Huduma za Kibenki zinazofuata kanuni na misngi ya kiislamu (Islamic Banking)  wa Benki ya NBC, Yassir Masoud akisalimiana na Askofu wa Kanisa la KKKT Dayosisi ya Morogoro, Jacob Ole Mameo (kulia),  katika hafla ya  futari waliyoandaa kwa wateja wao mkoani Morogoro hivi karibuni.
   Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa Benki ya NBC Tanzania, James Kinyanyi (katikati), Mkuu wa Huduma Rejereja za Kibenki wa benki hiyo, Musa Jallow (kushoto), wakizungumza na mmoja wa wateja wa NBC, Yasser Yusuf (kulia),  katika futari waliyoiandaa kwa wateja wa Jiji la Dar es Salaam hivi karibuni.

  0 0


  Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella, amewaapisha wakuu wapya wa Wilaya za Mkoa wa Mwanza na kuwapa vitendea kazi ikiwapo katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania na Ilani ya Chama Tawala Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya Mwaka 2015- 2020, kwaajili ya kwenda kutimiza wajibu wao wa kikatiba kwenye wilaya walizo pangiwa. 

  Akizungumza baada yakuwaapisha, Mhe. Mongella, amewataka waende wakasimamie shughuli za kuhimiza maendeleo, suala la ulinzi na usalama kwenye wilaya zao, huku akitilia mkazo ukomeshwaji wa mauwaji ya watu wenye ulemavu wa Ngozi albino pamoja na Vikongwe, amesema, ikiwa jamii ya watu hao itapata madhara basi ni dhahiri Mkuu huyo wa Wilaya atakuwa ameshindwa kusimamia majukumu yake.

  Mkuu huyo wa mkoa pia, amerudia kauli yake nakuwataka viongozi hao wapya watambue wanajukumu zito lililoko mbele yao, ikiwa ni pamoja na kukomesha Utumiaji wa dawa zakulevya. 

  Aidha ameonya uchezaji wa Pool na unywaji wa Pombe wakati wa saa kazi, huku akimsisitiza mkuu wa Wilaya ya Nyamagana kuhakikisha ifikapo Agosti mosi, suala la wafanya biashara wanaofanya biashara kwenye maeneo ambayo hayaruhusiwi liwe limepatiwa ufumbuzi.Mongella amesema, katika mkoa wa Mwanza, Hotel na Clabu, yeyote ile, iwe ya kawaida au ya Kitalii, ikibainika inafanya biashara ya Shisha, hawata ivumilia na badala yake wataifutia Leseni ya biashara. 

  Walio apa mbele ya Mkuu wa Mkoa, ambao waliteuliwa na Mhe. Rais Tarehe 26, Juni, 2016 ni Emmanuel Enock Kipole, Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Estomin Francis Chang’a Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe, Hadija Rashid Nyembo Mkuu wa Wilaya ya Magu, wengine ni Juma Samwel Sweda Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Dkt. Leonard Moses Masale Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Mary Onesmo Tesha Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana na Mhandisi Mtemi Msafiri Simioni Mkuu wa Wilaya ya Kwimba. 

  Imetolewa na 
  Atley J. Kuni 
  Afisa habari na Mahusiano 
  Ofisi ya Mkuu wa Mkoa. 
  MWANZA. 
  04, Julai, 2016.

  0 0

  IMG-20160703-WA0000 
  Bill Nass- Chafu Pozi 2.Raymond - Natafuta Kiki 3.Darasa ft Rich Mavoko -Kama Utanipenda 4.Rich Mavoko - Ibaki Story 5.Namjua – Shetta 6.Ali Kiba - Aje 7.Mr Blue na Ali Kiba - Mboga Saba 8.Ben Pol - MOYO MASHINE 9.Nuh Mziwanda Ft. Alikiba - Jike shupa 10.Dogo Janja-My Life Kupendekeza wimbo uingie katika top 10 ya Jumapili hii endelea kutembelea page yetu ya Instagram ya Global Publishers na Maisha Basement.

  0 0


  MBUNGE wa Viti maalum Asha Abdalla Juma (MSHUA) akisaini Kitabu cha Wageni katika Ukumbi wa CCM Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi B Zanzibar.
  MWENYEKITI wa WUT Mkoa wa Mjini Waride Juma Othman akimkaribisha mgeni Rasmi Mbunge wa Viti maalum Asha Abdalla Juma (MSHUA) kuzungumza na washiriki wa Mafunzo ya uwezeshaji Wanawake wa Mkoa wa Mjini Unguja, katika Ukumbi wa CCM Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi B Zanzibar.
  MGENI RASMI Mbunge wa Viti maalum Asha Abdalla Juma akizungumza na washiriki wa Mafunzo ya uwezeshaji Wanawake wa Mkoa wa Mjini Unguja katika Ukumbi wa CCM Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi B.
  WASHIRIKI mbalimbali waliohudhuria wa Mafunzo ya uwezeshaji Wanawake wa Mkoa wa Mjini Unguja.
  MHE Asha Abdalla Juma (MSHUA) akiendesha Mafunzo ya uwezeshaji Wanawake wa Mkoa wa Mjini katika Ukumbi wa CCM Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi B.
  MHE Asha Abdalla Juma (MSHUA) akiendesha Mafunzo ya uwezeshaji Wanawake wa Mkoa wa Mjini katika Ukumbi wa CCM Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi B.
  MSHIRIKI wa mafunzo Nuru Moh’d Ahmed kutoka Shehiya ya Kikwajuni akichangia mada katika mafunzo hayo.
  MKUFUNZI wa Mafunzo Mwatima Abdalla Juma akiwapatia elimu ya kilimo cha mboga mboga washiriki wa mafunzo hayo.(Picha zote na Abdalla Omar Habari Maelezo Zanzibar).

  0 0


  Sehemu ya wadau mbalimbali waliofika kwenye uzinduzi wa Tecno Camon C9,jijini Dar es Salaam.
   Mkuu wa Vodacom Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Domician Mkama akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya uzinduzi wa Tecno Camon C9 ambayo itapatika kwenye maduka yote ya Vodaco yalipo Nchi nzimaa kwa bei ya shilingi laki (395,000) za kitanzania leo jijini Dar es Salaam.
   Meneja Mauzo wa TECNO Mobile Tanzania, Fred Kadinala akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani juu ya kua TECNO inawajali watumiaji wa simu zake hivyo kuamua kuwapa zawadi kubwa na kuwaruhusu waagize simu kwa bei ndogo ili wapate simu hiyo mapema Zaidi. jijini Dar es Salaam.

  0 0

   His Excellence Egon Kochanke Ambassador of the Federal Republic of Germany learning about Mobisol's high quality solar appliances and HD solar Tv at Saba Saba Trade Fair. 

   Pic 2; Saba Saba visitor learning about Mobisol's HD solar TV and solar home systems at the Mobisol booth in Nkurumah Hall at Saba Saba Trade Fair --- Germany-based solar-service company Mobisol provides a range of solar home systems with an affordable payment plan and is currently showcasing its largest solar HD TV available at the ongoing Dar es Salaam International Trade Fair (Sabasaba). 


  Mobisol Tanzania Marketing Manager Allan Rwechungura said that the largest solar HD TV recently launched in other markets in East African countries has been optimized for the use with Mobisol’s 200W Solar Home Systems. “Our largest solar HD TV is of high quality and comes with a two year warranty.

   Our customers can pay for the solar TV using mobile money in convenient installments, as they acquire the high quality TV together with their Mobisol solar system. The TV was recently awarded by the The Global Lighting and Energy Access Partnership as one of the best off grid appliances and is featured in their 2016 guide for outstanding solar and off-grid appliances. 

  We encourage people to visit us at Sabasaba in Nkurumah Hall to see our products; apart from the TV buyers can also acquire other solar-powered appliances such as haircutters, music systems and radios, irons and business solutions such as multiple phone chargers. 

  Mobisol is also focusing on conserving the environment – while, at the same time, the electricity we provide offers an opportunity for people to utilize it for various income generating activities which improve their economic wellbeing”. 

  To date, Mobisol has installed over 50,000 solar home systems across East Africa. Their systems come in varying sizes from 80 to 200 Wp to match the various energy needs of different households and its solar home systems provide enough electricity to power entire households or businesses with bright LED lights, and run radios, charge mobile phones and power a variety of household and consumer appliances. 

  The larger systems can also power small businesses enabling entrepreneurial customers to create additional income. Mobisol has shops in most parts of Tanzania that are popular known as MobiShop. In 2015, Mobisol won the United Nations Framework Convention on Climate Change (UNFCCC)’s Momentum for Change Award and also a TV was recently awarded by LEAP as one of the best off grid appliances and is featured in their 2016 guide for outstanding solar and off-grid appliances. 


  "The Global Lighting and Energy Access Partnership (Global LEAP) is the Clean Energy Ministerial’s energy access initiative, and is led by the U.S. Department of Energy. Global LEAP was launched as a commitment to the Sustainable Energy for All campaign, and its programs and initiatives support the growth of sustainable commercial clean energy access markets throughout the developing world.

  0 0

   
   Baadhi ya wananchi wakisaidia kuokoa watu waliopata ajali katika ajali  iliyohusisha mabasi mawili ya abiria, ambayo imetokea katika eneo la Manyoni Mkoani Singida na kupelekea vifo vya abiria papo hapo na wengine kadhaa kujeruhiwa katika eneo la Kijiji cha Maweni kilichopo Tarafa ya Kintinku wilayani Manyoni Mkoani Singida leo.

  0 0


  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda (kushoto) akimuapisha Mhe.Sophia Mjema (kulia) kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala leo katika Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es Salaam. Mhe.Sophia Mjema (kulia) akionesha Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) aliyokabidhiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kushoto) mara baada ya kuapishwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala leo katika Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es Salaam.
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kushoto) akimuapisha Mhe.Hashim Mgandilwa (kulia) kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni leo katika Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es Salaam.
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kushoto) akimuapisha Mhe.Felix Lyaniva (kulia) kuwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke leo katika Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es Salaam.
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe.Paul Makonda akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wapya wa Wilaya za Mkoa wa Dar es Salaam (mbele) pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dar es Salaam (nyuma)mara baada ya kuisha kwa zoezi la kuapishwa lililofanyika leo nje ya Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es Salaam.
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kushoto) akimuapisha Mhe.Ally Hapi (kulia) kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni leo katika Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es Salaam. Picha zote na Jacquiline Mrisho – MAELEZO

  Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda amewataka Wakuu wapya wa Wilaya kuimarisha ulinzi na usalama kwa wananchi waliopo katika Wilaya zao ili kudumisha amani.

  Makonda alisema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na Wakuu wa Wilaya juu ya kuwalinda wananchi na mali zao na kuhakikisha usalama unakuwepo katika Wilaya wanazozisimamia.Alieleza kuwa kwa kuwa wao ndio wanaomuwakilisha Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli katika Wilaya zao, wanatakiwa kuhakikisha wametekeleza ahadi zilizotolewa na Mhe. Rais wakati wa kampeni.

  “Ningependa wakuu wangu wa Wilaya mchukiwe kwa kusimamia Haki na Sheria kuliko kukumbatia uovu kwa kuhitaji furaha ya muda mfupi, hakikisheni Sheria na Kanuni zilizopo kwenye Katiba ndio ziwe muongozo wenu”, alisema Makonda.

  Mkuu huyo wa Mkoa wa Dar es Salaam aliwataka Wakuu wa Wilaya zake kuwasimamia Wakurugenzi wao ili kuhakikisha wanatumia bajeti waliyopewa katika kutatua changamoto zilizopo katika Wilaya zao.Aidha, Makonda amewasisitiza kuhakikisha kuwa kuanzia Julai 11 mwaka huu maeneo yote yanayofanya biashara ya shisha kufungwa na kuweka maeneo maalumu kwa ajili ya kuvutia sigara.

  Wakuu wa Wilaya wapya wamepewa wiki mbili za kutengeneza mpango kazi kwa kusoma ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Hotuba ya Mhe.Rais John Magufuli aliyoisoma wakati wa ufunguzi wa Bunge la 11 la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na mazingira ya kazi katika maeneo yao.

  0 0

  Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inampongeza Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwa kupiga marufuku matumizi ya Shisha na uvutaji wa Sigara hadharani kama afua ya kupunguza madhara ya tumbaku na madawa ya kulevya katika jamii.

  Uchunguzi wa kitalaam uliofanyika umebaini kuwa Shisha ina madhara kwa afya ya watumiaji hasa vijana na watoto. Watumiaji wa Shisha wanatumia kiwango kikubwa cha tumbaku kwa muda mfupi, hali inayoongeza madhara yatokanayo na tumbaku kama vile: – Saratani, Magonjwa ya Mapafu, Kibofu cha mkojo, Tezi dume, Koo, Mdomo na Kiywa, Ngozi, Ini, Ubongo.

  Pia imebainika kwamba matumizi ya Shisha huambatana na kuongezewa dawa nyingine za kulevya na hivyo hufanya watumiaji wa Shisha kupata uraibu wa dawa za kulevya. Matumizi ya dawa hizo za kulevya ni kosa la jinai.

  Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inapenda kurejea na kusisitiza agizo lake la tarehe 12 Machi 2015 la kuzuia matumizi ya sigara na matumizi ya bidhaa za tumbaku katika maeneo ya umma

  Inakumbushwa kwamba agizo hili limezingatia utekelezaji wa Sheria ya Usimamizi wa Bidhaa za Tumbaku, Sura ya 121 T.L 2002, ya Sheria za Tanzania kipengele cha 12 (1) ambacho kinakataza matumizi ya Tumbaku katika Maeneo ya Umma.

  Madhumu ya Agizo hili ni kuilinda Jamii kwa ujumla kutokana na madhara yatokanayo na moshi wa sigara. Wizara inawakumbusha wananchi wanaotumia bidhaa za tumbaku kupunguza au kuacha kabisa matumizi ya tumbaku. Aidha, agizo hili linaijumuisha jamii yote katika kubaini madhara ya tumbaku na umuhimu wa kuzuia matumizi ya tumbaku katika maeneo ya kazi na maeneo yote ya umma.

  Agizo hili linawahusu wananchi wote nchini wanaopata huduma katika maeneo ya umma kama ilivyotafsiriwa na sheria husika.

  Matumizi ya tumbaku hayaruhusiwi katika maeneo yote ya umma. Maeneo haya yanajumuisha ofisi zote za Serikali na tasisi zake zote, watu binafsi, vyuo, vituo vya huduma za Afya zikiwemo Hospitali, vituo vya Afya na zahanati, vituo vya usafiri wa Anga, Mabasi, bandari na treni, sehemu za mikutano, mapumziko, bustani na fuko za maji,sherehe,michezo,masoko,maduka makubwa pamoja na sehemu za kuabudu.Na kwa mtu yeyote anayeendesha shughuli katika maeneo ya umma analazimika kutenga eneo maalum kwa ajili ya wavuta sigara.

  Kwa kuwa Mhe. Waziri mwenye dhamana na masuala ya Afya nchini ameona hatari hii ya Uvutaji wa sigara na utumiaji wa bidhaa za tumbaku kwa afya ya Wananchi, kuanzia leo tarehe 4/7/2016 matumizi ya Shisha nchini yamepigwa marufuku kwa wote wanaojihusisha na matumizi hayo, na kwa wafanyabiashara wote wanaojihusisha na upatikanaji wa Shisha nchini

  Hivyo basi, kwa agizo hili katika maeneo yote nchini ambako matumizi ya Shisha hufanyika ni marufuku matumizi hayo kuendelea kutumika.

  Aidha vyombo vya Dola na mamlaka husika vinahimizwa kusimamia kwa ukamilifu katazo hili.

  0 0


  Ofisa Mwamasishaji Mwandamizi wa Mamlaka ya Maeneo Maalumu ya Uzalishaji kwa Mauzo ya Nje (EPZA), Nakadongo Fares (kulia), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo kuhusu mambo mbalimbali yanayofanywa na mamlaka hiyo. Kushoto ni Meneja Uhamasishaji Uwekezaji, Grace Lemunge.

  Meneja Uhamasishaji Uwekezaji, Grace Lemunge (kushoto), akisisitiza jambo kwenye mkutano huo na wanahabari.

  Meneja Mkuu wa Kampuni ya Star Infrastructure Development (T) Limited, Ananth Bhat akizungumzia mradi wao wa uwekezaji uliopo mkoani Morogoro.

  Mkutano na wanahabari ukiendelea.
  —————————-

  Na Dotto Mwaibale

  MAMLAKA ya Maeneo Maalumu ya Uzalishaji kwa Mauzo ya Nje (EPZA) imeweza kutengeneza ajira 36,000 kwa watanzania kupitia makampuni 140 yaliyowekeza hapa nchini. 

  Hayo yamebainishwa na Ofisa Mwamasishaji Mwandamizi wa Mamlaka hiyo, Nakadongo Fares Dar es Salaam leo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mambo mbalimbali yanayofanywa na mamlaka hiyo kwenye maonesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam 2016. 

  “Kupitia makampuni 140 yaliyowekeza hapa nchini yameweza kutoa ajira kwa watanzania 36,000 huku watoa huduma wakiwa 300,000” alisema Fares. Alisema kazi kubwa ya mamlaka hiyo ni kuhasisha uwekezaji katika kanda maalumu za kiuchumi, kuvutia na kuhamasisha uhuishaji wa teknolojia mpya, kuhamasisha uwekezaji kwenye viwanda usindikikaji wa malighafi zinazopatikana nchini, kutengeneza fursa za ajira na kuongeza pato la fedha za kigeni nchi.

  0 0

  Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Leo imekamilisha zoezi la kuhakiki vyama vya siasa 21 kwa upande wa Tanzania Bara . Zoezi la uhakiki wa vyama vya Siasa visiwani Zanzibar litaanza  Julai 11 mwaka huu.

  Uhakiki wa Vyama utafanyika katika Ofisi za Vyama zilizopo Zanzibar kwa maana ya Unguja na Pemba, zoezi hilo litajumuisha uhakiki wa idadi ya wanachama ambao Chama cha Siasa kinapaswa kuwa nao kwa mujibu wa masharti yalipo kwenye Sheria ya Vyama vya Siasa yam waka 1992.
  Ikumbukwe kuwa ,zoezi hili ni moja kati ya shughuli za kawaida za Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ambalo hufanyika maramoja kila mwaka likilenga kufahamu utekelezaji wa masharti na matakwa ya sheria ya vyama vya siasa.MSA1 
  Bi. Esther Mwanri, Mwanansheria kutoka ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa (wa nne kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mara baada ya zoezi la uhakiki  katika ofisi iliyopo Kinondoni Jijini Dar es Salaam. stori & picha na :ORPP
  MSA2 
  Afisa Sheria kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Bi. Monica Mwailolo (kushoto) akikagua taarifa za Chama cha Tanzania Labour Party (TLP) wakati wa zoezi la uhakiki uliofanyika katika ofisi hiyo iliyopo Magomeni Jijini Dar es salaam, katikati ni Katibu Mkuu wa Chama cha Tanzania Labour Party (TLP) Bi. Nancy Mrikalia akifuatiwa na Mwenyekiti wa Chama hicho Bw. Augustine Mrema.
  MSA3 
  Willy Brown Nyantiga, Mhasibu kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini akielezea jambo wakati wa zoezi la uhakiki ulioanyika katika Ofisi za Chama cha Union for Multiparty Democracy (UMD). Kulia ni Mwenyekiti  Taifa wa chama hicho Bw.Kamana Masoud na  Kushoto ni Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa” Gharama za Uchaguzi na Elimu kwa Umma”” Bibi. Piencia Kiure

  0 0

  Wabunge wa Bunge la Vijana la mwaka 2016, kutoka Vyuo mbalimbali vya Elimu ya Juu wakila kiapo cha utii baada ya kuanza kwa mkutano wa tatu wa bunge hilo, mjini Dodoma. Picha na Ofisi ya Bunge.
  Spika wa Bunge la Vijana, Regnald Massawe (kushoto) kutoka Chuo cha Uhasibu Arusha akimuapisha Stella Wadson-kutoka Chuo cha Ustawi wa Jamii kuwa Naibu Spika wa Bunge hilo baada ya kuanza kwa mkutano wa tatu wa Bunge la Vijana la mwaka 2016, mjini Dodoma. Picha na Ofisi ya Bunge .
  Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano Ofisi ya Bunge, Owen Mwandumbya akihutubia alipokuwa akizundua rasmi Bunge la Vijana la mwaka 2016, katika Ukumbi wa Pius Msekwa, mjini Dodoma jana. Mkutano huo ni wa tatu toka kuanzishwa kwa Bunge la Vijana chini ya mradi Legislatures Support Project(LSP). Picha na Ofisi ya Bunge. 
  Wabunge wa bunge la vijana kutoka vyuo mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa bunge hilo.

  0 0


  Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, akizungumza katika hafla ya kuwaapisha wakuu wapya wa Wilaya za Mkoa wa Mwanza hii leo, Julai 04,2016 katika viunga vya ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.

  Na BMG

  Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, amewataka wakuu wapya wa Wilaya za Mkoa huo kuhakikisha wanashirikiana na kamati za ulinzi na usalama pamoja na wananchi kwenye wilaya hizo ili kukomesha mauaji dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi na vikongwe yanayochangiwa na imani potofu za kishirikina.

  Akizungumza baada ya kuwaapisha wakuu hao wa wilaya zote saba za mkoa wa Mwanza, Mongella amesema kwa muda mrefu mkoa wa Mwanza umekumbwa na matukio ya mauaji ya watu wenye ualbino na vikongwe kutokana na imani za kishirikina na kwamba wakati umefika kuhakikisha matukio hayo yanakwisha.Amesema mkoa huo umejipanga vyema kuhakikisha matukio hayo yanakuwa historia kwa kuwa hakuna binadamu mwenye mamlaka ya kutoa uhai wa binadamu mwenzake kwa sababu yoyote ile.

  Mkuu huyo wa mkoa amewapa mwezi mmoja wakuu hao wapya wa wilaya kumaliza tatizo la madawati pamoja na kuwachukulia hatua watumishi hewa 1,057 waliogundulika kwenye wilaya zote za mkoa wa Mwanza.Mongella amewata wakuu hao wa Wilaya kuhakikisha kwamba matumizi ya dawa za kulevya katika wilaya zao yanakomeshwa ambapo amepiga marufuku matumizi ya shisha katika hoteli na klabu zote za muziki pamoja uchezaji wa "pool table" na unywaji wa pombe saa za kazi huku akitanabaisha kwamba atakaeshindwa kutekeleza maagizo hayo ni dhahiri shahiri kwamba atakuwa ameshindwa kusimamia majukumu yake.

  Aidha Mongella amemtaka mkuu wa Wilaya ya Nyamagana kuhakikisha kwamba hadi ifikapo Agosti mosi mwaka huu awe amewaondoa wafanyabiashara ndogondogo waliosambaa kwenye maeneo mbalimbali ya katikati ya jiji Mwanza.Wakuu wapya wa Wilaya za Mkoa wa Mwanza walioapishwa, wamesema wamejipanga vyema kushirikiana na viongozi wengine pamoja na wananchi katika Wilaya zao ili kuhakikisha kwamba wanatekeleza vyema majukumu yao ikiwemo kuimarisha suala la ulinzi na usalama katika jamii.

  Wakuu wapya wa Wilaya saba za Mkoa wa Mwanza walioapishwa hii leo ni Mary Onesmo Tesha wa Nyamagana, Estomin Francis Chang’a wa Ukerewe, Hadija Rashid Nyembo wa Magu, Juma Samwel Sweda wa Misungwi, Emmanuel Enock Kipole wa Sengerema, Dkt.Leonard Moses Masale wa Ilemela na Mhandisi Mtemi Msafiri Simion wa Kwimba ambapo wote wamekabidhiwa vitendea kazi ikiwemo Katiba ya Tanzania pamoja na Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2015/20.
  Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Mh.Emmanuel Enock Kipole (kulia), akiapa mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella (kushoto).
  Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe, Mhe.Estomin Francis Chang’a (kushoto) akiapa mbele ya mkuu wa mkoa wa Mwanza, Mhe.John Mongella (kulia).
  Mkuu wa Wilaya ya Magu, Mhe.Hadija Rashid Nyembo, akiapa hii leo
  Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Mhe.Juma Samwel Sweda, akiapa mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe.John Mongella (kushoto).


  Mkuu wa Wilaya ya Ilmela, Mhe.Dkt.Leonard Moses Masale (kushoto) akiapa mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe.John Mongella (katikati).
  Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Mhe.Mary Onesmo Tesha, akiapa hii leo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe.John Mongella (kushoto)
  Mkuu wa Wilaya ya Kwimba, Mhandisi Mhe.Mtemi Msafiri Simion (kulia), akiapa mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe.John Mongella (katikati).
  Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, CP.Clodwin Mtweve, akizungumza katika hafla fupi ya kuwaapisha wakuu wapya wa Wilaya za Mkoa wa Mwanza iliyofanyika hii leo katika viunga vya ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.
  Sala kutoka kwa Sheikh mkuu wa Bakwata mkoani Mwanza, kabla ya kuwaapisha wakuu wapya wa Wilaya za mkoa wa Mwanza
  Sala kutoka kwa Kiongozi wa Umoja wa Makanisa Jijini Mwanza, kabla ya kuwaapisha wakuu wapya wa Wilaya za mkoa wa Mwanza
  Afisa Habari na Mahusiano kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza
  Baadhi ya Wakuu wa Wilaya waliomaliza muda wao, ambapo kushoto ni aliekuwa Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Baraka Konisaga maarufu kwa jina la Mtumishi wa Mungu akiwa pamoja na aliekuwa Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Manju Msambya.
  Meneja wa Shirika la Posta mkoani Mwanza akifuatilia shughuli ya kuwaapisha wakuu wapya wa Wilaya za Mkoa wa Mwanza
  Viongozi mbalimbali wa Serikali na Siasa mkoani Mwanza
  Viongozi wakifuatilia zoezi la kuwaapisha wakuu wapya wa Wilaya za Mkoa wa Mwanza
  Viongozi wa dini mkoani Mwanza, wakifuatilia zoezi la kuwaapisha wakuu wapya wa Wilaya za Mkoa wa Mwanza
  Baadhi ya viongozi kutoka kamati ya ulinzi na usalama mkoani Mwanza, wakifuatilia zoezi la kuwaapisha wakuu wapya wa Wilaya za Mkoa wa Mwanza

  Wakuu wapya wa Wilaya za Mkoa wa Mwanza
  Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, wa nne waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wapya wa Wilaya za Mkoa wa Mwanza (waliosimama nyuma) na viongozi wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Mwanza.

  0 0

  Balozi wa Korea, Song, Geum-young akizungumza na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Museru baada ya balozi huyo kumtembelea mkurugenzi huyo LEO. Mazungumzo hayo yalihusu maendeleo ya hispitali hiyo.Picha na John Stephen, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo, Profesa Museru akitoa historia fupi ya MNH LEO kwa Balozi Korea, Song, Geum-young. Kutoka kulia ni Mkuu wa Idara ya Mionzi, Dk Flora Lwakatare, Mkuu wa Idara ya Upasuaji, Dk Julieth Magandi na Mkurugenzi wa Uuguzi, Sister Agnes Mtawa wakifuatilia mazungumzo LEO katika ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa MNH. Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma, Aminiel Aligaesha (kushoto), Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali (EMD), Dk Juma Mfinanga (katikati) na Mkuu wa Idara ya Watoto, Merry Charles wakifuatilia mazungumzo hayo LEO. Balozi wa Korea, Song, Geum-young akisaini kitabu cha wageni.

  0 0


  Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Adam Mayingu, akiyekaa, akimuonyesha Mwanachama huyu wa Mfuko huo michango yake papo kwa hapo kwenye banda la Mfuko huo lililoko jengo la Wizara ya Fedha na Mipango, wakati wa maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, Julai 4, 2016. Mamia ya Wananchi wamekuwa wakimiminika kwenye banda hilo, ambapo jambp la kuvutia Mkurugenzi Mkuu huyo aliungana na wafanyakazi wake kutoa huduma kwa wananchi. Maonyesho hayo yanashirikisha jumla ya nchi 30 ambapo banda la PSPF limekuwa na idadi kubwa ya wananchi wanaotembelea kujua huduma zitolewazo kwa wananchi ambao si wanachama lakini pia kuwahudumia wanachama wake. (PICHA NA K-VIS MEDIA/KHALFAN SAID)
  Mama Anna Mkapa, (kulia), Mke wa Rais mstaafu Benjamin Mkapa, ambaye ni Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa Kwa Wote (EOTF), akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu, (kushoto) na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Abdul Njaidi, wakati Mkurugenzi huyo alipotembelea banda la EOTF linalokusanya wajasiriamali kutoka mikoa yote ya bara na vuisiwani. Kupitia mpango wa uchangiaji wa hiari yaani PSS, wajasiriamali hao wanaweza kujiunga na Mfuko huo na hivyo kufaidika na mafao mbalimbali yakiwemo ya kuboresha biashara zao
  Mama Salma Kikwete, (kulia), Mke wa Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete, akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu, walipokutana kwenye banda la EOTF kwenye maonyesho ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, Julai 4, 2016.


  Mamia ya wananchi wakiwa kwenye banda la PSPF Julai 4, 2016
  Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu, akimkabidhi kadi yake ya uanachama wa Mfuko huo, Mwanaidi Msangi baada ya kujiunga na mpango wa uchangiaji wa hiari (PSS), Julai 4, 2016
  Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu, akimkabidhi kadi yake ya uanachama wa Mfuko huo, Baturi J. Msusi, baada ya kujiunga na mpango wa uchangiaji wa hiari (PSS), Julai 4, 2016
  Baturi J. Msusi mwanachama mpya wa PSPF, kupitia mpango wa uchangiaji wa hiari, (PSS), akionyesha kadi yake ya uanachama baada ya kujiunga leo Julai 4, 2016 na kupatiwa papo hapo.
  Mwanaidi Msangi, mwanachama mpya wa PSPF, kupitia mpango wa uchangiaji wa hiari, (PSS), akionyesha kadi yake ya uanachama baada ya kujiunga leo Julai 4, 2016 na kupatiwa papo hapo.
  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dotto James, (katikati), na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali wizarani hapo, Ben Mwaipaja, wakipatiwa maelezo na Afisa wa UTT-AMIS, wakati Naibu Katibu Mkuu huyo alipotembelea taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo kwenye jengo la Wizara ya Fedha, viwanja vya Maonyesho ya Biashaya ya Kimataifa Mwalimu Nyerere, Maarufu kama Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
  Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Abdul Njaidi, (kushoto), akimpatia maelezo ya kiutendaji Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio, (watatu kushoto), Meneja Uhusiano wa PPF, Lulu Mengele (wapili kushoto), na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali Wizara ya Fedha na Mipango, Ben Mwaipaja, (kulia), wakati Mkurugenzi huyo alipotembelea banda la Wizara ya Fedha na Mipango ambayo Mifuko ya Hifadhi ya Jamii iko chini ya wizara hiyo.
  Afisa wa PSPF, Pensila (kushoto), akitoa elimu kwa wanachi waliotembelea banda la Mfuko huo kwenye maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, Julai 4, 2016
  Mkurugenzi Mkuu Mayingu, akimuhudumia Mwanachama huyu aliyefika kujua hali ya michango yake kwenye banda la Mfuko huo Julai 4, 2016
  Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu (aliyekaa0, akisaidiana na wafanyakazi wake kuhudumia wananchi Julai 4, 2016

older | 1 | .... | 900 | 901 | (Page 902) | 903 | 904 | .... | 1896 | newer