Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46202 articles
Browse latest View live

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ASHIRIKI MAADHIMISHO YA SIKU YA KIMATAIFA YA UTOKOMEZAJI WA UGONJWA WA FISTULA, JIJINI DAR

0
0

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na baba wa mtoto, Elizabeth Nora kutoka Dodoma aliyelazwa katika Hospitali ya CCBRT, wakati Makamu alipofika hospitalini hapo leo Mei 23, 2013 kwa ajili ya kushiriki katika Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Utokomezaji wa Ugonjwa wa Fistula.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Dokta wa Hospitali ya CCBRT, wakati alipokuwa akitembelea katika wodi za wagonjwa waliolazwa katika Hospitali hiyo, alipofika hospitalini hapo leo, kwa ajili ya kushiriki katika Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Utokomezaji wa Ugonjwa wa Fistula. Kulia ni Mtoto Boniface Patrick akiwa na Baba yake, Patrick Luwao, Wakazi wa Dodoma, akiwa amelazwa baada ya kufanyiwa upasuaji na kuongezewa sehemu ya mguu uliokuwa mfupi.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Stellah Nzyemba, ambaye awali alikuwa mgonjwa na baada ya kutibiwa katika Hospitali hiyo ya CCBRT na kupona ameajiriwa ili kuwasaidia wagonjwa wa Fistula. Makamu alifika hospitalini hapo leo kwa ajili ya kushiriki katika Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Utokomezaji wa Ugonjwa wa Fistula.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitembelea katika Wodi ya wagonjwa wa Fistula, wakati Makamu alipofika hospitalini hapo leo kwa ajili ya kushiriki katika Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Utokomezaji wa Ugonjwa wa Fistula.
 Makamu wa Rais Dkt Bilal, akimjulia hali mtoto mgonjwa aliyelazwa katika Hospitali hiyo ya CCBRT
 Baadhi ya wasichana waliokuwa wakiugua ugonjwa huo na kutibiwa katika Hospitali ya CCBRT, ambao kwa sasa wanapewa mafunzo ya kufanya kazi za mikono.
 Makamu wa Rais Dkt. Bilal, akiwasili katika eneo lililoandaliwa maalum kwa ajili ya kufanyia shughuli za maadhimisho hayo.Picha na OMR

DROO YA KWANZA YA WINDA NA USHINDE YAFANYIKA LEO JIJINI DAR.

0
0
 Meneja wa bia ya Serengeti Allan Chonjo, akiongea na mshindi wa droo ya kwanza ya Winda na Ushinde kwa njia ya simu iliyochezeshwa leo katika ofisi za Kampuni ya bia ya Serengeti jijini Dar es Salaam
 Meneja mauzo na masoko wa kampuni ya Push Mobile Media Rugambo Rodney(katikati) akiwaonesha kitu Afisa mwandamizi wa PWC Tumainieli Malisa(kushoto) na Meneja wa bia ya Serengeti Allan Chonjo(kulia)
Meneja wa Bia ya Serengeti Allan Chonjo (katikati) akizungumza kwa njia ya simu na mshindi wa 1,000,000 wakati wa kuchezesha droo ya kwanza ya Winda na Ushinde leo katika ofisi za Kampuni ya bia ya Serengeti, akiwa pamoja na Meneja mauzo na masoko Rugambo Rodney(kulia) na Afisa mwandamizi wa PWC Tumainieli Malisa(kushoto). 

Meneja wa bia ya Serengeti Allan Chonjo, akimtangaza Honest Minja(38) mshindi wa Tsh 1,000,000 wa droo ya kwanza ya Winda na Ushinde kwa wana habari katika droo iliyochezeshwa leo katika ofisi za Kampuni ya bia ya Serengeti jijini Dar es Salaam.

NAPE YUPO BERLIN, UJERUMANI

0
0
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, CCM, Nape Nnauye (katikati) akikaribishwa na baadhi ya viongozi wa chama cha SPD mjini Berlin, Ujerumani alipowasili jana kuhudhuria sherehe za miaka 150 ya kuzaliwa kwa chama hicho cha SPD.

MINISTRY OF TOURISM AND TOURISM PRIVATE SECTOR JOINTLY DISCUSSED TOURISM DEVELOPMENT LEV

0
0

 ONE OF THE REPRESENTATIVE OF TOURISM PRIVATE SECTOR EXPLAINING A POINT TO THE MINISTER OF NATURAL RESOURCES AND TOURISM, HON. KHAMIS KAGASHEKI DURING THE DIALOGUE.

The Ministry of Tourism and Natural Resources today hosted a dialogue forum with the Tourism Private Sector on the Tourism (Tourism Development levy) Regulations 2012 at Dar es Salaam Serena Hotel.

During the dialogue issues that were discussed included:-
.Effective partnership for tourism development
.Tourism development levy & regulations 2012 as well as
.Improving tourism investment - Business environment .

legal officers discussing that raised during the forum


RAIS KIKWETE AKUTANA NA TIMU YA TAIFA IKULU JIJINI DAR LEO

0
0
Rais Jakaya Kikwete akiongea na wachezaji wa timu ya mpira ya Taifa, Taifa Stars leo Ikulu jijini Dar es salaam alipokutana nao kuwapa hamasa waweze kupata ushindi katika mchezo wao dhidi ya Moroco utakaochezwa Juni 7, na michezo mingine ikiwa ni hatua ya kuiwezesha timu hiyo kukata tiketi ya kushiriki mashindano ya kombe la dunia mwaka 2014.
Rais Jakaya Kikwete akiwaaga wachezaji wa Timu ya Taifa Stars mara baada ya kukutana nao leo Ikulu Jijini Dar es salaam kuwahamasisha washinde mchezo dhidi ya timu ya Taifa ya Moroco utakaofanyika June 7 ikiwa ni sehemu ya Taifa Stars kutafuta ticketi ya kucheza mashindano ya Kombe la Dunia.
Meneja wa Timu ya Taifa Stars Bw. Mukebesi akiteta jambo na Kepteni wa Timu ya Taifa Stars Juma Kaseja Ikulu jijini Dar es salaam walipokutana na Rais Jakaya Kikwete.
Rais Jakaya Kikwete akiwa katika Picha ya Pamoja na wachezaji wa Timu ya Taifa , Taifa Stars, viongozi wa Wizara ya Habari, Vijana ,Utamaduni na Michezo na Viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Rais Jakaya Kikwete akiwa katika Picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya Taifa , Taifa Stars Ikulu jijini Dar es salaam. Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.

Na. Veronica Kazimoto –MAELEZO.

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete leo amekutana na timu ya Taifa (Taifa stars) kwa lengo la kuitia moyo katika mechi ijayo kati yake na timu ya Moroco ikiwa ni harakati za Tanzania kutafuta tiketi ya kucheza fainali za kombe la Dunia kwa mara ya kwanza mwaka 2014.

Rais Kikwete ameiambia timu hiyo kuwa ina uwezo mkubwa wa kusonga mbele kutokana na uwezo mkubwa waliouonesha katika mchezo wao dhidi ya Gambia ambapo walifanikiwa kupata ushindi wa bao 2-0.

“Maadamu mara ya kwanza mliwashinda Gambia, hakikisheni pia mnapata ushindi dhidi ya Moroco, mkishinda tunafurahi sana na mkishindwa tunanyong’onyea sana,” amesema Rais Kikwete.

Aidha amempongeza kocha wa timu hiyo Kim Poulsen pamoja na Kamati ya Taifa ya ushindi ya Taifa stars kwa kuisaidia timu hiyo kiasi cha shilingi milioni 30 ikiwa ni mkakati wa kuiongezea nguvu kwa hatua iliyofikia na kuwataka wachezaji kujituma ili kuwafurahisha watanzania ambao hivi sasa wanaipenda timu yao ya Taifa.

Nae Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Fenera Mukangara amesema Serikali itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa michezo nchini ili kuondoa changamoto zinazoikabili timu hiyo.

Kwa upande wake Kocha Poulsen, amemshukuru Rais Kikwete kwa kuwakaribisha na kuwatia moyo ambapo ameahidi kuifundisha vizuri timu hiyo ili kuhakikisha kuwa wanapata ushindi.

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji wenzake kaptaini wa timu hiyo Juma Kaseja amemshukuru Rais Kikwete na kuahidi kujituma kwenye mazoezi na hatimaye kuibuka washindi kwenye mechi zijazo.

Taifa stars ambayo inakamata nafasi ya pili katika kundi C inatarajia kucheza ugenini na Morocco mnamo Juni 7 mwaka huu.

Dar Stock Event- Triniti bar

0
0

WADAU CHANGAMKIENI NAFASI ZA KAZI PART TIME.

0
0

Consultant Position Available

CIDA funded Support to the Ethics Secretariat (SES) Project in Tanzania

Information & Communications Technology Specialist


Level of Effort: Up to 50 days from present to September 2015

Reports to: Field Project Director, SES Project


Overview:

This individual will design databases and create systems for the utilization of data for planning and reporting purposes as well as support ES website development as it relates to facilitating the electronic submission of relevant data.


Roles and Responsibilities:

·         Provide technical expertise and recommendations in assessing new IT software projects and initiatives;

·         Make recommendations on custom applications to support business operations;

·         Identify opportunities that can improve efficiency or business processes

·         Investigate and resolve application functionality related issues and provide first level support and troubleshooting;

·         Provide systems for storage, retrieval, security and back-up of ES data

·         Work with project consultants in developing a database system for collecting, reviewing and monitoring information collected for use by the ES to conduct investigative analysis and risk management of the same.

·         Work with project consultants in developing management information and statistic reports to assist ES management with supervision and oversight of staff performance indicators;

·         Develop internet-based data input and collection screens for data entry by solicited parties.

·         Coordinate application development for multiple projects;

·         Assist in managing an outsource relationship for 3rd party application development and programming (in the event one is needed);

·         Write technical procedures and documentation for the applications including operations, user guide, etc.;

·         Create design prototypes, including graphic design, site navigation, and layout of content, for the website;

·         Ensure that the layout of the content is accessible and logical; recommend improvements if necessary;

·         Create visual concepts that match the content and the image wanted by the program and ensure the site is easy to navigate;

·         Build the website using technologies that conform to standards and make sure that they are universally accessible;

·         Design security infrastructure system;

·         Create and provide support documentation and training on maintenance and update procedures;

·         Train on the management of day-to-day operational aspects for managing the website and communicate with external vendor and entities as required.



Qualifications:

Database & Website Design and Administration:

·         5-7 years‟ experience with website and database design and administration;

·         Advanced knowledge of XHTML, CSS, and use of digital imaging and illustration with Adobe

·         Support to the Ethics Secretariat (SES) Project in Tanzania 53 Inception Report



·         Photoshop, QuarkXPress, and Illustrator;

·         Knowledge of JavaScript, CSS, PHP and dynamic HTML;

·         Experience with Macromedia Flash;

·         Extensive experience working on PC platforms.

·         Knowledge and demonstrated experience with cross-browser and cross-platform issues (IE, Firefox, Safari, etc.)

·         Extensive knowledge of current web-design trends and techniques, with a strong portfolio displaying user-centred design and experience with web database solutions.

·         Experience in general management of the development, documentation, and implementation of Internet-based applications to support business operations.

·         Experience with security issues and structures for web systems handling sensitive information


Required Skills:

·         Web and database design and administration (5 Years preferred)

·         Experience with JavaScript (5 Years preferred))

·         XHTML, CSS, Photoshop, QuarkXPress, Illustrator (5 years preferred))

·         Maintaining and administering web server and middleware tools including SQL(5 years preferred))

·         Good English communication skills, both written and verbal

Preferred Assets:

·         BS degree, preferably in IS or Computer Science

·         Microsoft Certified in Microsoft word, Excel, and SQL Server.
Remuneration based on experience and past salary history

Send complete CV with references to sestanzania@gmail.com or deliver to Sukari House 3rd Floor Dar Es Salaam, Support to ethics Secretariat Project Office

Closing date: All CVs must be received no later than 31 May 2013


RAIS JAKAYA KIKWETE AFUNGUA MAONYESHO YA MFUMO WA MATOKEO MAKUBWA 'SASA' AWAMU YA KWANZA

0
0
 Rais Jakaya Kikwete, Makamu wake Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wakisikiliza maelezo kutoka kwa Ofisa Mtafiti Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Dkt. Mary Shetto, wakati walipokuwa wakitembelea Maonesho ya Mfumo wa Matokeo Makubwa Sasa Awamu ya Kwanza, baada ya kuyafungua rasmi leo katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, Jijini Dar es Salaam.
Rais Jakaya Kikwete, Makamu wake Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wakisikiliza maelezo kutoka kwa Mchambuzi Sera Mkuu wa Ofisi ya Rais na Mipango, Lorah Madete, wakati walipokuwa wakitembelea Maonesho ya Mfumo wa Matokeo Makubwa Sasa Awamu ya Kwanza, baada ya kuyafungua rasmi leo katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, Jijini Dar es Salaam. 
Rais Jakaya Kikwete, Makamu wake Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wakiwa kwenye Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa wakati wa Ufunguzi rasmi wa Maonesho ya Mfumo wa Matokeo Makubwa 'Sasa' Awamu ya Kwanza leo Mei 24, 2013
Rais Jakaya Kikwete, Makamu wake Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wakiwasili kwenye Ukumbi wa Jumba la Makumbusho ya Taifa, leo Mei 24, 2013 kwa ajili ya Kufungua rasmi Maonesho ya Mfumo wa Matokeo Makubwa 'Sasa' Awamu ya kwanza.
 Msanii maarufu wa kughani, Mrisho Mpoto, wakibinjuka Sarakasi, wakati kikundi chake na Bendi yake ya Mjomba ilipokuwa ikitoa burudani katika Maonesho ya Mfumo wa Matokeo Makubwa 'Sasa' Awamu ya Kwanza, yaliyofunguliwa na Rais Jakaya Kikwete, leo Mei 24, 2013. 

Wanamuziki wa Bendi ya Mjomba, wakiimba kutoa burudani katika Maonesho ya Mfumo wa Matokeo Makubwa 'Sasa' Awamu ya Kwanza, yaliyofunguliwa na Rais Jakaya Kikwete, leo Mei 24, 2013. Picha na OMR.

RATIBA YA SHEREHE ZA AU KESHO - KARIMJEE HALL

0
0

TENTATIVE PROGRAMME FOR THE CELEBRATIONS OF THE OAU/AU GOLDEN JUBILEE ON 25th MAY, 2013

Venue                  -        Karimjee Hall
Guest of Honour  -        Hon. Bernard Kamillius Membe (MP)
Minister for Foreign Affairs and International Cooperation

TIME
EVENT
RESPONSIBLEINSTITUTION
8.00
Arrival at the Ministry
All
8.30
Lighting of the OAU/AU Torch
Hon. Membe-Minister for Foreign Affairs and International Cooperation
8.35
Festive Procession led by Brass Band
Invitees
8.45
Arrival at the Karimjee Hall
Invitees
8.50-9.10
Folk Dances
Dance Troupes
9.15-9.25
Playing of the AU and the Tanzania Anthems
Brass Band
9.30-10.00
Opening Remarks
Guest of Honour (Hon. Membe)

10.10-11.20
Panel Discussion-Pan Africanism and African Renaissance
Key Speakers: Amb. W. M. Mangachi & Mme Tonia Kandiero
Moderator: Prof. A. Mhina
11.40-12.50
Panel Discussion-OAU/AU’s Role in the Liberation Struggle and Self-determination
Key Speakers: Amb. A. Kiwanuka & Amb. T.H. Chiliza
Moderator: Amb. M. Maundi
12.50
Closing Remarks
Dean of the African Diplomatic Group
12.50
Folk Dances
Dance Troupes
13.00
Luncheon
Caterer

serikali yaombwa kutoa ruzuku kwa shule binafsi na mikopo yenye riba nafuu

0
0

Serikali  imeombwa kutoa ruzuku kwa shule binafsi na mikopo  yenye riba ndogo kwa kiasi cha asilimia  saba pamoja na kuwepo kwa mfumo wa kuchagua wanafunzi katika shule binafsi.
 
Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa shirikisho la shule binafsi nyanda za juu kusini(TAMOSCO) CHERESTINO MOFUGA katika semina iliyofanyika kwenye ukumbi wa shule ya sekondari ya kitwiru.
 
Amesema kuwa lengo la semina hiyo ni kujenga uwezo mamaeneja wa shule binafsi kwani wengi wao wanaonekana kutokuwa na uwezo wa kuongoza na hivyo kuchangia shule nyingi kuanzishwa bila usajili.
 
Hata hivyo amesema kuwa shirikisho limetenga siku ya kupeana ujuzi ikiwemo kujifunza mambo ya uongozi,masuala ya uendeshaji biashara,ubora katikasuala la elimu pamoja na jinsi ya kujua kutafuta wadhamini.
 
Aidha amezitaja changamoto ambazo zinawakabili katika shirikisho hilo ni uendeshwaji wa shule pamoja na ushirikiano baina yao na serikali na semina hiyo itafanyika kwa siku mbili.

KUTOKA IRINGA:wakulima washauriwa kutumia vipimo vinavyokubalika na kukataa kurubuniwa na wafanyabiashara

0
0

Wakulima wa Mpunga, Mahindi na Viazi Mkoani Iringa Wametakiwa Kutumia Vipimo Vinavyo Kubalika na Wasirubuniwe na Wafanya Biashara kwa Kuuza kwa lumbesa.
 
 
Mkuu wa Mkoa Wa Iringa DK.CHRISTINE  ISHENGOMA,amesema kuwa wakulima hufanya hivyo kutokana na kurubuniwa na wafanyabiashara hao.
  
kufuatia mandamano yaliyofanyika pawaga baina ya wakulimaDR.  ISHENGOMA amekanusha na kusema kuwa si wakulima walioandamana bali ni wafanya biashara. Amesema Wafanya Biashara na Wasafirishaji Ndiyo Walijivika Kofia ya Wakulima na Sio Wakulima wa Pawaga bali ni Wafanya Biashara na Wasafirishaji.
 
WAKATI HUO HUO
 
Wananchi Mkoani Hapo Wametakiwa Kuchanganya Vyakula Ili Kukomesha na Kutokomeza Ugonjwa Wa UtapiaMlo Unao Likumba Taifa na Mkoa wa iringa kwa ujumla.
 
Akiongea na Waandishi wa Habari Ofisini Kwake Mkuu wa Mkoa wa Iringa DK.CHRISTINE ISHENGOMA Amesema kuwa Wanachi Watumie Elimu wanayo Pewa na Mama Lishe Ambao Wanapatikana Kila Wilaya.
 
 
Amesema Kuwa Utafiti Uliofanywa Umebaini Kuwa Tanzania Ni Nchi ya Tatu Kwa Kuathiriwa na UtapiaMlo Barani Afrika.
 

KUTOKA IRINGA:DIWANI WA KATA YA MIVINJENI FRANK NYALUSI AACHIWA HURU.

0
0

Mahakama ya hakimu mkazi manispaa ya Irnga imemuachia huru diwani wa kata ya mivinjeni FRANK NYALUSI na wenzake watatuJOSEPH MGIMWA,WILLIUM MGUNDA NA TIMOTHEO MSENJA  waliokuwa wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa makosa matatu.
 
Akiwasomea mashtaka yao katika mahakama ya hakimu mkazi mshtakiwa wa pili na watatu FRANK NYALUSI na JOSEPH MGIMWA wanashtakiwa kwa kosa la kuwashawishi watu kufanya fujo na kuandamana bila kibali hivyo kusababisha uvunjwaji wa amani katika barabara ya mashine tatu tarehe 19 mwezi huu.
 
Wakati huo huo mahakama imewashtaki watuhumiwa wote (4) kwa kosa la pili la kuandamana na kufanya mkutano bila kibali cha kamanda mkuu wa jehi la polisi hivyo kusababisha vurugu katika eneo la mashine tatu,na kosa la tatu mahakama ime washtaki watuhumiwa na 2 na namba tatu kwa kosa la kushawishi watu kufanya fujo na kufanya uhalibifu wa mali likiwemo gari la kikosi cha zima moto mkoani hapa.
 
Washitakiwa wote wameachiwa huru kwa dhamana ya shilingi milioni 1  huku mahakama ikiwataka washitakiwa wa nne kuto jihusisha na sehemu yoyote yenye dalili ya uvunjwaji wa amani.

Stanbic bank Tanzania yazidi kuboresha huduma zake.

0
0
 Mkurugenzi mkuu wa Stanbic Bank,Bwa Bashir Awale akimkabidhi zawadi ya heshima mgeni rasmi,Mwenyekiti wa kampuni ya ndege ya Precision Air,Bwa.Michael Shirima kwenye hafla ya benki hiyo iliyohusu maboresho zaidi katika huduma yake ya kibenki itolewayo kwa wateja wenye mahitaji maalum (Executive Banking), kwa lengo la kuwaondolea usumbufu, kuwapa huduma kwa kulingana na mahitaji yao maalum, kuhudumiwa kwa wakati wanaotaka wao na kuwapa faida zaidi.
Pichani ni Mgeni rasmi,Mwenyekiti wa kampuni ya ndege ya Precision Air,Bwa.Michael Shirima akizungumza mbele ya wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye hafla ya Stanbic Bank iliyohusu maboresho zaidi katika huduma yake ya kibenki itolewayo kwa wateja wenye mahitaji maalum (Executive Banking), kwa lengo la kuwaondolea usumbufu, kuwapa huduma kwa kulingana na mahitaji yao maalum, kuhudumiwa kwa wakati wanaotaka wao na kuwapa faida zaidi.Hafla hiyo imefanyika leo jioni ,ndani ya hotel ya Hyatt kempinsk jijini Dar.
Mkuu wa Masoko na Mahusiano katika Benki ya Stanbic  Tanzania,Bwa.Abdallah Singano akizungumza mbele ya wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye hafla ya Stanbic Bank iliyohusu maboresho zaidi katika huduma yake ya kibenki itolewayo kwa wateja wenye mahitaji maalum (Executive Banking product), kwa lengo la kuwaondolea usumbufu, kuwapa huduma kwa kulingana na mahitaji yao maalum, kuhudumiwa kwa wakati wanaotaka wao na kuwapa faida zaidi.Hafla hiyo imefanyika leo jioni ,ndani ya hotel ya Hyatt kempinsk jijini Dar.

Bwa.Singano alisema kuwa Wateja wa benki hiyo sasa wataepuka ulipaji wa ada mbali mbali na zisizotabirika, na hivyo kwa ada ya kila mwezi au kiasi kidogo cha akiba katika akaunti, mteja atahakikishiwa kupata faida nyingi na huduma bora kwa wakati wake. 
Mkuu wa Kitengo cha huduma za kibenki binafsi na za kibiashara, Paul Omara akizungumza wakati wa hafla ya kukuza mahusiano baina ya wafanyakazi wa benki hiyo na wateja, iliyofanyika  jioni ya leo katika hoteli ya Hyatt jijini Dar es Salaam, alisema kuwa huduma hiyo imesukwa upya na kuundwa kutokana na marejesho ya wateja ya jinsi gani wanahitaji wahudumiwe na maoni yao juu ya uboreshaji wa huduma za benki hiyo kwa ujumla.
Baadhi ya wafanyakazi  Stanbic Bank wakiwa katika picha ya pamoja







WATAALAM WA TIBA ZA ASILI NA TIBA MBADALA WAKUTANA JIJINI DAR ES SALAAM

0
0
 `Kaimu mganga mkuu wa serikali Dkt. Mohamed Mohamed akifungua mkutano wa Baraza la wataalam wa Tiba za Asili na Tiba mbadala leo jijini Dar es salaam waliokutana kujadili mafanikio, changamoto na mipango mbalimbali waliyonayo katika utoaji wa huduma bora za afya kwa wananchi. 
 Kaimu Mkurugenzi wa Masuala ya Tiba za Asili na Tiba Mbadala wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt.Paulo Mohammed akitoa ufafanuzi wa hali halisi ya Tiba za Asili na Tiba mbadala nchini Tanzania na mpango wa serikali wa kuendelea kuthamini huduma inayotolewa na wataalam hao wakati wa mkutano wa Baraza la wataalam wa Tiba za Asili na Tiba mbadala. 
Mratibu wa Tiba za Asili na Tiba Mbadala kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) Rose Shija akisoma salam za mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani nchini Tanzania Dkt. Rufaro Chatora leo jijini Dar es salaam ambaye amepongeza juhudi zinazofanywa na serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Afya kutatua changamoto zinazowakabili wataalam wa Tiba za Asili na Tiba mbadala.  
 Mtafiti mwandamizi mkuu wa Idara ya Utafiti wa Tiba Asili kutoka Taasisi ya Utafiti wa magonjwa ya Binadamu  Hamis Masanja Malebo akitoa mada kuhusu historia ya Tiba za Asili na uhusiano uliopo katika matumizi ya mimea ya asili kati ya tiba za asili  na tiba mbadala na tiba za kisasa katika utengenezaji wa dawa. Picha na Aron Msigwa - MAELEZO.
Sehemu ya wataalam wa Tiba za Asili na Tiba mbadala  waliohudhuria mkutano wa Baraza la Wataalam wa tiba hiyo wakifuatilia masuala mbalimbali wakati wa mkutano huo leo jijini Dar es salaam.

KUTOKA IRINGA:serikali yaombwa kuwashirikisha wadau wa elimu katika masuala ya mabadiliko ya elimu.

0
0
Serikali imeobwa kuwashirikisha wadau wa elimu katika masuala yanayohusu mabadiliko ya elimu kwani kwa kufany ahivyo itasaidia kuboresha elimu yetu ya Tanzania .
 
Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa shirikisho la shule binafsi nyanda za juu kusin CHERESTINO MOFUGA na hilo limetokana na suala la kuludia kusahihisha matokeo ya kidato cha nne.
 
Amesema kuwa kushuka kwa elimu wakati mwingine serikali inachangia kwani inaamua mambo bila kushirikisha wadau au vyama vya elimu huku akitolea mfano matokeo ya kidato cha nne waliyoomba yarudiwe wakati tayari kunawatoto wengine wameshapoteza maisha kutokana na kutangazwa kwa matokeo mabovu.
 
Hata hivyo amesema kutokanana hilo serikali inapaswa kutoa fidia kwa wazazi waliopoteza watoto wao na waliochangia matokeo kuwa mabaya wanapaswa kupewa adhabu.
 
Aidha ameongeza kwa kusema kuwa hata hivyo suala la kuludia usahihishaji wa matokeo kutasaidia kuwakomboa wengine ambao walikuwa wamekata tama kutokana na matokeo mabaya pengine wanaweza bahatika kuwa na matokeo mazuri.

TAARIFA KWA UMMA

0
0
Kufuatia taarifa za uzushi zinazosemekana zilitokana na kikao cha wabunge wote wa CCM (CCM party caucus) zilizoenezwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari na haswa kwenye mtandao wa kijamii na watu wenye nia ovu ya kutaka kuharibu jina zuri la Mhe. Mbunge wa Jimbo la Nzega, Dkt. Hamisi Kigwangalla (Mb.) kwa kuchafua taswira yake na heshima kubwa aliyojijengea kwa muda mrefu kwenye jamii, tumeelekezwa kutoa taarifa hii yenye lengo la kukanusha na kuweka kumbukumbu sawia kwa lengo la kuuelewesha umma.

Kwanza, anasema Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla (Mb.), hana tabia za kuwagawa watu kwa matabaka ya itikadi zao, dini ama makabila yao. Anasema msingi huu wa kuishi kwa kushirikiana na kupendana anautoa nyumbani kwao Nzega alipozaliwa na kukulia, kwa babu yake aliyekuwa Sheikh na muasisi wa Taasisi ya kiislam ya Nusratul qadiriyya (zawia) ambayo ilikuwa na wafadhili wakuu wakristo na kila mwaka walikuwa wakishiriki kwa hali na mali kwenye maulid na dua nyingine mbalimbali; miongoni mwa walezi na wafadhili hao ni pamoja na Hayati Chief Humbi Ziota, Mhe. Lucas Lumambo Selelii (Mb. Mstaafu wa Nzega na Katibu wa Makanisa ya Pentekoste Mkoa wa Tabora), Mhe. Steven Maziku Kahumbi (Mb. Mstaafu wa Bukene), Hayati Mhe. Mzukila (Mb. Mstaafu wa Nzega) – ambao walikuwa ni wa dini ya kikristo. Ni msingi huo uliomfundisha yeye kuwa mstari wa mbele kwenye kuunga mkono jitihada za watu wa dini zote na hata wasio na dini katika shughuli zao za kuendeleza imani zao ama kufanya shughuli za maendeleo bila kuingilia uhuru ama itikadi zao. 

Ni katika msingi huo huo amekuwa akishiriki kujitolea kujenga makanisa, misikiti na hata kuchangia kazi za wasanii wa kwaya mbalimbali bila kubagua kwa misingi ya udini. Watu wa Nzega ni mashuhuda kwa hili. Na zaidi ya hapo, Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla (Mb.) hawezi kuwa wa mstari wa mbele kuhamasisha ubaguzi wa kidini, jambo ambalo kila siku analipinga hadharani, na kwamba yeye binafsi ana Ndugu wa damu wenye wazazi wa kikristo, na waliooa ama kuolewa na wenza wenye dini ya kikristo na kuzaa watoto na wajukuu wa dini ya kikristo. Na pia si muumini wa kutafuta umaarufu kunuka unaotokana na kuwagawa watu kwa hoja dhaifu na mfu kabisa za udini.

Pili, Mhe. Hawa Ghasia (Mb.) na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), HAKUWEPO KABISA kwenye kikao, hivyo  yote yanayosemwa na wazushi hawa ni ya uongo na hayana msingi wowote. Maana Mhe. Ghasia, asingeweza kumshambulia Mbunge Mwenziye ilhali hakuwepo kabisa kwenye mkutano huo.

Tatu, Mhe. Munde Tambwe Abdallah (Mb.), HAKUZUNGUMZA hata mara moja. Hivyo yote yanayosemwa dhidi yake ni uzushi na uongo wa kupindukia. Nne, Mhe. Bernard Membe (Mb.) na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ni rafiki yake mkubwa na wa karibu sana na kama ingetokea akasemwa kwa nia ya ubaya ama kumharibia sifa na yeye akiwemo kwenye kikao hicho, bila shaka yoyote ile angesimama kumtetea. Hivyo hili la Mhe. Membe kusemwa, halikuwepo na ni UONGO wenye nia ovu ya kuwagawa wanaCCM katika makundi “hasimu ya kulazimisha” ambayo hayapo.

Tano, anawataka watu wenye mradi wa kumchafua wakome mara moja maana mradi huu ni dhahiri kabisa haujawalipa mpaka sasa na kamwe hautowalipa. Kama ni vita za Urais ama Ubunge basi wasubiri 2015 watapambana. Taarifa hizo za kizushi zilizosambazwa na namna zilivyowekwa ni wazi kabisa zinalenga kumchafua Mhe. Bernard Membe (Mb.), ambaye ni rafiki yake wa karibu na anatajwa tajwa kuwa na uwezekano wa kuwania Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 2015, na kwa maana hiyo haihitaji akili ya Albert Einstein kubaini kuwa ni nani aliye kazini kwenye hili. 

Ametutaka tuwaambie hao watu kuwa yeye hayuko tayari kamwe kumuunga mkono mgombea wao, mwenye tuhuma za kifisadi, ambazo hazikwepeki na hazisafishiki, mwenye tamaa ya mali na madaraka isiyokoma na kwa kuwa yeye siyo mnafiki, analiweka wazi hili. Na kwamba kama ikitokea kweli Mhe. Bernard Membe (Mb.) akachukua fomu ya kuwania Urais yeye Mhe. Dkt. Kigwangalla atakuwa tayari kumuunga mkono na kumfanyia kampeni ya kufa na kupona kwa kuwa anaamini katika usafi na uzalendo wake, umakini wake na uwezo wake wa kazi. Na kwa kuwa anaamini kuwa kama Mhe. Membe atakuwa Rais, basi nchi itakuwa kwenye mustakabali mwema.

Anawasishi wanahabari kusimama kwenye weledi na kuacha kuandika mambo ambayo hawana uhakika nayo na bila hata ya kuwahoji wahusika.

Taarifa hii imetolewa leo Tarehe 24/Mei/2013 na;

TeamHamisiKigwangalla

Ofisi ya Mbunge,

Jimbo la Nzega.


Kupinga Kwangu Ubaguzi Kulinifanya Niandamwe Na Vikundi Vya Kibaguzi Ulaya

0
0


Ndugu zangu,

Kufuatia vurugu za vijana na polisi,  zinazoendelea kwenye viunga vya Stockholm, Sweden, juzi hapa nilisimulia ushiriki wangu kwenye Kamati ya Kitaifa ya watu 12  nchini Sweden iliyoandaa rasimu iliyopelekea kuundwa kwa kituo cha kwanza cha kitaifa dhidi ya ubaguzi nchini Sweden. 

Ilikuwa mwaka 2003. Kazi hiyo ilipelekea wajumbe wote 12 kuandamwa na vikundi vya kibaguzi si tu katika Sweden, bali Ulaya pia. Hata hivyo, hatukukata tamaa. tuliifanya kazi hiyo hadi mwisho. Hapa chini ni moja  ya taarifa za moja ya vikundi hivyo vya kibaguzi ambapo jina langu pia limeorodhoshwa...

Message 174
From: Antiracist Laponia
Subject: CETRUM MOT RASISM, CMR like a copy of fake antiracist league NMR (...like a kind

Rais Kikwete awasili Addis Ababa kuhudhuria sherehe za miaka 50 za umoja wa nchi za afrika (AU)

0
0
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bole jijini Addis Ababa alipowasili Ijumaa usiku  tayari kujiunga na viongozi wenzie wa nchi za Afrika katika sherehe za miaka 50  tangu kuanzishwa kwa Umoja  wa  nchi za Afrika (AU) zinazofanyika leo katika makao makuu ya umoja huo
Rais Kikwete, Mama Salma Kikwete wakiwasili Addis Ababa
Rais Kikwete na Mama Salma Kikwete wakipata maelezo ya maandalizi ya sherehe hizo toka kwa balozi wa Tanzania nchini Ethiopia, Profesa Joram Biswaro mara baada ya kuwasili Addis Ababa.PICHA NA IKULU.

=========  ======  ======
Rais Jakaya Mrisho Kikwete ni miongomi mwa marais wa bara la Afrika watakaohudhuria Sherehe za kuadhimisha miaka 50 tangu kuanzishwa kwa Umoja  wa  nchi za Afrika (AU) zinazo fanyika rasmi leo Jumamosi Mei 25, 2013 katika makao makuu ya Umoja huo jijini Addis Ababa, Ethiopia. 

 Shamrashamra zimetawala kila pembe ya jiji la Addis, wakati viongozi wa nchi za Afrika wakiwasili mmoja baada ya mwingine katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Bole. 

 Muungano wa Afrika wakati huo ukijulikana kama OAU, ulizaliwa Mnamo Mei 25, 1963 jijini Addis Ababa, ukianza na nchi za 32 na baadaye nchi 21 zikajiunga miaka ilivyozidi kwenda, huku Afrika ya kusini ikijiunga kuwa mwanachama wa 53 mwaka 1994. 

Mwaka 2001 OAU iligeuzwa kuwa AU katika mkutano uliofanyika Lusaka, Zambia. Jumamosi hii kutakuwa na sherehe za kilele kuadhimisha miaka hiyo 50 ya AU na kuhudhuriwa na marais karibia wote wa Afrika. 

 Kauli mbiu ya sherehe za hapo kesho ni mjadala mkuu kuhusu ushirikiano wa nchi za Afrika na kuimarishwa kwa muungano huo. Mwenyekiti wa tume ya muungano huo, Dr Nkosazana Dlamini Zuma, anaseme kuwa hii itakuwa fursa kwa AU kujadili kuhusu uwezo wa bara hili na ambacho kinaweza kufikiwa katika miaka 50 ijayo

KAA TAYARI,INAKUJA KIVINGINE..! NI MWANA FA-THE FINEST.

0
0

DADA SILVIA ANAFUTA MCHUMBA KUANZIA MIAKA 35-40

0
0
Habari kaka Michuzi, nimekuwa nikiona wenzangu wanafanikiwa kupata wachumba na hatimaye ndoa kupitia blogu yako. Naomba na mimi uniwekee tangazo langu ndugu yangu, naitwa Silvia natafuta mchumba mwanaume ambaye yupo makini, mpole, na aliye tayari kuanzisha familia. Asiwe malaya, asiwe na watoto, asiwe na mke wala ambaye hajawahi kuoa, awe mkristo na pia awe na elimu ya chuo kikuu. Umri wake kuanzia miaka 35 mpaka 40. 
Napatikana kwenye email address: 


Asante kaka Michuzi
Viewing all 46202 articles
Browse latest View live




Latest Images