Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 7 | 8 | (Page 9) | 10 | 11 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na wanachama wa UVCCM wa vyuo vikuu mkoani Tabora waliomtembelea Ikulu ndogo mkoani humo usiku wa kuamkia leo. Pamoja na mambo mengine Rais Kikwete aliwataka vijana hao kuzingatia masomo kwa nguvu zao zote, akisisitiza kwamba elimu ni ufunguo wa maisha hivyo wasome kwa bidii ili nchi ipate wasomi waliobobea katika kila nyanja katika kusukuma mbele gurudumu la maendeleo.PICHA NA IKULU.
   Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe, Fatma Abubakar Mwassa (mwenye kitenge, kati) na Mkuu wa Wilaya ya Tabora mjini Mhe Suleiman Kumchaya (kulia) wakipozi na viongozi wa wanafunzi wa UVCCM vyuoni
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipozi na viongozi wa UVCCM wa vyuoni Tabora
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wa jumuiya hiyo vyuoni Tabora
   Juu na chini Rais Jakaya Mrisho Kikwete na wana UVCCM vyuoni Tabora

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na makada hao wa UVCCCM

  0 0  Lady J Dee.  Dully Sykes.

  Bloggers
  Nawaletea muendelezo wa 147 Critics ambapo leo tutawasikiliza wadau na wanamuziki muhimu kwenye Tasnia ya Muziki  wa kizazi kipya Judith D.M Wambura a.k.a Lady Jay Dee (3) na Dully Sykes (4)  ufahamu wao kuhusiana na marekebisho  ya sheria ya ushuru wa bidhaa Sura 147
  yanayogusa Muziki na Filamu.

  Tuwasikilize hawa katika wakati tofauti Critics 147:Judith D.M Wambura a.k.a Lady Jay Dee (3) na 147 Critics:Dully Sykes
  (4) wakiwa ni watu wa tatu na nne kuelezea maoni yao kupitia link hizi:-


  Wasalaam.
  E.N.M.Manase
  Mdau -TFCA

  0 0   Lady JayDee, Justin Bayo(cameraman) and Gastor(guide) walking towards Mandara Hut
   Gadner,  na Lady Jaydee heading towards Mandara Hut

   A group photo at Mandara Hut with Kinapa Staffs.

  Progress:
  8th Jan - Mandara Hut(2700m) to Horombo Hut(3720m)
  Walking hours; 5hrs
  9th Jan - Acclimitization Day at Horombo Hut
  Walking hours; 4hrs
  10th Jan - Horombo Hut(3720m) - Kibo Hut(4703m)
  Walking hours; 5hrs
  Later in the day they will start heading towards Uhuru Peak(5895m) through Gillman's point(5685m)

  Health
  Gadner, Lady Jaydee and their cameraman Mr. Justin are in good shape, strong and able to continue till next destinations
   Lady Jaydee.Bofya Hapa kwa picha zaidi.

  0 0


  Pichani juu na chini mapema leo asubuhi ni namna Mlima Kibo ulivyokuwa ukionekana ndani mji Moshi mkoa wa Kilimanjaro.

  0 0


  Barabara za MAJENGO, mjini Moshi, ambazo inaelezwa kuwa wakati huo zilikuwa za kiwango cha lami,lakini kwa sasa lami yote imekwisha,zimekuwa kama za vumbi,lakini pamoja na kuwa ni za vumbi lakini ziko swafi kabisa na zinang'aa kwa kufanyiwa usafi .

  0 0


   Eneo la kituo cha Gari Moshi a.k.a Treni (Stesheni) mjini Moshi mkoani kilimanjaro likiwa limedorola na kusahaulika kabisa kutokana na kusitishwa kwa huduma ya usafiri wa treni mkoani humo.

  0 0


  Lakeland Africa will launch its first weekend tours on the 26th January 2013 by starting a two days tour to Mikumi National Park that will leave Dar es Salaam on 26th January and return in the evening on Sunday 27th this year.
  Thereafter, the weekend trips will be scheduled on every Saturday and include more than six destinations.

  Here are the weekend tour destinations: Mikumi National Park, Selous Game Reserve, Pangani, Kilwa, Saadan National Park, Lushoto and Bagamoyo.
  The company uses overland trucks that can carry up to 24 tourists and it have experienced drivers, chefs and tour leaders.

  All accommodations are by camping within the National Parks as well as within cities visited. Meals are prepared by chef on board.
  Come see Tanzania at a reasonable price. Enjoy wildlife, culture and history from those who know it.

  ‘Always travel local to learn the world’
  For more details contact

  0 0

  Pichani ni sehemu ya mikoba ya akina dada iliyotengenezwa kwa vitambaa mbalimbali huku ikiwa imewekwa nakshi mbalimbali za rangi ili kuupendezesha zaidi

  0 0
 • 01/10/13--02:22: hakuna kazi rahisi
 • Baadhi ya Waendesha Bodaboda wa Maeneo ya Rau, Moshi mjini wakisubiri abiria.

  0 0
 • 01/10/13--04:27: kazi ni kazi tuu..!

 • Kijana ambaye jina lake halikupatikana mara moja, akiwa katika kuchambua na kuanika mtama ambao pia ni maarufu kwa kutengenezea pombe za kienyeji a.k.a asili ikiwemo Mbege na Kimpumu,picha hii imenaswa na mpiga picha maalum wa JIACHIE BLOG aliyeko mjini Moshi,mkoani Kilimanjaro mapema leo.

  0 0
 • 01/10/13--05:35: raha ya mkulima.

 • wafanyabiashara wa Matunda aina ya Embe, wakizunguka na Gari hili pichani huku wakitangaza biashara yao ya Maembe kwa wateja wao,mapema leo Moshi Mjini (Rau) .Picha imepigwa na Mpiga Picha Maalum wa JIACHIE BLOG aliyeko Mkoani Kilimanjaro.

  0 0

   Diwani Omary Kariati wa Kata ya Kwadelo, Kondoa mkoani Dodoma, akizungumza na wananchi wa Kata hiyo, baada ya kuwashili katika kata hiyo jana kuzindua Kampeni ya Kilimokwanza kwa Vijana wa Kata hiyo. Kutokana na juhudi za diwani huyo hivi sasa kata hiyo inayo matrekta 60 yanayotumika kwa kilimo cha mazao mbalimbali yakiwemo ya alizeti na ufuta.
   Wasanii wa filamu, kutoka kushoto; Jacob Steven 'J B',  Vicent Kigosi 'Ray', Irene Uwoya, Wema Sepetu na Single Mtambalike 'Rick Rich' walipowasili Kwadelo kwa ajili ya kushiri uzinduzi huo wa kampeni ya Kilimo Kwanza kwa vijana wa Kata hiyo.
   Wazee wa Kwadelo wakati wakimsubiri kuwasili kwa diwani wao pamoja wasanii hao
   Baadhi ya kinamama wa Kwadelo waliohudhuria hafla hiyo
   Ray akipozi picha na wazee wa Kwadelo
   Kariati akiwa na wasanii hao kwenye trekta kabla ya uzinduzi wa kampeni hiyo
   Wema Sepetu akiungurumisha trekta ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa kampeni hiyo. Wapili Kulia ni Omary Kariati
   Uwoya naye akilijaribu trekta kwenye uzindzi huo
  KWADELO HOYEEEEEE! J B akihamasisha wakati wakiwa kwenye trekta la kilimo wakati wa uzinduzi huo
   Treka likionyesha mfano wa ulimaji wa kisasa kwenye shamba la shule ya sekondari ya Kwadelo wakati wa uzinduzi huo
   KITUKO: Panzi! Panzi! Panzi!, Wema Sepetu (shati ya kijani) akifunika uso wake kwa kipochi chake, huku akipiga kelele na kujiingiza katika kundi la wazee,  kwa sababu ya kuogopa panzi aliyemdandia wakati wa shughuli za uzinduzi huo shambani
   J B na Wema wakila mapozi shambani wakati wakienda sehemu ya uzinduzi
   Wema akitangaza kuzindua kampeni hiyo
   BAADAYE: Wasanii hao wakimkabidhi sh. 500,000 mmoja wa wananchi wa Kwadelo walioathirika na mafuriko. Kwa mujibu wa Diwani Kariati (wapili kushoto), fedha hizo zimetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Meembe ambaye ni mzee wa heshima wa kata hiyo.
   Diwani Kariati akikagua maeneo yaliyoathiriwa na mafuriko katika moja ya vijiji vya Kata ya Kwadelo, kufuatia mvua zoinazoendelea katika maeneo mbalimbali nchini
   Kariati akionyeshwa maeneo yaliyoathirika
  Wazee wakiomba dua ya kheri baada ya shuguli za uzinduzi wa Kampeni ya kilimo kwanza na kukagua maeneo ya walioathiriwa na mafuriko: Picha zote na Bashir Nkoromo wa Daily Nkoromo Blog

  0 0


  Meneja Mahusiano wa Multichoice Tanzania Barbara Kambogi (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya Mkurugenzi wa MultiChoice Africa kwa ukanda wa Afrika Mashariki Stephen Isaboke ambapo amesema Wateja wa huduma za Dstv nchini Tanzania wametakiwa kutokuwa na hofu ya kupata muingiliano au kukatika kwa picha katika kipindi hichi cha kutoka analogia kwenda digitali.

  Barbara Kambogi amesema watanzania ambao wamejiunga na Dstv hawatahitaji kuhama kwa kuwa Dstv iko katika mfumo wa digital tangu awali. Ameoneza kuwa Dstv imekuwa ikitoa huduma za digital televisheni kwa Tanzania kwa kipindi cha miaka 17 iliyopita, ambapo wateja wake wameweza kupata channel nyingi zaidi za kuchagua zikiwa na picha safi na sauti bora.

  Kupitia vifurushi tofauti vinavyotolewa na Dstv wateja wanakuwa na maamuzi ya kuchagua kifurushi anachotaka na bei ambapo Ofa ya msimu wa Sikukuu za Krismas inaendelea pamoja na punguzo la asilimia 10 la kufanya malipo kabla ya muda uliolipia huduma kumalizika. Kulia ni Operation Manager wa Multichoice Tanzania Bw. Ronald Baraka Shelukindo.

  Operation Manager wa Multichoice Tanzania Ronald Baraka Shelukindo akifafanua jambo kuhusu Televisheni nyingine kuingizwa katika huduma za DStv na kusema suala hilo litategemeana na makubaliano na mikataba na wamiliki pamoja na kutegemea uwezo wa Satelite. Kwa Tanzania DStv inamkataba na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) la kuichukua TBC katika DStv Platform ambapo itakuwa inaonekana bure hata kama hujalipia king'amuzi chako chaneli hiyo haikatwi. Bw. Shelukindo amewataka Watanzania kuendelea kununua ving'amuzi vya DStv kabla ya kuisha kwa Ofa ya msimu wa Sikukuu za Krismas na Mwaka mpya.

  0 0

    Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini Mhe Radhia Msuya mara baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa Kimataikfa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea mkoani Tabora alikokuwa katika ziara ya kikazi ya siku tano kukagua shughuli za maendeleo na kuzindua miradi mbalimbali.PICHA NA IKULU
    Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuli (kulia)  na Waziri wa  Uchukuzi Dkt Harrison Mwakyembe wakiongea wakati wa sherehe za uzinduzi wa ujenzi wa uwanja wa ndege wa
  Tabora leo Januari 10, 2013
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete (yumo garini kushoto) akikagua sehemu ya kutua na kupaa ndege ya uwanja wa Tabora leo Januari 10, 2013 mara baada ya kuzindua rasmi ujenzi wake.

  ==============  ===========  ========  0 0

  Naibu Waziri wa TAMISEMI Mhe. Agrey Mwanri akipima kwa tape maalum urefu wa moja ya barabara zilizojengwa na Manispaa ya Sumbawanga katika Mji huo kuhakikisha kama barabara hiyo imejengwa kwa vipimo vilivyoanishwa kwenye mpango wa ujenzi huo (BOQ). Naibu Waziri huyo alitumia fursa hiyo kuziasa halmashauri zote nchini kusimamia vyema fedha za Serikali katika miradi kuhakikisha inafanana na thamani ya fedha zilizotumika, alilazimika kusema hayo baada ya kubaini mapungufu mbalimbali katika mradi huo wa barabara na miradi mingine aliyofanikiwa kuitembelea Mkoani Rukwa.
  Naibu Waziri wa TAMISEMI Mhe. Agrey Mwanri akikagua barabara za lami zilizo chini ya Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga zilizojengwa hivi karibuni. Katika ukaguzi huo alibaini mapungufu mbalimbali katika ujenzi huo na kuagiza Halmashauri hiyo kuhakikisha mapungufu hayo yanaondolewa. Aliitaka pia halmshauri hiyo kusimamia vyema kazi za Serikali kuepusha minong'ono inayotoka kwa wananchi juu ya utendaji mbovu wa baadhi ya watendaji Serikalini.
  Mhe. Agrey Mwanri akiweka jiwe la msingi kiwanda cha unga cha Malangali kinachomilikiwa na muwekezaji wa ndani mapema hivi leo. Kwa sasa Mkoa wa Rukwa una viwanda vitatu vya unga vinavyomiliwa na wawekezaji wa ndani. 
  Naibu wa Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Agrey Mwanri akikagua kiwanda cha unga cha Malangali Mjini Sumbawanga leo alipotembelea kiwandani hapo kwa ajili ya kuweka jiwe la msingi.

  Mhe. Mwanri akizungumza na wakazi wa Mji wa Sumbawanga katika Stendi kuu ya mabasi ya Mjini hapo ambapo alipokea kero mbalimbali ikiwepo ubovu wa miundombinu ya umeme na barabara katika stendi hiyo. Aliuagiza uongozi wa Manispaa ya Sumbawanga kufanya Mkutano wa hadhara na wananchi hao kuskiliza kero zao zote pamoja na kuzitaftia ufumbuzi na kumpelekea taarifa ya utekelezaji.
  Katika hali isiyotegemewa msafara wa Mhe. Mwanri ulipowasili katika kijiji cha Mlanda katika Manispaa ya Sumbawanga kwa ajili ya Mkutano wa hadhara ulikuta msiba ambapo walishiriki na kutoa ubani ambapo Mhe. Mwanri alitoa laki moja na alfu mbili na aliyekuwa Mbunge wa Sumbawanga Mjini CCM ambaye pia ni Mjumbe wa halmashauri kuu Taifa ya CCM (NEC) kupitia Mkoa wa Rukwa Aeshi Hillal alikabidhi shilingi alfu hamsini.  (Picha na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa - rukwareview.blogspot.com)

  0 0

   Naibu Waziri wa Ardhi,Makazi,Maji na Nishati Haji Mwadini Makame akimkabidhi zawadi mshindi wa kwanza katika mshindano hayo Nahodha Fundi Abuubakar kutoka Bumbwini.Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar. PICHA NA MAKAME MSHENGA-MAELEZO ZANZIBAR.
   Ngarawa mbili za mbele zikichuana vikali katika mashindano yalio fanyika huko forodha mchanga ikiwa ni shamra shamra za miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar.Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
   Ngarawa zikianza mashindano mara tu ilipopulizwa firimbi ya kuanza mashindano hayo huko forodha mchanga ikiwa ni shamra shamra za miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar.Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar. 
   Naibu Waziri wa Ardhi,Makazi,Maji na Nishati Haji Mwadini Makame akipuliza filimbi kuonyesha ishara ya kuanza kwa mashindano hayo.Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
   Wananchi wakishangiria jinsi mpambano ulivyokuwa mkali huko forodha mchanga ikiwa ni shamra shamra za miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar.Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

  Ngarawa zikianza mashindano mara tu ilipopulizwa firimbi ya kuanza mashindano hayo huko forodha mchanga ikiwa ni shamra shamra za miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar.Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

  0 0
 • 01/10/13--21:30: Viwanja vinauzwa
 • Viwanja vinauzwa,vimepimwa na vina hati,vipo eneo la Viwanda Mwanambaya Mkuranga barabarani na vimezingatia hifadhi ya barabara,vimepakana na kiwanda cha Cement,kiwanda cha Gypsum na Yad ya Scania used,Heka 4 bei yake ni sh mil.700,zipo heka 28 nyuma ya hicho mil 700,zipo heka 4 zinapakana na ukuta wa kiwanda cha Cement Mil.600.

  Zipo heka 6 hazijapimwa zipo barabarani  eneo hilo hilo mil 500. Mwandenga  zipo heka 67 Mil. 700,Zipo nyumba eneo la Gerezani  kariakoo Mil. 700 kwa Mil.900,Round about ya Kariakoo bilioni 1 na 200 milioni.Kariakoo stendi ya Kawe ni bilioni 1 na 200 mil. Ipo beach gezaulole Kigamboni Mil.600,pia vipo viwannja vya Mil.10 na vilivyopimwa kwa mil 25 Gezaulole-Kigamboni.

  Kwa mawasiliano piga namba 0652020343 

  0 0
 • 01/10/13--21:35: EXIM BANK VISITS TSN OFFICES
 • The Tanzania Standards (Newspapers) (TSN) Acting Managing Editor, Mr Gabriel Nderumaki (3rd right) introducing the TSN’s Human Resources Manager Ms. Amina Lumuli to the Exim Bank Tanzania Managing Director Mr. Anthony Grant (1st left), during the bank’s visit to the TSN’s Office yesterday in Dar es Salaam. Looking on, are TSN’s Manager of Standard Printers Mr. John Mcharo (1st right) and Exim Bank Customer Service Manager Frank Matoro (2nd left).
  The Tanzania Standards (Newspapers) (TSN) Manager of Standard Printers Mr. John Mcharo (2nd left) elaborates a point to the Exim Bank Tanzania Managing Director Mr. Anthony Grant (3rd right) on the newspapers’ printing procedures, during the bank’s visit to the TSN’s Office yesterday in Dar es Salaam. Looking on are TSN’s Acting Managing Editor, Mr Gabriel Nderumaki (1st left), Exim Bank Customer Service Manager Frank Matoro (1st right), Exim Bank Marketing Executive Mr Oscar Ruhasha (2nd right)
  he Tanzania Standards (Newspapers) (TSN) Manager of Standard Printers Mr. John Mcharo (1st left) elaborates a point to the Exim Bank Tanzania Managing Director Mr. Anthony Grant (2nd left) on the printing procedures of the newspapers, during the bank’s visit to the TSN’s Office yesterday in Dar es Salaam. Listening are TSN’s Acting Managing Editor, Mr Gabriel Nderumaki (center), Exim Bank Customer Service Manager Frank Matoro (3rd right), Exim Bank Corporate Manager Institutional Relations Mr Kinemo Kihomano (1st right).
  The Tanzania Standards (Newspapers) (TSN) Acting Managing Editor, Mr Gabriel Nderumaki (2nd right) elaborates a point to the Exim Bank Tanzania Managing Director Mr. Anthony Grant (2nd left) on the newspapers’ printing procedures, during the bank’s visit to the TSN’s Office yesterday in Dar es Salaam. Listening are, TSN’s Manager of Standard Printers Mr. John Mcharo (1st left), Exim Bank Customer Service Manager Frank Matoro (3rd left),Exim Bank Marketing Executive Fatma Kilinda(4th left) and Exim Bank Marketing Executive Mr Oscar Ruhasha (1st right).

  0 0


  Mayor of Ilala Municipal Council who also is The Councilor for the Gongo La Mboto Ward His worship Jerry Silaa visited various projects in his ward amongst them being in mtaa wa Gulukakwalala whereby he visited a dispensary which he built between 2005-2010 and he personally pledged to get it equipped with various instruments to measure diabetes, blood pressure and a portable ultrasound machine.

  0 0

  Mchungaji Daniel na Hoyce Mbowe, wanapenda kuwakaribisha wote wanaoongea Kiswahili hapa Ujerumani na marafiki wengine katika ibada ya pili ya Kiswahili itakayofanyika Jumapili hii tarehe 13.01.2013 .
  Muda wa Ibada: Saa saba mchana (13:00 hours) hadi saa tisa mchana ( 15:00 hours).

  Mahali: Evangelischen Friedenskirchengemeinde Bonn
  Anuani: Franz-Bücheler-Straße 10
  53129 Bonn.

  Ibada hii ya Kiswahili itakuwa ikifanyika kila Jumapili ya pili ya kila mwezi, ibada ya Kwanza ilifanyika tarehe 9 mwezi uliopita na kuhudhuriwa na watu wengi.
  Mawasiliano: dmbowe@hotmail.com or hoycembowe@hotmail.com
  Wote mnakaribishwa: Karibuni tumwabudu na tumsifu Mungu wetu.
  Maelezo ya Picha
  Picha ya kwanza : Baadhi ya waimbaji wa Kwaya ya Ambassador of Christ wakiimba katika ibada ya kwanza mwezi uliopita.

  Picha ya pili: Baadhi ya waumini waliohudhuria ibada ya kwanza wakibadilishana mawazo.

older | 1 | .... | 7 | 8 | (Page 9) | 10 | 11 | .... | 1897 | newer