Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live

Makala ya Sauti, kwa Kiswahili rahisi kabisa UK kujitoa EU - chanzo, kura ya maoni na athari kwa dunia na Afrika

$
0
0



KONGAMANO LA KUBADILISHANA UZOEFU WA MAFUNZO YA TAALUMA UFARANSA NA TANZANIA LAFANYIKA DAR

$
0
0
KONGAMANO kubwa la aina yake limefanyika mjini Dar es salaam ambapo washiriki walizungumzia namna ya kuendeleza rasilimali watu katika eneo la utaalamu na taaluma katika shughuli mbalimbali za uendelezaji wa makampuni na viwanda.

Kongamano hilo ambalo lilihudhuria na watu wenye kariba kubwa katika masuala ya viwanda na biashara akiwemo Dkt. Reginald Mengi ambaye ni Mwenyekiti wa makampuni ya IPP na Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF);na Balozi wa Ufaransa nchini Malika Berak liliangalia uhaba wa wataalamu na namna ya kuuondoa uhaba huo wakati taifa linaelekea katika uchumi wa kati unaotegemea viwanda.

Wengine waliokuwepo katika kongamano hilo Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Tonia Kandiero na maofisa wa serikali.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida akikaribisha washiriki na wadau wengine alisema kwamba mafunzo hayo yaliyoratibiwa kwa pamoja katika wataalamu wa Ufaransa, ESRF na Benki ya Maendeleo ya Afrika yamelenga kudadavua tatizo lililopo na kulipatia ufumbuzi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida (katikati) akisalimiana na mgeni rasmi Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), Dk. Reginald Mengi (kulia) alipowasili katika ofisi za ESRF jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Balozi wa Ufaransa nchini, Mh. Malika Berak.(Picha na Modewjiblog)

Taasisi ya utoaji mafunzo ya Ufaransa ya AFPA ndiyo ilikuwa inaendesha mafunzo hayo wakibadilishana uzoefu na wadau wa Tanzania kutoka sekta binafsi.

Akifafanua zaidi Dkt. Kida alisema kwamba kongamano hilo limelenga zaidi katika kubadilishana uzoefu kuhusu changamoto zinazojitokeza na fursa zilizopo katika mafunzo, ukuzaji na uendelezaji taaluma.

Dkt. Kida alifurahishwa na mchanganyiko wa watu kutoka sekta binafsi waliofika katika kongamano hilo ambao aliamini kwamba wataelezea uzoefu wao katika kukabiliana na changamoto za taaluma katika makampuni yao.

Aidha alisema kwamba wadau hao wa Tanzania watapata uzoefu wa timu ya wataalamu wanne kutoka kwa wakala wa mafunzo ya taaluma nchini Ufaransa (AFPA) ambao wataeleza miaka 60 ya uzoefu katika masuala ya mafunzo ya taaluma na uendelezaji wa utaalamu.

Balozi wa Ufaransa nchini, Mh. Malika Berak (kushoto) akibadilishana mawazo na mgeni rasmi Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), Dk. Reginald Mengi (kulia) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida katika ofisi za ESRF jijini Dar es Salaam.

Alisema anaamini kwamba mchanganyiko huo wa wadau utasaidia katika kukabiliana na tatizo la taaluma katika soko la ajira la Tanzania.

Alisema mazungumzo hayo ni muhimu sana katika kuibua fursa hasa wakati taifa hili linajipanga kuelekea katika uchumi wa kati wa viwanda na bila wataalamu wenye taaluma zao makamapuni na viwanda vingi vitakuwa na shida kubwa.

Alisema changamoto kubwa inayokabili taifa la Tanzania kuelekea nchi ya viwanda kama ilivyo katika nchi nyingine zinazoendelea ni ukosefu wa taaluma na utaalamu.

“Ukosefu wa wafanyakazi wenye taaluma katika ngazi zote ni tatizo kubwa linalokabili harakati za kuelekea uchumi wa viwanda” alisema Dkt. Kida.

Anasema pamoja na matatizo hayo taasisi yake tayari imeshaanza kushughulikia shida hiyo ya taaluma nchini Tanzania kwa kuwa na makongamano mbalimbali makubwa yanayokutanisha wadau kuzungumzia hali hiyo.
Balozi wa Ufaransa nchini, Mh. Malika Berak (kulia) akisalimiana na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Tonia Kandiero (kushoto) alipowasili ofisini kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida (katikati) kabla ya kuelekea kwenye ukumbi wa mikutano.

Alisema kwa mfano mwaka 2015 iliendesha jukwaa la mafunzo ya ufundi (VTEC) Africa. Katika jukwaa hilo lililofanyika Machi 10 -12 mwaka huo walizungumzia mafunzo ya utaalamu wa gesi na mafuta kwa mataifa ya Afrika. Jukwaa hilo liliendeshwa kwa kushirikiana na kampuni ya Uingereza ya Getenergy.

Aidha Oktoba 9, 2015 iliendesha semina kuhusu uumbaji wa programu za mafunzo kwa aili ya kupata wataalamu wa gesi na mafuta.

Lakini, alisema, kuanzia Julai 2014, ESRF imekuwa ikishirikiana na shirika la Maendeleo la Marekani (USAID) kutekeleza mpango wa miaka mitano wa mafunzo ya kinadharia na utaalamu yenye mfumo wa Ushiriki ambapo ESRF yenyewe hutoa msaada wa kitawala na lojistiki kwa wanafunzi ili waweze kwenda kuhudhuria mafunzo nje ya nchi.

Aidha ESRF imekuwa ikifanya tafiti mbalimbali na uchambuzi kuhusiana na uendelezaji wa taaluma nchini Tanzania na moja ya ya tafiti hiyo ni kudorora kwa ubora wa elimu Tanzania na namna ya kuzuia anguko hilo na kulibadili.

Mwaka 2014 na mwaka huu kuna mada inayozungumzia uendelezaji wa mafunzo ya taaluma na uwezo wa uzalishaji Tanzania.Mada hii ni sehemu ya taarifa ambazo zitapatikaa katika ripoti ya Maendeleo ya Binadamu ya mwaka 2017.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida (kulia) akiongozana na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Tonia Kandiero kuelekea kwenye ukumbi wa mikutano wa ESRF. Nyuma ni Balozi wa Ufaransa nchini, Mh. Malika Berak akibadilishana mawazo na mgeni rasmi Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), Dk. Reginald Mengi pamoja na Mkurugenzi wa Ajira Ofisi ya Waziri Mkuu, Ally Msaki.

Naye Balozi wa Ufaransa nchini, Mh. Malika Berack amesema kwamba kuwapo kwa taasisi hiyo ya Ufaransa kushea elimu na watanzania kutasaidia kuinua na kuboresha fursa za maendeleo hasa rasilimali watu katika utaalamu.

Alisema AFPA yenye uwezo wa miaka mingi katika kuendesha mafunzo ana tumaini itasaidia kuamsha ushindani na kuziba mapengo ya wafanyakazi wataalamu katika nafasi mbalimbali.

Aidha alitoa wito wa kuwapo kwa sera ambapo Tanzania na Ufaransa zitashirikiana kuhakikisha kwamba kunakuwapo na mwendelezo katika suala la utaalamu na taaluma kwani hiyo ndiyo inayoweza kusaidia kusukuma mbele maendeleo ya viwanda.

Alisema AFPA yenye wataalamu zaidi ya elfu 80 wakiwa wamebobea katika uandazi wa watu wanaotafuta kazi, kufundisha utaalamu na pia kuwezesha ushindani katika masuala ya biashara wataweza kusaidia watanzania kudadavua matatizo yao na kujiweka mbele katika kufanya mabadiliko ya kiuchumi na kitamaduni ili kusonga mbele.

Naye Dkt. Reginald Mengi ambaye ni Mwenyekiti wa makampuni ya IPP na Mwenyekiti wa TPSF alisema kwamba mafunzo hayo yamekuja wakati muafaka ambapo serikali imetoa mpango wake wa maendeleo wa miaka mitano ambao utekelezaji wake unategemea sana utaalamu na taaluma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida akitoa neno la ukaribisho kwa washiriki na wadau wengine katika kongamano hilo.

Alisema kwamba wakati serikali inajipanga taifa kuwa na uchumi wa kati mwaka 2025 taifa linatakiwa kujipanga katika kutengeneza rasilimali watu wenye taaluma ambao wanaweza kulifikisha taifa katika eneo hilo.

Alisema kwamba katika hali hiyo inafaa kuendelea kuratibu na kutengeneza mitaala inayofaa kwa ajili ya kuendeleza watu na hivyo kuendeleza taaluma kwa kushirikiana na sekta binafsi.

Inafaa, alisema Dk Mengi, utengenezaji wa watu wenye taaluma lazima uende sambamba na haja ya taifa katika mipango yake ya maendeleo kwa kutoa wataalamu walio bora ambao watatengeneza bidhaa bora na huduma bora zitakazoinua uchumi wa mtu mmoja na taifa.

Alisema ipo haja ya kuwapo kwa ushirikiano wa sekta binafsi na serikali katika kuhakikisha mazingira yanawezesha uzalishaji zaidi wa wataalamu ambao watakuwa na uhakika na ubunifu wa kuendeleza teknolojia na kuzitumia kwa ajili ya maendeleo.

Alisema awali uchumi ulitengenezwa kwa kuzingatia ujamaa ambapo serikali ilikuwa inafanyabiashara na kuzalisha lakini baada ya mabadiliko inatakiwa vile vile kubadilika ili kuweza kukidhi mahitaji ya sasa ambayo ni ya soko huria.
Balozi wa Ufaransa nchini, Mh. Malika Berak akizungumza kwenye kongamano hilo.

Aliwataka watanzania kubadilika katika fikira zao na kuona namna ya kuwezesha maendeleo ya rasilimali watu kwa kuzingatia mahitaji ya sasa ambayo yanahitaji utaalamu wa sasa hasa katika sekta binafsi.

Alisema ni lazima watu pia katika taaluma lazima kuwepo na uwajibikaji, uadilifu na uwezo katika kufanikisha maendeleo ya taaluma.

Akitolea mfano wa mtu aliye mlemavu nchini Japan alitaka watanzania watumie kile kilichopo tunachoweza ili kutengeneza maisha bora kabisa.

Alisema mlemavu huyo wa Japan ambaye alikuwa amepooza kuanzia shingoni ambaye kwa sasa ni milionea alimwambia kwamba alikuwa halilii ambavyo hana bali kile alichonacho alihakikisha anakitumia vyema.
Mgeni rasmi Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), Dk. Reginald Mengi akifungua kongamano hilo lililofanyika kwenye ukumbi wa mikutano ofisi za ESRF jijini Dar es Salaam.

Naye Katibu Mkuu Ofisi ya waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi na Ajira, Eric Shitindi katika hotuba yake iliyosomwa na Mkurugenzi wa Ajira Ofisi ya Waziri Mkuu, Ally Msaki alisema ipo haja ya wadau wote kuwa pamoja katika kuhakikisha elimu inaboreshwa na pia wataalamu wanasukwa kwa kuzingatia soko la ajira.

Alisema serikali kwa kushirikiana na sekta binafsi imechukua hatua kadha kuongeza utaalamu katika soko la ajira kwa kuanzisha mpango wa miaka mitano ambamo ndani yake yamezungumzwa masuala ya mafunzo ya ufundi na utaalamu .

Alisema hakuna maendeleo yanayokusudiwa bila kuwa na wataalamu na hivyo serikali itaendelea kushirikiana na wadua mbalimbali kuendeleza mafunzo kwa lengo la kusaidia soko la ajira.

Alisema bila kuwa na ushirikiano kati ya serikali, sekta binafsi na waajiri hapatakuwapo na wataalamu na hivyo itakuwa shida katika maendeleo ya taifa.
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Celestine Mushy (wa pili kushoto) na washiriki wengine wakifuatilia kwa umakini risala ya mgeni rasmi, Dk. Mengi.

Mkurugenzi wa Ajira Ofisi ya Waziri Mkuu, Ally Msaki akisoma hotuba kwa niaba ya Katibu Mkuu Ofisi ya waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi na Ajira, Eric Shitindi katika kongamano hilo.
Pichani juu na chini ni sehemu ya washiriki kutoka sekta binafsi, serikalini pamoja na taasisi mbalimbali walioshiriki kwenye kongamano hilo.




Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Dkt. Tonia Kandiero akichangia maoni kwenye kongamano hilo.
Mgeni rasmi Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), Dk. Reginald Mengi (kulia), akibadilishana mawazo na Balozi wa Ufaransa nchini, Mh. Malika Berak (wa pili kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida (kushoto) pamoja na kurugenzi wa Ajira Ofisi ya Waziri Mkuu, Ally Msaki wakati wakielekea kwenye eneo maalum kwa ajili ya zoezi la picha ya pamoja.
Mgeni rasmi Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), Dk. Reginald Mengi katika picha ya pamoja na wakala wa mafunzo ya taaluma nchini Ufaransa (AFPA) na wadau waliowezesha kongamano hilo kufanyika.
Mgeni rasmi Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), Dk. Reginald Mengi katika picha ya pamoja na sehemu ya washiriki wa kongamano hilo.
Mgeni rasmi Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), Dk. Reginald Mengi (kushoto) akifurahi jambo na Balozi wa Ufaransa nchini, Mh. Malika Berak (wa pili kulia), Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida (kulia), Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Celestine Mushy (katikati) pamoja na Prof. Prosper Ngowi kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe kampasi ya Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida (kulia) akiagana na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Dkt. Tonia Kandiero mara baada ya kumalika kwa kongamano hilo.

RC MAKALA AAGIZA KUKAMATWA KWA MKANDARASI WA UJENZI WA UWANJA WA NDEGE WA SONGWE BAADA YA KUSHINDWA KULIPA MAFAO YA VIBARUA ZAIDI YA 50.

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla,akitolea ufafanuzi na kujibu kero mbalimbali zilizotolewa na wananchi wa Mkoa wa Mbeya, katika kikao maalum cha kupokea kero za wananchi kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Mkapa, ambapo kubwa zaidi katika siku hii, Makala amesema serikali itahakikisha inamkamata mkandarasi wa ujenzi wa uwanja wa ndege wa Songwe kutoka kampuni ya Kundan Sigh, baada ya kushindwa kulipa mafao ya vibarua zaidi ya 50. 

Na Emanuel Madafa, Mbeya.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla ameagiza kukamatwa kwa mmiliki wa kampuni ya Kundan Singh, ambaye alipewa tenda ya kujenga uwanja wa ndege wa Songwe, baada ya kushindwa kulipa mafao ya vibarua zaidi ya 50.

Mkuu huyo wa Mkoa wa Mbeya ametoa kauli hiyo , wakati akijibu na kutatua kero mbalimbali za wananchi ambazo hazijapatiwa ufumbuzi kwa kipindi kirefu, hali iliyochangia wananchi kuichukia serikali kwa madai ya kushindwa kuwatendea haki.

Awali, akitoa malalamiko hayo kwa Mkuu wa Mkoa, Joshua Mwasilonde kwa niaba ya vibarua wenzake, amesema wamekuwa wakidai mafao yao tangu mwaka 2012/2013 katika mfuko wa hifadhi ya jamii NSSF na kwamba kila wanapofuatilia wamekuwa wakipigwa kalenda.

Akilizungumzia hilo, Makala amesema, kwakua serikali iliingia mkataba na kampuni hiyo na kumalizana nayo bila ya kuacha deni lolote hivyo mkandarasi huyo anapaswa kuwalipa vibarua hao na kuutaka uongozi wa NSSF, kuhakikisha unavishirikisha vyombo vya dola katika kumkamata mkandarasi huyo.

Meneja NSSF Kanda ya Nyanda za Juu kusini, Robert Kadege, akilitolea ufafanuzi suala hilo, amesema suala la vibarua hao linafanyiwa kazi na kwamba tayari mahakama imetoa hukumu na kuupa ushindi mfuko huo.

WABUNGE WAWILI WA CHADEMA WASIMAMISHWA KUHUDHURIA VIKAO VYA BUNGE KUANZIA LEO

$
0
0
Mbunge wa Ubungo Chadema Saed Kubenea amesimamishwa kuhudhuria vikao vitano vya bunge na Naibu Spika Dk Tulia Akson baada ya kubainika kusema uongo kwamba Waziri wa Ulinzi na JKT Dk Hussein Mwinyi ameingia Mkataba na kampuni ya China Henan International Cooperation Group Company wa ujenzi wa nyumba za JWTZ na nyumba ya Waziri huyo jambo ambalo sio kweli.
Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi amesimamishwa kuhudhuria vikao kumi vya bunge kuanzia leo June 30 mwaka huu baada ya kubainika kunyosha kidole cha kati kwa wabunge baada ya kukiri mbele ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka kwamba alifanya kitendo hicho. Hata baada ya kuhojiwa Mbunge Mbilinyi alishindwa kumtaja Mbunge wa CCM aliyedaiwa kumtukana ili nae achukuliwe hatua na kamati hiyo. Bunge limeridhia adhabu hiyo iliyotolewa na kamati.

SERIKALI YATANGAZA KIAMA CHA WAUZA DAWA NA VIPODOZI HATARI MITANDAONI.

$
0
0


Na Fatma Salum (MAELEZO).

Serikali kupitia Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) imesema hivi karibuni itaanza msako mkali wa kuwatafuta na kuwakamata wauzaji wa dawa zinazokatazwa pamoja na vipodozi vikali ambao wanajitangaza kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii.

Hayo yamesemwa na Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Umma kutoka TFDA Bi. Gaudensia Simwanza wakati wa mahojiano na mwandishi wa habari hii kuhusu kuibuka kwa watu wanaotangaza  biashara ya dawa na vipodozi ambavyo Serikali imevipiga marufuku. 

Akitaja bidhaa hizo Bi. Simwanza alisema ni pamoja na dawa za kuongeza ukubwa wa viungo vya mwili, kupunguza uzito wa mwili na vipodozi vyenye kemikali za kuchubua ngozi bidhaa ambazo zinasababisha madhara makubwa kwa binadamu ikiwemo ugonjwa wa Saratani.

“Kumezuka wafanyabiashara holela wanaotumia mitandao ya kijamii kama vile Instagram, Facebook, Whatsup Groups na kwengineko  kutangaza biashara ya dawa na vipodozi vyenye kemikali hatari ambavyo vimepigwa marufuku na TFDA hivyo wanaohusika wajiandae, hivi karibuni tutaanza kuwashughulikia.” Alisema Simwanza. 

Alibainisha kuwa bidhaa hizo nyingi hazijathibitishwa na kupewa kibali na TFDA hivyo wauzaji wanakiuka Sheria ya Chakula, Dawa na Vipodozi Sura ya 219 inayowataka wafanyabiashara wote wa bidhaa hizo kuzisajili kabla hazijaenda kwa  mtumiaji na kutofanya hivyo ni kwenda kinyume na Sheria.

Alieleza kuwa TFDA kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi wameandaa mkakati madhubuti wa kuhakikisha wanawabaini na kuwakamata wafanyabiashara wote wanaouza dawa na vipodozi hivyo kupitia mitandao na kuwachukulia hatua ikiwemo kuwafikisha mahakamani au kuwatoza faini. 

“Wengi wa wafanyabiashara hao hawaweki anuani za maeneo wanayopatikana na hawana maduka rasmi bali huweka namba za simu za mkononi lakini kwa kutumia vyombo vya dola tutawabaini tu na kuwatia mbaroni.” Alisisitiza Simwanza.

Kwa upande wake Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Bw. Innocent Mungy amewatahadharisha watumiaji wa huduma za mawasiliano hasa matangazo ya biashara kuwa makini na matangazo hayo kwani baadhi ya wafanyabiashara hizo wanaweza kuwa ni watu wenye nia mbaya. 

Hivi karibuni kumeibuka wimbi la wafanyabiashara wa dawa mbalimbali pamoja na vipodozi ambao wanajitangaza kupitia mitandao ya kijamii na kuna baadhi ya watu wananunua bidhaa hizo bila ya kuhakikisha usalama wake jambo ambalo ni hatari kwa afya zao.

Bodaboda waiomba serikali kuwachukulia hatua kali abiria wanaokataa kuvaa helmeti

$
0
0

Jonas Kamaleki, Maelezo

WAAENDESHA pikipiki maarufu kama bodaboda wameiomba serikali kuwachukulia hatua kali abiria wanaokataa kuvaa kofia ngumu (Helmet) ili kutoa fundisho kwa watu wengine wasihatarishe maisha yao.

Akiongea katika mahojiano maalum, mwendesha pikipiki, Nathanael Kiula wa Dar es Salaam amesema kuwa abiria wanaokataa kuvaa helmeti wachukuliwe hatua kali ikiwepo kutozwa faini isiopungua Tsh. 30,000/= ili liwe fundisho kwa wengine.

“Mimi nina helmeti mbili ya kwangu na abiria lakini abiria wengi hawataki kuvaa helmeti hasa akina mama kwa madai kuwa nywele zao zinaharibika pia wanadai kuwa zina uchafu.”alisema Kiula.

Kiula alisema kuwa elimu itolewe kwa abiria na waendesha pikipiki juu ya umuhimu wa kuvaa helmeti kwani ni kwa manufaa yao wanapopata ajali wasiumie sana au kupoteza maisha na si kwa ajili ya kuwakwepa matrafiki.

Mwendesha pikipiki aliyejitambulisha kwa jina la Isaac William alisema abiria wanaokataa kuvaa helmeti waadhibiwe vikali ili kukomesha tabia hii isiokubalika katika suala zima la usafirishaji.

“Abiria wangu baadhi wanakubali kuvaa helmeti lakini walio wengi hukataa kuzivaa kwa madai kuwa wanaogopa magonjwa ya kuambukizwa kupitia vifaa hivyo,”alisema William.

Naye abiria wa bodaboda ambaye ni mkazi wa Dar es Salaam, Bi Fatuma Abdallah amesema yeye hawezi kuvaa helmeti kwani zinatumiwa na watu wengi hivyo anaogopa kupatwa na magonjwa.



“Siwezi kuvaa mikofia yao kwani inatumiwa na watu wengi huwezijua wana magonjwa ya ngozi kiasi gani, kamwe sintoyavaa ng’o,”alisema Fatuma.

Kwa upande wake Kamanda Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchi, Mohamed Mpinga alisema kuwa uvaaji wa kofia ngumu kwa waendesha pikipiki ni lazima. Anayekaidi amri hiyo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

Kwa upande wake, Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Helmet Vaccine Initiative Tanzania Foundation, Bw. Alpherio Nchimbi alisema matumizi ya Helmeti hayaepukiki kwa usalama wa mwendesha pikipiki na abiria.

“Kwa umuhimu huo, Taasisi yetu inatoa msaada wa kiufundi kwa Jeshi la Magereza nchini kwa ajili ya uanzishwaji wa kiwanda cha kutengeneza kofia ngumu kwa kufuata viwango vya Shirika la Viwango nchini (TBS) na pia tunatoa elimu kwa bodaboda kuhusu matumizi ya kofia ngumu na madhara yatokanayo na kutovaa kofia hizo kuanzia ngazi ya familia hadi Taifa kwa ujumla,” alisema Nchimbi.

Kuhusu suala la kuvaa helmeti, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alisema kuwa mwendesha pikipiki na abiria ni lazima wavae helmeti na ifikapo Julai 1, 2016 hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya abiria au mwendesha pikipiki atakayekaidi amri hiyo.

“Nawaambia, hatutamvumilia mtu yeyote, mwendesha pikipiki na abiria asiyevaa helmeti tunawahesabu kuwa wana mpango wa kujiua,”alisema Makonda wakati wa Uzinduzi wa Mpango wa Taifa wa Usalama wa raia wa Jeshi la Polisi.

Suala la kuvaa kofia ngumu au helmeti kwa waendesha pikipiki na biria wao limekuwa likipuuzwa kwa muda mrefu ndio maana serikali ya Mkoa wa Dar es Salaam kwa kushirikiana na Jeshi la polisi wameandaa utaratibu wa kuwafuatilia na kuwachukulia hatua za kisheria kwa ajili ya kunusuru maisha yao. Mpango huu unaanza rasmi tarehe 1, 2016.

Ulinzi vituo vya DART kuimarishwa

$
0
0



Benjamin Sawe Maelezo

—————————–

Baadhi ya abiria wanaotumia usafiri wa mabasi yaendayo kasi maarufu kama mwendo kasi wameilalamikia kampuni hiyo kwa kushindwa kudhibiti vitendo vya wizi vinavyoendelea katika baadhi ya vituo hivyo.

Bw. Juma Ally mkazi wa Kimara mwisho anasema vitendo hivyo hutokea nyakati za usiku kwa baadhi ya vijana kujifanya nao ni miongoni mwa watumiaji daraja hilo na kupelekea abiria kuibiwa vitu vyao ikiwa ni pamoja na kujeruhiwa.

Aliongezea kuwa walinzi wa kituo hicho wamekuwa wakifanya kazi ya kuwapanga abiria na kusahau majukumu yao ya kulinda usalama wa kituo hicho pamoja na mali zao.

“Tunashangaa hawa walinzi wanaolinda vituo hivi, abiria wamekuwa wakilalamika kila siku kuibiwa nyakati za usiku lakini tunaona abiria wakiendelea kuibiwa sijui wahusika wapo wapi?”Aliuliza Bw. Ally.

Nae Bi. Herrieth Shangaa aliongezea kuwa licha ya vitendo vya wizi vinavyoendelea katika vituo hivyo kuna baadhi ya vitendo vikiwemo vya kujisaidia katika madaraja hayo hivyo kupelekea uchafuzi wa mazingira

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi msimamizi wa vituo hivyo ambae hakutaja kutajwa jina lake amesema kuna baadhi ya vituo ni vikubwa na wanawalinzi wachache hivyo wamejipanga kuongeza ulinzi ikiwa ni pamoja na kufunga mfumo wa kidigitali wa kudhibiti wahalifu

Mradi wa mabasi yaendayo haraka ulioanza rasmi terehe 10, mei, 2016 umeonesha ni jinsi gani kero ya foleni itakavyopungua kwa kuwa mabasi hayo yanatumia njia yake ambayo ni miundombinu iliyojengwa kwa gharama kubwa sana.

Mwenyekiti wa CCM Shinyanga Awafuturisha Waislam Mkoa Wa Shinyanga,Sheikh Mkuu Apongeza,Askofu Atoa Neno Kwa Magufuli

$
0
0


Juni 29,2016 kumefanyika tukio muhimu mjini Shinyanga ambapo Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Shinyanga ndugu Erasto Kwilasa (pichani) amewaandalia chakula cha pamoja “futari” waumini wa dini ya kiislamu mkoa wa Shinyanga ikiwa ni sehemu ya kuutukuza mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Tukio hilo limefanyika leo jioni/usiku kuanzia katika Ukumbi wa NSSF mjini Shinyanga na kuhudhuriwa na waumini na viongozi wa dini ya kiislamu wakiongozwa na Sheikh Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ismail Habibu Makusanya.Wengine waliohudhuria ni viongozi wa vyama vya siasa na serikali,viongozi wa madhehebu mengine ya dini wakiongozwa na Askofu wa Kanisa la Africa Inland Church Tanzania (AICT) Dayosisi ya Shinyanga, Askofu Dr. John Nkola na watu mbalimbali wenye mapenzi mema.
Akizungumza wakati wa kula chakula cha pamoja “Futari” mwandaaji wa chakula hicho ambaye ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Erasto Kwilasa alisema aliwashukuru waumini wa dini ya kiislamu kukubali kushiriki na kudai kuwa ameamua kufanya hivyo ili kuonesha kwa vitendo kuwa anawapenda watu wa Shinyanga bila kujali makabila,dini wala rangi zao.
“Nawashukuruni sana tumekusanyika hapa,tupo hapa katika kushirikiana pamoja kwa kupata futari ya pamoja,mimi binafsi naamini katika ibada hii tutakuwa tumetenda jambo jema mbele ya mwenyezi mungu hasa katika kutekeleza nguzo muhimu miongoni mwa nguzo tano za kiislamu,funga ya mwezi mtukufu”,alisema Kwilasa.

“Ndugu zangu mlikuwa na nfasi ya kutoa udhuru kwamba mimi ni kiongozi wa chama,lakini kwa upendo mlionionesha leo hii,mmedhihirisha ule usemi wa serikali na chama havina dini bali wanachama wake wana dini zao na hii ndiyo maana mmekuja kwa wingi na mpaka sasa tupo pamoja hapa bila ubaguzi wa aina yoyote”,aliongeza Kwilasa. Kwilasa alitumia fursa hiyo kuwataka wanasiasa kuacha kubaguana kwani binadamu wote ni wa mwenyezi mungu huku akimuomba mungu kupokea funga za waumini wote wa mkoa wa Shinyanga na taifa kwa ujumla.

“Kwa kutambua kazi nzuri zinazofanywa na rais John Pombe Magufuli na timu yake yote,naomba tuendelee kumuombea sana kwa mungu ili aweze kufanikisha malengo yake aliyowaahidi wananchi”,alisema Kwilasa. Katika hatua nyingine Kwilasa aliwaomba viongozi wote wa madhehebu ya dini kusaidiana na viongozi wa serikali mkoa wa Shinyanga kupiga vita vitendo vya mauaji dhidi ya vikongwe,ubakaji na ulawiti kwa watoto,utumiaji wa madawa ya kulevya na ukatili wa kijinsia.




Kwa upande wake Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sheikh Ismail Habibu Makusanya alimpongeza mwenyekiti huyo wa CCM kuandaa chakula cha pamoja kwa ajili ya waumini wa dini ya kiislamu na kusema kuwa kitendo alichokifanya kina dhawabu kubwa kwa mwenyezi mungu.



“Ukimuona mja anashughulika kuwalisha watu, wa kweli na wasio wakweli,wacha mungu na wasio wacha mungu huyu ameshika kazi ya mungu..sasa mwenyeji wetu ulichokifanya hapa sisi hatuwezi kukulipa lakini hiki ulichofanya ni kafara kubwa sana katika maisha yako ,ni hifadhi kubwa sana katika maisha yako,ni sadaka kubwa sana,kuwaita na kuwalisha waliofunga ni kazi kubwa,mungu akuzidishie pale ulipotoa”,aliongeza Sheikh Makusanya.



Naye Askofu wa Kanisa la Africa Inland Church Tanzania (AICT) Dayosisi ya Shinyanga, Askofu Dr. John Nkola alisema ni mara kwanza yake ya kwanza kukaribishwa kwenye futari kubwa kama hiyo na kuwashukuru waislamu kukusanyika pamoja kushiriki pamoja kwa futari na kwamba mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani ni kwa ajili ya utukufu wa mungu.



Askofu Nkola alitumia fursa hiyo kuwataka watanzania kujenga mshikamano na umoja uliopo kwani umoja wa madhehebu ya dini ndiyo uzima na amani ya taifa la Tanzania.



“Tukishikamana na kumhubiri mwenyezi mungu ambaye ni wa amani,nchi yetu itaendelea kuwa na amani sana,tuendelee kushikamana,na tuendelee kumuombea rais Magufuli anafanya mambo makubwa ambayo siyo kila mtanzania atayapenda hata kidogo”,alisema Askofu Nkola



“Sasa sisi kazi yetu siyo siasa lakini maandiko na misahafu inatuagiza kuwaombea wale ambao mwenyezi mungu amewapa madaraka ya kutawala,tumuombee sana rais wetu,pamoja na serikali yetu na nchi yote kwa ujumla tuendelee kutulia kwa amani,tuendelee kuwa kimbilio la wanyonge wanaonyanyaswa katika nchi zao”,aliongeza askofu Nkola.



Malunde1 blog huwa haipitwi na matukio,Mwandishi mkuu wa mtandao huu,Kadama Malunde alikuwepo eneo la tukio,ametusogezea picha 85..Shuhudia mwenyewe hapa chini








Wa kwanza kushoto ni Askofu wa Kanisa la Africa Inland Church Tanzania (AICT) Dayosisi ya Shinyanga, Askofu Dr. John Nkola,wa kwanza kulia ni Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sheikh Ismail Habibu Makusanya wakiwa katika ukumbi wa NSSF mjini Shinyanga usiku huu




Wa pili kutoka kushoto ni mstahiki meya wa manispaa ya Shinyanga Gulah Hafeez Mukadam akiwa na viongozi wa dini ya kiislam mkoa wa Shinyanga





Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga ambaye ndiye mwandaaji wa Futari hiyo ndugu Erasto Kwilasa akizungumza ukumbini na kuwashukuru waumini wa dini ya kiislamu kwa kujitokeza kwa wingi kufuturu kwa pamoja








Mwenyekiti huyo wa CCM mkoa wa Shinyanga ndugu Erasto Kwilasa alisema wamekusanyika hapo kwa ajili ya kuutukuza mwezi mtukufu wa Ramadhani







Tunamsikiliza Kwilasa.....







Kwilasa alisema ameandaa futari hiyo ikiwa ni ishara ya kuonesha ushirikiano kwa vitendo ikiwa ni mambo aliyousiwa na wazee wa mji wa Shinyanga alipokutana nao na kufanya mazungumzo kwamba miongoni mwa usia wao mkubwa ni kujitahidi kuwa karibu na watu.



Meza kuu wakitafakari...




Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga akitoa hotuba fupi




Tunafuatilia hotuba.....




Kwilasa akizungumza ukumbini ambapo aliwahakikishia wakazi wa Shinyanga kuwa atafanya kazi na kila kundi katika jamii kwa nguvu na bidii zake zote



Askofu wa Kanisa la Africa Inland Church Tanzania (AICT) Dayosisi ya Shinyanga, Askofu Dr. John Nkola akizungumza ukumbini ambapo aliwasihi watanzania kudumisha mshikamano walio nao ili kuhakikisha kuwa amani ya nchi haitoweki



Askofu wa Kanisa la Africa Inland Church Tanzania (AICT) Dayosisi ya Shinyanga, Askofu Dr. John Nkola akisisitiza umoja na mshikamano miongoni mwa watanzania bila kujali dini,makabila wala rangi zao.



Askofu John Nkola akifurahia jambo...


Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sheikh Ismail Habibu Makusanya akitoa shukrani za mualiko wa mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga kushiriki futari ya pamoja ambapo alisema hilo ni jambo jema linalofurahiwa sana na mwenyezi mungu






Meza kuu wakimsikiliza Sheikh Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ismail Makusanya








Sheikh Makusanya akizungumza ukumbini Tunamsikiliza Sheikh wa mkoa wa Shinyanga






Sheikh Makusanya alimpongeza Kwilasa kwa kuona umuhimu wa kuwakaribisha chakula waislamu waliofunga huku akiwahamasisha wanadamu kuwa na moyo wa kujitolea ili kupata dhawabu kutoka kwa mwenyezi mungu








Wa pili kutoka kulia ni mkuu wa polisi wilaya ya Shinyanga Richard Ngede Sheikh Makusanya akizungumza ukumbini ambapo pia alihamasisha watanzania kuendelea kushikamana ili kudumisha amani ya nchi






Meza kuu wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea...Wa kwanza kulia ni mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini Kanali mstaafu Tajiri Maulid










Waumini wa dini ya Kiislamu wakiwa ukumbini







Waumini wa dini ya kiislamu na wageni waalikwa,katikati ni Diwani wa Kata ya Kambarage katika manispaa ya Shinyanga Hassan Mwendapole







Washiriki wa tukio hilo wakifuatilia kilichokuwa kinajiri ukumbini







Tunafuturu pamoja.....








Washiriki wakiwa ukumbini





Tunafuatilia kinachoendelea ukumbini





Akina mama wakiwa ukumbini





Tunakunywa uji....





Viongozi wa CCM na dini ya kiislam wakiwa meza kuu,wa kwanza kushoto ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Erasto Kwilasa






Tunakula pamoja






Tunafuturu pamoja





Viongozi wa madhehebu ya dini,serikali na dini ya kiislamu wakiwa meza kuu huku washiriki wengine wakiwa katika mstari kwa ajili ya chakula





Meza kuu wakila chakula





Zoezi la kuchukua chakula linaendelea..





Tunachukua chakula





Zoezi la kuchukua chakula linaendelea





Tunakula chakula......





Meza kuu wakiendelea kula chakula





Tunakula...





Akina mama wakila chakula





Tunakula...








Akina mama wakiwa ukumbini


























Tunakula.....





Hapa ni kula tu....





Tunafuturu...








Tunaendelea kula...














Tunaendelea kula...




























Tunakula.....





Akina mama wakiendelea kula ukumbini



















Kila mmoja alikula....





Baada ya kumaliza kula...













Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Erasto Kwilasa akikumbatiana na Sheikh Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Ismail Habibu Makusanya





Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Erasto Kwilasa akikumbatiana na Askofu John Nkola





Hongera sana Kwa kuandaa Futari ndugu Kwilasa.....










Askofu John Nkola na Kanali Mstaafu Tajiri Maulid wakiondoka ukumbini baada ya kufuturu





Hongera kwa kazi nzuri....





Mweka hazina wa CCM mkoa wa Shinyanga bwana Mapalala akiwa na mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga baada ya shughuli kumalizika.


Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Wawekezaji wazawa wana haki kuwekeza kwenye gesi, mafuta

$
0
0

Na Greyson Mwase
Serikali imesema wawekezaji wazawa wana haki ya kuwekeza kwenye sekta za mafuta na gesi ili sekta hizo ziwe na mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa nchi.Hayo yamesemwa na mtaalam kutoka Idara ya Nishati, Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi  Petro Marwa kwenye  maonesho ya  kimataifa ya  sabasaba yanayoendelea katika  viwanja  vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es  Salaam.

Mhandisi Petro alisema kumekuwepo na dhana  kuwa  wawekezaji kutoka nje ya nchi wanapewa kipaumbele katika uwekezaji kwenye gesi na mafuta  jambo ambalo si sahihi.Alisema ili kuhakikisha kuwa kila mtanzania ananufaika na uwekezaji kwenye  sekta za  gesi na mafuta,  Serikali imeweka sheria nzuri za kuwezesha watanzania kuwa sehemu  ya uchumi wa gesi na mafuta.

“ Kwa mfano Sheria ya Mafuta ya Mwaka  2015 kifungu cha  218 kinaeleza ushiriki wa serikali  kupitia Kampuni ya  Mafuta ya  Taifa (National Oil Company) na kifungu cha  219  na 220 kinaainisha ushiriki  wa watanzania katika utoaji wa  huduma na bidhaa kwa makampuni yaliyowekeza nchini kwenye  sekta za mafuta na gesi,” alisema  Mhandisi Petro.

Mhandisi Petro aliendelea kusema kuwa  serikali imeweka mikakati mbalimbali kuhakikisha watanzania wanakuwa si watazamaji  kwenye uvunaji wa rasilimali za gesi na mafuta bali wanakuwa ni washiriki kamili na kuchangia  katika ukuaji wa uchumi  wa nchi.
D1 
Afisa Habari, Mhandisi  Yisambi Shiwa (kushoto) na Mkaguzi wa Madini Mwandamizi Jeremiah Hango (kulia) kutoka Wakala wa Ukaguzi wa Madini Nchini (TMAA), wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kuwahudumia wateja katika  Maonesho ya Kimataifa  ya Saba Saba (Dar es Salaam International  Trade  Fair)  yanayoendelea katika  Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
D2 
Afisa Habari, Mhandisi  Yisambi Shiwa (kulia) kutoka  Wakala wa Ukaguzi wa Madini Nchini (TMAA) akielezea madini ya dhahabu yanavyochenjuliwa kwa mteja aliyeshika sampuni ya madini hayo kwenye banda la TMAA katika maonesho hayo.
D3 
Mtaalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Phillip Mathayo  (kushoto) akielezea majukumu ya Wizara  kwa mteja aliyetembelea banda  hilo  katika Maonesho ya Kimataifa  ya Saba Saba (Dar es Salaam International  Trade  Fair)  yanayoendelea katika  Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
D5 
 Mmoja wa wateja (kushoto) akitoa maoni yake kwenye banda la Shirika la Madini la  Taifa (STAMICO) kwenye Maonesho ya Kimataifa  ya Saba Saba (Dar es Salaam International  Trade  Fair)  yanayoendelea katika  Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

D7 
Neema Mwambenja kutoka Taasisi ya  Environmental Foundation for  Tanzania (EFFORT) ambayo ni mdau wa Wakala wa Nishati  Vijijini (REA) (katikati) akitoa maelezo ya shughuli zinazofanywa na taasisi hiyo kwenye banda la  REA, kwenye Maonesho ya Kimataifa  ya Saba Saba (Dar es Salaam International  Trade  Fair)  yanayoendelea katika  Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Odriana Magige kutoka  taasisi hiyo.
D8 
Mhandisi Migodi kutoka Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Suleiman Khalid (katikati) akielezea shughuli zinazofanywa na shirika hilo. Kushoto ni Afisa Usalama na Mazingira kutoka  shirika hilo Paul Thobias.
D6 
Banda la Wizara ya Nishati na Madini na Tasisi zake kama linavyoonekana pichani  kwenye kwenye Maonesho ya Kimataifa  ya Saba Saba (Dar es Salaam International  Trade  Fair)  yanayoendelea katika  Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
———————————————
Akielezea mikakati hiyo, Mhandisi Petro alisema kuwa Serikali kupitia  Wizara ya Nishati na Madini  ilianzisha kozi mbalimbali zinazohusu mafuta na gesi katika  Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) na Chuo cha Madini (MRI).
Aliongeza kuwa Wizara imekuwa ikiwezesha  wanafunzi wanaofanya  vizuri katika masomo  ya sayansi kupata ufadhili wa kusomea masuala ya mafuta na gesi katika vyuo mbalimbali ndani na nje ya nchi.

Mhandisi Petro alitoa wito kwa watanzania wote kuchangamkia  fursa zilizopo katika sekta za mafuta na gesi ili nchi iweze kutoka kwenye kundi la nchi masikini  duniani na kuingia  katika orodha ya nchi zenye kipato cha kati ifikapo mwaka  2025 kama   Dira  ya Maendeleo ya Taifa inavyofafanua

SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA (NHC) LAANZA KUTOA HUDUMA KATIKA MAONESHO YA 40 YA KIMATAIFA ya SABASABA

$
0
0

Afisa Mauzo (NHC), Jasson Ipyana akimuelezea mwananchi kuhusina na miradi ya nyumba ya bei nafuu ilioko nchini.
Bw: Klison Sanane (kushoto), akifafanua miradi mbalimbali ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).
Aika Swai (kushoto), akielezea kuhusiana na utaratibu wa unaoutumika katika ununuzi wa nyumba za (NHC) huku baadhi ya wadau kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) wakimsikiliza kwa umakini.
 

Banda la Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) likiwa katika Maonesho ya 40 ya Kimataifa ya Biashara, yanayofanyika kila mwaka katika viwanja vya Mwalimu Nyerere Sabasaba jijini Dar es salaam tayari limeanza rasmi kutoa huduma zake katika viwanja hivyo.



Afisa Mawasiliano na Huduma kwa Jamii wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC),Bi Edith Nguruwe akiwapa maelezo wananchi waliotembelea banda la (NHC) kuhusina na huduma zinazotolewa na Shirika hilo.



Afisa Mauzo Mwandamizi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Emmanuel Limo (kushoto), akimuelezea Wananchi Kuhusiana na mradi wa SAFARI CITY uliopo Arusha alipotembelea banda hilo katika maonesho ya Sabasaba.


Afisa biashara (NHC), Clara Lubanga akitoa ufafanuzi kwa mmoja wa Wananchi aliotembelea banda hilo kuhusiana uzwaji wa nyumba (katikati), Afisa Mauzo wa (NHC), Joseph Haule.
PICHA ZOTE NA PHILEMON SOLOMON-FULLSHANGWEBLOG.

TUNDULISU AACHIWA KWA DHAMANA

$
0
0
 Na Mwene Said wa Globu ya Jamii, Dar es Salaam

Tundu Lissu (48) amesomewa mashtaka ya kutoa lugha ya uchochezi ikiwemo kudharaulisha watanzania dhidi ya mamlaka halali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Lissu alisomewa mashtaka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo Juni 30, 2016.

Upande wa Jamhuri ukiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu Bernad Kongola akisaidiana na Mawakili wa Serikali Waandamizi, Nassoro Katuga na Salum Mohammed.

Kongola alidai kuwa Juni 28,2016 eneo la Mahakama ya Kisutu Ilala Dar es Salaam mshtakiwa kwa nia ya kushawishi na kudharaurisha watanzania dhidi ya mamlaka halali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Alinukuu maneno ya Lissu kwamba"Mamlaka ya Serikali mbovu ya kidikteta uchwara inahitaji kupingwa na kila mtanzania kwa nguvu zote, huyu dikteta uchwara lazima apingwe kila sehemu kama uongozi utafanywa na utawala wa kijinga nchi inaingia  ndani ya giza nene"

Mshtakiwa alikana mashtaka hayo.

upande wa jamhuri ulidai upelelezi umekamilika na uliomba tarehe ya kusikilizwa maelezo ya awali.
Upande wa utetezi ukiongozwa na jopo la mawakili 11 akiwemo Michael Ngalo, Peter Kibatala na wenzao uliomba dhamana kwa mshtakiwa kwa kuwa ni mbunge atakuwa mwaminifu hataacha kufika mahakamani.

Hakimu Yongolo alisema mshtakiwa atakua nje kwa dhamana kwa kuwa na wadhamini wawili watakaosaini hati ya dhamana ya sh milini 2.

alitimiza masharti atasomewa maelezo ya awali Agosti 2,2016.

TAASISI YA UTAWALA BORA NA DEMOKRASIA NCHINI TANZANIA YAWAKUTANISHA WADAU WA MAZINGIRA.

$
0
0

Jimmy Luhende, Mkurugenzi wa Taasisi ya Utawala Bora na Demokrasia nchini (ADLG), akizungumza katika Mjadala wa Mwezi June uliofanyika hii leo Jijini Mwanza.

Taasisi ya ADLG huendesha mijadala tofauti tofauti kila mwisho wa mwezi ambapo wadau mbalimbali hukutana na kujadili mada husika. Mjada wa mwezi june umeangazia Fursa, changamoto na athari za kimazingira zitokanazo na shughuli za migodini.

Katika mjada huo, wadau wameishauri serikali kupia Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEC, kuboresha sheria ya usimamizi wa mazingira ili kuweza kuwafanyia tathmini za uchafunzi wa mazingira wachimbaji wadogo kwa kuwa baadhi yao wamekuwa wakichangia uchafunzi wa mazingira nchini.
Jamal Baruti ambae ni Mratibu wa Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC, Kanda ya Ziwa, akiwasilisha mada juu ya tathmini ya athari za mazingira zitokanazo na shughuli za uchimbaji wa madini.

Amesema tathimini ya uchafuzi wa mazingira imekuwa ikifanyika kwa wachimbaji wakubwa wa madini kabla na baada ya uchimbaji lakini wachimbaji wadogo wamekuwa hawaguswi na tathmini hiyo kutokana na kutojumuishwa katika tathimini hiyo kwa mjibu wa sheria ya mazingira.
Mmoja wa washiriki akichangia mada
Mmoja wa washiriki akichangia mada
Mdau wa Mazingira, Sheikh Saad Rwekaka ambae pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu BAKWATA mkoani Mwanza, akitoa maoni yake. Anasema ni vyema wachimbaji wadogo wadogo wakashirikishwa ipasavyo ili kuondokana na uchafuzi wa mazingira katika shughuli zao.

Mmoja wa washiriki akichangia mada



Wadau wa Mazingira



Wadau wa Mazingira


Wadau wa Mazingira
Mijadala ikiendelea
Wadau wa Mazingira
Wadau wa Mazingira
Wadau wa Mazingira
Wadau wa Mazingira
Ashraph Omary (katikati) ambae ni mdau wa Mazingira kutoka taasisi ya MEDTO (Mining and Environmental Transformation for Development Organisation), akifanyiwa mahojiano na mwanahabari.

Imeandaliwa na BMG

WADAU WAIPONGEZA MAMLAKA YA ELIMU UTEKELEZAJI WA MRADI WA UKARABATI WA SHULE KONGWE

WAZIRI MKUU: SERIKALI ITATOA WARAKA JUU YA UKUSANYAJI MAPATO KUPITIA MAWAKALA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Halmashauri zitaelekezwa kwa waraka ni vyanzo vipi vitahitaji kutumia wawakala wa ukusanyaji mapato kwani siyo kila chanzo cha mapato ya Halmashauri kitakusanywa kwa ufanisi kwa kutumia au kwa kutotumia mawakala.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo mchana (Alhamisi, Juni 30, 2016) wakati akitoa hoja ya kuhitimisha mkutano wa tatu wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye ukumbi wa Bunge mjini Dodoma.

Amesema katika ukusanyaji wa mapato, baadhi ya vyanzo vitapaswa kukusanywa na Halmashauri zenyewe kwa kuzingatia miongozo iliyotolewa na Serikali. “Moja ya miongozo hiyo ni kwamba kuanzia sasa, iwe kwa kutumia mawakala au Halmashauri zenyewe ni lazima fedha zinazokusanywa ziwekwe kwenye akaunti ya Halmashauri na kutumia mifumo ya kielektroniki ili kupunguza au kumaliza kabisa masuala ya kutumia malipo kwa fedha taslimu (cash transactions),” alisema.

Amesema katika kutekeleza agizo hilo, Halmashauri itabidi zikubaliane na wakala ni kiasi gani cha asilimia ya makusanyo kitalipwa kwa wakala na malipo yafanyike baada ya kukusanya na kuingizwa kwenye akaunti ya Halmashauri.

Amesema Sheria ya Fedha ya Serikali za Mitaa Sura ya 290, inazipa uwezo Mamlaka za Serikali za Serikali za Mitaa kutoza na kukusanya kodi, ushuru na ada mbalimbali kama vyanzo vya mapato vya Mamlaka za Serikali za Mitaa.

“Sheria hiyo pia inazipa mamlaka hizo kuteua mawakala wa kukusanya mapato hayo kwa niaba ya Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu. Lakini Serikali imebaini changamoto za kiufundi katika kufanya tathmini ya vyanzo vya mapato; ugumu katika kupata mawakala wenye weledi katika ukusanyaji mapato na kubuni vyanzo vipya vya mapato, na wakati mwingine watumishi wenyewe kujipa uwakala kinyume na taratibu zinazomzuia mtumishi kufanya biashara na taasisi yake,” alisema.

Amesema hatua ya Mamlaka za Serikali za Mitaa kutumia mawakala ni miongoni mwa mikakati ya kuboresha ukusanyaji mapato na pia kutoa muda mwingi zaidi kwa watumishi wa mamlaka hizo kushughulika na majukumu ya msingi ya Halmashauri na hasa utoaji wa huduma kwa wananchi na usimamizi wa miradi ya maendeleo.

“Pamoja na dhamira nzuri ya hatua hizo, tunayo mifano ya baadhi ya Halmashauri kama vile Nzega ambayo baadhi ya wahusika wameshinikiza wakitaka zabuni zote wapewe madiwani. Jambo hili halikubaliki na tena ni kinyume cha maadili ya utumishi,” alisisitiza.

Katika hatua nyingine,Waziri Mkuu ameziagiza Halmashauri zote nchini kwamba kuanzia Julai Mosi, 2016 zihakikishe zinatumia mifumo ya kielektroniki katika kukusanya mapato, katika kulipa, kuweka na kutekeleza kikamilifu mikakati madhubuti ya kuboresha makusanyo iwe yanakusanywa na Halmashauri au na wakala.

Amesema Mamlaka za Serikali za Mitaa zina wajibu wa kutoa taarifa kwa wananchi kuhusu mapato na matumizi ya Serikali pamoja na michango ya wananchi licha ya kuwa uzoefu unaonesha kuwa mamlaka hizo zina tatizo la kukaa na fedha kwa muda mrefu kabla ya kuzielekeza kwenye matumizi yaliyokusudiwa.

“Kuchelewesha kutoa fedha zilizotengwa kwa shughuli zilizopangwa ni kuchelewesha kufikisha huduma muhimu kwa wananchi. Napenda kuhimiza uzingatiaji wa utaratibu wa kutoa taarifa kwa wananchi kuhusu mapato na matumizi ya fedha za Serikali katika ngazi zote ili kuongeza uwazi na uwajibikaji katika sekta ya umma,” aliongeza.

Mkutano huo wa tatu wa Bunge ulioanza Aprili 19, 2016 ulikuwa mahsusi kwa ajili ya kujadili na kupitisha bajeti ya kwanza ya Serikali ya Awamu ya Tano pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa fedha 2016/2017. Bunge limeahirishwa hadi Septemba 6, mwaka huu litakapokutana tena mjini Dodoma.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,    
DODOMA.
ALHAMISI, JUNI 30, 2016

Waziri Mkuu awataka wabunge wa upinzani kurejea Bungeni

$
0
0

Na: Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa leo, Bungeni Mjini Dodoma amewataka wabunge wa upinzani ambao wamesusia vikao vya Bunge tangu Mei 30 kuingia Bungeni na kuacha kususia vikao vya Bunge kwani hakuna tija kwa Taifa. Mhe. Majaliwa ameyasema hayo alipokuwa akitoa hutuba ya kuhitimisha mkutano wa tatu wa Bunge la kumi na moja.

“kitendo cha baadhi ya waheshimiwa wabunge kususia vikao vya Bunge hakitoi picha nzuri kwa wananchi waliotuchagua kuwasilisha matatizo yao katika Bunge hili, hivyo natoa rai kwa waheshimiwa wabunge hao kutafakari upya uamuzi wao na niwasihi kwa busara zao waingie ili kwa pamoja na kwa ushirikiano tuweze kutoa ushauri kwa Serikali,” alisema Mhe. Majaliwa.

Aidha Mhe. Majaliwa alitoa ufafanuzi juu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ambayo imetoa haki na kinga kwa waheshimiwa wabunge ili kujadili na kuhoji utendaji wa Serikali kwa uhuru bila mashaka yoyote ya kuweza kushitakiwa wanapotimiza wajibu wao wakiwa Bungeni. Aliendelea kwa kusema kuwa kinga ya aina hiyo haijatolewa kwa mwananchi yeyote yule Nchini ila kwa Wabunge, hivyo basi hakuna mbunge aliyefungwa mdomo labda aamue kujifunga mdomo yeye mwenyewe.

Mhe. Majaliwa amesema kuwa Bunge linaongozwa na Katiba, Sheria na Kanuni za Kudumu za Bunge, hivyo ni vyema zikafuatwa kuondoa manung’uniko yasiyo ya lazima na endapo kuna utata katika jambo lolote ndani ya Bunge zipo taratibu zilizowekwa na kanuni za kufuata ili kupata ufumbuzi na si kwa kususa kuingia Bungeni kwani hakuna tija kwa Taifa.

Wabunge wa upinzani wamesusia vikao vya Bunge tangu Mei 30, 2016 mpaka leo Juni 30 ambapo Bunge limehitimishwa. Aidha wabunge hao wamekuwa wakiingia Bungeni kila asubuhi na jioni kisha kutoka mara tu Naibu Spika Mhe. Dkt. Tulia Ackson anapomaliza kusoma Dua maalum la kuliombea Bunge na Taifa.

GAZET LA MTANZANIA LA ZINDUA MWEONEKA MPYA “MTANZANIA LIMEBORESHWA

$
0
0


Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya New Habari (2006)Ltd, Absalom Kibanda, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuhusu uzinduzi wa mwonekano mpya wa Gazeti la Mtanzania lenye kauli mbiu ya “Mtanzania Limeboreshwa”.Kulia ni Mhariri Mtendaji wa Mtanzania, Dennis Msacky na Meneja Masoko wa kampuni hiyo.
Mhariri wa Gazeti la Mtanzania, Dennis Msacky.akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana. kuhusu uzinduzi wa mwonekano mpya wa Gazeti la Mtanzania lenye kauli mbiu ya “Mtanzania Limeboreshwa”Katikati ni Mhariri Mtendaji Kampuni ya New Habari(2006)Ltd, Absalom Kibanda na Meneja Masoko wa Kampuni hiyo, Michael Bugidira.

Picha na Mpiga Picha Wetu

Wanufaika wa Mikopo ya Elimu Juu watakiwa kurejesha mikopo waliyopewa.

$
0
0
Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma


Wanufaika wa Mikopo ya Elimu ya Juu ambao tayari wapo katika ajira wametakiwa kurejesha marejesho ya mikopo waliyopewa kutokana na mfuko wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) kutegemea fedha hizo kuendelea kuwakopesha wanafunzi wengine.

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa ameyasema hayo leo Bungeni, Mjini Dodoma alipokuwa akiwasilisha hotuba ya kuhitimisha mkutano wa tatu wa Bunge la kumi na moja.

“Uwezo wa Bodi ya mikopo ya Elimu ya Juu kuwahudumia walengwa unajengwa na fedha zinazotengwa kila mwaka katika mipango na Bajeti pamoja na marejesho ya mikopo iliyoiva kutoka kwa wanufaika,” alisisitiza Mhe. Majaliwa.

Aliendelea  kusema kuwa Serikali inaendelea kufanya maboresho ya kimfumo na kisheria ili kuimarisha urejeshwaji wa mikopo. Aidha amewaagiza waajiri wote Nchini kutekeleza wajibu wao wa kuingiza makato ya marejesho wa mikopo ya wanufaika kwa wakati na kwa viwango vinavyotakiwa baada ya kuwasiliana na Bodi ya Mikopo.

Vile vile Mhe. Majaliwa amesema kuwa Serikali inaendelea kuimarisha mfumo wa utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu sambamba na kushughulikia changamoto mbalimbali zilizopo katika Bodi ya mikopo ili kuhakikisha utoaji wa mikopo unafanyika kwa ufanisi.

Pia Serikali inategemea kubadilisha utaratibu wa kutoa mikopo ili kuwafikia wanafunzi wote wenye uhitaji zaidi wakiwemo yatima na wenye uwezo mdogo kiuchumi bila kujali aina gani ya program wanazozisomea.

HOTUBA YA RAIS DKT MAGUFULI MARA BAADA YA KUWAAPISHA WAKUU WAPYA WA MIKOA MITATU - JUNE 29 2016

RAIS DKT JOHN POMBE MAGUFULI AMPOKEA RAIS WA RWANDA MH.PAUL KAGAME NCHINI

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amempokea Mhe. Paul Kagame Rais wa Jamhuri ya Rwanda kwa ziara rasmi ya kiserikali. Rais Magufuli ameambatana na Mkewe Mama Janeth Magufuli na Rais Kagame ameambatana na mkewe Mama Jeannette Kagame. Ziara hii ni ya siku mbili.Baada ya Hapo ataelekea Ikulu jijini Dar es Salaam kwaajili ya Kufanya Mazungumzo.

Baada ya hapo wataelekea katika Viwanja vya Maonesho ya Kimataifa ya Sabasaba jijini Dar es Salaam kwa ajili ya ufunguzi rasmi wa maonesho hayo ya 40 ya Kimataifa katika viwanja vya Sabasaba ,jijini Dar.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aakiwa ameambatana na mgeni wake Mhe. Paul Kagame Rais wa Jamhuri ya Rwanda mara baada ya kuwasili asubuhi hii katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kwa ziara rasmi ya siku mbili ya kiserikali. Rais Magufuli ameambatana na Mkewe Mama Janeth Magufuli na Rais Kagame ameambatana na mkewe Mama Jeannette Kagame.  
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na mgeni wake Mhe. Paul Kagame Rais wa Jamhuri ya Rwanda wakipata Gwaride la heshima uwanjani hapo.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na mgeni wake Mhe. Paul Kagame Rais wa Jamhuri ya Rwanda wakitazama kikundi cha ngoma za asili kilichokuwa kikitumbuiza uwanjani hapo.
Rais Paul Kagame akiwapungi mkono baadhi ya wananchi mbalimbali waliofika kumlaki uwanjani hapo,kushoto kwake ni  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli .

Tume ya Taifa ya Uchaguzi yajionea urushaji vipindi vya Bunge

$
0
0

Mhandisi wa mitambo wa Studio za Bunge Bi. Upendo Mbele akitoa maelezo kwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva (wa kwanza kulia) na Ujumbe wake juu ya namna wanavyotekeleza majukumu ya kurusha vipindi kwa kuzingatia sheria na Kanuni za Bunge wakati wa Ziara iliyolenga kukabidhi ripoti ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015. Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva (wa kwanza kushoto) akifuatilia Kikao cha Bunge mapema Jana wakati wa ziara ya Tume hiyo Bungeni Mjini Dodoma kabla ya kuahirishwa kwa Mkutano wa tatu wa Bunge la kumi na moja .

Mkurugenzi wa Maktaba na Utafiti Bi. Justina Shauri akitoa maelezo kwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Ujumbe wake (hawapo pichani) wakati wa ziara yao Bungeni Mjini Dodoma ambapo walitembela Maktaba hiyo ili kujionea huduma zinazotolewa.
Kamishna wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Prof. Amon Chaligha akiwa ndani ya Maktaba ya Bunge wakati wa Ziara ya Tume hiyo Bungeni Mjini Dodoma. Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Ofisi ya Bunge Bw. Didas Wambura (wa kwanza kulia) akitoa maelezo kwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva (hayupo pichani) na Ujumbe wake wakati wa ziara ya Tume hiyo Bungeni Mjini Dodoma.(Picha na Frank Mvungi-Dodoma)
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live




Latest Images