Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46205 articles
Browse latest View live

ajali mbaya yatokea chang'ombe jijini dar,hakuna aliyepoteza maisha.

0
0

Lori la mafuta likiwa limelidondokea gari dogo baada ya kutoke ajali katika eneo la Chang’ombe jijini Dar es salaam ikihusishwa na daladala la abiria.
  Ajali mbaya inayohusisha Lori la Mafuta, Daladala pamoja na Gari aina ya Prado imetokea mapema leo maeneo ya Chang’ombe Machinjioni kwenye mataa Jijini Dar es Salaam baada ya dereva wa dalalala ambayo haikuwa na abiria kuingia vibaya katika makutano ya barabara na kusababisha dereva wa lori kugonga daladala na kuangukia Prado kama ionekanavyo pichani akijaribu kukwepa na kusababisha madhara.

 Hakuna mtu yoyote aliyepoteza maisha katika tukio hilo isipokuwa majeraha ya kawaida yamewapata madereva husika, Wananchi wameonekana eneo la tukio wakichota mafuta ya mawese yaliyomwagika kutoka kwenye lori lililopata ajali na mpaka sasa hatua zote za tahadhari zimeshachukuliwa.picha kwa hisani ya  http://differentsourcestz.com

13 WAJISHINDIA ZAWADI KATIKA DROO YA MAISHA BOMBA NA BARCLAYS BANK.

0
0

Mmoja wa wateja wa benki ya Blarclays ambaye pia ni Mwandishi wa Habari wa Magazeti ya Serikali, Regina Kumba akichagua moja ya majina katika droo ya bahati nasibu ya Beki hiyo ijulikanayo kama ‘Maisha Bomba na  Barclays Benki kupitia kampeni yake ya ya Sanduku la Dhahabu. Jumla ya washindi 13 walipatikana katika droo hiyo. Kutoka kushoto ni Meneja Masoko wa Barclays, Rahma Ngassa, Meneja wa Mawasiliano wa Barclays,Tunu Kavishe, Mwakilishi wa Michezo ya Kubahatisha, Humud Abdulhussein na Mkuu wa Bidhaa za Barclays  Samwel Mkuyu.
Meneja Masoko wa Barclays, Rahma Ngassa (kushoto) akizungusha pipa la bahati nasibu ya Beki hiyo ijulikanayo kama ‘Maisha Bomba na  Barclays Benki kupitia kampeni yake ya ya Sanduku la Dhahabu. Wengine pichani ni   Mwakilishi wa Michezo ya Kubahatisha, Humud Abdulhussein, Meneja wa Mawasiliano wa Barclays,Tunu Kavishe na Mkuu wa Bidhaa za Barclays  Samwel Mkuyu.
Meneja Masoko wa Barclays, Rahma Ngassa (kushoto) pamoja na viongozi wenzake wa Barclays Meneja wa Mawasiliano wa Barclays,Tunu Kavishe (katikati) na Mkuu wa Bidhaa za Barclays  Samwel Mkuyu wakiangalia pipa la bahati nasibu ya Beki hiyo ijulikanayo kama ‘Maisha Bomba na  Barclays Benki kupitia kampeni yake ya ya Sanduku la Dhahabu wakati wa kuchezesha droo za bahati nasibu hiyo leo.Picha kwa hisani ya Father Kidevu Blog.

Yanayotokea Mtwara Na Kinachohitajika Sasa.

0
0


Ndugu zangu,

 MTANZANIA mwenzetu marehemu Shaaban Robert anaandika;
” Wasadikika wana desturi ya kutafuta fimbo baada ya kuumwa na nyoka. Tumekwisha umwa na nyoka kwa matendo yetu mabaya ya zamani.

Nyoka mwenyewe amekwishakimbia. Hapatikani kwa kujilipiza kisasi, lakini, sumu yake imebakia katika jeraha tulilolipata. Sasa, shauri lililo jema ni kuzuia sumu hii isienee miilini mwetu ikaleta kifo. 
Maovu yana hatari kubwa kukaa kati yetu. Tumedumu nayo kwa muda mrefu. Hayakutuletea faida ila hasara, huzuni na kilio siku zote.”- Shaaban Bin Robert.


 Ndugu zangu,

Yanayotokea Mtwara yanatuletea mashaka kama taifa.  Linalohitajika sasa si tamko la Serikali tu, bali, tamko letu Watanzania kwenye mioyo yetu, kwamba, pamoja na haki yetu ya kimsingi ya kudai  haki, lakini, lililo la hekima na busara ni kutumia njia mujarab za kuitafuta haki hiyo. 
Na njia hiyo haiwezi kuwa ni matumizi ya nguvu ikiwamo kufanya vurugu. Hivyo, kufanya maovu ikiwamo kutoa roho za wenzetu na uharibifu wa mali, iwe imefanywa na wananchi au Serikali.

 Kama Watanzania huu ni wakati wa kufikiri kama taifa. Hii ni Nchi Yetu. Huu si wakati wa kufikiri kwa mitazamo ya kiitikadi au kiimani. Yanayotokea Mtwara yana madhara  kwa nchi nzima, na yakiachwa bila kupatiwa ufumbuzi  wa haraka, yatatawanya sumu mahala pengine pia.  Ni wakati wa Viongozi wa Serikali, Viongozi wa Chama Tawala, Viongozi wa Vyama Vya Upinzani , Viongozi wa kidini na kwa kuwashirikisha wazee wa Mtwara, kutoa matamko yatakayosisitiza umuhimu wa kutumia majadiliano  katika kupata ufumbuzi wa tatizo lililopo.

 Tukumbuke, kuwa nchi yetu ina mipaka, hivyo basi, ina maadui pia. Tusipotanguliza hekima na busara, yumkini tunaweza kutoa nafasi kwa maadui kutugombanisha zaidi. Na hivyo  ikawa hasara zaidi kwetu , na faida kwa wengine.

 Hakika,tunaweza kuyamaliza yetu kwa mazungumzo. Tuianze kazi hiyo sasa.
 Maggid Mjengwa,
Iringa.
0754 678 252

Rais Kikwete azindua ujenzi wa Barabara ya Dodoma Iringa Sehemu ya Migori-Fufu Escarpment

0
0
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Waziri wa Ujenzi John Pombe Magufuli(Wanne kushoto),Waziri wa Fedha Mgimwa(kushoto),Mwakilishi wa Balozi wa Japan Bwana Kazuyoshi Matsunaga(Wapili kushoto),Mwakilishi mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika(ADB) Bi.Tonia Kandiero(Wapili kulia) pamoja na mbunge wa Isimani William Lukuvi wakikata utepe kuzindua rasmi ujenzi wa Barabara ya Dodoma Iringa sehemu ya Migori-Fufu Escarpment na Migori Iringa mapema jana mchana.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho kikwete akiwahutubia wananchi waliohudhuria uzinduzi wa ujenzi wa Babarabara ya Dodoma Iringa jana mchana.
Baadhi ya Wananchi walihudhuria uzinduzi wa ujenzi wa Barabara ya Dodoma Iringa eneo la Migori  jana mchana. (picha na Freddy Maro)

CRDB YATOA VIFAA VYA MICHEZO KWA JWTZ KUPITIA AKAUNTI YAKE YA TANZANITE

0
0

 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akimkabidhi sehemu ya vifaa vya michezo vilivyotolewa na benki hiyo kupitia akaunti yake ya Tanzanite, Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Luteni Jenerali Samwel Ndomba kwa ajili ya wanajeshi wanaokwenda kulinda amani nchini Kongo. Hafla hiyo ilifanyika Makao Makuu ya Jeshi Upanga jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akimkabidhi sehemu ya vifaa vya michezo, Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Luteni Jenerali Samwel Ndomba kwa ajili ya wanajeshi wanaokwenda kulinda amani nchini Kongo. Hafla hiyo ilifanyika Makao Makuu ya Jeshi Upanga jijini Dar es Salaam
Mnadhimu Mkuu wa JWTZ, Luteni Jenerali, Samweli Ndomba akifafanua jambo wakati wa hafla ya kupokea vifaa vya michezo kutoka benki ya CRDB
Mnadhimu Mkuu wa JWTZ, Luteni Jenerali, Samweli Ndomba akifafanua jambo wakati wa hafla ya kupokea vifaa vya michezo kutoka benki ya CRDB.

Luteni Jenerali, Paul Mella akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa vya michezo vilivyotolewa na benki ya CRDB kupitia akaunti yake ya Tanzanite kwa ajili ya wapiganaji wanaokwenda kulinda amani nchini Kongo.
Luteni Jenerali, Paul Mella akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa vya michezo kwa wapiganaji wanaokwenda kulinda amani nchini Kongo.
Wapiganaji walioshiriki zoezi la kulinda amani nchini Darfur
Wapiganaji walioshiriki zoezi la kulinda amani nchini Dafur
Mkurugenzi Mkuu wa CRDB, Dk Charles Kimei akizungumza katika hafla hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa CRDB, Dk Charles Kimei akizungumza katika hafla hiyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akiagana na Mnadhimu Mkuu wa JWTZ, Luteni Jenerali, Samweli Ndomba. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akiagana na Lutni Jenerali, Paul Mella, huku Mnadhimu Mkuu wa JWTZ, Samweli Ndomba akiagana na Meneja Wateja Binafsi, Farida Mbwana Hamza. 
 Meneja wa Wateja Binafsi wa Benki ya CRDB, Farida Mbwana Hamza (kulia), Meneja Uhusiano wa Akaunti ya Tanzanite, Lucy Naivasha, na Meneja Mahusiano wa Benki ya CRDB, Godwin Semunyo wakiwa na  Brigedia Jenerali, Paul Peter Massao.
Maofisa wa Benki ya CRDB wakiwa katika picha ya pamoja na wapiganaji wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)
Meneja Mahusiano wa Benki  ya CRDB, Godwin Semunyu akimpa maelekezo Meja Erick Komba wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa vya michezo kwa ajili ya wanajeshi wanaokwenda kulinda amani nchini Kongo.

Brigedia Jenerali wa JWTZ, Paul Peter Massao akimkaribisha Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei Makao Makuu ya Jeshi hilo.
Mazungumzo

MWANA FA PRESENTS THE FINEST.

0
0

Shule za Kata Zajiendesha kwa Fedha za Walimu Wakuu

0
0

 Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Rombo, Judethadeus Mboya
 Mkuu Msaidizi wa Sekondari ya Nduweni, Venance Mramba
Mkuu wa Sekondari ya Tanya, Victus Kiwango

=====  ======  =======
Shule za Kata Zajiendesha kwa Fedha za Walimu Wakuu

Na Thehabari.com, Rombo

CHAMA cha Walimu Tanzania (CWT), Wilaya ya Rombo kimesema shule nyingi za Sekondari za Kata wilaya hiyo na maeneo mengine nchini zinajiendesha kwa kutegemea fedha za mifukoni kwa walimu wakuu wanaoziongoza shule hizo. 

Kauli hiyo imetolewa jana na Katibu wa CWT Wilaya ya Rombo, Erasmo Mwingira alipokuwa akifanya mahojiano na mwandishi wa habari hizi. Hata hivyo uchunguzi uliofanywa na gazeti hili hivi karibuni kwa kutembelea shule kadhaa za sekondari wilayani hapa umebaini kuwepo na mazingira magumu ya uendeshaji wa shule hizo kutokana na ugao wa fedha za uendeshaji shule hizo kutokuwa wa uhakika huku hata kiasi kinachozifikia hakitoshelezi gharama za uendeshaji.

Akifafanua Mwingira alisema fedha zinazotolewa kuziendesha shule hizo 'capitation' licha ya kuwa hazitoshi huwa hazifiki kabisa shuleni hali ambayo huwafanya walimu wakuu kubuni mbinu mbalimbali za uendeshaji wa shule zao ikiwemo kuweka utitiri wa michango kwa wazazi ili kuhakikisha mambo yanakwenda shuleni.

"Sasa hivi shule za msingi na sekondari (za serikali) zinaendeshwa na mifuko ya walimu wakuu...capitation haifiki kabisa shuleni, fedha inayowafikia ni kidogo sana na haiwezi kuendesha zile shule, walimu wanatumia mbinu zao kuziendesha shule ndio maana unaona michango inakuwa mingi shuleni," alisema Mwingira.

Alisema licha ya serikali kusema ada ya sekondari ni shilingi 20,000 kwa sasa michango katika shule hizo ni mingi kiasi cha kufikia 120,000 jambo ambalo limewafanya baadhi ya wazazi kuelemewa na mzigo wa michango na wengine kushindwa kabisa kuimudu. 

Uchunguzi uliofanywa na mwandishi wa habari hizi katika shule za Sekondari za Tanya, Nduweni, Urauri, Holili na Ngaleku na nyinginezo zote za wilayani Rombo umebaini uwepo wa utitiri wa michango jambo ambalo limelalamikiwa na baadhi ya wazazi na wadau wa elimu wilayani hapa. Mfano shule ya Sekondari Tanya jumla ya michango yake imefikia sh. 115,000; mgawanyiko wake ukiwa kama ifuatavyo:- Ada sh 20,000, Madawati sh 15,000, Chakula sh 60,000, Tahadhari sh 5,000, Ulinzi 5,000, Taaluma sh 5,000 na Kitambulisho sh 5,000.

Aidha uchunguzi zaidi umebaini shule nyingi za sekondari za kata hazina walimu wa masomo ya sayansi jambo ambalo huwalazimisha walimu wakuu kutafuta walimu wa kukodi hasa wanafunzi waliomaliza kidato cha sita kuja kuwafundisha wanafunzi masomo ya sanyansi kama Hisabati, Fizikia, Kemia, Baiolojia na mengineyo huku wakitumia mbinu anuai kukusanya michango kuwalipa walimu hao wa kukodi.

"Nashauri Serikali iongeze fungu la uendeshaji wa fedha shuleni maana fedha za michango zinazotolewa na wazazi hazitoshi kuendesha shule...huwa tunakodi walimu (wanafunzi waliomaliza kidato cha sita) kuja kutufundishia masomo ya sayansi kwa muda unakuta gharama zinakuwa kubwa za uendeshaji shule," alisema Mkuu wa Sekondari ya Tanya, Victus Kiwango.

"Sisi tumelazimika kuajiri kwa muda wanafunzi sita waliomaliza kidato cha sita kufundisha masomo ya sayansi kwa fedha za shule...tunajibanabana kwa michango pamoja na wazazi na kuhakikisha tunapata chochote kuwalipa walimu hawa wa muda bila hivyo mambo hayaendi," alisema Mkuu Msaidizi wa Sekondari ya Nduweni, Venance Mramba akizungumza na mwandishi wa habari hizi.

Kwa upande wake Mwingira alisema vijana wa kidato cha sita ambao hutumiwa na shule nyingi kuokoa jahazi ya masomo ya sayansi wamekuwa wakiwakaririsha wanafunzi kujibu mitihani na sio kuwafundisha jambo ambalo alisema ni hatari kwa elimu ya Tanzania. "Kujua kusoma na kuandika si kigezo cha kumfundisha mtu...vijana hawa wa kidato cha sita hawana mbinu za ufundishaji wanachokifanya ni kuwakaririsha wanafunzi. Pamoja na hayo aliishauri serikali kutojitoa katika jukumu la kuendesha shule za kata na kuwaachia wazazi kwani shule hizo ziko katika hali mbaya na zinahitaji kuongezewa fedha za uendeshaji.

Akizungumzia suala hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Rombo, Judethadeus Mboya alikiri kuwepo na tatizo la upungufu wa walimu wa sayansi katika shule nyingi za wilaya yake, hivyo walimu kulazimika kuajiri kwa muda vijana wa kidato cha sita kusaidia wanafunzi huku jitihada zikiendelea kufanya kukabiliana na tatizo hilo.

"Walimu wa sayansi ni tatizo Rombo hawatoshi...mwaka huu tumejitahidi na kuajiri takribani walimu 134 wakiwemo wachache wa masomo ya sayansi lakini tatizo bado lipo," alisema Mboya kikilitolea ufafanuzi suala hilo ofisini kwake wilayani Rombo hivi karibuni.

Imeandaliwa na www.thehabari.com

workshop: Leadership Skills for the Global Marketplace

0
0
BTG Group LTD ( www.btgforafrica.com ) is holding a one-day workshop titled: Leadership Skills for the Global Marketplace. Attendees will receive training in:

Business Negotiations
Cultural Intelligence
Leadership Values
Cyber Security Management

The quality of your business's employees is directly related to the success of your organization. The strategies and topics covered during this workshop will give your employees the edge in advancing your business.

Date: Thursday 6, June 2013
Time: 9AM - 4PM
Location: Holiday Inn, Dar es Salaam, City Centre

For registration and details, please visit:
www.btgforafrica.com/workshop

We hope to see you there!

DK. ASHA-ROSE ATAJA MAAZIMIO YA KIKAO CHA KAMATI KUU YA CCM

0
0
DODOMA, Tanzania.

Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro, akizungumza na waandishi wa habari leo, Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma. Amezungumzia kuhusu yaliyojiri kwenye kikao cha Kamati Kuu ya CCM, kilichofanyika jana, pia mjini Dodoma. (TAARIFA NA PICHA NA BASHIR NKOROMO

TAARIFA KAMILI KAMA ILIVYOTOLEWA NA DK. ASHA-ROSE

Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ilifanya kikao chake cha kawaida mjini Dodoma Mei 21, 2013 chini ya Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete. Pamoja na mambo mengine Kamati Kuu ilijadili na kutafakari masuala mbali mbali yanayohusu Uchumi, Ustawi wa Jamii na Maendeleo ya Taifa.

MIGOGORO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI
Migogoro ya  wakulima na wafugaji imekuwa mingi na imeenea sana katika taifa letu. Migogoro hii inatokana na sababu nyingi: mabadiliko ya tabia nchi; ongezeko la idadi ya watu na mifugo. Kamati Kuu inasikitishwa na kuendelea kwa migogoro hii ambayo imekuwa tishio la amani na usalama katika jamii, na pia kusababisha wakulima kupata hasara baada ya mazao yao kuliwa na mifugo. Tumeishuhudia migogoro hii mkoani Morogoro hivi karibuni, katika ziara ya Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana na imeripotiwa katika maeneo mengine ya nchi yetu.

Kamati Kuu inaiagiza Serikali kuishughulikia na kuitafutia ufumbuzi wa kudumu migogoro hii. Kamati Kuu inaiagiza Serikali kuharakisha zoezi la kutenga maeneo kwa ajili ya wakulima na wafugaji na kujenga miundombinu ya malisho, maji, na majosho ili kuwezesha wafugaji kutohamahama na mifugo yao.

KULINDA HIFADHI
Kamati Kuu imezungumzia suala la mahusiano kati ya Hifadhi za taifa, wafugaji na wananchi waishio katika vijiji vinavyozunguka Hifadhi hizo. Kamati Kuu inatambua umuhimu wa Hifadhi kwa manufaa ya taifa letu na vizazi vijavyo. Inasisitiza msimamo wake wa kuzilinda Hifadhi za taifa sanjari na kuanzisha na kuendeleza mahusiano hayo.

Kamati Kuu inaiagiza Serikali kuwashirikisha wananchi katika kutenga maeneo ya Hifadhi, kulinda maeneo ya wanyama pori na kutenga maeneo ya malisho ili kuondosha migogoro isiyo ya lazima katika maeneo yanayozunguka Hifadhi.

ZAO LA KOROSHO
Kamati Kuu ilijadili matatizo yanayolikabili zao la korosho ambayo ni: kuyumba kwa bei ya korosho, malipo ya wakulima kuchelewa, tozo nyingi wanazolipishwa wakulima na udhaifu wa baadhi ya vyama vya ushirika.
Tatizo hili limedumu kwa muda mrefu na linastahili kushughulikiwa kwa njia ya kipekee.

Kwa kutambua kwamba wapo  baadhi  ya viongozi  na watendaji wa Serikali, viongozi wa vyama vya ushirika na  wafanyabiashara binafsi wanaochangia  katika kuendeleza matatizo yanayowakabili wakulima  wa korosho:

Kamati Kuu inatamka kwamba hali hii haivumiliki. Kamati Kuu inaitaka Serikali kukaa na wadau wote na kuchukua hatua zitakazotoa ufumbuzi wa kudumu wa matatizo haya kwa zao la korosho. Kamati Kuu pia inaitaka Serikali kuwachukulia hatua za kisheria  hao wote wanaochangia kuendelea kwa matatizo haya  kwa wakulima wa korosho.

MIGOGORO YA KIDINI
Kamati Kuu imepokea taarifa ya namna migogoro ya kidini inavyoshughulikiwa na hatua zinazochukuliwa. Kamati Kuu inaipongeza Serikali na vyombo vya dola kwa namna inavyoendelea kukabiliana na wahalifu wanaotumia mgongo wa dini kuanzisha vurugu na uvunjifu wa amani katika nchi yetu. Kamati Kuu inatoa mwito kwa Watanzania kukataa vitendo vyote vinavyochochea migogoro ya kidini; wananchi wajihadhari na watu waovu wenye nia mbaya ya kuligawa taifa letu.

Pamoja na jitihada za vyombo vya dola hadi sasa, Kamati Kuu inaitaka Serikali iandae mkakati wa kuzuia migogoro ya kidini kabla haijajitokeza.

MAKAMPUNI NA VIWANDA VILIVYOBINAFSISHWA
Kamati Kuu imetafakari hali ya viwanda hivi. Ni muongo mmoja umepita tangu ubinafsishaji ulipokamilika. Kuuzwa kwa mashirika na viwanda vya umma kwa watu na makampuni binafsi kumekuwa na matokeo ya aina mbili:  yako yale yaliyobinafsishwa na yakawa  na maendeleo mazuri na kuchangia uchumi wa Taifa. Na yako ambayo yanaendeshwa kwa kiwango cha chini au yamefungwa.

Kamati  Kuu inasikitishwa na hali hii, kwani viwanda vilivyofungwa ni vile vilivyokuwa vikifanya kazi muhimu ya uzalishaji.

Viwanda hivi ni vya korosho, usindikaji wa pamba, mafuta ya kula, viwanda vya mazao ya ngozi, na vinginevyo. Hali hii inalikosesha Taifa fursa za ajira, kukua kwa mapato, kuimarika kwa uzalishaji na kuongezeka kwa uuzaji wa bidhaa zilizosindikwa na kuzalishwa nchini.

Imedhihirika kuwa wafanyabiashara waliochukua viwanda hivyo ndiyo hao hao wanaofanya biashara ya kununua mazao ya kilimo na mifugo na kuuza nje kama bidhaa ghafi, wakati huo huo wakiwa wamevifunga viwanda hivi.

Kamati Kuu inaiagiza Serikali kufanya tathmini ya viwanda vilivyobinafsishwa ili kuvitambua vile vilivyofungwa, na kuwataka waliouziwa wavifungue na iwapo watashindwa kutimiza masharti yaliyowekwa, Serikali iandae utaratibu wa kuwapa watu wenye uwezo wa kuviendesha.

WAKULIMA WADOGO WA MIWA -
Kumekuwapo na migogoro ya muda mrefu kati ya wakulima wadogo wa miwa na Kiwanda cha Sukari cha Mtibwa mkoani Morogoro. Matatizo haya yameshughulikiwa na watendaji mbalimbali bila ya kupatikana kwa ufumbuzi wa kudumu.

Kamati Kuu inaiagiza Serikali kuushughulikia mgogoro huu na kuyapatia ufumbuzi wa kudumu matatizo ya wakulima wadogo wa miwa haraka iwezekanavyo.

PEMBEJEO ZA KILIMO.

Chama kimejiridhisha kuwa suala la utoaji wa pembejeo za kilimo ni zuri na lenye mafanikio. Hata hivyo Kamati Kuu imepokea taarifa kuhusu matatizo yanayohusiana na usambazaji wa mbolea ya ruzuku.
Kwa baadhi ya maeneo mbolea ya ruzuku imekuwa ikitolewa kwa watu wasiohusika na wakati mwingine walanguzi wamekuwa wakiingilia kati ili kujinufaisha nayo.
Kamati Kuu inaiagiza Serikali kusimamia kwa umakini na kutafuta utaratibu bora zaidi na wenye tija wa kuwafikishia wakulima mbolea, kwa wakati na kwa uhakika.

MRADI WA UJENZI WA NYUMBA ZA WATUMISHI.

 Kamati Kuu  imepokea taarifa na kuipongeza Serikali  kwa kutayarisha mpango kabambe wa ujenzi wa nyumba za watumishi wake. Mpango huu utatoa fursa kwa wafanyakazi ya kupata mikopo yenye masharti nafuu na hivyo kuwawezesha kuwa na makaazi yenye uhakika.

MWISHO: 
Kamati Kuu imeitaka Serikali  kuwasilisha utekelezaji wa maagizo haya mara kwa mara.

IMETOLEWA NA:
Asha-Rose Migiro, 
Katibu WA NEC – Siasa Na Uhusiano wa Kimataifa,
Mei 22, Dodoma.

VIDEO YA RAIS KIKWETE ALIPOZUNGUMZIA VURUGU ZA MTWARA JANA

0
0

Jmosi Hii Pale Arcade-Watch UEFA Final na Burudani Safi ya GrooveBack Djs.

0
0

majambazi yapora sayansi mataa-kijitonyama kweupeee jijini dar,risasi zarindima.

0
0

 Pichani ndio matundu ya risasi zilivyorindima kwenye kioo cha dereva (risasi tatu) na kushoto risasi moja kama kionekanavyo kioo cha juu,mara majambazi hayo kufanikiwa kumjeruhi dereva sehemu ya bega na kufanikiwa kunyakua begi linalosadikiwa kuwa,lilikuwa na kiasi cha fedha shilingi milioni 40 na kutokomea nazo.
Pichani kulia ni Askari Usalama barabarani akichukuliwa maelezo yake kutokana kushuhudia tukio la ujambazi lililofanyika maeneo ya Sayansi mataa-Kijitonyama jijini Dar mapema leo mnamo majira ya saa tano kasoro.

Ambapo kwa mujibu wa mashuhuda waliokuwepo eneo la tukio wanaeleza kuwa majambazi hao walikuwa wapatao wanne wakiwa wamepanda piki piki,ghafla wakasimama na kulizunguka gari aina Vitz yenye usajili wa namba T929 CCX (pichani chini) kwa haraka,mmoja wao akiwa na mashine gun na wengine walikuwa na bastola.

Mmoja wao alifyatua risasi hewani kumtaka dereva asimame na ashushe vioo vya gari yake,kufuatia hali ya utata wa majibishano ya muda mfupi majambazi hao waliifyatulia risasi kadhaa gari hiyo upande wa dereva, bahati mbaya wakamjeruhi sehemu ya bega,ndipo wakafanikiwa kuondoka na begi kubwa linalosadikiwa kuwa lilikuwa na kiasi cha fedha shilingi milioni 40 (kwa mujibu wa dereva aliempeleka majeruhi hospitali),mara baada ya majambazi hayo kutimka wasamalia wema wakamchukua dereva huyo aliyekuwa akigugumia kwa maumivu ya jeraha lake na kumtafutia tax na hatimae kumkimbiza hospitali ya Kairuki kwa huduma ya haraka.
 Baadhi ya watu wakijaribu kubadilshana mawazo kwa kulitafakari tukio hilo la ujambazi.
 Gari iliyokuwa imevamiwa na majambazi ikikokotwa na gari la polisi mara baada ya kushindwa kuwaka.

India inajulikana kwa lipi zaidi?!

0
0

India inajulikana kwa lipi zaidi? Movies(Bollywood), shule bora au matibabu?? Sasa Airtel ya kuwezesha kulonga zaidi na walio india kwa bei nafuu,Kwa tsh 3000 tu utapata dakika 25, za kuwasiliana wiki nzima.
kujiunga piga*149*13# upate kuwasiliana kwa bei poa ya shilingi 2 kwa sekunde . Airtel Yatosha!!

Wakulima sasa kupata taarifa za kilimo kupitia simu

0
0
Balozi wa Finland nchini Tanzania, Sinikka Antila akisalimiana na Afisa maendeleo ya Biashara wa Vodacom Tanzania Nixon Bonaventure wakati wa hafla ya kuanzisha Ushirikiano kati ya kampuni hiyo na kampuni ya Sibenonke ya nchini Finland. Pamoja nao katika picha ni Waziri wa Mahusiano ya Ulaya na Biashara za kimataifa Alexander Stubb (katikati). Waziri wa maendeleo ya kimataifa Heidi Hautala ( wa pili kutoka kushoto) na Mkurugenzi wa kampuni ya Sibenonke Uwe Schwarz. Hafla hiyo ilifanyika nyumbani kwa balozi huyo.
Waziri wa mahusiano ya Ulaya na Biashara za kimataifa wa Finland, Alexander Stubb, akifanya mahojiano na Meneja Mahusiano wa Vodacom Tanzania, Bw.Matina Nkurlu katika hafla ya kuingia katika Ushirikiano utakao wawezesha wakulima kupata taarifa za kilimo kupitia simu za mkononi. Pamoja nao ni Waziri wa maendeleo ya kimataifa Heidi Hautala (wa pili kutoka kulia) na Mkurugenzi wa kampuni ya Sibenonke Uwe Schwarz.



==== ======== ========== 

Wakulima sasa kupata taarifa za kilimo kupitia simu



*       Ni kufuatia ushirikiano kati ya Finland na Vodacom
*       Sera ya Kilimo kwanza kuongezewa tija zaidi




Waziri wa Mahusiano ya Ulaya na Biashara za kimataifa wa Finland Alexander Stubb, amesema kuwa nchi yake sasa itawekeza zaidi katika kuwainua wakulima wadogo wa Tanzania kwa kuwawezesha kupata elimu, taarifa na mafunzo mbalimbali ya kilimo na ufugaji kupitia maendelea ya teknolojia.

Hayo yametanabaishwa na Waziri huyo wakati wa hafla ya kuingia katika Ushirikiano kati ya Kampuni ya Sibenonke ya nchini Finland na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom makubaliano yatakayo wawezesha wakulima kupata taarifa mbalimbali za kilimo kwa njia ya simu.

Waziri huyo amesema kuwa nchi yake imekuwa ikishirikiana na serikali ya Tanzania katika masuala mbalimbali na kwa sasa wameona ni vyema kuwekeza zaidi katika kuwasaidia wakulima wadogo ambao pia wamepewa kipaumbele na serikali kupitia sera yake ya Kilimo kwanza.




"Tanzania tangu awali imekuwa kilimo kama uti wa mgongo katika kujenga na kuliendeleza taifa,  tumetambua kuwa jitihada za kuwaendeleza wakulima zimekuwa zinakabiliwa na changamoto mbalimbali hasa upatikanaji wa taarifa muhimu, Ushirikiano huu sasa utawawezesha wakulima kupata taarifa hizo katika viganja vyao na kwa wakati wowote," alisema Stubb.




Aidha Waziri wa maendeleo ya kimataifa wa nchi hiyo, Heidi Hautala amesema kuwa ni vyema sasa wakulima wa Tanzania wakabadilika kwa kufanya kilimo cha kisasa na chenye tija. 
"Tanzania kwa kipindi kirefu imekuwa inafanya jitihada kubwa kuwainua wakulima, nasi kwa kushirikiana na kampuni na wadau wengine kutoka nchini Finland tumekuwa tukiwaunga mkono kuhakikisha inawasaidia wakulima kutumia teknolojia za kisasa, Ushirikiano huu utakuwa ni chachu kwa maendeleo ya wakulima wa Tanzania kwani sasa watarahisishiwa kupata taarifa za namna bora ya kuendesha kilimo," Alisema Hautala.



Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Rene Meza, amesema kuwa kuendelea kuwepo kwa miundombinu hafifu ya barabara na mawasiliano imekuwa kikwazo kwa wakulima kupata taarifa muhimu za kilimo na mafunzo, Ushirikiano huu wa Vodacom na Sibenonke utakuwa suruhisho kubwa katika kukabiliana na changamoto hizo za kipindi kirefu.




Twissa, aliongeza kuwa Kampuni ya Vodacom imekuwa katika jitihada za kutafuta njia bora katika kuboresha maisha ya Watanzania kupitia mtandao wake uliosambaa nchini kote. " Tunafuraha na faraja kuingia katika Ushirikiano na kampuni hii ya Sibenonke," alisema. "Maendeleo ya kilimo yamekuwa na changamoto kubwa kwa taifa hili, mpango huu wa kutoa taarifa kwa wakulima kupitia njia ya simu utakuwa na mchango mkubwa katika kuboresha sekta hii, tunawasihi Watanzania kutumia fursa hii ya kiteknolojia katika kuboresha kilimo nchini na pia kukuza uchumi wa nji yetu", alifafanua Twissa.




Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Sibenonke,  Uwe Schwarz, amesema ushirikiano huo na kampuni ya Vodacom Tanzania, umekuwa sehemu ya kuendelea kupanuka kwa mtandao wa huduma kwa kampuni hiyo katika ukanda wa Afrika ya Mashariki ambako maendeleo ya teknolojia yameendelea kuwa changamoto kwa muda mrefu.




 "Tunayo furaha kubwa kuingia katika ushirikiano huu na kampuni ya Vodacom katika kuwarahihishia huduma wakulima wa Tanzania, Tunaamini kuwa kwa pamoja tutaleta mapinduzi makubwa katika kilimo kwa kuongeza tija katika uzalishaji na mazao na usalama wa chakula. Suruhisho letu hili lisilo na gharama yoyote italeta maendeleo makubwa kwa Watanzania.




Mwenyekiti wa MOAT bwana Reginald Mengi, amesema kuwa vyombo vya habari vimefanya jitihada kubwa katika kufikisha taarifa kwa wakulima lakini bado changamoto imekuwa kubwa kuwafikia wote kulingana na maeneo waliyopo hivyo kwa Ushirikiano huu anaamini kuwa sasa taarifa zote za msingi zitawafikia wakulima hata walio katika maeneo yasiyofikiwa na vyombo vya habari.




"Ninawapongeza sana Vodacom kwa kuona umuhimu wa kuingia katika ushirikiano huu ambao unaleta mapinduzi katika sekta ya kilimo nchini. Sisi kama wadau wa vyombo vya habari tumefanya kazi kubwa hivyo kwa kutumia mtandao wa Vodacom ambao umesambaa nchini kote wakulima sasa wataweza kupata taarifa wanazohitaji kupitia simu zao za Mkononi, Alisema Bwana Mengi.

EXIM BANK SCOOPS BEST FINANCIAL INSTITUTIONS EXHIBITORS AWARD AT TANGA TRADE FAIR

0
0
The Minister for Industry and Trade Dr. Abdallah Kigoda (second left) hands over an award to the Exim Bank Tanzania –Tanga Branch Manager Deogratus Makwaia after emerging best exhibitor in the financial institutions Category during the just concluded Tanga Trade Fair.

GHANA, KENYA KUTINGA FAINALI GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE

0
0

  
 
Naab Jonathan Baan& Desmond Odaano: .Washindi wa kwanza wa nusu fainali ya kwanza ya Guiness Football Challengekutoka Ghana Naab Jonathan Baan(kushoto) na Desmond Odaano(kulia) katika picha ya pamoja na waendeshaji wa kipindi cha Pan-Africa Guinness Football Challenge Larry Asego na Mimi Kalinda.
Francis Wangari& Kepha Kimani: Washindi wa pili wa nusu fainali ya kwanza ya Guiness Football Challenge Francis Wangari(kushoto) na  Kepha Kimani(kulia) kutoka Kenya  katika picha ya pamoja na waendeshaji wa kipindi cha Pan-Africa Guinness Football Challenge Larry Asego na Mimi Kalinda.

=======  ======  =======


Dar es Salaam: Jana usiku kupitia televisheni za ITV na Clouds TV nusu fainali ya kwanza kabisa ya GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE™ ilirushwa hewani na katika runinga Afrika nzima   ambapo timu ya Ghana ilionesha ni kwanini  ni timu bora ambayo ndiyo imejishindia pesa nyingi mpaka sasa.

Jonathan Nabb na Desmond Odaano walionesha  uwezo na  ujasiri wao walipoibuka washindi zidi ya wapinzani wao timu kutoka Kenya katika mchezo wa jana. 

Katika hatua ya pesa ukutani walifanikiwa kulenga lango namba nne na hivyo kupata dola za kimarekani 12,000 wanazoziongeza katika dola 8,500 walizokuwa nazo awali katika hatua ya robo fainali.

Wakenya Francis Ngigi na Kepha Kimani ambao ni washindi wa pili katika nusu fainali hii wataungana na Ghana katika fainali. Ingawa waliikosakosa hatua ya ukuta wa pesa wa Guinness bado wana nafasi ya kuwa mabingwa katika fainali.

Marehemu Chinua Achebe kuzikwa leo Nigeria

0
0

Mwili wa mwandishi mashuhuri wa vitabu barani Afrika Chinua Achebe umewasili nyumbani kwake katika jimbo la Anambra nchini Nigeria.
Hafla mbali mbali zimekuwa zikiandaliwa nchini Nigeria kumuenzi bwana Achebe.
Mwandishi huyo mashuhuri alifariki mjini Boston,Marekani, akiwa na umri wa miaka 82 baada ya kuugua kwa muda mfupi. Jamaa na maafisa wa serikali walikuwa katika uwanja wa ndege Kusini mwa Nigeria kumpokea marehemu.
Hayati Achebe, anasifika sana kwa kuwa mwanzilishi wa fasihi ya kiafrika kwa kiingereza.  Kitabu chake alichokianda cha kwanza, mwaka 1958, Things Fall Apart, ambacho kilizungumzia sana athari za ukoloni barani Afrika, aliweza kuuza zaidi ya vitabu milioni kumi.
Mwandishi huyo na msomi, aliendelea na uandishi wake na kuandika vitabu vingine 20 baadhi vikikosoa sana wanasiasa na kile alichokitaja kama ukosefu wa uongozi nchini Nigeria.
Alikuwa anaishi nchini Marekani tangu mwaka 1990 baada ya ajali ya barabarani kumjeruhi kiasi cha kumlemaza. Makundi ya kitamaduni yalifanya tamasha mbali mbali nje ya uwanja wa ndege wa Enugu, huku ndege iliyokuwa inambeba marehemu Achebe ilipotua.
Inaarifiwa kuwa licha ya kuwa watu wana majonzi tele, lakini pia wanasherehekea maisha ya mwandishi huyo. Achebe atazikwa karibu na nyumbani kwa familia yake mjini Ogidi, mji mdogo kwenye vilima vya jimbo la Anambra.Habari kwa hisani ya BBC Swahili.

Rais Kikwete amwapisha Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria na Mabalozi Wapya wanne

0
0
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Makamu wa Rais Dkt.Mohamed Gharib Bilal  na Waziri wa Mambo ya Nje Bernard Membe wakiwa katika picha ya pamoja na mabalozi wapya waliopaishwa leo ikulu jijini Dar es Salaam.aliyesimama mbele kushoto no Balozi Liberata Mulamula anayekuwa Balozi Mpya wa Tanzania nchini Marekani.

Waliosimama nyuma kutoka kushoto ni Balozi mpya wa Tanzania Uholanzi Wilson Masilingi,Balozi mpya wa Tanzania katika visiwa vya Commoro Chabaka Kilumanga,Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania Umoja wa Mataifa Geneva Balozi Modest jonathan Mero na Balozi mpya wa Tanzania katika falme za Kiarabu(UAE)Mbarouk Nassor Mbarouk.Kabla ya uteuzi Balozi Liberata Mulamula alikuwa msaidi wa Rais Masuala ya kidiplomasia na aliwahi kuwa katibu mkuu wa nchi za  Maziwa Makuu.(picha na Freddy Maro).
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete leo ikulu jijini Dar es Salaam amemwapisha Jaji  Aloycius Mujuluzi kuwa Mwenyekiti wa  tume ya kurekebisha sheria pamoja na mabalozi wanne watakaoiwakilisha Tanzania nje ya nchi.Mabalozi walioapishwa leo ni pamoja na Balozi mpya katika umoja wa Falme za kiarabu(UAE) Mbarouk Nassor Mbarouk,Balozi mpya wa Tanzania nchini Uholanzi Wilson Masilingi,Balozi mpya wa Tanzania katika visiwa vya Commoro Chabaka Kilumanga na Mwakilishi wa  kudumu Tanzania Umoja wa mataifa Geneva Balozi Modest Jonathan Mero.
Balozi Masilingi-Uholanzi akiapa
Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (UAE) akiapa.
Balozi Mero-Geneva akiapa
Balozi Kilumanga-Commoro Akiapa

mkutano wa kamati ya kitaifa ya wataalam ya mabadiliko ya tabia nchi unaendelea mjini zanzibar.

0
0

Bw Sihaba Vuai afisa mazingira ofisi ya makamu wa kwanza wa rais zanzibar akizungumza kuhusu hali ya mazingira na zanzibar na mathara yatokanayo na mabadiliko ya tabia nchi katika mkutano wa kamati ya kitaifa ya wataalam ya mabadiliko ya tabia nchi unaoendelea mjini zanzibar. 
Wanakamati ya kitaifa ya kitaalam ya mabadiliko ya tabia nchi wakimsikiliza mtoa mada hayupo pichani katika mkutano unaoendelea mjini zanzibar (Picha na Evelyn Mkokoi) 

RAIS Jakaya Kikwete ATHIBITISHIA UMMA KWAMBA PSPF IKO IMARA NA HAITAKUFA‏

0
0

 Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa PSPF Ndugu. Adam H. Mayingu  tuzo ya kuwa Mfuko wa kwanza wa Hifadhi ya Jamii Tanzania kutoa mikopo ya nyumba kwa wanachama wake.  

Tuzo hiyo ilitolewa kwenye maadhimisho ya kilele cha Wiki ya Mifuko ya Jamii mjini Dodoma.  Mh. Raisi alisema PSPF ni mfuko madhubuti na una fursa nyingi za kimaendeleo kwa wananchi wa Tanzaniai na unauwezo mkubwa na salama katika uwekezaji .  

Aliongezea kwa kusema sio kweli kwamba Mfuko huu uko mahututi kama ilivyozungumziwa kwenye baadhi ya vyombo vya habari, bali Mfuko huu unadai wadai wake Trilioni 6 na kudai sio kufilisika tena. 

 1.   Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Jakaya Mrisho Kikwete akisoma kipeperushi cha nyumba za PSPF zinazokopeshwa kwa wanachama wa Mfuko huo, huku akimsikiliza Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa  Mfuko huo ndugu Adam H. Mayingu akimuelezea kuhusu nyumba hizo na fursa zingine zilizopo PSPF kwa Watanzania ikiwa ni pamoja na ujumbe kwa Watanzania kwamba mtu yeyote mwenye umri usiopungua miaka 18 anaweza kuwa mwanachama wa PSPF

  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF ndugu Adam H. Mayingu akimuelezea Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema J. Nchimbi kuhusu shughuli za Mfuko na fursa zilizopo kwa watanzania hususani mikopo ya nyumba na mafao ya aina mbalimbali ikiwemo fao la Ujasiliamali na Elimu.

   Mtangazaji wa TBC Amina Mollel akikabidhi fomu ya kujiunga na PSPF kwa Meneja Masoko wa Mfuko huo Bi. Costantina Martin mala baada ya kuvutiwa na kukata shauri ya kuwa mwanachama wa Mfuko wa kwa njia ya uchangiaji wa hiari

 Timu ya PSPF iliyokuwa kwenye maonyesho ya wiki ya hifadhi ya Jamii wakiwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wao ndugu Adamu Mayingu katikati.  Timu hiyo inastahili pongezi kutokana na uduma bora waliyokuwa wakiitoa kwa wananchi waliokuwa wakitembelea banda hilo la PSPF pale Nyerere squire Dodoma.

Wanachama wa PSPF wakipata taarifa mbalimbali ikiwapo historia ya michango yao na taarifa za uanachama.
Viewing all 46205 articles
Browse latest View live




Latest Images