Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 883 | 884 | (Page 885) | 886 | 887 | .... | 1897 | newer

  0 0


   Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais -TAMISEMI, George Simbachawene  akipokea hundi ya Shilingi  Milioni 39 kutoka DCB Benki kwa ajili ya kununulia Madawati, leo jijini Dar es Salaam.
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais -TAMISEMI, George Simbachawene  akikata utepe kuzindua  Tawi la Benjamin Mkapa City, leo jijini Dar es Salaam.
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais -TAMISEMI, George Simbachawene  akizungumza na wadau mbalimbali  wakati wa uzinduzi wa Tawi la Benki ya DCB linaloitwa Benjamin Mkapa-City.leo jijini Dar es Salaam.

   Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya DCB Benki Balozi, Paul Rupia akizungumza katika uzinduzi huo ulio fanyika leo jijini Dar es Salaam, Wakati wa Uzinduzi wa Tawi hilo.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais -TAMISEMI,
  George Simbachawene  akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa DCB Benki leo jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah J. Kairuki (MB.)(Pichani) amewataka Watumishi wa Umma nchini waliopewa dhamana serikalini kutekeleza majukumu yao kwa weledi mkubwa ili kuepuka malalamiko yasiyo ya lazima kwa wanaowahudumia.

  Waziri Kairuki aliyasema hayo jana alipokuwa akizindua Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwa mwaka 2016 mkoani Singida.

  “Najua miongoni mwa watumishi wa umma wapo watumishi waliopewa dhamana lakini utoaji wao wahuduma unatiliwa shaka. Hawapendi kusikiliza matatizo ya wateja wa ndani yaani watumishi wenzao,” Mhe. Kairuki alisema.

  Amewataka watumishi wenye tabia hizo kuacha mara moja na kuishi maisha ya kazi kama Mkataba wa Huduma kwa Mteja unavyowaongoza katika kutoa huduma kwa kiwango kwa wateja wote wa ndani na nje ya taasisi.

  Aidha, Mhe. Kairuki amewataka Watendaji kutenga muda wa kukaa na watumishi wao ili kusikiliza kero na changamoto zinazowakabili kwa lengo la kuzitafutia ufumbuzi.

  “Uzoefu unaonyesha kuwa watumishi wanaposhirikishwa katika masuala yanayowagusa kama tulivyo hapa basi huduma kwa wananchi na wadau wengine zitaboreka na kazi kufanyika kwa ari na hivyo kuongeza tija na ufanisi kazini,” Waziri Kairuki aliongeza.

  Katika hatua nyingine, Mhe. Kairuki alifanya ziara katika Chuo cha Utumishi wa Umma tawi la Singida na kuzungumza na watumishi wa chuo hicho ambapo aliwataka watumishi hao kuwa wabunifu katika kutekeleza majukumu yao na kuwajibika ili kuleta matokeo bora kwa taifa.

  “Tuwewabunifu, tuangalievipaumbele, tufundishe kozi ambazo hazifundishwi sehemu nyingine ili kuweza kupata soko zuri zaidi,” Waziri Kairuki alisisitiza.

  Aliwasisitiza watumishi hao kuwa na ushirikiano na vyuo mbalimbali hasa katika nyanja za utafiti, mafunzo na masuala mengine ya maendeleo ili kuboresha chuo hicho.

  Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma ambayo hufanyika kuanzia tarehe 16-23 Juni, kila mwaka, kwa mwaka 2016 yanafanyika kwa namna tofautia mbapo Viongozi na Watendaji wanakutana na wateja wao wa ndani na nje ya taasisi zao kwa lengo na kusikiliza kero zao na kuzitafutia ufumbuzi.

  Katika kutekeleza hilo, Mhe. Kairuki amezindua maadhimisho hayo kwakufanya vikao kazi na watumishi wa mkoa wa Singida kutoka katika kada mbalimbali za utumishi wa umma.
  Kauli Mbiu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma Barani Afrika kwa mwaka 2016 ni “Uongozi wa Umma kwa ukuajiJumuishi: kuelekea katika Afrika tunayoitaka.”

  Kaulimbiu hiyo inaambatana na kaulimbiu ndogo ambazo ni: Mchango wa Utumishi wa Umma katika Ukuaji wa Uchumi Barani Afrika na Mchango wa Utumishi wa Umma katika Kuiwezesha Ajenda ya Afrika ya 2063 ambayo inaweka mkazo katika Maendeleo ya Afrika na Haki za Wanawake.

  0 0


  Katika kusherekea siku maalum ya mtoto wa Afrika ambayo hufanyika Juni, 16 ya kila mwaka, Kamati ya Miss Universe Tanzania kupitia mpango wake mpya uitwao Binti Jasiri ilikutanisha kwa pamoja watoto 90 kutoka vituo mbalimbali vya mkoa wa Dar es Salaam ambapo halfa hiyo ilihudhuliwa na Miss Universe Tanzania 2015, Lorraine Marriot na mgeni rasmi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

  Akizungumza na watoto hao, Makonda aliwambia kuwa serikali ya awamu ya tano inawathamini watoto na hata kuwawekea elimu bure hivyo waongeze juhudi katika masomo yao ili nao waweze kuja kuwa na maisha mazuri na hata kuwasaidia wengine kama jinsi wao wanavyosaidiwa na watu wengine ambao wamefanikiwa.

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na watoto kutoka vituo mbalimbali vya kulea watoto kutoka mkoa wa Dar es Salaam katika halfa maalum ya kusherekea siku ya mtoto wa Afrika, Kushoto ni Miss Universe Tanzania 2015, Lorraine Marriot. (Picha zote na Rabi Hume, MO Blog).

  “Watu wenye maisha mazuri wasiwachanganye hata nyie mnaweza kuwa na maisha mazuri hata zaidi yao, mnatakiwa muongeze bidii katika masomo yenu ili na nyie mfanikiwe na kuwasaidia wenzenu kama jinsi mnavyosaidiwa na wengine kwa sasa,” alisema Makonda.

  Nae Miss Universe Tanzania 2015, Lorraine Marriot ambaye pamoja na kupata chakula cha pamoja na watoto hao pia alipata nafasi ya kuzungumza nao mambo mbalimbali kuhusu maisha, kuwashauri na kuwatia moyo ili waongeze bidii katika masomo yao na hata baadae waweze kufanikiwa kimaisha.

  Halfa hiyo ilisimamiwa na Magdalena Gisse na kuhudhuliwa na watoto kutoka Kituo cha Malaika Kids Orphanage, Kurasini Orphanage, Sarafina Orphanage na Makini Orphanage vyote kutoka mkoa wa Dar es Salaam.

  Na Rabi Hume, MO Blog
  Watoto wakimpigia makofi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda baada ya kumaliza kuzungumza nao katika halfa maalum ya kumbukumbu ya mtoto wa Afrika iliyofanyika katika Hoteli ya Golden Tulip.

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akimsalimu mmoja wa watoto waliohudhulia halfa maamul ya kumkumbuka mtoto wa Afrika, Aliyembeba mtoto huyo ni Miss Universe Tanzania 2015, Lorraine Marriot na katikati ni Mkurugenzi Kitaifa wa Miss Universe Tanzania, Maria Sarungi Tsehai.

  Watoto mbalimbali waliohudhuria halfa hiyo wakifurahi kwa pamoja.

  Baadhi ya watoto waliohudhuria halfa hiyo walio na imani ya Kiislamu wakisali.

  Meneja wa Taasisi ya Mo Dewji, Barbara Gonzalez akifuturu kwa pamoja na watoto kutoka vituo mbalimbali waliohudhuria halfa maalum ya kumbukumbu ya mtoto wa Afrika.

  Miss Universe Tanzania 2015, Lorraine Marriot akifuturu kwa pamoja na watoto waliohudhuria katika siku maalum ya kumbukumbu ya mtoto wa Afrika iliyofanyika katika Hoteli ya Golden Tulip.

  Miss Universe Tanzania 2015, Lorraine Marriot akimlisha mmoja wa watoto waliohudhuria halfa maalum ya kumkumbuka mtoto wa Afrika.

  Watoto mbalimbali waliohudhuria halfa hiyo wakifuturu na kujiburudisha na vinywaji kutoka Kampuni ya Mohammed Enterprises ambayo ilijitolea vinywaji katika halfa maalum ya kumkumbuka mtoto wa Afrika.
  Miss Universe Tanzania 2015, Lorraine Marriot akiwa katika picha ya pamoja na watoto waliohudhuria halfa hiyo.

  Meneja wa Taasisi ya Mo Dewji, Barbara Gonzalez akifurahi na watoto waliohudhuria halfa hiyo kwa kuwaonyesha jinsi mtandao wa kijamii wa Snapchat jinsi unavyotumika.

  Miss Universe Tanzania 2015, Lorraine Marriot akizungumza na watoto waliohudhuria halfa hiyo.

  Mmoja wa watu waliokulia katika kituo cha kulelea watoto cha DogoDogo, Dk. Yusuph akiwatia moyo watoto hao na jinsi ambavyo wanaweza kufanya ili na wao waweze kufanikiwa kama ilivyo kwake.

  Msimamizi wa halfa hiyo, Magdalena Gisse akiwashukuru watoto waliohudhuria halfa hiyo.

  Miss Universe Tanzania 2015, Lorraine Marriot akiwasaidia watoto kufungua maputo baada ya halfa hiyo kumalizika.

  Meneja wa Taasisi ya Mo Dewji, Barbara Gonzalez akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watoto waliohudhuria halfa maalum ya kumkumbuka mtoto wa Afrika iliyofanyika katika Hoteli ya Golden Tulip. Washiriki wa halfa maalum ya mtoto wa Afrika wakiwa katika picha ya pamoja.

  0 0


  Mhe. Wilson M. Masilingi, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Marekani akiwa na Bw. Makala Jasper alipotembelea ofisi za Ubalozi.

  Bw. Makala Jasper, Mkurugenzi Mwandamizi wa NGO ya Mpingo Conservation & Development Initiative (MCDI) ametunukiwa tuzo ya National Geographic Society/Buffett Award forLeadership in African Conservation. 


  Pichani: Rais wa National Geographic Society Bw. Gary E. Knell mara baada ya kumkabidhi Bw. Makala Jasper tuzo. Kulia ni Mhe. Balozi Wilson M. Masilingi na Bi.

  Bw. Makala Jasper akitoa shukurani kwa kupewa tuzo

  National Geographic Society/Buffett Award for Leadership in African Conservation


  Bw. Gary Knell akiwa na Bi. Mounia Mechbal, Mwakilishi wa Rolex, Bw. Lee Berger mshindi wa tuzo ya Explorer of the Year, na Terry Garcia, Mkuu wa Masuala ya Sayansi na Utafutaji, National Geographic

  Bi. Pasang Akita akipokea tuzo ya Adventurer of the Year

  Pichani katikati: Washindi wa Tuzo ya Hubbard Medal Bw. Nainoa Thompson na Bi. Meave Leakey

  0 0

  Ziara ya Kikundi cha Wajasiriamali Wanawake kutoka Tanzania (Tanzania Saccos for Women Enterprenuers) imezaa matunda baada ya kikundi hicho cha kina mama kufanikiwa kuingia mkataba wa ushirikiano (MoU) katika masuala ya biashara na Kukundi cha Wanawake Wajasiriamali wa Comoro (Association of Women Entrepreneurs in Comoro).

  Makubaliano hayo ya ushirikiano yalifikiwa kufuatia ziara ya siku mbili iliyofanywa na Kikundi cha Wajasiriamali Wanawake kutoka Tanzania nchini Komoro tarehe 14 Juni 2016. Lengo la ziara hiyo ilikuwa kutafuta masoko kwa ajili ya bidhaa za Tanzania nchini Komoro, pamoja na kukutana na wajasiriamali wa Komoro ili kuweza kubadilishana taarifa juu ya fursa mbalimbali za biashara kati ya Tanzania na Komoro.

  Tukio hilo la utiaji saini wa makubaliano ya ushirikiano baina ya vikundi hivyo vya Wajasiriamali akina mama kutoka Tanzania na Komoro lilishuhudiwa na Balozi wa Tanzania nchini Komoro Mhe. Chabaka F. Kilumanga. Katika hafla hiyo, Mhe. Balozi Kilumanga aliwapongeza wajasiriamali hao kwa hatua hiyo muhimu waliofikia na kuwa ana imani ushirikiano huo utakuwa ni wakudumu na wenye manufaa kwa pande zote mbili. Alieleza kuwa Tanzania na Komoro zinaweza kushirikiana katika nyanja mbalimbali za biashara na ana imani kuwa hii itakuwa ni chachu kwa wawekezaji wengine kutoka Tanzania kuja nchini Komoro kwa ajili ya kuekeza.

  Bi. Naila Thabeet wa Association of Women Enterpreneurs akibadilishana mkataba na Bi. Anna Matinde kutoka Tanzania Saccoss for Women Enterprenuers.

  Wadua wakishuhudia tukio la kihistoria ambapo ni mara ya kwanza vikundi vya akina mama kutoka Komoro na Tanzania wamekubaliana kushirikiana katika nyanja za biashara.

  0 0


  Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amosi Makalla mwenye miwani akitizama maendeleo ya ujenzi wa daraja Mbaka katika kijiji cha Kibhundughulu wilayani Rungwe Mkoani Mbeya ambalo ujenzi wake ulikwama kutokana na ukosefu wa fedha hali ambayo iliwalazimu wananchi wa kijiji hicho kupita juu ya daraja hilo kwa kutumia kamba kitendo ambacho kilikuwa kikihatarisha maisha yao.(PICHA E.MADAFA JAMIIMOJABLOG) .
  Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amosi Makalla mwenye miwani akijaribu kupita kwa lengo kukagua maendeleo ya ujenzi wa daraja la Mbaka katika kijiji cha Kibhundughulu katika Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe ambalo ujenzi wake ulianza toka mwaka 2015 na ulishindwa kukamilika kutokana na ukosefu wa fedha kiasi cha shilingi milioni 58 ambapo katika ziara hiyo mkuu huyo wa mkoa wa mbeya aliambatana na baadhi ya viongozi wa halmashauri hiyo.
  Mafundi wa kampuni ya Richer Ivestment ya Mkoani Mbeya ambao ndio wanajenga daraja hilo wakiendelea na ujenzi daraja hilo ambapo hadi kukamilika kwakwe linataji kukagharimu kiasi cha shilingi milioni 58 .
  Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amosi Makalla akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Kibhundughulu Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya ambao ndio watumiaji wa daraja hilo la Mbaka ambalo lilikwama kukamilika kutokana na ukosefu wa fedha hali iliyopelekea wananchi wa kuanza kutumia daraja hilo kwa kupita juu kwa kutumia kamba hali ambayo iliatalisha maisha yao.

  Katika mkutano huo Mkuu huyo wa Mkoa aliwataka wananchi wa kijiji hicho kuwapa ushirikiano mafundi wanaojenga daraja hilo ili liweze kukamilika kwa wakati .Aidha Makalla amekemea baadhi watu wasio waaminifu ambao walikuwa wakipita juu ya daraja hilo kabla ya kukamilika kwakwe kitendo ambacho kilikuwahatari kwa maisha ya wananchi hao.Aidha amemtaka mkarandasi anaye jenga daraja hilo kuhakikisha anakamilisha ujenzi huo katika kipindi cha wiki mbili ili kutoa fursa kwa wananchi hao kuanza kulitumia .
  Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amosi Makalla akisiadiana na mafundi wa kampuni ya Richer Investment ambao wanajenga daraja la Mbaka kwa kiasi cha fedha shilingi Milioni 58 mara baada ya kuzungumza na wananchi wa kijiji cha Kibhundughulu ambao ndio watumiaji wa daraja hilo.
  Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Mbaka Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe wakikatiza katika ya mto kutokana na Daraja walilokuwa wakitumia kuzuiwa na serikali ili kupisha ujenzi wake.

  0 0


  Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Hawa Ng’humbi akizungumza na baadhi ya wataalam wa masuala ya maafa walipomtembelea ofisini kwake ili kufanya tathimini ya utekelezaji wa mradi wa Kuijengea Jamii Uwezo wa Kujiandaa na Kupunguza Athari za Maafa katika Maeneo yaliyoathirika na Ukame Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Juni 16, 2016.
  Mnufaika wa mradi wa Kuijengea Jamii Uwezo wa Kujiandaa na Kupunguza Athari za Maafa Bi. Juliana Peter akifurahia mbuzi wa mradi huo wakati wa zoezi la Tathimini ya utekelezaji wa mradi huo lililofanywa na Wadau wa masuala ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Juni 16, 2016.
  Mratibu wa Kitaifa wa Mradi wa Kuijengea Jamii Uwezo wa Kujiandaa na Kupunguza Athari za Maafa katika Maeneo yaliyoathirika na Ukame Bw.Harrison Chinyuka (wa kwanza kulia) akifuatilia mtoa mada (hayupo pichani) wakati wa kikao cha Kujadili utekelezaji wa mradi huo, Wilaya ya Kishapu tarehe 16 Juni, 2016.
  Baadhi ya wanakikundi cha Muungano wakifurahia mafanikio ya kuongezeka kwa mbuzi ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Mradi wa Kuijengea Jamii Uwezo wa Kujiandaa na Kupunguza Athari za Maafa wakati wa tathimini ya utekelezaji wake iliyofanywa na Idara ya Maafa Ofisi ya Waziri mkuu tarehe 16 Juni, 2016 Wilaya ya Kishapu Shinyanga.
  Mmoja wa wanachama wa kikundi cha Mazingira Bi. Juliana Peter akichangia hoja wakati wa kikao cha tathimini ya utekelezaji wa Mradi wa Kuijengea Jamii Uwezo wa Kujiandaa na Kupunguza Athari za Maafa chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Juni 16, 2016.

  0 0


  0 0

  JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA.
  WATU NANE WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI BAADA YA KUKAMATWA NA POMBE AINA YA GONGO KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA MAENEO YA LUCHELELE WILAYANI NYAMAGANA.

  KWAMBA MNAMO TAREHE 16.06.2016 MAJIRA YA SAA MAJIRA YA SAA 14:00HRS KATIKA ENEO LA LUCHELELE WILAYA YA NYAMAGANA MKOA WA MWANZA, ASKARI POLISI WALIFIKA KATIKA ENEO HILO TAJWA NA KUFANYA MISAKO PAMOJA DORIA NAKUWEZA KUFANIKIWA KUKAMATA WATU NANE WAKIWA NA POMBE AINA YA GONGO PAMOJA NAMITAMBO YA KUTENGENEZEA POMBE HIYO KITENDO AMBACHO NI UVUNJWAJI WA SHERIA NA TARATIBU ZA NCHI.

  WATUHUMIWA WALIOKAMATWA, 1. JESCA SIMONI MIAKA [14], MWANAFUNZI, AMBAYE ALIKAMATWA AKIWA NA LITA 42 ZA POMBE AINA YA GONGO, 2.NYANGE BIHEMO MIAKA [46] ALIYEKAMATWA AKIWA NA MITAMBO MIWILI YA KUTENGENEZEA POMBE YA GONGO, 3. MARIAM OMARY MIAKA [28] ALIYEKAMATWA NA POMBE YA GONGO LITA 3, 4. 

  MAOLA LUCHUPA MIAKA 32 ALIYEKAMATWA AKIWA NA LITA 20 ZA POMBE AINA YA GONGO. WENGINE NI, 5. ELIZABETH JOHN MIAKA 35 ALIYEKAMATWA NA MITAMBO MITATU YA KUTENGENEZEA POMBE YA GONGO, 6. ANASTAZIA ALOYCE MIAKA 25 ALIYEKAMATWA NA POMBE YA GONGO LITA 2, 7. TEDY PIUS MIAKA 40 ALIYEKAMATWA NA LITA 30 ZA POMBE YA GONGO NA, 8. PASKAZIA THOMAS ALIYEKAMATWA NA MITAMBO MIWILI YA KUTENGENEZEA POMBE YA GONGO, WATUHUMIWA WOTE NI WAKAZI WA LUCHELELE.

  AIDHA INADAIWA KUWA WATUHUMIWA HUFANYA BIASHARA  HARAMU YA POMBE YA GONGO NA WAKAZI WA MAENEO HAYO, HUKU WAKIIHALALISHA BIASHARA HIYO KUWA KAMA CHANZO CHAO KIKUU CHA KIPATO CHA KILA SIKU KITENDO AMBACHO NI UVUNJWAJI WA SHERIA NA TARATIBU ZA NCHI. NDIPO JESHI LA POLISI LILIPOKEA TAARIFA ZA KIINTELEJENSIA KUHUSIANA NA UHALIFU HUO UNATENDWA NA BAADHI YA WAKAZI WA LUCHELELE NA KUFANIKIWA KUKAMATA WATUHUMIWA TAJWA HAPO JUU.

  WATUHUMIWA WOTE WAPO CHINI YA ULINZI WA JESHI LA POLISI HUKU MAHOJIANO DHIDI YA UHALIFU WANAOUFANYA WA KUJIHUSISHA NA BIASHARA HARAMU YA POMBE AINA YA GONGO UKIENDELEA, PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA WATAFIKISHWA MAHAKAMANI KUJIBU MASHITAKA YANAYO WAKABILI.

  KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WANANCHI WA JIJI NA MKOA WA MWANZA AKIWATAKA WAFANYE KAZI NYINGINE HALALI AMBAZO ZITAWAINGIZIA KIPATO, LAKINI BIASHARA HARAMU ZA POMBE YA GONGO NA MADAWA YA KULEVYA NAWAOMBA MUACHE KUJIHUSISHA NAZO KABISA, KWANI JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LIMEJIPANGA VIZURI KUKABILIANA NA WAHALIFU WA AINA KAMA HIYO NA KUHAKIKISHA WANAKAMATWA NA KUFIKISHWA KWENYE VYOMBO VYA SHERIA.

  IMETOLEWA NA:
  SACP: AHMED MSANGI
  KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA.

  0 0

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki Mhe,Augustino Mahiga alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo kwa mazungumzo.
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein akifuatana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki Mhe,Augustino Mahiga baada ya mazungumzo yao leo alipofika Ikulu Mjini
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein akiagana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki Mhe,Augustino Mahiga alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo baada ya  mazungumzo yao,[Picha na Ikulu.]17/06/2016. 

  0 0

  · Safari tano kwa siku ikiwamo za alfajiri kwa wasafiri wote wa Abu Dhabi na Qatar
  · Nyongeza ya safari za jioni kwa kipindi za kiangazi ikiwa ni maalumu kwa wafanyabiashara na wasafiri wanaoenda kutembea

  Shirika la Ndege la Etihad limesherehekea miaka 10 ya huduma ya usafiri wa anga kwa kuzindua safari tisa za ndege kutoka Abu Dhabi – Doha kipindi hiki cha kiangazi ikitimiza ahadi yake kuwa shirika bora la usafiri katika ukanda huo wa Gulf kibiashara.

  Kuanzia 1 Agosti 2016 shirika hili litaongeza safari za wiki kuelekea mji mkuu wa Qatar. Safari mpya za ndege za alfajiri pamoja na jioni siku ya Alhamisi na Jumamosi zitawawezesha wasafiri ambao ni wafanyabiashara kuweza kufanya shughuli zao kwa wakati kati ya Abu Dhabi na Doha.

  Safari hizo mpya zitawawezesha wasafiri kutoka Doha kuwa na chaguo la usafiri wa ndege za Shirika la Etihad zinazofanya safari zake maeneo mbalimbali ya Mashariki ya Kati, Ulaya, Afrika, Asia, na Amerika Kaskazini.Huduma hiyo mpya inaendana na kipindi hiki cha miezi ya kiangazi ambacho huwa na ongezo idadi ya wasafiri.

  Tangu kuanzishwa safari za Doha mwaka 2016, Shirika la Ndege la Etihad limekuwa likiboresha huduma zake ili kuendana na mahitaji halisi ikiwamo kuiunganisha dunia na huduma mbalimbali zinazopatikana Abu Dhabi.

  Makamu wa Rais wa Masoko katika Shirika la Ndege Etihad, Daniel Barranger alisema, “Qatar ni kitovu cha biashara kwa Shirika la Etihad. Tangu 2006 kumekuwapo maendeleo mazuri ya safari za ndege nne kwa siku kati ya Abu Dhabi na Doha, ndiyo sababu tunasherehekea kumiza miaka 10 kwa kuunganisha miji hii mikuu miwili kwa kuongeza safari za ndege tisa kila wiki ikiwa ni kuonyesha dhamira yetu kukuza biashara Doha.”

  Aliongeza kuwa, “Kwa kuboresha safari zetu kwenda na kurudi Doha, tumejenga mtandao imara na ni matumaini yetu wateja wetu watakuwa na wigo mpana wa kuchagua usafiri muda unaomfaa kwenda Abu Dhabi.”

  Wageni wanaosafiri kwenda Abu Dhabi watakuwa na fursa ya kupanga na kuchagua ndege aipendayo kufika Ulaya, ikiwamo miji ya London, Manchester, Paris, Dublin, Rome, Munich, Milan, Geneva, Madrid, Athens na Istanbul. Pia, Delhi, Mumbai, Kathmandu, Dhaka, Calicut, Cochin pamoja na Hyderabad miji inayounganisha India.

  Pia mteja anaweza kusafiri kwa ndege ya shirika la Etihad kutokea Doha na kutembelea miji mbalimbali ya USA; – New York, Chicago, San Francisco, Los Angeles, Washington na Dallas.

  Wasafiri pia watapata huduma ya kipekee ya US Pre-Clearance immigration and customs wakiwa katika uwanja wa ndende wa kimataifa wa Abu Dhabi.

  Hii humwezesha msafiri anapowasili Marekani kama msafiri wqa ndani kumpuguzia muda ambao angetumia kushughulikia na kukamilisha. masuala ya uhamiaji na taratibu za kuwasili.

  Safari za kila siku kati ya Abu Dhabi and Doha. Ratiba mpya ya usafiri wa ndege utakaoanza tarehe 1 Agosti, 2016.


  0 0
 • 06/17/16--02:30: Article 10


 • 0 0

  Kipindi cha Joto la Asubuhi cha EFM redio kinacho tangazwa na Gerald Hando, PJ na Adela Tilya kinachorushwa live kila mwisho wa wiki katika maeneo mbalimbali, leo siku ya Ijumaa ya tarehe 17/06/2016 kimewafikia wakazi wa Kariakoo huku kikiambatana na burudani kabambe kutoka kwa wasanii wa Singeli kama, Sholo Mwamba na Majid Migoma.
    Mashabiri wa 93.7 Efm Joto la Asubuhi ambao walifika asubuhi na mapema kwa ajili ya kushuhudia kipindi hicho live kutoka Kariakoo.
   Msanii Sholo Mwamba akiwaburudisha mashabiki wa Efm redio katika kipindi cha JOTO LA ASUBUHI Kariakoo.
   Watangazaji wa kipindi cha JOTO LA ASUBUHI, Gerald Hando, PJ na Adela Tilya wakijianda kutangaza live kipindi hicho live.
  Mashabiki wa Kariakoo wakisikiliza kipindi cha Joto la asubuhi live.

  0 0

  KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NDANI  AFUNGA MAFUNZO YA KOZI YA UONGOZI DARAJA LA PILI CHUO  CHA ZIMAMOTO NA UOKOAJI CHOGO,JIJINI TANGA.
   Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira(kushoto), akimvisha nyota mmoja wa wahitimu 156 wakati wa Mahafali ya kufunga Mafunzo ya Kozi ya Uongozi Daraja la Pili , yaliyofanyika Chuo cha Zimamoto na Uokoaji Chogo, Wilayani Handeni, jijini Tanga.
   Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira, akikagua gwaride la heshima lililoandaliwa wakati wa Mahafali ya kufunga Mafunzo ya Kozi ya Uongozi Daraja la Pili , yaliyofanyika Chuo cha Zimamoto na Uokoaji Chogo, Wilayani Handeni, jijini Tanga.
   Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira(kushoto), akimkabidhi cheti mmoja wa wahitimu 156 wakati wa Mahafali ya kufunga Mafunzo ya Kozi ya Uongozi Daraja la Pili , yaliyofanyika Chuo cha Zimamoto na Uokoaji Chogo, Wilayani Handeni, jijini Tanga.

   Gwaride la heshima likipita mbele ya Mgeni Rasmi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasiara,  wakati wa Mahafali ya kufunga Mafunzo ya Kozi ya Uongozi Daraja la Pili , yaliyofanyika Chuo cha Zimamoto na Uokoaji Chogo, Wilayani Handeni, jijini Tanga.
  Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira, akizungumza wakati wa Mahafali ya kufunga  Mafunzo ya Kozi ya Uongozi Daraja la Pili , yaliyofanyika Chuo cha Zimamoto na Uokoaji Chogo, Wilayani Handeni, jijini Tanga.Ambapo aliwaasa wahitimu kwenda kulihudumia Taifa kwa uadilifu.(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
  IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.


  0 0

   Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Bwn Sunil Colaso akiwa na waendesha pikipiki maarufu kama Bodaboda kabla ya kuingia sokoni kupeleka huduma ya facebook bure kwa wateja na watanzania kwa ujumla. Airtel wiki hii ilizindua huduma ya facebook bure inayowawezesha wateja wake kuunganishwa na ndugu jamaa na marafiki bure bila kuwa na haja ya kununua kifurushi chochote.
   Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Bwn Sunil Colaso akinyanyua bendera kuwaruhusu waendesha pikipiki maarufu kama Bodaboda kuingia sokoni na kupeleka huduma ya facebook bure kwa wateja na watanzania kwa ujumla.
   Helikopta maalum ikiruka angani na kusambaza ujumbe wa huduma ya facebook bure kwa wateja wa Airtel na watanzania ili kuwawezesha kuwasiliana na ndugu jamaa na marafiki  na kuendesha shughuli za kijamii, uchumi kupitia huduma ya facebook bila gharama yeyote.
  Baadhi ya waendesha pikipiki jijini  Dar es Salaam maarufu kama Bodaboda wakiondoka makao makuu ya Airtel kuingia  sokoni kupeleka huduma ya facebook bure kwa wateja na watanzania kwa ujumla.

  0 0

  Mwenyekiti wa taasisi ya kijamii ya Happy Children Tanzania (HCT) Bi Zainabu Makombe (katikati) akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na warsha ya wazi inayotarajiwa kufanyika kesho Jumamosi kwenye viwanja vya Mwembeyanga wilayani Temeke ikilenga kuhamasisha jamii kupambana na ukatiri dhidi ya watoto. Wengine ni Meneja Masoko msaidizi wa Benki ya Exim Tanzania, Bi Mariamu Mwapinga (kulia) na Mwenyekiti wa taasisi ya Glory of Africa ya nchini Sweden Bi.Victoria Lunderberg.

  Taasisi ya kijamii ya Happy Children Tanzania (HCT) imeandaa warsha ya wazi inayotarajiwa kufanyika kesho jumamosi ikilenga kuhamasisha jamii kupambana na ukatiri dhidi ya watoto ikiwa ni mwendelezo wa maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika yaliodhimishwa kote barani Afrika hivi karibuni. 

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana Mwenyekiti wa taasisi hiyo Bi Zainabu Makombe alisema warsha hiyo itakayohusisha baadhi ya taasisi zinazohusiana na utetezi wa haki za watoto itafanyika katika Viwanja vya Mwembeyanga wilayani Temeke kuanzia majira saa 3 asubuni hadi saa 7 mchana. 

  “Ni kwa kushirikiana na wenzetu taasisi ya Glory of Africa ya nchini Sweden tumeweza kuandaa shughuli hii. Tunarajia kwamba shughuli yetu itapambwa na mada mbalimbali za masuala ya afya na haki za watoto zitakazowasilishwa na wataalam kutoka Wizara ya Afya na mashirika kadhaa yanayohusiana namasuala ya watoto hapa nchini,’’ alitaja. 

  Aidha Bi Makombe alitowa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kwenye  viwanja hivyo sambamba na watoto wao ili wapate fursa ya kusikikiliza mada muhimu za watoto zitakazoambatana na burudani mbalimbali kutoka kwa wanafunzi wa shule mbalimbali za jijini Dar es Salaam. 

  Kwa upande wake Meneja Masoko msaidizi wa Benki ya Exim Tanzania, Bi Mariamu Mwapinga ambaye benki ni sehemu ya wadhamini wa warsha hiyo alisema benki hiyo imeamua kushirikiana na taasisi ya HCT kwa kuwa inatambua umuhimu wa watoto na haki zao ndani ya jamii. 

  “Si tu kwamba tunashirikiana nao katika kufanikisha maadhimisho haya bali pia tutaendelea kuwa nao pamoja katika mipango yao inayokuja kuhusiana na masuala ya watoto na haki zao...Exim tunaamini watoto ni sehemu ya wateja wetu leo na kesho,’’ alisema. 

  Mbali na Exim baadhi ya taasisi na kampuni zinazoshiriki katika kufanikisha warsha hiyo ni pamoja na Save the Children, PASADA, SOS, White Ribbon, GUTz, Coca Cola, AAR, YWCA na TTO.

  0 0


  Katibu Mkuu Wizara ra Fedha na Mipango, Dkt. Servacius Likwelile (kushoto), na mgeni wake, Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Maendeleo wa Kimataifa wa Sweden Mhe. Ulrika Modeer (kulia), wakipeana mikono na kubadilishana hati za mkataba baada ya kutiliana saini mkataba wa ushirikiano wa maendeleo wa miaka minne kuanzia mwaka 2016 hadi 2019, tukio lililofanyika katika Ofisi za Hazina Mjini Dodoma leo, Juni 16, 2016.
  Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Servacius Likwelile (kushoto), na mgeni wake, Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Maendeleo wa Kimataifa wa Sweden Mhe. Ulrika Modeer (kulia), wakipeana mikono na kubadilishana hati za mkataba baada ya kutiliana saini mkataba wa ushirikiano wa kimaendeleo wa miaka mine kuanzia mwaka 2016 hadi 2019, tukio lililofanyika katika Ofisi za Hazina Mjini Dodoma leo, Juni 16, 2016

  Baadhi ya Maofisa wa serikali ya Tanzania wakifuatilia kwa makini tukio la kutiliana saini mkataba wa ushirikiano wa kimaendeleo kati ya Tanzania na Sweden, utakao chukua miaka minne kuanzia 2016 hadi 2019, tukio lililofanyika katika Ofisi za Hazina Mjini Dodoma leo, Juni 16, 2016
  Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Maendeleo wa Kimataifa wa Sweden Mhe. Ulrika Modeer (kulia), akizungumza jambo wakati wa hafla fupi ya Tanzania na Sweden, kutiliana saini mkataba wa ushirikiano wa kimaendeleo wa miaka minne kuanzia 2016 hadi 2019, tukio lililofanyika katika Ofisi za Hazina Mjini Dodoma leo Juni 16, 2016.   Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Servacius Likwelile (kushoto), akizungumza jambo wakati wa hafla fupi ya Tanzania na Sweden, kutiliana saini mkataba wa ushirikiano wa kimaendeleo, wa miaka minne kuanzia 2016 hadi 2019, tukio lililofanyika katika Ofisi za Hazina Mjini Dodoma leo, Juni 16, 2016.


  Ujumbe wa Sweden ukiongozwa na Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Maendeleo wa Kimataifa wa Sweden Mhe. Ulrika Modeer (Katikati), wakifuatilia kwa makini tukio la kutiliana saini mkataba wa ushirikiano wa kimaendeleo kati ya Tanzania na Sweden, utakao chukua miaka mine kuanzia 2016 hadi 2019, tukio lililofanyika katika Ofisi za Hazina Mjini Dodoma leo, Juni 16, 2016
  Baadhi ya Maofisa wa serikali ya Tanzania akiwemo Mkurugenzi wa Tasaf Ladislaus Mwamanga (kushoto) wakifuatilia kwa makini tukio la kutiliana saini mkataba wa ushirikiano wa kimaendeleo kati ya Tanzania na Sweden, utakao chukua miaka minne kuanzia 2016 hadi 2019, tukio lililofanyika katika Ofisi za Hazina Mjini Dodoma leo, Juni 16, 2016.

   

  Benny Mwaipaja, WFM -DODOMA

  SERIKALI za Tanzania na Sweden zimetiliana saini mkataba wa ushirikiano wa miaka 4 kuanzia mwaka 2016 hadi mwaka 2019 utakaojikita kuimarisha uchumi wa nchi na maendeleo ya watu katika nyanja mbalimbali ikiwemo elimu, utafiti, nishati jadidifu na kupambana na umasikini.

  Tukio hilo limefanyika leo Juni 16, 2016, mjini Dodoma kati ya Katibu Mkuu na mlipaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Servacius Likwelile kwa upande wa Tanzania na Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Kimaendeleo wa Sweden, Mhe. Ulrika Modeer.

  Dkt. Likwelile ameeleza kuwa katika kipindi cha kuanzia mwaka 2013 hadi mwaka 2019, Serikali ya Sweden itatoa ruzuku ya fedha za Kiswidi, SEK 5.5 Biln, sawa na shilingi Trilioni 1.42 za Kitanzania.

  Amesema kuwa kutiwa saini kwa mkataba wa ushirikiano huo kutafuatiwa na utiwaji saini wa mikataba ya kifedha ambapo fedha hizo zitaelekezwa katika miradi kadhaa ikiwemo kusaidia Elimu, Maendeleo ya Jamii-TASAF, Utafiti, Nishati, Demokrasia, Haki za Binadamu, na Sekta Binafsi.

  "Ushirikiano huu umelenga kusaidia kujenga mazingira ya maendeleo endelevu na kuwapatia Watanzania maskini fursa za kujikwamua katika umaskini kwa kujipatia ajira na kuweza kuanzisha biashara za kujipatia kipato ambapo vikundi vinavyolengwa zaidi ni wanawake, watoto na vijana" Alisema Dkt. Likwelile

  Dkt. Servacius Likwelile ametoa wito kwa Serikali ya Sweden na nchi nyingine duniani kuwekeza katika biashara na vitega uchumi ili ziweze kunufaika na rasimali kubwa ambazo nchi imejaaliwa ikiwemo maliasili, ardhi yenye rutuba na jiografia ya kimkakati inayochochea uwekezaji na biashara

  Kwa upande wake Naibu Waziri wa Ushirikianno na Maendeleo ya Kimataifa wa Sweden Mhe. Ulrika Modeer, amepongeza uongozi mahili wa Rais wa Awamu ya Tano, Dkt. John Pombe Magufuli kwa kupambana na vitendo vya kifisadi ikiwemo rushwa.

  "Sweden inaunga mkono kwa nguvu zote hatua zinazochukuliwa na Rais Magufuli kupambana na mauvu nchini na tunaamini nchi itapiga hatua kubwa kimaendeleo" Alisistiza Modeer.

  Mhe. Ulrika Modeer ameahidi kuwa serikali yake itaendelea kushirikiana na Tanzania kwa kutoa fedha kupitia mfuko mkuu wa Bajeti ili kuwezesha kufanikisha miradi mbalimbali ya maendeleo inayogusa hifadhi ya mazingira, kilimo endelevu, kuwawezesha wananawake kiuchumi na kumsaidia mtoto wa kike na kiume kielimu.

  "Tunataka kuona kuwa maendeleo ya nchi yanakwenda sambamba na maendeleo ya wananchi wake ambapo tunaamini kuwa utafiti utasaidia kupata njia bora za kupambana na umasikini"Alisisitiza Mhe. Modeer

  Amesema kuwa pamoja na nchi yake kutaka kuyasaidia makundi mbalimbali wakiwemo watu wenye ulemavu, wanataka kuona suala la demokrasia na utawala bora vinapewa kipaumbele katika mipango mbalimbali ya maendeleo

  "Vilevile uwekezaji wetu mkubwa wa fedha katika maendeleo ya Taifa hautakuwa na maana sana kama suala la hifadhi ya mazingira halitapewa kipaumbele kwa kuanzisha miradi ya nishati jadidifu "Renewable energy" ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi: aliongeza Mhe. Ulrika Modeer

  Uhusiano wa Tanzania na Sweden umedumu tangu mwaka 1960 ambapo katika kipindi chote cha miaka 50, serikali hizi mbili zimeshirikiana katika kubuni na kutekeleza miradi kadhaa ya maendeleo

  Programu na miradi itakayotekelezwa katika ushirikiano uliosainiwa leo unaendena pia na Mpango wa Taifa wa Pili wa Miaka Mitano unaoanzia mwaka 2016/17 hadi 2020/21 na unalenga kuondoa utegemezi wa misaada kwa Tanzania.

  MWISHO

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki Mhe,Augustino Mahiga alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo kwa mazungumzo,  
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein akifuatana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki Mhe,Augustino Mahiga baada ya mazungumzo yao leo alipofika Ikulu Mjini,[Picha na Ikulu.]17/06/2016.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein akiagana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki Mhe,Augustino Mahiga alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo baada ya mazungumzo yao,[Picha na Ikulu.]17/06/2016.

  0 0

   Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Joel Laurent (katikati), akizungumza wakati wa hafla fupi ya kutiliana saini ya makubaliano ya ujenzi wa nyumba 40 za walimu wa Shule za Sekondari zitakazojengwa na Watumishi Housing Company katika mikoa 23 ya Tanzania Bara, ambapo familia 240 za walimu zitanufaika na ujenzi wa nyumba hizo. Kushoto ni Mkurugeni Mtendaji wa Watumishi Housing Company (WHC), Dk. Fred Msemwa na kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji wa TEA, Julius Rugemalila. (Picha na Francis Dande)
  Mkurugeni Mtendaji wa Watumishi Housing Company (WHC), Dk. Fred Msemwa (katikati) akizungumza wakati wa kutiliana saini ya makubaliano ya ujenzi wa nyumba 40 za walimu wa Shule za Sekondari.

  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA). Joel Laurent (kulia) na Mkurugeni Mtendaji wa Watumishi Housing Company (WHC), Dk. Fred Msemwa (katikati), wakisaini mkataba wa ujenzi wa nyumba 40 za walimu wa Shule za Sekondari zitakazojengwa katika mikoa 23 ya Tanzania Bara, ambapo familia 240 za walimu zitanufaika na ujenzi wa nyumba hizo. 
   Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA). Joel Laurent (kulia), akibadilishana hati na Mkurugeni Mtendaji wa Watumishi Housing Company (WHC), Dk. Fred Msemwa baada ya kusaini mkataba wa ujenzi wa nyumba 40 za walimu wa Shule za Sekondari zitakazojengwa katika mikoa 23 ya Tanzania Bara, ambapo familia 240 za walimu zitanufaika na ujenzi wa nyumba hizo.


  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA). Joel Laurent (kulia) na Mkurugeni Mtendaji wa Watumishi Housing Company (WHC), Dk. Fred Msemwa wakipongezana.

  Picha ya pamoja.
   Mkurugeni Mtendaji wa Watumishi Housing Company (WHC), Dk. Fred Msemwa akisaini kitabu cha wageni.
   Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA). Joel Laurent (katikati) na Mkurugeni Mtendaji wa Watumishi Housing Company (WHC), Dk. Fred Msemwa (kulia), wakizungumza mara baada ya kutiliana saini ya makubaliano ya ujenzi wa nyumba 40 za walimu wa Shule za Sekondari.

  0 0

  bug1 
  Mbunge wa Nchemba (CCM), Mhe. Juma Nkamia akifurahia jambo na Mbunge wa Kaliua (CUF), Mhe. Magnalena Sakaya wakati wakiingia katika viwanja vya Bunge leo mjini Dodoma  kuanza kipindi cha asubuhi cha Bunge hilo.
  bug2 
  Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba akibadilishana mawazo na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. George Masaju ndani ya ukumbi wa Bunge leo mjini Dodoma.
  bug3 
  Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira, Vijana na Ulemavu, Mhe. Antony Mavunde akijibu maswali ya Wabunge leo Bungeni mjini Dodoma wakati wa kipindi cha maswali na majibu.
  bug4 
  Mbunge wa Tabora Kaskazini (CCM), Mhe. Almas Maige akiuliza swali Bunge leo wakati wa kipindi cha maswali na majibu.
  bug5 
  Wabunge wa CCM Viti (Maalum) kutoka kushoto, Christine Ishengoma, Martha Umbulla na Magreth Sitta wakibadilishana mawazo ndani ya ukumbi wa Bunge wakati wa kipindi cha maswali na majibu ya Bunge hilo leo.
  bug6 
  Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Mhe. Halima Bulembo, akiuliza swali Bungeni leo wakati wa kipindi cha maswali na majibu ya Bunge hilo. Kulia ni Mbunge wa Busega, Mhe. Raphael Chegeni.
  bug7 
  Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt Tulia Ackson akibadilishana mawazo na Wabunge mara baada ya kuahirisha   kipindi cha asubuhi cha Bunge hilo mjini Dodoma.
  bug8 
  Naibu Spika wa Bunge, Mhe.Dkt. Tulia Ackson akifurahia jambo na Mbunge wa Kibiti, Mhe. Ally Ungando mara baada ya kuahirisha kipindi cha asubuhi cha Bunge hilo leo mjini Dodoma.(PICHA NA ISMAIL NGAYONGA- MAELEZO)

older | 1 | .... | 883 | 884 | (Page 885) | 886 | 887 | .... | 1897 | newer