Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 882 | 883 | (Page 884) | 885 | 886 | .... | 1897 | newer

  0 0

   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Makamu Mwenyekiti Mstaafu, John Malecela  katika futari aliyoiandaa kwenye makazi yake mjini Dodoma Juni 16, 2016.
    Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na  Mbunge wa Ulanga, Goodluck Mlinga katika futari aliyoiandaa kwenye makazi yake mjini Dodoma Juni 15, 2016.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika futari aliyoiandaa kwenye makazi yake mjini Dodoma Juni 15, 2016. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Dodoma, Alhaj Adam Kimbisa na Wapili kushoto ni Kaimu Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Ahmed Said.Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na mazingira, January Makamba.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana  na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba katika futari aliyoianda kwenye makazi yake mjini Dodoma Juni 15, 2016.

   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akisalimiana na Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson katika fuatari aliyondaa kwenye makazi kake mjini Dodoma Juni 15, 2016.


   (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema kila mkoa unatakiwa kuunda Kamati ya Amani kama njia ya kudumisha amani na utulivu kwenye mikoa yote nchini.

  Waziri Mkuu ametoa wito huo jana usiku (Jumatano, Juni 15, 2016) wakati akizungumza na viongozi wa dini wa mkoa wa Dodoma na baadhi ya wazee maarufu wa mkoa huo aliowaalika kwenye futari katika makazi yake mjini Dodoma.

  Amesema anatambua kuwa mkoa wa Dodoma uko shwari kwa sababu ya mshikamano uliopo baina viongozi wa dini za Kiislamu na Kikristo. "Nimegundua kuwa siri kubwa ya mkoa wa Dodoma kuwa na utulivu ni kuwepo kwa kamati ya amani yenye viongozi mahiri, kwani sote tunatambua kuwa kazi ya viongozi wa dini ni kuwaimarisha watu kiroho," alisema.

  Waziri Mkuu alisema ziko nchi zinatamani kuwa kama Tanzania kwa sababu wao hawana uhakika wa kulala na kuamka salama asubuhi. "Pamoja na yote sisi tuna uhakika wa asilimia 99 kulala usiku na kuamka salama asubuhi, kwa sababu ya amani iliyopo," alisema.

  Hadi sasa mikoa ambayo imekwishaunda kamati za amani ni Dar es Salaam, Mwanza, Geita, Dodoma, Arusha, Lindi, Mtwara, Tanga na Mbeya.

  Akigusia suala la mauaji ya hivi karibuni, Waziri Mkuu alisema anawaomba Watanzania kila mmoja kwa imani yake akemee kwa nguvu matendo hayo kwa sababu yeye haamini kama yamefanywa na Watanzania ambao wamelelewa kwenye misingi ya dini.

  "Siamini kama kuna mtoto aliyelelewa kwenye misingi ya Uislamu anaweza kuingia msikitini na kuwaua wenzake wakati wakimwomba Mungu. Na wala siamini kama kuna mtoto aliyelelewa na kukuzwa Kikristo anaweza kuingia kwenye nyumba ya ibada akakuta watu wanasali na kuamua kuwaua. Ninawaomba tukemee kwa nguvu zote tabia hii," alisisitiza.

  Aliwataka watanzania wote wawe na walinzi wa wenzao kwa sababu kila mmoja ana jukumu la kumlinda mwenzake. "Tusiachie majeshi kazi hii kwa sababu kila mmoja na jukumu la kwanza kujilinda yeye mwenyewe na kisha kumlinda jirani yake," alisema.

  Kwa upande wake, Kaimu Sheikh wa Mkoa wa Dodoma, Sheikh Ahmed Said alisema wanawaombea dua Mheshimiwa Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu katika kazi za kuleta maendeleo kwa Watanzania. "Pia tutaendelea kuiombea nchi yetu ili Mwenyezi Mungu azidishe amani yake na watu wake waishi kwa amani, upendo na utulivu," aliongeza.

  Naye Waziri Mkuu mstaafu, Dk. John S. Malecela ambaye alikuwa miongoni mwa wazee maarufu walioalikwa kwenye futari hiyo aliwataka waalikwa wenzake waendelee kuwaombea viongozi wa kitaifa na kusisitiza kuwa kila mmoja ana wajibu wa kuombea amani ya Tanzania ambayo imedumu kwa miaka mingi iendelee kuwepo.

  Katika hatua nyingine, Askofu wa Kanisa la Mennonite Tanzania Dayosisi ya Kati, Askofu Amos Muhagachi, ambaye alipewa fursa ya kutoa salamu fupi kwenye hafla hiyo, alisema kwenye mkoa huo hakuna magomvi ya kidini kwa sababu viongozi wa dini zote wanashirikiana kwa karibu sana.

  "Hapa Dodoma Maaskofu tunashirikiana vizuri na Masheikh. Hivi sasa, masheikh vijana na wachungaji vijana wameanza kuiga haya tunayofanya, na zaidi ya yote tunashirikiana pia kuwaombea Rais wetu, Makamu wa Rais pamoja na wewe Mheshimiwa Waziri Mkuu," alisema.

  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  S. L. P. 980,
  DODOMA.
  ALHAMISI, JUNI 16, 2016.

  0 0  Mhariri Mkuu Idara ya Habari Maelezo Zanzibar Ramadhan Ali akimkaribisha Mwenyekiti wa Chama cha Wakulima (AFP) ambae pia ni Waziri wa SMZ asie na Wizara Maalum Saidi Sudi azungumze na Waandishi wa Habari katika ukumbi wa Sanaa Rahaleo
  Mwenyekiti wa Chama cha Wakulima (AFP) Saidi Sudi akizungumza na waandishi wa Habari hawapo (pichani) kuhusiana na kadhia ya kukatwa mikarafuu, minazi na mihogo katika shamba lake lenye urefu wa eka moja na nusu huko Pemba.

  Baadhi ya wandishi wa Habari wakimsikiliza Mwenyekiti wa Chama cha Wakulima (AFP) Saidi Sudi hayo pichani katika ukumbi wa Sanaa Rahaleo Mjini Zanzibar. Picha na Makame Mshenga/Maelezo Zanzibar.

  Na Mwandishi wetu –Habari Maelezo Zanzibar

  Mwenyekiti wa Chama cha Wakulima ( A.F.P ) Said Suod Said amemshauri Msajili ya vyama vya siasa nchini kwenda kisiwani Pemba kufuatilia hujuma zinazoendea kufanyika kisiwani huko ili kuweza kuzipatia ufumbuzi .

  Hayo ameyasema huko katika ukumbi wa Sanaa Rahaleo wakati akizungumza na Waandishi wa habari baada ya kufanyiwa hujuma katika shamba lakeliliopo Mgelema Wilaya ya Chakechake.

  Alisema kwamba kuna baadhi ya watu wanafanya vitendo vya hujuma vinanyopelekea vinaashiria uvunjifu wa amani na wananchi kuogopa kuendelea kutoa huduma kisiwani humo.

  Alieleza kuwa baadhi ya hujuma hizo ni pamoja na kuchomewa moto kwa baadhi ya nyumba na kuharibu mashamba ya wananchi kukatiwa vipando ikiwemo mikarafuu, minazi na mashina ya muhogo hali ambayo inarejesha nyuma maendeleo na kutokukuwa uchumi wa nchi.

  “Vitendo hivyo vimekithiri watu kisiwani Pemba wamezidi siasa wanaifanya ushindani, watu wanashindana kwa kura sasa wao wanafanya hujuma mimi shamba langu wamenikatia mikarafuu 151 ikiwemo 14 tayari kuzaa, minazi 16 pamoja na mashina 250 yenye thamani ya sh. Milioni 200 inaniuma sana.” Alieleza Mwenyekiti huo.

  Alifahamisha kuwa siasa sio ugomvi kilichobakia ni kuleta maendelo ya nchi kwani uchaguzi umemalizika serikali tayari ipo madarakani hivyo wananchi wanatakiwa kushirikiana kwa pamoja ili kuweza kudumisha amani na kukuza uchumi wa nchi.

  Aidha amemuomba Rais wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kuzidisha ulinzi kisiwani Pemba kutokana na hujuma zinaendela kufanyika siku hadi siku kisiwani humo ili amani isije ikatoweka nchini.

  Amewataka Wazanzibar kuendelea kuwa wastahamilivu kutokana na hujuma zinaendelea kufanywa kisiwani huko kwani nchi inafuata sheria hivyo serikali inawajali wananchi wake na waendelee kudumisha amani.

  MWISHO 

  0 0
  Mwanasheria wa Property International Limited Hazel Chonya (wa pili kushoto) akimkabidhi mwanasheria wa Bayport, Mrisho Mohamed (wa pili kulia) baadhi ya hati za viwanja vilivyosajiliwa na wizara ya ardhi nyumba na maendeleo ya makazi kwa wateja wa Bayport kwa viwanja vya mradi wa Vikuruti Kibaha, mradi ambao unauzwa na kampuni ya Property International Limited kwa kushirikiana na Bayport. Kushoto) Ofisa Uendeshaji Property International,George Obado na Meneja Masoko wa Property International Leila Maingu.

  0 0

  JAMII imetakiwa kubadilika kwa kuacha kufanya ukatili wa watoto ili kuweza kuwa na watoto kwa kujitambua. Hayo ameyasema leo Mkugenzi Mtendaji wa Taasisi isiyo ya Kiserikali C-SEMA, Kiiya Joel, wakati wa maadhimisho ya siku mtoto wa Afrika iliyofanyika katika viwanja vya Jakaya Kikwete, amesema kesi nyingi za watoto kutelekezwa ambazo zimekuwa zikifikia kituomn hicho kupitia huduma ya simu mkononi. Kiiya amesema watoto wanatelekezwa na kufanya watoto kuishi mitaani na kuhitaji msaada wa kujikimu hali ambayo inafanya watoto kukosa haki ikiwemo kukosa elimu. 

  Amesema kuwa katika utoaji wa huduma ya simu C-SEMA imejipanga kuboresha huduma visiwani Zanzibar ili kuhakikisha vitendo viovu vya watoto vinapatiwa taarifa. "Tumepata fedha ambazo C sema itaboresha huduma kupiga ya simu kwa ajili ya kupata matukio ambayo yanakandamiza watoto visiwani Zanzibar ", amesema Kiiya. Kiiya amewataka watanzania kutoa ushirikiano kwa kupiga simu ya bure 116 na kutoa taarifa za matukio ya ukatili dhidi ya watoto ili yaweze kutatuliwa mara moja. 
   Watoto katika picha ya Pamoja .

  Amesema kuwa kituo cha huduma ya simu kwa mtoto kimekuwa hakipokei simu nyingi kutokana na kwamba huduma hiyo haijafahamika maeneo mengi ambapo kwa mwezi hupokea simu 30 kiwango ambacho ni kidogo kulingana na ukubwa wa tatizo. "Naomba watanzania wote popote pale walipo kupiga simu ya bure 116 pale wanaposikia taarifa za kuwepo kwa matukio ya ukatili dhidi ya watoto ili yaweze kufanyiwa kazi," amesema Amesema kuwa toka kituo hicho kianze Juni 16, mwaka 2013 wamekuwa wakipokea simu za matukio ya watoto kupewa ujauzito, matunzo ya watoto baada ya kutekelezwa, ulawiti na ubakaji. 

  Aliongeza kuwa wameamua kuadhimisha siku hiyo kwa kukutanisha watoto kutoka maeneo mbalimbali ikiwa pia ni sehemu ya kuanzishwa kwa huduma hiyo. Amesema C-Sema inataka kuona huduma za watoto nchini zinalenga maslahi ya mtoto na ndio maana kwa kushirikiana na serikali C-Sema imekuwa ikikusanya maoni ya watoto nchi nzima kupitia Huduma ya Simu kwa Mtoto (116), Barua za Maoni ya Watoto, na gazeti la Sema kwa ajili ya watoto. 
   Watoto katika michezo mbalimbali. 

  Amesema maoni haya hutumiwa na viongozi wa Manispaa katika kuongeza bajeti ya watoto ili kuboresha huduma za watoto kwa kupiga simu hiyo ya bure. Siku ya Mtoto wa Afrika uadhimishwa kila mwaka ifikapo Juni 16 na kwa hapa nchini kauli mbiu ya mwaka huu ni 'ubakaji na ulawiti kwa mtoto vinaepukika chukua hatua.
    Watoto wakiangalia mpira. 

  PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Na Zainab Nyamka

  SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF), limepitisha majina ya wachezaji wanne wapya wa Yanga, kipa Benno David Kakolanya, Hassan Hamisi Ramadhan ‘Kessy’, Vincent Andrew Chikupe na Juma Hassan Mahadhi kucheza Kombe la Shirikisho.

  Wachezaji hao wameongezwa kwenye kikosi hicho baada ya kusajiliwa Ikiwa ni lengo lao la kuongeza nguvu kwenye kikosi hicho ambacho kimeingia kwenye hatua ya makundi ya kombe la Shirikisho na wanatarajiwa kuanza kukipiga kwenye mechi ya kwanza ya kundi A dhidi ya Mo Bejala itakayopigwa nchini Afrika Kusini.

  Yanga kwa sasa wameweka kambi nchini Uturuki pamoja na nyota hao wanne wakiwa tayari wameshaingia kwenye mipango ya Kocha Mkuu Mholanzi Hans Van De Pluijm akisaidiwa na Juma Mwambusi.

  0 0

  Wafanyakazi wa Benki ya CRDB tawi la Water Front washerekea siku ya Mtoto wa Afrika na Watoto walipo katika Mahabusu ya watoto iliyopo maeneo ya Regency Hospitali jijini Dar es Salaam leo.

  Siku ya Mtoto wa Afrika ambayo hufanyika June 16 kila mwaka ambayo ni kumbukumbu ya Watoto wa Afrika kusini walikusanyika pamoja na kuandamana kwaajili ya kudai haki zao hasa haki zao.

  Hata hivyo wafanyakazi wa Benki  ya CRDB tawi la Water Front wametoa msaada wa vitu mbalimbali kwa watoto waliopo katika mahabusu hiyo kwaajili ya mahitaji yao madogo madogo mapoja na kunywa pamoja na watoto hao.
  Mwakilishi wa Meneja wa Tawi la Water Front, na  Meneja wa Mikopo wa Benki ya CRDB, Tawi la Water Front, Isaya Lyimo Meneja wa Kituo cha mabusu ya Watoto Dar es Salaam, Ramadhan Hassan  
  Keki ya watoto wa mahabusu ya watoto  Dar es Saslaam iliyoandaliwa na wafanyakazi wa Benki ya CRDB tawi la Water Front.
  Wafanyakazi wa Benki ya CRDB tawi la Water Front wakikamkabidhi Meneja wa Kituo cha mabusu ya Watoto Dar es Salaam, Ramadhan Hassan baadhi ya vitu walivyoenda navyo kwaajili ya watoto waliopo katika mahabusu hiyo jijini Dar es Salaam leo.
  Wafanyakazi wa benki ya CRDB tawi la Water Front akiwa katika picha ya Pamoja na Meneja wa Kituo cha mabusu ya Watoto Dar es Salaam, Ramadhan Hassan jijini Dar es Salaam leo.
   Meneja wa Kituo cha mahabusu ya Watoto Dar es Salaam, Ramadhan Hassan akizungumza na wafanyakazi wa Benki ya CRDB tawi la Water Front kuhusiana na vitu vinavyotakiwa pamoja na historia ya kituo cha Mahabusu ya Watoto jijin Dar es Salaam leo.
  Baadhi ya Wafanyakazi wa Benki ya CRDB tawi la Water Front  wakimsikiliza Meneja wa Kituo cha mabusu ya Watoto Dar es Salaam, Ramadhan Hassan wakati walipotembelea kituo hicho jijini Dar es Salaam leo.   Wafanyakazi wa Benki ya CRDB tawi la Water Front wakiingia kwenye kituo cha mahabusu cha Dar es Salaam jijini Dar es Salaam leo.
  Wafanyakazi wa Benki ya CRDB tawi la Water Front  wakiwa kwenye picha ya Pamoja na  Meneja wa Kituo cha mahabusu ya Watoto Dar es Salaam, Ramadhan Hassa. 
   Meneja wa Mikopo wa Benki ya CRDB, Tawi la Water Front, Isaya Lyimo akiwa kwenye kibao katika kituo cha mahabusu ya watoto Dar es Salaam jijini Dar es Salaam leo.
  Meneja wa Kituo cha mabusu ya Watoto Dar es Salaam, Ramadhan Hassan  akiwa kwenye  picha ya pamoja na Wafanyakazi wa Benki ya CRDB tawi la Water Front jijini Dar es Salaam leo.
   Meneja wa Mikopo wa Benki ya CRDB, Tawi la Water Front, Isaya Lyimo  akikabidhi tolori Meneja wa Kituo cha mabusu ya Watoto Dar es Salaam, Ramadhan Hassan  jijini Dar es Salaam leo.
  Meneja wa Kituo cha mabusu ya Watoto Dar es Salaam, Ramadhan Hassan akisaini fomu za kufungua akaunti ya kituo cha mahabusu mara baada ya kutembelewa na wafanyakazi wa benki ya CRDB Tawi la Water front jijini Dar es Salaam leo.

  0 0


  Meneja wa Uwajibikaji na Huduma za kijamii wa Kampuni ya Uchimbaji gesi ya PanAfrican Energy (CSR Manager) Andrew Kashangaki akifafanua jambo wakati wa hafla ya makabidhiano ya madawati kwaajili ya watoto wa shule za msingi wilayani Kilwa

  Baadhi ya madawati yaliyotolewa na Kampuni ya uchimbaji gesi ya PanAfrican Energy
  Meneja wa Uwajibikaji na Huduma za kijamii wa Kampuni ya Uchimbaji gesi ya PanAfrican Energy (CSR Manager) Andrew Kashangaki(kulia) akimkabidhi Mkuu wa Wilay ya Kilwa Juma A. Njwayo madawati kwa ajili ya wanafunzi wa shule za msingi wilayani mwake. Wanaoshuhudia ni baadhi ya viongozi wa halmashauri ya Kilwa, viongozi kutoka PanAfrican Energy na baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Masoko katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika Kilwa Masoko.
  Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Mh. Juma Abdallah Njwayo akiwaasa wanafunzi wa shule ya Msingi Masoko ambao ni moja ya wanufaikaji wa madawati 800 kutoka PanAfrican Energy kuyatunza madawati waliyopewa na kusoma kwa bidii.

  Meneja wa Uwajibikaji na Huduma za kijamii wa Kampuni ya Uchimbaji gesi ya PanAfrican Energy (CSR Manager) Andrew Kashangaki akitoa neno wakati akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Mh. Juma A. Njwayo madawati 800 yatakayosaidia watoto 2400 na kupunguza tatizo la uhaba wa madawati.

  Meneja wa Uwajibikaji na Huduma za kijamii wa Kampuni ya Uchimbaji gesi ya PanAfrican Energy (CSR Manager) Andrew Kashangaki akitoa neno wakati akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Mh. Juma A. Njwayo madawati 800 yatakayosaidia watoto 2400 na kupunguza tatizo la uhaba wa madawati.


  PANAFRICAN ENERGY TANZANIA YATOA MADAWATI 800 KWA WILAYA YA KILWA 

   Kapuni ya uchimbaji gesi asilia PanAfrican Energy jana imekabidhi madawati 800 kwa ajili ya shule za msingi wilayani Kilwa yenye thamani ya shilingi za kitanzania Milioni 104. Makabidhiano hayo yaliyofanyika katika Shule ya Msingi Masoko iliyopo wilayani humo katika hafla fupi iliyoandaliwa na Kampuni hiyo, huku ikishuhudiwa na wana habari, viongozi mbali mbali wa Halmashauri ya wilaya ya Kilwa wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo Mh. Juma Njwayo, walimu, wanafunzi na wananchi wa Kilwa Masoko. Msaada huo wa madawati kwa ajili ya wanafunzi wa shule za Msingi ni kuunga mkono Kampeni ya uchangiaji madawati iliyoanzishwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli.

  Akiongea wakati akipokea madawati hayo Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Mh. Juma Njwayo, ambaye alikua mgeni rasmi katika hafla hiyo aliwashukuru sana Kampuni ya PanAfrican Energy kwa msaada wao mkubwa wanaotoa kwa wilaya ya Kilwa. 
  “Kwa niaba ya wana Kilwa naomba kutoa shukrani zetu za dhati kabisa kwa PanAfrican Energy kwa siku zote kutuangalia kwa jicho la tatu kwa mmekua mkijitoa kawa hali na mali kuwezesha huduma mbali mbali katika Wilaya yangu Ya Kilwa. Leo napokea madawati 800 ambayo yatasaidia kupunguza uhaba wa madawati mashuleni kwani yatasaidia watoto 2400 kutokukaa chini, hili si jambo dogo kabisa hivyo mnahitaji pongezi. 
  Natoa wito kwa wadau wengine kuiga mfano huu walionesha PanAfrican Energy kwani bado tuna uhaba wa madawati katika shule zetu za msingi hapa Kilwa. Hapa katika Shule ya Msingi Masoko watapata madawati 145 ambayo yapo mbele yetu hapa na mengine 655 yaliyobakia yatagawiwa kwa shule zingine zenye uhaba huo. Tunategemea ifikapo katikati ya mwezi Julai tutakua tumemaliza tatizo la madawati katika shule za msingi wilayani humu. Pia alitoa wito kwa wanafunzi kutunza madawati hayo ili yaweze kunufaisha wanafunzi wengi zaidi.”

  “Mbali na kupata madawati pia tunawapongeza kwa kuwa na uzalendo na wilaya yetu kwani hata mzabuni aliyepata kazi ya kutengeneza madawati haya ni mwananchi wa Kilwa ambapo vijana kadhaa wamepata ajira kupitia kazi hiyo na kuongeza kipato chao. 
  Ukiachilia mbali swala la elimu Kampuni hii imekua mstari wa mbele katika swala la afya pia ambapo katika kuupunguza vifo vya kina mama na watoto wanatujengea jengo la Mama Ngojea katika hospitali yetu ya Wilaya ambako kabla yam waka huu kuisha tutakua tumeshakabidhiwa jengo hilo pia wanakarabati kituo cha afya cha Kilwa Masoko.” Aliongeza Mh. Njwayo.

  Naye Meneja wa Uwajibikaji na Huduma za jamii wa Kampuni ya Uchimbaji wa Gesi ya PanAfrican Energy Andrew Kashangaki alisema, “Ni furaha yetu kuona watoto wa kitanzania wanasoma kwa Amani bila kuwa na matatizo yeyote na ndomana tumesukumwa kuunga mkono sekta ya elimu nchini kwa kuanza na wilaya ya Kilwa. 
  Leo tunakabidhi madawati 800 kwa Mkuu wa Wilaya ya Kilwa yatakayosaidia kupunguza tatizo la watoto wetu kukaa chini na wadawati haya yatagawanywa kwa shule za msingi mbalimbali kutokana na uhitaji wao. Sisi kama wadau wa Elimu tumefanya kile tulichoweza kufanya hivyo tunaamini kwa madawati haya tunawawezesha watoto wa kitanzania watakaosomea katika shule hizo kutoa ujinga na tunatengeneza Taifa la wasomi.

  Aliongeza kwa kusema kuwa, “Tayari tuna programu ya kusomesha watoto kutoka kisiwa cha Songosongo ambako kila mwaka tunasomesha watoto 28, tumejenga mabweni kwaajili ya watoto wa kike kisiwani songosongo, pia ujenzi wa maabara za kisasa kwa ajili ya masomo ya sayansi kwa shule za Sekondari hiyo yote ni kuhakikisha tunaweka mazingira mazuri ya kusomea kwa watoto wetu.”

  Wilaya ya Kilwa ilikua ina uhaba mkubwa wa madawati tangu mwaka jana lakini inaaminika kuwa ifikapo katikati ya mwezi Julai watakua wameshatatua tatizo hilo. Wamepata madawati kutoka kwa wadau mbalimbali ikiwemo Kampuni ya Uchimbaji gesi ya PanAfrican Energy iliyotoa madawati mengi zaidi yaw engine, huu ni mfano wa kuigwa kwa wadau wengine kwani mtoto wa mwenzako ni wako na kila mtoto ana haki ya kusoma katika mazingira rafiki.

  0 0

  Wabunge wa Upinzani wakitoka Bungeni baada ya dua kusomwa na Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson Juni 16, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akijibu maswali bungeni mjini Dodoma Juni 16, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri .kuu)
  Wageni waliofika Bungeni mjini Dodoma kujionea shughuli  mbalimbali za bunge wakifuatilia kipindi cha maswali kwa Waziri Mkuu  Juni 16, 2016.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akiteta na Mbunge wa Nkansi Kaskazini, Ally Kessy bungeni mjini Dodoma Juni16, 2016.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa zamani wa Singida mjini , Mohammed Dewji kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Juni 16, 2016.

  0 0

  Mkurugenzi Msaidizi Maji Shirikishi kutoka Wizara ya Maji na Umwagiliaji Bw. Sylivester Matemu akiongea na waandishi (hayupo pichani) kuhusu Maadhimisho ya 6 ya Wiki ya Maji Barani Afrika na Mkutano wa 10 wa Baraza la Mawaziri wa Maji wa Nchi za Afrika utakaofanyika kuanzia tarehe 18-22 Julai 2016. Kulia ni Afisa Mawasiliano wa Wizara hiyo Bw. Dennis Kiilu.

  Frank Mvungi- Maelezo

  Tanzania Mwenyeji maadhimisho ya 6 ya wiki ya Maji Barani Afrika na Mkutano wa 10 wa Baraza la Mawaziri wa Maji wa Nchi za Afrika yatakayofanyika Julai,2016 Jijini Dar es salaam.

  Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi Msaidizi Maji Shirikishi kutoka Wizara ya Maji na Umwagiliaji Bw. Sylivester Matemu wakati wa mkutano na waandishi wa Habari leo jijini Dar es salaam.

  Mgeni Rasmi katika Ufunguzi wa Maonyesho ya Wiki ya maji yatakayofanyika kabla ya mkutano wa Baraza la Mawaziri atakuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa.

  Akifafanua Matemu amesema kuwa mkutano huo utahusisha washiriki zaidi ya 1000 kutoka mataifa 54 kutoka Bara la Afrika na wengine kutoka nje ya Afrika.Maadhimisho hayo yataambatana na maonyesho ya shughuli za wadau wa sekta ya maji na umwagiliaji, kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es salaam.

  Kauli mbiu ya kongomanao hilo ni “ Kufikia lengo la maendeleo Endelevu Juu ya usalama wa Maji na usafi wa mazingira” alibainisha Matemu.Mkutano huo utawasaidia wataalamu wa maji kutoka Mataifa mbalimbali ya Afrika kujadiliana kuhusu mikakati mbalimbali itakayosaidia kupambana na changamoto zinazoikabili sekta ya maji katika bara la Afrika.

  Akizungumzia faida za Mkutano huo Matemu amesema kuwa utasaidia kufungua fursa mbalimbali zilizopo katika sekta ya maji na Sekta nyingine ikiwemo kukuza na Kutangaza vivutio vilivyopo hapa nchini hali itakayosaidia kukuza Utalii.

  0 0


  Na. Immaculate Makilika- MAELEZO, Tarehe 16.06.2016

  WAFANYABIASHARA wa Tanzania wametakiwa kutumia fursa za biashara zinazopatikana katika soko la nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kuuza bidhaa zao ndani ya Jumuiya hiyo.

  Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Mindi Kasiga alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.

  “Wafanyabiashara wanatakiwa kuchangamkia fursa ya biashara katika soko la pamoja kwa kuwa ni haki yao na ni utekelezaji wa malengo ya Mkataba wa uanzishwaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kifungu cha tano ambapo ilianzishwa itifaki ya umoja wa forodha ” ,alisema Bi. Mindi

  Wafanyabiashara hao pamoja na wasafirishaji wanaotaka kufanya biashara katika soko la Jumuiya hiyo watatakiwa kuonesha cheti cha uasilia wa bidhaa wakati wakiingia nchi wananchama wa Jumuiya hasa kwa wafanyabiashara wadogo wenye bidhaa zisizozidi dola za kimarekani 2000, ambapo hawalazimiki kuwa na wakala wa forodha.


  Wanatakiwa kufuata utaratibu kwa kufika katika kituo chochote cha forodha kilichopo mpakani wakiwa na bidhaa zao ili wapewe cheti cha uasilia wa bidhaa.Naye, Mkurugenzi wa Biashara, Uwekezaji na Sekta za Uzalishaji, katika Wizara hiyo, Bw. Geofrey Mwambe, amesema ni vyema wafanyabiashara wakatoa taarifa endapo watakumbana na vikwazo visivyo vya kiforodha kupitia mfumo wa ujumbe mfupi kwa kuandika neno ‘NTB’ kwenda namba 15539.

  Bw. Mwambe amesema pia ,madereva wanaosafirisha mizigo kwenda nchi wanachama watakapokutana na vikwazo visivyo vya kiforodha barabarani watoe taarifa kwa Jeshi la Polisi kupitia namba 0713631780.

  Kwa mujibu wa Mkataba wa uanzishwaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kifungu namba 5 ambapo Jukuiya ilianzisha Itifaki ya Umoja wa Forodha (East African Community Customs Union) wafanyabiashara wa nchi wanachama wa Jumuiya hiyo wana fursa za kufanya biashara kwa kuuza bidhaa zao ndani ya nchiwanachama wa Jumuiya hiyo ambazo ni Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi bila kutozwa ushuru wa forodha ilimradi bidhaa zao zimezingatia vigezo na kufuata utaratibu ulioainishwa katika itifaki hiyo.

  Japokuwa Sudani ya Kusini imeridhia kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki bado fursa za kufanya biashara nchini humo hazijakamilika.

  0 0

  TANGAZO KWA UMMA

  KATIKA KUADHIMISHA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA OFISI YA MAKAMU WA RAIS INAWAKARIBISHA WANANCHI WENYE KERO/ MAONI/CHANGAMOTO KUHUSU MASUALA  YA  MUUNGANO NA MAZINGIRA, KUFIKA UKUMBI MDOGO WA KARIMJEE (COUNCIL CHAMBER) TAREHE 21 JUNE, 2016.  RATIBA YA KUWASIKILIZA WANANCHI ITAKUWA KUANZIA SAA SAA 3 HADI 7 MCHANA.

  0 0


  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dk. Stephen Kebwe mara baada ya kuwasili mkoani hapo ambapo atahudhuria sherehe ya siku wahitimu wa chuo cha Mzumbe ,juni 17, 20016 mjini hapo.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Manisapaa ya Morogoro mjini Ndugu Fikiri Juma mara baada ya kuwasili mkoani hapo ambapo atahudhuria sherehe ya siku wahitimu wa chuo cha Mzumbe ,juni 17, 20016 mjini hapo.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Viongozi wa chuo cha Mzumbe mara baada ya kuwasili mkoani hapo ambapo atahudhuria sherehe ya siku wahitimu wa chuo cha Mzumbe ,juni 17, 20016 mjini hapo


  0 0


  Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Bi. Salma Ali Hassan akiongea na waandishi wa Habari(hawapo pichani) kuhusu hali ya mtoto wa Tanzania na mazingira hatarishi wanayokutana nayo ikiwemo ubakaji, ulawiti na unyanyasaji wa kijinsia. Kushoto ni Mkurugenzi wa Haki za Binadamu kutoka Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Bw. Francis Nzuki 

  Mkurugenzi wa Haki za Binadamu kutoka Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Bw. Francis Nzuki akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu Mapendekezo ya Tume hiyo kwa Serikali na Jamii katika kuhakikisha Ulinzi na Usalama kwa Mtoto unaimarika. Katikati ni Kamishna wa Tume hiyo Bi. Salma Ali Hassan.


  0 0

  KATIKA kusherekea siku ya mtoto wa Africa, Benki ya CRDB Tawi la Mlimani City limetoa zawadi mbalimbali kwa watoto na kimama waliojifungua siku ya leo.

  Zawadi hizo zilizolenga kutambua mchango wa watoto wa kiafrica ambao ndio wajenzi wa taifa pamoja na wateja wa baadae wa taasisi za kibenki.

  “Katika kusherekea siku hii adhimu na muhimu, Benki ya CRDB kupitia tawi lake la Mlimani City tumekuja kutoa zawadi kwa mama zetu hawa maana huwezi kusherekea siku ya mtoto bila kumpongeza na mama pia pamoja na kuwatakia kila la kheri wale ambao wanatarajia kujifungua,” alisema Mkurugenzi wa tawi hilo, Allen Kilango.

  Zawadi hizo zenye thamani ya shillingi million 3.2 zilitolewa katika hospitali ya Sinza Palestina. Tawi hilo lilitoa sukari, maji, sabuni za kufulia, majani ya chai, Pampas pamoja na vifaa vingine kwa ajili ya kuwatunza watoto wachanga.

  Akitoa shukrani kwa niaba ya wazazi wengine waliopo wodini, Tunu Tebesi amesema wanashkuru sana kwa msaada huo na umewapa moyo sana kama wamama na pia kuwasaidia watoto wao maana wengine walikuwa hawana uwezo wa kununua baadhi ya vitu walivyopewa.
  Katika siku hiyo ya mtoto wa Africa leo, jumla ya watoto 45 walizaliwa katika hospitali hiyo jana, wakiume wakiwa 15 na wakike 30.
  Mkurugenzi wa benki ya CRDB tawi la Mlimani City, Allen Kilango akitoa msaada wa Pampers kwa mama aliyejifungua leo katika hospitali ya Palestina-Sinza jijini Dar es Salaam leo.ikiwa ni kuadhimisha siku ya Mtoto wa Afrika ambayo hufanyika kila Juni 16 kila mwaka.
  Wafanyakazi wa Benki ya CRDB wakiongozwa na Mkurugenzi wa CRDB tawi  la Mlimani City, Allen Kilango akiwa katika picha ya Pamoja na wafanyakazi wa Hospitali ya Palestina jijini Dar es Salaam leo.

  Wafanyakazi wa CRDB tawi la Mlimani City wakipangapanga vitu vya msaada wakati walipotembelea katika hospitali ya Palestina-Sinza jijini Dar es Salaam leo.

  Mkurugenzi wa tawi hilo, Bw Allen Kilango watatu kutoka kushoto akizungumza na wafanyakazi wa benki hiyo tawi la Mlimani City jijini Dar es Salaam leo katika hospitali ya Palestina-Sinza.
  Mkurugenzi wa benki ya CRDB tawi la Mlimani City, Allen Kilango akitoa msaada wa Pampers kwa mama aliyejifungua leo katika hospitali ya Palestina-Sinza jijini Dar es Salaam leo.
  Meneja uhusiano wa wateja wajasiriamali wa Benki ya CRDB Tawi la Mliamani City, Martha Ngowi akitoa msaada kwa kinamama waliojifungua leo katika hospitali ya Palestina-Sinza jijini Dar es Salaam.
  Afisa wa benki  ya CRDB Tawi la Mlimani City, Fatma Tinna akitoa msaada kwa mama aliyejifungua leo katika hospital ya Palestina-Sinza jijini Dar es Salaam ikiwa ni kuadhimisha siku ya Mtoto wa Afrika ambayo hufanyika kila Juni 16 kila mwaka.
  Meneja uhisiano wa wateja binafsi Stephen Makundikushoto msaada kwa mama aliyejifungua leo katika hospital ya Palestina-Sinza jijini Dar es Salaam ikiwa ni kuadhimisha siku ya Mtoto wa Afrika ambayo hufanyika kila Juni 16 kila mwaka.
  Wafanyakazi wa benki ya CRDB tawi la Mlimani City wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Hospitali ya Palestina-Sinza jijijini Dar es Salaam leo walipo tembelewa na wafanyakazi wa benki hiyo.

  0 0

  Sehemu ya wadau wa mawasiliano wakimsikiliza mkuu wa  mkoa hayupo pichani leo jijini Dar es Salaam.
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza katika mkutano wa wadau mawasiliano juu uzimwaji wa simu feki leo katika ukumbi wa Anatoglo jijini Dar es Salaam.

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
  Watanzania wametakiwa kutumia simu zenye viwango na kuachana simu bandia ambazo hata kiafya si salama kwa matumizi ya binadamu.

  Hayo ameyasema leo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda wakati mkutano wa wadau wa mawasiliano kuelekea uzimaji wa simu leo usiku wa kuamkia kesho, Makonda amesema TCRA imethubu kutoa huduma bora  kwa wananchi katika mawasiliano.

  Amesema TCRA imeweza kupambana tangu uzimaji wa analojia kuingia digitali ambapo Tanzania imekuwa nchi ya mfano katika utekelezaji wa vitendo katika masuala mawasiliano.

  Makonda amesema hata katika sheria ya mtandao baadhi ya watu walikuwa wanapinga ili kuweza kuendelea kutukana katika mitandao ambapo TCRA imeweza kufanikiwa kufanya hivyo.
  Makonda amewataka wadau kuja na mawazo ya kuboresha huduma ya mawasiliano nchini katika ulinzi wa taifa.

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Balozi wa Qatar hapa nchini Mhe Abdallah Jassim Al Maadadi Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 16, 2016
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Qatar hapa nchini Mhe Abdallah Jassim Al Maadadi Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 16, 2016.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiagana na Balozi wa Qatar hapa nchini Mhe Abdallah Jassim Al Maadadi baada ya kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 16, 2016
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Spika wa Bunge Mstaafu na mwenyekiti mpya wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF), Mama Anne Makinda Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 16, 2016
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiwa katika mazungumzo na Spika wa Bunge Mstaafu na mwenyekiti mpya wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF), Mama Anne Makinda Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni. PICHA NA IKULU.


  Tanzania inatarajia kufungua Ubalozi wake nchini Qatar kwa lengo la kuendeleza na kuimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano kati ya nchi hizo huku ikitilia mkazo katika sekta za gesi asilia, utalii, usafiri wa anga na mawasiliano.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema hayo leo tarehe 16 Juni, 2016 Ikulu Jijini Dar es salaam alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Qatar hapa nchini Mhe. Abdallah Jassim Al Maadadi.

  Pamoja na kutangaza kuufungua Ubalozi wake nchini Qatar Dkt. Magufuli amemuomba Balozi huyo kufikisha ujumbe kwa Kiongozi wa Qatar Sheikh Tamim bin Hamad Al Thani na Jumuiya ya wafanyabiashara wa Qatar kwamba zipo fursa nyingi za ushirikiano zinayoweza kufanyiwa kazi, huku akibainisha uwepo wa gesi asilia zaidi ya futi za ujazo Trilioni 57 na mpango wa kufufua shirika la ndege la taifa (ATCL).

  "Najua Qatar ina uzoefu katika maeneo hayo na sisi Tanzania tungependa tushirikiane nanyi kuwekeza na kubadilishana uzoefu ili fursa hizo zilete manufaa kwa pande zote mbili" Amesema Rais Magufuli.

  Kwa upande wake Balozi wa Qatar hapa nchini Mhe. Abdallah Jassim Al Maadadi amemshukuru Rais Magufuli kwa nia yake ya kufungua Ubalozi wa Tanzania nchini Qatar na kuimarisha zaidi ushirikiano na uhusiano na nchi hiyo, na amemuahidi kufikisha ujumbe kwa Kiongozi wa Qatar na Jumuiya ya wafanyabiashara wa nchi hiyo ili waje kuwekeza Tanzania. 

  Wakati huo huo, Rais Dkt. John Pombe Magufuli leo amekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ambaye pia Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anne Makinda, Ikulu Jijini Dar es salaam.

  Baada ya mazungumzo hayo Mhe. Makinda amesema mazungumzo yao yameuhusu Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya na kwamba amemhakikishia kuwa amejipanga kuhakikisha mfuko huo uliobeba matumaini ya huduma za  matibabu ya watanzania unaboreshwa zaidi na dosari zinazolalamikiwa na wanachama zinafanyiwa kazi. 


  Gerson Msigwa 
  Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU 
  Dar es salaam 
  16 Juni, 2016.

  0 0

  Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inawakumbusha walipakodi wote kulipa Kodi ya Mapato na Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kabla ya tarehe 30 Juni 2016 ili kuepuka usumbufu na msongamano.  TRA pia inawakumbusha wafanyabiashara wote wa Dar es Salaam ambao mauzo ghafi ni kati ya  shilingi millioni 14 na milioni 20 kwa mwaka kufika ofisi za TRA katika mikoa yao husika kuchukua mashine za EFDs kabla ya tarehe 30 Juni 2016. Baada ya tarehe 30 Juni, zoezi la kugawa bure mashine za EFDs katika mkoa wa Dar es Salaam litasitishwa.    Kwa maelezo zaidi tafadhali wasiliana na kituo cha huduma kwa wateja simu namba: 0800750075 au 0800780080   Limetolewa na:

  Idara ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi

  Mamlaka ya Mapato Tanzania

  Dar es Salaam.

   

  “PAMOJA TUNAJENGA TAIFA LETU”  0 0

  NA BASHIR NKOROMO.

  KITUO cha Ufundi cha Kilimo na Maendeleo Vijijini (Technical Centre for Agricultural and Rural Cooperation, CTA) chenye makao makuu mjini Wageningen, Uholanzi kimemteua Rais Mstaafu Dk. Jakaya Kikwete kuwa Balozi wa Heshima (Goodwill Ambassador) wa Maendeleo ya Kilimo katika Mabara ya Afrika, Karibiani na Pasafiki.

  Katika barua iliyokabidhiwa na mjumbe wa Bodi ya CTA, Prof. Faustin Kamuzora, CTA wameainisha kuwa Dk. Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM, Taifa, ameteuliwa kwa kutambua mchango wa juhudi zake katika kukiendeleza kilimo nchini Tanzania na barani Afrika.

  Katika wadhifa wake huo mpya, CTA imemuomba Dk. Kikwete aweze kuiwakilisha katika makongamano ya kimataifa ambapo atazungumzia umhimu wa kukiendeleza kilimo kwa ajili ya kutoa fursa ya ajira zenye staha kwa vijana na wanawake katika nchi za barani Afrika, Karibiani na Pasifiki. Pia ataisaidia CTA katika kuandaa makala na kufanya mahojiano na waandishi wa habari katika nchi mbalimbali.

  Dk. Kikwete amekubali uteuzi huo na kuahidi kushirikiana na CTA katika kutekeleza mambo ambayo ameombwa kuisaidia na taasisi hiyo ambayo ni ushirikiano wa Umoja wa Ulaya na Kundi la nchi za Afrika, Karibiani na Pasifiki wenye makao makuu mjini Brussels, Ubelijiji.

  Prof. Kamuzora ambaye pia ni Katibu Mkuu, Mawasiliano ni mjumbe wa Bodi ya CTA akiwakilisha nchi za ukanda wa Afrika Mashariki kwa miaka mitano tangu 2013 hadi 2018.

  0 0


  Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Bing’i  Issa, wa kwanza kushoto na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Kazi Duniani Mary Kawar, wa kwanza kulia, wakimkabidhi mfano wa cheki yenye thamani ya fedha za kitanzania 15,323,000/=kijana Gilbert Tarimo wa Inoge Rabbit Farm baada ya kuibuka mshindi namba moja kwa wajasiriamali wanaoanza katika shindano la michanganuo ya kibiashara lijulikanalo kama Ajira Yangu lililoratibiwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) kwa ushirikiano na Shirika la Kazi Duniani (ILO). Shindano hilo lilihusisha zaidi ya michanganuo ya kibiashara 800 kutoka kwa vijana mbalimbani nchini .
  Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi kiuchumi Bing’i Issa, wa kwanza kushoto na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Kazi Duniani Mary Kawar, wa kwanza kulia, wakimkabidhi mfano wa cheki yenye thamani ya fedha za kitanzani kijana Linda Nasson baada ya kuibuka mshindi namba nne kwa wajasiriamali wanaokua katika shindano la michanganuo ya kibiashara lijulikanalo kama Ajira Yangu lililoratibiwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) kwa ushiriano na Shirika la Kazi Duniani (ILO). Shindano hilo lilihusisha zaidi ya michanganuo ya kibiashara 800 kutoka kwa vijana mbalimbani nchini 
  Mgeni Rasmi Beng’i Issa, Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) akitoa hutuba wakati wa sherehe za kugawa zawadi kwa washindi wa shindano la Ajira Yangu siku ya Jumatatu ya tarehe 13/06/2016. Kongamano hilo liliandaliwa kwa pamoja na Baraza la Taifa la Uwwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) kwa ushirikiano na Shirima la Kazi Duniani (ILO) .

   Dr. Mary Kawar, Mkurugenzi Mkazi, Shirika la Kazi Duniani (ILO) akiongea na vijana (hawapo pichani) pamoja na wageni waalikwa wakati wa ufunguzi rasmi wa sherehe za kutoa zawadi kwa washindi wa shindano la kuandaa michanganao ya kibiashara lijulikanalo kama Ajira Yangu. Sherehe hizo zilifanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam na kukutanisha Zaidi ya vijana 400 kutoka mikoa mbalimbali nchini. Kongamano hilo liliandaliwa  kwa pamoja na Baraza la Taifa la Uwwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) kwa ushirikiano na Shirima la Kazi Duniani (ILO).

   Paul Mashauri, mjasiriamali na mwanzilishi wa Masterclass Worldwide (wa  kwanza kushoto) Mercy Kitomari, mjasiriamali na mwanzilishi wa NELWA Gelato ( katikati) na Immaculate Steven, mjasiriamali na mwanzilishi wa Lavender Catering ( wa kwanza kulia) wakisikiliza kwa makini maswali kutoka kwa vijana wakati wa kongamano la Ajira Yangu lililofanyika katika hoteli ya Serena siku ya tarehe 13/06/2016. Kongamano hilo liliandaliwa kwa pamoja na Baraza la Taifa la Uwwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) kwa ushirikiano na Shirima la Kazi Duniani (ILO) .
  Dr. Sebastian Ndege, mjasiriamali na Mkurugenzi wa Ndege Insurance Brokers (wa kwanza kushoto), Modesta Lilian Mbughuni, mjasiriamali na mwanzilishi wa The Professional Approach Group (katikati) na Ruge Mutahaba, Mkurugenzi wa Clouds Media Group wakijadili mada katika kongamano la Ajira Yangu lililofanyika katika hoteli ya Serena juni 13 2016


older | 1 | .... | 882 | 883 | (Page 884) | 885 | 886 | .... | 1897 | newer