Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 878 | 879 | (Page 880) | 881 | 882 | .... | 1896 | newer

  0 0

  Benjamin Sawe-Maelezo.

  HISTORIA ya jina la Kariakoo na soko la Kariakoo inaanzia tangu enzi za ukoloni wa Mjerumani wakati Tanzania Bara ikiitwa Tanganyika.Mahala lilipo soko hilo palijengwa jengo la utawala wa Wajerumani ambalo lilikusudiwa litumike kama ukumbi wa kuadhimisha sherehe za kutawazwa kwa Mfalme Kaiser Wilheim wa Ujerumani kwa wakati huo.

  Hata hivyo baada ya jengo kukamilika halikutumika kama ilivyokusudiwa kuwa na badala yake lilitumika kama kambi ya kikosi cha wapagazi waliobeba mizigo ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia waliojulikana kama Carrier Corps.

  Jina hilo la maaskari wabeba mizigo katika Kiswahili lilitamkwa ‘karia- koo’ na liliendelea kutumika kama jina la eneo lote linalozunguka jengo hili la Soko la Kariakoo.Meneja Mkuu wa Soko la Kariakoo, Florens Seiya anasema baada ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia kuisha rasmi mwaka 1919 na nchi Tanganyika kuanza kutawaliwa na Waingereza, jengo hilo lilianza kutumika kama soko na kuhudumia wakazi wa Dar es Salaam.

  Anasema wakati huo wafanyabiashara walikuwa wakiuza bidhaa zao sakafuni kwa sababu hapakuwa na meza. Wafanyabiashara hao waliendelea kufanya biashara zao sakafuni hadi miaka ya 1960, meza za saruji zilipojengwa. Seiya anasema kwa kadiri jiji la Dar es Salaam lilivyokua na wakazi wake kuongezeka, ndivyo soko hilo la lilivyozidiwa na kushindwa kumudu kutoa huduma nzuri kwa wananchi.

  Wafanyabiashara walifanya shughuli zao katika hali ngumu kwa sababu kulikuwa na msongamano mkubwa wa watu pia hapakuwepo ghala za kuhifadhia bidhaa.Hali hiyo iliwafanya viongozi wa halmashauri ya jiji kuona haja ya kuwa na soko kubwa na la kisasa kulingana na maendeleo ya jiji, na hivyo wakaanza kujadili uwezekano wa kujenga soko jipya kubwa na la kisasa. Uamuzi wa kujenga Soko Kuu la Kariakoo ulifanywa na serikali mwaka 1970 ambapo Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam iliagizwa kujenga soko jipya la kisasa ambalo lingechukua nafasi ya soko la zamani.

  Anasema matarajio ya serikali ya kujenga soko hilo yalikuwa ni kuwapatia wakazi wa jiji soko kubwa la chakula ambalo lingetosheleza mahitaji yao kwa muda wa miaka 50 hadi 70 Mipango ilikamilika na ujenzi ulianza rasmi Machi 1971.


  Ramani ya jengo la soko ilitayarishwa na mchoraji wa ramani za majengo Mtanzania Beda Amuli. Kwa mujibu ya machapisho yanayoelezea historia ya soko hilo, mkandarasi huyo alitakiwa kwenda kujifunza katika nchi za Accra – Ghana na Lusaka-Zambia, kuangalia masoko yaliyojengwa katika miji hiyo miwili, ndipo atengeneze ramani yake, ambalo ndiyo soko linaloonekana hivi sasa.

  Anasema kuwa, mkandarasi aliyechora jengo hili ameweka baadhi ya maumbo yanayofanana na majengo hayo aliyokwenda kuyatazama. Hii ndiyo sifa pekee inalolifanya soko hili la Kariakoo kuwa la tofauti na masoko mengine katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati.

  Ujenzi wa soko ulikamilika Novemba 1975 kwa gharama ya Sh milioni 22 na kufunguliwa rasmi Desemba mwaka huo huo ambapo Rais wa Kwanza wa Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere alikuwa mgeni rasmi. Jengo la Soko Kuu la Kariakoo lipo katika kiwanja namba 32 mtaani Kariakoo, katikati ya makutano ya mtaa wa Mkunguni na mtaa wa Nyamwezi na limezungukwa na mitaa ya Nyamwezi, Mkunguni, Sikukuu na Tandamti.

  Soko hilo lina majengo mawili ambayo yameunganishwa katika Ghorofa ya chini ya ardhi. Jengo la kwanza linaweza kuitwa soko kubwa na jengo la pili soko dogo. Soko kubwa limegawanyika katika sehemu tatu ambayo ni ghorofa ya kwanza, sehemu ya katikati na ya chini maarufu kama shimoni.
  Eneo la Shimoni kuna mabucha 16 yanayouza nyama iliyokaguliwa kiafya toka mikoa ya Dodoma, Mwanza na Shinyanga, na samaki wabichi toka maziwa na mito ya Tanzania. 

  Soko dogo ni la rejareja ambalo si tofauti na masoko mengine katika Jiji la Dar es Salaam.
  Ingawa eneo la Kariakoo limezungukwa na maduka yanayouza bidhaa mbalimbali, bado Soko la Kariakoo ndio soko kuu la mazao na bidhaa ya kilimo nchini. Linauza mazao kwa bei ya jumla ya rejareja pamoja na vifaa vya kilimo.Shirika la Masoko ya Kariakoo (SMK) linasimamia uendeshaji wa biashara za Soko la Kariakoo, kuweka kipaumbele katika shughuli za biashara mbili: Anasema shirika linakodisha ardhi ya biashara kwa wauzaji wa Rejareja.

  Pia eneo la soko hilo lina maduka 82 katika soko kuu, yanayokodishwa kwa SMK kwa wauzaji wa rejareja. Mbali na mazao ya kilimo, maduka mengi yanauza vifaa vya kilimo na elektroniki. Pia, soko linatoa baadhi ya maduka nje yanayouza mboga za majani za rejareja katika soko dogo la nje.Kuhusu uendeshaji wake shirika hilo linasimamia soko la jumla kwa mazao ya kilimo na jamii ya samaki wakavu linalofanyika eneo la soko. SMK inatoza asilimia ya faida ambayo si zaidi ya asilimia nane tu ya bei ya mauzo kwa biashara ya jumla. Vile vile shirika linawatoza wafanyabiashara wa jumla ada ya usajili.

  Kwa masoko ya jumla na rejareja, Shirika linaweka daraja kati ya wakulima na wateja, ili wateja waweze kupata mahitaji yao yote ya nyumbani katika sehemu moja kwa bei nafuu na kuleta uthabiti kwa sekta ya kilimo ya nchi. Seiya anasema Soko la Kariakoo limekua na kupanuka kwa kiasi kukubwa ikilinganishwa na wakati lilipofunguliwa rasmi mnamo Desemba 8, 1974.
  Kwa kuwa muendeshaji mkuu wa biashara za mazao yatokayo mikoani kuingia katika jiji la Dar es Salaam. Pamoja na mafanikio makubwa yaliyopatikana hivi sasa soko hilo linakabiliwa na changamoto kubwa ya miundombinu.

  Ili kukabiliana na changamoto hiyo kuu na nyinginezo za kuboresha huduma kwa watumiaji wa soko, shirika linategemea kuunda upya soko na kuanzisha soko la jumla Dar es Salaam. “Kuanzisha vituo vipya vya jumla ni njia mojawapo ya mipango ya maendeleo ya jiji na maeneo yao ya jirani.
  Anaelezea miradi inayotarajiwa kuanzishwa na shirika hilo kuwa ni ujenzi wa upanuzi wa soko la rejareja la Kariakoo la leo, kukuza idadi ya magenge na kurahisisha maegesho ya magari sokoni. “Kwa sasa soko la nje linakosa maegesho salama ya magari, maduka ya kisasa, ofisi, vyoo, sehemu za kukaa kwa ajili ya mikutano na mikusanyiko ya kijamii.

  Uundaji upya wa soko utalisaidia shirika kukabiliana na baadhi ya changamoto,” anasema Seiya. Vile vile ujenzi wa soko la kisasa, litakalokuwa Buguruni-Chanika, wilaya ya Ilala na ujenzi wa kituo kingine cha soko litakalokuwa Tabata kwa ajili ya biashara na shughuli za burudani.
  Ili kufanikisha haya, Shirika linahitaji mtaji wa kuanzia ili kufikia malengo hayo . Kwa juhudi na ufadhili wa serikali, itatoa fursa kwa ubia binafsi kuwekeza kwenye mradi huu

  0 0  0 0

   Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bi Joyce Fisso akizungumza katika kikao kati ya Bodi hiyo na wadau wa filamu nchini kujadili maendeleo ya sekta ya filamu, kushoto ni Mwanasheria wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw. Patrick Kipangula.
   Mwanasheria wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw. Patrick Kipangula akifafanua hoja za kisheria katika kikao kikao kati ya Bodiya Filamu Tanzania  na wadau wa filamu nchini kujadili maendeleo ya sekta ya filamu, kulia ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bi Joyce Fisso.
   Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) Bw. Simon Mwakifwamba akichangia hoja katika kikao kati ya Bodi ya Filamu Tanzania  na wadau wa filamu nchini kujadili maendeleo ya sekta ya filamu.
    Mjumbe wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) Bw. Wiliam .J. Mtitu akichangia hoja katika kikao kati ya Bodi ya Filamu Tanzania  na wadau wa filamu nchini kujadili maendeleo ya sekta ya filamu.
  Baadhi ya washiriki kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, waandaaji wa filamu na wasanii wakifuatilia kikao kati ya Bodi ya Filamu Tanzania  na wadau wa filamu nchini kujadili maendeleo ya sekta ya filamu.( Picha zote na Shamimu Nyaki- WHUSM)

  0 0

   * 'Alikula sahani moja' na vigogo kuwania Urais na Uspika wa Bunge 2015
  * Ni msomi wa Shahada ya uzamivu (PhD) katika masuala ya usimamizi wa Biashara
  * Asema Dk. Magufuli atarejesha nchi katika misingi ya Mwalimu Nyerere

  NA BASHIR NKOROMO.

  Baada ya Uchaguzi Mkuu uliofayika mwezi Oktoba, 2015, na kuiacha Tanzania ikiwa na Rais wa awamu ya tano, ambaye ni Rais Dk. John Pombe Magufuli, yapo mambo mengi yamebaki katika kumbukumbu za Watanzania walio wengi.

  Kwa upande wa mchakato ndani ya CCM wa kuwapata wagombea kwenye nafasi hizo, yapo mengi ya kukumbukwa, lakini mojawapo ni majina ya waliokuwa mstari wa mbele katika vinyang'anyiro katika nafasi mbalimbali vilivyokuwa katika Uchaguzi huo Mkuu, ikiwemo kinyang'anyiro cha Urais, Makamu wa Rais, Uspika, Wabunge/ Wawakilishi na madiwani.

  Walioshiriki katika kinyang'anyiro hicho wamebaki katika kumbukumbu za vichwa vya Watanzania kutokana na sababu mbalimbali, ikiwemo namna walivyokuwa wakionyesha ushiriki wao katika kuomba nafasi wanazoziomba kugombea kwa tiketi ya CCM, baadhi yao wakiwa vigogo na wengine ikiwa ni mara yao ya kwanza kuwania uongozi wa juu nchini.

  Bila Shaka, Kijana Leonce Mulenda ni miongoni mwa wanachama wa CCM wanaokumbukwa  kutokana na umahiri alioonyesha wakati akishiriki katika kinyang'anyiro hicho.

  Kwa waliofuatilia kwa karibu kinyang'anyiro cha kuwania nafasi ya urais na Uspika wa Bunge, ndani ya CCM watakubali kwamba  Mulenda mwenye umri wa miaka 44, ni kijana anayeonyesha ari, utashi na hamu kubwa ya kutaka kuwatumikia Watanzania katika kulijenga Taifa.

  Katika harakati zake za kuonyesha ari, utashi na hamu ya kutaka kuwatumikia Watanzania, wakati wa vuguvugu hilo la Uchaguzi Mkuu uliomalizika mwaka jana wa 2015, Mulenda ni miongoni mwa Wanachama wa CCM, walioingia kwa kasi kubwa  katika kinyang'anyiro cha kuomba kuteuliwa kugombea Urais kwa tiketi ya CCM.

  Mulenda ambaye alizaliwa Januari 25, 1972, Biharamulo mkoani Kagera, katika kudhihirisha kuwa hakuwa akifanya mzaha, baada ya kuchukua fomu ya kuwania kuteuliwa kugombea urais kwa tiketi ya CCM, aliweza kutembea katika mikoa 15 ikiwemo mitatu ya Zanzibar, na kupata wadhamini 450 waliotakiwa kwa mujibu wa utaratibu.

  Wakati wapo baadhi ya waliochukua fomu za kuomba kuteuliwa kuwania nafasi hiyo ya Urais, walishindwa kujerejesha fomu zao, Mulenda aliweza kuwasilisha fomu zake Juni 25, 2015, kwa Katibu wa NEC, Oganaizesheni Dk. Mohammed Seif Khatib ambaye alipangwa kupokea fomu za wagombea wote kwa niaba ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.


  Baadaye katika mchakato wa kumpata mgombea Urais, Mulenda alibaki miongoni mwa makumi ya waliokosa kuteuliwa, katika hatua za awali wakiwemo, vigogo wengi kama aliyekuwa Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Bilali, Mawaziri Wakuu wastaafu Frederick Sumaye na Edward Lowassa.

  Japo wengine waliamua kuisusa CCM na kuamua kuhamia vyama vya upinzani akiwemo Lowassa na Sumaye, kada huyo wa CCM, Mulenda ni miongoni mwa wanachama waliokosa kuteuliwa lakini wakaridhika kwa sababu walifahamu kuwa katika mchakato wa uchaguzi wagombea wakiwa wengi na nafasi ni moja lazima wawepo wanaokosa.

  Kadhalika wanachama hao wa CCM ambao hawakuteteleka akiwemo Mulenda, walitambua kwamba, ikiwa lengo lao ni kuongoza Watanzania, si lazima waongoze wakiwa tu katika nafasi ya Urais wanaweza kuongoza wakiwa katika eneo lolote la uongozi na pia ikiwa kiu yao ni urais basi uchaguzi wa 2015 siyo wa mwisho ikiwa kiyama hakitatokea hivi karibuni hivyo wakati ukijiri tena watagombea.

  Baada ya kivumbi cha mchakato wa kuomba kuteuliwa kuwania urais kwa tiketi ya CCM kupita, kiliingia kingine cha kuwania nafasi ya Uspika wa Bunge, ambapo katika kinyang'anyiro hiki nako walijitosa wagombea wengi tena vigogo ambao ni mahiri akiwemo Spika wa zamani Samweli Sitta.

  Kwa kufahamu kwamba demokrasia inamruhusu, Mulenda naye aliingia pia kuwania nafasi hiyo ya kuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambapo alichukua fomu Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam, na baadaye kuirejesha ikiwa imekamilika kujazwa kwa usahihi.

  Hata hivyo katika kinyang'anyiro hicho pia hakupita, na siyo yeye tu, walikosa wengi kwa kuwa walioomba walikuwa lukuki na kama ilivyokuwa kwa urais, nafasi ya Uspika wa Bunge nayo ilikuwa moja, hivyo ilikuwa lazima wawepo watakaokosa miongoni mwa wagombea.

  Baada ya michakato hiyo sasa Mulenda anaendelea na shughuli zake akiendelea kuamini kwamba Chama Cha Mapinduzi (CCM) ndicho chama pekee nchini kitakachoweza kuwakomboa Watanzania kuelekea maisha bora.

  "Unajua wapo watu wanaodhani kuwa kipo Chama kinachoweza kuwa mbadala wa CCM katika kuwaletea maendeleo wananchi, fikra hizo ni potofu kabisa, CCM bado ndicho chama pekee, imara na chenye sera bora zinazotekelezeka tofauti na vyama vingine", alisema Mulenda ambaye ana kadi ya CCM yenye namba Ab 1353192.

  Anasema, anaamini CCM ndicho chama kinachofaa kuongoza Watanzania kwa sababu ya uwezo wake ambao umejengwa chini ya misingi imara iliyowekwa na muasisi wake, Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Nyerere tangu enzi za chama cha Tanganyika African National Union (TANU) ambacho CCM inaendeleza misingi yake.

  "Kwa kuwa misingi iliyowekwa na Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere na Hayati Abeid Aman Karume kwa upande wa Zanzibar, bado ni imara hadi sasa, CCM haiwezi kutetereka hasa ikizingatiwa kwamba katika misingi hiyo iliyowekwa na Baba wa Taifa ni yenye mlengo endelevu wa kujali hali za wanyonge", alisema Mulenda.

  Anasema, kitu ambacho huteteresha na baadhi ya watu kudhani CCM si chama cha wanyonge, ni kutokana na baadhi ya viongozi kusahau au kuipuuza misingi hiyo iliyowekwa na Baba wa Taifa, na hivyo kuanza kujiwekea misingi bandia kwa lengo la kujinufaisha wao binafsi.

  "Lakini sasa, baada ya Tanzania kumpata Rais Dk. John Magufuli,  hali inaelekea kubadilika na huenda ikaimarika kabisa kutokana na Rais huyu anavyojaribu kuiweka Nchi katika misingi ile iliyoasisiwa na Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere na Hayati Karume", alisema Mulenda.

  Licha ya kupenda siasa, Mulenda ni msomi amabaye  kwa sasa anaendelea na masomo ya Shahada ya uzamivu (udaktari) katika masuala ya Usimamizi wa Biashara (PhD-Bus.Mgt. (on studies), mada anayotafiti katika masomo yake hayo ni "Effectiveness of Forecasting value chain on improving production costs of oil and gas through extractive induestries in Tanzania, na utafiti huo ataufanyia  katika Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC).

  Wakati akiendelea na masomo hayo ya PhD, tayari alikwishafuzu Shahada ya Uzamivu ya Sayansi ya Uhasibu na Fedha (MSc. A&F) aliyopata mwaka 2014, katika Chuo Kikuu Cha Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam, akiwa  tayari  amemaliza Stashahada ya Uzamili katika fani ya Usimamizi wa Fedha (PGDFM) katika Chuo cha Uhasibu kilichopo Njiro mkoani Arusha, mwaka 2006.

  Kabla ya kufikia kiwango hicho cha elimu, Mulenda alikuwa pia ameshahitimu Stashahada ya Juu  katika chuo Nyegezi Social Training Institute (NSTI) ambacho sasa ni Chuo Kikuu cha St. Augustine kilichopo Mwanza, mwaka 1998.

  Mulenda kwa sasa ni mtumishi wa umma katika Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali akiwa katika cheo cha Mkaguzi wa Hesabu daraja la kwanza, na pia ni mwanzilishi na Mwenyekiti wa Asasi isiyo ya Serikali (NGo) ambayo inashughulikia masuala ya Kijamii katika kukuza uchumi  na kupunguza umasikini (Economic Growth and Social Welfare Foundation Gwrowth and Social Welfare-EGOSF), yenye usajili namba ooNGO/ooooo7736.

  0 0

  Wanafunzi kutoka vyuo vikuu vya Tanzania wanaochukua fani ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) wakionyesha vyeti vyao mara baada ya kumaliza programu ya wiki tatu ya“Seeds for the future” ambayo ilifanyika katika makao makuu ya Huawei Technologies yaliyopo Shenzhen, China. Programu hiyo inaendeshwa na kudhaminiwa na Kampuni ya mawasiliano na teknolojia, Huawei Tanzania.
  Wanafunzi kutoka vyuo vikuu nchini Tanzania wanaochukua fani ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) wakizungumza na Balozi wa Tanzania nchini China Mhe. Lt. generali (Mstaafu) Abdulrahaman A. Shimbo katika ufunguzi rasmi wa programu ya “Seeds for the future” ambapo wanafunzi 10 kutoka Tanzania walipata fursa ya kujifunza kwa vitendo juu ya fani hiyo ya teknolojia na mawasiliano kwa muda wa wiki tatu, programu iliyodhaminiwa na kampuni ya mawasiliano na teknolojia, Huawei Tanzania.
  Wanafunzi 10 kutoka vyuo vikuu vya hapa nchini wanaochukua fani ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) wakiwa katika picha ya pamoja walipotembelea sehemu ya makumbusho katika mji wa Shenzhen nchini China walipokuwa nchini humo kushiriki mafunzo kwa vitendo kupitia programu ya Seeds for the Future” inayoendeshwa na kudhaminiwa na kampuni ya mawasiliano na teknolojia, Huawei Tanzania.

  Shenzhen, China. 08 Juni 2016. Wanafunzi kutoka vyuo vikuu vya hapa nchini ambao walikwenda China kuhudhuria mafunzo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano  (TEHAMA), wameipongeza Kampuni ya Huawei Tanzania kwa kuanzisha mradi huo wenye lengo la kuongeza ufanisi kwenye masuala ya TEHAMA nchini na kuongeza uelewa juu ya katika sekta ya mawasilino na kuhamasiha ushiriki wa kimataifa katika Teknolojia ya habari na mawasiliano.

  Wakizungumza wakati wa mahafali baada ya mafunzo ya programu ya Seeds fo the Future" katika makao makuu ya Huawei Shenzhen nchini China, walisema wanatambua mchango mkubwa unaotolewa na Huawei ili kuleta maendeleo katika sekta ya teknolojia ya habari na mawasiliano nchini Tanzania.


  Mwanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Zanzibar (SUZA), Ahmed Sufiani Makame (22) alisema mafunzo waliyopata yamewawezesha kufahamu teknolojia mpya kabisa ambayo awali hawakuwa nayo na hawakuipata  katika vyuo vya nchini Tanzania, jambo lililowapa changamoto ili kuweza kukabiliana na mabadiliko yaliyopo katika sekta ya ajira watakapoajiriwa hapo baadaye.

  "Alisema katika karne hii ya 21 waajiri huhitaji wafanyakazi ambao wanauzoefu wa kutosha na elimu bora. Wanahitaji waajiriwa wao wawe na ujuzi na mtazamo chanya. Ninashukuru sana Huawei kwa kutupa nafasi ya kuvumbua mapya katika ulimwengu wa teknolojia.

  Alisema kutokana na mafunzo waliyoyapata nchini China, kwa sasa wamepata ujuzi ambao watautumia kutatua changamoto zilizopo zilizopo kwenye kampuni za mawasilino nchini Tanzania. Aliongeza kuwa, kupitia elimu masafa (e-learning), usalama wa mitandao, mpangilio wa miji, mifumo ya mtandao, 3G, 4g, mifumo ya data serikalini na hospitali ni mojawapo ya  vitu ambavyo vitaifanya Tanzania kuwa miongoni mwa nchi zilizopiga hatua kimaendeleo  katika sekta ya TEHAMA.

  "Wakati wa mafunzo yetu China, tuliona ni namna gani Huawei imejipanga na mabadiliko ya kiteknolojia wakiwa na kaulimbiu yao 'ulimwengu uliounganishwa'. Mafunzo tuliyoyapata yametupa mwanga kuzishauri kampuni za mawasiliano pamoja na serikali kuwa wanapaswa waendane na maendeleo ya teknolojia ya kisasa ulimwenguni," alisema.

  Alisema  amepata uzoefu  wa mifumo ya 3G NA 4G na mifumo inayotumika kwenye kompyuta na namna ya kuzitengeneza na kuingiza huduma ya HSI,VolP na IPTV, siyo tu kwa kujifunza kwa nadharia  bali pia ameweza kuitumia kwa vitendo.

  Kwa mujibu wa Meneja Uhusiano wa Huawei, Jimmy Liguo alisema "Programu ya Seeds for the Future" inaendeshwa ulimwenguni kote. Miongoni mwa miradi ambayo Huawei imeipa kipaumbele ni huo na itaendelea kuwekeza kwa muda mrefu kwenye programu hiyo.

  "Programu hiyo ilianzishwa na Huawei mwaka 2008 kwa lengo la kukuza uelewa katika masuala ya TEHAMA,  kuimarisha sekta ya mawasiliano, kuhamasisha ushiriki katika jamii ya kidijitali," alisema.


  Mwaka 2008 Huawei ilizindua programu kuwaendeleza wataalamu ambao wanahitajika kwa haraka ili kuendeleza sekta teknolojia ya habari na mawasiliano katika nchi ambazo Huawei inafanya kazi zake. Huawei imeazimia kuwezesha mafunzo ambayo yataimarisha elimu inayotolewa darasani iendane na mahitaji halisi katika sekta ya TEHAMA ili elimu hiyo iwe endelevu.

  Alisema katika nchi nyingi, bado kuna tatizo la mafunzo yanayotolewa hayaendania na kile kinachohitajika katika soko la ajira ulimwenguni, Hivyo watu wenye ujuzi wanatakiwa kupewa fursa za mafunzo zaidi ili kuweza kuitumia teknolojia ya kisasa.Kupitia Mradi wa Seeds for Future" Huawei imewezesha kutatua tatizo hilo.

  0 0

   Mhandisi wa Miradi (TANROADS) Mkoa wa Dar es salaam Bw.Ngusa Julius akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu ujenzi wa  Barabara zinazoendelea kujengwa ili  kupunguza msongamano  wa magari katika jiji La Dar es salaam, Kulia ni Afisa Habari wa wakala huo Bi Aisha Malima.
   Afisa Habari wa wakala wa Barabara (TANROADS) Bi Aisha Malima akitoa wito kwa wananchi kutunza barabara zinazojengwa na wakala huo ili ziweze kudumu kwa matumizi ya sasa na baadae.Kushoto ni  Mhandisi wa miradi Mkoa wa Dar es salaam Bw.Ngusa Julius.
  Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano wa TANROADS na vyombo vya Habari leo jijini Dar es salaam uliolenga kutoa tathmini ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya ujenzi wa barabra katika jiji la Dar es salaam inayolenga kupunguza tatizo la msongamano wa magari. Kulia ni Afisa Habari wa wakala huo Bi Aisha Malima.(Picha na frank Mvungi-Maelezo).


  Frank Mvungi-Maelezo

  Serikali yatumia Bilioni 2 kulipa Fidia ili kusaidia kukamilisha mradi wa ujenzi wa Barabara kwa kiwango cha lami kati ya Tanki Bovu na Goba Jijini Dar es salaam.

  Kauli hiyo imetolewa na Mhandisi wa Miradi wa TANROADS Mkoa wa Dar es salaam Bw. Ngusa Julius wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam.Akifafanua Mhandisi Ngusa amesema kuwa fidia kwa wakazi hao itakamilika kulipwa wiki hii ili kazi ya ujenzi wa Barabara hiyo iweze kukamilishwa kwa wakati hali itakayosaidia kupunguza msongamano wa magari.

  “Ujenzi wa barabara hii ukikamilika utasaidia kwa Kiasi kikubwa kupunguza foleni kwa kuwa itakuwa kiungo kati ya wakazi wa Mbezi Beach na Kimara na maeneo mengine ya jiji la Dar es salaam.” Alisisitiza Mhandisi Ngusa.Kwa upande wa Barabara ya kinyerezi Kifuru Mhandisi Ngusa amesema kuwa Milioni 431 zimetumika kulipa fidia na ujenzi wa Barabara hiyo unaendelea.

  Miradi ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lamai inayotarajiwa kukamilika katika kipindi hiki cha mwaka wa fedha 2015/2016 itasaidia kupunguza msongamano wa magari kwa kiwango kikubwa katika jiji la Dar es salaam.Awamu ya Tatu ya ujenzi itahusisha barabara za Goba - Wazo hill -Tegeta Kibaoni (13.0Km), Mbezi Mwisho - Malambamawili- Kifuru (6kM), Goba - Makongo ardhi (9km ) na Pia kukamilisha usanifu wa outering road Bunju B - Mpiji Magohe - Victoria Kifuru hadi Pugu kiltex 33.7.

  Wakala wa Barabara nchini TANROADS unatekeleza miradi mbalimbali ya ujenzi wa barabara katika jiji la Dar es salaam kwa kiwango cha lami ambapo barabara hizo zinatarajiwa kuondoa tatizo la msongamano wa magari katika jiji hilo.

  0 0

  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Mwigulu Nchemba akila kiapo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli Leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli akimkabidhi hati ya kiapo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Mwigulu Nchemba mara baada ya kumuapisha Leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
   Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba akila kiapo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli Leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli akisaini hati ya kiapo mara baada ya kumuapisha Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba Leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
   Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Mwigulu Nchemba wakipongezana mara baada ya kuapishwa Leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli akimpongeza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Mwigulu Nchemba mara baada ya kumuapisha Leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli akimpongeza Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba mara baada ya kumuapisha Leo Ikulu Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Mwigulu Nchemba.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba (kulia) na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Mwigulu Nchemba mara baada ya kuwaapisha Leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO .

  0 0

  Na Hassan Silayo-MAELEZO

  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Mwigulu Nchemba amewataka wafanyabiashara haramu ya kuuza madawa ya kulevya kuacha mara moja biashara hiyo badala yake watafute shughuli halali za kujiingizia kipato.

  Waziri Nchemba ametoa agizo hilo mara baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aliyemteua kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Leo Ikulu Jijini Dar es Salaam kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Mh.Charles Kitwanga ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.

  Aidha Waziri Nchemba alisema kuwa atahakikisha anasimamia Ulinzi na Usalama wa Raia na Mali zao kwa kuziba mianya inayohatarisha amani na utulivu katika nchi.

  Naye Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba amesema kuwa atahakikisha anashirikiana na wataalum wa sekta tatu zilizo katika Wizara yake ili kufanya mapinduzi katika maeneo hayo yaliyoajiri zaidi ya asiimia 80 ya Watanzania.

  Pia Waziri Dkt. Tizeba alisema kuwa Wizara itahakikisha inashugahulikia changamoto zinazozokabili vyama vya ushirika ambavyo vimekuwa havifanyi vizuri katika miaka ya hivi karibuni.

  Mawaziri walioapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Leo Ikulu Jijini Dar es Salaam ni Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Mwigulu Nchemba aliyekuwa Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi anayejaza nafasi iliyoachwa wazi baada ya Rais kutengua uteuzi wa Mh. Charles Kitwanga.

  0 0


  Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya, Bi. Mariam Mtunguja, akifungua rasmi mkutano wa wadau wa PSPF uliofanyika Jijini Mbeya hivi karibuni.
  Afisa Mwandamizi wa PSPF, Bw. Msafiri Mugaka, akisoma hotuba ya makaribisho kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa PSPF Bw. Adam Mayingu wakati wa mkutano wa wadau wa PSPF uliofanyika Jijini Mbeya hivi karibuni.
  Sehemu ya wadau waliohudhuria mkutano wa wadau wa PSPF uliofanyika Jijini Mbeya .
  Afisa Mwandamizi wa PSPF, Bw. Msafiri Mugaka, akitoa elimu kwa wadau wa PSPF katika mkutano uliofanyika Jijini Mbeya
  Afisa Mfawidhi wa PSPF Mkoa wa Mbeya, Bw. Edwin Msavangwa, akijibu hoja ya mmoja wa wadau katika mkutano wa wadau wa PSPF, kulia ni Afisa fedha Mwandamizi wa PSPF Bi. Hidaya Mganga.


  Picha ya pamoja ya wajumbe wa mkutano wa wadau wa PSPF pamoja na Mgeni Rasmi (katikati). Mkutano huo uliofanyika Jijini Mbeya hivi karibuni.  PSPF imesifiwa kwa kubuni bidhaa mpya kwa kuwanufaisha wanachama wake. Sifa hizo zilitolewa na Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya, Bi. Mariam Mtunguja, alipokuwa akifungua mkutano wa PSPF pamoja na wadau wake Mkoani Mbeya hivi karibuni.

  Katibu Tawala Mkoa Mbeya alisema kuwa mkopo wa elimu, mkopo kwa waajiriwa wapya na fao la uzazi litakaloanza kutolewa Julai mwaka huu vitatoa haueni kwa wanachama wa PSPF. “Kila mtu anaelewa jinsi vijana wetu wanavyopata tabu wanapoajiriwa, kwani unapopata ajira au wakati wa uzazi mahitaji yanakuwa mengi sana, hivyo kwa PSPF kuja na bidhaa hizi mpya mtakuwa mnasaidia vijana wetu kwa kiwango kikubwa” alisema Bi. Mtunguja.

  Kwa upande wa mkopo wa elimu, Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya, alipongeza PSPF kwa kuunga mkono juhudi za Serikali za kuhakikisha kila mtanzania anapata elimu. “Sisi wa upande wetu Serikalini tunajitahidi, lakini sasa tunafarijika kwa kuona PSPF nanyi mnasaidia eneo hili muhimu, asanteni na hongereni.”

  Katibu Tawala Mkoa Mbeya aliishukuru PSPF kwa kutoa misaada katika maeneo elimu, afya, uhifadhi wa mazingira na maendeleo ya jamii kwa lengo la kuunga mkono juhudi za Serikali za kuhakikisha kila mtanzania anapata maisha bora.

  Kwa upande wa washiriki, Katibu Tawala Mkoa Mbeya, aliwaasa kutumia vizuri fursa hii iliyotolewa na PSPF kwa kutatua changamoto wanazokabiliana nazo kuhusiana na mafao ya wanachama wa PSPF na kupata ufafanuzi sahihi kutoka taarifa potofu dhidi ya Mfuko.

  Kwa upande wa PSPF, mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa PSPF Adam Mayingu , Bw. Msafiri Mugaka, alisema Mfuko kwa upande wake umekuwa ukitekeleza vyema miongozo na maelekezo kutoka Serikalini na mamlaka zote. Akiainisha changamoto zilizopo, Bw. Mugaka, alisema changamoto kubwa ni kwa watumishi ambao wanakaribia kustaafu kushindwa kuwasilisha nyaraka muhimu zinazohitajika hivyo kuleta usumbufu kuandaa mafao kwa wakati. Aliomba wadau wa mkutano kuwaelimisha wanachama wa PSPF juu ya umuhimu wa kuwa na nyaraka sahihi na kuziwasilisha kwa wakati ili kuepusha usumbufu.

  Waliohudhuria ni maafisa utumishi, makatibu afya, maafisa kilimo, waratibu wa elimu kata pamoja na maafisa elimu msingi na sekondari.

  0 0


  Waziri wa Afya Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo akisalimiana na viongozi wa Chama na Serikali alipowasili Chaani Masingini kukagua kituo cha Afya cha kijiji hicho kufuatia mwaliko wa Mwakilishi wa Jimbo hilo Nadir Abdul- latif.
  Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo akitoa maelekezo kwa Mkuu wa Wilaya Kaskazi ‘A’ Hassan Ali Kombo na Daktari dhamana wa Wilaya hiyo Rahma Abdalla Maisra wakati akikitembelea kituo cha Afya cha Chaani Masingini.
  Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo akifuatana na viongozi wa Jimbo la Chaani wakiangalia tanuri la kuchomea taka za kituo cha Afya cha Chaani Masingini alipotembelea kituo hicho.

  Mwakilishi wa Jimbo la Chaani Nadir Abdul-latif akimkaribisha Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo kuzungumza na wananchi waliofika kituo cha Afya cha Chaani Masingi ambacho kinahitaji matengenezo makubwa.
  Waziri Mahmoud Thabit Kombo akizungumza na wafanyakazi wa kituo cha afya cha Donge na Kamati Kiongozi ya Jimbo hilo katika Kituo cha Afya cha Donge Wilaya Kaskazini B.
  Mkuu wa kituo cha Afya Donge vijibweni Miza Ali Ussi akitoa maelezo kwa Waziri wa Afya (hayupo pichani) alipotembelea kituo hicho kujua changamoto zinazowakabili.
  Mwakilishi wa Jimbo la Donge Dkt. Khalid Salum Mohammed akizungumza katika mkutano huo (kulia kwake) ni Mkuu wa kituo cha Afya Donge Miza Ali Ussi. Picha zote na Makame Mshenga/Maelezo Zanzibar.  Na RAMADHANI ALI/MAELEZO ZANZIBAR .

  Waziri wa Afya Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo amezitaka Kamati Kiongozi za Majibo kusimamia kikamilifu vituo vyao vya Afya na kuhakikisha majukumu waliyopangiwa wanayatekeleza kikamilifu ili kuimarisha huduma katika vituo hivyo.

  Alisema Serikali imebadili mfumo katika kusimamia vituo vya afya kwa kuvipeleka moja kwa moja kwa jamii kusaidia huduma ndogo ndogo huku Serikali kuu ikibakia na jukumu lake la msingi la kuvipatia vifaa vya matibabu, dawa na mishahara ya wafanyakazi.

  Waziri Mahmoud Thabit Kombo alieleza hayo alipofanya ziara ya kutembelea vituo vya Afya vya Mkoa wa Kaskazini Unguja kujua changamoto zinazowakabili wafanyakazi wa vituo hivyo katika kutoa huduma bora.

  Alisema huduma ya matengenezo madogo madogo, kulipia umeme na maji, kuviwekea uzio na ulinzi sasa vipo chini ya Kamati Kiongozi za Majimbo ambazo zinaundwa na Wabunge, Wawakilishi, Madiwani, Masheha na Mkuu wa kituo cha Afya husika.

  Aliongeza kuwa hivi sasa Serikali haitoa kipaumbele kujenga vituo vipya vya Afya bali inaelekeza nguvu zake kuviimarisha vituo viliopo kwa kushirikiana na mradi wa ORIO na Milele pamoja na Kamati Kiongozi za Majimbo.

  Aliwahakikishia wananchi wa Jimbo la Chaani kwamba kituo chao cha Afya cha Chaani Masingini, ambacho kimesitisha kutoa huduma kwa miaka mitano kutokana na kuwa kibovu, kitaanza kufanyiwa matengenezo makubwa hivi karibuni kupitia Mradi wa ORIO.

  Waziri wa Afya aliwataka viongozi na wafanyakazi wa sekta ya Afya kuwapa ushirikiano wa karibu wakunga wa jadi ambao wanatoa mchango mkubwa katika kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto wachanga wakati wa kujifungua.

  Alisema wakunga wa jadi bado wanaendelea kuaminiwa na wanachi wengi, hasa sehemu za vijijini, kutokana na huduma nzuri wanazotoa kwa wateja wao na ameshauri wapatiwe vitambulisho maalum ili waweze kutambulika.

  Aidha alisema Zanzibar imepata sifa kubwa mbele ya Jamii ya Kimataifa katika kupambana na Malaria na maradhi mengine yaliyokuwa yakiwasumbua wananchi, lakini hali sio nzuri katika kupunguza vifo vya wajawazito na watoto wachanga hivyo ametaka juhudi zaidi ifanywe kukabiliana na tatizo hilo.

  Akinamama wa Jimbo la Chaani walimueleza Waziri wa Afya kuwa wanapendelea zaidi kujifungua kwa wakunga wa jadi kutokana na kauli zisizoridhisha kutoka kwa wakunga wa vituo vya Afya wanapokwenda kujifungua.

  Walishauri kutolewa elimu ya ukarimu na upole kwa wakunga wa vituo vya afya ili kuwajengea imani wajawazito kwenda kujifungulia kwa wingi katika vituo hivyo.

  Mwakilishi wa Jimbo la Chaani Nadir Abdul-latif alimuhakikishia Waziri wa Afya kwamba yupo tayari kutoa kila msaada unaotakiwa ili kuona huduma za Afya katika Jimbo hilo zinaimarika.

  Waziri wa Afya alitembelea vituo vya Afya vya Chaani Masingini, Chaani Kikobweni na Kituo cha Afya Donge.

  0 0

  Mhandisi wa Miradi (TANROADS) Mkoa wa Dar es salaam Bw.Ngusa Julius akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu ujenzi wa  Barabara zinazoendelea kujengwa ili  kupunguza msongamano  wa magari katika jiji La Dar es salaam, Kulia ni Afisa Habari wa wakala huo Bi Aisha Malima.

  Frank Mvungi-Maelezo.
  SERIKALI yatumia Bilioni 2 kulipa Fidia ili kusaidia kukamilisha mradi wa ujenzi wa Barabara kwa kiwango cha lami kati ya Tanki Bovu na Goba Jijini Dar es salaam.

  Kauli hiyo imetolewa na Mhandisi wa Miradi wa TANROADS  Mkoa wa Dar es salaam Bw. Ngusa Julius wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam.

  Akifafanua Mhandisi Ngusa amesema kuwa fidia kwa wakazi hao itakamilika kulipwa wiki hii ili kazi ya ujenzi wa Barabara hiyo iweze kukamilishwa  kwa wakati hali itakayosaidia kupunguza msongamano wa magari.

  “Ujenzi wa barabara hii ukikamilika utasaidia kwa Kiasi kikubwa kupunguza foleni kwa kuwa itakuwa kiungo kati ya wakazi wa Mbezi Beach na Kimara na maeneo mengine ya jiji la Dar es salaam.” Alisisitiza Mhandisi Ngusa.

  Kwa upande wa Barabara ya kinyerezi  Kifuru Mhandisi Ngusa amesema kuwa Milioni 431 zimetumika kulipa fidia na ujenzi wa Barabara hiyo unaendelea.

  Miradi  ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lamai inayotarajiwa kukamilika katika kipindi hiki cha mwaka wa fedha 2015/2016  itasaidia kupunguza msongamano wa magari kwa kiwango kikubwa  katika jiji la Dar es salaam.

  Awamu ya Tatu  ya ujenzi itahusisha barabara za Goba - Wazo hill -Tegeta Kibaoni (13.0Km), Mbezi Mwisho - Malambamawili- Kifuru (6kM), Goba - Makongo ardhi (9km ) na Pia kukamilisha usanifu wa outering road Bunju B - Mpiji Magohe - Victoria Kifuru hadi Pugu kiltex 33.7.

  Wakala wa Barabara nchini TANROADS unatekeleza miradi mbalimbali ya ujenzi wa barabara katika jiji la Dar es salaam kwa kiwango cha lami ambapo barabara hizo zinatarajiwa kuondoa tatizo la msongamano wa magari katika jiji hilo.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiteremka kwenye basi la mwendo kasi baada ya kupanda na kujionea ubora na uzuri wa mabasi hayo ambayo yamerahisisha usafiri kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam.( Picna na OMR)

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati wa shughuli ya kukabidhi Futari na Chakula kwa watu wenye mahitaji maalum katika ofisi za UDA-RT Jangwani jijini Dar es Salaam.

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki dua maalumu wakati wa shughuli ya kukabidhi Futari na Chakula kwa watu wenye mahitaji maalum katika ofisi za UDA-RT Jangwani jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam akiongoza dua hiyo Mussa Salum .

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Futari Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake wa Baraza la Waislam mkoa wa Dar es Salaam Bibi Pili Abdala Mwale wakati wa shughuli hiyo maalum ya kukabidhi furati na chakula kwa watu wenye mahitaji maalum, Jangwani jijini Dar es salaam.( Picna na OMR)

  Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake wa Baraza la Waislam mkoa wa Dar es Salaam Bibi Pili Abdala Mwaleakitoa neno la shukrani kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan mara baada ya shughuli ya kukabidhi futari na chakula kwa watu wenye mahitaji maalum kukamilika.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa ndani ya moja ya mabasi ya mradi wa mabasi ya mwendo kasi ya UDA-RT jijini Dar es salaam ambayo kwa kiasi kikubwa yamerahisisha usafiri na kutaka wananchi kuyatunza mabasi hayo.

  0 0

  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh, Mwigulu Nchemba(kulia), na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira(kushoto) wakimsikiliza Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhandisi Hamad Masauni, muda mfupi baada ya Rais Dkt. John Magufuli kumwapisha Waziri Mwigulu Nchemba kuongoza wizara hiyo leo. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mwigulu Nchemba(Kushoto), akikaribishwa Makao Makao ya Wizara hiyo na Katibu Mkuu Meja Jenerali Projest Rwegasira.Katikati ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhandisi Hamad Masauni na wa kwanza kulia ni Naibu Katibu Mkuu Balozi Yahya Simba. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, akisalimiana na Mkuu wa Kitengo cha Teknolojia ya Mawasiliano, Jane Massawe, mara baada ya kupokelewa Makao Makuu ya Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo.

  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, akiweka saini mara baada ya kuwasili Makao Makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi muda mfupi baada ya kuapishwa kwake. Katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira na kushoto ni Naibu Katibu Mkuu, Balozi Yahya Simba.(Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).

  0 0

  Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, Masha Mshomba, akitoa hotuba kwenye ufunguzi wa mafunzo ya siku tano kwa madaktari kutoka mikoa ya Nyanda za Juu Kusini, yanayofanyika mjini Mbeya Juni 13, 2016.Mafunzo hayo ni muendelezo wa kampeni ya WCF kwa kushirikiana na Shirika la Kazi Duniani, ILO, kuwapatia mafunzo Madaktari kote nchini, ili kujenga uwezowa kufanya tathmini ya madhara aliyoyapata mfanyakazimahala pa kazi kabla ya kupatiwa fidia. WCF itaanza kutoa Fidia kwa Wafanyakazi Kuanzia Julai 1, 2016.

  Baadhi ya madaktari waliohudhuria mafunzo hayo
   (PICHA ZOTE NA EMMANULE MADAFA).

  0 0

  Na Ismail Ngayonga-MAELEZO
  Dodoma

  SERIKALI katika mwaka 2016/17 imepanga kujenga nyumba 4139 za askari wa jeshi la Polisi nchini, hatua itakayosaidia kukabiliana na uchache wa nyumba za kuishi kwa askari hao.

  Awamu ya kwanza ya nyumba hizo zinatarajiwa kujengwa katika mikoa 17 nchini ikihusisha mikoa ya Tanzania Bara pamoja na mikoa ya Unguja na Pemba.

  Akijibu  swali la Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Faida Mohammed Bakar, Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, William Ole Nasha alisema Serikali itaendelea kuboresha makazi ya askari na ofisi za polisi kwa awamu kwa kadri hali ya kiuchumi itavyoimarika.

  Ole Nasha alisema Serikali inatambua changamoto zinazowakabili askari polisi katika maeneo mbaliombali nchini ikiwemo uchakavu wa ofisi, ambapo kwa kuanzia imeamua kuanza mpango wa kukarabati ofisi na makazi ya askari wake.

  Aidha alisema Serikali pia imekusudia kuhakikisha kuwa inatoa mikopo ya vyombo vya usafiri kwa askari wake ambao wanaishi mbali na vituo vyao vya kazi ili kuwasaidia kuwahi katika maeneo yao ya kazi kwa wakati.

  “Serikali inatambua changamoto inayowakabili askari wetu nchini ikiwemo wale wa Kusini Pemba, katika kukabiliana na hali hiyo tumepanga sasa kuifanyaia ukarabati miundombinu ya ofisi hiyo sambamba na ujenzi wa makazi bora kwa askari wetu” alisema Ole Nasha.

  Katika swali lake, mbunge huyo alitaka kufahamu mikakati ya Serikali ya kujenga nyumba za kuishi Na ofisi za kisasa katika kituo cha mkoani na kengeja Pemba.

  0 0

  Na Ismail Ngayonga-MAELEZO

  Dodoma


  SERIKALI katika mwaka 2016/17 imetenga kiasi cha Tsh. Milioni 430 kwa ajili ya upembuzi yakinifu na usanifu wa barabara ya Tarime-Nyamwaga- mugumu ambayo itajengwa kwa kiwango cha lami.

  Aidha Serikali pia imetenga kiasi cha Bilioni 1 kwa ajili ya ujenzi wa Daraja la Mara katika barabara ya Tarime-Nyamwaga-Mugumu.

  Akijibu swali la Mbunge wa Tarime Vijijini (CHADEMA), Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani alisema kwa kutambua umuhimu wa barabara hiyo hususani katika sekta ya utalii, Serikali imekusudia kuijenga barabara hiyo kwa awamu.

  Alisema barabara hiyo imeanza kujengwa kutoka Tarime kuelekea mugumu, ambapo hadi sasa jumla ya kilometa 6 za barabara hiyo zimekamilika kwa kiwango cha lami katika eneo la Tarime mjini.

  Aidha Mhandisi Ngonyani alisema ujenzi wa kilometa 2 unaendelea na unatarajiwa kukamilika kabla ya mwisho wa mwaka 2015/16.

  “Barabara ya Tarime-Nyamwaga- Mugumu (Serengeti) ni barabara ya mkoa yenye urefu wa kilometa 86 ni kiungo muhimu sana kiuchumi na kijamii kwa Wilaya za Tarime na Serengeti” alisema Ngonyani.

  Katika swali lake, Mbunge Heche alitaka kufahamu Serikali itaijenga lini barabara ya Tarime-Nyamwaga- Serengeti kwa kiwango cha lami.

  0 0

  Jonas Kamaleki-Maelezo
  Dodoma

  Serikali imeunda kikosi kazi kwa ajili ya kushughulikia uharibifu wa kimazingira ikiwemo kudhibiti uvuvi haramu wa kutumia mabomu ili kulinda mazalia ya samaki na kulinda ikolojia ya bahari.
  Kauli hiyo imetolewa leo Bungeni Dodoma na Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mhe. Wiliam Ole Nasha alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Chambani (CCM), Mhe. Yusuf Salim Hussein aliyetaka kujua hatua zinazochukuliwa na serikali kuzuia uvuvi haramu wa kutumia mabomu.
  Ole Nasha alitaja wajumbe wanoaunda kikosi kazi hicho kuwa ni Ofisi ya Rais, Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka, Wizara za Mambo ya Ndani ya Nchi, Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Wizara ya Nishati na Madini.

  Alizitaja Ofisi nyingine kuwa ni Wizara ya Maliasili na Utalii, Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC), ambapo kikazi kazi hicho kitaratibiwa na Ofisi ya Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini.
  “Kuna uhusiano mkubwa kati ya ugaidi na uvuvi wa kutumia vilipuzi, hivyo suala hili ni la kiusalama zaidi na kwa kutambua hilo Serikali imeanzisha vituo 5 vya kudhibiti uvuvi huo na baadhi ya vituo hivyo viko Pemba na Tanga,” alisema Ole Nasha.
  Ole Nasha alisema inaendelea kuziagiza Halmashauri za Ukanda wa Pwani ya Bahari ya Hindi kushirikiana na jamii kusimamia kwa ukamilifu udhibiti wa uvuvi haramu wa kutumia mabomu kuwachukulia hatua kali za kisheria wale wanaojihusisha na uvuvi huo.
  “Sheria ya Uvuvi ya Na. 22 ya Mwaka 2003 na Kanuni zake za Mwaka 2009 zimekasimu Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi wa Raslimali za Uvuvi katika Halmashauri zote nchini,”Alisema Ole Nasha.Alisema kuwa Wizara ina jukumu la kuanda Sera, Sheria, Kanuni zinazotumika katika Uhifadhi, Udhibiti na Usimamizi wa waza Uvuvi nchini.
  Ole Nasha aliongeza kuwa ili kuongeza nguvu ya kudhibiti uvuvi haramu, Serikali ilianzisha mfumo wa kushirikisha jamii kupitia vikundi vya usimamizi shirikishi wa Raslimali za Uvuvi (BMUs) ili kuwaelimisha wananchi juu ya athari ya matumizi ya mabomu na uvuvi haramu.
  Alisema matumizi ya mabomu katika uvuvi yana athari kubwa kwa samaki na mazingira ya baharini kwa kuwa huua samaki na viumbe wengine na uharibu matumbawe ambayo ni mazalia ya samaki.

  Ole Nasha alibainisha athari nyingine kuwa ni kupungua kwa rasilimali za uvuvi, kupoteza kipato, kuongezeka kwa mmomonyoko wa fukwe za bahari, pammoja na kuathiri afya za walaji.

  0 0

  Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO

  Manispaa ya Ilala kwa kushirikiana na Shirika la Misaada la Korea (KOICA) inatarajia kutumia kiasi cha shilingi bilioni 18 kukamilisha Ujenzi wa Hospitali ya kisasa ya kutolea huduma za matibabu kwa mama na mtoto katika Kata ya Chanika,wilayani Ilala.

  Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Afisa Habari wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, David Langa wakati akitoa ufafanuzi kuhusu maboresho yanayofanywa katika Sekta ya Afya ndani ya Manispaa hiyo.

  Amesema hospitali hiyo itakamilika mwishoni mwa mwaka huu na kuongeza kuwa itakuwa na vitanda 266 pamoja na mashine zote za upasuaji na matatibu ya magonjwa yote ya wanawake na watoto.

  “Ujenzi wa Hospitali hii kubwa ya wanawake na watoto unaendelea, tutatumia shilingi bilioni 18 kukamilisha kazi ya ujenzi na kuweka vifaa vya kisasa”,amesema Langa.

  Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Hospitali ya Amana, Dkt. Meshach Simwela amesema kuwa hospitali hiyo itakapokamilika itakuwa na vifaa vya kisasa pamoja na madaktari bingwa kutoka hospitali ya Taifa Muhimbili, Amana, Mnazi Mmoja pamoja na hospitali nyingine za Serikali.

  “Mpaka sasa jumla ya waganga watano na wauguzi sita wameshapelekwa Korea kujifunza namna ya kutoa huduma na jinsi ya kutumia vifaa vipya vitakavyoletwa mara baada ya Hospitali hii kukamilika”, alisema Simwela.

  Ameongeza kuwa ujenzi huo unategemewa kukamilika mwaka huu na unategemewa kufunguliwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli au Makamu wa Rais Mhe.Mama Samia Suluhu kwa kuwa ni Hospitali ya kwanza nchini Tanzania kuwa na hadhi kubwa kama hiyo.

  0 0

  Wabunge wa Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni wakitoka nje ya ukumbi wa Bunge mara baadya kumalizika kwa sala ya kuliombea Bunge leo asubuhi mjini Dodoma na wakiendelea na msimamo wao wa kutomtambua Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson. Mbunge wa Ukonga (CHADEMA) Mhe. Waitara Mwikwabe akiwa pamoja na Mbunge wa Same Mashariki (CHADEMA) Mhe. Naghenjwa Kaboyoka (katikati) na Mbunge wa Viti Maalum (CHADEMA) Mary wakitoka nje ya ukumbi wa Bunge hilo leo mjini Dodoma kuendeleas na msimamo wao wa wao wa kutomtambua Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson. Mbunge wa Igunga (CCM), Dkt. Dalali Kafumu akibadilishana mawazo na Wabunge wa Viti Maalum (CHADEMA), Mhe. Mariam Msabaha (kushoto) na Lucy Magereli (katikati) mara baada ya kumalizika kwa kikao cha Bunge hilo leo asubuhi mjini Dodoma. Mbunge wa Igunga (CCM), Dkt. Dalali Kafumu akibadilishana mawazo na Wabunge wa Viti Maalum (CHADEMA), Mhe. Mariam Msabaha (kushoto), Lucy Magereli na Mbunge wa Tarime Mjini (CHADEMA), Ester Matiku mara baada ya kumalizika kwa kikao cha asubuhi cha Bunge hiloi leo mjini Dodoma. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utumishina Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki akibadilishana mawazo na Mbunge wa Sengerema (CCM), Mhe. William Ngeleja na Mbunge wa Kibaha Vijijini (CCM), Mhe. Hamoud Jumaa (CCM) mara baada ya kumalizika kwa kikao cha asubuhi cha Bunge hilo linaloendelea mjini Dodoma. Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje, ushirikiano wa afrika mashariki na Kikanda, Mhe. Susan Kolimba, akisalimiana na Mbunge wa Muleba Kusini, Mhe. Anna Tibaijuka mara baada ya kumalizika kwa kikao cha asubuhi cha Bunge hilo leo mjini Dodoma. Wabunge wa CCM kutoka kushoto Sadifa Juma (Donge), Augustine Vuma (Kasulu Kusini) na Innocent Bilakwate (Kyerwa) wakibadilishana mawazo nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma mara baada ya kumalizika kwa kikao cha asubuhi cha Bunge hilo leo.(PICHA NA ISMAIL NGAYONGA).

  0 0  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
  Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha mchezaji wa zamani wa timu ya soka ya Mtibwa Sugar ya Morogoro inayoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, John Mabula(Mwenye jenzi ya njano)

  Mbali ya Mtibwa Sugar, taarifa za Mabula ambaye pia amewahi kuchezea Moro United ya Morogoro na Shinyanga Shooting ya Shinyanya kwa mafanikio nafasi ya ulinzi kwa muda mrefu katika timu hizo, aliuawa kwa kuchomwa kisu na mwenzake alipokuwa akiamulia ugomvi huko Kitunda - nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

  Rais Jamal Malinzi amemwelezea Mabula kuwa ni mchezaji aliyekuwa na uwezo na uadilifu na mchango wake katika soka utabaki katika dhana ya kumbukumbu ya wachezaji mahiri wa Tanzania waliotokea kucheza nafasi ya ulinzi japokuwa ametangulia mbele za haki.

  Rais Jamal Malinzi ametuma salamu za rambirambi kwa uongozi wa timu ambazo alicheza ambazo ni Mtibwa Sugar, Moro United na Shinyanga Shooting; kadhalika familia ya marehemu, ndugu, jamaa, marafiki walioguswa na msiba huo wa gwiji huyo aliyepata pia kucheza timu ya taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 20 ‘Ngorongoro Heroes’ ya mwaka 2002-2004.

  Rais Malinzi amewaasa wadau wote kuwa watulivu wakati huu mgumu wa msiba wa mpendwa wetu Mabula hasa kutokana na mazingira ya kifo. Bwana ametoa, Bwana Ametwaa, Jina la Bwana lihimidiwe. Amina.

older | 1 | .... | 878 | 879 | (Page 880) | 881 | 882 | .... | 1896 | newer