Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46205 articles
Browse latest View live

FLAVIANA MATATA ASHIRIKI MISA YA AJALI YA MV BUKOBA

0
0
 Flaviana Matata akiwa na Baba yake mzazi (suti nyeusi) katika Misa ya  maombelezo  Ajali ya MV Bukoba ambapo Flaviana alimpoteza Mama yake mzazi, Igoma,Mwanza leo
 Flaviana Matata akiwasha mshumaa ikiwa ni ishara ya kuomboleza katika Makaburi ya Igoma Mwanza walikozikwa baadhi wananchi walopoteza maisha yao miaka 17 iliyopita.

Flaviana Matata akiwa na marafiki na baadhi ya waombolezaji waliopoteza ndugu zao katika ajali hiyo. Picha na Shamim Mwasha
 Flaviana Matata akiwa ofisini kwa Bw. Projest Samson Kaija ambaye ni General Manager wa Marine Services Company ltd ambao hushirikiana nae kila mwaka katika maombolezo ya Ajali hii ambapo mwaka jana aliwapa msaada wa maboya ya kujiokoa.

Wakazi wa Tanga sasa kulipia maji kupitia Vodacom M-Pesa na Airtel Money

0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya maji safi Mkoa wa Tanga,(UWASA) Injinia Joshua Mgenyekwa(katikati)akimshuhudia Mkuu wa kitengo cha biashara cha M-pesa Vodacom Tanzania,Bw.Jackson Kiswaga kushoto akisaini mkataba kwa ajili ya kutoa huduma ya M-pesa kwa wakazi wa mkoa wa Tanga,ambapo watakuwa wakilipia Ankara za maji kwa mara ya kwanza  kupitia huduma hiyo na Airtel Money,kulia ni Meneja wa kanda ya kaskazini wa Airtel Bw.Stephen Kimea.
 Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya maji safi(UWASA) Mkoa wa Tanga,Injinia Joshua Mgenyekwa(katikati)akibadilishana nyaraka walizosainiana zinazohusu makubaliano ya kutoa huduma ya M-PESA na Mkuu wa kitengo cha biashara cha M-pesa Vodacom Tanzania,Bw.Jackson Kiswaga.Ambapo wakazi wa mkoa huo watakuwa wakilipia Ankara za maji kwa mara ya kwanza  kupitia huduma hiyo na Airtel Money,kulia ni Meneja wa kanda ya kaskazini wa Airtel Bw.Stephen Kimea.
Baadhi ya wafanyakazi wa taasisi ya maji safi Mkoa wa Tanga,(UWASA)wakiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania na Airtel,mara baada ya kusainiana mkataba wa kampuni hizo mbili kutoa huduma ya malipo ya Ankara za maji kupitia huduma ya M-PESA NA Airtel Money.



======

Zaidi ya wananchi 700,000 waishio katika manispaa ya Tanga sasa hawatahitaji tena kupanga foleni ili kulipia ankara za maji. Hii inafuatia ushirikiano baina ya Vodacom Tanzania na mamlaka ya maji safi na maji taka ya Tanga (UWASA) utakaowezesha malipo hayo kufanyika kupitia huduma ya M-Pesa na Airtel Money. 

(UWASA) ni mamlaka iliyoundwa kisheria chini ya sheria ya utoaji maji kifungu cha 272 ili kuendesha shughuli za upatikanaji wa maji safi na kusimamia maji taka mjini Tanga.(UWASA) ilianza kufanya kazi zake kama taasisi huru mwezi Januari, 1998.

 Huduma ya M-Pesa ina mawakala zaidi ya 40,000 nchi nzima, hivyo kuwezesha urahisi wa malipo ya huduma ya maji kama hii mahala popote pale nchini. Katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa UWASA,Injinia Joshua Mgenyekwa, alizungumzia jinsi ambavyo kwa kiwango kikubwa wakazi wa Tanga wataepuka usumbufu wa kutumia muda mrefu kwenye foleni za kulipia huduma ya maji na kusema: 

"Huduma hizi ni hatua ya kipekee hasa ikizingatiwa kuwa kuanzia sasa muda ambao mteja angeutumia kusubiri kwenye foleni, badala yake atauingiza katika shughuli nyingine za kila siku kama kazi au biashara. Pia kufanya malipo kupitia M-Pesa au Airtel Money kutarahisisha ufanyaji kazi wa mamlaka na kutoa nafasi ya kuongeza ubora wa huduma." 

Mkuu wa kitengo cha biashara cha M-pesa Vodacom Tanzania,Bw.Jackson Kiswaga alisema: "Nawahimiza wakazi wa Tanga watumie huduma ya M-Pesa kulipia ankara za maji kutokana na kuwa ni huduma ya haraka na salama. Hii ni njia ya uhakika ya kuokoa muda malighafi muhimu wa muda, na hivyo ni vyema sote kuitumia."

WAZAZI WA WANAFUNZI WASIORIPOTI KIDATO CHA KWANZA MAKETE KUKIONA CHA MOTO

0
0
Mkuu wa wilaya ya makete Mh. Josephine Matiro akisoma taarifa ya utekelezaji wa shughuli za serikali wilayani hapo kwa kipindi cha Januari-Aprili 2013 katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Makete leo Mei 20,2013
=======  ====== ====== =====
Wilaya ya Makete mkoani Njombe imejipanga kuhakikisha inawachukulia hatua za kisheria wazazi wa wanafunzi ambao hawajaripoti shuleni hasa wa kidato cha kwanza, kutokana na wazazi wengi kuwa ndiyo sababu inayopelekea wanafunzi hao kutofika shuleni

Hayo yamesemwa na mkuu wa wilaya ya Makete mh Josephine Matiro wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa shughuli za serikali kwa kipindi cha Januari-Aprili 2013 katika wilaya yake.

Matiro amesema amegundua wapo baadhi ya wazazi wa Makete ambao huwatorosha watoto wao na kwenda kuwapeleka kufanya kazi hasa za ndani nje ya wilaya yake ilihali watoto hao walifaulu kwenda kidato cha kwanza

“Wazazi mnatakiwa kufahamu urithi wa mtoto ni elimu na inasikitisha sana kama humpeleki mtoto wako shule ili akawe housegirl au houseboy mijini, naimani watoto hao lazima waje kuwalaumu nyie wazazi kwa kutompa elimu” alisema Matiro

Amesema kwa hivi sasa tayari wameanza kuushirikisha uongozi wa kata na vijiji kuwasaka wazazi na walezi wa watoto ambao hawajaripoti shuleni ili kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.

Jumla ya wanafunzi 2,173 waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza wilaya ya Makete mwaka huu 532 hawajajiunga na masomo hayo hadi sasa.

Taarifa hiyo ya mkuu wa wilaya iligusa Nyanja mbalimbali ikiwemo, Elimu, afya, maji, kilimo, barabara, maliasili na utalii.

Na Edwin Moshi), Makete

Kutoka iringa: Wanahabari washauriwa kupambana na vikwazo vinavyowanyima kupata habari na kukemea maovu.

0
0

Wandishi wa habari wameshauriwa kukemea vikwazo vinavyowanyima kupata haki yao ya habari pamoja na kukemea maovu wanayotendewa.


Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa IPC FRENK LEONARD wakati akizungumza na wandishi wa habari katika ofisi za ipc.


Amesema kuwa wakati mwingine wanahabri wanachangia wao wenyewe kujiwekea mazingira magumu katika utendaji wao wa kazi huku sababu ya kwanza akiitaja kuwa ni kuonesha itikadi zao za vyama.


Amesema kuwa mwandishi hazuiliwi kuwa na itikadi yoyote ya chama cha siasa lakini hapaswi kuonesha itikadi yake ya chama katika kazi kwani kwa  kufanya hivyo kutamjengea mazingira magumu ya kufanya kazi.


Aidha mwenyekiti huyo ameongeza kwa kusema kuwa mwandishi anapaswa kutembea na kitambulisho cha kazi wakati wowote ili kumrahisishia kazi yake na kumuepusha na matukio ya kinyama yanayojitokeza  sasa kwa wandishi.



Kutoka Iringa;sakata la machinga wa mashinetatu linajadilika-diwani jescar

0
0
Diwani wa Kata ya Miyomboni – Kitanzini Jescar Msambatavangu (CCM) amesema suala la wafanyabiashara ndogondogo (Machinga) wanaofanyia biashara zao Mashinetatu katika Manispaa ya Iringa linawezekana kukaa na kujadiliwa.

Akizungumza na wanahabari leo katika ofisi ya chama cha waandishi wa habari Mkoa wa Iringa (IPC)amesema bado kuna haja ya kukaa mezani kwa ajili ya kufanya majadiliano ili kulimaliza suala la machinga hao ili waweze kufanya biashara zao kwa utulivu.


Amesema licha ya  kuwa kuna haja ya kukaa mezani na wafanyabiashara hao bado kuna ugumu wa machinga kuendelea kufanyia biashara katika barabara hiyo ya mashine tatu  kutona na ongezeko la matumizi ya barabara hiyo.


Msambatavangu ambaye pia ni mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Iringa amesema kuendelea kuwaacha machinga barabarani siyo vyema kwa usalama wa maisha yao na watu mbalimbali.


Aidha ameongeza kwa kusema kuwa wananchi wanapaswa kutoa mtizamo wa kisiasa kuwa suala la mashinetatu linafanyika kisiasa. 

Rais kikwete kuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa barabara ya Iringa-Dodoma kesho.

0
0

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Jakaya Mrisho Kikwete ,kesho anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa bara bara ya Iringa- Dodoma kwa ajili ya kuweka jiwe la msingi.

Akizungumza mkuu wa mkoa wa Iringa,Mh  christin Inshengoma amesema kuwa Rais anatarajiwa kuwasili kesho majira ya saa tatu asubuhi katika kata ya migoli tarafa ya ismani.


ISHENGOMA amesema kuwa mbali na rais KIKWETE kuweka jiwe la msingi bado barabara hiyo inaendelea na ujenzi na inatarajiwa kukamilika mnamo mwaka 2015. Hata hivyo amesema kuwa barabara hiyo imegharimu zaidi ya shilingi billion 84.


Kwa upande mwingine mkuu wa mkoa huyo ametowa rai kwa wananchi kuwa watulivu  kufuatia vurugu zilizo tokea siku ya jumapili tarehe 19 ya mwezi huu katika manispaa ya iringa na kuongeza kuwa wananchi waache kuyumbishwa na vyama vya kisiasa ili kuhakikisha manispaa ya Iringa inakuwa salama. 

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKUTANA NA MWENYEKITI MSTAAFU WA KAMATI TENDAJI YA BUNGE LA CHINA NA UJUMBE WAKE

0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti Mstaafu wa Bunge la China, Lu Youngxiang (wa tatu kushoto) aliyeongozana na ujumbe wake baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Mei 21, 2013


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Makamu Mwenyekiti Mstaafu wa Bunge la China, Lu Youngxiang (wa pili kushoto) aliyeongozana na ujumbe wake wakati walipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Mei 21, 2013 kwa mazungumzo. Picha na OMR

ccm yaonya na kuwapiga marufuku makada wake kujipitisha pitisha kwa wapiga kura.

0
0


CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimewaonya na kuwapiga marufuku, makada na wanachama wake wenye nia ya kuwania nafasi mbalimbali katika uchaguzi mkuu ujao, kutothubutu kuanza kujipitipitisha kwa wapiga kura na kusema atakayefanya hivyo asimlaumu mtu kwa kitakachoamuliwa dhidi yake. Kimesema sheria kanuni na taratibu zinazokiongoza Chama katika kupata wagombea wake ziko palepale na kwamba hakitamvumilia yeyote atakayebainika kuzikiuka.

Onyo hilo lilitolewa jana Dar es Salaam na Katibu wa Halmashauri Kuu ya 
Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, wakati akiongea na waandishi wa habari kuhususu mkutano kati ya CCM na wabunge wake uliofanyika mwishoni mwa wiki mjini Dodoma.
"Viko vyombo vya habari ambavyo kwa makusudi vimepotosha ukweli kuhusu tulichoafikiana katika kikao kati ya CCM na wabunge wake. Si Mwenyekiti wa taifa wala Chama kilichoruhusu wenye nia ya kuwania nafasi mbalimbali kujipitishapitisha kwa wananchi.

"Nasisitiza nukuu hiyo ya baadhi ya vyombo vya habari si sahihi na ni ya kupotosha ukweli. Inaelekea kuna kikundi cha watu wenye mgombea wao wa kuchonga ambaye bila shaka anapungukiwa sifa, hivyo wanajaribu kumuongezea sifa kwa kumlisha Mwenyekiti maneno na kuwapa baadhi ya waandishi wa habari. Uhuni huo haukubaliki," alisema Nape. Kwa mujibu wa Nape, licha ya ajenda kuhusu wana-CCM wenye nia ya kuwania nafasi mbalimbali ikiwemo udiwani, ubunge na urais kujadiliwa kwa kina katika kikao hicho, hitimisho na majumuisho ya Mwenyekiti wa CCM .

Taifa ilikuwa ni kukemea kwa nguvu zote pirikapirika hizo ambazo ni uvunjifu wa makusudi wa kanuni za Chama.Alisema kimsingi pirikapirika zinazofanywa na baadhi ya makada zinaweza kukigawa Chama na kuvuruga mshikamano na umoja uliopo ndani ya CCM. Nape alisema CCM ina kanuni na taratibu zinazoisimamia na kuiongoza katika kufanya shughuli zake mbalimbali zikiwemo za mchakato wa kuwapata wagombea wake katika ngazi mbalimbali kuanzia shina hadi taifa. Kanuni hizo ni pamoja na za uteuzi wa wagombea wa Chama kuingia kwenye vyombo vya dola toleo la Februari, mwaka 2010 na kanuni za uchaguzi wa CCM, toleo la mwaka 2012.

“Ni mwiko kwa kiongozi au mwanachama yeyote wa CCM kuunda vikundi visivyo rasmi ndani ya chama, au kushiriki katika kampeni za uchaguzi za chini chini kinyume na ratiba ya uchaguzi na taratibu rasmi zilizowekwa” alisema.Katibu huyo alisema iwapo mwanachama yeyote atakiuka kwa makusudi na kuvunja taratibu hizo, Chama kitamwajibisha bila ya kumuonea haya na kwamba itakapofikia hapo asilaumiwe yeyote kwa kuwa ndivyo taratibu zinavyoagiza.

Akizungumzia malengo ya kikao hicho, alisema kililenga kutathimini utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM majimboni na kuangalia namna bora ya kuweka msukumo mpya na mkubwa zaidi kwa sehemu iliyobaki ya utekelezaji wake katika kipindi cha mwaka 2010/2015, ili kuhakikisha ahadi za Chama na wagombea wake zinatekelezwa kwa kiwango kikubwa.

Baadhi ya magazeti (Uhuru halimo) katika matoleo yao ya juzi, yalimnukuu Mwenyekiti wa Taifa wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, akiwaruhusu wanaotaka kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao mwaka 2015 kuendelea na mchakato. Magazeti hayo yalidai kuwa Rais aliruhusu hilo kutendeka huku  akiwatahadharisha watakaokuwa tayari kufanya hivyo kuendesha kampeni zao kwa ustaarabu bila kuibua chuki na kujenga makundi kwa kuwa ni hatari kwa uhai wa Chama.

Serikali kuanzisha sera na Sheria ya usalama wa bidhaa nchini - Katibu.

0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko, Bi. Joyce Mapunjo, akifungua warsha ya kujadili mpango wa ukaguzi wa bidhaa kabla ya kuingizwa nchini (PVoC) uliofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Bureau Veritas, Bw. Jean-Michel Marnoto (katikati), akifuatilia hotuba ya ufunguzi wa Warsha ya kujadili mpango wa ukaguzi wa bidhaa kabla ya kuingizwa nchini (PVoC) uliofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Mratibu wa Bureau Veritas, Bw. Michael Maryogo na wa tatu ni Meneja wa Bureau Veritas Tanzania, Bw. Cedric Serre.
Baadhi ya wadau wakifanya usajili kabla ya kuingia kwenye warsha ya kujadili mpango wa ukaguzi wa bidhaa kabla ya kuingizwa nchini (PVoC) uliofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Mkutano huo ulifunguliwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko, Bi. Joyce Mapunjo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko, Bi. Joyce Mapunjo, akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufungua warsha ya siku moja iliyojadili mpango wa usalama na ubora wa bidhaa nchini (PVoC) pamoja nae ni Meneja wa Bureau Veritas Tanzania, Bw. Cedric Serre.
Wadau mbalimbali wakifuatilia kwa umakini hotuba ya ufunguzi wa Warsha ya kujadili Mpango wa Ukaguzi wa Bidhaa kabla ya kuingizwa nchini (PVoC) uliofanyika kwenye Hotel ya Serena jijini Dar es Salaam.



=======   =========  ==========

Serikali kuanzisha sera na Sheria ya usalama wa bidhaa nchini - Katibu.
Dar es Salaam, MEI 21, 2013 … Wakala wa Kimataifa wa ukaguzi wa ubora na viwango vya bidhaa, Bureau Veritas (BV), kwa kushirikiana na Shirika la Viwango Tanzania (TBS),  wametoa tahadhali kwa wafanyabiashara na wazalishaji wa bidhaa nchini kuzingatia uzalishaji na biashara zenye tija na viwango vya ubora kulingana na muktadha wa soko la leo kimataifa, vinginevyo watashindwa kushindana.
Akizungumza kwenye warsha iliyojumuisha wafanyabiashara na wazalishaji wa bidhaa mbalimbali katika hoteli ya Serena, Dar es Salaam,  Makamu wa Rais wa Bureau Veritas, Jean-Michel Marnoto, alisema taifa lolote linalozalisha bidhaa kwa kuzingatia ubora ni dhahiri hujisafishia njia ya kufikia maendeleo kwa nyanja zote, hususan kiuchumi na kijamii.
“Ndio sababu tumekutana hapa ili kuelimishana na kubadilishana mawazo ya namna ya kukidhi viwango na ubora kulingana na mahitaji ya soko. Na kikubwa kinachotupa matumaini ni jinsi serikali ya Tanzania ilivyojitoa na kuonesha dhamira ya dhati katika kuhakikisha siku hadi siku inaweka mazingira bora katika sekta ya viwanda na uzalishaji kwa maendeleo endelevu ya taifa na watu wake,” alisema Marnoto
Marnoto aliongeza kuwa BV kama wakala anayetambulika Kimataifa katika ukaguzi wa bidhaa sanjari na kuthibitisha na kisha kutoa cheti cha ubora kwa bidhaa husika, kwa kipindi kirefu imejijengea mwonekano mzuri na kukubalika kimataifa, huku ikiamini hiyo ni fahari, heshima na jambo la kujivunia  na la thamani katika taswira ya dunia.

“Tunachukua fursa hii kuungana na wateja wetu na watanzania kwa ujumla katika kubadilishana mazuri tuliyonayo kwa ustawi na maendeleo, jambo la kuungana ndio hasa azma yetu kufikia dira ya kule tunakokwenda,” alisemaMarnoto

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko, Joyce Mapunjo, alisema kwa miaka mingi sasa nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania, zimekuwa zikifanya jitihada kuhakikisha zinakidhi vigezo vya uzalishaji wa bidhaa zake kulingana na mahitaji ya soko, jitihada ambazo hata hivyo zimekuwa zikikwamishwa na changamoto kadhaa zikiwemo rushwa na mifumo thabiti ya usimamizi.
Aliongeza kwa kuwahakikishia wadau wa sekta hiyo kuwa serikali kwa kushirikiana na jumuiya za kimataifa na taasisi zisizo za kiserikali (NGOs) imeazimia kuboresha mazingira ya kiufanisi katika kufikia malengo, viwango na vigezo vya ubora kulingana na uhalisia sambamba na mahitaji ya soko kwa bidhaa husika.
Bureau Veritas ilianzishwa mwaka 1828, lengo likiwa ni kushirikiana na taasisi za serikali ya nchi husika zinazotoa huduma ya ukaguzi wa viwango na ubora wa bidhaa na kuthibitisha ubora wake, na kisha kutoa cheti cha ubora kwa kampuni au taasisi husika iliyokidhi viwango na ubora, kinachojulikana kama ‘Certificate of Conformity CoS’

MWISHO…
Mhina Shabani
0764 615 481

NEW ARRIVAL @AK CLASSIC COSMETICS!!

0
0
 WALE MABINGWA WA COSMETICS ZA UKWEE KUTOKA MAREKANI, AK CLASSIC COSMETICS SASA WAMEWASHUSHIA MZIGO WA VITU VYA UHAKIKA KABISA KAMA KAWAIDA YAO  KUANZIA PRODUCTs ZA KUPUNGUA,PRODUCT ZA NYWELE,TIBA ZA CHUNUSI,PRODUCTs ZA KUNG'ARISHA NGOZI YAKO,DAWA ZA KUONDOA STRETCH MARKS,PERFUMES ZA MADESIGNER'S!! NA BIDHAA ZINGINE ZA KILA AINA!!KWA HAKIKA WATU WALIOTUMIA BIDHAA ZAO WAMEJIONEA UTOFAUTI,BADO WEWE!!

 KWA MAELEZO NA PICHA ZAIDI WATEMBELEE www.akclassic.blogspot.com
 KUWEKA ODA NA KUFIKISHIWA BIDHAA MPAKA ULIPO PIGA  0753-482909/0713-468393.


Malalamiko ya Watani zetu wa Jadi dhidi ya Obama na Tanzania

0
0
Leo hii tumepata bahati ya kusikiliza malalamiko ya watani zetu wa jadi, yaani ninamaana watani zetu ! jirani zetu Kenya,si unajua nao wanatulalamikia kuwa tunapendelewa sana ...lakini sikiliza mwenyewe mamaliko yao ! kwa nini? Tanzania wanamega tonge kubwa

msafara wa mamba kenge hawakosi:FANI YA UANDISHI WA HABARI IMEVAMIWA, TUSIPOZIBA UFA TUTAJENGA UKUTA.

0
0

Pichani ni waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa katika maandamano ya amani (Picha na Maktaba).
 ---
Watu wengi kwa sasa wameibuka na kutokea kuipenda fani ya uandishi wa habari bila kujua misingi na miiko ya uandishi wa habari. Tatizo moja ambalo limeonekana ni kubwa sana ni utandawazi ambao umekuwepo na kutokea ibuko la kila kijana kufungua gazeti tando (blog).

Hatukatai kuja kwa magazeti tando ila naomba tujiulize, yanatumika ipasavyo ama ndiyo limekuwa ni wimbi vamizi lenye kutoa ama kusambaza habari hata zile zisizokuwa na vyanzo kamili na visivyojitosheleza.Kwa sasa imezuka tabia ya wanaojiita wamiliki wa magazeti tando,wengi wao kukopi na kupaste vitu wanavyoviokota katika mitandao ya kijamii ikiwemo Twitter, facebook na mingine mingi.

Sina nia ya kumsema mtu bali napenda tuelimishane kama vijana wenzangu,ambao wametokea kuipenda fani ya uandishi wa habari, wakumbuke kuwa fani ya uandishi wa habari ina miiko na maadili yake, mfano. Katika kuandika habari za mazingira, siasa, elimu, uchumi, michezo, burudani ukiangalia habari hizi zote zina misingi na miiko yake. Leo hauwezi kumchukua mwandishi wa habari za michezo ukamwambia aandike habari za uchumi kwa vile hatakuwa na takwimu za uchumi na hata akiandika hiyo habari na kuisoma utakuwa unajiuliza maswali mengi bila kupata majibu.

Vile vile ni vizuri vijana wenzangu kutambua kuwa kila kazi ina mipaka na misingi yake, juzi juzi nilisoma habari katika gazeti tando moja wapo ikisema, 'ALIYEONGOZA MAANDAMANO YA IRINGA MHESHIMIWA MCHUNGAJI MSIGWA ASWEKWA NDANI' nilijiuliza maswali mengi ambayo kiukweli nilikosa majibu yake, kuona huyu aliyeandika hiki kichwa cha habari kweli amepitia fani ya uandishi wa habari ama ndio ule upepo vamizi?

Maana unapoandika habari za mahakamani, polisi kuna misemo yake, hauwezi kumuhukumu mtu moja kwa moja kwa kusema fulani ni mwizi, hata hao polisi ambao huwa wanakwenda kukamata watu eneo la tukio hawawezi kusema fulani ni mwizi mpaka apelekwe mahakamani ndipo sheria ichukue mkondo wake na kumbaini huyo aliyekamatwa ni mwizi.

Naomba tufike mahali tuheshimu utu wa watu na kuepuka udhalilishaji wa bila kujua naamini baadhi ya vijana wengi walioamua kufungua magazeti hayo tando ambayo yanatoa habari, hawana taaluma ya uandishi wa habari.

Napenda kuwapongeza wale walioamua kufungua magazeti tando katika milengo yao tofauti ikiwemo kutoa habari kwa njia ya 'kufundisha masuala ya urembo, mapishi, kuwasaidia kuwatangaza vijana katika muziki na hata wale walioamua kuandika habari zao binafsi.

Nayasema yote hayo kwa vile kumezuka wimbi la vijana wanaotaka kuichafua fani ya uandishi wa habari na ionekane si fani ya watu walioenda shule bali ni ya wahuni tu wasiojua mambo, naomba vijana tuelimike na tujifunze kwa watu wanayoyajua mambo ili tuweze kufika mbele zaidi.
Namalizia kwa kusema tusipoziba ufa tutajenga ukuta.

Asanteni sana kwa kusoma.
Imeandikwa na Cathbert A. Kajuna

HUDUMA ZA NIC BANK ZAZIDI KUPAA KANDA YA ZIWA SASA ZAIMARIKA AFRIKA MASHARIKI

0
0
Mkurugenzi wa NIC Bank James Muchiri akiitambulisha safu wa watendaji wa benki hiyo kwa makao yake makuu hapa nchini yaliyopo jijini dar  kwa wafanyabiashara, wawekezaji na wateja wa NIC mkoa wa Mwanza, katika hafla ya chakula cha jioni ilifanyika katika ukumbi wa Nyerere Gold Crest Hotel jijini humo. 

NIC Bank imekuja na program mpya ya T24, mfumo mpya wa kisasa wa kikopyuta unaorahisisha uendeshaji wa shughuli za kibenki ambao unawasaidia wateja wao kuwahudumia kwa haraka na kwa muda muafaka.  
Meneja wa Tawi la Mwanza Richard Dotunatus akiitambulisha safu ya wafanyakazi wa NIC Bank tawi la Mwanza na vitengo vyao husika.


Kwa mpango huu NIC Bank ndani ya soko la Jumuiya ya Afrika Mashariki inatoa tafsiri ya kujizatiti na kujiimarisha kiutendaji kwa kutoa huduma kwa eneo lote bila usumbufu hivyo kuwa tegemeo linapokuja suala la huduma za kibenki. 




Wateja wa benki ya NIC wakiwa ndani ya ukumbi wa Nyerere Gold Crest Hotel kwaajili ya kupata chakula cha jioni kilichoandaliwa na benki hiyo.






Wateja ambao ni wafanyabiashara wa jijini Mwanza wakijadiliana ndani ya Hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na benki ya NIC.


Wadau wa biashara wamekutana kwenye Hafla hii kwa mazungumzo mafupi na kubadilishana uzoefu.


Wadau wa NIC Benk. 


Moja kati ya faida ya huduma mpya ya T24 ni kuwa, kupitia mtandao (On line banking) mteja anaweza kukaa nyumbani au kuwa mahali popote pale akapata huduma za kibenki kupitia SMS banking. 


Ushauri wa sisi kwa sisi wateja wa NIC.


Ni moja kati ya meza waliyokaa wafanyabiashara maarufu jijini Mwanza.


"Temenos T24 is comprehesive business functionality with an advanced, secure, scalable technology and market challenges of today and tomorrow" Said 'Mc Stopper' 


Wadau wakijipatia chakula kizuri kilichoandaliwa na NIC Bank kwenye hafla na wateja wake jijini Mwanza.


Samaki au kuku?


Chakula time.


Starter ...


Futher to embracing technology advancement, within the last 12 months the bank has opened two additional branches. Its 5th branc in Kahama town Shinyanga Region and a 6th branch in Kariakoo along Sikukuu Street in Dar es salaam.

Airtel yazindua ofa kabambe kupiga simu kwenda nje ya nchi

0
0

 Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya Airtel Tanzania, Beatrice Singano (kushoto) na Meneja Biashara za Kimataifa wa Kampuni hiyo, Prisca Tembo (wa pili kutoka kulia) wakizindua huduma mpya ya kupiga simu kwenda India kwa gharama nafuu. Wengine ni Balozi wa India hapa nchini, Debnath Shaw (katikati) na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo, Sunil Colaso.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Airtel Tanzania, Sunil Colaso (wa pili kutoka kulia), akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya kupiga simu kwenda India kwa gharama nafuu. Wengine ni Meneja Biashara za Kimataifa wa Kampuni hiyo, Prisca Tembo (kulia), Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni hiyo, Beatrice Singano na Balozi wa India hapa nchini, Debnath Shaw.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya Airtel Tanzania, Beatrice Singano (kushoto) akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya kupiga simu kwenda India kwa gharama nafuu. Wengine wanaofuatia ni Balozi wa India hapa nchini, Debnath Shaw, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo, Sunil Colaso na Meneja Biashara za Kimataifa wa Kampuni hiyo, Prisca Tembo.


=======  ======= ========
Airtel yazindua ofa kabambe kupiga simu kwenda nje ya nchi


•       Wateja kupata kifurushi cha dakika 25 kupiga simu kwenda India
•       Ofa hii inapatikana masaa 24 siku 7 za wiki,



Kampuni ya Bharti (“Airtel”) inayoongeza kwa kutoa huduma za
mawasiliano inayoendesha shughuli zake katika nchi 20 barani Afrika na
Asia leo imetangaza uzinduzi wa ofa itakayowawezesha wateja wa Airtel
Tanzania kupiga simu kwenda nje kwa gharam nafuu zaidi.



Ofa hii inaendelea kuonyesha dhamira ya Airtel Tanzania ya kuendelea
kuwanganisha watanzania katika mtandao wa mawasiliano na kuwapa huduma 
bora zenye gharama nafuu. Uzinduzi huu unafatia utambulsho wa huduma 
kabambe ya Airtel yatosha  iliyofanyika week chache zilizopita.



Akiongea wakati wa uzinduzi wa huduma hii mpya, Mkurugenzi mkuu wa
Airtel Bwn. Sunil Colaso alisema ”baada ya uzinduzi wa mafanikio ya
huduma yetu ya Airtel yatosha. leo tunazindua ofa ya mawasiliano ya
gharama nafuu  na kuwawezesha wateja wetu kuwasiliana na familia
,marafiki na washirika wa kibiashara walioko nje ya mipaka ya nchi.

Kwa kiasi cha chini cha hadi shilingi3, 000 sasa wateja wa Airtel
wanaweza kupiga simu India masaa 24 kwa siku 7 za wiki. Ofa hii
itampatia mteja dakika 25 za muda wamaongezi kwa muda wa wiki nzima.



Aliongeza “Hii ni ya kwanza kutoka Airtel, na tunaendelea
kuwahakikishia wateja wetu nchi nzima huduma bora, za uhakika na
gharama nafuu za mawasiliano wakati wote. Tumesikiliza kile wateja
wetu wanachokitaka na kutengeneza ofa inayokidhi mahitaji yao hivyo
tutaendelea kutekeleza dhamira kwa watanzania ya kuleta huduma zenye
ubunifu, bora na gharama nafuu ambazo kwa uhakika zitaleta uhuru wa
kuongea nje ya mipaka. 

Ofa hii itawawezesha wateja wanaosafiri au
kuwasiliana na India iwe kimasomo, kibiashara , wanaotembelea India
kimatibabu kuwa na mawasiliano na familia zao kwa gharama za
kiushindani zilizo nafuu zaidi. Uzinduzi huu ni mwanzo wa kuleta
mapinduzi ya mawasiliano katika soko la Tanzania.



Kwa upande wake Balozi wa India nchini Tanzania, H.E. Mr.Debnath Shaw
alisema” Tunawapongeza Airtel kwa kuzindua ofa hii itakayoendelea
kutuunganisha na kuendeleza ushirikiano wetu kati ya India na
Tanzania. nchi hizi mbili zimekuwa na ushirikiano wa karibu si
kibiashara tu bali katika sekta ya elimu, Afya na shughuli nyingine za
kijamii. 

Ninayofuraha kuona Airtel ikiwa mstari wa mbele kuleta
gharama nafuu katika soko la Tanzania. Nchini India Airtel ni mtandao
unaoongoza uliowekeza katika technologia ya hali ya juu, mtandao bora
na unaotoa huduma bora za gharama nafuu kwa wateja wake. Ninayofuraha
kuona huduma za mawasiliano zinabadilika kwa kasi na kufanana kama za
India katika soko la Airtel barani Afrika.”



“Tunaamini hii ni fulsa pekee kwa wafanyabiashara , wanafunzi waliko
India na wengine wanaotembelea India kwa sababu mbalimbali kuwasiliana
na familia, marafiki na washirika wa kibishara waliko Tanzania kwa
gharama nafuu



Akifafanua kuhusu ofa hii Meneja wa biashara za kimataifa wa Airtel bi
Prisca Tembo alisema” ofa hii inapatikana katika kifurushi cha muda wa
maongezi ambapo kwa bei moja ya shilingi 3000 mteja atapata dakika 25
atakazozitumia masaa 24 kwa siku 7. Kifurushi hiki kitatozwa kwa
sekunde na kudumu kwa muda wa wiki nzima. Sambamba na hilo, Simu
zitakazopigwa kwenda nchi nyingine nje ya ofa hii zitatozwa kwa bei ya
kawaida”



“Ili kujiunga na ofa hii mteja anatakiwa kupiga*149*13# na kuweza
kufurahia ofa hii. Na huduma hii ni kwa wateja wa malipo ya awali nchi
nzima” aliongeza Tembo



Hivi karibuni Airtel ilizindua huduma ya Airtel yatosha inayotoa ofa
ya vifurushi vya muda wa mongezi, ujumbe mfupi na internet
zinavyomuwezesha mteja kuwasiliana na mtandao wowote nchini. Ikiwa
katika mwendelezo wake wa kuboresha huduma zake Airtel imezindua ofa
mpya ya kupiga simu kwenda nje ya nchi inayompatia mteja kifurushi cha
muda wa maongezi kupiga simu kwenda India. Ili kupata huduma hii piga
*149*13# na unganishwe sasa.

DK. ASHA-ROSE AZUNGUMZA NA WANAHABARI LEO DODOMA

0
0
 Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro akizungunza na waandishi wa habari, leo katika ukumbi wa Sekretarieti, Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma. Amezungumzia masuala mbalimbali yaliyojiri kwenye kikao cha Kamati Kuu ya CCM kilichomalizika jana. (Picha na Bashir Nkoromo).

Makamu wa Rais wa TBF Magesa akutana na Kocha Mkuu wa Kikapu Albert Sokaitis

0
0
Makamu wa Rais wa TBF Ndg. Phares Magesa akiwa na Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania Albert Sokaitis mara baada ya mazungumzo ya kupanga mikakati ya kuendeleza Michezo wa Kakapu Tanzania, VIJANA wengi watafaidika na Mpango huu wa mafunzo yatakayolenga kunyanyua kiwango Cha Michezo nchini kupitia Kocha huyu. Kutokana Na mpango huu baadhi ya vijana wetu watapata nafasi za kwenda kusoma na kucheza kikapu katika vyuo via Marekani, Vijana wetu muwe tayari... Chamsingi Ni kuwa Na Uwezo Mzuri wa Michezo na pia kuzingatia masomo (shule).

HAYAWIHAYAWI, SASA YAMEKUWA! USIKU WA HIP HOP, THE VODACOM MIC KING KURINDIMA J’MOSI HII DAR LIVE

0
0
Wakali tisa wa Hip Hop wanaowania gari aina ya Toyota FunCargo (new model), katika pozi mbele ya gari lao.

ILIPANGWA, ikapangika. Baada ya kusubiririwa kwa muda mrefu, hatimaye msimu mpya wa shoo ya Usiku wa Hip Hop (2013) unachukuwa nafasi Jumamosi hii ndani ya Ukumbi wa Dar live, Mbagala-Zakhem, jijini Dar.

Wasanii wanaotamba kwenye gemu la Hip Hop, Kala Jeremiah, Fid Q, Nay wa Mitego, Joh Makini, Stamina na wengine kibao pamoja na washiriki wa Shindano la The Vodacom Mic King watakamua shoo baab’kubwa kuweka historia mpya ya burudani.


Meneja Matukio wa Ukumbi wa Dar Live, Abdallah Mrisho ‘Abby Cool’ amewahakikishia mashabiki wote wa muziki wa Hip Hop kuwa Jumamosi kutasheheni matukio kibao, ulinzi mzito utakuwepo pamoja na parking kubwa ya magari hivyo watu wafike kwa wingi watainjoi kwa nafasi na kuondoka salama ukumbini.


“Vijana tisa waliosalia katika Shindano la The Vodacom Mic King watapanda jukwaani na kushusha mistari ambapo mshiriki mmoja anatarajiwa kuondoka na gari jipya aina ya Toyota FunCargo (new model),” alisema Abby Cool na kuongeza: “Mashabiki wanaweza kulifuatilia shindano hilo kupitia Runinga ya DTV kuweza kujua jinsi ya kuwapigia kura.”


Washiriki hao na namba zao za ushiriki kwenye mabano ni Ally (MK 02), Anold (MK 03), Bahati (MK 05), Boniface (MK 07), Emmanuel (MK 10), Ibrahim (MK 12), Karrys (MK 13), Lusajo (MK 14) na Martin (MK15). Jinsi ya kuwapigia kura, wasomaji wanatakiwa kuandika neno MK wakiambatanisha na namba ya mshiriki kisha kutuma ujumbe huo kwenda namba 15564.



OFA ZAIDI KWA MSHINDI

Mbali na mshindi kuondoka na gari, Mrisho aliongeza kuwa washindi watatu wa nafasi za juu watajipatia dili la kurekodi singo mojamoja kutoka kwa prodyuza kiwango aliyezalisha ngoma kali Bongo ikiwemo ya Kundi la Kigoma All Stars iitwayo Leka Dutigite, Tudd Thomas.


TUZO KUTOLEWA

Mrisho alitiririka na mistari kuwa, mbali na shoo kali kutoka kwa wakali hao wa Hip Hop, kutakuwa na kipengele cha kutoa tuzo za muziki wa Hip Hop katika vipengele tofauti hivyo mashabiki pia waendelee kuwapigia kura wasanii wanaowapenda.



Vipengele vitakavyotolewa tuzo ni Mwanamuziki Bora wa Hip Hop (Legendary) ambapo yamepita majina matatu; Fid Q, Joh Makini na Profesa Jay. Pia kipengele cha Mwanamuziki Bora wa Hip Hop (Chipukizi) ambacho kina majina kama Young Killer, P The Mc na Tabla huku akianisha kipengele cha mwisho ambacho ni Wimbo Bora wa Hip Hop (2012/13) chenye nyimbo kali za Dear God (Kala Jeremiah), Sihitaji Marafiki (Fid Q) na Najuta Kubalehe (Stamina).

“Ili kuwapigia kura, mashabiki wanatakiwa kuandika neno BHL wakiambatanisha na jina la msanii husika kwenda namba 15564 katika kipengele cha Msanii Bora wa Hip Hop (Legendary).
“Kipengele cha Mwanamuziki Bora wa Hip Hop (Chipukizi), mashabiki waandike neno BUA na kufuatiwa na jina la msanii wanayempenda kwenda namba 15564,” alisema Abby Cool na kuongeza:
“Kipengele cha Wimbo Bora wa Mwaka, mashabiki waandike neno BHS likifuatiwa na jina la msanii wanayempenda kisha watume ujumbe huo kwenda namba 15564.”


KUWAENZI WASANII/SOKA KWENYE SKRINI KUBWA

Abby Cool aliweka bayana kuwa katika shoo hiyo kutakuwepo na documentary maalumu ya kuwakumbuka wasanii wa Hip Hop waliotangulia mbele za haki kupitia skrini kubwa bila kusahau mashabiki wa soka watapata fursa ya kushuhudia fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya (Uefa) kati ya Bayern Munich na Borrusia Dortmund. Twendeni Dar Live J’mosi!

kamati ya kitaifa ya kitaalam ya mabadiliko ya tabia nchi

0
0


Picha ya pamoja ya  washiriki wa mkutano wa kamati ya kitaifa ya kitaalam ya mabadikio ya tabia nchi.



 ==========  ======= =========

Serikali ya jamuhuri ya muungano wa tanzania imechukua hatua mbali mbali katika kukabiliana na adhari za mabadiliko ya tabia nchi ilikwa ni pamoja na kuandaa mwongozo wa kitaifa wa kuhimili mabadiliko ya tabia nchi mkakati wa kitaifa wa kuhimili mabadiliko ya tabia nchi na makakati wa mawasiliano wa mabadiliko ya tabaia nchi. Hayo yameelezwa leo na naibu katibu mkuu kutoka ofisi ya makamu wa rais injinia ngosi mwihava wakati wa ufunguzi wa wa mkutano wa kamati ya kitaifa ya kitaalam ya mabadiliko ya tabia nchi inayokutana mjini zanzibar kwa siku mbili.

injinia mwihava ameeleza washiriki kuwa katika sekta zote husika kuna umuhimu wa kulijadili suala la mbadiliko ya tabia nchi kutokana na kuwa athari zinaonekana wazi nchini ikiwa ni pamoja na hali ya ukame, kuongezeka kwa kina cha bahari, kupungua kwa barafu katika mlima kilimanjaro, kupungua kwa maji kunakopelekea upungufu wa umeme, kuongezeka kwa mazalia ya mbu katika maeneo ambayo awali haikuwa kawaida, mafuriko, ongezeko la gesi joto utokanao na shuguli za kibinadamu kama vile ukataji wa miti na  kuongezeka kwa taka kunakosababisha kuongezeka kwa gesi joto aina ya methane na kuleta mabadiliko ya hali ya anga.


‘kuna umuhimu katika utendaji wetu kujadili suala la mabadiliko ya tabia nchi ili kufikia malengo. alisisitiza.’ na kuongeza kuwa kuwe na mipango inayoangalia kuwa kuna uharibifu wa mazingira na njia za kuweza kukabiliana na athari zitokanazo na mabadiliko ya tabuia nchi. awali, kwa upande wake katibu wa kamati hiyo.

Bwana richard muyungi  ameeleza kuwa lengo hasa la kamati kukutana zanzibar ni kupitia na kuratibu shughuli mbali mbali za mkataba wa mabadiliko ya tabia nchi, kutembelea miradi mbali mbali ya mabadiliko ya tabia nchi, na redd ambayo inafadhiliwa na serikali ya japan kupitia shirika la maendeleo la umoja wa mataifa undp.

mkutano huo wa kamati ya kitaifa ya kitaalam ya mabadiliko ya tabia nchi unahusha washiriki kutoka sekata mbali mbali zikiwemo nemc,tma,wizara ya maliasili na utalii, kilimo , maji, nishati na madini, mifugo, habari ofisi ya makamo wa kwanza wa rais zanzibar ,ofisi ya makamu wa rais nataasisi ya rasilimali asili ya udsm.


evelyn mkokoi

afisa habari ofisi ya makamo wa rais

22/5/2013

zanzibar. 

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA MAONYESHO YA NANE YA KAMISHENI YA VYUO VIKUU MBALIMBALI JIJINI DAR

0
0



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa maonyesho hayo.

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake ya ufunguzi wa Maonyesho ya Nane ya Vyuo Vikuu kutoka nchi mbalimbali, yatakayofanyika kwa siku tatu katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam. Maonyesho hayo yamefunguliwa leo. Picha zote na Muhidin Sufiani-OMR
Baadhi ya washiriki  wa maonyesho ya Nane ya Vyuo Vikuu kutoka nchi mbalimbali, wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati akisoma hotuba yake ya kufungua rasmi maonyesho hayo ya siku tatu katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Maofisa wa mfuko wa PPF, kutoka (kushoto) ni Meneja wa Kanda ya Ilala, Evans Musiba, Meneja Uhusiano, Lulu Mengele na Ofisa Masoko, Sereki Michael, wakati alipotembelea katika banda la maonyesho la PPF, leo kwenye maonyesho ya Nane ya Vyuo Vikuu kutoka nchi mbalimbali yanayofanyika kwa siku tatu katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mhitimu wa Chuo Kikuu cha Makerere, Africa Junior, kuhusu Kituo cha utafiti wa Usafirishaji, wakati alipotembelea kwenye banda la Chuo Kikuu cha Makerere kwenye Maonyesho ya Nane ya Vyuo Vikuu kutoka nchi mbalimbali yanayofanyika kwa siku tatu katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa, Ofisa Udahiri Mwandamizi wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania, Hilder Kawiche, wakati alipotembelea Banda hilo kwenye Maonyesho ya Nane ya Vyuo Vikuu kutoka nchi mbalimbali yanayofanyika kwa siku tatu katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa, Makamu Mwenyekiti wa Chuo Kikuu cha United African-Tanzania, Jo, Do Hyun, kuhusu matumizi ya gari ndogo inayotumia Chaji ya Umeme wakati alipotembelea katikia Banda hilo,kwenye Maonyesho ya Nane ya Vyuo Vikuu kutoka nchi mbalimbali yanayofanyika kwa siku tatu katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Sakina Taki (kushoto) na Tannaz Naseri, kutoka 'University of the Future' , Kuala Lumpur, wakati alipotembelea Banda hilo kwenye Maonyesho ya Nane ya Vyuo Vikuu kutoka nchi mbalimbali yanayofanyika kwa siku tatu katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa, Msimamizi Mkuu wa Teknolojia wa Chuo Kikuu cha SUA, Gaudencia Donati, wakati alipotembelea Banda hilo kwenye Maonyesho ya Nane ya Vyuo Vikuu kutoka nchi mbalimbali yanayofanyika kwa siku tatu katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Akitembelea katika Mabanda ya maonyesho ya Nane ya Vyuo Vikuu kutoka nchi mbalimbali ndani ya Ukumbi wa Diamond Jubilee, leo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa maonyesho hayo.

TANGAZO KWA UMMA

0
0

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII


  
TANGAZO KWA UMMA

Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kupitia Tangazo lake kwenye Gazeti la Habari Leo la tarehe20 Aprili, 2013 siku ya Jumamosi na la tarehe 23 Aprili, 2013 siku ya Jumanne na kwenye tovuti ya Wizara, ilitangaza nafasi mbalimbali  za kazi za Kada ya Afya zikiwemo za Maafisa Ustawi wa Jamii, Maafisa Ustawi wa Jamii Wasaidizi, Walezi wa Watoto, Maafisa Lishe na Maafisa Lishe Wasaidizi.

Wizara inapenda kuwajulisha waombaji wa nafasi za Kada tajwa hapo juu zitashughulikiwa na Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira.

Hivyo, waombaji wote waliotuma maombi yao Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, wanajulishwa kuwa maombi yao yatapelekwa Sekretarieti ya Ajira kwa ajili ya uchambuzi na usaili.

Tangazo hili halihusu waombaji walioomba Kada mbalimbali za Afya ambazo zitashughulikiwa moja kwa moja na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
  

Kaimu Katibu Mkuu
WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII
22 Mei, 2013
Viewing all 46205 articles
Browse latest View live




Latest Images