Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live

Rais Magufuli afanya mabadiliko madogo katika Baraza la Mawaziri

$
0
0


Aliyekuwa Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba ameteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.


Mbunge wa Buchosha Dkt. Charles John Tizeba ameteuliwa kuwa Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi.






 


B​ARCLAYS CUSTOMERS TO OPEN A BANK ACCOUNT IN 20 MINUTES.

$
0
0

Barclays Bank Tanzania (BBT) Head of Customers Network, Emmanuel Katuba (second left) and banks Head of Operations, Msungu Mwilingo (second right), displaying placard to official launch the Barclays 20 minutes account opening service in Dar es Salaam at the weekend. Looking on from left are, BBT Head of Change, Aleem Thawar and banks Head of IT, Dakshit Pandya.
Barclays Bank Tanzania (BBT) Head of Customers Network, Emmanuel Katuba (second left) addresses a media conference in Dar es Salaam at the weekend during the official launching ceremony of the Barclays 20 minutes account opening service in Dar es Salaam at the weekend. Looking on from left are, BBT Head of Change, Aleem Thawar, Ag. Head of Marketing and Corporate Affairs, Joe Bendera, Head of Operations, Msungu Mwilingo and banks Head of IT, Dakshit Pandya.
Barclays Bank Tanzania (BBT) Ag. Head of Marketing and Corporate Relations, Joe Bendera (centre), addresses a media conference in Dar es Salaam at the weekend during the official launching ceremony of Barclays 20 minutes account opening service in Dar es Salaam at the weekend. Looking on from left are, BBT Head of Change, Aleem Thawar, Head of Customers Network, Emmanuel Katuba, Head of Operations, Msungu Mwilingo and banks Head of IT, Dakshit Pandya.
Barclays Bank Tanzania (BBT) Head of Customers Network, Emmanuel Katuba (centre) addresses a media conference in Dar es Salaam at the weekend during the official launching ceremony of the Barclays 20 minutes account opening service in Dar es Salaam at the weekend. Looking on from left are, BBT Head of Change, Aleem Thawar, Ag. Head of Marketing and Corporate Affairs, Joe Bendera, Head of Operations, Msungu Mwilingo and banks Head of IT, Dakshit Pandya.

CUSTOMERS at Barclays Bank Tanzania (BBT), will now have priveledge to open a bank account within 20 minutes.

Speaking during the launching of a program namely 'Barclays Operating Customers' (BOC) in the City of Dar es Salaam at the weekend, BBT Ag. Head of Marketing and Corporate Relations, Joel Bendera said that the bank becomes the first bank in Tanzania to start the system that can help customers to open an account for a maximum period of 20 minutes.

The Barclays marketing chief said the operation for this program will be started in two branches. “We will start the operation in two branches Sleep Way and Ohio branches and we hope to expand the operation” he said.

He moreover said this program will help customers to save their time to open an account and not only saving the time to open an account but also even the requirements are very simple which are work identity, settlements identification and sources of income of the customer.

On his part, Barclays Head of Customers Network Retail Banking, Emmanuel Katuma said they have research and testing much the operating system and approve that it can work effectively and accurately.

“We are sure that this program will be successfully and the first in the country because we have spend our time and resources to come up with” said Katuma.

He however said that this program will help the bank to get many customers especially the new account openers, where as one customer may require only 20 minutes maximum to open a new account.

“Before starting this operating we were having the capacity of opening ten to twenty account in one branch but now we will have ability to open one account in every twenty minutes you can see how many accounts can be opened per day in one branch” he added.

Barclays bank has 17 branches in the country and expecting to open new branches soon. The branches are available in 10 regions in the country.

NI MANJI,SANGA TENA YANGA AFRICANS.

$
0
0
Mwenyekiti wa Yanga alipokuwa akisoma hotuba yake mbele ya mamia ya wanachama (hawapo pichani) kupitia simu yake ya kiganjani,hapo jana ndani ya ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar

Mchakato mzima wa uchaguzi katika club ya Yanga Africans umemalizika salama na matokeo yapo kama ifuatavyo.

Mwenyekiti Yusuph Manji ametangazwa mshindi baada  kupata kura 1,468 kati ya 1,470 zilizopigwa huku kura mbili tu zikiharibika na hakukuwa na kura ya hapana,m manji hakuwa na mpizani kwenye nafasi hiyo.

Makamu mwenyekiti Clement Sanga ambaye alikuwa akipigania nafasi hiyo na Titus Osoro, ameibuka mshindi  baada ya kujizolea kura 1,428 kati ya 1,508 zilizopigwa. Mpinzani wake aliambulia kura 80 tu.

Nafasi za ujumbe Wagombea waliku jumla 20 walioibuka na ushindi katika uchaguzi ni
1. Siza Augustino Lymo (1027)
2. Omary Said Amir (1069)
3. Tobias Lingalangala (889)
4. Salim Mkemi (894)
5. Ayoub Nyenzi (889)
6. Samuel Lucumay (818)
7. Hashim Abdallah (727)
8. Hussein Nyika (770)

Idadi ya wajumbe 12 wameshindwa kuibuka na ushindi baada ya Kura kuwa pungufu ambao ni 1. David Luhago (582)
2. Godfrey Mheluka (430)
3. Ramadhani Kampira (182)
4. Edgar Chibura (72)
5. Mchafu Chakoma (69)
6. George Manyama (249)
7. Bakari Malima (577)
8. Lameck Nyambaya (655)
9. Beda Tindwa (452)
10. Athumani Kihamia (558)
11. Pascal Lizer (178)
12. Silvester Haule (197)

JE WAJUA UNAJUA NINI KUHUSU MNYAMA TEMBO?

$
0
0
Na Geofrey Chambua
#1.TEMBO unayemjua wewe kwa wastani ana uzito wa kilogramu elfu kumi kwenda mbele (Hapa namuongelea tembo mkubwa)  Tembo pamoja na ukubwa wake akitembea hana kishindo kabisa miguu yake kwa chini ni kama ina sponge hivi.

#2. Wakati mwanamke anabeba ujauzito kwa kipindi cha miezi tisa, TEMBO mkubwa wa kike anabeba ujauzito kwa jumla ya miaka miwili yaani miezi ishirini na minne kabla hajazaa.
#3. Ukimwondoa mwanadamu ambaye ana KIDEVU, Tembo ndiye mnyama mwinginbe  ambaye pia anacho kidevu…..
#4. Tembo anao uwezo wa kumsikia Tembo mwenzake akilia kutoka umbali wa kilometa tano….Tembo hana uwezo mkubwa wa kutambua vitu kwa kuona. hutegemea zaidi pua na masikio kuweza kufanikisha shughuli zake. kutokana na hali hiyo, mara nyingi ukiwa porini unashauriwa kumpiga picha tembo BILA ya kutumia flash. hii inatoka na kwamba, endapo utatumia flash wakati unampiga picha, tembo atajenga hisia ya kutoelewa nini kimetokea. kwa kifupi hataweza kutofautisha kama ni kitu cha kawaida au ni hatari. katika mazingira haya, huanza ku-charge kuelekea upande ule ambao mwanga
 #5. Ni Tembo wa Afrika pekee mwenye uwezo wa kutofautisha kabila, jinsia na umri wa mwanadamu. Ikiwa jana alijeruhiwa na mtu anayezungumza kiingereza, akisikia kiingereza anakumbuka upesi…
#6. Takribani Tembo mia moja huuwawa kila siku kwa sababu ya pembe zao….
#7. Kila mnyama kuna kitu anakiogopa sana, lakini ni ajabu sana kwa Tembo ambaye anamuogopa nyuki kuliko kitu chochote.
#8. Tembo mkubwa na mzito kupita wote anapatikana Afrika…
#9. Ikiwa mwanadamu hulala walau masaa nane kwa siku, kwa Tembo ni tofauti… Tembo hulala masaa mawili hadi matatu kwa siku!!
#10. Kuhusiana na mambo ya kula na kunywa… Tembo mkubwa huitaji walau kilo mia tatu za chakula na maji lita 160 kwa siku!!! Kama unahitaji kumfuga ujiandae……
11. Tembo anategemea sana uwezo wake wa kunusa ili kuweza kutambua mazingira aliyopo na vitu vinavyomzunguka. Sambamba na harufu, tembo pia ana uwezo mkubwa wa kusikia kupitia masikio yake makubwa (by the way, tembo porini huitwa Masikio).
12 Tembo ana fanya mapenzi kwa masaa 12; masaa 6 ya mwanzo anamuandaa mwenzi wake na 6yanayobaki ndio shughuli yenyewe na hiyo ni ile raundi ya kwanza.
13 Tembo dume huwa na wanawake wawili mpaka wanne
14. Akipiga bao tembo dume manii zake ni ujazo wa lita tano

DARAJA LA MTO SIBITI KUKAMILIKA HIVI KARIBUNI; PROF. MBARAWA

$
0
0
Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), mkoa wa Singida Eng. Leonard Kapongo (wa kwanza kushoto), akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (wa pili kushoto) kuhusu mradi wa ujenzi wa Daraja la Mto Sibiti linalounganisha Wilaya ya Mkalama mkoani Singida na Meatu mkoani Simiyu.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (wa pili kushoto) akitoa maelekezo kwa Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), mkoa wa Singida Eng. Leonard Kapongo (wa kwanza kushoto) kuhusu usimamizi wa ujenzi wa Daraja la mto Sibiti.
Muonekano wa moja ya nguzo inayoshikilia Daraja la Mto Sibiti linalounganisha Wilaya ya Mkalama mkoani Singida na Meatu mkoani Simiyu.
Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Bw. Christopher Ngubiagai (katikati), akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (wa kwanza kushoto) alipokagua ujenzi wa Daraja la Mto Sibiti.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (wa kwanza kushoto) akikagua jengo la nyumba ya Mkuu wa Wilaya ya Mkalama linalojengwa na Wakala wa Majengo nchini (TBA) mkoani Singida.
Muonekano wa juu wa Daraja la Msingi lenye urefu wa mita 75 linalounganisha Wilaya ya Mkalama na Iramba, lililopo mkoani Singida.
Muonekano wa jengo la ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama inavyoonekana katika hatua za awali za ujenzi wake. Zaidi ya milioni 758 zinatarajiwa kutumika katika ujenzi huo.
Msimamizi wa jengo la ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama (wa kwanza kulia), akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (wa kwanza kushoto), kuhusu hatua za ujenzi wa ofisi hizo mkoani Singida.


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amemtaka mkandarasi Hainan International Limited anayejenga Daraja la mto Sibiti ambalo linaunganisha mkoa wa Singida na Simiyu kuendelea na ujenzi wake.

Amesema hayo mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo na kuwahakikishia wananchi kuwa daraja hilo litakamilika katika kipindi cha hivi karibuni baada ya Serikali kuanza kumlipa mkandarasi huyo.

“Tumeanza kumlipa mkandarasi fedha hivyo tunawahakikishia kwamba katika kipindi kifupi kijacho litakamilika ili kufungua shughuli za kiuchumi kwa wakazi wa Wilaya ya Mkalama na Meatu” , amesema Prof. Mbarawa.

Aidha Waziri huyo wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano amekemea tabia ya baadhi ya wananchi kutoza ushuru katika mto huo na kusisitiza kwamba tabia hiyo iachwe mara moja na atakayefanya hivyo anakiuka sheria na hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

“Wananchi wanatakiwa kupita hapa bila ya kulipa gharama yoyote katika mto huu, nimemuagiza Mkuu wa Wilaya na Meneja wa TANROADS mkoa wa Singida waboreshe eneo la kuvukia ili wakati ujenzi unaendelea huduma za kuvuka ziendelee kama kawaida”, amesisitiza Waziri Prof. Mbarawa.

Naye Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), mkoa wa Singida Eng. Leonard Kapongo amemhakikishia waziri kuwa ujenzi wa Daraja la mto sibiti pia utahusisha barabara ya maingilio yenye urefu wa kilomita 25 inayounganisha wilaya ya Mkalama na Meatu.

“Ujenzi wa barabara za maingilio unahusisha makalvati makubwa 10 na madogo 55 ili kuruhusu maji kupita kwa kasi na hivyo kudhibiti mafuriko”, amefafanua Eng. Kapongo.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Bw. Christopher Ngubiagai amemshukuru Waziri Prof. Mbarawa kwa jitihada zake za kutaka kuunganisha wilaya yake na Meatu kwani kukamilika kwa daraja hilo kutaimarisha fursa za usafirishaji wa mazao na huduma za usafiri katika Wilaya hizo.

Zaidi ya shilingi bilioni 18.2 zinatarajiwa kutumika katika ujenzi wa Daraja la mto Sibiti lenye urefu wa mita 82 na upana wa mita 10.5 ambapo tayari Serikali imeshalipa zaidi ya shilingi bilioni 4 mpaka sasa.

Katika hatua nyingine Prof. Mbarawa amekagua ujenzi wa nyumba za viongozi wa Wilaya ya Mkalama na jengo la Halmashauri ya Wilaya hiyo na kuwataka makandarasi wanaoendelea na ujenzi wa miradi hiyo kuongeza kasi na kutumia fedha wanazopata kujenga jengo moja moja kwa awamu ili kupunguza changamoto ya makazi na ofisi Wilayani humo badala ya utaratibu wa sasa wa kujenga majengo yote kwa pamoja.

.”Msisubiri mpate fedha zote kwa nyumba zote, kamilisheni ujenzi wa nyumba moja moja kadri mnavyopata fedha ili kupunguza changamoto za makazi na ofisi”, amesisitiza Prof. Mbarawa.

Prof. Mbarawa yuko katika siku ya pili ya ziara yake ya siku nne mkoani Singida ya kukagua miradi ya ujenzi wa miundombinu ya barabara, nyumba na Mawasiliano.

MHE. WAZIRI MKUU MSTAAFU MIZENGO PINDA ATEMBELEA SHULE YA MSINGI YA MCHEPUO WA KIINGEREZA

$
0
0
Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda akiongea na wanafunzi wa darasa la kwanza wa shule ya Msingi ya Mchepuo wa Kiingereza ya Katavi iliyopo Mikwambe, Kigamboni Wilayani Temeke wakati alipoitembelea shule hiyo hivi karibuni ili kuwasalimia wanafunzi na kujionea maendeleo ya shule hiyo.
Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda akimsikiliza Glorius Nkinda ambaye ni mwanafunzi wa darasa la kwanza katika shule ya Msingi ya Mchepuo wa Kiingereza ya Katavi iliyopo Mikwambe, Kigamboni Wilayani Temeke wakati akijibu swali la Hesabu alilomuuliza. Mhe. Pinda alitembelea shule hiyo hivi karibuni kwa ajili ya kuwasalimia wanafunzi na kujionea maendeleo ya shule hiyo.

Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda akimsikiliza Kelvin Agustino mwanafunzi wa darasa la kwanza katika shule ya Msingi ya Mchepuo wa Kiingereza ya Katavi iliyopo Mikwambe, Kigamboni Wilayani Temeke alipokuwa akisoma kitabu cha Kiingereza wakati alipoitembelea shule hiyo hivi karibuni ili kuwasalimia wanafunzi na kujionea maendeleo ya shule hiyo.

Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda akiwauliza maswali wanafunzi wa shule ya awali wa shule ya Msingi ya Mchepuo wa Kiingereza ya Katavi iliyopo Mikwambe, Kigamboni Wilayani Temeke wakati alipotembelea shule hiyo hivi karibuni ili kuwasalimia wanafunzi na kujionea maendeleo ya shule hiyo.
Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda akiwauliza maswali wanafunzi wa shule ya awali wa shule ya Msingi ya Mchepuo wa Kiingereza ya Katavi iliyopo Mikwambe, Kigamboni Wilayani Temeke wakati alipotembelea shule hiyo hivi karibuni ili kuwasalimia wanafunzi na kujionea maendeleo ya shule hiyo.
Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda akiwa katika picha ya pamoja na walimu pamoja na wanafunzi wa darasa la tatu wakati alipoitembelea shule ya Msingi ya Mchepuo wa Kiingereza ya Katavi iliyopo Mikwambe, Kigamboni Wilayani Temeke wakati alipotembelea shule hiyo hivi karibuni ili kuwasalimia wanafunzi na kujionea maendeleo ya shule hiyo. Picha na Mpigapicha wetu

KUMI WENGINE WAWA MAMILIONEA KATIKA DROO YA TATU YA PROMOSHENI YA TUSKER

$
0
0

Afisa Mwandamizi wa ukaguzi kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha nchini Tanzania ,Emmanuel Ndaki akihakiki taarifa za mmoja wa washindi waliotangazwa katika droo ya tatu,kushoto kwake ni meneja wa bia ya tusker Jasper Maston.Meneja wa bia ya tusker Jasper Maston akitoa maelezo kuhusu promosheni ya millioni mia moja na tusker fanya kweli uwini katika droo ya tatu iliyofanyika jijini dar es salaam mwishoni mwa wiki.
droo ikichezeshwa kupata washindi kumi wa tusker fanya kweli uwini.


 Ni wiki nne zimepita sasa na tayari washindi 20 wameshakabidhiwa vitita vyao kupitia promosheni inayoendeshwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti ijulikanayo kama Milioni 100 na Tusker Fanya Kweli Uwini na kumi wengine kumi wametajwa leo katika droo ya tatu ya promosheni hiyo inayofanyika kila wiki. Wiki mbili zilizopita tulishuhudia washindi kumi kila wiki kutoka mikoa mbalimbali nchini wakiondoka na Million moja kila mmoja kupitia promosheni hiyo inayoendelea. Katika droo ya tatu iliyochezeshwa leo, ambako washindi wengine kumi walitangazwa.

Katika droo hiyo iliyofanyika ITV na kushuhudiwa na maofisa kutoka Bodi ya kusimamia Michezo ya Kubahatisha na wakaguzi wa nje, walitangazwa washindi kumi ambao ni Julius Lucas, Damas Mathei, Dustan Mhina, Hussein Shaban kutoka Dar es Salaam, Teddy Tarimo kutoka Kilimanjaro, Mwahu Hamis - Arusha, Mary Steve na Marietha Thomas - Morogoro, Domino Juma Shinyanga pamoja na Edison Maxini kutoka Mwanza.

Mbali na washindi wa pesa taslim, pia kuna washindi kibao waliojishindia bia za bure papo hapo tangu promosheni ilipoanza. Mpaka sasa tayari takribani bia za bure zaidi ya 3000 zimeshagawiwa kwa watumiaji wa bia ya Tusker na zawadi nyingine kibao kama vile tshirt na kofia.

Akizungumza wakati wa droo hiyo Meneja wa Bia ya Tusker Jasper Maston alieleza kuwa, promosheni ya ‘Tusker Fanya Kweli Uwini’ bado inaendelea na tayari washindi wa droo ya kwanza na ya pili wameshakabidhiwa vitita vyao. “Kwa kweli promosheni inaendelea vyema kabisa na washindi wanaendelea kushinda kutoka kila pande za Tanzania ambako sasa watumuaji wa Tusker wanaendelea kujitokeza kwa wingi kabisa kushiriki promosheni hii.

Hali hii inaendelea kutupa moyo na kuona kuwa wateja wetu wapo pamoja nasi kutupa sapoti. Leo tumeshuhudia wenyewe washindi kutoka karibu kanda zote nchi nzima Mwanza, Shinyanga, Morogoro, Arusha, Kilimanjaro and Dar es Salaam. Tunapenda kuwakumbusha wateja wetu kuwa promosheni bado inaendelea na bado tuna mamilioni kwa ajili yao, tunaamini kuwa ndani ya wiki saba zilizobakia tutapata washindi wengine wapya watakaoshiriki.”

Naye mmoja wa washindi Mary Steve kutoka Morogoro aliishukuru sana Kampuni ya Bia ya Serengeti kwani ilikua kama miujiza kwake kupata kiasi hicho cha pesa kwa kipindi hiki. “Nipata taarifa kuhusu promosheni hii kupitia maonesho ya barabarani nami kama mtumiaji mzuri wa Tusker nikaona nijaribu.

Sikutegemea kama naweza kuwa kati ya wale wenye bahati, nilikua na shida sana na pesa kwa ajili ya kuongeza mtaji katika biashara yangu sasa naona Tusker imeniokoa na kutatua tatizo langu, nimepata pesa ya kufanyia biashara zangu nawashukuru sana. Ntaendelea kushiriki mara nyingi maana huwezi jua nikawa mshindi tena kwa mara nyingine.” Aliendelea kwa kuipongeza Kampuni ya Bia ya Serengeti kwa kuendesha promosheni kama hiyo inayogusa maisha ya wateja wake kwa kubadili sehemu au maisha yote kwa ujumla.

Washindi wote waliotangazwa leo watakabidhiwa vitata vyao katika hafla fupi zitakazofanyika sehemu mbalimbali wiki ijayo.

NSSF YAWAFIKIA MADEREVA WA BODABODA MKOANI DODOMA

$
0
0
Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii NSSF limefanya semina na kuzindua mpango wa kuwaandikisha madereva wa Bodaboda Mkoani Dodoma, Mpango huo ulifanywa kwa ushirikiano wa Manispaa ya Mji wa Dodoma, VETA , Trafiki Mkoa na NSSF umezinduliwa na Waziri wa Nchi , Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira,Vijana na Watu wenye Ulemavu Jenista Mhagama.

Pamoja na Uzinduzi wa Uandikishaji Waziri Jenista Mhagama aliwapatia Vifaa vya Usalama Madereva hao wa BodaBoda Mkoani Dodoma vifaa hivyo ni Kofia ya Usalama na Kikoti Maalumu cha Usalama ambavyo vimeandikwa Namba kulingana na Kituo cha Bodaboda Wanachofanyia Kazi. Pia Waziri amezindua mfumo wa kuvipa namba na kuviweka alama Vibao vituo vyote vya Bodaboda mkoani Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Prof. Godius Kahyarara akiongea na Madereva wa Bodaboda (hawapo pichani) wakati wa Uzinduzi rasmi wa Kampeni ya Kuandikisha Madereva wa Bodaboda Mkoani Dodoma.
Waziri wa Nchi , Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira,Vijana na Watu wenye Ulemavu Jenista Mhagama akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa Mpango wa kuwaandikisha madereva wa Bodaboda Mkoani Dodoma.
Meneja wa NSSF Mkoa wa Dodoma Rehema Chuma akitoa elimu kwa Madereva wa Bodaboda wa Mkoa wa Dodoma waliouzulia zoezi la uzinduzi wa kampeni rasmi ya kuwatambua na kuwaandikisha NSSF madereva wa Bodaboda.
Waziri akikabidhi moja ya pikipiki ambazo wamekopeshwa madereva wa Bodaboda Dodoma na Manispaa ya Dodoma. Wakishuhudia ni Mwakilishi wa Kamanda wa Trafiiki Mkoa, Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF na Mkuu wa Chuo cha VETA Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu Jenista Mhagama akimvalisha mmoja wa Madereva wa Bodaboda Kofia Ngumu ya Usalama iliyotolewa na NSSF. Anayeshuhudia kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Prof, Godius Kahyarara.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu Jenista Mhagama akimvesha Jaketi maalumu la Usalama Dereva wa Bodaboda Mkoa Dodoma akimsaidia Waziri ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Bahi Francis Mwonga.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu Jenista Mhagama akikabidhi mfano wa Kituo Cha Bodaboda kwa Mwenyekiti wa Bodaboda Mkoani Dodoma Bang'ara Lucas Kang'alo akishuhudia katikati Mkurugenzi wa NSSF Prof Godius Kahyarara.
Mwenyekiti wa Bodaboda Mkoa wa Dodoma akiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri wa Nchi Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu Jenista Mhagama, Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ambaye ni Mkuu wa Wilaya wa Bahi Francis Mwonga( Wa Kwanza kulia kwa Waziri), Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Prof Godius Kahyarara (Kushoto kwa Waziri) na Mkuu wa Chuo cha Veta Dodoma Bw. Mattaka baada ya kupokea mfano wa kadi ya Mwanachama ya NSSF akiwa mmoja ya wanachama wapya waliojiunga NSSF.

VIONGOZI WA MFUKO WA MAENDELEO YA PAMBA WAUMBULIWA

$
0
0

MKUU wa wilaya ya Nyang’hwale mkoani Geita, Ibrahimu Marwa amesema viongozi wa Mfuko wa Wakfu wa maendeleo ya zao la pamba uliwapelekea wakulima pembejeo feki na kuwasababishia hasara.

Amesema hatua hiyo inatokana wafanyabiashara na viongozi wa mfuko huo kuwa na maslahi binafsi katika zao la pamba hivyo kushindwa kuwasaidia wakulima ipasavyo.

Marwa aliyasema hayo jana (Jumamosi, Juni 11, 2016) wakati Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu, Ezekiel Kyunga alipokuwa akisoma taarifa ya Mkoa huo kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipowasili Mkoani hapo.

Alisema mara baada ya wakulima kupelekewa pembejeo hizo na kubaini kuwa na kasoro walizipeleka katika Kiituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ukirigulu kilichoko mkoani Mwanza ambacho nacho kilithibitisha kuwepo kwa kasoro.Kwa upande wake Waziri Mkuu amewataka Maofisa Kilimo kuhakikisha wanatimiza wajibu wao na kuwasaidia wakulima wa pamba ili waweze kupata tija.

Ametaka Maofisa Kilimo na viongozi wa maeneo yanayolima pamba kujipanga upya baada ya kumalizika kwa msimu wa mwaka kwa kuanza mikakati ya kufanya utafiti wa mbegu bora za pamba na kuziandaa za kutosheleza wakulima wote.Alisema hakuna sababu ya kuendelea kuwa na Maofisa Kilimo ambao wanashindwa kutimiza majukumu yao kwa sababu mashamba ya wakulima yanashindwa kuendelea kwa kuwa hakuna mtu anayewafuatilia.

“Mwakani muanze kufanya utafiti kuanzia hatua za awali na kituo cha Ukirigulu kipewe kazi ya kusimamia zao hili na kiwe na shamba darasa kwa ajili ya kufundishia wakulima. Lengo ni kuhakikisha zao hili linakuwa na tija,” alisema.Hata hivyo Waziri Mkuu ameziagiza Halmashauri za Wilaya zinazolima pamba zifanye utafiti ili kujua sababu zilizosababisha wakulima kupunguza ari ya kulima zao hilo.

Pia amewataka waachane na mfumo wa kilimo cha mkataba kwa sababu hauna tija kwa mkulima kwani hautengenezi ushindani na badala yake wajifunze mfumo unaotumika katika uuzaji wa zao la korosho.

USAHILI WA MAISHA PLUS EAST AFRIKA 2016 KUFANYIKA JUMAMOSI TAREHE 18/06 JIJINI DAR ES SALAAM

WATANZANIA WATAKIWA KUSHIRIKIANA KUPIGA VITA MATUKIO YA MAUAJI

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Watanzania, viongozi wa dini zote kushirikiana kwa pamoja kupiga vita matukio maovu ya mauaji yaliyotokea katika maeneo mbalimbali nchini.

Amesema anatarajia hali ya amani, usalama na utulivu inaendelea kuwepo nchini, hivyo wananchi hawana budi kushirikiana na kushikamana na Serikali katika kuhakikisha matendo maovu hayatokei katika maeneo yao.

Waziri Mkuu ameyasema hayo jana (Jumamosi, Juni 11, 2016) wakati alipowasili mkoani Geita kwa ajili ya kuhudhuria ibada ya kuwekwa wakfu Padre Flavian Kassala kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki Geita.

“Mfano tukio la Mwanza watu wanavaa kanzu na wanaingia msikitini na kukuta wenzao wanafanya ibada kisha wakawachinja, hii haiwezekani kwa binadamu wa kawaida hivyo tushirikiane katika kupiga vita matendo haya,” alisisitiza.

Hivi karibuni jumla ya watu 15 waliuawa kwa kukatwakatwa na mapanga katika mikoa ya Mwanza,Tanga, Dar es Salaam na Mara.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Geita, Meja Jenerali Mstaafu, Ezekiel Kyunga amesema vitendo vya watu kuuawa kwa kukatwa mapanga vimepungua baada ya kuanzisha kampeni maalumu ya kukemea mauaji hayo.

Alisema katika kampeni hiyo wameamua kuwatumia walimu, viongozi wa dini mbalimbali pamoja na wauguzi ambao wamekuwa wakiwaelimisha wananchi kuachana na imani potofu za kishirikina na badala yake wajikite katika masuala ya maendeleo.

IMETOLEWA NA OFISI YA WAZIRI MKUU

JUMAPILI, JUNI 12, 2016.

OLE SENDEKA AWATAKA JAMII YA WAMASAI KUTEUA CHIFU MPYA MWENYE HEKIMA NA BUSARA YA KUTOSHA

$
0
0

Na Bashir Nkoromo, Kibaha

Msemaji Mkuu wa CCM, Christopher Ole Sendeka, ameongoza shughuli ya arobaini ya Kiongozi wa Jamii ya Wamasai wa kundi la Parakuyo, katika Kanda ya mikoa ya Tanga, Pwani, Morogoro, Mbeya na Iringa, Chifu Moreto Ole Maitei, iliyofanyika leo katika Kijiji cha Kigoda, Kata ya Gwata, Kibaha Vijijini katika mkoa wa Pwani.

Katika shughuli hiyo ambayo ilifanyika kimila, Sendeka ambaye alialikwa kuongoza shughuli hiyo Kama kiongozi wa Kimasai anayeheshimika, aliwataka Jamii ya Wamasai Kanada za mikoa hiyo, kuwa na Umoja na kutumia hekima na busara katika kumpata mrithi wa nafasi iliyoachwa na Chifu Ole Maitei.

Aliwataka kumteua Chifu au Laiboni, mwenye sifa zinazostahili ambazo hata kama Chifu Ole Maitei angekuwepo angerithika kuwa anafaa kuwa mrithi wake.

Kwa heshima aliyopewa katika shughuli hiyo Ole Sendeka, aliweka kwenye kaburi kibuyu na usinga ambavyo ni vifaa alivyokuwa akitumia Chifu Ole Maitei ambaye ndani ya Jamii hiyo anatambuliwa zaidi kwa cheo cha Laiboni ambaye ni kiongozi mkuu wa viongozi wanaofuatia hadhi yake wanaoitwa Laigwanani. Uwekaji vifaa hivyo ulifayika huku ukishuhudiwa na ndugu jamaa na wanajamii hiyo, Mjane na Dada wa Marehem.

Mmoja wa Malaigwanani waliohudhuria shughuli hiyo, alisema, Kibuyu hicho alichoweka Ole Sedeka kwenye kaburi, ndani kilikuwa na mawe ambayo Chifu Ole Maitei alikuwa akiyatumia kubashiri yanayoweza kutokea mbele ya safari huku usinga akiutumia kupungia kuwasalimia wageni au kufukuzia mbali mifarakano na balaa katika jamii yao.

Kabla ya kuweka vifaa hivyo kwenye kaburi, Sendeka alitanguliwa na watoto wote wa kiume kumwaga kwenye kaburi hilo asali, maziwa ya ng'ombe na mafuta ya kidari cha dume maalum la ng'ombe kama ishara ya kutekeleza mila na desturi.

Chifu Ole Maitei ambaye alikuwa kiungo muhimu kwa kuunganisha jamii hiyo ya Kimasai hasa katika utatuzi wa migogoro yawafugaji kutoka jamii hiyo na wakulima katika maeneo mbalimbali ya mikoa ya Tanga, Pwani, Morogoro, Mbeya na Iringa alipokea nafasi ya Uchifu kutoka kwa Laibon Labani Moreto ambaye alifariki miaka ya 2005. PICHA KEM KEM ZA TUKIO HILO>BOFYA HAPA

NEWZ ALERT:OLE MEDEYE ATIMKA CHADEMA NA KUHAMIA UDP LEO

$
0
0
Kada wa Chadema na mbunge wa zamani wa Arumeru Magharibi, Goodluck Ole Medeye ametangaza leo rasmi kuhamia chama cha UDP.Ole Medeye amezungumza hayo mbele ya mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika katika ofisi za Makao Makuu ya chama hicho,Mwananyamala jijini Dar.

Medeye amezungumza kwa kujipambanua kuwa yeye anasimamia haki na demokrasia, na kwamba amekerwa sana na tabia ya vyama vya Upinzani kutomheshimu Naibu Spika,Dkt. Tulia Ackson Mwansasu,pichani kati ni Mwenyekiti wa chama cha UDP,Mh.John Cheyo akishuhudia tukio hilo.
 Kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Dkt.Goodluck Ole Medeye, akionesha kadi yake ya uanachama mbele ya Waandishir wa habari (hawapo pichani),kuashiria kuwa sasa ni mwanachama halali wa chama hicho cha United Democratic Party UDP,shoto ni Mwenyekiti wa chama hicho John Momose Cheyo.
  Dkt.Goodluck Ole Medeye, akikabidhiwa kadi ya uanachama mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani) na Mwenyekiti wa chama hicho John Momose Cheyo.
Kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, aliyedumu na chama hicho kwa miezi kumi na moja Goodluck Ole Medeye, amekihama chama hicho na kujiunga na United Democratic Party UDP.

Bw. Medeye aliyewahi kuwa Mwanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM na kuitumikia serikali katika nafasi ya Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, ametangaza uamuzi wa kuhama Chadema jijini Dar es Salaam na kukabidhiwa kadi ya UDP na Mwenyekiti wa Chama hicho John Momose Cheyo.

Mbunge huyo wa zamani wa jimbo la Arumeru Magharibi amejiunga na UDP akiwa na Mkewe, pamoja na watu wengine tisa wakiwemo waliokuwa kwenye vyama tofauti na wengine waliodai hawakuwahi kuwa kwenye siasa, ambapo katika maelezo yake, Ole Medeye amesema awali alitaka kuunda chama kipya lakini baada ya kupitia katiba za vyama akaona UDP ni sehemu sahihi.

Kuhusu masuala mbalimbali yanayoendelea nchini, wanasiasa hao wamelaani uminywaji wa demokrasia katika kipindi hiki, hususan ndani ya Bunge, na kushauri wabunge wa kambi ya upinzani wanaosusia vikao kurejea ndani ya ukumbi wa Bunge kwa vile njia wanayotumia haitabadili utaratibu wa kibunge hususan kumuondoa Naibu Spika kwenye kiti chake.

Waziri Mkuu Kassim majaliwa ahudhuria sherehe za kumsimika askofu wa jimbo la geita Flavian Kassal

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Maliwa akiwapungia waumini wa Kanisa katoliki  jimbo la Geita baada ya kuhudhuria sherehe za kumsimika Askofu wa jimbo hilo, Flavian Kassala  zilizofanyika mjini Geita Juni 12, 2016. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Geita na Mbunge wa Geita Vijijini Joseph Msukuma.
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akiwa katika picha ya pamoja na Maaskofu wa Kanisa katoliki katika sherehe za kumsimika Askofu wa jimbo la Geita, Flavian Kassala  (kushoto kwake) zilizofanyika kwenye kanisa kuu katoliki mjini Geita Juni 12, 2016.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

 
WAZIRI MKUU AWATAKA VIONGOZI WA DINI KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KUPAMBANA NA RUSHWA, UFISADI

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka viongozi wa dini kushirikiana na Serikali katika kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazoikabili zikiwemo za rushwa, ufisadi na matumizi mabaya ya fedha za umma.

Amesema siku zote kumekuwa na ushirikiano mzuri kati ya Serikali na Asasi mbalimbali ikiwa ni pamoja na madhehebu ya Dini katika kuwapatia huduma za kijamii kama vile, afya, elimu, maji, utunzaji wa mazingira na nyingi nyingine.

Waziri Mkuu Majaliwa ameyasema hayo leo mchana (Jumapili, Juni 12, 2016) wakati alipomuwakilisha Mheshimiwa Rais Dk. John Magufuli katika Ibada ya kuwekwa wakfu na kusimikwa kuwa Mhashamu Askofu Flavian Kassala kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki Geita.

“Serikali inatambua jitihada kubwa zilizowekwa na Kanisa Katoliki katika Jimbo hili la Geita na Tanzania kwa ujumla hivyo wito wangu kwa Baba Askofu na Waumini wa Kanisa kwa ujumla wenu ni kuwaomba muendelee na kazi hii nzuri ya kutoa huduma muhimu kwa jamii,” amesema.

Amesema maendeleo ya nchi yanawategemea wote hivyo ushirikiano kati ya Kanisa na Serikali utawezesha maendeleo ya Taifa kupatikana kwa kasi zaidi na kunufaisha wananchi wote.

Waziri Mkuu amesema jukumu la Serikali ni kuweka mazingira wezeshi ambayo yatasaidia Mtanzania kujikomboa na umaskini na kwamba kazi kubwa ya viongozi wa dini kuunganisha jamii na wala siyo kuwatenganisha.

Hata hivyo Waziri Mkuu amesema kinachotakiwa kufanywa na wote ni kumwuomba Mwenyezi Mungu awawezesha kuwaelewa viongozi walioko madarakani na kutii maelekezo yanayotolewa kwani hata vitabu vya dini vinaelekeza kutii mamlaka.

Amesema iwapo waumini watatii na kuzingatia mafundisho ya kiroho yanayotolewa na viongozi wao wa dini ni dhahiri kwamba yatajenga imani miongoni mwao na upendo utatawala katika jamii nzima.

Waziri Mkuu amesema Serikali itaendelea kushirikiana na Madhehebu yote katika kuwahudumia Watanzania wote bila ubaguzi, hivyo aliwasihi waendelee kuwekeza katika huduma za jamii ikiwemo Shule, Vyuo, Zahanati kwa kuwa wana jukumu la kushirikiana kwa pamoja kujenga taifa.

Wakati huo huo Waziri Mkuu aliwaomba wote kwa pamoja waunge mkono juhudi za Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli katika kupambana na uzembe, ubadhirifu na wote wanao kiuka maadili ya utendaji wa kazi.

Kwa upande wake Askofu Renatus Nkwande wa Jimbo la Bunda ambaye alikuwa msimamizi wa Kitume Jimbo Katoliki Geita amewaomba waumini kumpa ushirikiano Askofu mpya wa jimbo hilo.


IMETOLEWA NA OFISI YA WAZIRI MKUU
JUMAPILI, JUNI 12, 2016

WANAWAKE WA KANISA LA MORAVIAN MTONI KIJICHI KUFANYA MAOMBI MAKUBWA YA KUJIOMBEA NA TAIFA KWA UJUMLA

$
0
0

Wanawake wa Kanisa la Moravian Usharika wa Mtoni Kijichi wakiwa mbele ya kanisa lao Dar es Salaam leo asubuhi. Wanawake hao Julai 10 mwaka huu wanatarajia kufanya maombi ya kuwaombea wanawake wote nchini, familia zao pamoja na Taifa kwa ujumla.

Na Dotto Mwaibale

WANAWAKE wa Kanisa la Moravian Usharika wa Mtoni Kijichi wanarajia kufanya maombi makubwa kwa ajili ya wanawake nchini, familia zao pamoja na taifa kwa ujumla yenye lengo ya kumshuru mwenyezi mungu.

Akizungumza na mtandao wa www. habari za jamii.com Mratibu wa tukio hilo Mwalimu Mary Anyitike alisema lengo la maombi hayo ambayo ni rami ni kumshukuru mungu kwa kuzaliwa wanawake.

Anyitke alisema maombi hayo yatafanyika katika kanisa hilo Julai 10, mwaka huu saa tatu asubuhi ambapo aliwaomba wanawake wote bila ya kujali dini na madhehebu yao kujitokeza kushiriki maombi hayo ambayo yapo kwa ajili yao.

"Maombi haya ni muhimu kwetu na familia zetu na kauli mbiu yetu ni wanawake ni jeshi kubwa" alisema Anyitike.

Aliongeza kuwa katika maombi hayo kutakuwa na sadaka ya kumskuru mungu pamoja na changizo la upatikana wa fedha za ujenzi wa kanisa hilo katika usharika huo.

PROF. MBARAWA; ATOA MWEZI MMOJA DATA CENTRE IANZE KAZI

$
0
0
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akihakiki usahihi wa moja ya kifaa cha kupimia hali ya hewa katika ofisi za Mamlaka hiyo mkoani Singida. Kushoto ni Meneja wa Mamlaka ya Hali ya Hewa mkoani Singida Bw. Florian Rweyongeza. Mkurugenzi wa Kampuni ya Simu nchini (TTCL), Kanda ya Kaskazini Bw. Peter Lusama(wa tatu kulia), akitoa taarifa kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (wa pili kulia), kuhusu maendeleo ya ujenzi wa mkongo wa taifa mkoani Singida. Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Simu nchini (TTCL), Kanda ya Kaskazini Bw. Peter Lusama umuhimu wa kupitisha mkongo wa mawasiliano juu katika eneo la Msamvu linaloathiriwa na mafuriko mara kwa mara mkoani Singida. Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa TEHAMA kutoka sekta ya Mawasiliano Eng. Peter Mwasalyanda wakati akikagua kituo cha kutunza taarifa mbalimbali (data centre), jijini Dar es Salaam. Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akitizama kwa karibu mtambo wa kuratibu usalama katika kituo cha kutunza taarifa mbalimbali (data centre) jijini Dar es Salaam. Kituo hicho cha kwanza kujengwa nchini kitatunza taarifa za Serikali na sekta binafsi.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (wa tatu kulia), akitoa maelekezo kwa Meneja wa Kiwanja cha Ndege mkoani Singida (wa pili kulia), kuhusu mkakati wa Serikali wa ukarabati na upanuzi wa viwanja vya ndege kumi na moja ikiwemo kiwanja hicho cha Singida.Muonekano wa njia ya kurukia ndege katika Kiwanja cha Ndege cha Singida. Kiwanja hiki ni miongoni mwa viwanja vya ndege 11 ambavyo vipo katika mkakati wa Serikali wa kuviboresha. Mbunge wa jimbo la Singida Mjini Mhe. Mussa Sima (wa nne kulia), akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (wa pili kulia), wakati alipokagua kiwanja cha ndege cha Singida.   

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa ametoa mwezi mmoja kwa Katibu Mkuu wa Wizara anayeshughulikia Sekta ya Mawasiliano na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu nchini (TTCL), kuhakikisha kituo cha kutunzia taarifa (Data Centre) kilichopo Kijitonyama jijini Dar es Salaam kinaanza kufanya kazi.

Prof. Mbarawa ametoa agizo hilo kufuatia kukamilika kwa Data Centre hiyo miezi kadhaa iliyopita na mahitaji ya wadau wa huduma ya kutunza kumbukumbu za taasisi zao katika kituo hicho kuongezeka.

“Katibu Mkuu wa Sekta ya Mawasiliano na Mtendaji mkuu wa TTCL hakikisheni kituo hiki kilichojengwa kwa gharama kubwa kinaanza kutumika na kuwezesha mashirika na taasisi mbalimbali kutunza kumbukumbu zao na kuiletea Serikali mapato”, amesema Waziri Prof. Mbarawa.

Prof. Mbarawa amesema huduma ya mtandao katika kituo cha Data Centre imeimarishwa kutokana na kuunganishwa na Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano hivyo itawarahisishia wateja wake kuweka na kuchukua taarifa zao kwa haraka.

Akizungumza mara baada ya kukagua maeneo mbalimbali unapopita Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano Prof. Mbarawa amemtaka Mkurugenzi wa TTCL kanda ya Kaskazini Bw. Peter Lusama kuhakikisha Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano unapitishwa juu ya nyaya katika maeneo yenye changamoto za mafuriko ili kuepuka uharibifu wa mara kwa mara na usumbufu kwa watumiaji.

Aidha amezitaka taasisi za Serikali na binafsi kukitumia kituo cha kisasa cha kuhifadhi taarifa DATA CENTRE kutunza taarifa zao ili kuzihakikishia usalama na uhakika wa kuzitumia wakati wote, ambapo asilimia 75 imetengwa kwa ajili ya kutunza taarifa kutoka sekta binafsi na 25 itatunza taarifa za Serikali.

Kituo hicho ambacho ni cha kwanza kujengwa katika nchi za ukanda wa Afrika Mashariki na Kati ni fursa mpya kwa wafanyabiashara na wadau mbalimbali wenye taarifa nyingi kuzihifadhi na kuzitumia wanapozihitaji kinamilikiwa na Serikali na ujenzi wake umegharimu takribani dola za kimarekani milioni 93.

Katika hatua nyingine Prof. Mbarawa amekagua uwanja wa ndege wa Singida na mahali utakapojengwa uwanja mpya na kusisitiza umuhimu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini kusimamia kikamilifu ujenzi wa uwanja wa ndege wa sasa ambao upembuzi yakinifu wake umekamilika.

Amesema tayari Serikali imebainisha viwanja 11 vya ndege nchini kote na kuvifanyia upembuzi yakinifu kabla ya kuanza kuvijenga ili viweze kukidhi mahitaji ya soko.

Amevitaja viwanja hivyo kuwa ni Lake Manyara, Musoma, Iringa, Tanga, Songea, Kilwa Masoko, Lindi, Moshi, Njombe, Simiyu na Singida ambavyo vitapanuliwa na kujengwa kwa kiwango cha lami.

DC BAGAMOYO AMTUMBUA MWEKEZAJI MKOREA KWA KUMPOKONYA ARDHI NA KUIRUDISHA KWA WANANCHI

$
0
0




Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Majid Mwanga akizungumza na wananchi wa kijiji cha mwavi kata ta Fukayosi Wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani katika mkutano maalumu na kutatua sakata la mgogoro wa ardhi baina yao pamoja na mwekezaji Mkorea, ambaye amepokonywa hekari 131 na zimerudishwa kwa wananchi wenyewe.(PICHA NA VICTOR MASANGU)
Baadhi ya wawekezaji hao ambao ni wakorea wakiwa wanamsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo katika mkutano huo.

NA VICTOR MASANGU, BAGAMOYO 

SAKATA la mgogoro wa ardhi kwa wananchi wa kijiji cha mwavi kata ya Fukayosi kilichopo Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani na mwekezaji ambaye ni mkorea limechukua sura mpya baada ya mkuu wa Wilaya hiyo kuamua kuliingilia kati suala hilo kwa lego la kurudisha hali ya amani na utulivu pamoja na kumaliza tofauti zilizokuwepo. 

Mgogoro huo ambao umeonekana kuwa na mvutano mkubwa kutokana na mwekezaji huyo kupatiwa eneo lenye ukumbwa wa hekari 231 za serikali ya kijiji pasipo kuwashirikisha wananchi wenyewe kitu ambacho kilichangia kwa kiasi kikubwa kutoelewana kati ya wanakijiji na mwekezaji huyo. 

Akizungumzia kuhusina na sakata hilo Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Majid Mwanga alisema kwamba baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi hao aliamua kufanya uchunguzi wa kina na kubaini mwekezaji huyo alipewa eneo hilo kwa ajili ya uwekezaji,ambapo kwa sasa wamekubaliana naye hekari 131 zirudishwe kwa wananchi wenyewe na yeye abakiwe na hekari 100 tu. 

“Jamani wananchi wa kijiji cha mwavi mimi baada ya kuniletea malalamiko hayo nimeyafanyia kazi kwa kina kabisa ambapo nimekutana na mwekezaji huyo tumeongea naye juu ya suala hilo na amekubali kuzirudisha hekari 131za ardhi kwa wananchi nayeye atabakiwa na hekari 100 kwa ajili uwekezaji katika eneo hilo ambapo atajenga kituo cha kilimo, shule, zahanati pamoja na mambo mengine hivyo tuwe watulivu tumwone kama ataziendeleza kama tulivyokubaliana. 

Alisema kwamba serikali ya awamu ya tano ambayo inangozwa na Rais Dr John Pombe Magufuli itahakikisha kwamba inaleta mabadiliko chanya kwa kuzingatia usawa bila ya kuwa na uonevu wowote ule hasa katika masuala ya ardhi ambayo yameonekana kuwa ni changamoto kubwa katika Wilaya ya bagamoyo na maeneo mengine, na kuahidi kushirikiana nao mambo yote ya kimaendeleo. 

Aidha amepiga marufuku kwa wenyekiti wa vijiji na vitongoji vyote kutouza ardhi kiholela bila ya kuzingatia sheria na taratibu zilizowekwa na badala yake tabia hiyo waiche mara moja vinginevyo atawachukulia hataua kali za kisheri ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hiyo. 

“Hii tabia ya watendaji wetu kufanya jambo la kuuza ardhi bila kuzingatia sheria ni baya sana na ndio maana linatufukisha katika hatua kama hii ya kugombania ardhi na kusababisha migogoro sasa sitaki kuona hali hiyo, kwani huna mamlaka yoyote ya kuuza ardhi hata mita mbili kwa hiyo naomba hili lizingatiwe sitaki kuona migogoro ya ardhi katika Wilaya ya Bagamoyo, alisema Mwanga. 

Kwa upande wao wananchi wa kijiji hicho akiwemo Ramadhani Mfaume,Salum Hamad,Kulwa Ramadhani pamoja na Semeni Manga wakizungumza kwa nyakati tofauti katika mkutano huo wamesema kwamba walikuwa wanashindwa kufanya shughuli zozote za kimaendeleo kutokana na kuwepo kwa mgogoro huo wa ardhi baina yao na mwekezaji huyo. 

Walisema kwamba mwekezaji huyo alipewa eneo hilo tangu mwaka 1997 na baadhi ya watendaji wa kijiji kwa ajili ya uwekezaji lakini wanashangaa ameshindwa kuliendeleza kitu ambacho waliamua kwenda kutoa kilio chao kwa mkuu wa Wilaya kuhusiana na hekali hizo ambapo wanashukuru ameweza kulishughulikia suala hilo na kufanikiwa kuzirudisha hekari 131 za kijiji. 

“Kwa weli sisi kama wananchi wa kijiji cha mwavi tulikuwa katika hali ya mvutano mkubwa wa siku nyine na mwekezaji huyo ambaye ni mkorea, juu ya kutuchukulia ardhi yetu lakini tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa Mkuu wetu wa Wilaya kuweza kulitatua suala hilo ambalo lilikuwa inatumbumbua kwa muda mrefu, walisema wanakijiji hao. 

Pia waliongeza kuwa kurudishwa kwa hekari hizo 131 zitaweza kuwapa fursa ya kuweza kufanya shughuli mbali za kimaendeleo ikiwemo kujenga ujenzi wa shule kwa ajili ya watoto wao,masoko, pamoja na zahanati kwani hapo awali walikuwa hawana huduma za karibu katika kijiji hicho. 

Pia mwandishi wa habari hizi iliweza kupata fursa ya kuzungumza na mmwekezaji huyo ambaye ni Mkorea anayejulikana kwa jina la Yum Yun Hwa ambapo alisema kwamba lengo lake kubwa la kuchukua eneo hilo ni kwa ajili ya kuwasaidia wananchi wa eneo hilo kwa kuweka viwanda, shule, zahanati pamoja na kuanzsiha kituo maalumu cha kilimo. 

Yum hwa alibainisha kwamba katika kuunga juhudi za serikali ya Tanzania katika kuendeeza kilimo cha kisasa amepanga kuwaleta wataalamu kutoka nchini korea ambapo watakuja katika kituo hicho kwa ajili ya kufundisha masuala mbali mbali ya kilimo, na kuongeza kuwa tayari wameshafanya ununuzi wa vifaa ikiwemo matrekta,Power tila ambayo yatakuwa kwa ajili ya shughuli za kilimo. 

Kijiji hicho cha mwavi kilichopo kata ya Fukayosi Wilayani Bagamoyo kiliingia katika mgogoro wa ardhi na mwekezaji huyo tangu mwaka 1997, ambapo kutokana na juhudi zilizofanywa na Mkuu wa Wiaya ya Bgamoyo kuamua kuingilia katia sakata hili kumeweza kusaidia kutokana na mwekezaji huyo kukubali kuwarudhishia ardhi yao wananchi yenye ukumbwa wa hekari 131.

ZAIDI YA DOLA ZA KIMAREKANI MILIONI 36 ZIMETUMIKA KATIKA KUFIKISHA HUDUMA ZA MAWASILIANO YA SIMU KATIKA MAENEO YA VIJIJINI

$
0
0

Na: Frank Shija,MAELEZO

Zaidi ya dola za kimarekani milioni 36 zimetumika katika kufikisha huduma za mawasiliano ya simu katika maeneo ya vijijini yasiyo na mvuto wa kibiashara nchini.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Idara ya Uendeshaji wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Albert Richard wakati wa maonyesho ya SIMU EXPO 2016 leo jijini Dar es Salaam.

Mfuko wa Mawasiliano kwa wote unashiriki maonyesho hayo ili kutoa elimu kwa umma juu ya shughuli mbalimbali zinazofanywa na mfuko huo.

Albert amesema kuwa kazi kubwa ya Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote ni kufikisha huduma za mawasiliano ya simu katika maeneo yote ya vijini yasiyo na mvuto wa kibiashara ambapo makampuni ya simu yanasuasua kupeleka huduma hiyo.

“Sisi kama Taasisi ya Serikali kazi yetu kubwa ni kufikisha huduma za mawasiliano katika maeneo yote ya vijini ambayo makampuni binafsi yanasuasua kupeleka huduma kutokana na msukumo wa kibiashara.” Alisema Albert.

Aliongeza kuwa mradi wa kwanza uliotekelezwa na mfuko huo umegharimu takribani Dola za Kimarekani milioni 5.8 ambapo jumla ya Kata 52 zimenufaika na mradi huu kwa kuunganishwa na huduma za mawasiliano ya simuK.

Pamoja na jitihada za Serikali kuhakikisha kuwa wananchi wote wanapata huduma za mawasiliano ya simu kumekuwa na changamoto katika kutekeleza azma hiyo kwa wakati kutokana na ufinyi wa bajeti na kukosekana kwa miundombinu rafiki kama vile Barabara na Umeme.

Kutokana na changamaoto hizo Albert ametoa rai kwa jamii kuwa na subira wakati utekelezaji wa miradi ya kupeleka huduma za mawasiliano ya simu katika maeneo yao ukiendela hatua kwa hatua kadri fedha zinavyopatikana.

Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) ni Taasisi ya Serikali iliyoanzishwa mwaka 2006 kwa lengo la kupeleka na kufanikisha mmawasiliano kwa wananchi waishio katika maeneo machache ya mijini na maeneo mengi ya vijijini yasiyo na mvuto wa kibiashara kwa watoa huduma ya mawasiliano.
Mkuu wa Idara ya Uendeshaji wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Albert Richard akimuonyesha ramani inayoonyesha maeneo ambayo mfuko umetekeleza miradi ya kupeleka huduma za mawasiliano baadhi ya wa wananchi waliotembelea banda la mfuko huo katika maonyesho ya SIMU EXPO leo jijini Dar es Salaam. Mkuu wa Idara ya Uendeshaji wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Albert Richard akiwaelezea jambo baadhi ya wa es Salaam wananchi waliotembelea banda la mfuko huo katika maonyesho ya SIMU EXPO . Mwanasheria wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Ambokile Mwakaje (Kulia) akimuelekeza baadhi ya maeneo walipotekeleza miradi ya huduma za mawasiliano mmoja wa mwananchi aliyetembelea banda la mfuko huo katika maonyesho ya SIMU EXPO. Afisa Uendeshaji wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Edwin Makala akiwaelezea jambo baadhi ya wa es Salaam wananchi waliotembelea banda la mfuko huo katika maonyesho ya SIMU EXPO. Mkuu wa Idara ya Uendeshaji wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Albert Richard akiwaelezea jambo baadhi ya wa es Salaam wananchi waliotembelea banda la mfuko huo katika maonyesho ya SIMU EXPO. Baadhi ya wananchi wakiwa katika banda la Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) wakati wa maonyesho ya SIMU EXPO 2016 leo jijini Dar es Salaam. Picha zote na Frank Shija
 

SHIRIKA LA BIMA LA TAIFA (NIC) LAWAPIGA MSASA MAWAKALA WAKE

$
0
0
Bi. Rose Lutu Lawa Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Bima la Taifa NIC akizungumza na Mawakala wa bima ya Ajali na Mali wakati wa mafunzo ya mawakala hao katika kutoa huduma bora kwa wateja na mikakati ya kuuza bidhaa za shirika hilo kwa ufanisi mafunzo hao yalifanyika mwishoni mwa wiki kwenye makao makuu ya shirika hilo jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na baadhi ya watendaji kutoka vitengo kadhaa ambao pia walitoa mada kadhaa katika kuboresha huduma za shirika la Bima.Bi. Rose Lutu Lawa Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Bima la Taifa NIC akifafanua jambo kwa Mawakala wa bima ya Ajali na Mali wakati wa mafunzohayo yaliyofanyika kwenye makao makuu ya shirika la Bima la Taifa NIC jijini Dar es salaam.Baadhi ya washiriki wakiwa katika mafunzo hayo wakifuatilia kwa makini maelezo ya Bi Rose Lutu Kaimu Mkurugenzi wa NIC.
Mafunzo yakiendelea.
Kaimu Mkurugenzi wa MasokoElisante Maleko akimuelekeza jambo kwenye ratiba Bi. Tabu Kingu Kaimu Mhasibu Mkuu wa shirika la Bima la Taifa NIC ambaye pia alikuwa mtoa mada katika mafunzo hayo.Bi. Tabu Kingu Kaimu Mhasibu Mkuu wa shirika la Bima la Taifa NIC ambaye pia alikuwa mtoa mada katika mafunzo hayo akiandika mambo muimu yaliyokuwa yakijadiliwa katika mafunzo hayo.Kaimu Mkurugenzi wa MasokoElisante Maleko kulia akiwa pamoja na baadhi ya wakuu wa vitengo wa shirika hilo wakati mafunzo hayo yakiendelea.

NAIBU WAZIRI LUHANGA MPINA AWAASA WASOMI KWENYE TAMASHA LA AJIRA NA UJASIRIAMALI

$
0
0
Mgeni Rasmi Tamasha la Ajira na Ujasiriamali Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano Mh Luhanga Mpina Akikagua Maonyesho ya Kazi Mbalimbali Kwenye Tamasha la Ajira na Ujasiriamali Lililofanyika Chuo Kikuu Mzumbe Mkoani Mbeya.
Katika kutengeneza Msingi Mzuri kwa Wanafunzi wake na kuwajengea uwezo Chuo Kikuu cha Mzumbe kampasi ya Mbeya kilifanya maonyesho makubwa ya Ajira na Ujasiriamali siku yatarehe 11 June 2015 mjini Mbeya. Tukio hilo la aina yake, pia lilishirikisha wanafunzi wa vyuo wingine vya nyanda za juu kusini.
Afisa Mtendaji Mkuu waEAG group Imani Kajula Akitoa Mada kwenye Tamasha La Ajira na Ujasiriamali Lililofanyika Mkoani Mbeya
Upatikanaji wa ajira za uhakika imekuwa changamoto kubwa sana kwa vijana wengi wanaomaliza vyuo Nchini Tanzania hivyo ujasiriamali ni njia moja muhimu ya kutatua changamoto hiyo.Wanafunzi wengi walioshiriki walieleza Furaha yao kwa Maonyesho hayo. Mgeni rasmi Mh.Mpina aliwataka Wanafunzi kutumia fursa zilizopo kujiletea Maendeleo na kujiajiri.
Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji Clouds Media Group Ruge Mutahaba  Ambaye naye alitoa Mada Mbalimbali Namna ya Kukabiliana na Changamoto ya Ajira Hapa Nchini
Katika kufanikisha siku hiyo wataalam na wabobeaji wa biashara na fursa za ajira walialikwa kutoa mada na kushare uzoefu wao kwenye ujasiriamali na utendaji kazini. Watoa mada walio alikwa kwenye kongamano hili kubwani; 

Imani Kajula ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa EAG Group, Ruge Mutahaba ambaye ni Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji Clouds Media Group. Wakili Alberto Msando – Wakili maarufu wa kujitegemea na Mjasiriamali, Victor Kikoti Compliance Manager – LAPF na Ephraim Lwila – Meneja wa Tawi la CRDB Mbeya. Mgeni Rasmi wa Kongamano hilo alikuwa Naibu Waziri wa Mazingira na Muungano Mh.Luhaga Mpina.
Washiriki wa Tamasha Hilo wakisikiliza Kwa Makini Mada Mbalimbali Zilizowasilishwa  Kwenye Tamasha la Ajira na Ujasiriamali Lililofanyika Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Mbeya
Pia katika kuhitimisha siku hiyo, Timu za wanafunzi wa Mzumbe Mbeya na TIA Mbeya walicheza Mechi ya mpira wa miguu, ambapo chuo cha Mzumbe kiliifunga TIA kwanjia ya penati. Mkurugenzi wa EAG Group Imani Kajula alikabidhi zawadi kwa timu zote mbili.
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live




Latest Images