Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 876 | 877 | (Page 878) | 879 | 880 | .... | 1903 | newer

  0 0

   Mbunge wa Momba (CHADEMA), David Silinde akizungumza na waandishi wa habari kuelezea msimamo wa kambi rasmi ya upinzani bungeni kuhusu bajeti kuu ya Serikali ya mwaka 2016/17. Katikati ni Mbunge wa Vunjo, James Mbatia na Mbunge wa Viti Maalum (CUF), Riziki Mngwali.
   Mbunge wa Vunjo (NCCR- Mageuzi), James Mbatia akizungumza na waandishi wa habari kuelezea msimamo wa kambi rasmi ya upinzani bungeni kuhusu bajeti kuu ya Serikali ya mwaka 2016/17. Kushoto ni Mbunge wa Momba (CHADEMA), David Silinde na Mbunge wa Viti Maalum (CUF), Riziki Mngwali.(PICHA NA ISMAIL NGAYONGA- MAELEZO)

  Na Jonas Kamaleki-MaelezoDodoma


  KAMBI rasmi ya Upinzani Bungeni  imemuunga mkono Rais, Dkt. John Pombe Magufuli katika juhudi zake za kupunguza matumizi yasiyo ya lazima na kuelekeza fedha hizo katika miradi ya maendeleo na huduma za jamii kama ujenzi wa miundombinu ya barabara na reli.

  Pongezi hizo zimetolewa leo mjini Dodoma na Mbunge wa Momba (CHADEMA), David Silinde wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya  maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani kuhusu bajeti kuu ya Serikali ya mwaka 2016/17.

  “Tunamuunga mkono Mhe. Rais John Pombe Magufuli kwa kuondoa posho za vikao (Sitting Allowances) na tunamwomba aondoe posho hizo kwa wabunge nao watumie mishahara yao ili kuwe na usawa,” alisema Silinde.

  Silinde alisema kuwa Kambi Rasmi ya Upinzani inaunga mkono juhudi za Mhe Rais Magufuli za kukusanya kodi ambayo inabidi ielekezwe kwenye miradi ya maendeleo na huduma za kijamii.

  “Tunaungana na Serikali kukata kodi kwenye kiinua mgongo cha wabunge lakini tunamuomba Mheshimiwa Rais apanue wigo wa kodi hiyo hadi kwa wakuu wa Mikoa na Wilaya,” alisema Silinde.

  Kwa upande wake, mbunge wa Jimbo la Vunjo (NCCR-Mageuzi), Mhe. James Mbatia amesema kuwa Kambi Rasmi ya Upinzani inamuomba Mhe. Rais Magufuli kufuta posho za vikao kwa wabunge haraka ili kuleta usawa kwa watanzania wote.

  0 0

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Jaji Shaaban Ali Lila kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani Ikulu jijini Dar es Salaam.

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Jaji Ferdinand Leons Katipwa Wambali kuwa Jaji Kiongozi, Ikulu Jijini Dar es Salaam.


   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Jaji wa Mahakama ya Rufani Jaji Shaaban Ali Lila(kushoto) pamoja na Jaji kiongozi Jaji Ferdinand Leons Katipwa Wambali, wengine katika picha ni Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Jaji mkuu wa Tanzania Mohamed Chande Othmani mara baada ya tukio la uapisho wa Majaji hao Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Jaji wa Mahakama ya Rufani Jaji Shaaban Ali Lila(kushoto) pamoja na Jaji kiongozi Jaji Ferdinand Leons Katipwa Wambali, wengine katika picha ni Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Jaji mkuu wa Tanzania Mohamed Chande Othmani pamoja na Majaji mbalimbali wa Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufani Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Balozi wa Oman hapa nchini Soud Al Ruqaishi ambaye anamaliza muda wake wa kufanya kazi hapa nchini Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Picha na IKULU.  0 0

  Mbunge wa Chemba (CCM) (katikati) na Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Martha Mlata wakifurahia jambo mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa asubuhi wa kikao cha Bunge linaloendelea mjini Dodoma. Naibu Spika, Mhe Dkt. Tulia Ackson akibadilishana mawazo na Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mhe. Amina Iddy mara baada ya kumalizika kwa kikao cha asubuhi cha Bunge hilo leo mjini Dodoma. 
  Wabunge wa CCM Mhe. Asha Abdallah Juma (Viti Maalum) na Emmanuel Mwakasaka (Tabora Mjini) wakiingia katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma kuanza vipindi vya asubuhi vya Biunge hilo leo vinavyoendelea mjini Dodoma. Nyuma ni Mbunge wa Vunjo, Mhe. James Mbatia (NCCR Mageuzi).  
  Wabunge wa CCM, Mhe. Hawa Mchafu Viti (Maalum) na Joseph Madaba (Madaba) wakiingia katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma kuanza vipindi vya asubuhi vya Biunge hilo leo vinavyoendelea mjini Dodoma.  
  Mbunge wa Hanang’ Mhe. Mary Nagu akiingia katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma kuanza vipindi vya asubuhi vya Biunge hilo leo vinavyoendelea mjini Dodoma.  
  Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Angelina Mabulla na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani wakiingia katika katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma kuanza vipindi vya asubuhi vya Biunge hilo leo vinavyoendelea mjini Dodoma. Wanafunzi wa shule ya Msingi ya Kawekamo Montesori kutoka Jijini Mwanza wakifuatilia mjadala wa vikao vya Bunge vinavyoendelea mjini Dodoma.
   

  (PICHA NA ISMAIL NGAYONGA- MAELEZO)

  0 0

   Mwanamuziki nguli wa nchini Marekani na jaji mkuu wa shindano la Airtel Trace Music Stars, Keri Hilson akiongea wakati wa mkutano na waandishi wa habari ulifanyika lagos nchini Nigeria
   Mwanamuziki nguli wa nchini Marekani na jaji mkuu wa shindano la Airtel Trace Music Stars, Keri Hilson akiongea wakati wa mkutano na waandishi wa habari ulifanyika lagos nchini Nigeria. Akishuhudia ni Mkurugenzi wa Masoko Airtel Afrika, Dia Ezzaoudi
   Mshindi wa Airtel Trace Music Stars Afrika 2015, Nalimi Mayunga akiongea wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Lagos nchini Nigeria. 
   Mwanamuziki nguli wa nchini Marekani na jaji mkuu wa shindano la Airtel Trace Music Stars, Keri Hilson akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza mkutano na waandishi wa habari
   Mwanamuziki nguli wa nchini Marekani na jaji mkuu wa shindano la Airtel Trace Music Stars, Keri Hilson akiwa katika picha  pamoja na Mshindi wa Airtel Trace Music Stars Afrika 2015, Nalimi Mayunga
  Wafanyakazi wa Airtel kutoka nchi mbalimbali wakiwa katika picha pamoja na Mwanamuziki nguli wa nchini Marekani na jaji mkuu wa shindano la Airtel Trace Music Stars, Keri Hilson mara baada ya kumaliza mkutano na waandishi wa habari. Pichani (wa pili kushot) Afisa uhusiano wa Airtel Tanzania , Bi Jane Matinde

  Mwanamuziki nguli nchini Marekani, Keri Hilson ameingi nchini Nigeria ili kushiriki  katika shindano la Airtel Trace Music Stars Afrika linaloshirikisha nchi 9 barani Afrika ambapo Tanzania inawakilishwa na mwanadada Melisa John.

  Keri Hilson atashirikiana pamoja na majaji wengine katika kumtafuta mshindi wa Airtel Trace Music Stars Afrika kwa mwaka 2016. Ambapo Taji la ushindi wa Airtel Trace Music Stars 2015 linashikiliwa na Nalimi Mayunga kutoka Tanzania

  Siku moja baada ya kuwasili , Keri Hilson ameshiriki katika mkutano na waandishi wa habari ambapo alihainisha kuvutiwa kwake na washiriki na kukiri kwamba bara la Afrika lina  vipaji vingi vya muziki na kuwapongeza Airtel na Trace kwa kuanzisha mpango huu wenye lengo la kuinua vipaji na kuwawezesha vijana kufikia ndoto zao

  “ naamini fainali itakuwa na mvuto sana nimekutana na washiriki  na kushuhudia vipaji vya kutosha.  Mambo makuu tutakayoangali wakati wa  fainali ni pamoja na  uwezo wa mshiriki kuweza kutoa burdani , uwezo wa sauti yake na jinsi gani anaweza kutoa burdani kwa mashabiki. Naamini mashindano ya kesho yatakuwa na mvuto na nimejiandaa vyema kufanya kazi na mshiriki atakayeshinda kwa mwaka huu”

  0 0

  Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge akifungua koki ya maji katika mradi wa maji wa Chiruku Wilayani Chemba. nyuma ni Mbunge wa Chemba Alhaji Juma Nkamia.
  Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Lwenge akimtwisha ndoo ya maji Rawiya Hassani mkazi wa Chiruku.
  Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Lwenge akikagua moja ya matanki ya maji katika mradi wa maji wa Ntomoko Wilayani Chemba.
  Waziri wa Maji na Umwagiliaji akiongea na wakazi wa Itolwa Wilayani Chemba kabla ya kuhitimisha ziara yake katika wilaya hiyo.


  Na Athumani Shariff;

  Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge ametaka watendaji wa Halmashauri nchini kuwashtaki watu wanaohujumu miundombinu ya maji kama wahujumu uchumi.

  Hayo aliyasema leo alipofanya ziara katika kijiji cha Bumila kata ya Lupeta Halmashauri ya Mpwapwa baada ya kupokea taarifa ya hali ya huduma ya maji katika kijiji hicho.

  “Naagiza Halmashauri muwatafute watu wote waliohujumu miundombinu ya maji na washitakiwe kama wahujumu uchumi, hatuwezi kuwaachia watu wanaosababisha wananchi wasio na hatia kukosa huduma muhimu ya maji”

  Miundombinu ya maji katika kijiji cha Bumila imehujumiwa kwa mabomba zaidi ya 40 ya nchi 2 yenye urefu wa mita 6 kwa kila kipande cha bomba kung’olewa na hatimaye maji kutokuwafikia wananchi. 

  Katika hali ya kulikabili tatizo la maji katika kijiji hicho Mhandisi Lwenge ameiagiza Halmashauri ya Mpwapwa kuchimba kisima katika kijiji cha Bumila haraka ili kuwaondolea adha wananchi wa kijiji hicho.

  Katika hatua nyingine Waziri Lwenge amewataka viongozi na watendaji wote nchini kushughulikia maswala ya maji badala ya kuachiwa yeye Waziri wa Maji peke yake.

  “Kila mmoja wetu kwa nafasi yake ana jukumu la kufatilia maswala haya sio ya waziri wa maji peke yake, Wilayani mkishindwa mpeleke Mkoani nao wakishindwa wataleta Wizarani nasi tukishindwa tutapeleka kwa Magufuli kitu ambacho sitegemei” Alisema Waziri Lwenge.

  Akiwa Wilayani Chemba, Waziri Lwenge amekataza tabia ya baadhi ya vijiji, kata na jamii za watu wanao wabagua jamii nyingine katika miradi ya maji. Akiwa wilayani humo Lwenge aliagiza kuwa miradi yote ya maji ni mali ya serikali hivyo jamii zote bila kujali mipaka ya kijiografia kupata huduma hiyo.

  “Maji yote ni mali ya serikali, hamna mtu wala kikundi cha mtu chenye kumiliki maji, hivyo hairuhusiwi kwa mtu au kikundi cha watu kujimilikisha maji na kubagua baadhi ya jamii ya watu wengine wasipate maj, sisi sote ni watanzania”. Alisema Waziri Lwenge.

  Ziara ya Waziri Lwenge ilianza katika Halmashauri za Chemba na Kondoa na kuishia katika halmashauri ya Mpwapwa ikiwa ni ahadi aliyoitoa bungeni kwa mbunge wa Chemba Juma Nkamia na Mpwapwa George Lubeleje.

  0 0


  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akiwasili Kituo cha Polisi Runzewe kilichopo Kata ya Uyovu wilayani Bukombe ambacho Mbunge wa Jimbo hilo, Dotto Biteko aliuliza swali la nyongeza Bungeni hivi karibuni akisema kituo hicho kinahitaji matengenezo makubwa na kumuomba Naibu Waziri huyo kufanya ziara jimboni kwake kujionea kituo hicho. Hata hivyo, Masauni alisema Serikali yake itahakikisha kituo hicho kitakuwa katika hali nzuri.

  Mkuu wa Kituo cha Polisi Runzewe kilichopo Kata ya Uyovu wilayani Bukombe, Jackson Kirahuka akimuonyesha Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto aliyevaa koti) sehemu mbalimbali za kituo hicho ambacho Mbunge wa Jimbo la Bukombe, Dotto Biteko (katikati) aliuliza swali la nyongeza Bungeni hivi karibuni akisema kituo hicho kinahitaji matengenezo makubwa na kumuomba Naibu Waziri huyo kufanya ziara jimboni kwake kujionea kituo hicho. Hata hivyo, Masauni alisema Serikali yake itahakikisha kituo hicho kitakuwa katika hali nzuri. Aliyevaa Kaunda suti ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Amani Mwenegoha.

  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wa pili kushoto) akizungumza jambo na Mkuu wa Mkoa wa Geita, Meja Jenerali, Mstaafu Ezekiel Kyunga (meza kuu), Mbunge wa Jimbo la Geita Vijijini, Joseph Msukuma (kulia), na Mkuu wa Jeshi la Polisi mkoani humo, Mponjoli Mwabulambo, wakati Naibu Waziri huyo alipofanya ziara ya kikazi mkoani humo.

  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akimfafanulia jambo Mbunge wa Jimbo la Geita Vijijini, Joseph Msukuma (watatu kulia), na Mkuu wa Jeshi la Polisi mkoani humo, Mponjoli Mwabulambo (wapili kushoto), wakati Naibu Waziri huyo alipofanya ziara ya kikazi mkoani humo. 


  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na mamia ya wananchi wa Kijiji cha Nyakabale, Kata ya Mgusu, mkoani Geita ambao ni majirani wa Kampuni ya Uchimbaji wa Dhahabu ya GGM mkoani humo. Wananchi hao wamelalamika kuwepo na vitendo vya ukatili dhidi yao vinavyofanywa na baadhi wa askari wa kampuni hiyo. Hata hivyo Mhandisi Masauni aliwataka Polisi mkoani humo kufanya uchunguzi wa haraka dhidi ya tuhuma hizo.

  Mkazi wa Kijiji cha Nyakabale, Kata ya Mgusu, mkoani Geita, Biosi Makongoro akitoa kero yake kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto aliyekaa) dhidi ya Kampuni ya Uchimbaji wa Dhahabu ya GGM mkoani humo ambayo ipo jirani na kijiji hicho, kuwa askari wa kampuni hiyo wanadaiwa kuwanyanyasa wananchi hao wanapopita katika eneo la Kampuni hiyo. Hata hivyo Mhandisi Masauni aliwataka Polisi mkoani humo kufanya uchunguzi wa haraka dhidi ya tuhuma hizo.

  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akitoka ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bukendo, Amani Mwenegoha (kushoto) mara baada ya kumaliza kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya hiyo iliyopo mkoani Geita. Naibu Waziri alifanya ziara ya kikazi mkoani Geita. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

  0 0


  0 0

  WANAFUNZI wa chuo cha kodi(TRA) waaswa kutoa elimu ya maswala mbalimbali ya kodi kwa vijana wenzao ili kujifunza na kukuza uelewa wa kulipa kodi kwa hiyari.

  Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Elimu na Huduma kwa Mlipa Kodi, Richard Kayombo wakati wa ufunguzi wa Jumuiya ya wanafunzi wa kodi vyuoni jijini Dar es Salaam leo. Amesema kuwa vijana wapewe elimu ya kulipa kodi kwa hiyari mapema ili kipindi watakapoanza kupata mapato waweze kulipa kodi bila kushurtishwa.

  Amesema kuwa Jumuiya ya wanafunzi wa kodi vyuoni iliyofunguliwa leo iwe taa kwa jamii nzima na wanachama wa jumuiya hiyo waweze kutoa elimu ya kodi watakayoipata kwa wenzao ndani na nje ya mazingira ya chuo.

  Kutoka kushoto ni Rais wa serikali ya wanafunzi wa chuo cha Kodi(TRA)-ITA, Juma Nadhiru, Mkuu wa huduma za wanafunzi  wa chuo cha kodi- ITA, Rashid Mzava, Mkurugenzi wa Elimu na Huduma kwa Mlipa Kodi wa TRA, Richard Kayombo , Meneja huduma kwa mlipa kodi wa TRA, Honesta Ndunguru na Afisa Huduma na Elimu kwa Mlipa kodi TRA, Julieth Shehiza wakiwa katika ufunguzi wa Jumuiya ya wanafunzi wa Kodi vyuoni katika chuo cha Kodi jijini Dar es Salaam.


  Mkurugenzi wa Elimu na Huduma kwa Mlipa Kodi, Richard Kayombo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa ufunguzi wa Jumuiya ya wanafunzi wa Kodi vyuoni katika chuo cha Kodi jijini Dar es Salaam.
  Mkuu wa huduma za wanafunzi  wa chuo cha kodi- ITA, Rashid Mzava akizungumza na wanafunzi wa chuo cha kodi jijini Dar es Salaam leo wakati wa ufunguzi wa wakati wa ufunguzi wa Jumuiya ya wanafunzi wa Kodi vyuoni katika chuo cha Kodi.
  Rais wa serikali ya wanafunzi wa chuo cha Kodi(TRA)-ITA, Juma Nadhiru (Aliyesimamama) akizungumza na wanafunzi wa chuo cha kodi wakati wa ufunguzi wa Jumuiya ya wanafunzi wa Kodi vyuoni katika chuo cha Kodi jijini Dar es Salaam leo, Pia amemshukuru mgeni rasmi kwa kufika katika chuo chao na kuwahamasisha wanafunzi wa chuo hicho kujifunza zaidi katika kuhamasisha jamii kulipa kodi kwa hiyari. Kaliokaa kutoka kushoto ni Mkuu wa huduma za wanafunzi  wa chuo cha kodi- ITA, Rashid Mzava, Mkurugenzi wa Elimu na Huduma kwa Mlipa Kodi wa TRA, Richard Kayombo , Meneja huduma kwa mlipa kodi wa TRA, Honesta Ndunguru na Afisa Huduma na Elimu kwa Mlipa kodi TRA, Julieth Shehiza.

   Afisa Mahusiano wa chuo cha kodi (TRA), Rachel Mkundai akiwakaribisha na kuwatambulisha wageni waalikwa katika ufunguzi wa Jumuiya ya wanafunzi wa Kodi vyuoni katika chuo cha Kodi jijini Dar es Salaam leo.
   Wanafunzi wa chuo cha kodi(TRA) wakiwa katika ufunguzi wa Jumuiya ya wanafunzi wa Kodi vyuoni katika chuo cha Kodi jijini Dar es Salaam leo.
  Mwanafunzi wa chuo cha kodi (TRA), Busenene Malkia akichangia maada mbele ya mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa Jumuiya ya wanafunzi wa Kodi vyuoni katika chuo cha Kodi jijini Dar es Salaam leo.

  0 0

  MKO8 
  Waziri Mkuu Kassim Majliwa akizungumza na waalikwa   katika futari  aliyoiandaa kwenye makazi yake jijini Dar es salaam Juni 10, 2016.

  MKO6 
  Mke wa Waziri Mkuu,  Mary  Majaliwa  akiwa na baadhi ya  waalikwa  katika  futari ilyoandaliwa na  Waziri Mkuu, kwenye makazi yake  jijini Dar es salaam  Juni 10, 2016.  Wapili kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema. (Picha na Ofisi ya Waziri  Mkuu)
  MKO7Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi CCM akishiriki pamoja na waalikwa wengine katika futari hiyo iliyoandaliwa kwenye makazi ya Waziri mkuu.
  MKO3 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akisalimiana na baadhi ya waalikwa waliohudhuria futari aliyoiandaa kwenye makazi yake jiji Dar es salaam  10, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  MKO4 
   Waziri Mkuu,  Mh Kassim Majaliwa  akisalimiana na baadhi ya waalikwa walioshiriki katika futari  iliyoandaliwa na  Waziri Mkuu kwenye Makazi  yake jijini Dar es salaam Juni 10, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  MKO5 
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa pamoja na baadhi ya  waalikwa  wakishiriki katika  swala ya jioni kabla ya futari  iliyoandaliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwenye makazi yake  jijini Dar es salaam Juni 10, 2016.
  MKO9 
  Waziri Mkuu Kassim Majliwa akisalimiana na  Bw. Seif Ali Seif   katika futari  aliyoiandaa kwenye makazi yake jijini Dar es salaam Juni 10, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  MKO10 
  Waziri Mkuu Kassim Majliwa akisalimiana na  Mh. Raymond Mushi Mkuu wa wilaya ya Ilala  katika futari  aliyoiandaa kwenye makazi yake jijini Dar es salaam Juni 10, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  MKO11 
  Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na wanawake walioshiriki katika futari aliyoiandaa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwenye makazi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Juni 10, 2016. Kulia  kwake  ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke Sophia Mjema. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  MAJ5 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mwenyekiti wa Jumuiya  ya Wazazi Tanzania , Abdallah Buelembo katika futari aliyoiandaa kwenye makazi yake  jijini Dar es salaam Juni 10, 2016. (Picha na Ofisi  ya Waziri Mkuu)
  MAJ1 
  Mke wa Waziri Mkuu, Mary Majaliwa akisalimiana na Mke wa Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Dar es salaam Azalina Madabida katika futari aliyoiandaa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwenye Makazi yake jijini Dar es salaam Juni 10, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  MAJ2 
  Mke wa Waziri Mkuu, Mary Majaliwa (kushoto) akisalimiana na  Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema  katika futari aliyoiandaa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwenye makazi yake jijini Dares salaam Juni 10, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  MAJ3 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Happi  (kushoto) na Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es salaam , Simon Siro katika futari  aliyoiandaa kwenye makazi yake jijini Dar es salaam Juni 10, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  MAJ4 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Kamanda  wa Kanda Maalum  ya  Dar es salaam , Simon Siro  katika futari aliyoiandaa kwenye Makazi yake  jijini  Dar es salaam Juni 10, 2016.  Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Happi (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  MKO1 
  Waziri Mkuum Kassim  Majaliwa akisalimiana  na Katibu Kamati ya Amani ya Viongozi wa Dini ya mkoa wa Dar es salaam, Padri John Solomon wa Kanisa la Anglikani (kulia) na Mwenyekiti wa Kamati  hiyo, Sheikh wa Mkoa wa Dar es salaam , AlhajiMussa Salum katika Futari iliyoandaliwa na Waziri Mkuu kwenye makazi yake jijini Dar es salaam Juni10, 2016.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  MKO2 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akisalimiana na baadhi ya waalikwa waliohudhuria futari aliyoiandaa kwenye makazi yake jiji Dar es salaam  10, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


  0 0


  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewahakikishia Watanzania kwamba Serikali inaendelea na jitihada za kuondoa tatizo la uhaba wa sukari nchini ambapo jumla ya tani 20,000 zilisambazwa jana katika maeneo mbalimbali nchini.

  Amesema shehena nyingine ya tani 35,000 inatarajiwa kusambazwa hivi karibuni katika kanda zote nchini hivyo amewataka wafanyabiashara watakapoipokea kuiuza kwa wananchi bila ya kuificha na bei isizidi shilingi 2,200.

  Waziri Mkuu Majaliwa ameyasema hayo jana jioni ( Ijumaa, Juni 10, 2016) wakati akizungumza na Masheikh na Viongozi wa Kamati ya Amani ya mkoa wa Dar es Salaam alipowaalika katika futari aliyoiandaa nyumbani kwake.

  Amesema tayari viwanda vimeanza kufunguliwa na tani 300 zilizotoka katika kiwanda cha Sukari cha Kagera zitasambazwa katika wilaya za Kakonko, Kibondo, Kasulu, Uvinza na Kigoma ili kutosheleza maeneo hayo.

  Hata hivyo amewataka Maofisa Biashara katika Halmashauri zote nchini kuendelea kufanya ufuatiliaji katika maduka ili kuhakikisha bidhaa hiyo inapatikana na hakuna mfanyabiashara atakayeificha.

  Katika hatua nyingine Waziri Mkuu aliwataka wafanyabiashara kote nchini kutopandisha bei za vyakula katika kipindi cha mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

  Akizungumza kuhusu tabia za baadhi ya wafanyabiashara wanaopandisha bei za bidhaa hasa vyakula katika kipindi hiki cha mfungo amewataka kumuogopa Mwenyezi Mungu kwa sababu kitendo hicho kinawapa wafungaji wakati mgumu.

  “Kufunga Ramadhani si jambo la anasa, si matashi binafsi bali ni jambo la kiimani hivyo tusipandishe bei ya bidhaa kwa lengo la kuwaadhibu Waislam kwa sababu tu wamefunga.

  “Katika Quran surat Baqarah aya ya 183 inasema kwamba enyi mlioamin imefaradhishwa kwenu kufunga kama walivyoamrishwa kufunga kwa waliopita kabla yenu ili muwe wachamungu, hivyo hatuna budi kufunga” alisisitiza.

  Alisema tabia hiyo si nzuri na imekuwa ikijitokeza mara kwa mara unapofika wakati wa mfungo kwa wafanyabiashara kuamua kupandisha bei hivyo aliwataka waiache kwani Serikali haitawavumilia na atakayethubutu hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.


  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU
  2 MTAA WA MAGOGONI,
  S. L. P. 3021,
  11410 DAR ES SALAAM

  0 0

   Ni mwaka mmoja bila wewe katika maisha yetu ya kila siku ,tunakukumbuka daima.UPENDO uliotuonyesha katika maisha ya kila siku,hatuna la kusema,umetuacha tukiwa bado tunahitaji mawazo yako.

  Tunamshukuru Mwenyezi MUNGU kwa muda wote uliokuwa nasi.
  Daima tutaendelea kukukumbuka hekima na busara zako huku tukiwa na tumaini la kuwa siku moja tutaonana nawe.

  Daima unakumbukwa na Mumeo Julius,mwanao John,Mama yako,wifi zako,shemeji zako,Dada na kaka zako,Maraafiki,majirani wa Bahari Beach na Ubungo Kibangu na watu wote waliokufahamu ktk uhai wako.

  Misa ya kumuombea Marehemu itafanyika ktk kanisa la Mt. Andrea liliop Bahari Bech – DSM tarehe 12/06/2016.Wote mnakaribishwa.
   

  0 0

  Jonas Kamaleki-Maelezo Dodoma

  WABUNGE  wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Tanzania wameaswa kutumia mifumo ya ufuatiliaji wa fedha za umma ili kuhakikisha kuwa fedha zinazotolewa na Serikali zinatumika katika malengo yaliyokusudiwa.

  Wito huo umetolewa leo mjini hapa na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt. Colman Titus Msoka wakati wa semina ya Wajumbe wa  Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC).

  Dkt. Msoka alisema wajibu na nafasi ya Mbunge katika chombo hicho cha kisheria ni pamoja na suala zima la kuisimamia Serikali, hivyo aliwataka Wabunge kuhakikisha wanafuatila matumizi ya fedha za umma kila zinapotengwa na jinsi zinavyotumika.

  “Wekeni mifumo ya ufuatiliaji wa matumizi ya fedha za umma kwenye majimbo yenu, kaeni pamoja na wataalamu wawafundishe watu wenu na muombe ufafanuzi wa matumizi hayo kwa wahusikia ili kuepukana na ubadhirifu wa fedha” alisema Dkt. Msoka.

  Kwa upande wake Mtafiti Mwandamizi kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kupunguza Umasikini nchini (REPOA), Bw. Solomon Baregu alisema ili kuwepo na ufanisi katika ufuatiliaji na usimamizi wa bajeti ya fedha zinazotengwa na Serikali kunahitaji kuwepo na sera kabambe zinazoanisha mikakati ya uondoaji wa umaskini kwa wananchi.

  Aliongeza kuwa ufuatiliaji na usimamizi kupitia sera  kutaifanya bajeti kuwa nyenzo ya utengaji wa rasilimali  zitakazosaidia kutimiza malengo yaliyokusudiwa katika Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini(MKUKUTA) na Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa miaka mitano 2016/17- 2020/21 sambamba na Dira ya Maendeleoya Taifa ya 2025.

  Naye Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Ruvuma, Mhe. Jacquiline Ngonyani alisema semina hizo hazina budi kufanyika kabla ya kukamilika kwa bajeti ili kuwapa nafasi wabunge kuweza kuchangia wakiwa na uelewa wa kutosha.

  “Kamati zinapaswa kutembelea sehemu miradi inapotekelezwa badala ya kusubiri kulalamika wakati miradi hiyo imeshatekelezwa na kubaini upungufu,” alisema Ngonyani.

  Mbunge wa Kasulu (CCM), Daniel Nsanzugwanko alisema ni wajibu wa wabunge kufuatilia matumizi ya fedha za umma katika miradi ya serikali ili miradi hiyo iweze kuleta tija mwa wananchi na taifa kwa ujumla.

  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali itamchukua hatua kiongozi yeyote atakayedonoa fedha za michango ya madawati inayotolewa na wadau mbalimbali wa maendeleo.

  Pia amewaagiza watendaji wote wa Serikali, Walimu Wakuu wa Shule za Msingi na Sekondari, Maofisa Elimu, Wakurugenzi wa Halmashauri, Wakuu wa Wilaya na Wakuu wa Mikoa, kuhakikisha michango hiyo inayotolewa inawafikia walengwa.

  Aidha, amezitaka wilaya zote nchini zianzishe mpango endelevu wa kuhakikisha kwamba upungufu wa madawati unasahaulika kabisa katika maeneo yao na kwamba utendaji wa viongozi wa elimu na Serikali katika ngazi mbalimbali utapimwa kutokana na jinsi ambavyo wametekeleza maagizo hayo.

  Waziri Mkuu Majaliwa ameyasema hayo leo (Jumamosi, Juni 11, 2016) wakati wa matembezi ya hisani ya kukusanya fedha za kununulia madawati kama sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa Benki Kuu ya Tanzania (BOT).

  Katika maadhimisho hayo yaliyoanzia BOT hadi viwanjja vya Mnazi Mmoja, Gavana wa BOT, Profesa Benno Ndulu alimkabidhi Waziri Mkuu hundi ya shilingi milioni 263 zilizochangwa na benki hiyo pamoja na watumishi wake kama mchango wao kwa ajili ya ununuzi wa madawati.

  Waziri Mkuu aliwapongeza watumishi wa BOT kwa kushirikiana na Serikali katika kutatua changamoto hiyo ambapo alitoa wito kwa taasisi zote katika sekta ya umma na binafsi pamoja na watu binafsi kuchangia uboreshaji wa elimu nchini kama sehemu ya “Majukumu ya Taasisi kwa Jamii” (Corporate Social Responsibility).

  Amesema kuwa na elimu bora, siyo tu faida kwa Taifa, bali kwa waajiri pia, kwani itahakikisha kwamba taasisi za umma na binafsi zinapata wafanyakazi ambao wameiva na wenye weledi wa kutekeleza majukumu mbalimbali ya uzalishaji katika taasisi hizo.

  “Nitoe wito pia kwa wanafunzi wote ambao watafaidika na kuboreshwa kwa mazingira ya kusomea, ikiwemo kupewa madawati na mahitaji mengine, kuhakikisha wanasoma kwa bidii kwa faida yao na Taifa kwa ujumla na kwa kufanya hivyo, wanafunzi watakuwa wanaenzi jitihada za Serikali, taasisi za umma, taasisi binafsi na watu binafsi katika kuboresha elimu nchini,” amesema.

  Amesema Serikali ya Awamu ya Tano imeazimia kupambana na changamoto za sekta ya elimu na kwamba tangu Uhuru, Serikali za Awamu zote zimekuwa zikifanya jitihada mbalimbali katika kuboresha elimu kwa wananchi wake.


  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU
  2 MTAA WA MAGOGONI,
  S. L. P. 3021,
  11410 DAR ES SALAAM

  0 0  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mhe. Angellah Kairuki akiongea na waandishi wa Habari kuhusu Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma mwaka 2016.
   
  Na. Aron Msigwa – Dar es salaam.

  SERIKALI imetangaza utaratibu mpya utakaofuatwa wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kuanzia Juni 16 hadi 23, 2016 ambapo imewaagiza Watendaji Wakuu katika Wizara, Idara zinazojitegemea, Wakala na Taasisi za Serikali kutenga siku moja ya kukutana na watumishi katika sehemu zao za kazi kwa lengo la kusikiliza kero mbalimbali zinazowakabili na kuzitafutia ufumbuzi.

  Aidha, imewaagiza watendaji hao kutenga siku nyingine moja kwa ajili ya kukutana na wananchi, kusikiliza na kuzitafutia ufumbuzi kero zao zinazohusiana na huduma zinazotolewa na Taasisi zao.

  Akitangaza utaratibu huo leo jijini Dar es salaam Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mhe. Angellah Kairuki amesema kuwa Serikali imeamua kubadili mfumo wa maadhimisho hayo kwa lengo la kuongeza ushiriki wa wananchi na watumishi wa umma katika maadhimisho hayo.

  Ameongeza kuwa wakati wa maadhimisho hayo Watendaji hao watatakiwa kukutana wananchi na kusikiliza kero zinazohusiana na huduma zinazotolewa na taasisi zao pia kukutana na watumishi wa umma katika sehemu zao za kazi kusikiliza kwa lengo la kusikiliza kero zinazowakabili zikiwemo za upandishwaji wa vyeo, madai mbalimbali na taratibu mbalimbali kuhusu utumishi wa umma.

  Amesema kuwa baada ya maadhimisho hayo kila Wizara, Mamlaka ya Serikali za Mitaa na Taasisi ya Umma itapaswa kuandaa taarifa jinsi ilivyotekeleza maagizo yaliyotolewa kwa kuiwasilisha Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma kabla ya Juni 30, 2016.

  Ameeleza kuwa Tanzania inaungana na mataifa mengine ya Bara la Afrika kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma Barani Afrika chini ya Kaulimbiu isemayo Uongozi wa Umma kwa Ukuaji Jumuishi:kuelekea katika Afrika tunayoitaka.

  Mhe. Angellah amebainisha kuwa maadhimisho ya mwaka huu yatajikita katika kuangalia mchango wa Utumishi wa Umma katika ukuaji wa uchumi Barani Afrika, mchango wa Utumishi wa Umma katika kuiwezesha Ajenda ya Afrika ya 20163 ambayo inaweka mkazo katika maendeleo ya Afrika na Haki za Wanawake.

  Amesisitiza kuwa malengo na mkakati wa Serikali ya awamu ya tano ni kufikia uchumi wa viwanda uliofungamanishwa na maendeleo ya watu, Tanzania ikiwa imejiwekea malengo ya kupiga hatua katika ukuaji wa uchumi kupitia maendeleo ya viwanda.

  Amesema ili kufikia azma hiyo Serikali kupitia Utumishi wa Umma ina wajibu wa kuwawezesha wananchi kushiriki katika shughuli za uzalishaji ili kukuza uchumi huku watumishi wa umma wakitakiwa kufanya kazi kwa bidii, maarifa na weledi, kutoa huduma kwa wananchi wote kwa wakati pasipo urasimu wala ukiritimba pia kuepuka vitendo vya rushwa katika utekelezaji wa majukumu yao.

  “Katika hili Watumishi wa umma lazima wawe na utendaji unaoweza kupimika, ili kulitekeleza hili kuanzia tarehe 1 Julai tutaanzisha dhana ya mfumo wa utendaji wa taasisi mbalimbali kwa lengo la kupima utendaji wa taasisi kulingana na matokeo tunayoyapata” Amesisitiza.

  Ameongeza kuwa watumishi wa umma Serikalini wanatakiwa kuwa na utendaji unaojali matokeo, kuepuka vitendo vya wizi, ufisadi na udanganyifu vinavyosababisha upotevu wa fedha za Serikali.

  Akizungumza kuhusu Haki za Wanawake katika utumishi wa umma amesema kuwa Serikali itaendelea kuhakikisha kuwa kuna uwiano wa jinsia katika nafasi na fursa mbalimbali katika ajira , Uteuzi wa nafasi za uongozi , mafunzo kazini na upandishwaji vyeo.

  UFAFANUZI KUHUSU WATUMISHI HEWA.

  Kuhusu suala la kuwaondoa Watumishi hewa katika orodha ya malipo ya Serikali Mhe. Angellah amefafanua kuwa tayari Ofisi yake imekwishatoa maelekezo kwa Makatibu Wakuu, Wakuu wa Taasisi zote za Umma pamoja na Mamlaka za Serikali za Mitaa yanayowataka kuwasilisha taarifa ya mwisho ya watumishi hewa ifikapo Juni 15, 2016.

  Amesema taarifa itakayowasilishwa itatakiwa kubainisha majina , namba za utambulisho wa watumishi hewa/ cheki namba, tarehe waliyotakiwa kuondolewa kwenye mfumo wa malipo na kiasi kilichopotea na kile kilichookolewa ikiwa imesainiwa na Mkuu wa Wizara, Mamlaka ya Serikali za Mitaa na Taasisi husika.

  Ameeleza kuwa mara baada ya kuzipokea taarifa hizo Serikali itazifanyia tathmini ili kupata uhakika wa zoezi zima la kuondoa watumishi hao kuanzia kuanzia tarehe 15 Machi 2016.

  “Kama mmekuwa mkifuatilia taarifa mbalimbali Serikali tumekuwa tukilishughulikia kwa nguvu suala hili la watumishi hewa kuanzia mwezi Machi mwaka huu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipotoa maagizo ya kuwaondoa watumishi hewa katika orodha ya malipo ya Serikali” Ameeleza.

  Aidha, amebainisha kuwa kuwa kuanzia Machi, 1, 2016 hadi Mei 30, 2016 watumishi 12,246 wameondolewa kwenye mfumo wa malipo ya mishahara kwa sababu mbalimbali zikiwemo za kutimiza umri wa kustaafu kwa lazima au kufukuzwa kazi ,vifo,kuhitimishwa kwa mikataba na ugonjwa.

  Jumla ya shilingi 25,091,292,688.82 zingepotea kama watumishi hao wasingeondolewa kwenye mfumo wa malipo ikilinganishwa na watumishi 10,295 walioondolewa kwenye mfumo hadi Aprili 30, 201 huku kiasi kilichookolewa kikifikia shilingi 23,206,547,598.82 likiwa ni ongezeko la watumishi 1,951 na shilingi 1,884,745,090.

  0 0


   Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wa pili kushoto) akimuuliza jambo Mkuu wa Jeshi la Polisi mkoani Mwanza, Ahmed Msangi (kushoto) wakati walipokuwa wanawasili msikiti wa Rahmani mkoani humo uliovamiwa na majambazi na kuua waumini watatu ndani ya msikini huo.
   Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa Kaunda suti) akiwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi mkoani humo, Ahmed Msangi (wa tatu kushoto) pamoja na askari wengine wa jeshi hilo, wakiyaangalia mapango ya utemini, jijini Mwanza ambako kulifanyika operesheni ya kupambana na majambazi baada ya majambazi hao kufanya mauaji katika msikiti wa Rahmani uliopo Kata ya Mkolani jijini humo.
   wa Jeshi la Polisi mkoani Mwanza, Ahmed Msangi (kulia) wakati walipokuwa wanatoka msikitini mara baada ya kuzungumza na waumini wa msikiti huo wa Rahmani mkoani humo. Msikiti huo ulivamiwa na majambazi hivi karinbuni na watu watatu waliuawa.
   Mzee wa Msikiti wa Rahmani uliopo Mkolani, jijini Mwanza, Abeid Gati (kushoto), akimpa fedha mke wa mmoja wa watu waliouawa na majambazi ndani ya msikiti huo. Fedha hizo zilitolewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa Kaunda suti) ikiwa ni rambirambi yake kwa wafiwa wote watatu ambao walipoteza wenza wao katika mauaji hayo. Hata hivyo Naibu Waziri alisema Serikali imesikitishwa na tukio hilo la kikatili na pia jeshi lake lipo makini na linaendelea kulinda usalama wa wananchi na mali zao.

   Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa Kaunda suti) akitoka kukagua nyumba za makazi ya askari Polisi zilizopo katika Kambi ya Mabatini jijini Mwanza, nyumba hizo zimetengewa fedha kwa ajili ya kumaliza ujenzi katika mwaka ujao wa fedha. Kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi mkoani Mwanza, Ahmed Msangi.
   Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akimpa pole askari Polisi, Mageni Kaseha aliyepigwa risasi ya mguu na majambazi wakati wa mapambano kati ya polisi na majamabazi hao katika mapango ya utemini, jijini Mwanza. Askari huyo amelazwa katika Zahanati ya Jeshi hilo iliyopo katika Kambi ya Mabatini, jijini humo.
   Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akizungumza na askari polisi katika Kambi ya Mabatini jijini Mwanza, ambao walipambana na majambazi na kufanikiwa kuwakamata wakati wa operesheni hiyo. Majambazi hayo yalijificha katika mapango ya Utemini jijini humo na ndipo yakavamiwa na polisi mara baada ya kuvamia msikiti wa Rahmani uliopo Mkolani jijini humo na kufanya mauaji. Masauni aliwapongeza askari hao kwa kupambana na majambazi hayo na kuwasisitiza kuwa kazi bado inaendelea wazidi kupambana mchana usiku ili wananchi waweze kuishi kwa amani. 
  Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella kimpa taarifa ya hali ya usalama mkoani humo, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wa tatu kulia) wakati kiongozi huyo wa Wizara alipofanya ziara mkoani humo. Katika ziara yake, Masauni alitembelea mapango ya Utemini mkoani humo ambapo mapambano kati ya polisi na majambazi yalifanyika, pia alienda kuuona msikiti wa Rahman uliovamiwa na majambazi, pia alizungumza na wafiwa na baadaye akamaliza ziara yake kwa kuzungumza na askari polisi ambapo aliwapa pongezi kwa kazi nzuri ya kupambana na majambazi hao. 
  Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 


  0 0

   Bodi ya Wakurugenzi wa TTB. Kutoka kushoto ni Bw. Agustine Kungu H. Olal, Bw. Mark Leveri, Bibi Zubein Mahita, Jaji Mstaafu Thomas Mihayo (Mwenyekiti), Bi Devota Mdachi (Katibu), Bw. Ibrahimu Mussa na Balozi Josiph Sokine 
   Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa TTB katika picha ya pamoja na Menejimenti ya TTB.
  Mkuu wa Kitengo cha IT cha TTB bw. Rossan Mduma (wa kwanza kulia) akiwaelezea wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi namna tovuti maalumu ya TTB (Portal) inavyofanyakazi na inavyoweza kutumiwa na wadau mbalimbali wa Utalii.
   Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya TTB katika kikao na Menejimenti ya TTB.

  Na Geofrey Tengeneza.

  Bodi mpya ya Wakurugenzi wa TTB iliyoteuliwa hivi karibuni imekutana leo katika ofisi za TTB jijini Dar es salaam katika mkutano wake wa kwanza toka iingie madarakani.

  Mkutano huo ambao ulikuwa mahsusi kwa ajili ya wajumbe wa Bodi hiyo kufahamu zaidi kazi na majukumu ya Bodi ya Utalii Tanzania(TTB) ulifanyika chini ya uenyekiti wa Jaji Mstaafu Thomas Mihayo na kuhudhuriwa pia na Menejimenti ya TTB.

  Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania Bi Devota Mdachi alitumia pia mkutano huo kuwatambulisha wajumbe wa Menejimenti ya TTB kwa Mwenyekiti na Wakurugenzi hao wa Bodi. Bodi ya wakurugenzi iliyoteuliwa mwezi Mei mwaka huu ina wajumbe sita ambao ni Bw. Ibrahimu Mussa ambaye ni Mkurugenzi wa Masoko na Utalii wa TANAPA; Balozi Joseiph Sokoine , Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje, Afrika Mashariki, Ushirikiano wa Kimataifa na Kikanda; Bw. Mark Leveri, Mtaalamu wa filamu na matangazo.

  Wengine ni  Bw. Richard Rugimbana, Bw. Richard Rugimbana, Mtendaji Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Utalii Tanzania (TCT), Bibi Zubein Muhaji Mhita, Bibi Zabein Muhaji Mhita, Mbunge Mstaafu na Mkurugenzi wa Elimu ya Msingi  Msataafu na Bw. Agustine Kungu H. Olal, Kamishna Msaidizi wa Sera na Uchumi, Wizara ya fedha na Mipango. Mjumbe mwingine ni Mkurugenzi Mwendeshaji wa TTB Devota Mdachi ambaye pia ni Katibu wa Bodi hiyo ya Wakurugenzi.

  Mwenyekiti na Wajumbe hao wa Bodi ya Wakurungenzi wa TTB  watakuwa madarakani kwa miaka mitatu kuanzia tarehe 24/04/2016 hadi tarehe 23/04/2019 .


  0 0

   Wasimamizi wa Uchaguzi Mkuu wa Klabu ya Yanga, wakiwa tayari kwa kazi hiyo ya uchaguzi unaoendelea kufanyika hivi sasa kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, Jijini Dar es salaam.
   Mgombea pekee wa nafasi ya Uenyekiti wa Klabu ya Yanga, Yussuf Manji akiandikishwa na Msimamizi wa Uchaguzi huo, unaofanyika hivi sasa kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, Jijini Dar es salaam.
  Mgombea pekee wa nafasi ya Uenyekiti wa Klabu ya Yanga, Yussuf Manji akitumbukiza karatasi kwenye sanduku la kupigia kura, katika unaofanyika hivi sasa kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, Jijini Dar es salaam.
   Kocha Mkuu wa Timu ya Yanga, Hans van Pluijm nae ni Mmoja wa Wanachama wa Yanga wanaopiga kura leo kuchagua uongozi mpya wa Klabu hiyo.
  Wanachama wakipiga kura.
   Mgombea pekee wa nafasi ya Uenyekiti wa Klabu ya Yanga, Yussuf Manji akifurahia jambo na Mlezi wa timu ya Yanga,Mama Shadya Karume mapema leo ndani ya ukumbi wa Diamond kabla ya uchaguzi kufanyika
  Mgombea pekee wa nafasi ya Uenyekiti wa Klabu ya Yanga, Yussuf Manji   akisoma hotuba yake fupi kupitia simu yake ya Kiganjani mbele ya mamia ya wanachama wa Klabu hiyo ya Yanga (hawapo pichani),mapema leo mchana kabla ya uchaguzi kufanyika
  Mgombea pekee wa nafasi ya Uenyekiti wa Klabu ya Yanga, Yussuf Manji  pichani kulia akiteta jambo na Kocha Mkuu wa Timu ya Yanga, Hans van Pluijm 
   Baadhi ya Wanachama wakisubiri kupiga kura kuwachagua viongozi wao


  BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

  0 0


   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na wasanii wa Benki Kuu baada ya kuongoza matembezi  kuchangia madawati ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya Benki kuu ya Tanzania. Matembezi hayo yalianzia Benki Kuu hadi viwanaj vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam Juni 11, 2016.  Zaidi ya shilingi milioni263 zilichangwa.
  Bendi ya Poli ikiongoza matembezi  ya kuchangia madawati ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya Benki kuu ya Tanzania. Matembezi hayo yalianzia Benki Kuu hadi viwanaj vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam Juni 11, 2016.Zaidi ya shilingi263 milioni zilichangwa.
     Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongoza matembezi ya kuchangia madawati ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya Benki kuu ya Tanzania. Matembezi hayo yalianzia Benki Kuu ha viwanaj vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam Juni 11, 2016.Kushoto kwake ni Gavana wa Benki Kuu, Benno Ndulu na kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda. Zaidi ya shilingi milioni 262 zilichangwa.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza  baada ya kuongoza  matembezi ya kuchangia madawati ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya Benki kuu ya Tanzania. Matembezi hayo yalianzia Benki Kuu hadi viwanaj vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam Juni 11, 2016. Zaidi ya shilingi milioni 263 zilichangwa. 
  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

   
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa kushoto Ndugu David Shambwe akiwa na mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Arusha Ndugu Felix Daudi Ntibenda wakipiga makofi kuashiria furaha ya ukaribisho wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Safaricity Matevez Arusha leo. 
  aimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa kushoto Ndugu David Misonge Shambwe akiwa na mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Arusha Ndugu Felix Daudi Ntibenda na Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha Calist Lazaro wakipiga makofi wakati wa uzinduzi wa Mradi wa #SafariCity Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa kushoto Ndugu David Shambwe akizungumza na wananchi pamoja na wafanya Biashara wa Jiji la Arusha wakati akimkaribisha Mgeni Rasmi 
  Mmoja wa wafanyabiashara wakubwa wa Jijini Arusha akisimama baada ya kutambulishwa na Mgeni rasmi Mh Felix Daudi Ntibenda katika hafla ya uzinduzi wa #SafariCity 
  Baadhi ya wawekezaji na waendelezaji wakifuatilia tukio hilo Muhimu la uzinduzi wa #SafariCity 
  Baadhi ya wawekezaji na waendelezaji wakifuatilia tukio hilo Muhimu la uzinduzi wa #SafariCity 
  Mgeni rasmi katika uzinduzi wa #SafariCity Mh Felix Daudi Ntibenda akipanda mti pamoja na Mstahiku Meya wa Jiji la Arusha Calist Lazaro ikiwa ni ishara ya Uzinduzi wa #SafariCity
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa kushoto Ndugu David Shambwe akizungumza na wananchi pamoja na wafanya Biashara wa Jiji la Arusha wakati akimkaribisha Mgeni Rasmi
  Mgeni rasmi katika uzinduzi wa #SafariCity Mh Felix Daudi Ntibenda akipanda mti pamoja na Mstahiku Meya wa Jiji la Arusha Calist Lazaro ikiwa ni ishara ya Uzinduzi wa mji wa #SafariCity

  0 0


  Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Benno Ndulu (kushoto) akimkabidhi Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (kulia) mfano wa hundi ya Sh. 273,089,338 leo jijini Dar es salaam kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano kuchangia ununuzi wa madawati.

  Hussein Makame-MAELEZO.

  Benki Kuu ya Tanzania (BOT) na wafanyakazi wake wa matawi yote nchini kwa kushirikana na baadhi ya Taasisi za kifedha na kampuni za simu nchini, imetoa Shilingi Milioni 273 kuchangia ununuzi wa madawati ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 50 ya Benki hiyo.

  Fedha hizo zilikabidhiwa leo kupitia hundi ya mfano kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa baada ya matembezi ya hisani yaliyolenga kuchangia madawati, yaliyoanzia Ofisi za BOT hadi kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.Akizungumza kabla ya kukabidhi fedha hizo, Gavana wa BOT Prof. Benno Ndulu alisema lengo la mchango huo ni kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano katika kuongeza ubora wa elimu kupitia upatikanaji wa madawati kwa shule za msingi na sekondari nchini.

  “Tunatambua kwamba changamoto hiyo (uhaba wa madawati) ni kubwa, lakini tunaamini mchango wetu utasaidia kupunguza makali ya tatizo hilo na kuongeza idadi ya watoto wetu ambao wanasoma wakiwa wamekaa kwenye madawati” alisema Gavana Prof. Ndulu.

  Akifafanua mchango huo, Gavana Prof. Ndulu alisema kati ya fedha hizo, BOT imetoa Shilingi Milioni 167, Wafanyakazi Milioni 29.8, Taasisi za Kifedha Milioni 22 na kampuni za simu Milioni 54.3 na kwamba madawati hayo yatasambazwa kwenye shule zenye upungufu au ukosefu wa madawati za Dar es Salaam na zilizoko mikoa ambayo Benki hiyo ina matawi yake.

  Alitaja mikoa hiyo na fedha zilizochangwa na wafanyakazi wa BOT wa matawi ya mikoa hiyo kuwa ni Makao Makuu Dar es Salaam waliochangia Shilingi Milioni 22, Mwanza (Milioni 1.24), Chuo cha Benki Mwanza (680,000) Arusha (Milioni 1.23) Mbeya (Milioni 1.186), Mtwara (850,000) na Dodoma (Milioni 1.18).

  Alisema taasisi zilizochangia fedha hizo ni Benki ya India Shilingi Milioni 5, Benki ya Habib (Milioni 5), Benki ya Exim (Milioni 5), Benki ya UBA (United Bank for Africa, Milioni 2), Tanzania Mortgage Refinance (Milioni 2), China Community Bank (Milioni 2) na NIC Bank aliyotoa Milioni 1.

  Kwa upande wa kampuni za simu zilizotoa fedha ni kampuni ya Vodacom iliyotoa Dola za Kimarekani 10,000, kampuni ya Tigo Dola za Kimarekani 10,000 na kampuni ya Selcom iliyotoa Dola za Kimarekani 5,000.

  Akizungumza baada ya kupokea hundi ya mfano, Waziri Mkuu Majaliwa alisisitiza fedha hizo zitumike kama zilivyokusudiwa na yeyote atakayetumia fedha hizo kinyume na malengo achukuliwe hatua mara moja.Katika kuthamini sekta ya elimu nchini, Gavana Prof. Ndulu alisema benki hiyo ilianzisha Mfuko wa Udhamini wa Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere ambapo hadi sasa umetoa ufadhili kwa wanafunzi 22 kusoma shahada za kwanza na za uzamivu katika vyuo vikuu hapa nchini katika masomo ya sayansi, hisabati, uchumi, fedha, uhasibu na TEHAMA.

  “Lengo kubwa la mfuko huu ni kuhamasisha wanafunzi wa kike kusoma masomo ya sayansi na hisabati yakiwemo masomo kuhusu gesi na mafuta.Katika idadi hiyo, 16 ni wanafunzi wa kike na waliobaki 8 ni wanaume” alisema Gavana Prof. Ndulu.Benki Kuu ya Tanzania (BOT) ilianza kutoa huduma kwa wananchi mnamo tarehe 14 Juni mwaka 1966 na Juni 14 mwaka huu inatimiza Miaka 50 na katika kuadhimisha miaka hiyo wafanyakaz wa matawi yote nchini wanafanya matembezi hayo ili kutoa mchango kwa jamii.

older | 1 | .... | 876 | 877 | (Page 878) | 879 | 880 | .... | 1903 | newer