Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46205 articles
Browse latest View live

RC MWANZA AKABIDHI VISIWA KWA MALIASILI.

0
0
 Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella akihutubia, wakufunzi, wakurufunzi na jamii inayozunguka chuo hicho, hawapo pichani wakati wa uzinduzi wa maonesho ya miaka 50 ya chuo hicho.(Picha zote na Afisa Habari wa Mkoa wa Mwanza)
 Hapa picha ya pamoja ni muhimu kwaajili ya kalenda ijayo ya Mwaka, hii nikatika miaka 50 ya chuo cha wanyamapori Pasiansi.
 Mkuu wa mkoa akipokea mti kutoka kwa mkuu wa chuo hicho Bibi Lowael Damalu, tayari kwaajili yakuupanda.
 Mkuu wa mkoa wa akipanda, mti katika taasisi hiyo, ikiwa ni sehemu ya ukumbusho wa miaka hamsini toka kuanza kwa chuo hicho.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella, akisalimiana na mmoja wa wakufunzi katika chuo cha taasisi ya mafunzo ya wanyamapori Pasiansi jiji Mwanza, alipofika kwenye uzinduzi wa maonesho ya miaka 50.

RC MWANZA AKABIDHI VISIWA KWA MALIASILI.

Na Atley Kuni- RS Mwanza.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella, ameiagiza taasisi ya taaluma ya wanyamapori Pasiansi kuanza kutumia visiwa na majabali makubwa yaliopo mkoani humo kwaajili ya mazoezi ili kuweza kusaidia kupambambana na uhalifu ulioanza kujitokeza katika siku za karibuni katika mkoa huo.

Akizungumza katika uzinduzi wa maonesho ya sherehe za maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa chuo hicho nchini Tanzania, Mongella amesema badala ya wakurufunzi hao kwenda kufanya mazoezi kwenye maeneo ya nje ya mkoa ni vema kuanzia sasa mkaanza kutumia visiwa vyetu,

“Ndani ya ziwa viktoria, hasa huko visiwani kuna watu wanafanya uvuvi haramu sasa ni vema wakati wa mazoezi mkawa mnafanyia kwenye maeneo hao ambayo yamekithiri kwa uvuvi usio na tija”, alisema Mongella na kuongeza, “lakini sio kukomesha tuu, uvuvi haramu bali pia itachagiza kwenye suala zima la utunzaji wa mazingira na maliasili”

Amesema kuwa, endapo taasisi hiyo ikitumia sehemu ya mafunzo kwa vitendo, kama mkoa utakuwa hauna haja yakufunga shughuli za uvuvi kwa msimu na badala yake itasaidia kwenye uzazi salama wa samaki na viumbe wengine wa majini.

Kwa upande wake mkuu wa chuo hicho bi Lowael Damalu, amemuelezea mkuu wa mkoa kuwa chuo hicho hivi sasa, kinauwezo wakudahili wakurufunzi 415 kwa msimu mmoja, ambalo ni ongezeko kubwa ikilinganishwa na wakurufunzi 50, waliokuwa wakidahiliwa na chuo hicho wakati kinaanza mwaka 1966, amesema mafanikio mengine yaliyopatikana ni pamoja na kupata ithibati ya kutoka baraza la Elimu ya ufundi, ongezeko la kozi za askari kuwa (basic technician, Law Enforcement, uboreshaji wa maslahi ya watumishi, mafanikio mengine ameyataja kuwa ni kuongezeka kwa miundombinu na vifaa vya kufundishia, lakini pia taasisi kuwa na tovuti yake ya www.pasiansiwildlife.ac.tz sambamba na taasisi kujipatia ardhi.

Mkuu huyo wa chuo amesema mbali yakuwa na mafanikio chuo hicho bado kinakabiliwa na matatizo ya uchakavu wa baadhi ya mabweni, uchache wa nyumba za watumishi, vilevila kutokuwepo kwa sheria ya uanzishwaji wa taasisi sambamba na uhaba wa ajira kwa wakurufunzi wanao hitimu katika chuo hicho.

DUKA LA VIFAA LA AZAM FC LAZINDULIWA LEO NDANI YA BOTI YA KILIMANJARO 6.

0
0
Wafanyakazi wa Duka la Azam wakionyesha baadhi ya Jezi za  Timu ya Azam zinazopatikana katika Duka Maalum lililofungulia ndani yaboti ya Kilimanjaro 6 leo.
Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba  akizungumza Michuz TV wakati wa uzinduzi wa duka la vifaa vya vya michezo pamoja na vitu mbalimbali vya Azam duka hilo limezinduliwa ndani ya boti ya Kilimanjaro 6 leo.
Wafanyakazi wa Duka la Azam wakionyesha baadhi ya skafu na vitamaa vya  Timu ya Azam zinazopatikana katika Duka Maalum lililozinduliwa ndani ya boti ya Kilimanjaro 6 leo.

SIKU YA MTOTO WA AFRIKA 2016 YAANDALIWA

0
0
WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO
 MAADHIMISHO YA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA JUNI 16, 2106 
Tarehe 16 Juni ya kila mwaka, ni kilele cha  Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika. Katika siku hii, Tanzania inaungana na nchi nyingine wanachama wa Umoja wa Afrika kuadhimisha Siku hii kwa mujibu wa Azimio lililopitishwa na nchi 51 za Umoja huo mnamo mwaka 1990.  
Azimio hili lilipitishwa kwa ajili ya kukumbuka mauaji ya watoto wa shule  yaliyofanyika  katika kitongoji cha Soweto, Afrika ya Kusini tarehe 16 Juni, 1976. Katika tukio hilo la kusikitisha, inakadiriwa kuwa watoto wapatao 2,000 waliuawa kikatili na utawala ulioundwa na  Serikali ya Makaburu. Watoto hawa walikuwa kwenye harakati za kudai haki yao ya msingi ya kutokubaguliwa kutokana na rangi yao.

Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika kwa mwaka 2016 yataadhimishwa katika ngazi ya Mikoa kwa kuzingatia taratibu za mikoa husika. 

Lengo kuu la Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika tarehe 16 Juni, 2016, ni kuwa na siku maalum ya  kuelimisha na kuwakumbusha wazazi, walezi na wadau mbalimbali kuitikia utekelezaji wa wajibu na majukumu yetu katika kuwapatia watoto haki zao za msingi. Haki hizi ni pamoja na haki ya kuishi, kulindwa, kuendelezwa, kushiriki na kutobaguliwa. Katika siku hii watoto hupata nafasi maalum ya kujieleza, kusikilizwa, kushiriki na kuonyesha vipaji vyao mbele ya wazazi, walezi na jamii kwa ujumla.

Maadhimisho haya, huambatana na kaulimbiu ambayo inalenga kuhamasisha jamii kutatua changamoto wanazokabiliana nazo watoto wa Tanzania. Kaulimbiu ya Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika 2016 ni “Ubakaji na Ulawiti kwa Watoto Vinaepukika: Chukua Hatua Kumlinda Mtoto”.     

Ni matarajio yangu kuwa kila mwananchi atashiriki maadhimisho haya kwa kuchukua hatua thabiti za kuwalinda watoto katika jamii zetu. 

S. Nkinga
KATIBU MKUU
10/6/2016.

MTU MMOJA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA UTAPELI WILAYANI NYAMAGANA.

0
0


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA.
TELEGRAMS:   POLISI,                                                    OFISI YA
TELEPHONE: 2500712                                           KAMANDA WA POLISI,
Fax: 2502310                                           MKOA WA MWANZA,
E-mail: mwapol@yahoo.com                                                                                    S.L.P.120,
           rpc.mwanza@tpf.go.tz                                                                                  MWANZA.
TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA.

MWANAMKE MMOJA AMEKUTWA AKIWA AMEJINYONGA HADI KUFARIKI DUNIA WILAYANI MAGU.

MTU MMOJA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA UTAPELI WILAYANI NYAMAGANA.

KWAMBA MNAMO TAREHE 08.06.2016 MAJIRA YA SAA 23:00HRS KATIKA KITONGOJI CHA MAKALE KIJIJI CHA KAYENZE B KATA YA NKUNGURU TARAFA YA NDAGULA WILAYA YA MAGU MKOA WA MWANZA , MARIAM NHABAGULA MIAKA 33 MKAZI WA KAYENZE B ALIKUTWA AKIWA AMEJINYONGA  HADI KUFARIKI PAPO HAPO KWENYE MTI KWA KUTUMIA KAMBA YA KATANI.
INADAIWA KUWA MAREHEMU KABLA YA KUCHUKUA MAAMUZI YA KUJINYONGA ALIKWENDA KUPIMA AFYA YAKE NDIPO ALIPOKEA MAJIBU KUWA NIMUATHIRIKA WA VIRUSI VYA UKIMWI, HALI ILIYOPELEKEA  KUAMUA KUJINYONGA HADI KUFARIKI DUNIA.
MWILI WA MAREHEMU TAYARI UMEFANYIWA UCHUNGUZI NA DAKTARI NA KUKABIDHIWA KWA NDUGU WA MAREHEMU KWA AJILI YA MAZISHI, JESHI LA POLISI BADO LINAENDELEA NA UCHUNGUZI JUU YA TUKIO HILO ILI KUWEZA KUJIRIDHISHA JUU YA MADAI YA KIFO HICHO.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED MSANGI AMEWATAKA WANANCHI WA MKOA WA MWANZA KUISHI KWA UPENDO NA USHIRIKIANO PAMOJA NA KUFARIJIANA KATIKA KILA HALI, ILI KUWEZA KUZUIA VIFO VINAVYOWEZA KUEPUKIKA KATIKA JAMII ZETU.
KATIKA TUKIO LA PILI
KWAMBA TAREHE 09.06.2016 MAJIRA YA SAA 14:00HRS KATIKA MTAA WA LIBERTY KATA YA PAMBA KATIKATI YA JIJI LA MWANZA, ASKARI WAKIWA KWENYE MISAKO NA DORIA WALIFANIKIWA KUMKAMATA MATONDO JAMES MIAKA 39 MKAZI WA IGOMA AKIWA NA PAKITI MOJA [01] YA MADINI YAZANIWAYO KUWA NI BANDIA WAKIYATUMIA KUTAPELI WATU KATIKA MITAA BARABARANI NA KWENYE MABENKI KITENDO AMBACHO NI UVUNJWAJI WA SHERIA NA TARATIBU ZA NCHI.
AIDHA MTUHUMIWA YUPO KATIKA MAHOJIANO NA JESHI LA POLISI, NA TAYARI WATU WENGINE WATATU AMBAO MAJINA YAO YAMEHIFADHIWA WAMEKAMATWA HIVI PUNDE NA JESHI LA POLISI WAKIHUSIANISHWA KUSHIRIKIANA NA MTUHUMIWA KATIKA KUFANYA UHALIFU HUO KATIKA JIJI LA MWANZA.
INADAIWA KUWA MTUHUMIWA AKISHIRIKIANA NA WENZAKE HUFANYA KAZI YA KUWATAPELI WAPITA NJIA NA WATEJE WA MABENKI KUWA WANAUZA MADINI, HIVYO HUWAAMBIA WANAUZA MADINI YA AINA YA ZAHABU NA MARA NYINGINE HUWAANBIA WANAUZA ALMASI LAKINI KIPINDI HICHO WANAKUWA WAMEYAFUNGA MADINI HAYO BANDIA KWENYE PAKITI NA HUMSHAWISHI MNUNUAJIA AKAIFUNGUE PAKITI HIYO YENYE MADINI SEHEMU WANAPO NUNUA MADINI, PINDI MPITA NJIA AKIKUBALI KUUZIWA MADINI HAYO ANAKUWA TAYARI WAMEMTAPELI NA MATAPELI HAO HUTOROKA MUDA HUO MAHALI WALIPOFANYA UHALIFU.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WANANCHI AKIWATAKA KUTOA USHIRIKIANO KWA JESHI LA POLISI ILI KUWEZA KUWAKAMATA WATU WANAOJIHUSISHA NA UTAPELI WA AINA KAMA HIYO NA KUWAFIKISHA KWENYE VYOMBO VYA SHERIA, LAKINI PIA AKIWATAKA WANANCHI KUSHIRIKIANA NA VIONGOZI WA SERIKALI ZA MITAA KWA KUTOA TAARIFA MAPEMA ZA MTU AU WATU WANAOZANIWA KUWA WAHALIFU ILI WAWEZE KUKAMATWA NA KUFIKISHWA MAHAKAMANI.
IMESAINIWA NA:
SACP: AHMED MSANGI


KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA

SERIKALI YA TANZANIA NA ZAMBIA ZASAINI MAKUBALIANO YA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO ZA KUDHIBITI USAFIRISHAJI WA MAZAO YA MISITU NA MAGOGO KUPITIA MIPAKA YA NCHI HIZO

0
0
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili, Maj. Gen. Gaudence Milanzi (katikati) akisaini hati ya makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na Zambia,  jijini Dar es Salaam jana kwa ajili ya kukabiliana na changamoto za udhibiti wa usafirishaji wa mazao ya misitu hususan magogo katika mipaka ya nchi hizo mbili. Wanaoshuhudia kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki, Wizara ya Maliasili, Gladynes Mkamba na Kaimu Mtendaji Mkuu TFS, Richard Kamwenda (kushoto). Waliosimama kulia ni Mwanasheria wa TFS, David Mung’ong’o na Mwanasheria wa Wizara ya Maliasili, Stephen Mwamasenjele. 
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Maliasili na Hifadhi ya Mazingira wa Serikali ya Zambia, Trevor Kaunda akisaini  makubaliano hayo.

Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili, Maj. Gen. Gaudence Milanzi (kushoto) na Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Maliasili na Hifadhi ya Mazingira wa Serikali ya Zambia, Trevor Kaunda wakibadilishana hati ya makubaliano waliyosaini kwa ajili ya kukabiliana na changamoto za udhibiti wa usafirishaji wa mazao ya misitu hususani magogo katika mipaka ya nchi hizo. 
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili, Maj. Gen. Gaudence Milanzi akizungumza katika hafla fupi ya kuweka makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na Zambia jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kukabiliana na changamoto za udhibiti wa usafirishaji wa mazao ya misitu hususani magogo katika mipaka ya nchi hizo. Kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Maliasili na Hifadhi ya Mazingira wa Serikali ya Zambia, Trevor Kaunda. Maj. Gen. Milanzi alisema kuwa ushirikiano huo utaleta tija katika udhibiti wa biashara haramu ya uvunaji na usafirishaji wa magogo kutoka katika nchi hizo kwenda nchi nyingine kupitia mipaka ya nchi hizo na bandari ya Dar es Salaam. Aliwataka watanzania wanaojihusisha na biashara haramu ya uvunaji na usafirishaji wa magogo nje ya nchi waache mara moja kwani Serikali imejipanga kuhakikisha wanakamatwa na sheria kali zitachukuliwa dhidi yao.
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili, Maj. Gen. Gaudence Milanzi (kulia) na Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Maliasili na Hifadhi ya Mazingira wa Serikali ya Zambia, Trevor Kaunda wakiteta jambo wakati wakikagua Makontena 103 ya magogo (nyuma pichani) yaliyokamatwa hivi karibuni katika bandari ya Dar es Salaam kutoka nchini Zambia na DRC. Makatibu Wakuu hao wamesaini makubaliano ya kukabiliana na changamoto za udhibiti wa usafirishaji wa mazao ya misitu hususani magogo kwenye mipaka wa nchi hizo.
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili, Maj. Gen. Gaudence Milanzi (kushoto) na Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Maliasili na Hifadhi ya Mazingira wa Serikali ya Zambia, Trevor Kaunda wakiangalia sehemu ya magogo yaliyokamatwa hivi karibuni katika bandari ya Dar es Salaam kutoka nchini Zambia na DRC. Makatibu Wakuu hao wamesaini makubaliano ya kukabiliana na changamoto za udhibiti wa usafirishaji wa mazao ya misitu hususani magogo kwenye mipaka wa nchi hizo. (Picha na Hamza Temba - Wizara ya Maliasili na Utalii)

AMKA NA BBC Juni 10, 2016......Obama atangaza rasmi kumuunga mkono Hillary Clinton

0
0
Rais wa Marekani Barack Obama ametangaza kumuunga mkono Hillary Clinton kuwa mgombea urais wa chama cha Democratic katika uchaguzi mkuu utakaofanyika baadaye mwaka huu nchini Marekani.
Amechukua hatua hiyo muda mfupi baada ya kukutana na seneta wa Vermont Bernie Sanders ambaye amekuwa akikabiliana na Bi Clinton katika kinyang’anyiro cha kumchagua mgombea wa chama hicho.

WATOTO WALIOZALIWA NA MAMBUKIZI YA VVU MATUMAINI DODOMA, WAITAKA JAMII KUWAKUMBUKA

0
0
Imeelezwa ili kuwawezesha watoto yatima ambao walizaliwa wakiwa na Virusi vya UKIMWI ambao wanapatikana katika Kituo cha Matumaini kilichopo Manispaa ya Dodoma, Watanzania wametakiwa kuungana kwa pamoja na kuwasaidia watoto hao ambao wanaishi katika kituo hicho ili kuwawezesha kuishi mazingira bora pamoja na kupata huduma za bora za afya.

Hayo yalisemwa na Msimamizi wa Kituo cha Matumaini, Sister Maria Rosaria Gargiulo, alisema kituo hicho chenye watoto 151 wakati kimeanzishwa kilikuwa kikipokea msaada kutoka Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na TACAIDS lakini kwa sasa msaada umesimama na hivyo kuwafanya kwa sasa kuishi katika mazingira magumu.

Sister Maria alisema kuwa hali ya maisha kwa watoto hao ni ngumu na hivyo kuwataka Watanzania kuwakumbuka watoto hao ambao walizaliwa wakiwa na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI ili waweze kupata huduma bora ambazo zitawawezesha kuishi katika mazingira bora, kupata elimu na kupata dawa ambazo zitaimarisha afya zao.
Mlimbwende wa Taji la Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu (kushoto) na mfanyakazi mwenzake Beatrice Mkiramweni wakiongozwa na Msimamizi wa Kijiji cha Matumaini, Sista Rosaria Gargiulo mara baada ya kuwasili katika kituo hicho kilichopo katika manispaa ya Dodoma karibu na Hoteli ya Mtakatifu Gasper.(Imeandaliwa na Zainul Mzige wa Modewjiblog)

“Hapa wanakuja tu watu wa hapa Dodoma mara nyingi siku za Jumamosi na Jumapili ila tofauti na hivyo hatuna msaada mwingine, watoto hawa wanahitaji faraja kutoka kwa watu wengine inapendeza kuona watu wanakuja kuwaona na kuwasaidia nao wanafurahi,

“Ukiangalia hali ya kimaisha inazidi kupanda tunafanya jitihada kujisimamia sisi wenyewe lakini tunashindwa bado tunahitaji msaada sisi tumejitoa kuwasaidia hawa watoto hata hatulipwi lakini tunahitaji sana msaada wa Watanzania,” alisema Sister Maria.

Nae Mlimbwende wa Taji la Miss Tanzania 1999 na Mtalaam wa Mawasiliano wa Shirika la Umoja wa Mataifa (UN), Hoyce Temu ambaye alifika kituoni hapo kwa ajili ya kutoa msaada ambapo alituma ujumbe kwa Watanzania wengine ambao wamekuwa hawana utaratibu wa kutoa misaada kwa wahitaji na kuwataka kubadilika.

Bi. Temu alisema kuwa mazingira ambayo wanaishi watoto hao ni magumu na hawana wazazi kutokana na wazazi wao kuwa wamefariki hivyo kuwataka Watanzania kujitoa kwa pamoja na kuwasaidia watoto hao kwa chochote ambacho kinaweza kuwasaidia kuimarisha maisha yao ili waishi mazingira bora.

“Jamani kama watu wanasema tunapoishi kuna shida basi hakuna, shida zipo huku, ukiangalia kuna watoto wengine wana wiki moja na hawana wazazi wametupwa wanahitaji kupata misaada ya Watanzania,

Mlimbwende wa Taji la Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu akimsikiliza kwa makini mmoja wa watoto wanaoishi kituoni hapo aliyewahi kumuona mara ya kwanza alipofika kituoni hapo.

“Nitoe rai kwa Watanzania wenzangu kama una pesa au nguo au chochote ambacho kinaweza kuwasaidia tutoe kwa watoto hawa mazingira yao ni magumu sana, hawana makosa hawa hata mbele za Mungu naomba tuwasaidie,” alisema Bi. Temu.

Kwa yoyote atakayeguswa na angependa kufika kituoni hapo kusaidia anaweza kupiga simu kwa Msimamizi wa Kituo cha Matumaini, Sister Maria Rosaria Gargiulo +255754272707
Mlimbwende wa Taji la Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu (kulia) na mfanyakazi mwenzake Beatrice Mkiramweni wakiwa wamewabeba watoto yatima wanaoishi kituoni hapo.
Mlimbwende wa Taji la Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu akifurahia jambo mara tu baada ya kuwasili katika kijiji cha Matumaini kilichopo mkoani Dodoma kinacholea watoto yatima ambao 98% wanaishi na Virusi vya Ukimwi.
Mlimbwende wa Taji la Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu akiwa kwenye wodi ya watoto wachanga ambao ni yatima wanaoishi waliozaliwa na maambuki ya Virusi vya Ukimwi.
Mlimbwende wa Taji la Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu na mfanyakazi mwenzake Beatrice Mkiramweni pamoja na Msimamizi wa Kijiji cha Matumaini, Sista Rosaria Gargiulo (kulia) walipotembelea wodi ya watoto wachanga waliozaliwa na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi.
Mlimbwende wa Taji la Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu akifurahi na watoto wachanga ambao ni yatima waliozaliwa na maaumbikizi ya Virusi vya Ukimwi waliolazwa katika wodi ya watoto kijiji cha Matumaini kilichopo mkoani Dodoma.
Wewe acheka afurahi kumuona Aunty....Jiji jiji jiji.....jamani acheka....Ni maneno ya Mlimbwende Hoyce Temu akicheza na mmoja wa watoto hao katika wodi hiyo.
Meneja Mwendeshaji wa mtandao wa Habari wa Modewjiblog, Zainul Mzige akimbeleza mmoja wa watoto waliozaliwa na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi wanaolelewa katika kijiji cha Matumaini kilichopo mkoani Dodoma.
Eweee Mwenyezi Mungu, mwingi wa Rehema, tunakuomba wajaalie Malaika wako hawa afya njema, maisha marefu, wape uponyaji viumbe hawa wasiokuwa na hatia, Amen!
Msimamizi wa Kijiji cha Matumaini, Sista Rosaria Gargiulo akimsimulia Mlimbwende wa Taji la Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu historia ya mtoto Richard aliyeshikwa mikono na mlimbwende huyo.
Mmoja wa Masista wanaohudumia watoto hao Sista Mary Shayo akifurahi jambo wodini mbele ya kamera ya Modewjiblog.
Mlimbwende wa Taji la Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu akicheza kwaya ya wimbo maalum aliokuwa akiimbiwa na bendi ya kijiji cha Matumaini kabla ya kukabidhi msaada wa vitu mbalimbali.
Hoyce Temu akigawa zawadi kwa watoto wanaolelewa kwenye kijiji cha Matumaini mkoani Dodoma.
Mlimbwende wa Taji la Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu akikabidhi 'Pampers' kwa mmoja wafanyakazi wanaohudumia (jina lake halikuweza kupatikana) watoto kituoni hapo.
Mlimbwende wa Taji la Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu akikabidhi mfuko wa sukari.
Mlimbwende wa Taji la Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu akikabidhi makopo ya maziwa. (Picha zaidi ingia hapa).

UZINDUZI WA HOTEL YA KISASA KUSILE RESTAURANT AND LODGE MJINI MBINGAULIOFANYIKA NA MWENGE WA UHURU 2016.

0
0

Mkurugenzi wa kampuni ya Ovans Construction Company Limited, ambao ni wamiliki wa Kusile Restaurant and Lodge, Valence Urio upande wa kulia akiwa ameshika Mwenge wa Uhuru mara baada ya Kiongozi wa mbio za Mwenge George Mbijima kufungua rasmi hoteli hiyo iliyopo Mbinga mjini mkoani Ruvuma. Ni Hoteli ya kisasa iliyopo Mbinga mjini mkoani Ruvuma ikiwa ni Hotel ya kwanza na ya kisasa katika wilaya hiyo
Msimamizi wa hoteli ya Kusile Restaurant and Lodge, Mary Thomas upande wa kushoto akisoma taarifa ya maendeleo juu ya ujenzi wa hoteli hiyo ya kisasa kwa Kiongozi wa mbio za Mwenge, George Mbijima wa pili kutoka kulia. Wa pili kutoka kushoto ni mmiliki wa hoteli hiyo, Verena Urio. Mradi huu umefanikiwa pia kuwawezesha wakulima wadogo wadogo 10 kuanzisha kilimo cha mboga mboga maalumu ambazo hazipatikani Mbinga, hivyo kutengeneza soko la uhakika kwa mboga mboga hizo na zile za kawaida pia imefanikiwa kutengeneza ajira 22 ambapo kati ya hizo wanawake wapo 16 na wanaume sita.
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, George Mbijimi akiondoa kitambaa ikiwa ni ishara ya ufunguzi rasmi wa hoteli ya kisasa ya Kusile Restaurant and Lodge iliyopo Mbinga mjini mkoani Ruvuma. Ambapo Kiongozi huyo wa mbio za Mwenge, aliwataka watoa huduma katika hoteli hiyo wahakikishe kwamba wanatoa huduma zinazolingana na hadhi ya jengo hilo, ili biashara wanazozifanya ziweze kuwa endelevu.Hata hivyo Mbijima amewapongeza wamiliki wa jengo hilo la biashara, kwa ubunifu walioufanya ambao utasaidia kupunguza uhaba wa nyumba ya kisasa ya kulala wageni na kuweza kupata huduma bora ya chakula.
Mkurugenzi wa kampuni ya Ovans Construction Company Limited, ambao ni wamiliki wa Kusile Restaurant and Lodge, Valence Urio akimwelekeza kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa 2016 George Mbijima
Mkurugenzi wa Kusile Restaurant and Lodge akisalimiana na kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa 2016 George Mbijima. Hotel hiyo ipo mkabara na stand kuu ya Mabasi mjini Mbinga.Kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana nao 067 609 660/ 0784 609 660. (picha zote na ruvumahabari.blogspot.com)

Naibu Waziri akutana na Ujumbe wa UNDP

0
0

MPI3Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mh. Luhaga Mpina akimkaribisha Bi. Awa Dabo Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa. Mazungumzo baina yao yamefanyika leo Mtaa wa Luthuli, jijini Dar es Salaam.
MPI1Ujumbe kutoka Shirika la Maendeleo ya Umoja wa Mataifa, kutoka kushoto ni Bw. Nehemia Murusuri, Bi. Getrude Lyatuu na Bi. Awa Dabo, walipomtembelea Naibu Waziri Mh. Luhaga Mpina hii leo.
MPI2Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mh. Luhaga Mpina akiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe wa kutoka Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa na Wataalamu kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais mara baada ya mazungumzo baina yao.
…………………………………………………………………………………………………
Na Lulu Mussa
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mh. Luhaga Mpina hii leo amefanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Bi. Awa Dabo pamoja na ujumbe aliombatana nao, Ofisini kwake Dar es Salaam.

Katika mazungumzo yao ujumbe huo umeonyesha nia ya kufanya kazi kwa karibu na Ofisi ya Makamu wa Rais hususan katika nyanja ya Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira ikiwa ni pamoja na kupambana na mabadiliko ya Tabianchi na nishati mbadala.

Awali Naibu Waziri Mpina aliwafahamisha kuwa Ofisi yake imeandaa Mpango Mkakati wa Kitaifa wa kupanda miti nchi nzima na kuwataka wadau wa maendeleo kuwaunga mkono. “Tunaendelea na jitihada za kupanda Miti mingi iwezekanavyo na katika mwaka huu wa fedha Serikali imetenga fedha kwa ajili ya kazi hiyo” alisisitiza Naibu Waziri Mpina.

Aidha, Naibu Waziri Mpina ametoa wito kwa wadau wengine wa maendeleo kujitokeza kuunga mkono kampeni hii kubwa ya upandaji miti nchi nzima na kusisitiza kuwa uhai wa viumbe vyote unategema Mazingira hivyo ni vema kuyahifadhi na kuyalinda kwa faida ya vizazi vya sasa na vijavyo.

Mheshimiwa Mpina pia amesema Ofisi yake kwa sasa inafanya marekebisho ya Sera ya Mazingira na kujenga uwezo kwa watendaji wa ngazi zote juu ya kusimamia Sheria ya Mazingira ya mwaka 2004 pamoja na kuelimisha Umma juu ya kampeni ya Usafi ya kila mwisho mwa mwezi.

kwa upande wake Bi. Dabo amesema kuwa shirika lake limeweka vipaumbele vya kutekeleza ndani ya miaka mitano ambavyo vinaendana na Mpango wa Maendeleo wa Taifa, sambamba na kusaidia vikundi mbalimbali katika ngazi za vijiji juu ya kutunza vyanzo vya maji na kuhifadhi mazingira.

Bi Dabo ameahidi kushirikiana na Ofisi ya Makamu wa Rais katika jitihada za  kukabiliana na changamoto za Mabadiliko ya Tabianchi.

SERIKALI: MFUMO WA MALIPO YA UZEENI UPO MBIONI KUANZA

0
0

MIU1 
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akifuatilia neno la ukaribisho alipofungua Mkutano Mkuu wa mwaka wa Mtandao wa Asasi zinazojishughulisha na Wazee Tanzania katika ukumbi wa Maktaba Kuu ya mkoa wa Dodoma juzi.
MIU2 
Baadhi ya wazee wa Mkoa wa Dodoma wakijitambulisha kwa Waziri wakati wa Mkutano huo.
MIU3 
Msoma risala ya wazee wote wa Tanzania Bi Clotrida Kokupima kutoka wilaya Kasulu Mkoani Kigoma akisoma risala hiyo.
MIU4Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akitoa hotuba yake alipofungua Mkutano Mkuu wa mwaka wa Mtandao wa Asasi zinazojishughulisha na Wazee Tanzania katika ukumbi wa Maktaba Kuu ya mkoa wa Dodoma juzi.
MIU5 
Wazee wakifuatilia hotuba ya Waziri
MIU6 
Baadhi ya wazee wakiwa katika mkutano huo.
MIU7Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiteta jambo na Mganga Mkuu wa Manispaa ya Dodoma Dkt. Tom Mtoi mara baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa mwaka wa Mtandao wa Asasi zinazojishughulisha na Wazee Tanzania katika ukumbi wa Maktaba Kuu ya mkoa wa Dodoma juzi.

Ramadhani Juma, OFISI YA MKURUGENZI DODOMA

SERIKALI imesema mchakato wa kuwaingiza wazee wote wasio katika ajira rasmi hapa nchini kwenye mfumo wa malipo ya uzeeni uko katika hatua za mwisho na kwamba wakati wowote kundi hilo litaanza kunufaika na mpango huo.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati akizungumza na wazee mkoani Dododma alipofungua Mkutano Mkuu wa mwaka wa asasi zinazojishughulisha  na wazee Tanzania katika ukumbi wa Maktaba Kuu ya Mkoa wa Dodoma juzi.

Alisema wazee wasio katika ajira rasmi wamefanya mambo makubwa katika maendeleo ya nchi kwa muda mrefu sasa hivyo sio sahihi kuachwa nje mfumo wa pensheni ya uzeeni na kwamba sasa ni wakati muafaka kutambua uwepo wao na mchango mkubwa katika uchumi wa Taifa.

Amebainisha kuwa, Serikali ya awamu ya tano chini ya Mh. Rais Dkt. John Magufuli haitashindwa kuwahudumia wazee wa nchi hii ambao idadi yao kwa sasa inakadiriwa kuwa milioni 2.5 na kwamba hilo ni kundi kubwa ambalo halipaswi kutengwa.

Waziri Ummy Mwalimu pia ametoa agizo kwa Halmashauri zote nchini kutenga vyumba maalum kwa ajili ya kuwapatia huduma za afya wazee na kuondokana na dhana ya ‘dirisha la wazee’ huku akiimwagia sifa Halmashauri ya Wilaya Magu Mkoani Mwanza kwa kuonesha mfano huo na kwamba wilaya nyingine ziige hatua hiyo.

Katika hatua nyingine Waziri huyo ametoa wito kwa taasisi za fedha nchini kuwaamini na kutoa mikopo kwa wazee badala ya kuwaona kama kundi lisiloweza kuzalisha kwani mzee anaweza kufanya shughuli za kuichumi hata akiwa na umri wa miaka 75 hadi 80.

“Wazee wengi wameendelea na shughuli za kuzalisha mali hadi wanafikia umri wa 75 hadi 80 hivyo mabenki yasiwatenge wazee katika kuwawezesha kimitaji ili waendelee na uzalishaji” alisema.

Bodi ya Wakala wa Uagizaji wa Mafuta kwa pamoja nchini (PBPA) yazinduliwa jijini Dar leo

0
0

 BP2 
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati anayeshughulikia Nishati,Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo wapili kushoto, akimkabidhi vitendea kazi, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja ( PBPA) Dkt. Steve Mdachi( wa pili kulia) wanao shuhudia ni mjumbe wa bodi hiyo Salum Mnuna( kulia) na Mkurugenzi wa PBPA Michael Mjinja( kulia)
BP3 
Wajumbe wa Bodi ya PBPA pamoja na watendaji wengine wa Wizara ya Nishati na Madini wakiwa pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulia Nishati Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo ( katikati) mara baada ya kuzindua rasmi bodi hiyo.
BP1 
Baadhi ya wafanyakazi wa PBPA wakifuatilia uzinduzi wa bodi yao katika ukumbi wa mikutano wa Wakala huyo jijini Dar es salaam hivi karibuni.

Na Zuena Msuya, Dar es salaam
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo amezindua Bodi ya Wakala wa Uagizaji wa Mafuta kwa pamoja  nchini (PBPA).

Akizungumza mara baada ya kuzindua Bodi hiyo jijini Dar es salaam, Dkt Pallangyo alisema kuwa PBPA inapaswa kufanya kazi kama ilivyoelekezwa ili kuleta ufanisi kwa taifa.

Alisema kuwa Bodi hiyo imeaminiwa na ndiyo maana imepewa dhamana ya kusimamia Wakala wa Uagizaji wa Mafuta kwa pamoja nchini, hivyo ni vyema kuthibitisha uaminifu huo kwa kufanya kazi kwa kiwango kinachotakiwa.

Wakala huo ulianzishwa rasmi mwaka 2015 kwa lengo la kusimamia usalama wa mafuta ya Petroli, Diseli, Mafuta ya ndege JET na Mafuta ya taa; Pia, kuhakikisha uwepo wa mafuta nchini wakati wote na kuhakikisha kuwa wale wote walioagiza mafuta wanapata  malipo stahiki na kwa wakati.

Aidha Dkt Pallangyo alisema kuwa bodi hiyo inapaswa kumshauri Waziri wa Nishati na Madini juu ya muundo mzima la uagizaji mafuta kwa pamoja ili kuongeza ufanisi wa huduma hiyo.Majukumu menhine ni kusimamia mapato na matumizi ya wakala huyo, ajira, usalama kazini na miongozo yote inayohusu PBPA.Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi husika Dkt. Steve Mdachi aliahidi kuwa hawataingusha Serikali na pia watatimiza kile kilichokusudiwa ili kuleta tija na ufanisi kwa taifa.

Dkt. Mdachi alisema kuwa kazi yao ya kwanza ni kuhakikisha kuwa wafanyakazi wa PBPA wanakuwa katika mazingira mazuri na bora ya kazi ili waweze kutimiza majukumu yao kwa viwango vinavyotakiwa.Bodi ya PBPA imeteuliwa na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo hivi karibuni na itaongozwa na wajumbe watano akiwemo Mwenyekiti pamoja na wajumbe wanne.

BARABARA DODOMA MAYAMAYA KUKAMILIKA OKTOBA MWAKA HUU

0
0

UJE4Muonekano wa Sehemu ya barabara ya Mayamaya-Mela-Bonga yenye urefu wa  (KM 188.15) ambapo ujenzi wake kwa kiwango cha lami unaendelea.
UJE5 
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng.Joseph Nyamhanga (Wa Kwanza), akikagua moja ya daraja lililopo katika Barabara ya Mayamaya-Mela-Bonga (KM 188.15) ambapo Ujenzi wake umekamilika.
UJE6 
Mhandisi Mkazi wa Ujenzi Barabara ya Mayamaya-Mela-Bonga (KM 188.15) Eng. Kini Kuyonza (Wa nne) akitoa maelezo  juu ya Ujenzi wa  Moja la daraja lililopo katika barabara hiyo kwa Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Wa pili, Eng. Joseph Nyamhanga wakati wa ukaguzi wa barabara hiyo Mkoani Dodoma.
UJE1 
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng.Joseph Nyamhanga (Wa pili kushoto) akipata maelezo juu ya Ujenzi wa Barabara ya Dodoma –Mayamaya (KM 43.65) Kutoka kwa Meneja wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) Mkoa wa Dodoma  Eng. Leonard Chimagu( Wa tatu kushoto), wakati wa ukaguzi wa barabara hiyo Mkoani Dodoma.
UJE2 
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamhanga (Wa pili kushoto) akitoa maelekezo kwa Meneja wa Wakala wa Brabara Nchini (TANROADS), Eng. Leonard Chimagu (Wa tatu kulia), Juu ya Ujenzi wa barabara ya Dodoma-Mayamaya (KM 43.65) Mkoani Dodoma
UJE3 
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamhanga (Mwenye Suti), akisoma taarifa ya Ujenzi wa Barabara ya Mayamaya-Mela-Bonga (KM 188.15) wakati alipokagua ujenzi wa barabara hiyo Mkoani Dodoma. Kulia ni Meneja wa Wakala wa barabara Nchini (TANROADS) Mkoa wa Dodoma Eng. Leonard Chimagu.


………………………………………

Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Eng. Joseph Nyamhanga amemuagiza Mkandarasi anayejenga Barabara ya Dodoma –Mayamaya yenye urefu wa KM 43.65 kumalizia kipande cha barabara ya kutoka Dodoma hadi Msalato yenye urefu wa KM 8 ifikapo Oktoba mwaka huu.

Eng. Nyamhanga ametoa agizo hilo Mkoani Dodoma alipokuwa akikagua ujenzi wa barabara ya Dodoma –Mayamaya (KM 43.65), Mayamaya –Mela –Mela –Bonga (KM 188.15) ambapo ujenzi wake kwa kiwango cha lami unaendelea.“Hakikisheni mnakamilisha ujenzi wa kipande hiki cha KM 8 kutoka Dodoma hadi Msalato mapema kabla ya Oktoba mwaka huu”. amesema Eng. Nyamhanga.

Aidha, Eng. Nyamhanga amewataka Makandarasi wote wanaotekelea Miradi ya Ujenzi wa Barabara nchini kuongeza kasi ya ujenzi ili kuweza kukamilisha ujenzi wa barabara hizo kwa wakati ili zianze kutumika na kuleta maendeleo kwa wananchi.

Amesema kuwa barabara hizi ni Kiungo muhimu cha Miundombinu ya Barabara Tanzania kwani inaunganisha mikoa maarufu ya Kilimo ya Nyanda za juu kusini, Nyanda ya kati na Nyanda za kaskazini za mikoa ya Manyara na Arusha na pia ni kiungo kikuu kwenda nchi za SADC kupitia Dodoma.

Eng. Nyamhanga ameongeza kuwa Serikali kupitia Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) itaendelea kusimamia Ujenzi wa barabara hizo ili kuhakikisha zinajengwa kwa ubora unaotakiwaa kulingana na thamani ya fedha ili ziweze kudumu kwa muda mrefu.

“Sisi kwa upande wa Serikali kupitia wakala wetu TANROADS tutahakikisha barabara hizi zinajengwa kwa ubora unaotakiwa ili zidumu kwa muda mrefu”. amesisitiza Eng.Nyamhanga.Aidha, Eng. Nyamhanga amewaomba wakazi walio karibu na Miradi hiyo ya ujenzi wa Barabara hizo kushirikina na Makandarasi kwa kulinda vifaa vinavyotumika kwa ajili ya ujenzi kwani barabara hizo zinajengwa kwa faida na matumizi ya wananchi wote.

“Serikali inajenga barabara hizi kwa ajili ya wananchi wote hivyo ni vema mkashirikiana na Makandarasi wetu kwa kutunza vifaa vya ujenzi”.amesisitiza Eng. Nyamhanga.Naye Mkandarasi wa kampuni ya Sinohydro Coropration anayejenga sehemu ya barabara ya Dodoma-Mayamaya yenye urefu wa (KM 43.65) Eng. Zeng Yun amemuhakikishia Katibu mkuu huyo kuwa ujenzi wa Barabara hiyo utakamilika kwa wakati uliopangwa.

Barabara ya Dodoma –Mayamaya, Mayamaya –Mela-Bonga yenye urefu wa (KM 188.15) ni sehemu ya Barabara ya Kuu ya Kaskazini (The great North Road) kutoka Iringa kwenda Arusha kupitia Mikoa ya Dodoma na Manyara.

INTERNEWS yawafunda waandishi sheria ya ardhi

0
0
ai1MWANASHERIA kutoka taasisi ya HAKIARDHI jijini Dar es Salaam Mafole Baraka, akitoa somo kuhusu sheria ya ardhi ya Tanzania kwa waandishi wa habari katika mafunzo yaliyoandaliwa na Shirika la Kimataifa, INTERNEWS na kufanyika Wanyama Hotel, Sinza Dar es Salaam kuanzia Juni 8 hadi 9, 2016.
ai3MSIMAMIZI Mkuu wa INTERNEWS Bi. Alakok Mayombo (wa pili kushoto mstari wa mbele) na Mkurugenzi wake Wence Mushi (kushoto kwake), wakiwa katika picha ya pamoja na waandishi walioshiriki mafyunzo yahusuyo gesi, mafuta ba haki ya ardhi jijini Dar es Salaam.
ai2MKURUGENZI Mkuu wa Shirika la INTERNEWS Tanzania Wence Mushi, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari waliopata mafunzo juu ya rasimali za gesi, mafuta na haki ya ardhi katika Wanyama Hotel jijini Dare es Salaam kuanzia Juni 8 hadi 9, 2016. (Picha na Salum Vuai-Maelezo, Zanzibar).

Na Salum Vuai, DAR ES SALAAM
MIGOGORO mingi ya ardhi inayotokea sehemu mbalimbali nchini Tanzania, husababishwa na kutoeleweka kwa sheria ya ardhi miongoni mwa wananchi wengi.

Mwanasheria kutoka taasisi ya HAKIARDHI ya Dar es Salaam Mafole Baraka, amesema katika mafunzo ya waandishi wa habari yaliyofanyika Wanyama Hotel jijini humo, kwamba watu wengi hujikuta wakipoteza haki zao kirahisi, kwa kuwa hawaelewi chochote kuhusu sheria hiyo.

Katika mafunzo hayo ya siku mbili yaliyoandaliwa na shirika la kimataifa la kuwainua waandishi wa habari (INTERNEWS), Baraka alisema migogoro hiyo imekuwa ikisababisha ugomvi kati ya wanafamilia, wanavijiji na halmashauri za maeneo husika.Aliyataja baadhi ya mambo yanayoibua migogoro kuwa ni pamoja na kujitokeza kwa kadhia nyingi za ardhi kuuzwa zaidi ya mara moja, na wakati mwengine viongozi wa familia kuamua kuuza bila kushirikisha wenzao.  

Alifahamisha kuwa kuundwa kwa taasisi ya HAKIARDHI kumelenga kusaidia kupunguza migogoro ya aina hiyo kama si kuyamaliza kabisa.Alibainisha baadhi ya mafanikio yaliyopatikana na taasisi yake katika kupunguza migogoro hiyo kuwa na kuweza kushawishi uundaji wa mabaraza ya ardhi ya vijiji, kusuluhisha baadhi ya migogoro, huku kesi nyengine zikiwa zinaendelea katika mahakama mbalimbali.

Aidha alisema hadi sasa wamefanikiwa kuvifikia zaidi ya vijiji elfu mbili, na kwamba wananchi wameelimika vya kutosha na kuweza kudai na kutetea haki zao mara baada kupata elimu juu ya sheria za ardhi.“Si hayo tu, bali pia tumefanikiwa kushawishi watunga sera kuziimarisha sheria za ardhi ikiwemo kutajwa kwenye rasimu ya katiba mpya,” alieleza mwanasheria huyo.Hata hivyo, alisema kumekuwa na changamoto kadhaa ikiwemo ya kifedha, ambayo inahitajika ili malengo ya taasisi kuifikia nchi nzima yaweze kufanikiwa.

Baraka alisema mbali na hayo, utashi wa kisiasa nao umekuwa ukichangia sana kuendelea kwa migogoro mingi ya ardhi.Ili kuipatia ufumbuzi migogoro hiyo, alishauri kuendelea kutolewa elimu kwa wananchi, kuheshimu sheria za ardhi, kupima maeneo na kuviimarisha vyombo vya utatuzi wa migogoro hiyo.

Mapema, Mkurugenzi wa INTERNEWS Tanzania Wence Mushi, alisema ni jukumu la waandishi wa habari kutumia taaluma yao kuibua na kuelekeza njia ya kumaliza changamoto mbalimbali zinazowagusa wananchi ikiwemo migogoro ya ardhi.Alisema tasnia ya habari ina nafasi kubwa ya kuleta mabadiliko chanya katika nchi yoyote, hivyo ni vyema wajikite katika kufanya uchunguzi na kuandika kadhia za aina hiyo, pamoja na mafanikio yanayopatikana baada ya mamlaka za juu kuzinduka kutokana na taarifa zinazoandikwa.

Katika siku ya kwanza ya mafunzo hayo, mkufunzi kutoka taasisi ya FAWOPA (Faidika Wote Pamoja) Balthazar Komba, alizungumzia kwa kina kuhusu miradi ya gesi nchini, changamoto zake na matumaini ya Watanzania kushuhudia matunda ya nishati hiyo.

Akitoa shukurani kwa niaba ya washiriki wenzake, mwandishi wa kituo cha televisheni cha Chanel Ten David Ramadhan, alisema mafunzo waliyopata yamewapa uelewa kubwa juu ya namna ya kuripoti masuala mbalimbali yanayogusa maslahi ya umma na taifa.Alisema hiyo ni hatua muhimu na kuahidi kuwa wataongeza jitihada  katika kuibua na kuandika mambo tofauti yanayohitaji kupatiwa majibu kwa lengo ya kuinua maisha ya Watanzania.

Best Nasso - "Ukweli Uko Wapi?"

0
0

Halmashauri ya Mji wa Kibaha yakamilisha miradi mitano ya maji

0
0
Na Lilian Lundo –Maelezo.
10/06/2016

Halmashauri ya Mji wa Kibaha imeeleza kuwa upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama kwa wakazi  wa mji huo kwa sasa  ni asilimia 56 kupitia miradi mbalimbali inayotekelezwa na Halmashauri hiyo.

Akiongea kwa njia ya simu Afisa Habari wa Halmashauri hiyo Bw. Innocent Byarugaba amesema kuwa Halmashauri ina jumla ya miradi 11 ya maji ambayo mitano imekamilika na sita iliyobaki iko katika hatua za mwisho.

“Maji safi na salama yanapatikana kwa asilimia 56 ikiwa ni juhudi za Halmashauri za kukabiliana na tatizo la maji na mpaka sasa miradi mitano imekamilika ambayo hutoa huduma ya maji kwa wananchi,” alisema Bw. Byarugaba.

Katika kuhakikisha huduma ya upatikanaji wa maji unakuwa bora zaidi, Byarugaba amesema kuwa jitihada za kukamilisha upatikanaji wa maji unafikia asilimia 100 ambapo wanaendelea kukamilisha miradi mbalimbali inayofanywa na Halmashauri hiyo.

Aliongeza kwa kutaja miradi iliyokamilika kuwa ni pamoja na Mradi wa maji Mtaa wa kwa mfipa Galagaza kata ya Msangani, Vikawe kata ya Pangani, Sagale kata ya Viziwaziwa, Zojosa kata ya Misugusugu na Mwanalugali kata ya Tumbi.

Aidha alianisha miradi mingine ya maji inayotegemewa kukamilika kwa mwaka wa fedha 2016/17 kuwa ni mtaa wa Sofu kata ya Sofu, Muheza kata ya Mailimoja, Kibenge kata ya Msangani, Kibugalo kata ya Visiga, Kalabaka kata ya Misugusugu na Mikongeni kata ya Viziwaziwa.

Bw. Byarugaba alitoa wito kwa kuwataka wananchi kuwafichua watu wanaokata mabomba ya maji na kujiunganishia maji kinyemela kwani kwa kufanya hivyo kunapunguza kasi ya maji na kusababisha watu wengine kukosa maji.

Rais Dkt John Pombe Magufuli awaapisha Majaji wawili June 10, 2016

0
0

Makonda kuzindua maonyesho ya kwanza ya simu Original (Simu Expo).

0
0
Na Daudi Manongi-MAELEZO.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe.Paul Makonda atazindua maonyesho ya kwanza ya simu original katika viwanja vya Posta jumamosi ya Tarehe 11 mwezi huu kuanzia saa 3 asubuhi mpaka saa 12 jioni.

Lengo kuu la kufanyika kwa maonyesho hayo ni kuwapa elimu wateja wa simu kujua ipi ni simu fake na ipi ni original kutoka kwa makampuni hayo ya simu,pia kwa kushirikiana na TCRA watatoa elimu kuhusu matumizi sahihi ya simu na mitandao ya kijamii.

Lengo la tatu ni kuhakikisha wateja wanajipatia simu original kwa bei nafuu kabla ya simu fake kuzimwa tarehe 16 mwezi huu.Nae Kaimu Katibu mtendaji wa Baraza la watumiaji wa huduma za mawasiliano(TCRA-CCC),Mary Msuya amewashauri watumiaji wa simu nchini kununua simu katika maduka ya simu na kuomba risiti ya dhamana ya muda wa matumizi ya bidhaa usiopungua miezi 12.

Aidha aliwataka wafanyabishara wasio waaminifu kuacha mara moja kuingiza bidhaa feki nchini kwa njia za panya kwani serikali iko makini katika kusimamia suala hilo.Kwa upande wake mwakilishi wa makampuni ya simu Meneja mauzo wa kampuni ya Tecno Bw.Fred Kadilana ametoa wito kwa watumiaji wa simu kuja kwa wingi ili kujipatia simu zenye ubora wa hali ya juu kutoka kampuni mbalimbali.

Wateja wa simu za mkononi watajipatia simu original kutoka katika maonyesho hayo kwa bei nafuu kutoka kwa makampuni ya simu ya Samsung,Tecno,Startimes,Huawei na Itel uku kukiwa na ushiriki wa makampuni ya simu ya Vodacom,Tigo na TTCL.

Katika maonyesho hayo Taasisi mbalimbali za serikali zitashiriki kama mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA), Baraza la ushauri la watumiaji wa huduma za mawasiliano (TCRA-CCC) na Mfuko wa mawasiliano kwa wote (UCSAF).

NIDA YAANZA KUTOA VITAMBULISHO VYENYE SAINI

0
0

Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini kutoka Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) Bi. Rose Mdami akiwaeleza waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu zoezi la utoaji wa vitambulisho vipya vyenye saini ya mwenye kitambulisho. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Uzalishaji Vitambulisho Bw. Alphonce Malibicha na kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mifumo ya Kompyuta Bw. Mohamed Khamis.
Kaimu Mkurugenzi Mifumo ya Kompyuta Bw. Mohamed Khamis akifafanua kwa waandishi wa habari kuhusu faida za vitambulisho vya taifa leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Uzalishaji Vitambulisho Bw. Alphonce Malibicha na kushoto ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Bi. Rose Mdami.
Baadhi ya waandishi wa habari wakiangalia video ya faida za vitambulisho vya Taifa iliyoandaliwa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kwa ajili ya kuelimisha umma kwenye mkutano wa Mamlaka hiyo na waandishi wa habari uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.Picha na Fatma Salum (MAELEZO).


Frank Mvungi-Maelezo

Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imeanza kutoa vitambulisho vya Taifa vyenye saini ya mwombaji kuanzia mwezi Juni mwaka huu.

Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Mamlaka hiyo Bi. Rose Mdami wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam. 

Akifafanua Mdami alisema kuwa lengo la Mamlaka hiyo ni kuhakikisha kuwa Watanzania wote wanapata vitambulisho vya Taifa ambapo katika hatua ya kwanza mamlaka hiyo inachakata taarifa za wananchi walizotoa wakati wa kujiandikisha kwenye Daftari la Wapiga Kura kipindi cha Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana.Utoaji wa vitambulisho hivi vyenye saini ya mwombaji utasaidia kuwatambua wahusika pale wanapohitaji huduma mbalimbali za kijamii. 

“Upatikanaji wa vitambulisho vyaTaifa utasaidia Serikali kuondokana na tatizo la Watumishi hewa kwa kuwa mfumo wetu utaunganishwa na mifumo mingine inayosimamia utumishi wa umma” alisisitizaMdami. 

Utoaji huo wa vitambulisho utaanza kwa kutoa namba za utambulisho kwa wananchi ilizisaidie katika upatikanaji wa huduma mbalimbali wakati mchakato wa kuzalisha vitambulisho hivyo ukiendelea.Mdami alifafanua kuwa baada ya kuchakata taarifa kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi zitarudishwa kwenye mitaa na vijiji husika kwa ajili ya uhakiki wa taarifa hizo.

Lengo la Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa ni kuhakikisha kuwa ifikapo Desemba mwaka huu wananchi wote wawe wamepatiwa namba ya utambulisho .

MAADHIMISHO YA SIKU YA WACHANGIA DAMU DUNIANI KUFANYIKA KITAIFA MKOANI DODOMA

0
0
 .       Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya siku ya wachangia damu duniani yanayotarajia kufanyika tarehe 14 Juni mwaka huu. Maadhimisho hayo kitaifa yanatarajia kufanyika mkoani Dodoma. Kushoto ni Meneja Uendeshaji wa Mapngo wa Taifa wa damu salama, Dkt. Abdu Juma.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya siku ya wachangia damu duniani yanayotarajia kufanyika tarehe 14 Juni mwaka huu. Maadhimisho hayo kitaifa yanatarajia kufanyika mkoani Dodoma. Kushoto ni Meneja Uendeshaji wa Mapngo wa Taifa wa damu salama, Dkt. Abdu Juma na kulia ni Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Caroline Damian.(PICHA NA ISMAIL NGAYONGA- MAELEZO)


Watanzania waombwa kushiriki siku ya Mtoto wa Afrika.

0
0
Lilian Lundo – MAELEZO

Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imewataka watanzania kushiriki kikamilifu katika maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika yanayoadhimishwa Juni 16, kila mwaka.

Kupitia taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Sihaba Nkinga imeeleza kuwa lengo la maadhimisho hayo ni kuwa na siku maalum ya kuelimisha na kuwakumbusha wazazi, walezi na wadau mbalimbali kuitikia utekelezaji wa wajibu na majukumu yao katika kuwapatia watoto haki zao za msingi.


“Tarehe 16 Juni ya kila mwaka, ni kilele cha maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika, katika siku hii, Tanzania inaungana na nchi nyingine wanachama wa Umoja wa Afrika kuadhimisha siku hii kwa mujibu wa Azimio lililopitishwa na nchi 51 za Umoja huo mwaka 1990,” imefafanua taarifa hiyo.

Aidha taarifa hiyo imeeleza kuwa Azimio hilo lilipitishwa kwa ajili ya kukumbuka mauaji ya watoto wa shule yaliyofanyika katika kitongoji cha Soweto, Afrika ya Kusini Juni 16, 1976, ambapo watoto wapatao 2,000 waliuawa kikatili na Makaburu wakiwa katika harakati za kutetea haki zao za msingi za kutobaguliwa kutokana na rangi yao.

Katika siku hiyo watoto hupata nafasi maalum ya kujieleza, kusikilizwa, kushirikina kuonyesha vipaji vyao mbele ya wazazi, walezi na jamii kwa ujumla. Watoto wanahaki ya kuishi, kulindwa, kuendelezwa, kushiriki na kutobaguliwa

Kauli mbiu ya maadhimisho hayo kwa mwaka huu ni “Ubakaji na Ulawiti kwa Watoto Vinaepukika: Chukua Hatua Kumlinda Mtoto.”
Viewing all 46205 articles
Browse latest View live




Latest Images