Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 874 | 875 | (Page 876) | 877 | 878 | .... | 1903 | newer

  0 0

  Kutokana na kudaiwa deni la zaidi ya mil 100 kanisa la Sinza Christian Center  latupiwa nje vyombo vyake na dalali aliyepewa tenda hiyo bwana Joshua aliyeteuliwa na Mahakama na mmiliki jengo hilo Bwana Prosper Rwendera , akizungumza na Dar es salaam yetu Blog  mke wa mmiliki  wa jengo Hilo Bi. Patricia Prosper Alisema; “huyu aliyepanga hapa hakufuata utaratibu wowote na ndiyo maana tukapewa jengo letu." 
  Alipotafutwa msemaji wa Kanisa ambaye ni Askofu anayedaiwa kuvamia jengo hilo, hakupatikana kuzungumzia sakata hilo na hata waumini wa kanisa hilo walipotafutwa walikataa kwa madai hawana mamlaka ya kuzungumzia lolote kuhusiana na sakata hilo.
  Hili ni eneo la Kanisa Hilo
  Viti  vyote vikiwa vimetolewa nje
   Vyombo vya Muziki vikiwa nje
   Magari yakiwa yanatolewa nje
   Vitu vikiwa nje ya Jengo hilo ambapo mpaka sasa kuna sinto fahamu vinapelekwa wapi
   Vikombe nje
   Wametoa vitu vyote
  Magodoro na vitanda vyote nje  
   Baadhi ya Magari yaliyotolewa katika Jengo hilo ambapo hapo awali ilikuwa ni Kanisa
  Kushoto kwa mbali ni Mke wa Mmiliki wa Jengo hilo Bi. Patricia Prosper akiendelea na majukumu huku pembeni vijana wakipata maelekezo ya kuendelea kutoa vitu.
   Picha zote na Fredy Njeje/ Blogs za Mikoa

  0 0

   Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(katikati)akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salam leo(hawapo pichani)wakati wa Uzinduzi wa  Promosheni ya ‘Kamata Mpunga’itakayowawezesha wateja wa mtandao huo kujishindia pesa taslimu kuanzia shilingi Milioni 1 hadi 100.Ili mteja aweze kushiriki katika promosheni hii anatakiwa kutuma neno “GO”kwenda namba 15544 aidha mteja anaweza kujiunga moja kwa moja kwa kutuma neon”WIN”kwenda namba 15544 na mteja atapata ujumbe wa kujibu maswali,Kushoto ni Mkuu wa kitengo cha huduma za ziada wa kampuni hiyo,Saurabh Jaiswal na Meneja wa huduma za ziada,Mathew Kampambe.
   Mkuu wa kitengo cha huduma za ziada wa Vodacom Tanzania,Saurabh Jaiswal(kushoto)na Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo,Matina Nkurlu,wakimsikiliza Meneja wa huduma za ziada wa kampuni hiyo,Mathew Kampambe(kulia)akifafanua jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani)kuhusiana na Uzinduzi wa Promosheni ya ‘Kamata Mpunga’ jijini Dar es Salaam leo itakayowawezesha wateja wa mtandao huo kujishindia pesa taslimu kuanzia shilingi Milioni 1 hadi 100.Ili mteja aweze kushiriki katika promosheni hii anatakiwa kutuma neno “GO”kwenda namba 15544 aidha mteja anaweza kujiunga moja kwa moja kwa kutuma neon”WIN”kwenda namba 15544 na mteja atapata ujumbe wa kujibu maswali.
   Baadhi ya waandishi wa habari na wafanyakazi wa Vodacom Tanzania,wakiwa kwenye mkutano wa Uzinduzi wa Promosheni ya ‘Kamata Mpunga’ jijini Dar es Salaam leo itakayowawezesha wateja wa mtandao huo kujishindia pesa taslimu kuanzia shilingi Milioni 1 hadi 100.Ili mteja aweze kushiriki katika promosheni hii anatakiwa kutuma neno “GO”kwenda namba 15544 aidha mteja anaweza kujiunga moja kwa moja kwa kutuma neon”WIN”kwenda namba 15544 na mteja atapata ujumbe wa kujibu maswali.


  0 0


  Mkurugenzi wa fedha toka benki ya Posta Tanzania (TPB) Bi.Regina Semakafu akifurahi jambo na baadhi ya walimu na wanafunzi wa shule ya sekondari Mbeya Day jijini Mbeya mara baada ya kukabidhi madawati thelathini yenye thamani ya shilingi milioni moja na laki tano kama sehemu ya mchango wa benki hiyo katika sekta ya elimu June 8- 2015. (Picha zote na Emmanuel Madafa)
  Mwalimu Mkuu wa shule ya sekondari Mbeya Day (kushoto) Bi Magreth Haule akimshukuru Mkurugenzi wa fedha toka benki ya posta, Rigina Semakafu kwa msaada wa madawati thelathini yaliyotolewa na benki hiyo, hafla ambayo imefanyika katika viwanja vya shule hiyo june 8 mwaka huu.

  Mkurugenzi wa fedha benki ya Posta Tanzania (TPB) Regina Semakafu (kulia) akifurahi jambo na Mwalimu mkuu wa shule ya sekondari Mbeya Day (katikati) pamoja na Meneja Benki ya Posta Tanzania Tawi la Mbeya Humphrey Julias katika hafla ya utoaji wa msaada wa madawati thelathini yenye thamani ya shilingi milioni moja na laki tano June 8 mwaka huu.
  Mkurugenzi wa fedha benki ya Posta Tanzania (TPB) Regina Semakafu akizungumza na na wanafunzi pamoja na walimu (hawapo pichani) mara baada ya kukamilisha zoezi la utoaji wa madawati kama msaada uliotolewa na benki ambapo ni thelathini .

  Meneja Benki ya Posta Tanzania (TPB) tawi la Mbeya Humphrey Julias akizungumza katika hafla ya utoaji madwati kwa shule ya hiyo ya Mbeya Day kutoka benki ya Posta Tanzania.

  Mkurugenzi wa fedha kutoka benki ya Posta Tanzania Regina Semakafu (kushoto) pamoja na uongozi wa benki hiyo Tawi la Mbeyakatika picha ya pamoja na wananfunzi wa shule hiyo ya Mbeya Day.

  0 0


  Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh. Raymond Mushi, akisaidiana na Mwenyekiti wa Banki ya Diamond Trust (DTB), Bw. Abdul Samji, kukata utepe katika uzinduzi wa tawi jipya la benki hiyo la CBD. Kushoto ni Bi. Nasim Devji Mkurugenzi Mkuu wa Benki hiyo nchini, kulia ni Mwakilishi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Hezron Gyimri. Tawi la CBD linakuwa ni tawi la 25 la benki hiyo nchini Tanzania na la 11 jijini Dar es Salaam.

  Na Imma Matukio Blog

  Benki ya Diamond Trust Tanzania, (DTB Tanzania),leo imezindua rasmi tawi la CBD lilipolo katikati ya jiji la Dar es Salaam kwenye jengo la Diamond Plaza, makutano ya barabara ya Samora na mtaa wa Mirambo. Tawi la CBD ni la ishirini na tano nchini na la kumi na moja katika jiji la Dar es Salaam.

  Tawi la CBD litafunguliwa jumatatu hadi ijumaa, saa 2:30 asubuhi hadi saa 10:30 jioni na Jumamosi saa 3:30 asubuhi hadi sa 7:00 mchana.

  Akihutubia katika hafla fupi iliyofanyika ndani ya benki, Mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mheshimiwa Raymond Mushi, alitoa pongezi kwa uongozi wa benki ya DTB Tanzania kwa ufunguzi wa takriban matawi mawili kila mwaka licha ya changamoto zinazokabili sekta ya fedha nchini na duniani kwa ujumla. Benki ya DTB imefanikiwa kufungua matawi ishirini na moja katika miji kumi na tatu ndani ya mika minane (2007 – 2016).

  “Ninawapongeza na kuwashukuru kwa jitihada zenu za kusogeza huduma za kibenki karibu na wananchi na kuwajenga watanzania kiuchumi. Enzi za kusafiri masaa kwenda kwenye benki na kisha kupanga foleni kwa muda mrefu kwa ajili ya kupata huduma za kibenki imeshapita” Ndugugu Mushi iliongeza.

  Naye mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi, Ndugu Abdul Samji, alitoa pongezi kwa menejimenti ya Benki kwa matokeo bora ya biashara ya kwa mwaka uliopita 2015, ambapo Benki ilitangaza mafanikio makubwa katika matokeo ya biashara.

  “katika ripoti hiyo, akiba za wateja zilikukua kwa asilimia 26.8% kutoka shilingi bilioni 581 mwaka 2014 hadi shilingi bilioni 737 mwaka 2015. Aidha, kulingana na ripoti za mabenki zilizotolewa kwa mwaka 2015, DTB ni benki ya sita kwa ukubwa wa amana za wateja nchini. Benki ya DTB Tanzania pia inashikilia nafasi ya 4 katika viwango vya faida katika matokeo ya biashara ya miezi mitatu ya kwanza mwaka huu.

  Taarifa hiyo inaonyesha kuwa faida kabla ya kodi mwaka 2015 ilikuwa shilingi bilioni 27.33 sawa na ongezeko la asilimia 36.03% ikilinganishwa na shilingi bilioni 20.1 mwaka 2014. Ripoti hiyo inaonyesha kuwa DTB inakua kwa kasi ukilinganishwa na ukuaji katika sekta ya kibenki nchimni.

  DTB Tanzania ina matawi 25 nchini, ikiwa na matawi kumi na moja (11) jijini Dar es Salaam (Mtaa wa Jamaat, Masaki, Morocco, Magomeni, Mbezi, Mbagala, barabara ya Nyerere, Msimbazi - Kariakoo, barbara ya Nelson Mandela, Upanga katika barabara ya umoja wa mataifa na katika makutano ya barabara ya Mirambo na mtaa wa Samora). Vile vile ina matawi katika miji ya Arusha (2), Mwanza (2) na katika miji ya Dodoma, Kahama, Mbeya, Morogoro, Moshi, Mtwara, Mwanza, Tabora , Tanga na Zanzibar.

  DTB Tanzania ni mshirika wa mtandao wa maendeleo ya kiuchumi wa Aga Khan - Aga Khan Fund for Economic Development (AKFED) ambao ni sehemu ya mtandao wa maendeleo wa Aga Khan Development Network). DTB Kenya ni miongoni mwa wanahisa muhimu wa DTB Tanzania.

  0 0

  Mwimbaji wa nyimbo za Injili nchini,Vanessa Laban, kutoka Jijini Mwanza, anatarajia kuachia Album yake mpya iitwayo "Sifa Zivume" iliyo katika mfumo wa Sauti/ Audio na Picha Nyongevu/ Video.

   Albam hiyo inasambazwa na Kampuni ya Vipaji Entertainment inayosimamiwa na Maganga Gwensaga, ambae ni Meneja wa Kituo cha Radio cha HHC Alive cha Jijini Mwanza.

  Bonyeza HAPA Au Play Hapo Chini Kusikiliza Wimbo uitwayo "Ni Kwa Neema" ulioimbwa na Vanessa Laban.

  0 0


  kwaya ya vijana wa kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Iringa wakiwa bungeni mjini Dodoma juni 8 mwaka huu baada ya kumaliza mashindano yao ya uimbaji kitaifa yaliyofanyika Kanisa la Martin Luther mjini hapa na kwaya hiyo kushika nafasi ya pili kitaifa picha na Richard Mwaikenda
  Waimbaji wa kwaya ya vijana wakiwa wamesimama wakati wakitambulishwa na naibu spika bungeni jana
  Mbunge wa jimbo la Kilolo Bw Venance Mwamoto katikati aliyevaa tai akiwa na mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati katika picha ya pamoja na waimbaji wa kwaya ya vijana KKKT dayosisi ya Iringa walipotembelea bunge Juni 8 mwaka huu (picha na Richard Mwaikenda

  0 0


  Meneja Biashara wa Bayport Financial Services, Thabit Mndeme, katikati akizungumza baada ya kumpa hati yake mteja wao wa viwanja vya Vikuruti, wilayani Kibaha, mkoani Pwani, Ibrahim D Mahinya. Kulia ni Afisa Sheria wa Bayport, Mrisho Mohamed.

  TAASISI ya Kifedha ya Bayport inayojihusisha na mikopo imeendelea kugawa hati za viwanja kwa wateja wao walionunua viwanja katika mradi wao uliopo Vikuruti, wilayani Kibaha, mkoani Pwani, uliozinduliwa rasmi mwezi Mei mwaka jana.

  Wateja waliokabidhiwa hati zao ni pamoja na Ibrahim D Mahinya na Desdery Selestine Mkenda ambao wote kwa pamoja walikuwa miongoni mwa wateja waliojiunga na huduma hiyo ya mikopo ya viwanja vya Bayport.
  Ibrahim Mahinya kushoto akizungumza jambo baada ya kukabidhiwa hati ya kiwanja cha Vikuruti, kutoka Bayport Financial Services, jijini Dar es Salaam leo asubuhi. Mwenye miwani ni Meneja Biashara wa Bayport Financial Services, Thabit Mndeme na Mrisho Mohamed, Afisa Sheria wa Taasisi hiyo inayohusisha na mikopo ya fedha na bidhaa vikiwamo viwanja.

  Akizungumza jijini Dar es Salaam katika makabidhiano hayo, Meneja Biashara wa Bayport Financial Services, Thabit Mndeme, alisema kusudio lao ni kugawa hati kwa wateja wao mapema iwezekanavyo ili kujitofautisha na wadau wengine wanaojihusisha na mambo ya uuzaji wa ardhi kwa njia mbalimbali.
  Meneja Biashara wa Bayport Financial Services, Thabit Mndeme katikati akimkabidhi hati ya kiwanja cha Vikuruti mteja wao Desdery Selestine Mkenda. Kulia ni Mrisho Mohamed, Afisa Sheria wa Taasisi hiyo inayohusisha na mikopo ya fedha na bidhaa vikiwamo viwanja.

  Alisema kwamba hati zinazotoka kwa mwaka huu ni zile zinazohusu wateja walionunua viwanja hivyo katika mradi wa Vikuruti, Mlandizi, wilayani Kibaha, mkoani Pwani, mradi uliopokewa vizuri na Watanzania, jambo lililochangia Bayport kupanua wigo huo kwa kuanzisha miradi mingine ya Bagamoyo, Kigamboni, Chalinze, Kibaha na Kilwa.
  Meneja Biashara wa Bayport Financial Services, Thabit Mndeme, akimkabidhi hati ya kiwanja cha Vikuruti, wilayani Kibaha, mkoani Pwani Ibrahim D Mahinya.
  Mteja wa kiwanja cha Vikuruti vinavyotolewa na Bayport, Ibrahim D Mahinya akizungumza jambo.
  Ibrahim Mahinya, akitia sahihi ya dole gumba kama njia ya kukamilisha utaratibu wa makabidhiano ya hati yake.
  Thabit Mndeme katikati akizungumza kwenye makabidhiano hayo ya hati za viwanja.
  Mteja wa viwanja vya Vikuruti, Desdery Mkenda kushoto akishuhudia nyaraka zinazohusiana na mambo ya hati yake aliyokabidhiwa baada ya kuwa miongoni mwa Watanzania waliojitokeza kununua viwanja vya Bayport vilivyopo Vikuruti, wilayani Kibaha, mkoani Pwani. Katikati ni Meneja Biashara wa Bayport, Thabit Mndeme na Afisa Sheria wa taasisi hiyo Mrisho Mohamed.
  eneja Biashara wa Bayport Financial Services, Thabit Mndeme, kulia akipeana mkono wa na mteja wao Ibrahim Mahinya baada ya makabidhiano ya hati yake ya kiwanja cha Vikuruti kukamilika.

  “Tumepania kuwa tofauti na wadau wengine wanaotoa huduma ya ardhi, kwa kuhakikisha mteja wetu anapata hati yake haraka na bila usumbufu wowote kwa ajili ya kumuondolea kero za ufuatiliaji wa hati.

  “Tunawaomba Watanzania waendelee kuiunga mkono Bayport kwa kuchangamkia fursa za mikopo katika miradi yetu yote ukiwamo wa Chalinze, Kigamboni, Kilwa, Kibaha na Bagamoyo ambayo vinauzwa kwa mita moja ya mraba Sh 10,000 Bagamoyo, Chalinze Sh 4500, Kibaha Sh 9000, Kilwa Sh 2000 na Kigamboni Sh 10000,” Alisema Mndeme.

  Naye Mahinya aliyekabidhiwa hati yake kutoka Bayport alisema kwamba amefurahishwa kupewa hati kwa haraka jambo ambalo ni tofauti na matarajio yake kutokana na suala hilo kuwa na mzunguuko mkubwa.

  “Nimepata hati yangu kwa haraka mno, hii ni tofauti na matarajio yangu kwa sababu nafahamu suala la hati linavyokuwa na mkanganyiko mkubwa kwa sababu linashirikisha mikono ya watu wengi na lina mambo mengi pia, ila kwa Bayport kila kitu kinakwenda vizuri, hivyo nalazimika kusema kuwa utaratibu wa kazi wa taasisi hii umenivutia,” Alisema.

  Mteja mwingine Mkenda aliwashukuru Bayport kwa kumpatia hati yake, baada ya kuwa mmoja wa Watanzania aliyejipatia viwanja vya Vikuruti vilivyozinduliwa na taasisi hiyo mwaka jana mwezi wa tano, huku huduma hiyo ya viwanja ikipatikana katika ofisi zote za Bayport.

  Mbali na mikopo ya viwanja, Bayport pia wanatoa huduma ya mikopo ya haraka ya fedha taslimu kwa watumishi wa umma na wafanyakazi wa kampuni zilizoidhinishwa, huku mikopo hiyo ikiwa haina amana wala dhamana.

  0 0

   Mratibu  Programu ya MIVARF Zanzibar ,  Khalfan Salim Masoud akifafanua masuala ya utekelezaji wa Programu hiyo  kwa upande wa Zanzibar kwa waandishi wa habari  (hawapo pichani) tarehe 09 Juni,
  2016.
   Sehemu ya barabara iliyopo kijijini Matale, Pemba iliyojengwa na Programu ya MIVARF kwa kiwango cha changarawe  ambayo wakulima wa mazao ya ndizi wanatumia kusafirisha mazao yao kuelekea eneo la soko.
  Baadhi ya wakulima wa Mkoa kusini Zanzibar wakikagua mazao ya ndimu kabla la kusafirisha mazao hayo kwenda sokoni. Usafirishaji wa mazao hayo umekuwa rahisi baada ya Programu ya MIVARF kujenga  barabara za viwango vya changarawe mkoani humo.

  Na.  Mwandishi Maalum.

  Serikali kupitia Ofisi ya waziri Mkuu chini ya Programu ya uboreshaji
  wa miundombinu ya masoko, uongezaji thamani mazao na huduma za kifedha vijijini (MIVARF) imefanikiwa kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi
  endelevu kwa  kuziwezesha kaya 63, 562 za Ungunja na Pemba kunufaika
  miundombinu ya masoko kwa  kukarabati na kujenga barabara za vijijini
  zinazotoka mashambani na kuelekea eneo la masoko.

  Programu hiyo katika kuboresha miundo mbinu ya masoko Zanzibar,
  imeweza kujenga barabara kwa kiwango cha changarawe  zenye urefu wa
  Km. 149.5, ikiwa Km. 69.1 kwa upande wa Unguja na Km. 80.4 kwa upande
  wa Pemba.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam tarehe 09
  Juni, 2016, Mratibu Mradi huo Taifa, Bw. Walter Swai amesema malengo
  ya mradi ni kufanikisha azma ya Serikali ya kupunguza umaskini na
  kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi endelevu kwa kuziwesha kaya za
  vijijini kujiongeza kipato na usalama wa chakula. Uboreshaji wa miundo
  mbinu ya masoko, umeweza kuongeza thamani mazao ya kilimo, na
  kuwajengea wananchi waishio vijijini uwezo wa kuyafikia masoko.

  “Miundo mbinu ya barabara iliyojengwa visiwani Zanzibar imewasaidia
  wakulima kupata barabara za uhakika ambazo zinapitika kwa msimu wote
  lakini pia uwepo wa barabara hizo umewasaidia wakulima kupunguza muda wa kusafirirsha mazao toka shambani hadi sokoni” alisema Swai.

  Naye mratibu wa Programu hiyo Zanzibar, Khalfan Salim, alifafanua kuwa
  Programu itahakikisha kuwa  inafanikisha malengo yake kwa kuboresha
  miundo mbinu ya masoko, kuongeza thamani mazao ya kilimo kwa ujenzi wa maghala ya kuhifadhi mazao yao kwa lengo la kuongeza mnyororo wa
  thamani wa mazao.

  “Programu ya MIVARF inaendelea kutekeleza uboreshaji wa miundo mbinu
  ya masoko hapa zanzibar kwa kujenga masoko na maghala yenye mahitaji
  maalum kwa kuwa yatakuwa na vyumba maalum vya vipozeo kwa mazao ya matunda  na mbogamboga katika hatua za mwisho” alisisitiza Salim

  Kwa nyakati tofauti baadhi ya wakulima wa visiwani Pemba na Unguja
  wanaojishughulisha na kilimo cha ndimu, mananasi , ndizi na mbogamboga
  walibainisha kuwa kabla ya ujenzi wa barabara walikuwa wanasafiriisha
  mazao hayo kwa saa moja kutoka shambani hadi sokoni lakini kwa sasa
  wanasafirisha mazao yao kwa muda wa dakika nne kufika eneo la soko.

  Mkulima wa ndizi kijijini Matale, Pemba, Said Ramadhani alifafanua
  kuwa ujenzi wa miundo mbinu ya barabara umesaidia thamani ya mazao yao kuongezeka kwa kuwa wanao uwezo wa kusafirisha mazao yao kwa usalama hivyo kuweza kuyafikisha mazao yao sokoni kwa usalama na kwa haraka bila kuharibika na kuptea shambani.

  Programu ya Miundo Mbinu ya Masoko na Huduma za Kifedha Vijijini
  (MIVARF) ni Programu ya miaka saba ambayo utekelezaji wake umeanza
  rasmi mwaka 2011. Programu hiyo inagharamiwa na serikali ya Tanzania
  ikishirikiana na Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) na
  Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB chini ya uratibu wa   Ofisi ya
  Waziri Mkuu.

  0 0

  Balozi wa Tanzania Nchini Nigeria Balozi Daniel Ole Njolaay akikabidhi hundi ya dola 2000 za Kimarekani sawa na kiasi cha zaidi ya shilingi milioni nne Mh. Dk Angelina Mabula Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za Rais Dk. John Pombe Magufuli katika kuhakikisha shule za msingi zinakuwa na madawati ya kutosha hapa nchini, Hafla hiyo ilifanyika kwenye ubalozi wa Tanzania jijini Abuja nchini Nigeria mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa Maendeleo ya Makazi jijini humo.Mh. Dk Angelina Mabula Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makaziakizungumza katika hafla hiyo huku Balozi Daniel Ole Njolaay akimsikiliza.Mh. Dk Angelina Mabula Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazipamoja na Balozi wa Tanzania nchini Nigeria Balozi Daniel Ole Njolaay wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya maofisa wa ubalizi huo na Shirika la Nyumba la Taifa NHC.Mh. Dk Angelina Mabula Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Balozi Daniel Ole Njolaay pamoja na maofisa waubalozi huo na Shirika la Nyumba Tanzania NHC wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya hafla hiyo.

  0 0


  Kaimu Kamishna wa Nishati anayeshughulikia umeme,Mhandisi Leornard Masanja( wa pili kulia) akikagua baadhi ya trasfoma zilizobiwa mafuta katika ofisi ya Tanesco wilayani Bagamoyo, kulia ni Meneja wa Tanesco Mkoa wa Pwani, Mhandisi Martin Madulu na Meneja Tanesco Wilaya ya Bagamoyo ( kushoto ) .
  Baadhi ya transfoma zilizoibwa mafuta zikiwa katika ofisi ya Tanesco Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani.
  Kaimu Kamishna wa Nishati anayeshughulikia umeme,Mhandisi Leornard Masanja( wa pili kulia) akikagua baadhi ya trasfoma zilizobiwa mafuta katika ofisi ya Tanesco wilayani Bagamoyo, kulia ni Meneja wa Tanesco Mkoa wa Pwani, Mhandisi Martin Madulu na Meneja Tanesco Wilaya ya Bagamoyo ( kushoto )

  Na Zuena Msuya, Bagamoyo Pwani

  Wizara ya Nishati na Madini imesema itaendelea kuimarisha miundombuni ya upatikanaji wa huduma ya umeme wilayani Bagamoyo mkoani Pwani ili kuondoa malalamiko ya mara kwa mara yanayotolewa na wateja.

  Kaimu Kamishna wa Nishati anayeshughulikia umeme, Mhandisi Leornard Masanja alisema hayo wilayani Bagamoyo baada ya kufanya ziara katika Ofisi ya shirika la umeme nchini (Tanesco) hivi karibuni.

  Akiwa katika ziara hiyo, Mhandisi Masanja alielezwa kuwa transfoma 56 ziliibwa mafuta na kusababisha wananchi wengi kulalamikia Tanesco kwa kuchelewa kuwapatia huduma ya umeme licha ya kukamilisha hatua zote za kuunganishwa na huduma hiyo na umeme kukatika mara kwa mara.

  Pia alielezwa kuwa, Tanesco imekuwa ikichelewa kutatua changamoto zinazowakabili wananchi wa maeneo hayo pindi inapotokea hitilafu ya umeme au kukatika kwa huduma ya umeme katika eneo fulani la Wilaya na Mkoa huo.

  Baada ya kupokea malalamiko hayo, Mhandisi Masanja aliwataka Meneja Tanesco, Mkoa wa Pwani Mhandisi Martin Madulu pamoja na Meneja wa Wilaya ya Tanesco wa Wilaya ya Bagamoyo, Mhandisi Julius Doyi kutoa ufafanizi wa namna ya kukabiliana na changamoto hizo pamoja na kutatua malalamiko hayo kutoka kwa Meneja Tanesco, Mkoa wa Pwani Mhandisi Martin Madulu pamoja na Meneja wa Wilaya ya Tanesco Wilaya ya Bagamoyo, Mhandisi Julius Doyi.

  Kwa upande wake Meneja Tanesco, Mkoa wa Pwani Mhandisi Martin Madulu, alisema kuwa malalamiko hayo yanatokana na uchache wa miundombinu hasa kwa wale wanaohitaji kuunganishiwa huduma ya umeme.

  Aidha alifafanua kuwa watumishi wachache waliofukuzwa wamekuwa wakidaiwa kuhujumu shughuli nzima za kuunganisha huduma za umeme kwa wananchi kwa kudai rushwa kwanza jambo lililokuwa likiwakatisha tamaa wananchi.

  Hata hivyo alielezwa kuwa, tayari wafanyakazi wanane wamefukuzwa kazi wilayani bagamoyo kwa makosa mbalimbali ikiwemo rushwa,matumizi mabaya ya ofisi na kuchelewesha huduma kwa wananchi.

  Naye Meneja wa Tanesco wilayani Pwani Mhandisi Julias Doyi alisema kuwa tatizo la kuchelewa kuwahudumia wananchi hasa wale wanaopata tatizo la kukatika huduma ya umeme linatokana na miundombinu mibovu ya kuwafikia wananchi hao na kuwa na Gari moja la kutoa huduma kwa wilaya nzima.

  Aliongeza kuwa Tanesco wamekuwa wakichelewa kupata taarifa kutoka kwa wananchi kutokana na wengi wao kutoa taarifa hizo kupitia Viongozi wa Serikali za mitaa na kusababisha taarifa hizo kuchelewa kuwafikia Tanesco.

  0 0

   Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya makazi, William Lukuvi akisalimiana na Mpima ardhi mkuu wa kanda ya kaskazini Nina Rutakyamirwa, alipofika wilayani Kiteto kuzindua Baraza la Ardhi na Nyumba la wilaya hiyo (kushoto) ni mkuu wa Mkoa huo, Dk Joel Bendera.
   Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya makazi, William Lukuvi akisalimiana na Kaimu Msajili msaidizi wa baraza la ardhi na nyumba wa kanda ya kaskazini Zena Happe alipofika wilayani Kiteto kuzindua Baraza la Ardhi na Nyumba la wilaya hiyo (kushoto) ni mkuu wa Mkoa huo, Dk Joel Bendera.
  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya makazi, William Lukuvi akimtambulisha kwa wananchi Mwenyekiti wa Baraza la ardhi na nyumba la Wilaya ya Kiteto Charles Mnzava, alipozindua baraza hilo.

  WANANCHI wa Wilaya ya Kiteto Mkoani Manyara waliokuwa wanasafiri kwa kilometa 320 kwenda Wilayani Simanjiro na kurudi kufuata huduma ya Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya, hvi sasa wamemaliziwa kero hiyo baada ya Wziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya makazi, William Lukuvi kuzindua Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya ya Kiteto.

  Waziri Lukuvi akizungumza wakati akizindua baraza hilo alisema, kero ya wananchi wa wilaya ya Kiteto kufuata huduma hiyo umbali wa kilometa 320 kwenda na kurudi wilayani Simanjiro ambapo kuna baraza kama hilo, ili kufungua mashauri yao kwenye masuala ya ardhi au nyumba limemalizika.

  “Baraza hilo litawasaidia wananchi wa Kiteto kuondoa kero ya kufuata huduma hiyo wilayani Simanjiro kwani kati ya kesi 150 zinazofanyika kwa mwaka wilayani Simanjiro, kesi 100 zinawahusu watu wa wilaya ya Kiteto,” alisema Lukuvi.

  Alisema mpango wa matumizi bora ya ardhi utasababisha wakulima na wafugaji kutogombana kwani kila kijiji kitatenga eneo la mashamba, malisho ya mifugo, makazi, sehemu za ibada na huduma nyingine na kuondokana na migogoro.

  Kwa upande wake, mkuu wa mkoa wa Manyara, Dk Joel Bendera alisema baraza hilo litasaidia kumaliza tatizo la migogoro ya ardhi iliyokithiri kwani awali wananchi wengi walikuwa wanafika mjini Babati kutoa malalamiko yao ya migogoro ya ardhi.

  Dk Bendera aliwataka Mwenyekiti wa baraza hilo la Kiteto Charles Mnzava na wazee wa baraza kutenda haki kwa wananchi wa Kiteto wakati wa kuendesha mashauri hayo ili jamii ione faida ya kuwepo kwa baraza hilo.

  Hata hivyo, Mbunge wa jimbo la Kiteto, Emmanuel Papian alimshukuru Waziri Lukuvi kwa kuzindua baraza hilo kwani litasaidia kwa namna moja au nyingine kumaliza migogoro ya ardhi ambayo ilikuwa imekithiri kwenye eneo hilo la Kiteto.

  Papian alisema kupitia baraza la ardhi na nyumba hapa Kiteto huo ndiyo utakuwa mwisho wa kuwepo kwa migogoro ya ardhi kwani awali walikuwa wanateseka kwenda Simanjiro kwani jamii ilikuwa inatumia gharama kubwa.

  0 0

  Na: Lilian Lundo

  Serikali imebainisha kuwa kodi ya usajili wa namba binafsi kwenye magari unategemea kupanda kutoka shilingi 5,000,000 mpaka shilingi 10,000,000 kila baada ya miaka mitatu.

  Hayo yamesemwa jana Bungeni na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango alipokuwa akiwasilisha Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa Fedha 2016/17.

  “Napendekeza kufanya marekebisho kwenye Sheria ya Magari inayohusu kodi ya Usajili na Uhamisho wa Umiliki wa magari na kufanya ada ya usajili wa namba binafsi kupanda kutoka 5,000,000 hadi shilingi 10,000,000 kila baada ya miaka mitatu,” alisema Dkt. Mpango

  Akitoa sababu ya kupandisha kodi hiyo, Dkt. Mpango amesema kuwa kodi hiyo imepanda ili kuhuisha viwango vinavyopendekezwa kulingana na thamani halisi ya fedha nchini.
  Aidha, Dkt Mpango alitaja kodi nyingine zinazopanda katika sheria ya magari ni pamoja na usajili wa magari kutoka shilingi 150,000 hadi shilingi 250,000 na pikipiki kutoka shilingi 45,000 hadi shilingi 95,000.

  Katika hatua hiyo, Dkt. Mpango amesisitiza kuwa ongezeko hilo la kodi katika Sheria hiyo inayohusisha magari na pikipiki utaongeza mapato ya Serikali kwa kiasi cha shilingi milioni 26,915.9. 
   
  Bajeti ya Kuu ya Serikali ya mwaka 2016/17 yenye jumla ya Shilingi Trilioni 29.5 imewasilishwa Juni 8, 2016 inategemewa kujadiliwa kwa muda wa siku saba na Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzia Juni 10, hadi 20, 2016 ambapo mjadala utahitimishwa kwa kura ya wazi itakayopigwa na Wabunge.

  0 0

   
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Mchezaji wa Mpira wa kulipwa wa Kikapu NBA Marekani Hashim Thabit, wakati alipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu Dar es salaam leo Juni 09,2016 kwa ajili ya kumuelezea kuhusu lengo na mpango wake wa  kuanzisha na kukuza vituo vya Michezo hapa Nchini.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipokea Zawadi ya Mpira kutoka kwa Mchezaji wa Mpira wa kulipwa wa Kikapu NBA Marekani Hashim Thabit, wakati alipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu Dar es salaam leo Juni 09,2016 kwa ajili ya kumuelezea kuhusu lengo na mpango wake wa  kuanzisha na kukuza vituo vya Michezo hapa Nchini.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,katikati akiwa katika picha ya pamoja na Mchezaji wa Mpira wa kulipwa wa Kikapu NBA Marekani Hashim Thabit, wakati alipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu Dar es salaam leo Juni 09,2016 kwa ajili ya kumuelezea kuhusu lengo na mpango wake wa  kuanzisha na kukuza vituo vya Michezo hapa Nchini. (PIcha na OMR).

  0 0


  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira, Vijana na Ulemavu), Mhe. Jenister Mhagama akizungumza na Wakurugenzi wa Mifuko ya Hifadhi za Jamii kuhusu adhma ya utekelezaji wa agizo la ujenzi wa uchumi unaotegemea viwanda. Kushoto ni Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mwigulu Nchemba na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage.
  1. Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Godius Kahyarara (katikati) akizungumza katika kikao baina ya mifuho ya hifadhi ya jamii na Serikali kilichozungumzia adhma ya utekelezaji wa agizo la ujenzi wa uchumi unaotegemea viwanda. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa PPF, Bw. William Urio na kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya hifadhi ya Jamii (SSRA), Irene Isaka.
  Baadhi ya wajumbe wa kikao cha mashauriano ya pamoja baina ya Serikali na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kuhusu adhma ya ujenzi wa viwanda nchini wakifuatilia kwa makini kikao hicho kilichoitishwa na Serikali kupitia Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji pamoja Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira, Vijana na Ulemavu). Kikao hicho kilifanyika leo mjini Dodoma.
  Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Godius Kahyarara (katikati) akizungumza katika kikao baina ya mifuho ya hifadhi ya jamii na Serikali kilichozungumzia adhma ya utekelezaji wa agizo la ujenzi wa uchumi unaotegemea viwanda. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa PPF, Bw. William Urio na kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya hifadhi ya Jamii (SSRA), Irene Isaka.

  Jonas Kamaleki-Maelezo

  Serikali imekubaliana na mifuko ya hifadhi ya jamii kuanza utekelezaji wa ujenzi wa viwanda nchini ili kuhakikisha kuwa adhma ya Tanzania ya kufikia uchumi wa viwanda inafanikiwa ifikapo mwaka 2020.

  Hatua hiyo ni utekelezaji wa agizo la Rais John Pombe Magufuli aliyeitaka mifuko hiyo kuwekeza katika ujenzi wa viwanda nchini.

  Akizungumza mara baada ya kikao cha pamoja baina ya Serikali na mifuko hiyo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Ulemavu, Jenister Mhagama alisema Serikali imekusudia kuhakikisha uanzishwaji wa viwanda unaanza haraka na kuongeza fursa za ajira nchini.

  Mhagama alisema kuwa mali ghafi na nguvu kazi ya kutosha zipo hapa nchini hivyo hakuna sababu ya kuchelewa kuanza, ambapo Serikali imepanga hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2016, utekelezaji wa adhma hiyo inaanza kuonekana machoni mwa Watanzania.

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa sekta ya hifadhi ya Jamii (SSRA)alisema, Irene Isaka alisema ni agizo hilo limekuja katika wakati mwafaka kwa kuzingatia kuwa kwa mifuko ya Hifadhi ya jamii imekusudia kutekeleza kwa vitendo adhma ya Serikali ya awamu ya tano inayosisitiza kuijenga Tanzania kupitia uchumi wa viwanda.

  Kwa mujibu wa Isaka alisema kuwa kanuni na mifumo ya mifuko hiyo inaruhusu suala la uwekezaji katika viwanda ama kwa njia ya ubia au ya hati fungani au kutoa mikopo kwa wanotaka kuwekeza katika viwanda.

  Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt, Adelhelm Meru alisema uwekezaji katika viwanda ni suala ambalo linawashirikisha wadau wengi zikiwemo wizara za Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa ajili ya malighafi za viwandani, Elimu kwa ajili ya ujuzi wa watu wa kufanya kazi viwandani na Wizara ya Nishati na Madini kwa ajili ya nishati ya kuendesha viwanda.

  “Kwa kuangalia raslimali tulizo nazo tumewaomba wadau waanze na viwanda ambavyo vilikuwepo lakini kwa sasa havifanyi kazi kama vile Shirika la Usagishaji la Taifa (NMC), General Tyre, NARCO na Kiwanda cha Viwadudu cha Kibaha, alisema Dr. Meru na kuongeza kuwa malighafi za viwanda hivi zinapatikana hapa nchini.

  0 0

   Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Ally Hapi leo mchana ametembelea Rais mstaafu wa awamu ya pili Mh. Mzee Ali Hassan Mwinyi nyumbani kwake Mikocheni jijini Dar es salaam. 
   
  Akiwa nyumbani kwa Mzee Ali Hassan Mwinyi, Rais mstaafu na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni walizungumzia mambo mbalimbali yahusuyo maendeleo ya Kinondoni na historia ya nchi kwa ujumla. 
   
  Rais mstaafu alimshukuru Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni  kwa uamuzi wake wa kumtembelea na kumtakia kheri katika majukumu yake.Aidha mh. Mkuu wa Wilaya alimshukuru Rais mstaafu Mh. Ali Hassan Mwinyi na kumtakia afya njema na maisha ma

  0 0

  Na. Immaculate Makilika- MAELEZO,

  Dar es Salaam.

  SERIKALI imejipanga kukomesha mtandao wa watu wasiowaaminifu ambao wanajihusisha na biashara ya kusafirisha binadamu kwenda nchi mbalimbali duniani.

  Mtandao huo unahusisha raia wa Tanzania waliopo ndani na nje ya nchi kwa kushirikiana na raia wa kigeni kutoka nchi za India, Malaysia, nchi za Falme za Kiarabu na Mashariki ya Kati.

  Hayo yamesemwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Mindi Kasiga alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.

  “Serikali kwa kushirikiana na Jumuiya ya Watanzania wanaoishi katika nchi za Bara la Asia pamoja na baadhi ya wahanga wa biashara hiyo inashughulikia kupata majina ya wahusika wote, ikiwemo walioko kwenye Balozi ambao wanawezesha upatikanaji wa visa kuwakamata na kuwafikisha katika mkono wa sheria” alisema Mindi.

  Ili kukomesha mtandao huo, Serikali imeanda utaratibu maalumu kwa wafanyakazi wanaokwenda katika nchi za ukanda huo ikiwa ni pamoja na kuandaa mikataba kulingana sheria za nchi husika.

  Mindi amesema kuwa kwa nchi ya Omani tangu mwezi Machi 2011 hadi Septemba 2015, Serikali kupitia Ubalozi imeratibu ajira za Watanzania 4358 ambapo kati ya hizo ajira 4033 ni za watumishi wa majumbani.

  Aliongeza kuwa, kwa upande wa nchi za Mashariki ya Kati, kuanzia mwezi Juni, 2015 Serikali ilikataza rasmi Watanzania kwenda kufanyakazi zisizo na ujuzi au za ndani katika nchi hizo hadi hapo ilipopata ufumbuzi wa changangamoto zilizokuwa zikisababishwa na mtandao uliokuwa unajihusisha na usafirishaji wa binadamu.

  Aidha, ili kuwasaidia Watanzania kupata fursa za ajira nje ya nchi, Serikali inaendelea na jitihada za kusaini mikataba ya Ushirikiano na nchi hizo ikiwemo mkataba wa Tanzania na Qatar. Mtandao huo wa kusafirisha binadamu umekua ukitoa ahadi za ajira kwa wasichana wenye umri wa kati ya miaka 18 na 24, kwa kuwalaghai kuwa na fursa za ajira katika mahoteli, migahawa, maduka makubwa au kazi za nyumbani, kitu ambacho si ukweli.

  Hata hivyo, wengi wa Watanzania wanaoenda nje ya nchi kwa kusaidiwa na mtandao huo wamekuwa wakipata matatizo kadhaa, ikiwemo mateso, mikataba yao kukiukwa, kulazimishwa kufanya ukahaba, na hatimaye kukimbilia Ubalozini ili kupatiwa misaada mbalimbali.

  Aidha, imedhihirika kuwa Watanzania walio katika nchi za Bara la Asia, Falme za Kiarabu na Mashariki ya Kati wamekuwa wakiomba misaada ya kurudishwa nchini kupitia Balozi hizo wakiwemo watanzania 500 waliopo nchini India.

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein akizungumza na Waandishi wa Habari wa Vyombo vya Serikali pamoja na Viongozi wa Wizara ya Habari katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo.9/06/1026. MKurugenzi Mkuu wa Shirika la Habari la Utangazji Zanzibar (ZBC) Hassan Mitawi alipokuwa akitoa mchango wake wakati wa mkutano uliofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein kuzungumza na waandishi wa Habari wa Vyombo vya Serikali leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja.Mwandishi wa Shirika la Habari la Utangazji Zanzibar (ZBC)Tv Maulid Kipevu akitoa mchango wake wakati wa mkutano uliofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein kuzungumza na waandishi wa Habari wa Vyombo vya Serikali leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja.Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein akizungumza na Waandishi wa Habari wa Vyombo vya Serikali pamoja na Viongozi wa Wizara ya Habari katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo.Baadhi ya Waandishi wa habari wa Taasisi za Serikali wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein alipokuwa akizungumza nao leo pamoja na Viongozi wa Wizara ya Habari katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja.Baadhi ya Waandishi wa habari wa Taasisi za Serikali wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein alipokuwa akizungumza nao leo pamoja na Viongozi wa Wizara ya Habari katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja.Mwandishi mwandamizi wa Shirika la Habari la Utangazji ZBC Tv Khamis Fakih akitoa mchango wake wakati wa mkutano uliofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein kuzungumza na waandishi wa Habari wa Vyombo vya Serikali leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.]09/06/1026. Mwandishi wa Gazeti la Zanzibar leo Hapsa Golo akisisitiza jambo wakati alipokuwa akitoa mchango wake wakati wa mkutano uliofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein kuzungumza na waandishi wa Habari wa Vyombo vya Serikali leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.]09/06/1026

  0 0

  Na Jacquiline Mrisho - MAELEZO

  Halmashauri ya Manispaa ya Ilala imetoa agizo kwa wamiliki wa majengo wa Manispaa hiyo kupaka rangi majengo yaliyochakaa na kuweka taa ili kuimarisha ulinzi na usalama katika maeneo yao.

  Agizo hilo limetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Isaya Mngurumi ambaye amesisitiza kuwa suala hilo lipo kisheria kwahiyo, wamiliki wote wa majengo wanatakiwa kutekeleza agizo hilo ili kuepuka kuchukuliwa hatua stahiki za kisheria.

  “Sheria ya Mipango Miji inasema kuwa majengo yote yapakwe rangi zinazoeleweka na wamiliki wote wanaombwa kufata sheria na kutekeleza agizo hilo kwa muda uliopangwa ili kuondokana na usumbufu kwa hatua zitakazochukuliwa kwa atakayekaidi agizo hili”,alisema Mngurumi.

  Ameongeza kuwa sio tu sheria hiyo pekee bali Sheria ya Mazingira inahusika katika kuendeleza na kupendezesha Miji kwahiyo, zoezi la  kuweka taa na kupaka rangi majengo chakavu ni moja ya njia ya kuendeleza na kuupendezesha Mji.

  Mngurumi amefafanua kuwa baada ya jengo kupakwa rangi linatakiwa kupakwa tena kila baada ya miaka miwili na kwa mwaka huu zoezi limeanza rasmi Aprili na limepangwa kuisha mwishoni mwa mwezi Juni.

  Aidha, Mkurugenzi huyo ametoa rai kwa wamiliki wa makampuni mbalimbali kutopaka rangi za matangazo kwenye majengo bila kuthibitishwa na kupewa kibali na Halmashauri husika kwa kuwa kutokufanya hivyo ni kukiuka sheria za Mipango Miji.

  Wamiliki wote wa majengo katika Manispaa ya Ilala wanatakiwa kupata kibali kutoka katika ofisi ya Halmashauri hiyo ili kuweza kuweka matangazo mbalimbali katika majengo yoyote yaliyopo kwenye Manispaa hiyo.

  0 0  al1Mwenyekiti wa Jumuiya ya watu wenye Alibinism Tanzania (TAS) Nemes Temba akizungumza na waandishi wa Habari (hawapopichani) leo jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujulisha umma siku ya maadhimisho ya Albino duniani.Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa TAS Dar es Salaam, Gabriel Aluga, Katibu Mkuu wa TAS, Musa Katimba na Mratibu kutoka asasi ya kiraia ya BADEF.
  al2Mwenyekiti wa Mfuko wa Good Hope Star na mjumbe wa kamati ya maandalizi ya maadhimisho ya siku ya Albino duniani Al Shamaymaa Kwegyir akifafanua jambo wakati wa mkutano wa waandishi wa Habari (hawapopichani) leo jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujulisha umma siku ya maadhimisho ya Albino duniani.Kutoka kuliani Mwenyektiwa TAS Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa TAS, Musa Katimba (kushoto) na Mwenyekiti wa  TAS Taifa Nemes Temba.
  al3Wandishi wa habari wakichukua matukio wakati wa mkunano baina ya TAS na waandishi wahabari katika ukumbi wa  Idara ya Habari – MAELEZO leo jijini Dar es Salaam.NA: Frank Shija,MAELEZO.
  …………………………………
  Na: Lilian Lundo,MAELEZO
  Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli anatarajiwa  kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kuongeza uelewa kuhusu ualbino yatakayofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.

  Akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa chama cha Watu Wenye Ualbino Nchini  (Tanzania Albinism Society) Nemes Temba ameeleza kuwa kupitia maadhimisho hayo jamii itapata fursa ya kupewa elimu muhimu kuhusu ualbino ili kuondoka na dhana potofu hususani ushirikina.

  “Maadhimisho haya ambayo yataanza Juni 11 hadi Juni 13, 2016 yatasindikizwa na mambo mbalimbali ikiwemo  huduma za afya hususani uchunguzi na matibabu ya saratani ya ngozi pamoja na nasaha za viongozi na mabalozi, utambulisho wa Miss Albino Tanzania na uzinduzi wa kamusi ya ulemavu,” alisema Temba.

  Temba aliendelea kuainisha kwamba  siku hiyo itawapa fursa watoto wenye ualbino waishio kwenye vituo mbalimbali nchini kutembelea mji wa Bagamoyo kujionea mambo mbalimbali chini ya ufadhili wa shirika la UNICEF.

  Aidha Mwenyekiti huyo amemshukuru Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuwapa vipaumbele watu wenye ulemavu akiwemo Dkt. Abdallah Possi ambaye ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Bunge, Sera, Ajira, Kazi na Watu Wenye Ulemavu hii inadhihirisha kuwa ulemavu si hoja bali utendaji kazi ndio kitu umuhimu.

  0 0

   Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe.  Dkt. Philip Mpango (Mb), akipokea hundi kifani yenye thamani ya shilingi Bilioni 4.5 kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Puma Energy Dkt. Ben Mosha, wakati wa Hafla fupi ya serikali kukabidhiwa Hundi za Mfano zenye thamani ya shilingi Bilioni 23 kutoka kwa Kampuni za Puma Energy, Tiper (T) na NBC Bank PLC, ambazo imewekeza hisa zake, katika ukumbi wa Hazina (Treasury Squire) Mjini Dodoma
   Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dk. Medard Kalemani, akizungumza jambo wakati wa Hafla fupi ya serikali kukabidhiwa Hundi za Mfano zenye thamani ya shilingi Bilioni 23 kutoka kwa Kampuni za Puma Energy, Tiper (T) na NBC Bank PLC, ambazo imewekeza hisa zake, katika ukumbi wa Hazina (Treasury Squire) Mjini Dodoma
   Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt Philip Mpango(Mb), (Katikati) akimwelekeza jambo Msajili wa Hazina Laurence Mafuru, wakati wa Hafla fupi ya serikali kukabidhiwa Hundi za Mfano zenye thamani ya shilingi Bilioni 23 kutoka  Kampuni za Puma Energy, Tiper (T) na NBC Bank PLC, ambazo imewekeza hisa zake, katika ukumbi wa Hazina (Treasury Squire) Mjini Dodoma
   Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dorothy Mwanyika, akipokea mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi Bil. 2.0 kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Tiper (T), Prof. Abdulkarim Mruma, wakati wa Hafla fupi ya serikali kukabidhiwa Hundi za Mfano zenye thamani ya shilingi Bilioni 23 kutoka Kampuni za Puma Energy, Tiper (T) na NBC Bank PLC, ambazo imewekeza hisa zake, katika ukumbi wa Hazina (Treasury Squire) Mjini Dodoma
   Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage (Mb) akizungumza jambo wakati wa Hafla fupi ya serikali kukabidhiwa Hundi za Mfano zenye thamani ya shilingi Bilioni 23 kutoka Kampuni za Puma Energy, Tiper (T) na NBC Bank PLC, ambazo imewekeza hisa zake, katika ukumbi wa Hazina (Treasury Squire) Mjini Dodoma
  Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt Philip Mpango(Mb), (Katikati) akinyoosha dole gumba kuashiria "mambo safi", wakati akipokea hundi ya shilingi Biln 16.5 kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Ineke Bussemaker, wakati wa Hafla fupi ya serikali kukabidhiwa Hundi za Mfano zenye thamani ya shilingi Bilioni 23 kutoka  Kampuni za Puma Energy, Tiper (T) na NBC Bank PLC, ambazo imewekeza hisa zake, katika ukumbi wa Hazina (Treasury Squire) Mjini Dodoma.
   Msajili wa Hazina, Laurence Mafuru, akifafanua jambo wakati wa Hafla fupi ya serikali kukabidhiwa Hundi za Mfano zenye thamani ya shilingi Bilioni 23 kutoka kwa Kampuni za Puma Energy, Tiper (T) na NBC Bank PLC, ambazo imewekeza hisa zake, katika ukumbi wa Hazina Mjini Dodoma
   Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Puma Energy Dkt Ben Mosha, akizungumza Jambo wakati wa Hafla fupi ya serikali kukabidhiwa Hundi za Mfano zenye thamani ya shilingi Bilioni 23 kutoka kwa Kampuni za Puma Energy, Tiper (T) na NBC Bank PLC, ambazo imewekeza hisa zake, katika ukumbi wa Hazina Mini Dodoma


  hazitoi gawio zikisingizia kupata hasara kwenye biashara wakati hawafungi biashara hizo" Alisisitiza Dk. Mpango

  Dk. Mpango pia amevitaka vyombo vya dola kufanya uchunguzi, ili kubaini mianya ya upotevu wa mafuta bandarini na kuagiza wale wote walihusika na upotevu huo wachukuliwe hatua.

  " Haiwezekani wajanja wachache wanafaidika halafu wananchi wanyonge wanalala chini hospitalini, Nilisema jana na leo narudia yeyote anayetukwamisha kwenye maendeleo ni msaliti lazima washughulikiwe kwa mujibu wa sheria bila huruma,” alisema.

  Awali Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk. Medard Kalemani, amezipongeza kampuni hizo kwa kutoa gawio hilo na kumhakikishia Waziri wa Fedha na Mipango, Dokta Philip Mpango, kuwa gawio litaongezeka kwa kasi kubwa katika miaka ijayo ili kuiwezesha serikali kuwa na uwezo zaidi wa kuwahudumia wananchi.

  “Mwaka 2014 tulipata gawio la Sh bilioni 3 kutoka Kampuni ya PUMA Energy, mwaka huu tumepata bilioni 4.5 ni matarajio ya Serikali kwa mwendo huu mwakani tunaweza kupata bilioni 6" alisema Dkt. Kalemani.

  Alitoa wito pia kwa kampuni nyingine zenye ubia na Serikali ambazo hazitoi gawio zianze sasa kutoa akieleza kuwa mantiki ya gawio ni kwamba kampuni inafanya kazi na inapata faida, inapokuwa haitoi gawio mantiki yake ni kwamba kampuni inafanya kazi haipati faida.

  “Lakini ni vigumu kuamini kama kampuni hazipati faida kwa mfululizo wa miaka 10 na inafanya kazi, sisi tunaamini wanapata faida, na zipo kampuni nyingi ambazo si busara kuzitaja hapa zinadai kupata hasara kila mwaka,” alisema.

  Kuhusu upotevu wa mafuta bandarini, Dk. Kalemani alisema tatizo hilo hivi sasa limedhibitiwa, baada ya Serikali kuanzisha chombo maalumu kinachoratibu na kudhibiti upotevu huo.

  Alikuwa akijibu changamoto iliyotolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya Puma Energy, Dkt. Ben Moshi, aliyeelezea kuwa katika kipindi cha mwaka 2014/2015 kampuni hiyo imepata hasara ya Dola za Marekani milioni 1.4 ambazo ni zaidi ya Sh bilioni 2.5 kutokana na upotevu huo wa mafuta.

  Kwaupande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Tiper (T), inayojihusisha na uhifadhi wa mafuta, ambapo amesema tangu mwaka 2010, kampuni hiyo imetoa gawio la shilingi Bil. 6.4 kwa serikali na kuahidi kuwa gawio hilo litaongezeka siku za usoni.

  Naye Mkurugenzi wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker, amesema kuwa benki yake inajisikia fahari kubwa kugawa faida iliyopata katika biashara zake kwa mbia wake ambaye ni serikali.

  Amesema kuwa pamoja na serikali kuwa mbia kwa hisa ya asilimia 31.8, lakini pia ni mteja mkubwa wa benki hiyo ambayo hurudisha faida ya uwekezaji kwa wananchi kupitia gawio hilo na kutoa wito kwa watanzania kuitumia benki hiyo kuweka amana na kukopa

  Hafla hiyo imehudhuriwa pia na Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage ambaye ametoa wito kwa wawekezaji wakiwemo wale wanaofanya biashara zao kwa kushirikiana na serikali kufanyakazi zao kwa uaminifu kwa kutangaza faida wanazopata kihalali ili serikali iweze kupata mapato yake yatakayosaidia kuboresha maisha ya wananchi

  Naye Msajili wa Hazina, Laurence Mafuru, ameahidi kuyafuatilia na kuyasimamia mashirika yote ya umma na yale ambayo serikali imewekeza, ili kuhakikisha kuwa hawakwepi kulipa gawio ili kuiwezesha serikali kupata mapato yake


  Imetolewa na


  Benny Mwaipaja

  Kaimu Msemaji wa Wizara ya Fedha na Mipango

  0787087878older | 1 | .... | 874 | 875 | (Page 876) | 877 | 878 | .... | 1903 | newer